Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII DK.HAMISI KIGWANGALLA AHANI MSIBA WA RUGE

$
0
0
NA ANDREW CHALE. 

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba na kutoa pole za msiba ambapo pia ameweza kumwelezea marehemu Ruge kama mtu mwenye uthubutu kwa jamii.

Dk.Kigwangalla ameweza kuonana na kutoa pole kwa wafiwa ndugu,jamaa na marafiki akiwemo Baba mzazi Mzee Mutahaba pamoja Mama wa Ruge Bi. Cristina Mutahaba na kutoa pole zake hizo pamoja na rambirambi alizokabidhi kwa Mama mzazi.

Dk Kigwangalla amemuelezea marehemu kama mtu wa kuigwa kwani alijituma katika kuhakikisha anatimiza malengo yake aliyopangiwa ama kujipangia. 

"Ruge alikuwa mtu wa watu. na alisimama katika mipango sahihi hata nikamchagua kwenye Kamati za kuendeleza masuala ya Utalii ikiwemo ile ya Tanzania Unforgettable." alieleza Dk Kigwangalla. 

Aidha, Dk Kigwangalla ameweza kuungana na viongozi wengine pamoja na ndugu na jamaa.

Awali taaifa ya Msemaji wa Familia Bw. Anic Kashasha amesema kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utawasili Ijumaa na utaagwa rasmi siku ya jumamosi jijini Dar es salaam, Baada ya kuagwa utasafirishwa kwenda Bukoba siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu huko Bukoba mkoani Kagera. 
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa pole kwa Mama mzazi wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge pole wa Kigoma Zitto Kabwe katika msiba wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.

Taasisi ya Tulia Trust yafanikisha kugharamia matibabu ya Amos

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Taasisi ya Tulia Trust yafanikisha kugharamia matibabu ya kijana Amos Gabriel ya kwenda kutibiwa katika Hospitali Neurogen ya nchini India.

Kijana huyo na mzazi wake wanatarajia kuondoka Machi Tatu ikiwa taratibu zote za matibabu zimeshafanyika pamoja na gharama Hospitali hiyo zimeshalipwa tayari.

Akizungumza wakati kukabidhi Taasisi ya Tulia Trust na wadau mbalimbali wameweza kufanikisha sh. milioni 33 kwa matibabu ya kijana huyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya sh.milioni 33 kwa mzazi wa Amos amesema kuwa wanamuombea Mungu aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na muendelea na masomo.

Amesema kuwa waliguswa baada ya kuona taarifa katika vyombo vya habari juu madhila yanayomkuta kijana huyo.Amesema kuwa kijana Amos ana ndoto ya shule hivyo isiweze kukatishwa.

Ameshukuru wadau kwa kuungana katika kufanikisha matibabu ya kijana huyo.Mzazi wa Amos amesema anamshukuru Naibu Spika kwa kijitoa na watanzania katika kufanikisha gharama ya matibabu ya kwenda kutibiwa nchini India.

Amesema kuwa kuwa yeye sio bora sana kwani kuna watu wengine wanataka msaada huo.Mgonjwa wa Amos Gabriel amesema kuwa anawashukuru watanzania kupitia Tulia Trust kwa kumuona inahitaji msaada baada ya kuona taarifa katika vyombo vya habari.

Gabriel anatatizo la uti wa mgongo uliotokana na kuanguka katika mti wakati akikata fimbo ya mwalimu kwa ajili ya kuwachapia wanafunzi.
 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akimkabidhi hundi ya  sh.milioni 33 mzazi wa Mtoto Amos ,Swaum Ramadhan kwa ajili ya matibabu nchini India.

 Naibu Spika Dkt Tulia Ackson akipokea Mkono wa shukrani kutoka Amos ambaye anatarajia kwenda katika matibabu ya magogo nchini India.
 Balozi wa Tulia Trust Lameck Ditto akizungumza ana waandishi habari wa kuhusiana na Taasisi hiyo kutoa msaada kwa Amos kwa ajili matibabu nchini India.

Naibu Spika Dkt.Tulia Ackson akizungumza wakati alikwenda kupeleka msaada wa matibabu ya Amos nchini India ambayo Fedha hiyo imetolewa na Taasisi ya Tulia Trust na wadau wengine.
 Amos Gabriel akieleza namna ya umuhimu watanzania kuguswa na kuchangia kwa ajili ya matibabu ya nchini India.
Mzazi wa Amos, Swaum Ramadhan akizungumza kuhusiana na Taasisi ya Tulia Trust kufanikisha matibabu ya mwanae

Tanzania Yaingia Makubaliano Kuendeleza Kiswahili Sudan Kusini

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kulia) na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai wakiweka saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili jana jijini Dodoma. 
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kulia) akifurahia wakati Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai akionyesha hati ya mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini mara baada ya kuweka saini jana jijini Dodoma. (Picha na: Frank Shija – MAELEZO, Dodoma)
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasili katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu jana kwa ajili ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika Lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kulia) jana jijini Dodoma. Kushoto ni Balozi wa Sudan Kusini nchini Tanzania, Mhe.Mariano Deng Ngor. 
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kushoto) jana jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ave Maria Semakafu. 
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Elimu hususan katika lugha ya Kiswahili na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudani Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai (kushoto) jana jijini Dodoma. 
Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubalina ya ushirikiano katika sekta ya elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini jana jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako 
Balozi wa Sudan Kusini nchini Tanzania, Mhe.Mariano Deng Ngor akitoa neno la shukrani wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa makubalina ya ushirikiano katika sekta ya elimu baina ya Tanzania na Sudan Kusini jana jijini Dodoma. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako na Waziri wa Elimu na Mafunzo wa Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Deng Deng Hoc Yai(katikati). 

UAMUZI WA SERIKALI WA KUWABANA WATUMISHI WA UMMA WAZAA MATUNDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakuu wa Idara za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwafariji wanawake waliolazwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amempakata mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo, hivi sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtoto huyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wakuu wa Idara za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke wakati alipotembelea hospitali hiyo, Februari 27, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa amempakata mototo Natasha Chriswell wakati alipotembelea Kliniki ya Methadone katika hospitali ya Mwananyamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019. Kulia ni mama wa mtoto huyo, Zaynab Hamisi ambaye miaka saba iliyopita alikuwa ni muathirika wa dawa za kulevya na amepatiwa matibabu katika Kiliniki hiyo, hivi sasa ni mzima, ameolewa na amebahatika kupata mtooto huyo. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam, Paul Makonda na wa pili kulia ni Mkuu wa kitengo cha Methadone hospitalini hapo, Dkt. Sosthenes Hongo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapa pole wagonjwa wakati alipotembelea wodi ya watoto katika Hospitali ya Mwayamala wilayani Kinondoni, Februari 27, 2019.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


*Wananchi waipongeza kwa kuwa umeimarisha utoaji wa huduma za afya

WANANCHI wameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwabana watumishi wa umma, kwa sababu uamuzi huo umezaa matunda na sasa hali ya utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo ya hospitali yameimarika.

Kauli hiyo imetolewa leo (Jumatano, Februari 27, 2019) na wagonjwa waliolazwa katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hospitali hapo.

“Huduma zimeimarishwa dawa tunapata, hakuna lugha chafu wala kuombwa rushwa. Tunahudumiwa vizuri na kuna wakati hadi tunabembelezwa kunywa dawa mambo ambayo hapo nyuma hayakuwepo, hivyo tunaishikuru Serikali.”

Mmoja wa wagonjwa hao ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo baada ya kujifungua, Mwajuma Mohammed amesema baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuingia madarakani na kuwabana watumishi wa umma sasa kuna mabadiliko makubwa sana ya kiutendaji.

Amesema zamani baadhi ya wauguzi hususani wanaofanyakazi kwenye wodi ya wazazi hawakuwa na lugha nzuri walikuwa wakiwatukana na kuwakashifu jambo ambalo kwa sasa halipo, kwani wakifika wapokelewa vizuri.

Mama mwingine aliyelazwa kwenye wodi hiyo, Crista Moyo amemuomba Waziri Mkuu kuisadia hospitali hiyo kwa kuiongezea watumishi kwa kuwa walipo ni wachache ukilinganisha na idadi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kila siku.

Crista ameishauri Serikali ikiwezekana iajiri hata watu wasiokuwa na taaluma ya udaktari au uuguzi ili wakafanyekazi ambazo hazihitaji ujuzi kama za kuwasaidia wagojwa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amezishauri Halmashauri jijini Dar es Salaam zihakikishe zinaendelea kuimarisha vituo vya afya na kuongeza vingine ili utoaji kupunguza msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali za rufaa.Pia ameshauri ianzishwe miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika hospitali hizo kwa lengo ya kuwezesha utoaji wa huduma mbalimbali zikiwemo za dharura kwa wakati.

“Rais Dkt. Magufuli anataka wananchi wapate huduma za afya karibu na makazi yao ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo. Ndio maana tunajenga vituo vya afya vilivyokamilika vinavyotoa huduma zote muhimu kama maabara, upasuaji na mama na mtoto.”

Waziri Mkuu amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua utoaji wa huduma za afya zinazotolewa katika hospitali hizo na kubaini kama kuna changamoto ili Serikali iweze kuzitambua na kuzitafutia ufumbuzi.“Tumesikia changamoto zinazowakabili madaktari, tumezichukua na tutazifanyia kazi ikiwepo ya upungufu wa watumishi mbalimbali kama madaktari na wauguzi ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema dhamira ya dhati ya Serikali kwao ni ya kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, hivyo waendelee kuwa wazalendo na washirikiane na Serikali yao. Wafanye kazi kwa bidii.Naye,Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Amaani Malima amesema hospitali hiyo inahudumia wagonjwa wa nje 1,800 hadi 2,000 kwa siku na wagonjwa wa ndani 250 hadi 300. Wagonjwa hao watoka wilaya mbalimbali.

Dkt. Malima amesema hospitali hiyo ina jumla ya watumishi 439 kati yao madaktari bingwa ni 16, madaktari 76 na wauguzi 209 na watumishi wengine 138. “Idadi hii ni ndogo kulingana na mahitaji ya hospitali kwani tuna upungufu wa watumishi 278 sawa na asilimia 39.”

Akizungumzia hali ya upatikanaji wa dawa muhimu kwenye hospitali hiyo, Dkt. Malima amesema kwa kipindi cha Januari upatikanaji ulikuwa wa kuridhisha kwa asilimia 85 ya kiasi cha dawa na vifaa tiba vilivyohitajika.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala ambapo alikagua mradi wa ujenzi wa jengo la kuhudumia wagonjwa mashuhuri ambalo lilianza tangu mwaka 2014 na bado halijakamilika.

Hivyo, ameishauri Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuangalia namna ya kuweza kusaidia ujenzi wa jengo hilo ili mradi huo uweze kukamilika na hatimaye huduma zilizokusudiwa kutolewa katika jengo ziweze kufanyika.Pia, Waziri Mkuu amewataka Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Daniel Nkungu na Kiongozi wa Wauguzi, Wambura wahakikishe wanaimarisha ushirikiano wao na hata wanapotoa maagizo kwa wasaidizi wao wawe wanataarifiana.

Kwa upande wa watumishi wanaofanya kazi katika idara za maabara amewataka wawe wanawahi kutoa huduma kwa sababu kuna malalamiko ya ucheleweshwaji wa huduma katika eneo hilo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka watumishi wanaofanya kazi katika kitengo cha radiolojia kwenye hospitali za Rufaa za Mkoa za Mwananyamala na Temeke jijini Dar es Salaam waache urasimu na wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.

TAHADHARI KUHUSU VITENDO VYA UDANGANYIFU NA UTAPELI

OFISI YA MWANASHERIA MKUU KUWA NA MFUMO WA KUSIMAMIA VIASHIRIA HATARISHI

$
0
0
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Evaristo Longopa akifungua mafunzo ya Uelewa Juu ya Usimamizi wa Viashiria Haratishi ( Risk Management) kwa Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mafunzo hayo ya siku tatu na ambayo yatakuwa shirikishi yataiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuandaa Mwongozo wake wa Usimamizi wa Viasharia Hatarishi. Mwongozo ambao utaendana na majukumu na mazingira ya Ofisi.



Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mafunzo ya uelewa juu ya usimamizi wa viashiria hatarishi kwa watumishi wake ( Risk Management) 

Mafunzo hayo yanayotolewa na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Onesmo Mbekange yatafayika kwa siku tatu, na yamefunguliwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Evaristo Longopa. 

Akifungua mafunzo hayo siku ya jumanne, yaliyoanza na Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Dk. Longopa amesema, mafunzo hayo ni muhimu sana kwa yatasaidia na kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. 

Dk. Longopa vilevile ameyataja mafunzo hayo kuwa , yatawezesha watumishi wote kuwa na uelewa wa pamoja wa viashiria hatarishi ambavyo kama havitathibitiwa mapema vinaweza kukwamisha kufikiwa wa malengo ambayo Ofisi imejiwekea. 

Akasema , hapana shaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama ilivyo kwa Taasisi nyingine, ina viashiria vingi vya hatari na hivyo kuwataka watumishi wote kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo kujijengea uelewa ili kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Naibu Mwanasheria Mkuu amewaeleza wakuu hao wa divisheni na vitengo kwamba, baada ya mafunzo hayo ambayo yatakuwa shirikishi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itakamilisha mchakato wa kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi ( Risk Management Framework). 

Katika mafunzo hayo, Bw. Onesmo Mbekange, ameeleza kuwa kila Wizara na Taasisi za Serikali bila la kujali ukubwa au udogo wake zinapashwa kuwa na Mwongozo wa namna ya kukabiliana na viashiria hatarishi vinavyotokana na utekelezaji wa majumu yao ya kitaasisi au ki-wizara. 

Akasisitiza kuwa endapo Taasisi inakuwa tayari na mfumo au mwongozo wa usimamizi wa viashiria hatarishi, unaipa mwanga na utayari Taasisi wa nini kitatokea na namna gani ya kukabiliana na hatari hizo kabla hazijatokea. 

“Ukiwa na Mwongozo kunaiwezesha Menejimenti ya Taasisi kufanya maamuzi sahihi na mapema kabla ya tukio halijatokea badala ya kusubiri mpaka tatizo litokee” Amesema Bw.Mbekange. 

Aidha amebainisha kwamba, Mwongozo wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi pia unaiwezesha Taasisi kufikia malengo ambayo Taasisi imejiwekea, na gharama ndogo na utendaji wa Taasisi unaimarika. 

Ameeleza zaidi kwamba, Wizara au Taasisi za Serikali kutokuwa na Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine kunapelekea ukiukwaji na kutokuzingatiwa kwa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. 

Mwaka 2012 Wizara ya Fedha na Mipango iliandaa Mwongoao wa Kitaifa wa Maandalizi na Usimamizi wa Vihatarishi na kuagiza Wizara na Taasisi za Serikali kuandaa Miongozi itakayotekeleza agizo hilo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali 
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

PICHA MBALIMBALI ZA RUGE MUTAHABA AKIWA KAZINI ENZI ZA UHAI WAKE

$
0
0
Aliwapika na kuwajenga mwenyewe kwa mambo mengi na mwisho alikiri  wazi kuwa sasa vijana hawa wameiva,Ruge hakuwaacha hivi hivi aliwapa zawadi ama cheti cha shukurani,kama ambayo anaonekana pichani akimkabidhi msanii wa bongofleva Mwasiti Almasi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muziki katika kituo cha nyumba ya vipaji THT
Ruge hakuwaacha vijana wake hivi hivi ,aliwapa zawadi ama cheti cha shukurani,kama ambayo anaonekana pichani akiwakabidhi baadhi ya wasanii wa bongofleva cheti cha kuhitimu mafunzo ya muziki katika kituo cha nyumba ya vipaji THT




Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishali wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akizungumza jambo kwenye moja ya hafla za kampuni hiyo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Joseph Kussaga,huku wakiwa wamezungukwa na baadhi ya wafanyakazi
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Joseph Kussaga akiungumza jambo huku Ruge Mutahaba akisikiliza kwa makini,kweye moja ya hafla za kampuni hiyo.
Ruge Mutahaba,mara nyingi hakupenda makuu,aliwaacha vijana aliowafungulia Dunia kuonesha umahiri wao katika mambo mbalimbali na yeye kukaa pembeni yao huku akiwatazama na kuwasikiliza,kama ambavyo anaonekana kwenye picha hizi.
Ruge Mutahaba alianzisha jukwaa la Fursa la kuwawezesha vijana katika mambo mbalimbali,pamoja na kuwa mwanzilishi kuna wakati aliamka na kutoa neno kama anavyoonekana pichani
Ruge Mutahaba akimuongoza aliyekuwa Waziri Mkuu awamu ya nne,Mh Fredrick Sumaye alipokwenda kutembelea kampuni hiyo ya Clouds Media Group na kuoneshwa mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na kampuni hiyo.
Ruge akiwa na mgeni wake Mh Sumaye  ndani ya Studio za Clouds FM akimfafanulia jambo hatua kwa hatua.
Ruge Mutahaba pia hakuwa mkimya muda wote,wakati mwingine alijichangana na sehemu za watoto kama hivi na kutoa maono yake kwa jambo husika ikiwemo na kushauri nini kifanyike kusoga mbele zaidi 
Vijana wengi walipenda kumsikiliza Ruge,hasa kwa lugha alizokuwa akitumia nyepesi na zenye kutia hamasa ya kusikiliza zaidi kama anavyoonekana pichani

Ruge hakuacha kuwaelekeza ama kuwakumbusha jambo vijana wake wakati wowote na mahali popote pindi akutanapo,pichani alikuwa akizungumza jambo na mmoja wa watangazaji wa Clouds FM Hamis Mandi almaarufu kwa jina la Bdozen
Ruge Mutahaba akionekana na baadhi ya wasanii wa bongofleva walipokwenda kumjulia hali Mzee Njenje nyumbani kwake Sahare mkoani Tanga

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI,FEBRUARI 28,2019


Habari za UN Februari 27, 2019

VOA SWAHILI: Duniani Leo February 27th, 2019

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 27.02.2019

JIJI LA MBEYA SASA KUFUMULIWA NA KUSUKWA UPYA, MKATABA WA UPANGAJI WA MIJI WASANIWA

Mwasiti: THT itaendelea kuibua vipaji kama kawaida, Ruge ameacha darasa

BYE BYE RUGE TRACK by AKIL THE BRAIN - 2019

WAZIRI MKUU ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU RUGE

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  na mkewe Mary (wa pili kulia) wakimfariji mama Mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba, Christiana Mutahaba wakati  walipokwenda nyumbani kwao  marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia ,  Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba wakati alipokwanda nyumbani kwao marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam  kutoa pole kwa familia, Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu Ruge Mutahaba, Mikocheni jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia , Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI ZISIZOTUMIKA MKOANI MOROGORO WAKALIA KUTI KAVU

$
0
0

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maelekezo kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kupata idadi ya nyumba zinazotakiwa kulipiwa kodi ya Majengo, wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro, kushoto ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Bw. Emmanuel Maro.
Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya katika Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maagizizo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu andiko la miradi ya kimkakati itakayosaidia halmashauri zao kujitegemea kimapato.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari, akiwataka Wakurugenzi kuwajibika ili kuwaletea wananchi maendeleo stahiki wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bw. Mohamed Utaly na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi, wakizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Mchembe, akiitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kushirikiana na uongozi wa Wilaya ili kufanikisha lengo la makusanyo ya Kodi zinazopangwa katika ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.

Na Peter Haule, WFM, Morogoro
Serikali imeahidi kulifanyiakazi suala la Leseni mfu za uchimbaji madini mkoani Morogoro, ili kutoa fursa ya wachimbaji wadogo  kuchimba madini hayo na kulipa kodi stahiki kwa manufaa mapana ya Taifa. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipofanya Mkutano na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Morogoro na wadau wengine.

Maelekezo hayo yanafuatia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, ambaye pamoja na kuishukuru Serikali kwa  kutoa fedha zenye lengo la kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato na akaiomba Serikali kuhakikisha inafuta Leseni mfu za wachimba madini takribani 174 ambao wanazuia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za kujipatia kipato kutokana na  madini na kulipa kodi.

Dkt. Kabwe alimweleza Dkt. Kijaji kwamba mkoa wa Morogoro umesheheni madini ya kila aina na jambo linalosababisha ukosefu wa mapato unachangiwa pia na  utoroshaji wa madini ambapo ameeleza kuwa mikakati ya Mkoa huo ni kuanzisha Soko la Madini mkoani humo ili kuepusha utoroshaji huo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa kama wapo watu wenye Leseni za uchimbaji madini 178 na wanaolipa kodi ni wanne pekee hakukuwa na sababu ya kuendelea kuwa nao, hivyo atalifikisha suala hilo kwa Waziri mwenye dhamana ya madini ili kuangalia ni namna gani wachimbaji wadogo wataweza kupewa fursa hiyo ili waweze kujipatia kipato na kulipa kodi.

Akizungumza kuhusu uwezo wa nchi kujitegemea kimapato, Dkt. Kijaji alisema kuwa Tanzania imepunguza  utegemezi na kufikia asilimia 12, na kwamba  fursa nyingi za kimapato hazijatumika kikamilifu na kutoa wito kwa kila kiongozi na watumishi kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao ya kazi ili Taifa liweze kujitegemea zaidi.

 “Wanafalsafa mbalimbali wanasema Taifa lisilojitegemea kimapato ni watumwa, Taifa lisilojisimamia kwa mapato yake halijapata uhuru kamili kwa sababu mapato ndio moyo wa Taifa lolote na  mapato ya Taifa lolote ndio usalama wa Taifa hilo”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema Taifa likiwa imara kimapato hakuna yeyote atakae lichezea hasa likiwa limejiimarisha kwa mapato ya ndani,  kwa kuwa  mapato yanasababisha kuwa na uhuru wa kufikiri na kupanga mipango ya maendeleo bila kusubiri kupangiwa na watu wengine.

Naibu Waziri huyo alibainisha kuwa ni lazima kuhakikisha  mianya yote ya ukwepaji kodi inafungwa na  kuzuia matumizi yote yasiyo ya lazima ili kuzielekeza fedha hizo kwenye maeneo yenye maslahi mapana ya Taifa.

Alisema kodi zinazokusanywa, matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo umefikia asilimia 42 katika utekelezaji wake.

Aidha vijiji zaidi ya 3,500 vimewashwa umeme ndani ya miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Tano, Hospitali 67 kwenye halmashauri nchini zimeanza kujengwa na  Tanzania inaangaza Dunia baada ya kununua ndege zake kwa  mapato ya ndani kutokana na  kuiishi falsafa ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Amewataka viongozi wa Mkoa huo na watumishi wengine kuhakikisha wanatenda kile walichoamriwa katika nafasi zao kwa bidii na kuepukana na rushwa kwa kuwa Taifa litajengwa na wazalendo  na sio wenye meno.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Mchembe alieleza kuwa  ni vema kuwa na uhusiano mzuri kati ya Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji na mitaa ili kuwa na kanzi data hasa ya majengo ili kuhakikisha makusanyo yanaongezeka na lengo la Mkoa kukusanya Sh.  Bilioni 91 kwa mwaka linafikiwa.

Dkt. Kijaji anaendelea na ziara ya kukagua miradi iliyopewa fedha na Serikali ikiwemo ya Kimkakati Mkoani Morogoro iliyo na lengo za kuzisaidia Halmashauri kujitegemea kimapato

KATIBU MKUU CHAULA ATEMBELEA TAASISI YA JKCI

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwelezea Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya, Dkt. Zainab Chaula jinsi duka la dawa linavyohudumia wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto kutumia mtambo wa Cathlab wakati katibu mkuu huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiangalia moja ya chumba cha VIP kilichopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Kutoka kulia kwa Katibu mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.

Wafanyakazi wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi zao kwa umoja, kuwasaidia wahitaji na kuwatendea haki wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula alipokuwa akizungumza  na wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Chaula alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni ngumu na ni ibada hivyo basi kutokana na matendo mema watakayowatendea wagonjwa ambao ni wahitaji Mwenyezi Mungu atawalipa kwa  kuwajalia afya njema ili waweze kuwahudumia kwa miaka mingi zaidi.

“Nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya ya kuwahudumia wagonjwa  wenye matatizo ya moyo, kazi hii ni  ngumu jambo la muhimu ni kuwa na upendo  baina yenu na wagonjwa mnaowahudumia. Hakika Mwenyezi Mungu atawalipa kwa huduma yenu mnayoitoa”, alisisitiza Dkt. Chaula.

Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi hao kufanya kazi zao  kwa bidii, wakati  na kutimiza wajibu  wao kwani hakuna  kisichowezekana katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa vitu  vyote vipo ndani ya uwezo wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea Taasisi hiyo na kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa.

Prof. Janabi  alisema idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kutoa mfano wa wagonjwa wa nje 8557 waliotibiwa mwezi wa kwanza ukilinganisha na wagonjwa 7222 waliowaona mwezi wa Desemba mwaka jana.

Alisema   idadi ya wagonjwa wanaolazwa imeongezeka kutoka wagonjwa 282 kwa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana hadi kufikia 312 waliolazwa mwezi wa kwanza mwaka huu.

“Tunaona wagonjwa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ila wagonjwa wetu wengi zaidi wanatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Pemba,Katavi, Kigoma Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Unguja ”, alisema Prof. Janabi.

Onesheni uzalendo kwa kurejesha mikopo ya HESLB – RC Gambo

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) Dkt. Richard Masika tuzo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kufuatia AUWASA kuwa mmoja wa waajiri wanaotekeleza vizuri Sheria ya HESLB. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB) 
 Mwakilishi wa kiwanda cha vinywaji baridi cha Bonite cha mjini Moshi Frank Hamba akipokea tuzo ya utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gamba kufuatia kampuni hiyo kuwa moja ya taasisi zinazotekeleza vizuri sheria ya Bodi ya Mikopo. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo  (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB). 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimkabidhi tuzo ya utambuzi Mwakilishi wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) Moreen Mwaimale kufuatia mamlaka hiyo kuwa moja ya taasisi zinazotekeleza vizuri Sheria ya HESLB. Hafla hiyo imefanyika jijini Arusha leo (Jumatano, Feb., 27, 2019). (Picha na HESLB)


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kuonesha uzalendo kwa kujitokeza na kuanza kurejesha ili watanzania wengine wanufaike.

Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo leo (Jumatano, Feb. 27, 2019) jijini Arusha katika hafla fupi ya kukabidhi tuzo za utambuzi kwa waajiri 12 kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambao wanatekeleza vizuri sheria ya Bodi ya Mikopo.

Taasisi hizo kutoka mkoani Arusha ni World Vision Tanzania, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Kampuni ya Off-Grid Electric, Vision Fund Tanzania, Shule ya Mtakatifu Jude na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha ambazo kwa jumla zina wanufaika 410 wanaorejesha Tshs 74.08 milioni kwa mwezi.

Kwa mkoa wa Kilimanjaro, taasisi zilizopokea tuzo ni Mamlaka ya Uendelezaji wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KADCO), Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mwenge, Tanganyika Planting Company, Kampuni ya Vinywaji ya Bonite, Kampuni ya Marenga Investment na Benki ya Biashara ya Uchumi ambazo kwa ujumla zina wanufaika 142 wanaorejesha Tshs 23.8 milioni kwa mwezi.

“Lazima wajiulize, kama Bodi (ya mikopo) isingekuwepo, labda wasingeweza kusoma, na kama wasingesoma, wangekuwa wapi?” aliuliza Mkuu huyo wa mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi na kuongeza:

“Ili kuonesha uzalendo, wanapaswa kuwa ‘honest’ na kuwataarifu waajiri wao kuwa walinufaika na mikopo na kuanza kurejesha,” aliongeza katika hafla iliyohudhuriwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Mikopo Dkt. Richard Masika ambaye pia ni Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na majitaka Arusha.

Gambo aliwakumbusha waajiri waliopokea tuzo kuwa Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya fedha za mikopo ili kusomesha watanzania wengi ambao baada ya kuhitimu masomo huajiriwa na taasisi mbalimbali.

“Tangu kuingia madarakani mwaka 2015, Serikali ya Awamu Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, imeongeza bajeti ya fedha za mikopo kutoka TZS 322.4 bilioni mwaka 2014/2015 hadi kufikia TZS 427.5 bilioni mwaka wa masomo 2018/2019,” alisema na kuongeza kuwa idadi ya wanufaika nayo imeongezeka kutoka 100,937 hadi 124,000 katika kipindi hicho.

Awali akiongea katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru alisema katika mwaka wa fedha 2017/2018, Bodi ya Mikopo ilikusanya Tshs 181.4 bilioni, na kati ya hizo, Tshs 17.4 bilioni zilikusanywa kutoka kwa taasisi binafsi na umma kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.  

Aidha, Badru alieleza kuwa sheria ya HESLB imetoa wajibu wa aina nne kwa waajiri.

“Kwanza wanapaswa kuwasilisha kwa HESLB orodha ya waajiriwa wapya ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri. Pili, kukata asilimia 15 kutoka kwenye mshahara ghafi wa mnufaika na kuwasilisha kwa HESLB makato hayo ndani ya wiki mbili baada ya mwisho wa mwezi,” alisema Badru.

Mkurugenzi Mtendaji huyo aliongeza kuwa waajiri pia wanapaswa pia kutoa taarifa pale mnufaika anapoanza kazi, kufukuzwa au kufariki ili kuiwezesha Bodi ya Mikopo kuhuisha taarifa zake.
Kwa mujibu wa Badru, wajibu mwingine wa kisheria ni kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Bodi ya Mikopo wanapokuwa katika ziara za kikazi kwa waajiri ikiwemo kufanya kaguzi.

Bodi ya Mikopo ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa kitanzania wenye sifa za kujiunga na taasisi za elimu ya juu lakini hawana uwezo wa kiuchumi kumudu gharama hizo. Jukumu jingine ni kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika waliopata mikopo kutoka serikalini tangu mwaka 1994/1995.

UBUNGO WACHAMBUA BAJETI YAO YA FEDHA,WAJIPANGA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA KWA JAMII

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MEYA wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam Boniface Jacob  ametaja vipaumbele 11 vya halmashauri yai vilivyomo katika Bajeti ya fedha kwa mwaka 2019/2020 ambayo pamoja na mambo nengine imejikita kuboresha utoaji huduma kwa jamii kwa kuongeza fedha za kujengea Makao makuu ya Halmashauri kiasi cha Sh.millioni 700.

Pia bajeti hiyo inaonesha kuanza ujenzi wa kujenga Hospitali ya wilaya kwa kiasi cha sh.Millioni 250,pamoja na kutengwa fedha za kujenga machinjio ya kisasa kiasi cha sh.Millioni 250 pamoja fedha Sh.milioni 300 ambazo zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mbezi( kwa ajili ya wamachinga).

Akizungumza zaidi kuhusu makadirio ya fedha hizo za bajeti jana wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam ,Meya Jacob amefanunua kuwa  Serikali itatoa ruzuku ya Sh.Billioni 65.5, Sh.Millioni 750 ni michango ya Wananchi na Sh.billioni 18.4 ni makusanyo ya ndani.

Pia amesema Sh.,Billioni 72.3 ni Mishahara ya watumishi na Sh.billioni 12.3 zimeelekezwa katika miradi Mbalimbali ya Maendeleo.Aidha ameweka msisitizo kuwa Kiasi cha Sh.billioni 8.3 sawa na asilimia 60,za mapato yanayokusanywa na Halmashauri zitatumika kwa ajili ya Miradi ya maendeleo.

Jacob amezungumzia pia uimarishwaji wa Utawala bora kwa kuwatengea fedha za kiinua Mgongo ,wenyeviti wa Serikali za mitaa wanaomaliza muda wao mwaka 2019

"Kuongeza Mapato kwa kuboresha miundombinu ya ukusanyaji,kubuni vyanzo vipya,Uanzishaji wa stendi za daladala Mloganzila na Msumi,Uanzishwaji wa Masoko mapya Kiasi cha Sh.Billioni 1.7 zimetengwa

" Tumedhamiria kuongeza kiwango cha uzoaji taka Nlngumu kwa manispaa kwa kununua vifaa vya ubebaji taka kama magari na mitambo,Kiasi cha sh.billioni 3.02 kimetengwa,Ujenzi wa Mabweni ya Wavulana na Wasichana shule ya Sekondari Goba sh.Millioni 230 zimetengwa,"amesema.

 Akiizungumzia zaidi bajeti hiyo amesema halmashauri itatoa mikopo kwa Vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu ambapo Sh.billioni 1.38 zimetengwa. Pia kupima maeneo ya Umma,kwa kutoa hati miliki na kutwaa Maeneo ya miradi ya uwekezaji Sh.billioni 1.4 zimetengwa

Amesema bajeti hiyo itajikita pia kuboresha na kujenga niundombinu ya elimu msingi na Sekondari kwa kujenga madarasa na Nyumba za walimu, ambapo sh. billioni 1.168 zimetengwa kwa kazi hiyo.

Meya amesisitiza kuwa,Halmashauri ni chombo cha wananchi ambacho kimewekwa kisheria katika kukuza uchumi na kusogeza ajira kwa Vijana ili kupunguza Umasikini hasa wa kipato ili Kujiletea Maisha Bora.
 Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Mkori akizungumza na  Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo  waliofika  katika mkutano wa  baraza la Madiwani la kupitisha  Bajeti ya 2019/2020 leo jijini Dar es Salaam.
 Mstahiki Meya wa Halmashauri  Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob (kulia) akisoma hotuba yake  katika mkutano wa kupitisha bajeti ya mwa 2019-2020 leo jijini Dar es Salaam.(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Mkori
 Mkurugenzi wa wa Halmashauri ya Manispaa ya  Ubungo,Betrice (kulia) akizungumza  Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo  katika mkutano wa kupitisha bajeti ya Julai,2019-Juni,2020 leo jijini Dar es Salaam.
 .Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Boniface Jacob wakati wa mkutano  wa  baraza la Madiwani la kupitisha  Bajeti ya 2019/2020 leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Madiwani wa Halmashauri wilaya ya Bungo  waliofika katika mkutano wa  kupitisha  Bajeti ya 2019/2020 wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Kisare Makori.

T-PESA NA PBZ WASAINI KUSHIRIKIANA KIBIASHARA

$
0
0
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa kwanza kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar kati ya pande zote mbili. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (wa pili kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte (wa pili kulia) wakionesha nakala za mkataba wa makubaliano kufanya kazi kwa ushirikiano kibiashara leo mjini Zanzibar mara baada ya kutiliana saini. 
Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya kutiliana saini makubaliano ya kufanya kazi kiushirikiano kibiashara. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte akiwa katika hafla hiyo. 
Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa PBZ na TTCL (T PESA) walioshiriki katika hafla ya kuingia makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara. 


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kupitia kampuni yake tanzu ya T-PESA imesaini makubaliano ya kufanya kazi na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ambapo mawakala wa T-PESA watahudumiwa na benki hiyo.

Makubaliano hayo ya ushirikiano kibiashara kati ya PBZ na T-PESA yamefanyika leo mjini Zanzibar, ambapo Mkuu wa Huduma za T- PESA, Moses Alponce amesema yatawawezesha mawakala wao kupata huduma za kifedha kupitia PBZ.

Alisema T-PESA wanajivunia kufanikiwa katika ushirikiano huo kibiashara kwani utaiwezesha huduma zao kuenea kwa kasi zaidi, hasa ukizinga kuwa PBZ ni taasisi kubwa ya kifedha inayotoa huduma Zanzibar, Pemba na hata Tanzania Bara.

Miongoni mwa maeneo ambayo yamo katika mkataba wa ushirikiano huo kibiashara, mbali na PBZ kutoa huduma kwa mawakala wa T-PESA ya kutoa na kupokea fedha pia itakuwa ikitumia sehemu ya huduma za TTCL kama huduma za sauti na vifurushi, pamoja na huduma za simu.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bi Khadija Shamte alisema benki hiyo inamtawanyiko mkubwa wa matawi yake kuanzia mjini na vijijini huku wakiwa na uzoefu mkubwa katika kutoa huduma za fedha kupitia simu za viganjani.Kupitia mtawanyiko huo mkubwa kihuduma, tunapenda kuwahakikishia ushirikiano mzuri katika makubaliano hayo na jamii kwa ujumla watanufaika na kufurahia huduma zetu.

Aidha aliongeza kuwa Benki ya PBZ ni moja ya taasisi za fedha kongwe nchini Tanzania, ambayo inamilikiwa kwa asilimia 100 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). PBZ inalimiliki soko kwa takribani asilimia 50 huku ikiwa na wateja zaidi ya milioni 1.0.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images