Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

Walimu wa Kiswahili Kupata Ajira Sudan Kusini


AWILO LONGOMBA TOKA KUONGOZWA HADI KUMILIKI KUNDI LAKE

$
0
0
Awilo Longomba ni majina maarufu miongoni mwa wapenzi wa muziki wa dansi sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki na Kati. Unaweza kumfananisha kwa kiasi fulani na mwanamuziki Bileku Mpasi kufuatia historia zao katika muziki kushabihiana. Wakati Awilo alianza kupata umaarufu akiwa akicharaza drums katika bendi mbalimbali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Bileku alikuwa maarufu kwa ‘kurap’ pia umahiri wa kunengua katika bendi ya Empire Bakuba, chini ya Kabasele Yampanya ‘Pepe Kalle’

Hivi sasa wanamuziki hao wanamiliki bendi zao. Muziki wake umekuwa wa Kimataifa baada ya kulishirikisha wanamuziki wengine wakimataifa likiwemo kudi la PSqure toka nchini Nigeria. Awilo amekuwa kivutio kikubwa katika maonesho takriban yote kufuatia uwezo wake wa kuimba na kunengua pia uchangamfu wake jukwaani.

Wengi tumezoea kumuita Awilo Longomba, lakini majina yake halisi aliyopewa na wazazi wake baada ya kuzaliwa ni Albert William Longomba. Baba yake mzee Vicky Longomba alikuwa akitokea katika mkoa wa Mongo na mama yake Mkoa wa Ngombe huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Awilo anatalanta za kupiga drums, kutunga na kuimba nyimbo, aliyepata fursa ya kufanya kazi katika bendi kadhaa nchini humo zikiwemo za Stukas Mombombo Kayima, iliyokuwa ikiongozwa na Lita Bembo, Viva la Musica ya marehemu Papa Wemba, Loketo group iliyokuwa ikiongozwa na Aurlus Mabele, Nouvelle Generation pamoja na Bongo Wende.

Bendi yake ya mwisho kwake kuitumikia ilikuwa ya La Nouvelle Generation. Mnamo mwaka 1995 Awilo aliamua kuwa mwanamuziki wa kujitegemea ‘Solo artist’. Ili kuonesha kuwa yeye ni mkali katika muziki, alitoa albamu yake ya kwanza ya ‘Moto Pamba’ mwaka huohuo akiwa amejiongeza yeye mwenyewe kutunga na kuimba nyimbo zote pamoja na kupiga drums.

Albamu hiyo aliifyatua baada ya kupata msaada kutoka baadhi ya wanamuziki wakubwa akina Shimita El Diego, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko, Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star. Awilo katika albamu hiyo iliyopokelewa vilivyo na mashabiki wake, ilimtambulisha mkali huyo hadi kupelekea kupata mialiko lukuki ndani na nje ya nchi yake.

Albamu hiyo ya ‘Moto Pamba’ ilimpa tuzo ya kwanza ya kuwa mwanamuziki bora Afrika ya Kati zilizoandaliwa na Kora Music Awards zilizofanyika katika jiji la Sun City nchini Afrika ya Kusini mwaka 1996.

Mwaka 1998 alithibitisha kuwa hatanii, aliingia tena studio ambako alirekodi albamu yake ya pili iliyopewa majina ya Coupe Bibamba ikiwa na maudhui ya kuelezea hali ya umasikini katika nchi za Kiafrika.

Kwenye albamu hiyo baadhi ya nyimbo alimshrikisha mwanadada kutoka kundi la Cassav aitwae Jocelyne Berourd. Coupe Bibamba iliweza kumsafishia njia Awillo Longomba kupata mafanikio na ndoto zake kuzidi kutimia. Baadhi ya mafanikio yake yalidhihirika mnamo mwaka 2001 alipopata tena tuzo nyingine ya Kora Music Awards iliyoitwa ‘Judges Special Award’ kupitia albamu yake ya tatu Kafou Kafou.

Awillo mwenye machachari jukwaani, alitoka tena na albamu ya ‘Mondongo’ aliyoifyatua mwaka 2004. Katika albamu hiyo alifanikiwa kuwashirikisha  wanamuziki wengine wenye majina makubwa katika muziki nchini DRC, akina Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky Kiambukuta na Simaro Lutumba.

Awilo ni mwanamuziki anayejituma vilivyo katika kuandaa kazi za muziki hali iliyopelekea kupata mialiko mingi katika nchi nyingi Barani Afrika.
Baadhi ya nchi hizo ni Tanzania, Mali, Togo, Benin, Ivory Coast, Kenya, Burkina Faso, Nigeria na Cameroon. Aidha Awilo alivuka mipaka ya Bara la Afrika hadi nchi za Barani Ulaya zikiwemo za Uingereza, Ubelgiji, Switzerland, Ufaransa pamoja na bara la Amerika ikiwemo Canada.

Huko aliambatana na kundi la kitamaduni la kimataifa la kusakata au kucheza ngoma (Nabtry International Cultural Dancers). Kundi hilo lilikuwa la Kiafrika lililokuwa likicheza ngoma lililoanzishwa mwaka wa 2007 na Grace Haukwa. Ubunifu wake wa kurudia upya wimbo wa ‘Maze’ wa Tabu Ley Rochereau, alifanikiwa ‘kuwakamata’ wapenzi na mashabiki wake.

Kama Wahenga walivyotangulia kusema kuwa “Mtoto wa nyoka ni nyoka”. Awilo anatoka katika familia ya wanamuziki ikizingatia kwamba baba yake Victor Longomba ‘Vicky’, alikuwa katika sekta ya muziki akiwa mwanachama mwanzilishi wa bendi iliyokuwa kubwa nchini humo ya Tout Puissant OK. Jazz (TP OK. Jazz)  ya Franco Luanzo Makiadi.

Katika bendi hiyo Vicky Longomba alikuwa ni mwimbaji kiongozi wa bendi hiyo.Familia ya mzee Vicky Longomba ilikuwa ni ya wanamuziki zaidi. Ikumbukwe kuwa hata kaka yake Lovy Longomba ambaye ni marehemu, alitamba sana wakati akiwa katika bendi za Super Mazembe na Shika Shika katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

Baadaye Lovy Longomba akahamia nchini Tanzania ambapo alijiunga katika bendi ya African Sound Orchestra (Afriso Ngoma).Pia Lovy alikuwa baba wa familia yenye watoto wanamuziki akiwamo binti yake aliyerithi uimbaji aliyejulika kwa majina ya Elly Longomba.

Aidha alikuwa na watoto mapacha Christian na Lovy, ambao wote ni nyota katika muziki wa Hip-hop, wakimiliki Kampuni ya ‘Longambas’ ambalo ni maarufu la Afro-Fusion lenye makao katika jiji la Nairobi nchini Kenya.Maisha ya nguli Lovy Longomba yalikatishwa ghafla katika ajali ya gari iliyosababisha kifo chake katika ardhi ya Tanzania mwaka 1996.

Siri kubwa ya mafanikio ya Awilo Longomba katika muziki ni kitendo cha kushirikiana na wanamuziki wengine wakubwa. Mfano aliungana kupiga muziki na wanamuziki kama Kanda Bongoman, Oliver Ngoma, Tshala Muana na hata kundi la PSquare la nchini Nigeria.

Mnamo 2008 Awilo Longomba alitoa albamu mpya ya Super-Man, ambayo ilikuwa fanikio lingine kubwa. Kutokana na kura za umaarufu na ushindi wa kihistoria katika Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu huku nchi zaidi ya 120 zikipiga kura, albamu mpya ya Awilo, Super-Man, ilishinda tuzo la mtumbuizaji bora wa Soukous wa mwaka 2009.

Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Nabtry Grace Haukwa ambaye anamwakilisha Awilo nchini USA alikuwepo kupokea tuzo hilo kwa niaba ya Awilo katika sherehe ya Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu.

Awilo Longomba kwa sasa anaishi katika jiji la Paris nchini Ufaransa, akiwa na uhusiano wa karibu wa kimapenzi na mwanamuziki Barbara Kanam. Hivi karibuni Awilo ameachia wimbo mpya wa ‘Bundelele’,ambapo ameonekana kuwa karibu na wasanii wakubwa wa Nigeria. Lakini picha iliyowekwa na Peter Okoyo wa P-Square inaashiria neema zaidi kwa Longomba aliyepo nchini Nigeria kujitangaza zaidi

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI SHINYANGA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Edward K. Mulumba (kulia) wa Wizara ya Maji  yanayohusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Shinyanga (KASHWASA). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Picha ya Jengo la Madarasa ya Chuo cha Ualimu SHYCOM ambalo Makamu wa Rais alitembelea na kutaka kujua kwa nini ujenzi wake umesimama. Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa haamini macho yake kuona uchafu uliokithiri mara baada ya kutembelea jiko la kupikia chakula cha wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Taleck (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho John Nandi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM Happyness Kasuku akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) changamoto ya maktaba ya kusomea ambayo ni ndogo na ina vitabu vichache. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akkizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Wanafunzi Nchambi Nsile (kulia) anayesoma darasa la 7 akiwa amempakata mwenzake Nyazobe Sembe darasa la 4 wa Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wa kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo.
Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM) Mhe. Azza Hilal Hamad akiwa amempakata mmoja wa wanafunzi Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo. Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Jumuishi Buhangija (hawapo pichani) mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bi. Sharifa Salum (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bw. Dotto Ntumba (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

SERIKALI YA AWAMU YA TANO ITAENDELEA KULINDA NA KUKUZA HAKI ZA BINADAMU -PROF KABUDI

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu na ustawi wa jamii kama kipaumbele chake na  itaendelea kushirikiana na Baraza hilo kuhakikisha haki za binadamu nchini na duniani kote zinadumishwa.
Prof. Kabudi amesema hayo alipolihutubia Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika jijini Geneva nchini Uswisi. Prof. Kabudi amesema Serikali ya Tanzania imelenga pamoja na mambo mengine kuimarisha haki za binadamu, utawala bora na utii wa sheria nchini na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu. 
“Serikali imelenga kuimarisha haki za binadamu, utawala bora, utii wa sheria na kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, kwa sasa tunatekeleza mpango mkakati wa kitaifa wa kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa mwaka 2017/18 - 2021/22, lengo likiwa ni kulinda na kudumisha haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu,” alisema Prof. Kabudi.
Amesema Serikali pia inazingatia suala la kuwapatia haki kwa haraka wananchi wasio na uwezo kwa kutolea maamuzi kwa haraka mashauri yanayowahusu watu wasio na uwezo na kuwapatia msaada wa kisheria kupitia utekelezaji wa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 ili wananchi hao waweze kupata haki zao kwa wakati. 
Aidha, Prof. Kabudi amelihakikishia Baraza hilo kuwa Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya habari nchini na imeendelea kuhakikisha uhuru wa vyombo hivyo unalindwa huku jumla ya vituo vya redio 152, televisheni 34, magazeti 172  nchini kote yamesajiliwa na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira stahiki yatakayowezesha vyombo vya habari kufanya kazi zao kwa uhuru.
Ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuleta ustawi wa jamii kwa kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 na kunadi kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa haki ya kupata elimu, afya na maji zinawafikia wananchi wote. 
“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha kuwa haki ya kupata elimu, afya na maji zinawafikia wananchi wote na kuongeza kuwa Serikali inatumia zaidi ya Shilingi Bilioni 23 kwa mwezi kutoa elimu pasipo malipo na hivyo kuongeza udahili wa watoto wanaojiunga darasa la kwanza kwa asilimia 35.2 na asilimia 20.1 kwa wanaojiunga na kidato cha kwanza,” alisema. 
Prof. Kabudi pia amesema Serikali imedhamiria kufikisha huduma za afya karibu na watanzania wote ambapo imeongeza bajeti ya afya kutoka Shilingi bilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi Shilingi bilioni 269 mwaka 2017/2018 na kuongeza kuwa Serikali inatekeleza mikakati ya kujenga vituo vya afya ambapo hadi sasa imejenga vituo 304, na nyumba za watumishi wa afya 578 zimejengwa nchini kote.
Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ni chombo cha Umoja wa Mataifa chenye jukumu la kukuza na kulinda haki za binadamu duniani kote na kushughulikia uvunjwaji wa haki za binadamu unaotokea katika nchi wanachama wa umoja huo na kushauri hatua za kuchukuliwa ili kuboresha haki za binadamu duniani. 
Baraza hilo pamoja na mambo mengine linatarajia kupokea taarifa mbalimbali kuhusu haki za binadamu duniani na kutoa nafasi kwa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa maelezo yao kuhusu utekeelezaji wa wajibu wao wa kulinda na kukuza haki za biandamu katika nchi zao.

KIFO CHA RUGE MUTAHABA NI PIGO KWA SERIKALI-WAZIRI MKUU

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kifo cha mmoja wa waasisi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ni pigo kubwa kwa Serikali kwani enzi za uhai wake ametoa mchango mkubwa kuhakikisha maono ya viongozi yanapata fursa ya kutekelezwa kwa vitendo.

Majaliwa amesema hayo leo Februari 27 , nyumbani kwa wazazi wake Ruge jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za Serikali kutokana na kifo hicho ambapo amesema ni pigo kwa familia na zaidi ni pigo kwa Serikali. "Nimekuja hapa nyumbani kutoa salamu za pole kwa wazazi, familia, watoto, ndugu, jamii, marafiki na Watanzania wote kwa kuondokewa na Ruge Mutahaba.Kifo chake ni pigo kubwa kwa Serikali kwa nyakati tofauti tulikuwa tunashirikiana naye.Alikuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana kuipenda nchi yao kwa vitendo.

"Ruge alitumia akili na aina ya maarifa yake kwa ajili ya kusaidia wengine, aliwahimiza vijana kufanya kazi kwa bidii. Alisisimama imara kufanikisha falsafa za viongozi wakuu wa nchini kuanzia Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete na Rais wetu Dk.John Magufuli kuhakikisha vijana wanatumia fursa zilizopo nchini kufanya maendeleo. Tunaamini Ruge alikuwa ni kiongozi wa vijana wengine nchini,"amesema Waziri Mkuu.

Amefafanua kwamba wakati wote na kwa nyakati tofauti Watanzania walikuwa wakimuombea ili Ruge apate nafuu lakini ukweli leo hii hatunaye tena na kubwa zaidi ni kuendelea kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ampe pumziko la milele.

"Nirudie tena kifo cha Ruge ni pigo kubwa , alitumia fedha na mali zake kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na amefanya mambo makubwa sana na ameshiriki kwa vitendo katika harakati za maendeleo ndani ya nchi yetu.Ruge amezunguka nchi nzima kupitia kampeni mbalimbali kuelezea umuhimu wa vijana kutambua nchi yao na kuwajengea uelewa wa kufanya mambo makubwa, "amesema Waziri Mkuu. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi 'ubani wa msiba' Baba wa Marehemu Prof Mutahaba,alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia baadhi ya viongozi waliofika kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam. 
 WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga ,alipokwenda alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
 


TGNP MTANDAO KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KINGONO KWA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
* Serikali yahaidi ushirikiano, yaasa wanajamii kushiriki katika kuwalinda watoto

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo cha unyanyaji wa kingono hasa kwa watoto na wanawake huku Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa ikionekana kuongoza kwa vitendo hivyo,mtandao wa ujinsia nchini TGNP umezindua rasmi kampeni ya kupinga vitendo hivyo na kuhimiza kuwa watoto wote wana haki ya  kulindwa dhidi ya vitendo hivyo.

Akizindua kampeni hiyo Kaimu mkuu wa jeshi la Polisi na Mkuu wa dawati la jinsia nchini DCP Mary Nziku amesema kuwa kampeni hiyo ni ya nchi nzima na kila mmoja kwa nafasi yake awajibike katika kuwalinda watoto  dhidi ya vitendo hivyo hasa kwa wanaotendewa kutoa taarifa panapohusika na anayetenda makosa hayo achukuliwe hatua kali za kisheria.

Aidha amesema kuwa kuna madawati 420 ya jinsia nchini yanayotoa huduma pamoja na askari wenye mafunzo na serikali imechukua  hatua kadhaa ikiwemo kuwepo kwa huduma ya mkono kwa mkono katika hospitali ambapo muathirika wa vitendo hivyo hupata huduma zote kisheria na afya katika hospitali na kuwepo kwa ofisi ya ulinzi katika kata kote nchini.

Pia amewaasa wazazi kuzungumza na watoto wao na kuwakagua kwa kuwa vitendo hivyo hufanywa na watu wa karibu wakiwemo baba, wajomba na ndugu wa karibu zaidi. Vilevile amesema kuwa watakaotenda makosa hayo hatua kali za kisheria zitawachukuliwa mara moja na katika hilo hakuna ridhaa, kama mtoto alikubali ila yupo chini ya miaka 18 kosa hilo ni la ubakaji.

Pia amewaomba viongozi wa dini kushirikiana na Serikali na taasisi kama TGNP kwa kuweka ajenda ya mahubiri ya watoto ili kujenga uelewa na kuweza kujenga taifa ambalo halina maumivu. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa TGNP Lilian Liundi amesema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwakomboa watoto na wanawake dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono na kujenga taifa lisilo la makovu.

Lilian amesema kuwa viongozi wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wamekuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vya unyanyasaji wa kingono na amewataka viongozi wengine kutumia vyema majukwaa katika kukemea vitendo hivyo vya kiudhalilishaji hasa mimba za utotoni na vitendo vya ulawiti.

Na amewataka wanajamii kushirikiana katika kampeni hiyo ambayo itaokoa maisha ya watoto wengi na kujenga taifa bora zaidi. 

Mkurugenzi mtendaji wa mtandao wa jinsia nchini TGNP Lilian Liundi akizungumza wakati uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupinga ukatili dhidi ya vitendo vya kingono kwa wanawake na watoto na amewataka wanajamii kushiriki katika kampeni hiyo ili kujenga taifa bora leo jijini Dar es salaam.
 Kaimu  Mkuu wa jeshi la polisi na Mkuu wa dawati la Jinsia nchini DCP Mary Nziku akizungumza wakati uzinduzi wa kampeni hiyo ya kupinga ukatili dhidi ya vitendo vya kingono kwa wanawake na watoto leo jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi na wazazi wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali zinazopinga vitendo vya ukatili katika uzinduzi wa kampeni ya kupinga vitendo vya ukatili wa kingono leo kwa wanawake na watoto leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa kampeni hiyo wakiwa katika kampeni hiyo ambayo imelenga kufika nchi nzima na kukomesha vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto leo jijini Dar es Salaam.

RUGE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUWASAIDIA VIJANA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao na watambue fursa za maendeleo zilizopo na wasiwe walalamikaji.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 27, alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema vijana nchini walikuwa na kiongozi aliyekuwa akiwaongoza kwa kuwafungua kimawazo na kuwaonesha fursa mbalimbali zitakazowawezesha kuwakwamua kifikra na kiuchumi ili waweze kujitegemea.

Waziri Mkuu amesema msiba huo ni wa wote kwani marehemu amefanya kazi kubwa ya kushirikiana na Serikali kuhamasisha vijana kujitambua na kutambua fursa zilizpo na kuzifanyia kazi. “Ruge ametoa mchango mkubwa kwa Taifa

Amesema marehemu Ruge katika kipindi cha uhai wake amefanya kazi kubwa kwa upande wa Serikali, kuanzia awamu ya nne hadi ya tano hususani katika suala la kuhamasisha vijana kujikwamua na kutokuwa wategemezi.

Pia, Waziri Mkuu amesema historia yake inaeleza namna alivyozunguka nchi nzima na kukutana na makundi ya vijana mbalimbali na kuwaelimisha namna ya kutambua fursa zilizopo nchini huku akiwahamasisha wawe wazalendo.

"Marehemu alikuwa akitoa hadi fedha zake binafsi kwa ajili ya kuwawezesha vijana hasa wale ambao hawakuwa na uwezo wa kiuchumi ili nao washiriki katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali na hatimaye waondokane na utegemezi.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametoa wito kwa wazazi, watoto wa marehemu pamoja na wananchi kwa ujumla waendelee kuwa na subira na watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao. 


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 27, 2019.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

FAMILIA YATOA RATIBA MSIBA WA RUGE, MWILI KUWASILI IJUMAA, KUAGWA JUMAMOSI DAR

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

FAMILIA ya Ruge Mutahaba imetoa utaratibu wa mazishi ya ndugu yao, ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo mkoani Kagera.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam ,Msemaji wa familia ya Ruge, aliyejitambulisha kwa jina la  Kashasha amesema mipango iliyopangwa na familia ni kuhakikisha wanaufikisha mwili wa Ruge Dar es Salaam siku ya Ijumaa na kuagwa Jumamosi katika ukumbi wa Karimjee.

"Familia imeamua kwamba mwili wa ndugu yetu Ruge utapumzishwa nyumbani mkoani Bukoba siku ya Jumatatu.Siku hiyo ndio tutampumzisha katika nyumba yake ya milele,"amesema.

Ruge Mutahaba  aliyezaliwa mwaka 1970, ni mmoja wa waasisi na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group amefariki dunia jana jioni Februari 26 akiwa Afrika Kusini ambako alikuwa anapatiwa matibabu.


ikumbukwe kuwa Ruge ni mmoja wa waanzilishi na waasisi wa Clouds Media.


FIFA KUMFUNGIA MAISHA ODEN MBAGA KUTOJIHUSISHA NA MASUALA YA MPIRA WA MIGUU.

$
0
0

Na Agness Francis, blogu ya Jamii. 

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) chini ya Mwenyekiti wake Vassilios Skouris imemfungia maisha Mwamuzi wa zamani wa Kimataifa ambaye pia ni Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Oden Charles Mbaga,  kwa kujihusisha na masuala ya rushwa kwa  kupanga matokeo.

Baada ya uchunguzi uliofanyika kuanzia July 11,2018 Mbaga amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye upangaji wa matokeo ikiwa ni kinyume na kanuni za maadili za FIFA. 

Afisa Habari na Mawasiliano Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)  Cliford Ndimbo amesema kuwa muamuzi huyo amevunja Ibara ya 11 ya Kanuni ya rushwa ya FIFA ya mwaka 2009,kinachompelekea kufungiwa maisha kutojihusisha na shughuli zozote za Mpira wa Miguu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 7j ya Kanuni za Maadili za FIFA za mwaka 2018 pamoja na Ibara ya 22 ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA.

Aidha Mbaga anatakiwa kulipa faini ya kiasi cha fedha ya Uswis Faranga 200,000 ndani ya siku 30 tokea amepata taarifa hizo ambapo pia  anaweza kulipa kwa fedha ya Swiss au kwa dola za Kimarekani. 

Vile vile anatakiwa kulipa gharama za shauri hilo kiasi cha Faranga za KiSwiss 1,000 ndani ya siku 30 tokea amepata taarifa.

Mbaga anaweza kukata rufaa kwenye mahakama ya kimichezo ya FIFA CAS,rufaa ambayo inawasilishwa moja kwa moja CAS ndani ya siku 21 tokea maamuzi yalipofanyika na ndani ya siku 10 baada ya kumalizika siku 21.

"Kutokana na makosa yake Mbaga ambaye ni Katibu wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT) anapoteza sifa ya nafasi hiyo kutokana na adhabu ya kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya Mpira wa Miguu"amesema Ndimbo.

MWIGULU ASEMA RUGE AMEACHA ALAMA, MAISHA YAKE NI KITABU

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii 

RUGE Mutahaba ni kielezo cha mfano na ameacha alama!Ndivyo Mbunge Mwigulu Nchemba anavyomuelezea Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ambaye amefariki dunia jana nchini Afrika Kusini. 

Mwigulu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anaelezea kusikitishwa kwake na kifo cha Ruge Mutahaba ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa pamoja na kwamba Ruge ametanguliwa mbele ya haki lakini ameacha alama kutokana na mambo ambayo ameyafanya kwa ajili ya nchi yetu. 

"Nilikutana na Ruge kwa mara ya kwanza baada ya mimi kuteuliwa na Chama changu cha CCM kuwa mweka Hazina.Tulioonana tulizungumza mengi na alinipa ushauri ambao hakika ulinisaidia katika kufanya kazi zangu ndani ya Chama.Alikuwa akisaidia vijana kutimiza ndoto zao, aliamsha fikra za watu waliolala,"amesema. 

Ameongeza kwa kazi nzuri ambayo ameifanya Ruge kwa ajili ya nchi yake itabaki kuwa kilelezo cha kijana bora na mzalendo kwa Taifa letu."Maisha ya Ruge ni kitabu kutokana na aina ya maisha ambayo ameyaishi.Nachoweza kusema amethibitisha kuwa kuishi muda mrefu sio kipimo cha mafanikio kwani Ruge ameishi muda mfupi lakini amefanya mambo makubwa yenye mafanikio ya hali ya juu." 

Ametumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wazazi, familia, Kampuni ya Clouds Media Group kutokana na msiba wa Ruge na kuongeza kuwa kauli yake ya kwamba akifa watu washerehekee inaonesha ni kwa namna gani ambavyo alijua anayoyafanya yabaki ya kukumbwa na Watanzania wengi hasa kwa kuzingatia vijana wengi wamepita kwenye mikono yake. 

Wakati huo huo, viongozi wa ngazi mbalimbali na wananchi wamefika nyumbani kwa wazazi wake Ruge Mutahaba ili kutoa pole ambapo idadi kubwa ya watu wamefika nyumbani hapo. Wakizungumzia Ruge Mutahaba baadhi ya wananchi waliofika msibani hapo wamesema kifo chake kimeacha pigo kubwa kwani enzi za uhai wake alijitoa kimaisha kusaidia wengine.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge Mwigulu Nchemba alipokwenda kuhani msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba kwa niaba ya Serikali, nyumbani kwa wazazi wa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

MKUTANO WA 11 WA KUTATHMINI SEKTA YA AFYA WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Jamala Adam Taibu akizungumza katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Muakilishi wa W,H,O Zanzibar Dkt,Ghirmany Andermichael akizungumza katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Katibu Mkuu Wizara ya  Afya Asha Ali Abdalla akitoahotuba yake katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa hotuba ya ufunguzi katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua  Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud katikati akiwa na Naibu Waziri Wizara ya Afya Harusi Saidi Suleiman(kushoto yake)na Viongozi mbalimbali katika Picha ya pamoja katika hafla ya Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Jamala Adam Taibu akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Ufunguzi wa Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
 Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Afya waliohudhuria katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.
Mtaalamu wa masuala ya Afya ya Uzazi kutoka shirika la UNFPA Zanzibar Batula Abdi akitoa mchango wake katika Mkutano wa 11 wa kutathmini Sekta ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Verde Hotel mjini Unguja.

PICHA Na YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

KATIBU MKUU CHAULA ATEMBELEA TAASISI YA JKCI

$
0
0
Wafanyakazi wa Taasisis ya Moyo Jakaya Kikwete wametakiwa kufanya kazi zao kwa umoja, kuwasaidia wahitaji na kuwatendea haki wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula alipokuwa akizungumza  na wafanyakazi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Chaula alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni ngumu na ni ibada hivyo basi kutokana na matendo mema watakayowatendea wagonjwa ambao ni wahitaji Mwenyezi Mungu atawalipa kwa  kuwajalia afya njema ili waweze kuwahudumia kwa miaka mingi zaidi.

“Nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya ya kuwahudumia wagonjwa  wenye matatizo ya moyo, kazi hii ni  ngumu jambo la muhimu ni kuwa na upendo  baina yenu na wagonjwa mnaowahudumia. Hakika Mwenyezi Mungu atawalipa kwa huduma yenu mnayoitoa”, alisisitiza Dkt. Chaula.

Alimalizia kwa kuwataka wafanyakazi hao kufanya kazi zao  kwa bidii, wakati  na kutimiza wajibu  wao kwani hakuna  kisichowezekana katika kutoa huduma bora kwa wagonjwa vitu  vyote vipo ndani ya uwezo wao.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi alimshukuru Katibu Mkuu huyo kwa kutembelea Taasisi hiyo na kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa.

Prof. Janabi  alisema idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku na kutoa mfano wa wagonjwa wa nje 8557 waliotibiwa mwezi wa kwanza ukilinganisha na wagonjwa 7222 waliowaona mwezi wa Desemba mwaka jana.

Alisema   idadi ya wagonjwa wanaolazwa imeongezeka kutoka wagonjwa 282 kwa mwezi wa kumi na mbili mwaka jana hadi kufikia 312 waliolazwa mwezi wa kwanza mwaka huu.

“Tunaona wagonjwa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani ila wagonjwa wetu wengi zaidi wanatoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mbeya, Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Pemba,Katavi, Kigoma Kilimanjaro, Lindi, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Unguja ”, alisema Prof. Janabi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwelezea Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya, Dkt. Zainab Chaula jinsi duka la dawa linavyohudumia wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. 
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godfrey Mbawala akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua kwa watoto kutumia mtambo wa Cathlab wakati katibu mkuu huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Idara kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiangalia moja ya chumba cha VIP kilichopo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa. Kutoka kulia kwa Katibu mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.

WAMILIKI WA LESENI ZA UCHIMBAJI MADINI ZISIZOTUMIKA MKOANI MOROGORO WAKALIA KUTI KAVU

$
0
0
Na Peter Haule, WFM, Morogoro
Serikali imeahidi kulifanyiakazi suala la Leseni mfu za uchimbaji madini mkoani Morogoro, ili kutoa fursa ya wachimbaji wadogo  kuchimba madini hayo na kulipa kodi stahiki kwa manufaa mapana ya Taifa. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipofanya Mkutano na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoani Morogoro na wadau wengine.

Maelekezo hayo yanafuatia maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe, ambaye pamoja na kuishukuru Serikali kwa  kutoa fedha zenye lengo la kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato na akaiomba Serikali kuhakikisha inafuta Leseni mfu za wachimba madini takribani 174 ambao wanazuia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za kujipatia kipato kutokana na  madini na kulipa kodi.

Dkt. Kabwe alimweleza Dkt. Kijaji kwamba mkoa wa Morogoro umesheheni madini ya kila aina na jambo linalosababisha ukosefu wa mapato unachangiwa pia na  utoroshaji wa madini ambapo ameeleza kuwa mikakati ya Mkoa huo ni kuanzisha Soko la Madini mkoani humo ili kuepusha utoroshaji huo.

Dkt. Kijaji alisema kuwa kama wapo watu wenye Leseni za uchimbaji madini 178 na wanaolipa kodi ni wanne pekee hakukuwa na sababu ya kuendelea kuwa nao, hivyo atalifikisha suala hilo kwa Waziri mwenye dhamana ya madini ili kuangalia ni namna gani wachimbaji wadogo wataweza kupewa fursa hiyo ili waweze kujipatia kipato na kulipa kodi.

Akizungumza kuhusu uwezo wa nchi kujitegemea kimapato, Dkt. Kijaji alisema kuwa Tanzania imepunguza  utegemezi na kufikia asilimia 12, na kwamba  fursa nyingi za kimapato hazijatumika kikamilifu na kutoa wito kwa kila kiongozi na watumishi kuwajibika kikamilifu katika maeneo yao ya kazi ili Taifa liweze kujitegemea zaidi.

 “Wanafalsafa mbalimbali wanasema Taifa lisilojitegemea kimapato ni watumwa, Taifa lisilojisimamia kwa mapato yake halijapata uhuru kamili kwa sababu mapato ndio moyo wa Taifa lolote na  mapato ya Taifa lolote ndio usalama wa Taifa hilo”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema Taifa likiwa imara kimapato hakuna yeyote atakae lichezea hasa likiwa limejiimarisha kwa mapato ya ndani,  kwa kuwa  mapato yanasababisha kuwa na uhuru wa kufikiri na kupanga mipango ya maendeleo bila kusubiri kupangiwa na watu wengine.

Naibu Waziri huyo alibainisha kuwa ni lazima kuhakikisha  mianya yote ya ukwepaji kodi inafungwa na  kuzuia matumizi yote yasiyo ya lazima ili kuzielekeza fedha hizo kwenye maeneo yenye maslahi mapana ya Taifa.

Alisema kodi zinazokusanywa, matokeo yake yanaonekana ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ambapo umefikia asilimia 42 katika utekelezaji wake.

Aidha vijiji zaidi ya 3,500 vimewashwa umeme ndani ya miaka miwili ya uongozi wa awamu ya Tano, Hospitali 67 kwenye halmashauri nchini zimeanza kujengwa na  Tanzania inaangaza Dunia baada ya kununua ndege zake kwa  mapato ya ndani kutokana na  kuiishi falsafa ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Amewataka viongozi wa Mkoa huo na watumishi wengine kuhakikisha wanatenda kile walichoamriwa katika nafasi zao kwa bidii na kuepukana na rushwa kwa kuwa Taifa litajengwa na wazalendo  na sio wenye meno.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Mchembe alieleza kuwa  ni vema kuwa na uhusiano mzuri kati ya Uongozi wa Mkoa, Wilaya na Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji na mitaa ili kuwa na kanzi data hasa ya majengo ili kuhakikisha makusanyo yanaongezeka na lengo la Mkoa kukusanya Sh.  Bilioni 91 kwa mwaka linafikiwa.

Dkt. Kijaji anaendelea na ziara ya kukagua miradi iliyopewa fedha na Serikali ikiwemo ya Kimkakati Mkoani Morogoro iliyo na lengo za kuzisaidia Halmashauri kujitegemea kimapato

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akitoa maelekezo kwa wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kupata idadi ya nyumba zinazotakiwa kulipiwa kodi ya Majengo, wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri huyo na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro, kushoto ni Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Morogoro Bw. Emmanuel Maro.

Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya katika Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maagizizo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) kuhusu andiko la miradi ya kimkakati itakayosaidia halmashauri zao kujitegemea kimapato.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Clifford Tandari, akiwataka Wakurugenzi kuwajibika ili kuwaletea wananchi maendeleo stahiki wakati wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bw. Mohamed Utaly na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Bw. Adam Mgoyi, wakizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa TRA, Mkoani Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Mchembe, akiitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kushirikiana na uongozi wa Wilaya ili kufanikisha lengo la makusanyo ya Kodi zinazopangwa katika ngazi ya Wilaya hadi Mkoa.

VIGOGO WATATU WA RAHCO KUSOMEWA MAELEZO YA AWALI MWEZI UJAO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepanga kuwasomea maelezo ya awali (PH), Machi 3, 2019 vigogo watatu wa kampuni Hodhi ya mali za Reli, (Rahaco).

Hatua hiyo imefikwa leo Februari 27.2019 baada ya upande wa mashtaka mara ya mwisho kuitaarifu mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umeishakamilika na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuipatia mamlaka mahakama hiyo ya Kisutu kusikiliza kesi hiyo.

katika kesi hiyo, watuhumiwa wanakailiwa na mashtaka nane ya uhujumu uchumi likiwemo shtaka la kuisababishia Serikali hasara ya USD 527,540.

Mapema wakili wa Serikali, Maghela Ndimbo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba, alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilka hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya usikilizwaji wa awali. hata hivyo, kabla ya kesi hiyo kuahirishwa washtakiwa walisomea upya mashtaka yao ambapo wote kwa pamoja walikana kutenda makosa hayo.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito, Mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wadaiwa kati ya Septemba Mosi, 2014 na Septemba 30, 2015 kwa nia ya kutenda kosa walikula njama kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Tito, anadaiwa kuwa Februari 27, 2015 katika ofisi za Rahco zilizopo Ilala alitumia madaraka yake vibaya kwa kuiajiri Kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Ltd kama mshauri wa mradi wa uimarishaji wa reli ya kati, bila idhini ya Bodi ya Rahco.

WAZIRI MKUU ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU RUGE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  na mkewe Mary (wa pili kulia) wakimfariji mama Mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba, Christiana Mutahaba wakati  walipokwenda nyumbani kwao  marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia ,  Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba wakati alipokwanda nyumbani kwao marehemu, Mikocheni jijini Dar es salaam  kutoa pole kwa familia, Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe wakati alipokwenda nyumbani kwao marehemu Ruge Mutahaba, Mikocheni jijini Dar es salaam kutoa pole kwa familia , Februari 27, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Benki ya CRDB yakanusha kufunga tawi lake la Chato

$
0
0
Benki ya CRDB imekanusha taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa imefunga tawi lake la Chato kutokana na kukosa biashara. 

Akizungumza na Globu ya Jamii jioni hii, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa amesema kuwa taarifa hizo si za ukweli kwani tawi hilo linaendelea vyema na biashara na ni moja ya matawi yaliyofanya vizuri zaidi katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita.

 "Tumeshangazwa sana na taarifa hizi kwani hata ukiangalia taarifa yenyewe haina ubora unaoendana na taaluma yetu. Mimi ndiye mhusika mkuu wa kutoa matangazo yote kwenye magazeti na vyombo vyote vya habari, Naomba kusema kuwa silitambui tangazo hilo”.

Aliendelea kusema “Nichukue fursa hii kuwatangazia wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa Benki ya CRDB haijafunya na wala haina mpango wa kufunga tawi lolote nchini" kiukweli, benki ya CRDB iko katika mkakati kabambe wa kutanua wigo wa utoaji huduma zake kwa kutumia ubunifu na teknolojia ili kuwafikia watanzania wengi vijijini kupitia uwakala. Mwaka huu tunataka kuongeza mawakala zaidi ya 10,000”. alisema Bi. Mwambapa

LORI LAPIGA MWELEKA

$
0
0


Lori lililokuwa likitoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoa wa Pwani limepiga mweleka na kuingia mtaroni katika barabara ya Morogoro eneo la Kibamba wilaya ya Ubungo jijini Dar as Salaam leo, chanzo cha ajali hiyo inadaiwa gari ilishindwa kupanda katika mlima wenye mwinuko mkali (picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii).
Baadhai ya wakazi wa eneo hilo wakipita pembeni ya lori hilo lililo piga mweleka na kuingia mtaroni barabara ya Morogoro eneo la Kibamba wilaya ya Ubungo jijini Dar as Salaam leo, chanzo cha ajali hiyo gari  inaelezwa gari ilishindwa kupanda mlima wenye mwinuko mkali.

KAMATI YA AMANI YA MKOA WA DAR ES SALAAM YAMTEMBELEA KATIBU WA BUNGE OFISINI KWAKE

$
0
0

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai (Kulia) akimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma. Waziri Dkt. Mwakyembe aliongozana na Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salim na Katibu wa Kamati hiyo Mchungaji Jackson Sosthenes. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai (Kulia) akimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akifurahi jambo na wageni wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salim na Katibu wa Kamati hiyo Mchungaji Jackson Sosthenes walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma. 
Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harison Mwakyembe, Mwenyekiti wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salim na Katibu wa Kamati hiyo Mchungaji Jackson Sosthenes walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma. 
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Maafisa Utamaduni Waagizwa Kusimamia na Kutekeleza Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) katika Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. Wa Kwanza Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi.Susan Mlawi na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bw.Boniface Kadili. 

Na.Shamimu Nyaki -WHUSM 

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amewaagiza Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia na kutekeleza Sera ya Utamaduni ya Mwaka 1997 kwakua ni ndio muongozo wa kukuza na kuendeleza Utamaduni wa Nchi yetu. 

Mhe. Waziri ameyasema hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha 11 cha Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kilichoandaliwa na Wizara yake ambapo amesema kuwa Kikao kazi hicho kitasaidia kuibua changamoto na kutafuta namna ya kuzikabili pamoja na kubuni fursa zilizopo katika Sekta hiyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akizungumza na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini (hawapo katika picha) katika Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Boniface Kadili akizungumza katika Kikao Kazi cha 11 cha Maafisa Utamaduni chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 

“Naamini kikao kazi hiki kitatoka na maadhimio mazuri yanayoelezea namna bora ya kuondoa mmomonyoko wa maadili unaotokana na kudharau, kupuuza na kudidimiza mila na desturi za nchi yetu na kufuata tamaduni za nje zisizofaa.” Amesema Dkt Mwakyembe. 

Aidha Mhe. Mwakyembe amewataka maafisa Utamaduni hao kutumia falsafa ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere inayosema, “Utamaduni ni kielelezo cha uhai na Utashi wa Taifa lolote lile, hivyo Taifa lisilo na Utamaduni ni Taifa mfu”. Hivyo amewataka Maafisa hao kutumia taaluma yao kuwahimiza Watanzania kujivunia Utamaduni wetu. 

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Susan Mlawi ameeleza kuwa kikao hicho kitakumbusha Maafisa Utamaduni kujadili mambo mbalimbali ya msingi, kubaini fursa pamoja na kuweka maazimio yatakayosaidia kuendeleza Utamaduni wa nchi yetu. 
Baadhi ya Maaafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini wakiwa katika Kikao kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo chenye chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Viongozi wa Wizara yake na Maafisa Utamaduni wa Mikoa na Halmashauri zote nchini baada ya kufungua Kikao Kazi cha 11 kilichoandaliwa na Wizara yake chenye lengo la kujadili changamoto na fursa zilizopo katika Sekta hiyo kinachoongozwa na Kauli Mbiu “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu”Kinachofanyika leo na kesho Jijini Dodoma. 

Kikao kazi hicho kinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Umoja Upendo na Kazi Asili ya Utamaduni wetu” 

Mbali na hayo Waziri, Dkt.Mwakyembe ametoa salamu za pole kwa Uongozi na Wafanyakazi wa Clouds Media Group, ndugu jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Muanzilishi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba ambaye alifariki jana Nchini Afrika Kusini. 

Katika hatua nyingine Mhe.Waziri Mwakyembe ameliagiza Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini kumchukilia hatua za kinidhamu Msanii wa muziki wa kizazi kipya Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya kutokana na maneno aliyoyatoa ya kumdhihaki marehemu Ruge Mutahaba aliyekuwa Muanzilishi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi Clouds Media Group ambaye alifariki jana Nchini Afrika Kusini

Ruge, naomba nisikilize kidogo.

$
0
0


Ruge Mutahaba enzi za uhai wake

Na January Makamba

Ndugu yangu Ruge, najua ndio umewasili huko upande wa pili na si ajabu una mambo mengi na bado unasalimiana na jamaa zetu wengi waliotangulia. Lakini naomba uchukue muda wako kidogo kunisikiliza. Nimeumia sana na nimelia peke yangu kwamba umetuacha namna hii. Sawa, umeitwa kwa wakati wako na sisi hatuna kauli kwenye suala la wakati wa kuitwa lakini nilitegemea, na sikuwa na shaka kabisa, kwamba tutakamilisha yale mawazo yako mengi mazuri uliyoniambia.

Sikuwa na shaka kwasababu nilishuhudia pale Hospitali ya Kairuki kabla hujaenda India, ulivyorudi kutoka India, na siku nimekuona Afrika Kusini, ulivyokuwa unapigana kupona -  hadi madaktari wa Afrika Kusini wakakupa jina “Ruge, The Fighter”. Jina sahihi kabisa lililotafsiri harakati za maisha yako.  

Unajua nini? Nilikuwa nangoja urudi Dar nikwambie nilichogundua mara ya mwisho nilivyokuona hospitali. Lakini ngoja tu nikwambie kabla sijaja huko uliko. Ile kiu kubwa ya kupona niliyoiona kwenye macho yako haikuwa kwa ajili yako wewe, bali kwa ajili ya kutoiangusha familia yako nzima iliyosimamisha kila kitu kukuuguza na Watanzania wote waliokuwa wanakuombea. Ulipigana kupona, sio kwa ajili yako, bali kwa ajili yetu. Hukuamka kitandani lakini hukushindwa mapambano kwasababu umeamkia ndani ya mioyo ya Watanzania. 

Huku tuliko karibu watu wote tunakumbuka ulivyotugusa. Jamaa yangu, tunakuomboleza wakati huu, halafu tutabaki tunafurahia nuru yako katika maisha ya wengi kwa urefu wa uhai wetu. Umekimbia mbio njema, umemaliza safari yako vyema.

Majonzi yangu ni kwamba umeondoka kabla sijalipa kwa ukamilifu deni langu kwako. Deni la upendo na urafiki wa kweli. Ulinipa heshima kubwa ya kuwa msiri wako – kwa kuniamini na kunielezea wasiwasi wako, ndoto zako, matumaini yako, harakati zako, mipango yako. Ulinipa heshima ya kunipa fursa ya kubishana nawe kuhusu mawazo na fikra zako.

Majonzi yangu ni kwamba kuna vitu fulani vikubwa na vizuri tulivipanga – mimi na marafiki na wadogo zako, kwa ajili yako, kwa staili yako – mapema mwezi Machi, ambavyo naamini vingekupa tabasamu. Kama unaweza, hapo ulipolala, tupe ishara tufanyeje.

Nafarijika kidogo kwamba nilipata nafasi ya kukukumbatia kwa mara ya mwisho. Sikujua kwamba tunaagana. Ulinishika mkono kwa nguvu, hukutaka kuuachia, na ulitabasamu niliposema nakungoja Dar tukae pale THT, kama kawaida yetu, kujadili mawazo na mipango yako mingi.

Ingawa umeshawasili huko upande wa pili, familia yako na watu wengi watauaga mwili wako kwa heshima kubwa. Utajengewa kaburi. Nadhani litawekwa marumaru. Lakini tukitaka kukusalimia tena hatutakutafuta kaburini kwako. Tutakutafuta kwenye nyoyo za watu uliowagusa na kuwasaidia. Na ni wengi kweli. Kumbukumbu yako itabaki kwenye nyoyo zao na kwenye mafanikio yao. Watoto wako hawapo peke yao. Watalia sana, lakini ni kwa muda tu; kwasababu watafunikwa kwa upendo wetu sote na watafarijika, na watakuwa na fahari, kwa jinsi unavyosemwa na unavyokumbukwa.

Ndugu yangu, nisikuchoshe. Mengine tutaongea tutakapokutana tena kwasababu kwa hakika sisi sote, mmoja mmoja na kwa wakati wetu, kwa kadri ya mipango yay eye aliyetuumba, tutakufuata huko. Miaka yote nimekujua, sijawahi kukuona umepumzika. Pumzika kwa amani kwa sasa – na milele.

Ndimi, rafiki yako,
 January Makamba
 27 Februari 2019
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images