Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109605 articles
Browse latest View live

MIPANGO YA SERIKALI KUHUSU GESI YA KUSINI IKO PALEPALE - MGALU

0
0
Na Veronica Simba – Lindi
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka watanzania kuondoa shaka kuhusu mipango ya serikali kufuatia gesi iliyogunduliwa mikoa ya kusini, kwani haijabadilika na inaendelea kutekelezwa. Aliyasema hayo jana Februari 27, 2019 kijijini Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku nne mkoani Lindi ambapo alikagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, kuwasha umeme katika vijiji mbalimbali na kuzungumza na wananchi.

“Nataka niwaaminishe wana-kusini, yale ambayo serikali iliahidi baada ya kugundua gesi, mipango yake iko palepale na inafanyiwa kazi,” alisema.

Akifafanua zaidi, Naibu Waziri Mgalu alisema moja ya mambo ambayo serikali iliahidi ni umeme wa uhakika utakaowezesha uwekezaji. Alisema hadi sasa, taratibu za kukamilisha ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa gesi Mtwara wenye megawati 300 na Somanga Fungu wenye megawati 330 ziko katika hatua za mwisho.

“Mradi utaanza ndani ya mwaka huu wa fedha ambao utawezesha mikoa hii kuzalisha umeme wa kutosha kuweza kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.” Aidha, aliongeza kuwa, jambo jingine kubwa ni kuviwezesha viwanda vya maeneo husika kupata umeme wa gesi ambapo alisema tayari kiwanda cha saruji cha Dangote kimeshaunganishiwa.

Pia, alisema, serikali inaendelea kuzungumza na viwanda vya mbolea ili vizalishe mbolea inayotokana na gesi ili pamoja na mambo mengine viongeze ajira kwa wananchi. Vilevile, alisema kwa Mkoa wa Lindi, eneo la Likongo, serikali inatarajia kujenga kiwanda cha kusindika gesi iwe katika hali ya kimiminika ambapo Rais John Magufuli ametoa mwongozo wa kufanya mazungumzo na mbia mmoja mmoja. Alisema mazungumzo yanaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alizungumzia tathmini ya ziara yake mkoani Lindi, ambapo alisema imekuwa yenye mafanikio. Alisema, kazi ya kuwaunganishia wananchi umeme vijijini inaendelea na ametoa wito kwa mkandarasi husika kuboresha utendaji wake ili kuhakikisha anafikia malengo ya kukamilisha kazi yote kwa mujibu wa mkataba ifikapo Juni 30, mwaka huu ambapo ndipo mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa kwanza utakuwa unahitimishwa.

Naibu Waziri alisema yeyé pamoja na viongozi wengine wa Lindi akiwemo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya na Wabunge wamekubaliana kumsimamia mkandarasi husika katika kuhakikisha anatimiza wajibu wake ipasavyo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, ambaye alifuatana na Waziri wakati akihitimisha ziara yake, aliwahakikishia wananchi wa eneo husika kuwa yeyé pamoja na viongozi wenzake watamsimamia mkandarasi husika ili kuhakikisha kazi inatekelezwa kwa ufanisi.

“Tumekabidhiwa hawa tuwasimamie, kwa hiyo nichukue nafasi hii kuwathibitishia kwamba tutawasimamia kwelikweli ili kuhakikisha zoezi hili linakamilika vizuri sana,” alisisitiza. Naye Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye, aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa upande wa nishati ambapo alisema imekuwa ikifanya kazi nzuri sana.

“Tunawashukuru sana Wizara ya Nishati kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kama kuna Wizara inafanya vizuri, basi Wizara hii inafanya vizuri.” Hata hivyo, Nnape alisema anatambua kiu kubwa ya umeme waliyonayo wananchi na kuwasihi kuwa wastahimilivu maana zoezi la kuunganisha umeme ni hatua kwa hatua, awamu kwa awamu. Alisema anayo imani kubwa kwamba vijiji vyote vitafikiwa na huduma hiyo kabla ya mradi kuisha.

Mkuregenzi wa kampuni ya State Grid, ambayo ndiyo inatekeleza uunganishaji wau meme mkoani Lindi, Charles Mlawa, akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara hiyo, aliahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Naibu Waziri katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi.

Katika ziara hiyo, viongozi wa ngazi mbalimbali walipongeza utendaji kazi wa Wizara pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuomba jitihada zinazofanyika ziendelee. Katika Miradi ya Umeme Vijijini, Mzunguko wa Kwanza (REA III – 1), jumla ya vijiji takribani 133 vitaunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi bilioni 1.9. Matarajio ni kuwaunganishia wananchi takribani 5337.

Akiwa Lindi vijijini, Naibu Waziri aliwasha umeme katika vijiji vya Ntauna, Mvuleni na Tulieni.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiwasha rasmi umeme katika kijiji cha Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 27, 2019. Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga (kushoto), Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (wa pili-kushoto) na Afisa wa TANESCO Lindi.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Mvuleni, Lindi Vijijini, Februari 27, 2019. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga na wa pili kutoka kushoto ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza wakati wa hafla ya uwashaji rasmi wa umeme katika kijiji cha Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 27, 2019.
 Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye akizungumza, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha njano - meza kuu) kijijini Ntauna, Kata ya Rondo, Lindi Vijijini, Februari 27, 2019. Naibu Waziri aliwasha rasmi umeme kijijini hapo.
 Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Mvuleni, Lindi Vijijini, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kabla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Februari 27, 2019.
Viongozi mbalimbali wa Serikali mkoani Lindi, wataalamu kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (aliyesimama), wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mvuleni, Lindi Vijijini, alipokuwa katika ziara ya kazi, Februari 27, 2019. Naibu Waziri aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho.

WAAJIRI WANAOKWAMISHA USHUGHULIKIAJI WA RUFAA ZA MASHAURI YA WATUMISHI WA UMMA KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU

0
0
Watendaji katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala, Mamlaka, Sekretarieti za mikoa na Halmashauri za wilaya nchini wametakiwa kutokwamisha jitihada za Tume ya Utumishi wa Umma katika kushughulikia rufaa za mashauri ya watumishi wa umma kwa kutuma vielelezo sahihi vinavyohitajika.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam. Mhe. Mkuchika amesema kuwa, baadhi ya waajiri na watumishi wa umma wamekuwa wakikaidi au kuchelewa kutekeleza maelekezo ya Tume ya Utumishi wa Umma ya kuwataka kuwasilisha vielelezo vinavyowezesha ushughulikiaji wa rufaa za mashauri ya watumishi jambo linalokwamisha ushughulikiaji wa rufaa za watumishi.

Amewataka waajiri na watumishi wa umma nchini kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tume ya Utumishi wa Umma kila wanapotakiwa kufanya hivyo na kumwagiza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kuorodhesha waajiri wote watakaoendelea kukaidi maagizo ya Tume ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Mhe. Mkuchika amewatahadharisha watumishi na waajiri wanaokwamisha michakato ya ushughulikiaji wa rufaa za watumishi kuwa wanaathiri dhana nzima ya utawala bora na wanakwamisha utoaji wa haki kwa watumishi wa umma na kusisitiza kuwa hatomvumilia mwajiri au mtumishi yeyote anayeharibu heshima yake aliyoijenga kwa miaka mingi.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, Naibu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Rosy Elipenda amemhakikishia Waziri Mkuchika kuyafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa na kuongeza kuwa Tume itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uadilifu bila upendeleo wowote.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bi. Immaculate Ngwale alipowasili Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam kuzungumza na watumishi wa Tume hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi kati yake na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji Mstaafu, Dkt. Stephen Bwana.
 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Jaji Mstaafu Dkt. Stephen Bwana akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) kuzungumza na watumishi wa Tume wakati wa kikao kazi kilichofanyika Ofisi ya Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo.
 Kaimu Katibu, Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Richard Odongo akitoa neno la utangulizi wakati wa kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kilichofanyika Ofisi za Tume ya Utumishi wa Umma, Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.

MENO YA TEMBO NA UHUJUMU UCHUMI VYAMFIKISHA MFANYABIASHARA KORTINI

0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MFANYABIASHARA  Isack Mwasenga (40) Mkazi wa Kanga Chunya mkoani Mwanza,  amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya  uhujumu uchumi likiwemo la kukutwa na vipande 14 vya meno ya tembo na utakatishaji fedha.

Mwasenga amefikishwa mahakamani hapo leo Februari 28, 2019  na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi Augustino Rwizile.

Akisoma hati ya mashitaka, Wakili wa Serikali, Wankyo Simon amedai, Desemba 21, mwaka jana huko katika nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ubungo jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa na vipande 14 vya meno ya tembo vyenye thamani ya USD, 45,000 sawa na sh. 102,150,000 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Pia imedaiwa, mshitakiwa baada ya kukutwa na vipande hivyo, alitumia fedha hizo wakati akijua kwamba ni zao la uwindaji haramu. Hata hivyo, mshitakiwa haruhusiwi kujibu chochote mahakamani hapo kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida zinasikilizwa mahakama kuu au mpaka mahakama itakapopewa kibali na DPP

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 12, mwaka huu kesi itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Mshitakiwa amerudishwa rumande 

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB ABDULMAJID NSEKELA AOMBOLEZA KIFO CHA RUGE MUTAHABA

0
0
Kwa niaba ya familia nzima ya Benki ya CRDB nitoe pole kwa familia nzima ya Clouds Media Group, familia ya Prof. Mutahaba, Tasnia nzima ya Habari na Burudani na Watanzania wote kwa ujumla kwa kuondokewa na rafiki, ndugu na kaka yetu kipenzi Ruge Mutahaba. Amahakika Taifa limepoteza mtu mahiri sana katika tasnia ya habari na burudani.

Pamoja na majonzi makubwa tuliyonayo, sisi Wanafamilia wa Benki ya CRDB, tunajivunia sana ndugu yetu Ruge Mutahaba. Ruge pamoja na Joseph Kusaga ndio waasisi wa uhusiano huu mkubwa tunaouona leo hii baina ya Benki yetu ya CRDB na Clouds Media. Tukiwa Benki ya Kizalendo azma yetu kubwa nikuona tunaishi ndoto za Watanzania walio wengi.

Wakati Ruge na Kusaga wanakuja na wazo kuanzisha redio, ili kuwa ni ndoto, lakini uthubutu wao wa kufuata fursa ndio ulioishawishi Benki yetu kuwaamini na kuwapa mkopo wa kiasi cha shilingi milioni 40 uliofanikisha kuanzishwa kwa Clouds FM redio. Sasa hivi Clouds FM inazaidi ya miaka 19, pamoja na kuanzishwa kwa media nyengine Choice FM, Clouds TV, Clouds International, Clouds Digital pamoja na kuvuka mipaka na kuingia Rwanda, Botswana na Abudhabi.

Hizi zote ni jitihada na maono ya ndugu yetu Ruge Mtahaba, hakuna asiyefahamu bidii na umahiri wake katika kazi na ndio maana sisi Wanafamilia ya CRDB tutaendelea kumshukuru Mungu kwa ajili yake, tumejifunza mengi kutoka kwakwe na tunamshukuru kwa kutupa nafasi ya kuishi ndoto hii ya Clouds Media Group ambayo leo hii imewafungulia dunia Watanzania wengi hususani vijana.

Katika sifa kuu aliyokuwa nayo ndugu yetu Ruge Mutahaba kubwa zaidi alipenda sana maendeleo ya watu wengine, nadhani hii inajidhihirisha kupitia program yake fursa. Siku zote alikuwa akitambua umuhimu wa kuielimisha jamii katika masuala mbalimbali. Amekuwa na mchango mkubwa sana katika kutusaidia kufikisha elimu juu ya huduma zetu za kifedha kupitia Clouds Media, tumekuwa tukishirikiana kwa karibu sana.

Utayari wetu wa kushirikiana na Clouds Media katika nyanja mbalimbali ni kwasababu siku zote tumekuwa tukijuwa msimamo wake katika kuboresha maisha ya jamii inayotuzunguuka. Maisha yake yamekuwa ni baraka kwa wengine na daima tutaendelea kumuenzi. Mioyo yetu imejawa na huzuni, lakini daima tutakwenda kusherekea maisha ya ndugu yetu Ruge Mutahaba.

Inna lilah wa inna ilayh raji’un

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza nawaandishi wa habari alipofika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba, kuhani msiba. Mikocheni jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajidi Nsekela akiwa na baadhi ya waombolezaji wengine waliofika kwenye msiba wa Ruge Mutahaba, Mikocheni jijini Dar es salaam leo.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ARIDHISHWA NA KASI YA UKALIMISHWAJI WA OFISI YAKE

0
0
Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, amesema, anaridhishwa  sana   na kasi ya ukamilishaji wa jengo la Ofisi ya Mwanasheria  Mkuu linalojengwa  katika  mji wa Kiserikali   ulipo katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma
Jana ( Jumatano) Profesa Kilangi aliwoongoza   Wakurugenzi,  Wakurugenzi  Wasaidizi na Wakuu wa  Vitengo kukagua kazi inayoendelea katika ukamilishaji wa jengo hilo.
“Ninaridhishwa   na ninafurahi sana kwa kasi na kazi nzuri  ya  ukamilishaji wa jengo hili.  Kila ninapofika hapa kwenye site nakuta kazi mpya inaendelea, hongera sana Injinia kwa usimamizi wako  pamoja na timu yako” amesema.
Akiogozwa na Injinia Suma Atupele. Mwanasheria Mkuu na ujumbe wake alipita  na kukagua kila Ofisi huku akitoa maelekezo kwa Naibu Mwanasheria Mkuu na  Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali  Watu juu ya mpangilio na mgawanyo wa Ofisi kwa  kuzingatia  muundo   na majukumu  ya Ofisi.
Katika  maelekezo yake kwa viongozi hao, Profesa Kliangi amesisitiza   katika upangaji  wa Ofisi kuhakikisha kwamba, Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi  na   maafisa walio chini yao hasa kutoka Divisheni za   kisheria wanakuwa katika utaratibu wa kuhamia katika jengo hilo pale litakapokuwa tayari kuhamia.
 Baada ya  kukagua maendeleo ya  ukamilishaji  wa jengo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na timu yake alipata pia fursa ya kuangalia eneo zima lenye ukubwa wa ekari tano  ambalo limetengwa kwa ajili ya  ujenzi wa awamu ya pili wa Jengo  kubwa zaidi ambalo litakuwa na uwezo wa kutosheleza watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu pamoja na matumizi mengine yakiwamo ya ujenzi wa Chuo  maalum kitakachokuwa kikitoa mafunzo kwa Mawakili wa Serikali.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi akifafanua  juu ya mgawanyo wa  Ofisi kwa    baadhi ya wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi  na wakuu wa vitengo wakati walipotembelea  kukagua  maendeleo ya kazi ya ukamilishwaji wa jengo la awamu ya kwanza  la  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa  Serikali linaojengwa katika Mji wa Kiserikali  katika Kata ya Mitumba- Ihumwa nje kidogo ya Jiji la Dodoma. Mwanasheria Mkuu  amesema anaridhishwa  kasi ya kukamilishwa   kwa kazi zilizobaki katika  jengo hilo
 Injinia Mwanadada  Suma Atupele ambaye amekuwa akisimamia kazi  za ujenzi wa Jengo la Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  tangu jengo hilo lilipoanza kujengwa akitoa maelezo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ujumbe wake namna  Ofisi zitakavyo fanyiwa  mgawanyo ( partitioning).
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi akielezea  kwa  kuchora  ardhini mgawanyo na  matumizi ya sehemu ya eneo la ukubwa wa ekari  karibu tano ikiwamo sehemu ambayo limejengwa jengo la awali   ambalo  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu  imepewa na  Serikali katika  Mji wa Kiserikali  Mitumba- Ihumwa.
 Kazi ya uwekeaji  wa (vigae)tiles ukiendelea,  kama inavyoonekana katika  chumba hiki.  
     Kazi ya upakaji rangi nje ya jengo  ikiwa inaendelea kama  inavyoonekana

DKT. KIJAJI ASHITUKIA GHARAMA ZA MRADI WA UKARABATI WA SHULE YA SEKONDARI MZUMBE MKOANI MOROGORO

0
0
Na Peter Haule, WFM, Morogoro
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Wavulana-Mzumbe, ulioingiwa kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Shirika la Nyumba la Taifa-NHC ili kujiridhisha kuhusu gharama halisi za mradi baada ya kubaini kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kinatofautiana na fedha halisi zilizotolewa na Serikali

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya wavulana ya Mzumbe iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kuelezwa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemoo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokuwa na taarifa zozote kuhusu mradi huo.

Dkt. Kijaji alishangazwa na utofauti wa kiwango cha fedha kilichoainishwa katika taarifa ya gharama ya ukarabati wa shule hiyo kwamba ilikuwa shilingi milioni 999.7 wakati kiasi cha fedha kilichotolewa na Serikali ni zaidi ya shilingi bilioni 1.

Alitoa wito kwa wakuu wa wilaya kote nchini kufuatilia kwa karibu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ili kujiridhisha kuhusu fedha zinazotumika kwenye miradi hiyo, kukagua thamani ya fedha kwenye miadi husika, pamoja na mikataba yote inayohusika ili kujua mawanda (scope) ya miradi hiyo

"Kila anayekuja kutekeleza miradi katika Wilaya ni vema akaulizwa amekuja kufanya nini na kwa namna gani kwa kuwa lengo ni kuwasaidia wananchi wa maeneo husika na Taifa kwa ujumla na hakuna siri kwenye miradi hiyo kwa hiyo ni lazima muijue kwa undani" alisema Dkt. Kijaji

Alisema kuwa,  Shule Kongwe ya Mzumbe imekarabatiwa na mabadiliko yanaonekana lakini ni vigumu kujua ilitakiwa kukarabatiwa kwa kiwango kipi na maeneo gani kwa kuwa wahusika wakiwemo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Mkuu wa Shule hiyo hawafahamu mawanda ya mradi huo.

"Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mvomero hakikisheni mnapata mkataba wa ukarabati wa shule hii ili kupata uhakika wa nini kilitakiwa kifanyike kwa kuwa bado maeneo mengi hayajakarabatiwa na Mkandarasi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa lakini tayari amekabidhi kazi" alisisitiza Dkt Kijaji.

“Dhamana ya Wizara ya Fedha na Mipango ni kutafuta fedha, kupeleka maeneo husika kwa ajili kubadili maisha ya watanzania na kukagua matumizi yake, hivyo hali hiyo iliyojitokeza inaenda kufanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza ushirikiano”, alieleza Dkt. Kijaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kyombo, aliishauri Serikali kuona namna bora ya kuboresha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa miradi kama hiyo kuanzia kwenye upembuzi yakinifu wa majengo yanayokarabatiwa, nini kikarabatiwe, wakati gani, na kuwahusisha wataalam wa wilaya wakati wa kukagua na kutathimini kazi iliyofanyika kabla ya mkandarasi kulipwa

Naye Mkuu wa Shule hiyo Kongwe ya Mzumbe Bw.Wal Kihongosi, aliishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuboresha shule hiyo ya vipaji maalum kwa kuwa hapo awali mazingira yake yalikua hayasadifu hadhi ya kuwa na wanafunzi wenye vipaji.

Pia akaiomba Serikali kusaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi, kuongeza vifaa vya maabara kwa kuwa havitoshi, kujengewa jengo moja jipya kwa ajili ya ofisi ya taaluma pamoja na idara zake tisa  na pia kuongeza idadi ya watumishi wakiwemo wapishi na walinzi walioajiriwa wa muda mrefu badala ya waliopo ambao ni wa mkataba wa mda mfupi ambao udhibiti wake kulingana na unyeti wa kazi hizo ni mgumu.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Bw. Mohamed Utaly, alipotembelea na kukagua ukarabati wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wavulana ya Mzumbe.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akihoji baadhi ya maeneo ya ukarabati wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Wavulana Mzumbe, alipotembelea na kukagua ukarabati wa Shule hiyo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
 Mkurugenzi wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Bw. Florent Kyombo, akiiomba Serikali kushirikisha uongozi wa Wilaya katika hatua za awali za utekelezaji wa miradi, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipotembelea na kukagua ukarabati wa Shule Kongwe ya Sekondari ya Mzumbe.
 Mkuu wa Shule Kongwe ya Wavulana ya  Mzumbe Bw. Wal Kihongosi, akitoa maelezo ya maeneo yaliyokarabatiwa huku wadau wengine wakitazama picha za majengo hayo, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) alipotembelea na kukagua ukarabati wa Shule hiyo.
 Mkuu wa Shule Kongwe ya Wavulana ya  Mzumbe Bw. Wal Kihongosi, akisoma kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ukarabati wa Shule yake ambacho kilikua kinatofautiana na kiasi alichowasilisha cha kutekeleza maboresho hayo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb).
 Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Bw. Mohamed Utaly, akiuliza jambo wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia), alipotembelea majiko ya Gesi yaliyo karabatiwa katika Shule Kongwe ya Wavulana Mzumbe, Mkoani Morogoro .
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kulia), akiongozwa na Mkuu wa Shule Kongwe ya Wavulana Mzumbe, Bw. Wal Kihongosi (kulia) kukagua ukarabati wa shule yake.
Muonekano wamajengo ya Shule Kongwe ya Wavulana ya  Mzumbe, yaliyokarabatiwa na kubadilisha mandhari ya shule hiyo yenye wanafunzi wenye vipaji.

(Picha na Peter Haule, Wizara ya Fedha na Mipango)

WAZIRI MKUU AZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA WA KATI NA WADOGO WA KARIAKOO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na  wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaa,, Februari 28, 2019.  Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza kaika kikao cha wafanyabiashara wa kati na wadogo alichokiitisha, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa  Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya wafanyabiashara wa kati na wadogo wa Kariakoo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Anatouglo jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

YANGA YATUA MWANZA KUIKABILI ALLIANCE SIKU YA JUMAMOSI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KIKOSIcha Yanga kimewasili mkoani Mwanza mapema asubuhi ya leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Alliance ya jijini humo utakaochezwa siku ya Jumamosi.

Yanga watacheza mchezo wa 26 wa ligi kuu baada ya kutoka kucheza mchezo wa hatua ya 16 bora ya kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Namungo na kufanikwia kutinga hatua ya nane bora.

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa mchezo huo ni muhimu sana kwao na kuhakikisha wanaondoka na alama tatu ili kujiweka zaidi kwenye uongozi wa ligi.

Amesema, mchezo huo dhidi ya Alliance ni mgumu sana ila wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo na watajituma kufanikisha wanawapa furaha mashabiki wa timu hiyo.
Yanga imesafiri na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na benchi la ufundi wakiongozwa na viongozi wa timu hiyo na watacheza mechi mbili katika kanda ya ziwa.

Kwa upande wa benchi  la ufundi wa Alliance wao wamejizatiti kuhakikisha wanabakisha alama tatu katika Uwanja wa nyumbani ikiwemo na kuonesha mpira safi kwa wanajangwani hao.

Kocha mkuu wa Alliance, Malale Hamsini amesema wanatambua ushindani uliopo na namna kikosi cha Yanga kilivyo bora ila kazi yao ni moja tu kubeba alama tatu ingawa anafahamu uzoefu waliokuwa nao.

"Tayari kwa sasa vijana wameshajibu na mfumo umeanza kueleweka na ndo maana unaona tunapata matokeo chanya, tunaiheshimu Yanga kutokana na uzoefu wao lakini tumejipanga kubeba pointi tatu nyumbani.

Alliance wataikaribisha Yanga ambao ni vinara wakiwa na pointi 61 baada ya kucheza michezo 25 huku wao wakiwa nafasi ya 7 na wakiwa wamekusanya pointi 36 baada ya kucheza michezo 28.

AZAM FC KUSAKA ALAMA TATU DHIDI YA LYON KESHO UWANJA WA UHURU

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
TIMU ya Azam Fc itakuwa na kibarua kingine kigumu dhidi ya African Lyon katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara (TPL) utakaofanyika kesho kwenye Uwanja wa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha wa muda Iddy Cheche baada ya kupokea mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo  Hans Pluijm pamoja na Juma Mwambusi kukatishiwa mkataba na matajiri hao wa Azam.

Baada ya kukabidhiwa timu hiyo mwanzoni mwa wiki hii, Cheche amefanikiwa kuifanikisha timu hiyo na kutinga hatua ya nane bora ya kombe la Shirikisho, na kesho atakuwa na mtihani wake wa kwanza wa TPL dhidi ya African Lyon.

Azam itakaribishwa na African Lyon kwenye mchezo wa ligi utakaopigwa Uwanja wa Uhuru ikiwa ni mara ya kwanza kuongoza jahazi bila uwepo wa Pluij kwenye benchi.

Cheche amesema kuwa anawatambua vizuri wachezaji wake na anajua namna ya kuwatumia hivyo hana mashaka katika kazi yake.


"Nawatambua wachezaji wangu kutokana na uzoefu nilionao hapa kwenye kikosi sina mashaka naamini kila kitu kitakuwa sawa," amesema Cheche.

Kwa mujibu wa mratibu wa Azam FC, Philip Alando kuhusu mchakato wa makocha amesema zaidi ya maocha 10 wameomba kazi kwa kutuma CV zao kwenye email hivyo watazipitia ili kujua nani atabeba mikoba ya Pluijm.

BENKI YA CRDB YAWAPA SEMINA WATEJA WAKE MKONIA IRINGA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa wafanyabiashara na wateja wa Benki ya CRDB Mkoani Iringa, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani, Februari 26, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wafanyabiashara na wateja wa Benki ya CRDB Mkoani Iringa, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani, Februari 26, 2019.
Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Neema Mori akizungumza wakati wa semina ya siku moja kwa wafanyabiashara na wateja wa Benki ya CRDB Mkoani Iringa, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani, Februari 26, 2019.
Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakitoa mada kwa wafanyabiashana na wateja wa Benki ya CRDB waliohudhulia semima hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifafanua jambo wakati wa semina ya siku moja kwa wafanyabiashara na wateja wa Benki ya CRDB Mkoani Iringa, iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kichangani, Februari 26, 2019.
























RC MAHENGE ATAMBULISHA MRADI WA LISHE ENDELEVU DODOMA

0
0
Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto la Save the Children kwa kushirikiana na Delloite,Manoff na PANITA limetambulisha rasmi mradi wa lishe endelevu kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma ili kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake,vijana na watoto.
Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 28,2019 katika ukumbi wa Morena Hoteli Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Mheshimiwa Binilith Mahenge.
Mradi huo wa Lishe Endelevu unalenga kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano ambao ni waathirika wakubwa wa lishe duni.
Mahenge alisema mradi wa Lishe Endelevu ni fursa kwa wananchi wa Dodoma hivyo kuwaomba watendaji wa serikali kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau wanaotekeleza mradi huo ili wafanye kazi katika mazingira ya amani na utulivu kufikia malengo ya mradi.
“Malengo ya mradi huu kimsingi yanaimarisha afya na lishe ya jamii ambayo ni mtaji mkubwa katika kuimarisha nguvu kazi ya taifa haswa katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchumi wa kati”,alieleza mkuu huyo wa mkoa. 
“Tunawakaribisha sana wadau wetu wa Lishe Endelevu na tuwatakia heri na mafanikio makubwa katika utekelezaji wa malengo ya mradi. Twendeni tukiwa tunakumbuka kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Jamii, mkoa na Taifa kwa ujumla, viongozi na watendaji wa mradi huu tekelezeni majukumu yenu kama yalivyoainishwa kwenye malengo ya mradi”,alisema.
Katika hatua nyingine alisema Lishe duni haiathiri tu maendeleo ya mtoto lakini pia inaathiri ukuaji wake kimwili na kiakili kutoka kipindi cha ujauzito na hatimaye kuathiri mchango wake katika maendeleo ya taifa kwa kipindi chote cha uhai wake hivyo mradi huo utasaidia kuondokana na changamoto hizo.
Aidha aliwaomba wadau wa lishe mkoani Dodoma kuongeza jitihada kupunguza utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano ingawa  takwimu za hivi karibuni (TDHS 2015/16) zimebaini kuwa Udumavu umepungua kutoka asilimia 56.0 (2010) hadi asilimia 36.5 mkoani humo. 
“Hali ya lishe ya wanawake walio katika umri wa uzazi (miaka 15-49) nayo bado ni mbaya; sote tunajua, hali ya lishe ya mama ikiwa mbaya inaathiri hali ya mtoto toka tumboni pamoja na malezi na makuzi ya mtoto. Tafiti za hivi karibuni zimebaini kwamba, kati ya wanawake kumi, wastani wa wawili wana utapiamlo",aliongeza. 
Alibainisha kuwa lishe duni kwa wanawake wajawazito inachochea hatari ya kujifungua watoto njiti, waliodumaa au kuharibu mimba hivyo vifo vya wanawake wajawazito vitapungua sana endapo serikali kwa kushirikiana na wadau watakuwa na mikakati ya pamoja ya kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili mama mjamzito, aliyejifungua na mtoto chini ya miaka mitano.
Kwa upande wake,Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Dodoma Benety Malima aliwaomba wadau wa lishe mkoani humo na serikali kushirikiana katika kutekeleza mradi huo ambao utasaidia kuimarisha hali ya lishe kwa wanawake walio katika umri wa kuzaa, wajawazito na wanaonyonyesha, vijana wa rika la balehe na watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.
Malima alisema  mradi huo unatekelezwa katika mikoa minne ya Dodoma, Rukwa, Iringa na Morogoro kwa kipindi cha miaka minne Kwa miaka minne mradi utagharimu USD 19.7 Milioni ukifadhiliwa na Mfuko wa Watu wa Marekani ‘USAID’.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge akizungumza wakati mradi wa Lishe endelevu ukitambulishwa Dodoma



Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na Delloite,Manoff na PANITA likitambulisha mradi wa lishe endelevu kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati mradi wa lishe endelevu ukitambulishwa kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Dodoma Benety Malima akiandika dondoo muhimu wakati Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Binilith Mahenge akitoa hotuba wakati mradi wa lishe endelevu ukitambulishwa kwa viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma.
Viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma wakiwa ukumbini.
Picha ya pamoja viongozi, watendaji na wadau wa maendeleo mkoa wa Dodoma baada ya mradi mradi wa lishe endelevu kutambulisha.

WILAYA YA MBULU YAJIVUNIA ZAO LA MAHARAGE KUONGEZA MAPATO YA NDANI

0
0
 Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara,Moses Nduligu akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea wilaya hiyo kuona usambazi wa teknolojia za mbegu bora za maharage zilizofanyiwa utafiti ili kumwongezea mkulima tija.
 Mkulima wa maharage katika Kijiji cha Moringa Kata ya Daudi wilaya ya Mbulu,Julitha Cosmas akiwa katika shamba lake linalotumiwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo(TARI-Selian) Arusha kutoa mafunzo kwa wakulima wengine. 
 Mtafiti wa taasisi ya The International Center for Tropical Agriculture(CIAT),Redegunda Kessy akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo.
 Mkulima wa maharage katika Kijiji cha Moringa Kata ya Daudi wilaya ya Mbulu,Rose Cyprian akiwa katika shamba lake,amefurahia mbegu bora aina ya Selian 14 inayotoa mazao bora.
 Mkulima wa maharage eneo la Hydom wilaya ya Mbulu,Abel Bayda akikagua shamba lake linalotumiwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo(TARI-Selian) Arusha kutoa mafunzo kwa wakulima wengine.
Mtafiti wa taasisi ya The International Center for Tropical Agriculture(CIAT),Redegunda Kessy akizungumza jambo na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo.

NENDA SALAMA RUGE BY THT & MRISHO MPOTO

SERIKALI YA WATAKA WAFANYABIASHARA WA MADINI KUWA WAWAZI KWENYE SHUGHULI ZAO

Zanzibar kuendeleza ushirikiano na Saudi Arabia, Waziri mkuu Kassim majaliwa ahani msiba wa Ruge


Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu awataka Wajasiliamali wadogo wawe na vitambulisho

0
0
Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ametoa angalizo kwa Wajasiliamali wadogo kuhakikisha wale ambao hawana vitambulisho hivyo wanakuwa navyo kwani ndio mkombozi wao kibiashara.

Gavana Shilatu aliyasema hayo kijijini Mihambwe kilichopo kata ya Mihambwe, Tarafa ya Mihambwe wakati akiendelea na zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Wajasiliamali kwa ambao wamelipia Tsh. Elfu ishirini.

*"Wajasiliamali wadogo changamkieni fursa hii adimu na adhimu ya kuwa na vitambulisho vitakavyowafanya msisumbuliwe na mkuze mitaji na maisha yenu. Fursa ya wanufaika imeongezeka, tuvichangamkie."* alisema Gavana Shilatu.

Zoezi la utoaji wa vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo lilizinduliwa na Rais Magufuli kwa lengo la kuwasaidia Wajasiliamali wadogo wasisumbuliwe na wakuze mitaji yao.

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA TEMINARL III

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.


Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.

Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo eneo la maegesho ya ndege linaweza kuegesha ndege 19 za darala C, na 11 daraja E na jengo linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa muda ambao abiria ni wengi.

Mhandisi Mfugale amemhakikishia Mhe,. Majaliwa kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa, na kwamba jengo hilo litakabidhiwa kwa serikali tarehe 31 Mei, 2019.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya umaliziaji wa ujenzi wa Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Teminal Three  jijini Dar es salaam, Februari 28, 2019. Ujenzi wa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 95 na unatajiwa kukabidhiwa kwa serikali Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale akisoma taarifa ya  Ujenzi wa mradi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), leo alipowasili kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
  Kiongozi Mkuu wa Timu ya Wataalam wa Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Julius Ndyamukama (aliyenyoosha mkono) akimuonesha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ukumbi wa abiria wanaoondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia aina ya viti vya abiria vitakavyotumika kwenye Jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) alipotembelea leo. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Bi. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Ilala na wa pili kushoto ni Mhandisi Julius Ndyamukama, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda.


  1. Menejimenti ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Vedastus Fabian (watatu kulia) wakitoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya ziara ya waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kumalizika leo.
Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 

 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
 Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiaga wakati alipoondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal Three, jijini Dar es salaam baada ya kukagua ujenzi wa uwanja huo ambao umekamilika kwa asilimin 95 na unarajiwa kukamilika Mei mwaka huu. 
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu na TAAA

IGP SIRRO ATEMBELEA MRADI WA SGR

JOSEPH KUSAGA AMUONGELEA RUGE

WANACHAMA wa chama cha wachimbaji wa madini Mkoani Manyara Marema Tawi la Mirerani wapata uongozi

0
0
WANACHAMA wa chama cha wachimbaji wa madini Mkoani Manyara Marema Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro, wamechagua Mwenyekiti wao mpya, baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wao Samuel Rugemalira kujiuzulu nafasi hiyo hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Marema mkoa wa Manyara, Justin Nyari akizungumza jana kwenye uchaguzi huo uliofanyika mji mdogo wa Mirerani alisema Shwaibu Mushi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Marema Tawi la Mirerani baada ya kuwabwaga wagombea wenzake watatu.
Nyari alisema Mushi alipata kura 36 na kuwabwaga wapinzani wake watatu akiwemo Hossea Palangyo Shilingi aliyepata kura 15, Abubakari Madiwa aliyepata kura tisa na Ramadhan Msumba aliyepata kura tano.
Hata hivyo alisema mgombea Hossea Palangyo (Shilingi) alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Marema baada ya kushika nafasi ya pili ya uenyekiti kwa kura 15 hivyo atajaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na Mushi.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo, Mushi alisema ataendelea kuifanya Marema kuwa bora zaidi ya jana na juzi.
Mushi aliwashukuru wale wote waliomchagua na waliompa ushirikiano kwenye nafasi ya Kaimu Mwenyekiti wa Marema wakiwemo viongozi wenzake wa ngazi ya Tawi, Mkoa na wachimbaji kwa ujumla.
Alisema ataendelea kuwa kiungo bora kati ya wachimbaji madini na serikali ili kuhakikisha madini hayo yanawanufaisha watanzania.
Kwa upande wake, Palangyo akizungumza baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo alisema yeye huwa anawajibika kwa wachimbaji na ataendelea kufanya hivyo huku akiwa na msimamo bila kuyumbisha au kuwayumbisha wachimbaji.
Hata hivyo, Ofisa madini mkazi wa Simanjiro Daudi Ntalima aliwataka viongozi hao wa Marema kutojiingiza kwenye unaharakati hivyo kutenganisha na shughuli zao za madini na kufarakanisha wachimbaji na serikali.
“Mimi ni mlezi wenu sasa ntashangazwa kama kuna baadhi ya viongozi wa Marema mnakuwa wana harakati na kuacha kufanya shughuli za kuwaunganisha wachimbaji na serikali na kujiingiza kwenye uanaharakati ambao hauna maana yeyote ile,” alisema Ntalima.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Afya, mazingira na usalama migodini wa shirikisho la wachimbaji madini nchini (Femata) Dkt Bernad Joseph akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.


Ofisa madini wa mkazi wa Simanjiro Daudi Ntalima akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani.
Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji madini mkoani Manyara (Marema), Justin Nyari akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Marema Tawi la Manyara, ambapo Shwaibu Mushi alichaguliwa kushika nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara Marema Tawi la Mirreani Shwaibu Mushi akiwashukuru wapiga kura waliomchagua kuwa Mwenyekiti wa Tawi hilo kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa diwani mstaafu Lucas Zacharia wa Kazamoyo Inn.

Viewing all 109605 articles
Browse latest View live




Latest Images