Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

TANZANIA INAUMWA KWA AJILI YAKO RUGE

$
0
0
Ruge Mutahaba.

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MAISHA yangu ya uandishi wa habari kwa miaka 19 sasa, hakuna siku hata moja nimewahi kuandika makala, maelezo, maoni au ushauri kuhusu Mtanzania ambaye anasumbuliwa na maradhi.

Nimekuwa na utamaduni wa kutoa pole au kushiriki kwenye maombi ya kuhakikisha mwenzetu anayeumwa, Mwenyezi Mungu ampe unafuu na apone haraka. Nimekuwa nikifanya hivyo kadiri ninapopata taarifa. Ila sijawaji kuandika maelezo mareeefu kumzungumzia mgonjwa!

Kwa mara ya kwanza leo naomba nivunje mwiko huo. Iwapo nitakuwa nakosea naomba nisamehewe. Nimeshindwa kuvumilia, nimeshindwa kukaa kimya. Nimeshindwa kuzungumza na moyo wangu na kisha kubaki nayo kichwani. Hapana nimeshindwa. Naomba ruhusa niandike kuhusu Ruge Mutahaba.

Ndio! Nataka kumzunguzia Ruge Mutahaba. Huyu huyu Bosi Ruge, ni huyu huyu Ruge ambaye wengi wamefanikiwa kupitia kwenye mikono yake. Ruge ambaye ukisikia atazungumza na Watanzania kupitia vyombo vya habari vya Clouds Media Group wote tunasubiri. Tunaka kufahamu anazungumza kuhusu nini. Ruge ambaye tunamuita Scofield wa Tanzania.

Mungu Muumba wa mbingu na ardhi, nipe ujasiri wa kuandika maelezo ambayo yatanyooka na kueleweka kwa haraka. Unapotaka kumzungumzia Ruge Mutahaba lazima kichwa kitulie, lazima uwe na hakika ya kile ambacho unataka kukisema.

Najua na Watanzania wanajua kwa sasa Bosi Ruge yupo kitandani. Ruge anaumwa. Pole kaka. Natoa pole kwako bosi Ruge. Nina hakika Mungu atakunyanyua na kusimama tena. Mungu atakuponya, Watanzania kila mmoja kwa imani yake wanakuombea Ruge upone haraka. Pole kaka, pole rafiki, pole swahiba wa Watanzania.

Taarifa za kuumwa kwako nimezipata kupitia taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu wewe. Sebastian Maganga alitoa taarifa rasmi kuhusu kuumwa kwako.

Na juzi hapa nimemsikia mdogo wako Mbaki Mutahaba, aliyetoa maelezo kuhusu hali yako. Nimemsikia akitoa taarifa ya gharama ya fedha ambayo inatumika kila siku kwa ajili ya matibababu yako.

Ruge narudia tena, sina shaka hata kidogo, afya yako itaimarika na kurejea kwenye majukumu yako ya kila siku. Nikiri sijawahi kukutana na wewe 'Live' tukazungumza au kujadili chochote. Huo ndio ukweli. Hata hivyo kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano, nimekuwa nikikutana na wewe kupitia vyombo vya habari mbalimbali na hasa vile ambavyo unavisimamia vya Clouds Media Group.

Kaka kupitia wewe umenibadilisha kwenye mambo mengi. Umenifundisha maisha ni nini? Ili uishi unatakiwa kufanya nini? Unatakiwa kufanya mambo ya aina gani kufikia mafanikio. Ruge Mutahaba pole kaka. Katika maisha kuna watu ambao najua umekutana nao na kuzungumza nao.

Najua ni wengi lakini idadi yao haizidi wale ambao umewafikia kupitia vyombo vya habari. Sitaki kuzungumzia wasanii wa fani mbalimbali. Sisemi uliokutana nao kwenye jukwaa la fursa ambalo huambatana na tamasha la Fiesta.

Ruge wewe ni mwalimu wa kila kitu. Mwenyezi Mungu aliamua kuweka vitu ndani yako kwa ajili ya wengine. Leo unaumwa, mioyo yetu inaumizwa na kuumwa kwako. Pona kaka. Tunaumia kwa sababu kukosekana kwako katika kipindi hiki yapo baadhi ya mambo hayaendi sawa. Kuna kitu tunaona kinakosekana. Tunamuomba Mungu akupe afya njema na urejee nyumbani.Tunakuhitaji sana.

Amka Ruge wetu, amka Bosi Ruge, amka Scofield wa Tanzania. Najua umekaa kwa muda mrefu kitandani lakini huu ni wakati sahihi kwako kumka tena.Tunakusubiri kaka, tunakusubiri kaka mkubwa. Njoo tuendelee na maisha ya kuijenga Tanzania yetu.

Uwezo wako, maarifa yako, akili yako na ubunifu wako umechangia kwa kiasi kikubwa nchi yetu kupiga hatua kimaendeleo. Unaweza usione moja kwa moja lakini namna ambavyo umetengeneza fursa na Watanzania wakazitumia vema wengi wao wamebadilika. Wamepiga hatua kubwa za kimaendeleo.

Muangalie Nasibu Abdul a.k.a Diamond. Amepita kwenye mikono yako. Wapo wengi ambao wamenufaika kimaisha kupitia akili yako. Njoo kaka tunakusubiri nyumbani Tanzania. Kama binadamu najua huwezi kufanya kila kitu kikafurahisha watu wote lakini ukweli utabaki kuwa wengi wamenufaika kupitia wewe.

Naandika huku nikikumbuka ile kauli mbiu 'Fungulia Dunia kuwa unachotoka'. Kaka Ruge binafsi nimekuwa ninachotaka. Nikwambie kaka Ruge kuumwa kwako, tunaumwa wengi. Huo ndio ukweli.

Mungu amekupa akili ya kujua ufanye nini na kwenye jambo gani. Umekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania wengi. Hakuna kampeni ambayo ulianzisha ikakwama. Nimekumbuka wimbo wa Tuulinde na Amani ambao uliishirikisha wasanii mbalimbali.

Kaka Ruge tumekuzoea kukuona unaumiza kichwa kuhakikisha mambo yanakwenda. Rudi brother tuijenge nchi yetu. Sioni mahali ambapo Ruge ulitaka kufika ukakwama. Kila mahali ambako ulitamani kufika ulifanya hivyo.

Ruge ni wewe ambaye ukiamua jambo liwe linakuwa. Kikubwa zaidi ambacho najifunza kutoka kwako ni uwezo wako mkubwa wa kuchuja kipi uzungumze sasa na kipi uzungumze baadaye.

Tanzania imesimama, inakusuburi uamke kitandani. Inakusubiri urudi. Rudi kaka Ruge, Rudi Bosi Ruge. Njoo tuungane kwenye harakati za maisha yetu ya kila siku.

Kukuzungumzia wewe unaweza kutumia siku, wiki, mwezi na hata mwaka bila kumaliza. Umefanya mengi na natamani kuona ukiendelea kufanya mengi zaidi. Moyo wangu unaumia, machozi yanatoka. Ugonjwa wako unatuliza wengi. Amka ndugu yetu, amka Mzee wa vipaji lukuki.

Nikiri nimefarijika kuona kuna kampeni maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia matibabu yako. Tumeambiwa kwa siku gharama ni kati ya Sh5 mpaka 6 milioni kila siku.

Ruge Mutahaba (kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mh.Paul Makonda
 
Ni wakati wetu Watanzania kuungana kuchangia matibabu yako. Ni matumaini yangu Watanzania tutaendelea kukuombea na kukuchangia kadiri ya uwezo wetu. Familia kwa nafasi yake imeendelea kutimiza majukumu ya kuhakikisha mwanafamilia wao anapata matibabu.

Rais Dk. John Magufuli alikuwa wa kwanza kutoa fedha kwa ajili ya matibabu ya Ruge.

Kaka Ruge siku zote umekuwa mstari wa mbele kuchangia wengine, hivyo nasi tunayo nafasi ya kukuchangia. Nia yetu ni kuona afya yako inakuwa imara. Ulitumia nafasi yako kuwashika mkono Watanzania waliopoteza matumaini, ni wakati wetu nasi kukushika mkono. 

Uliwapa faraja waliokosa faraja, ni wakati wetu kukupa faraja.Tanzania All Stars uliwatumia mara kwa mara pale ulipoona iko haja ya kusaidia jamii iliyo kwenye mataabiko. Ni matumaini yangu Tanzania All Stars nao watakushika mkono.

Kaka Ruge wewe ni bonge la binadamu. Mungu amekupa utu na ubinadamu. Vyote unavyo. Nitakuombea kwa Mungu akuponye maradhi yanayokusibu. Nitakuombea kila sekunde, kila dakika na kila saa.

Nihitimishe kaka Ruge pole kwa kuumwa. Watanzania tunakuombea. Ukiupata ujumbe huu naomba utambue bado tunakupenda na tuko pamoja nawe.

Hata hivyo nikiri tu naumia sana ninaposikia baadhi ya watu wakiwamo wasanii ambao umewajenga kupitia vyombo vyako vya habari, wakitoa lugha za kejeli, dharau na kiburi dhidi yako. Inaumiza sana. Nawasikiliza wee kisha nasema Mungu wahurumie. Bosi Ruge pole. Pole kaka.

Simu: 0713833822.

MADAKTARI BINGWA WA UPASUAJI UBONGO,MGONGO,MISHIPA YA FAHAMU KUTOKA CHINA WATUA MOI

$
0
0
*Lengo ni kutoa mafunzo kwa nadharia,kusimamia kambi ya upasuaji 

Na Khamisi Mussa

MADAKTARI Bingwa watatu wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya Fahamu (Neurosurgeon) kutoka Hospitali ya kimataifa ya Chuo Kikuu cha Peking cha nchini China wamepokelewa MOI ambapo wataendesha mafunzo ya nadharia leo na Februari 25,2019 wataendesha  kambi ya upasuaji.

Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Charles Mkonyi amesema ujio wa madaktari bingwa hao umewezekana kutokana na maagizo yaliyotolewa na RaisDk. John Magufuli ya kuhakikisha Hospitali ya MOI na Chuo kikuu MUHAS zinaingia mkataba wa ushirikinao na Hospitali ya Peking jambo ambalo limetekelezwa chini ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto inayoongozwa na Mwalimu.

Amefafanua katika utekelezaji huo, Taasisi ya MOI na Peking ziliingia mkataba wa ushirikiano katika maeneo ya tiba, utafiti na mafunzo. Mkataba huo ulisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface pamoja na Rais wa Peking Profesa Hongxia Yu 

Ambapo MOI inanufaika katika kuboresha huduma za kibingwa za daraja la juu (Super specialised services) katika maeneo ya upasuaji wa Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Respicious Boniface amesema ujio wao utasaidia kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kwa kuwapa mbinu mpya za upasuaji na hivyo watanzania kupata huduma bora na za kibingwa za Mifupa, Ubongo,Mgongo na Mishipa ya Fahamu bila kwenda nje ya nchi.

“Tunamshukuru sana Rais Dk. Magufuli kwa kutuletea wataalamu hawa, Hospitali yetu ya MOI itanufaika sana kwani wenzetu hawa wana uzoefu mkubwa katika utoaji wa huduma hususani hizi ambazo tunatoa hapa MOI, binafsi nilifanikiwa kuiona hospitali yao kwakweli ni ya viwango vya kimatifa, sisi pia tunatamani kufikia viwango hivyo” alisema Dkt. Boniface.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Mseru amesema ushirikiano huu utakuwa wenye manufaa makubwa kwa Watanzania kwani Hospitali ya Peking ni bora kutokana na uzoefu wa wataalamu wake pamoja na miundo mbinu ya kisasa  hivyo kufanya huduma zake kuwa bora.

“Mwaka jana mimi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI tulipata fursa ya kutembelea hospitali hii ya Peking, kwa kweli ni Hospitali kubwa ,nzuri na yenye huduma bora sana, naamini kupitia ushirikiano huu watashirikiana nasi kuboresha huduma hapa nchini” alisema Prof. Museru.
 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza kuhusu hali ya utoaji huduma wa Taasisi ya MOI katika hafla ya kupokea jopo la madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Prof. Lawrence Mseru akichangia mada katika hafla ya kupokea mdaktari bingwa kutoka kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China
 Profesa Yuanli Zhao kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China akiwasilisha mada kuhusu Hospitali hiyo inavyotoa huduma za Kibingwa za hali ya juu kwa kutumia teknolojia ya kisasa
 Daktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu MOI Dkt. Nicephorus Rutabansibwa akitoa taarifa ya hali ya huduma za matibabu na upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu katika Taasisi ya MOI
 Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti wa Taasisi ya MOI na MNH wakifuatilia jambo katika hafla ya kuwapokea madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China
 Mkuu wa Kitengo cha dharura cha Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt Juma Mfinanga akiwasilisha mada katika hafla ya kupokea madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China
Bwana Nathan Chimoto akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma katika kitengo cha uangalizi maalum cha MOI katika hafla ya kupokea madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Peking cha China. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

Waogeleaji 29 kuiwakilisha Bluefins mashindano ya Isamilo

$
0
0
Muogeleaji wa klabu ya Bluefins Husain Hassanali akichapa maji katika mashindano ya Taliss-IST. Husain ni miongoni mwa waogeleaji watakao shindana katika mashindano ya Isamilo.

Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Klabu inayokuja juu kwa kasi katika mchezo wa kuogelea nchini, Bluefins imetangaza kikosi cha waogeleaji 29 kwa ajili ya kushindana katika mashindano ya  Isamilo yaliyopangwa kuanza ijuu mkoani Mwanza.

Muasisi na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rahim Alidina aliwataja waogeleaji  wa kile kuwa ni Alexis Misabo, Filbertha Demello, Maryam Ipilinga, Viva Pujari, Sarah Shariff, Aminaz Kachra, Fatema Manji, Muskan Gaikwad, Aliyana Kachra, Zainab Moosajee na Lina Goyayi.

Waogeleaji wa kiume ni Moiz Kaderbhai, Idris Zavery, Sahal Harunani, Isaac Mukani, Enrico Barretto, Zac Okumu, Hassan Harunani, Mohamedhussein Imran, Husain Hassanali, Burhanuddin Mustansir na Ayaan Shariff.

Wengine ni Kaysan Kachra, Parth Motichand, Shuneal Bharwani, Sahil Chudasama, Salman Yasser, Christian Fernandes na Revocatus Josephat.

 Alidina alisema kuwa wamewajumuisha waogeleaji wenye umri wa miaka  saba (7) kwa lengo la kuwapa uzoefu wa mashindano kabla ya kushindana katika mashindano ya Taifa yaliyopangwa kufanyika  mwezi Aprili.

Alisema kuwa waogeleaji hao wapo katika maandalizi ya mwisho na wanatarajia kuondoka jijini kabla ya Ijumaa ya wiki hii kwenda kuonyesha uwezo wao.

“Haya ni mashindano ya tatu kwa mwaka huu, tulianza na Morogoro na baadaye Taliss-IST. Yote hayo tumefanya vizuri,” alisema.

Alisema kuwa wanatarajia kufanya vyema katika mashindano hayo pamoja na waogeleaji wao kuweka muda mpya wa kuogelea (PBS).

"Timu yetu imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano hayo ambayo yanaandaliwa na klabu ya kuogelea ya Mwanza (MSC). Tulishinda mwaka 2016 na mwaka 2017 na 2018 tulimaliza katika nafasi ya pili. Mikakati yetu ni kuweka historia mwaka huu,” alisema.

KATIBU WA ACT WAZALENDO NA WENZAKE 162 WAJIUNGA CCM WILYANI MUFINDI ,WASEMA JPM ANATOSHA

$
0
0


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Mkoa wa Iringa,Dkt.Abel Nyamahanga akipokea bendera ya chama cha ACT wazalendo kutoka kwa Ambi Daudi ambae ni Katibu wa ACT wazalendo wilaya ya Mufindi aliyejiunga na CCM leo hii katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi ccm.

……………………………………………………………

Maadhimisho hayo yamefanyika kwa wilayani Mufindi kwa kushiriki katika shughuli za kijamii huku Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akishirikiana na Kaimu katibu wa CCM Mkoa Marco Mbaga,Mkuu wa wilaya ya Mfindi Jamhuri David pamoja,Wabunge pamoja na viongozi wa ccm wilaya ya Mufindi,wanachama na wananchi,wameshiriki madhimisho hayo kwa kuchimba msingi wa ujenzi wa vyoo mbora katika shule ya sekondari Upendo,kujenga daraja,kukabidhi mifuko 49 ya saruji kwa kikundi cha vijana wajasilimali wanaojishughuliisha na utengenezaji wa tofali katika eneo la soko la Mafinga Mjini na shule ya sekondari upendo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo pamoja pia wamezungumza na walimu wa wilaya ya Mufindi.

Katika maadhimisho hayo jumla ya wanachama wapya 162 wamejiunga na chama cha mapiduzi ccm,na kusema kuwa wamekunwa na utendaji mzuri wa Rais Magufuli.PICHA NA ESTA MALIBICHE
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Dkt. Abel Nyamahanga akivalishwa skafu mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Mufindi leo asubuhi.

Badhi ya wanachama wapya waliojiunga na chama cha mapinduzi CCM leo katika maadhimisho ya miaka 42 ya kuzaliwa CCMm,yaliyoadhimishwa wilayani humo.


Kiongozi wa soko la Mafinga akipokea mifuko ya saruji kwa ajili ya kikundi cha vijana wajasiliamali wanaojishughulisha na utengenezaji wa tofali.

Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Iringa Dkt.Abel Nyamahanga pamoja na Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wilium wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya sekondari Upendo iliyopo Mafinga Mjini.

Mbunge wa Mufindi Kusini Mendrad Kigola akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika shule ya sekondari Upendo iliyopo Mafinga Mjini.





Ujenzi wa daraja katika kata ya Upendo Mfinga mjini zikiendelea









MTENDAJI MKUU TEMESA ZIARANI MIKOA YA IRINGA, NJOMBE, MBEYA, RUKWA NA KATAVI

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mojawapo ya mashine iliyopo katika karakana ya wakala huo mkoa wa Njombe wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi, kushoto ni Kaimu Meneja wa Temesa Mkoa wa Njombe Mhandisi Saidi Mawazo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akiichunguza mashine ya kuchongea vipuri vya mitambo mbalimbali wakati akikagua chumba cha kuhifadhia mashine hizo katika karakana ya mkoa wa Mbeya. Kulia ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Sunday Kyungai.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Katavi Mhandisi Stembrige Rushatila katikati akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto eneo la karakana wanapotegemea kupaboresha ili kuongeza uzalishaji wakati wa ziara ya mtendaji mkuu kukagua miundombinu ya karakana za wakala.  

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Iringa Mhandisi Ian Makule kulia akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Y. Maselle mashine ya kisasa ya kutoa na kubadilishia matairi ya magari iliyopo katika karakana ya mkoa huo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TEMESA mkoa wa Iringa mara baada kuzungumza nao na kusikiliza changamoto wanazokutana nazo katika utendaji kazi. Kulia kwake ni Meneja wa TEMESA Mkoani humo Mhandisi Ian Makule.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle akitoa msisitizo wakati akizungumza na wafanyakazi wa wakala huo mkoani Rukwa alipokua ziarani kukagua utendaji kazi. Pembeni yake ni Meneja wa Mkoa huo Mhandisi Fidol Tumbi.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)

Wasabato Bagamoyo watakiwa kushirikiana

$
0
0

Na Sophia Mtakasimba , Bagamoyo

WAUMINI wa kanisa la Waadventista Wasabato Bagamoyo wametakiwa kufanya kazi ya kushirikiana ili kuweza kusaidia kazi ya Mungu kusonga mbele na kuwafikia  watu wengi.


Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Mashariki kati mwa Tanzania , Mchungaji Joseph Mngwabi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kanisa jipya la kisasa la Waadiventista wasabato Bagamoyo uliofanyika jana (jumamosi) wilayani Bagamoyo mkoani Pwani .


“Mkifanya kazi kwa kushirikiana na kwa lengo moja ,mtafanikiwa sana kufikia malengo mliyojiwekea na hii itasaidia sana kufanya kazi ya Mungu isonge mbele”alisema Mchungaji Mngwabi.


Awali katika hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi Mchungaji wa mtaa wa Bagamoyo Mch.Melkizedeki Wanjala, alisema kuwa kanisa la Waadventista Wasabato Bagamoyo lilitengwa kuwa Kanisa kutoka Kanisa mama la Mwenge mnamo  mwaka 1995,ambapo hadi kufika mwaka 2001  Kanisa lilifanikiwa kuwa wa jengo lake la kuabudia eneo la Tandika-Bagamoyo. Lakini kufikia mwaka 2013 idadi kubwa ya waumini iliongezeka,hali hii ilipelekea jengo la awali kutotosha ,hivyo kuwa na hitaji la kuwa na Kanisa kubwa zaidi.


Akizungumzia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa Mchungaji Wanjara amesema kuwa jengo hilo litagharimu jumla ya Shilingi za kitanzania Milioni Mia Nne na Hamsini (450,000,000) hadi kukamilika kwake ,hivyo amewataka washiriki kushirikiana kwa hali na mali  ili kukamilisha ujenzi huo huku akinukuu Maandiko Matakatifu kutoka kitabu cha Kutoka 25:8 yanayosema “nao wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao.

Askofu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo la Mashriki Kati mwa Tanzania ,Mchungaji Joseph Ngwambi(Kushoto) , akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kanisa la Waadventista wa Sabato Bagamoyo, Kulia ni wa Jimbo la mashariki kati mwa Tanzania Ndg.Enock Rabieth .


Pep Guardiola: Ushindi wa Manchester United dhidi ya Liverpool utaimarisha ushindani wa EPL

$
0
0

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatumai kwamba Manchester United itailaza Liverpool siku ya Jumapili ili timu yake kupanda juu katika kilele cha jedwali.

City inelanga kulihifadhi kombe la Carabao kwa kuishinda Chelsea katika uwanja wa Wembley baada ya United kucheza dhidi ya Liverpool ambao wako sawa kwa pointi na City katika uwanja wa Old Trafford.

''Ni wazi kwamba itakuwa bora iwapo United itapata ushindi'' , alisema Guradiola.''Lakini sasa ni mwezi Februari na ni ndoto kuzungumzia kushinda mataji manne''.

City ilikuwa nyuma kwa pointi saba mnamo tarehe 19 mwezi Januari lakini mchezo mzuri wa kikosi cha Guardiola umemfanya kocha huyo kuwa na matumaini zaidi ya kuweza kushinda makombe manne ya ligi kuu nchini Uingereza.

Mbali na kutetea mataji yao ya ligi ya Uingereza pamoja na kombe la Carabao City imefika katika hatua ya robo fainali ya kombe la FA dhidi ya against Swansea na ilichukua uongozi wa 3-2 dhidi ya Schalke nchini Ujerumani katika mkondo wa kwanza wa kombe la vilabu bingwa Ulaya wiki hii.

Guardiola ambaye ametaja makombe hayo matatu kuwa furaha kubwa, alisema kuwa tuko katika fainali na tunapofika fainali itakuwa mechi muhimu zaidi msimu huu.

''Pengine kwa United au Liverpool kombe la ligi sio muhimu kwa sababu wana mataji mengi sana lakini sio kama sisi''.

''Kulihifadhi kombe hilo itakuwa kitu muhimu, kushiriki katika fainali ni vyema''.''Niulize swali hili kuhusu kushinda mataji manne mnamo mwezi Aprili ama Mei na nitajibu swali lako. Siwezi kukudanganya mwezi Mei''.

"lakini sasa mwezi Februari na haiwezekani kuzungumzia hilo. ni kama kiwiliwili .''Ni mara ngapi nchini Uingereza ambapo tmu moja imeshinda mataji manne msimu mmoja''.

''Musituwekee shinikizo hiyo . Historia ya Alex Ferguson haukuweza kufanya hivyo ''.''Liverpool miaka ya 80 walishinda mataji mengi ya kombe la vilabu bingwa lakini haikuweza kufanya hivyo''.

DKT MPANGO AZIONYA TAASISI ZA SERIKALI ZISIZOTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI KUKUSANYA MAPATO

$
0
0


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akitoa ufafanunuzi wa kero zilizowasilishwa na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali wakati wa kikao na Wafanyabiashara hao, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akiwakaribisha Waheshimiwa Mawaziri, Wakuu wa Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali (hawapo pichani), waliohudhuria kikao kilicholenga kutatua kero mbalimbali zinazokwamisha biashara mkoani humo kilichofanyika Jijini Arusha.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akisalimiana na Wenyeviti wa Taasisi Binafsi waliohudhuria mkutano uliowakutanisha Mawaziri mbalimbali, Wakuu wa Taasisi za Serikali na Wafanyabiashara uliolenga kukuza biashara mkoani humo, kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiorodhesha baadhi ya hoja zilizowasilishwa na Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali wakati wa kikao na Wafanyabiashara hao, kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha, Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki.
Viongozi mbalimbali wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa kikao kilichowajumuisha viongozi hao, Wakuu wa Taasisi za Serikali, Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha.

…………………………………………………………………………..

Na Josephine Majura na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amezitaka Taasisi zote za Serikali kutumia kikamilifu mfumo wa malipo wa Serikali wa kielektroniki (GePG), ili kutimiza azma ya Serikali ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za Umma.

Dkt. Mpango ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wafanyabiashara wa sekta ya madini, utalii, mahotel na viwanda wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

Akijibu hoja na kutolea ufafanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyabiashara hao, Dkt. Mpango alisema Serikali ilishatoa maagizo kwa Taasisi zote za Serikali kuwa malipo yote yafanyike kwa kutumia mfumo wa malipo ya Serikali, na endapo itatokea Taasisi yoyote itashindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali iliziagiza Taasisi zote kuanza kutumia mfumo wa malipo ya Serikali ifikapo mwezi Juni, 2019, na nina agiza kuanzia leo mwananchi yeyote asikubali kulipa malipo yoyote yasiyotumia mfumo huu” alisisitiza Dkt. Mpango.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki alisema Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.

Mkutano huo uliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, kwa lengo la kutatua kero mbalimbali za Wafanyabiashara wa Mkoa huo, na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Joseph Kakunda, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Kangi Lugola, Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu ya Rais Mazingira Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Eng. Isack Kamwele, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu, na Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mhe.Anthony Mavunde.

ATCL ILIPOZINDUA SAFARI ZAKE ZA ZAMBIA NA ZIMBABWE

$
0
0
Wageni wakisubiriwa kushuka katika ndege hiyo ya ATCL 
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhandisi Isack Kamwele akisalimiana na Waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira, mara baada ya ndege aina ya air bus A220-300 kutua kwa mara ya kwanza katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Robert Gabriel Mugabe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza safari katika nchi za Zambia na Zimbabwe.
Kaimu waziri wa uchukuzi wa Zambia Mutolwe Kafwaya akikata keki maalum juzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kenneth Kaunda Lusaka Zambia wakati wa uzinduzi rasmi wa safari za ndege za Air Tanzania katika nchi hiyo kuanzia Feb.22,kulia ni waziri wa Uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Izack Kamwelwe,na kushoto ni balozi wa Zambia nchini Tanzania Benson Chali. 
Waziri wa Mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhurua hafla ya uzinduzi wa safari ya ya shirika la ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe Harare Zimbambwe juzi kulia ni baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo akiwemo waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Isack Kamwele.


************

Shirika la ndege la Tanzania ATCL limezindua rasmi safari za ndege katika nchi za kusini mwa bara la afrika zikiwemo Zambia na Zimbabwe ambapo imeelezwa kuwa itachangia kuchagiza maendeleo ya kiuchumi, baina ya nchi hizo tatu na itafungua milango ya biashara lakini pia kupunguza gharama,muda na usumbufu ambao abiria kutoka katika nchi hizo walikuwa wakiupata kwani walilazimika kuzunguka mpaka nchi jirani ili wafike Zambia au Zimbabwe.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati ndege aina AIRBUS A 220-300 ikiruka kwa mara ya kwanza kutoka kiwanja cha ndege cha kimataifa cha JKN Dar es salaam kuelekea katika nchi hizo na kutua nchini Zimbabwe na Zambia.

Uzinduzi rasmi wa ndege hiyo umefanyika katika viwanja viwili tofauti kikiwemo kile cha Robert Gabriel Mugabe Harare- Zimbabwe na baadae uwanja wa Kenneth Kaunda Lusaka- Zambia, huku abiria hao wakipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza katika sekta ya anga ambayo zaidi ya miaka ishirini ilionekana kuyumba.

Baadhi ya abiria Mahenye Muya mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo kutoka Arusha alisema kuwa kuzinduliwa kwa ndege hiyo kumewasaidia kupunguza gharama na mzunguko usiokuwa wa lazima ambao awali ili kufika Lusaka walilazimika kupitia Ethiopia. 

“Kutoka Tanzania mpaka Harare ni kama saa 1.dakika 50 na Lusaka ni saa 1.dakika 45 muda wa safari umepungua kwa saa tano,unajua sisi wafanyabiashara muda ni pesa kwa kutumia ATCL nimesave muda na pesa”alisema Muya

Waziri wa uchukuzi na mawasiliano mhandisi Izak Kamwelwe amesema shirika hilo limedhamiria kujiimarusha katika sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya ndege lakini pia kuhakikisha linafika katika nchi mbalimbali barani Afrika na bara la Asia.

“hivi karibuni tutaanza kwenda India ambayo ni mwisho wa mwezi Machi,na mwezi April mwishoni au Mei tutaanza kusafiri kwenda China kwa sababu tupo katika hatua nzuri ya mazungumzo.”alisema Kamwelwe.

Alisema serikali itaendeleza na wimbi la kununua ndege ambapo mwezi November itapokea ndege nyingine aina ya Dreamliner na Bombadier hivyo kufanya serikali ya Jamhuri ya muungano kuwa na ndege 11.

Akizungumzia namna shirika hilo lilivyojipanga katika kutoa huduma hiyo ya anga karika nchi mbalimbali barani Afrika Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege nchini Mhandisi Ladislaus Matindi alisema ATCL imejipanga kutoa huduma safi na ndege zake ni za uhakika.“ATC imejipanga kulihudumia soko hilo kwa hiyo hatufanyi majaribio wala hatufanyi kitu tusichokuwa na uhakika nacho tunahakika na hili soko”alisema Matindi

Kwa upande wake waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira na kaimu waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia Kafwaya Mutotwe wamesema kuanza kwa safari hizo kutaendeleza kuimarisha uhusiano uliopo wa muda mrefu uliowekwa na waasisi wa mataifa hayo katika Nyanja mbalimbali.

“Leo historia inaandikwa tena baada ya miaka ishirini ndege za Tanzania kugusa ardhi ya Zimbabwe naamini uzinduzi huu unatarajiwa kufungua furs azote kuanzia kiuchumi,na raia wetu kufurahia mawasiliano ya uhakika kufikia vivutio vya utalii na biashara”alisema Mupfumira

Ndege hiyo aina ya AIRBUS A 220-300 ya Shirika la ndege la Tanzania itakuwa ikisafiri mara tatu kwa wiki kuelekea katika nchi za Zambia na Zimbabwe ambapo mpaka sasa ndege hizo zitakuwa zikifika katika nchi nne za Afrika ikiwemo Uganda na Burundi.

MAKAMU WA RAIS ASEMA UPATIKANAJI WA MAJI KALIUA KUFIKIA ASILIMIA 50 MWAKA 2020

$
0
0

NA TIGANYA VINCENT

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itahakikisha tatizo la maji wilayani Kaliua linatafutiwa ufumbuzi ili kuwatua ndoa kichwani wakinamama.

Alisema ifikapo mwaka 2020 hali ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kaliua utaongezeka kutoka asilimia 25 za sasa na kufikia asilimia 50

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua ikiwa ni siku nne ya ziara yake mkoani Tabora .

Alisema Serikali itahakikisha inachimba visima na kujenga mabwawa katika maeneo ambayo maji kutoka Ziwa Victoria yatakaposhindwa kufika ili kuwaondelea shida na upatikanaji wa maji safi na salama wananchi.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ametoa onyo kwa watu ambao wameanza kuingia katika hifadhi za mistu na kuendesha uharibifu ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti na kuendesha kilimo ndani ya hifadhi.

Alisema tamko la Rais wa Jamhuri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli lilihusu vijiji ambavyo vilikuwa tayari ndani ya maeneo ya hifadhi na vilivyo ainishwa na sio kuanzisha makazi mapya ndani ya hifadhi.

Makamu wa Rais alisema mtu akayeingia katika Hifadhi atachukuliwa hatua za kisheria na kuwataka Watendaji mbalimbali kuhakikisha wanawaondoa watu ambao wameanza kuvamilia mistu na kuongeza kuwa Rais Magufuli hakusema watu waanze kuingia katika hifadhi ya mistu.

Wakati huo huo Makamu wa Rais alisema ifikapo mwaka 2023 vijiji vyote nchini vitakuwa na umeme. Aliwataka wananchi kutumia upatikanaji wa umeme katika masuala ya maendeleo ya viwanda vya kati na vikubwa.


SERIKALI HAITOMUACHA SALAMA MTUMISHI YEYOTE ATAKAEKULA FEDHA ZA UMMA KWA MASILAHI BINAFSI

$
0
0


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Baadhi ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani), wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa akimueleza Dkt. Mwanjelwa hatua alizochukua dhidi ya changamoto ya ubadhirifu wa fedha za umma wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF Wilayani Bagamoyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa wakisikiliza maelezo ya kiutumishi toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bw. Shabani Milao wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi wa Halmashauri hiyo chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza nidhamu katika matumizi ya fedha za umma kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji.

…………………..

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amesema Serikali haitosita kumchukulia hatua kali za kinidhamu na kisheria mtumishi wa umma yeyote atakaebainika kula fedha za umma ambazo zinatolewa na Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, mara baada ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo ili kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa umma wote nchini kuwa waaminifu na waadilifu katika kutumia vema fedha za umma ambazo malengo yake ni kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanaoishi katika maeneo ya vijijini.

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa wito kwa watumishi wa umma kubadilika na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu, akitoa mfano wa fedha zaidi ya shilingi milioni 457 ambazo zilitolewa na Serikali kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambazo zilitumika kinyume na utaratibu, na kuongeza kuwa, halmashauri hiyo ililazimika kuzirejesha baada ya Serikali kubaini ubadhirifu huo na kuamuru zirejeshwe.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Mhe. Zainab R. Kawawa amemueleza Dkt. Mwanjelwa kuwa, baada ya kuwachukulia hatua watumishi wabadhirifu katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, mapato ya Halmashauri hiyo yaliongezeka kutoka milioni 400 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2018 na kufikia milioni 760 kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba, 2018 na kuongeza kuwa, kutokana na hatua iliyochukuliwa anaamini mapato ya Halmashauri hiyo yataongezeka na inawezekana yakafikia bilioni moja katika kipindi hiki cha kuanzia mwezi Januari hadi Machi, 2019.

Mhe. Kawawa ameahidi kuendelea kuwashughulikia ipasavyo watumishi wote wanaohujumu mapato ya Serikali katika wilaya yake kwani atahakikisha mapato yanaongeza, na kufafanua kuwa pasipo shaka wapo watumishi wachache wanaohujumu vyanzo vya mapato na kufanya ubadhirifu hivyo amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuendelea kuchukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria kwa watumishi wote waliobainika kujihusisha na kuhujumu mapato na kushiriki katika ubadhirifu wa fedha.

Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) anaendelea na ziara ya kikazi kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma Mkoani Pwani, mpaka sasa ameshakutana na watumishi katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ambapo amewataka watumishi hao kuwa waadilifu, kufanya kazi kwa bidii, maarifa na kuzingatia weledi katika utendaji kazi.

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI SONGWE

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kwa walimu wa halaiki mara baada ya kukagua na kujionea hatua za awali za maandalizi ya vijana wa halaiki.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi (wa pili kutoka kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipotembea Uwanja wa Mlowo kujionea hali ya maandalizi. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Mhandisi Tanu Deule akitoa maelezo kuhusu Uwanja kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (watano kutoka kushoto) alipotembelea na kukagua hali ya Uwanja na miundombinu mbalimbali katika uwanja wa Mlowo zitakapofanyika Sherehe hizo(mwenye miwani) ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela. (Wa tatu kutoka kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)






Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Viongozi na watendaji wa Mkoa wa Songwe mara baada ya kuwasili Mkoani hapo wakati wa ziara yake ya kukagua maandalizi hayo Mkoani humo. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela akitoa taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipowasili mkoani humo kukagua maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipitia kwa makini ripoti ya maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alipowasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe kupokea taarifa hiyo. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Bw. Elinico Mkola.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya maandalizi alipofanya kikao kifupi na baadhi ya Wanakamati ya Maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Songwe. (Kushoto) ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Songwe Bw. Elinico Mkola.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Songwe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizopo Vwawa, Mkoani Songwe.
Vijana wa Halaiki wakitengeneza umbo la Mlima Kilimanjaro kuashiria kupandisha Bendera ya Taifa katika mlima Kilimanjaro wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipotembea vijana hao katika shule ya msingi ya Ichenjezya ambapo vijana hao wa halaiki wanafanya maandalizi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na vijana wa halaiki mara baada ya kuwasili shule ya msingi ya Ichenjezya iliyopo Vwawa kujionea maandalizi ya Vijana hao.


……………………….

Na; OWM (KVAU) – Songwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara na kukagua maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru zinazotarajiwa kufanyika tarehe 2 Aprili, 2019 Mkoani Songwe.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye kamati ya Maandalizi, Waziri Mhagama alieleza kuridhishwa na hatua za awali za maandalizi na kuipongeza kamati ya Mkoa kwa kusimamia vyema na kuratibu shughuli za maandalizi hayo.

“Niwapongeze kwa hatua hizi mlizofikia katika kuhakikisha shughuli hii ya kitaifa inafana, maana maandalizi bora yataleta heshima kwa Mkoa katika kufanikisha jukumu hilo muhimu, hivyo mzingatie masuala yote ya msingi na kufanya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Songwe una kuwa wa kihistoria,” alisema Waziri Mhagama

Aliongeza kuwa, Mbio za Mwenge wa Uhuru zinahistoria kubwa katika Taifa letu, ikiwa ni mwaka wa 55 sasa tunaadhimisha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa na ni mwaka wa 27 toka kuanzishwa mfumo wa vyama vingi ikiwa ni kielelezo tosha cha kukua kwa demokrasia nchini.

Vilevile ni miaka 20 ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere hivyo ni vyema vijana wakatambua historia ya Taifa na kujifunza falsafa za Baba wa Taifa kwa kuwa na umoja, mshikamano, uzalendo, kujitolea na zaidi kuchochea maendeleo ya nchi.

“Kupitia shughuli hii ya kitaifa vijana wanapaswa kutumia fursa hiyo kuelewa historia ya Taifa lao pamoja na Mwenge wa Uhuru kama kielelezo muhimu cha Utaifa,” alisisitiza Mhagama

Hata hivyo, Mhe. Mhagama aliusihi uongozi wa Mkoa kutumia nafasi hiyo kutangaza vivutio vya utalii, fursa za kiuchumi na shughuli mbalimbali zilizopo ndani ya mkoa wa Songwe. Pia aliwataka waendelee kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali (Mst.), Nicodemus Mwangela, alipokea maelezo yaliyotolewa na kuahidi kusimamia shughuli zote za maandalizi kwa ufanisi na kukamilisha ndani ya muda uliopangwa.

“Nikuhakikishie maandalizi yataendelea kwa kasi na yatakamilika kwa wakati ili kuwawezesha wananchi wa Mkoa wa Songwe wanashiriki katika tukio hilo muhimu na kuitumia fursa hiyo ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kujitangaza kama Mkoa,” alisisitiza Mhe. Mwangela

WAZIRI MKUU ATEMBELEA HOSPITALI YA KIBONG’OTO

$
0
0
Aweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara, afarijika kuona lengo la Rais likitekelezwa

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa maabara ya afya ya jamii kwenye Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi ya Kibong’oto na kusema kuwa amefarijika kuona lengo la Rais Dkt. John Magufuli katika sekta ya afya likitekelezwa.

Amesema Rais Dkt. Magufuli anataka kuona watanzania wote wanapata huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo za afya karibu na makazi yao, hivyo wananchi hawana budi kuendelea kumuamini na kushirikiana na Serikali yao.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 24, 2019) alipotembelea hospitali hiyo ya Kibong’oto iliyoko kwenye mtaa wa Mae kata ya Ivaeny wilayani Siha akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro. 

“Rais wetu Dkt. Magufuli ana nia thabiti ya kuwahudumia Watanzania wote walioko katika maeneo yote nchini. Wananchi wote wanapata huduma sawa bila ya ubaguzi wa aina yoyote, hivyo endeleeni kuiamini Serikali yenu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema wilaya hiyo imepewa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuhusu upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kwa sasa umefikia asilimia 95.

Awali, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kibong’oto Dkt. Riziki Kisonga alisema ujenzi wa jengo hilo utafanyika kwa awamu tatu, awamu ya kwanza itagharimu sh. bilioni 2.183 na ilianza Septemba 2018 na inatarajiwa kukamilika Julai mwaka huu.

Dkt. Kisonga alisema jengo hilo ni la ghorofa tatu zenye pande mbili pacha, upande wa kwanza ni kwa ajili ya kazi za maabara kwa uchunguzi wa vimelea hatari na hatarishi sana na virusi vinavyosababisha milipuko ya magonjwa kama marburg, ebola, chikungunya na dengue.

Alisema mradi huo mpaka kukamilika unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 8.86, ambazo zinaonekana kuwa zipo juu kutokana na uhitaji wa kitaalamu wa uwekaji wa mifumo thabiti ya kuchuja hewa ambayo itahimili kazi zinazotarajiwa kufanyika.

“Umuhimu wa maabara hii ni kusaidia kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa ambukizi yakiwemo ya kifua kikuu na magonjwa mengine yasiyoambukiza katika ubora unaotambulika kimataifa.”

Dkt. Kisonga alisema maabara iliyopo hospitalini hapo kwa sasa imepata ithibati ya kimataifa ya kufanya vipimo vya ngazi ya daraja la pili, hivyo baada ya kukamilisha ujenzi huo watakuwa na uwezo wa kufanya vipimo vya ngazi ya daraja la tatu.

Alisema maabara hiyo itakapokamilika watatoa huduma za uchunguzi wa magonjwa yanayoibuka na mapya, ambayo ni hatarishi kwa usalama wa Taifa na Kimataifa hasa tatizo kubwa la usugu wa vimelea kwa dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali.

Ujenzi Mji wa Serikali Mbioni Kukamilika

SERIKALI INATAMBUA NA KUTHAMINI MCHANGO WA WATUMISHI WA UMMA KATIKA KULETA MAENDELEO YA NCHI

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akisalimiana na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kabla ya kuingia katika ukumbi wa halmashauri hiyo kuzungumza na watumishi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi (hawapo pichani) katika kikao kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo. Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, Bi. Rehema Madenge na kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga akitoa neno la shukrani baada ya kikao kazi kati ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) na watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Urasimishaji Ardhi ni Kichocheo cha Maendeleo Endelevu -MKURABITA

$
0
0

Mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) Bi Seraphia Mgembe akionesha hati milki ya kimila ya kumiliki ardhi na kusisitiza umuhimu wa wananchi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kuchukua hati milki hizo baada ya kurasimisha mashamba yao ili waweze kujiletea maendeleo.
Meneja Urasimishaji Ardhi Vijijini kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) Bw. Antony Temu akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi waliorasimisha mashamba yao katika kijiji cha Membe Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.



Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Chamwino Bi Juliana Mtolera akisisitiza jambo wakati wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 katika kijiji cha Membe Wilayani humo wakati wa mafunzo yakuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha kwa tija, mafunzo hayo yameandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania ( MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya hiyo.



Sehemu ya wakulima zaidi ya 100 wa kijiji cha Membe Wilayani Chamwino wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha kwa tija baada ya kurasimisha mashamba yao.

……………………………………………………………………………………………………

Na; Frank Mvungi, Dodoma

Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA ) kwa kuwawezesha wananchi kurasimisha ardhi wanazomiliki yakiwemo mashamba na kupatiwa hati za kimila za kumiliki ardhi.

Ni vyema wananchi Wilayanis Chamwino na maeneo mengine ambayo ymeshanufaika na urasimishaji wakatambua kuwa jukumu lao sasa ni kutumia fursa zitokanazo na urasimishaji kujiletea maendeleo.

Sasa wananchi wote mlionufaika na urasimishaji tambueni kuwa Serikali imewekeza kwenu kwa kuwajengea uwezo hali inayowawezesha kujikwamua na kujiletea maendeleo ikiwemo kupata mikopo katika Taasisi za fedha kama mabenki kupitia hati za kimila za kumiliki ardhi.

Dhamira hii safi ya Serikali inapaswa kuungwa mkono na wananchi wote ambao wameshanufaika na urasimishaji uwe wa ardhi au biashara, nalisema hili kwa kuwa nimeshudia hivi karibuni Mratibu wa MKURABITA Bi Seraphia Mgembe akihamasisha wananchi wa Wilaya ya Chamwino na maeneo mengine hapa nchini kujitokeza kuchukua hati zao ambazo ni ukombozi wa kiuchumi na mwarobaini wa umasikini kwa wananchi wanyonge.

Uhamasishaji huu nimeushuhudia ukifanyika mara kwa mara na hata wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 na viongozi 10 wa Kijiji cha Membe, Wilayani Chamwino Bi Mgembe alionekana kuguswa na suala la wananchi kuchelewa kuchukua hati zao za kimila baada kurasimishiwa mashamba yao, akionesha shauku yake ya kutaka kuona wananchi wanajikwamua kiuchumi kupitia hati hizo.

Kutokana na urasimishaji huo ambao umefanyika katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma jumla ya mashamba 1145 yalipimwa katika Kijiji cha Membe ambapo hatimiliki 1000 zimeweza kuandaliwa na sehemu kubwa ya hati hizo hazijachukuliwa na wananchi na kuzitumia katika suala zima la kujenga uchumi na kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo alizeti.

Dhamira hii njema ya Serikali inatekelezwa na Ofisi ya Rais- MKURABITA ambayo imejipambanua kwa vitendo kutokana na kutekeleza dhana yakujenga uchumi shirikishi au jumuishi unalenga kuwawezesha wananchi kupitia rasilimali zilizopo katika maeneo yao ikiwemo ardhi.

Hati hizo ziwe chachu kwa wananchi kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono nia hii njema ya Serikali ya kuwaletea maendeleo; katika hili ni wazi kuwa wananchi wa Wilaya ya Chamwino wamepata ukombozi wa kiuchumi ambapo sasa wanapaswa kuunga mkono juhudi hizi kwa kuchukua hati hizi.

Aidha, jambo jingine muhimu ni wananchi wote ambao tayari maeneo yao yamepimwa na kupatiwa hati ni kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuendana na dhana ya ujenzi wa viwanda ambavyo vinategemea malighafi kutoka katika sekta ya kilimo.

Aidha, faida za urasimishaji ni kama ; kuhakikisha usalama wa milki kwa kuiongezea thamani ardhi husika, Kuweza kujipatia mikopo na kuwawezesha wamiliki kuingia ubia katika uwekezaji kwenye ardhi na kilimo kupitia wadau mbalimbali.

MKURABITA imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa dhamira ya Serikali kuwezesha wananchi kiuchumi inatimia kwa wakati kutokana na mkazo inaouweka katika kuwezesha wananchi kurasimisha mashamba yao, viwanja na biashara zao katika maeneo mbalimbali yaliyofikiwa na mpango huu.

Ujenzi Mji wa Serikali Mbioni Kukamilika

$
0
0
  Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa tenki la maji ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
 Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
 Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara ya Fedha na Mipango linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
 Muonekano wa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora katika mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma. 
  Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiongea na mafundi katika jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.


 Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiongea na Mkandarasi na Mshitiri katika jengo la Wizara ya Kilimo linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.

MAKAMU WA RAIS AIPONGEZA HALMASHAURI KALIUA KWA KUWAINUA WANAWAKE,VIJANA NA WALEMAVU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018.

Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo leo wakati akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kolimba, Kaliua moani Tabora. 

Aidha katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameridhia kuondolewa mara moja kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kaliua Mhandisi Fikiri Samadi baada ya kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.5.

“Ziara hizi ni ziara za kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo hivyo yeyote atakayekwamisha atachukuliwa hatua mara moja”alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema wilaya ya Kaliua ni mfano wa kuigwa kwa kujenga jingo la upasuaji pamoja na wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuchukua vitanda 24 katika kituo cha afya Kaliua kwa mapato yao ya ndani pamoja na michango kutoka chama cha msingi Nsungwa ambapo mpaka kukamilika wametumia shilingi 159,703,199.98.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri TAMISEMI amesema vikundi vinavyopewa mikopo na Halmashauri lazima virejeshe mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengine akizungumzia kwa wilaya ya Kaliua peke yake ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa mpaka sasa zimerudishwa milioni 89 tu.

Akizungumzia suala la uchaguzi katika kata 3 za Igombe Mkuluu, Mirambo na Kanindo zilizopo katika jimbo la Ulyankulu, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara amesema lazima usalama wa Taifa uzingatiwe na upewe kipaumbeke kwani kwenye maeneo hayo kuna waliopewa uraia na kuna wakimbizi hivyo Serikali itakapojiridhisha wanaweza shiriki katika uchaguzi ujao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya kutengeneza sabuni bora kutoka kwa Mwenyekiti wa kikundi cha Wazalendo Ndugu Imani Matabula wakati wa maonyesho yua wajasiriamali katika viwanja vya Kolimba wilaya ya Kaliua mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kaliua na Waziri wa Zamani katika Wizara mbali mbali Profesa Juma Kapuya(kushoto) mara baada ya kumaliza kuhutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kushoto) kabla ya kuhutubia  wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

VIJANA MWANZA WAKUTANA KWENYE BONANZA LA MICHEZO

$
0
0
Vijana wametakiwa kutokata tamaa,kuondoa hofu na kuwa makini katika maisha licha ya changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ili waweze kufikia ndoto zao za maisha. 


Ushauri huo umetolewa Februari 23,2019 na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa Bonanza la Michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza. 

Klabu hizo zinasimamiwa na asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC). 

Akifungua Bonanza hilo,lililofanyika katika Viwanja vya Lessa Garden Hotel jijini Mwanza, Olotu aliwashauri vijana kujiamini na kutokubali kukata tamaa lakini pia kuwa wasikivu wanapoelekezwa mambo ya msingi katika maisha. 

“Kupitia michezo hii mmefurahi pamoja, mmefahamiana,mmepata marafiki wapya na kujifunza mambo kadha wa kadhaa kupitia michezo,naomba muendelee kujiamini na kuzingatia ushauri mnaopewa ili mtimize ndoto zenu, ni vyema pia kuwa wamoja na kuendelea kushirikiana”,aliongeza Olotu. 

Kwa upande wake, Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona alisema AGPAHI imekuwa ikiandaa michezo kwa watoto na vijana ili kuwapa msaada wa kisaikolojia kwani asasi hiyo inajali watoto ili wakue na kuishi katika matumaini chanya. 

Alisema bonanza hilo limeshirikisha vijana balehe zaidi ya 50 kutoka kwenye vituo vya tiba na matunzo kwenye halmashauri za wilaya mkoani Mwanza lengo likiwa ni kujifunza kwa njia ya michezo kuimarisha afya zao. 

Miongoni mwa michezo iliyofanyika wakati wa bonanza hilo ni kukimbia mita 100,mbio za magunia,kabute,landrover na mchezo wa kufunga vitambaa usoni. 
Muuguzi mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akifungua bonanza la michezo lililokutanisha vijana kutoka kwenye klabu za vijana kutoka halmashauri za wilaya za Misungwi,Nyamagana,Sengerema na Kwimba mkoani Mwanza - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akiwahamasisha vijana kuwa wamoja na kushirikiana sambamba na kutokata tamaa ili wafikie ndoto zao za maisha. Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona.Wa kwanza kushoto ni Pudensia Mbwiliza na Joan John ambao ni Walimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akielezea malengo ya bonanza la michezo ambayo ni kuburudika na kujifunza kwa njia ya michezo. 
Vijana wakicheza kwa kushika vichwa wakati wa bonanza hilo. 
Mchezo wa Landrover ukiendelea. 
Vijana wakiunga mstari kumfuata mshindi katika mchezo wa karatasi,jiwe na mkasi. 
Vijana wa kike wakichuana kwenye mbio za mita 100. 
Mchezo wa mbio za mita 100 ukiendelea kwa vijana wa kiume. 
Mbio za magunia zikiendelea.
Mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo : Kulia ni Mwalimu wa vijana Douglas Renatus kutoka hospitali ya rufaa Bugando akitoa maelekezo kwa washiriki juu ya mambo ya kufanya huku wamefungwa vitambaa usoni. 
Washiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo wakiendelea kutembea huku wakipewa maelekezo kutoka kwa vijana waliowazunguka. 
Mshiriki wa mchezo wa kuvuka vikwazo ili kuweza kufikia malengo baada ya kuvuka kikwazo namba mbili akichukua zawadi ya limao. Watu wazima nao hawakubaki nyuma katika michezo hiyo ili kuwatia moyo vijana. 
Mwalimu wa vijana Pudensia Mbwiliza akiwasisitiza vijana kutokata tamaa na kuepuka hofu katika maisha.
Mwalimu wa vijana Joan John akiwafurahisha vijana.
Vijana wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea. 
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza,Cecilia Yona akitoa mwongozo wa kugawa zawadi kwa washindi wa michezo mbalimbali iliyofanyika pamoja na zawadi za jumla kwa washiriki. Wa kwanza kushoto ni Nicholaus Michael na Douglas Renatus ambao ni walimu wa vijana kutoka hospitali ya rufaa Bugando. Kulia ni Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu. 




Mshindi wa mbio za mita 100 kwa vijana wa kike akipokea zawadi ya saa kutoka kwa mgeni rasmi Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu. Wa kwanza kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza,Joan John akitaja majina ya washindi katika michezo.Wa pili kutoka kulia ni Mwalimu wa vijana kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando Jijini Mwanza, John Shayo. 




Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu akikabidhi zawadi ya saa kwa mshindi wa mbio za mita 100 kwa kundi la vijana wa kiume. 




Kijana akiangalia zawadi ya saa baada ya kukabidhiwa. 




Kijana akishikana mkono na Muuguzi mkunga mstaafu aliyebobea katika fani ya ushauri nasaha, Gladness Olotu wakati wa zoezi la kugawa zawadi za jumla kwa washiriki wa bonanza. 




Vijana wakiendelea kupokea zawadi za chupa za maji. 




Picha ya pamoja washiriki wa bonanza la michezo. 




Washiriki wa bonanza la michezo wakiwa katika picha za vurugu. 


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

BENKI YA NMB YAWATAJA 6 WANAOKWENDA KULA BATA DUBAI

$
0
0

  BENKI ya NMB imewatangaza wateja watatu ambao wameibuka washindi katika droo ya mwisho ya kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' maarufu kwa jina la 'MastaBata'.

Wateja hao watatu katika shindano hilo, EINSTEIN STEPHEN MAGEBO, SIMON CHACHA, pamoja na NUIS PAUL KASAMBALA wakiwa na wenza wao wanatarajia kusafirishwa na Benki ya NMB kwenda nchini Dubai kula Bata kwa siku nne mfululisho safari iliyogharamiwa na NMB kila kitu.

Akizungumza katika tukio hilo, Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala alisema washindi hao wamepatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya mwisho ya Shindano la MastaBata lililoendeshwa kuhamasisha matumizi ya mfumo wa 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' kwa wateja wao.

Aliongeza kuwa mbali na washindi hao wateja kibao wa NMB waliotumia mfumo huo wa malipo pia wamejishindia shilingi 100,000/- kila mmoja na wengine wengi kujishindia simu janja za kisasa aina ya 'Samsung S9+'.

Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir akifuatilia tukio hilo.
Meneja Mwandamizi Huduma za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Stephen Jilala (katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kupatikana kwa washindi watatu wa NMB kwenye shindano la MastaBata ambao pamoja na wenza wao watasafiri kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata'. Kulia ni Meneja Huduma za Kadi NMB, Bw. Philbert Casmir pamoja na Meneja Mwandamizi kitengo cha kadi NMB, Bw. Manfredy Kayala (kushoto) wakifuatilia tukio hilo.
Mtangazaji kutoka kituo cha EFM, Emmanuel Kapanga (katikati) akizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo. Kushoto ni Bi. Saumu Rajabu kutoka Selcom.
Watangazaji wa kituo cha EFM radio na TV, Emmanuel Kapanga (katikati) na Tunu Hussein (kushoto waliokaa), wakizungumza kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa Shindano la MastaBata lililoendeshwa na Benki ya NMB ambaye amejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. Kulia ni Ofisa Mwandamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Abdallah Hemed akisimamia droo hiyo.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakishuhudia kutangazwa kwa washindi watatu wa droo ya mwisho ya shindano la MastaBata. Washindi wa mejishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai kwa siku nne kula 'Bata' na mwenza wake. Jumla ya washindi watatu pamoja na wenza wao wataambatana katika safari hiyo iliyolipiwa kila kitu na Benki ya NMB. 
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images