Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

KILIMO WEZESHENI WATAFITI WA MICHIKICHI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iwawezeshe watafiti katika kituo cha Utafiti cha zao la michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma ili waweze kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu bora za zao hilo. Amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu kwenye zao hilo la michikichi, hivyo Wizara ya Kilimo haina budi kukiwezesha kituo hicho kwa lengo la kuzalisha mbegu bora zitakazosambazwa kwa wakulima.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 17) wakati alipotembelea kituo cha Kihinga kwa ajili ya kukagua shughuliza uzalishaji wa mbegu za michikichi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma. Amesema Serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, ambapo kwa mwaka inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.

“Wizara ya Kilimo iwawezeshe watu wa utafiti ili waendelee na shughuli hiyo kwa kasi, iwaongeze watumishi kituoni hapa na ongezeni nguvu kwenye zao la michikichi kama yalivyofanya Mataifa mengine ya Costa Rica na Malaysia.” Amesema wakulima wa zao hilo wanahitaji kupata mafanikio, hivyo kituo hakina budi kuongeza nguvu ya uzalishaji wa mbegu bora. Ili wafikie malengo amewasahauri washirikiane na taasisi binafsi zinazozalisha mbegu.

Pia Waziri Mkuu amesema chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga, kiendelee kutoa elimu na Wizara ya Kilimo ijenge majengo yake inayoyahitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za utafiti. Eneo la chuo linaukubwa kwa hekta 920. Kwa upande wake, Mratibu wa Utafiti wa Kilimo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo amesema michikichi iliyopo sasa inauwezo wa kuzalisha tani 1.6 ya mawese kwa hekta moja ambao kidogo na hauna tija.

Amesema mbegu wanazozizalisha zinalenga kumuongeza tija mkulima kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani nne kwa hekta, pia wanaendelea kuangalia vinasaba vya mbegu vilivyopo ili wazalishe mbegu bora zaidi. “Tutakusanya vinasaba vyote vya mbegu tulivyonavyo na kuvitathimini na kuona uwezo wake na ikibidi tutaagiza kutoka nje ya nchi ili kuboresha zaidi.” Miche ya michikichi inachukua muda wa miezi 18 kutoka hatua ya uchavushaji hadi kusambazwa kwa wakulima.

Baada ya kumaliza shughuli ya ukaguaji wa uzalishaji wa mbegu kituoni hapo, Waziri Mkuu alikagua shamba la michikichi la Gereza la Kwitanga  lenye ukubwa wa ekari 400 na kupanda mche kama ishara ya uzinduzi wa upandaji wa miche bora shambani hapo. Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu katika zao hilo na inategemea taasisi zake mbili za Jeshi la Magereza (Kwitanga) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT-Bulombora), ambazo zinamashamba makubwa ya michikichi.

Kadhalika Waziri Mkuu ameagiza elimu kuhusu kilimo cha zao la michikichi kuanzia hatua za awali hadi uzalishaji wa mafuta itolewe mashuleni ili wanafunzi waanze kupata ulewa na ifikishwe hadi kwa wananchi.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mbegu ya mchikichi inayoonyesha tabaka la  mafuta wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Mwandamizi na Mratibu wa Utafiti wa Kilimo mkoani Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha  Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya mchikichi iliyochavushwa kitlaam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dkt. Gwajima Atua Dar na Kampeni ‘Coordination’

$
0
0
Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, amefanya ziara mkoani Dar-Es-Salaam huku akiendeleza kampeni yake ya kufanya kazi kwa ushirikiano aliyoianza mkoani Dodoma kwakuwataka watendaji serikali kutambua na kuheshimu ubunifu wa mtumishi mmoja mmoja.

“Viongozi wote ngazi zote tuzidi kuungana kutambua juhudi za kila mtumishi na hasa junior Staff, kwani ipo siri kubwa katika nguvu ya kutambua na kupongeza amabapo hata changamoto zitageuka kuwa fursa” alisema Gwajima

Gwajima alisema kuwa, mapungufu na uhaba vitageuka kuwa fursa kwakua macho na akili ya ndani vitafunguka na kukabiliana na hayo yote na kupata ufumbuzi wa matatizo mbalimbali katika sehemu za kazi wanapo watia moyo watumishi.

Katika ziara yake ya kwanza, aliyoifanya mkoani Dodoma Dkt.Gajima alikutana na Sekretarieti ya mkoa huo chini ya katibu Tawala wa Mkoa na hatimaye kufanya kikaokazi na Kamati ya Afya ya Mkoa, ambapo katika vikao vyote viwili alihimiza utendaji kazi wa pamoja (coordination, Harmonization, Involvement and Motivation)

Katika ziara hiyo ya Mkoa wa Dar-Es-Salaam, alipongeza jitihada za mtumishi Muuguzi Sarah John wa Zahanati ya Malambamawili Kata ya Msigani, Manispaa Ubungo kwa jitihada zake alizo onesha katika utendaji uliotukuka hasa katika kuhamasisha watu kwenda kwenye huduma za afya.

Dkt. Gwajima. Alisema, Muunguzi Sarah John katika Zahanati hiyo amekuwa chachu yakuhamasisha wateja wao kwa kuwatungia nyimbo, kuimba na kucheza nao hali iliyo pelekea watu katika Kata hiyo kumpenda kwa uwezo wake huo wakuhamasisha na kuwafanya watu wengi kuhudhuria katika huduma za afya kwenye kituo hicho kilicho anzishwa Julai, 2018 ndani ya kata hiyo.

“Siyo Rahisi kwa Muuguzi kujishusha hadi kucheza na wateja wake, inahitaji Moyo wa kupenda kazi, kulipenda taifa na uzalendo wa hali ya juu kutoka Moyoni” alisema Gwajima.

Bi. Sarah amekuwa akienda sambamba na Kauli mbiu ya Mhe. Rais yakutaka kila mtu azae bila kupangiwa idadi ya watoto, ila wazingatie malezi kwa wototo atakao wazaa kwa kuwapatia huduma za msingi.

Hii imekuwa ni ziara yake ya pili tokea Dkt. Gwajima, ateuliwe na Mhe. Rais kushika wadhfa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) ambapo katika ziara hiyo, waliungana na uongozi wa Kata ya Msigani na wananchi na watendaji kisha kufanya hamasa ya watu kushiriki katika huduma za afya msingi huku rai yake kubwa akiilekeza kwenye kufanya kazi kama timu moja ili kufikia maendeleo endelevu kwa watu kuwa na afya njema.
 Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dorothy Gwajima, akiwa katika picha ya Pamoja na Muunguzi Sarah John na watumishi wengine wa Zahanati ya Malambamawili, mkoani Dar-es-salaam wakati wa ziara hiyo.
 Dkt. Doroth Gwajima, alipowasili katika  hicho  Zahanati hiyo ya Malambamawili, akisaini kitabu cha wageni huku, watumishi wakiwa wamesimama nyuma yake kabla yakuanza ziara kwenye kituo hicho na kufanya hamasa ya huduma za Afya
Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza jambo  wakati wa ziara yake mikoani, akihimiza masuala yakufanya kazi kama timu ili kupata tija katika utendaji.  

GEREZA LA KWITANGA NA JKT BULOMBORA KUWA VITUO VYA KUZALISHA MICHE YA ZAO LA CHIKICHI KIGOMA.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WAZIRI mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali imechagua gereza la kwitanga na kambi ya JKT Bulombora kuwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche ya zao la chikichi.

Hayo ameyasema leo kwenye kambi ya bulombora wakati akiongea na wananchi pamoja na vijana wa JKT Bulombora wakati akiwa kwenye siku ya pili ya ziara yake kikazi.

Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa gereza la kwitanga kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao hilo ikiwa ni sambamba na kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha zao la mchikichi.

"Wataalamu wowote kutoka duniani kote watakaotaka kujifunza kilimo cha zao la chikichi tutawaleta hapa Bulombora JKT na gereza la kwitanga pamoja na Ilagala haya maeneo yatatumika kama shamba darasa la zao hilo"alisema Majaliwa

Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Wilaya zote na halmashauri ambazo zao la chikichi linastawi vizuri kutoa elimu na kuhamasisha wananchi jinsi ya kulima zao hilo kisasa ambapo mbegu(miche)ambapo wananchi watakuwa wanapewa bure kwenye halmashauri husika.

Alisema Wizara ya kilimo wanatakiwa kusimamia maeneo yote ambayo zao la chikichi linalimwa kisasa na wananchi.

"Nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT)kambi ya hapa Bulombora kwa kuandaa eneo lenye hekta zaidi ya 480 kwaajili ya kilimo cha zao la chikichi lakini hapa malengo yetu ni kulima hekta 2000,Gereza la kwitanga napo nimekuta wanasafisha shamba la hekta 450 na wao wanatakiwa kulima hekta zaidi ya 2000,tulime maeneo tunayo yakutosha"Alisema Waziri Mkuu.

Waziri mkuu amewataka wakulima wakubwa makampuni na taasisi binafsi kuja kuwekeza kigoma kwenye zao la chikichi kwenye vitalu vya mbegu bora,pia watapata maeneo ya kulima ili wawekeze kwenye kilimo chenyewe.

"Kwakweli tukifikia hatua hiyo nchi yetu ya Tanzania hatutakuwa na shida ya kuagiza mafuta ghafi toka nje ya nchi na dola zitabaki ndani"alisema Majaliwa.

Naibu waziri wa Kilimo Mgumba naye alisema tayari Wizara imeshatenga kwenye bajeti shilingi bilioni 10 kwaajili ya uendelezaji wa zao hilo,ambapo kwenye bunge lijalo.

"Mhe.Waziri Mkuu lakini hatuwezi kusubiria hadi hizo bilioni 10 hadi zipitishwe mwezi wa saba tumeanza kujibana matumizi yetu katika bajeti iliyopita ya mwaka jana,ili tuweze kutekeleza azma ya serekali ya kuendeleza zao la mchikichi nchini na kumaliza tatizo la mafuta"alisema Naibu waziri wa Kilimo

Alisema mpaka sasa wameshapeleka watumishi wawili waliobobea katika utafiti wa zao hilo katika kituo cha utafiti cha Kihinga na ndani ya wiki hii watakuja watafiti wengine 10 kutoka vyuo mbalimbali vya utafiti wa zao mchikichi na kwenda Kihinga.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Peter Serukamba alimwambia Waziri Mkuu changamoto inayowakabili wakulima wa zao hilo ni upatikanaji wa mbegu bora,hivyo aliiomba serikali wakulima wapate mbegu bora na za kisasa pi matumizi hafifu ya teknolojia ya kilimo hicho.
 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizindua matreka mawili katika gereza la kwitanga ambayo yatatumika katika  shamba la Kwitanga kuendeleza za la chikichi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya zao la chikichi iliyochavushwa kitaalam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa michikicho cha Kihinga Kilichopo Wilayani Kigoma

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mche wa zao la chikichi katika shamba la JKT Bulombora ikiwa ni uhamasisha wa kulima zao hilo na kulifanya zao la kimkakati.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akipanda mche wa zao la chikichi kwenye shamba la JKT Bulombora katika kuhamasisha kulima zao hilo
 

BENKI YA CRDB YAKABIDHI MADARASA MADARASA MAWILI NA MADAWATI SHULE YA MSINGI USA RIVER, JIJINI ARUSHA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola (katikati) akishirikiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro pamoja na Mkuu wa Shule ya Msingi Usa River, Mwalimu Abdul kukata utepe wakati wa ufunguzi rasmi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, kwa gharama ya kiasi cha shilingi milioni sitini (60 milioni) yaliyojumuishwa pamoja na madawati, wakati wa hafla ya ufunguzi iliyofanyika mwishini mwa wiki, Wilayani Arumeru jijini Arusha.
Sasa imefunguliwa rasmi na tayari kwa kutumiwa kwa mafunzo ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usa River.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akishirikiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (wa pili kulia) kufungua kitambaa kwenye jiwe la msingi wakati wa hafla ya ufunguzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Wilayani Arumeru, jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza machache kabla ya kumkabidhi rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola madarasa mawili ya mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akizungumza baada ya kupokea madarasa hayo pamoja na madawati yake.
Meza Kuu.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akizungumza wakati akitoa hotuba yake katika hafla ya ufunguzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Wilayani Arumeru, jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Wilayani Arumeru, jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Usa River, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Benki ya CRDB, iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Wilayani Arumeru, jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akizungumza wakati akitoa shukrani kwa uongozi wa Benki ya CRDB kwa kufanikisha ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi Usa River, iliyopo katika wilaya yake.


















Serikali Kuboresha Mazingira ya Upatikanaji wa Elimu kwa Watoto wenye Mahitaji Maalum

$
0
0
Serikali  imesema kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa sasa ni kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanakuwa na mazingira salama na rafiki katika mchakato wa kujifunza ili kuwawezesha kupata elimu bora.
Kauli ya Serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu wakati akifunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye  lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kundi la watoto wenye mahitaji maalum linasaulika hata unapoangalia miradi ya elimu  inayoletwa na wafadhili mara nyingi inaangalia matatizo ya mimba au mila kandamizi lakini wanasahaulika,  kundi hili ambalo  ni wahanga namba moja wa mila hizo kandamizi ambazo zinawakosesha fursa ya kupata elimu.
 “Watoto wenye mahitaji  maalum wanasaulika hata wenzetu wafadhili wanapokuja  kuanzisha  miradi mara nyingi wanapenda kuongelea mambo ya mimba na mila kandamizi  lakini  wanasahaulika   kwamba kundi hili la watoto wenye mahitaji maalum ambao unapoongelea mila kandamizi wao ni wahanga namba moja haijalishi kama wamepata mimba lakini tumewawekea alama kutokana na maumbile yao ” alisemaDkt. Semakafu.
Dkt. Semakafu amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia limeweka kipaumbele kwa kundi hili kwa kuhakikisha miundombinu ya shule ambazo zinachukua watoto wenye mahitaji maalum zinapewa kipaumbele katika kuboreshwa, kununua visaidizi vya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kusoma na kupata elimu yao katika mazingira yaliyoboreshwa na salama.
Aidha, amesema kwamba mkaka ti mwingine wa serikali ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na shule maalum kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ili kuwezesha kuwalinda watoto bora kama watoto wengineiliwawezekujisaidiakatikamaishayaoyabaadaye.
Naye Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola (COL), Profesa Asha Kanwaramwe ataka washiriki wanaoutekeleza muda huo kutoa chakuutekeleza kwasababu yeyote ile kwani unadabadili maisha ya wasichana wengi nakutaka nchi ishiriki kuimarisha elimu masafa ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wasicha na wanaopata mimba.
Mradiwa Girls Inspire unalenga kuzuia ndoa za utotoni unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Msumbiji, Bangladesh, India na Pakistani na kufadhiliwa na serikali za Canada na Australia ambapo kwa Tanzania umatekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Shirika lisilo la Serikali Kiota Women Health and Development, (KIHOWEDE).

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akifunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye  lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola (COL), Profesa Asha Kanwaramwe akizungumza wakati wahafla ya kufunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye  lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na TEW)

RAIS DKT SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA KASKAZINI A UNGUJA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar. Mhe Riziki Pembe Juma, baada ya kuweka jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, leo.lililojengwa na Kampuni ya And Beyond Island Lodge ya Hoteli ya Mnemba, hafla hiyo imefanyika katika eneo la Skuli hiyo Kijini Matembe.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akielekea sehemu iliotengwa kwa ajili ya kuzungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kijini na Mbuyu Tende, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja.(Picha na Ikulu)
 /WANANCHI wa Vijiji vya Kijini na Mbuyu Tende Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja wakiwa katika viwanja Skuli ya Kijini Matemwe wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe.(Picha na Ikulu)
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Bi. Madina Mjaka,akizungumza na kutoa Taarifa ya Kitaalamu ya Ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Skuli hiyo, uliofanyika leo.17-2-2019.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Riziki Pembe Juma, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Kijini, uliofanyika katika viwanja vya Skuli hiyo, kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohemed Shein, kuwahutubia Wananchi wa Jimbo la Kijini Wilaya ya Kaskazini 'A'Unguja,LEO 17-2-2019.(Picha na Ikulu)
 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A'Unguja, kushoto Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, na kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar.Dr. Abdallah Juma Mabodi.(Picha na Ikulu)
 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Lagema Nungwi kuzungumza na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini 'A'Unguja akiwa katika ziara yake ya kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja leo.17-2-2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akielekea katika ukumbi wa mkutano katika Hoteli ya Lagema Nungwi, kulia Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mwinyi na kushoto Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini UngujaNdg. Iddi Ali Ame.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo wa "Sisi Sote Tumegomboka" alipowasili katika ukumbi wa Hoteli ya Lagema, kuzungumza na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini "A" Unguja, akiwa katika ziara yake Mkoa wa Kaskazini Unguja, leo 17-2-2019.(PIcha na Ikulu)
 WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya Lagema Nungwi wakiimba wimbo wa "Sisi Sote Tumegombioka" wakati wa kuwasiliu Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kuzungumza na Wanachama wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini "A"Unguja leo.17-2-2019.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.,Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa CCM wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika ukumbi wa Hoteli ya Lagema Nungwi leo, akiwa katika ziara yake.(Picha na Ikulu)

WALIMU WA WATAKIWA KUTUMIA ZAIDI ZANA ZA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA WANAPOFUNDISHA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma amesema wakati umefika sasa kwa walimu wa skuli kutumia zaidi zana na vielelezo katika kufundisha wanafunzi badala ya kutumia chaki, mdomo na ubao pekee.

Alisema iwapo vitendea kazi na vielelezo vitatumika vizuri na kwa muda sahihi kuna uwezekano mkubwa kiwango cha ufahamu kwa wanafunzi wengi kuongezeka na kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya Taifa na kuinua kiwango cha elimu.

Waziri wa Elimu alitoa maelezo hayo Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kampasi ya Nkrumah kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya zana za kufundishia na kujifunzia katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Idrissa Muslim Hija.

Alisema matumizi ya zana na vielelezo ni muhimu sana katika kumuandaa mwanafunzi kukabiliana na mitihani yake na amebainisha kuwa utaratibu uliozoeleka wa mwalimu kukaa mbele ya darasa na chaki ni potofu kwa sasa na inachangia kushuka kiwango cha elimu. 

Alishauri kutumika mpango wa Maendeleo  ya Elimu ya kutengeneza na kutumia zana zinazopatikana katika mazingira yaliyotuzunguka ambazo zinagharama nafuu.

Alisema vifaa hivyo vilivyotengenezwa na wanafunzi wanaosoma kada ya ualimu Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar  vinatrajiwa kuwa suluhisho kwa baadhi ya wanafunzi wa skuli wenye ufahamu mdogo katika masomo.

Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kufanya juhudi ya kuongeza vifaa vya kufundishia na kujifunzia lakini kutokana na idadi ya wanafunzi kuongezeka kwa kasi, kuna umuhimu kwa walimu waliopatiwa mafunzo ya kutengeneza vifaa hivyo kuuedeleza katika skuli watakazo pangiwa baada ya kumaliza chuo.

Mkuu wa Skuli ya Elimu ya SUZA Dk. Maryam Jaffar Ismail alisema wanafanya juhudi ya kuwaandaa walimu wanaosoma chuoni hapo kutengeneza zana za kusomeshea kwa kutumia vitu vilivyopo katika mazingira yaliyowazunguka ambavyo havina gharama kubwa ili kuwasaidia wanafunzi wao na kuongeza ufanisi katika kazi hiyo.

Alisema tokea walipoanza mpango huo miaka mitano iliyopita ufanisi wa kutengeneza vifaa umekuwa ukiongezeka na wamekuwa kigenzo kwa vyuo vikuu vya nchi jirani kutaka kuja kujifunza .

Akielelezea changamoto inayoikabili kada ya elimu nchini ni vijana wengi kukataa kujiunga na kada hiyo na wanaojiunga ni vijana wanaokosa  masomo katika fani nyengine jambo ambalo alisema sio sahihi.

Akitoa neno la shukrani katika maonyesho hayo, Mkufunzi wa Mradi wa kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzaia wa SUZA Maalim Said Yunus alisema vifaa vyote wanavyotumia kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia vinaweza kupatikana sehemu yeyote ya Zanzibar bila kutumia gharama kubwa.

Alisema hatua ya kutengeneza zana hizo itaziba pengo la upungufu wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia  unaozikabili skuli nyingi za Zanzibar ambavyo vimekuwa vikiagizwa na Serikali kwa gharama kubwa.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Dk. Idrissa Muslim Hija akipata maelezo ya chombo kinachotumika kupitisha umeme kutoka kwa mwanafunzi Husna Sharif wa Sekondari ya SUZA katika maonyesho ya zana za kufundishia na kujifunzia yaliyofanyika Kampasi ya Nkrumah.
  Mkufunzi wa somo la kutengeneza zana za kufundishia na kujifunzia wa SUZA Maalim Said Yussuf akieleza Mradi huo unavyoendelea kuwaandaa walimu wanafunzi wanaosomo chuoni hapo katika maonyesho yaliyofanyika Kampasi ya Nkrumah.
  Baadhi ya walimu wanafunzi wanaosoma SUZA wakifuatilia ufunguzi wa maonyesho ya zana za kufundishia na kujifunzia yaliyofanyika Kampasi ya Nkrumahi
 Mkuu wa Skuli ya Elimu ya SUZA Dk. Maryam Jaffar Ismail akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya zana za kufundishia na kujifunzia yaliyofanyika Kampasi ya Nkrumah.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Taasisi mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara walioalikwa ufunguzi wa maonyesho ya zana za kufundishia na kujifunzia yaliyofanyika Kampasi ya Nkrumah. Picha na Ramadhani Ali

USIPITWE NA HII: Choo cha kisasa kisichotumia maji...


HATUTAMVUMILIA ATAKAYEHUJUMU MKAKATI WA KUFUFUA ZAO LA MICHIKICHI -MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitomvumia mtu yeyote atakayebainika kuhujumu mkakati wake wa kulifufua zao la michikichi nchini.
Amesema wanataka kuona wakulima zao hilo wakinufaika kama wengine wa mazao makuu ya biashara, hivyo haitomfumbia macho mtu atakayezembea.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Februari 17) mara baada ya kukagua shamba la michikichi la kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Bulombora. Alisema Serikali inataka kuona wakulima wa zao hilo wakinufaika kama ilivyokuwa kwa wakulima wa korosho, chai, kahawa, pamba na tumbaku.

Alisema Serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula kwani inatumia fedha nyingi kuagiza nje ya nchi. Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaagiza viongozi mkoani Kigoma kwamba suala la kilimo cha michikichi liwe ajenda ya kudumu kwenye vikao vyao.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliiagiza Wizara ya Kilimo ianzishe shamba darasa la zao la michikichi ili wananchi waweze kujifunza mbinu bora za kulima zao hilo. Awali, Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba alisema Serikali imetenga zaidi ya sh. bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha zao la michikicho.

Waziri huyo alisema kiasi hicho cha fedha kimetengwa katika bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2019/2020 kwa ajili ya kuboresha kilimo cha michikichi nchini. Alisema iwapo kilimo cha zao hilo kitaboreshwa kitasaidia Serikali kuokoa fedha nyingi za kigeni zilizokuwa zikitumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi.

Pia, Waziri Mgumba alisema tayari wizara hiyo imeshaongeza watafiti zaidi ya 10 wa zao la michikichi katika kituo cha utafiti wa zao hilo cha Kihinga. Waziri Mgumba alipongeza Jeshi la Magereza  na JKT kwa ushirikiano wanaoutoa kwa wizara katika kipindi hiki cha ufufuaji wa zao la michikichi.

Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi alimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa maelekezo yote aliyoyatoa kuhusu kilimo cha michikichi watayatekeleza.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja  Jenerali , Martin Busungu wakati alipowasili kwenye Kambi ya JKT ya Bulombora wilayani Uvinza, kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi, Februari 17, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Hussein Mwinyi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary (kushoto) wakitazama sabuni zinazotengenezwa na Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa katika Kambi ya Bulombora wilayani Uvinza wakati alipotembelea  kambi hiyo kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi, Februari 17, 2019.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akiwasha trekta ikiwa ni ishara ya kuzindua trekta hilo katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora wilayani Uvinza, Februri 17, 2019. Mheshimiwa Majaliwa yuko mkoani Kigoma kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha ufufuaji wa zao la michikichi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akipanda mchikichi ikiwa ni ishara ya kuzindua upanuzi wa shamba la zao hilo katika Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Bulombora  wilayani Uvinza, Februari 17, 2019. Mheshimiwa Majaliwa yuko mkoani Kigoma kwa ziara yenye lengo la kuhamasisha  ufufuaji wa zao la michikichi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAPA MBINU ZA KUDAI MASLAHI YAO WABEBA MIZIGO NA WAONGOZA WATALII KILIMANJARO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewashauri wabeba mizigo na waongoza watalii katika  Mlima Kilimanjaro wapunguze utitiri wa vyama walivyoviunda  vya kutetea  maslahi yao  badala yake  wabaki na vyama viwili ambavyo vitakuwa na nguvu ya kudai haki na kupigania maslahi yao.

Pia ameyataka Makampuni ya watalii kuwalipa malipo yao wabeba mizigo na waongoza watalii kwa mujibu wa sheria  badala ya kuwapunja malipo yao huku wakidai kuwa malipo hayo hayatekelezeki kisheria. Kwa mujibu wa sheria waongoza watalii katika mlima huo wanapaswa kulipwa si chini ya Dola 20 za Marekani kwa siku sawa na mbeba mizigo Dola 10 za Marekani kwa siku.

Aidha, Amewataka wabeba mizigo na waongoza watalii hao wawe wanatoa taarifa kwa siri kwa yale makampuni yanayowalipa pesa kidogo na kwamba  yale Makampuni  yatakayobainika  yafutwe kwa kosa la kukiuka sheria hiyo.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na wadau wa Utalii katika  Mkoa wa Kilimanjaro wakati alipofanya ziara kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro lengo likiwa ni kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wadau hao katika sekta ya Utalii.

Amesema haiwezekani vyama zaidi ya nane vikawa vinafanya kazi moja ya kupigania na kudai maslahi ya wabeba mizigo na waongoza watalii halafu kukawa na ufanisi kwanza. Daniel Maro, mbeba mizigo ya watalii amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa wamekuwa wanalipwa na baadhi ya Makampuni ya watalii malipo kiduchu ya kiasi cha shilingi 5,000 na muda mwingine shilingi 8,000 badala  ya elfu 20,000 kwa siku.

Amesema malipo hayo ni madogo sana ukilinganisha na ugumu wa kazi hiyo na wamekuwa hawana pa kulalamikia na  wale wote ambao wamekuwa wakibainika kulalamika  wamekuwa wakikosa  kupata kazi tena kutoka kwenye kampuni hayo.

Naye, Walter Mbambwo ambaye ni Muongoza watalii katika Mlima huo  amesema kutokana na tatizo la ajira wamekuwa wakilazimika kutoa rushwa ya kiasi shilingi 20,000 ili wapate kazi  hiyo lakini wamekuwa wakilipwa kiasi cha shilingi 5,000 au 8,000 tu.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amekitaka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kiangalie uwezekano wa kusambaza mtaala wa Waongoza watalii kwa vyuo vingine ikiwemo Chuo cha Taifa cha Taifa cha Utalii pamoja na VETA ili kuweza kutoa fursa kwa wadau hao kuweza kusoma mahali popote nchini badala ya utaratibu uliopo sasa unaowalazimisha kuwa  lazima wasome katika Chuo hicho pekee nchini huku akiwaahidi kuwa suala la ukubwa wa ada wanayotozwa atalifanyia kazi.

Awali,  Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kippi Warioba amewahakikishia wadau hao  kuwa ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya  kuwasaidia ili kuifanya sekta ya utalii katika  mkoa wake uendelee kufanya vizuri. Hata hivyo amewataka waongoza watalii na wabeba mizigo ya watalii kuachana na vyama  vile vinavyolenga kuwakandamiza badala ya kupigania maslahi yao wakati ofisi yake ikiangalia namna ya kuwasaidia namna ya  kuondokana na kulipwa ujira mdogo.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wabeba mizigo na waongoza watalii kuhusu maslahi yao kiduchu wanayolipwa na baadhi ya Makampuni ya Watalii ambayo ni kinyume cha sheria wakati alipotembelea  katika Hifadhi ya Taifa ya  Mlima Kilimanjaro katika geti la Mweka kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzifanyia kazi katika ziara yake ya kikazi ya  siku mbili katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. 
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) akimsikiliza Mhadhiri wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka anayetoa mafunzo kwa vitendo kwa  wabeba mizigo na waongoza watalii, Filbert Kimaro  wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea   Hifadhi ya Taifa ya  Mlima Kilimanjaro  katika ziara yake ya kikazi ya  siku mbili aliyoifanya  katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro. Wa kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro, Beatrice Looiboki pamoja na Mhifadhi Charles Ngendo,
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipewa maelezo kuhusu mfumo wa malipo ya elektoniki yanavyofanyika kwa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro na Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Charles Ngendo, Wa kwanza  kushoto ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya  hiyo Beatrice Looiboki 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watalii wakati alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro katika geti la kuingilia la Mweka.
Baadhi ya kibao kinachoonesha kilomita za kupanda Mlima Kilimanjaro kwa upande wa geti la Mweka.

(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)

BREAKING NEWS: Wema Sepetu afunguliwa rasmi na bodi ya filamu

$
0
0
Kufatia bodi ya filamu kumfungia msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu kutojihusisha na kazi za filamu kwa muda usiojulikana kutokana na video iliyosambaa ya kukiuka maadili ya kitanzania. 

Leo bodi hiyo imemfungulia msanii huyo kuendelea na kazi zake za sanaa kutokana na  kujidhihirisha pamoja na masharti waliyompatia kuyatekeleza na kuhaidi kujirekebisha.

Taarifa kamili inakuijia hivi punde

TAMASHA LA LADY IN RED KURINDIMA JUMAMOSI HII, LALENGA KUIBUA VIPAJI KWA VIJANA

$
0
0
* Waandaaji waishukuru Serikali kwa ushirikiano, yawahimiza vijana kujituma kwa kufanya kazi kwa bidii

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
JUKWAA la ubunifu nchini maarufu kama Lady in Red linatarajiwa kufanyika usiku wa jumamosi ya tarehe 18 mwaka huu ikiwa ni mara ya 16 tangu kuanza kufanyika kwake chini ya mwanzilishi wake Asya Idarous.

Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa jukwaa hilo Didas Katona amesema kuwa jukwaa hilo ni kwa ajili ya kukuza sanaa na wabunifu chipukizi ili kuweza kuwasaidia kuweza kufikia malengo yao.

Amesema kuwa tamasha hilo litafanyika viwanja vya Escape One, siku ya tarehe 18 mwezi huu kuanzia majira ya saa moja jioni na kuwataka wapenzi wa  mitindo na ubunifu kujitokeza kwa wingi na kushuhudia wabunifu hao chipukizi watakavyoonesha ubunifu wa mavazi.

Katona amesema kuwa; " Walimbwende (models) 30 pamoja na wabunifu 10 watapata fursa ya kuonesha ubunifu wao na kujitangaza  na tuna imani watafika mbali zaidi kwa kuwa hali ya ubunifu kwa sasa ni nzuri na serikali inatuunga mkono, hivyo hii ni fursa kwao katika kujitangaza ili waweze kufika mbali zaidi" ameeleza.

Pia ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Joseph Magufuli, Baraza la sanaa la taifa (BASATA) na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuwa pamoja kuonesha ushirikiano wa hali ya juu na wasanii katika kuikuza na kuiendeleza sanaa nchini. 

VIJANA ANZISHENI MASHAMBA YA MICHIKICHI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana mkoani Kigoma waanzishe mashamba ya michikichi kwa kuwa zao hilo litawapatia kipato cha uhakika. Amesema Serikari imedhamiria kufufua zao la michikichi ili kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwenye mafuta ya kula na kuokoa fedha za kigeni.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 18, 2019) alipowasalimia wananchi wa kijiji cha Nyakitondo wilayani Kasulu akiwa njiani kwenda Kibondo.
Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufufua kilimo cha michikichi amesema ni vema wananchi wakachangamkia fursa hiyo.

“Vijana limeni michikichi kwani ukipanda ukiwa darasa la tano baada ya miaka mitatu utaanza kuvuna na kujipatia kipato ambacho kitakuwezesha kujikimu.” Amesema kilimo cha zao la michikichi kitawawezesha wananchi hususani vijana kupata mitaji ya uhakika kwa ajili ya shughuli zingine za kiuchumi

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inaongoza kwa kilimo cha zao la michikichi katika nchi za Afrika Mashariki. Kadhalika, Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi hao wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili wawe na uhakika wa matibabu kwa yao na familia zao.
Wakati huohuo Waziri Mkuu ametembelea kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo na kukagua shule ya msingi Kassim Majaliwa na baadae wodi ya wazazi katika Hospitali Nduta.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye  Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua madaftari ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa wakati alipotembelea baadhi ya madarasa ya  Shule hiyo, Februari 18, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  wakati alipokagua madarasa ya Shule hiyo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Kibao kinachoonesha ilipo Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo ambayo ilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HATIMA YA DHAMANA YA KESI INAYOWAKABILI MWENYEKITI WA CHADEMA PAMOJA NA MBUNGE WA TARIME BADO IKO CHINI YA MAHAKAMA YA RUFANI NCHINI

$
0
0
 Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akitoka Mahakama leo Februari 18, 2019.

 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii 

MAHAKAMA ya Rufani nchini inaendelea kushikilia hatima ya dhamana ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko baada ya jopo la Majaji watatu wa Mahakama hiyo kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) na kusema watatangaza siku ya kutolewa kwa uamuzi.

Jopo la Majaji likiongozwa na Mwenyekiti wao, Jaji Stella Mgasha, Mwanaisha Kwariko na Gerald Ndika, Leo Februari 18, 2019  wamesema uamuzi huo utatolewa baada ya kusikiliza hoja za upande wa mashitaka na upande wa utetezi zilizowasilishwa mahakamani hapo. Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko

Hata hivyo, washtakiwa hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika nae baada  kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Hata hivyo,  DPP alikata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama Kuu kukubaliwa kusikiliza rufaa hiyo. 

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, upande wa DPP, umewakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi na Paul Kadushi, huku upande wa wajibu rufani ukiongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, Jeriamiah Ntobesya na Rugemeleza Nshala.

Akiwasilisha hoja tatu za upande wa serikali,  wakili Nchimbi ameeleza katika hoja yao ya kwanza kuwa Jaji Sam Rumanyika, alipotoka kisheria kuhusu kukubali na kupanga usikilizwaji wa rufaa ya Mbowe na Matiko ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kupinga dhamana yao.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa akiwasili Mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wake pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini.


Pia hoja nyingine ya pili ambayo Majaji walimtaka Nchimbi aiondoe ni kwamba Jaji Rumanyika alipendelea kwa kupotoka kisheria ambapo alilazimisha usikilizwaji wa Rufani wakati akijua kuna ukiukwaji wa kisheria.

Hata hivyo Jaji Mgasha alimuuliza Nchimbi kwa jinsi gani Jaji Rumanyika alipendelea na je kitu kisichozumgumzwa katika Mahakama Kuu, je Mahakama hiyo inaweza kuijibu...?

Kufuatia hayo,  Nchimbi aliiondoa hoja hiyo na kubakiwa na hoja mbili.

Katika hoja ya pili, Nchimbi alidai Mahakama Kuu haikuwapatia haki ya kutosha ya kusikilizwa na kwamba kunyimwa kwa haki hiyo ya kusikilizwa kunaonesha kuwa Jaji alipotoshwa kisheria kwa kuwanyima waomba rufaa haki ya kusikilizwa.

Ameendelea kudai kuwa siku ya kwanza kufika mahakamani waliwasilisha maombi ya kupatiwa muda wa kutosha wa kujiandaa ili kujitetea katika rufaa ya (Mbowe na Matiko) lakini hawakupatiwa muda wa kufanya hivyo kwani uamuzi ulisomwa saa 6 badala ya saa 8  hali iliyosababisha kushindwa kujiandaa kuwasilisha mapingamizi yao.


"Katika mchakato wa rufaa haki ya kusikilizwa ni muhimu na itaonekana mchakato wake utakapoonekana. Ni maoni yangu kuwa Jaji Rumanyika alikuwa na upendeleo na alijikuta anaangukia kwenye upotofu wa sheria wa kuendelea na rufaa hiyo,’’ alidai.

Aidha, ameiomba mahakama ione kwamba rufaa iliyopo Mahakama Kuu ina mapungufu na haipo sahihi kuwepo na kwamba inafaa kuondolewa ili warufani waweze kufuata utaratibu kwa mujibu wa sheria.

Katika hoja yake ya tatu, amedai Mahakama Kuu haikuzingatia haki ya kutosha ya kuwasikiliza.

Hata hivyo,  Jopo la Majaji walimuuliza ni sehemu gani inayoonyesha wamenyimwa haki ya kusikilizwa.

Wakili Nchimbi akadai, walinyimwa baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kusikiliza Rufaa ya Mbowe na Matiko.

Akijibu hoja Hizo,  wakili wa Utetezi Peter Kibatala ameiomba Mahakama hiyo itupilie mbali rufani hiyo kwa kuwa imeletwa bila sababu za msingi, kwani hata warufani wenyewe wamekiri katika hoja yao ya kwanza. 

Kwa upande waje,  Dk.Nshala amedai kuwa ni rai yao kwamba Warufani walipewa muda wa kutosha wa kusikilizwa na kwamba rufani iliyoletwa hapa imeletwa kwa nia mbaya na kuomba mahakama itupiliwe mbali.
Baada ya kutoa hoja hizo, Jaji Mgasha alisema mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili na itapanga tarehe kwa ajili ya kutolewa kwa uamuzi.

Mbali na Mbowe na Matiko, washitakiwa wengine katika kesi ya msingi ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI SINGIDA MJINI LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vituo vya afya 350 vitakuwa vimekamilika nchi nzima ndani ya miaka mitano ya Uongozi wa Awamu ya tano

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Sokoine wilayani ya Singida mkoa wa Singida ikiwa muendelezo wa ziara yake ya kikazi ambapo amekuwa akikagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

“Kulikuwa na hospitali 65 za wilaya lakini tulivyoingia madarakani zimejengwa hospitali 67 na lengo kuu ni kuwapa wananchi huduma bora ya afya” alisema Makamu wa Rais.

Aidha Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitokubalina na misaada ya masharti na imejidhatiti kufanya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alizindua barabara ya Karume ambayo inajumuisha mradi wa mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 6.1 ambazo nibarabara ya Karume yenyewe , Boma Kinyeto, Double Road Junction (Semali Singida-Dodoma ).

Sambamba na hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya Migori ambapo alijionea maendeleo ya ujenzi ambao unatazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi machi, pia alitembelea shule ya sekondari ya Mwanamema Shein ambapo alizungumza na wanafunzi na kujionea maendeleo ya ujenzi wa bweni la wanafunzi pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa maji ameahidi kutoa tanki la maji la lita 10,000 kwa ajili ya kituo cha afya cha Karume ikiwa kama jitihada za kumuunga mkono Makamu wa Rais ambaye amejitoa kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa salama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Migori wilayani Singida kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa Wilaya Dayness Rwehumbiza. Kituo cha afya cha Migori ni moja ya vituo vilivyopata shilingi milioni 400 za kitanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Mkuu wa Sule ya Sekondari ya Mwanamema Shein Bi. Zainab Mtindu wakati akiwasili kwenye shule hiyo iliyopo Migori, wilayani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori, Singida ambapo aliwasihi wasome kwa bidii ili waje kuwa viongozi bora.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda katika shule ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo Singida mjini ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndio alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo Singida mjini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi  kwenye  ufunguzi wa barabara ya Karume iliyopo Singida mjini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



RAIS DKT.SHEIN AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA KASKAZINI WILAYA YA KASKAZINI B UNGUJA

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi, Maryam Juma, Mabodi akitowa taarifa ya kitaalam wakati wa ziara yake kukagua shimo la uchimbaji wa Mchanga la Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo.kushoto kwa Katibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliani na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa Mwamboya.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea bonde la mchanga la Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskaszini B Unguja leo, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi. Maryam Juma Mabodi, Wasili wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr. Sira Ubwa Mwaboya na Waziri wa Ardhi,Maji Nishati na Makaazi Mhe. Salama Aboud Talib, wakifuatilia hafla hiyo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakitembelea Bonge la machimbo ya mchanga la Pangatupu Wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati wa ziara yake kukagua eneo hilo la uchimbaji akiwa katika ziara yake, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mwinyi, wakati akiwa katika ziara yake kutembelea mashimo ya uchimbaji wa mchanga katika maeneo ya Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskazini B Unguja, leo muonekano wa nyuma ni eneo hilo lililokuwa likichimbwa mchanga na kusimamisha uchimbaji wa mchana.katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri. 
MBUNGE Mstaaf wa Jimbo la Donge Ali Ameir Mohammed akiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakati wa mkutano wa Majumuisho ya  ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja, yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff,(Picha na Ikulu)
 ENEO la Panga Tupu na Chechele Jimbo la Bumbwini Shehia ya Kidazini, lililosimamisha shughuli za uchimbaji wa mchanga, kama linavyoonekana picha wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake katika Wilaya ya Kaskazini  B Unguja leo, kujionea hali hiyo.(Picha na Ikulu).
 BAADHI ya Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar wakiwa katika hafla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea mashimo ya Uchimbaji wa Mchanga katika maeneo Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo,akiwa katika ziara yake.
 BAADHI ya Vijana wanaofanya shughuli zao katika mashimo ya mchanga ya Panatupu na Chechele wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea eneo hilo akiwa katika ziara yake katiuka Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo.

Watu 34 washikiliwa na Polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma mbalimbali

$
0
0
JESHI la polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 34 kwa tuhuma mbalimbali na hiyo ni baada ya kufanyika kwa misako katika maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Mbeya na makosa hayo ni  pamoja na:

Kukamatwa kwa pombe ya moshi ( gongo) ambapo jeshi la polisi mkoani humo limeeleza kuwa mnamo tarehe 17 februari mwaka huu majira ya saa tano asubuhi  katika kata ya Nkuyu tarafa ya Unyakyusya, Wilayani Kyela polisi walimkamata Hohn Mwaseba (31) mkazi wa Nkuyu akiwa na pombe ya haramu ya moshi yenye ujazo wa lita 13 uchunguzi unaonesha mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hiyo na upelelezi unaendelea.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi Mkoani humo limemkamata Prisca Peter (32)  kwa tuhuma za kuingiza bidhaa nchini bila kibali, imeelezwa kuwa mnano tarehe 16 Februari majira ya  saa tatu usiku jeshi la polisi lilimkamata mtuhumiwa akiwa na pombe aina ya Prince chupa 20, kinywaji cha Power chupa  60,  maziwa aina super shake chupa 12, na biskuti aina ya chiko dazani 2 ambazo hazikulipiwa ushuru akiwa anazisafirisha kwa usafiri wa coaster kutika Tunduma kwenda Kyela na chanzo cha tukio hilo imeeleza kujipatia kipato kikubwa kwa kukwepa kulipa kodi na mtuhumiwa amekiri kutenda makosa hayo na upelelezi unaendelea na baadaye mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine jeshi la polisi Mkoani humo katika eneo la Kalumbulu Wilayani Kyela lilimkamata  Stewart Ntulo akiwa na lita 60 za mafuta ya Cook well bidhaa iliyokuwa inaingizwa nchini kutoka nchi jirani ya Malawi bila kibali na upelelezi unaendelea.

Vilevile jeshi la polisi limeeleza kuwa  usiku wa tarehe 15 mwezi huu katika kata ya Tembela wilaya ya kipilisi ya Mbalali jeshi la polisi  liliwakamata watuhumiwa kadhaa kwa tuhuma za kumjeruhi Majuto Mahowe (32) mkazi wa Ifiga kwa kumtuhumu ameiba mtoto.

Aidha jeshi la polisi Mkoani humo linawashikilia watu 18 kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko kinyume na taratibu huko katika kataa ya Itagano tarafa ya Sisino jijini Mbeya.

Wakati huo huo jeshi la polisi linamshikilia Joshua Frank (32) kwa kukutwa na mali zinazosadikika kuwa ni za wizi, maali hizo ni pamoja na printer kubwa 2 aina ya Epson,  laptop 2 ( Accer na Fujistu) na vifaa vingine vingi vya umeme na upelelezi unaendelea kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.

Waziri Dkt. Mwakyembe Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Hispania Nchini Tanzania

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Hispania nchini Tanzania Francisca Pedros wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Hispania na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 18 Februari 2019.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akimuonesha Balozi wa Hispania nchini Tanzania Francisca Pedros maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa Taifa kuelekea mashindano ya AFCON chini ya miaka 17 wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Hispania na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 18 Februari 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Hispania nchini Tanzania Francisca Pedros wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Hispania na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 18 Februari 2019.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam

WADAU WA MITINDO NA UREMBO WAALIKWA KUSHIRIKI MAONESHO NCHINI CHINA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Maonyesho ya Wachina Maarufu kama China International Beauty Expo African Hall, Rex Chan akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  Maonesho urembo yatakayofanyika mjini Guanzhou nchini China.
 Mkurugenzi Msaidizi na Mratibu wa Maonyesho hayo katika ukanda Afrika, Hifan Zhonga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna gani watanzania wanaweza kushiriki maonyesho hayo.
 Mwandishi wa Habari wa Chanel Ten, Kibwana Dachi akiuliza swali kuhusu vipodozi vitakavyoingizwa hapa nchini kutokea china.
 Baadhi ya Wadau na Waandishi wa Habari walioshiriki katika mkutano huo wakifatilia mada zinazowasilishwa kwa Makini.
Sehemu ya waandishi na wadau wa urembo walioshiriki Mkutano huo wakionekana kwa nyuma kama walivyopigwa.

WANARIADHA 28 KUINGIA KAMBINI KUJIANDAA NA MBIO ZA NYIKA NCHINI DENMARK

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
SHIRIKISHO la riadha Tanzania (RT) limetangaza majina ya wanariadha 28 wenye umri wa chini ya miaka 18 na zaidi kwa ajili ya kuingia kambini jijini Arusha. Vijana hao walitangazwa na  Katibu Mkuu wa RT Wilhem Gidabuday na wataingia kambini kwa ajili ya mbio za nyika  zitakazofanyika nchini Denmark mwaka huu.

Amesema mbio hizo zitahusisha wanariadha chini ya miaka 18 na zaidi ya miaka kumi na nane kwa ajili ya maandalizi rasmi ya mbio za Olimpiki zinazofanyika Tokyo nchini Japani kila mwaka. Gidabuday amesema wanariadha hao wataingia kambini  februari 20 mwaka huu ambapo wakiwa kambini watafanya mchujo utakaofikia wanariadha 20 watakaoenda katika mashindano ya mbio za nyika nchini Denmark.

Gidabuday amesema kwa mwaka huu wamekuwa na matarajio ya wanariadha wa Tanzania kupeperusha vyema bendera ya taifa katika kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini. Mshindi wa kwanza wa mbio za nyika nchini Denmark atazawadiwa kitita cha EURO elfu 60 na zawadi za medali za dhahabu na silva zitatolewa.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>