Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WAZIRI SHEKILANGO AFARIKI KWA AJALI YA NDEGE 1980 ARUSHA, BARABARA YA "SINZA KWA WAJANJA" YAPEWA JINA LAKE -: "SHEKILANGO ROAD"!!!

$
0
0
1. Shekilango Road

Watanzania wengi wamewahi kuisikia au kuitumia moja ya barabara maarufu jijini Dar Es Salaam iitwayo "Shekilango Road". Barabara hii, kwa wale ambao hawaifahamu, inaanzia maungio ya "Morogoro road"  karibu kabisa na nyumba za NHC zilizo mkabala na kiwanda cha Urafiki ikielekea na kukutana na barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kituo cha Bamaga.

Ingawa wengi wanaifahamu barabara hii, hata hivyo wengi pia, hasa vijana wa Dot.com, hawaelewi jina hili limetokea wapi na wengine wanafikiri limetokana na aina ya miti iliyokuwa ikipatikana maeneo hayo!. La hasha!.

2. Shekilango Road imetokana na nini?

Jina "Shekilango Road" limetokana na jina la marehemu Mh. HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO. Huyu alikuwa ni Mbunge wa Korogwe (1975-1980)
na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye kabla ya ubunge alikuwa Meneja Mkuu wa "National Milling Cooperation".

3. Mh. Shekilango Alipewa Kazi Maalum Uganda na Mwalimu

Baba wa Taifa, Rais JULIUS KAMBARAGE NYERERE alimpa Mh. SHEKILANGO jukumu maalum la kuwa mratibu kati ya serikali ya Uganda na Tanzania baada ya kumalizika vita vya Kagera. Hii ilikuwa ni heshma kubwa kwa Mh. SHEKILANGO na jukumu zito.

Ikumbukwe kuwa baada ya vita hivyo, kilipita kipindi cha mpito cha utawala wa Mh. YUSUPH KIRONDWE LULE na Mh. GODFREY LUKONGWA BINAISA kilichokuwa na sintofahamu na machafuko makubwa.

Hivyo, Mwalimu alimteua Mh. SHEKILANGO chini ya usaidizi wa Mh. Balozi FARAJI A. KILUMANGA, aliyekuwa balozi wetu nchini Uganda, kuisaidia serikali ya Uganda isimame. Kazi hii waliifanya kuanzia Juni 1979.

4. Mh. Shikilango apanga miadi kukutana na Mwalimu Arusha:

Siku ya Jumapili, tarehe 11.5.1980, Mh. Waziri SHEKILANGO na Mh. Balozi KILIMUNGA walikuwa na miadi ya kukutana na Mwalimu jijini Arusha kwavile Rais NYERERE alikuwa kwenye ziara ya kiserikali jijini humo.

Viongozi hawa walikuwa wakienda kumtaarifu Baba wa Taifa juu ya hali ya usalama ya Uganda baada ya mfarakano kati ya Rais BINAISA na General DAVID OYITE OJOK aliyekuwa Mnadhim Mkuu wa Jeshi UG, mfarakano ulioonesha dalili zote za kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

5. Mh. Shekilango Akwea "Pipa" kwenda "Geneva ya Afrika"

Asubuhi na mapema siku hiyo ya Jumapili, tarehe 11.5.1980, Mh. SHEKILANGO aliongoza msafara wa maofisa wa serikali ya Tanzania uliokuwa ukitoka Uganda kuelekea Arusha kwa ndege ndogo aina ya Casena 402 yenye uwezo wa kuchukua watu 8.

Watu waliokuwemo kwenye msafara huo walikuwa 7:

1. Mh. Waziri HUSSEIN SHEKILANGO
2. Balozi FARAJI KILUMANGA
3. Mwanadiplomasia IDD MSECHU
4. Cpl. PETRO KALEGI MAGUNDA
5. Pte  STEVE MTAWA
6.Luteni MALLYA
7. Luteni LUOGA 

6. Mh. Shekilango na Msafara wake Wafariki kwa Ajali ya Ndege

Mwalimu NYERERE akiwa jijini Arusha akisubiri kuhabarishwa na Mh. SHEKILANGO kuhusu hali ilivyo nchini Uganda, alishangaa kuona muda wa miadi ukiwa umepita sana bila ya viongozi hao kufika ili kuonana naye.

Baada ya muda kupita, Mwalimu aliletewa habari za kuhuzunisha na kusikitisha sana na hakuamini maskio yake alipoelezwa kwamba ndege hiyo ndogo iliyokuwa imembeba Mh. SHEKILANGO na msafara wake ilianguka wakati tayari ilikuwa imeishaingia anga ya mkoani Arusha!.

Ndege hiyo ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) iliyokuwa ikiruka kati ya mita 5000 na 7000 kutoka usawa wa bahari ikielekea KIA ilipata ajali na kuanguka kati ya saa 4 na 5 asubuhi katika kijiji cha Engwiki wilaya ya Monduli, Arusha.

Vijana wawili kutoka kijiji cha Engwiki, Bw. MUNDEREI ANGERUKAI na Bw. NUSERIEKI NJONJOLOI ndio waliokuwa mashuhuda wa kwanza wa ajali hiyo waliosaidia kupatikana kwa ndege hiyo iliyolipuka baada ya kugonga kilima cha Kolomoniki kutokana na ukungu mkubwa uliokuws umetamalaki eneo hilo. Askari wa Chuo cha Uongozi wa Kijeshi Monduli walitumia masaa 5 kuitafuta ndege hiyo na vijana hao wawili hatimaye waliweza kuwaonesha ndege hiyo jioni ya Jumapili hiyo ya huzuni ambapo abiria wote walifariki na miili yao kuchukuliwa.

7. Mh. Shekilango azikwa na mamia Korogwe:

Mh. Waziri SHEKILANGO aliyekuwa kipenzi cha wana-Korogwe alizikwa  Jitengeni, Mombo, Korogwe , Tanga ambapo mazishi hayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu ulioweka rekodi ya aina yake wilayani Korogwe. Katika kumuenzi, shule moja eilayani Korogwe imepewa jina lake.

8. Barabara ya "Sinza kwa Wajanja" yapewa jina la Shekilango:

Kwakuwa wakati huo ujenzi wa barabara ya Sinza ndio ulikuwa umeanza, Uongozi wa jiji la Dar Es Salaam ukaamua kumuenzi marehemu SHEKILANGO kwa kuipa barabara hiyo jina lake. Ingawa wakazi wa Sinza ambao wengi ni wapangaji huji-mwambafy na kuita eneo hilo "Sinza kwa Wajanja", lakini miaka ya zamani Sinza ilikuwa ni usweken na eneo lote hilo la Sinza yalikuwa ni mashamba ya mipunga ambao ulikuwa ukistawi sana kwani maji hayako mbali chini ya ardhi na ndio maana hadi leo mvua ikinyesha kidogo tu Sinza , eneo lote huwa ni mafuriko matupu!.

9. Mh. Shekilango Aacha Mjane Ngangari:

Marehemu SHEKILANGO, aliyekuwa "amekwenda hewani" aliacha watoto ambao walikuwa wakifahamika kwa urahisi kutokana na urefu wao, pamoja na mkewe Mama ZAPPORA. Marehemu SHIKILANGO alikuwa akiishi Sea View, Dar Es Salaam kwa muda mrefu na baadae familia yake  ikahamia kwenye nyumba yao iliyopo Kinondoni Bwawani Kiwanja Na.401 Kitalu 42.

Mama ZAPPORA aliyezaliwa mwaka 1938 alikuwa ni mwalimu hodari sana na amefundisha shule nyingi hapa nchini. Aidha, alikuwa "Headmistress" shule za wasichana Zanaki, Kisutu, Jangwani, Forodhani, Msalato na Iringa girls sec school. Mama ZAPPORA, ambaye ni mmoja wa ma-Headmistress walioweka rekodi ya kuongoza shule nyingi nchini, alifariki tarehe 1.9.2018. Licha ya marehemu SHEKILANGO kufariki, lakini mwanamke huyu ngangari aliweza kuwalea wanae vizuri.

Mwisho:
Hivi ndivyo marehemu Waziri HUSSEIN SHEKILANGO alivyofariki na kupelekea barabara maarufu ya Sinza kupewa jina lake.


MWANARIADHA FAILUNA AFANIKIWA KUTETEA NAFASI YAKE MBIO ZA TAIFA ZA NYIKA

$
0
0
Na  Dixon Busagaga was Globu ya Jamii Kanda ya kaskazini.

MWANARIADHA Failuna Abdi Matanga amefanikiwa kutetea nafasi yake ya kwanza katika mashindano ya Mbio za Taifa za Nyika zilizopewa jina la Ngorongoro National cross Country 2019 kwa upande wa wanawake baada ya kumaliza wa kwanza akitumia muda wa 34:55:99 .

Nafasi ya pili kwa upande wa wanawake ilichukuliwa na Mwanariadha Magdalena Shauri aliyetumia muda wa dakika 35:20:32 akifuatiwa na Angelina Tsere aliyeshika nafasi ya tatu akitumia muda wa dakika 36:45:83.

Kwa upande wa wanaume Mwanariadha  Faraja Damas amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kuhitimisha mbio akitumia muda wa dakika 30:17:19.

Nafasi ya pili kwa wanaume imechukuliwa na Joseph Panga aliyemaliza mbio akitumia muda wa dakika 30:29:37 na nafasi ya tatu kuchukuliwa na Marco Sylvester Monko aliyetumia muda wa dakika 30:29:36.


Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi Katibu mkuu was shirkisho la riadha Tanzania,Whilheam Gidabuday amesema mashindano hayo yalikua na lengo la kupata wanariadha watakaounda timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya Dunia ya mbio za nyika nchini Denmark mwezi ujao.
Mwanaridha Faraja Damas akihitimisha mbio kwa kuruka mara baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Taifa ya Nyika yaliyofanyika mjini Moshi.
Wanariadha was mbio za Km 10 katika Mashindano ya Mbio za Taifa za Nyika wakianza kuondoka katika eneo la kuanzia Mbio hizo zilizo fanyika katika viwanja vya Moshi Club.
Mgeni rasmi katika mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika,mwakilishi wa mkuu was chuo cha polisi Moshi,Kamishna Msaidizi,Mihayo akiwa na wawakilishi wa taasisi na kampuni zilizo dhamini Mbio hizo zilizofanyika mjini Moshi ambao no Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Kampuni ya Mult Choice.

KANYASU ATAKA UJENZI IHUMWA UTUMIE ZAIDI VYUMA BADALA YA MBAO

$
0
0

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe

Constantine Kanyasu ametaka ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali yanayojengwa katika eneo la Ihumwa yajikite kutumia vyuma badala ya kutumia mbao ngumu ambapo kwa sasa Wizara ipo kwenye kampeni kubwa ya kuzuia matumizi ya miti hiyo ambayo ipo hatarini kutoweka

Amesema Wizara kwa sasa imepiga marufuku ukataji na usafirishaji wa magogo yanayozalisha mbao ngumu.Hayo yamesemwa na Naibu Waziri huyo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua hatua za ujenzi wa jengo hilo unaoendelea jijini Dodoma.

Amesema endapo majengo ya Wizara zote yatatumia mbao za aina hizo zaidi ya magogo ya miti 300 itakatwa.

Aidha, Mhe.Kanyasu ameshauri Jengo la Wizara hiyo lisitumie nguzo za mbao kwa upande wa mbele katika sehemu ya kuingilia kama inavyoonekana kwenye ramani badala yake itumie nguzo za zege ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Pia, Mhe.Constantine Kanyasu ametaka timu ya wataalam mbalimbali ifanye kazi kwa pamoja katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa jengo hilo la Wizara katika mji wa Kiserikali wa Ihumwa.

Amesema licha ya kuwa hatua ya ujenzi wa jengo hilo ni ya kuridhisha ila ametaka nguvu ziongezwe ili kuweza kulikamilisha jengo hilo ndani ya muda wa wiki mbili zijazo licha ya kuwa muda uliotolewa na Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tayari umeshapita.

Katika nyingine, Mhe Kanyasu ameshauri hatua za kupanda miti pamoja kuandaa bustani za maua zianze mapema katika jengo hilo ili likishakamilika liwe kwenye madhari nzuri badala ya kusubili hadi pale jengo litakapokamilika kabisa

Kwa upande wake, Mkandarasi wa Suma JKT, Clement Shaibu amemueleza Naibu huyo kuwa ujenzi unaendelea vizuri na wanatarajia kukamilisha ndani ya wiki mbili zijazo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja Wakandarasi akikagua jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii wakati alipotembelea eneo la Ihumwa jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akioneshwa mtindo wa paa kwa ndani utakavyokuwa katika jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkandarasi Clement Shaibu wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua jengo hilo linalojengwa Ihumwa jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa pamoja Wakandarasi akikagua jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ndani wakati alipotembelea eneo la Ihumwa jijini Dodoma.
Muonekano wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii katika hatua za mwisho wa kukamilika kwake katika mji wa kiserikali wa Ihumwa jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii (katikati) akiwa na Mkandarasi pamoja na Katibu wake, Zulu Ngondya (kulia) wakiangalia baadhi ya ramani ya jengo la Wizara hiyo mara baada itakapokamilika.(PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA)

KUAHIRISHWA UCHAGUZI NIGERIA WAZUA MJADALA KOTE NCHINI

$
0
0
Mwanamke huyu alikuwa tayari amefika katika kituo cha kupiga kura.

Hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais na ubunge nchini Nigeria saa tano kabla ya zoezi la upigaji imezua mjadala mkali kote nchini humo.

Baadhi ya watu ambao hawakua na habari uchaguzi umeahirishwa walikuwa wamefika klatika vituo vyao vya kupigia kura.

Musa Abubakar, ambaye alisafiri umbali wa kilomita 550 (340 miles) kutoka mji mkuu wa Abuja ili kupiga kura katika mji wa kaskazini wa Daura, ameiambia BBC "haamini" kilichotokea.

Yeye ni mmoja wa raia wengi wa Nigeria waliyosafiri kutoka mji mmoja hadi mwingine kushiriki zoezi la upigaji kura.

"Sijui la kufanya. Sijafurahia hatua hii hata kidogo," alisema bw Abubakar.

Sasa anakabiliwa na kibarua cha kuamua ikiwa atasubiri kupiga kura Daura kisha arudi kazini Abuja ama ajiandae kwa safari ya pili au kuachana kabisa na shughuli hiyo

Baadhi ya watu waliamua kuangazia hasira zao katika mtando wa kijamii wa Twitter, kwa kutumia Hashtag ya "waahirishwa", "kuahirishwa" na "Inec".

Bobby Ezidi, alisema tume ya uchaguzi imezembea katika kazi yake .Wengine wamekuwa wakisambaza kanda ya video inayomuonesha bw Yakubu akisisitiza kuwa kila kitu kiko shwari "uchaguzi hautaahirishwai" na kujiuliza nini kilichobadilika.

Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza hatua hiyo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura hii leo Jumamosi.

"Haiwezekani kuendelea na zoezi la uchaguzi kama ilivyopangwa," mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu amesema, akitaja hitilafu za kimipango.

Amesema uamuzi huo mgumu umehitajika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki.

KATIBU MKUU UWT TAIFA ANOGESHA MAADHIMISHO YA MIAKA 42 YA CCM SEKONDARI YA MSALATO MKOANI DODOMA

$
0
0
Katibu Mkuu Uwt Taifa Queen Mlozi ametembea shule sekondari ya Msalato iliyopo mkoani Dodoma na kutoa zawadi mbalimbali katika shule hiyo  ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 42 ya Chama cha Mapinduzi
 Katibu mkuu Uwt Taifa Queen Mlozi akikata Keki Jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 42 ya Chama cha Mapinduzi

WAZIRI LUGOLA AIPA POLISI WIKI MOJA KUFANYA UCHUNGUZI, KUWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WANAWAKE MTO WA MBU MKOANI ARUSHA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA-Monduli

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki moja, Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina kwa kuwakamata watuhumiwa waliofanya matukio ya kikatili ya ubakaji na mauaji ya wanawake yaliyotokea Mto wa Mbu Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha.

Akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Mto wa Mbu, wilayani humo, leo, kutokana na matukio hayo, Waziri Lugola amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, kushirikiana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, kuhakikisha uchunguzi wa kitelijensia unafanyika juu ya watu wanaohusika kufanya vitendo hivyo vya kikatili katika eneo hilo.

Lugola aliongeza kuwa, haiwezekani wananchi wa eneo hilo wawe wanaishi kwa wasiwasi, wanateswa, kuuawa na kudhalilishwa wakati Serikali ya Rais Dkt John Magufuli ipo, Polisi wapo, pamoja na wananchi wapo, kwa hatua hiyo lazima mauaji hayo yafikie kikomo.

"Ndugu wananchi Serikali ya Dkt Magufuli haiwezi kuchzewa hata kidogo, lazima tudhibiti hii taaruki, na tusipofanya hivi, hii hali itaendelea kushika kasi jambo ambalo Serikali haiwezi kukaa kimya,” alisema Lugola na kuongeza;

“Wakina mama wataisha kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na lazima tuwe na uchungu sasa, Jeshi la Polisi lijipange vizuri kwa kufanya kazi ya weledi kwa muda wa wiki moja hakikisheni mnafanya kazi nzuri ipasavyo ili kuwatia mbaroni hao watuhumiwa na kufunguliwa mashtaka haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola.

Lugola aliwatoa wasiwasi akina mama wa mji huo na kuwataka kuleta taarifa za siri kuhusiana na wahusika hao kwasababu hawatoki mbali bali katika mazingira hayo hayo wanayoishi.

“Mmependekeza mpige kura za kimya kimya kwa kuwa uwanjani mkiandika majina ya watuhumiwa, mkihofia mkipeleka taarifa Kituo cha Polisi kwa njia ya siri mnahofia mtakuja julikana, sijakataa njia mliopendekeza, lakini Polisi watafanya kazi hii ya kiitelejinsia hapa kwa umakini na watawakamata watuhumiwa,” alisema Lugola.

Lugola pia aliwataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa kina kwa polisi hao wakati wanafanya kazi zao, pia aliwapa angalizo polisi hao wasije wakakurupuka wakati wanafanya uchunguzi huo, wasiwaonee wananchi, wahakikishe wanakua makini ili wasije wakawasumbua ambao wananchi ambao wanafanya shughuli zao za kibiashara.

Aidha, Mjumbe wa Kijiji cha Kigongoni, Kata ya Mto wa Mbu, Tarafa ya Manyara, Wilayani humo, Devotha Steven alisema wanaiomba Serikali iongeze nguvu katika kuwalinda wanawake wa Mto wa Mbu kwani vitendo vya kikatili vimekuwa vya kusikitisha na pia wanakosa amani popote wanapofanya shughuli zao za kutafuta ridhiki.

"Mheshimiwa Waziri, ninazungumza kwa machungu, kwanini tunateseka na Serikali ipo, tunaamini mtasambaratisha haya mauaji, nasema kwa uchungu yatima wanaongezeka, tunaomba tupige kura na wanachi waitwe kutoka tarafa ya Manyara na Makuyuni ili wahusika wapatikane na tunaomba ulinzi utolewe kwa wale wananchi wanaotoa siri walindwe," alisema Devotha.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga, alifurahia ujio wa Waziri huyo, na pia alimwomba kiongozi huyo kupitia Jeshi lake, wawakamate wahalifu hao ambao wanafanya vitendo vya kikatili, ili ukatili huo uweze kukomeshwa.

Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake zilizopo ndani ya Wizara yake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mjumbe wa Kijiji cha Kigongoni, Kata ya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha, Devotha Steven, alipokuwa anaiomba Serikali iwakamate watuhumiwa wa mauaji ya wanawake katika Kata hiyo. Lugola ametoa wiki moja, Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina na kuwakamata watuhumiwa hao. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpa maelekezo Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha, Longinus Tibishubwamu (kushoto), kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya wanawake katika Kata ya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Wilaya ya Monduli, Gilbert Ngaizi, na wapili kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mto wa Mbu, Peter Ngoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mji wa Mto wa Mbu, wakati Waziri huyo alipohudhuria Sikukuu ya Maulidi iliyofanyika mjini humo, leo. Lugola aliwataka viongozi wa dini kuhubiri amani ili wananchi waache kufanya matukio ya uhalifu katika mji huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Dkt. Gwajima Atua Dar na Kampeni ‘Coordination’

$
0
0
Na. Atley Kuni- OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dkt. Dorothy Gwajima, amefanya ziara mkoani Dar-Es-Salaam huku akiendeleza kampeni yake ya kufanya kazi kwa ushirikiano aliyoianza mkoani Dodoma kwakuwataka watendaji serikali kutambua na kuheshimu ubunifu wa mtumishi mmoja mmoja.

“Viongozi wote ngazi zote tuzidi kuungana kutambua juhudi za kila mtumishi na hasa junior Staff, kwani ipo siri kubwa katika nguvu ya kutambua na kupongeza amabapo hata changamoto zitageuka kuwa fursa” alisema Gwajima

Gwajima alisema kuwa, mapungufu na uhaba vitageuka kuwa fursa kwakua macho na akili ya ndani vitafunguka na kukabiliana na hayo yote na kupata ufumbuzi wa matatizo mbalimbali katika sehemu za kazi wanapo watia moyo watumishi.

Katika ziara yake ya kwanza, aliyoifanya mkoani Dodoma Dkt.Gajima alikutana na Sekretarieti ya mkoa huo chini ya katibu Tawala wa Mkoa na hatimaye kufanya kikaokazi na Kamati ya Afya ya Mkoa, ambapo katika vikao vyote viwili alihimiza utendaji kazi wa pamoja (coordination, Harmonization, Involvement and Motivation)

Katika ziara hiyo ya Mkoa wa Dar-Es-Salaam, alipongeza jitihada za mtumishi Muuguzi Sarah John wa Zahanati ya Malambamawili Kata ya Msigani, Manispaa Ubungo kwa jitihada zake alizo onesha katika utendaji uliotukuka hasa katika kuhamasisha watu kwenda kwenye huduma za afya.

Dkt. Gwajima. Alisema, Muunguzi Sarah John katika Zahanati hiyo amekuwa chachu yakuhamasisha wateja wao kwa kuwatungia nyimbo, kuimba na kucheza nao hali iliyo pelekea watu katika Kata hiyo kumpenda kwa uwezo wake huo wakuhamasisha na kuwafanya watu wengi kuhudhuria katika huduma za afya kwenye kituo hicho kilicho anzishwa Julai, 2018 ndani ya kata hiyo.

“Siyo Rahisi kwa Muuguzi kujishusha hadi kucheza na wateja wake, inahitaji Moyo wa kupenda kazi, kulipenda taifa na uzalendo wa hali ya juu kutoka Moyoni” alisema Gwajima.

Bi. Sarah amekuwa akienda sambamba na Kauli mbiu ya Mhe. Rais yakutaka kila mtu azae bila kupangiwa idadi ya watoto, ila wazingatie malezi kwa wototo atakao wazaa kwa kuwapatia huduma za msingi.

Hii imekuwa ni ziara yake ya pili tokea Dkt. Gwajima, ateuliwe na Mhe. Rais kushika wadhfa Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI (Afya) ambapo katika ziara hiyo, waliungana na uongozi wa Kata ya Msigani na wananchi na watendaji kisha kufanya hamasa ya watu kushiriki katika huduma za afya msingi huku rai yake kubwa akiilekeza kwenye kufanya kazi kama timu moja ili kufikia maendeleo endelevu kwa watu kuwa na afya njema.
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Dorothy Gwajima, akiwa katika picha ya Pamoja na Muunguzi Sarah John na watumishi wengine wa Zahanati ya Malambamawili, mkoani Dar-es-salaam wakati wa ziara hiyo.
Dkt. Doroth Gwajima, alipowasili katika hicho Zahanati hiyo ya Malambamawili, akisaini kitabu cha wageni huku, watumishi wakiwa wamesimama nyuma yake kabla yakuanza ziara kwenye kituo hicho na kufanya hamasa ya huduma za Afya
Dkt. Dorothy Gwajima wakati wa ziara yake mikoani, akihimiza masuala yakufanya kazi kama timu ili kupata tija katika utendaji.

WANANCHI NJOMBE WASHAURI SERIKALI KUTOA ELIMU YA UMUHIMU WA KAYA KUWA KARIBU.

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Njombe

Wananchi mkoani Njombe wameishauri Serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya Kaya kuzingatia kukaa karibu ili kuongeza usalama na kuepuka vitendo vya utekaji na mauaji ya Watoto na vitendo vyote vya kihalifu.

Ushauri huo umetolewa leo wakati Timu ya Wataalam wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe walipoitembelea familia zilizopoteza watoto kutoka na vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto kwa lengo la kutoa pole na kutoa msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii. .

Wakiwa katika Familia ya Bw. Dau Ng'aala ya Kambarage Halmashauri ya Mji wa Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto wao Oliver Ng'aala(5) aliyepotea Desemba 07/2019 na kupatikana Desemba 08 akiwa amefariki.

Familia hiyo imesema kuwa suala la kaya kukaa mbali mbali imekuwa ni suala mbalo kwa sasa linatakiwa kufanyiwa kazi kwani kukaa karibu kunaongeza usalama kwao.

Bw. Dau Ng'aala ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Njombe kwa kuwekea mkazo katika uchunguzi wa matukio ya utekeaji na mauji ya watoto kwani yamesababisha huzuni kubwa kwa familia mkoa wa Njombe na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa wao kama familia watatoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya mamlaka katika kuhakikisha watuhumiwa wafikishwa katika sehemu husika na Sheria inafuata mkondo wake kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya kinyama.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bi. Teresa Yomo ameihakikishia ushirikiano familia ya Bw. Dau Ng'aala na familia zote zilizopatawa na matatizo kuwwa atahakikisha wanapata msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii ili kurudi katika hali ya kawaida.

“Tupo pamoja na tutahakikisha mnapata msaada wa kisaikolojia na kijamii kwani utawasaidia mrudi katika hali yenu ya kawaida kama zamani” alisema

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesisitiza umoja na mshikamano katika familia wakati huu huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku za uzalishaji mali.
Timu ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe (waliokaa watatu upande kulia) wakitoa huduma  kisaikolojia na kijamii kwa  Familia ya Bw. Danford Nziku iliyopoteza watoto watatu kutokana na vitendo vya utekeaji na mauaji ya Watoto vilivyotokea mkoani Njombe.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MRADI WA MAJI IKUNGI AMBAO UTAWANUFAISHA WANANCHI 2,628

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi wakifurahia mara baada ya Makamu wa Rais kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti ambapo mradi huo wa maji utawahudumia wakazi 2628.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma kibao cha zahanati ya Kijiji cha Mang’onyi mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo

ATAKAYEDOKOA FEDHA ZA SERIKALI ATAZITAPIKA-DC MBONEKO

$
0
0



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (pichani) amewataka watendaji wa serikali kutumia fedha zinazotolewa na serikali kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuepuka tamaa vinginevyo watakao kwenda kinyume watazitapika fedha hizo.

Mboneko ametoa kauli hiyo Februari 16,2019 wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM) Mhe.Azza Hilal Hamad akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Usule kuhusu shilingi milioni 146.6 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule ya msingi Masunula iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watu wote watakaobanika kutumia vibaya fedha za serikali. “Msithubutu kudokoa fedha za serikali, hakuna pesa ya serikali itapotea,ukidokoa utazitapika au tutakupeleka gerezani,fedha za serikali zinapokuja zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa,mnaponunua vifaa vya ujenzi nunueni kwa bei ya jumla na siyo reja reja”,alisema Mboneko. Aidha aliwataka wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwani serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu huku akisisitiza kuwa kuna maendeleo yanaletwa na serikali lakini mengine yanatokana na wananchi wenyewe.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad alisema kupatikana shilingi milioni 146.6 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za walimu na madarasa mawili kunatokana na jitihada kubwa aliyofanya kama mbunge kuipigania shule ya Msingi Masunula ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba.

“Shule ya Msingi Masunula kwa miaka mitatu mfululizo 2016,2017 na 2018 imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali kiwilaya na mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba…baada ya kulijua hilo, mimi nilisikitika na ninasikitika sana kusikia kwamba pamoja na jitihada kubwa za walimu wanazozifanya,eti walimu hapa shuleni hawana nyumba za kuishi lakini hata vyoo tu hawana”, “Hivi hawa walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa watoto wetu sisi tumeshindwa kujenga hata vyoo?,kweli ndugu zangu,kuna kitu gani hapa,yaani kabisa tunasimama tunasema shule yetu inaongoza kimkoa kwa ufaulu,kweli tuko sawa sawa kwa hili?”,alihoji Azza.

“Niliumia sana kuambiwa hakuna nyumba ya mwalimu hata mmoja,matokeo yake walimu wengine wanakaa Didia,nikaamua kulibeba na kwenda kulisemea kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipopita Tinde,nikaiomba serikali iangalie ya msingi Masunula na kwa sababu serikali yetu ni sikivu baada ya kuomba fedha Julai 2018,serikali imetuletea fedha shilingi milioni 146.6 mwezi Januari 2019”,alisema Azza.

Mh. Azza alieleza kuwa kati ya shule zote zilizopewa fedha,Masunula ndiyo shule iliyopewa fedha nyingi kama motisha kwa sababu ya matokeo mazuri na siyo vinginevyo. “Sasa ni jukumu letu wananchi kuhakikisha kuwa fedha tulizopewa twende tukajitolee,tukafanye nguvu kazi ili tuwe na uchungu,ni jukumu letu sasa kwamba tumepewa fedha ya kujenga nyumba mbili sisi tujenge tatu,kufanya kwenu vizuri itaonesha shukrani kwa serikali”,alisema.

“Nataka tuibadilishe Masunula,tuibadilishe kata ya Usule,Masunula ifanane na yale matokeo mazuri ya mtihani wa darasa la saba yanayosomeka kule, sasa siyo matokeo mazuri halafu wazazi hamtaki kuwaunga mkono watoto wetu,kwa sababu kama watoto wapo kwenye mazingira magumu,na walimu wanafundisha kwenye mazingira magumu na mazingira ndiyo haya,tukiwaboreshea mazingira matokeo yatakuwa mazuri zaidi,si mnaweza kusikia darasa la zima limefaulu!”,aliongeza Azza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masunula kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwahimiza watendaji wa serikali na wananchi kutumia fedha zinazotolewa na serikali kwa malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masunula kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akiwasisitiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wananchi wa kata ya Usule.

Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM).

Mwananchi akiuliza swali kwa viongozi waliofika katika kata hiyo.
Wananchi wakiwa katika eneo la mkutano.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi bati moja ikiwa ni sehemu ya mabati 20 aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Andrew Mitumba akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutoa mabati 20.
Mwenyekiti wa kijiji cha Masunula Kiyenze Majinge (kwenye nguo ya bluu) akiwaongoza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad na viongozi mbalimbali kwenda kuona eneo ambapo patajengwa nyumba za walimu pamoja na madarasa katika shule ya msingi Masunula.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masunula Gadius Kuyerwa ( wa nne kutoka kulia) akionesha na kuelezea kuhusu eneo ambapo patajengwa nyumba za walimu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko(wa pili kulia) na diwani wa kata ya Usule, Amina Bundala wakioneshana eneo la ujenzi wa nyumba za walimu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ametekeleza ahadi ya kuchangia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule zilizopo katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Azza amekabidhi mabati hayo yenye futi 10,Februari 16,2019 kwa viongozi wa vijiji vya Masunula na Usule ikiwa ni ahadi aliyotoa Oktoba 15,2018, alipotembelea kata ya Usule na kuelezwa kuwa shule hizo zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Akizungumza wakati wa zoezi kukabidhi mabati lililoshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko, Azza alisema mchango wake huo ni sehemu ya kuboresha shule ya Masunula ambayo kwa miaka mitatu mfululizo (2016,2017 na 2018) imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba. 

“Nilipewa malalamiko ya vyoo shule ya msingi Usule na shule ya msingi Masunula,nikaahidi kuchangia mabati 20,leo nimekuja kukamilisha ahadi yangu,hivyo nakabidhi mabati 10 yenye futi 10 kwa kila shule”,alisema. 

Mheshimiwa Azza aliwataka wananchi kuacha kufanya siasa kwenye masuala ya maendeleo huku akiwahamasisha wananchi kujenga vyoo kwenye nyumba zao. Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala alimshukuru mbunge huyo kutekeleza ahadi yake na kuongeza kuwa tayari matundu 14 ya vyoo yamejengwa katika shule ya Masunula na sasa wanaendelea na shughuli ya kuezeka majengo ya vyoo hivyo. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kusomesha watoto wao na kuachana na tamaa za kuwaozesha huku akiwataka kutumia fedha wanazopata kutokana na kilimo kujenga nyumba za kisasa. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Masunula, Kiyenze Majinge (CUF). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Usule na Masunula.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika eneo ambapo pamejengwa vyoo vya shule katika shule ya msingi Masunula. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akieleza jambo katika eneo la ujenzi wa vyoo kwenye shule ya msingi Masunula. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA ZAO LA MICHIKICHI CHA KIHINGA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mbegu ya mchikichi inayoonyesha tabaka la mafuta wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Mwandamizi na Mratibu wa Utafiti wa Kilimo mkoani Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya mchikichi iliyochavushwa kitlaam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



KILIMO WEZESHENI WATAFITI WA MICHIKICHI-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iwawezeshe watafiti katika kituo cha Utafiti cha zao la michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma ili waweze kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu bora za zao hilo.

Amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu kwenye zao hilo la michikichi, hivyo Wizara ya Kilimo haina budi kukiwezesha kituo hicho kwa lengo la kuzalisha mbegu bora zitakazosambazwa kwa wakulima.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 17) wakati alipotembelea kituo cha Kihinga kwa ajili ya kukagua shughuliza uzalishaji wa mbegu za michikichi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Amesema Serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, ambapo kwa mwaka inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.“Wizara ya Kilimo iwawezeshe watu wa utafiti ili waendelee na shughuli hiyo kwa kasi, iwaongeze watumishi kituoni hapa na ongezeni nguvu kwenye zao la michikichi kama yalivyofanya Mataifa mengine ya Costa Rica na Malaysia.”

Amesema wakulima wa zao hilo wanahitaji kupata mafanikio, hivyo kituo hakina budi kuongeza nguvu ya uzalishaji wa mbegu bora. Ili wafikie malengo amewasahauri washirikiane na taasisi binafsi zinazozalisha mbegu.

Pia Waziri Mkuu amesema chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga, kiendelee kutoa elimu na Wizara ya Kilimo ijenge majengo yake inayoyahitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za utafiti. Eneo la chuo linaukubwa kwa hekta 920.Kwa upande wake, Mratibu wa Utafiti wa Kilimo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo amesema michikichi iliyopo sasa inauwezo wa kuzalisha tani 1.6 ya mawese kwa hekta moja ambao kidogo na hauna tija.

Amesema mbegu wanazozizalisha zinalenga kumuongeza tija mkulima kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani nne kwa hekta, pia wanaendelea kuangalia vinasaba vya mbegu vilivyopo ili wazalishe mbegu bora zaidi.

“Tutakusanya vinasaba vyote vya mbegu tulivyonavyo na kuvitathimini na kuona uwezo wake na ikibidi tutaagiza kutoka nje ya nchi ili kuboresha zaidi.” Miche ya michikichi inachukua muda wa miezi 18 kutoka hatua ya uchavushaji hadi kusambazwa kwa wakulima.

Baada ya kumaliza shughuli ya ukaguaji wa uzalishaji wa mbegu kituoni hapo, Waziri Mkuu alikagua shamba la michikichi la Gereza la Kwitanga lenye ukubwa wa ekari 400 na kupanda mche kama ishara ya uzinduzi wa upandaji wa miche bora shambani hapo.Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu katika zao hilo na inategemea taasisi zake mbili za Jeshi la Magereza (Kwitanga) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT-Bulombora), ambazo zinamashamba makubwa ya michikichi.

Kadhalika Waziri Mkuu ameagiza elimu kuhusu kilimo cha zao la michikichi kuanzia hatua za awali hadi uzalishaji wa mafuta itolewe mashuleni ili wanafunzi waanze kupata ulewa na ifikishwe hadi kwa wananchi.

Mwelekeo Wa Mvua Za Masika Machi Hadi Mei 2019 huu hapa

RC NDIKILO AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA AFYA IKWIRIRI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo ameweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Ikwiriri, Rufiji, ambacho kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charles Kabeho alikataa kuweka jiwe hilo July 2018,kutokana na mkanganyiko wa taarifa baina ya wilaya na mkoa .

Akizungumza baada ya kuweka jiwe hilo la msingi, Ndikilo alisema walichukua hatua ya kufanya uchunguzi kupitia vyombo vya dola na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na kubaini hakuna wizi uliofanyika kwenye ujenzi huo. 

"Kama kuna miundombinu kwa baadhi ya majengo haijakamilika iangaliwe namna ya kuikamilisha ,katika vituo vyote vya afya vinavyojengwa mkoani hapa "alisema Ndikilo .Aidha, alieleza wamepokea bilioni 8.2 kwa ujenzi wa vituo vya afya na bilioni 4.5 kwa ajili ya hospital tatu za wilaya. 

Ndikilo, aliwaomba watumishi wa afya kutoa huduma bora ya afya kwa wananchi wanaofuata matibabu mbalimbali. 

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Rufiji, Mohammed Mchengelwa aliishukuru serikali, kwa kuimarisha sekta hiyo na imeshatoa zaidi ya sh. milioni 320 kuboresha sekta ya afya wilayani Rufiji. 

Awali, mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo alibainisha, wamejiridhisha kiwilaya hivyo kumuomba mkuu wa mkoa kufanya zoezi hilo. 

Njwayo, alimpongeza Kabeho kwa ufuatiliaji aliouonyesha wakati wa mbio za mwenge hali iliyosababisha kila halmashauri kuwa makini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 


TBS YAMALIZA KAMPENI YAKE KANDAA YA ZIWA,YAWAFIKIA WANANCHI WENGI ZAIDI

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake kanda ya Ziwa ya kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika shule za msingi na sekondari, maeneo ya Soko,Stendi,Minadani na maeneo mengine ya wazi ambako
wananchi walijitokeza kupata elimu sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi Bi.Gladness Kaseka amezidi kuwakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote,Kaseka alisema kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 14, 929 kati yao wajasiriamali 127,wanafunzi wa Sekondari na Shule ya msingi 3868 na wananchi 10,934.

Aliongeza pia wananchi wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko lao na kuhakikisha wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali kama nafaka,sabuni, maziwa,asali na unga lishe,juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS na kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.Kampeni hii imefanyika kwenye ngazi ya wilaya ikiwamo wilaya ya Bukoba,Kahama,Tarime na Nyamagana.

Pichani ni Mhandisi Paul Ndege kutoka TBS akitoa Elimu kwa Wafanyabiashara, wafugaji na wananchi kam walivyokutwa mnadani Tarime
Elimu juu ya Udhibiti Ubora ikiendelea kutolewa Shuleni Sirari na Mhandisi Paul Ndege wa (Afisa udhibiti Ubora TBS, Tarime.)
Sehemu ya Wajasiriamali Wa Kahama waliohudhulia semina ya Siku moja kujifunza elimu ya Udhibiti Ubora Mkoani Shinyanga.
Pichani Bwn Evarist Mrema (Kaimu Mkuu TBS Kanda ya ziwa) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza.
Pichani ni Afisa Uhusiano wa TBS Neema Mtemvu akigawa kipeperushi kwa Mkazi wa Bukoba, Mkoani Kagera mara baada ya kuelimishwa juu ya Utambuzi wa bidhaa hafifu
Pichani ni Afisa Masoko mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka akikagua bidhaa kwa mjasiliamali wa vitafunwa, maeneo ya Soko Kuu Bukoba Kagera.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA IKUNGI MKOANI SINGIDA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imetekeleza kwa asilimia kubwa mambo yaliohaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015. Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi zaidi ya 2600 wa kijiji cha Ulyampiti, wilayani Ikungi mkoa wa Singida.

Ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Singida, Makamu wa Rais ametoa agizo kwa Wizara ya Maji kuhakikisha katika mpango wa visima 20 wilayani Ikungi kimoja kichimbwe kijiji cha Mang’onyi. Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alitembelea zahanati ya Mang’onyi na kituo cha afya cha Ihanja na kujionea maboresho mbali mbali ikiwa pamoja na kufungwa mashine mpya ya upasuaji.

Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Ihanja Madukani Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi hao ikiwa na kuzitaka mamlaka husika kutoa elimu ya kutosha ili kila mwananchi aelewe mpango wa Serikali wa Bima kwa wote. Aidha Makamu wa Rais amewataka wakazi wa Ihanja kutoruhusu mimba za utotoni kwani zinawanyima fursa ya mabinti wao kuja kuwa viongozi na wataalam wa badae, pia aliwasihi wananchi kuacha kukeketa mabinti kwani ukeketaji una athari nyingi zikiwemo vifo wakati wa kujifungua.

Makamu wa Rais amechangia mabati 200 kuunga mkono juhudi za Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi. Wakati huohuo Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu amesema Chama na Serikali ni kitu kimoja kwani wanashirikiana katika kila jambo la kuleta maendeleo kwa wananchi ambapo ilani ya uchaguzi imetekelezwa kwa kiwango kikubwa. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.
Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi wakifurahia mara baada ya Makamu wa Rais kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti ambapo mradi huo wa maji utawahudumia wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

GEREZA LA KWITANGA LIPATIWE KIWANDA CHA KISASA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Viwanda na Biashara ihakikishe gereza la Kwitanga mkoani Kigoma linapata kiwanda bora na cha kisasa cha kukamulia mafuta ya mawese kitakachoonesha dhamira ya Serikali ya kufufua zao la michikichi nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na jitihada zilizofanywa na Jeshi la Magereza katika kuboresha shamba lake la michikichi pamoja na mabadiliko waliyoyafanya kwenye kiwanda chao cha kuzalisha mafuta.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 17) wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga kwa ajili ya kukagua shamba la michikichi na kuzindua trekta na kufungua sero moja iliyojengwa gerezani hapo.
Amesema amefurahishwa baada ya kukuta mashine mpya ya kukamulia mafuta ya mawese inafungwa kwenye kiwanda cha gereza hilo ambayo itakuwa inatumia mota tofauti za zamani wapolikuwa wanatumia mashine ya kusukumwa na mikono.

Kadhalika Waziri Mkuu ameliagiza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) waimarishe teknolojia ya kukamua mafuta kwenye kiwanda hicho ili kiweze kuzalisha kwa tija.

Katika kuhakikisha gereza hilo linakuwa la mfano kwenye kilimo cha zao la michikichi, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inunue gari lenye winchi litakalorahisisha uvunaji wa chikichi.

Waziri Mkuu amesema njia inayotumiwa kwa sasa ya kupanda juu ya mchikichi wakati wa mavuno si salama kwa mvunaji, hivyo ni vema wakatumia magari hayo yenye winchi kwa ajili ya kurahisisha shughuli ya uvunaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, Leonard Burushi amesema wamefanikiwa kuongeza uzalishaji wa mafuta kutoka pipa 63.4 kwa mwaka 2016/2017 na kufikia pipa 97 kwa mwaka 2018/2019 na zoezi la uvunaji bado linaendelea.

Amesema mafanikio hayo yametokana na maagizo yalitolewa na Waziri Mkuu alipotembelea gereza hilo Julai, 2018, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaagiza waboreshe eneo la kukamulia mafuta ili waongeze uzalishaji.

Kiongozi huyo wa Magereza mkoa wa Kigoma amesema eneo la ekari 20 limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kukamua mafuta ya mawese, maghala ya kutunzia mafuta machafu na upanuzi wa kiwanda baadae.

Amesema maelekezo mengine yaliyotolewa na Waziri Mkuu ni pamoja na Magereza ya Kwitanga na Ilagala yaongeze eneo la mashamba yake kwa ajili ya kupanda michikichi mipya ambalo limetekelezwa. Amesema tayari gereza la Ilagala limeandaa jumla ya ekari 150 zenye uwezo wa kupandwa michikichi aina ya tanera 8,550 na Kwitanga ekari 400 ambazo zitapandwa miche 22,800 ya michikichi aina ya tanera.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Kamishina wa  Magereza Nchini, Fhaustine Kasike wakati alipowasili kwenye Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma  akiwa katika ziara ya kufufua zao la michikichi mkoani humo Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mchikichi ikiwa ni ishara ya kuzindua mpango wa kupanua mashamba ya michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Sero katika Gereza la Kwitanga  Mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. Gereza hilo ni maarufu kwa kilimo cha michikichi.  Kulia ni mkewe Mama Mary na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenrali Mstaafu, Emmanuel Maganga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama mashine ya kukamua mafuta ya mawese wakati alipotembelea Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma ambalo ni maarufu kwa kilimo cha michikichi, Februari  17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary wakitoka baada ya kuzindua  sero  katika Gereza la Kwitanga, maarufu kwa kilimo cha michikichi, Mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. Walikuwa katika ziara yenye lengo la kufufua zao la michikichi mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua matrekta mawili aina ya Ursus yenye thamani ya shilingi milioni 145 yatakayosaidia kuinua kilimo cha michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma Februari 17, 2019.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha Trekta aina ya Ursus wakati alipozindua matrekta mawili yatakayosaidia kuinua kilimo cha michikichi katika Gereza la Kwitanga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019.(Picha na Ofisi a Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Wizara ya Elimu alipowasi katika viwanja vya Skuli ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A'Unguja akiendelea na ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Program Meneja wa Africa Foundation ya Hoteli ya Mnemba Ndg. Mkomeni Erinest Mgono, Taasisi hiyo imejenga majengo ya madara manne kwa ajili ya Skuli ya Sekondari ya Kijini.alipowasili katika viwanja vya majengo ya Skuli hiyo kuweka jiwe la Msingi akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiri kuweka jiwe la Msingi la Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kazkiazini 'A' Unguja akiwa katika ziara yake kutewmbelea Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja leo, 17-2-2019.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kufungua Madaraza ya Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe, wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja Wilaya ka Skazini 'A' akishuhudua Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kuonesha Ilani ya CCM, wakati ufunguzi wa Madarasa ya Skuli ya Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja akiwa katika ziara yake katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.17-2-2019.(Picha na Ikulu)

 WANANCHI wa Kijiji cha Kijini na Mbuyu Tende Malemwe wakimasikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Majengo ya Madarasa ya Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe leo 17-2-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Kijini na Mbuyu Tende Matemwe wakati wa hafla ya ufunguzi wa Madarasa Mnne ya Skuli ya Seondari ya Kijini yaliojengwa kupitia Kampuni ya And Beyond ya Mnemba  Island Lodge Matembe Zanzibar.(Picha na Ikulu)   

DStv, Ngorongoro wafanikisha kupatikana timu ya taifa

$
0
0
Mashindano ya taifa ya Mbio za Nyika yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini moshi kwa udhamini wa DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, yamefanikisha uteuzi wa timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za nyika yatakayofanika nchini Denmark mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Akitangaza timu hiyo mara baada ya mashindano hayo ambayo yanaelezewa kuwa na washiriki wengi ukilinganisha na miaka ya nyuma, katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania Wilhelm Godabuday amesema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ufanisi mkubwa kwani yameshirikisha wanariadha wengi na pia kumekuwa na wanariadha wapya ambao wameonyesha uwezo mkubwa.

Timu hiyo ya taifa inajumuisha jumla ya wachezaji 28 katika Makundi manne ambapo kundi la kwanza ni wanaume wa umri wa zaidi ya miaka 18, la pili ni wanawake umri zaidi ya miaka 18, la tatu ni wavulana chini ya miaka 18 na la nne ni wasichana chini ya miaka 18

Wachezaji watakaokua katika kundi la wanaume weney umri wa zaidi ya miaka 18 ni Faraja Damas(Arusha), Joseph Panga(Arusha), Sylvester Marco (Arusha), Stephano Huche (Arusha), Deogratius Nade (Manyara), Yohane Elisante (Arusha) na Bazil Sule (Polisi)

Kwa upande wa wanawake katika kundi hilo ni Failuna abdi (Arusha), Magdalena Shauri (JKT)Anjelina Daniel (Arusha), Amina Mohamed (Arusha), Marselina Issa (Arusha) na Neema Msuad (Arusha).

Kundi la wavulana chini ya miaka 18 litakuwa na wachezaji saba ambao ni Michael Kishimba (Arusha), Daniel Sinda (Arusha) Emmanuel Joseph (Manyara) Francis Damiano (Mbulu), Saimon Francis (Arusha) na Nicodemo Joseph (Mbulu) wakati wasichana watakuwa ni Agnes Protus (Arusha), Anastazia Ndoromongo (Arusha) Aisha Luguna (Arusha) Sara Hiti (JKT) Gace Jackson (JKT) Noela Lemmy (Arusha na Catherine Philipo (Manyara).

Kambi hiyo itakuwa chini ya jopo la wataalamu nane wakiongozwa na Kocha wa riadha Meta Petro kutoka Klabu ya Riadha ya Rift Valley. wengine ni Anthony Mwingereza (JWTZ), Anrea Panga (JKT), Thomas Tlanka (Arusha) na Juma Jambau (Singida). Mwanariadha maarufu mstaafu Marcelina Gwandu ameteuliwa kua muangalizi (Matron) wa Kambi hiyo huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Hamad Ndee akipewa jukumu la kuratibu mafunzo hayo

Akizungumza muda mfupi baada ya Mashindano hayo, Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania (DStv) Johnson Mshana, amesema kuwa DStv imekuwa ikishiriki kwa muda mrefu sasa katika kuinua mchezo wa riadha hapa nchini na kwamba ushiriki wao katika kufanikisha mashindano hayo ni katika mkakati wake endelevu wa kuhakikisha kuwa vipaji vya wanariadha wetu vinakuzwa na hatimaye kuweza kuliletea taifa medali katika mashindano ya kimataifa.

“Tuna mkakati kabambe wa ‘Ni Zamu Yetu’ ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa wimbo wetu wa taifa unapigwa katika michuano ya Olympic – hii ikimaanisha kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata medali katika mashindano hayo makubwa “ alisema Mshana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo pia kutaifanya riadha kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya ajira na kipato kwa wanariadha na taifa kwa ujumla huku pia ukiwa ni ulingo mzuri wa kuitangaza nchi yetu kimataifa.

Timu hiyo ya taifa itaweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia kambi ambayo inafadhiliwa na DStv na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
 Wanariadha wa kundi la wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wakicuana vikali katika mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
 Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johsnon Mshana (Kushoto) akizungumza wakati wa kutangazwa kwa timu ya taifa yam bio za nyika mjini Moshi. Timu hiyo imetangazwa baada ya mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo ndiyo yaliyozalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
 Wanariadha wa kundi la wavulana wenye umri wa chini ya miaka 18 wakikata mbuga wakati wa mashindano ya taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
 Mwanariadha kinda ambaye pia ni balozi maalum wa DStv Francis Damiano damasi (mwenye namba 074) akiongoza katika kundi la wavulana wenye umri wa chini ya miaka 18 wakati wa mashindano ya taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Wengine ni Katibu mkuu wa shirikisho la riadha tanzania Wilhelm Gidabuday(kulia) na  Makamu rais wa shirikisho la riadha Tanzania
DStv, Ngorongoro wafanikisha kupatikana timu ya taifa Mashindano ya taifa ya Mbio za Nyika yaliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini moshi kwa udhamini wa DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, yamefanikisha uteuzi wa timu ya taifa itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mbio za nyika yatakayofanika nchini Denmark mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. Akitangaza timu hiyo mara baada ya mashindano hayo ambayo yanaelezewa kuwa na washiriki wengi ukilinganisha na miaka ya nyuma, katibu mkuu wa shirikisho la riadha Tanzania Wilhelm Godabuday amesema mashindano ya mwaka huu yamekuwa na ufanisi mkubwa kwani yameshirikisha wanariadha wengi na pia kumekuwa na wanariadha wapya ambao wameonyesha uwezo mkubwa. Timu hiyo ya taifa inajumuisha jumla ya wachezaji 28 katika Makundi manne ambapo kundi la kwanza ni wanaume wa umri wa zaidi ya miaka 18, la pili ni wanawake umri zaidi ya miaka 18, la tatu ni wavulana chini ya miaka 18 na la nne ni wasichana chini ya miaka 18 Wachezaji watakaokua katika kundi la wanaume weney umri wa zaidi ya miaka 18 ni Faraja Damas(Arusha), Joseph Panga(Arusha), Sylvester Marco (Arusha), Stephano Huche (Arusha), Deogratius Nade (Manyara), Yohane Elisante (Arusha) na Bazil Sule (Polisi) Kwa upande wa wanawake katika kundi hilo ni Failuna abdi (Arusha), Magdalena Shauri (JKT)Anjelina Daniel (Arusha), Amina Mohamed (Arusha), Marselina Issa (Arusha) na Neema Msuad (Arusha). Kundi la wavulana chini ya miaka 18 litakuwa na wachezaji saba ambao ni Michael Kishimba (Arusha), Daniel Sinda (Arusha) Emmanuel Joseph (Manyara) Francis Damiano (Mbulu), Saimon Francis (Arusha) na Nicodemo Joseph (Mbulu) wakati wasichana watakuwa ni Agnes Protus (Arusha), Anastazia Ndoromongo (Arusha) Aisha Luguna (Arusha) Sara Hiti (JKT) Gace Jackson (JKT) Noela Lemmy (Arusha na Catherine Philipo (Manyara). Kambi hiyo itakuwa chini ya jopo la wataalamu nane wakiongozwa na Kocha wa riadha Meta Petro kutoka Klabu ya Riadha ya Rift Valley. wengine ni Anthony Mwingereza (JWTZ), Anrea Panga (JKT), Thomas Tlanka (Arusha) na Juma Jambau (Singida). Mwanariadha maarufu mstaafu Marcelina Gwandu ameteuliwa kua muangalizi (Matron) wa Kambi hiyo huku Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Hamad Ndee akipewa jukumu la kuratibu mafunzo hayo Akizungumza muda mfupi baada ya Mashindano hayo, Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania (DStv) Johnson Mshana, amesema kuwa DStv imekuwa ikishiriki kwa muda mrefu sasa katika kuinua mchezo wa riadha hapa nchini na kwamba ushiriki wao katika kufanikisha mashindano hayo ni katika mkakati wake endelevu wa kuhakikisha kuwa vipaji vya wanariadha wetu vinakuzwa na hatimaye kuweza kuliletea taifa medali katika mashindano ya kimataifa. “Tuna mkakati kabambe wa ‘Ni Zamu Yetu’ ambao lengo lake kubwa ni kuhakikisha kuwa wimbo wetu wa taifa unapigwa katika michuano ya Olympic – hii ikimaanisha kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata medali katika mashindano hayo makubwa “ alisema Mshana na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo pia kutaifanya riadha kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya ajira na kipato kwa wanariadha na taifa kwa ujumla huku pia ukiwa ni ulingo mzuri wa kuitangaza nchi yetu kimataifa. Timu hiyo ya taifa itaweka kambi jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya dunia kambi ambayo inafadhiliwa na DStv na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro. Caption: Photo 1: Wanariadha wa kundi la wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 18 wakicuana vikali katika mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Caption: Photo 1.1: Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Johsnon Mshana (Kushoto) akizungumza wakati wa kutangazwa kwa timu ya taifa yam bio za nyika mjini Moshi. Timu hiyo imetangazwa baada ya mashindano ya taifa yam bio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo ndiyo yaliyozalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Caption: Photo 2: Wanariadha wa kundi la wavulana wenye umri wa chini ya miaka 18 wakikata mbuga wakati wa mashindano ya taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Caption: Photo 3: Mwanariadha kinda ambaye pia ni balozi maalum wa DStv Francis Damiano damasi (mwenye namba 074) akiongoza katika kundi la wavulana wenye umri wa chini ya miaka 18 wakati wa mashindano ya taifa ya mbio za nyika yaliyofanyika Moshi mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yamezalisha timu itakayoliwakilisha taifa kwenye mashindano ya dunia ya mbio hizo yatakayofanyia kwishoni mwa mwezi Machi nchini Denmark. Mashindano hayo yalidhaminiwa na DStv na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Wengine ni Katibu mkuu wa shirikisho la riadha tanzania Wilhelm Gidabuday(kulia) na Makamu rais wa shirikisho la riadha Tanzania

WANANCHI NJOMBE WASHAURI SERIKALI KUTOA ELIMU YA UMUHIMU WA KAYA KUWA KARIBU

$
0
0
Wananchi mkoani Njombe wameishauri Serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya Kaya kuzingatia kukaa karibu ili kuongeza usalama na  kuepuka vitendo vya  utekaji na mauaji ya Watoto na vitendo vyote vya kihalifu.

Ushauri huo umetolewa leo wakati Timu ya Wataalam wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe walipoitembelea familia zilizopoteza watoto kutoka na vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto kwa lengo la kutoa pole na kutoa msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii.  .

Wakiwa katika Familia ya Bw. Dau Ng'aala ya Kambarage Halmashauri ya Mji wa Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto wao Oliver Ng'aala(5) aliyepotea Desemba 07/2019 na kupatikana  Desemba 08 akiwa amefariki.

 Familia hiyo imesema kuwa suala la kaya kukaa mbali mbali imekuwa ni suala mbalo kwa sasa linatakiwa kufanyiwa kazi kwani kukaa karibu kunaongeza usalama kwao.

Bw. Dau Ng'aala ameishukuru Serikali ya Mkoa wa Njombe kwa kuwekea mkazo katika uchunguzi wa matukio ya utekeaji na mauji ya watoto kwani yamesababisha huzuni kubwa kwa familia mkoa wa Njombe na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa wao kama familia watatoa ushirikiano kwa vyombo vyote vya mamlaka katika kuhakikisha watuhumiwa wafikishwa katika sehemu husika na Sheria inafuata mkondo wake kwa wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya kinyama.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bi. Teresa Yomo ameihakikishia  ushirikiano familia ya  Bw. Dau Ng'aala na familia zote zilizopatawa na matatizo kuwwa atahakikisha wanapata msaada wa huduma za kisaikolojia na kijamii ili kurudi katika hali ya kawaida.

“Tupo pamoja na tutahakikisha mnapata msaada wa kisaikolojia na  kijamii kwani utawasaidia mrudi katika hali yenu ya kawaida kama zamani” alisema

Kwa upande wake Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesisitiza umoja na mshikamano katika familia wakati huu huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku za uzalishaji mali.
Timu ya Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mkoa wa Njombe (waliokaa watatu upande kulia) wakitoa huduma  kisaikolojia na kijamii kwa  Familia ya Bw. Danford Nziku iliyopoteza watoto watatu kutokana na vitendo vya utekeaji na mauaji ya Watoto vilivyotokea mkoani Njombe. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images