Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI NISHATI AWATAKA WANA-PWANI WACHANGAMKIE UMEME WA REA

$
0
0
Na Veronica Simba – Pwani 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani, hususan wanaopitiwa na Mradi wa Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuchangamkia fursa hiyo kutokana na unafuu wa gharama zake.

Alitoa rai hiyo jana, Februari 15, 2019 kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi katika wilaya za Rufiji na Kibiti.

Alisema, gharama za uunganishaji umeme wa REA kwa kila mwananchi ni shilingi 27,000 tu lakini pindi mradi huo utakapoisha muda wake, gharama za uunganishaji zitakuwa kubwa zaidi. 

Hivyo, aliwaasa wananchi kutumia fursa hiyo ipasavyo kwa kujitokeza kwa wingi kulipia ili waunganishiwe.Aidha, Naibu Waziri aliwataka wananchi walio katika maeneo ambayo miradi mbalimbali ya umeme ilikwishapita na hawakufikiwa, kutulia kwani iko miradi mingine itakayotekelezwa katika maeneo yao hususan mradi wa ujazilizi (Densification).

Akifafanua, alisema, hakuna mwananchi au eneo ambalo litaachwa pasipo kupelekewa huduma ya umeme; ndiyo maana serikali kupitia Wizara ya Nishati, inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuyafikia maeneo yote na kuhakikisha wananchi wote wanapata umeme, zoezi linalofanyika hatua kwa hatua.

Vilevile, Naibu Waziri Mgalu aliutaja mradi mkubwa wa umeme wa maji ya mto Rufiji maarufu kama Stiegler’s, ambao tayari mkandarasi amekabidhiwa rasmi kuanza kuujenga; kuwa utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Pwani ambao ndiyo mkoa unaoubeba mradi husika.

Akiwa wilayani Rufiji, aliwataka kuzitumia fursa zitakazotokana na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Rufiji katika eneo lao kwa kuwa wabunifu ili kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali.“Mradi wa Stiegler’s utaanza na ni fursa kwenu wana-Rufiji. Rai yangu tujipange kutumia fursa hizo. Rufiji hii itakuwa nyingine.”

Akiwa katika Kata ya Ngarambe, Naibu Waziri alitoa taa zinazotumia nguvu ya jua (solar), kwa wauguzi wa Zahanati za Ngarambe na Tapika wilayani Rufiji, ili kusaidia utoaji huduma kwa wagonjwa, wakati wakisubiri kufikiwa na huduma ya umeme. Pia, alitoa msaada wa mashuka katika Zahanati hizo.

Kwa upande wao, viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kibiti na Rufiji, viongozi wa Halmashauri na Mbunge wa Kibiti, walipongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Nishati, katika kuhakikisha maeneo mbalimbali yanafikiwa na huduma ya umeme.

Waliomba jitihada hizo ziendelee kwa kasi ili kuyafikia maeneo yote hususan ya vijijini.Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Mgalu aliambatana na viongozi na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA. Alitembelea vijiji vya Ngarambe, Azimio, Umwe, Kitembo na Mkupuka.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akiwakabidhi wauguzi wa Zahanati za Ngarambe na Tapika wilayani Rufiji, vifaa mbalimbali zikiwemo Taa zinazotumia umeme jua (solar) ili kuboresha utoaji huduma kwa wagonjwa. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi wilayani humo Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngarambe, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisalimiana na watumishi mbalimbali wa Halamshauri ya Wilaya ya Rufiji, alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo (mwenye fulana ya njano), alipomtembelea ofisini kwake, Februari 15, 2019 akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na wataalamu kutoka wizarani, REA na TANESCO.
Mmoja wa wakazi wa Ngarambe wilayani Rufiji, akitoa maoni yake kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (hayupo pichani); wakati wa ziara yake wilayani humo, Februari 15, 2019.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha pinki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, maafisa kutoka wizarani, REA na TANESCO. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi wilayani humo, Februari 15, 2019.

IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

$
0
0
NA OWM (KVAU) - KONGWA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameridhishwa na utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Wilaya ya Kongwa.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo kuangalia hali ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Akitoa pongezi hizo, Naibu Waziri, Ikupa alisema kuwa ushirikishwaji wa kundi hilo maalum ni jambo la msingi katika kuhakikisha haliachwi nyuma kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.“Endeleeni kuwajali na kuweka mipango thabiti yenye kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa kama wengine,” alisema Ikupa. 

Pia, aliipongeza wilaya ya kongwa kwa kusaidia Watu wenye Ulemavu kuhudhuria maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa yanayofanyika hapa nchini.
“Matukio hayo yamekuwa yakiwapa hamasa kubwa na kuona fursa ambazo zinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi,” alieleza Ikupa

Aidha, Mhe. Ikupa alitoa rai kwa Watu wenye Ulemavu kuwa wabunifu na kuweza kutambua fursa kutokana na mazingira waliyopo na kuzitumia kujiongezea kipato.

Hata hivyo, Naibu Waziri Ikupa alihimiza uboreshwaji wa miundombinu rafiki zitakazowesha kundi hilo, kuelimisha jamii juu ya haki za watu wenye ulemavu, uundwaji wa kamati za kuhudumia kundi hilo maalum na kuwapatia taarifa watu wenye ulemavu kuhusu fursa za mikopo zinazotolewa na halmashauri, ajira na upatikanaji wa dawa, mafuta ya wenye ualbino na vifaa saidizi. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi alimshukuru Mhe. Ikupa kwa kufanya ziara Wilayani humo, na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa kundi hilo maalum ikiwemo asilimia 2 ya mapato ya ndani ya halmashauri zinatengwa na kutoa mikopo kwa Vikundi vya Watu wenye Ulemavu, pia kuhakikisha kamati za Watu wenye Ulemavu zinaundwa katika kila Kijiji na kufanya kazi kulingana na miongozo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri, Ikupa alitembelea Kituo cha Utengamao kilichopo Mlali na Shule maalum Kongwa Kitengo cha Viziwi. Pia alitembelea Wilaya ya Mpwapwa, Shule ya msingi Chazungwa na Mpwapwa Sekondari ambazo zina wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (wa kwanza kutoka kulia) akizungumza kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu alipofanya ziara Wilaya ya Kongwa kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa.
Mwalimu wa Shule ya msingi Kongwa, Kitengo Maalum cha Viziwi, Bi. Anitha Massawe akiwafafanulia wanafunzi wenye uziwi kwa lugha ya alama maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea shule hiyo.
Daktari wa Mazoezi ya Viungo kutoka Kituo cha Utengamao Mlali, Dkt. Nshashuku Joseph akimwelezea Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa aina ya mazoezi wanayoyatoa kwa Watoto wenye ulemavu wa viungo. (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi.
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea Kituo cha Utengamano kilichopo Mlali, Wilaya ya Kongwa.

Uchaguzi Nigeria 2019: Upigaji kura umeahirishwa kwa wiki moja

$
0
0
Uchaguzi wa urais na ubunge nchini Nigeria umesukumwa mbele kwa wiki moja.

Tume huru ya kitaifa ya uchaguzi (INEC) ilitangaza hatua hiyo saa tano tu kabla ya wapiga kura kuelekea katika vituo vya upigaji kura hii leo Jumamosi.

"haiwezekani kuendelea na zoezi la uchaguzi kama ilivyopangwa," mwenyekiti wa tume hiyo Mahmood Yakubu amesema, akitaja hitilafu za kimipango.

Amesema uamuzi huo mgumu umehitajika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa huru na haki.Uchaguzi wa urais na ubunge umepangiwa sasa kufanyika Jumamosi ijayo Februari 23.

Uchaguzi wa Ugavana, wawakilishi wa majimbo na mabaraza ya manispaa yamepangiwa kufanyika Jumamosi Machi 9.Uamuzi huo umetolewa baada ya mkutano wa dharura katika makao makuu ya tume hiyo ya uchaguzi katika mji mkuu Abuja.

Ni kwanini Uchaguzi umeahirishwa?

Bwana Yakubu amesema uamuzi huo umechukuliwa baada ya 'ukaguzi wa makini' wa 'mpango wa namna uchaguzi utakavyofanyika', akiongeza kwamba kuna 'jitihada kubwa za kuhakikisha kuna uchaguzi wa huru, haki na wa kuaminika'.

Amesema ni muhimu kuchelewesha uchaguzi huo kuipa tume nafasi ya kukabiliana namasuala muhimu na pia "kusalia na hadhi katika uchaguzi", lakini hakutoa ufafanuzi zaidi.


Je unalijua chimbuko la Boda Boda ?

$
0
0
Chimbuko ya bodaboda ni utashi wa wajasiriamali kuvuka mpaka wa Uganda kwenda Kenya, mwaka 1972 - muda mfupi baada ya Idi Amin kuipundua serikali ya Milton Obote katika 1971.

Uhaba wa vitu muhimu majumbani Uganda, uliwafanya wafanyabiashara kutaka usafiri bora wa kuvusha bidhaa kama sukari na chumvi, masafa ya kilomita moja hivi kutoka Kenya, eneo la Busia.

Kama biashara ndogo ya faida, bodaboda inavutia vizito na mabepari kwa mikopo;.Kwa wingi wake, inavutia wenye vyeo na vyama; kwa wepesi wake, inavutia wahalifu.

Kwa hesabu za mwaka 2013, Uganda ilitumia zaidi ya $30m kuagiza pikipiki, siku hizi zinaundiwa nchini.

Huku 70% ya Waganda wakitegemea uchukuzi wa umma, teknolojia ya kurahisha usafiri ikizidi kusasishwa, mustakabali wa bodaboda ni mzuri, licha changamoto za utovu wa sheria barabarani, ajali, na uhalifu.

Tangu bodaboda izinduliwe, kama mfumo wa uchukuzi miaka 47 iliopita, sasa ni ya pili kwa ajira, baada ya kilimo.

Kama kiserema katika kilimo, mwanzo duni wa bodaboda, ulikuwa Baskeli.

Neno Boda Boda limetoka wapi?
Asili ya neno bodaboda, mwasisi wa mfumo huo, Pascali Bwire, anasema, ilikuwa utashi wa wafanyabiashara kuvuka kienyeji masafa ya maili moja, kati ya mpaka wa Uganda na Kenya kwa baskeli, kubeba bidhaa kama sukari, chumvi, unga na sabuni mwaka 1972.

Biashara 'nzuri' wakati huo.

Leo bodaboda ime-sasishwa, toka kengele na magurudmu mawili ya spoki, hadi Pikipiki; na si mpakani tu.Imesambaa mijini na vijijini Uganda. Inakisiwa nusu milioni ziko ndani na kuizunguka Kampala peke yake.

ENDELEA BBC Swahili.

SHUGHULI ZA KIBINADAMU ZINAVYOTISHIA UWEPO WA BWAWA LA MINDU MOROGORO

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii

MJI kasoro bahari!Hivyo ndivyo utasikia baadhi ya wenyeweji wa Mkoa wa Morogoro wakiamua kuuzungumzia mkoa wao ambao umejaaliwa kuwa na kila kitu lakini ukakosa bahari.

Hata hivyo wenyeji hao wanajivunia kuwa na bwawa la maji la Mindu.Ni bwawa marufu sana, ni bwawa ambalo limekuwa na historia ya aina yake na hasa kwa wananchi wanaozunguka bwawa hilo.Ni jambo la kawaida hata kwa wasafiri wanaokuwa kwenye vyombo vya usafiri wakifika katika Bwawa la Mindu kulinyooshea kidole.Utasikia "Umelionaa bwawa la Mindu?Ndio lileeee..."

Uwepo wa bwawa hilo umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa Manispaa ya Morogoro pamoja na maeneo mengine.Hata hivyo kuna baadhi ya watu hadi leo hii wanaamini bwawa hilo ni la asili kwa maana ya kwamba limekuwepo enzi na enzi.Waamini ni bwawa ambalo hakuna aliyelipeleka zaidi ya Muumba wa mbingu na ardhi.

Ukweli uko hivi pamoja na umaarufu wa bwawa hilo wa muda mrefu pamoja na ukubwa wake wote, ifahamike tu Bwawa hilo la Mindu ambalo katika Manispaa hiyo limechimbwa kuanzia mwaka 1984 hadi 1985 kwa ajili maji katika mji huo kutokana na ukame wa maji katika eneo hilo.

Historia inaeleza kuwa kutokana na ukame uliokuwa katika maeneo hayo ilionekana iko haja ya kuchimbwa bwawa la maji ambalo litakuwa chanzo cha upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kibinadamu.

Hata hivyo kabla ya kuchimbwa kwa bwawa hilo mwaka 1974 ilitungwa sheria ya Usimamizi wa Maji pamoja na mabwawa ili kuweza kusimamia katika sheria.Kutokana na sheria hiyo mwaka 1979 wananchi waliokuwa wakiendesha shughuli za kibidamu katika eneo la Mindu waliwahamisha wananchi kwa ajili ya upishaji Bwawa la Mindu na kuwalipa fidia ili shughuli za kibidamu zisiweze kuingiliana na kusitokee uchafuzi wa maji na udhibiti wa mazingira.

Tangu kuchimbwa kwa bwawa hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikiendelea za kuhakikisha shughuli za kibadamu haziathiri bwawa hilo. Hata hivyo kuongeza kwa idadi ya watu kwenye eneo hilo nako kumefanya baadhi ya watu kutamani kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa bwawa hilo.Uzuri ni kwamba wanaosimamia bwawa hilo wako makini na hivyo muda wote wamekuwa wakifuatilia kwa karibu na lengo ni kuona bwawa hilo linabaki kuwa salama kwa maslahi ya wananchi walio wengi.

Hivi karibuni, mawaziri nane wa Serikali ya Awamu ya Tano wakiongozwa na Mwenyekiti wao William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi walifanya ziara ya kutembelea bwawa la Mindu na kujionea hali halisi ya bwawa hilo ilivyo kwa sasa.

Akizungumza mbele ya mawaziri hao pamoja na maofisa wengine wa ngazi mbalimbali serikalini akiwa eneo la Bwawa la Mindu Ofisa wa Maji wa Bonde la Wami/ Ruvu Mhandisi Simon Ngonyani amesema Bonde la Wami/Ruvu ndio wasimamizi wa vyanzo vya maji kwa kulinda vizazi vya sasa vijavyo hivyo lazima vilindwe kwa gharama yeyote.

Hakusita kueleza kuwa uwepo wa wananchi katika bwawa la Mindu kunahatarisha uwepo wa bwawa hilo ambalo kina chake kimeshapungua na sababu kubwa inatokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea kufanyika.Wananchi wa maeneo hayo wengi wameshindwa kuwa sehemu ya walinzi wa bwawa hilo na baala yake wamekuwa wakiliharibu kwa kufanya shughuli ambazo kimsingi hazikupaswa kufanywa ndani ya eneo hilo la bwawa.

Mhandisi Ngonyani anasema kwa mujibu wa sheria, wananchi wanatakiwa kuwa umbali wa mita 500 kutoka usawa wa bwawa. Aidha amesema katika Bwawa la Mindu kuna watu walifikia hatua kuendesha shughuli za uvuvi na kufanya wananchi hao kuwa na mlipuko wa magonjwa kikiwemo kipindupindu baada ya kuzuia shughuli hizo ugonjwa huo umepungua.

Anafafanua ukweli ni kwamba uwepo wa wananchi katika eneo hilo la bwawa ni hatari kubwa kwani kutokana na mabadiliko ya tabianchi linaweza kupasuka ambapo janga lake litakuwa kubwa kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro na Taifa kwa ujumla.

Mhandisi Ngonyani anasema katika nchi nyingi zenye mabwawa kama hayo wananchi ambao wanaishi karibu nayo wamepata madhara makubwa , hivyo ni vema hatua mbalimbali zikachukuliwa kwa lengo la kuchukua tahadhari ikiwa ni sehemu ya kulinda wananchi.

"Hatuna sababu kuwaacha wananchi wetu katika bwawa la Mindu ni hatari kuwepo kwao,sio kufumbia macho na sheria ipo na fidia walishalipwa kilichofanyika kwa watu waliolipwa waliamua kuwauzia wengine ambapo hawawezi kulipwa fidia,"anasema Mhandisi Ngonyani.

Hata hivyo anasema mbali ya usimamizi wa sheria, anaeleza wazi uwepo wa shughuli za kibidamu ikiwemo kilimo kumeongeza gharama kwa Mamlaka ya Safi na Majitaka Morogoro (Muruwasa) kwa ajili ya kuyatibu maji kwa mahitaji ya asilimia 80 kwa Manispaa Morogoro.

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo za kisekta na sheria, Rais Dk.John Pombe Magufuli aliunda jopo la mawaziri kwa lengo la kufuatilia changamoto za wananchi ikiwemo kwa waliopo Bwawa la Mindu kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Jopo la Mawaziri hao, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Mamlaka ya Mkoa yahakikishe inasitisha ujenzi wa makazi katika maeneo ya bwawa la Mindu pamoja kuandika barua kwa waziri mwenye dhamana ya maji ili kutoa kibali cha utekelezaji wa sheria kwa wananchi hao.

Pia Lukuvi amesema utekelezaji wa sheria ya kuwaondoa wananchi isitishwe mpaka Waziri atoe kibali.Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Steven Kebwe amesema wananchi wanatengeneza utaratibu wa kutafuta maeneo ya kuwahamishia katika mpango wa upimaji wa viwanja 3000 na kununua kwa fedha ndogo wananchi kuingia au kufanya shughuli yeyote katika chanzo cha maji.

Jopo la Mawaziri hao watapita katika maeneo yenye changamoto katika Mikoa Morogoro, Mbeya, Kigoma, Mara, Geita pamoja na Mwanza na kuja na suluhisho bora ya wananchi katika kuondoa migogoro.Mawaziri hao katika Wizara Ofisi ya Rais-Tamisemi, Kilimo, Ulinzi na Jeshi kujenga Taifa, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano - Mazingira,Maliasili na Utalii,Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Ma kazi,Maji pamoja na Mifugo na Uvuvi.

SERIKALI YA UINGEREZA YATOA MABILIONI YA FEDHA KUSAIDIA JAMII KUPITIA ASASI ZA KIRAIA, YAJIZATITI KUPAMBANA NA RUSHWA

$
0
0
* Yahimiza uwazi na uwajibikaji kwa taasisi hizo, Serikali yahaidi ushirikiano

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
SERIKALI imehaidi kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Serikali ya Uingereza pamoja na asasi za kiraia katika kuhakikisha masuala ya uwazi na uwajibikaji yanaimarika zaidi huku mapambano dhidi ya rushwa yakikomeshwa nchini na hiyo ni baada ya serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la maendeleo la kimataifa (The Development for International Development -DFID) kuzindua rasmi mpango mkakati wa miaka 5 wa Uwajibikaji Tanzania ambao umelenga kuzisaidia asasi za kiraia katika kuhamasisha wananchi kushiriki katika masuala ya maendeleo nchini, shughuli iliyofanyika leo katika makazi ya balozi wa Uingereza nchini jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi huo Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa azaki katika kujenga jamii mpya licha ya kuwa na changamoto mbalimbali hasa ya baadhi ya maeneo kutofikiwa na huduma zao.

Ameeleza kuwa azaki zitakazopata fungu hilo watumie kwa malengo yaliyopangwa na hiyo ni kwa kuzingatia uwazi na kuwajibika na asasi ambazo hazitafuata matakwa ya sheria zitachukuliwa hatua kali ikiwemo kuzifuta kabisa.

Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi ya DFIF nchini Beth Arthy amesema kuwa urafiki baina ya Tanzania na Uingereza umekuwa wa muda mrefu na hiyo inaenda sambamba na kushirikiana katika masuala ya kimaendeleo na mpango huu umelenga kugusa mapambano dhidi ya rushwa, Mabadiliko ya tabia ya nchi, usawa wa kijinsia na ujumuishwaji wa wananchi katika maamuzi ya kimaendeleo na utagharimu takribani shilingi Bilioni 126.

Amesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi kwa ukaribu zaidi na serikali, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) pamoja na asasi mbalimbali ambazo zote kwa pamoja zililenga kushirikisha jamii katika shughuli za kimaendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Ernest Sungura amesema kuwa miradi hiyo ya uwajibikaji inaleta uwazi na uwajibikaji na kupambana na vitendo vya rushwa kama Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Joseph Magufuli inavyotekeleza hayo.

Ameeleza kuwa kupitia vyombo vya habari vya Uhuru vipindi mbalimbali vya uwajibikaji na kupinga rushwa vitaendelea kurushwa na kuchapishwa ili kuzidi kuelimisha Umma zaidi.

Awamu ya kwanza ya mpango huu ulianza rasmi mwaka 2009 hadi 2015 na katika awamu hiyo takribani wananchi milioni 7.5 walifikiwa moja kwa moja na wananchi milioni 22.5 wakifikiwa kwa namna nyingine tofauti.

Na takribani ya jumla ya shilingi Bilioni 392 zilitolewa na kutumika katika ufanyaji maboresho katika kuongeza bajeti ya huduma za kijamii, kuongeza kasi ua ulipaji kodi kwa Serikali, ufuatiliaji, utekelezaji wa Sheria, ugawaji wa ardhi, kupunguza vikwazo masokoni na kuboresha vipato vya Wakulima.

Katika warsha hiyo taasisi mbalimbali za kiraia zilishiriki zikiwemo taasisi ya Wajibu na Haki Elimu.

Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga akizungumza kwenye warsha ya uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka 5 wa uwajibikaji nchini uliolenga kuwahusisha wananchi kushiriki shuguli za kimaendeleo kupitia asasi za kiraia nchini.
Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Uhuru Media Ernest Sungura (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa jamii forum Maxence Melo (kushoto) na Mkurugenzi wa taasisi ya TWAWEZA Aidan Yakuze mara baada ya warsha hiyo leo jijini Dar es salaam.
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga(kulia) akikagua mabanda mbalimbali ya taasisi hizo, pamoja na kupata maelezo ya namna zinazofanya kazi na katika warsha hiyo amewahimiza kufanya kazi kwa kufuata matakwa ya kisheria hasa uwazi na uwajibikaji, katikati ni Mkuu wa Ofisi ha DFIF nchini Berth Arthy.
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga(katikati) akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Uhuru Media Ernest Sungura mara baada ya Warsha hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa ofisi ya DFIF nchini Beth Arthy (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Uhuru Media, Ernest Sungura (kulia) mara baada ya warsha hiyo, ambapo Sungura amesema kuwa vipindi vya kupiga vita rushwa vitarushwa na kuchapishwa kupitia vyombo vya habari vya uhuru.
Mkuu wa ofisi ya DFIF nchini Berth Arthy (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja naMsajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga(wa pili kulia) na Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa Uhuru Media Ernest Sungura(kulia) mara baada ya kuzindua rasmi mpango mkakati huo.

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI ATEMBELEA MRADI WA VISIMA, AITAKA DAWASA KUVIKAMILISHA KWA WAKATI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa sita toka kushoto) na viongozi wengine alioambatana nao akimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni atembelea mradi wa visima unaotekelezwa unaotekelezwa na Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) katika Wilaya yake huku akiitaka mamlaka hiyo kumaliza miradi hiyo kwa wakati. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza ziara yake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amesema ipo haja ya kumaliza miradi kwa wakati ili kuweza kuwapa wananchi huduma stahiki.

 "Niwashuruku DAWASA kwa kutenga baadhi ya miradi na kuisimamia mpaka ikamilike kwa asilimia 100, ili sasa tunavyotatua changamoto za wananchi tujue kwamba Kimbiji, Gezaulole na Vijibweni hakuna tatizo la maji ili tuendelee na miradi mingine kuliko kuwa na miradi mingi alafu rasilimali ni chache alafu tunaendelea kuibua miradi mingine tunakuwa na viporo ambavyo havijakamilika", Amesema Msafiri Amesema Kigamboni kuna changamnoto kubwa ya miradi ya maji na umeme, kukamilika kwa wakati jambo ambalo linaweza kukwamisha ujenzi wa viwanda kwani kwa sehemu kubwa viwnada vinategemea maji na umeme wa uhakika. 

 "Leo tumeanza kutembelea miradi ya maji, hasa miradi inayotekelezwa kwenye ngazi ya Taasisi ambazo hazipo chini ya Manispaa ya Kigamboni na tumetembelea miradi mbalimbali na miradi mingi ni ya muda mrefu kwa mfano mradi wa Kimbiji wenye visima 12, kwa sasa DAWASA wameona wajielekeze kwenye baadhi ya visima, wamechukua visima viwili wamalize kabisa waendelee na usambazaji wa maji kwa wananchi watu waendelee kupata maji", Amesema Msafiri. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri, akiwa ofisini kwake pamoja na maafisa wa DAWASA kabla ya kuanza ziara. Ameongeza kuwa "Lakini tuna mradi mwengine kama ule wa Geza Ulole, Maradi ule ni wa muda mrefu sana, Tafrisi yake ni nini kama taasisi, kumbe wanaweza kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya mipya yenye changamoto ya kibajeti lakini tungetumia fedha hizo kufanya marekebisho", 

 Naye Mratibu wa Miradi kutoka DAWASA, Charles Makoye, amesema Mradi wa Gezaulole ulijengwa zamani na ndio kilikuwa chanzo kikuu cha maji kwa eneo la Gezaulole, Kibungomo na Mjimwema. "Chanzo kikuu cha mradi huu ambao umejengwa mwaka 1970 ni kisima kilichopo eneo la Gezaulole chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita 28, 000 elfu klwa saa na kilikuwa kikitumia pampu ya dizeli" Amesema Makoye. 

 meongeza kuwa Mradi huo ulikarabatiwa na DAWASA baada ya kuacha kufanya kazi kwa zaidi ya 18. Amesema ukarabati wa mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la maji kwa maeneo ya Gezaulole, Mbwa Maji na Kibungumo maeneo ambayo hayana mfumo rasmi wa maji pia Dawasa inatekeleza mradi wa maji wa Vijibweni unaoendela kujengwa ambapo Gharama kuuz a ukarabati wa mradi huo ni Tsh. 683,173,200.00.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwaa na viongozi wengine alioambatana nao wakimuangalia Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi akionja maji yaliyo matika moja ya kisima wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwa na viongozi wengine alioambatana nao wakimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kulia) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akipata maelezo toka kwa  Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye (wa kwanza kushoto) juu ya mradi wa maji Gezaulole ambao ulijengwa toka mwaka 1970 na sasa DAWASA wameamua kuukarabati ili kutoa huduma ya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa DAWASA Ole juu ya mradi wa maji utakaovuka bahari kwa upande wa Kigamboni kwenda Kijichi na kuwapatia wakazi wa Kigamboni Majisafi na Salama.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiongea na wanahabari kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali ya maendeleo, changamoto zinazoikabiri wilaya hiyo mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbali mbali.

KUMBILAMOTO AKUTANA NA WAJANE NA WALEMAVU ZAIDI YA 200 NA KUGAWA MIKATE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wajane zaidi ya  200 na Makundi ya watu wenye ulemavu kutoka kata ya Vingunguti wamekutana katika ukumbi wa Mashujaa Vingunguti jijini Dar es Salaam Kujadili Changamoto zao zinazo wakabili na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali.

Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,ambae ndio chachu ya mkutano huo na mwanzilishi wa makundi hayo amewataka wakazi hao ambao wako katika kundi maalum kudumisha upendo na mshikamano katika Vikundi walivyoanzisha ili waweze kukopesheka.

Kumbilamoto amesema kumekuwa na ufinyu wa taarifa za fursa za watu wenye makundi maaalum kutokana na wao kujitenga na jamii inayowazunguka na kujiona wanyonge ,hivyo kupitia vikundi hivyo walivyounda wataweza kukaa pamoja na kupokea taarifa mbalimbali na fursa zinazopatikana kutoka katika taasisi za ndani na nje ya nchi.

"Iwe rahisi mtu kukufata nyumbani kwako kwa kuwa wewe mjane akakupa mkopo au fursa iliyopo mahali, lakini kupitia vikundi hivi mtaweza kukopesheka na Halmashauri yenu pamoja na mabenki kwa Halmashauri imetenga fungu maalum kwa ajili ya Vijana Walemavu na Wanawake ambalo mkopo wake auna riba hivyo ni vymea mkachangamkia fursa hii kwa kusajili vikundi vyenu na kukopa mapesa ya Rais Magufuli"alisema Kumbilamoto.

Aidha katika kusanyiko hilo kumbilamoto aliweza kugawa mikate miwili miwili kwa kila mjane na mlemavu waliofika katika mkutano huo kama kifungua kinywa kwa siku ya kesho.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na kundi la Wajane na Walemavu wa kata ya Vingunguti
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Omary Kumbilamoto akigawa Mikate kwa Wanawake wajane na watu wenye ulemavu.
Sehemu ya Wanawake Wajane na Watu Wenye ulemavu waishio Vingunguti wakisubiri neno kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto.

WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.

$
0
0
Na  Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Kassim Majaliwa amewasili leo Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Lengo la ziara yake imeelezwa kuwa ni kuweka msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na kukagua vitalu vya mashamba ili kuliboresha zaidi zao hilo.

Aidha katiaka ziara yake,Waziri Mkuu atatembelea katika Wilaya ya Kigoma Uvinza,Kibondo na Kakonko,sambamba na kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani kibondo na kuzungumza nao.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege kigoma
 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma
 Waziri mkuu akifurahi pamoja na kikundi cha ngoma cha akina mama
 Waziri mkuu Kassimu Majaliwa akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa kigoma, baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya kikazi.

Taasisi ya MISA Tanzania yawapiga msasa wanahabari Kanda ya Ziwa

$
0
0
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Internews imeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu sheria mpya za vyombo vya habari na haki ya upatikanaji taarifa. 

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia leo Februa 16, 2019 yanafanyika Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini Tanzania ambayo yamekuwa yakitolewa na MISA Tanzania.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika utetezi wa haki za binadamu.
Mafunzo hayo yanagusia sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016, Sheria ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Mitandao ya Kijamii ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Clonel Mwegendao (kulia) kutoka SACHITA FM iliyopo Tarime mkoani Mara akieleza matarajio yake ambapo amesema anatarajia kutambua sheria mpya za habari, changamoto zake na namna ya kukabiliana nazo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Edna Elisha (kulia) kutoka Jembe FM ya Jijini Mwanza amesema mafunzo hayo yatamjengea uelewa mpana kuhusu sheria ya huduma za habari na hivyo kutimiza vyema majukumu yake.
Mshiriki wa mafunzo, Hellen Mteremko kutoka City FM Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki Raphael Okelo wa Gazeti Majira kutoka Bunda mkoani Mara akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Dinna Maningo akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Derick Milton wa Gazeti Mtanzania mkoani Simiyu akieleza matarajio yake baada ya mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Machunda Nicholaus wa Sibuka FM mkoani Simiyu akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Hassan Ramadhan wa Star TV Jijini Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Neema Evance wa Azam TV mkoani Simiyu amesema sheria yoyote mpya inakuja na changamoto zake hivyo mafunzo hayo yatamjengea uwezo kutambua sheria mbalimbali za vyombo vya habari na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Afisa Utawala na Fedha kutoka taasisi ya MISA Tanzania, Andrew Marawiti (kushoto) akiteta jambo na Afisa Habari na Utafiti wa taasisi hiyo, Neema Kasabuliro (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini

LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Arumeru 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku na kutoa onyo kali kwa magari ya polisi nchini kutumika kubeba au kusindikiza dawa za kulenya. 

Lugola amesema wapo baadhi ya polisi wanatuhumiwa kufanya matukio ya kubeba bangi, mirungi pamoja na dawa aina mbalimbali za kulenya hapa nchini wakitumia magari ya Jeshi la Polisi ambapo ni kinyume cha sheria. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Mkoani Arusha, jana, mara baada ya kukabidhiwa gari la polisi lililokarabitiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (CFC) ya hapa nchini kwa gharama ya shilingi milioni 15, amesema kitendo hicho kinalifedhehesha Jeshi la Polisi ambalo linatakiwa kuwa mfano wa kukabiliana na uhalifu. 

Kutokana na tabia mbaya hiyo walionayo baadhi ya polisi nchini wasiokua waadilifu, Waziri Lugola amesema polisi yeyote akikamatwa kushiriki kufanya tukio hilo hata muonea huruma kamwe, ataondolewa katika nafasi hiyo na kushtakiwa. 

“Polisi wakikamatwa wanasindikiza au kubeba dawa za kulevya, polisi hao tutawafukuza kazi pamoja na kuwashtaki, gari hili la polisi ambalo limekarabatiwa na Taasisi hii, litumike vizuri kwa kupambana na wahalifu na siyo vinginevyo,” alisema Lugola. 

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum wa CCM Wilayani humo, Amina Mollel alimlalamikia Waziri Lugola akisema ndani ya Wilaya hiyo kuna kesi ambazo zinachukua mda mrefu katika vituo vya polisi kwa kisingizio cha upelelezi kuwa haujakamilika hasa kesi za ubakaji ambapo alitoa namba ya faili mkutanoni hapo. 

“Mheshimiwa Waziri, licha ya kuwa Polisi wanafanya kazi vizuri wilayani hapa Arumeru lakini kuna tatizo la kesi mbalimbali zinachukua muda mrefu katika vituo vya polisi hasa kesi za kubaka, na kuwafanya wananchi kuchelewa kupata haki zao, kesi inachukua miezi sita bado ipo katika upepelezi, huo muda ni mrefu sana” alisema Amina. 

Hata hivyo, Waziri Lugola kutokana na tuhuma hiyo, alimuagiza Mkuu wa Polisi wilayani humo (OCD) kutafuta faili la kesi zilizotajwa na Mbunge huyo ili aweze kumletea katika mkutano huo kabla ya kumaliza mkutano huo. 

Baada ya kutoa agizo hilo, OCD alileta faili hilo katika mkutano huo, na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo, ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Jerry Murro, ili aweze kumkabidhi Waziri Lugola na aweze kutoa maelekezo zaidi. 

Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake ambazo zipo ndani ya Wizara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni, Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, leo, akitoa onyo kwa baadhi ya Polisi nchini wenye tabia ya kubeba, kusindikiza dawa za kulevya kwa kutumia magari ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Arusha, Amina Mollel. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akipokea ufunguo wa gari la Polisi namba PT 0747, kutoka kwa Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (FCF), Mratibu wa Shughuli za Kudhibiti Ujangili, William Mallya (kulia) ambayo ilikarabati gari hilo la Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola mara baada ya kulikabidhi gari hilo kwa Jeshi la Polisi wilayani humo, alitaka gari hilo litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akilikagua gari la Polisi namba PT 0747 ambalo limekarabatiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund kwa ajili ya Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola alikabidhiwa gari hilo na pia naye akalikabidhi kwa Jeshi la Polisi Wilaya hiyo na kuagiza litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kusindikiza dawa za kulevya. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto, akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro (katikati), wakati Waziri huyo alipokuwa anaelekea kupokea madarasa yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule ya Msingi Usa-River, Wilayani humo, Mkoa wa Arusha. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, James Mchembe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NUKUU ZA NDG POLEPOLE KWENYE KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYA YA LONGIDO

$
0
0

16 Februari 2019

1. "Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imefanikisha ujenzi wa kiwanda cha nyama hapa kinachoendelea kujengwa kitakuwa kinapokea Ng’ombe 50 na Mbuzi 2000 kwa siku bidhaa zote za mifugo zitatengenezwa hapa na wanufaika wa msingi ni wananchi wote, huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM” Ndg. Polepole

2. "Tunataka Serikali yetu ipate mapato kutokana na biashara ya mifugo na mapato hayo yawe ya haki, mapato yasiwe yana mgandamiza mfanyabishara na yatakayo kuwa rafiki kwa wafanyabishara” Ndg. Polepole

3. "Nasi kama Chama tunasema kulipa kodi hakuna mjadala lakini lazima kodi hiyo iwe inayozingatia haki” Ndg. Polepole

4. "Hapa kuna wafanyabishara wanapitisha mifugo kwenye njia za magendo na sababu  mmesema ni kodi kubwa ila wengine ni kwa sababu ya ukorofi wao tu wakuto tii sheria” Ndg. Polepole

5. "Tumezungumza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Naibu Waziri wake na Katibu Mkuu wa Wizara  Chama kimeelekeza waje hapa Longido wazifanyie kazi changamoto zenu na ndani ya siku mbili kutoka leo Naibu Waziri atakuwa hapa” Ndg. Polepole

6. "Naye Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi atafika hapa kesho kuwasikiliza tunataka suala la usumbufu barabarani kwa wafanyabiashara wa mifugo nalo liishe, Serikali yetu ni sikivu tunaamini litakwisha” Ndg. Polepole

7. "Msimamo wetu kama Chama tozo hizi kwa wafanyabiashara wa mifugo zipungue ziwe rafiki kwa wafanyabiashara, wao wapate faida na Serikali ipate faida, wao wawe matajiri na Serikali iwe vizuri kimapato ilete maendeleo makubwa kwa wananchi” Ndg. Polepole

8. "Lengo letu kama Chama tunataka kila changamoto iliyokatika uwezo wa binaadam kutatuliwa tuitatue” Ndg. Polepole

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

 

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKOANI SINGIDA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni na kupokea taarifa ya mkoa katika ukumbi wa Halmashauri Manyoni ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo mkoani humo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Daniel Mtuka mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni tayari kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Singida

VIONGOZI WA CCM KAGUENI MIRADI-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya  ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma kuzungumza na  viongozi wa CCM, serikali na wabunge, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM, Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM, Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa CCM,Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Mkoa na Wilaya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanakagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao na wajiridhishe kama inalingana na thamani halisi ya kiasi cha fedha kilichotumika.

Amesema iwapo viongozi hao hawataridhishwa na utekelezwaji wa mradi husika wasisite kuchukua hatua kwa kutoa taarifa katika ngazi huzika, lengo ni kuhakikisha miradi yote inakuwa na ubora na inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 16, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kigoma kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM mkoa wa Kigoma amesema ni muhimu kwa viongozi hao kujiridhisha na muenendo wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yao zikiwemo za afya, maji, elimu na kilimo.

Amesema CCM itaendelea kuimarisha misingi ya utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi, hivyo amewataka viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Serikali washikamane ili malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo yatimie.

“CCM ni chama imara chenye mipango inayotekelezeka na kilicholenga kuwaletea wananchi maendeleo na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili na ndicho chama pekee chenye kuleta matumaini kwa Watanzania wote.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya CCM kwa viongozi hao.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga alisoma taarifa ya mkoa huo, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linaloendelea kwenye mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2018 jumla ya wahamiaji haramu zaidi ya 4,135 walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

DKT. MPANGO ATETA NA WAFANYAKAZI NA KUHIMIZA MAADIDLI NA UWAJIBIKAJI KAZINI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo na kuzungumza nao namna bora ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema Wizara ya Fedha na Mipango ni kitovu cha Serikali hivyo Watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija.

Amesema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa weledi, bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha utendaji kazi na kukuza uhusiano mahala pa kazi.

Aidha Waziri Mpango aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, Uchambuzi wa Sera za Taifa na uanzishwaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki-GePG.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu amemhakikishia Waziri Mpango kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa ukamilifu ili kuboresha utendaji kazi wa Wizara hiyo.




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), katika kikao na Watumishi hao Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akifafanua jambo wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), Jijini Dodoma.

Mjumbe wa TUGHE Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mariam Kihange, akichangia mada wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Gisela Mugumira akifafanua jambo wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Alfred Dede.

Mwakilishi wa Kamishna wa Bajeti Bw. Sigsbert Kavishe akichangia hoja katika wa kikao na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu, kulia ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Victus Tesha Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM

Waziri wa Nishati, azindua Bodi mpya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoa maelekezo

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, leo amezindua Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kutoa maelekezo mbalimbali kwa Bodi hiyo yatakayopelekea kazi ya usambazaji umeme vijijini kufanyika kwa kasi na ufanisi.

Kikao cha Waziri na Bodi hiyo kimefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga na watendaji wengine kutoka Wizara na REA.

Akizungumza na Bodi hiyo, Dkt Kalemani alieleza sababu mbalimbali za kuvunjwa kwa Bodi iliyopita tarehe 12 Novemba, 2018 kuwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kushindwa kusimamia vizuri Wakala wa Nishati Vijijini.

“ Leo tunawakabidhi majukumu yenu lakini suala la msingi ni kuwatumikia wananchi kwani tunawajibika kwao hivyo yaliyotokea kwenye Bodi iliyopita, yasitokee kwenye Bodi yenu”. Alisema Dkt Kalemani

Alitaja majukumu ya Bodi hiyo kuwa ni kusimamia Wakala wa Nishati Vijijini ili utekeleze majukumu yake kwa ufanisi na weledi na kusimamia shughuli za Wakala ili zifanyike kwa malengo na Dira ya Serikali ya kusambaza umeme katika Vijiji vyote nchini.

Aliongeza kuwa, majukumu mengine ya Bodi hiyo ni kusimamia Fedha za Mfuko wa Nishati Vijijini ili tija yake ionekane na kuitaka Bodi hiyo kutokuwa chanzo cha migogoro inayoweza kuchelewesha au kukwamisha kazi za Wakala.

Aidha, ameiagiza Bodi hiyo kuharakisha utekelezaji wa kusambaza umeme katika Vijiji, vitongoji na miradi mbalimbali ya kijamii na kuwasimamia ipasavyo wakandarasi wa umeme vijijini ili kazi zao ziende kwa haraka kwani wengi wao hawafanyi kazi zao inavyotakiwa.

Dkt. Kalemani amezindua Bodi hiyo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kumteua Bw. Michael Nyagoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo tarehe 14 Februari 2019.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni Oswald Urassa, Mhandisi Styden Rwebangila, Francis Songela, Louis Accaro, Dailin Leonard, Henry Mwimbe na Dkt. Andrew Komba.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika kikao hicho pia walihudhuria Watendaji wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza na Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo imezinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo imezinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika kikao hicho pia walihudhuria Watendaji wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Michael Nyagoga kitabu cha Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005 ikiwa ni muongozo wa majukumu ya Bodi hiyo katika kusimamia Wakala huo.

CCM ZANZIBAR YATOA ZAWADI KWA WANAFUNZI 1,222.

$
0
0

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameeleza kwamba ustawi wa elimu nchini umetokana na matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12 mwaka 1964.

Hayo ameyasema katika hafla ya kuwapatia zawadi Wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2018 waliofaulu kiwango daraja la I,II kwa shule mbali mbali za Zanzibar, hafla iliyofanyika katika kiwanja cha Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja.

Dk.Mabodi amesema baada ya kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar serikali ya wakati huo ikatangaza kuwa suala la elimu ni bure sambamba na kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi.

Amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuenzi Tunu ya Mapinduzi kutokana na mambo mema yaliyotekelezwa kwa haraka mara baada ya kufanyika mapinduzi hayo na wananchi wakapata uhuru na kunufaika na fursa ya elimu iliyotolewa kwa ubaguzi kabla ya mapinduzi.

Ameeleza kuwa kwa sasa Zanzibar imekuwa ni kitovu cha wasomi na watu wenye taaluma mbali mbali ambao chanzo cha mafanikio hayo kimetokana na kukua kwa sekta ya elimu nchini.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi amewapongeza wanafunzi mbali mbali waliofaulu vizuri masomo yao ya kidatu cha nne pamoja na kuwasihi waliofeli kuwa wasikate tamaa bali wajiendeleze kupitia sekta ya mafunzo ya amali ili wawe na ujuzi.

Amesema katika kuunga mkono suala la elimu CCM imeandaa mpango maalum wa kuwasaidia vijana mbali mbali waliofeli masomo yao katika ngazi tofauti za kielimu ili nao wapate ujuzi wa kujiajiri wenyewe.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wafaulu vizuri kidato cha sita na kujiunga na vyuo vikuu.Amesema elimu ni jambo muhimu kwa maisha ya binadamu hivyo ni lazima wajitume katika safari yao ya kutafuta taaluma.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi.Angelina Adam Malembeka amewasisitiza wanafunzi hao kuwa bado wana safari ndefu ya kutafuta elimu hivyo waendelee kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao.

Jumla ya wanafunzi 1,222 waliofaulu mitihani ya kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili(I,II) wamepatiwa zawadi mbali mbali na Chama Cha Mapinduzi ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza na kuwahamasisha waendelee kusoma kwa bidii na kufaulu katika ngazi mbali mbali hadi Vyuo vikuu.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ akiwahutubia wanafunzi 1,222 waliofaulu kwa kiwango cha daraja la I,II katika mitihani ya Kitato cha Nne mwaka 2018.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’(kulia) akimkabidhi zawadi Mwanafunzi bora wa kiume Zanzibar ndugu Hassan Hamid Ussi aliyefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza katika masomo ya Sayansi katika mitihani ya kidato cha Nne mwaka 2018.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’(kulia) akimkabidhi zawadi Mwanafunzi bora wa kike Zanzibar ndugu Faiza Shamim Khamis aliyefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza katika masomo ya Sayansi katika mitihani ya kidato cha Nne mwaka 2018.
WANAFUNZI wa kidato cha Nne mwaka 2018 waliofaulu daraja la Kwanza na la Pili Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Zawadi na Chama Cha Mapinduzi Zanzibar(PICHA NA IS-HAKA OMAR).

SIMBA YAMALIZA MZIZI WA FITNA WA KARIAKOO DERBY

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mtanange wa Watani wa Jadi Yanga na Simba umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli 1-0. Mchezo huo ulipigwa leo katika Uwanja wa Taifa kwa kuwakutanisha watani hao wa jadi.

Mechi hiyo ilianza kwa kila upande kumshambulia mpinzani wake kwa zamu bila mafanikio yoyote.Yanga walishindwa kutumia nafasi walizozipata kwenye Kipindi cha kwanza sambamba na watani wao wa jadi.

Mpaka mpira unaenda mapumziko, timu hizo zilienda vyumbani wakitoshana nguvu jwa 0-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kulisakama lango la Yanga baada ya kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kiungo wa Kimataifa kutoka Zambia Clotous Chama na kumuingiza Hassan Dilunga.

Yanga nao walifanya mabadiliko kwa kumtoa mshambuliaji wa Kimataifa raia wa Burundu Amisi Tambwe na nafasi yake kuchukuliwa na Mrisho Ngasa ambapo mabadiliko hayo ya safu ya ushambuliaji wa Yanga ikasalia na Heritier Makambo.

Benchi la ufundi la Yanga likafanya mabadiliko ya kiufundi kwa kumtoa Nahodha Ibrahim Ajib na kumuingiza Mohamed Issa ‘Banka’.Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu ila safu za ulinzi zikiwa makini kila upande na katika Dakika ya 71, mshambuliaji wa Kamataifa wa Rwanda Meddie Kagere akaipatia timu yake goli la kuongoza akitumia madhaifu ya safu ya ulinzi ya Yanga baada ya kukosa maelewano.

Goli hilo liliwapa Simba motisha na kuanza kulisakama lango la Yanga na wapinzani wao Yanga wakijitahidi kutafuta goli la kusawazisha.Mpaka mwamuzi Hance Mabena anamaliza dakika 90 za mchezo huo timu ya Simba inaondoka na ushindi wa goli 1-0 na kujinyakulia alama tatu na kufikisha alama 39 akisalia nafasi ya Tatu ya Ligi.

Na baada ya matokeo hayo Yanga wanakuwa wamepoteza mchezo wa pili wa ligi lakini wakiendelea kusalia katika nafasi ya kwanza kwa alama 58 akifuatiwa na Azam wenye alama 45.

Timu hizo zitacheza mchezo mwingine wa Ligi ambapo Simba watasafiri kwenda Arusha kucheza na African Lyon Feb 19, na Yanga wakielekea Mbao Februari 20.


Kikosi cha Simba kilichoanza.Picha kwa hisani ya Francis Dande).
Kikosi cha Yanga kilichoanza. 
Moja ya hekaheka katika lango la Yanga.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA WELEDI WALIONAO KUIELIMISHA JAMII KUHUSU AFYA YA UZAZI NA NDOA ZA UTOTONI

$
0
0

Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Arusha wakifuatili kwa makini kongamano hilo lililowakutanisha kwa pamoja katika Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Arusha
Mafunzo yakiendele juu ya maswala ya Afya ya uzazi chini ya vijana wenye umri wa miaka 18,ndoa xa utotoni, na mimba za utotoni.



Na. Vero Ignatus Arusha

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kutumia ujuzi na weredi katika kuelimisha jamii juu ya elimu ya uzazi kwa vijana chini ya umri miaka kumi na nane pamoja na kupinga vita ndoa za utotoni hali ambayo inapelekea vijana wengi kuacha kuendelea na masomo yao.

Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha waandishi habari wa vyombo tofauti mkoani Arusha katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Arusha Muuguzi mkuu wa mkoa Bi Getrude Anderson amesema lengo la kongamano hilo ili kuwapa elimu wandishi wa habari juu ya maswala ya afya ya uzazi ili waweze kutumia elimu hiyo katika kuwahabarisha jamii athari za mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na elimu ya uzazi wa mpango.

Aidha Bi Getrude amesema kupitia kongamano hilo waandishi wanauwezo mkubwa wa kutumia weledi na ujuzi walionao katika kuihabarisha jamii habari za afya zenye uhakika kwani elimu huwafikia walengwaa kwa kutumia vyombo vya habari.

“Tumeamua kuandaa kongamano hili kwa kuwaaitisha waandishi habari ili kuwapa elimu waandi hawa wa vyombo mbali mbali juu ya maswala ya uzazi kwa vijana kwani waandishi hawa wakianda vipindi mbali mbali vya elimu ya uzazi vijana wataelewa mambo ya wahusuyo lakini sio hivyo tu hawawezi kuanda habari zenye weledi bila kupata ujuzi kutoka kwetu sisi wataalam wa afya,tumewataka pia waanandae makundi mbali mbali ya waandishi wa habari mbali n kuwahabarisha pia wawafuate hukuo huko vijana wawape elimu” Alisema

Alisema kupitia waandishi watapata mafanikio ya kuwafikia jamii na vijana kwani vijana wengi hufutilia sana mitandao ya kijamii ya kijamii,na hufuatilia habari hivyo wanamategemeo kupitia kongamano hilo lililofanyika italeta mafanikio mazuri sambamba kuwashauri vijana kutengeneza vikundi,na vipindi mbalimbali vya ili kufikisha elimu kwa walengwa

Alisema siku ya leo 17 februari 2019 wameaandaa tamasha ambalo litawakutanisha vijana mbali mbali mkoani arusha ambapo Tamasha hilo lita fanyika katika viwanja vya kumbu kumbu la azimio la Arusha katika mnara wa Mwenge ambapo kutakuwa nafursa za upimaji wa afya kama vile upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi,virusi vya ukimwi na magonjwa mengineyo.,

Nae Mratibu wa mradi wa tupange pamoja Bwana Waziri Njau amesema lengo la kuwakutanisha waandishi habari ni kwa ajili ya kumtanisha kijana kwa kuandaa klabu mbalimbali na wameamua kuandaa matamasha ya vijana kupitia wandi habari ili kuwapa habari zenye weledi

BIBI TITI MOHAMED: MWANAMAMA SHUPAVU NA MPIGANIA UHURU HODARI ALIYETINGISHA NA KUHESHIMIKA AFRIKA MASHARIKI NZIMA!!!

$
0
0

1. Usuli:

1.1 TITI Kuzaliwa:
TITI MOHAMED SALUM MANDWAGA alizaliwa mwezi Juni 1926 jijini Dsm.

1.2 Wazazi Wa TITI: Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji.

Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima.

2. Elimu:

2.1 Baba Agoma TITI Asisome:
Baba yake alikataa katukatu kwamba TITI asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri.

2.2 Mama Ampeleka TITI Shule:
Baba yake alifariki TITI akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka TITI Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4.

3. TITI Aolewa na MHENGA akiwa na miaka 14 tu:
TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu. 

4. TITI Ajifungua Mtoto wa Kike:
TITI alijifungua mtoto wa kike aitwae HALIambaye alikuja kuolewa na MZEE IDD HAMIS, Mshambuliaji hatari wa Cosmopolitans, klabu ya kwanza kutwaa ubingwa TZ ambapo walikuwa wakiishi mtaa wa Skukuu na Udowe na kubahatika kupata watoto 3 wa kiume.

4. TITI Aachana na mumewe:
TITI aliachana na mume huyo kijeba ambaye alikuwa ni baba wa HALIMA , mume ambaye hakuwa chaguo lake.

5. TITI Awa Maarufu kwa ngoma za Maulid:
TITI alianza kuwa maarufu angali mdogo alipokuwa kiongozi wa ngoma za maulid ambazo zilimjenga uwezo wa kujiamini na hivyo akawa maarufu sana.

6. TITI Aolewa na BOI SELEMAN:
TITI aliolewa na dreva wa teksi aitwae Boi Selemani, baada ya ndoa yake ya kwanza kusambaratika.

6. TITI Ajiunga na TANU:
TANU ilizaliwa tarehe 7.7.1954. Wanachama wa mwanzo kupata kadi za TANU walikuwa NYERERE(Kadi na.1), A. SYKES Na.2, A. SYSKES No.3 D. AZZIZ No.4, DENIS PHOMBEAH No.5, DOME OKOCH Na.6, J. RUPIA Na.7.

Bw. BOI, mme wa TITI, alikuwa ni rafiki wa Bw. SCHNEIDER PLANTAN aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAA. Siku moja, Bw. PLANTAN alienda nyumbani kwa BOI na kumweleza kuwa ametumwa kumweleza TITI ajiunge na TANU.

BOI alikubali na akajinunulia kadi na.15 ya TANU na pia akamnunulia TITI kadi na.16. Jumla alitoa TZS 12/= kwani kila kadi iliuzwa TZS 6/=.Ndivyo walivyojiunga TANU. BOI pia alichangia TSH 10/= kwa ajili ya nauli ya Mwalimu NYERERE kwenda UNO (TSH 5/= kila mmoja).

7. TITI Asomba wamama Lukuki Kujiunga TANU!!!

Tarehe 8.7.1955, TITI akiwa Mwenyekiti wa Tawi la Wanawake wa TANU, alifanya mkutano mkubwa na kuvuna wanachama 400 na ndani ya miezi 3 tu akawa amepata wanachama 5,000:
"Nilizungumza na mama Swalehe Kubunju, Kiongozi wa "Tongakusema" na akawaita wakinamama wote wa Tongakusema. Nikakutana nao Livingstone street alikokuwa akiishi mama Kubunju ambaye alihimiza: -"Ewe mwanamke, TITI anakuita, TITI yuko hapa". Hivyo wamama wakawa wanakuja kirahisi. Wakija nikawa nawaambia tunataka uhuru lakini hatuwezi kuupata kabla ya kujiunga TANU. Wanawake ndio nguvu ya dunia, hawa wanaume wote tumewazaa. Nilizunguka Tanganyika nzima. Safari ya kwanza mikoani tulienda Tanga tarehe 1.1.1956 mimi, Bwana mkubwa na RAJAB DIWANI na tukazunguka Tanga nzima kwa siku 21. Tuliporudi Kamati Kuu ikanipa ruhusa ya kusafiri peke yangu. Pia nilifanya safari nyingi na OSCAR KAMBONA. Tukiwa na KAMBONA tulikuwa tukipita nyumba hadi nyumba, usiku na mchana".

8. TITI Atia Fora Mikutano ya NYERERE:
TITI ndiye aliyekuwa akiimbisha na kuhutubia kwanza kabla ya NYERERE kupanda jukwaani "kushusha" nondo. Kwa hakika, TITI alikuwa akikonga nyoyo kwa kiswahili chake cha pwani na nyimbo zake:  (Hongera mwanangu eeh na mi nihongere eeh hongera X 2) na (Mama Usungu, Mama Usungu X 2).

9. KENYA Wamuomba TITI "Awapige Tafu" Kudai Uhuru"
Uwezo mkubwa wa kushawishi na kujiamini kulifanya jina la TITI livuke mipaka ya Tanganyika. Wapigania uhuru wa Kenya TOM MBOYA, JARAMOGI OGINGA ODINGA nk walipopata sifa za TITI walituma ujumbe kumuomba aende Kenya kusaidia kuishawishi serikali ya mkoloni kumwachia huru JOMO KENYATTA.

TITI alienda Kenya na alitia fora sana maeneo ya Nairobi, Machakos, Kisumu na Mombasa.

Miaka michache baada ya KENYATTA kuachiwa, mara moja alikuja TZ. KENYATTA alihutubia mkutano mkubwa Jangwani akiwa na suaruali ya kodrai ya udongo na koti kubwa la kijivu huku akipeperusha usinga mweusi alimshukuru sana TITI kwa jitihada zake mujarab alipokuwa nchini Kenya.

Ni katika mkutano huu ndipo Mwalimu NYERERE alisema yuko tayari kuona Tanganyika inachelewa kupata uhuru ili Kenya ipate uhuru wake na ziweze kuungana.

10. TITI Amsindikiza NYERERE Airport kwenda UNO:
Tarehe 17.2.1955, TITI alikuwa mmoja wa wanaTANU waliomsindikiza NYERERE Airport kwenda UNO kuwaeleza kuwa "Tanganyika lazma kieleweke".

11. TITI Akumbana na changamoto kedekede:
Katika harakati zake za kuwashawishi wanawake na wanaume kujiunga na TANU, TITI alikumbana na changamoto lukuki. Kwanza aliambiwa ni mwizi wa waume za watu na pia akaambiwa anatafuna michango ya TANU:
"Kulikuwa na changamoto nyingi sana. Siku moja nilienda nyumba moja kuarifu mkutano wa TANU. Nikakuta wanawake wamekusanyika na kudai eti nimeenda kuiba waume wa watu. Lakini mmoja wao akawaambia huyu mama ndiye anaetangaza chama cha NYERERE nilimuona pia nyumba ya mbele, hana lengo baya".

12. BOI Alalamika kwa PLANTAN  kuwa Amegeuka Housegirl:
Mmewe TITI, BOI alilalamika vikali kwa PLANTAN kuwa TITI hatulii nyumbani kutokana na harakati za TANU hadi yeye kugeuka yaya wa kujipikia na kujifulia nguo na hakuona tena faida ya ndoa. BOI akamshutumu PLANTAN kwa kumuingiza TITI kwenye chama cha TANU. 

BOI pia wivu ulikuwa umerindima kwenye "medula oblangata yake" hadi akabwabwaja'- "TITI ni mwanamke wa kiislam, kasoma madrasa, kapanda jukwaani bila baibui. Hii si sawa kabisa".

13. Ndoa ya TITI Yaparaganyika Sababu ya Harakati za Kudai Uhuru:
Kutokana na mishemishe na safari zisizoisha za TITI, ndoa ya TITI ikaparanganyika kama alivyoelezea mwenyewe:
"BOI mwenyewe ndie aliyeniruhusu kujiunga na TANU na tena ndiye aliyeninunulia kadi ya uanachama. TANU pia ilimwandikia barua anisaidue mambo ya TANU.Lakini mwisho hizi safari zilimshinda. Nilikuwa nakaa nje ya Dsm hata kwa miezi 3 na nikirudi sikai hata siku 10, nasafiri tena. BOI akaniambia anataka kuoa mke mwingine. Nikamwambia sawa, niache na kazi yangu kwani nimeizoea. Kwahiyo BOI akamuoa Bi. KHADIJA lakini wakashindwana wakaachana. Nilifunga mizigo yangu nikaondoka kwa BOI".

TITI akaja kuolewa tena.

14. NYERERE na TITI "Waangusha" rhumba "La kufa mtu" siku ya uhuru".

Tarehe 9.12.1961, ilikuwa siku ya kipekee kwa Mwalimu NYERERE na TITI ambao kwa miaka kadhaa hapo nyuma walizunguka kila kona ya Tanganyika kuhimiza wananchi kujiunga na TANU na kudai uhuru.

Siku hiyo, Mwalimu NYERERE na TITI walikaa "High Table" na usiku wakiwa nadhifu walifungua muziki wa kuukaribisha uhuru kwa kusakata rhumba kwa bashasha kubwa!.

15. TITI Ashinda Ubunge Rufiji:
TITI alishinda ubunge Rufiji na kuteuliwa kuwa Waziri mdogo wa wizara ya Utamaduni na Maendeleo. Pia alishika wadhifa wa Waziri mdogo wa Afya na pia Uwaziri mdogo wizara ya Maendeleo ya Jamii. Aidha, tarehe 2.11.1962, Rais NYERERE aliagiza vyama vyote vya wanawake vivunjwe na iundwe UWT na TITI akawa ndiye Mwenyekiti.

Mwaka 1965, TITI alishindwa ubunge huko Rufiji.

16. TITI Apelekea KISWAHILI Kutumika Bungeni:
TITI alikuwa ameishia darasa la 4 tu hivyo alikuwa hawezi "kutema yai" kwa ufasaha. Siku moja mwanzoni mwa 1960s akiwa bungeni akatoa hoja kwamba wananchi wa magomeni wanataka nao wawe na taa za barabarani ambapo alisema -: "We want fire in Magomeni.... We want fire in small bottles". 

Wabunge wengi walicheka pamoja na NYERERE akiwa PM ambapo aliamuru KISWAHILI kianze kutumika bungeni.

17. TITI Alitolea nje Azimio la Arusha:

Mwaka 1967, TITI, bila kupepesa macho wala kutikisa pua, akabwaga manyanga na kujiuzulu ujumbe wa Kamati Kuu ya TANU kwani alikuwa hakubaliani na Kipengele cha 5(a) cha Azimio la Arusha kuhusu maadili kwamba ni marufuku kiongozi wa serikali au TANU kuwa na nyumba ya kupangisha.

TITI alikuwa na nyumba 2 ambapo moja aliijenga kwa kuuza vito vyake vya dhahabu na nyingine ni ya mkopo. Nyumba moja ipo Upanga mkabala na Makao Makuu, JWTZ na nyingine ipo Temeke.

Uhusiano wa NYERERE na TITI ukawa umelegalega.

18. TITI Akamatwa na Kushtakiwa kwa Uhaini:
TITI alikamatwa mwezi Octoba 1969 na kudaiwa kuwa alikula njama pamoja na OSCAR KAMBONA, GREY MATTAKA, JOHN CHIPAKA, MICHAEL KAMALIZA, WILLIAM CHACHA na ALFRED MILLINGA, kuipindua serikali. TITI alikuwa ni mwanamke pekee katika kesi hiyo.Walidaiwa kupanga kutekeleza azma hiyo wakati Rais NYERERE atakapokuwa nje ya nchi. Kesi ilianza kurindima 6.6.1970 chini ya Jaji Mkuu, Georges, CJ na upande wa mashtaka ukiongozwa na MARK BOMANI.

Kesi ilinguruma kwa siku 127. TITI  ns wenzake kasoro Bw. MILLINGS walitiwa hatiani kutokana na ushahidi madhubuti na kupewa kifungo cha maisha. TITI akaenda kutumikia kifungo gereza la Isanga, Dodoma.

19. Mume wa TITI Amwacha solemba!
Baada ya TITI kukumbwa na dhahama ya kesi ya uhaini, mmewe akaamua kumuacha kwani aliona hiyo ni fedheha kubwa isiyovumilika!.

20. Nyumba 2 za Bibi TITI Zataifishwa:
Wakati akiwa anatumikia kifungo chake cha maisha, serikali ikataifisha nyumba zake mbili zilizotajwa hapo juu.

21. MWANAMAMA Mkenya Amuomba Mwalimu Amsamehe TITI:

Mwanamama mmoja mwanasiasa machachali wa Kenya baada ya kupata habari za TITI kufungwa maisha alikuja Butiama na akaomba aonane na Mwalimu na mama yake. Alipoonana nao akasema:
"Utakuwa ni wizi wa fadhila kama wewe NYERERE utaendelea kumfunga TITI licha ya yote aliyokufanyia wewe, TZ na sehemu hii ya dunia. Tafadhali sana nimetumwa na wanawake wa Kenya nikuombe umwachie huru kama yeye alivyopigania kuachiwa huru kwa JOMO KENYATTA".

Mwalimu NYERERE alimjibu mama huyo kuwa maombi hayo ameyapokea na atayafanyia kazi.

22. TITI Achiwa kwa Msamaha wa Rais, 1972:
Rais NYERERE, akitumia mamlaka yake chini ya ibara ya 45 ya Katiba, alimsamehe TITI mwezi April 1972.

23. TITI Akwea "gogo" kuja Dsm:
Baada ya kusikia msamaha huo, TITI hakuamini maskio yake kwani aliishaamua kupambana na hali yake na alijua angefia gerezani. Hivyo, alipanda garimoshi na kuja Dsm akiwa na furaha tele na meno yote 32 nje. 

Ndugu zake walimlaki kwa bashasha na akaenda kuishi kwenye nyumba kuukuu ya mama yake iliyoko Temeke. Mama yake, aliyekuwa mtu mzima sana, almanusra azimie kwa mshtuko wa kumuona mwanae!.

24. MH. MALECELA Atumwa Kenya kuekeza TITI Yuko Huru:
Rais NYERERE alimtuma Mh. JOHN SAMWELI CIYEGWEYAMIS MALECELA , Waziri wa Mambo ya Nje, kwenda Kenya kumweleza yule mama Mwanasiasa machachali kuwa TITI ameachiwa. Baada ya kupata ujumbe huo, Mwanamama huyo aliyejawa na furaha akasema: "Naomba kamwambie Mwalimu NYERERE kwa niaba ya wanawake wote wa Kenya na wananchi wa Afrika Mashariki, nasema asante sana kwa uungwana wake".

25. TITI Aishi Maisha ya Kifukara:
Baada ya kuachiwa toka Lupango, TITI alienda kuishi Temeke. Maisha yake yalikuwa ya kipweke sana kwani ndugu na marafiki walimnyanyapaa: "Mtu angeweza kufikiri kwamba nina ugonjwa wa kuambukiza". TITI akawa muda mwingi anakaa kibarazani kwao akiuza mafuta ya taa ya rejareja ili kuweza kumudu maisha!.

26. BIBI TITI Arudishiwa nyumba zake:
Rais ALI HASSAN MWINYI alimrudishia BIBI TITI nyumba zake zote 2. Hivyo, Bibi TITI akahamia nyumba ya Upanga.

27. BIBI TITI Afariki:
BIBI TITI alifariki tarehe 5.11.2000 katika hospitali ya Net care, Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu.

28. BIBI TITI Apewa Mtaa, Dsm:
Kama kumbukizi ya kuheshimu mchango mkubwa wa mwanamama huyu wa kipekee, mtaa mmoja maarufu jijini Dsm umepewa jina lake "Barabara ya Bibi TITI".


MWISHO:

Huyu ndiye BIBI TITI MOHEMED, Mwanamama shupavu aliyetoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika aliyekuwa si mnafiki na hapindishi maneno kwa kile alichokiamini wala hamwogopi binadamu yeyote zaidi ya Mungu!!








Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>