Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

$
0
0
Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu na mmoja kati ya wavulana saba hufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.

Alisema hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia  Grace Mwangwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.

Mafunzo hayo kwa Maafisa hao yafanyika Mjini kasulu kwa lengo la kuwapatia mafunzo ya Kitini cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto na kuwawezesha  kupata mbinu na uwezo wa kuwajengea  wazazi na walezi maarifa na washiriki hao wanatoka kwenye Mikoa yenye kiwango kikubwa cha mimba na ndoa za utotoni.

Aidha Bi. Mwangwa aliwambia wajumbe wa mafunzo hayo kuwa viwango vya ukatili wa kimwili ni asilimia 72 kwa wasichana na asilimia 71 ni wavulana ambavyo vinasababishwa zaidi na wazazi, walezi wakiwemo  walimu.

Bi. Mwangwa alisema pia kuwa  robo tatu ya watoto huadhirika zaidi na ukatili wa kihisia kutokana na kutukanwa matusi, kubaguliwa na kupuuzwa akiongeza kuwa Vitendo vyote hivi vinasababishwa na desturi na kanuni za jamii zenye madhara na zinazounga mkono kutumia ukatili katika kumlea mtoto.

‘’Ukosefu wa uelewa, maarifa na stadi zinazohusu njia za malezi zisizo za ukatili na umma kutoelimishwa vya kutosha kuhusu haki za mtoto pamoja na umaskini wa kaya unaosababisha wazazi au walezi kuwatelekeza watoto, uhamiaji kutoka vijijini kwenda mijini ambapo watoto hutolewa vijijini na ndugu zao kwa ahadi za maisha mazuri na kudhoofika kwa mifumo ya asili ya kijamii. Alisikika akisema Bi. Mwangwa.

Aliwaambia washiriki wa kikao hicho kuwa nafahamu dhihiri kuwa,mfumo wa ulinzi wa mtoto ni msingi imara ambao unapelekea uwekaji wa mazingira ya ulinzi kwa watoto wetu kuanzia ngazi ya taifa,jamii na familia kwa ujumla.

Bi. Mwangwa aliendelea kusema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau imedhamiria kushughulikia ukatili dhidi ya watoto kwa kuweka sera, sheria na mipango inayolenga kulinda haki za mtoto.

Kupitia Kitini hiki cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto washiriki  watapata mbinu na kuwa na uwezo wa kuwajengea  wazazi/ walezi maarifa na stadi  juu ya mikakati ya kijamii ya kuzuia aina  zote za ukatili dhidi ya watoto kupitia elimu madhubuti ya malezi chanya yanayofaa katika jamii.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Grace Mwangwa pamoja na Kaimu Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Msafiri Nzunuri  wakifuatilia jambo  wakati wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Grace Mwangwa akitoa maelekezo wakati wa  ufunguzi wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii anyeshughulikia masuala ya malezi kwa watoto na familia Bw. Emmanuel Burton akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma Mapema leo katika mji mdogo wa Kasulu Mkoani Kigoma.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Katavi na Kigoma wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Kitini cha Elimu ya Malezi ya Familia kwa Watoto yanayotolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii leo katika mji mdogo wa Kasulu.

RAIS DKT.SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA KASKAZINI B, UNGUJA

$
0
0
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza wakati wa mkutano wake wa Majumuisho ya ziara yake katika Wilaya ya Kaskazini B, Unguja, yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff Kama Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo 18-2-2019.(Picha na Ikulu)
 BAADHI ya Wanachama  wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini B, Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara yake Wilaya ya Kaskazini B, Unguja, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdallah Juma Mabodi, akizungumza wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Sheid, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo, yaliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Sea Cliff Kama.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri, akizungumza wakati wa mkutano wa Majumuisho ya Ziuara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, katika Wilaya ya Kaskazini B, Unguja leo, yaliofanytika katika ukumbi wa Hotewli ya Sea Cliff Kama
MBUNGE Mstaafu wa Jimbo la Donge Ali Ameir Mohammed akiwa na Viongozi wa Serikali na Chama wakati wa mkutano wa Majumuisho ya  ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja,yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff.(Picha na Ikulu) 
MKUU wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Ndg. Rajab .Ali.Rajab, akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji ya Wilaya yake wakati wa Majumuisho ya ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Sheini, baada ya kumaliza ziara yake kutembelea Miradi ya Maendeleo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, hafla hiyo imefanytika katika ukumbi wa haoteli ya Sea Cliff.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri, MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Dr. Abdallah Juma Mabodi, wakifuatilia ripoti ya utewkelezaji wa Wilaya ya Kaskaziniu B Unguja, ikiwasilishwa nac Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B,Unguja Ndg. Rajab Ali Rajab. wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara yake.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibare na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mbunge Mstaaf wa Jimbo la Donge Mkoa wa Kaskaszini Unguja. Mzee Ali Ameir Mohammed, baada ya kumalizika kwa mkutano wa Majumbisho ya Ziara yake Wilaya ya Kaskazini B, Unguja baada ya kumalizika hafla hiyo katika ukumbi wa hoteli ya Sea Cliff Kama Unguja.(Picha na Ikulu) 

INTRODUCING "NITASAHAU" OFFICIAL VIDEO BY TAYCE

ALIYOYASEMA KAIMU MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NCHINI BI. NEEMA MWANGA BAADA YA KUTEMBELEA BAADHI YA MASHIRIKA YALIYOPO MKOANI KILIMANJARO

MAKONTENA YA DRC YALIYOKWAMA BANDARINI DAR ES SALAAM YAANZA KUONDOKA

Kampuni ya bima ya UAP Old Mutual yawanoa mawakala kwa stadi mpya za biashara

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Kukuza Biashara wa UAP Old Mutual Insurance Jabir Kigoda akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya mawakala yaliyoandaliwa kwa ajili ya mawakala wa kampuni hiyo hivi majuzi jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya mawakala wa UAP Old Mutual Insurance wakifuatilia mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es salaam hivi majuzi.

Meneja wa Kukuza Biashara wa Old Mutual Insurance , Charles Magori, akiwasilisha mada katika mafunzo kwa mawakala wa kampuni hiyo Dar es Salaam hivi majuzi. 


Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya bima ya Old Mutual Insurance hivi majuzi waliendesha mafunzo ya siku moja kwa mawakala wake ambayo ililenga kuwanoa katika stadi mpya za biashara katika sekta hiyo inayokuwa kwa kasi.

Mfunzo hayo, yaliyohudhuriwa na mawakala 60 wa kampuni hiyo kutka maeneo mabalimbali ilijikita katika kuwapa mawakala stadi mpya katika Nyanja mbalimbali kuanzia bidhaa, mauzo na kanuni mbalimbali za uendeshaji.

“ Mafunzo ya aina hii vilevile yanantoa fursa ya kuwasiliana ana kwa ana na mawakala ambayo ni njia rafiki . Isitoshe, mawakala wanapata fursa ya kutambua maswala mbalimbali yanayojitokeza mara kwa mara katika soko la bima kwa ujumla,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Kukuza Biashara wa UAP Jabir Kigoda, alipokuwa akifafanua dhana ya mafunzo hayo.

Kati ya maeneo yaliyoguswa na mafunzo hayo ni namna ya kukidhi matakwa ya sheria mbalimbali za udhibiti biashara ya bima, kitu ambacho ni muhimu kuwezesha mawakala kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa sheria zilizopo. “ Hii itasaidia sana kuhakikisha kuwa mawakala hawavunji sheria na hivyo kuondoa mikwaruzano isiyo ya lazima na vyombo vya sheria, kanuni na taratibu,” alisema Kigoda.

Akifafanua kwa jinsi mafunzo hayo yalivyoendana na wakati, Kigoda alisema “ Mafunzo haya yamekuja katika muda muafaka kwa kuwa azma yetu daima ni kuwapa wateja wetu huduma bora. Nina uhakika yatasaidia kwa kiwango kikubwa kuwafanya mawakala kutambua namna ya kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi kwa siku za usoni .”

BREAKING NYUZZZZ...... MALKIA WA TEMBO NA WENZAKE WAWILI WATIWA HATIANI KESI YA MENO YA TEMBO

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtia hatiani raia wa China, Yang Feng Glan (66) maarufu kama Malkia wa tembo, na wenzake Wawili baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi kumi na moja upande wa mashtaka Katika mashitaka ya kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 13, kinyume cha sheria.

Mbali na Feng washtakiwa wengine waliotiwa hatiani ni,  wafanyabiashara raia wa Tanzania, Salvius Matembo na Philemon Manase, ambao wote walikuwa wakitetewa na mawakili Nehemia Nkoko na Hassan Kiangio.

Hukumu imeahirishwa baada ya dakika 30 ili washitakiwa wajitetee kabla ya kuhukumiwa. 

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

KAMPUNI YA BLOCKBONDS KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA I & M WAZINDUA HUDUMA YA SPENN

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii. 
Kampuni ya Blockbonds yenye makao makuu yake nchini Norway kwa kushirikiana na Benki ya I & M ya Tanzania  wamezindua rasmi huduma mpya  bunifu ijulikanayo kwa jina la SPENN yenyekuweza kufanya malipo bure ya kutuma na kutoa hela. 

Huduma hiyo bunifu itapatikana kupitia Benki ya I &M  itakayokuwezesha kufanya miamala mbali mbali  bure, ambapo utaweza kufungua akaunti binafsi na ya biashara kiganjani mwako. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo  Afisa Mtendaji  Mkuu wa Blockbonds na SPENN  Jens Glaso Jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa anafuraha kubwa kuingiza rasmi huduma hiyo katika soko lingine barani Afrika baada ya kufanikisha kuizindua  rasmi nchini Rwanda mnamo Mwaka jana ambayo mpaka sasa inawatumiaji zaidi ya 130,000  nchini humo. 

"Ni rahisi sana mtu yoyote anayemiliki  simu aina ya Smartphone  (simu janja)  anaweza kujisajili na huduma ya SPENN  Kwa urahisi ambapo ili kujisajili unapaswa kuwa na namba ya simu, jina kamili pamoja na namba ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA"amesema bwana Glaso. 

Aidha mkurugenzi mtendaji  Benki ya I&M  Baseer Mohammed  amesema kuwa benki hiyo imejikita   zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ambayo huduma hiyo inalenga kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja  wake. 

"Huduma hiyo inayobadilisha namna ambavyo watanzania wanafanya miamala yao ya kifedha na kufanya mfumo mzima wa kufanya miamala kuwa na ufanisi zaidi, wenye usalama na pasipo kuwa na gharama, vilevile tunaamini kabisa huduma ya SPENN  itachangia katika kuboresha maisha ya Watanzania "amesema Baseer Mohammed. 

Hata hivyo Meneja masoko na mawasiliano Benki ya I & M Emmanuel Kiondo amesema kuwa sababu ya kutimia simu janja kupakua App ya SPENN  na kufanya miamala yote iliyotajwa wamezingatia sababu za kiusalama zaidi.
Afisa Mtendaji  Mkuu wa Blockbonds na SPENN  Jens Glaso  akizungumza wakati wa uzinduzi huo   kuhusu huduma hiyo ya SPENN inavyoweza kufanya kazi na kurahisisha kufanya kazi kwa kuondoa mfumo wa uchumi unaohitaji fedha taslimu kufanya miamala  Jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi mtendaji  Benki ya I&M  Baseer Mohammed akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam kuwa Benki ya I &M imejikita zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ikiwa  malengo yao ni kukidhi matarajio ya Wateja.
.Wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo wa huduma ya SPENN kwa kushirikiana na benki ya I & M   Jijini Dar es Salaam

Yahaya Makolija akabidhiwa mamilioni ya biko

$
0
0
Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Yahaya Hassan Makolija, leo amekabidhiwa fedha zake jumla ya shilingi milioni 10 alizoshinda kwenye bahati nasibu ya Biko inayotesa katika viunga vya nchi yetu.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mratibu wa Matukio wa Biko Hassan Melles, ambapo katika droo ya jana Jumapili, wengine pia waliibuka na bodaboda na mamilioni kutoka Biko. 

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Makolija aliishukuru Biko kwa kumkabidhi fedha zake akisema kuwa itamsaidia kwa kiasi kikubwa katika maisha yake ya kila siku.

Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati  watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.
 Yahaya Makolija akiwa na shangwe kubwa baada ya kukabidhiwa sh million 10 alizoshinda kutoka kwenye droo kubwa ya Bahati nasibu ya Biko iliyofanyika juzi Jumapili jijini Dar es Salaam. Droo nyingine kubwa hufanyika kila Jumatano na Jumapili bila kusahau zawadi za papo kwa hapo zinazoenda kwa washindi kila wakati. 
Mshindi wa sh milioni 10 wa droo ya 182 wa bahati nasibu ya Biko, Yahaya Hassan Makolija, kulia akipokea fedha zake kwa furaha kubwa kutoka kwa Mratibu wa matukio wa Biko, Hassan Melles, katika makabidhiano yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ikiwa siku moja tu baada ya kuibuka na ushindi kwenye droo iliyofanyika Jumapili, ambapo droo hizo kubwa hufanyika kila Jumatano na Jumapili.

Tamasha la Mkeka na Mvinyo Lafana Dar

$
0
0
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na wapendwa wao mwishoni mwa wiki walipata fursa ya  kufurahia pamoja siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’.

Hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam, ilishuhudiwa wakazi hao wakijitokeza kwa wingi sambamba na wapendwa wao ili kufurahia siku hiyo maalum ambapo pamoja na vinywaji vingine waliweza kufurahia mvinyo wa aina mbalimbali unaozalishwa hapa nchini.

Mbali na burudani nzuri ya muziki laini kutoka msanii Maximilian Rioba maarufu kwa jina la Milian, kivutio kingine kwenye hafla hiyo kilikuwa ni matumizi ya mikeka ambapo baadhi ya washiriki walipata fursa ya kuketi kwenye mikeka iliyoandaliwa sambamba na meza fupi wakipata vinywaji, vyakula huku wakifuatilia burudani ya muziki iliyokuwa inaendelea.

“Hii ni hafla yetu ya kwanza ya Mkeka na Mvinyo kati ya hafla nyingine nyingi za aina hii zitakazo fanyika SikuKuu ya Pasaka, Msimu wa Sabasaba, na mwisho wa mwaka yaani Likizo Time. Tunashukuru kuona hafla hii imepokelewa vizuri na wadau na  tunawaahidi mambo mazuri zaidi yanakuja kupitia Mkeka na Mvinyo waendelee kutuunga mkono,’’ alisema Bi Caroline Kirwanda Mratibu wa hafla hiyo kutoka kampuni ya Real PR Solutions (RPR).

Aliwashukuru baadhi ya wadau muhimu katika kufanikisha hafla hiyo kuwa ni pamoja na  kampuni ya uzalishaji wa mvinyo ya Alko Vintages ya jijini Dodoma, Hoteli ya Whitesands, Bodi ya Utalii  Tanzania, (TTB), GS 1, pamoja na kampuni ya magazeti ya TSN wazalishaji wa magazeti ya Daily News pamoja na Habari Leo.

Bi Kirwanda aliongeza kuwa hafla hiyo ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo utakaozinduliwa hivi karibuni unaolenga kutangaza utalii wa ndani pamoja kuvumbua fursa mbalimbali za kibiashara ndani ya nchini kwa lengo la kukuza uchumi unaofahamika kwa jina la ‘Domestic Tourism Promotion Initiative’ (DTPI).

“Tunahitaji kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa za ndani ili kukuza uchumi wetu kama taifa,’’ aliongeza  bi Kirwanda.

Kwa upande wake, Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Alco Vintages , Sweetbertha Rwabizi alisema ushiriki wao kama wazalishaji wa  mvinyo wa ndani  kwenye hafla hiyo unalenga kuhamasisha zaidi matumizi ya bidhaa hizo kwa kuwa tofauti na kuuza bidhaa zao pia walipata fursa ya kukutana moja kwa moja na watumiaji wa bidhaa hizo na hivyo kupata mrejesho kutoka kwao huku pia wakijenga uelewa zaidi kwa watumiaji kuhusu vinywaji hivyo.

“Iwapo watanzania watabadirika na kuanza kutumia bidhaa hii ya mvinyo unaozalishwa hapa nchini, inaweza kukuza soko la wakulima kwa zaidi ya asilimia 80 kutokana na bidhaa hii kuzidi kupata watumiaji kadiri siku zinavyokwenda.’’ Alisema.
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya uzalishaji wa mvinyo ya Alko Vintages ya jijini Dodoma, Sweetbertha Rwabizi (kulia) akimuhudia mmoja wa  wageni waliojitokeza kufurahia pamoja siku ya wapendanao yaani Valentine Day katika hafla maalum inayofahamika kama ‘Mkeka na Mvinyo’ iliyofanyika katika hoteli ya Whitesands jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja na agenda nyingine hafla hiyo inalenga kuhamasisha matumizi ya mvinyo unaozalishwa hapa nchini.

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MWEKA HAZINA KIBONDO

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Thomas Chogolo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma  zinazomkabili za ubadhilifu wa makusanyo ya mapato ya halmashauri hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amewataka watendaji wa halmashauri huyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na maelekezo yake.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.

 “Katika Serikali hii suala la ukusanyaji wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema wananchi wa halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika maeneo yao lakini  Mweka Hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali. “Jambo hili halivumiliki.”

Amesema mbali na fedha za makusanyo ya kodi pia matumizi ya fedha mbalimbali zinazopelekwa na Serikali katika halmashauri hiyo nayo hayaridhizishi. Ametoa mfano wa fedha za sekta ya Afya ambapo zaidi ya bilioni mbili zimepelekwa na dawa hakuna.

Waziri Mkuu amesema uaminifu na uadilifu ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na watumishi wa umma, hivyo amewataka watumishi hao wasijiingize kwenye mambo ambayo hayana tija katika utumishi wao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imewapa dhamana watumishi hao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si kutanguliza maslahi yao binafsi, amewataka wajirekebishe kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Serikali haitawapa nafasi ya kuendeleza migogoro yenu kila mmoja lazima atambue majukumu yake na kuyatekeleza. Serikali haiitaji mtumishi mvivu, masiyekuwa muadilifu na wala anayejihusisha na vitendo vya rushwa.”

Amesema ni lazima wakamaliza migogoro ya kiutendaji ambayo imesababisha watendaji wa halmashauri kutoelewana na kugawanyika katika makundi na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati  alipozungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo,  Februari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Februari 19, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya  ya Kibondo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibondo, Februari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VIJANA WAASWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha
Wataalam wa afya kwa kushirikiana na shirika la Tupange pamoja wamekutana na vijana mbali mbali mkoani Arusha katika kuhamasisha upimaji wa afya pamoja na kutoa elimu ya uzazi kwa vijana 

Wataalamu hao wamekuta na vijana katika eneo la makumbusho ya Azimio la Arusha lengo la kukutana na vijana hao ikiwa ni kuwapa elimu ya uzazi pamoja na kuchangia damu sambamba na kupima afya zao

Akizungumza na Michuzi Blog Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wilaya Arusha Bi Laura chua amesema wameemua kuwa kutanisha ilikuwapa elimu ya uzazi kwani wengi wao hawana elimu ya uzazi hali inayopelekea vijana (kike) nchini kupata mimba zisizo tarajiwa.

“Siku ya leo tumekutana na vijana mbali mbali na vijana waishio hapa mkoani arusha katika kuwapa elimu na kuwa hamasisha katika uchangiaji damu pamoja na upimaji virusi vya ukimwi kwa hiyari pia tuna mikakati mingi kwa mwaka huu katika kuwafikia vijana hawa tumepanga kuweka matamsha mengi ya uhamasishaji na wiki ijayo tumepanga tumeandaa tamasha ambalo litafanyika katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid ili tuwahamasishe vijana.Alisema

Mbali na matamasha ambayo wataandaa wamesema watatumia waandishi habari,pamoja na wasanii katika kuhamasisha vijana kwani vijana wengi wamejawa na imani potofu za kutoamini maswala ya afya hivyo kupelekea vijana wa kike na wakiume kupoteza ndoto zao.

Aidha mratibu wa Mradi wa tupange pamoja amesema vijana wengi hawapati fursa ya kutaka kujifunza hivyo kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wamepanga mikakati ya kuwafuata vijana na kuwahamasisha ili watambue maswala ya husuyo afya ya uzazi kwa kuandaa matamasha na kuwatumia waandishi habari katika kuaanda vipindi mbali mbali za uhamasishaji.

Alisisitiza vijana wajitokeze katika fursa hizo ambazo zinatokea katika mkoa wa Arusha kwani wakiwekeza zaidi katika kujifunza na kushiriki katika upimaji wa afya zao watakuwa wanajiwekea usalama katika maisha ya ujana.
Pichani ni baadhi ya vijana waliojitokeza kupata Elimu ya Afya ya Uzazi katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Jijini Arusha
Mmoja wa waandishi habari Bw onesmo loy akiteta nawili matatu na vijana waliojitokeza maeneo hayo
Baadhi ya watalam wa afya kutoka katika zahanati ya levolosi iliopo arusha(watatu waliosimama) wakiwa tayari kwa ajili yakutoa elimu kwa vijana.

TIMU YA MAKATIBU WAKUU YATEMBELEA VIJIJI NA VITONGOJI VILIVYOMO NDANI YA HIFADHI

$
0
0
Timu ya Makatibu wakuu wa Wizara za kisekta zinazohusika na urasimishaji vijiji na vitongoji vilivyoanzishwa na kusajiliwa ndani ya Hifadhi imeanza ziara yake ya kutembelea vijiji na vitongoji  vilivyomo ndani ya maeneo ya Hifadhi ili kujionea na kutoa ushauri wa namna bora ya kurasimisha vijiji hivyo bila kuathiri uhifadhi endelevu. Wizara hizo ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Ofisi ya Rais Tamisemi.

Hatua hii inafuatia agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Wizara za Kisekta kuangalia namna bora ya kurasimisha vijiji na vitongoji vilivyoanzishwa na kusajiliwa ndani ya Hifadhi. Kufuatia agizo lililotolewa na Rais Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi aliwaagiza Makatibu wakuu wa Wizara za Kisekta, kuunda kamati kwa ajili ya kuchambua kwa kina maeneo ya vijiji na vitongoji vilivyomo ndani ya Hifadhi ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais Magufuli.

Akizungumza na Waandishi wa Habari walipotembelea Pori la Akiba la Swagaswaga, Mwenyekiti wa Timu hiyo ya Makatibu Wakuu, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi Bibi Dorothy Mwanyika, amesema mapendekezo yatakayotolewa na timu ya Makatibu Wakuu hao, yatasaidia katika utekelezaji mzuri wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu urasimishaji wa vijiji hivyo na vitomgoji vilivyomo ndani ya Hifadhi huku suala zima la uhifadhi endelevu likizingatiwa.

Bibi Dorothy amesema, ziara hii ni ya kwanza ikifuatiwa na ziara katika mkoa wa Arusha na Njombe. Amesema, timu ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta wanaendelea na Ziara kama hiyo katika mikoa mingine na tayari wametembelea mikoa ya Morogoro na Kigoma. Wakiwa katika Pori la Akiba la Swagaswaga, timu hiyo ya Makatibu Wakuu ilijionea kuwa baadhi ya vijiji viko katika maeneo ya vyanzo vya maji na mapito ya wanyama. 

Akifafanua zaidi kuhusu umuhimu wa ziara hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa, ziara katika vijiji hivyo na vitongaji vilivyoko ndani ya Hifadhi zitaiwezesha timu hiyo ya makatibu wakuu kujionea hali halisi ya vijiji hivyo ikiwemo mipaka, hali halisi ya Hifadhi kwa sasa na maeneo muhimu ya Hifadhi ambayo yanapaswa kulindwa kwa faida ya nchi na hivyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa ushauri utakaosaidia katika utekelezaji wa agizo la  Rais  Dkt. John Pombe Magufuli      
Akizungumza na timu hiyo ya Makatibu Wakuu wa Wizara saba za Kisekta zinazohusika na urasimishaji vijiji na vitongoji vilivyoanzishwa na kusajiliwa ndani ya Hifadhi, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bwana Simon Odunga ameishauri kamati hiyo kuangalia namna bora ya kuhifadhi maeneo oevu na vyanzo vya maji vilivyoko kwenye Pori la Akiba la Swagaswaga kwani vyanzo hivyo ndivyo vinavyopeleka maji kwenye mto Mtera.

Bwana Odunga ameongeza kuwa tunahitaji kulinda vyanzo vya maji ili kuepusha nchi kuwa jangwa na kuwa, pamoja na kuangalia mahitaji ya wananchi wetu kama alivyoelekeza Rais lakini  tukumbuke Rais alisisitiza kuwa bado tunahitaji kuhifadhi.  Odunga ameongeza kuwa tunahitaji kuangalia suala zima la Uhifadhi wa Maliasili zetu kwa manufaa ya Taifa na vizazi vijavyo huku tukizingatia mahitaji ya wananchi kwa maendeleo endelevu. Awali, akizungumza kuhusu umuhimu wa Pori la Akiba la Swagaswaga kiuchumi na kiikolojia, Meneja wa Pori la Swagaswaga Bwana Alex Choya amesema, eneo hili ni muhimu kwa mazalia ( breeding Site) ya wanyamapori walio hatarini kutoweka kama vile Korongo na Tandala wadogo na malisho (Feeding) na Mtawanyiko ( Dispersal area) kwa wanyamapori.

Bwana Choya ameongeza kuwa, Pori hili ni kiungo muhimu kiikolojia kati ya Hifadhi ya Tarangire (upande wa Kaskazini), Msitu wa Hifadhi wa Jamii Mgori na Mapori ya Akiba ya Rungwa/ Kizigo/ Muhesi ( upande wa kusini magharibi) mwa Tanzania. Ameongeza kuwa Pori hili linachangia mapato asilimia 25 ya ada ya wanyamapori wanaowindwa kupitia uwindaji wa Kitalii kwa Halmashauri za Wilaya za Kondoa na Chemba. Meneja huyo wa Swagaswaga, amesisitiza kuwa Pori la Akiba Swagaswaga ni chanzo muhimu cha mto Bubu ambao hutiririsha maji yake kuelekea Bwawa la ufuaji umeme la Mtera. 

Pori la Akiba la Swagaswaga lina Rasilimali mbali mbali zikiwemo za Wanyamapori, misitu na uoto wa asili uliotawaliwa na miti ya miombo, mimea ya aina mbalimbali, vichaka vifupi pamoja na miinuko na milima midogo yenye miamba, majabali na mapango makubwa. Wanyamapori waliopo katika Pori la Akiba Swagaswaga ni pamoja na Tandala (Greater and Lesser Kudu), Tembo, Korongo (Roan antelope), Nyati, Pundamilia, Swalapala, Pofu, Chui, Twiga, Simba, Kongoni, Pongo, Ngiri, Nguruwe pori, Nsya, Nyani, Tumbili na Mbuzi mawe.

Pori hili pia, lina utajiri mkubwa wa michoro ya miambani (Rock Art Paintings) ambayo ni kivutio cha Utalii na kuna jumla ya maeneo hamsini na mbili (52) yenye michoro ya miambani (Rock Painting Sites). Aidha, Pori la Akiba Swagaswaga pia lina umuhimu wake kihistoria kwani lina njia iliyokuwa ikitumika kusafirisha watumwa (Pario msomali/veterinary stock route) kutoka mikoa ya kigoma, Tabora hadi Handeni – Tanga. Pori la Swagaswaga lilipandishwa hadhi na kuwa Pori la Akiba kwa tangazo la Serikali Na. 72 la tarehe 21/02/1997 likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 871 na mzingo wa kilomita 183.184.  Pori la Akiba Swagaswaga ni Hifadhi pekee ya Wanyamapori iliyoko karibu na jiji la Dodoma na linazungukwa na vijiji 17 vilivyopo katika Mkoa wa Dodoma na Singida.
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bwana  Simon Odunga akitoa maelezo kwa timu ya Makatibu Wakuu kuhusiana na mipaka ya vijiji  vilivyoko kwenye Pori la Akiba  Swagaswaga 
 Timu ya Makatibu Wakuu wakishuhudia Mifugo ikinywa maji kwenye mto Bubu ambao  hutiririsha maji yake kuelekea Bwawa la ufuaji umeme la Mtera. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda, Akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja wa Pori la Akiba Swagaswaga Bw. Alex Choya  ( Hayumo Pichani)  kuhusu umuhimu wa Pori la Akiba Swagaswaga. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi  Prof. Elisante  Ole Gabriel na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bwana Simon Odunga.
 Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bwana Simon Odunga akiwaelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel walipotembelea Pori la Akiba Swagaswaga kuhusiana na Suala la urasimishaji wa vjiji vilivyomo ndani ya Hifadhi. 
Timu ya Makatibu Wakuu wakishuhudia Mifugo ikinywa maji kwenye mto Bubu ambao  hutiririsha maji yake kuelekea Bwawa la ufuaji umeme la Mtera.

WANADIASPORA WA SAUDIA WAPIGWA MSASA UHAMIAJI MTANDAO

$
0
0
Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia “Tanzania Welfare Society” hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza.

Wanajumuiya walipata fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali yakiwemo uwekezaji na uchumi, ajira nchini Saudi Arabia, masomo nchini Saudi Arabia. Aidha, wanajumuiya walipata maelezo kuhusu matumizi ya mfumo mpya uhamiaji mtandao “e-immigration” ambapo walifahamishwa na kutakiwa kuanza rasmi kuomba pasi mpya za kusafiria za ki-electronic, hati za dharura za kusafiria za ki-electronic. Pia wanajumuiya walitakiwa kuwahamasisha wageni kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii, uwekezaji na biashara, na pia sasa wanaweza kuomba viza za kuingia Tanzania kwa njia ya mtandao “e-visa”. 

Wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania.
Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah, Bw. Salim Ali Shatri, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akihutubia, kujibu maswali na kutoa ufafanuzi, mwisho kulia ni Mweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania ya Jeddah, Bw. Abdallah Faris.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakiwa mkutanoni. 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident Jeddah. 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakipata chakula
Wanajumuiya wakipata chakula

SIMBA VITANI KUIKABILI AFRICAN LYON LEO

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) Simba inashuka dimbani leo kucheza na African Lyon Jijini Arusha.Mchezo huo ni muendelezo wa. Ligi Kuu na utakuwa mchezo wake wa 17 wa Ligi utapigwa kwene dimba la Shekhe Amri Abeid kuanzia sa 10 alasiri.

Simba watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka kuwafunga watani wao wa jadi Yanga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Ofisa habari ww Simba Hajji Manara amesema kikosi kimejiaandaa kwa ajili ya mchezo huo na matumaini makubwa ni kuona wanaweza kupata alama tatu ugenini.

"Tunawaheshimu African Lyon ni timu nzuri, ila nasi pia hatuna budi kufanya kile ambacho mashabiki wanahitaji, tayari wachezaji na uongozi umeweza kuimudu hali ya hewa ya huku Arusha, ni wakati tu, sapoti ya mashabiki pamoja na dua ni vitu muhimu," amesema Manara.

Timu hiyo yenye alama 39 wakiwa nafasi ya tatu ya Ligi inatarajia kuwakosa wachezaji wake wa kimataifa Meddie Kagere na Emanuel Okwi. Baada ya mchezo huo, Simba waterejea Jijini Dar es Salaam kuvaana na Azam Fc ikiwa ni mchezo wa kiporo wa mzunguko wa kwanza wa TPL.

Mechi zingine za Ligi ni Coastal Union wakiwa nyumbani wakiwakaribisha Azam Fc, Mwadui akicheza na Biashara United pamoja na Kagera akicheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mlandizi.

Waziri Dkt. Mwakyembe Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Italia Nchini Tanzania

$
0
0
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Italia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 19 Februari 2019.
 Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Italia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 19 Februari 2019.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (kushoto) akifafanua jambo kwa  Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Italia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 19 Februari 2019.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akifafanua jambo kwa Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni (hayupo pichani) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Italia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 19 Februari 2019.
 Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea Waziri Mwakyembe katika ofisi ndogo ya wizara hiyo iliyoko jijini Dar es salaam na kuzungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Italia na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mazungumzo hayo yamefanyika leo 19 Februari 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Roberto Mengoni pamoja na watumishi wa wizara.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

DC MAKORI AZINDUA MRADI WA MAJI MSAKUZI JIJINI DAR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori amemzindua mradi wa maji wa Msakuzi utakaohudumia kaya 3500 za eneo hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi huo, Makori amesema kuwa anawapongeza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) kwa hatua kubwa waliyoifanya ya kuleta maji katika eneo la Msakuzi.

Makori amesema, kupatikana kwa maji kwenye eneo hili litaondoa kero ya maji iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu. Mkuu wa Wilaya ameweza pia kuzindua vizimba vitatu vitakavyohudumia wananchi 18,000 kwa kwa siku na pia itasaidia kwa wale ambao hawatakuwa wameunganishwa.

Akiongea kwa niaba ya DAWASA Meneja wa Mkoa wa Ubungo Mhandisi Pascal Fumbuka amesema Mradi wa Msakuzi wa Km 2.1 utahudumia kaya kaya 3500 sawa na wananchi zaidi ya Laki mbili (200,000) wa eneo lote na mpaka sasa wananchi 500 wameshajaza fomu bado kuunganishiwa maji tu.

Kuongezeka kwa wateja wa eneo la Msakuzi, Fumbuka amesema wanatarajia kuongeza pato la Kimkoa na kufikia Bilion 1.5 kwa mwezi na pia wizi wa maji utapungua baada ya wananchi wa eneo hilo kuunganishiwa maji. Ameeleza kuwa huduma ya kuunganishiwa maji wananchi ni la mkopo na utaandikishwa mkataba baina ya DAWASA na mwananchi ambao utalipwa ndani ya mwaka mmoja.
 

DAWASA wanaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waliokuwa nje ya mradi kwa muda mrefu na kuwapelekea huduma hiyo muhimu ambapo wananchi wengi wameshukuru jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kisare Makori akimtua ndoo ya maji mama kichwani baada ya kuzindua kizimba cha maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mbezi Msakuzi utakaohudumia na kuwanufaisha wananchi zaidi ya laki mbili (200,000).
Mkuu wa Wilaya Kisare Makori akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mbezi Msakuzi utakaohudumia na kuwanufaisha wananchi zaidi ya laki mbili (200,000).
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akizindua moja ya kati ya vizimba vitatu vilivyopo katika mradi wa maji wa Mbezi Msakuzi utakaohudumia na kuwanufaisha zaidi ya wananchi laki mbili kwa siku (200,000).
Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Pascal Fumbuka akielelezea mradi wa maji wa Mbezi Msakuzi na wakiendelea kuwaunganishia maji wananchi waliokwisha jaza fomu ili kupata huduma ya majisafi na salama.

Wananchi wa eneo la Mbezi Msakuzi wakiendelea kujipatia huduma ya maji katika moja ya Kizimba kilichopo eneo hilo.

WARAGHABISHI WAKUTANA DODOMA KWENYE MKUTANO WA DIGITALI NA MAENDELEO

$
0
0
Na Vero Ignatus, Dodoma
Serikali imewapongeza waandishi wa habari za mtandao kwa kufikisha taarifa kwa jamii kwa haraka hali inayopelekea wananchi kuchukua hatua katika kuleta mabadiliko. Akizungumza katika mkutano mkuu wa Waragabishi ulioandaliwa Shirika la Oxfam Tanzania Jijini Dodoma  Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaac Kamwele wakati akitoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa Dijitali kwa maendeleo

Waziri amesema kuwa  Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika matumizi ya mitandao katika mifumo mbalimbali ya shughuli za serikali kila siku ili kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma Bora, umoja na muunganiko wa wananchi uwajibikaji na uwazi ndani ya Serikali uwajibikaji wa wananchi katika maendeleo

Akitoa hotuba kwa  niaba ya makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Mhandisi  Kamwele amesema kuwa Waandishi wa habari za mtandao wana nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko kwani wanawafikia watu wengi kwa muda mchache. Sambamba na hayo ametoa wito kwa wananchi wanaomiliki simu janja kutumia simu zao vizuri katika kuleta mabadiliko kiuchumi na kuacha tabia ya kutumia simu zao kwa mambo yanayovunja maadili katika jamii.

'' Tunazidi kuboresha ili kwamba Mtanzania popote alipo aweze kupata habari hizi , na tumeanzisha mfuko ili kuhakikisha minara sasa inakwenda mpaka vijijini  kwani miundombinu mingi ya mitandao iko mijini''Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Odokorach Francis amesema kuwa Shirika la Oxfam kupitia mradi wa chukuaHatua limefanikiwa kuwamilikisha Ardhi wanawake 300 katika halmashauri za Mbogwe,Shinyanga vijijini,Kishapu na Hanang. Francis amesema Oxfam pia imefanikiwa kuwafikia wanawake wanaoishi maisha duni katika kambi za wakimbizi za kigoma kwa kuwafikishia huduma za maji na huduma zingine muhimu za kijamii

Shirika la Oxfam limejitosa kuwawezesha watetezi wa haki za binadamu katika matumizi ya teknolojia ya digitali ili kupata majibu ya haraka ya changamoto za kijamii na haki za binadamu kutoka kwa viongozi wa serikali

Aidha Oxfam walitoa mafunzo ya matumizi ya teknolojia ya digitali kupitia mitandao ya kijamii kama Twitter, Facebook na Whatsapp kwa watetezi mbalimbali wa mikoa ya Mtwara, Kigoma , Arusha na Geita ambao wanaitwa (WARAGHBISHI) ili waweze kuleta maendeleo katika jamii zao

'' Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)inashiriki kama mdau muhimu sana katika eneo hili la matumizi ya mitandao ili kutetea haki za binadamu''Alisema

Mkutano huo uliofanyika Dodoma - African Dreams Hotel ambapo watatoa taarifa za mafanikio na changamoto katika matumizi ya  teknolojia ya mtandao katika kuleta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za kijamii. Mkutano huo wa  siku mbili  Dijitali kwa maendeleo imejumuisha wadau zaidi ya 150 kutoka mikoa mbali mbali nchini kwa lengo la kujifunza mafanikio ya Dijitali katika kuleta maendeleo.
 Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwele akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa waraghabishi uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Oxfam nchini Tanzania Odokorach Francis akizungumza na waraghabishi zaidi ya 150 waliohudhuria katika mkutano huo leo Jijini Dodoma
 Baadhi ya Waraghabishi kutoka katika mikoa mbalimbali wakiwa katika mkutano katika ukumbi wa African Dream's Jijini Dodoma
 Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia akiwa anachangia mjadala katika mkutano leo Dodoma
 Mbunge wa Mbogwe Geita Augustino Masele akichangia mada katika mkutano wa Digitalikwa maendeleo leo Jijini Dodoma
 Mbunge wa Hanang'Mary Nagu akifuatia taarifa kupitia simu yake ya kiganjani. (Picha/ habari na Vero Ignatus ) 

WAZIRI MKUU AFUNGA SOKO LA NDUTA

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amefunga soko la wakimbizi na wananchi lililoanzishwa nje ya kambi ya Nduta iliyopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma. Hatua hiyo imekuja baada ya soko hilo kubainika kuwa  chanzo cha  wakimbizi kutoka nje ya kambi kiholela na kushiriki katika kufanya matukio ya kiharifu.

Waziri Mkuu ametangaza uamuzi huo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa umma katika ya Halmashauri ya Kibondo. ”Vitendo vya uhalifu wilayani Kibondo vikiwemo vya utekaji wa watoto vimeongezeka na kusababisha hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.”

Waziri Mkuu amesema ni vema halmashauri hiyo ikaandaa utaratibu wa kutoa vibali vitakavyowaruhusu Watanzania kupeleka bidhaa ndani ya kambi hivyo. Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wananchi waliopewa dhamana ya kufanya kazi kwenye kambi za wakimbizi wawe waadilifu na wasimamie sheria.

“Nafahamu tunao watendaji wetu ambao wapo kambini kusimamia shughuli mbalimbali za wakimbizi,  tekelezeni wajibu wenu ipasavyo na si vinginevyo.” Baada ya kuzungumza na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Kibondo, Waziri Mkuu alikwenda wilayani Kakonko na kukagua mradi wa maji Muhange. Pia Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Kakonko unaotarajiwa kugharimu sh. bilioni 4.5. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Maji wa  Muhange wilayani Kakonko kukagua mradi huo, Februari 19, 2019. Kulia ni mkewe Mary na kushoto ni Mbunge wa Buyungu, Mhandishi Christopher Chiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha  Muhange wilayani Kakonko wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokagua Mradi wa Maji kijijini hapo, Februari 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kakagua Mradi wa Maji wa Muhange wilayani Kakonko, Februari 19, 2019.  Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga, Mbunge wa Buyungu Mhandisi Christopher Chiza, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Diwani wa Kata ya Muhange wilayani Kakonko, Ibrahim Katunzi jumla ya shilingi milioni moja kwa ajili ya Mradi wa Maji na Zahanati katika Kata hiyo, Februari  19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibaga wilaya ya Mkalama ambao waliusimamisha msafara wake kwa lengo la kumsalimu ,Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kikazi mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso akijibu hoja za wananchi wa Ibaga (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassanakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi(wa pili kulia) wakati wa ukaguzi wa daraja la Sibiti  ambalo limekamilika kwa asilimia 94.8%.
 Muonekano wa daraja la Sibiti ambalo kwa mujibu wa taarifa za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) walizozitoa wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassa ambapo wamesema ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 94.8%. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa daraja la Sibiti kutoka kwa Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Singida Mhandisi Matari J. Masige (kushoto) ambalo limekamilika kwa asilimia 94.8%,kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu akimsalimia Lailat Ramadhani mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Iguguno wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images