Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Wamiliki wa radio wasiwabinye wanahabari ili sote tunufaike na matangazo ya radio- Msikilizaji

$
0
0
Miongoni mwa wananchi hao ni George Miyango mkazi wa Buyekera mjini Bukoba ambaye katika mazungumzo na Nicolas Ngaiza wa Radio washirika Kasibante FM anaanza kwa kuelezea ufahamu wake kuhusu radio.

“Mimi ninavyofahamu redio ni kitovu cha mawasiliano makubwa na kuweza kupeleka habari kwa muda mfupi tofauti na ule upelekaji wa habari uliokuwepo, taarifa moja inaweza kuwafikia watu maelfu na maelfu kwa muda mfupi kuliko iliyokuwa inapeleka habari kwa farasi, kwa magari au kwa njia ya kupeleka vifurushi.”

Alipoulizwa kuwa radio inamsaidia vipi, Bwana Miyango amesema, “inanisaidia kupata habari za kijamii, kiuchumi na habari hata za vifo na vitu vingine ambavyo ninaweza kuwa sivielewi. Ninasikiliza redio hata nikiwa kwenye shughuli zangu na ninakuwa na redio.”

Hata hivyo amesema kuna changamoto kwenye kupata maudhui sahihi kwenye redio kwa sababu baadhi ya redio zina muegemeo mmoja au wa upande fulani kutokana na msimamo wa mmiliki wa radio.

Kwa mantiki hiyo amesema ni vyema wamiliki wa vyombo vya habari wasiegemee upande wowote na mamlaka zihakikishwe waandishi wa habari wako huru.

Amesihi watu wasio na hulka ya kusikiliza redio wabadili mitazamo yao na kuanza kusikiliza redio kwa sababu “maarifa yanatafutwa, unaposoma ukisaidiana na magazeti na redio ndipo unakuwa kama unanoa maarifa yako na unaweza kuwa mwanajamii bora na mwenye maarifa.”

HABARI KWA HISANI YA https://news.un.org/sw/

Kampuni ya Mafuta ya TOTAL, yapunguza Bei ya Mafuta ya TOTAL EXCELLIUM, kama Zawadi ya Valentine.

$
0
0
Kampuni ya Mafuta ya TOTAL, imepunguza bei ya mafuta ya  TOTAL EXCELLIUM  kwa kutoa punguzo la TZS 70 kwa kila lita ya mafuta, muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 13/02/2019 mpaka 15/02/2019 katika baadhi ya vituo vya TOTAL vilivyopo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro
Taarifa hiyo imetolewa na Network Operations Manager wa vituo vya TOTAL, William Fillet, amesema uamuzi huo wa kupunguza bei ya mafuta ya TOTAL EXCELLIUM katika baadhi ya vituo vya TOTAL ni ili kuwapatia zawadi ya sikukuu ya wapendanao ya Valentine wateja wao, kwa kuonyesha ishara ya upendo na kuwawezesha kusherehekea sikukuu ya Valentine kwa Upendo.
Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa TOTAL, Marsha Msuya Kileo, amesema sambamba na punguzo hilo la bei kwenye mafuta, pia wateja wote wa watakaonunua chochote kwenye maduka ya Café Bonjour, yaliyoko kwenye vituo Total vilivyochaguliwa, watapatiwa zawadi ya maua ya Valentine kuonyesha upendo.
Marsha amesema, punguzo hilo, lenye kauli mbiu ya “Fill Up With Love”, yaani jaza mafuta kwa mapenzi. Marsha amewakumbusha watanzania, kuwa ukijaza mafuta kwenye kituo cha TOTAL, haujazi mafuta tuu, bali unajaza mafuta ya TOTAL EXCELLIUM yenye viambata vya kuifanya gari yako itumie mafuta kidogo na kwenda umbali mrefu, huku mafuta hayo yakiboresha injini ya gari yako.
Jumla ya vituo  vya TOTAL 16 vimeteuliwa kuendesha zoezi hilo, katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Moshi, Mwanza Mbeya na Morogoro.

TAARIFA RASMI MSIBA WA MSANII GODZILLA (Golden Jacob Mbunda)

$
0
0
KIFO: (Kutoka kwa Familia)

Godzilla aliugua ghafla majuzi kwa kulalamika anaumwa tumbo na kutapika. Alienda kwenye Zahanati ya jirani na kwao, akagundulika ana Malaria. Wakati ameanza matibabu aliendelea kutapika, na kutokula vizuri, hii ikachangia Sukari kupanda na BP kushuka. Mnamo juzi usiku hali ilibadilika ghafla na wanafamilia wakamkimbiza hospitali ya Lugalo, ambapo ndio alifariki.

MSIBA:
Msiba upo nyumbani kwao na marehemu, Salasala, karibu na Shule ya Sekondari ya Green Acres. Sio mbali kutoka kituo cha Mbezi Africana. 

UTARATIBU WA MAZISHI:
Wanasubiriwa Ndugu kutoka Mwanza (Kaka wa Marehemu) na ndugu wengine kutoka Songea, na pia kukamilisha Mipango ya kuendesha msiba.Matarajio ni kwa Mazishi kufanyika Siku ya Jumamosi katika Makaburi ya Kinondoni, Dar Es Salaam. Utaratibu wa kuaga Mwili na Misa utatolewa muda muafaka ukiwadia baada ya taratibu husika kutimia. 

RAMBI RAMBI:
Michango yote ya Wasanii kutoka kwenye ma-group ya Wasanii inapokelewa na @soggydoggyanter 0754772220 (Anselm Ngaiza), ambayo inajumuisha Hip Hop Community, Umoja Wa Wasanii, Tanzania Urban Music Association (TUMA), nk. 
Marafiki wa Zillah katika Social Media (Twitter, Instagram, Facebook) wanaweza kutuma mchango kwa namba hizi 

TIGOPESA
0659421111 Mansour Rashid @papichulo_chuly 
0717367673 Webiro Wasira @wakazimusic 

MPESA
0745368485 Webiro Wasira 
0769991190 Prince Kessy @esilovey1 

Ila kama kuna mtu anataka kutuma mchango peke yake, basi anaruhusiwa kufanya hivyo kupitia Namba ya Mama Mzazi Wa Marehemu. MARY CHARLES MBUNDA 0652810084 .

KING ZILLAH ALIISHI KAMA MFALME... HEBU TUMPE HESHIMA YA MWISHO NA KUMLAZA KWENYE NYUMBA YAKE YA MILELE KAMA MFALME PIA "Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe"

TAARIFA YA KUMBU KUMBU

Benjamin Mkapa Hospitali na Tiba ya Moyo ya Kisasa

WATAALAM KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WASHIRIKI KIPINDI UPLANDS FM

R.i.P Godzilla by R. Name

Bodi inueni Stamico kwenda kibiashara zaidi-Waziri Biteko

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Madini Dotto Biteko ameiagiza Bodi ya Shirika la Taifa la Madini (Stamico) kuhakikisha inafanya kazi ya kuliinua Shirika kuwa la kibiashara.
Biteko aliyasema hayo wakati akizindua Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam amesema Shirika limekuwa likijiendesha kwa hasara huku serikali ikifanya uwekezaji na kushindwa kutoa gawio.

Amesema Stamico ihakikishe inaongeza mchango kwenye Pato la Taifa kwa kulipia mrahaba na kodi mbalimbali za serikali pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania kupitia uwekezaji katika sekta ya Madini. Biteko amesema kuwa wakurugenzi waliopo wana kaimu kwa muda mrefu ambapo kukaimu kwao huko kunatokana na Shirika kushindwa kuzalisha na wasipoleta matokeo wataendelea kukaimu.

Aidha ameitaka bodi kushughulikia hisa  za kampuni ya Tanzania Industries Ltd (TGI) ambapo Stamico ina umiliki lakini ilikuwa haifuatiliwi tangu ilivyosajiliwa mwaka 1969. Amesema kuwa GTI ni Kampuni Tanzu ya ilisajiliwa na Stamico mwaka 1969 kwa kujishughulisha na uchimbaji wa Madini ya Vito na ilikuwa inamiliki Kampuni ya Mundarara Ruby Mining Limited kwa ubia wa asilimia 50 kwa 50 na kampuni ya Tan Ruby na Germstone.

Biteko amesema Mundarara inamiliki kitalu cha madini ya Ruby wilayani Longido ilijiendesha kwa hasara mpaka kufikia kufilisiwa na benki ya TIB kwa uangalizi wa PCRC lakini TGI bado iko chini ya Stamico
Nae Mwenyekiti wa Bodi wa Stamico Meja Jenerali Mstaafu Michael Isanhyo amesema kuwa watahakikisha wanasimamia mikataba yote watayoingia kwa umakini. Amesema kuwa watahakikisha Shirika linatoa gawio kwa serikali kufikia Juni mwaka huu.

Isanhyo amesema Shirika hilo watakuwa wabunifu katika kuhakikisha linafanya vizuri kwa Maendeleo ya Taifa na kuonyesha imani kwa aliyemteua pamoja na wajumbe walioteuliwa.
 Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Taifa la Madini(Stamico) kabla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Madini Stanislaus Nyongo akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Stamico jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Menejimeti ya Stamico katika uzinduzi wa Bodi ya Stamico.



WATAALAM KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WASHIRIKI KIPINDI UPLANDS FM

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini, afanya IARA YA PAMOJA YA NAIBU WAZIRI WA FEDHA MPAKANI HOROHORO

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia Mhe. Balozi Theresia Samaria.  Mazungumzo hayo  ambayo yalijikita kwenye masuala ya kuimarsha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili,  yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 13 Februari 2019.
Mazungumzo yakiendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa pamoja wamefanya ziara kwenye kijiji cha Jasini na Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja Mpakani cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga. Pamoja na Mambo mengine Naibu Mawaziri hao waliweza kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo ukusanyaji wa mapato kituoni hapo, pamoja na kuzungumza na wanakijiji cha Jasini na Watendaji wa Kituo hicho.   
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza  wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza  Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani 

Dkt. Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni cha kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, kabla ya kuanza ziara kwenye kijiji hicho

Naibu Mawaziri pamoja na wadau mbalimbali wakiwa wamesimama kwenye moja ya jiwe ambalo linaonyesha Mpaka wa Tanzania na Kenya.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt.  Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya.  Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro
Mhe. Dkt. Kijaji akitizama kitambulisho cha mjasiriamali mdogo huku Dkt. Ndumbaro akishuhudia tukio hilo. Mjasiriamali huyo aliwavuti Naibu Mawaziri hao kwa mwitikio wake chanya katika kuhakikisha kila mjasiriamali nchini anapata kitambulisho cha kufanyia biashara
Mmoja wa wanakijiji akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kijijini hapo ikiwamo upatikanaji wa elimu kwa watoto wao ambao wanalazimika kwenda kusoma Kenya na jioni kurejea Tanzania.
Wanakijiji wakiwasikiliza kwa makini Naibu Mawaziri hawapo pichani

Naibu Mawaziri hao wakizungumza na baadhi ya wananchi wa Jasini mara baada ya kumaliza ziara kijijini hapo
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula  wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani.

WAZIRI KAIRUKI: SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI NA ENDELEVU KATIKA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Serikali imedhamiria kuendelea kujenga mazingira wezeshi na endelevu katika Sekta ya Kilimo kupitia sera imara na zenye kutekelezeka.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakati akifungua Kongamano la Tano la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Sera Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 13Februari, 2019.

Waziri alieleza kuwa, dhamira ya Serikali inaenda sambamba na mchango wa sekta ya Kilimo katika uzalishaji pamoja na ukuaji wa uchumi nchini kwa kuzingatia namna sekta hiyo inavyochangia katika maeneo mengi ikiwemo,utoaji wa ajira kwa wananchi waliowengi.

“Ni mambo ambayo yanajieleza yenyewe na kila mmoja wetu anayajua vizuri.  Asilimia 65.5 ya Watanzania wanategemea ajira na maisha yao kwenye kilimo, pia kinachangia asilimia 95 ya mahitaji ya chakula nchini na asilimia 65 ya mali ghafi ya viwanda vyetu,”alisema Kairuki

Aidha aliongezea kuwa, asilimia 30 ya fedha za kigeni hutokana na mauzo ya nje ya mazao na bidhaa za kilimo na huchangia asilimia 25 kwenye pato la Taifa. Sambamba na hilo waziri alieleza kuwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano tangu imeingia madarakani imeendelea kutambua umuhimu wa kilimo katika kuongeza tija maeneo ya uzalishaji na mna haja ya kuleta msukumo zaidi katika kukiendeleza.

Pamoja na jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta hiyo, Waziri alibainisha baadhi ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo ikiwemo na sehemu kubwa ya kilimo kutegemea jembe la mkono, matumizi madogo ya mbegu bora zinazotoa mazao mengi na kuhimili maradhi na athari za kimazingira, matumizi ya maji ni kidogo mno pamoja na kilimo kutegemea mvua  bila kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji chenye uhakika.

“Tunategemea mno mvua ya Mwenyezi Mungu hatujatumia vya kutosha maji aliyotuwekea juu ya ardhi na chini ya ardhi kwa kilimo katika hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo nchini hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha kumwagilia lakini ni asilimia 1 tu ya ardhi hiyo inamwagiliwa. Tumejipa lengo la kuongeza kilimo kinachomwagiliwa nchini,”alisisitiza Kairuki

Kairuki alihamasha wakulima kuendelea kutumia mbolea kutokana na Tanzania kutumia wastani wa kilo19 kwa hekta kiwango ambacho ni kidogo kulinganisha kiwango cha takribani kilo 50 kwa hekta kinachotumiwa na Jumuiya na Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kwa upande wake Naibu Waziri Kilimo, Mhe.Omari Mgumba alieleza jitihada za serikali kuendelea kuhakiki madai ya madeni yenye ukakasi ya Wakala wa pembejeo wanaosambaza mbegu na mbolea wanaoidai serikali kiasi cha shilingi bilioni 35.

“kama mnavyofahamu mwaka ukipita wa fedha madeni yanahamia Wizara ya Fedha kwa hatua zingine ikiwemo kuyachunguza na kujiridhisha ambapo hadi sasa yamebainika kuwa na ukakasi katika takwimu na tofauti ya taarifa na Serikali inaendelea kufuatilia hujuma zilizofanyika ili kujiridhisha,”alisisitiza Mgumba.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Chuo cha Kilimo cha Sokoine ,Jackline Mkindi alipongeza uwepo wa kongamano hilo ambalo litatoa fursa za kujadili na kueleza changamoto wanazokumbana nazo hususani upande wa usambazaji wa Pembejeo  nchini na madeni yaliyopo ambayo hadi sasa ni sh.bilioni 39.9 ambazo zinapaswa kulipwa na serikali.

“Tunaimba Serikali ishushe bei na kuendelea kulipa madai sahihi kwa wanao stahili pamoja na kutataua changamoto za wakulima kutofikia gharama za pembejeo na kuwasaidia kujikamua katika uzalishaji kwa kuwa na pembejeo bora na kwa wakati,”alisema Mkindi.

Kongamano limeandaliwa na Jukwaa la Uchambuzi wa Sera za kilimo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta binafsi na za umma ili kuleta mageuzi katika sekta ya Kilimo na kuchangia katika ukuaji wa Viwanda na kuhudhuriwa na takribani zaidi ya washiriki 300 nchini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akihutubia washiriki wa Kongamano la Tano al Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina Dodoma Februari 13, 2019 kwa lengo la Kuchambua na Kujadili sera ili kuboresha maeneo ya kisera ya kilimo lililoratibiwa na Jukwaa la Watafiti na Wachambuzi wa Sera za kilimo kwa kushirikisha wadau mbalimbali nchini.
 Naibu Waziri Kilimo Mhe.Omari Mgumba akiwasilisha hotuba yake wakati wa kongamano hilo.
 Sehemu ya wajumbe walioshiriki kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki linaloendelea Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia tarehe 13 hadi 15 Februari, 2019.
 Sehemu ya wajumbe walioshiriki kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) linaloendelea Jijini Dodoma.
 Mratibu wa Jukwaa la Uchambuzi wa Sera za Kilimo Prof.David Nyange akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo.
 Mwenyekiri TPSF Bw.Salum Shamte akieleza masuala yanayohusu sekta Binafsi wakati wa Kongamano hilo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Joseph Kiraiya akizungumza jambo kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi hiyo anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi.Dorothy Mwaluko wakati wa Kongamano hilo.
Mwenyekiti Mwenza wa Timu ya Wadau Bi.Michellle Cornize akichangia jambo wakati wa Kongamano hilo.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus – Misenyi, Kagera. 

Kufuatia Uzinduzi wa Kampeni ya Lishe na Usindikaji kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mbali mbali Wilayani Misenyi, imegundulika kuwa sababu nyingine inayopelekea uwepo wa lishe duni kwa baadhi ya kaya Wilayani humo, ni kutokana na ukosefu wa maeneo ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kilimo na uzalishaji. 

Kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi mapema Februari 11 Mwaka huu na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kupitia mradi wa urejeshaji hali kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mkoani Kagera, unaotekelezwa chini ya Shirika la Chakula Duniani “FAO” Wilaya ya Misenyi ikiwa ni miongoni mwa Wilaya tano zenye wahanga, Imebainika kuwa ukiacha sababu za Tetemeko, Mvua, Magonjwa ya mimea na mazao, pia sababu nyingine ni ukosefu wa sehemu ya kutosha kufanya shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uzalishaji kwa baadhi ya maeneo lengwa. 

Kijiji Nkerenge kilichopo Kata Mtukula Wilayani Misenyi ni miongoni mwa Vijiji vilivyolengwa kufikiwa na mradi huo, licha ya kubainika kuwa Kaya 68 kati ya 720 Zinazopatikana Eneo la Mkagando, hazina sehemu ya kutosha kufanya shughuli za kilimo kufuatia changamoto kubwa ya Uwepo wa Kitalu namba 19, kinachomilikiwa na NARCO. 

 Bwana Martin Adam (58) Mkazi wa Kijiji Nkerenge eneo la Mkagando, ni mhanga wa mgogoro huo wa Ardhi kati ya NARCO na wananchi hao ambae anasema kuwa awali kabla ya kitalu hicho walikuwa na mashamba ya kutosha kuweza kulima mazao mbalimbali, tofauti na sasa baada ya kuhamishwa maeneo yao na kupewa heka mbili mbili kwa kila kaya, hivyo mazao mengine ambayo walizoea kulima kama mazao ya mbogamboga, kwa sasa yamepotea kulingana na ardhi kuwa finyu. Hivyo Bwn Martin anapeleka kilio chake kwa Serikali kuwatenegea maeneo ya kutosha ili kuweza kuzinusuru kaya hizi nazo ziweze kukabiliana na Utapiamlo na magonjwa yanayoweza kuvikabili vizazi vyao kufuatia ukosefu wa lishe bora. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Kaimu Mratibu wa mradi huo Ndg, Amoni Lugeiyamu, anasema kuwa Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji wamelenga kuvifikia Vijiji vinne Wilayani humo ambavyo ni Nyankere, Nkerenge, Minziro na Kikono, huku ikiwa tayari mafunzo hayo yamekwishawafikia wanavikundi wa Vijiji vitatu vya Nkerenge, Nyankere na Minziro na yatahitimishwa katika kijiji cha kikono Kata Buyango Wilayani Misenyi. 

Vijiji hivi kupitia mradi wa urejeshaji hali unaofadhiliwa na FAO tayari vimegawiwa Mbegu (vipando), kuku na vifaranga vya Samaki, maharage yenye virutubisho aina ya Jesca, na sasa Kampeni hii inalenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kusindika mazao yanayopatikana kupitia mavuno ya Vpando na Mbegu walizogawiwa awali. 

Kutokana na mazao hayo tayari Vikundi vimejengewa uwezo wa kutengeneza vyakula mbalimbali kwa ajili ya lishe bora, ikiwemo uji wa lishe, keki, andazi, supu ya maharage, uji wa unga wa maharage, pilau la maharage, pilau la viazi lishe na maharage n.k
 Pichani ni chungu cha pilau ya Viazi Lishe na Maharage kikiendelea kupikwa baada ya somo katika Kampeni ya Lishe na Usindikaji Mutukula.
Ndugu Amoni Lugeiyamu akitoa ufafanuzi kwa Vikundi vya Wakulima na wafugaji kuhusu Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji, katika Kijiji cha Minziro Wilayani Misenyi
Martin Adamu Mkazi wa Mkagando Kijiji Nkerenge ni mmoja kati ya kaya 68 zilizoathiriwa na Kitalu namba 19, na kusababisha ukosefu wa Lishe Bora kwenye familia yake, kufuatia ufinyu wa ardhi kwa shughuli za Kilimo
Fredrick Kitone Mkulima na Msindikaji wa Vyakula akiendelea na somo la Mapishi ya keki itokanayo na Viazi Lishe, Wakati wa mafunzo ya Lishe na Usindikaji Mutukula Misenyi
 Pichani ni Bi Frola Paul Mkazi wa Minziro akimywesha uji mwanae Mara baada ya kupata mafunzo ya upikaji Lishe ya Uji wa Maharage ya Jesca.

BENKI KUU SASA YAZINDUA MFUMO WA MALIPO YA PAPO KWA PAPO

$
0
0
  Naibu Gavana wa BoT Dk.Benard Kibese akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa  Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania Instant Payment System (TIPS) katika ukumbimwa mikutano wa benki hiyo jana.
  Benald Jeremia Dadi Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa Ndani ya Benki Kuu wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa  Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania Instant Payment System (TIPS)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela akitoa ujumbe wake kutoka muungano wa mabenki Tanzania TBA katika uzinduzi huo.
 Sosthenes Kewe Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania naye akitoa neno katika uzinduzi huo. Sosthenes Kewe Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania naye akitoa neno katika uzinduzi huo.





Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu (BoT) imezindua Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania(TIPS) wenye lengo la kurahisha kufanya malipo mbalimbali ya miamala ya fedha kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa uhakika na salama zaidi.

Uzinduzi huo umefanyika Benki Kuu ya Tanzania(BoT) jijini Dar es Salaam ambapo  viongozi wa ngazi mbalimbali kutoka taasisi za fedha na serikalini wamehudhuria huku Naibu Gavana wa BoT Dk.Benard Kibese akitumia uzinduzi huo kufafanua umuhimu wa mfumo huo kwa kina.

Akizungumza zaidi wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo wa Taifa ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Dadi amesema Mfumo wa Malipo ya Papo kwa Papo Tanzania(Tanzania Instant Payment System) utamuwezesha utumaji wa fedha toka taasisi moja kwenda nyingine kufanya malipo bila kutumia fedha za kampuni nyingine.

"Kwa hiyo tutakuwa mfumo pale BOT ambao sasa mteja wa kampuni moja kwa mfano Vodacom anaweza kutuma fedha kwenda kwenye benki yoyote ile bila gharama. Kwa mfumo huu tutakuwa na majina sehemu moja kwa hiyo ukituma fedha ule muamala ambao umetumwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi wa jipa kwani kupitia mfumo huu utachukua jina kamili na kutuma kwa mteja tena kwa usalama kwani jina na fedha zitakuwa zimehakikiwa.

"Mfumo huu tunatarajia utajengwa ndani ya miezi 18 kupitia watalaamu wetu wa ndani ya BoT pamoja na wataalam wa taasisi nyingine za fedha na baada ya hapo sasa tutakwenda ndani zaidi kwa kuhakikisha tunamhudumia mteja wa kijijini kwa haraka na uhakika zaidi.Hivyo kupitia mfumo huu tunaamini sasa huduma za kufanya malipo ya fedha uko salama zaidi,"amesema.

Amefafanua sababu za kuiita mfumo huo ni Instant maana yake ni kwamba ndani ya sekunde moja hadi mbili fedha itakuwa imemfikia mteja tena ikiwa kamili bila kukosewa wakati kabla ya mfumo huo wapo ambao wamekuwa wakilalamika fedha kwenda kwa watu ambao si walengwa kutokana na kukosewa kwa jina au namba iliyokusudiwa.

Dadi ameongeza kuwa mfumo huo wanaamini utaleta ufanisi zaidi katika utumaji wa fedha, pia utaleta udhibiti na kwamba badala ya kwenda kuomba taarifa kwenye kampuni sasa hizo taarifa zitapatikana BoT."Kwa kutumia mfumo huu BoT tutakuwa tunajua miamala ambayo inafanyika kwa kila mwezi,hivyo hata Serikali itapata kodi stahiki kutokana na huduma hizo za malipo ya fedha."

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza  Sekta ya Fedha Tanzania Sosthenes Kewe  amesema mfumo huo ambao maandalizi yake umezinduliwa leo unathamani kubwa kwa maisha ya watu kwani utakapoanza kufanya kazi utapunguza gharama za utumaji wa fedha na kutoa taarifa mbalimbali za wanaotumia huduma za fedha kwa kufanya miamala mbalimbali

Amesema inafahamika katika maisha ya mtu ya kila siku watu wanafanya miamala mingi sana na kwa kutumia fedha tasilimu ambapo gharama yake inakuwa kubwa lakini kupitia mfumo huo sasa utarahisisha muda na gharama."Kwa sasa mtu akitaka kufanya malipo atalazimika kwenda benki ambapo ili afanye kwa haraka atachukua na bodaboda ambayo nayo ni gharama lakini mfumo huu malipo yatafanyika kwa urahisi na haraka bila kusababisha gharama yoyote."

Pia amesema mfumo huo utasaidia wakulima kulipa au kupokea fedha kirahisi, wafanyabiashara wataweza nao kufanya malipo ya miamala mbalimbali na kubwa zaidi utasaidia kupunguza adha kwa watu mbalimbali katika kufanya miamala na kwamba hata Serikali itakuwa na urahisi wa kulipa fedha katika taasisi mbalimbali.

"Tuone kwamba hii ni bahati ya pekee kwa watanzania kuwa na mfumo kama huo na tunawaomba wadau wote washiriki kikamilifu katika kuandaa mfumo huo ambao una tija kubwa kwa Watanzania wote nchini,"amesisitiza.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB ambaye pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Mabenki Tanzania Abdulmajid Nsekela amesema mfumo huo ni ubunifu ambao umesubiriwa kwa muda mrefu, hivyo kuzinduliwa kwake utasaidia benki zote nchini kutoa huduma mbalimbali za fedha kwa haraka na wakati.

"Pia mfumo huu utasadia benki nyingi kujitawanya maeneo mengi ya nchi yetu kwa gharama nafuu kwani kujenga tawi moja gharama yake ni kubwa lakini sasa kupitia mfumo huu benki zitaendelea kutoa huduma kwa wateja wao kwa urahisi zaidi.Lakini kikubwa zaidi utapunguza matumizi ya fedha tasilimu ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa wananchi wengi, hivi sasa ukitaka kufanya malipo mbalimbali utatumia mfumo huu na hivyo utaondoa usumbufu.Tunawapongeza Benki Kuu kutokana na kuja na mfumo huu ambao pia unafanya taarifa nyingi zinakuwa sehemu moja.

"Kwa sasa ukienda mtaani utakutana na mawakala wengi na mmoja anahudumia karibu kampuni tano za mitandao ya simu anapotaka kufanya muamala kwa ajili ya mteja wake.Sasa mfumo huu wakala hana sababu ya kusumbuka kwa kuwa na kampuni nyingi kwani mfumo utamuwezesha kutumia sehemu moja kufanya aina yoyote ya miamala.CRDB tunapongeza ubunifu wa aina hii wenye lengo la kuboresha sekta ya huduma za fedha,"amesisitiza.

TANZANIA AND KAZAKHSTAN ESTABLISH DIPLOMATIC RELATIONS

$
0
0
The Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, H.E Ambassador Modest J. Mero (R) and Permanent Representative of Republic of Kazakhstan to the United Nations, H.E Ambassador Kairat Umarov signing a communique to establish diplomatic relations between their Nations. The signing ceremonies took place in New York on 13th February 2019. 
Ambassador Mero exchanges the signed communique with his counterpart, Ambassador Umarov. 
Ambassador Mero and Ambassador Umarov posing for a photo after signing a communique to establish diplomatic relations between the two countries. 


MAMA SAMIA ASEMA WASANII NI MUHIMU KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NCHINI

$
0
0

*Asema wamebeba kundi kubwa katika jamii ambalo linawasikiliza, linawahusudu
*Awaomba waibadilishe jamii ili iachane na dawa za kulevya, atoa neno kwa jamii 


Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MAKAMU wa Raia Samia Suluhu Hassan amesema wasanii ni muhimu sana katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini kwani nyuma yao wamebeba kundi kubwa katika jamii ambalo liwasikiliza , linawafuatilia, linawahusudu na linawaamini, hivyo wanaouwezo wa kubadilisha jamii kuachana na dawa za kulevya ambazo madhara yake ni makubwa kwa Taifa.

Hata hivyo imeelezwa kwa sasa Serikali imefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa uingiaji wa dawa za kulevya na takwimu zinaonesha wamedhibiti kwa asilimia 90 , hivyo imebakia asilimia 10 ambapo imewaomba watanzania kushiriki katika kukomesha dawa za kulenya nchini.


Akizungumza na wasanii kwenye kongamano la wasanii kujadili athari za dawa za kulevya lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam Mama 

Samia amesema tatizo la matumizi haramu ya dawa za kulevya duniani ni kubwa na linazidi kuongezeka siku hadi siku. Idadi ya watumiaji na waathirika wa dawa za kulevya inazidi kuongezeka 
hapa nchini na wasanii ni moja kati ya makundi ambayo yameathirika zaidi na janga hilo.

"Hivi sasa watumiaji wanapatikana maeneo yote si mjini tu bali hata vijijini na la kusikitisha zaidi matumizi hayo sasa yameanza kujitokeza miongoni mwa wasanii wengi nchini.Jambo la kuumiza zaidi hata baadhi ya watoto wanaonekana kutumia dawa za kulevya .Watoto wetu wako katika hatari kubwa ya kutumbukia kwenye janga hili , hii ni kutokana na ukweli hawana uwezo wa kujilinda na hawajui namna ya kukabiliana na janga hili.Mara nyingi wamekuwa wakirubuniwa na kujikuta wametumbukia kwenye lindi la matumizi ya dawa hizo hatari,"amesema Mama Samia.

Ameongeza matumizi ya dawa za kulevya yana madhara mengi kiuchumi, kisiasa, mazingira ,kiafya na kijamii na kusisitiza pia hudhoofisha afya za watumiaji na kuathiri uwezo wao wa kufanya kazi na kwa upande wa afya husababisha magonjwa yakiwemo ya akili, homa ya ini , kifua kikuu , moyo na kuenea kwa kifua kikuu sugu.

"Nimefurahishwa kuwa kongamano hili linalenga katika kuangalia na kujadili namna ya kukabiliana na kutatua kwa pamoja tatizo la dawa za kulevya nchini hasa katika kundi la wasanii na katika jamii kwa ujumla.Tunafahamu dawa za kulevya vilevile zimechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili,hivyo ni matarajio yangu mtaangalia kwa kina tatizo la mmomonyo huo kwa wasanii na jamii kwa ujumla kutokana na matumizi ya dawa za kulevya,"amesema.

Wakati huo huo Mama Samia amesema amefurahishwa na taarifa za kukamatwa kwa dawa mbalimbali na kusababisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watuhumiwa 4,602.Ameviomba vyombo vya sheria kuhakikisha wote wanaopatikana na hatia wanapewa adhabu kali ili fundisho kwa wengine.

Ameishauri Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya pamoja na kuanzisha vituo sita vya huduma ya methadone ambapo kwa ujumla waathirika 6300 wametibiwa lakini kuna waraibu wengi zaidi ambao hawajafikiwa, hivyo bajeti yao ikiruhusu vituo vijengwe nchi nzima kwa kuanza na maeneo yenye waaathirika wengi.

"Ila ni vema mkawekeza kwenye kutoa elimu zaidi kuhusu madhara ya dawa za kulevya kwa vijana na jamii kwa ujumla kuliko kujenga vituo kwa kuwa waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba.Kuhusu utoaji wa elimu kwa jamii na hasa vijana niwaombe muwatumie wasanii.Pia wanangu wasanii ninyi muwe mfano bora kwa jamii kwa kuhakikisha mbali na maisha ya sanaa , maisha yenu halisi yaendane na majukumu yenu ya kuwa kioo chetu,"amesema.



Kuhusu changamoto ya matumizi mabaya ya dawa za hospitali zenye asili ya kulevya amepata taarifa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeshapeleka taarifa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) na Pharma Council ili waje na muongozo wa namna ya kudhibiti dawa 


hizo kuanzia inavyoingizwa nchini mpaka kwa mtumiaji wa mwisho.

Pia amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuzidisha misako kwenye maeneo yote hasa mipakani na bandari bubu na kwamba hawalifu wa dawa za kulevya wanambinu nyingi , hivyo ni vema maofisa wa uhamiaji wakajengewa uwezo ili kuhakikisha mipaka ya nchi inakuwa salama.

Kwa upande wake Kamishna wa Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi pamoja na kueleza kwa kina athari za matumizi ya dawa hizo amesema mamlaka chini ya uongozi wa Kamishina General Roger Sianga wamefanikiwa kudhibiti uingizwaji wa dawa kwa asilimia 90.

"Tunapambana na asilimia 10 ambayo imebakia na tayari tumeweka mikakati ya kukabiliana na wafayabishara wa dawa za kulevya , wanatumia njia ya Kusini kwa maana dawa chache ambazo zinaingizwa nchini zinatoke katika nchi ya Msumbiji.Kwetu tutaendelea na mapambano na sehemu 
kubwa ya wafanyabiashara hiyo wako magerezani na wengine wamekimbia nchini na wale wachache waliopo tunaendelea kuwasaka na kuwabaini,"amesema Dk.Mfisi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wasanii wa fani mbali mbali waliohudhuria  Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam

MICHAEL WAMBURA AENDELEA KUSOTA RUMANDE, MAHAKAMA YAMWAMBIA HAINA UWEZO WA KUMFUTIA KESI, KUMPA DHAMANA

$
0
0

Na Karama Kenyunko globu ya Jamii.
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura (52), kuaendelea kusota rumande baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kueleza kwamba haina mamlaka ya kumfutia kesi wala kumpa dhamana katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili.

Hatua hiyo imefikiwa leo Februari 14.2019 baada Mahakama kupitia Hakimu Mkazi, Mwandamizi Kelvin Mhina kutupilia mbali mapingamizi yaliyowasilisha na upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Majura Magafu akisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya chochote katika kesi hiyo hadi hapo itakapopata kibali cha kusikiliza kesi hiyo kutoka kwa DPP.

Katika mapingamizi yao, Magafu aliiomba Mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo sababu katika mashitaka yote 17 yalilofunguliwa chini ya Sheria ya Uhujumu uchumi yalitakiwa yafunguliwe kama mashitaka ya kawaida ya jinai ambayo yanamruhusu mshitakiwa kujibu.

Pia alidai kuwa katika maudhui ya hati ya mashitaka hakuna hata kosa moja la uhujumu uchumi kama ilivyoainishwa kwamba ni kesi namba 10 ya uhujumu uchumi.Alidai kwa mujibu wa kifungu cha 129 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai( CPA) kinaipa mamlaka mahakama kukataa kusajili kesi endapo zitakuwa na makosa na kwamba sheria hiyo inampa Hakimu mamlaka ya kuikataa na kuitupilia
mbali.

Katika uamuzi wake,Hakimu Mhina amesema amepitia hoja za pande zote na anatupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi.Akifanua sababu za kutupilia mbali, Amesema, pamoja na kifungu hicho cha 129 cha CPA, kifungu cha 3 cha Sheria ta Uhujumu Uchumi, kinaondoa mamlaka kwa mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi, isipokuwa DPP atakapowasilisha kibali cha kuiruhusu mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo.

Hakimu Mhina amesema Mahakama hiyo ina mamlaka ya kumsomea mashitaka mshitakiwa na kusikiliza maelezo ya mashahidi (Commital) lakini haina mamlaka ya kuondoa kesi hiyo na kwamba masuala ya kisheria yaliyowasilishwa na upande wa utetezi, yanatakiwa kuelekezwa katika mahakama yenye mamlaka ambayo ni Mahakama Kuu.

"Mahakama imefungwa mikono na haina mamlaka ya kuondoa au kufanya maamuzi yoyote katika hati hii ya mashitaka, mpaka kitakapoletwa kibali kutoka kwa DPP," amesema Hakimu Mhina.Hata hivyo, baada ya kueleza hayo alisema upande wa utetezi wana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi hayo endapo haujaridhika.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi, Februari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande.Katika kesi hiyo Wambura anakabiliwa na mashitaka ya kughushi, mashitaka ya kutoa nyaraka za uongo, mashitaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashitaka mawili ya kutakatisha fedha.Wakili wa Serikali, George Barasa alidai kuwa mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo katika ofisi za TFF, kati ya Julai, 2004 na mwaka 2015.

Alidai kuwa Julai 6, mwaka 2004, mahali pasipojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam, Wambura alighushi barua ambayo aliiwasilisha TFF akijifanya barua hiyo imeandikwa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jek System Limited, E Maganga akidai malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 zilizokopwa na TFF pamoja na riba.

Katika mashitaka ya kutoa nyaraka ya uongo ilidaiwa, mshitakiwa alitoa barua iliyokuwa haina kumbukumbu namba ya tarehe 6/7/2004 akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck system Ltd. akidai kuwa anadai mkopo wa Dola za Marekani 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Katika mashitaka ya tatu hadi la 15, Wambura anadaiwa alijipatia kiasi jumla ya zaidi ya Sh milioni 95 kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na riba kutoka kwa Jeck huku akijua kuwa siyo kweli.Wambura pia anadaiwa Juni 17 mwaka 2015 huko katika ofisi za TFF kwa njia ya udanganyifu, alijipayia Sh milioni 10 kutoka TFF kwa kuonyesha kuwa ni malipo ya Dola za Marekani 30,000 pamoja na riba kutoka kwenye kampuni hiyo ya Jeck jambo ambalo siyo kweli.

Kati ya Agosti 15 na Oktoba 21 mwaka 2014 huko katika ofisi za TFF, Wambura anadaiwa alijipatia Sh 25,050,000 kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.Pia ilidaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 mwaka 2015 mshitakiwa alijipatia sh. 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali zimetokana na shitaka la kughushi.
ALIYEKUWA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura (52)

NAIBU WAZIRI WA MAJI, JUMAA AWESO AIAGIZA TAKUKURU KUUCHUNGUZA MRADI WA MAJI WA RUAHA MBUYUNI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuuchunguza ujenzi wa kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.
Mbunge wa jimbo la kilolo vennance Mwamoto akimuelezea Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso juu ya mradi huo wa maji unavyoleta changamoto kwa wananchi wa jimbo la kilolo
Hichi ndio kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.



NA FREDY MGUNDA,IRINGA

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuuchunguza ujenzi wa kibanda cha kuhifadhia jenereta ya kuvuta maji katika mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa kinachodaiwa kujengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20.

Aliyasema hayo juzi katika ziara yake ya siku moja wilayani humo kukagua miradi mbalimbali ya maji, ikiwemo ile inayosuasua kwasababu mbalimbali.

“Nimepata taarifa eti kibanda hiki kimejengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 20,” alisema na kuuliza ukweli wa taarifa hizo kwa mhandisi wa maji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Enock Basyagire aliyesema hakuwepo katika halmashauri hiyo wakati kikijengwa na kuomba akapitie nyaraka ili kujiridhisha. 

Aliwahimiza Takukuru kulifuatilia jambo hilo kwa haraka na kama kutakuwa na kile alichoita “matumizi mabaya ya fedha za umma” wahusika wakamatwe na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Wakati huo huo, waziri Aweso ameoneshwa kusikitishwa kwake kuona katika mradi huo, tenki kubwa la kuhifadhi maji limejengwa katika eneo lisilo na chanzo cha maji; ambalo kwa mujibu wa taarifa ya mhandisi wa halmashauri hiyo, gharama yake ni zaidi ya Sh Milioni 45. 

“Huu ni uhuni, mmejenga tenki la Sh Milioni 45 na halijawahi kuwa na maji; mimi sio mtaalamu wa maji lakini najua, huwezi kujenga tenki katika eneo lisilo na chanzo cha uhakika cha maji, ni bora hapa mngechimba kisima kirefu huenda mngepata maji kwa ajili ya wananchi hawa wakati mkisubiri mradi mkubwa,” alisema. 

Akitoa onyo kwa wahandisi wa maji kuacha kucheza na fedha za umma huku akiwataka wataalamu wa maji kutoka Bonde la Rufiji kufanya utafiti kujua eneo linaloweza kuwa na maji yatakayonusuru mradi huo ambao utekelezaji wake ulianza awamu ya nne ya Dk Jakaya Kikwete, Aweso alisema: 

“Serikali haipo tayari kuona wataalamu wanaotakiwa kuwasaidia wananchi kupata maji, wanatengeneza mazingira ya kula fedha za umma. Alimuita mhandisi huyo mbele ya wananchi waliokuwepo wakati akikagua tenki hilo na kumtaka kuwaomba radhi kwa ujenzi huo ulioshindwa kuzingatia mambo ya kitaalamu; ombi lililopokelewa vizuri na wananchi hao. 

Katika kukabiliana na changamoto za matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji inayosimamiwa na halmashauri, alisema Wizara imeamua kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini hatua inayotarajiwa kusaidia kukomesha tabia hiyo. 

Alisema wakala hiyo itakapoanza itasaidia kupunguza au kumaliza ulaji wa fedha za miradi ya maji na wahandisi wasio na nia njema katika kushughulikia kwa weledi changamoto za maji katika maeneo yao, wataondolewa na nafasi zao watapewa wengine. 

Awali Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto alimwambia naibu waziri huyo kwamba kata ya Ruaha Mbuyuni ni moja ya maeneo yenye changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi na salama katika jimbo hilo. Mwamoto alisema ukosefu wa maji safi na salama katika kata hiyo umewaweka wananchi wake katika mazingira hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipundupindu ambacho hutokea mara kwa mara. 

“Leo umekuja mwenyewe, umejionea na umesikia kutoka kwa baadhi ya wananchi, naomba uwaondoe hofu wananchi hawa,” alisema huku naibu waziri akiahidi kuishughulikia changamoto hiyo kwa kasi kubwa. Mwenyekiti wa Kijiji cha Ruaha Mbuyuni, Adam Danando alisema sehemu kubwa ya wananchi wa kijiji na kata hiyo wamekuwa wakitegemea maji ya bonde la mto Lukosi yenye chumvi na bakteria ambao ni hatari kwa afya zao. 

ASILIMIA KUBWA YA VIJIJI NCHINI KUONDOKANA NA TATIZO LA KUKOSA UMEME IFIKAPO 2020

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi akiwa amesimama na baadhi ya wajumbe wa bodi kujadili maendeleo mazuri ya ujenzi unaoendelea katika eneo hilo la lemuguru kata ya kisongo,nakupewa maelekezo na Mratibu wa mradi wa ujenzi Mhandisi Peter Kagady
Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi nchini mhandisi Alexander kyaruzi(Alievaa miwani) akipewa muongozo wa ujenzi utakaoendelea katika eneo hilo la legumuru kata ya kisongo na mratibu wa mradi mhandisi peter kigadya( alievaa koti la langi ya chungwa) mbele ya wajumbe ya bodi
Mwenyekiti wa bodi ya wakaguzi nchini Mhandisi alexander kyaruzi kati kati akikakagua moja ya mashimo yanguzo aliochimbwa kwaajili ya kusimamisha minara mikubwa ya umeme.
Baadhi ya vijana wanaojishughurisha na ujenzi wa upandishwaji wa nguzo kubwa za umeme wilayani monduli , ikiwa ni moja ya mradi unaondelea katika njia za usambazaji wa umeme vijijini.
Mwenyekiti wa bodi ya ukaguzi nchini Mhandisi Alexander Kyaruzi pamoja na wajumbe wa bodi ya ukaguzi wakijadilianana kupeana maelekezo pamoja na waratibu wa ujenzi wa kituo cha kupooza na kusambasa umeme lemuguru kata ya kisongo mkoani arusha.
Eneo la ujenzi utakaofanyika wa kupooza na usambazaji umeme uliopo lemuguru kata ya kisongo mkoani arusha ambapo magari yanabeba udongo usiofaa kwa ujenzi na kuweka udongo unaofa kwa ujenzi




Na. Vero Ignatus Arusha


Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco nchini Mhandishi Alexander Kyaruzi kwa kushirikiana na wajumbe wa bodi hiyo wamefanya ukaguzi katika kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza umeme uliopo Lemguru Kata ya Kisongo mkoani Arusha

Akizungumza wakati walipotembelea mradi huo Mhandisi Kyaruzi amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea maendeleo, hali ya usimamizi ya miradi, ambapo hadi sasa vipo vituo viwili ambacho cha Lemguru wanaongeza kilovet 400 - 420 eneo lingine linaloboreshwa ni kutoka Iringa mpaka Shinyanga lenye msongo wa kilovet 400 

Kwa mujibu wa Mhandisi Kyaruzi mradi huo mkubwa wa kupooza na kusambaza umeme unaunganisha nchi za Zambia, Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania, ambapo utaweza kuleta uhakika wa umeme unatokea katika mikondo mbali mbali ya maji,kama vile Uganda unatumia mto ambao unasambaza umeme katika nchi nyingine za Africa ikiwemo Tanzania

Aidha Mhandisi Alexander Kyaruzi amefurahishwa, na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa juhudi zinazofanywa,katika kusimamia vyema pamoja na kuwapa vijana nafasi za ajira katika maeneo hayo huku akiwatakaa kuzidisha kasi ya uendeshaji wa mradi hadi kufikia mwaka 2020

‘‘Tulivyo kuja hapa kwanza tulifurahi pamoja na kwamba ni mwanzo na kwenye mwanzo mzuri unaoneka,lakini hapa tunaona wanaondoa kwanza udongo na kubadilisha udongo ambao haufai kwa ujenzi na kuweka udongo kwa ajili ya ujenzi ndipo waaanze ujenzi maana ujenzi huu wa mradi tumeweka mikakati mpaka mwaka ujao uwe umekamilika,na ukitoka hapa unaelekea Singida mpaka Namanga’’ Alisema

Alisema mradi unategemea mpaka kufikia mwaka 2020 uwe umekamilika na mradi utaleta faida za umeme katika vijiji vyote nchini,na pia utaleta manufaa kwa vijana wasio na ajira na wanaokaa vijiweni kupata fursa za ajira

Hata hivyo mratibu wa mradi wa njia za kusafirisha umeme wa msongo wa kilovet 400 Afrika ya Mashariki katika nchi za Zambia,Kenya,Uganda na Tanzania Mhandisi Peter Kigadya amesema mpaka sasa maendeleo ya mradi yamefikia pazuri na mradi umeunganishwa kutokea Kenya mpaka Arusha na kuelekea Singida.

Amesema mradi mzima wa una sehemu kubwa tatu ujenzi wa njia za umeme na njia kuu za kupoozea umeme,pamoja na usafirishaji wa umeme katika vijiji,sehemu ya kwanza kwanza Iinatoka Singida mpaka babati,na sehemu ya pili ni babati mpaka arusha, na sehemu ya tatu arusha mpaka namanga na njia zote tatu zipo katika ujenzi na mpaka sasa njia hizo wameziwekea msingi.

NAIBU WAZIRI IKUPA ATEMBELEA KUKUNDI CHA WAJASIRIAMALI WENYE ULEMAVU NA SHULE YA VIZIWI DODOMA

$
0
0
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu  Mhe. Stella Ikupa akizungumza na wanachama wa Sulungai,  alipokuwa kwenye ziara kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma. (Kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU) Bw. Stanley Jumbe akimweleza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu  Mhe. Stella Ikupa namna ya kuandaa viatu vya wazi aina ya Makobazi. 
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akitengeneza viatu vya wazi (Makobazi) alipotembelea Chama cha Walemavu Salungai kilichopo Kata ya Ipagala, Jijini Dodoma. (Kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akinunua viatu vya wazi aina ya Makobazi kwa Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU) alipotembeleaa Kikundi hicho kilichopo Kata ya Ipagala kujionea shughuli zinazofanywa na wajasiriamali hao.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na Chama cha Walemavu Sulungai (CHAWASU), Viongozi na Watendaji wa Jiji la Dodoma alipokuwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa  akieleza jambo wanafunzi wa shule viziwi iliyopo Jijini Dodoma(hawapo pichani), alipotembelea shule hiyo kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
 Mwananfunzi mwenye Uziwi wa darasa la Tatu, Shadia Kizamo akitaja jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri y Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kwa lugha ya alama swali aliloulizwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa  (hayupo pichani).
 Mwananfunzi mwenye Uziwi wa darasa la Saba, Eliabi Chilongola akimweleza kwa lugha ya alama Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, teknolojia aliyoivumbua ya Umwagiliaji.

 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akimsikiliza Mratibu wa Shule maalumu ya Viziwi Dodoma, Bw. Robin Donilergoed (wa pili kutoka kulia) alipokuwa akikagua miundombinu ya Shule hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wenye Uziwi wanaojishughulisha na ufundi wa Ushonaji.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

WALIOFAULU MKIDATO CHA NNE WAKIRI KUSAIDIWA NA KAMBI ZA KITAALUMA

$
0
0
Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza (pointi saba) na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyefanya vizuri kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo na kuongoza kimkoa (wasichana), wakionesha kadi zao za akaunti ambazo wamekabidhiwa (katika hafla maalum ya kuwapongeza iliyofanyika shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari13, 2019 ) baada ya kufunguliwa akaunti na kuwekewa zawadi hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na Mwanafunzi kutoka Shule ya Kata Nkololo aliyeongoza kimkoa katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 kwa kupata daraja la kwanza(pointi saba) ,Ibrahimu Buyungumya(kushoto) na Mwanafunzi wa Kike Kwandu Maduhu kutoka Shule ya Sekondari Biashara aliyeongoza kwa upande wa wasichana kwa kupata daraja la kwanza (pointi 11) katika mtihani huo, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kimkoa, iliyofanyika katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(mwenye suti kulia) akishuhudia wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi wakifanya mazoezi kwa vitendo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa shuleni hapo, Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akiwakabidhi zawadi ya ngao viongozi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi ambayo iliongoza kimkoa na kushika nafasi ya tisa kati ya halmashauri zaidi ya 185 nchini katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018, (kushoto na wa pili kushoto) ni wanafunzi walifanya vizuri Kimkoa kutoka shule za Serikali), wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa nne kushoto mbele) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi , walimu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wanafunzi walawili walioongoza katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na wazazi wao, baada ya hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo akizungumza na viongozi, walimu, wazazi na wanafunzi katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018 iliyofanyika kimkoa, katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Biashara Mwalimu Mathias Joseph akionesha zawadi ya shilingi 460,000/= iliyotolewa kama motisha kwa walimu wa shule hiyo waliofanikisha kutoa jumla ya alama A 23 katika Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2018, wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani huo iliyofanyika kimkoa katika shule ya sekondari Nkololo wilayani Bariadi Februari 13, 2019.



Na Stella Kalinga, Simiyu

Wanafunzi wa shule za Serikali (kata) Wilayani Bariadi, Ibrahim Buyungumya kutoka Shule ya Sekondari Nkololo , aliyepata daraja la kwanza alama (points) saba na Kwandu Maduhu wa Biashara Sekondari aliyepata daraja la kwanza alama kumi na moja, wamekiri kuwa kambi za kitaaluma zimechangia kuongeza ufaulu wao katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2018.

Wanafunzi hao wameyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 Kimkoa na kuufanya mkoa kushika nafasi ya Tisa Kitaifa, iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Nkololo wilayani Bariadi, Februari 13, 2019.

Wanafunzi hao wamesema pamoja na kumuomba Mungu, juhudi zao binafsi za kujisomea, jitihada za walimu, malezi kutoka kwa wazazi wanakiri kambi za kitaaluma zilizofanyika mkoani Simiyu kwa madarasa yote ya mitihani ziliwasaidia kuwaandaa na mtihani huo wa Taifa, huku wakisisitiza kambi hizo ziwe endelevu na wakapendekeza kuwa kwa mwaka 2019 ziongezewe muda na zianze mapema zaidi.

“ Namshukuru Mungu kunifanikisha kupata daraja la kwanza alama saba, nawashukuru walimu wangu, wazazi wangu kwa namna walivyokuwa msaada kwangu; pia kipekee namshukuru Mkuu wetu wa Mkoa kwa kutuletea kambi, zimetusaidia sana maana tulipata nafasi ya kukutana na wanafunzi wenzetu na walimu mahiri kutoka shule mbalimbali na zilitusaidia kuelewa masomo kwa mawanda mapana zaidi” alisema Ibrahimu Buyungumya.

“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata daraja la kwanza alama 11, nawashukuru wazazi, walimu pia nashukuru uwepo wa kambi za kitaaluma ambazo zilitusaidia sana kujiandaa vema na mtihani wetu, nashauri kambi hizi zianze mapema na muda uongezwe ili ziwasaidie wadogo zetu wafaulu vizuri zaidi yetu sisi” alisema Kwandu Maduhu.

Mkuu wa Shule ya sekondari Biashara, Mwl. Mathias Joseph ambaye shule yake ilifanya vzuri kwa kupata alama A 23 na alama B 79 amesema pamoja na kambi za kitaaluma siri nyingine ya kufanya vizuri ni jitihada zilizofanywa na walimu pamoja na usimamizi mzuri wa mikakati iliyowekwa na idara ya Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi na mitihani ya mara kwa mara.

Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza walimu waliofanikisha na wanafunzi waliofanya vizuri katika Matokeo ya mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne mwaka 2018 katika mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amewapongeza viongozi, walimu, wanafunzi, wazazi na wadau wote wa elimu mkoani humo, kwa jitihada walizofanya katika kuongeza ufaulu.

Aidha, Mtaka ameelekeza kamati zote za shule zikutane na wazazi wa wanafunzi wa madarasa ya mtihani ili wakubaliane juu ya wanafunzi hao kuanza kambi za kitaaluma na wazazi hao wachangie chakula ambacho watoto wao wangekula wakiwa majumbani kwao kitumike wakiwa kambini.

“Nilishatoa maelekezo na nayarudia; kamati za shule zikae na wazazi wakubaliane madarasa yote ya mtihani watoto waanze kambi za kitaaluma na wazazi wachangie chakula kile kile ambacho watoto wangekula wakiwa nyumbani, ili watoto wapate nafasi nzuri ya kusoma na kujiandaa na mtihani wa Taifa” alisema Mtaka.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo ametoa wito kwa wazazi mkoani humo kuhimiza watoto kusoma ili waweze kufikia ndoto zao akakemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwaachisha masomo watoto wa kike na kuwaozesha.

Jumla ya wanafunzi 7094 kati yao wavulana ni 4224 na wasichana 2875 walifanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018 mkoani Simiyu na kuwezesha mkoa kushika nafasi ya tisa Kitaifa kati ya mikoa 31, ambapo umepanda kwa nafasi mbili ikilinganishwa na mwaka 2017 ambapo ulishika nafasi ya 11 Kitaifa.

Katika pongezi zilizotolewa kwa walimu na wanafunzi mwanafunzi wa kiume aliyeongoza Kimkoa amezawadiwa shilingi milioni Moja, mwanafunzi bora wa kike shilingi laki tano (wote wamefunguliwa akaunti) na kuahidiwa kupewa mahitaji yote muhimu watakapochaguliwa kidato cha tano, huku walimu sitini kila mwalimu akipewa shilingi elfu ishirini kwa kila alama A iliyopatikana kwenye somo lake.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images