Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MAAFISA NA WASHIRIKI WA KOZI WA CHUO CHA ULINZI CHA TAIFA (NDC) WAFANYA ZIARA

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (kushoto) akisalimiana na Mkufunzi Mkuu Kanali Erick E. Mhor (kulia). Wa pili toka kushoto ni Mkalimani toka Jeshi la China, Brig. Jenerali Liang Hongshan na wapili toka kulia ni Brig. Jenerali M.N.Mkeremy.

 Mkuu wa Msafara Commodore Mumanga (kushoto) akimkabidhi Naibu Kamishna wa Magereza John Masunga,  zawadi maalum ya Mkuu wa Jeshi hilo.

 . Insp. Mwasimba Boge wa Jeshi la Magereza (wa pili kulia) akitoa maelezo ya baadhi ya nguo zinazoshonwa na wafungwa kama njia mojawapo ya Urekebishaji ndani ya Kiwanda cha Ukonga.
 Mkuu wa msafara wa Maafisa na washirirki wa kozi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) Commodore (Brig. Jenerali-Navy) M.M.Mumanga (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Viwanda Vidogo Vidogo wa Jeshi la Magereza Naibu Kamishna John Masunga. Kulia ni Naibu Kamishna Jeremiah Katungu.

 Mkuu wa msafara Commodore Mumanga(kushoto) akitoa neon la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza (hayupo pichani). Kulia ni Brig. Jenerali Zhang Yongxi ambaye ni Mkufunzi Mkuu toka Jeshi la China.

 Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM) wakiwaonesha wakufunzi na wanafunzi toka Chuo cha Ulinzi cha Taifa jinsi ya kukabiliana na wahalifu wakorofi.


Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jenerali Phaustine Kasike (wan ne toka kushoto, walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Jeshi la Magereza, Viongozi Waandamizi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa pamoja na wanafunzi wa Chuo hicho.




UAMUZI DHAMANA YA MBOWE, MATIKO KUTOLEWA NA MAHAKAMA YA RUFAA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema uamuzi wa Mahakama ya rufaa dhidi dhamana ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko utatolewa na Mahakama ya Rufaa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kelvin Mhina amesema hayo leo Februari 14, 2019 wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa mahakamani hapo ambapo amesema mpaka sasa kesi hiyo haijaaanza kusikilizwa, mpaka watakapopata majalada ya maamuzi kutoka Mahakama ya Rufaa.

Mapema,  Wakili wa Serikali, Ester Martin amedai kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 28, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa wakati wakisubiri Rufaa  yao Ambayo tasikilizwa Februari 18, mwaka huu.Novemba 23, mwaka jana,Jaji Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, alifuta dhamana kwa Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka  masharti ya dhamana.

Baada ya uamuzi huo , washitakiwa hao wakiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya mahakama hiyo ya kufuta dhamana.Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.

Upande wa Serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi alidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.

Hata hivyo, baada ya upande wa serikali kuwasilisha rufaa yao,  kuliibuka malumbano ya kisheria baina ya mawakili wa pande zote, huku mawakili wa kina Mbowe wakiongozwa na Wakili Peter Kibatala, walipinga uhalali wa taarifa ya serikali ya kusudio la kukata rufaa kwa madai hawajafahamishwa na Msajili wa Mahakama Kuu kuhusu kuwepo kwa taarifa hiyo.

Jaji Rumanyika alisema kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) anapewa mamlaka ya kukata rufaa kwa uamuzi mdogo chini ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa na kwamba kunapokuwepo taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani, mahakama ya chini haiwezi kuendelea na shauri.

Jaji  Rumanyika alisema mahakama yake imefungwa mikono hivyo anasitisha usikilizwaji wa rufani hiyo hadi hapo itakapotolewa uamuzi katika Mahakama ya Rufani.Mbali na Mbowe na Matiko, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.

Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka  2018 maeneo ya Dar es Salaam.



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko wakitoka kwenye viunga vya mahakama leo.

NYONGO ATAKA WATUMISHI MADINI KUEPUKA RUSHWA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi lililofanyika tarehe 13 Februari, 2019.

 Naibu Waziri wa Madini Sanslaus Nyongo na Viongozi Waandamizi wa Wizara pamoja na Viongozi wa TUGHE Taifa na TUGHE Tawi la Wizara ya Madini, wakiimba wimbo Maalum wa kuhamasisha Umoja wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo na Wawakilishi kutoka Taasisi za Wizara.

 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakifuatilia mkutano huo.

 Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Madini, Joyce Manyama akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.

 Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Madini.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Madini. 




Na Asteria Muhozya, Dodoma 

Naibu wa Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amewataka watumishi wa Wizara ya Madini kujiepusha na vitendo vya rushwa ikiwemo kuzuia rushwa katika sehemu zao za kazi kwani suala hilo linasababisha migogoro kwenye sekta ya madini. 

Naibu Waziri Nyongo aliyasema hayo Februari 13 wakati akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi la wizara na kuongeza kuwa, serikali inafuatilia mienendo ya watumishi wa sekta husika. 

Alisema kuwa, wako watumishi wanaomiliki leseni kwa dhuluma suala ambalo pia limechangia kuwepo kwa migogoro mingi kwenye sekta na kueleza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli anasisitiza suala la kuzingatia maadili katika utumishi wa umma na hususan katika sekta ya madini. 

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo alilitaka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuhakikisha linajiendesha kwa faida na kusisitiza kuwa Serikali inataka gawio. 

Aidha, aliutaka uongozi wa STAMICO kuzingatia maslahi ya watumishi kwa kutoa motisha mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwapatia mafunzo lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi wa shirika kwa ujumla. 

Akizungumzia mafanikio makubwa katika Sekta ya Madini, Naibu Waziri Nyongo alisema kuwa ni pamoja na mabadiliko ya Sheria ya Madini na kusisitiza kuwa kwa Afrika Tanzania imekuwa mfano kama nchi bora inayosimamia vyema rasilimali za madini. 

“Sifa bora kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini zisitufanye tubweteke bali tuendelee kufanya kazi kwa ubunifu wa hali ya juu huku tukizingatia maadili ya kazi,” alisema Nyongo 

Nyongo aliendelea kusema kuwa, kama moja ya mikakati ya kutoa motisha kwa watumishi, uongozi wa Wizara unatakiwa kutoa fursa mbalimbali kwa watumishi ikiwa ni pamoja na mafunzo. 

Wakati huo huo, akizungumza kwa niaba ya watumishi, Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Tawi la Wizara ya Madini, Joyce Manyama alisema kuwa watumishi kupitia chama chao watafanya kazi bega kwa bega na uongozi wa Wizara ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na viwanda vingi vya uongezaji thamani madini ili kufikia malengo ya Serikali kupitia mchango wa Sekta ya Madini kwenye ukuaji wa Pato la Taifa. 

Aidha, Manyama alichukua fursa hiyo kuishukuru Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Shirika la Vyama vya Wachimbaji wa Madini Nchini (FEMATA), wachimbaji wadogo kwa kuitisha mkutano uliofanyika hivi karibuni baina yao na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli 

Vilevile, aliishukuru Wizara kwa kuanzisha mfumo mpya wa utunzaji wa kumbukumbu za Wizara unaojulikana kama Electronic Filing Management System ambao utaboresha utunzaji wa kumbukumbu na kurahisisha upatikanaji wake pindi zinapohitajika. Pia, aliiomba Wizara kuendelea kusimamia zoezi la upandishwaji wa vyeo ili watumishi waweze kupandishwa vyeo kulingana na sifa wanazokuwa nazo. 

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema kuwa Wizara itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kazi ili kila mtumishi afanye kazi kwa ubunifu zaidi. 

Aliongeza kuwa, kwa sasa Wizara inafanya vizuri ambapo Sekta ya Madini imekua kwa asilimia 18 huku mchango wa sekta kwa fedha za kigeni ikiwa ya tatu nyuma ya Kilimo na Utalii na kueleza kwamba, pamoja na mafanikio hayo, bado kuna rushwa na kukosekana uadilifu.

AZAM FC YAJIZATITI KUONDOKA NA ALAMA TATU SOKOINE

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KIKOSI cha Azam kimejidhatiti kufanya kweli kwenye mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prison baada ya kutoka katika mchezo wake dhidi ya Lipuli uliomalizika kwa kupata  sare ya bao 1-1.


Kocha Msaidizi wa Azam, Juma Mwambusi, aliwapongeza wachezaji kwa kutoka nyuma na hatimaye kupata sare ya ugenini.


“Mchezo ulikuwa ni mzuri na mgumu, Azam kipindi cha kwanza hatukuweza kucheza vizuri kwa sababu wachezaji waliingia kwenye mchezo wakiwa na kasi ya chini, kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na hali ya uwanja kwa sababu ilinyesha mvua kabla ya mpira kuanza kwa hiyo walicheza kwa tahadhari zaidi ili wasiweze kupata majeraha na kusababisha matatizo langoni,” alisema.

Alisema waliweza kufanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kucheza mpira wa kushambulia kutokea pembeni na katikati hadi kufanikiwa kusawazisha bao wailotanguliwa kipindi cha kwanza na Lipuli.

“Pengine tungeweza kutulia zaidi kwa washambuliaji wetu tungeweza kushinda mabao mawili au matatu na kuondoka na pointi tatu katika mechi hii, yote kwa yote tunajipanga kwa mchezo unaokuja (Tanzania Prisons,” alisema.

Matokeo dhidi ya Lipuli  yameifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 49 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikizidiwa pointi tisa na vinara Yanga waliokuwa nazo 58, lakini matajiri hao wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

TIMAYA ATAJA SABABU ZA KUMSHIRIKISHA ALI KIBA KWENYE ALBAM YA CHULO VIBES

$
0
0

Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII wa muziki kutoka nchini Nigeria  Enitimi Alfred a.k.a Timaya ameamua kufungua kwa kuweka wazi sababu za kumshirikisha mkali wa Bongofleva nchini Tanzania Alikiba kwenye album yake mpya.

Timaya ambaye amejijengea umaarufu kutokana na staili yake ya uimbaji, amesema kuwa ndoto yake ya muda mrefu ilikuwa ni kuhakikisha siku moja anafanya kazi na Alikiba kwani pamoja na uwezo wake mkubwa pia ni shabiki wake amekuwa akimfatilia kwa muda mrefu sana.

"Nilikutana nae kwa mara ya kwanza kwenye kazi iliyokutanisha wasanii wa nchi mbalimbali kama amani wa Kenya,R.kelly,Navio na wengine wengi lengo ni kuleta karibu mataifa hayo mawili Afrika na Amerika pamoja na kudumisha amani,furaha na upendo ," amesema Timaya

.Hata hivyo amefafanua katika album yake mpya iitwayo Chulo vibes amemshirikisha Alikiba pamoja na Msanii Burnaboy kutoka Nigeria ambaye kwa sasa anafanya vizuri na kwamba Burnaboy ni msanii anayedumisha utamaduni wa kiafrika kwa ujumla na ni mfano mzuri wa kuigwa kutokana na nyimbo zake kama YE,On the low na Gbona zenye mahadhi na midundo ya kiafrika zaidi na hata video zake zinahamasisha utamaduni wa kiafrika kuanzia mavazi na washiriki wa video hizo.

"Matarajio yangu ni kufanya ngoma na wasanii wa Afrika mashariki kwa nchi za Kenya,uganda na Burundi maana wasanii wa nchi hizo nao wanafanya vizuri," amesema Timaya.Ameongeza kuwa anataka kufanya kazi na wasanii ambao hajawahi kufanya nao kazi na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa na anafurahia kuona muitikio umekua mzuri,hivyo basi anategemea kufika mbali zaidi kimuziki na ndio maana ndani ya albamu hiyo mpya ameshirikisha wasanii tofauti kabisa ambao hakuwahi kufanya kazi nao.

MWANJELWA AAGIZA KUPEWA MCHANGANUO WA MATUMIZI YA SHILINGI MILIONI 101 ZILIZOTOLEWA NA TASAF KUJENGA UZIO WA SHULE MAALUM YA MSINGI PONGWE ILIYOPO JIJINI TANGA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanafunzi na walimu wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe pamoja na wakazi wa mtaa wa Pongwe Kaskazini, jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na wanafunzi na walimu wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe pamoja na wakazi wa mtaa wa Pongwe Kaskazini, jijini Tanga, katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishiriki kuimba wimbo na wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe ya jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo wenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bw. Daudi Mayeji (hayupo pichani) kuwasilisha mchanganuo wa matumizi ya fedha zilizotolewa na TASAF kwa lengo la kujenga uzio ili kuimarisha usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika Shule Maalum ya Msingi Pongwe jijini Tanga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo na wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe ya jijini Tanga, alipotembelea shule hiyo kwa lengo la kukagua, kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio katika Shule hiyo wenye lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 




Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb), amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Bw. Daudi Mayeji kuwasilisha mchanganuo wa shilingi 101, 089,736.65/= zilizotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kujenga uzio wa Shule Maalum ya Msingi Pongwe kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi wa jamii ya albino katika shule hiyo. 

Agizo hilo amelitoa jijini Tanga, alipotembelea mradi wa ujenzi wa uzio katika shule hiyo maalum ili kujionea na kujiridhisha na utekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani Tanga. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amefafanua kuwa, licha ya kuridhika na kazi nzuri iliyofanywa na Mkurugenzi huyo pamoja na wasaidizi wake ya ujenzi wenye viwango, lakini anataka maelezo ya kina ya matumizi ya fedha hizo baada ya kuangalia uzio uliojengwa na kiwango cha fedha kilichotolewa na TASAF ambapo ameelezwa kwamba gharama za uzio huo ni shilingi milioni 75 hivyo, anataka kujua kiasi kilichobakia kimetumikaje. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa fedha iliyotolewa na TASAF imefanya kazi nzuri na kusisitiza kuwa, fedha iliyotolewa kutekeleza mradi wa ujenzi wa uzio huo ni lazima kazi yake iwe ya kiuhalisia kulingana na fedha iliyotolewa na sio vinginevyo. 

Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa uzio huo, Kaimu Mtendaji, Mtaa wa Pongwe, Bi. Dorah Senkondo amesema, ujenzi wa uzio wa mita 738 katika Shule Maalum ya Msingi Pongwe utaimarisha ulinzi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa ngozi kutokana na changamoto ya kiusalama iliyopo kwa jamii ya albino. 

Bi. Senkondo ameainisha kuwa, serikali kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini, imetoa kiasi cha shilingi 101, 089,736.65/= ikiwa ni fedha za awamu ya kwanza ili kutekeleza ujenzi wa mradi huo, ambapo jumla ya mita 496 zimejengwa hadi hivi sasa, hivyo kubakiza ujenzi wa uzio wa mita 242 utakaokamilika kupitia fedha za awamu ya pili zitakazotolewa. 

Ujenzi wa uzio huo unahusisha mchango wa jamii na usimamizi kutoka katika Halmashauri ya jiji la Tanga ili kuweza kufikia lengo la kuimarisha ulinzi na usalama kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Pongwe iliyopo mtaa wa Pongwe Kaskazini jijini Tanga. 


IMETOLEWA NA; 
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI 
OFISI YA RAIS (UTUMISHI) 
TAREHE 14 FEBRUARI, 2019 

MWAKINYO, ZARIKA WAJIFUA UINGEREZA KUELEKEA PAMBANO LA MACHI 23.

$
0
0
Bondia namba moja wa uzito wa Super Welterweight, Hassan Mwakinyo na bondia nyota wa kike nchini Kenya, Fatuma Zarika wamewasili mjini Liverpool kujiandaa na pambano la ngumi za kulipwa mjini Nairobi, Kenya mwezi ujao.

Mwakinyo na Zarika ambapo wapo chini ya udhamini wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa, watapambana na mabondia tofauti katika pambano lililopewa jina la Nairobi Fight Night katika ukumbi ambao utatangazwa hapo baadaye.

Mwakinyo ambaye bondia namba 16 kati ya mabondia 1,842 kwa mujibu wa viwango vya mtandao maarufu wa ngumi za kulipwa Duniani, Boxrec, Bondia huyo mzawa wa mkoa wa Tanga,  kwa sasa ana rekodi ya kushinda mapambano 24, kati ya hayo, 10 kwa knockout (KO) na kupoteza mawaili ikiwa moja kwa KO.

Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema kuwa mabondia hao wawili watakuwa chini ya kocha wa bondia  nyota, Tony Bellew ambaye alimchapa kwa TKO mara mbili, bondia maarufu, David Haye.

Abbas alisema kuwa Mwakinyo na Zarika watarejea moja kwa moja nchini Kenya Machi 16 tayari kwa mapambano yao. Zarika ambaye ni maarufu kwa jina la “Irone Fist”  atatetea ubingwa wake wa Baraza la Ngumi za Kulipwa (WBC) wa uzito wa Super Bantamweight, atapambana na bondia nyota kutoka Zambia, Catherine Phiri. 

“Lengo la kuwatafutia kambi ya mazoezi nchini Uingereza ni kuwaboresha ukali wao ili waendelee kutamba katika mchezo wa ngumi za kulipwa Duniani. SportPesa inajivunia kuwa na mabondia hawa na tunaamini hawatatuangusha katika mapambano yao,” alisema Abbas.

Abbas aliwaomba mashabiki wa ngumi za kulipwa kufika kwa wingi wakati wa mapambano hayo ili kuwapa hamasa mabondia hao ambao ni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kwa upande wake, Mwakinyo aliishukuru kampuni ya SportPesa kwa kuwatafutia kambi ya mazoezi, jambo ambalo  hakuwa anafanya kabla ya kupata umaarufu.

“Ni faraja kwangu na mchezo wa ngumi za kulipwa pia. Naamini mabondia wengine wataongeza bidii ili kuweza kufikia kiwango change na kupata wadhamini kama SportPesa ambao wamenyesha njia kwangu,” alisema Mwakinyo.

African Union launches 2019 Year of Refugees, Returnees and Internally Displaced People

$
0
0

The African Union (AU), at a top level summit meeting in the Ethiopian capital of Addis Ababa this week, formally launched 2019 as the “Year of Refugees, Returnees and IDPs: Towards Durable Solutions to Forced Displacement in Africa.” 

The launch of the 2019 theme at the 32nd AU Summit comes at a time when forced displacement remains a major issue confronting the African continent. More than a third of the world’s forcibly displaced people are in Africa, including 6.3 million refugees and asylum-seekers and 14.5 million internally displaced people. 

But the AU heads of state and government attending the gathering noted that there has also been progress in tackling forced displacement. UN Secretary-General António Guterres praised Africa’s approach and noted that the AU and UN are working together across the continent to tackle the scourge. 

“Africa hosts nearly a third of the world’s refugees and internally displaced people. Despite the continent’s own social, economic and security challenges, Africa’s governments and people have kept borders, doors and hearts open to millions in need,” Guterres, former head of UNHCR, the UN Refugee Agency, for 10 years. 

In his closing remarks, Egypt’s President Abdul Fattah Al-Sisi, the new chairperson of the African Union called for a focusing of efforts “to solve the problem of refugees, IDPs and migrants in a comprehensive manner along with post construction and development plans and programmes.” 

The AU’s 2019 focus on the forcibly displaced comes at a particularly appropriate time. This year marks the 50th anniversary of the adoption of the 1969 Organization of African Unity Convention on Refugees and the 10th anniversary of the 2009 AU Convention on IDPs in Africa (Kampala Convention). The AU and its partners, including UNHCR, plan several commemorative events across the continent during the year. 

Over the weekend, the AU and the UN Refugee Agency co-organised a roundtable conference aimed at tackling the root causes of forced displacement in Africa and achieving durable solutions. UN High Commissioner Filippo Grandi addressed the meeting and also attended the AU Summit. He also held productive bilateral meetings in Addis Ababa with the leaders of several African countries that are faced with the problem of forced displacement. 

The AU and UNHCR also organised a high-level dialogue on the theme of the year. Speakers included the African Union Commission chairperson Moussa Faki Mahamat; UNHCR’s Filippo Grandi; UN Emergency Relief Coordinator Mark Lowcock; and Director General of the International Organization for Migration Antonio Vitorino. Others were the Executive Director of UNAIDS Michel Sidibe; Secretary General of the International Federation of the Red Cross Elhadj As Sy; the United Nations High Commissioner for Human Rights Michelle Bachelet Jeria, and UNDP’s Administrator Achim Steiner. 

For more information, please contact: Sulaiman Momodu momodu@unhcr.org (+251930470524) or Suleyman Ali alisul@unhcr.org (+251911079548).
Heads of State and Government at the closing ceremony of the AU Summit

TMA YATOA MWELEKEO WA MVUA ZA MASIKA MACHI HADI MEI

$
0
0
*Yatoa ushauri na tahadhari kwa wananchi na sekta mbalimbali katika kukabiliana na mvua hizo za muda mfupi.

Na Leandra Gabriel blogu ya jamii
MAMLAKA ya hali ya hewa nchini (TMA) imetoa mwelekeo na hali ya mvua za masika kwa mwezi Machi hadi Mei mwaka huu  kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua na kutoa angalizo kwa wananchi kufuatilia mirejesho inayotolewa na mamlaka hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Dkt. Agnes Kijazi amesema kuwa mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka na kueleza kuwa maeneo ya Nyanda za juu Kaskazini mashariki yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Dkt. Kijazi amesema kuwa mvua za masika ni mahususi katika maeneo ya Nyanda za juu kaskazini Mashariki, Pwani ya Kaskazini na visiwa vya Unguja na Pemba, Ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini wa Mkoa wa Kigoma na sehemu kubwa ya maeneo hayo yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani katika msimu wa masika kwa mwaka 2019 na katika baadhi ya maeneo ya nyanda za juu Kaskazini mashariki hasa katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro uwezekano wa wa kunyesha kwa mvua za juu ya wastani ni mkubwa.

Akifafanua hali ya kunyesha kwa mvua hizo Dkt.Kijazi amesema kuwa kwa maeneo ya ukanda wa ziwa Viktoria kwa Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita,Simiyu na Shinyanga Dkt. Kijazi amesema kuwa mvua kwa maeneo hayo zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya nne ya mwezi Februari katika Mkoa wa Kagera na kusambaa katika mikoa ya Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga katika wiki ya pili ya mwezi Machi. Na mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi na upungufu wa mvua unatarajiwa katika maeneo machache Mkoa wa Kagera na Wilaya ya Kibondo.

Amesema kuwa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikihusisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga Pwani, Visiwa vya unguja na Pemba pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro ambapo mvua katika maeneo hayo zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya kwanza ya mwezi Machi katika Mkoa wa Dar es salaam, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba na kusambaa katika Mkoa wa Tanga na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro katika Wiki ya kwanza ya mwezi Machi na mvua hizo zinatarajiwa kuwa hadi juu ya wastani katika maneo mengi na upungufu wa mvua unatarajiwa kutokea katika Mkoa wa Morogoro.

Kwa upande wa nyanda za juu Kaskazini Mashariki ikiwa ni kwa Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara mvua kwa maeneo haya zinatarajiwa kuwa za juu za wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kwa maeneo ya Mashariki mwa mkoa wa Kilimanjaro (same) na maneo mengi ya Mkoa wa Manyara yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Vilevile Dkt. Kijazi amesema kuwa kwa maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua zilizoanza kunyesha Novemba mwaka jana mvua zinandelea  na zinatarajiwa kuwa za wastani katika maeneo mengi na zile za chini ya wastani zinatarajiwa katika maeneo ya kati ya nchi( Mikoa ya Dodoma na Singida)  na katika Mkoa wa Ruvuma.

Wakati huo huo mamlaka hiyo imetoa ushauri kwa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, mifugo, nishati na madini, mamlaka za maji, sekta za afya, menejimenti ya maafa na vyombo vya habari kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua za masika  ikiwa ni pamoja na kupata na kufuata ushauri wa wataalamu wa mamlaka hiyo kwa kuzingatia mvua hizi zitanyesha kwa muda mfupi, na pia amewataka wananchi kufuatilia taarifa zinazotolewa na mamalaka hiyo kila wakati na kusisitiza kuwa Mamlaka ya hali ya hewa nchini itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.

RAIS DKT. SHEIN AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYA YA MAGHARIBI B UNGUJA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akiwa na mke wake mama Mwanamwema Shein (wamwanzo)na Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali Riziki Pembe Juma wakikunjuwa Pazia kuashiria Uwekaji wa Jiwe la Msingi Skuli ya Msingi Kwarara ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake ya kuangalia miradi mbalimbali ya Serikali katika Wilaya ya Magharibi B unguja..
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akitoa hotuba  katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Skuli ya Msingi Kwarara Ikiwa ni miongoni mwa  ziara yake  kuangalia miradi mbalimbali ya Serikali katika Wilaya ya Magharibi B unguja.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma akitoa hotuba ya Makaribisho kwa Mgeni Rasmi  Rais wa Zanzibar katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Skuli ya Msingi Kwarara Ikiwa ni miongoni mwa  ziara yake  kuangalia miradi mbalimbali ya Serikali katika Wilaya ya Magharibi B unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Kampuni ya (SRAT CONSULT )ya Mwanza Tanzania Salim Rajab Twaakyondo kuhusiana na ujenzi wa Skuli ya Msingi Kwarara ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake ya kuangalia miradi mbalimbali ya Serikali katika Wilaya ya Magharibi B unguja.
 Baadhi ya Wanafunzi wa Skuli ya Msingi na Sekondari  Kwarara wakiwa katika sehemu ya Jengo la Skuli ya Msingi ambalo Limewekewa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanizbar Dk Ali Mohamed Shein ikiwa ni miongoni mwa Ziara yake ya kuangalia miradi mbalimbali ya Serikali katika Wilaya ya Magharibi B unguja..
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Shirika la Railway Children latoa mafunzo kwa waandishi wa habari

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Railway Children, Mussa Mgata akitolea ufafanuzi kuhusu mazingira wanayoyapitia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa warsha iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.

Meneja Miradi wa Shirika la Railway Children, Mary Gatama akitoa mada kuhusu watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa warsha iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano wa Shirika la Railway Children, Henry Mazunda akiwasilisha mada ya namna kuwalinda watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na namna ya kutoa elimu ya jinsi ya kuwalinda watoto hao wakati wa warsha ya iliyowakutanisha waandishi wa katika mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto yatakayofanyika leo katika hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habariwakiwa kwenye semina ya mafunzo ya namna ya kuandika habari za watoto iliyoandaliwa na Shirika la Railway Children iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka Blogu ya Jamii

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA NEMBO MAALUMU FAINALI ZA AFCON-U17

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, leo, Februari 14, 2019 amezindua nembo maalumu ya Fainali za Afrika za Vijana chini ya miaka 17 yatakayofanyika mapema mwezi Aprili mwaka huu,ambapo  Tanzania ndiyo mwenyeji wa mashindano hayo.

WAZIRI LUGOLA ATAKA ASKARI WAPANDISHWE VYEO, WAREKEBISHIWE MISHAHARA, WALIPWE FEDHA ZA UHAMISHO NA LIKIZO

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara yake nchini, wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha za likizo. Lugola amesema kuna idadi kubwa ya askari wanaostahili kupandishwa na kurekibishiwa mishahara, kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli askari hao wana haki kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Askari na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo. Lugola alisema katika uongozi wake hataki kusikia askari wananyanyaswa, na pia changamoto hizo zinapunguza nguvu ya utendaji kazi wa askari hao wanaofanya kazi ngumu. Lugola alisema alitoa agizo la askari wanaostahili kupandishwa cheo, kurekebishiwa mishahara yao, wanaodai kulipwa fedha za uhamisho pamoja na changamoto mbalimbali zingine alizozielekeza, ziwe zimetatuliwa tangu mwaka jana, hata hivyo amesema kwa wale wenye sifa amewataka askari hao wamuamini kwakuwa watapewa vyeo vyao hivi karibuni.

“Kwanini bado hamjapanda vyeo na kubadilishiwa mishahara yenu mpaka sasa wakati nilishatoa maelekezo mpandishwe, nitahakikisha nalifuatilia hili mapema zaidi ili nijue tatizo ni nini, lakini naamini kila kitu kinaenda vizuri na ahadi niliyoitoa itakamilisha kwa wale askari ambao wanasifa watapewa vyeo hivi karibuni,” Alisema Lugola. Pia Lugola alizungumzia kuhusu ukosefu wa nyumba za makazi ya askari, kuwa licha ya Rais Dkt. John Magufuli anatoa mchango mkubwa kwa kulisaidia Jeshi, lakini bado kuna upungufu mkubwa wa nyumba hizo.

“Pamoja na fedha kidogo tunazopata lakini bado tuna tatizo la ukosefu wa makazi wa nyumba za askari, lakini bado Serikali inatafuta fedha ili kuhakikisha changamoto hiyo inaisha,” alisema Lugola. Pia Lugola alisema changamoto nyingine inayowakabili askari wa vyombo vyake ni kutopata fedha za kuhamishwa na atahakikisha madai yote ya askari hao yanafanyiwa kazi. 

Lugola alisema jambo ambalo linamuumiza kichwa ni kuhusu madai ya askari na watumishi wa wizara yake ambayo anasema kama wafanyakazi hawatalipwa haki zao na utendaji wa kazi utapungua. Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kikazi na tayari amemaliza ziara yake Makao Makuu ya Mkoa na leo yupo Wilaya ya Arusha, na baadae ataenda Wilaya ya Meru, Arumeru, baadaye Longido, Monduli, Karatu na ataimaliza ziara yake akiwa Wilaya ya Loliondo mkoani humo.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Sehemu ya askari na watumishi raia wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola (hayupo pichani), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake, jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Askari wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Arusha, CP Meshaki akizungumza katika Mkutano aliouhitisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani). Askari huyo alimuomba Waziri huyo atatue changamoto mbalimbali zinazowakabili mkoani humo. Hata hivyo Waziri Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani), jijini Arusha leo, kuhusu masuala mbalimbali ya watumishi hao. Lugola aliwaagiza viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake wahakikishe wanawapandisha vyeo, wanarekebisha mishahara, pamoja na kulipwa fedha askari wote waliopo katika Taasisi zao. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Longinus Tibishubwamu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Na Felix Mwagara, MOHA-Arusha.

TTCL YAPEWA MWEZI MMOJA KUONGEZA UPATIKANAJI WA BIDHAA ZAKE VIJIJINI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye(Mb) amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation kuongeza juhudi katika kusambaza Huduma za Mawasiliano ili kuwafikia Wananchi wote katika pembe zote za Nchi,

Akizungumza na Menejimenti ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL katika ziara yake ya siku moja kukagua utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo, Mhe Nditiye amesema, Serikali inathamini mchango mkubwa wa Shirika hilo na inataka kuona jitihada zaidi zikichukuliwa katika kuboresha ufanisi wa Shirika na Sekta ya Mawasiliano Nchini.

“TTCL ni Shirika la Umma, Nawapongeza kwa yote mazuri mnayoyafanya na hasa kwa ubunifu wa huduma na gharama nafuu za huduma hizo kwa Wananchi, Huduma ya Video Conference imetoa matokeo mazuri sana, itaokoa muda na gharama kwa kuwawezesha Watendaji wa Serikali kuwasiliana bila kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine. Napongeza pia huduma ya malipo kwa kadi inayotarajia kuanza hivi karibuni, hizi ni juhudi ambazo Serikali inaziunga mkono.”

Pamoja na kupongeza juhudi za TTCL zilizowezesha Shirika hilo kuongeza mapato, idadi ya Wateja wake na wigo wa upatikanaji wa huduma Nchi nzima, Mhe Nditiye ametoa Siku 30 kwa Menejimenti ya Shirika hilo kuhakikisha kuwa linaondoa kero ya upatikanaji wa Vocha na Laini za simu(Simcards) katika maeneo mbalimbali Nchini.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Corporation Mhandisi Omari Nundu amesema, baada ya kufanya vyema katika mwaka 2018, TTCL imejipanga vyema kufanikisha malengo yake kwa mwaka 2019 ambapo limekusudia kuimarisha Idara na Vitengo vyake ili kuongeza viwango vya ubora wa huduma kwa Wateja sambamba na kutekeleza majukumu ya Shirika kwa Umma.

“Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa mwaka unaoishia Desemba 2018 inaonesha TTCL kuwa Shirika linalokuwa kwa kasi na kuongeza idadi ya Wateja na wigo wa huduma zake huku huduma za T PESA nazo zikistawi kwa kasi kubwa. Hadi kufikia Januari mwaka huu, T PESA ina Wateja zaidi ya laki tatu, Mawakala elfu kumi na moja na miamala ya takribani Tsh bilioni nne. Nikuhakikishie Mhe Naibu Waziri kwamba mwaka huu 2019 tutapata mafanikio zaidi kwa kuwa tuna mikakati thabiti itakayotupa matokeo mazuri”, amesema Mwenyekiti Nundu. 
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akizungumza jambo na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (Sekta ya Mawasiliano) akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation (hawapo pichani) alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati mbele) anayesimamia sekta ya Mawasiliano akisisitiza jambo kwa Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation (hawapo pichani) alipotembelea shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakitoka kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL. Kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Sekta ya Mawasiliano, Dk. Jim Yonaz, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Mhandisi Omary Nundu na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakiongozana na naibu waziri. 
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye anayesimamia Sekta ya Mawasiliano (mbele kushoto) pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation wakiwa na Naibu Waziri Nditiye mara baada ya kutembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano unaosimamiwa na Shirika la TTCL.
Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia mbele) akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega pamoja na Menejimenti ya Shirikisho la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Corporation alipotembelea miundombinu ya mkongo wa taifa wa mawasiliano inayosimamiwa na Shirika la TTCL.

MAPIGANO DHIDI YA KUNDI LA KUNDI LA IS YAPAMBA MOTO SYRIA

$
0
0
Na Ripota  Wetu.

WANAMGAMBO wa itikadi kali wanaojiita "Dola la kiislam"-IS wamejaribu kuiokoa ngome yao ya mwisho mashariki mwa Syria huku wake na watoto wao wakiyapa kisogo mapigano makali katika eneo hilo.

Vikosi vya wanamgambo wa kiarabu na kikurdi vinavyopigania kidemokrasi nchini Syria, SDF vimeanzisha opereshini kubwa jumamosi iliyopita kwa lengo la kuwatimua wapiganaji wa dola la kiislam , IS au Daesh kutoka ngome yao ya mwisho miongoni mwa ngome walizokuwa wakizizidhibiti tangu mwaka 2014 nchini Syria na Iraq.

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia mnamo siku za hivi karibuni kutoka kile kinachojulikana kama eneo la Baghouz", karibu na mpaka wa Iraq, wengi wao ni wanawake na watoto, ingawa wanamgambo wa itikadi kali pia ni miongoni mwao.

Taarifa ya Mwandishi Hamidou Oummilkheir/AFP ambayo imehaririwa na Iddi Ssessanga imesema kuwa tangu Desemba mwaka jana zaidi ya watu 38, 000, wengi wao wake na watoto wa wapiganaji wa itikadi kali wameyakimbia maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na IS.

"Tumevikomboa vituo kadhaa vilivyokuwa hapo awali vikidhibitiwa na IS". msemaji wa vikosi vinavyopigania demokrasi nchini Syria, SDF, Mustafa Bali amesema.Shirika la Syria linalosimamia masuala ya haki za binadamu limesema wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani wanasonga mbele kidogo kidogo. 

"Miripuko imetegwa kila mahala katika eneo hilo" amesema kiongozi wa shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza, Rami Abdul Rahman.Vikosi vinavyopigania demokrasia nchini Syria SDF vimeanzisha opereshini ya kijeshi kuwatimua wapiganaji wa itikadi kali wa Is toka mkoa tajiri kwa mafuta wa Deir Ezzor tangu Septemba mwaka jana na kwamba tangu wakati huo zaidi ya wapiganaji 1300 wa SDF na wanajihadi 650 wameuliwa huku raia zaidi ya 400 wakipoteza pia maisha yao.

Rais Donald Trump wa Marekani aliashiria uwezekano kwa vikosi vya muungano kutangaza ushindi mnamo siku chache zinazokuja dhidi ya IS. Ushindi wa vikosi hivyo katika kijiji cha Baghouz utaiwezesha Marekani kuwahamisha wanajeshi wake 2000 kutoka Syria, kama alivyotangaza rais Trump decemba mwaka jana.

"Tunaambatana na wakati ili kuweza kuheshimu ahadi tuliyotoa" amesema kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alipokuwa ziarani nchini Iraq jana bila ya kutaja lini hasa wanajeshi wa Marekani wataondolewa Syria. CHANZO DW .

Balozi Seif ashiriki mkutano wa Mbunge Shinyanga

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema Viongozi pamoja na Vijana wa CCM wakati Taifa wakati huu linakaribia kuingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hawana muda wa kujiingiza katika Siasa za Makundi ambazo zikiendekezwa zinaweza kupunguza nguvu za Chama hicho.

Alisema Katiba ya Chama imeweka wazi kwamba CCM lazima ishinde  wakati wa Uchaguzi na pale inapobainika kuwepo kwa Mwanachama au kiongozi wa CCM kakataa kumpigia kura Mwanachama mwenzake kwa sababu tu sio chaguo lake kwenye mchakato wa kura za Maoni, huo utaeleweka kuwa ni usaliti.

Balozi Seif  Ali Iddi alitoa kauli hiyo alipokaribishwa katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mh. Steven Julius Masele alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kipindi cha Miaka Mitatu zilizofanyika katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.

Mkutano huo ulikwenda sambamba na maadhimisho ya Sherehe za Kutimia Miaka 42 tokea kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi uliojumuisha pia uwepo wa Viongozi na Wanachama wa CCM wa Majimbo pamoja na Wilaya nyengine zilizomo ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Balozi Seif ambae ni Mlezi wa Mkoa huo wa Shinyanga na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Wana CCM  hao kwamba Chama kinahaki ya kumfukuza Uanachama Mwanachama ye yote mwenye hulka kama  hiyo inayofanana na yule mwenye tabia ya kuvaa sare ya kijani na manjano wakati wa mchana na kubadilika nyakati za usiku.

Ameupongeza ushirikiano wa pamoja wa Wabunge wote wa Majimbo ya Wilaya zilizomo ndani ya Mkoa wa Shinyanga kwa kazi kubwa wanazozifanya za kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya CCM  ambazo zimekuwa zikishuhudiwa na Viongozi pamoja na Wananchi wa Majimbo yao.

Balozi Seif  akiwa Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga aliahidi kwa nafasi ya kipekee kumsaidia Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mh. Steven Julius Masele popote atakapokwama ili kumuongezea nguvu alizozielekeza kwenye Jimbo lake katika dhana nzima ya kuwatumikia Wananchi Wapiga kura wake.

Akizunguzungumzia suala la wahisani Mlezi huyo wa Mkoa wa Shinyanga alisema Taifa  lazima lifikie wakati kuwa na uwezo wake kamili wa kujitegemea ili kuwepuka misaada na Mikopo ya Wafadhili yenye muelekeo wa Masharti yasiyotekelezeka.

Balozi Seif alisema yapo masharti ya Mikopo na Misaada inayotolewa na baadhi ya Wafadhili ambayo mengine imekuwa ikishuhudiwa kulenga kwenda kinyume na Mila, Silka na Utamaduni wa Taifa.

Mapema akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Kipindi cha Miaka Mitatu iliyopita ndani ya Jimbo la Shinyanga Mjini, Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Steven Julius Masele alisema yale aliyoahidi katika kipindi cha Kampeni za Uchaguzi tayari ameshayatekeleza kwa asilimia kubwa.

Mh. Masele alisema miradi ya Jamii kama huduma za Afya pamoja na  Elimu katika Kata na vijiji mbali mbali vya Jimbo hilo imepata msukumo mkubwa kutokana na Wananchi wenye kujitolea katika kuianzisha kasi iliyomtia ari ka kuchangia nguvu za uwezeshaji.

Alisema ipo miradi ya Maendeleo ya kiuchumi kama bara bara imetekelezwa ndani ya kipindi cha Miaka Mitatu na kuwezesha kuwaondoshea usumbufu wa huduma za mawasiliano ya Usafiri Wananchi wake mbali na ile mikubwa inayotengewa Bajeti ya Serikali Kuu.

Mh.Masele alifafanua kwamba zaidi ya shilingi Milioni 36.3 zimetumika kuchangaia nguvu za  kuendeleza miradi ya Wananchi na kuahidi kusimamia kazi ya kuifanya Shinyanga mpya inayolengwa kuelekea katika  hadhi ya Mji wa Paris.

Mapema asubuhi mlezi huyo wa Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya kulizindua Shina la Wakereketwa wa Umoja wa Vijana wa CCM la Japanes Coner  kwa kupandisha Bendera.

Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bibi Haula Kachomba alisema Mashina kama hayo yalikuwa yamepotea na Chama cha Mapinduzi ngazi ya Mkoa kimeamua kuyafufua tena Mashina yake kwa kukumbuka kuwa ndio nguvu ya Chama.

Uzinduzi huo ulikwenda sambamba pia na Balozi Seif  kuwatembelea Wanashina la Wakereketwa wa CCM  Nambari Tatu la Mtaa wa Mkongo lililokamilisha safu ya Uongozi na kuwapongeza kwa uamuzi wao wa kujikusanya pamoja mbali ya kuimarisha chama lakini pia husaidia kuchangia ubunifu wa miradi ya kujikidhi Kiuchumi.

Baadae Balozi Seif  alishiriki kazi za ujenzi wa Taifa na kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa  Jeile la zamani lililovunjwa kutokana na kukosa ubora wa Majengo yanayopendekezwa na Chama.

Katika kuendeleza jengo hilo mbali ya Balozi Seif kuchangia Shilingi Milioni Moja lakini Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi alitoa wazo la kufanywa mchango wa papo kwa papo kwa waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ofisi hiyo ya CCM.

Wazo la Mama Asha liliweza kuibua Mchango wa Shilingi Milioni 1,208,000/- Taslimu, ahadi ya fedha taslim shilingi Laki Tano, ahadi ya Saruji inayokadiriwa kufikia Paketi 180 kutoka kwa Waheshimiwa Wabunge, Viongozi tofauti pamoja na Wananchi binafsi.
 Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Kichama Balozi Seif Ali Iddi akipandisha Bendera kuashiria kulizindua Shina la Wakereketwa wa Umoja wa Vijana wa CCM la Japanese Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga.
 Balozi Seif na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi wakijenga kuashirika kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Chama cha Mapinduzi ya Kata ya Kitangili Mjini Shinyanga.
 Mke wa Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Kichama Mama Asha Suleiman Iddi akihamasisha Wana CCM Kuchangia ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kitangili Mjini Shinyanga uliopelekea kupatikana kwa Shilingi Milioni 1.2  na ahadi ya saruji Mifuko 180.
 Kikundi cha Wasanii cha Mabawa ndani ya Manispaa ya Shinyanga mjini kikitoa Burdani kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mh. Steven Julius Masele wa uwasilishaji wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha Miaka Mitatu.
 Balozi Seif akimpokea Mkereketwa wa Chama cha Demokrasia ya Maendeleo {CHADEMA} Nd. Singu aliyeamua kukihama chama hicho na kuomba kujiunga na CCM.
 Wanachama Wapya 347 wa CCM wa Jimbo la Shinyanga Mjini wakila kiapo cha uaminifu baada ya kukabidhiwa Kadi za Wanachama Wapya wa Chama hicho katikwa Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga.
Balozi Seif  akimlisha Keki Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Nd. Mabala Mlolwa kusherehekea Chama cha Mapinduzi kutimia Miaka 42 katika Uwanja wa Zimamoto Mjini Shinyanga. Wa Kwanza kutoka Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Steven Julius Masele. Picha na – OMPR – ZNZ.

MAVUNDE AWATOA MACHOZI AKINA MAMA WAJAWAZITO WA DODOMA MJINI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewatembelea wakina mama wajawazito katika vituo vya afya na zahanati katika Jiji la Dodoma na kutoa msaada wa vifaa vya kujifungulia.

Baadhi ya vifaa hivyo ni Delivery Pack 350 yenye thamani ya Sh.milioni saba, mashuka 100 yenye thamani ya Sh.milioni 1.1, pakiti 40 za dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Sh.milioni moja, na Carton 30 za Maji ya Kunywa ambapo msaada huo umesababisha uwepo wa furaha kubwa kwa wakina mama wajawazito na kushindwa kuficha hisia zao na kudondosha machozi ya furaha.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi msaada huo Mavunde amesema ameamua kutumia siku ya leo ya Februari 14,2019 kuonesha upendo kwa wakina mama hao wa Dodoma kwa kusaidia vifaa hivyo muhimu wakati wa kujifungua na hiyo ni  shukrani anayoirudisha kwa mama zake hao kutokana na upendo wao mkuu.

Akimshukuru Mbunge Mavunde kwa msaada huo mkubwa,Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dk.Gatete Mahava amemuomba Mbunge Mavunde kuendelea kusaidiana na Serikali kutatua changamoto katika sekta ya Afya hasa katika kituo cha Afya cha Makole ambacho kimefanyiwa upanuzi mskubwa baada ya kukamilika ujenzi wa wodi ya wakina mama kupitia fedha kiasi cha Sh.milioni 500 zilizotolewa na Serikali ya Rais Magufuli katika Ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya.

Katika tukio hilo Mavunde aliambatana na viongozi wa CCM Wilaya,Mbunge wa Viti Maalum Bura, madiwani wa Kata,Wasaniii na Mama Lishe wa Soko kuu Majengo.
Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vitu kwa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.

Baadhiya vifaa mbali mbali vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde kwa akina mama Waja wazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde na ujumbe wake akiwasili kwenye moja ya zahanati jijini Dodoma kukabidhi baadhi ya vitu kwa akina Mama wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia (Delivery Pack)350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa. 

Pichani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo akikabidhi baadhi ya vifaa mmoja wa akina mama mara baada kuwatembelea akina mama hao wajawazito katika vituo vya Afya na Zahanati Jijini Dodoma na kutoa Msaada wa Mifuko ya Vifaa vya kujifungulia*(Delivery Pack) 350 yenye thamani ya Tsh 7m,Mashuka 100 yenye thamani ya Tsh 1.1m ,Pakiti 40 za Dawa aina ya Dinoprostone zenye thamani ya Tsh 1m na Carton 30 za Maji ya Kunywa.
Picha ya pamoja

Kampeni ya “FURAHA YANGU” yatekelezwa vyema na watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.Prisca Shewali akifanya kipimo cha VVU katika zoezi la upimaji wa afya lililokuwa likifanyika leo katika Ofisi za Wizara kwa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” kushoto ni Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Makole Jijini Dodoma Hadasa Haruni. 
 Afisa  Bunge Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Francis Songoro akifanya kipimo cha VVU katika zoezi la upimaji wa afya lililokuwa likifanyika leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma kwa utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” kushoto ni Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Makole Bibi.Hadasa Haruni.
 Katibu Muhtasi Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Bibi.Niuka Chande akipima Shinikizo la Damu wakati wa zoezi la upimaji wa afya  kwa watumishi wa wizara kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU” lililokuwa likiendelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma na wataalamu kutoka Hospitali ya Makole (kushoto ) Daktari Janeth Mtenga.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika foleni ya kupima afya zao wakati wa zoezi la upimaji wa afya kazini kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa alipozindua Kampeni ya “Furaha YANGU”  lililokuwa likiendelea leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma. Na Anitha Jonas – WHUSM

MABULA AAGIZA WANANCHI KWIMBA KUPATIWA VIWANJA NDANI YA MIEZI MITATU

$
0
0
Na Munir Shemweta, KWIMBA
Naibu Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza kuwapatia viwanja ama fedha wananchi 44 waliotakiwa kupatiwa viwanja katika eneo la Ngungumalwa wilayani humo ndani ya miezi mitatu na wasipotekeleza waliohusika katika suala hilo watawajibishwa.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo jana tarehe 13 Januari 2019 katika wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza akiwa katika ziara yake ya kuhamasisha ulipaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi katika kanda ya Ziwa.

Aidha, ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kufanya uchunguzi wa kiasi cha fedha takriban milioni 74 zilizotolewa na wananchi kwa ajili ya kupimiwa na kupatiwa viwanja eneo la Ngungumalwa ambazo hazikutumika kwa kazi hiyo ili kubaini zilitumika katika mazingira gani tofauti na malengo yaliyokusudiwa.

Dkt Mabula alisema iwapo wananchi hao hawatapatiwa viwanja ama kurudishiwa fedha zao ndani ya muda wa miezi mitatu aliotoa basi wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine watawajibishwa ili kurudisha imani kwa wananchi.

‘’Kuchukua fedha za wananchi bila kupatiwa maeneo kunawafanya kukosa imani na serikali yao na mimi sitakubali kuona wananchi wakidhulumiwa haki yao na halmashauri ya Kwimba ina wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapatiwa maeneo haraka iwezekanavyo’’ alisema Mabula.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kwimba Pendo Malabeja alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi kuwa halmashauri yake ilishaanza kuwalipa baadhi ya wananchi ingawa hakuainisha kiasi na idadi ya wananchi waliolipwa na kubainisha kuwa suala hilo bado linaendelea kufanyiwa kazi.

Vile vile, Dkt Mabula ameitaka halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kupanga na kupima maeneo yote ambayo yanakuwa kwa kasi na kuacha kujikita katika zoezi la uarasimishaji ambapo alifafanua kitendo cha kuacha kupanga na kupima maeneo yanayokuwa kwa kasi kutasabaisha ujenzi holela.

Aliongeza kuwa, Wilaya ya Kwimba iko nyuma sana katika kupima na kupanga maeneo jambo linaloifanya halmashauri hiyo kushindwa kujikusanyia mapato mengi kupitia sekta ya ardhi ambapo alitolea mfano wa jiji la Dodoma kuwa limekuwa likoongoza katika ukusanyaji mapato ya serikali ambapo mengi yanatokana na kupima na kuuza viwanja.

Ameitaka halmashauri hiyo kijipanga vizuri na kuitumia Ofisi ya Ardhi Kanda ya Ziwa pamoja na halmashauri jirani kama Misungwi kusaidia katika zoezi la kupima viwanja ili kuhakikisha linapanga na kupima maeneo mengi sambamba na kuwa na mji uliopangika huku ikijiongezea mapato.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Senyi Ngaga alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa wilaya yake ilikuwa nyuma katika masuala ya ardhi lakini sasa wamejiwekea mkakati maalum kuhakikisha inakuwa na maeneo mengi yalipangwa na kupimwa na suala la kwanza ni kuhakikisha idara ya ardhi inapatiwa fedha ya kutosha kwa nia ya kufanya kazi zake kwa ufanisi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo (wa pili kulia) wakati alipofanya ziara katika halamashauri ya wilaya ya Kwimba kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Senyi Ngaga.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati alipofanya ziara katika halamashauri hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Senyi Ngaga na wa kwanza kulia ni Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba Pendo Malabeja.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua majalada katika masijala ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati wakati alipofanya ziara katika halmashauri hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua moja ya majalada katika masijala ya ardhi ya halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati wakati alipofanya ziara katika halamashauri hiyo kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza wakati wakati alipofanya ziara katika halamashauri ya wilaya ya Kwimba kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Senyi Ngaga.

KAMPUNI YA JERVOIS YAONESHA NIA KUWEKEZA KABANGA

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Wawakilishi wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika mradi wa Nikel- Colbat, Kabanga.  
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko ameendelea kusisitiza kuhusu kufuatwa kwa Sheria na taratibu kwa wenye nia ya kuwekeza katika Sekta ya Madini na kueleza kuwa, kwa upande wa Wizara, inafanya jitihada za kuondoa urasimu kwenye uwekezaji katika sekta husika.

“ Tunataka mwekezaji mwenye nia anapoonesha dhamira ya kuwekeza baada ya taratibu zote kukamilika basi aanze mara moja,” amesema Waziri Biteko. Akizungumza katika kikao hicho mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo Balozi Mstaafu Andrew Mcalister, amesema kuwa, nchi ya Tanzania inaweza kuwa mzalishaji mkubwa wa madini ya Colbat kutokana na ubora wake na mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini ikiwemo uwazi.
Mbali na Waziri Biteko, wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na wataalam wengine wa wizara.
 Waziri wa Madini Doto Biteko (kulia) akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia   Balozi Mstaafu Andrew Mcalister (katikati). Kushoto ni Naibu Waziri Stanslaus Nyongo. Wengine ni wawakilishi wa kampuni hiyo.
 Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jervois Mining Limited ya Australia Brye Croker.
Baadhi ya Wataalam wa Wizara ya Madini wakifuatilia kikao baina ya Waziri wa Madini na wawakilishi wa kampuni ya Jervois Mining Limited.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images