Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

VICHEKESHO VYA MIZENGWE SI MCHEZO, WAWAVUNJA MBAVU WALIOHUDHURIA KONGAMANO LA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

KUNDI la vichekesho la Mizengwe linaloundwa na watu limewavunja watu mbavu kutokana na vichekesho vyao walivyokuwa wanavitoa katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wasanii hao wa vichekesho ambao wapo watano leo baada ya kupanda jukwaani walisema kuwa wamefika wanne kwani mwenzao mmoja amekwenda nchini India kwa ajili ya mazungumzo na Amitha Bachan.

Kitendo cha kueleza mwenzao yupo nchini India na anamazungumzo na Amitha Bachan watu waliokuwa ukumbini waliangua kucheka kwa sauti kubwa.

"Kundi la Mizengwe linaundwa na watu watano,ila leo mwenzetu mmoja anayefahamika kwa jina la Mzee Matata amekwenda India kuzungumza na Amitha Bachan.Hivyo tupo sisi tu," amesema  mmoja wa wasanii hao...watu kicheko.

Hata hivyo Mchekeshaji wa kundi hilo Rashid Coster a.k.a Mkongoman aliamua kutoa vichekesho vya aina yake na aliwavunja mbavu watu baada ya kusema kwao muhimu ni kuvaa kwani kula nani anakuona.

"Kwetu sisi Wasanii kula sio jambo muhimu sana kwani tumbo halina kioo lakini kuvaa ndio muhimu sana kwani nguo ndio zinaonekana," amesema Mkongaman.

Kwa upande wake Mwanadada pekee katika kundi hilo la Mizengwe Jesca alitumia nafasi hiyo kwa kutumia sanaa yake ya uigizaji kuzungumzia athari za dawa za kulevya.

Amesema wanaotumia dawa za kulevya hata ndoto za maisha yao zinatoweka na hivyo kuwaomba Watanzania na hasa wa wasanii kwa ujumla kuacha kutumia dawa za kulevya.

WASANII WA FANI MBALIMBALI WAFURIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE DAR ...BURUDANI KAMA KAWAIDA YAO

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WASANII mbalimbali nchini wamejitokeza kwa wingi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam ambako kunafanyika Kongamano linalohusu elimu ya athari za dawa za kulevya.

Kongamano hilo limeandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo kabla ya kuanza rasmi kwa kongamano hilo wasanii wa fani mbalimbali waliendelea kutoa burudani kwa wageni walioko ukumbini hapo.Kwa lugha ya mjini Kongamano la dawa za kulevya linalohusu kuzungumzia athari za dawa za kulevya limenoga.

Mwanamuziki Charles Baba na Kalala Junior ni miongoni mwa wanamuziki ambao wameonesha umahiri wao wa kuimba ambapo mashairi ya wimbo wa Kuachwa ulionekana kupagawisha wageni waalikwa kiasi cha kushindwa kuficha hisia zao.

Charles Baba wakati anaanza kuimba aliamua kutoa burudani ya vichekesho alivyokuwa anafanya lakini alipoamua kuimba shangwe zililipuka ukumbini hapo.

Moja ya eneo ambalo liliwafurahisha walioko ukumbini hapo ni pale alipokuwa anaimba hivi "Kuacha kuachwa ...kuachwa ni shughuli pevu...mbaya zaidi kwa yule uliyempenda...wewe unakonda...yeye ananenepa kwa mawazo..."

Hata hivyo katika kunogesha wimbo huo Charles Baba akasema "Ukitaka kufaidi mapenzi ni vema ukampata mwanamke anayedaiwa kodi ya nyumba." Waliokuwa ukumbini kicheko cha nguvu.

Mbali ya Charles Baba na Kalala kutoa burudani ,wasanii wengine wakiwamo wa mashairi na ngoma za asili walitumia fursa hiyo kuonesha umahiri wao.

Wakati huo huo wanamuziki wa nyimbo za Injili nao hawakuwa nyuma kutokana na kutumia nafasi hiyo kuimba nyimbo za Injili ambazo zilikuwa zinavuta hisia za walio wengi hasa wenye imani ya dini ya Kikristo.Hata hivyo kila msanii alikuwa anatoa ujumbe unaozuia matumizi ya dawa za kulevya.

Mwanamuziki Stara Thomas aliamua kuimba wimbo unaozungumzia athari za dawa za kulevya ambapo kiitikio cha wimbo huo ulisema wasanii bila ya dawa za kulevya inawezekana.Kongamano hilo ndio kwanza limeanza na Michuzi Blog itaendelea kukujuza kila kinachoendelea ukumbini hapo.

YALIYOJIRI KATIKA ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE DAVID KAFULILA WILAYANI ILEJE

$
0
0


 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akitembea kukagua kaya zinazonufaika na Mpango wa TASAF katika Kijiji cha Ilulu Wilayani Ileje ili kujionea utekelezaji wa mpango huo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje ambapo amewasisitiza kutimiza majuku yao na kutii sheria na kanuni za utumishi wa umma.
2
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila ambaye amewasisitiza kutimiza majuku yao na kutii sheria na kanuni za utumishi wa umma.
4
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akikagua baadhi ya nyaraka katika Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji cha Ilulu Wilayani Ileje wakati akikagua utekelezaji Mpango wa TASAF katika Kijiji hicho.


……………….

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amefanya ziara Wilayani Ileje ambapo ameanza kwa kuzungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo, amekagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ileje na kutembelea kaya za Wanufaika wa Mpango wa TASAF ambapo haya ndiyo yaliyojiri;
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila amekuja kuwakumbusha sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma kwakuwa yeye ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma Mkoa wa Songwe- Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki
Napenda kuwakumbusha watumishi wote kuheshimu mamlaka zilizopo Kisheria na kuzingatia sheria zote za utumishi wa umma – Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Utumishi, Chele Ndaki

iii. Watumishi hakikisheni kuwa mnatimiza majukumu yenu wakati mnadai maslahi yenu yaani kama kuna mambo mnadai sio sababu ya kuweka uzembe katika utumishi wenu- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila .

Tulisaini Mkataba wa utumishi kwenye sekta za elimu na afya kwa kuwekeana vigezo ambavyo vitapimwa mwezi huu wa pili na mwezi wa tatu tutafanya tathmini, wale watakao shindwa kufikia vigezo hivyo tutawaondoa ili wawekwe wengine ambao watafanya vizuri – Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila

Kwa mujibu wa sheria za utumishi zinaruhusu mtumishi aliyeshindwa kutimiza wajibu wake kufukuzwa kazi au kunyang’anywa cheo, sio mpaka uibe – Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila
Kama taasisi wote tunatakiwa kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa kazi zetu, kama Mkoa tumeanzisha mfumo wa kupima utendaji wa watumishi unaoitwa Songwe Task Information Management System, kwa mfumo huu tutakuwa wa kwanza kuutumia nchini na utawezesha kufahamu utendaji wa kila siku wa watumishi wote- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila

vii. Mtendaji yeyote atakaye shindwa kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli la kuhakikisha kila mjasiriamali mdogo anapatiwa kitambulisho, hususani kwa kipindi kilichobaki cha wiki tatu, hilo ni kosa ambalo linatosha kumfukuzisha kazi- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila

viii. Ujenzi katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje Umesitishwa mpaka hapo kasoro zilizooneka zirekebishwe, awali ili ripotiwa kuwa kwenye beam kuna ufa na kusababisha mpasuko kwa ndani na Kupinda lakini tumekagua na kubaini sehemu ya juu imetitia kwa ndani, hili ni tatizo kubwa kuliko lilivyo ripotiwa awali- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila .

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje ahakikishe waliohusika wote na ujenzi mbovu katika Hospitali ya Ileje popote pale walipo watafutwe na wachukuliwe hatua kali lakini pia Mkurugenzi ahakikishe ifikapo Juni 30, 2019 fedha zilizoletwa na serikali shilingi Bilioni 1.5 ziwe zimetumika kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kurekebisha maeneo hayo yenye dosari -Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila.

Kuna umuhimu mkubwa wa kurekebisha makossa hayo yaliyojitokeza na kuendeleza ujenzi bila kufanya hivyo kunaweza kusababisha maafa yaani jengo hili kuanguka, Makosa yaliyofanyika ni ya design ndio maana eneo lililotitia limesababishwa na uzito wake wenyewe hivyo huwezi kuendelea na ujenzi wa ghorofa hili la hospitali- Meneja wa TARURA Wilaya ya Ileje Mhandisi Lugano Mwambingu.

Tunakiri hatukuona matatizo hayo mapema ila nia yetu ni kuhakikisha marekebisho hayo yanatekelezwa, jambo hili limetuathiri kwani nasi tulitarajia ghorofa hili likamilike ili wananchi wetu wanufaike na huduma katika hospitali hii- Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome

xii. Katika ziara hii pia nimebaini kuwa Kuna tatizo la serikali la vijiji kuendeshwa kwa kutofuata taratibu hasa kutofanya mikutano ya vijiji na kutotunza kumbumbuku za vijiji licha ya kuwa serikali imeajiri watendaji wenye diploma – Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila

xiii. Nawaagiza wakurugenzi wote Mkoa wa Songwe wafuatilie utendaji wa serikali ngazi ya vijiji, ili mapato na matumizi yabandikwe, vikao vya kisheria vifanyike na kuwepo file la mihtasari ya vikao vyote vya kijiji kwakuwa haya ni matakwa ya kisheria – Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila

xiv. Wajibu wa Halmashauri na waratibu wa TASAF ni kuhakikisha fedha zinawafikia walengwa na hakuna kaya hewa aidha wakaguzi wa ndani wakague fedha za TASAF kama mfuko maalumu tofauti na sasa wanavyofanya ukaguzi wa jumla ukizingatia hizi ni fedha nyingi kwani serikali kwa mkoa wa Songwe ni imetoa zaidi ya bilioni 14 kwa mpango huo- Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila 

Halmashauri itaendelea kusimamia watendaji wa vijiji na kata ili watimize majukumu yao kisheria, tumekuwa tukiwachukulia hatua watendaji ambao hawatimizi majukumu yao na tutaendelea kufanya hivyo – Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Joseph Mchome

xvi. Tunashukuru mpango wa TASAF kwakuwa umetukomboa kimaisha, ijapokuwa mimi ni mjane nimeweza kupata mbolea na chakula kupitia fedha za TASAF, hivyo nawashukuru sana walio anzisha mpango huu-Hana Mtawa Mkaji wa Kijiji cha Ilulu, Ileje na Mnufaika wa TASAF

WAZIRI LUGOLA AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI ARUSHA

$
0
0



 
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola
 
Na. Vero Ignatus, Arusha

WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi,Kangi Lugola amelitaka Jeshi la Polisi nchini kushirikiana na mamlaka ya ya Mawasiliano nchini TCRA,ili kuweza kuwabaini wale wote wanaovunja Amani ya nchi,kwa kutumia njia ya Mtandao.

Ameyasema hayo Jijini Arusha Wakati akiwa katika ziara yake ya siku nane,lengo likiwa ni kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza maoni ya wananchi juu ya Usalama anaousimamia.Lugola amesema kuwa kwa sasa nchi ina Amani ya Kutosha na hivyo asitokee mtu wa kuvuruga Amani hiyo.

Aidha waziri Lugola ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi ,katika ufanisi wa kazi zao za kulinda raia na mali zake.Amesema mitandao ya kijamii inaweza kutumika kuleta maendeleo badala ya kuchochea Uvunjifu wa Amani.

Waziri Lugola yupo mmkoani Arusha ambapo anatarajiwa kufanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea Wilaya zote Saba za Mkoa wa Arusha.

KAMPENI YA TBS YAWAFIKIA WANANCHI WA TARIME NA RORYA

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Kampeni yake katika Wilaya ya Tarime na Rorya ya kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika Maeneo ya Soko jipya la REBU,Stendi ya Tarime Mjini,Mnada wa Mtana na maeneo mengine ya Halmashauri ya Mji na Wilaya.

wananchi walijitokeza kupata elimu sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.Kwa upande wake Afisa Udhibiti ubora, Mhandisi Paul Ndege amezidi kuwakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote, Hivyo,wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko lao na kuhakikisha wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali kama nafaka,sabuni, maziwa,asali na unga lishe,juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS na kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.

Wajasiriamali wengi walionyeshwa kufurahishwa na elimu waliyoipata na kushukuru TBS kwa kuja kutoa elimu hiyo ambayo itawapa matokeo yenye tija kwenye shughuli zao za uzalishaji.Semina hii ilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime

Kampeni hii inaendelea Wilaya ya Nyamagana .

 TBS ikiendelea na kampeni ya elimu kwa umma katika shule ya msingi Nyamisangura na Shule ya sekondari Sirari Wilayani Tarime.
 Afisa Udhibiti Ubora,Mhandisi Paul Ndege akiwaelekeza wajasiriamali  utaratibu  wa kupata leseni ya ubora ya TBS bila gharama yoyote,katika semina iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri Wilayani Tarime.
 Pichani ni Mhandisi Paul Ndege, Afisa Uthibiti Ubora akitoa somo kwa mjasiliamali kuhusu umuhimu wa kuuza bidhaa zilizothibitishwa na TBS
Mhandisi Paul Ndege akiendelea na semina ya Elimu kwa Umma juu ya kutambua Bidhaa hafifu Mjini Mara.

UKOSEFU WA MAENEO YA KILIMO UNACHANGIA LISHE DUNI MISENYI

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus – Misenyi, Kagera. 

Kufuatia Uzinduzi wa Kampeni ya Lishe na Usindikaji kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mbali mbali Wilayani Misenyi, imegundulika kuwa sababu nyingine inayopelekea uwepo wa lishe duni kwa baadhi ya kaya Wilayani humo, ni kutokana na ukosefu wa maeneo ya kutosha kwa ajili ya shughuli za kilimo na uzalishaji. 

Kampeni hiyo iliyozinduliwa rasmi mapema Februari 11 Mwaka huu na Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi kupitia mradi wa urejeshaji hali kwa maeneo yaliyokumbwa na majanga Mkoani Kagera, unaotekelezwa chini ya Shirika la Chakula Duniani “FAO” Wilaya ya Misenyi ikiwa ni miongoni mwa Wilaya tano zenye wahanga, Imebainika kuwa ukiacha sababu za Tetemeko, Mvua, Magonjwa ya mimea na mazao, pia sababu nyingine ni ukosefu wa sehemu ya kutosha kufanya shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uzalishaji kwa baadhi ya maeneo lengwa. 

Kijiji Nkerenge kilichopo Kata Mtukula Wilayani Misenyi ni miongoni mwa Vijiji vilivyolengwa kufikiwa na mradi huo, licha ya kubainika kuwa Kaya 68 kati ya 720 Zinazopatikana Eneo la Mkagando, hazina sehemu ya kutosha kufanya shughuli za kilimo kufuatia changamoto kubwa ya Uwepo wa Kitalu namba 19, kinachomilikiwa na NARCO. 

 Bwana Martin Adam (58) Mkazi wa Kijiji Nkerenge eneo la Mkagando, ni mhanga wa mgogoro huo wa Ardhi kati ya NARCO na wananchi hao ambae anasema kuwa awali kabla ya kitalu hicho walikuwa na mashamba ya kutosha kuweza kulima mazao mbalimbali, tofauti na sasa baada ya kuhamishwa maeneo yao na kupewa heka mbili mbili kwa kila kaya, hivyo mazao mengine ambayo walizoea kulima kama mazao ya mbogamboga, kwa sasa yamepotea kulingana na ardhi kuwa finyu. Hivyo Bwn Martin anapeleka kilio chake kwa Serikali kuwatenegea maeneo ya kutosha ili kuweza kuzinusuru kaya hizi nazo ziweze kukabiliana na Utapiamlo na magonjwa yanayoweza kuvikabili vizazi vyao kufuatia ukosefu wa lishe bora. 

Kwa mujibu wa ripoti ya Kaimu Mratibu wa mradi huo Ndg, Amoni Lugeiyamu, anasema kuwa Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji wamelenga kuvifikia Vijiji vinne Wilayani humo ambavyo ni Nyankere, Nkerenge, Minziro na Kikono, huku ikiwa tayari mafunzo hayo yamekwishawafikia wanavikundi wa Vijiji vitatu vya Nkerenge, Nyankere na Minziro na yatahitimishwa katika kijiji cha kikono Kata Buyango Wilayani Misenyi. 

Vijiji hivi kupitia mradi wa urejeshaji hali unaofadhiliwa na FAO tayari vimegawiwa Mbegu (vipando), kuku na vifaranga vya Samaki, maharage yenye virutubisho aina ya Jesca, na sasa Kampeni hii inalenga kuwajengea uwezo wa kuzalisha na kusindika mazao yanayopatikana kupitia mavuno ya Vpando na Mbegu walizogawiwa awali. 

Kutokana na mazao hayo tayari Vikundi vimejengewa uwezo wa kutengeneza vyakula mbalimbali kwa ajili ya lishe bora, ikiwemo uji wa lishe, keki, andazi, supu ya maharage, uji wa unga wa maharage, pilau la maharage, pilau la viazi lishe na maharage n.k
 Pichani ni chungu cha pilau ya Viazi Lishe na Maharage kikiendelea kupikwa baada ya somo katika Kampeni ya Lishe na Usindikaji Mutukula.
Ndugu Amoni Lugeiyamu akitoa ufafanuzi kwa Vikundi vya Wakulima na wafugaji kuhusu Kampeni ya Mafunzo ya Lishe na Usindikaji, katika Kijiji cha Minziro Wilayani Misenyi
Martin Adamu Mkazi wa Mkagando Kijiji Nkerenge ni mmoja kati ya kaya 68 zilizoathiriwa na Kitalu namba 19, na kusababisha ukosefu wa Lishe Bora kwenye familia yake, kufuatia ufinyu wa ardhi kwa shughuli za Kilimo
Fredrick Kitone Mkulima na Msindikaji wa Vyakula akiendelea na somo la Mapishi ya keki itokanayo na Viazi Lishe, Wakati wa mafunzo ya Lishe na Usindikaji Mutukula Misenyi
 Pichani ni Bi Frola Paul Mkazi wa Minziro akimywesha uji mwanae Mara baada ya kupata mafunzo ya upikaji Lishe ya Uji wa Maharage ya Jesca.

SERIKALI YAZITAKA HOSPITALI BINAFSI KUCHANGIA GHARAMA ZA DAMU

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua idadi ya Wananchi waliofika kupata huduma wakati alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua jokofu la kuhifadhia sampuli ya Damu pindi alipofanya ziara katika Mpango wa Taifa wa Damu salama jijini Dar es salaam. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Mashine yakupima Sampuli za Damu, Mpango wa Taifa wa Damu salama, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu. 
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo wakati akiongea na Watumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama, alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu katika taasisi hiyo. 
Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo, akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt.Faustine Ndugulile (hayupo kwenye picha) wakati wa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu. 
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kumaliza ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma na kuangalia mashine mpya za kielektroniki za kupima sampuli ya Damu.
………………………. 


Na WAMJW – DSM 

Mpango wa Taifa wa Damu salama imetakiwa kuhakikisha Hospitali Binafsi zote zinaanza kuchangia gharama za huduma za afya ili kupata mgao wa damu. 

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua mashine za kupima sampuli za damu na utendaji kazi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama. 

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa ni lazima Mpango huyo uhakikishe unajiendesha wenyewe na kuhakikisha unapunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali katika kutimiza majukumu yake. 

“Ni lazima kupunguza gharama za utegemezi kwa Wafadhili na Serikali kwa kuanzisha mfumo wa uchangiaji gharama za huduma za Afya wakati Sera inaelekea kukamilika, Mpango unapendekeza kurudisha gharama kutoka Hospitali binafsi kupitia njia ya Bima” Alisema Dkt. Ndugulile 

Dkt. Ndugulile alisema kuwa Idadi kubwa ya wanaokuja kuchukua Damu katika Taasisi hiyo ni Hospitali Binafsi ukilinganisha na Hospitali za Umma, ambapo mfumo wake ni wakutoza huduma kwa Wananchi (Biashara) 

“Wanaokuja kuchukua Damu nyingi hapa, wengi ni Hospitali Binafsi, kuliko hata za kwetu za umma, Damu nyingi tunawapa, lakini hawa tukiwapa Damu hizi, wao wanaenda wanatoza pesa, kwahiyo sisi tunawatengenezea bidhaa bure halafu wao wanaenda kutoza pesa, hata senti tano sisi hatupati, sio sahihi” alisema Dkt. Ndugulile. 

Aidha, Dkt. Ndugulile amewaagiza viongozi wa Mpango wa Taifa wa Damu salama kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuangalia ni namna gani Damu iwe ni moja ya vitu vitakavyo gharamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. 

“Muwahusishe Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kuangalia jinsi gani damu itakuwa inagharamiwa na Bima ya Afya, mtuletee mapendekezo na sisi tutafanya maamuzi” Alisema Dkt. Ndugulile. 

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile ameagiza kufanya maboresho ya mfumo wa Takwimu kuanzia kwenye ukusanyaji wa mapato mpaka hatua ambayo mgonjwa anapata damu hiyo jambo litakalosaidia kuboresha huduma kwa wananchi. 

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameagiza kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawabakishia wachangiaji Damu ambao wanakuja kuchangia, hii inatokana na takwimu kuonesha Wachangiaji wa Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% mwaka 2017-2018. 

“Taarifa yenu ya Mwaka 2017-2018 inaonesha kwamba, wachangiaji Damu wa hiari wanapungua kutoka 67% mpaka 63% , maana yake bado kuna changamoto, na kuna kazi tunatakiwa kufanya ikiwemo kuweka mikakati ya kuhakikisha kwamba tunaowapata Mara ya kwanza kuendelea kuwa nao” Alisema Dkt. Ndugulile 

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Damu salama Dkt. Magdalena Lyimo amesema kuwa Mpango una mkakati wa kuboresha mfumo wa ukusanyaji taarifa na Takwimu za kielektroniki unaunganishwa nchi nzima ili kuleta tija na ubora wa huduma za damu salama nchini. 

Kwa upande mwingine Dkt. Lyimo amesema kuwa Mpango umefanikiwa katika kipindi cha Mwaka 2018 kwa kushirikiana na timu za Mikoa na Halmashauri ulikusanya jumla ya chupa 307,835 ambayo ni sawa na Chupa 6 kwa kila watu 1000, huku Shirika la Afya Duniani linapendekeza kukusanya chupa 10 kwa kila watu 1000, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la chupa 73,882 sawa na 32% ikilinganishwa na Takwimu za 2017. 

Dkt. Magdalena Lyimo aliendelea kusema kuwa kwa Mwaka 2018, Wastani wa chupa 25,653 zilikusanywa kila mwezi na damu zote zilipimwa magonjwa ya HIV,Kaswende pamoja na makundi ya damu, huku matarajio ni kuongeza damu hadi kufikia chupa 375,000 kwa Mwaka 2019.

ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa pamoja wamefanya ziara kwenye kijiji cha Jasini na Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja Mpakani cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga. Pamoja na Mambo mengine Naibu Mawaziri hao waliweza kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo ukusanyaji wa mapato kituoni hapo, pamoja na kuzungumza na wanakijiji cha Jasini na Watendaji wa Kituo hicho. 
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza 
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) 
Mkutano ukiendelea 
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja 
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro 
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali 
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani 
Dkt. Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni cha kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, kabla ya kuanza ziara kwenye kijiji hicho
Naibu Mawaziri pamoja na wadau mbalimbali wakiwa wamesimama kwenye moja ya jiwe ambalo linaonyesha Mpaka wa Tanzania na Kenya. 
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya. Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania 
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo 
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka 
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro 
Mhe. Dkt. Kijaji akitizama kitambulisho cha mjasiriamali mdogo huku Dkt. Ndumbaro akishuhudia tukio hilo. Mjasiriamali huyo aliwavuti Naibu Mawaziri hao kwa mwitikio wake chanya katika kuhakikisha kila mjasiriamali nchini anapata kitambulisho cha kufanyia biashara 
Mmoja wa wanakijiji akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kijijini hapo ikiwamo upatikanaji wa elimu kwa watoto wao ambao wanalazimika kwenda kusoma Kenya na jioni kurejea Tanzania.
Wanakijiji wakiwasikiliza kwa makini Naibu Mawaziri hawapo pichani
Naibu Mawaziri hao wakizungumza na baadhi ya wananchi wa Jasini mara baada ya kumaliza ziara kijijini hapo 
Waandishi wa habari wakiwa kazini 
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani.









ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho yanafikiwa.

Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.

Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha 2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo yaliyowekwa.

Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi ya milioni 10.

Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho kutozinduliwa rasmi hadi leo.

Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.

Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau mara tatu kwa wiki.

Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua stahiki.

Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.



Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Februari 2019

WANACCM KAGERA WACHANGIA UJENZI WA DARASA LA SEKONDARI

$
0
0
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga (aliyevaa shati ya rangi ya njano) akiwaongoza makada wenzake wa chama hicho katika ujenzi wa chumba cha darasa katika Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Bw. Ramadan Kambuga akipanda mti katika eneo la shule hiyo.


WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa Kushirikiana na viongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya Bukoba mjini mkoani Kagera wameshiriki zoezi la usombaji mawe kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa katika Shule ya Sekondari ya Kalema Kata Buendangabo na kupanda miti ikiwa ni kuazimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama hicho. 

Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa chama hicho Mkoa wa Kagera, Ramadan Kambuga (aliyevaa shati ya rangi ya njano) ambaye pia ameshiriki zoezi hilo,amesema kuwa ujenzi wa chumba hicho cha darasa ni utekelezaji wa ilani ya CCM. 

Kutokana na msongamano wa manafunzi darasani katika shule hiyo Bwana Kambuga ametoa kiasi cha shilingi laki moja ili isaidie kuongeza nguvu na kuweza kuondoa adha hiyo ambayo inawakabili wanafunzi wa shule hiyo. 

Bwana Kambuga pia amesema wao kama wadau wa maendeleo na wasimamizi wa serikali kupitia Chama cha Mapinduzi wataendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Bw. Ramadan Kambuga, akiwa na makada wenzake wakati wa ujenzi wa darasa hilo. 

TANTRADE INALETA FURSA KWA WADAU WA ZAO LA PARACHICHI NCHINI

TANGAZO LA MNADA

$
0
0
Wiki hili jumamosi, karibu kwenye mnada wa Ubalozi wa Switzerland, Finland, Norway, Europian Union, World Bank na UNICEF.

Kuna Furniture nyingi za Nyumbani na za Ofisi, Magari na Genereta. Universal Auction Centre kwa idhini tuliyopewa tutauza mali hizo kuanzia Saa 3:30 Asubuhi, Golden Resort, Sinza

Mali zote zinaweza kukaguliwa kuanzia kesho Golden Resort Sinza karibu na Lion Hotel.

Kwa Maelezo zaidi piga simu no: +255 754 284 926 au Email:  universalauction@hotmail.com

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA WASANII KWENYE KONGAMANO LA WASANII TANZANIA KUHUSU ATHARI ZA MATUMIZI NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wasanii wa fani mbali mbali waliohudhuria  Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza viongozi wa meza kuu na wasanii kusimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop Tanzania Golden Jacob Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo kabla ya kuanza kuhutubia  Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kwa umakini Sanaa ya maigizo iliyokuwa ikionyeshwa na wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA) waliokuwa wakionyesha madhara ya dawa ya kulevya wakati wa Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 .Kongamano hilo limefanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Heshima kwa Godzilla; Wasanii wa Filamu na Muziki wakiwa wamesimama kwa dakika moja kama ishara ya kumkumbuka msanii wa hiphop Tanzania Golden Jacob Mbunda aliyefariki asubuhi ya leo kabla ya kuanza kuhutubia  Kongamano Kuhusu Tatizo la Dawa za Kulevya kwa Wasanii lililoandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo februari 13, 2019 lililofanyika katika  Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

UJENZI WA MAGHALA NA VIHENGE VYA KISASA UNAENDELEA DODOMA

$
0
0




Mafundi na wahandisi wa Kampuni ya FEERUM SA wakikamilisha ujenzi wa msingi wa moja ya maghala katika Mradi wa Ujenzi wa Maghala na Vihenge vya Kisasa vya kuhifadhia chakula unaojengwa  na Serikali katika eneo la Kizota jijini Dodoma, Februari 13, 2019. Ujenzi huo umepangwa kukamilika  Desemba mwaka huu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAITARA AMPA WIKI TATU MWALIMU MKUU SHULE YA MSINGI KILIMANGWIDO KUKAMILISHA JENGO LA SHULE WILAYANI PANGANI

$
0
0
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara akizungumza na viongozi wa wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya siku moja kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange 
Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Naibu wWaziri wa Tamisemi Mwita Waitara kushoto ni Mwenyekiti wa Hlamashauri ya Pangani 
Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa ziara hiyo 
Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashim akizungumza katika ziara hiyo 
Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Mbenje Isaya akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto ni Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashim 
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara kushoto akisalimia na Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara katika akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah kushoto na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero wakiwa kwenye kivuko cha Mto Pangani kuelekea ng'ambo ya pili ya mji huo wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara katika akiwa na viongozi mbalimbali wakitoka kwenye kivuko cha Mto Pangani wakati wa ziara yake 
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Kilimangwidu wilayani Pangani wakati wa ziara yake 
Jengo linalojengwa kwenye shule ya Msingi Kilimanwidu wilayani Pangani ambalo Naibu Waziri huyo alitoa muda wa wiki tatu liwe limekamilika
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara akilikagua jengo la shule ya Msingi Kilimangwidu wilayani Pangani katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah 
NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara akikagua madaftari ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kilimangwido
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kilimangwido wilayani Pangani mkoani Tanga Sufiani Ramadhani katikati akitoa maelezo kwa NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara kushoto 



NAIBU Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara atoa muda wa wiki tatu kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kilimangwido wilayani Pangani mkoani Tanga Sufiani Ramadhani kuhakikisha jengo linalojengwa kwenye shule hiyo linakamilika la sivyo cheo chake atakuwa amekiweka rehani.

Waitara alitoa wito huo wakati wa ziara yake wilayani Pangani iliyoambatana na kuzungumza na watumishi wa Halmashauri na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye shule za msingi na sekondari wilayani humo.

Akiwa kwenye shule hiyo alizungumza na wanafunzi na baadae kutembelea Jengo ambalo linajengwa shuleni hapo ambalo ujenzi wake umechukua muda mrefu ndipo alipoonyeshwa kutokuridhishwa nalo na baadae kuamua kutoa maamuzi hayo kutokana na darasa hilo moja kujengwa kwa kipindi cha miezi sita lakini halijakamilika.

Naibu Waziri huyo alihoji kwanini jengo hilo ambalo lilipaswa kukamilika mwezi Mei mwaka 2018 lakini mpaka sasa bado halijakamilika na kueleza kwamba umefanyika uzembe mkubwa huku akimuonya Mkuu huyo wa shule kutokurudia vitendo vya namna hiyo kwa wakati mengine.

“Ni jambo la kushangaza sana tokea mwaka jana fedha zipo kwenye akaunti eti mnasubiri mfumo ufunguke hii sio sawa kabisa hata usafi mwalimu haufanyi leo ni February 11 kwa sababu hiyo nawapa wiki tatu mnatakiwa muwe mmelimaliza jengo la shule hili “Alisema

Hata hivyo Naibu Waziri huyo alimtaka Afisa Elimu Msingi wa wilaya hiyo Mwalimui Mbwana Mohamed kuhakikisha wanasimamia vyema miradi ya elimu badala ya kukaa ofisini ili kuweza kubaini changamoto zilizopo na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi kwa pamoja.
“Lakini pia sipendi viongozi wanapokuja ndio wanaelezwa matatizo mfumo mfumo mpo kwenye ngazi ya wilaya kusaidia viongozi wa chini mnaweze kwenda kwa Meneja wa hiyo benki mkalifanyia kazi…huu ni uzembe mkubwa umefanywa wa kutokulimaza jengo hilo kwa wakati wa sababu mna ela yakumalizi na mlipokuwa nayo tokea mwaka jana mwezi machi lakini hamjafanya hivyo,nataka ubadilike vyenginevyo cheo chao hutakuwa huna sababu ya kuendelea kuwepo kwenye nafasi yakeo “Alisema.

Awali akizunggumza Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Sufiani Ramadhanalimueleza Naibu Waziri huyo kwamba baada kupokea fedha hizo maelekezo ajenge msingi atengeneza jamvi apandishe ukuta aezeke na kupanua na kuweka mlango darasa lakini changamoto kubwa waliokumbana nayo ni
mfumo wa kibenki.Alimueleza Naibu Waziri huyo darasa hilo halijakamilika kwa sababu kwenye mfumo kuna tatizo ela hamna lakini benki zipo hivyo wakawawanashindwa kufanya matumizi.

Naya kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani Mbenje Isaya alimueleza Naibu Waziri huyo baada ya kufika alijaribu kufuatilia hilo suala akagundua kuna tatizo la wao kuingiza lakini wameendele kutumia fedha zilizopo kwenye vifungu vyengine wametumia zaidi ya milioni 12
kwenye jengo hilo.

Alisema alichowaambia kwamba wahakikisha vile vifungu zitumike ili laki saba itumike kwenye kazi iliyobaki lakini pia wanachangamoto za kwao zilizopelekea kazi hiyo kuchelewa hivyo ni bora wakaziweka wazi kwako ili uweze kuzitambua.

KIWANDA CHA GLOBAL PACKAGING CHAPUNGUZA CHANGAMOTO YA UAGIZAJI VIFUNGASHIO

$
0
0
Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya kuzalisha vifungashio vya aina mbalimbali. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.

Mitambo ya wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani kama inavyoonekana katika picha, hiki ni moja ya kiwanda kinachozalisha vifungashio hapa nchini ikiwa ni matokeo ya dhana ya ujenzi wa uchumi wa viwanda inayosisistizwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Wafanyakazi wa kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani wakiendelea na kazi ya uzalishaji vifungashio kwa kutumia mitambo ya kisasa. Kiwanda hicho kinazalisha tani 150 za vifungashio kwa mwezi na kutoa ajira kwa mamia ya watanzania na pia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa vifungashio hapa nchini.


Sehemu ya mitambo ya kuzalisha vifungashio katika Kiwanda cha Global Packaging (T) Ltd cha Kibaha mkoani Pwani.
(Picha zote na MAELEZO)


Na Lilian Lundo – MAELEZO


Kiwanda cha Global Packaging (T) Limited kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani kimepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio nje ya nchi.

Hayo yameelezwa mapema wiki hii na Meneja Mradi wa kiwanda hicho, Hatibu Njuwila wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.“Kiwanda kilianza uzalishaji Januari, 2017 na kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli , kinazalisha tani 150 za mifuko au vifungashio kwa mwezi,” amesema Njuwila.

Ameendelea kusema, wateja wakubwa wa kiwanda hicho ni wakulima wanaozalisha bidhaa za nafaka kama vile mahindi, mtama na mchele, bidhaa zinazotokana na madini na mazao mengine yanayohitaji vifungashio.Amesema, lengo la uanzishwaji wa kiwanda hicho ni kupunguza uagizaji wa vifungashio nje ya nchi kutokana na kuwepo na uigizaji mkubwa wa vifungashio kutoka nje ya nchi kwa gharama kubwa.

Aidha amesema, mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka miwili tangu kuanza kwa uzalishaji wa kiwanda hicho ni pamoja na kuajili wafanyakazi 98 ambao wote ni Watanzania, ambapo kwa asilimia kubwa ni kutoka Halmashauri ya Kibaha.Mafanikio mengine ni kupunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa vifungashio kutoka nje ya nchi, kulipa kodi mbalimbali za Serikali Kuu pamoja na Halmashauri ambapo imeongezea Serikali mapato.

Matarajio ya kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio vyenye ubora na ambavyo vinakidhi mahitaji ya wateja ambayo itaongeza thamani ya mazao na uhifadhi na kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.Global Packaging (T) Limited imejipanga vyema kutekeleza sera ya Serikali ya viwanda kwanza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

NAIBU WAZIRI IKUPA AHIMIZA VYAMA VYA WATU WENYE ULEMAVU KUSHIRIKIANA NA SERIKALI

$
0
0


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akisalimiana na Viongozi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa mara baada ya kuwasili ofisini hapo katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akipitia kwa makini taarifa ya utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu ya Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Germana Orota.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge akimweleza jambo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (Kushoto) jinsi Mkoa wa Dodoma umekuwa ukitekeleza na kuhudumia watu wenye ulemavu.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa akizungumza na viongozi wa Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Dodoma. (Kushoto) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini Bw. Edward Mpogolo (Kulia) ni Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Felisiana Mboya
Mkalimani wa lugha za alama Bw. Adrian Chiyenje (aliyesimama) akumfafanulia Mwenyekiti Chama cha Viziwi Mkoa wa Dodoma, Bw. Mazengo Kusentha (wenye uziwi) maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Afisa Ustawi wa Jamii Jiji la Dodoma, Bi. Rebeka Ndaki akieleza utekelezaji wa shughuli za watu wenye ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).
Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima akiwasilisha taarifa ya Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) walipokutana kwenye ukumbi mpya wa Ofisi za Jiji la Dodoma.

Katibu Chama cha Watu Wenye Ualbino Dodoma, Bw. Hudson Seme akichangia mada kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino wakati wa mkutano na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani).


Baadhi ya washiriki wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu), Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) wakati wa ziara yake alipokuwa akikagua utekelezaji wa masuala ya watu wenye Ulemavu.
PICHA ZOTE NA OFISI NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)


Na; OWM (KVAU) – Dodoma

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameviasa Vyama vya Watu wenye Ulemavu nchini kuhakikisha wanashirikiana na Serikali katika kuendeleza ustawi wa Watu wenye Ulemavu.

Naibu Waziri Ikupa ameyasema hayo alipofanya ziara Mkoani Dodoma kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ndani ya mkoa huo, ambapo alikutana na viongozi Mkoa na Vyama vya Watu wenye Ulemavu.

Mhe. Ikupa alieleza kuwa ushirikiano baina ya Serikali na vyama vya watu wenye ulemavu ni muhimu katika kuhakisha haki na masilahi ya watu wenye ulemavu yanalidwa kwa kuzingatia Sera, Sheria na Miongozo mbalimbali.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua na kutekeleza jukumu lake la kuhamasisha na kuwalinda watu wenye ulemavu nchini kwa kuhakikisha haki za kundi hilo maalumu zinatekelezwa,” alisema Ikupa .Aidha, alisisitiza uongozi wa Mkoa kuhakikisha unahusisha mahitaji maalumu ya wenye ulemavu katika bajeti wanazozitenga, kutoa elimu na taarifa juu ya upatikanaji wa dawa, mafuta ya watu wenye ualbino na vifaa saidizi, na uundwaji wa kamati za kuhudumia wenye ulemavu.

Aliongezea kuwa, ni vyema Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa ustawi wa jamii wakahakikisha wanawasaidia watu wenye ulemavu wanapokabiliana na changamoto kwenye uandikaji wa maandiko ya kuomba mikopo. “Unakuta kikundi cha watu wenye ulemavu wanakuwa wabunifu na wanawazo zuri la kuanzisha mradi au biashara lakini wanakumbana na changamoto ya kuaandaa andiko la miradi yao na hivyo kuwafanya wakate tamaa mapema,” alisema Ikupa

Pia, aliwasii Maafisa Ustawi wa Jamii kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu wenye ulemavu na kuendelea kuweka mifumo mizuri ya kutunza taarifa hizo. Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Bw. Edward Mpogolo aliunga mkono na kuyapokea maelekezo yote ya Naibu Waziri na kumhakikishia kuwa Mkoa wa Dodoma utakuwa mstari wa mbele katika kutekeleza maagizo aliyoyatoa.

“Tutafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Vyama vya Watu wenye Ulemavu ili kuangalia namna bora ya kuwahudumia kwa kuzingatia mahitaji yao,” alisema Mpogolo. Naye Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Bw. Justus Ng’wantalima alimpongeza Naibu Waziri kwa jitihada ambazo amekuwa akizifanya katika kutetea Watu wenye Ulemavu.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Ikupa, alitembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Chama cha Walemavu Sulungai kinachojishughulisha na ushonaji wa viatu vya wazi (kobasi) na utengenezaji wa majiko. Vilevile Mhe. Ikupa alitembelea shule ya Viziwi iliyopo Jijini Dodoma.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUARI 14,2019

umoja wa Tanzania Ujerumani hawataki mkutano na viongozi wa vyama vya kisiasa

Kampeni za Uchaguzi zafungwa Nigeria,Uchaguzi kufanyika jumamosi.

$
0
0
Alhamisi ndio siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi nchini Nigeria, siku ya jumamosi nchi hiyo itafanya uchaguzi wa urais. Nigeria ilifanikiwa kuingia katika uongozi wa Kidemokrasia miaka minne tu iliyopita licha ya matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo hivi sasa.

Kampeni za uchaguzi zikisindikizwa na tungo za muziki kutoka kwa waimbaji mbalimbali, Rais wa sasa na Mgombea Mohamud Buhari ameahidi kupeleka nchi hii katika hatua nyingine endapo atachaguliwa.

Buhari ndie alikua mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa nchi hiyo.Mapema wakati akifungua kampeni zake mwaka jana alisema kuwa vita ilianza muhula wa kwanza nahitaji kuendelea.

''tunawajibika kuwa kazi tuliyoanza muhula wa kwanza, ya kuhakikisha mali za nchi na rasilimali zinakua na umuhimu kwa wananchi wa kawaida'' alisema Buhari.

Lakini kuna maswali juu ya Afya ya Buhari mwenye umri wa miaka 76, amekua akisafiri mara kwa mara kwenda London kwa matibabu ya ungonjwa ambao umewekwa siri.

Kuna wagombea wengine 72 wa kiti cha urais, lakini mshindani mkuu ni Atiku Aboubakar , ikiwa ni mara yake ya nne kugombea kiti hiko.Anasifika kuwa mfanyabiashara mzuri, lakini suala la Rushwa wakati alipokua makamu wa rais linatia doa jitihada zake.

''katika uchunguzi wote uliofanywa dhidi yangu, kama mimi ni mla rushwa ama la, hakuna ushahidi uliopatikana, na kama kuna yoyote mwenye ushahidi ajitokeze, sijawahi kutuhumiwa kuhusu rushwa'' alisisitza Atiku Aboubakar.
Rais Muhammad Buhari.

KUSOMA ZAIDI BOFYA BBC Swahili.

JE WAJUA SIRI MASHUKA YA KIGOMA.!

$
0
0
Mashuka yenye urembo wa maua ya kushonwa na rangi za kuvutia yamening'inizwa pembezoni mwa barabara na nje ya nyumba kama uzio, ni ishara inayoweza kukujulisha kuwa umefika Kigoma.

Ni katika mji mkongwe wa Ujiji uliopo Kigoma Kaskazini, Magharibi mwa Tanzania eneo ambalo ni zaidi ya kilomita 1000 kutoka jiji la kibiashara la Dar es Salaam.

Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza, maana uwepo wa mashuka hayo si kwa ajili ya kujipatia kipato tu bali ni mila na desturi kama lilivyo vazi la khanga.Na kuchagua mashuka mazuri, unahitaji usaidi wa kujua majina na ujumbe uliopo kwenye shuka unalolichagua.

Kila shuka lina jina lake, ambapo mengi yamebatizwa majina ya watu maarufu, wakiwemo viongozi wa kisiasa kama Mbunge wa mkoa huo Zitto Kabwe, Obama, Magufuli, Lowasa, Wema Sepetu na mengine mengi.

Huku majina mengine yakiwasilisha wanyama na vitu mbalimbali kama vile Pundamilia, Tausi, Nanasi, samaki wa kigoma, mwanamke mazingira, jumba la maneno, msala, pembe la ng'ombe, mwiba na kapu la kigoma.

Joslyn Anthon alianza kufuma tangu mwaka 1996 na anasema biashara hii inamfanya mwanamke ashughulike na kupata kipato.

"Huu ni utamaduni wetu kigoma , ukitafuta shuka za kufuma utazipata kigoma, Wanawake wa mkoa huu ni karibu wote wanajua kufuma mashuka haya na jambo muhimu kwao si kujipatia kipato tu bali ni kutunza mila na desturi yao."

KUENDELEA KUSOMA MAKALA HII BOFYA BBC swahili
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images