Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

BILIONI MBILI ZATENGWA KUBORESHA SEKTA YA AFYA JIMBO LA SEGEREA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Segerea Mh Bonnah Kaluwa amekutana na Wananchi wake na kufanya Mkutano uliozungumzia changamoto mbalimbali na kutengeneza mikakati ya kuhakikisha jimbo hilo linapiga hatua za kimaendeleo.

Kaluwa amefanya mkutano huo jana Jumapili februari 10/2019 na Wananchi wa kata ya Vingunguti ,viwanja vya relini ambapo mambo mbalimbali ya maendeleo yamejadiliwa huku wananchi wakikishirikishwa kueleza mawazo yao.

Akizungumza kwenye mkutano huo,Kaluwa alisema kuwa moja kati ya mambo ambayo aliyazungumzia ni suala la barabara ya Vingunguti ambayo imekuwa kero kwa wananchi wake,Kalua amewaeleza wananchi ambavyo amekuwa akifuatilia kuhusu ujenzi wa bara bara hiyo,akawafafanulia kuwa ujenzi wa barabara hiyo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

" Kabla ya kuanza ujenzi wa barabara nawaomba Wananchi waliojenga juu ya mitaro kupisha mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa ujenzi huo",aliwathahadharisha Wananchi hao. 

Alisema pamoja na mambo mengine pia lilijadiliwa suala la Afya,ambapo ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuelekeza kiasi cha fedha takribani bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya afya jimboni Segerea.

"Ndugu wanannchi wa jimbo la Segerea naamini tunakwenda vizuri na tuko pamoja,kiukweli namshukuru sana Rais wetu Dkt Magufuli,ambaye amekuwa akihakikisha usiku na mchana nchi yetu inapiga hatua za kimaendeleo,hivyo fedha tulizopewa nna hakika sekta ya afya jimboni kwetu itaimarika maradufu" alisema Kaluwa.

Katika Mkutano wake,Kaluwa aliambatana na Naibu Meya wa Manispaaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti Mh Omari Kumbilamoto.
Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akimuelekeza jambo mmoja wa wananchi wake  aliefika kumsikiliza kwenye mkutano wake.

 Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao Mh Bonnah Kaluwa (hayupo pichani).
 Mh.Bonnah Kaluwa akiteta jambo na baadhi ya wananchi wake 
 Mmoja wa akina mama akichangia jambo kwenye mkutano huo wa kuhakikisha jimbo la Segerea linapiga hatua kimaendeleo 
 Mbunge wa jimbo la Segerea,Mh Bonnah Kaluwa akizungumza na wananchi wake  .

MTOTO ALIYENUSURIKA KUUAWA NJOMBE AFARIKI DUNIA,AZIKWA

$
0
0
Na  Ripota Wetu Njombe.

Mtoto Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo amefariki dunia Februari 09 akiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya alipokwenda kuangaliwa maendeleo ya hali yake.

Mtoto huyo aliokotwa barabarani jirani na porini akiwa amejeruhiwa kwa kukatwa koromeo Desemba 23 mwaka Jana majira ya saa 4 asubuhi mtaa wa mji mwema.

Akizungumza katika mazishi ya mtoto huyo jana katika kijiji cha Ngalanga mjini Njombe, mjomba wa marehemu Gisbeth Mlelwa,alisema marehemu alijeruhiwa na watu wasiojulikana na kupelekwa Hospital ya Mkoa Kibena na kisha kupewa rufaa kwenda Mbeya.

"Marehemu alilazwa na kupatiwa matibabu na baadae Januari 19 mwaka huu aliruhusiwa,na Februari 8 alirudi tena Mbeya kuonana na daktari ambapo Febuari 9 alifariki dunia"alisema Mlelwa.

Akizungumzia tukio hilo lililotokea Desemba 23 mwaka Jana Mwenyekiti wa mtaa wa mji mwema Alanus Mwalongo alisema alipata taarifa kuwa kuna mtoto kachinjwa kutoka kwa Balozi wake.

"Alinipigia simu nikiwa dukani kwangu kwamba mwenyekiti kuna tukio limetokea hapa kanisa la Aglikan kuna mtoto kachinjwa nikawaambia wamlete mje nae huku na walipomleta na mtoto bahati nzuri kuna kijana mmoja alikuwa anapita maeneo akawa amemuona mtoto anatokea porini na kuja barabarani ndiye aliyetoa taarifa"alisema Mwalongo.

Alisema baada ya kumuona mtoto akiwa amekatwa koromeo walimchukua na kumpeleka Hospital ya Kibena ambapo baadae alipata rufaa kwenda mbeya.Mwalongo alisema kwa kishirikiana na Jeshi la Polisi walienda hadi katikati ya msitu alipotokea mtoto na kuliona eneo alilochinjiwa.

"Majira kama ya saa 10 jioni Polisi walinipigia kuwa wanakuja kuona eneo aliloonekana mtoto tuliondoka pale tukaanza kutoka na ule msitu ambao ni viwanja vya Mekson tulipokua tunakwenda kule kijana alipoelekeza tulipokua katikati tukakuta kweli yule mtoto alipolazwa na kufanyiwa unyama ule tukakuta hapa wameweka ndala zake,sweta hapa suruali walimvua nguo zote na barabarani alikutwa uchi"alisema Mwalongo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio la mtoto huyo Jeni Chanda alisema alimuona mtoto akiwa na kijana akiwa amechinjwa na alipomuuliza alimwambia alimuona anatokea porini akiwa uchi na hivyo alimfunika.

"Mimi nilikua napita ndio nikamuona akiwa na kijana mmoja kutoka na hali aliyokuwa nayo nikachukua nguo zangu nikamfunika ili kumpeleka hospitality"alisema Jeni.Akitoa Salamu za Wizara ya Afya, Maendeelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizarani humo Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Wizara inatoa pole kwa familia hiyo na kutoa wito kwa wananchi wa Njombe kuhakikisha wanamlinda mtoto asipatwe na majanga kama hayo.

“Tumesikitishwa na tukio hilo na matukio yote yaliyotokea mkoani Njombe wazazi tuwalinde watoto wetu” alisema.Mpaka sasa vifo vya watoto wadogo kutekwa na kukutwa wakiwa wamechinjwa vimefika nane.
  Ndugu wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake akitengeneza tuta la kaburi mara baada ya mazishi ya mtoto huyo.
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kutoka kuuzika  mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakizika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake. 



 Katibu Tawala wa Wilaya ya Njombe Bw. Emmanuel George akiwaongoza wananchi wa kijiji cha Ngalanga kubeba jeneza liliokuwa na mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.
 Ndugu wakiuaga mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake. 
 Wanachi wa Kijiji cha Ngalanga wakiwa wamebeba  kwenda kuuzika mwili wa Marehemu Meshack Myonga(4)mkazi wa mji mwema halmashauri mji Njombe Mkoani Njombe aliyejeruhiwa kwa kukatwa koromeo  na kufarikia dunia akiwa hospital ya rufaa mbeya alipokwenda kutazamiwa maendeleo ya hali yake.

MAZISHI YA MTOTO MESHACK MYONGA 4 MKAZI WA MJI MWEMA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE MKOANI NJOMBE

DC NJOMBE AFUNGA MAOMBI YA KUUOMBEA MKOA WA NJOMBE KUAONDOKANA NA MAUAJI YA WATOTO

ALAT YAHUISHA TUZO YA MEYA, 2019

$
0
0
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania Mhe. Mhe.Gullam Hafeez Mukadam akiwa na Katibu Mkuu wa ALAT Abdallah S. Ngodu wakielezea kuhusu Tuzo za Meya.

Mratibu wa Mradi wa Tuzo za Meya Wilman Ndile(kulia) akizungumza namna Tuzo za Meya zitakavyoshindanishwa kwa Halmashauri zote Tanzania. 
 
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu ALAT Taifa Abdallah S. Ngodu, Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mhe. Gullam Hafeez Mukadam, Makamu Mwenyekiti Stephene Mhapa akifuatiwa na Diwani wa Kata ya Maboga Iringa Dc Mhe Veny Muyinga wakati wa utambulisho wa Tuzo ya Meya kwa mwaka 2019.

……………………………………………………………………………….
 

Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) imehuisha Tuzo ya Meya na kwa mara nyingine tena zitafanyika kuanzia Mwaka huu 2019, ambapo Halmashauri zote nchini zitashindanishwa kupata halmashauri moja katika kila kipengele na hatimaye kupatikana Halmauri yenye kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi.

Akizungumza jijini hapa, Mratibu wa Tuzo ya Meya toka ALAT, Wilman Ndile alisema uzinduzi wa tuzo hiyo unatarajia kufanyika Juni mwaka huu katika jiji la Mwanza.

Alisema tuzo hiyo inalenga kuibua ari na ushindani katika kuwahudumia wananchi na zaidi kuwafanya viongozi na watendaji wa Halmashauri zote kujituma na kubuni miradi itakayowaongezea mapato huku wakimuwezesha mwananchi kutumia njia bora kujiletea maendeleo..

Ndile alisema mchakato wa uteuzi katika mashindano utahusisha umma wa watanzania ambao watatuma ujumbe mfupi kuchagua halmashauri bora, na kuongeza kwamba majaji watatembelea halmashauri husika kabla ya kufanya uamuzi wa mwisho wa kuchagua manispaa bora.

Ndile aliongeza kuwa maombi ya kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho yatahusisha ujazaji wa fomu ambazo kwa wakati huu fomu hizo ni rafiki na unaweza kuzijaza hata kwa njia ya mtandaoni na si zile za kuandika kwa mkono kama ilivyokua hapo awali hivyo halmashauri zote zitajulishwa na kutumiwa fomu hizo kwa njia ya posta lakini pia kwa barua pepe na wao watachagua njia rahisi kwao katika ujazaji wa fomu hizo.

“Baadhi vipengele ambavyo vitashindwanishwa ni kama vile Halmashauri iliyofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, Halmashauri iliyoleta uvumbuzi na teknolojia katika utoaji wa huduma pamoja na Halmashauri iliyotekeleza miradi kwa ubora unaotakiwa” alisema Ndile.

Vipengele vingine ni pamoja na Halmashauri iliyotoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa mujibu ya mapato yao, Halmashauri iliyowajengewa wananchi uwezo wa kujikwamua kiuchumi, na Halmashauri inayofanya vizuri katika Utawala bora.

Tuzo hizi zilzoanzishwa Mwaka 2015 zimejikita katika kutunza utendaji kazi bora na jitihada zisizo za kawaida, ugunduzi, moyo wa kujitolea na utayari unaozidi kiwango cha kawaida kinachotarajiwa kwenye kazi za halmashauri

NGOMA AFRICA BAND NA CD YAO MPYA AWAMU YA TANO HAPA KAZI

$
0
0

 Si wengine ni hile bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni ,inayoongozwa na mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wenye makao yao nchini Ujerumani,bendi hiyo iliyojizolea umarufu kila kona barani ulaya na kufanikiwa kuteka washabiki kwa kutumia muziki wao wa dansi wa bongo.

Ngoma Africa band ukipenda waite FFU ughaibuni au viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" mara hii wamepakua CD yao "Awamu Ya Tano Uwanjani" yenye nyimbo mbili za "Amkeni Kumekucha" na "Awamu ya Tano Sasa Kazi" nyimbo hizo ni utunzi na uimbaji wake Kamanda Ras Makunja akimshirikisha Chris-B Bakotesa ambaye pia ni solo gitaa na kundi zima la FFU wa Ngoma Africa band wakisindikiza kwa mdundo mzima wa Hapa Kazi Kumpigia Saluti na kumuunga mkono Rais Magufuli


INTRODUCING: Masai Izoo Domy-Hongera

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN, AJUMUIKA NA VIJANA WALIOSHIRIKI SHEREHE ZA MAPINDUZI ZA MIAKA 55

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati akiwasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar, kuhudhuria hafla ya chakula cha mchana alichowaandalia Vijana walishoriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maul;id na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Kiongozi wa Vijana wa HJalaiki Ndg. Ali Mohammed Bakari.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid na kushoto Kiongozi wa Vijana wa Walioshiri Halaiki za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Ndg. Ali,Mohammed Bakari, wakiwa wamesimama wakipiga makofi baada ya kuwasili mgeni rasmin Rais wa Zanzibar, kujumuika na Vijana katika chakula maalum alichowaandalia katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni kuhudhuria hafla ya chakula alichowaandalia Vijana Walioshiriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika Kisiwani Pemba.
VIJANA Walioshiriki Halaiki ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, wakipiga makofi baada ya kuwasili kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar,(Picha na Ikulu)
VIJANA Waliuoshiriki katika Halaiki ya kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba, wakijumuika katika chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

KIONGOZI wa Halaiki Ndg. Ali Mohammed Bakari, akitowa shukrani kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa hafla ya chakula maalumu kilichoandaliwa kwa ajili yao katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar,kwa Vijana walioshiriki Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa meza kuu kulia Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.Mhe. Zuberi Ali Maulid, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma na kushoto Kiongozi wa Vijana wa Halaiki Ndg Ali Mohammed Bakari, wakijumuika na Vijana wakiimba “Wimbo wa Sisi Sote Tumegomboka” wakati wa hafla hiyo.

VIJANA Walioshiriki Halaiki ya Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya wakishiriki katika kuimba “Wimbo wa Sisi Sote Tumegombaka” wakati wa hafla hiyo ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, zilizofanyika katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
/WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, akizungumza na kutowa shukrani za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kwa Vijana walioshirki katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
VIJANA Walioshiriki Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika kisiwani Pemba mwezi Januari 2019, wakifuatilia hafla hiyo ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WATAMBUE MAGWIJI WA KARATE VISIWA VYA OKINAWA

$
0
0
 Kururunfa kata,  huko Okinawa,Japan. 
 Shihan Magoma na sensei Rumadha Fundi 1980 Zanaki Dojo, maadhimisho ya miaka 7 ya Goju Ryu Jundokan Tanzania.
Shishochin kata, Okinawa, Japan 


Baada ya kumaliza kongamano la maadhimisho ya miaka 65 ya chama cha Goju Ryu Karate -Do Jundokan mwezi wa November mwaka 2018 huko Tomigusuku, Okinawa, Japan, sensei Rumadha Fundi na wenzie washiriki toka nchi zaidi ya 25 walitembelea makumbusho ya sanaa ya Karate iliyomo ndani ya ukumbi maalum kwa shughuli za karate. Ukumbi huo maarufu wa  " Okinawa Karate Kaikan" ulifunguliwa miaka michache na mfalme Akihito wa japan kwa lengo la kuwa na maadhimisho ya michezo ya Karate visiwani humo.


Mambo mengi muhimu katika ziara hiyo ilikuwa pia kuona vitabu na video mbalimbali za waasisi wa mchezo wa karate kabla hata karate kuwa imebuniwa mnamo karne ya 18,ikiwa ni mafunzo ya siri na ikiwa imegawanywa katika vitongoji vitatu vya visiwani hapo. Utamaduni huo wa Okinawa wa sanaa hii wakati huo ilikuwa unaitwa " Te", ikimaanisha mkono. Hivyo ndivyo kila kitongoji kimoja kati hivyo vitatu yaani hiyo miji ya Shuri, Tomari na Naha ikajipatia sanaa ya kujilinda kwa majina ya, Shuri-Te, Tomari-Te, na Naha-Te


SHURI-TE:

Watu muhimu sana katika mchango wa sanaa ya Karate huko Okinawa na huenda watu na mashabiki wengi wa Karate hawamfahamu, ni mwalimu aitwae Matsumura Sokon, alifundisha magwiji wengi waliokuja baadae kuanzisha mitindo mingi sana ya Karate huko Okinawa. 

Baadhi ya walimu maarufu na niwanafunzi wa Matsumura Sokon ( Alijifunza sanaa ya kujilinda toka kwa Sakugawa Kanga), ni:Anko Asato, Anko Itosu  (mpaka hii leo anajulikana kama baba wa karate ya kisasa ), moja ya wanafunzi wa Itosu ni Gichin Funakoshi wa Shotokan, Chotoku Kyan ( Kachangia sana mtindo wa Shorin Ryu), Choshin  Chibana ( mwanzilishi wa mtindo wa Shorin Ryu), na Gichin Funakoshi( Mwanzilishi wa mtindo wa Shotokan),  ambae aliendelea na mafunzo chini ya Anko Itosu. Pia vile vile yupo mwengine ambae ni mwanafunzi wa Matsumura Sokon, anaitwa Kenwa Mabuni na Tatsuo Shimabuku ( Mwanzilishi wa mtindo wa Isshin Ryu).


Mitindo ya sasa ya Karate iliyozaliwa na ushawishi wa misingi ya Shuri-Te ni: Shotokan, Wado Ryu, Motobu Ryu, Shorin Ryu, Shudokan, na Shorinji Ryu ( Mtindo uliobuniwa na Sakugawa Kanga, mwalimu wa Matsumura Sokon).


TOMARI-TE:

Chanzo cha sanaa hii ni kitongoji cha Tomari ambayo ni bandari kuu kisiwani hapo tokea mnamo karne ya 17. Walimu muhimi toka hapo walikuwa ni:


Kosaku Matsumura, Motobu Choki (Mwanzilishi wa Motobu Ryu), Yamazato Gikei, Kyan Chotoku ni baadhi ya walimu waliokuwa wanajifunza sanaa za vitongoji zaidi ya kimoja.


Mitindo iliyozaliwa chini ya ushawishi wa Tomari-Te ni: Motobu Ryu, Shorinji Ryu, Matsubayashi Ryu, na Gohaku kai. Hapo mitindo iliyorudiwa mara mbili inamaanisha waasisi hao walijifunza pande zote mbili za miji hito ya Okinawa.


NAHA-TE.

Kabla ya vita kuu ya pili ya duania, mji wa Naha ulikuwa ndio mjimmaarufu wa biashara katika visiwa vya Ryu Kyu. Hivyo ndivyo uliwavutia wafanya biashara wengi toka China . Hivyo ndivyo sanaa ya Naha-Te ilikuwa na ushawishi mwingi wa mbinu toka kusini mwa China hasa kwa mbinu za "Fujian White Cranes Systems". 

Kulikuwa na msongamano mkubwa wa wahamiaji wa kibiashara wa China katika mji wa Naha. Mtu ambaye alikwenda China kujifunza mbinu hizo za kichina na baadae kurudi Okinawa , alikuwa mwalimu Karyo Higaonna ambaye ndio kiini kikubwa cha kuiunganisha sanaa ya Kichina na Naha-Te mnamo moaka ya 1880.


Baadhi ya walimu wachache maarufu toka mji wa Naha ni:


Karyo Higaonna (Mwalimu wa Chojun Miyagi), Chojun Miyagi (Mwanzilishi wa mtindo wa Goju Ryu) ambaye pia alikwenda China ya kusini kujifunza sanaa za Kichina, Kyoda Juhatsu, Kenwa Mabuni (Mwanzilishi wa mtindo wa Shito Ryu), na Uechi Kanbun (Mwanzilishi wa mtindo wa Uechi Ryu).

Mitindo ya  karate iliyozaliwa chini ya ushawishi wa Naha-Te ni:

Okinawa Goju Ryu, Uechi Ryu na Shito Ryu.


Pia vilevile kwa manufaa ya kuwaelimisha wanakarate wa cha na historia za Kata mitindo tofauti, napenda vilevile kusitaja kata hizo na kimbuko lake kila moja.


Kata za Shuri-Te ni : Naihanchi, Pinan, Kusanku, Passai, Jion, Jitte, Rohai, Chinto na Gojushisho.


Kata za  Tomari-Te ni:Naihanchi, Rohai, Passai, Wankan, Wansu na Sesan.

Kata za Naha -Te ni : Sanchin, Saifa, Seiyunchin, Shisochin, Seipai, Seisa, Tensho, Kururunfa, na Suparinpei.


Nakala hii imenukuliwa na Sensei Rumadha Fundi toka makumbusho ya Karate katika "Okinawa Karate Kaikan”, huko Tomigusuku, Okinawa, Japan.

CCM ZANZIBAR YAVUNJA NGOME YA UKAWA YAVUNA VIGOGO 7

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesambaratisha ngome ya uliokuwa Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA) kwa kung’oa vigogo saba na wanachama wengine wa Chama kilichokuwa mshirika wa umoja huo.

Vigogo hao waliong’oka kutoka Chama Cha ukombozi wa umma(CHAUMMA) ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama Taifa wa Chama hicho Ndugu Salma Mohamed Juma, Mwenyekiti wa Vijana wa Wilaya ya Mjini wa Chama hicho Ndugu Salamuu Abdalla Juma.

Wengine ni Katibu wa Vijana Wilaya ya Mjini ndugu  Mwanabaraka Ali Mohamed, Mjumbe wa chama hicho Wilaya ya Mjini Shadya Juma Khamis, Mjumbe wa Chama hicho  Mkoa wa Magharibi Mariam Peter John  pamoja na Mjumbe wa  ngazi ya wilaya ya Mjini Raya Ali Masoud.

Viongozi hao wa CHAUMA leo wamejiunga rasmi na CCM na kupewa kadi za Chama Cha Mapinduzi na Umoja wa Wanawake wa Tanzania(UWT) hafla iliyofanyika katika Afisiu ya UWT Wilaya ya Dimani Unguja.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CCM, aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CHAUMA Taifa, ndugu Salma Mohamed Juma, amekiri kwamba sababu ya kurejea CCM ni kutokana na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM unaosimamiwa na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Ndugu Salma ameweka wazi kwamba mwananchi yeyote ambaye ni mzalendo,mpenda maendeleo ,anayechukia rushwa na ufisadi kwa vitendo hawezi kuendelea kubaki katika Vyama vya upinzani na ndio msaana wao wakaamua kujitoa na kujiunga na CCM.

Kupitia hafla hiyo Kigogo huyo, ametoboa siri ya vyama vya upinzani hasa vilivyounda UKAWA alidai kwamba Chama hivyo vinaongozwa na viongozi mafisadi, wala rushwa,wabinafsi na mawakala wa Mataifa ya kigeni yenye mikakati ya kuhujumu uchumi na maendeleo ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Leo najihisi kama nimetoka jela kwani huko tulipokuwa kulikuwa hakuna Demokrasia, Uhuru wa kutoa na kupokea maoni wala kumthamini Mwanamke kama mtu anayesitahiki haki na fursa kama walivyo watu wengine,,,baada ya kunyanyaswa kisiasa kwa muda mrefu ndani ya CHAUMA tumeamua kurudi katika Chama chetu cha asili kinachojali utu na haki za watu wote ambacho ni CCM.

Nimekuwa kiongozi wa ngazi za juu ndani ya CHAUMA nimekutana na vikwazo vingi mpaka nikafikia hatua ya kuacha cheo changu na kuwa mwanachama wa kawaida ndani ya CCM mjue kuwa huko katika upinzani sio sehemu salama ya watu wenye akili timamu kuishi nami nawakaribisha akina mama wenzangu wajiunge na CCM taasisi huru ya kisiasa inayojali maisha ya watu wote.”,alisema Salma.

Naye aliyekuwa kiongozi wa Vijana wa Chama hicho Wilaya ya Mjini ndugu SalamuuAbdallah Juma, alitoa wito kwa vijana waliopo katika vyama vya upinzani kufanya maamuzi sahihi ya kujiunga na CCM kabla ya mwaka 2020 ili wapate uwanja mpana wa kunufaika na fursa mbali mbali za kimaendeleo.

Alisema Vyama vya upinzani vinawaandaa vijana kuwa mabalozi wa vurugu,uchochezi,fitna na siasa za jino kwa jino na sio kuwarithisha elimu na nafasi za uongozi kama kilivyo Chama Cha Mapinduzi.

“ Mimi ni kijana nimeamua kwa ridhaa yangu kujiunga na CCM ili kusaidiana na vijana wenzangu wa Chama hiki  kuendeleza mambo mema ya kuzijenga kiuchumi na kijamii nchi zetu,sambamba na kulinda kwa vitendo dhana ya Umoja na Utulivu kwani ndio chimbuko la maendeleo ya taifa lolote.

Akipokea wanachama hao wapya wa CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadalla ‘Mabodi’ , ameeleza kwamba Chama Cha Mapinduzi ndio kimbilio la wananchi wa makundi yote katika jamii.

Ameeleza wananchi wanaotoka katika vyama vya upinzani na kujiunga na CCM sio kwa bahati mbaya wala kushawishiwa bali wanajiunga na taasisi hiyo kutokana na mifumo imara ya kisiasa inayoongoza sera za maendeleo ambazo ni kivutio kwa wananchi wa rika zote.

Alisisitiza kuwa Wapinzani wataendelea ‘kupata tabu sana’ kwani wapo wafuasi wa vyama hivyo makundi kwa makundi wakiwemo vigogo wa ngazi za juu wapo tayari kujiunga na CCM visiwani Zanzibar ambapo kwa sasa wanaandaliwa utaratibu wa kikatiba ili waweze kurudi CCM.

Aliweka wazi kwamba CCM inaendeleza msimamo wake wa kipigo kama kile cha kimbunga cha ‘Sunami’ ndani ya vyama vya upinzani kwa kuhakikisha kabla ya mwaka 2020 vyama hivyo vinabaki bila wanachama na hatima yake vinakosa sifa ya kuwa wawakilishi wa wananchi.

Ameeleza kwamba wanawake wa kiafrika kwa upande wa Zanzibar walidhalilishwa,kudhulmiwa na kuteswa kwa muda mrefu kabla ya Mapinduzi suala lililoondolewa na Chama cha ASP iliyoungana na TANU kasha kuzaliwa kwa CCM inayowathamini wanawake na kuwapa haki na fursa zote za kiuchumi,kijamii na kisiasa.

Dk.Mabodi alieleza kwamba Wanawake wana historia kubwa na ya kipekee ndani ya CCM kwani kundi hilo ndio lililoshiriki kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mapinduzi ya Januari 12,mwaka 1964 yaliyowapatia haki,utu na fursa za kimaendeleo jamii ya wakwezi, wakulima na wafanyakazi.

Aliongeza kwamba mbali na hilo Wanawake ndio walioshiriki kuchangia fedha za kujenga jingo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar kisiwandui kwa michango ya fedha kupitia jumuiya ndogo ndogo za Akina mama kwa wakati huo.

 Akitaja tathimini ya uchapakazi kwa wanawake wa UWT alisema wamekuwa wakipigania asilimia 50 kwa kila Nyanja na kwa sasa tayari kinadharia wamefikia asilimia 30 na kwa vitendo wamefikia asilimia 60 hatua ambayo ni ya kupongezwa na kila mpenda maendeleo na umoja na mshikamano.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi amesisitiza umuhimu wa Vijana kuthamini Tunu za Taifa ambazo ni Muungano, Mapinduzi, Utu pamoja na Lugha ya Taifa kwani mambo hayo ndiyo yanayochochea umoja na mshikamano kwa wananchi.

Alisema wananchi wanatakiwa kutathimini na kuweka katika uzani mambo yanayotekelezwa na CCM na walinganishe na yale yanayofanywa na Vyama vingine vyenye ruzuku Kisha 2020 watoe hukumu sitahiki kwa kila taasisi ya kisiasa nchini.

Aidha amewakumbusha akina Mama hao kuchangamkia fursa za kuanzisha vikundi vya ujasiriama ili wanufaike na mikopo nafuu kutoka Serikalini ambayo kwa sasa zimetengwa kiasi cha shilingi bilioni 3.6 kwa ajili ya vikundi.

Sambamba na hayo amewasihi wanawake wa UWT katika Wilaya ya Dimani kuachana na tabia za fitna na kumakundi ya kuwania nafasi za uongozi kwani mambo hayo yasipochukuliwa hatua za kinidhamu yanaweza kuharibu sifa ya maendeleo ndani ya Wilaya hiyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Thuwayba Kisasi, aliwashukru akina mama wote waliojiunga na CCM pamoja na umoja huo, na kuwaeleza kuwa taasisi hiyo haina ubaguzi wala siasa za chuki na visasi hivyo akawasihi akina mama na vijana warudi nyumbani kumenoga.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar ndugu Tunu Juma Kondo, aliseleza kwamba kipaumbele mahsusi cha taasisi hiyo ni kuongeza wanachama kwa wingi ndani ya CCM na UWT ili 2020 CCM iendelee kushinda na kubaki madarakani.

Alisema hafla hiyo ni miongoni mwa mwendelezo wa ziara yake ya kujitambulisha kwa wanachama na viongozi wa CCM na Jumuiya zake toka ateuliwe kushika nafasi hiyo, pia amewashukru wanachama wote walioshiriki katika mapokezi yake.

Katika taarifa yao UWT Wilaya ya Dimani, wameeleza kwamba taasisi hiyo imeanzisha miradi ya ufugaji wa kuku wa nyama na mayai ili kuondokana na mifumo ya utegemezi wa ajira kutoka serikalini ambapo miradi hiyo imetolewa na Wawakilishi wa Viti Maalum ndani ya Wilaya hiyo.

Pamoja na hayo ameeleza kwamba katika kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa CCM wamefanya ziara ya kuwafariji Watoto yatima wa Kituo cha African Muslim Agency kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Kupitia taarifa hiyo walieleza kuwa ndani ya Wilaya hiyo Wabunge, Wawakilishi, Madiwani, CCM,UWT,Jumuiya ya Wazazi na UVCCM wanashirikiana katika masuala mbali mbali ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’  akivishwa sikafu na Vijana wa kikundi maalum cha UVCCM Wilaya ya Dimani mara baada ya kuwasili katika hafla hiyo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’  akizungumza na Wajumbe wa Kamati tekelezaji ya UWT Wilaya ya Dimani katika hafla ya kupokea wanachama wapya wa CCM na Umoja huo.
 MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa ndugu Thuwayba Kisasi akizungumza kabla ya mgenbi rasmi katika hafla hiyo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’  akizungumza na Wajumbe wa Kamati tekelezaji ya UWT Wilaya ya Dimani katika hafla ya kupokea wanachama wapya wa CCM na Umoja huo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’  na viongozi wengine wa CCM na UWT wakikabidhiwa kadi ya CHAUMA na aliyekuwa Mwenyekiti wa Akina Mama Taifa wa Chama hicho ndugu Salma Mohamed Juma mara baada ya kujiunga na CCM.

UPELELEZI KESI YA AMBER RUTTY NA MUMEWE WAKAMILIKA, KUUNGURUMA MARCH 07

$
0
0
 Upelelezi katika kesi ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary maarufu Kama Amber Rutty na mume wake Said Mtopali umekamilika na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma Machi 7 kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameeleza hayo leo Februari 11.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili Nguka amedai, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kufuatia taarifa hiyo,  Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi March 7, 2019. Amber Rutty na mumewe walifikishwa mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na wawili hao, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KWENYE MKUTANO WA (AU)

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais FIFA Gianni Infantino, katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais FIFA Gianni Infantino, katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia picha za Viongozi Waasisi wa Ukombozi wa Afrika, ndani ya ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma kitabu, kwenye ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Richard Sezibera, katika ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA VENANCE MABEYO AWASILI MKOANI NJOMBE KWA ZIARA YA SIKU MBILI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF, Venance Mabeyo, amewasili Mkoa wa Njombe na kupokelewa na  Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa lengo la kujua nini chanzo cha matukio ya mauaji ya watoto yaliotokea siku za hivi karibuni. (Picha na Jeshi la Polisi).     
 Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF Venance Mabeyo, akiteta jambo na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo. (Picha na Jeshi la Polisi).    
Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania CDF Venance Mabeyo, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani Njombe na kushoto kwake ni  Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas. (Picha na Jeshi la Polisi).     

MAKAMBAKO YAZIDHATITI KUMLINDA MTOTO DHIDI YA VITENDO VYA KIKATILI

$
0
0
Halmashauri ya Mji wa Makambako imejidhatiti katika kuhakikisha wanamlinda mtoto na vitendo vyote vya kikatili dhidhi yake vinavyokatisha ndoto zake vimewemo mimba na ndoa za utotoni, utekaji na mauaji ya watoto.

Hayo yamebainika leo katika kikao kazi cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Makambako ilipokutana mjini hapo kujadiliana namna bora ya kuondoka na vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bw.Paul Malala amesema imejiwekea Mikakati kwa kutoa maelekezo kwa watendaji wa vijiji na mitaa kuhakikisha watoto wanalindwa ipasavyo.

Ameongeza kuwa watendaji wa Kata na Vijiji wamepewa maelekezo kuhakikisha wanafuatiliwa wale wote wanaowafanyia vitendo vya kikatili na taarifa zao kufika sehemu husika.

“Tutahakikisha kwamba mtoto na mwanamke analindwa watendaji wa vijiji na mitaa wahakikishe watoto na wanawake wanalindwa ipasavyo” alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa lengo la wataalam hao kuja katika Mji wa Makambako ni kushirikiana na Wataalam wa mji huo kupanga mpango mkakati bora wa ndani ya kuondoka na na vitendo vya ukatili dhoidi ya wanawake na watoto.

Amesema  kikubwa Kamati ya Ulinzi dhidi ya Maanamke na Mtoto inawajibu wa kutoa elimu kwa  wanajamii kuhusiana na malezi namatunzo kwa mtoto na kumlinda dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto katika maeneo yao.

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Kamati hizo zina majukumu makubwa ya kuhakikisha mtoto na mwanamke analindwa katika kuweka mikakti ya kuwalinda watoto na kuhakikisha wahanga wa vitendo vya ukatili wanapata huduma stahiki na kwa wakati.

 Aidha akielezea kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Mtoto namba 21 ya Mwaka 2009, Mwanasheria kutoka Wizaraya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Denis Bashaka amesema kuwa  Sheria ya Mtoto inatoa adhabu kali kwa wale watakahusika na kumfanyia vitendo vya ukatili Mtoto.

Ameongeza kuwa vitendo vingi kwa mkoa wa Njombe vinaushishwa na imani za kishirikiana ila bado vitendo hivyo ni kinyume cha Sheria ya Uchawi Sura 18 2002 inakataza upigaji wa ramli ambapo waganga wengi wa Jadi wamekuwa wakiusishwa katika kupiga ramli ambazo ni chonganishi zinazopelekea mfarakano katika jamii.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bw.Paul Malala akizungumza na Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto pampja na Halmashauri ya Mji huo katika  kazi kilichowakutanisha kujadili namna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto Bi. Hanifa Selengu akieleza lengo la ujio wa Wataalam hao katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadili namna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Mwanaisha Moyo akileza umuhimu wa Kamati ya Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto katika kusaidia ulinzi na usalama kwao katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadili nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya,  Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Denis Bashaka akieleza namana Sheri ya Mtoto na ya Mwaka 2009 inavyomlinda Mtoto wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha kujadilia nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi ya MWanamke na Mtoto ya Halmashauri ya Mji wa Makambako wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao kazi kilichowakutanisha kujadilia nnamna bora katika kupambana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

RC NDIKILO AWAGEUKIA WAFUGAJI MAGINDU

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo amemuagiza mkuu wa kituo cha polisi Mlandizi, ofisa tarafa na watendaji wa kata ya Magindu kuwakamata wafugaji kumi wanaodaiwa kuingiza mifugo yao kwenye mazao ya wakulima na kuwasababishia hasara pasipo kuchukuliwa hatua za kisheria tangu mwaka 2016.

Aidha ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kibaha, kuweka upya mpango wa matumizi bora ya ardhi,  katika kijiji cha Magindu, Lukenge na Mizuguni ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji. Akitoa maagizo hayo, wakati akizungumza na wakazi wa Magindu, katika ziara yake, Ndikilo alisema wafugaji wasipewe kichwa kutokana na uwezo wao ili kukandamiza wakulima. 
"Hii ni mara ya mwisho, nipo serious ,sifanyi mzaha, wasimamieni kikamilifu wafugaji hawa, wanalisha mifugo yao usiku katika mashamba ya watu, wanatamba Magindu ,Ni lazima haki itendeke, pasipo kukandamiza walio wanyonge"alisisitiza Ndikilo. Mkuu huyo wa mkoa aliwaasa ,wakulima na wafugaji kila mmoja kumheshimu mwenzake ili kuishi kwa amani na upendo. 

Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi wa migogoro ya wakulima na wafugaji Magindu, Iddi Ngozoma alibainisha, tangu kamati iundwe miaka mitatu sasa ,mkulima hajawahi kushinda kesi hivyo,  wananchi hawana imani na utendaji kazi wa mahakama ya mwanzo Magindu. Akitolea ufafanuzi suala hilo, mkuu wa idara ya ardhi na maliasili wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Greison Gozibath alisema, kijiji cha Magindu kilipimwa 2007 ,pia kilifanyiwa matumizi bora ya ardhi 2010.

Alieleza, wakati huo kijiji cha Mizuguni hakikuwepo ambapo kilizaliwa 2013-2014. Gozibath alibainisha, kwasasa inatakiwa kufanya mpango huo kwa vijiji vyote na wanatarajia kuviingiza katika matumizi bora ya ardhi kwenye bajeti 2019-2020. Hata hivyo, utekelezaji huo utawataka wananchi kugharamia kulingana na kijiji husika ambapo gharama huanzia sh. milioni 12 hadi milioni 15-18.

TUNAENDELEA KUDHIBITI NJIA ZINAZOTUMIKA KUINGIZA DAWA ZA KULEVYA NCHINI-KAMISHNA JENERAL SIAN'GA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya Jamii
KAMISHNA Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers Sian'ga amesema kwa sasa wamefanikiwa kidhibiti njia ambazo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kupitia dawa hizo ili kuziingiza nchini Tanzania.

Amesema kwa sasa njia ambayo inatumiwa na baadhi ya wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa hizo imebaki ya Kusini ambako dawa zinapitishwa kutokea nchini Msumbiji na tayari wameweka mikakati ya kuidhibiti njia hiyo. Sian'ga amesema hayo leo Februari 11, 2019 jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia Kongamano linalotarajiwa kufanyika Februari 13 mwaka huu ambalo litawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali nchini ili kujadili athari za dawa za kulevya.Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na kuzungumzia kongamano hilo, waandishi walitaka kufahamu ni kiwango gani Mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini ambapo Sian'ga amejibu uingizwaji wa dawa upo lakini umepungua kwa kiwango kikubwa sana ikilinganisha na miaka ya zamani kabla ya mamlaka hiyo kuwepo. " Kwanza ifahamike kuwa usafirishaji wa dawa za kulevya sio Tanzania peke yake bali lipo katika nchi mbalimbali duniani.Tunashirikiana na nchi nyingine katika kupambana na dawa za kulevya na kuna njia ya Kusini ndio imeibuka.

"Katika mapambano hayo katika njia ya baharini mwaka jana zimekamatwa tani 9000 kutokana na ushirikiano wa nchi mbalimbali katika ukanda wa baharini.Pia mwaka jana dawa za kulevya aina ya heroin zilikamatwa kilo 185 na sehemu chache ya dawa hizo zilikwenda nchini Msumbiji,"amesema. Amefafanua kwa ujumla kiwango cha uingizwaji dawa za kulevya nchini kimepungua na kwa sasa hata wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo wameingia woga na kiasi wanachoingia ni kidogo ambacho ni kati ya kilo nne hadi kilo tano na kwamba mkakati uliopo ni kudhibiti njia ya Kusini ambapo dawa zinaingizwa nchini Tanzania kutokea nchini Msumbiji.

Pia amesema dawa za kulevya aina ya Heroin na Cocaini matumizi yamepungua na hivyo dawa ambazo zinatumika ni dawa za hospitali. Kuhusu kongamano la Februari 13 mwaka huu ,Kamishna Jeneral Sian'ga amsema lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wanaunganisha nguvu katika mapambano ya dawa za kulevya.

Hivyo, kupitia kongamano hilo ambalo litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini ambapo kupitia kongamano hilo itatolewa elimu inayohusu athari za matumizi ya dawa za kulevya, hivyo ametoa rai ya wasanii kujitokeza kwa wingi ili nao watoe maoni yao ya nini kifanyike kukomesha uingizwaji wa dawa za kulevya. Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi amezungumzia umuhimu wa wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo hasa kwa kuzingatia kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakitumia dawa za kulevya na wengine wanatumika kukubebeshwa dawa.

"Tatizo la dawa za kulevya ni la dunia nzima na wanaoatharika zaidi ni vijana wakiwamo wasanii maarufu ambao wengi wao wameathirika zaidi na wengine wamepoteza maisha kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya. "Si kwamba wasanii hawajui kuwa dawa za kulevya zina athari,wanajua lakini wanaangalia leo lakini ukweli athari zake ni nyingi sana.Kwa bahati mbaya wanaotumia athari zake ni kubwa. Wapo wasanii ambao wametumika kubeba dawa za kulevya kutokana na ahadi za fedha badala ya kuelezwa na matatizo yanayopatikana kupitia dawa hizo. Hivyo kupitia kongamano hilo wataeleza athari zake," amesema Dk.Mfisi.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Joyce Fissoo ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo huku akifafanua kundi ambalo linaathirika na utumiaji wa dawa za kulevya ni la wasanii. "Tunaamini kuwa kupitia kongamano hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ,wasanii watapa fursa ya kupata elimu inayohusu athari za dawa za kulevya.Tunaomba wasanii wote wajitokeze kwa wingi na wale wa mikoani tanaomba wafuatilie kongamano hilo kupitia vyombo vya habari,"amesema Fissoo.

BREANKING NYUZZZZZ.......: MICHAEL WAMBURA APANDISHWA KIZIMBANI LEO, ASOMEWA MASHTAKA 17 YAKIWEMO YA KUTAKATISHA FEDHA

$
0
0
 Aliyekuwa Makamu  wa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Michael Wambura akiwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri Kusomewa mashtaka yake ya yanayomkabili. Wambura anadaiwa kuwa na mashtaka zaidi ya kumi
 Aliyekuwa Makamu  wa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Michael Wambura akimsikiliza wakili wake, wakati akiwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri Kusomewa mashtaka yake ya yanayomkabili.
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 

Aliyekuwa makamu wa rais wa Shirikisho la  mpira wa miguu nchini (TFF), Michael Wambura amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Katika kesi hiyo mshtakiwa wambura anakabiliwa na shtaka moja la kughushi, Shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali George Barasa akisaidiana na  Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina imedaiwa mshtakiwa alitenda kosa la kughushi Julai 6,2004 mahali pasipojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam. 

Imedaiwa siku ya tukio mshtakiwa Wambura kwa nia ya kutapeli  alitengeneza barua ya  kughushi ambayo haina kumbu kumbu namba akionyesha  imeandikwa na E Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa  kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.

Katika shtaka la kutoa Nyaraka ya uongo imedaiwa, mshtakiwa  alitoa barua iliyokuwa haina kumbu kumbu namba  ya tarehe 6/7/2004 akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck system ltd. akidai kuwa  anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Aidha katika shtaka la 3 hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi jumla ya zaidi ya sh. Milioni 95 
 kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na riba kutoka kwa Jek huku akijua kuwa siyo kweli.

 Katika moja ya mashtaka hayo ya kujipatia fedh kwa njia ya udanganyifu imedaiwa, Juni 17.2015 huko katika ofisi za TFF kwa njia ya udanganyifu, Wambura alijipayia sh. Milioni 10 kutoka TFF kwa kuonesha kuwa ni malipo ya USD 30,000 pamoja na riba kutoka kwenye kampuni hiyo ha Jeck jambo ambalo siyo kweli.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha imedaiwa, kati ya Agosti 15 na Oktoba 21 huko katika ofisi za TFF mshtakiwa alijipatia sh. Milioni 25,050,000   kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

Pia imedaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 2015 mshtakiwa alijipatia sh. Milioni 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali zimetokana na shtaka la kughushi.
Hata hivyo. Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi hiyo imefunguliwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi ambapo mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika
Baada ya upande wa mashtaka kumaliza kumsomea wambura mashtaka yake, wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu mashtaka yote 17 hakuna shtaka hata moja lilolofunguliwa chini umya sheria ya uhujumi uchumi hivyo yalitakiwa yafunguliwe kama mashtaka ya kesi ya kawaida ya jinai ambayo yanamruhusu mshtakiwa kujibu.

Kufuatia hoja hiyo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi, Wambura amerudishwa rumande.

Wananchi Maili Moja Wafurahia Kero ya Maji Kutatuliwa

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO
Wananchi wa Maili Moja, mtaa wa Muheza, Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameishukuru serikali kwa kumaliza kero ya maji iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu. 
Furaha ya wananchi hao ilionekana wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wetu mwisho wa wiki iliyopita. Wengi wa wananchi waliohojiwa wameonyesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuwapatia wananchi wa eneo hilo huduma ya maji safi na salama na wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake kwa kutatua kero ya maji iliyokuwa inawakabili kwa muda mrefu.  
"Kabla ya mradi huu kukamilika tulikuwa tukitembea umbali mrefu kutafuta maji ambapo tulikuwa tunalazimika kuamka saa nane za usiku na kurudi saa mbili asubuhi lakini kwa sasa tumesogezewa huduma ya maji karibu na makazi yetu tena kwa gharama ndogo," amesema Zawia Salum.
Filemoni Shila, mkazi wa siku nyingi eneo hilo amesema kusogezwa karibu huduma ya maji kwenye makazi yao kumesaidia kupata muda wa kufanya shughuli za kuwaingizia kipato ambapo kabla ya kuwepo mradi huo  muda mwingi walikuwa wakitumia kutafuta maji.
Naye mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maili Moja, Hamisi Salum Ally, amesema alikuwa anafuata maji mabondeni kwa ajili kufulia sare zake za shule lakini kutokana na kusogezewa huduma ya maji karibu imemsaidia kupata muda wa kujisomea. 
Akizungumzia mradi huo, Mhandisi wa Maji Mji Kibaha, Grace Lyimo amesema mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa kwa wakazi wa Muheza ambapo ulikuwa na lengo la kuhudumia wananchi 911 lakini mpaka sasa unahudumia zaidi ya wananchi 2000.
"Mradi wa maji Muheza umejengwa kwa Shilingi Milioni 359 ambapo hutoa lita 100,000 kwa siku," ameongeza mhandisi Grace.
Mradi huo wa maji unaendeshwa na wananchi wa eneo hilo, ambapo hukusanya mapato ya mradi huo na kuziweka benki ambapo matumizi ya fedha hiyo ni pamoja na matengenezo madogo madogo ya mradi huo. 
  Mkazi wa Mtaa wa Muheza, Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani Bi Zawia Salum akiteka  maji katika kituo  kimojawapo cha maji kilichojengwa na Serikali ya Awamu ya Tano kinachohudumia wananchi zaidi ya 2000 katika mtaa huo. Mradi huo umeigharimu Serikali Milioni 359 na kuzalisha lita 100,000 kwa siku ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.
 Tanki la maji Mtaa wa Muheza, Halmashauri ya Mji Kibaha, Mkoani Pwani kama linavyoonekana  katika picha, mradi huo umesaidia kuondoa adha ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo na unahudumia wananchi zaidi ya 2000.  (Picha zote na MAELEZO)

BOSI WA ZAMANI WA UDART, ROBERT KISEMA AFIKISHWA MAHAKAMANI, ASOMEWA MASHTAKA 19

$
0
0
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 

Mkurugenzi wa UDART, Robert Kisena (46) na wenzake watatu akiwemo raia wa China,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka 19 yakiwemo ya utakatishaji na  kusababishia UDART hasara ya zaidi ya BIL. 2.41.

Mbali ya Kisena, washitakiwa wengine ambao wote wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Cheni Shi (32). Raia wa China. 

Katika mashtaka hayo, lipo shtaka moja La kuongoza uhalifu, shtaka moja la kujenga kituo cha mafuta bila kibali,  shtaka moja la kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa na shtaka la wizi wakiwa Wakurugenzi, 

Pia wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha, mashtaka manne ya kughushi, mashtaka manne ya kutoa nyaraka za uongo, mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la kuisababishia mamlaka hasara. Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali, George Barasa, Moza Kasubi na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Katika kosa la kuisababishia UDART hasara, linalowakabili washitakiwa wote inadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 Washtakiwa  hao kwa mamlaka waliyonayo waliisababishia UDART hasara ya Bil 2.41.

Pia Robert Kisena na Shi, wanadaiwa Mei 26, 2016 wakiwa NMB Bank Ilala kwa pamoja wakiwa Wakurugenzi wa Longway Engineering huku Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART walihamisha Sh. Mil.603 kutoka akaunti ya benki ya UDART kwenda kwenye akaunti ya Longway ambapo ndani ya siku mbili walizitoa fedha hizo huku wakijuwa kuwa fedha ni zao la  kosa la kughushi.
Katika shtaka la kujipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu, imedaiwa,  Robert Kisena na Shi,  Mei 30, 2016  katika Benki ya NMB Ilala walijipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu kutoka katika benki hiyo ikiwa na jina la Fund Transfer Request Form ya Aprili 6, 2016 kwa lengo la kuonyesha kiasi cha Sh.Mil 750 zimelipwa na Kampuni ya Longway kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha Mwendokasi Kimara, Kivukoni, Ubungo na Morocco huku wakijua kuwa siyo kweli.

Katika kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, linamkabili  Robert Kisena na Shi wanadaiwa June 8, 2016 katika benki ya NMB Ilala washtakiwa kwa njia ya uongo walijipatia Mil.594.92 kutoka UDART kwa kuonyesha zimelipwa na kampuni ya Longway ambayo imehusika katika kutengeza vitu mbalimbali.

Pia katika kosa la kughushi,  Kisena anadaiwa April 6, 2016 katika benki ya NMB Ilala alighushi nyaraka yenye tarehe April 6, 2016 kwa lengo la kuonyesha Mil.594 zimelipwa kwa kampuni ya Longway ambayo imejihusisha na uandaaji, utengenezaji wa vitu mbalimbali huku wakijua kuwa siyo kweli. 
Katika kosa jingine la utakatishaji fedha linawakibili washitakiwa wote wanadaiwa kati ya Mei 25, 2015 na December 31, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa na lengo hovu walibadilisha thamani ya mafuta ya zaidi ya Bil.1.21 kuwa fedha ambayo ni Bil 1.21 baada ya kuyauza mafuta hayo, huku wakijua mafuta hayo ni zao la kosa la wizi.

Robert Kisena na Kulwa Kisena wanadaiwa kati ya Januari 1, 2015 na December 31, 2017 huko Katika maeneo ya Jangwani Ilala, wakiwa Wakurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil and Gas Ltd 
walijenga kituo cha Mafuta bila ya kupata kibali kutoka EWURA. 

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za Uhujumu uchumi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Februari 23, 2019 washitakiwa wamerudishwa rumande.

RAIS DKT. SHEIN AJUMUIKA NA ASKARI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA WALIOSHIRIKI GWARIDE LA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  ameungana pamoja na Wapiganaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama waliovyoshiriki katika Maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chakula maalum cha mchana alichowaandalia.

Chakula hicho maalum cha mchana aliwaandalia kutokana na ushiriki wao kwenye sherehe hizo za miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika Januari 12 mwaka huu 2019 huko katika uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba.

Hafla hiyo ya chakula maalum ilifanyika leo katika  Kambi ya Mafunzo ya Jeshi ya Chukwani ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri, Manaibu Mawaziri na viongozi wengine pamoja na Wapiganaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shukurani zake Dk. Shein kwa Wapiganaji hao zilizotolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu alitoa pongezi kwa Wapiganaji hao kwa kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo adhimu.

Alieleza kuwa hatua hiyo ya Dk. Shein ya kuwaandalia chakula maalum cha mchana ni utamaduni aliouweka kila mwaka baada ya kumaliza sherehe hizo ambayo inaonesha wazi jinsi alivyokuwa na upendo pamoja na imani kubwa na wananchi wote anaowaongoza.

Hivyo,  Waziri Gavu alisisitiza haja kwa Vikosi hivyo vya Ulinzi na Usalama kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulinda amani, utulivu na mshikamano ambapo pia, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi maalum kwa ushiriki wao mzuri katika sherehe hizo.

Waziri Gavu alitoa shukurani za dhati kwa vikosi hivyo kwa kuazimisha kwa hali ya juu kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Waziri Gavu alisema kuwa gwaride hilo lililovutia sana lilikuwa ni kielelezo cha kutosha cha Mapinduzi ya Januari 12.1964 yaliyowakomboa Wazanzibari wote ambayo yataendelea kulindwa, kuenziwa na kutunzwa daima.

“ Imani ya kiongozi mwema siku zote haitafutwi kwenye jarida bali inatafutwa katika nafsi na nyonyo za watu anaowaongoza........na sote tunaona jinsi ya upendo ulionao kwa wananchi wa Zanzibar na Tanznia nzima kwa jumla”.

“ .....hongereni sana sana sana Vikosi vyetu vya Ulinzi na Usalama kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi yetu ”,alisisitiza Waziri Gavu.

Aidha, alitoa shukurani kwa Wapiganaji wote pamoja na viongozi wao kwa kufanikisha kilele cha sherehe hizo na kusisitiza haja kwa vikosi hivyo kuendelea kusimamia amani, utulivu na mshikamano hatua ambayo itawapelekea viongozi wengine kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Nae Kaimu Brigedi Kamanda 101 KV Zanzibar Kanal Salum Serengo Mugoba alitoa shukurani na pongezi kwa Dk. Shein kwa kuendelea kuvijali vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na kuendeleza utamaduni wake huo aliouweka kwa kila mwaka mara baada ya sherehe za Mapinduzi ambapo Dk. Shein huwandalia chakula maalum cha mchana Wapiganaji hao na kula nao pamoja.

Kanal Mugoba alieleza kufarajika kwao na hatua hiyo ya Dk. Shein na kutoa pongezi na shukurani kwa niaba ya Wapiganaji wote walioshiri katika hafla hiyo adhimu.

Ni utamaduni aliouweka Dk. Shein wa kuwaandalia chakula cha mchana Vikosi vya Ulinzi vinavyoshiriki katika gwaride la sherehe za Mapinduzi pamoja na vijana na Wanafunzi ambao hushiriki sherehe hizo kwa kila mwaka ambapo hapo jana aliwaandalia vijana na Wanafunzi  chakula hicho huko katika Makao Makuu ya KVZ, Mtoni mjini Zanzibar.

Katika hafla hiyo pia, Kikundi cha Taarab cha Taifa kilitumbuiza pamoja na Grassbanda ya JWTZ.


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali.S.S.Mugoba, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwaka huu 2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Kambi ya JWTZ Chukwani Zanzibar, kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama, ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kambi ya Chukwani kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kujumuika katika chakula maalum aliowaandalia kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar, Kanali S.S.Mugoba na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Mhe. Haji Omar Kheri,(Picha na Ikulu)
 KAIMU Kamanda Brigedi ya 101 KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, akizungumza wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aki Mohamed Shein, kwa ajili ya Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika mwaka huu kisiwani Pemba January,12, 2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika katika chakula maalum aliowaandalia, Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika kambi ya chukwani  walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zilizofanyika Kisiwani Pemba katika uwanja wa gombani.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika Kambi ya Chukwani Zanzibar.
 ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakijumuika katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images