Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

UVCCM MKOA WA PWANI YATOA MAFUNZO YA UJASILIAMALI WILAYA YA KISARAWE

$
0
0
Umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa pwani umeendelea kutoa mafunzo ya ujasiliamali kwa vijana na wananchi wa Kisarawe yaliyoyofunguliwa jana na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo.

Akifungua Mafunzo hayo DC Jokate amesisitiza vijana kuchangamkia FURSA na amewapongeza Uvccm Mkoa wa Pwani kwa kuandaa Mafunzo hayo katika wilaya hiyo.

DC Jokate ameahidi kuwapa ushirikiano washiriki wa mafunzo hayo na amesema wajasiliamali wajitume kufanya kazi kwa maendeleo ya kisarawe.

"Niwasihi Vijana Wenzangu Mjikite kwenye Ujasiliamali wa Kilimo ambapo kwa ardhi ya wilaya yetu inakubali nasi viongozi wenu tutahakikisha tunawatafutia soko la uhakika na wadau wa kilimo hicho;

"Kwa Sasa wilaya yetu tunafanya vizuri Sana katika sekta mbalimbali mfano nilipokuja hapa wilaya nzima matokeo ya kidato cha nne daraja la kwanza wanafunzi walikuwa wanatoka 4 tu Ila kwa kampeni yetu ya Tokomeza Zero Kisarawe Imesaidia kwa Sasa wanafunzi 41" Alisema DC Jokate.

Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani Cde Charangwa Selemani, amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuwapa vijana ujuzi katika wilaya zote za Mkoa wa pwani na mpaka sasa wameshafanya wilaya mbili ikiwemo RUFIJI na KISARAWE. 

Aidha Mwenyekiti Charangwa amesisitiza umoja na mshikamano katika kazi na wao kama viongozi watahakikisha wanawapa vijana ujuzi Ili waweze kujiajiri.

Comrade Charangwa amewapongeza Viongozi wa Chama na serikali kwa Uchapakazi na amempongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.John Joseph Pombe Magufuli, kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Watanzania.

"Mwaka Huu Kuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Vijana Ndo Injini ya Chama Shirikianeni na Chama Kuhakikisha Wilaya ya Kisarawe Tunapata Ushindi wa Kishindo pia Mafunzo Haya Myafanyie Kazi Tengenezeni Bidhaa za Ushindani katika Soko" Alisema Cde Chalangwa.

Katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo, Amemshukuru mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa pwani kwa namna anavyoshirikiana nao katika kuwapelekea fursa na wameahidi kuzifanyia kazi.

mafunzo hayo ya ujasiliamali yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Mkoa wa Pwani,Abdallah Makelo, Katibu Msaidizi wa Mwenyekiti Taifa, Abdulrahaman Killo, Katibu wa Uvccm Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto, Viongozi wa UWT wilaya ya Kisarawe, viongozi wa jumuiya ya wazazi wilaya kisarawe,Katibu Uvccm wilaya kisarawe, waheshimiwa madiwani , DAS wa wilaya ya kisarawe,afisa maendeleo wa wilaya na afisa vijana wa wilaya.

Vijana wa Wilaya ya kisarawe walijifunza mambo mbalimbali ikiwemo Kilimo ,Ufugaji wa Kuku,Uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za viwandani Mafunzo yaliyo tolewa na Taasisi ya TAEDO chini ya Mkurugenzi wake Kenani Kihongosi.

Mafunzo hayo yalifungwa na mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Kigoma,Cde Silvia Sigula ambaye aliwaasa vijana kutumia fursa zilizopo na kufanyia kazi mafunzo waliyopewa katika kujiongezea kipatao chao.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (katikati) akifungua Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wa wilaya hiyo  yatakayowasaidia kujikwamua kiuchumi. Mafunzo Hayo yameandaliwa na Taasisi ya Taedo na Uvccm Mkoa wa Pwani. Kulia Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani, Chalangwa Seleman na Mwenyekiti Uvccm Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
 Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Pwani, Chalangwa Seleman (katikati) akichanganya dawa kwenye maji wakati wa mafunzo ya Ujasiliamali wa vitu mbalimbali wilayani Kisarawe jana. Wa Kwanza Kushoto ni Mwenyekuti wa Uvccm wa Wilaya ya Kisarawe,Asha Lusonzo. 
 
 Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (Uvccm), Chalangwa Selemani akizungumza katika Mafunzo ya Ujasiliamali kwa Vijana wilayani Kisarawe, kushoto ni Mkuu wa Wilaya Hiyo, Jokate Mwegelo.
Picha ya pamoja.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO –IHUMWA.

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. Mpango ameyasema hayo leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo ambazo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 

‘Nafikiri tunaenda vizuri, quality of work inanifurahisha, ikifika tarehe 1 Machi, 2019, nijisikie  nipo huru sasa nabadilisha ofisi nipo Ihumwa’ alisema. Aidha Dkt. Mpango ameuagiza Uongozi wa Wizara kuanza mchakato wa ujenzi wa Jengo kubwa la Ofisi ili kuweza kutosheleza Watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi hizo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi Elisante Ulomi amesema ujenzi wa awamu ya kwanza umejumuisha Ofisi ya Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Wakuu, ukumbi wa mikutano, ofisi za madereva, pamoja na ofisi za Wakurugenzi saba.

Mhandisi Ulomi amesema ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 92, na utakamilika tarehe 28 Februari,2019.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (katikati) akipata maelezo namna ujenzi wa Ofisi za Wizara unavyoendelea kutoka kwa Mhandisi Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alipotembelea eneo la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (watatu kulia) akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bi. Grace Sheshui (wakwanza kulia), wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango akisaini kitabu cha wageni alipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (kushoto) akioneshwa ramani ya majengo Wizara hiyo kutoka kwa Mhandisi Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alipotembelea eneo la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali- WFM)

WABUNGE CCM WAAMUA KUFAFANUA MISWAADA ILIYOJADILIWA BUNGENI

$
0
0
 Katibu wa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jason Rweikiza(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu miswada ambayo imejadiliwa bungeni.
Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa Sheria ya Vyama vya Siasa

*Wazungumzia umuhimu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na faida zake kwa Watanzania 

 Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 

 WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wameazimia kufafanua mambo mbalimbali ambayo yalijiri katika vikao vya Bunge ambalo limemalizika vikao vyake Bungeni Mjini Dodoma hivi karibuni. Kwa mujibu wa Katibu wa Wabunge hao Jason Rweikiza pamoja na mambo mengine wamejikita kuzungumzia miswaada sita ambayo imepitishwa na Bunge hilo na kufafanua kuhusu Sheria ya vya siasa kwa undani zaidi ili umma wa Watanzania ufahamu kinagaubaga. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Rweikiza amesema wameona ni vema wakafafanua mambo mbalimbali yakiwemo ya Sheria ya Vyama vya siasa iliyopitishwa kwenye vikao hivyo kwasababu inaonesha wananchi wengi sio tu hawajahifahamu sawasawa bali pia kuna upotoshaji mwingi.

 "Wabunge wa CCM kwa umoja wetu tumedhamiria kuufahamisha umma kuhusu mambo ambayo yamejadiliwa bungeni , na hasa miswada sita ambayo imepitishwa na kuwa sheria.Tanalojukumu la kuhahakikisha Watanzania wanafahamu vema kila ambacho kimejadiliwa bungeni kwani wabunge tunaotokana na Chama hiki tunayo dhamana ya kuelezea kwa ufasaha mambo yanavyokwenda,"amesema Rweikiza. 

Amefafanua Bunge lilimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuwa mahususi kwa ajili ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka Kamati za Bunge ikiwemo miswada sita ambayo imepitishwa."Tumekuja kwenu waandishi wa habari tukiamini mtakuwa daraja la kufikisha haya tunayoyazungumza kwa wananchi." 

Akizungumzia zaidi kuhusu Sheria ya Vyama vya Siasa, Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda amesema sheria hiyo ni muhimu kwani sasa Chama cha siasa ambacho kitaanzishwa kitakuwa kinazingatia maslahi mapana ya nchi yetu badala ya kuwa chama cha mfukoni au cha kifamilia. "Ni ukweli usiopinginga kuna vyama hapa vya siasa ambavyo namna vinavyoendeshwa si kwa ajili ya maslahi mapana ya Watanzania bali ni vyama kwa ajili ya kunufaisha watu na familia zao.

Hivyo ujio wa Sheria ya Vyama vya Siasa utasaidida kuweka mambo sawa na kuwa na Chama cha siasa ambacho kitakuwa kimezingatia mambo yote muhimu ambayo yanatambulika kwa mujibu wa sheria hiyo,"amesema. 

Amefafanua kuwa wameona umuhimu wa kuzungumzia sheria hiyo pamoja na nyingine kwa kuwa wao ndio wenye Serikali na ndio watakaobeba lawama siku mambo yakiharibika."Tumekutana nanyi hapa leo hii kufafanua mambo yalijiri bungeni maana hatutaki kuona wengine wakipotosha, hivyo ni jukumu letu kuwaambia ukweli ili umma ujue." 

Mapunda amesema tangu nchi yetu iingie kwenye mfumo wa Vyama vingi tumefikisha miaka 26 na katika kipindi chote hicho kuna mambo mengi kama Taifa limejifunza na hivyo sasa wameamua kuja na Sheria ambayo itaimatisha vyama vya siasa na hasa kuwa kama taasisi inayoeleweka na sio kuwa na vyama vya siasa ambavyo ni vya mifukoni.

 "Tumeshuhudia malalamiko mengi kutoka kwenye baadhi ya vyama vya siasa , kumekuwepo na malalamiko ya matumizi ya fedha.Kuna vyama vya siasa imefikia mahali Mwenyekiti anakopesha fedha kwa chama.Kupitia Sheria ya Vyama vya Siasa inakwenda kuweka utaratibu mzuri wa namna gani chama cha siasa kinatakiwa kuendeshwa,"amesema Mapunda na kuongeza Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu sheria hiyo. 

 Wakati huo huo Mbunge wa Mlalo mkoani Tanga Rashid Shangazi ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hatua ya baadhi ya mapori kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za Taifa ambapo mbali ya kutunza na kuhifadhi mazingira, ni fursa muhimu kwa wawekezaji kuwekeza katika hifadhi hizo kwa kujenga hoteli za kitalii. 

Ametaja hifadhi hizo ni hifadhi ya Taifa Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Chief Rumanyika ambapo amesema pia ni vema TANAPA wakakaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuangalia namna ya kuangalia namna gani wanaweza kuweka mazingira mazuri ya msamaha wa kodi kwa baadhi ya vifa kwani TANAPA watakuwa na jukumu la kujenga miundombinu mbalimbali kwenye hifadhi hiyo. 

 Pamoja na mambo mengine wabunge hao wa CCM wametoa ufafanuzi kuhusu madai ya kupotea kwa fedha Sh.trilioni 1.5 ambapo wamefafanua madai hayo hakuna ukweli wowote bali kuna moja wa Bunge anachokifanya ni kupotosha umma. Wabunge hao wamesema hata Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) imethibitisha hakuna upotevu wa fedha hizo na hivyo wamewahakikishia Watanzania kupuuza madai ya uwepo wa upotevu wa fedha hizo.

Kocha KMC na mchezaji wa Alliance wakabidhiwa tuzo za Bikosports

$
0
0
 
Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije akiwa pamoja na Mchezaji wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania, Dickson Ambundo.
Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije, akionyesha furaha baada kupokea tuzo ya Bikosports Tanzania, kufuatia kuwa kocha kocha bora wa mwezi Januari, ambapo Kampuni ya BikoSports waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Picha na Mpigapicha Wetu.
Mchezaji wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania, Dickson Ambundo, akiwa mwenye shangwe nyingi baada ya kupokea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi January kutoka kwa Msemaji wa Bikosports, Geofrey Lea, waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani ambao ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

WAENDESHAJI wa mchezo wa kubashiri matokeo wa Bikosports, jana wamewakabidhi tuzo zao,  Etiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na mchezaji wa Alliance FC ya jijini Mwanza, Dickson Ambundo, baada ya kuibuka kocha bora na mchezaji bora wa mwezi January.

Makabidhiano ya tuzo hizo yalifanyika Makao Makuu ya Bikosports jijini Dar es Salaam, huku tuzo hizo zikiwa na lengo mahususi la kuongeza ari katika harakati za kukuza na kuendesha mpira wa miguu nchini Tanzania.

Akizungumzia tuzo hiyo, Kocha wa KMC, Etiene Ndayiragije, aliwashukuru Bikosports kwa kuamua kuingia kwenye tuzo hizo akiamini kuwa kwa pamoja zitafanikisha sekta ya mpira wa miguu kupiga hatua kubwa.

"Nawashukuru walioniona kwamba nastahili kuwa kocha bora wa mwezi January, huku tuzo hii nikiamini nimeipata kwa sababu ya sapoti kubwa ninayoipata kutoka kwa wachezaji wangu wote pamja na uongozi wangu wa KMC," Alisema Ndayiragije.

Naye Ambundo aliyeibuka kwenye Mchezaji Bora wa mwezi January, alisema kwa kupata tuzo ya Bikosports anaamini ataongeza bidii kubwa katika safari yake ya mpira wa miguu, jambo ambalo limechangiwa na nguvu kubwa anayoiweka katika timu yao ya Alliance yenye ndoto kubwa ya kufanya vizuri.

"Nadhani nimestahili kabisa kuitwaa tuzo hii na ninaamini kuwa naweza kuipata tena kwa sababu lengo langu ni kucheza mpira mzuri na kuisaidia timu yangu ya Alliance, hivyo ninachofanya ni kuongeza nguvu katika kumsikiliza mwalimu wangu, kuishi vizuri na wachezaji wenzangu ili wote tufikie malengo yetu," Alisema Ambundo.

Akizungumzia tuzo hiyo, Msemaji wa Bikosports, Geofrey Lea alisema kuanzisha tuzo hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kwamba mpira unakuwa kwa kiasi kikubwa, huku wakiomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu wakiwamo wanaobashiri matokeo kwa kupitia kampuni yao ya Bikosports.
"Hii ni safari nzuri ya kukuza mpira wa miguu hivyo wadau wote kwa pamoja tunaomba ushirikiano wao, ambapo katika nyanja ya ubashiri wa matokeo, 

Bikosports ndio Kampuni inayotoa zawadi kwa haraka huku jamvi lao likiwa ni rahisi kushinda kuliko michezo yoyote Tanzania, ambapo namba ya Kampuni ni 101010, huku mchezaji akiweza kubashiri kwa simu ndogo kwa namba *149*89# au wanaobashiri kwa mtandao https://www.bikosports.co.tz/ ambao ni rahisi kucheza na kushinda pia," Alisema Jeff Lea.

Kuanzishwa kwa tuzo ya Bikosports kwa kocha bora na mchezaji bora ni sehemu muhimu ya kuhakikisha kwamba wachezaji na makocha wao wanaongeza bidii kubwa katika kuhakikisha kwamba wanapata maendeleo makubwa ndani ya uwanja, ambapo mbali na tuzo hizo, pia huambatana na Sh Milioni moja.
mwisho

Mloganzila yapongezwa kuimarisha huduma kwa wananchi

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Charles Majinge (kulia) akizungumza katika kikao cha kawaida cha bodi hiyo kilichofanyika katika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka, Oktoba hadi Desemba, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Charles Majinge alipokua akizungumza katika kikao hicho.
Mjumbe wa bodi Dkt. Grace Magembe akichangia jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika Hospitali ya Mloganzila.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Andrea Pembe (kushoto) akizungumza katika kikao hicho, kulia ni Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo.
Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wapili kushoto) akiwaelezea wajumbe wa bodi utoaji wa huduma katika hospitali hiyo. Wajumbe hao wamepata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma katika hospitali hiyo.



Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeupongeza Uongozi wa kwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali ya Mloganzila.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Prof. Charles Majinge katika kikao cha kawaida cha Bodi hiyo kilichofanyika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka cha Oktoba hadi Desemba, 2018.

Nafahamu kumekuwa na changamoto kadhaa katika Hospitali hii ya Mloganzila, lakini nafurahi kuona kila siku Menejimenti inavyotatua changamoto hizo na hivyo wananchi kuitikia wito wa kutumia huduma zinazopatikana hapa, aliema Prof. Majinge.

“Napenda kwa dhati kabisa mfahamu kuwa Bodi yangu tunaridhishwa sana na utendaji kazi wa Hospitali ya Mloganzila kwani hata malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi kuhusu utoaji wa huduma yanaendelea kupungua siku hadi siku, hivyo hii ni hatua nzuri na ya kupongezwa”, alisema Prof. Majinge.

Sisi kama Bodi ya Wadhamini, tunaomba kila mmoja wenu atimize wajibu wake mahali pake pa kazi ili Mloganzila iwe moja ya hospitali bora hapa nchini katika kutoa huduma za kibingwa, kufundisha na kufanya tafiti, alisisitiza Prof. Majinge.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ambaye pia ndiye mwenye dhamana ya kusimamia Hospitali ya Mloganzila alisema pamoja na hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, Menejimenti imejipanga kuhakikisha inatoa huduma za kibingwa na za kibobezi kama ilivyokusudiwa.

Naye Kaimu, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema kumekuwa na ongezeko la wagonjwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka ambapo wagonjwa wa nje 20,173 walihudumiwa ukilinganisha na wagonjwa 17,116 waliohudumiwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 17.8.

Dkt. Magandi amesema upande wa wagonjwa waliolazwa kulikuwa na ongezeko la asilimia 29.6 kutoka wagonjwa 1,459 hadi 1,891, wakati upande wa huduma za upasuaji jumla ya wagonjwa 649 walifanyiwa upasuaji ukilinganisha na upasuaji wa wagonjwa 267 katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ambalo ni ongezeko la asilimia 143.


Kwa upande wa huduma za tiba shirikishi inayojumuisha maabara na huduma za radiolojia kulikuwa na ongezeko la huduma ambapo maabara ilipokea jumla ya sampuli za vipimo mbalimbali 28,907 kwa wagonjwa waliolazwa na wa nje ukilinganisha na sampuli 16,233 katika robo ya kwanza ya mwaka ikionesha ongezeko la sampuli 12,674 ni sawa na asilimia 78, alisema Dkt. Magandi.

Dkt. Magandi alisema katika huduma za radiolojia zinazojumuisha vipimo vya CT scan, MRI, X-ray n.k kulikuwa na ongezeko la vipimo asilimia 47 ambapo vipimo 5,221 vilipimwa katika kipindi hicho ukilinganisha na vipimo 3,541 na huduma katika maeneo yote ya Hospitali zinaendelea kuimarishwa siku hadi siku.

Oktoba 3, 2018 Serikali iliiweka Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC) Mloganzila chini ya Mamlaka ya Usimamizi na Uendeshaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

MNH inasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru hivyo ili kuhakikisha shughuli za utoaji huduma zinaendelea kutekelezwa, Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kikao chake cha 18 kilichofanyika Oktoba 12, 2018 ilimteua Dkt. Julieth Magandi kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mloganzila. Kutokana na uteuzi huo Dkt. Magandi anaripoti chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ili kusimamia shughuli za kila siku za hospitali hiyo.

Kwa sasa MNH imeweka mikakati ya kuimarisha huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kibingwa ili kutimiza majukumu yake kama ilivyokusudiwa. Hospitali hiyo ina vitanda 608.

Hospitali ya Mloganzila ni inatoa huduma za tiba za kibingwa na kibobezi, mafunzo na tafiti. Hospitali hiyo ilifunguliwa rasmi tarehe 25 Novemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

UCHUNGUZI WA AFYA KWA WATOTO WACHANGA BILA MALIPO - CCBRT.

Airtel yakusanya pesa kusaidia bima ya afya kwa watoto wenye mazingira magumu

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kupitia kitengo chake cha Huduma kwa wateja wakubwa wameshiriki kampeni maalum yakusaidi jamii inayojulikana kama Aitel Tunakujali kwa kuandaa hafla maalum ya Chai ya asubuhi (breakfast) iliyowakutanisha na wateja wao wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha ili kuwasaidia watoto zaidi ya 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama za kuwalipia huduma za afya.

Airtel Tunakujali ni programu maalum ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo uchangia sehemu ya kipato chao kwa ajili ya huduma za kijamii na hasa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akiongea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa wateja wakubwa Boniface Mbwambo alisema kuwa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakubwa na makampuni wameamua kuja pamoja na kukusanya fedha hizo ambazo zitaelekezwa kwenye ksaidia kufanikisha kuwapa bima afya kwa watoto 100 hapa nchini. 
 

‘Kama unavyoona hapa leo hawa wote ni wafanyakazi wa Airtel ambao tumeungana na baadhi ya wateja wetu ambapo tumeamua kuja pamoja na kukusanya fedha kwa lengo ya kuasaidia Jamii yetu inayotuzunguka na yenye uhitaji maalum. Kwa miaka kadhaa sisi wafanyakazi tumekuwa tukifanya hivi na kwa kweli tumeona ni kwa jinsi gani Jamii imekuwa ikiguzwa na michango yetu, alisema Mbwambo.

Tumeona ni vyema tuelekeza makusanyo yetu ya siku ya leo kwenye kusaidia afya kwa watoto ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa bidii kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata tiba pale atapohitaji, Mbwambo.

Mbwambo aliongeza kuwa tukio la leo la kukusanya fedha limefanikiwa sana kwani muitikio ni mkubwa mno. ‘ Natoa pongezi zangu za dhati kwa wanafanyakazi wenzangu wa muitikio na hamasa yenu mkubwa. Lazima niwaambie ya kwamba kuwepo kuweni hapai hii ya leo ndio kumeifanya tukio letu kupata mafanikio. Vile vile, napenda kutoa pongezi kwa uongozi wa Airtel, vitengo vingine na wadau wote kwa kutuunga mkono, alisema Mbwambo.
Kwa upande wake, Teddy Chamsama Meneja wa Airtel kitengo cha wateja wakubwa alisema kuwa Airtel Tunakujali imekuwa ikisaidia Jamii yenye uhitaji maalum kwa lengo la kuonyesha kujali na pia kuwafanya wajisijikie kama wenzao kwenye Jamii.


Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw Sunil Colaso akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Airtel waliohudhuria hafla ya chai ya asubuhi maalum kwa kuchangisha fedhazitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel. katika hafla hiyo zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Airtel wanaohudumia wateja maalum na makampuni wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na kitengo hicho kwa lengo la kukusanya fedha zitakazolipia BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kumudu gharama hizo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wafanyakazia wa Airtel pamoja na baadhi ya wateja wake, zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa


Mkurugenzi kitengo cha wateja wakubwa na Makampuni wa Airtel Bw, Boniface Mwambo akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa wakala wa barabara nchini (Tanroad) wakati wa hafla ya chai ya asubuhi iliyoandaliwa na Airtel kitengo cha wateja wakubwa kwa lengo la kukusanya fedha zitakazotumika kulipa BIMA ya Afya kwa zaidi ya watoto 100 ambao wazazi wao wameshindwa kulipia bima watoto wao. Hafla hiyo ilifanyika katika makao makuu ya Airtel mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na wafanyakazia na baadhi ya wateja wa Airtel.zaidi ya shilingi milioni 6 zilikusanywa

Waziri Mwakyembe amtaka Mhandisi Jengo la Wizara kuongeza juhudi ili kumaliza kwa wakati

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 akisaini kitabu cha wageni alipofika katika kiwanja ambacho ujenzi wa ofisi ya wizara unaendelea katika Mji wa Serikali uliyopo maeneo ya Ihumwa jijini Dodoma,kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi huo ambao unatakiwa kumalizika hivi karibuni,anayemulikia tochi ni Mhandisi Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo la Wizara Bw. Hagay Mziray kutoka Kampuni ya Mzinga Holding Company Ltd.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akimsikiliza Mhandisi Hagay Mziray (kulia) kutoka Kampuni ya Mzinga Holding Company Ltd alipokuwa akitoa maelezo kuhusu hatua walizofikia katika ujenzi wa ofisi hiyo ya Wizara,usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 wakati Mheshimiwa Waziri huyo alipotembelea eneo hilo la ujenzi kufuatila utendaji kazi na kasi ya ujenzi ya ofisi hiyo unaotarajiwa kumalizika hivi karibuni, katika Mji wa Serikali uliyopo eneo la Ihumwa Jijini Dodoma,wapili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Hagay Mziray Mzinga Holding Company Ltd ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo la wizara kwa kumtaka aongeze juhudi ili waweze kumalizi kazi hiyo kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya wizara unaondelea katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Hagay Mziray Mzinga Holding Company Ltd ambaye ndiye msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo la wizara kwa kumtaka aongeze juhudi ili waweze kumalizi kazi hiyo kwa wakati, alipofanya ziara ya kukagua ujenzi huo usiku wa kuamkia leo Jumatatu Februari 11,2019 kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya wizara unaondelea katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

………………………………………………………………………..

Na Anitha Jonas – WHUSM- Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt.Harrison Mwakyembe amemtaka Mhandisi wa Ujenzi wa Jengo la Wizara katika Mji wa Serikali kuongeza juhudi ili kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa maagizo hayo usiku wa kuamkia Februari 11,2019 alipofanya ziara yake katika eneo hilo panapojengwa katika Ofisi za Wizara eneo la Ihumwa Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo na kasi ya utendaji kazi kwa masaa ishirini na nne ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliyopangwa.

‘’Kwanza nawapongeza kwa jitihada mnazozionyesha kwa kuifanya kazi hii kwa masaa ishirini na nne na kwa kazi mliyokwisha kuifanya mpaka sasa, ila nataka niwasisitize kuwa mnahitaji kuongeza juhudi zaidi ili muweze kumaliza ndani ya muda uliyopangwa na mjue kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu anatarajia kuja kukagua ujenzi huu hivi karibuni,hivyo basi mkumbuke mlimwaahidi nini kwani atahitaji mkamilishe ahadi mliyompa,’’alisema Mhe.Dkt.Mwakyembe.

Naye Mkandarasi Msimamizi wa Ujenzi wa Jengo hilo la Ofisi za Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kutoka Kampuni ya Mzinga Holdings Company Ltd Mhandisi Hagay Mziray alimweleza Mheshimiwa Waziri Mwakyembe kuwa kwa sasa kazi zinazoendelea ni pamoja na upakaji wa rangi nyeupi kabla ya kupaka rangi,usimikaji wa mabomba ya vyoo na umeme na wanatarajia kufunikia chemba za maji taka pamoja na shughuli nyingine mbalimbali.

‘’Hatua ya ujenzi wa jengo ilipofikia kwa sasa ni sawa na majengo mengine ya ofisi za wizara mbalimbali yaliyopo katika Mji huu wa Serikali kwa sasa na wote tunajitahidi kukamilisha kazi hii kwa wakati, ila kufuatia changamoto mbalimbali tuliandika barua ya kuomba kuongezewa siku za kukabidhi jengo hili kuweza kuwa Februari 28,2019 badala ya Februari 15,2019,’’alisema Mhandisi Mziray.

Akiendelea kuzungumza Mhandisi Mziray alisema pamoja na hapo awali jengo hilo kuonekana kuwepo nyuma katika ujenzi wake kwa sasa hatua walizofikia ni nzuri na hatua wanayoelekea kwa sasa ni ukamilishaji wa ujenzi huo ikiwemo kupaka rangi na kuanza kuweka tiles na kuweka celing board.

Halikadhalika nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu Bibi. Prisca Shewali alimsitisiza mhandisi huyo kuhakikisha wanafunika mashimo hayo ya maji taka kwa zege haraka ili kuepusha athari zinazoweza kutokea kutona na shughuli nza ujenzi zinazoendelea mahali hapo.

DODOMA IKO TAYARI KWA MAPOKEZI YA RAIS MAGUFULI –ASKOFU MALLASY

$
0
0

*Asema Mkesha Mkubwa wa Kitaifa mwaka huu utafanyika Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC), Dk. Godfrey Mallasy amesema Jiji la Dodoma kwa sasa ni shwari na liko tayari kwa ujio wa Rais, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumapili, Februari 11, 2019) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye kanisa la Dodoma Christian Centre mara baada ya kumaliza ibada maalumu ya kuombea ujio wa Rais Magufuli jijini Dodoma.

Askofu Mallasy alikuwa akihitimisha semina ya siku nne ya jinsi ya kutambua madhabahu zinazokutesa na kuzivunja na kisha kufunguliwa.

Alisema TFC iliandaa semina hiyo kwa kushirikiana na makanisa mengine na kuamua kuhitimisha kwa maombi ya kuvunja madhabahu za mkoa wa Dodoma na kujenga madhababu ya kitaifa.

“Ndoto ya Serikali kuhamia Dodoma inakaribia kutimia kwa sababu wizara zote zimeshahamia hapa na Mheshimiwa Rais wetu anakaribia kuhamia. Kwa hiyo, viongozi wa kiroho tunao wajibu wa kumuandalia makazi yake ya kiroho. Jambo lolote likitokea, basi ujue limeanzia rohoni,” alisema.

“Leo tuko Dodoma, madhabahu ya hapa inasema kila kitu kitadidimia (kutokana na asili ya neno Dodoma – idodomya- linalomaanisha kudidimia). Na falme za hapa zimetamka hilo lakini baada ya maombi haya, sisi tunasema Dodoma haitadidimia, bali itaamka.”

Alisema maneno hayo kupinga hali ya uduni wa Dodoma, yanaendana na ujasiri wa Serikali ya awamu ya tano kuhamishia shughuli zake zifanyike makao makuu ya nchi, Dodoma.

“Rais wetu anakuja hapa na ana ndoto kubwa, je ndoto hizo zitaenda wapi? Jeshi la Mungu liko hapa, kwa hiyo ndoto hizo hazitadidimia kama jina lilivyo. Kupitia kuangusha ngome na madhababu za Dodoma, mambo yanaenda kubadilika,” alisisitiza.

Alisema maombi hayo yamefanyika ili Rais Magufuli aweze kutawala kwa amani na kutekeleza ndoto zake za kuijenga Tanzania mpya kwa mafanikio makubwa. Alisisitiza Watanzania wote, kuanzia kwenye ngazi ya familia, waendelee kuliombea Taifa liwe na amani kwa sababu pasipokuwa na amani, hakuna kinachoweza kufanyika.

Mapema, katika ibada hiyo, Askofu Mallasy aliwaongoza wachungaji wengine 20 wa TFC kutoka mikoa mbalimbali nchini pamoja na wachungaji kutoka makanisa ya FPCT, EAGT, TAG, KKKT na Anglikana kuimba wimbo wa Taifa na kufanya kitendo cha kumpokea Rais Magufuli.

Pia aliongoza waumini mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo kuvunja madhabahu kwenye mihimili yote mitatu ya nchi yaani mahakama, Bunge na Serikali kwa kutaja wizara mbalimbali, kuwaombea wakuu wa mikoa yote, wilaya zote, wakurugenzi wa halmashauri zote za Majiji, miji, manispaa na wilaya.

Wakati huohuo, Askofu Mallasy ametangaza kwamba Mkesha Mkubwa wa Kitaifa ambao hufanyika tarehe 31 Desemba kila mwaka kwa ajili ya kuliombea Taifa, mwaka huu utafanyika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Mkesha wa kuliombea Taifa, umekuwa ukifanyika nchini kila mwaka kuanzia mwaka 1997.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Fellowship of Churches (TFC), Dk. Godfrey Mallasy (kushoto) akiwaongoza wachungaji mbalimbali kuimba wimbo wa Taifa ikiwa ni ishara ya kumpokea Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika katika kanisa la TFC Dodoma Christian Centre tarehe 10 Februari, 2019. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Dodoma Christian Centre, Rose Amani.



Mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar)

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkuurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar)Bw. Mahmoud OmarHamad na kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango toka Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Zanzibar) Bi. Saum Ali Said.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango toka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Bw. Petro Lyatuu (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakiendelea na kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa mkutano wa ushirikiano kati ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (Tanzania Bara) na Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale (Zanzibar) wakiendelea na kikao cha kujengeana uwezo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM –Dar es Salaam

KIKAO KAZI KILICHOWAKUTANISHA WATAALAM KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII NA MJI WA MAKAMBAKO

Ziara ya Kaimu Balozi wa Marekani mkoani Mara

$
0
0


Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson alipotembelea mkoani Mara leo (Februari 11). Katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mh. Vincent Anny Naanu (kulia), Bi. Karolina Mpapula, Katibu Tawala mkoa wa Mara (wa pili Kulia), na Bw. Emmanuel Kisongo (kushoto) Afisa Elimu Mkoa wa Mara.

Kaimu Balozi wa Marekani Dkt. Inmi Patterson akifurahi pamoja na walimu na wazazi wa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Mwisenge iliyopo mkoani Mara leo (Februari 11). Katika Ziara yake mkoani humo, Kaimu Balozi Dkt. Patterson pia anatembelea miradi mbalimbali iliyopo eneo la Ziwa Victoria inayofadhiliwa na serikali ya Marekani. (Picha: Ubalozi wa Marekani)

MAAFISA WA DRC WAWASILI NCHINI KUJIFUNZA SHUGHULI ZA TASAF.

$
0
0
Mkurgenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga (wa tatu kulia ) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka DRC ambao uko nchini kujifunza shughuli za huduma ya hifadhi ya jamii 
Ujumbe kutoka DRC ukimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,(anayeitazama kamera) kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya TASAF jijini DSM.

Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa JKCI na BENJAMIN MKAPA (BMH) waanza uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo

$
0
0


Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakimfanyia mgonjwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi kwa mara ya kwanza leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
Madaktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kufanya uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa mgonjwa wa kwanza kwa kutumia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwafundisha wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma kuhusu madhara ya moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure) kabla ya kuanza kwa uchunguzi wa mishipa ya damu ya moyo (coronary angiogram) kwa wagonjwa kupitia mtambo wa Cathlab. Mtambo huo wa Cathlab ambao ni maabara ya uchunguzi na matibabu ya mishipa ya moyo umeanza kufanya kazi leo na kuweza kutoa huduma kwa wagonjwa watano.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma pamoja na timu ya wataalamu wa Taasisi hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa kuzibua mishipa ya moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab (Catheterization) kupitia tundu dogo linalitobolewa kwenye paja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa BMH Dkt. Alphonce Chandika.Picha na JKCI

TUNAMFUNGA AL AHLY KATIKA UWANJA WETU WA NYUMBANI - SIMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MTANANGE wa michuano ya Klabu Bingwa kati ya timu ya Simba na Al Ahly y Nchini Misri unatarajiwa kuchezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa.
Mchezo huo umebakiza masaa machache kuweza kufikia majira ya saa 10 alasiri ya Februari 12, 2019.

Kuelekea mechi hiyo, Nahodha wa timu ya Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema kuwa anaamini mchezo huo utakuwa ni mgumu kwao ila watahakikisha wanautumia vizuri uwanja wa nyumbani. Tshabalala amesema, katika mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli nyingi sana ila alama zinazopatikana ni tatu kwahiyo wao kama wachezaji wamejizatiti kuweza kupata alama hizo wakiwa nyumbani.

“Tunaamini mchezo wetu wa kesho tunashinda na kikubwa ushindi wowote tutakaoupata alama ni zile zile tatu, ingawa wao walitufunga kwa goli nyingi ila sisi tutatumia uwanja wetu wa nyumbani kupata matokeo,”amesema. Amesema, kikubwa ni wachezaji kujituna uwanjani katika dakika zote 90 na pia mashabiki kujitokeza kwao kwa wingi uwanjani ni moja ya hamasa kubwa sana kwao. 

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa klabu ya Al Ahly kutoka Uarabuni amesema haiofii klabu ya Simba kwani waliweza kupata matokeo wakiwa nyumbani kwa ushindi mnono wa goli tano na wanaamini wanaweza kushinda tena hata wakiwa ugenini.

Simba atashuka tena dimbani  na Waarabu mapema kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo katika kundi D Al Ahly amekuwa kinara kwa kuwa na alama 7 akifuatiwa na Alh Alhy mwenye alama 4, Simba akishika nafasi ya tatu kwa alama 3 na JS Saoura akiwa na alama 2. Ikumbukwe  katika mchezo wao kwa kwanza uliopigwa Februari 02 dhidi ya Al Alhly Simba alikubali kupigo cha goli 5-0 akiwa ugenini nchini Misri.
Nahodha wa Simba Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuelekea mchezo wao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Alh Alhly utakaochezwa kesho katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Waziri Biteko afungua warsha kwa wadau wa madini Jijini Mwanza

$
0
0
Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani) amefungua warsha ya siku mbili kuanzia leo Februari 11, 2019 kwa wadau wa madini inayolenga kujadili maudhui ya kanuni mpya za uanzishwaji masoko ya madini kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni.

Warsha hiyo inayofanyika Jijini Mwanza imeandaliwa na Wizara ya Madini kupitia uratibu wa taasisi ya Uongozi Institute na kuwashirikisha wadau na viongozi mbalimbali kutoka mikoa 12 nchini. 
Waziri wa Madini, Doto Biteko (wa watu kushoto waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimali akiwemo Katibu Mkuu Tume ya Madini, Profesa Simon Msanjila, (wa pili kushoto waliokaa), Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wakuu wa Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo. 

Wengine waliokaa ni Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda (wa pili kulia) aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza pamoja na Mkuu wa Idara ya Mafunzo kwa Viongozi kutoka taasisi ya UONGOZI Institute, Kadari Singo (wa kwanza kulia) aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashari za Wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na Makatibu Tawala kutoka wilaya zilizoshiriki warsha hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wachimbaji wadogo wa madini.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa taasisi ya UONGOZI Institute.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AJUMUIKA NA ASKARI WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA WALIOSHIRIKI GWARIDE LA MIAKA 55 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

$
0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali.S.S.Mugoba, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwaka huu 2019.(Picha na Ikulu)
IMG_3471
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Kambi ya JWTZ Chukwani Zanzibar, kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na
IMG_3479
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama, ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kambi ya Chukwani kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kujumuika katika chakula maalum aliowaandalia kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar, Kanali S.S.Mugoba na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Mhe. Haji Omar Kheri,(Picha na Ikulu)
IMG_3485
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika Kambi ya Chukwani Zanzibar..(Picha na Ikulu)
IMG_3501
KAIMU Kamanda Brigedi ya 101 KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, akizungumza wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aki Mohamed Shein, kwa ajili ya Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika mwaka huu kisiwani Pemba January,12, 2019.(Picha na Ikulu)
IMG_3505
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika katika chakula maalum aliowaandalia, Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika kambi ya chukwani  walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zilizofanyika Kisiwani Pemba katika uwanja wa gombani.(Picha na Ikulu)
IMG_3519
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakijumuika katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_3522
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_3528
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)
IMG_3533
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAFANYABIASHARA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WAONESHA NIA YA KUITUMIA BANDARI YA TANGA KUPITISHA SHEHENA YA MIZIGO YAO

$
0
0
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Bandari hiyo kwa wafanyabiashara wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini waliotembelea na kuvutiwa kupitisha shehena za mizigo yao
Wafanyabiashara hao wakiendelea kupata ufafanuizi wa masuala mbalimbali
 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama kushoto akiwa na Katibu tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro wakitembelea eneo la Bandari ya Tanga

 Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na wafanyabiashara hao
 Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya akizungumza ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.
 Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro akizungumza kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima akizungumza katika hafla hiyo
 Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiashara kutoka mikoa ya Kanda ya Kaskazini wakifuatilia nyumba anayefuatilia ni Moni Jarufu PRO wa Bandari ya Tanga akifuatilia mkutano huo
 Wadau mbalimbali nao wakifuatilia ziara hiyo
Sehemu ya wafanyabishara wakifuatilia mkutano huo katikati ni Meneja wa Bohari ya Mafuta ya GBP mkoani Tanga Amour

WAFANYABIASHARA wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wameonesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kupitisha shehena ya mizigo yao baada ya kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa Bandari hiyo.

Wameonesha nia hiyo kwenye mkutano wa siku moja baina ya Uongozi wa mamlaka hiyo na wafanyabiashara hao na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha.

Katika mkutano huo wafanyabiashara hao waliongozwa na viongozi wa vyama vya Chemba za Biashara,Kilimo na Viwanda(TCCIA),Katibu tawala Msaidizi wa oa wa Kilimanjaro na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini na uongozi wa mamlaka ya Bandari Tanga.

Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama amefafanua kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake imeboresha miundombinu na mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo.

Amesema kuwa kutokana na maboresho hayo taratibu za uchukuaji wa mizigo zinatumia muda mchache tofauti na awali kutokana mamlaka zote za serikali zinazohusika na Bandari zipo kwenye jengo moja.

" Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi Bandari ya Tanga ni nzuri,salama kwa mizigo na ni ya uhakika kutokana tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi,miundombinu,utendaji kazi na Tehama" alisema.

Alieongeza " Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu" alisema.

Katika kusogeza huduma zake kwa wateja wa mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha tayari uongozi wa mkoa wa Arusha kupitia mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 500 eneo la Malula katika wilaya ya Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.

" Wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro mtakuwa hamna haja ya kuja hadi Tanga kuchukua mizigo mtakuwa mnasubiri mizigo yenu huko huko Arusha sisi tunamiambia gharama zetu tu mnalipia moja kwa moja na sisi tutajuana na Shirika la Reli( TRC) ambao tunategemea ukarabati wa reli ukikamilika uwatumie wao" alisema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya aliwasihi wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima amesema kuwa waliikimbia Bandari ya Tanga na kuhamia Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na urasimu uliokuwa unafanywa na taasisi za serikali zilizokuwa zinahusika na utoaji wa mizigo jambo ambalo lilikuwa linachelewesha mizigo.

" Leo mmetufumbua masikio kusikia haya mabadiliko sasa tunaahidi kutumia Bandari yetu kwa ajili ya kuingizia mapato serikali yetu, kwani neno Bandari ya Tanga tuliisahau kabisa" alisema.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Arusha Walter Maeda aliongeza kuwa kwa wafanyabiashara wa Arusha wanafahamu kuwa kikwazo kikubwa katika bandari ya Tanga ni taasisi za serikali katika kuchelewesha mizigo ndiyo maana waliachana nayo.

" Sisi tuliikimbia Bandari ya Tanga na kuamua kutumia Bandari ya Mombasa kutokana na nenda rudi zilizokuwa zinafanywa na TRA,TFDA,TBS kwa kweli walikuwa hawana ushirikiano mzuri hali iliyotuletea tabu sisi wafanyabiashara " alisema.

TANZANIA YAPIGA HATUA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia picha za Viongozi Waasisi wa Ukombozi wa Afrika, ndani ya ukumbi wa mkutano wa kimataifa wa (AU) mjini Addis Ababa Ethiopia Februari 11, 2019 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 11, 2019) wakati akitoa muhtasari wa yaliyojiri kwenye Mkutano wa 32 wa Wakuu wa nchi za Afrika (AU) unaofanyika Addis Ababa, Ethiopa. 

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo amesema katika mkutano huo pamoja na mambo mengine Serikali barani Afrika zimesisitizwa kupambana na wala rushwa, ambapo Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua katika mapambano hayo.

Mbali na kupiga hatua katika mapambano dhidi ya rushwa, pia Waziri Mkuu amesema ripoti ya kamati maalumu iliyoundwa kuhusu masuala ya afya inaonesha Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanya vizuri.

Waziri Mkuu amesema Tanzania imefanya vizuri katika kusimamia na kudhibiti malaria, mapambano dhidi ya ukimwi pamoja na utoaji wa huduma za afya kwa wananchi mpaka vijijini.

“Imetupa faraja kwa sababu ukaguzi uliofanywa na kamati maalumu ya maendeleo ya afya, iliyotembelea nchi za Afrika kuona mwenendo wa utoaji wa huduma za afya imeonesha kwamba Tanzania tupo kwenye kiwango kizuri.”

Waziri Mkuu amesema mafanikio hayo yamekuja baada ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kuongeza bajeti ya afya wizara kutoka sh. bilioni 37 hadi kufikia sh. bilioni 269.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema viongozi hao walizungumzia kuhusu mwenendo wa biashara kwa kutumia anga, bahari na biashara za nchi kavu ambazo zinafanywa na Bara la Afrika na Tanzania ni miongoni mwa ambazo zilikubaliana na uundwaji wa mkataba wa korido ya biashara.

Amesema viongozi hao wametakiwa waimarishe biashara na Serikali imetoa fursa ya wazi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje waje wawekeze na Tanzania iko tayari kuungana na Mataifa yakayofanya biashara nchini.

Katika mkutano huo, viongozi wa AU wamekutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu biashara, wakimbizi na usalama, pia wamemchagua Rais wa Misri, Abdul Fatta Al Sisi kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja huo.Al Sisi anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kumaliza muda wake baada ya kushika wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amesema licha ya changamoto zote zinazolikabili bara la Afrika, bara hilo limeacha milango yake wazi kwa wakimbizi, hivyo ameyataka nchi za Ulaya ambazo zimefunga milango yake kwa wakimbizi zijifunze kutoka kwa Afrika.

Guterres ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa 32 wa viongozi wa nchi wanachama za AU ambao kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu nı " Wakimbizi na waliorejea makwao".

Kiongozi huo wa AU ameongeza kuwa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto kuu tatu ambazo ni amani na usalama, maendeleo endelevu pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, FEBRUARI 11, 2019.

‘FAO’ NA H/W MISSENYI WAFANIKIWA KUREJESHA HALI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI WENYE MAJANGA.

$
0
0
Anaandika Abdullatif Yunus – Missenyi, Kagera.

Shirika la chakula Duniani FAO linalotekeleza mradi wa kurejesha hali kwa Wakulima waliopatwa na majanga mbalimbali kwa kushirirkiana na Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Lipo katika hatua za mwisho kukamilisha mradi huo ulioanza tangu Mwaka 2017, unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu huku mradi huo ukionekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mapema Akizungumza na waandishi wa habari Februari 11, 2019 wakati wa Kampeni ya Lishe na Mafunzo ya usindikaji, Kaimu Mratibu wa Mradi huo Bwn. Amoni Lugeiyamu ambae pia ni Afisa Kilimo Wilayani Missenyi, mafunzo yaliyofanyika katika kijiji cha Nyankere, amethibitisha juu ya Mafanikio hayo ambapo amesema kuwa, FAO Kupitia Halmashauri ya Wilaya Missenyi chini ya Timu ya wataalamu kutoka katika Idara ya Kilimo na Maendeleo ya jamii pamoja na kitengo kinachoshughulikia masuala ya lishe na Udumavu, mpaka sasa wamefanikiwa kuwajengea uwezo Wakulima kupitia semina na mafunzo mbalimbali, kugawa Vipando, Mbegu, Kuku na Vifaranga vya Samaki, Kutoa Elimu ya Lishe kwa Vijiji vinne, Kutekeleza Kampeini ya Lishe na Usindikaji kwa Vijiji Vinne vinavyolengwa na mradi huo, kuongeza uhakika wa chakula kwa kaya lengwa, sambamba na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kinga njaa (mihogo na viazi).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanufaika wa mradi huo wameshukuruku Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya Missenyi kuwa nao bega kwa bega kwa kipindi chote tangu kutokea kwa majanga hayo, na zaidi kuonekana kufurahishwa na uzalishaji wanaofanya kwa sasa lakini kubwa ikiwa ni elimu na mafunzo mbalimbali ambayo wamekuwa wakipatiwa, ambayo yamekuwa chachu ya kufikia malengo ya mradi. 

 Kwa Wilaya ya Misenyi tayari FAO wametekeleza kwa Mafanikio makubwa Mradi Huo kwa Kuzifikia kaya za Wakulima zipatazo 709 Ndani ya Vijiji (5) vya Minziro, Karagala, Kikono, Nkerenge na Nyankere, ambapo wanufaika wa mradi huo ni pamoja na Vikundi vya Kijamii, akina mama, wajasiliamali, wafugaji, na Wakulima kwa jumla yake ni Vikundi 20.

Mradi kama huo pia unatekelezwa katika Wilaya za Bukoba Manispaa, Bukoba Vijijini, Kyerwa na Muleba hivyo kufanya jumla ya Wilaya (5) ndani ya Mkoa wa Kagera. Wilaya hizo ni zile ambazo kwa kiasi kikubwa zimekumbwa na majanga mbalimbali Mkoani Kagera , yakiwemo yale ya Ukame, Mvua, Tetemeko, na Magonjwa ya mimea.

Bi. Nailath Idrisa (63) Mkazi wa Kijiji cha Nyankere akifanya majaribio ya kukata kukata Viazi lishe kwa kutumia mashine maalumu wakati wa mafunzo yanayotekelezwa na FAO kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Missenyi.
Pichani ni Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bi Zenath Hassan (Mratibu wa lishe) akiendelea kufundisha masuala ya lishe kwa Wakazi na Kijiji cha Nyankere Wilayani Misenyi.
Pichani Ni Kaimu Mratibu wa Mradi wa FAO Bwn. Amon Lugeiyamu (Afisa Kilimo, Missenyi) akizungumza na Vyombo vya Habari juu ya Mafanikio ya Utekelezwaji wa mradi wa urejeshaji hali kwa Wakulima na Wafugaji waliopatwa na Majanga Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.
Pichani anaonekana BIi. Godbeltha Reveliani (53) Mkazi wa Kitongoji Kigarama Kata Mabale, akifurahia somo la usindikaji na utengenezaji chichili, katika Kampeni ya Lishe na Usindikaji, pembeni ni rafiki yake Bi. Grace John (54).
Pichani ni Bwn. Abdulkadiri Biligenda (44) Mkazi wa Nyankere akisaidiwa na mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Fredrick Kitone jinsi ya ukataji wa viazi lishe katika vipande vidogo (crips) tayari kwa kukaangwa na kuliwa.
Pichani baadhi ya akina mama kutoka Vikundi mbalimbali kaya tofauti Kijiji Nyankere, Wilayani Missenyi, wakimenya Viazi lishe tayari kwa usindikaji, wakati wa mafunzi ya lishe yaliyortibiwa na FAO kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Missenyi Februari 11, 2019. (Picha zote na Abdullatif Yunus).
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images