Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Mahojiano kamili na Balozi Masilingi na Mbunge Tundu Lissu


Kikao cha wadau wa sekta ya madini kwa ajili ya kujadili rasimu ya mwongozo wa ufungaji Migodi chafanyika Jijini Dodoma

$
0
0
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo akifungua kikao cha wadau wa sekta ya madini kwa ajili ya kujadili rasimu ya mwongozo wa ufungaji Migodi leo Jijini Dodoma.Kushoto kwake ni  Katibu Mtendaji Tume ya Madini Prof Shukrani Manya na Kulia kwake ni Mkurugenzi Ukaguzi wa Madini na Biashara ya Madini Venance Mwase na Mkurugenzi wa Ukaguzi migodi na Mazingira Dkt.Abdurahman Mwanga.
 Naibu Waziri wa Madini Mhe.Stanslaus Nyongo akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  kikao cha wadau wa sekta ya madini kwa ajili ya kujadili rasimu ya mwongozo wa ufungaji Migodi leo Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Ukaguzi migodi na Mazingira Dkt.Abdurahman Mwanga akiwasilisha muhtasari wa rasimu ya mwongozo wa ufungaji  migodi leo Jijini Dodoma.
 Katibu Mtendaji Tume ya Madini Prof Shukrani Manya akizungumza na wadau wa sekta ya madini kwa ajili ya kujadili rasimu ya mwongozo wa ufungaji Migodi leo Jijini Dodoma.

Washiriki wa kikao cha wadau wa sekta ya madini kwa ajili ya kujadili rasimu ya mwongozo wa ufungaji Migodi wakifuatilia  majadiliano mbalimbali  leo Jijini Dodoma.

Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.

VIJANA WATAKIWA KUBUNI TEKNOLOJIA ZA VIWANDANI

$
0
0
Ahmed Mahmoud,Arusha.
Vijana nchini wametakiwa kubuni teknolojia Zitakazowasaidia wajasiriamali walioko kwenye viwanda vidogo vidogo ili waweze kuuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa bora zinazohimili ushindani wa soko .

Hayo yameelezwa na Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda la Sido mkoani Arusha Linah Nchimbi  alipotembelewa na Vijana kutoka Majukwaa  ya Vijana yaliyoandaliwa na shirika la INFOY ambapo amewataka vijana wa kitanzania kubuni teknolojia badala ya kuwa tegemezi kwa kutumia teknolojia kutoka mataifa ya nje jambo ambalo linawanufaisha kuliko wao.

Nchimbi alisema kuwa Sido inatoa fursa kwa vijana kufika na kutumia ubunifu wao ambao unaweza kubadilishwa na kuingia kwenye mfumo wa kibiashara hivyo kuwanufaisha.

Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali La INFOY ,Bw.Laurent Sabuni aliyefanya ziara SIDO kuangalia teknolojia zilizobuniwa na wazawa huku  akiongozana na vijana kutoka katika majukwaa ya Vijana katika Wilaya ya Arusha amesema kuwa vijana wanapaswa kuwa wabunifu Na kubuni teknolojia ambazo zutasaidia taifa kusonga mbele kuelekea uchumi wa viwanda..

Sabuni alisema kuwa ziara hiyo inalenga kuhamasisha vijana kuongeza hamasa ya kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kutumia ubunifu na fursa zinazowazunguka. “Nchi yoyote haiwezi kuendelea kama hakuna ubunifu wa teknolojia na bidhaa mbalimbali ambazo nchi inaweza kuviuza katika masoko ya nje na kuleta faida” Alisema Sabuni

Johnson Joseph Mmoja kati ya vijana wameeleza kuwa suala la ubunifu kwa vijana linapaswa kuhimizwa na  kuhakikisha linaungwa mkono na wadau wa maendeleo kwa kutenga maeneo ya uzalishaji..

Alisema kuwa kwa sasa wameanza kujifunza kuanzisha miradi mbalimbali itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini ikiwemo ufugaji kuku,na usindikaji wa bidhaa za nafaka.
 Mratibu wa Shirika la INFOY Laurent Sabuni akifafanua jambo katika Mafunzo ya Ujasiriamali yaliyofanyika SIDO Mkoa wa Arusha
 Meneja wa SIDO mkoa wa Arusha Linah Nchimbi akitoa mada kwa vijana kutoka majukwaa ya vijana wilaya ya Arusha waliotembelea makao makuu ya SIDO mkoa wa Arusha kujifunza mambo mbalimbali.
 Baadhi ya Vijana kutoka majukwaa ya vijana Wilaya ya Arusha wakiangalia Mashine zilizotengenezwa na Wabunifu wazawa katika karakana za SIDO mkoa wa Arusha, ziara iliyoratibiwa na shirika lisilokua la kiserikali la INFOY la jijini hapa. Picha na Ahmed Mahmoud 
Vijana wakitembelea viwanda vidogo vidogo kwenye eneo la SIDO

YALIYOJIRI LEO BUNGENI JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Urambo, Margreth Sitta kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Busanda, Lolesia Bukwimba kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa, bungeni jijini Dodoma, Februari 8, 2019.

 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akiteta na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde, bungeni jijini Dodoma, Februari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiteta na Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso, bungeni jijini Dodoma, Februari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU LA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
  Spika wa Bunge Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Shirikisho la Mpira  wa Miguu la Watu wenye Ulemavu Tanzania.
 Rais wa Shirikisho la Mpira  wa Miguu la Watu wenye Ulemavu Tanzania Peter Sarungi  akimueleza jambo Spika wa Bunge Job Ndugai wakati walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Rais wa Shirikisho la Mpira  wa Miguu la Watu wenye Ulemavu Tanzania Peter Sarungi  (katikati) akimkabidhi jezi Spika wa Bunge Job Ndugai walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge Job Ndugai (wa pili kutoka kushoto) katika picha ya pamoja  na Viongozi wa Shirikisho la Mpira  wa Miguu la Watu wenye Ulemavu Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma.
PICHA NA BUNGE

Tanzania na Kuwait Zajadili Udhibiti wa Mipaka

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa yote nchini iliyopo mipakani

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa ya mipakani

“Kama Serikali tuna vipaumbele katika kudhibiti  mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu huo”alisema Masauni

Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti  wa mipaka.

“Tuna uhusiano mzuri baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak

Katika mazungumzo hayo pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika shughuli za uokozi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Balozi  wa  Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia),  juu  ya  kubadilishana  uzoefu katika Udhibiti  wa  Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni   juu ya kubadilishana  uzoefu  katika  Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi  Ndogo  ya  wizara, jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan  akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiagana na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo  hayo  yamefanyika  leo, Ofisi  Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mashua ya plastiki yatua Zanzibar, UN yapongeza SMZ kwa kukabili taka za plastiki

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kushoto), pamoja na Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (kulia) wakiongozana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (katikati) alipowasili  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume tayari kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kupitia Mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iliyopo kwenye fukwe za Forodhani visiwani humo. 
 Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kushoto), Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (katikati) pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (kulia) wakiwa kwenye chumba maalum cha wageni mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
 Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler (katikati) akitazama zawadi ya shati la kitenge alilokabidhiwa na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano-Afrika wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Mohamed Atani (kulia) huku Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya akishuhudia tukio hilo katika chumba maalum cha wageni mashuhuri mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

 Mashua iliyotengenezwa kwa taka za plastiki ikiwa imetia nanga kwenye fukwe za Forodhani visiwani Zanzibar iliyofanya safari kutokea LAMU-ZANZIBAR huku njiani ikiendelea na kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kupitia Mashua hiyo.
 Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler akishiriki zoezi la kusafisha pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Wakazi wa visiwani Zanzibar wakiwemo wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na watalii wakishiriki zoezi la kusafisha pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikani akishiriki zoezi hilo kwa kuokota taka za plastiki pembezoni mwa fukwe za Serena Hoteli kwa kuokota taka za plastiki ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Wananchi, wakazi wa Zanzibar na watalii wakitazama Mashua ya plastiki iliyotia nanga katika fukwe za Forodhani ikiwa ni kampeni ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akiagana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za wizara hiyo visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akifurahi jambo na Mwakilishi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya (kushoto) mara ya mazungumzo na ugeni kutoka UNEA uliofika ofisini kwake visiwani Zanzibar
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyefika ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo. Kushoto ni Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ugeni huo visiwani Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa kwenye mazungumzo na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyefika ofisini kwake visiwani Zanzibar kwa ajili ya kampeni maalum ya kuhamasisha kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika picha ya pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler na ujumbe aliombatana nao kutoka Umoja wa Mataifa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza jambo na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira (ZEMA), Sheha Juma.
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid katika picha ya pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler aliyeambatana na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa nje ya jengo la Baraza la Wawakilishi visiwani Zanzibar.
 Kikundi burudani cha ngoma ya Kibati kikiimba wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Siti and The Band ikitoa burudani ya wimbo maalum unaohamasisha utunzaji wa mazingira unaoitwa “Tudumishe” wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wawekezaji wa Sekta ya Utalii Zanzibar (ZATI), Julia Bishop akitoa salamu za Umoja huo kuunga juhudi za kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na Mwanzilishi wa mradi wa Flipflopi –Clean Seas Expedition, Ben Morison wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iliyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe kabla kuelekea kupanda mashua hiyo alipowasili kwenye fukwe za Serena Hoteli visiwani humo. 
 Bidhaa zilizotengenezwa na Plastiki zikiwa kwenye banda la maonyesho wakati wa hafla ya kampeni ya kukabiliana na uchafu wa taka za plastiki baharini na fukwe iliyofanyika viwanja vya Forodhani visiwani Zanzibar.
 Hyuka Hwang kutoka ofisi za UNEP Tanzania akifurahia jambo alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi visiwani Zanzibar, Ayoub Mahmoud akizungumza machache kabla ya kumrabisha mgeni rasmi wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.
 Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki iluyotia nanga kwenye fukwe za Forodhani yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini na fukwe visiwani Zanzibar.

Na Mwandishi wetu
MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa kusimama kidete kupambana na taka za plastiki.
Aidha alisema kutokana na dhamira ya dhati  ya kukabiliana na taka za plastiki taifa hilo linatekeleza mkakati wa kupunguza umaskini na kukuza uchumi wa taifa pamoja na kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa lengo namba kumi na nne la kulinda uhai chini ya maji na lengo namba kumi na tano la kulinda uhai juu ya ardhi.
Mratibu huyo alisema hayo kwenye mapokezi ya mashua iliyotengenezwa kwa plastiki mjini hapa yenye kupeleka ujumbe wa kupambana na taka za plastiki baharini.
Katika hafla hiyo ambayo viongozi wengi wakiwemo wa serikali walihutubia, Alvaro aliipongeza Tanzania kwa kutenga maeneo ya hifadhi kwa ajili ya manufaa ya wananchi na dunia kwa ujumla na kutia saini mikataba mbalimbali ya hifadhi ikiwamo viumbe wanaotoweka.
Mashua hiyo iliyotengenezwa kwa kutumia mabaki ya plastiki yaliyokusanywa kutoka katika fukwe za Kenya, imeingia nchini juzi ikitokea kwenye mji wa Lamu.
Mashua hii iliyosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 500 imesimama katika visiwa kadhaa ili kueneza ujumbe kuhusu madhara yanayotokana na matumizi ya plastiki katika bahari.
Hassan Shafi mmoja wa waliounda mashua hiyo, anasema kilichosababisha ubunifu huu ni uwapo wa takataka nyingi za plastiki ambazo zinapatikana baharini na katika fukwe zinazotishia mazingira ya bahari na viumbe hai.
Alvaro katika mazungumzo yake alisema kutokana na kuzagaa kwa takataka upokeaji wa kampeni ya kusafisha bahari dhidi ya taka za plastiki unaonesha ni kwa namna gani Tanzania ipo tayari kuhifadhi mazingira kwa malengo hayo mawili.
Alisema tatizo la uchafuzi wa bahari limekuwa ni la kidunia na changamoto zake zinaangukia kwa wanaozunguka bahari.
Alisema dunia inatakiwa kuchukua hatua kama Zanzibar za kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki na pia mirija ya kunywea soda, chupa za plastiki na kuendesha kampeni vyombo vya baharini kuacha kutupa uchafu wa plastiki baharini. 
Pamoja na juhudi hizo ametaka kuongezwa kwa jitihada zaidi hasa katika kuelimisha jamii kuchukua jukumu la kutunza mazingira na kupambana na uchafuzi wa plastiki.
Alisema juhudi lazima zifanyike ili kuhakikisha kwamba tishio la kupoteza viumbe wanaoishi baharini katika miaka 30 ijayo linafutwa.
“Utafiti uliofanywa na UNEP unaonesha kwamba dunia itapoteza samaki na viumbe wengine wa baharini miaka 30 ijayo kama kasi ya uchafuzi wa mazingira kwa plastiki utaendelea kama ulivyo sasa” alisema.
Naye Rais wa Baraza Kuu la Kimataifa la Mazingira (UN Environment Assembly-UNEA), Siim Valmar Kiisler ambaye alifika nchini kwa ajili ya hafla hiyo, akizungumza na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mohamed Abood ofisini kwake Vuga, alisema wananchi wengi wanaozungukwa na ukanda wa bahari wapo hatarini kukabiliwa na magonjwa mbalimbali kutokana na ulaji wao wa  samaki ambao nao wengi huguguna taka za plastiki kama chakula chao cha kila siku.
Alisema watu wengi wamekuwa wakifurahia ulaji wa samaki bila ya kufahamu chakula anachokula samaki kuwa kinaweza kuwa na sumu isiyoweza kuonekana wala kuathiri kwa haraka.
Alieleza katika kujiepusha na mazingira hayo hatarishi jamii haina budi kutunza na kuenzi mazingira ya bahari ikiwemo kuacha tabia ya kutupa taka zote za plastiki katika maeneo ya bahari.
‘’Kuna watu ndani ya jamii yetu hususani wanaoishi kwenye ukanda huu wa bahari wanashindwa kujua kuwa taka zitokanazo na plastiki huweza kudumu hadi kwa miaka 500 baharini bila kuharibika’’aliongezea.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed alisema kuna changamoto mbali mbali za utunzaji na uhifadhi wa mazingira visiwani hapa.
Alisema jamii bado ina mwamko mdogo wa kutunza mazingira jambo ambalo amekiri kuwa ni changamoto ambayo inahitaji kusimamiwa ipasavyo.
Hata hivyo alisema anaamini ujio wa mashua hiyo iliyotengezwa kwa taka za plastiki utaleta ujumbe tosha kwa wananchi wa Zanzibar na maeneo mengine kuhifadhi mazingira yao yanayowazunguka.


RC TABORA ATOA MWEZI MMOJA KWA MA DC NA MADED MKOANI HUMO KUHAKIKISHA VITAMBULISHO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO VINAKWISHA

$
0
0
Na Tiganya Vincent
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imetoa mwezi mmoja kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji wote kuhakikisha zoezi la utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo linakamilika. Hatua hiyi imefikiwa baada ya kuona utekelezaji wa zoezi hilo unasua sua kwani hadi sasa ni vitambulisho elfu saba tu vilivyogawiwa kati ya elfu 25 vya awamu ya kwanza.

Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akikabidhi vitambulisho vingine elfu 40 kwa  Halmashauri  nane za Mkoa huo.   Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo ndicho kitakuwa kipimo cha utendaji kazi wao.

Alisema hatawavumilia watendaji hao watakaoshindwa kukamilisha zopezi hilo katika muda waliokubaliana na kuongeza Mtendaji atakayeshinwa atawajibishwa kwa kushindwa kutekeleza agizo wa Rais. Mwanri aliwaagiza Wakuu wa Wilaya zote mkoani humo kuongeza kasi ya ufuatiliaji ili wafanyabiashara wadogo wachukue vitambulisho hivyo na waweze kufanya biashara zao wakiwa uhuru.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema  zoezi la utoaji vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo hadi sasa ni asilimia 28 tu ndo vimegawiwa. Alisema kuwa hadi Februari 7 mwaka huu ni vitambulisho 7,013 ndivyo vilivyokwisha gawiwa kwa wafanyabiashara hao kati vitambulisho 25 elfu vilivyopokelewa  awamu ya kwanza.

Makungu alisema kwamba kiasi cha fedha kilichokusnywa kutokana na gharama za uchangiaji wa vitambulisho hivyo ni shilingi milioni 140.2 na zilizokwisha pelekwa mamlaka ya mapato ni milioni 135.9. Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) ndiyo inaongoza kwa kugawa vitambulisho vingi kwa wafanyabiashara wadogo kwani hadi sasa imegawa 2,529 kati ya 3125 ilvyopewa awamu ya kwanza.

Makungu alisema kuwa Desemba 19 mwaka jana kila Halmashauri ilipewa vitambulisho 3,125 kwa ajili ya wafanyabiashara hao lakini  baadhi yake zimegawa chini ya asilimia kumi hadi sasa wakati wahusika wapo. Katibu Tawala huyo Mkoa alisema Manispaa ya Tabora ndiyo imegawa vitambulisho vichache kwa wafanyabiashara hao kwani hadi sasa waliopata ni 150 sawa na asilima tano tangu zoezi hilo lilipoanza mwishoni mwa mwaka jana.
 Baadhi ya watendaji kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tabora wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali leo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa taarifa fupi ya idadi ya vitambulisho ambavyo vimeshagawiwa kwa wajasiriamali hadi kufikia leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maagizo leo kwa Watendaji wa Wilaya zote  ya kuhakikisha vitambulisho vyote vya wafanyabaishara ndogo ndogo viwe vimeshamalizika ifikapo Machi 8. 
 Wakuu wa Wilaya ya Mkoa wa Tabora( walio mstari wa mbele) wakisikiliza kwa makini maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha ) leo yakuwataka  kuhakikisha vitambulisho vyote vya wafanyabaishara ndogo ndogo viwe vimeshamalizika ifikapo Machi 8.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo(kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Abel Busalama (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 10,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Godfrey Ngupula (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo katika Halmashauri zake mbili za Wilaya hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri(kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kushoto) akimkabidhi vitambulisho 5,000 leo  Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa  (kulia) kwa ajili ya kugawiwa wafanyabiashara wadogo wadogo. Picha na Tiganya Vincent

NHC YAKABIDHI MIFUKO 200 YA SIMENTI KWA MKUU WA WILAYA NA KINONDONI

$
0
0

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imekabidhi jumla ya mifuko ya simenti 200 kwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Daniel  Chongolo ikiwa ni mchango wake kwa jamii katika kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa.

Akiongea wakati wa kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Chongolo, pamoja na kulishukuru Shirika la Nyumba la Taifa ameuelekeza msaada huo katika ujenzi wa madarasa katika shule za Sekondari ili kupunguza pengo la madarasa 100 yanayohitajika kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa kijuninga na elimu ya sekondari Januari Mwaka huu.

Alisema kuwa Wilaya ya Kinondoni ilipata baraka ya kusajili watoto wengi kwaajili ya kujiunga na elimu ya kidato cha kwanza na kwamba elimu bila malipo imehamaisha watoto wengi kujiunga na elimu hiyo na hivyo kusababisha kuwa na upungufu wa vyumba vya kujifunzia.

Alisema uongozi wa wilaya kwa maana ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri pamoja na watendaji wote kwa ujumla walichukua jukumu la kuendesha harambee itakayowezesha kujenga angalau madarasa 100 ili kukabili upungufu wa madarasa na yakamilike kabla ya Machi mwaka huu.

“Napenda kuwahakikishia wadau na watoto wetu waliobahatika kujiunga na elimu ya sekondari mwaka huu kwa wilaya ya Kinondoni kwamba, madarasa tunayoyapigia kampeni ya kuyajenga yatakamilika Machi na watoto kuingia, pamoja na changamoto ndogo ndogo tulizo nazo ambazo tutawaomba wadau waendelee kutuunga mkono kuzimaliza,” alisema Chongolo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani alisema kuwa Shirika limetoa vifaa hivyo ili kuhakikisha wanafunzi hawakosi masomo na wanasomea katika mazingira mazuri.
Alisema Shirika la Nyumba la Taifa liayo sera iliyojikita katika kusaidia vijana na kwamba sera hiyo imeshasaidia vijana takribani 6,000 nchi nzima kwa kuwapatia mashine za kufyatulia tofali za kufungamana kwa ajili ya kujengea nyumba na hivyo kujiongezea kipato.

“Pamoja na sera hii ya Shirika kujikita kuwasaidia vijana kujiajiri, pia shirika linasaidia katika sekta za afya na majanga mbalimbali yanayojitokeza ili kuwaokoa wanaokutikana na majanga,” alisema.

Alisema hii ni sehemu tu ta jitihada zao katika kuhakikisha sekta za elimu na afya, hasa kwa kizazi kijacho zinahudumia wananchi katika hali ya ubora.

Alisema kuwa sekta ya elimu ina changamoto nyingi lakini Shirika kwa kushirikiana na wananchi watahakikisha wanazikabili kwa kutoa misaada mbalimbali iliyomo ndani ya uwezo wao ili kuboresha mazingira ya usomaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akipokea mifuko 200 ya Saruji kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Shehena ya mifuko 200 ya Saruji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa, iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni. Kutoka kushoto ni Dereva wa Shirika la Nyumba la Taifa, Jackson Bagera, Afisa Manunuzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Paskalina Monko, Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Msigwa, Yahya Charahani na Kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Afisa Huduma kwa Jamii, Yamlihery Ndullah na wa kwanza kulia ni Abeld Ngassa Joram Afisa wa NHC.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (kulia) akisalimiana na Afisa elimu Sekondari wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Msigwa wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa, Yahya Charahani.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akisalimiana na Afisa Manunuzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Paskalina Monko.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akisalimiana na Dereva wa Shirika la Nyumba la Taifa, Jackson Bagera.
Shehena ya mifuko 200 iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya katika Shule ya Sekondari Turiani, Kinondoni ikiingizwa ndani ya ghala la kuhifadhia.

MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA BIDHAA ZA NGOZI CHA KARANGA, MOSHI WASAINIWA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Eliud Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa TIRDO (waliosimama) wakishuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mjini Moshi, uliosainiwa kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya viatu ya Karanga, Mhandisi Masoud Omari (katikati) na Mwakilishi wa Kampuni ya Italia ya ITALPROGETTI, Sergio Dani (kulia), leo februari 8, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya viatu ya Karanga, Mhandisi Masoud Omari (katikati) akibadilishana Mikataba ya utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga, mjini Moshi na Mwakilishi wa Kampuni ya Italia ya ITALPROGETTI, Sergio Dani (kulia) leo februari 8, 2019 jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Eliud Sanga (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa TIRDO (waliosimama) wakishuhudia utiwaji saini wa Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mjini Moshi, uliosainiwa kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya viatu ya Karanga, Mhandisi Masoud Omari (katikati) na Mwakilishi wa Mwakilishi wa Kampuni ya Italia ya TMC, Danielle Feradini. (kulia), leo februari 8, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Eliud Sanga akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utiwaji saini wa Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mjini Moshi, iliyofanyika leo februari 8, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akizungumza kabla ya hafla ya utianaji saini Mkataba huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Eliud Sanga akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike, wakati wa wakati wa hafla hiyo ya utiwaji saini wa Mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga, kilichopo mjini Moshi, iliyofanyika leo februari 8, 2019 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa wa Jeshi la Magereza waliohudhulia hafla hiyo.
Baadhi ya Maafisa wa Mfuko wa PSSSF na Wajumbe wa Bodi ya Karanga.
Meza kuu.


Picha ya pamoja.

MAKATIBU WAKUU WA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA KUJADILIANA MASUALA YA MUUNGANO

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kushoto) akiendesha kikao kazi cha Makatibu Wakuu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili juu ya uratibu na ufuatiliaji wa masuala ya Muungano.  Kulia ni Bw. Abdallah Mitawi Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ambae ni Mwenyekiti Mwenza. Kikao hicho kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma.
 Sehemu ya Wajumbe wa kikao hicho ambao ni Makatibu Wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) wakifuatilia kikao hicho. Jumla ya Makatibu Wakuu 26 kutoka Tanzania Bara wamehudhuria kikao hicho.
Sehemu ya Wajumbe wa kikao hicho ambao ni Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma. Jumla ya Makatibu Wakuu 13 kutoka Zanzibar wamehudhuria ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Kamati ya pamoja kitakachofanyika siku ya kesho Mjini Dodoma.

DStv yatangaza ofa kabambe ya Family!

$
0
0
Alhamisi Februari 07, 2019. Punde tu baada ya kumaliza ofa mahsusi ya kufunga mwaka iliyokuwa ikifahamika kama ‘’Muda wa kukiwasha na DStv’’ MultiChoice Tanzania leo imetangaza neema kwa wateja wake wapya watakaojiunga na DStv katika msimu huu wa wapendanao ambapo watajipatia zawadi kabambe ya kifurushi cha DStv Family kwa kipindi cha miezi miwili !

Ofa hiyo maalumu ijulikanayo kama ‘Jiunge na Family ya DStv’ ambayo imeanza mwezi huu itaendelea kwa muda wa miezi miwili hadi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu. Katika kipindi hicho wateja wote wapya wa DStv, wataweza kupata vifaa vyote vya DStv kwa shilingi 79,000 tu na kisha kupata ofa ya kifurushi cha DStv Family cha miezi miwili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo katika ofisi za MultiChoice Tanzania, Meneja Masoko Alpha Mria amesema kuwa ofa hii ni muendelezo wa ofa kedekede zinazoletwa na kampuni ya MultiChoice kwa wateja wake mara kwa mara.
Meneja Masoko MultiChoice Tanzania Bw. Alpha Mria akizungumza na waandishi wakati uzinduzi wa ofa mpya ya “Jiunge na Family Yetu” mapema leo katika makao makuu ya ofisi za MultiChoice Tanzania.

Amesema tofauti na ofa iliyopita ya muda wa kukiwasha na DStv ambapo mteja alikuwa anapatiwa mwezi mmoja wa kifurushi cha DStv Bomba 19,000/- sasa hivi ofa ya kifurushi imeongezwa thamani hivyo mteja mpya sasa anapata ofa ya kifurushi cha DStv Family 39,000/- tena siyo kwa mwezi mmoja tu, bali miezi miwili.

‘’Tunatambua kuwa huu ni mwanzo wa mwaka na majukumu huwa ni mengi hivyo tumeamua kuwatunuku wateja wetu wanaojiunga nasi wakati huu kwa kuwazawadia kifurushi cha Family chenye chaneli zaidi ya 90 kwa miezi miwili” alisema Alpha na kuongeza “Kwa kifurushi hiki, mteja wetu atafurahia maudhui mbalimbali ikiwemo tamthlia maarufu za ndani na nje, michuano ya ligi maarufu za soka duniani kama ligi ya Uingereza, Ligi ya Hispania (La Liga) Ligi ya Italia (Serie A), michezo na burudani nyingine kadha wa kadha kama mieleka, Taikondo, Ndondi, muziki bila kusahau Habari na vipindi vya elimu” huku akifurahia ligi maarufu kama Serie A, La Liga, Ligi kuu ya Uingereza, burudani ya mieleka WWE, ,filamu na tamthilia kali za kitanzania kama HUBA, Kapuni, Rebeca, Kitimtim bila kusahau kipindi maarufu cha umbea maarufu kama Shilawadu Xtra na vingine vingi ndani ya Maisha Magic Bongo DStv channeli (160).

Kwa upande wake, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Salum Salum amesema ofa hiyo ni kwa wateja wote wapya wanaojiunga na DStv kuanzia leo na kwamba ofa hiyo ni kwa nchi nzima. “Ofa hii ni kwa nchi nzima. Popote mteja alipo anaweza kupata huduma zetu kwani tuna mawakala nchi nzima” amesema Salum.
Mkuu wa kitengo cha mauzo na usambazaji MultiChoice Tanzania Salum Salum akifafanua kwa undani kuhusiana na Ofa mpya ya DStv inayojulikana kama “Jiunge na Family Yetu” mapema leo katika makao makuu ya ofisi za MultiChoice Tanzania.

“Mbali na kuendelea kufungua ofisi katika mikoa mbalimbali, tuna mawakala wakubwa na wadogo kila pembe ya nchi hii. Zaidi ya yote, mtu yeyote anayetaka kuunganishiwa DStv anaweza kutupigia simu maalum 0659 070707 au kutembelea kurasa zetu za Kijamii kama @Dstvtanzania Instagram, @DStv Facebook , @DStv_Tz Twitter na akitujulisha alipo tunamuunganisha na mawakala na mafundi wetu walio katika eneo husika” amesisitiza Salum. Kuhusu wateja waliopo, Salum amebainisha kuwa hivi karibuni MultiChoice itazindua promosheni kubwa na ya aina yake kwa wateja wake hivyo wakae mkao wa kula.
Wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania katika picha ya pamoja mara ya Uzinduzi wa ofa mpya ya “Jiunge na Family yetu” kutoka DStv.

Klabu tisa kuchuana kuogelea mashindano ya Taliss-IST Jumamosi na Jumpili

$
0
0
 Jumla ya vilabu tisa vimethibitisha kushiriki katika mashindano ya kuogelea ya Taliss-IST yaliyopangwa kuanza kesho kwenye Bwawa la Kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga Jumamosi na Jumapili.

Meneja wa klabu ya Taliss-IST, Hadija Shebe amezitaja klabu hizo kuwa ni Shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM), Wahoo (Zanzibar), FK (Dar es Salaam), ISM (Arusha),  Dar es Salaam Swimming Club (Dar es Salaam), Bluefins (Dar es Salaam) na Mwanza Swimming Club.

Pia katika orodha hiyo, kuna klabu ya Mis Piranhas (Morogoro), Champions Rise (Dar es Salaam) na wenyeji wa mashindani hao, Taliss-IST katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na  DStv, Jubilee Insurance,  Azam, Pepsi, K&K Company, SDS, RK Technotronics, Kaka's Restaurant, Wazazi wa waogeleaji wa klabu ya Taliss-IST  na  Subway Osterbay.

Hadija alisema kuwa vilabu hivyo vinatarajia kuleta zaidi wa waogeleaji 250 ambao watapambana katika umri tofauti. Kutakuwa na kundi la waogeleaji chini ya miaka 8, 9 na 10, 11 na 12, 13 na 14, na zaidi ya miaka 15.

Alisema kuwa mbali ya staili tano za kuogelea, waogeleaji hao watahsindanai katika relei ambayo kwa mtindo wa Individual Medley (IM) na Freestyle. Kwenye IM, waogeaji watachanganya staili nne ambazo ni butterfly, backstroke, breaststroke, na freestyle.

Zaidi ya waogeleaji 250 watashindana katika mashindano hayo ambayo washindi watazawadiwa medali na vikombe.

DAWASA YAJIBU KERO YA MAJI KWA WAKAZI WA MBEZI KWA MSUGULI NA VITONGOJI VYAKE

$
0
0
 Wakazi wa Mbezi Kwa Msuguli na vitongoji vyake jijini Dar es Salaam wanatarajia kuanza kupata maji bila ya mgao mara baada ya kukamilika uunganishwaji wa bomba jipya. Bomba hilo jipya la Mamlaka ya MajiSafi na MajiSafi (DAWASA) litajibu kero ya mgao waliyokuwa wakipata wakazi wa Bwaloni, Msaki, Saranga, Majengo mapya mpaka Malamba Mawili, Msingwa, Kanisa la Udongo, Kisiwani na vitingoji vyake. 

Akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la utomboaji wa Bomba, Msimamizi wa bomba kubwa la MajiSafi wa DAWASA Mhandisi Gibson Baragula amesema kwa kazi hiyo ilikuwa ni kutoa toleo la nchi 8 katika bomba kubwa la nchi 40 ambapo kazi imefanyika usiku wa kuamkia leo na zoezi hili linaenda kukamilika haraka. 

"Niwaombe wakazi wa Mbezi wa Msuguli na Vitongoji vyake wavumilie tumalize ili waweze kupata ya uhakika kwa vile yatakuwa na presha ya kutosha na wataweza kupata wote kwa wakati mmoja," amesema Mhandisi Baragula. 

Nae Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka amesema kazi kubwa imefanyika na inatarajiwa kumalizika mara baada ya masaa 48 na kuzaa matunda ili kuweza kuwapatia maji wakazi wa maeneo ya Mbezi kwa Msuguli na vitingoji vyake maji. "Kazi kubwa ilinakaribia kukamilika na wakazi wa Mbezi kwa Msuguli wakae mkao wa kunywa maji safi na salama," amesema. 

Ametoa wito kwa wakazi wote wa maeneo hayo kuendelea kuwa mabalozi wema kwa kuendelea kulipia bili zao za maji kwa wakati ili wawepe huduma bora. "Sisi wajibu wetu tunaenda kuukamilisha hivyo basi niwaombe wale wote wanaodaiwa kulipa madeni yao na pia tutapita nyumba kwa nyumba kufanya msako wa uhakiki wa wateja, Amesema. Maeneo ya Mbezi kwa Msuguli yamekuwa wakikosa huduma ya maji safi na salama kwa kipindi kirefu kutokana na miundombinu na jografia ya maeneo hayo.
Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka (kulia) na Msimamizi wa Bomba kubwa la MajiSafi na MajiTaka la DAWASA Mhandishi Gibson Baragula (kushoto) wakimwonyesha mwanahabari bomba lililotobolewa ili kuweza kusambazia maji wakazi wa Mbezi kwa Msuguli jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.

Wafanyakazi wa DAWASA wakiendelea na zoezi la uunganishaji wa mabomba. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Mkazi wa Arusha akabidhiwa mamilioni ya biko akiwa na mkewe

$
0
0

Mstaafu kutoka Wizara ya Kilimo, Daniel Shigela na mkewe wamekabidhiwa sh milioni tano kutoka kwenye bahati nasibu ya biko inayoendesha bahati nasibu nchini, huku ikitoa fursa za Watanzania kuibuka mamilionea kwa kushinda kwenye mchezo huo.

Makabidhiano hayo yamefanyika mkoani Arusha, akiwa sambamba na mkewe Edith Shigela ikiwa ni siku moja tu baada ya kushinda.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Shigela aliishukuru Biko kwa kumpatia fedha zake hizo akisema kuwa fedha hizo zitawanufaisha yeye na mkewe kwenye familia yao hiyo.

Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati  watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili

 Mstaafu kutoka Wizara ya Kilimo, Daniel Shigela, mwenye maskani yake Sombetini jijini Arusha, akiwa na nyuso ya furaha na mke wake Edith Shigela baada ya kukabidhiwa fedha zao sh milioni tano alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko inayondelea kumwaga mamilioni kwa Watanzania wanaocheza Biko mchezo huo ambapo sasa droo ya wapendanao ikichezeshwa na watu kuvuna fedha pamoja na bodaboda. Picha na Mpigapicha Wetu.
 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aongoza Kikao kazi cha Shirikisho za Kiuchumi za Afrika.

$
0
0
Addis Ababa, 7 February 2019.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana aliendesha kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 

Katika Mwaka 2017. Malaria iliua watu 435,000 duniani, wengi wao wakiwa ni watoto. Asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Africa. Pamoja na kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kutokomeza malaria, Ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kubwa katika juhudi za maendeleo. Ni katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria imeonelea ishirikiane na shirikisho hizo za kikanda kuwa na mikakati ya pamoja katika kutokomeza malaria.

Mhe. Kikwete aliitambulisha rasmi taasisi hiyo ya kutokomeza malaria kwa wajumbe. Taasisi hiyo iliyoanzishwa na Bill Gates pamoja na Ray Chambers kwa kushirikiana na taasisi ya wadau wa malaria inayojulikana kama Roll Back Malaria Partnership to end Malaria inajumuisha viongozi wenye nguvu za ushawishi na pia watu wenye uwezo wa kifedha ambao huziwekesha kwenye shughuli za maendeleo. 

 Wajumbe kwenye taasisi hiyo ni Bill Gates, Ray Chambers .Peter Chernin, Aliko Dangote, Mhe.Jakaya Kikwete, Graça Machel, Luis Alberto Moreno, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, na mwenyekiti wa ALMA ambaye kwa kipindi hiki ni Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini.

Ikumbukwe kuwa Mhe. Kikwete ni mkereketwa mkubwa katika masuala ya Afya. Katika kipindi chake cha urais aliweza kushirikisha maraisi wa Afrika kupambana na malaria kupitia chombo alichokianzisha kinachojulikana kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA). Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa secretariat ya chombo hicho alimshukuru Mhe. Kikwete kwa kuanzisha chombo hicho ambacho kilianza na marais nane na sasa kinajumuisha marais wote wa Africa. 

 Naye Katibu Mkuu wa SADC Dr. Stergomena Tax, alisema taasisi yake ipo tayari kufanya kazi na Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria, kwani kwa SADC suala la malaria limepewa kipaumbele kikubwa. Wajumbe wote waliokuwapo katika kikao hicho wakiwemo wawakilishi wa umoja wa Afrika na RBM walimpongeza mhe. 

Kikwete kwa uongozi wake katika masuala ya malaria na kuelezea utayari wao wa kufanya kazi pamoja naye na na taasisi ya kutokomeza malaria. 
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) (wa pili kulia)  jana akiendesha kikao kazi cha wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana akiendesha kikao kazi cha wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 

 Picha ya pamoja 

TRA YAFUNGUA KITUO CHA USHAURI KWA WALIPAKODI DAR ES SALAAM.

Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula.
Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Ndumbaro (Mb.) akizungumza kwenye Mkutano na wadau mbalimbali pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo. 
Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Maganda naye akizungumza na wadau pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo 
Wadau kutoka upande wa Tanzania wakisikiliza kwa makini wakati Naibu Mawaziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Maganda walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliyofanyika mpakani wa Tanzania na Uganda-Mtukula 
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa na Mhe. Maganda wakisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau iliyokuwa ikiwasilishwa kwenye mkutano. 
Mwakilishi wa jumuiya ya wafanya biashara akichangia mada kwenye mkutano
Mmbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Uganda naye akichangia mada wakati wa mkutano huo ukiendelea.
Ujumbe wa Uganda nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini. 
Viongozi wa pande zote mbili walipata fursa ya kuzungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo na kuwaelezea yaliyojiri kwenye mkutano. 
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano. 
Viongozi hao wakifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha pamoja na kujione namana watendaji wanavyo fanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali ikiwemo namna ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko. 
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola.. 
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Julius wakiendelea na kukagua Kituo ili kujionea namna watendaji wake wanavyotoa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili. 
Katika picha ni jengo la Kituo cha kutolea hudmua kwa pamoja Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda. 



Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema lengo la ziara yao katika kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja Mtukula ni pamoja na kujionea mafanikio na kubaini changamoto zinazokabili utendaji wa kazi na kuzipatia ufumbuzi. 

Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.

Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo. 


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.

KAMPENI YA TBS YAWAFIKIA WANAFUNZI KAHAMA

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea na Kampeni yake katika Wilaya ya Kahama  kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma pia ilifanyika katika  Shule ya Msingi Malunga Mjini Kahama mapema Februari  09, 2019 huku wanafunzi zaidi ya 1000(elfu moja) wakipata elimu juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano Bi. Neema Mtemvu aliwasisitiza  wanafunzi  hao kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote (Wananchi na Shirika), Hivyo, tunaamini wao watakuwa mabalozi wazuri katika kuelimisha wengine na vilevile na wao kujenga tamaduni ya kuthamini ubora tangu wakiwa wadogo. Hivyo,wahakikishe wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS, pale wanapotumwa madukani na masokoni.

Kampeni hiyo inaendelea tena Mkoani Mara Mara baada ya kufanyika mikoa ya Kagera, na Shinyanga.
 Pichani: Ni Afisa Uhusiano wa TBS Bi. Neema Mtemvu akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Malunga ya Mjini Kahama Mkoani Shinyanga, namna ya kutambua bidhaa hafifu ambazo hazijathibitishwa.

Bima Ya Kilimo Kuwa Mkombozi Kwa Wakulima Nchini

$
0
0
Na Erick Msuya - MAELEZO 

Wakati serikali ya Awamu ya Tano ikiwahangaikia wakulima nchini katika kuwawezesha kimaendeleo, wakululima na wadau wake wenye viwanda vya kilimo wameanza kuhamasishwa kufungua Bima ya wakulima itakayo wasaidia katika mazao yao. 

Zaidi ya asilimia 70 ya watanzania nchini ni wakulima na ndio tegemeo kutokana na kilimo kuwa uti wa mgongo kwa taifa, hivyo kuwa na bima katika kilimo ni jambo ili kuzuia majanga katika mchakato wa kilimo kwa kuepuka moto, mafuriko, magonjwa ya mazao na mengine kadhaa. 

Tanzania Insurance Regulatory Authority (TIRA) ni wadau wanao wanaosimamia shughuli za bima nchini na hivyo kuwa na nafasi ya kushiriki katika sekta ya kilimo kwa wakulima kuwa na bima 

Katika semina ya siku mbili  februari 7 – 8, iliyofanyika jijini Dar es S alaam kwa lengo la kuwainua wakulima kwa kufungua bima za mazao ili kuwaokoa kiuchumi, wadau mbalimbali wa kilimo, sekta binafsi pamoja na serikali zimewataka wakulima kujiungta na bima ili iwasaidie pindi wanapokutana na majanga. 

Akizungumza na Maelezo, Mkurugenzi wa Leseni na Mwenendo wa Soko kutoka Mamlaka ya Bima Tanzania, Samweli Mwiru amewataka wakulima nchini wajiandae kwa ujio huo wa bima katika mashamba yao pia watambue bima ni kitu muhimu hasa katika mazao yao na kilimo kwa ujumla.. 

“Bima itasaidia endapo patatokea majanga yoyote katika kilimo na mazao, makampuni ya bima nchini yataweza kuwalipa hizo gharama ili kumfanya mkulima kutofilisika na kumfanya aendelee na shughuli zake za kilimo” alisema Samweli Mwiru 

Sambamba na hilo, amesema bima hiyo ya kilimo itamlinda mkulima katika maeneo mengi tofauti tofauti ikiwa na majanga yatokanayo na hali ya hewa, mjanga yatokanayo na Magonjwa mbalimbali ya Mimea, hivyo akaongezea kuwa bima hiyo itakuwa mahususi kukinga majanga yatokanayo na hali ya hewa. 

Naye Afisa Habari wa Mamlaka hiyo, Eyuke Faustin amesema asilimia 68 ya wakulima wadogo wadogo elimu yao ni ndogo juu ya uelewa wa bima hivyo amewataka wadau mbalimbali wa bima hizo ingefaa waandae mchakato wa bidhaa za bei rahisi zitakazo weza kujibu maswali na changamoto zitakazo weza kumkabili mkulima. 

“swala la bima kwa wakulima wadogo wadogo bado ni changamoto, kutokana na takwimu zilizopo zilizotolewa na Waziri wa kilimo, asilimia 68 ya wakulima wadogo wadogo elimu yao ni kuanzia elimu za msingi … kampuni za bima ziandae bidhaa rahisi zitakazo eleweka vizuri kwa kujibu hoja ama maswali ya mkulima mdogo mdogo” alisema, Eyuke Faustin. 

Katika siku ya mwisho ya seminahiyo, matumaini yao ni kuandaa hatua za kuchukua katika kuendeleza soko la bima za kilimo, kuundwa kwa kikosi kazi maalumu kitakachoweza kuandaa ripoti itakayopelekwa wizarani ili mikakati itakayoandaliwa iweze kusaidia Mamlaka ya Bima pamoja na taasisi mbalimbali zilizo wadau.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images