Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Wabunge wa EALA walivyotoa Elimu ya Mtangamano wa EAC

$
0
0
Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga akitoa mada kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuhusu shghuli za taasisi hiyo. Alisema taasisi yake inashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu mbalimbali kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa biashara katika nchi za EAC inafanyika bila vikwazo. 
Waheshimiwa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili kwa pamoja na Mkurugenzi wa TMEA kuhusu mchango wa taasisi hiyo katika kuboresha mwenendo wa biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine za EAC. 
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakijadili mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA. 



Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam
Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akijadili jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar Es Salaam mara baada ya kuwasili katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu EAC. 
Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akipata chakula cha mchana na wanafunzi wa UDSM katika Cafteria Namba moja ya Chuo hicho. Mwenye nguo za bluu ni Mbunge mwenzake wa EALA, Mhe. Pamela Maasay. 
Wanafunzi wa UDSM wakipata chakula cha mchana ambapo Wabunge wa EALA walijumuika nao katika chakula hicho. 
Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian (kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa UDSM wakati wakipata kwa pamoja chakula cha mchana Cafteria. 
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiwa katika meza kuu kwenye Ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuongea na wanafunzi kuhusu fursa za EAC. 
Mbunge wa EALA, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe akiwasilisha mada kuhusu EAC kwa wanafunzi wa UDSM. 
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiongea na wanafunzi wa UDSM kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Wanafunzi walioshiriki kwenye mazungumzo na Wabunge wa EALA. Mwenye suti ya bluu ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. 
Washiriki wengine katika mazungumzo hayo. 
Wanafunzi wakiuliza maswali na kutoa maoni namna Watanzania watakavyofaidika na Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki 
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakikabidhi bendera ya EAC kwa viongozi wa UDSM ili iwe inapeperushwa chuoni hapo. Walitoa wito kwa taasisi nyingine, hususan za Serikali kupeperusha bendera hiyo.

Mkutano na Asasi za Kiraia
Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian akitoa elimu kuhusu EAC kwa wawakilishi wa Asasi za Kiraia zilizopo hapa nchini. 
Majadiliano baina ya Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia kuhusu ushiriki wa asasi hizo katika masuala ya EAC. 
Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge walisisitiza umuhimu wa wimbo huo kupigwa katika shughuli rasmi za Serikali. 
Mdau akifanya tafrisi ya lugha ya ishara kwa watu wenye ulemavu wa kusikia. 

BOTI ILIOTENGENEZWA KWA PLASTIKI NCHINI KENYA YAWASILI ZANZIBAR.

$
0
0
Boti ya Beach Clianup iliotengenezwa kwa Plastiki iliowasili Zanzibar ikitokea Nchini Kenya ambayo imebeba Ujumbe wa Kuhifadhi mazingira ikiwa katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar.
Nahodha Muundaji wa Boti ya Plastiki Ali Abdalla Ali(SKANDA)akisalimiana na Wananchi wa Zanzibar na kuwapa ujumbe wa kuhifadhi mazingira katika hafla iliofanyika Bustani ya Forodhani ya kuipokea Boti iliotengenezwa kwa Plastiki iliobeba ujumbe wa kuhifadhi mazingira iliowasili Zanzibar ikitokea nchini Kenya.
Rais wa Baraza la Mazingira Duniani Siim Kiisler akitoa hotuba kuhusiana na Mazingira katika hafla iliofanyika Bustani ya Forodhani ya kuipokea Boti iliotengenezwa kwa Plastiki iliobeba ujumbe wa kuhifadhi mazingira iliowasili Zanzibar ikitokea nchini Kenya.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akitoa hotuba kuhusiana na kuhifadhi mazingira mara baada ya kuipokea Boti iliotengenezwa kwa Plastiki iliobeba ujumbe wa kuhifadhi mazingira iliowasili Zanzibar ikitokea nchini Kenya.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas katikati akiwapamoja na viongozi mbalimbali wakifanya usafi wa mazingira kuondosha Chupa na Mifuko ya Plastiki na uchafu mwengine katika ufukwe wa Bahari ya Forodhani katika hafla ya kuipokea Boti iliotengenezwa kwa Plastiki iliobeba ujumbe wa kuhifadhi mazingira iliowasili Zanzibar ikitokea nchini Kenya.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akizungumza na Wananchi na Vikundi mbalimbali vilivyoshiriki Usafi wa Mazingira katika ufukwe wa Bahari ya Forodhani katika hafla ya kuipokea Boti iliotengenezwa kwa Plastiki iliobeba ujumbe wa kuhifadhi mazingira iliowasili Zanzibar ikitokea nchini Kenya.

TOP 10 AFRICAN COUNTRIES TO INVEST IN 2019

BALOZI SEIF: UJIO WA MASHUA YA MAZINGIRA NI DARASA KWA WANANCHI WALIOWENGI NCHINI

$
0
0

Rais wa Taasisi inayosimamia mazingira ya Umoja wa Mataifa Bwana Siim Valmar Kiislar amesema wakati umefika kwa Mataifa yote Ulimwenguni kuwa na mfumo Mmoja unaoeleweka wa utunzaji wa Mazingira utakaosaidia kuifanya Dunia iendelee kubakia salama.

Bwana Siim Valmar Kiislar alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Zanzibar bado inaendelea kuathirika na mabadiliko ya Tabia Nchi akatolea mfano ufukwe wa Bahari ya Msuka uliopo kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba ambao tayari umeshaliwa na mawimbi ya Bahari kwa sehemu kubwa.

Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo ujio wa mashua ya Mazingira katika Visiwa vya Unguja na Pemba utasaidia mfano wa Darasa kwa Wananchi waliowengi kuwa na muelekeo wa jitihada za mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabia Nchi yanayoikumba Dunia hivi sasa na kuleta athari kubwa ya Kimazingira.

Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)
Fubuari 07, 2019.





MSANII PETER MSECHU AWATOLEA UVIVU WATANZANIA WENYE MOYO WA CHOYO

$
0
0
*Asema wasipofurahia treni ya umeme,mnataka wafurahie ya dizeli?

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MSANII maarufu nchini Peter Msechu amesema anashangazwa na moyo wa choyo walionao baadhi ya Watanzania ambao kwao ni ngumu kupongeza juhudi za Serikali na badala yake kazi yao ni kutukana wale wanaoamua kutembelea miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Msechu ametoa kauli hiyo akiwa njiani kuelekea mkoani Morogoro akitokea Dar es Salaam kwa usafiri wa treni yeye pamoja na wasanii wengine wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Wasanii wa fani mbalimbali nchini leo Februari 7,2019 wamepata fursa ya kutembelea ujenzi wa reli ya treni ya kisasa ambayo itatumia umeme ambapo Msechu amepongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa fedha za ndani.

"Tumefurahi kuwa sehemu ya Watanzania ambao tuliobahatika kuutembelea ujenzi huu wa reli ya kisasa.Ila inasikitisha sana tunapoonekana kwenye miradi mikubwa kama hii ambayo ina tija kwa Taifa letu baadhi ya watu wanatutukana na kusema tumenunuliwa," amesema Msechu.

Ameongeza kuwa ingekuwa leo Makonda angeamua kuwachukua wasanii wa Kenya na Uganda anaamini Watanzania wangelalamika kwanini wamechukuliwa wasanii wa Tanzania hawakuchukuliwa kwenda kuona utekelezaji wa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.

"Leo Mkuu wa Mkoa kaamua kutuchukua sisi tuambatane naye msema....mnataka mtuone wapi?Mara ooh mmelipwa sasa sisi kazi yetu nini.Kwani tukilipwa na sisi tukalika kodi Serikalini kuna tatizo gani?

" Mnataka kutuambia huu mradi wa reli ya kisasa hauna manufaa kwa Watanzania wakati kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamika Serikali haiboreshi reli ya kati,leo hii inaboreshwa mnataka tubeze,"amesema Msechu.

Ameongeza msanii huyo kuwa "Serikali hii ni yangu,Rais Magufuli huyu ni wangu ,kodi nalipa kwa fedha yangu,mazuri nitayasema kwa nguvu zangu zote.Niache kufurahia treni ya umeme nifurahie treni ya dizel?Hata mwehu atanicheka."

MSANII maarufu nchini Peter Msechu akiwa na Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda

Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii

$
0
0
Jumia inakupenda ‘Valentine’ hii
  • Zawadi zote zimesogezwa karibu nawe mtandaoni.
  • Faidi vocha ya manunuzi mpaka ya shilingi 50,000.

Miongoni mwa mambo ambayo huufanya mwezi wa Februari kuwa mashuhuri ni uwepo wa sikukuu ya wapendanao au ‘Valentine’s Day.’ Sikukuu hii huadhimishwa kila ifikapo Februari 14 ya kila mwaka ambapo watu huwatumia wapendwa wao kadi na maua yenye jumbe mbalimbali za upendo pamoja na zawadi.
     
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya sikukuu hii kuadhimishwa, tayari maandalizi yamekwishaanza kupitia matangazo tofauti kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Katika kuhakikisha Watanzania wanasherehekea sikukuu hii wakiwa na furaha na tabasamu katika nyuso zao, Jumia imezindua kampeni inayokwenda kwa jina laJUMIA LOVES YOU.’ Kampeni hii ambayo itafikia ukomo Februari 16, imezisogeza zawadi zote kwa ajili ya wapendanao karibu na wateja ili waweze kuzinunua kwa njia ya mtandaoni.    

Hakuna mtu asiyependa zawadi, kwasababu humfanya mpokeaji kujisikia wa umuhimu na thamani katika maisha ya aliyeitoa. Kwa upande wa zawadi Jumia imekuja na orodha ya bidhaa zifuatazo ambazo kwa hakika zitajaza tabasamu katika nyuso za wapendwa wote ‘Valentine’ hii:

Marashi na manukato. Je, utapendezwa kupata kumbato au kutumia muda mwingi na mpendwa wako akiwa na harufu isiyovutia puani mwako? Usijali, sikukuu hii hilo litakoma kwasababu kuna ‘dili za kufa mtu’ kwa upande wa marashi na manukato. Kuna orodha kubwa ya marashi na manukato mbalimbali kwa ajili ya wanawake yanapatikana kwa bei nafuu. Mfanye mpendwa wako anukie ili uwe huru kuwa karibu naye muda wowote.    
Vito vya thamani.Boresha mwonekano wa mpendwa wako kwa kumnunulia vito kama vile saa za mkononi, vidani vya shingoni na mkononi pamoja na hereni. Vitu hivi vina mchango mkubwa zaidi katika kumfanya mtu kupendeza na kuvutia au kuonekana wa kisasa zaidi. Bila ya shaka ungependa mpendwa au mpenzi wako kuvutia kila atakapoonekana mbele za watu. Jumia imekuondolea usumbufu ambao unaufikiria ungeupata kwenda kuzunguka kwenye maduka ya sonara. Vito vyote vya thamani unavyovihitaji vimesogezwa karibu nawe kwa njia ya mtandaoni.       
Vinywaji.Bila ya shaka katika kusherehekea sikukuu hii ya ‘Valentine’ utatenga muda maalum wa kupata chakula na mpendwa wako, iwe ni nyumbani au mgahawani. Nogesha mlo au mtoko wako kwa kuagiza kinywaji kupitia Jumia na uletewa mpaka hapo ulipo. Huduma hii ikiwa imetambulishwa hivi karibuni imekurahisishia kupata vinywaji vya aina zote kama vile juisi, bia, mvinyo, wiski, nakadhalika katika sehemu moja. Ingia mtandaoni uperuzi, uchague na uletewe mpaka hapo ulipo. Bila ya shaka utakuwa unafahamu ni kinywaji gani mpendwa wako anakipendelea zaidi.  
Luninga. Yale mambo ya ‘bebi njoo home tu-chill na kucheki movie’ unaweza kuyafanya ‘Valentine’ hii. Kuna luninga za kisasa na mpya kabisa zinapatikana kwa punguzo kubwa la bei pamoja na kupatiwa vocha za bure ya mpaka shilingi 30,000 ili kukurahisishia manunuzi yako. Kwa hiyo, cha kufanya ni kuingia tu mtandaoni, chagua luninga unayoipendelea, weka vocha ya bure ya manunuzi, utashangaa bei itakavyopungua na kisha agiza uletewe mpaka hapo ulipo.   
Simu. Inawezekana umekuwa ukipata tabu kuwasiliana na mpendwa wako kwa njia ya simu kwa muda mrefu. Hali ya kiuchumi, ukizingatia bado watu wanapona majeraha yaliyoachwa na mwezi wa Januari, hivyo basi uwezekano wa kuwa na fedha za kutosha au kutokuwa nazo kabisa ni mkubwa. Usijali, kuna orodha ndefu ya simu mpya, kali na za kisasa zikiwa zimepunguzwa bei pamoja na vocha ya bure ya manunuzi ya mpaka shilingi 40,000! Wahi sasa, ingia mtandaoni na ufanye manunuzi ya simu ili umshangaze mpendwa wako na kumfanya aikumbuke ‘Valentine’ hii mwaka mzima.      
Vyombo vya jikoni. Kwanini usipendezeshe jiko la mpendwa wako msimu huu wa ‘Valentine’? Najua akina mama au dada wanaopenda kupika watakukumbuka sikukuu zote endapo utawashangaza na zawadi ya vyombo vya jikoni. Kuzipata bidhaa zote za aina hii pitia kwenye orodha yenye vyombo vya nyumbani.   

Kampeni ya ‘Jumia Loves You’ itafikia ukomo Februari 16, na siku ya Ijumaa ya kesho kutakuwa na ‘FLASH SALE.’ Kutakuwa na bidhaa zaidi ya 12 zitakazouzwa kwa punguzo zaidi ya 70% kuanzia saa 6 ya usiku wa leo mpaka saa 5.59 ya usiku wa kesho. Miongoni mwa dili ambazo hautakiwi kuzikosa ni ya luninga mpya ya STAR X yenye ukubwa wa inch 32 itakayouzwa kwa shilingi 299,000 punguzo kutoka shilingi 500,000; pamoja na saa ya kisasa aina ya NAVIFORCE itakayouzwa kwa shilingi 55,000 punguzo kutoka shilingi 100,000!   


Ili kupata taarifa zaidi za mara kwa mara, hakikisha hauchezi mbali na tovuti ya Jumia pamoja na kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

WAZIRI ENG. KAMWELWE AZUNGUMZA NA TATOA

$
0
0



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa malori nchini (TATOA) Bw, Elius Lukumay hayuko pichani katika kikao kazi cha kujadiliana namna bora ya kufuata sheria ya kudhibiti uzito wa magari ili kulinda barabara nchini kilichofanyika mjini Dodoma leo. 
2-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akisisitiza jambo katika kikao cha wataalam wa Wizara yake na viongozi wa TATOA kilichofanyika mjini Dodoma, (kulia) ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mh. Elias Kwandikwa na (kushoto) ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditie.
3-min
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Kamwelwe akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa TATOA  Bw, Elius Lukumay katika kikao cha viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na TATOA cha kujadiliana namna bora ya kufuata sheria ya kudhibiti uzito wa magari ili kulinda barabara na madaraja hapa nchini. 

PWANI YAPOKEA BILIONI 4.5 KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITAL TATU ZA WILAYA -RC NDIKILO

$
0
0

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA .

KATIKA kukabiliana na changamoto ya utoaji wa huduma ya afya kwa wananchi, serikali ya awamu ya tano inajenga hospitali za wilaya tatu za kisasa , halmashauri ya Kibaha Mjini, Kibaha Vijijini na Kibiti mkoani Pwani ambazo zitagharimu kiasi cha sh. bilioni 4.5. 

Akizungumza wakati alipotembelea ujenzi wa hospital ya halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lulanzi kata ya Pichandege, kwenye ziara yake inayoendelea kukagua miradi ya maendeleo, mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema kukamilika kwa hospital hizo, kutaondoa kero ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu. 

“Kila hospital inatarajiwa kugharimu bilioni 1.5 ,matarajio yetu ni kuona ujenzi unakamilika na sio kuanza mradi na kisha kusuasua “alieleza Ndikilo.
Aidha ameelezea, fedha zote zinazoelekezwa katika miradi hiyo muhimu zitumike kwa wakati na kwa matumizi lengwa bila kuziacha kubaki viporo. 

Hata hivyo Ndikilo, aliwaasa wahandisi wa halmashauri ya Kibaha Mji na wa serikali ya mkoa huo kujiwekea utaratibu wa kutoka maofisi kwenda kutembelea miradi pasipo kusubiria ziara ama kiongozi kutembelea ndipo nao watoke maofisini. 

Nae mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama alitoa rai kwa jamii kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu na kujitolea kwenye miradi ya kimaendeleo. 


Diwani wa kata ya Picha ya ndege Robert Machumbe alieleza, nia ya serikali ni kuwaletea wananchi mabadiliko chanya ya kimaendeleo ambapo amefafanua kwamba, eneo hilo linalojengwa hospital lina ukubwa wa hekari 25 lipo eneo linalojengwa shule ya sekondari Lulanzi lenye ukubwa wa hekari 11.7

MKAKATI KUTOKOMEZA JANI LA GUGU KAROTI LINALOUA WANYAMA,KUPUNGUZA MAZAO WAANZA

$
0
0
Na Seif Mangwangi,Arusha

UONGOZI wa shamba la Serikali la kuzalisha aina tofauti za mbegu (ASA), lililopo Ngaramtoni wilayani Arumeru , umeanza mikakati ya kutokomeza jani aina ya Gugu karoti (pyrthrum), ambalo limekuwa likiua wanyama na kupunguza mazao endapo litaingia shambani.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa mapambano dhidi ya jani hilo chini ya wajumbe wa kamati ya mkoa ya mapambano dhidi ya jani hilo, Meneja wa shamba hilo la mbegu, Zawadieli Mrinji alisema jani hilo ambalo limeonekana pembezoni mwa mashamba ya mbegu ni hatari na linatakiwa kutokomezwa haraka sana.

Alisema tayari uongozi wa shamba umeanza kupuliza sumu kuua kabisa jani hilo ambalo alisema utafiti unaonyesha limekuwa likisambaa kwa kasi kubwa kufuatia mbegu zake kutawanywa na upepo pamoja na mafuriko.

Mrinji,alisema shamba hilo lina zalisha mbegu mbalimbali zikiwemo Maharage, Mahindi, Alizeti na Ngano ,hivyo inahitajika nguvu ya pamoja na haraka kutokomeza gugu hilo ambalo limeshaonyesha madhara makubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya mkoa wa Arusha ya kutokomeza gugu karoti Ndelikwa Kaaya alisema kikao hicho kimeitishwa ili kuwa na mkakati wa pamoja wa kuzuia gugu karoti lisiingie kwenye mashamba ya mbegu ya serikali na matokeo yake kuathiri uzalishaji wa mbegu bora .

Alitahadharisha kuwa gugu hilo linaweza kuingia hadi ndani ya hifadhi za taifa ambapo wanyama pori wengi wakiwemo Pundamilia wanauwezekano mkubwa wa kupoteza maisha kwa kula majani hayo.

Kaaya, alisema kuwa kamati yake katika kukabiliana na gugu hilo, imefanikiwa kulifikisha ofisi ya Makamu wa Rais na sasa suala hilo limekuwa ni la kitaifa ambapo tayari serikali baada ya kutambua athari zake imeunda timu maalumu au kikosi kazi kwa lengo la kutokomeza gugu hilo.

Mkurugenzi mstaafu wa kituo cha utafiti wa kilimo SARI, Dk Mbwana Ally,alisema kutokana na watu kutolifahamu gugu hilo wamekuwa wakilitumia kama sehemu ya mapambo kwenye harusi na baada ya hapo mbegu zake huwa zinatupwa hivyo kilichopo sasa ni kuendela kuelimisha wananchi ngazi mbalimbali ili kulitokomeza.

Wakichangia katika kikao hicho wadau wengi walionyesha wasi wasi wa Gugu karoti kuingia kwenye hifadhi za taifa za Ngorongoro na Serengeti na hivyo linaweza kuathiri shughuli za utalii kwa asilimia 60 hadi 70 iwapo hakutakuwepo na juhudi kubwa za kulitokomeza .

Katika utafiti uliofanywa na taasisi ya TPRI gugu hilo linaweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binaadam ikiwemo Kansa ,kupatwa na mzio wa ngozi, kuathiri uzalishaji wa mazao na kuathiri mifugo.

Wamesema gugu hilo hivi sasa limeshaenea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Arusha,Kilimanjaro, Kagera na Geita.
 Meneja wa shamba la kuzalisha mbegu ASA, Zawadiel Mrinji akimuonyesha mmoja wa wadau jani aina ya gugu karoti linavyokua kwa kasi pembezoni mwa barabara ya Arusha -Namanga wakati wa zoezi la kung'oa jani hilo.
Gugu Karoti linavyokua kwa kasi pembezoni mwa barabara ya Arusha -Namanga wakati wa zoezi la kung'oa jani hilo.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UWT ZANZIBAR

$
0
0




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).Bi. Thuwaiba Kisasi , akiwa na Ujumbe wa Viongozi wa (UWT) Afisi Kuu ya Zanzibar,walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.7-2-2019
IMG_2386-minIMG_2384-min
RAIS wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 7-2-2019.ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa (UWT.)Bi. Thuwaiba Editon Kisasi.(Picha na Ikulu)

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAFANYA UFUATILIAJI WA UTEKELEZAJI WA WARAKA WA MAVAZI KWA WATUMISHI WAKE

$
0
0

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akihimiza uzingatiaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa Umma nchini mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa sehemu ya mapokezi kusaini kitabu cha mahudhurio wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanywa na Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo na kuwahi kazini.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uadilifu wa ofisi hiyo wakati wa zoezi la ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 lililofanyika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uzingatiaji wa waraka huo kwa watumishi wa umma nchini.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uadilifu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Constantino L. Kinawiro (mwenye suti) akipongezwa na mtumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kamati hiyo kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo.

…………………………..

Idara ya Ukuzaji Maadili, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Kamati ya Uadilifu ya ofisi hiyo, imefanya ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007 kwa watumishi wa ofisi hiyo kwa lengo la kujiridhisha na kiwango cha utekelezaji wake, ikiwa ni pamoja na kuhimiza watumishi wa umma nchini kuzingatia waraka huo mahala pa kazi.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Ukuzaji Maadili, Sehemu ya Ufuatiliaji Uzingatiaji wa Maadili, Bibi Janeth Mishinga mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Waraka huo kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambao unawaelekeza watumishi wa umma aina ya mavazi wanayostahili kuyavaa mahala pa kazi.

Bibi Mishinga amesema, Ofisi ya Rais-Utumishi ni msimamizi wa miongozo mbalimbali ya kiutumishi ikiwemo Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma ambapo kanuni ya kwanza inaelekeza utoaji wa huduma bora na kuongeza kuwa moja ya kigezo cha watumishi wa umma kutoa huduma bora ni pamoja na kuvaa mavazi yenye staha.

Bibi Mishinga amefafanua kuwa, zoezi hilo la ukaguzi katika ofisi ya Rais-Utumishi limebaini kuwa asilimia 95 ya watumishi wameonekana kutekeleza vema waraka huo wa mavazi ikiwemo kuwahi kazini na asilimia tano ya watumishi waliobainika kutotekeleza waraka huo wamekumbushwa kuuzingatia.

Aidha, Bibi Mishinga ametoa wito kwa wasimamizi wa taasisi zote za umma nchini kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa waraka huo na kuwahimiza watumishi walio chini yao kuwahi kazini kwa ili kutoa huduma bora na kwa wakati kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anavyohimiza.

Bibi Mishinga amesisitiza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ikiwa ndio msimamizi wa waraka huo wa mavazi itaendelea kufanya ukaguzi na ufuatiliaji katika taasisi zote za umma nchini na haitosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wa umma watakaobainika kuukiuka.

Serikali imejiandaa Vyema Kunufaika na Ujio wa Mashindano ya AFCON

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu swali la Mbunge wa Konde Mhe.Khatib Haji (CUF) kuhusu mgao wa fedha za FIFA zinazopelekwa TFF na utaratibu unaotumiwa na TFF kuwapatia fedha hizo Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) leo Bungeni jijini Dodoma

……………………..

Na Anitha Jonas – WHUSM,Dodoma.

Serikali kwa kushirikiana na taasisi zote muhimu imejiandaa kupokea wageni wote watakao shiriki mashindano ya AFCON yanayotarajia kufanyika nchini hivi karibuni .

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (CCM) wakati wa maswali ya papo kwa papo ya wabunge.

“Serikali inatambua maandalizi yanayofanyika na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadau mbalimbali na tunatambua kuwa tutapokea wageni wengi akiwemo Rais wa Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA)”,alisema Mhe.Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha,Mheshimiwa Waziri Mkuu aliendelea kusema kuwa kupitia mashindano hayo serikali imehamasisha Mikoa ya jirani kujipanga kunufaika na mashindano hayo na jumla ya viwanja vitatu vitatumika na nijukumu la watanzania wote kushirikiana ili kuhakikisha tunanufaika kwa ujio huu mkubwa.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Majaliwa aliendelea kuwasisitiza TFF kuimarisha maandalizi ya timu hiyo itayoshiriki ili taifa liweze kuibuka kidedea,vilevile aliwasihi watanzania wote kuonyesha uzalendo kwa timu yao ili kuweza kuwatia moyo kwa kuwa na imani kuwa timu hiyo itaweza kushinda.

Nae Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ametoa majibu ya swali la Mbunge wa Konde Mhe.Khatibu Haji (CUF) lilihoji kuhusu mgao wa fedha zinazotolewa na FIFA kwa TFF kuwa ni kiasi gani zimekwisha pelekwa kwa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kwa kusema kuwa kuwa kufuatia changamoto TFF kutokukidhi vigezo vya utawala bora na uwazi katika matumizi ya fedha kwa zaidi ya miaka mitatu wamekuwa hawapati mgao na FIFA ila kwa kuanzia mapema mwaka huu wanatarajia kuanza kupata mgao huo baada ya kutatua changamoto hizo.

Halikadhalika katika swali la nyongeza Mhe.Naibu Waziri Shonza alijibu kuwa si kweli kuwa ZFA haijawahi kupatiwa msaada wa TFF kwani wameshawahi kupatiwa msaada wa miradi moja wapo ni ujenzi wa ukarabati wa uwanja wa Gombani Pemba na kufafanua kuwa ZFA ni sehemu ya TFF hivyo fedha zinazoletwa na FIFA kwa TFF hugawiwa kwa mashirikisho yote na ZFA hawaletewi fungu lao peke yao kwani ZFA siyo mwanachama FIFA wala CAF.

Watumishi wa Umma Kuweni na Subira Ongezeko la Mishahara - Waziri Mkuu Majaliwa

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa, amewataka watumishi wa umma kuwa na subira kwa sababu Serikali inaendelea na mchakato wa kuwatambua watumishi wa umma halali na kufanya ulinganifu wa mishahara katika kada mbalimbali ili watumishi hao waanze kulipwa mishahara stahiki. 

Waziri Mkuu Majaliwa ameyazungumza hayo leo Jijini Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Mhe Pascal Haonga, lililohoji juu ya ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma chini ya Sheria ya Utumishi wa Umma.

Mhe. Majaliwa amefafanua kuwa mwanzoni nchi ilikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa ambapo wote kwa pamoja walikuwa wakilipwa mishahara na posho mbalimbali hivyo, ili kuwatambua watumishi halali Serikali iliamua kufanya uchunguzi na kuwagundua watumishi hao hewa.

Pia, Serikali ilifanya uchunguzi mwingine wa kuwatambua watumishi wenye vyeti stahiki vya kufanya kazi mbalimbali Serikalini kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa baada ya kumaliza utambuzi wa watumishi halali, Rais Dkt. Magufuli aliunda Tume ya Mishahara na Motisha kwa ajili ya kufanya mapitio ya kada zote za Utumishi wa Umma na viwango vya mishahara ili kutambua ulinganifu kati ya stahiki ya mshahara na kada husika.

"Lengo la Rais Magufuli kuunda tume hiyo ni kufanya tathmini nzuri ili kutambua weledi wa kazi, uwajibikaji na tija inayopatikana mahala pa kazi, hivyo baada ya kukamilika Serikali itatoa taarifa," alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai kwa Watumishi wa Umma kuendelea kuiamini serikali kwani ina nia ya dhati kuhakikisha watumishi wote wanapata haki zao stahiki vile vile mpaka sasa mjadala kati ya Serikali na Vyama vya Wafanyakazi unaendelea vizuri.

CCM YAWAONYA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA WASIO WAJIBIKA,YAAHIDI KUTOWARUDISHA KATIKA UCHAGUZI WA 2019

$
0
0
Akiwa katika ziara ya Kata kwa kata ya uhuishaji wa hai wa Chama na ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha Mjini katika Kata za Engutoto, Lemara, Muriet, Terrat, Olasiti na Osunyai Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi amesema CCM inawaonya viongozi wake wote wa Serikali za Mitaa wasiowajibika kusoma mapato na matumizi na chama kimeahidi kutowarudisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2019.

Akifafanua suala hilo Ndg. Polepole amesema kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa viongozi wote wasiowajibika, wasio soma mapato na matumizi kwa mujibu wa sheria, wenye tabia za kupokea au kutoa rushwa Chama hakitawavumilia na hawatapewa fursa ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019.

"Tunaposimamisha wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 tunahitaji watu mwenye tabia nzuri, waaminifu, wanyenyekevu, wachapakazi, wapole lakini wakali kwenye mambo ya hovyo na wanaokubalika kwa watu” amesisitiza Ndg. Polepole

Aidha akiwa katika ziara hiyo Ndg. Polepole amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa jengo la cha Wagonjwa wa Nje (OPD) la hospitali ya Wilaya ya Arusha Jiji lililopo katika Kata Engutoto, Ujenzi wa barabara kuu ya mchepuko (kilometa 42. 4 kwa kiwango cha lami) yenye madaraja 7, ujenzi wa maabara  katika shule ya Sekondari Terrati katika Kata ya Muriet, Ujenzi wa madarasa manne katika shule ya msingi muriet Darajani na ujenzi wa barabara ya Sombetini FFU yenye urefu wa kilometa 2.1 kwa kiwango cha lami.

Huu ni muendelezo wa Ziara za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2015 – 2020.

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM

MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 8,2019


"HAJI MANARA KAPOTOSHA, TUTAMUITA" MWANASHERIA

Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SPIKA Mstaafu, Anne Makinda, ameshauri kuboresha sekta ya elimu ili kuwahakikisha vigezo vya elimu vya Tanzania vinaendana na vigezo vya kimataifa na Dunia ndiyo inataka tuende hivyo.

Akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu cha Aga Khan yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, Makinda amesema Tanzania haina budi kufanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya dunia na haina soko lake yenyewe ya kuajiri hivyo wahitimu wetu wanaweza kufanya kazi Duniani kutokana na elimu waliopata.

“Kama tuko katika dunia vigezo vyetu lazima viendane na wenzetu ili tuwe na elimu itakayotuwezesha kushindana katika soko la dunia, hatuna soko la Tanzania peke yake Aga Khan wamethubu katika uwekezaji katika elimu” amesema Spika Makinda. Makinda amesema ameshangazwa na wastani wa walimu na wanafunzi chuoni hao hali inayoashiria kuwa chuo hicho kinafuata vigezo vya kimataifa katika ufundishaji kwa Mwanafunzi watatu kwa Mwalimu Mmoja. 

“Ni mara yangu ya kwanza kufika katika chuo hiki, lakini nafahamu kuwa ndicho chuo cha kwanza Tanzania kutoa shahada ya uuguzi Ila nimeshangazwa na idadi ya walimu yaani walimu wako ishirini wanafunzi 59 inamaana kila mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi watatu” alisema Makinda.

Aliwashauri wahitimu wa kada mbalimbali nchini kujitoalea kwa moyo wao wote kusaidia jamii na kutokubali kukatishwa tama na changamoto wanazokutana nazo.Makinda amesema endapo kila mhitimu mmoja wa shahada ya uuguzi na ukunga chuoni hapo atajitolea walau asilimia 35 tu ya muda wake kuwahudumia wagonjwa itawatia nguvu.

Rais wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Firoz Rasul Amesema chuo hicho kimeendelea kuhakikisha kinatoa elimu bora ambapo mwaka jana mhitimu wa chuo hicho tawi la Dar es Salaam alitajwa kama tuzo ya mwalimu bora wa mwaka nchini Kenya.

"Zaidi ni kwamba kwa mara ya pili mhitimu wa Aga Khan ametajwa katika fainali ya kuwania zawadi ya dola milioni katika tuzo za kimataifa za walimu" amesema .Amesema programu mbalimbali wamefanikiwa kuwajengea uwezo na mbinu mpya za ufundishaji zaidi ya walimu 3,000 ambazo zimewanufaisha zaidi ya wanafunzi 100,000.

Amesema kwa sasa wanajipanga kuanzisha stashahada ya ualimu kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuwaongezea uwezo walimu wa shule za misingi.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo Kikuu Aga Khan Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande akimtunuku shahada ya Uzamili Abdallah Hoza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chuo Kikuu Aga Khan Firoz Rasul akizungumza akitoa maelezo ya Chuo Kikuu Aga Khan katika Mahafali ya 14 yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu Aga Khan wakiingia Ukumbini katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho.
Wahitimu wakiingia katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

MPOTO ASEMA RAIS MAGUFULI NI MMOJA WA SHABIKI WA NYIMBO ZAKE

$
0
0

Na Khadija Seif,Globu ya jamii

MSANII wa Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba amewashauri wasanii nchini kutengeneza tungo zitakazofichua uovu huku akielezea furaha yake kutokana na nyimbo zake kukubalika hata kwa Rais Dk.John Magufuli.

Akizungumza na Michuzi Blog Mpoto amesema nyimbo nyingi kwa sasa zimejikita zaidi kwenye mapenzi, na kusababisha wasanii wengi kuonekana ni wa aina moja.

Aidha ameeleza si kufanana kwa tungo tu bali pia hata miondoko ya uimbaji imekua ya kufanana sana kiasi kutokujua sauti ya nani pindi unaposikia wimbo kwenye redio.

Wakati huo huo Mpoto amesema amefurahishwa na juhudi za Rais Dk.John Magufuli kwa kuwa shabiki wa kazi zake kutokana na ustadi wa mashairi yake jinsi anavyomkumbusha baadhi ya mazuri pamoja na maovu yanayoendelea katika jamii.

"Sitegemei kutoa ngoma kwa sasa kutokana na wimbo wa Sizonje unaendelea kufanya vizuri sana toka nilipouachia na muitikio umekua mkubwa hadi Rais Magufuli ameweza kung'amua baadhi ya mashairi yanazungumza nini na kueleza anamjua Sizonje" alisema Mpoto .

Kuhusu utunzi wa nyimbo zake,Mpoto amesema baadhi ya kazi huchukua siku,wiki,mwezi hadi mwaka huku akiangalia na kuzingatia sana hadhira inahitaji kusikia kipi kwani mashairi yake yanakusudia kuigusa jamii zote hasa wa hali ya chini .

Pia amesema mambo yanabadlika anaweza kwa mwaka huu mashabiki zake watamshuhudia akivaa viatu.

Ametoa mwito kwa wasanii kujitengenezea utambulisho wao wa kipekee kwa hadhira ili kusaidia kazi zisiibiwe na maharamia .

TANGA UWASA YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI VYENYE THAMANI YA MILIONI 10 SHULE YA SEKONDARI MIKANJUNI

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akipokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 10 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondari Mikanjuni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Rahma Msofe kulia jana ambao walikabidhi vifaa hivyo ili viweze kutumika kwenye ujenzi huo ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim 
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa katikati akipokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya sh.milioni 10 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondari Mikanjuni kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Rahma Msofe kulia jana ambao walikabidhi vifaa hivyo ili viweze kutumika kwenye ujenzi huo ili kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim 
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano 
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Rahma Msofe akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza katika halfa hiyo 
Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu akizungumza katika halfa hiyo 
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo akizungumza katika halfa hiyo 
Afisa Elimu Taaluma Jiji la Tanga akizungumza katima hafla hiyo 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikanjuni Kaana Erasto akitoa taarifa ya shule hiyo 
Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo 
Sehemu ya walimu wa shule hiyo wakifuatilia halfa hiyo ya makabidhiano
Sehemu ya walimu wa shule hiyo wakifuatilia halfa hiyo ya makabidhiano
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia akiamkaribisha Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Mikanjuni
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kamabidhiano hayo 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akiwaongoza viongozi mbalimbali wakati walipotembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule ya Sekondari Mikanjuni 
Sehemu ya watumishi wa Tanga Uwasa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tanga
MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akiagana na watumishi wa mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) mara baada ya kumalizika kwa halfa hiyo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim
Sehemu ya Kokoto zilizokabidhiwa

MKUU wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto akitokea nondo 60 kwa ajili ya ujenzi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Rahma Msofe kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly 



MAMLAKA ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imekabidhiwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya milioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa kwenye shule ya sekondari Mikanjuni ikiwa ni mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali kuondosha changamoto zinazoikabili sekta hiyo. 

Halfa ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye shule hapa baina ya Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Rahma Msofe na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa wakiwemo Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Mhandisi Geofrey Hilly na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Faidha Salim. 

Vifaa vilivyokabidhiwa shuleni hapo kwa ajili ya kumalizia madarasa matatu ni pamoja na saruji mifuko 100, nondo 60, shehena za kokoto, mchanga, mbao, waya na vifaa vingine vyot ambavyo vitasaidia ujenzi huo ili kutoa fursa wanafunzi kupata fursa ya kusoma bila kuwepo kwa vikwazo vyovyote. 

Akizungumza mara baada ya kutokea msaada huo wa vifaa hivyo vya ujenzi Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alipongeza juhudi ambazo zimefanywa na mamlaka hiyo kwa kusaidia kuondosha changamoto za elimu kwenye shule hiyo. 

Mwilapwa alisema juhudi ambazo zimefanywa na mamlaka hiyo zinapaswa kuungwa mkono na mashirika ya Umma na makampuni binafsi kuhakikisha yanachangia masuala ya elimu ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na uhaba wa madarasa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali inakabiliwa na changamoto kubwa hasa katika sera yake ya elimu bure kutokana na idadi ya wanafunzi wanaofaulu toka darasa la saba kwenda kidato cha kwanza kuongezeka siku hadi siku na kupelekea uhaba wa vyumba vya madarasa.

Alisema mamlaka hiyo mbali na jitihada za kuimarisha huduma ya maji nam usafi wa mazingira Jijini Tanga pia imechukua dhamana ya kuimarisha miundombinu ya shule hiyo ambayo inauhitaji wa madarasa kutokana na ongezeko la wananfunzi.

Awali akizungumza katika halfa hiyo ya makabidhiano Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Rahma Msofe alisema kilichofanywa na Mamlaka hiyo ni sehemu ya kuchangiaji wa huduma za kijamii ili kumuunga mkono Rais Magufuli katika harakati zake za kuiboresha elimu.

Msofe alisema vifaa vilivyotolewa shuleni hapo kwa ajili ya kumaliziamadarasa matatu ni pamoja na saruji mifuko 100, nondo 60, shehena za kokoto, mchanga, mbao,waya na vifaa vingine vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 10.

“Malengo yetu si kuhudumia sekta ya maji tu bali tutaendelea kujikita katika kusaidia huduma za kijamii pale tutakapoona upo ulazima wa kufanya hivyo bila ya kuathiri utendaji wa kazi zetu”Alisema Msofe.

Awali akisoma taariafa fupi mbele ya mgeni rasmi Mkuu wa Shule hiyo Kaana Erasto alisema shule hiyo iliyo na wanafunzi 1319 inauhitaji wa madarasa 33 huku yaliyopo 24 ambapo kunaupungufu wa vyumba 9 ili kutoa fursa kwa wananfunzi kupata sehemu ya kujisomea.Alisema jitihada za wadau zimeanza na tayari ujenzi wa vyumba vitatu kati ya tisa umekwisha anza na majengo yapo katika hatua za mwisho ili kuweza kukabiliana na uhaba huo na kutoa fursa kwa wanafunzi ambao wamekosa mahala pa kujisomea.

Erasto alisema wanafunzi waliopata nafasi ya kujiunga na shule hiyo kidato cha kwanza mwaka 2019 ni 405 huku 150 ndio waliopo madarasani ambapo wanafunzi 255 wakikosa mahala ma kujisomea na kupelekea wahisani kujitolea katika ujenzi wa madarasa.

INTRODUCING:Fatuma - Candle Light (video)

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images