Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Serikali Mbioni Kuondoa Tofauti za Mishahara


ZAIDI YA SH. BIL. 500 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zaidi ya sh. bilioni 500 zimelipwa kwa wakulima wa korosho kati ya sh. bilioni 700 zinazotarajiwa na kwamba malipo hayo bado yanaendelea kulipwa kwa wakulima wengine waliosalia. Amesema tamko la Rais Dkt. John Magufuli la kwamba Serikali itanunua korosho kwa bei ya sh. 3,300 ni kwa ajili ya korosho za daraja la kwanza  na bei ya korosho za daraja la pili ni asilimia 80 ya zile za daraja la kwanza.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Februari 7, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka. Mbunge huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu malipo kwa wakulima wa korosho ambao walikuwa wakilipwa sh. 2,600 kwa kilo wakati Rais Dkt.  Magufuli alisema Serikali itanunua kilo moja ya korosho kwa sh. 3,300.

“Malipo yanaendelea na sehemu kubwa ni kwa wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500, Serikali itanunua korosho zote kama ilivyoelezwa. Taratibu zinazofanyika ni kuhakikisha anayelipwa ni muhusika. Wananchi endeleeni kuiamini Serikali yenu.” Waziri Mkuu amesema ilikuwa ni lazima kwa Serikali ifanye uhakiki kwa wakulima hususani wale wenye kilo zaidi ya 1,500 ili kujiridhisha kama ni wakulima, hivyo baada ya kuhakikiwa wakulima wote watalipwa fedha zao.

Amesema Januari 27, 2019 alitoa maagizo kwa Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wahakikishe hadi Februari 15 mwaka huu wawe wamekamilisha zoezi la uhakiki na kuwalipa wakulima wote wa zao la korosho. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao kilichofanyika mkoani Mtwara, lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupata taarifa juu ya mwenendo mzima wa bidhaa hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali haijakiuka sheria kuhusu suala la watumishi kupandishwa mishahara na kwamba ina nia njema ya kuhakikisha wanalipwa mishahara na posho nzuri. Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga aliyedai Serikali imekiuka sheria ya utumishi kwa kutopandisha mishahara, ambapo Waziri Mkuu amesema  Serikali haikukiuka sheria, bali iliamua kushughulikia suala hilo kwa kuanza na uhakiki wa watumishi.

Waziri Mkuu amesema baada ya kufanya uhakiki na kubaini uwepo kwa watumishi hewa pamoja na waliokuwa wakitumia vyeti vya kugushi, iliwaondoa na sasa Bodi ya Mishahara na Maslahi ya Watumishi wa Umma inafanya mapitio ya mishahara baada ya kubaini tofauti, hivyo watumishi waendelee kuwa watulivu.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka  Mbunge wa Mchinga, Hamidu Hassan Bobali ambaye aliuliza swali katika kipindi  cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Uwekezaji , Angela Kairuki baada ya kujibu vizuri sana maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

UJENZI WA RELI YA KISASA WAMKUNA SHISHY BABY, APELEKA OMBI KWA JPM

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

OMBI la Shishy Baby kwa JPM si mchezo !

Msanii maarufu nchini kwenye tasnia ya uigizaji wa filamu za kibongo nchini pamoja na kuomba nyimbo za Bongo Fleva Zuwena Mohammed a.k.a Shishy Baby ametoa ombi maalumu kwa Rais Dk.John Magufuli.

Shishy a.k.a Shilole hakuwa na muda wa kujivunga yaani baada ya kupata nafasi tu ya kuambiwa anamwambia nini Rais John Magufuli , basi yeye akasema lake kwa Rais ni moja tu nalo ni kwamba anaomba reli ya kisasa inayotumia umeme itakapokamilika basi yeye amruhusu awe anauza chakula tu kwani hiyo itamtosha kuliko akipewa fedha.

Unajua kayasema wapi hayo?Shishy amesema hayo leo Februari 7 mwaka 2019 ndani ya treni wakati anazungumzia safari ya kwenda kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambayo inajengwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli.

"Kwanza nimefurahi kuwepo hapa na kwenda kuangalia namna ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unavyoendelea.Ni muhimu kwenda kuangalia ujenzi huu ambao Rais wetu anasema ujenzi wake unatokana na fedha zetu watanzania kupitia kodi, na mimi kwenye kazi zangu nakatwa kodi,"amesema Shishy Baby.

Ameongeza anaamini reli hiyo itakapokamilika utasaidia kujenga uchumi wa nchi yetu kwani watanzania watakuwa na fursa ya kusafiri kati ya eneo moja na jingine kwa haraka."Hivyo hata kwa wanaofanya biashara watakuwa na uwezo wa kusafiri kwa haraka na mambo yakaenda.Itakapokamilika reli hii tutakuwa tumepiga hatua na tuna kila sababu ya kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ya kuleta maendeleo."

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya wasanii ambao wanaitwa na viongozi lakini wanashindwa kufika, Shishy Baby amejibu ni vema wasanii wanapoitwa na viongozi wao wakafika kwani ni sehemu ya kuonesha nidhamu na heshima na kujichanganya na wengine kuna faida nyingi ikiwemo ya kupata mawazo tofauti na kukutana na watu tofauti.

"Unapoitwa na kiongozi halafu ukakataa kwenda huo ni utovu wa nidhamu.Tunashuhudia wasanii maarufu katika nchi mbalimbali duniani wanapoitwa na viongozi wao wanakwenda na wanazungumza bila tatizo.Hivyo wasanii tunapoitwa na viongozi ni vema tukaenda kusikiliza,"amesema.

Kuhusu treni hiyo amesema , kubwa ambalo kwake linamfurahisha ni kwamba inapita Igunga mkoani Tabora , hivyo matarajio yake itakapokamilika atafanya biashara ambapo akatumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa rais kuwa ,anatamani kufanya biashara ndani ya treni ya kisaa."Rais wangu Magufuli naomba jambo moja tu kwako, hii reli ikamilika na treni ikaanza kufanya safari basi uniruhusu niwe nafanya biashara tu.Hii itanitosha sana kuliko kuewa fedha." 

Wakati huo huo Shishy Baby au Shilole amesema kikubwa ambacho kimemfurahisha kwenye safari hiyo ya kwenda kuangalia ujenzi wa reli ya kisasa, ni kwamba amekutana na wasanii wengi maarufu na wengine hajawahi kuwaona ana kwa ana lakini leo imewezekana.

Kiongozi wa msafara huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambapo ameelezea umuhimu wa wasanii kushuhudia ujenzi wa SGR na kufafanua Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania wote.

DUDE AWAGEUZIA KIBAO WANAOBEZA JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Na Khadija Seif ,Globu ya jamii

MSANII wa Bongomovie Kulwa Kikumba a.k.a Dude awaonya watanzania wanaobeza uhudi za Serikali ya awamu ya tano.

Dude ameyasema hayo leo Februari 7,2019 wakati wa kutembelea mradi wa reli wa kisasa (SGR) ambapo amesisitiza ni wakati wa kupongeza na kuonesha ushirikiano kwa maendeleo yanayoletwa nchini chini ya Rais Dk. John Magufuli kwani Tanzania kwa sasa ni madhubuti na imara kwa kila sekta hasa ya uchukuzi.

"Hivi karibuni tulishuhudia ndege mbili zikikabidhiwa hiyo ni wazi kuwa Rais Magufuli lengo lake ni kuhakikisha Watanzania hatuko nyuma katika suala la maendeleo,"amesema Dude.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wasanii kuwa mabolozi kwa kueleza mambo mambo mazuri yanayofanywa na Serikali na kwamba treni ya kisasa itakapoaza kutoa huduma ya kusafirisha abiria watoe hamasa ili wananchi wengi waitumie treni hiyo katika safari zao mbalimbali.

Wakati huo huo Dude ametumia nafasi hiyo kuwataka wasanii kuwa na umoja ambao utaleta tija kwa maslahi yao pamoja na kuboresha tasnia na kusiwepo kwa matabaka yatakayofanya tasnia kushuka kiwango.
MSANII wa Bongomovie Kulwa Kikumba a.k.a Dude  

WAZIRI WA KILIMO MHE JAPHET HASUNGA AFUNGUA SEMINA YA BIMA KWA MAJANGA YA KILIMO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili ya Bima kwa majanga ya kilimo inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Baadhi ya washiriki wa Bima kwa majanga ya kilimo wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) akifatilia kwa makini mkutano wa Bima kwa majanga ya kilimo mara baada ya ufunguzi inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.
Picha ya pamoja ya Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) na baadhi ya washiriki wa semina ya Bima kwa majanga ya kilimo inayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam kuanzia leo tarehe 7 Februari 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 7 Februari 2019 amefungua semina ya siku mbili ya Bima kwa majanga ya kilimo nayofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa BOT Jijini Dar es salaam

Akizungumza katika semina hiyo Mhe Hasunga amesema kuwa hiyo ni hatua nzuri katika kuhuisha utoaji wa huduma bora za bima za kilimo kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Bima ya Mwaka 2009, Sheria na Mipango Mbalimbali katika sekta ya kilimo; kwa kutafutia ufumbuzi wa pamoja changamoto zinazokabili sekta ya kilimo na wakulima nchini. 

Waziri Hasunga ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) kwa kuandaa mkutano huo muhimu wa wadau wa bima katika kilimo kwani utakuwa na fursa ya kujadili na kuchambua namna ya kuboresha tija kwa wakulima kwa kuwaingiza katika Bima ya Mazao.

Alisema kuwa jitihada hizo za sekta ya bima nchini ni kuunga mkono mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwani Viwanda ni Kilimo, na kilimo bora chenye tija hukingwa na bima.

Amesema kuwa semina hiyo ikiongozwa na dhima inayosema “Bima za Kilimo Nchini Tanzania: Nafasi na Wajibu katika Utekelezaji” inalenga kuleta majibu katika changamoto ambazo serikali imejikita katika kukabiliana nazo hususani kwa wakulima kote nchini. 

Aliwataka Wataalamu wa Bima waliohudhuria katika semina hiyo kutambua kuwa sekta ya bima ni kichocheo muhimu katika uchumi wa viwanda na Kilimo chenye tija. Kwa kukinga majanga mbalimbali katika Mnyororo mzima wa sekta ya kilimo kwa sehemu kubwa kuimarisha viwanda.

Waziri hasunga amewataka wataalamu katika sekta ya bima na wa upande wa Sekta ya Kilimo kujiuliza na kujibu maswali ya Kwanini mwamko wa wananchi katika bima hususani Bima za kilimo upo chini? (kwa mujibu wa takwimu ni 15% tu ya watanzania hupata huduma za bima) kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na zaidi ya 75% ya wanojihusisha na kilimo.

Ni lini na kwa namna gani wakulima na wafugaji wadogo wa Tanzania wataanza kunufaika na bima za Mazao na Mifugo?, na Njia zipi zitumike kuhakikisha kuwa huduma za bima za kilimo zinakuwa nafuu na zenye tija katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Mengine, Ni njia zipi zinaweza kutumika kuwahamasisha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutumia huduma za bima katika kazi zao na Ni jinsi gani Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inaweza kutumika katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za bima za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Pia, amehimiza kuelekea lengo la kuhakikisha angalau asilimia 50 ya watu wazima wanapata huduma ya bima ya chini ifikapo mwaka 2028, kutafakari jinsi Tanzania inavyoweza kuimarisha teknolojia zinazojitokeza kama vile majukwaa ya biashara ya digitali na mifumo ya malipo ya simu kutoa huduma za bima na huduma kwa wakulima wanaofikia milioni 38. Ubunifu na ushirikiano katika kupata masoko mapya hususani ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutumia njia mbadala vitaimarisha ubia kati ya sekta ya kilimo na bima.

Awali, Kamishna wa Bima Tanzania Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa wazo kuu la kuandaa mkutano huo ni kuendeleza kwa dhati ushirikiano kati ya Taasisi za Umma, Makampuni Binafsi na Mashirika ya Kijamii ili kutoa huduma ya Bima ya kilimo katika jamii kwa wigo mpana.

Alisema kuwa kuanzia mwaka 2016/2017 serikali ilizindua mpango wa miaka mitano uliojikita katika kuifanya Tanzania iwe nchi ya uchumi wa kati kwa kutegemea viwanda.

Aliongeza kuwa maeneo muhimu ambayo sekta ya Bima (Binafsi) na Taasisi za umma zinaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuongeza ufanisi katika shughuli za Bima ya kilimo kwa kuwa na sera ya Taifa ya Bima, Kuwa na taarifa za wakulima (Data Base), vilevile wananchi kuwa na imani (Kuamini) biashara na huduma za Bima.

Zingine ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma na wigo wa huduma za Bima nchini, Teknolojia rahisi na rafiki kwa ajili ya kusambaza Bima, kuuza Bima, Kulipa mafao/Madai ya Bima, kusikiliza maoni na mahitaji ya wananchi, na kuchakata maombi ya Bima.

Serikali ya Tanzania na Misri kusainiana mkataba wa makubaliano wa kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja kwa lengo la kuinua kilimo cha ngano, mpunga na pamba

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akimkaribisha Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa ajili ya mazungumzo na Mwenyeji wake
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakiongoza kikao kazi kati ya Wataalam wa Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara ya Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa sambamba na Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri Mhe. Dkt. Ezzidine Abu Stiet wakati wa majadiliano na Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo Tanzania na Wataalam wa Wizara ya Kilimo ya Misri katika Ukumbi wa Wizara (Kilimo IV) Jijini Dodoma


Serikali ya Tanzania na Misri zinatarajia kusainiana mkataba wa makubaliano wa kuanzisha mashamba makubwa ya pamoja kwa lengo la kuinua kilimo cha ngano, mpunga na pamba

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga mara baada ya kufanya mazungumzo na timu ya Wataalamu wa kilimo kutoka Misri wakiongozwa na Waziri wa Kilimo na Ardhi wan chi hiyo, Dk Ezzidine Abu Stiet.Mhe. Hasunga amesema katika mazungumzo hayo wamekubaliana kushirikiana katia Sekta ya Kilimo husan katika mazao ya mpunga, ngano na pamba ambapo tande zote mbili zitakuwa na mashamba ya pamoja.

“Kama mnavyojua Misri wamepiga hatua katika kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji na tekinolojia hivyo tumekubaliana mafaniko hayo yahamie hapa nchini.”

Waziri Hasunga aliongeza: “Baada ya mazungumzo ya kina na makubaliano katika maeneo ya ushirikiano, tumepeana miezi miwili ili ifikapo mwezi Mei mwaka huu, tutasaini mkataba wa makubaliano na kuanza utekelezaji.

Amesema eneo lingine ambapo wamekubaliana ni kuimarisha Vituo vya Utafiti wa mazao ili kupata mbegu bora na namna bora ya kuzitumia mbegu hizo na pia kuhamisha ujuzi na zana kutoka Misri ambao utasidia kuinua kilimo hapa nchini.

Waziri Hasunga alisema kwa sasa Wataalam wa kilimo wa nchi hizo mbili watatumia muda huu wa miez miwili kutembelea maeneo mbalimbali ili kubainisha maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo.“Mfano tuliwaza kupeleka kilimo cha ngano wilayani Misenyi mkoani Kagera lakini wamesema eneo hilo ni dogo, hivyo wataalamu wa Misri na wale wa Tanzania watapita maeneo mbalimbali kuangalia maeneo yanayofaa na baadaye tusainiane mkataba wa makubaliano,” alisema.

Naye Waziri wa Kilimo na Ardhi wa Misri, Stiet alisema wamekuwa na mazungumzo mazuri na yenye mafanikio na kukubalianakushirikiana katika mafunzo, utafiti na tekinolojia katika sekta ya kilimo ili kuboresha mazao ya kimkakati ya pamba, mbunga na ngano..

“Makubaliano hayo yanaongeza wigo wa ushirikiano kati ya nchi hizi mbili ambayo ni ya muda mrefu, tumekubaliana kuinua kilimo katika mazao matatu kwa manufaa ya wananchi wa Tanzania. Baada ya kusainiana mkataba tunategemea utekelezaji wa haraka,” alimalizia.

Balozi Seif afanya mazungumzo na Rais wa Taasisi inyosimamia mazungira kutoka UN

$
0
0
Rais wa Taasisi inayosimamia mazingira ya Umoja wa Mataifa Bwana Siim Valmar Kiislar amesema wakati umefika kwa Mataifa yote Ulimwenguni kuwa na mfumo Mmoja unaoeleweka wa utunzaji wa Mazingira utakaosaidia kuifanya Dunia iendelee kubakia salama.

Alisema tabia ya baadhi ya Mataifa kuendelea kukwepa mikataba na baadhi ya kanuni zinazowekwa Kimataifa pamoja na kuweka vikwazo vyenye nia ya kulinda maslahi yao binafsi vitapelekea kuongezeka kwa wasi wasi utakaoifanya Dunia hii ibakie katika mazingira hatarishi.

Bwana Siim Valmar Kiislar alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Rais huyo akiuongoza Ujumbe mzito wa Taasisi hiyo ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa amekuja kushuhudia uzinduzi wa Kampeni ya Kidunia ya uzinduzi wa usafi wa Mazingira katika Fukwe ya Forodhani Visiwani Zanzibar ulioambatana na ujio la Mashua ya Mazingira iliyotengenezwa kutokana na malighafi ya Plastiki kutoka Nchini Kenya.

Bwana Siim Valmar ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Wananchi wake kwa umakini wao wa kusimamia masuala ya Mazingia katika kuitikia kampeni ya Kimataifa ya kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi.

Alisema kitendo cha Zanzibar kufanikiwa katika mapambano yake ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya Plastiki mbali ya kuwa mfano kwa Mataifa ya Ukanda wa Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, lakini pia kimeleta faraja kwa Umoja wa Mataifa kupitia Taasisi yake hiyo  inayosimamia masuala ya Mazingira.

Naye Mratibu Mkaazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi Nchini Tanzania Bwana Alvaro Rodriguez alisema bado Mataifa Ulimwenguni yana wajibu wa kushirikiana katika mapambano yake dhidi ya uchafuzi wa Mazingira.

Bwana Alvaro alisema ustawi wa Jamii pamoja na viumbe vilivyomo  ndani ya Dunia vitaendelea kuishi kwa amani bila ya vikwao endapo ushirikiano huo utaimarishwa na kuendelea kuwa wa kudumu kama inavyoonekana katika baadhi ya maeneo.

Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar bado inaendelea kuathirika na mabadiliko ya Tabia Nchi akatolea mfano ufukwe wa Bahari ya Msuka uliopo kaskazini mwa Kisiwa cha Pemba ambao tayari umeshaliwa na mawimbi ya Bahari kwa sehemu kubwa.

Balozi Seif aliueleza Ujumbe huo wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa unaosimamia Mazingira kwamba Zanzibar imeanza mikakati ya kupiga marufuku matumizi na uingizwaji wa Mifuko ya Plastiki tokea mwanzoni mwa Miaka ya 90 na kufanikiwa vyema katika azma yake ya kulinda mazingira.

Alisema ujio wa mashua ya Mazingira katika Visiwa vya Unguja na Pemba utasaidia mfano wa Darasa kwa Wananchi waliowengi kuwa na muelekeo wa jitihada za mapambano dhidi ya mabadiliko ya Tabia Nchi yanayoikumbwa Dunia hivi sasa na kuleta athari kubwa ya Kimazingira.
 Rais wa Taasisi inayosimamia mazingira ya Umoja wa Mataifa Bwana Siim Valmar Kiislar kiipongeza Zanzibar kwa mapambano yake ya kusimamia vyema mazingira alipokuwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani.
 Balozi Seif Ali Iddi Kulia akisisitiza jambo wakati akizaungumza na  Bwana Siim Valmar Kiislar aliyewasili Zanzibar kushuhudia Uzinduzi wa usafi wa mazingira Kidunia katika Fukwe ya Forodhani.
 Balozi Seif Kulia na Mgeni wake Rais wa Taasisi inayosimamia mazingira ya Umoja wa Mataifa Bwana Siim Valmar Kiislar wakitoa nje ya Ofisi baada ya kumaliza mazungumzo yao.
 Bwana Siim Valmar Kiislar kati kati  akibadilishana mawazo na Balozi Seif baada ya mazungumzo yao huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed akishuhudia.
 Balozi Seif  wa Nne kutoka Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Uongozi wa Juu wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa inayosimamia Mazingira nje ya Jengo la Baraza la Wawakilishi baada ya kumaliza mazungumzo yao. Kulia ya Balozi Seif ni Rais wa Taasisi hiyo Bwana Siim Valmar Kiislar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed, Mratibu Mkaazi wa Mashirika ya Umoja wa Mtaifa Nchini Tanzania Bw. Bwana Alvaro Rodriguez na Ofisa wa Uratibu katika masuala ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bibi Clara Makenya. Kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Zanzibar Bibi Farhat Farhat Ali Mbarouk na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mohamed Haji Hamza. Picha na – OMPR – ZNZ.

WAKUU WA SHULE ZA JWTZ WAWEKA MIKAKATI TISA KUBORESHA MATOKEO KIDATO CHA NNE NA SITA

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Wakuu wa Shule zinazomilikiwa na jeshi la ulinzi la wananchi JWTZ wametakiwa  kuboresha uendeshaji wa shule hizo ili kuendana na kasi ya Serikali na kukidhi mahitaji  na mwongozo wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu  Dkt John Magufuli kuwa nchi ya uchumi wa kati kwa kuzalisha wahitimu wanaoendana na azimio hilo.

Maagizo hayo yalitolewa na Mkuu wa mafunzo na Utendaji Kivita JWTZ  Meja Jenerali Alfred Kapinga wakati wa Kikao na Wakuu hao wa Shule yenye lengo la kutathmini na kuweka maazimio kikao kilichofanyika Makao Makuu ya Jeshi Jijini Dar es Salaam.

Alisema kufanya vizuri kwa shule za Jeshi ni wajibu ambao pia umekuwa ukisisistizwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance mabeyo kutokana na mazingira ya Shule husika.

“ Hatuna sababu kuacha  kujitofautisha na shule za kiraia kutokana na mazingira ya shule zetu ziliko na Walimu katika shule hizo wakiwemo ambao ni wanajeshi hivyo ni matarajio ya Mkuu wa Majeshi kuona Utofauti huo kutokana na wananfunzi wanaohitimu katika shule hizo.” Alisema Meja jenerali Kapinga.

Aliongeza kuwa mwanafunzi anayemaliza katika Shule ya jeshi la Anga Ngerengere na Anayemaliza katika Shule ya Wanamaji Kigamboni na anayemaliza Makongo na shule nyingine Wanatakiwa kuwa tofauti kutokana na Elimu ya Ziada iliyotokana na Fursa ya Uwepo wa shule katika mazingira husika.

Pia aliwataka Kuanzisha Mafunzo ya Ufundi Stadi ili nayo kuwa Sehemu ya Utofauti wa Shule hizo kwa kuzalisha Wataalamu wa kati na wa chini watakaojiajiri lakini pia kuajiriwa katika Viwanda na fani husika.

“ Navy  niliwaelekeza wameanza na wameanza kwa mafanikio sasa kilichobaki ni kuboresha  elimu inayotolewa na chuo ili kuweza pia kujitangaza na kuwa fursa ya kupata Wanafunzi wa Kutosha  na kutoa Mchango stahili kwa Nchi”.  Alisema Mkuu huyo wa Mafunzo na utendaji Kivita.

 Aliongeza kuwa nidhamu ni kitu muhimu hivyo wanafunzi wanaomaliza katika Shule za kijeshi wanatakiwa kuwa na nidhamu zaidi kuliko wanafunzi katika shule nyingine wakiakisi Nidhamu iliyoko katika jeshi ingawa yasiwe mafunzo kama ilivyokuwa kwa Shule ya  Wavulana ya Tabora.

Wakuu hao wa shule za JWTZ wameahidi kufanyia kazi maazimio hayo ikiwa pia ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kurejesha majina ya shule za jeshi  ikiwemo uanzishaji wa vyuo vya ufundi kwa fani zilizokaribu na shule husika

Miongoni mwa maazimio walioweka ni uanzisjhaji masomo ya Sayansi ya Kijeshi, kusimamia ipasavyo walimu,nidhamu, uboreshaji miundombinu uanzishwaji klabu za hesabu,kufufua vipaji kwa shule za michezo na kuboresha mahusiano na wadau wengine wa elimu ili kuendana na mabadiliko.

Pia  Wakuu hao wa Shule wameazimia Kuongeza Ufaulu kwa kuondoa  Divisheni  O  kwa baadhi ya Shule zilizopata matokeo hayo na  Divisheni IV  kwa shule zenye ufaulu wa mwisho wa Divisheni IV kwa wahitimu wa Kidato cha Nne  na Sita na Ufaulu wa chini kubakia Divisheni III.

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania linamiliki Shule 10 Nchini ambazo ni Nyuki  Unguja , Al Khamis Camp  Pemba, Airwing,  Makongo Jitegemee  na Kigambo zilizoko Dar es salaam, Ruhuwiko Songea,Unyanyembe Tabora, Kawawa Mafinga Iringa  na Kizuka Morogoro.

Uanzishwaji wa shule hizo ulikuwa na  Lengo la kutoa Elimu kwa Askari wake na baadae kutoa Elimu kwa Familia za Askari husika lakini baadae kwa jamii Nzima ambayo imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na Shule hizo
 Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga Katikati akizungumza na wakuu wa Shule zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ hawako pichani katika kikao cha Utendaji kuhusu maboresho ya Shule hizo Jijini Dar es Salaaam kulia na Mkurugenzi wa wa Mafunzo na Elimu Brigedia Jenerali Maurius Mhagama. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita Meja Jenerali Alfred Kapinga Katikati akizungumza na wakuu wa Shule zinazomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika kikao cha Utendaji kuhusu maboresho ya Shule hizo Jijini Dar es Salaaam. ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Tuboreshe Sekta ya Elimu katika soko la ajira kimataifa-Makinda

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 SPIKA Mstaafu, Anne Makinda, ameshauri kuboresha  sekta ya elimu ili kuwahakikisha vigezo vya elimu vya Tanzania vinaendana na vigezo vya kimataifa na Dunia ndiyo inataka tuende hivyo Akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu cha Aga Khan yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, Makinda amesema Tanzania haina budi kufanya hivyo kwa sababu ni sehemu ya dunia na haina soko lake yenyewe ya kuajiri hivyo wahitimu wetu wanaweza kufanya kazi Duniani kutokana na elimu waliopata.

“Kama tuko katika dunia vigezo vyetu lazima viendane na wenzetu ili tuwe na elimu itakayotuwezesha kushindana katika soko la dunia, hatuna soko la Tanzania peke yake Aga Khan wamethubu katika uwekezaji katika elimu” amesema Spika Makinda. Makinda amesema ameshangazwa na wastani wa walimu na wanafunzi chuoni hao hali inayoashiria kuwa chuo hicho kinafuata vigezo vya kimataifa katika ufundishaji kwa Mwanafunzi watatu  kwa Mwalimu Mmoja. 

“Ni mara yangu ya kwanza kufika katika chuo hiki, lakini nafahamu kuwa ndicho chuo cha kwanza Tanzania kutoa shahada ya uuguzi Ila nimeshangazwa na idadi ya walimu yaani walimu wako ishirini wanafunzi 59 inamaana kila mwalimu mmoja anahudumia wanafunzi watatu” alisema Makinda.

Aliwashauri wahitimu wa kada mbalimbali nchini kujitoalea kwa moyo wao wote kusaidia jamii na kutokubali kukatishwa tama na changamoto wanazokutana  nazo. Makinda amesema endapo kila mhitimu mmoja wa shahada ya uuguzi na ukunga chuoni hapo atajitolea walau asilimia 35 tu ya muda wake kuwahudumia wagonjwa itawatia nguvu.

Rais wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Firoz Rasul amesema chuo hicho kimeendelea kuhakikisha kinatoa elimu bora ambapo mwaka jana mhitimu wa chuo hicho tawi la Dar es Salaam alitajwa kama tuzo ya mwalimu bora wa mwaka nchini Kenya. "Zaidi ni kwamba kwa mara ya pili mhitimu wa Aga Khan ametajwa katika fainali ya kuwania zawadi ya dola milioni katika tuzo za kimataifa za walimu" amesema 

Amesema programu mbalimbali wamefanikiwa kuwajengea uwezo na mbinu mpya za ufundishaji zaidi ya walimu 3,000 ambazo zimewanufaisha zaidi ya wanafunzi 100,000. Amesema kwa sasa wanajipanga kuanzisha stashahada ya ualimu kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuwaongezea uwezo walimu wa shule za misingi.
 Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu  Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Chuo Kikuu Aga Khan Firoz Rasul akizungumza akitoa maelezo ya Chuo Kikuu Aga Khan katika Mahafali ya 14 yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo Kikuu Aga Khan Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande akimtunuku shahada ya Uzamili Abdallah Hoza katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu wakiingia katika mahafali ya 14 ya Chuo Kikuu Aga Khan yaliyofanyika katika viwanja vya Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu Aga Khan wakiingia Ukumbini katika mahafali ya 14 ya Chuo hicho.

Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) jijini Dar es Salaam kesho Februari 8, 2019-

$
0
0

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania Limited itazindua kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) kilichoko katika eneo la viwanda la Chang'ombe- Temeke, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania kuwa ndio kampuni pekee ya kimataifa nchini Tanzania yenye kutengeneza vilainishi vyake yenyewe ambapo inatarajiwa itazalisha zaidi ya tani 15,000 za vilainishi kwa ajili ya soko la ndani ya nchi na ziada itauzwa nje nchi.
Kwa zaidi ya miaka 50 ya uwepo wake nchini Tanzania, Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania ilikuwa ikiagiza vilainishi vyake kutoka nje ya nchi lakini kuanzia sasa, vilainishi hivyo vinatengenezwa humu humu nchini.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania Limited kuunga mkono kwa vitendo, mkakati wa rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda. Kiwanda hiki licha ya kuchangia katika maendeleo ya taifa kiuchumi na kitekinolojia, pia kitatoa nafasi za ajira kwa Watanzania.
Kwa upande wao, wamiliki wa  moja ya vituo vya mafuta vya Total, Total Tageta, Vincent Lymo na mkewe Mary Vincent Lymo,  waliishukuru kampuni ya Total kwa kuwaonyesha fursa kutoka kuutumia uwanja huo kwa kufyatulia motafali, hadi kuwa kituo cha kwanza cha mafuta chenye hadhi ya kimataifa, ambacho sasa kitauza vilainishi vya Total
Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta
Total ipo katika nchi zaidi ya 130,  na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika. End
Kuhusu Kampuni ya Total
Total ni kampuni ya kimataifa ya nishati ya mafuta na gesi ni ni moja ya makapini ya kwanza kabisa ya kimataifa kujihusisha katika nishati ya jua duniani kote.  Ina wafanyakazi 100 000 wenye kuchangia dhima ya kampuni : kuzalisha nishati bora na safi na salama,  na kuizalisha kwa ufanisi zaidi, nguvu zaidi na  ubunifu wa hali ya juu, huku ikiwa ni nishati ya gharama nafuu ili  watu wengi waweze kuimudu.
 Total ipo katika nchi zaidi ya 130,  na inafanya kila linalowezekana kuboresha maisha watu wa nchi hizo kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira husika.

Total imeanzisha kampeni kabambe utafutaji na uzalishaji wa mafuta kwa kuongeza idadi ya visima vya mafuta huku ikijitahidi kupata nishati endelevu kwa ajili ya Bara la Afrika kwa sasa na baadae. Total imejikita katika uhamasishaji wa utafutaji vya vyanzo vipya vya nishati kutoa kipaumbele cha elimu ya nishati kwa vijana ili kuendeleza uwezo wa kipekee wa bara hili la Afika kujiletea maendeleo. Mbali na hilo,Kampuni ya Total   ndio sambazaji wa kwanza wa bidhaa za mafuta (mafuta ya petroli, dizeli, mafuta ya taa , lami,  na GPL, nk) katika bara la Afrika. Shukrani kwa mizizi yake ya kihistoria, ubora wa bidhaa na huduma zake, kutoka jumla ya vituo 4200 vya mafuta  katika nchi arobaini barani Afrika.  Vituo vya mafuta vya Total ni vituo tegemeo kwa wafanya biashara binafsi na wateja wake. Lengo letu ni kuwezesha upatikanaji mkubwa zaidi wa nishati, ambayo pia inahusisha kuendeleza upatikana wa vyanzo vingi na mbadala vya nishati na kwa gharama nafuu -  kama vile nishati ya jua, kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua
Total tunasikiliza mahitaji ya wadau wetu, na sisi kwenda nao pamoja nao katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na afya. www.total.com

Kuhusu Total Tanzania



Total Tanzania ni kampuni ya Mafuta ya petroli iliingia nchini Tanzania tangu mwaka1969. Biashara ya Total Tanzania inalenga katika kutoa huduma za usambazaji na uuzaji wa mafuta ya petroli, dizeli vilainishi na bidhaa za mafuta, ambayo ni kuuzwa katika vituo mbalimbali vya mafuta na pia katika idara maalum ndani ya wake shirika hilo. Total Tanzania Limited inatumia utaalamu wake katika kutoa huduma za  kuaminika kwa wateja wake kwa mfumo wa kadi maalum “ Kadi ya Total” kwa ajili ya ununuzi wa mafuta na huduma mbalimbali magari katika vituo vya mafuta vya Total Katika kujitanua kibiashara kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala, kampuni ya Total Tanzania Limited kupitia mradi wake wa Total Access to Solar (TATS) project, inasambaza taa za nishati jua zinazoitwa  AWANGO kwa jamii ya Watanzania.
Vincent Lyimo na mkewe Mary Lyimo, wamiliki wa Kituo cha Total Tegeta cha jijini Dar es salaam wakizungumza siku ya uzinduzi wa kituo chao hivi karibuni.

TPSF YAJADILI MAPENDEKEZO YA SERA YA KODI BAJETI YA 2019/2020

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na Wadau wake kukamilisha zoezi la kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Kodi kuelekea Bajeti ya 2019/2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya msisitizo wa Mhe. Rais kuwa na haja ya kuangalia au kufumua upya mfumo wa Kodi pamoja na Sera yenyewe  inayoonekana kuwa mzigo mkubwa kwa Wafanyabiashara.

Simbeye amesema kazi hiyo imeanza tangu Novemba, 2018 , amesema wamekuwa wakikusanya maoni  tofauti ili kujadiliana kwa pamoja na kupata maoni hayo yatakayopelekwa Serikalini kwa ajili yakuingia kwenye maboresho ya sera ya Kodi au mfumo wa Kodi nchini.

‘’Sisi kama Sekta Binafsi tunatimiza wajibu wetu kuchangia mawazo namna gani bora ambavyo tunaweza kuweka mfumo wa Kodi ili iwe rahisi kufanya biashara Tanzania nakuweza kukuza Uwekezaji’’, amesema Simbeye.

Kwa upande wake, Mmoja wa Wanachama wa Sekta hiyo, Mwakilishi kutoka Chama cha Waajiri nchini (ATE), Dan Sora Tandasi amesema lengo lakukutana kama Wadau kutilia mkazo kwenye masuala ya Kodi, amesema Wafanyabiashara wanapata fursa kujadili changamoto zao katika Kodi.

MATUKIO MBALIMBALI YA BUNGENI LEO JIJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo, Dkt.  Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizunguma na Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent  Bashungwa, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.  Phillip Mpango, bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Mbunge wa zamani, Semindu Pawa akitambulishwa bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya Kilosa mkoani Morogoro kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Monica ya Arusha kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso na kulia kwa Waziri Mkuu ni  Mwalimu Mkuu  wa shule Msaidizi, Sista Colletah.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi  ya Assumption ya Arusha, Ritta Deo Moshi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Mtoto huyo na wenzake walikwenda bungeni kujifunza shughuli mbalimbali za Bunge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HALIMA MDEE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI AKIMUUGUZA MBUNGE MWENZAKE

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii. 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,  leo Februari 7, 2019 imeshindwa kuendelea na usikilizwaji wa kesi kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee baada mahakama kupewa taarifa kuwa ameshindwa kufika  kwa  madai kuwa anamuuguza Mbunge Bunda mjini  Ester Bulaya mkoani Dodoma. 

Hayo yameelezwa mdhamini wa Mdee,  Faris Lupomo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa 

Lupomo amedai, aliwasiliana na mbunge huyo na kumueleza kuwa atashindwa kufika mahakamani kwa kuwa anamuuguza mbunge mwenzie Bulaya ambaye anaishi naye Dodoma nyumbani kwake na anamuuguzia Katika hospitali ya Bunge mkoani humo. 

Wakili wa Utetezi Hekima Mwasipu naye alikiri Mahakamani hapo kwa  mshtakiwa huyo hayupo na amepewa taarifa na mdhamini huyo kuwa anamuuguza Bulaya mjini Dodoma. 

Baada ya kusikiliza maelezo hayo, Hakimu Simba amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini huyo kuhusiana na kushindwa kufika mahakamani kwa mshtakiwa  zinaleta ukakasi na kubainisha kuwa zina lengo la kuifanya kesi hiyo isimalizike kwa wakati kwa sababu wapo madaktari na wabunge wengine wanawake ambao wanaweza kumuuguza, sasa tukiruhusu haya yaendelee tutashindwa kumaliza kesi. 

"Kiukweli jambo hili linakwaza na linatia wasiwasi kama hii kesi tutaweza kumaliza kwa mwendo huu, tunakubali sababu hiyo ya kuuguza lakini kwa shingo upande, 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi, Februari 28, mwaka huu kwa aji

Mpaka sasa mashahidi watatu wamekwisha kutoa ushahidi katika kesi hiyo akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu wa Polisi Batseba Kasanga.

Mdee anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 3, mwaka jana maeneo ya Ofisi za Chadema zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alimtukana Rais Dk John Magufuli kwamba "anaongea hovyohovyo anatakiwa afunge break", kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

WASHTAKIWA SABA WA KESI YA BOMBA LA MAFUTA WAFUTIWA KESI NA KUACHIWA HURU

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru, washtakiwa saba kati ya 12 waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka ya kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania ( TPA).

Washtakiwa hao wameachiwa huru leo Februari 7.2019 baada ya upande wa mashtaka kuomba kuliondoa shtaka hilo. Mapema,  wakili wa Serikali mwandamizi , Patrick Mwita aliieleza mahakama kuwa, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuwaondolea baadhi ya washtakiwa mashtaka yao kwa sababu hana nia ya kuendelea na kesi dhidi yao

Washtakiwa hao saba wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai  (CPA), sura ya 20 , iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002. Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba  amesema kupitia kifungu hicho kilochowasilishwa,  mahakama hiyo imewafutia mashtaka washtakiwa hao saba na imewaachia huru.

Waliofutiwa  mashtaka ni Samwel Nyakirang'ani(63)ambaye ni  mfanyakazi mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia(Tazama), ) na Nyangi Mataro( 54) ambaye ni mwalimu wa shule ya  msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni.

Wengine ni Farijia Ahmed(39)mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni;  Malaki Mathias(39) mkazi wa Magogoni; Kristomsi Angelus(25) mkazi wa Soko Maziwa;  Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko(40) mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick (38) mkazi wa Tungi Kigamboni.

Kuhusu mshtakiwa waliobaki ambao wa nane hadi wa 12, upande wa mashtaka umedai, unaendeleaje kulifanyia kazi jalada hilo na  upelelezi wakei  bado haujakamilika. Mwita amewaja washtakiwa ambao bado wanashikiliwa kuwa ni, Audai Ismail (43) ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Washtakiwa hao watano, wamerudishwa rumande hadi Februari 21, 2019 kesi hiyo itakapotajwa. Inadaiwa kuwa kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoka katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali.

Katika shtaka la pili ambalo ni kuharibu miundo mbinu, inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa walitoboa bomba la hilo, ambalo lilikuwa likitumika kufirisha mafuta,  mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA). Pia wanadaiwa kuharibu bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA).

SERIKALI YATENGA TRIL 3 KUMALIZA MIRADI YA MAJI MIJINI NA VIJIJINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii.
SERIKALI imesema imetenga zaidi ya sh Tril. 3 kwa ajili ya miradi ya maji mijini na vijijini ili kuhakikisha tatizo la maji linamalizika kabisa nchini. Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, leo Februari 7, 2019 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo amesema hadi sasa miradi mikubwa 477 inatekelezwa vijijini huku 71 ikiwa mijini na mpaka sasa tayari mradi 71 imekamilika kwa vijijini.

Mkumbo amesema,  mwaka 2015 wakati serikali ikiingia madarakani hali ya upatikanaji wa maji vijijini ilikuwa asilimia 53 lakini hadi kufikia Desemba mwaka jana hali ya upatikanaji wa maji imeongezeka na kufika asilimia 59, huku upande wa mijini kwa awamu Hizo, upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka asilimia 68 mpaka asilimia 78,

Akiongelea kuhusu miradi mbalimbalii ya maji inayoendelea kutekelezwa na serikali,  Mkumbo amesema, katika kuhakikisha wanamaliza matatizo hayo hasa kwa miaka iliyoko juu mfano Kanda ya Ziwa wanategemea kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria ambapo miradi 17 itatumia maji kutoka ziwa hilo na zimetengwa Sh. Bilioni 788 kukamilisha hilo.

"Hadi sasa tayari kuna vituo 123,000 vyenye uwezo wa kuhudumia wananchi asilimia 85 kama vingefanya kazi lakini kwasababu havifanyi kazi kwasasa vinauwezo wa kuhudumia asilimia 59 tu ya watu," amesma.

Aidha ameongeza kuwa, katika kudhibiti matumizi mabaya ya miradi ya maji, wameshapeleka muswada wa sheria ya majisafi na mazingira ambao utasaidia mambo mengi ikiwemo kuanzishwa kwa wakala wa maji vijijini (Ruwasa), pia utatoa maelekezo ya wasimamizi wa miradi hiyo, kuwaadhibu watendaji wasio waadilifu na wameongeza adhabu kwa waharibifu wa miundombinu.

Aidha katika kudhibiti upotevu wa maji ambapo kwasasa umefikia asilimia 40 katika jiji la Dar es Salaam, wanafanya ukarabati wa miundombinu ambapo Dola za kimarekani Mil. 20 zimetengwa ambapo watafumua mabomba ya mchina ambayo utafiti mdogo umeonyesha hayana nguvu ya kuhimili msukumo wa maji yanayotoka kwasasa.

"Mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita mpaka mwaka. Na pia tupo kwenye mchakato wa kununua mtambo mpya wa kudhibiti maji," ameongeza Mkumbo

Ameongeza katika wizara hiyo wanakabiliana na changamoto mbali mbali Kwani,  mahitaji ni makubwa kuliko rasilimali zilizopo.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA UWT ZANZIBAR

$
0
0
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).Bi. Thuwaiba Kisasi , akiwa na Ujumbe wa Viongozi wa (UWT) Afisi Kuu ya Zanzibar,walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.7-2-2019.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 7-2-2019.ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa (UWT.)Bi. Thuwaiba Editon Kisasi.(Picha na Ikulu)

KAMATI YA BAJETI YAKUTANA NA WIZARA MBALIMBALI KWA AJILI YA MUSWADA MPYA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupokea na kujadili muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali Na.2 wa mwaka 2019 hii leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge.
 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupokea na kujadili muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali Na.2 wa mwaka 2019 hii leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati), akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti katika ilipokutana na Waziri huyo, Waziri wa Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kupokea na kujadili muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali Na.2 wa mwaka 2019 hii leo katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma. Picha na Ofisi ya Bunge.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA VIONGOZI CHAMA CHA WAMILIKI WA MAKAMPUNI YA KITALII TANZANIA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na viongozi kutoka Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania walipomtembelea leo tarehe 7 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Mjumbe Bodi ya wadhamini Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania, Ndg. Merywn Nunes (katikati) walipomtembelea leo tarehe 7 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania, Ndg. Henry kimambo
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa tatu kushoto) akimsikiliza Mhe. Immaculate Semesi (aliesimama) wakati walipokutana na viongozi Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania leo tarehe 7 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) katika picha ya pamoja na Mjumbe Bodi ya wadhamini Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania, Ndg. Merywn Nunes alipomtembelea leo tarehe 7 Februari, 2019 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Chama cha wamiliki wa Makampuni ya kitalii Tanzania walipomtembelea leo tarehe 7 Februari, 2019 ofisini kwke Bungeni Jijini Dodoma.

(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

TAARIFA KWA UMMA: UBADILISHAJI PESA ZA KIGENI

Fundi magari Tabata akabidhiwa bodaboda yake kutoka biko

$
0
0
Fundi magari mwenye maskani yake Tabata jijini Dar es Salaam, Saimon Mushi, amekabidhiwa bodaboda yake aliyoshinda jana kwenye droo kubwa ya Jumatamu Jenga, huku akishinda sambamba na wenzake watano kutoka kwenye bahati nasibu hiyo, ambapo washindi wawili waliibuka na bodaboda na sh milioni moja huku wengine wanne wakishinda mamilioni ya wapendanao.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mratibu Msaidizi wa Matukio wa Biko Hassan Ahmed.Akizungumza katika makabidhiano hayo, fundi huyo aliishukuru Biko kwa kumkabidhi bodaboda yake akisema kuwa itamsaidia kwa kiasi kikubwa katika maisha yake kwa namna moja aka nyingine.

Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.
 Mshindi wa bodaboda na sh milioni moja kutoka bahati nasibu ya Biko wa droo ya 179, Saimon Mushi wa Tabata jijini Dar es Salaam, akipokea bodaboda yake aliyoshinda kwenye droo kubwa iliyofanyika Jumatano, maarufu kama Jumatano Jenga ambapo washindi sita walipatikana wakiwamo wa mamilioni na wawili wa bodaboda. Makabidhiano hayo yameongozwa na Mratibu Msaidizi wa matukio wa biko Hassan Ahmed. Picha na Mpigapicha Wetu.
 
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images