Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WAZIRI BITEKO AKUTANA NA WATUMISHI TUME YA MADINI

$
0
0
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akisikiliza mapendekezo mbalimbali yaliyokuwa yanawasilishwa na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akifafanua jambo katika kikao hicho.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akiwatambulisha viongozi wa Tume ya Madini pamoja na wafanyakazi.
Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Waziri wa Madini, Doto Biteko na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula wakifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wafanyakazi wa Tume.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizugumza na watumishi wa Tume ya Madini (hawapo pichani).
Watumishi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)
Watumishi wa Tume ya Madini wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani)


Waziri wa Madini, Doto Biteko leo tarehe 06 Februari, 2019 amekutana na watendaji na watumishi wa Tume ya Madini katika makao makuu ya Tume yaliyopo jijini Dodoma, lengo likiwa ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Tume. 

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kutoka Wizara ya Madini, Issa Nchasi na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula. 

Wengine ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya, Wakurugenzi, Mameneja pamoja na watumishi wa Tume ya Madini. 

Katika kikao hicho Waziri Biteko ametoa maelekezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya ukaguzi wa madini ya ujenzi kufufuliwa, kikao cha kamati tendaji kukutana mara kwa mara kwa ajili ya kupitia na kuidhinisha maombi mbalimbali ya leseni za madini na watumishi kufanya kazi kwa uadilifu.

MAMBO YA SOKO LA KIMATAIFA LA SAMAKI LA FERI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Wafanyabiashara wa Samaki katika soko la Samaki la kimataifa Feri wakiendelea na shughuli zao mbalimbali katika soko hilo leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG).
 Mchuuzi wa Samaki wa soko la Samaki feri akimkata kata samaki aina ya Songoro kwa ajili ya kupeleka mtaani kuuzwa.
 Wajasilimali katika Soko kuu la samaki  la kimataifa Feri jijini Dar es Salaam  wakitayarisha Samaki kwa lengo la kuwauza kwa wateja  mbalimbali watakao fika katika soko hilo.
 Wafanyabiashara wa Samaki wa soko la Samaki la kimataifa Feri wakipara Samaki 

Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwaonyesha jengo la TAMISEMI (halipo pichani) wakati wa ziara yake na Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi kuwaonyesha mfano bora wa matumizi ya Force Account
Muonekano wa Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwasili katika jengo la TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa kuwaonyesha Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi mfano bora wa matumizi ya Force Account.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akielezea namna jengo la TAMISEMI litakavyokuwa wakati wa ziara yake na Makatibu Tawala, Wenyeviti wa halmashauri na Wakurugenzi kuwaonyesha mfano bora wa matumizi ya Force Account.

Majid Abdulkarim 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameonyesha matumizi bora ya utekelezaji wa miradi bila kutumia mkandarasi maarufu kama ‘Force Account ‘ kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ,Wenye viti wa Halmashauri, Wakurungezi na Maafisa mipango wa Halmashauri kwa kuwapeleka kwenye mradi wa Ofisi za Jengo la Ofisi ya Rais TAMISEMI linaloendelea kujengwa katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. 

Jafo amefanya ziara hiyo baada ya kikao chake cha maelekezo kwa viongozi hao ambao halmashauri zao zilifaulu vigezo na kusaini fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati awamu ya Pili. 

Akizungumzia Force Account Jafo alisema kuwa nimeamua kutekeleza kwa vitendo yale ninayowaagizaga wakati wote wa maelekezo yangu kuhusu kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yenu. 

Katika ujenzi wa Jengo hili la Ofisi za Wizara tuliamua na kukubaliana kwa pamoja kutumia mfumo ule ule ambao unatumika katika halmashauri zetu sio sisi tunatoa tu maagizo lakin hatutendi na sasa kupitia mradi huu tumeamua kuwa mfano halisi wa yale tunayoyazungumza alisema Jafo. 

Aliongeza kuwa katika mfumo huu wa force Account tumeweza kusimamia jengo hili kupitia kamati nne ambazo ni Kamati ya manunuzi, Kamati ya Vifaa, Kamati ya ujenzi na ile ya usimamizi na ufuatiliaji. 

“Mradi huu umekuwa na tija pia kwa jamii kwani umetengeneza ajira kwa vijana wetu kwani wao ndo wamekua nguvu katika kufanya shughuli zote za ujenzi kuendelea kwa mujibu wa maelekzo ya wahandishi ambao wanatokea Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na msimamizi wa mradi huu”Amesema Jafo 

Wakati huo huo Jafo aliongeza kuwa ujenzi wa Jengo hili la kisasa zaidi linagharimu shilingi billion moja tu Fedha zilizo tolewa na Rais Magufuli kwa kila Wizara kwa ajili ya kujenga Ofisi katika Mji wa Serikali Ihumwa. 

“Nataka niwahakikishie kuwa ujenzi wa jengo hilo umeratibiwa na mimi mwenyewe Waziri wa TAMISEMI ambapo niliwaunganisha viongozi wote wakuu wa Wizara pamoja na watendaji wa Wizara ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka” 

Sasa kama mimi nimeweza wewe kwanini ushindwe na jengo hili limeanza kujengwa mwezi Disemba 2018 na kama mnavyoona sasa hivi jengo limeshafikia hatua ya mtamba wa panya kwahiyo kasi ya ujenzi iko vizuri sana na tutamaliza ujenzi huu ndani ya muda mfupi ujao; Nataka na nyie mkafanye hivi kwenye maeneo yenu alimalizia Jafo. 

Kwa kuongezea Jafo amazitaka halmashauri zilizo pata fedha ya kutekeleza miradi ya Kimkakati kuanza mipango ya utekelezaji wa miradi hiyo mapema iwezekanavyo ili fedha hizo zitakapo wasili katika halmashauri hizo miradi ianze mara moja na ili iweze kumalizika kwa wakati ulopangwa. 

Aidha naye Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Eng.. Zenah Saidi ametoa shukrani za dhati kwa Mhe.Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa fedha hizo na kuhaidi kusimamia kwa umakini na kuhakikisha zinatekeleza miradi huska kwa ufasa na ubora wa miradi hiyo kuendana na thamani ya fedha hiyo. 

“Ni toe wito kwa viongozi wa halmashauri kuwa sasa ni wakati wa kutekeleza miradi hii kwa kutumia mfumo wa Force Account kwani kila mmoja wetu kapata kushuhudia kwa macho yake namna ya mfumo huu unavyo tumika na faida zake kazieleza Bi.Zenah 

Kwa kuhitimisha Bi.Zena amewataka viongozi wenzake kuwa makini wakati wa kutafuta wakandarasi wa kutekeleza miradi kwa wengi wao katika makaratasi wanakuwa vizuri lakini katika utekelezaji hakuna kitu. 

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI FEBRUALI 7, 2019

Waziri Lukuvi Akata Mzizi wa Fitna Suala la Kufuta Mashamba

WAZIRI MPINA ATOA MAAGIZO MAZITO

$
0
0

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina 



Na John Mapepele, Mpwapwa

WAZIRI waMifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amemuagiza Mkurugenzi waUtafiti, Mafunzo na Ugani kuandaa haraka kanuni na mwongozo utakaosimamia kuanzia uvunaji wa mbegu, uuzaji, usambazaji na uhimilishaji na uhamilisha mifugo kabla ya mwezi Machi mwaka huu ili kuwadhibiti madalali wote wanaokwenda kuwaumiza wananchi kwakutumia kivuli cha Serikali. 

Akizungumza mara baada ya kutembelea Mradi wa uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya viinitete na uhawilishaji (MOET) unaotekelezwa na TaasisiyaUtafitiwaMifugo (TALIRI) Kituo cha Mpwampwa mkoani Dodoma, Waziri Mpina alisema watanzania wajivunie mradi huo ambao niwa kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati. 

Alisema kupatikana kwa teknolojiaya MOET kumeiwezesha Tanzania kuwa na njia tatu za kuboresha Koosafu ya mifugoa mbapo ni njia ya asili ya kutumia madume bora, uhimilishaji (AI) na Uhamilishaji (MOET) ambapo itachochea mageuzi makubwa ya uboreshaji wakoosafu ya mifugo ambayo itaongeza uzalishaji wa maziwa, nyama, ngozi na mazao mengine ya mifugo. 

Aidha aliagiza kuwa kila ifikapo mwezi Machi ya kila mwaka idara yake iwe imepeleka ajenda za kufanyiwa utafiti kwenye Taasisi ya Utafiti wa Mifugo ili kupata matokeo ya tafiti ambazo watanzania wanaumiza vichwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili na kuweka utaratibu wakupokea tafiti kutoka nje ya nchi.

Pia amemwagiza Mkurugenzi huyo waUtafiti, Mafunzo na Ugani kukutana na wazalishajiwamayai, vifaranga, ng’ombe, kuku, mbuzi, kondoo, punda, nguruwe, viwanda vya nyama, ngozi na maziwa ili kujua mahitaji yao kwasasa ni yepi kwani waondio wataotengeneza ajenda za utafiti zenye uhitaji kwasasa. 

Amekosoa mfumo wa uendeshaji wa tafiti za mifugo nchini kwakutokuwa na ajenda mahususi zinazohitajika kufanyiwa tafiti badala yake watafiti wengi wamekuwa wakiendesha tafiti za biashara kwa mataifa mengine ambazo hazina msaada kwa watanzania. 

Amesema mfumo wakuibua ajenda za utafiti haufahamiki huku kukiwa na ushirikishwaji dhaifu wa wadau hali inayosababisha tafiti nyingi kushindwa kutoa majawabu ya matatizo katika sekta ya mifugo nchini huku matokeo na mazao yatafiti hizo yakiwafikia watu wachache kinyume na malengoyaSerikali. 

Waziri Mpina alisema pamoja na kuwepo kwa njia zote hizo za uboreshaji Koosafu za mifugo bado kuna kasoro nyingi katika utaratibu unaotumika kuzalisha, kununua, kusambaza na kupandisha mifugo halii nayopelekea zoezi kuwa la kusuasua. 

Alisema pamoja na mbegu hizo kuzalishwa na Serikali na kuuzwamrijammojakwash 3,000 lakini kutokana na kutokuwepo mfumo madhubuti wa usimamizi na kuachiwa wafanyabiashara binafsi kwenda kuwauzia wafugaji katiyash 20,000 hadish 60,000 kwa mrija jambo linawakatisha tamaa wafugaji na kutofikiwa malengo ya Serikali. 

Hivyo Waziri Mpina alisema juhudi zote zinazofanywa na Serikali za kuzalisha mbegu bora katika vituo vyake vya NAIC Arusha na Taliri Mpwapwa haitakuwa na maana kama kasoro zilizopo sasa hazitaondolewa. 

Kwa upande wake MkurungeziwaUtafiti, Mafunzo na UganiwaWizarayaMifugo na Uvuvi, Dk. Angello Mwila waalimhakikishia Waziri Mpina kuwa atasimamia kikamilifu utekelezaji wa maagizo yake ili kuhakikisha wafugaji wananufaika na jitihadahizozinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika mkakati wake wauboreshaji wa koosafu ya mifugo nchini. 

Naye Mkurungezi Mkuu wa TARILI, Dk. Eligy Shirima alisema mradi huo wa MOET unafadhili na COSTECH kwa gharama ya sh milioni 400 kwa ajili ya kununua vifaa vitakavyowezesha kukamua mbegu za dume na kuziweka kwenye jike maalum lililoandaliwa. 

Dk Shirima alisema jike hilo baada ya kuwekewa hormones husaidia mayai mengi kuiva kwa maramoja na kurutubishwa ambapo mbegu zilizorutubishwa hunyonywa na kuhifadhiwa na kisha kusambazwa kwa wafugaji kwaajili ya uhamilishaji hatua ambayo itawezesha kupatika namifugo bora. 

KKKT MERU YAWEKA BARAKA UJENZI WA MADARASA

$
0
0

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Baba Elias Kitoi Nassari amepongeza kampeni ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa inayofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Cornel Muro ambapo amesema kanisa mbali na kupongeza linaunga mkono jitihada hizo.

Askofu Nassari amezungumza hayo jana Februari 6/2019 alipomtembelea Mkuu wa wilaya ya Arumeru ofisini kwake kwa lengo la kumpongeza kwa kazi Kubwa anayoifanya katika sekta ya Elimu na Afya huku akiwa ameambatana na Uongozi Mkuu wa kanisa Dayosisi ya Meru akiwepo Mchungaji Ndelekwa Kuvavanael Pallangyo Msaidizi wa Askofu, Ndugu Lazaro Andrew Katibu Mkuu wa Dayosisi na Ndugu Elisate Manyaeli Maturo Mtunza Hazina Wote ni kutoka KKKT Dayosisi ya Meru

Katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Baba Askofu Nassari amemkabidhi Lori lililoleta shehena ya mifuko ya saruji Kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika halmashauri ya Meru.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro mbali na kupokea pongezi na salamu za Kanisa, ameshukuru msaada wa shehena ya mifuko ya saruji iliyotolewa na kanisa, ambapo amemuhakikisha Baba Askofu Nassari kuwa Serikali ya wilaya ya Arumeru itaendelea kushirikiana na kanisa katika sekta zote za utoaji wa huduma Kwa wananchi.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Mh.Jerry Cornel akimshukuru Askofu Nassari kwa mchango alioutoa katika kuunga mkono kampeni ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa aliyekuwa sambamba na Uongozi Mkuu wa kanisa Dayosisi ya Meru akiwepo Mchungaji Ndelekwa Kuvavanael Pallangyo Msaidizi wa Askofu, Ndugu Lazaro Andrew Katibu Mkuu wa Dayosisi na Ndugu Elisate Manyaeli Maturo Mtunza Hazina Wote ni kutoka KKKT Dayosisi ya Meru

Askofu Nassari akimpongeza Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Mh.Jerry Cornel Muro ofisini kwake kwa kazi Kubwa anayoifanya katika sekta ya Elimu na Afya huku akiwa ameambatana na Uongozi Mkuu wa kanisa Dayosisi ya Meru akiwepo Mchungaji Ndelekwa Kuvavanael Pallangyo Msaidizi wa Askofu, Ndugu Lazaro Andrew Katibu Mkuu wa Dayosisi na Ndugu Elisate Manyaeli Maturo Mtunza Hazina Wote ni kutoka KKKT Dayosisi ya Meru
Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Mh.Jerry Cornel akimshukuru Askofu Nassari kwa mchango alioutoa katika kuunga mkono kampeni ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa

TAARIFA


DC NAMTUMBO AIOMBA MAHAKAMA KUTOA HUDUMA KIZALENDO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ameiomba mahakama kutoa huduma ya sheria kwa wananchi kizalendo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Sheria wilayani humo jana katika uwanja wa Taifa mjini Namtumbo Mkuu wa wilaya huyo aliwataka wanasheria kutenda haki katika kuzingatia uzalendo katika nchi yao.

Aidha Mkuu wa wilaya huyo alidai yapo malalamiko machache kuhusu kukilalamikia chombo hicho cha mahakama katika ofisi yake hali inayoonesha sehemu kubwa ya chombo hicho kinatenda haki alisema mkuu wa wilaya huyo.

Hata hivyo aliwataka wananchi wilayani hapa kukitumia chombo hicho cha mahakama kuwafikisha wahalifu wanaoweka mimba wanafunzi badala ya wazazi kuendesha mashauri ya mimba majumbani na kumaliziana kinyumbani huku wanafunzi wa kike wakikosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wilaya ya Namtumbo Bi. Gloria Lwomile alimwambia Mkuu wa wilaya changamoto ya kucheleweshwa kwa upelelezi kutoka jeshi la polisi husababisha kesi nyingi kuchukua muda mrefu pamoja na changamoto ya uchache wa watumishi wa mahakama wilayani humo.

Lwomile alidai mahitaji ya watumishi wilayani humo ni mahakimu 2 katika mahakama ya mwanzo na aliopo ni mmoja na pia katika mahakama ya wilaya mahitaji ya mahakimu ni watumishi 9 na waliopo ni watumishi 7.

Iddi Chowo mkazi wa Namtumbo alisema maadhimisho ya siku ya sheria yameweza kumwongezea ufahamu hasa katika swala la kumwekea mtu dhamana haihitajiki kutoa fedha bali kinachohitajika ni kukamilisha taratibu za kumwekea mtu dhamana alisema bwana chowo.

Kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria wilayani Namtumbo yalifanyika katika kiwanja cha Taifa mjini Namtumbo ambapo awali yalitanguliwa na utoaji elimu kwa wananchi kuhusu kufahamu mambo ya sheria.

 Picha ya kwanza inaonesha Mkuu wa wilaya Namtumbo akiwa katika picha ya pamoja na wanasheria mara baada ya kumaliza kuadhimisha siku ya sheria wilayani Namtumbo ambapo waliaswa kutumia taaluma zao kutenda haki kwa wananchi.

RC MAKONDA AONGOZA MSAFARA WA WASANII NA WAANDISHI WA HABARI KUTEMBELEA MRADI WA SGR.

$
0
0

MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli (TRC)Bw. Masanja Kadogosa wakati alipowasili tayari kwa kuongoza wasanii na waandishi wa habari kwa ajili ya kutembelea na kujionea namna shughuli za ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme Starndard Gauge Railway (SGR) kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro unavyoendelea, ambapo treni hiyo imeondoka leo na wasanii wa fani mbalimbali pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE)
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza jambo kabla ya kukagua mradi huo eneo la kamata na kisha kuanza safari na waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Reli (TRC) Bw. Masanja Kadogosa. 
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akifanya ukaguzi mdogo wamradi huo eneo la kamata kabla ya kuondoka na msafara huo kushoto ni Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa na kulia ni Steve Nyerere Mratibu wa ziara hiyo. 
MKuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TRC Bw. Masanja Kadogosa wakati akifanya ukaguzi mdogo wa mradi huo eneo la Kamata kabla ya kuondoka na msafara huo kushoto ni Steve Nyerere Mratibu wa ziara hiyo. 
Mafundi wa kampuni ya Yapi Merkezi wakiendelea na kazi ya kujenga nguzo. 
Meneja wa WCB Babu Tale na Promota wa ngumi Bw. Kaike ni miongoni mwa watu waliojiambatana na wasanii wengine katika ziara hiyo 
Wasanii Peter Msechu na Mrisho Mpoto wakiwa katika ziara hiyo pia. 
Picha zikionyesha wasanii mbalimbai ambao wapo katika ziara hiyo kabla ya kupanda treni na kuanza safari ya kwenda Morogoro. 

Vodacom, CCBRT waungana kutokomeza fistula.

$
0
0
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (wa pili kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi. 
Mkurugenzi wa Vodacom Foundation Tanzania, Bi Rosalynn Mworia (kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. Wa kwanza kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi. 
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia (kulia) akisalimiana na baadhi ya wagonjwa wanaopata matibabu ya Fistula mara baada ya kuwasili kwenye Hospitali ya CCBRT wakati wa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Taasisi ya Vodacom Foundation Tanzania kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. 



Katika kuunga mkono na kuongeza nguvu juhudi za kutokomeza fistula nchini, Taasisi ya Vodacom Tanzania Faundation kwa kushirikiana na hospitali ya CCBRT wametoa mafunzo ya kuwatambua wanawake wenye Fistula na kuwawezesha kufika hospitali kupata matibabu kwa kutumia mfumo wa Vodacom M-Pesa kwa mabalozi wapya 50. M-Pesa inatumika kuwatumia waathirika pesa ambazo zinakidhi mahitaji yao na usafiri mpaka kufika CCBRT au hospitali washirika kupata matibabu. 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wafanyakazi wa vituo vya afya na wadau mbalimbali kutoka ofisi za serikali. Programu hii ya “Fistula inatibika” ilianza mwaka 2012 na imelenga kuwasaidia wanawake wanaoishi na hali ya fistula kupata matibabu ya kiafya na kisaikolojia kwa sababu wengi wao hutengwa na jamii zinazowazunguka kutokana na ugonjwa huo, pamoja na kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida na kujumuika kwenye jamii zao. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Bi Rosalynn Mworia alisema, “Mabalozi hawa wanaungana na mabalozi wengine zaidi ya 3000 wa fistula waliopo sehemu mbalimbali nchini, wenye uwezo wa kutambua na kuwawezesha waathirika wa Fistula kufika hospitali ya CCBRT au vituo vingine vya afya vinavyotoa matibabu hayo kama; Bugando (Mwanza), KCMC (Kilimanjaro), Nkinga (Tabora), Peramiho Mission Hospital (Ruvuma), Kabanga Mission Hospital (Kigoma), Songea Regional Hospital (Ruvuma) na Selian (Arusha) kwa kutumia mfumo wa M-Pesa. Nawasihi mabalozi hawa kutoa mafunzo kwa jamii zao kuhusu fistula kwa kuandaa semina ambazo zitaambatana na majadiliano ya changamoto mbali mbali zinazotokana na fistula”. 

Shirika la Afya duniani (WHO) linakadiria kwamba wanawake 3000 hupata tatizo la fistula kila mwaka nchini Tanzania. Hivyo mpango huu ulianzishwa na Vodacom Tanzania Foundation kama sehemu ya kuisaidia serikali kuboresha huduma za afya nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

“Fistula ni hali inayozuilika na kutibika hivyo inabidi tuidhibiti kabisa. Katika karne hii hakuna mwanamke anayestahili kutengwa au kunyanyapaliwa na jamii yake kwa sababu ya fistula. Ninapongeza juhudi za taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation katika kukabiliana na matatizo ya kiafya yatokanayo na uzazi nchini. Tunahitaji kukabiliana na mzigo huu wa akina mama wenye matatizo haya katika jamii zetu,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa hospitali ya CCBRT bi Brenda Msangi. 

Wanawake wenye fistula wana changamoto kubwa ya kutengwa katika jamii zao na wengi wao hawatambui kama hali hii inatibika kutokana na ukosefu wa elimu na taarifa. Utumiaji wa mabalozi wa Fistula ni hatua muhimu zaidi maana wao hutumika katika kuwatambua na kuwapa rufaa wanawake wanoishi na hali ya Fistula 

“Mwaka wa kwanza baada ya kuanza kutumia M-pesa kutoka Vodacom katika mfumo wetu wa rufaa tulishuhudia ongezeko la asilima 65 ya wanawake waliotibiwa ugonjwa wa fistula, kufikia mwaka 2016, asilimia 87 ya wagonjwa wa fistula walipata rufaa kupitia mfumo wa M-Pesa ambao tunashirikiana na Vodacom Tanzania Foundation, wakafanikiwa kufika CCBRT ambapo tulifanya upasuaji wa wagonjwa 1,012”, aliongeza Bi Msangi.

WARSHA YA WADAU KWA AJILI YA KUPITIA RASIMU YA RIPOTI YA HALI YA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU

$
0
0
 Mkurugenzi wa Mazingira wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa William Mwegoha akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua warsha ya Wadau kwa ajili ya kupitia rasimu ya Ripoti ya hali ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu iliyofanyika jijini Dodoma.
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya  Sera na Mipango  kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Paul Sangawe, akisoma hotuba ya ufunguzi wa Warsha hiyo ikiwa anamuwakilisha Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais.  Waliokaa kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa William Mwegoha na kushoto ni Mkurugenz i Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Magdalena Mtenga.
 Sehemu ya Washiriki waliohudhuria Warsha hiyo ya kupitia rasimu ya Ripoti ya Wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wote waliohudhuria Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. 

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA EU NCHINI, MJUMBE MAALUMU WA RAIS WA ZIMBABWE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Charles Stuart aliyemtembelea na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya  mazungumzo na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Charles Stuart aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kuagana na Kaimu Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Charles Stuart aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji, Mazingira na Makazi vijijini wa Zimbabwe na Mjumbe Maalumu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Pretence Shiri alipokutana nan a kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji, Mazingira na Makazi vijijini wa Zimbabwe na Mjumbe Maalumu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Pretence Shiri akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Mhe. Martin Tavenyika alipokutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kuamuaga baada ya mazungumzo  Waziri wa Ardhi, Kilimo, Maji, Mazingira na Makazi vijijini wa Zimbabwe na Mjumbe Maalumu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Pretence Shiri Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 7, 2019. PICHA NA IKULU

WAZIRI MKUU ATOA MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Blog ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majali ametoa msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa mkakati wake ni kuendelea kuhamsisha uwekezaji nchini huku akitoa mwito kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali kwani mazingira ya uwekezaji ni salama.

Ametoa kauli hiyo leo Februari 7 , 2019 Bungeni Mjini Dodoma wakati anajibu maswali ya papo kwa papo ambapo moja ya swali aliloulizwa ilikuwa ni kufahamu msimamo wa Serikali kuhusu wawekezaji nchini ambapo alianza kujibu kwa kueleza kuwa msimamo wa Serikali ni kuendelea kuhamasisha wawakezaji kuwekeza nchini.

"Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli imeendelea kuwahamasisha wawakezaji wakiwamo wa nje kuja kuwekeza nchini na ndio maana mazingira mazuri ya uwekezaji yamekuwa yakiandaliwa nchini kwetu.Hivyo msimamo wa Serikali ni kuendelea kuwahamasisha wawakezaji waje kuwekeza.

"Mazingira ya kuwekeza katika nchi yetu ni mazuri na yako salama salama sana.Tutanaahidi tutaendelea kulinda wawekezaji mbalimbali ambao wamewekeza nchini wakiwamo waliwekeza kwa kujenga viwanda ndani ya nchi yetu,"amesema .

Waziri Mkuu huku akisisitiza jukumu la Serikali ni kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji.Wakati huo huo Waziri Mkuu aliulizwa ni hatua gani ambazo Serikali inachukua katika kuboresha mazingira ya biashara nchini, ambapo amejibu kuwa zipo hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa kuhakikisha mazingira ya ufanyaji biashara unakuwa rafikia.

Amefafanua hata uamuzi wa Rais Dk.John Magufuli kugawa vitambulisho kwa ajili ya wafayabiashara wadogowadogo ni mkakati wa kuendelea kuweka mazingira mazuri ya wananchi kufanya biashara bila kusumbuliwa."Kama nilivyojibu kuhusu mazingira ya uwekezaji yaliyopo nchini, ndivyo ambavyo Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara.Kuna mambo mengi yamekuwa yakifanyika kuboresha mazingira ya biashara nchini kwetu,"amesema Waziri Mkuu.

ACB WAJIZATITI KUWAINUA KIUCHUMI WAJASILIAMALI WADOGO NA WA KATI KWA MWAKA 2019

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya Akiba Commercial (ACB)   imejizatiti katika kuwainua wajasiliamali wadogo na wa kati (MSMEs) kwa kuwapatia mikopo nafuu na ya muda mrefu.

Hayo yalisemwa wakati benki hiyo wakitangaza matokeo mazuri ya fedha ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax ya Bilion 1.2 ikwia ni katika ukuaji wa asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017.

Akizumgumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Augustine Akowuah amesema anafarijika na matokeo hayo ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwani mizania ya malengo yao kuanzia mwaka yamesababisha kuwa na muelekeo mzuri wakati wakifungua mwaka.

Amesema kuwa, wamefurahi hatua hiyo kwa kuwa mikakati mingi waliyojiwekea imeleta mabadiliko kwenye benki yao kwa muda mrefu japokuwa hali haikuwa nzuri mwanzoni mwa mwaka.

"Katika kipindi cha mwaka 2018, ilitelekeza mikakati ya kupunguza mikopo chechefu, kuimarisha makusanyo ya madeni sugu na utoaji wa mikopo mipya kwa kuzingatia ubora, hatua tulizochukua ikiwemo kunadilisha na kupitia majukumu ya kazi zililenga zaidi kwenye kuimarisha hatari zinazotokana na ukopeshaji,"amesema Akowuah. 

Afisa Biashara wa ACB, Felician Girambo amesema kuwa benki hiyo kwa mwaka huu 2019 wamejizatiti kuendelea na matokeo chanya kwani wamelenga kujena maendeleo chanya yaliyopatikana kwa mwaka 2018 ikiwemo jukumu pelee la kusaidia wajasiriamali wadogo na waka kati (MSMEs) nchini Tanzania kwa kutumia huduma bora za kifedha.

Girambo amesema mjasiriamali yoyote mwenye leseni ya biashara ana uwezo wa kupata mkopo hata kama hatakuwa na akaunti katika benki yao ila itamlazimu afungue kwa wakati huo, pia amesema mjasiriamali itamtaka awe na msingi utakaokuwa mara ya mbili ya mkopo anaohuitaji kwa wakati huo.

Ameongezea kuwa, kwa mwaka 2019 wamedhamiria kufikia lengo la kuwapatia mikopo wajasiriamali  12,000 kwa mwaka mzima na mikopo yao inarejeshwa kulingana na aina ya mkopo uliochukua.

Benki hiyo inajumla ya miaka 20 toka kuanzishwa kwake na ina matawi 18 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Mbeya, Moshi na Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji Benki  ya Akiba Commercial (ACB) Augustine Akowuah akizungumzia matokeo mazuri ya fedha ya nusu ya pili ya mwaka 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax ya Bilion 1.2 ikwia ni katika ukuaji wa asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2017.
Afisa Biashara wa Benki ya Akiba Commercial (ACB)
, Felician Girambo akizungumzia mikopo kwa 
 wajasiriamali wadogo na waka kati (MSMEs) nchini Tanzania kwa kutumia huduma bora za kifedha.
Meneja Mkuu Kitengo cha Fedha wa Benki ya Akiba Commercial (ACB) Bertha Simon akielezea mikakati waliyojiwekea katika mwaka 2019 ya kuhakikishia wanafikia malengo yao.


ZAIDI YA SH. BIL. 500 ZIMELIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema zaidi ya sh. bilioni 500 zimelipwa kwa wakulima wa korosho kati ya sh. bilioni 700 zinazotarajiwa na kwamba malipo hayo bado yanaendelea kulipwa kwa wakulima wengine waliosalia.

Amesema tamko la Rais Dkt. John Magufuli la kwamba Serikali itanunua korosho kwa bei ya sh. 3,300 ni kwa ajili ya korosho za daraja la kwanza  na bei ya korosho za daraja la pili ni asilimia 80 ya zile za daraja la kwanza.

Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Alhamisi, Februari 7, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka.

Mbunge huyo alitaka kupata kauli ya Serikali kuhusu malipo kwa wakulima wa korosho ambao walikuwa wakilipwa sh. 2,600 kwa kilo wakati Rais Dkt.  Magufuli alisema Serikali itanunua kilo moja ya korosho kwa sh. 3,300.

“Malipo yanaendelea na sehemu kubwa ni kwa wakulima wenye kilo zaidi ya 1,500, Serikali itanunua korosho zote kama ilivyoelezwa. Taratibu zinazofanyika ni kuhakikisha anayelipwa ni muhusika. Wananchi endeleeni kuiamini Serikali yenu.”

Waziri Mkuu amesema ilikuwa ni lazima kwa Serikali ifanye uhakiki kwa wakulima hususani wale wenye kilo zaidi ya 1,500 ili kujiridhisha kama ni wakulima, hivyo baada ya kuhakikiwa wakulima wote watalipwa fedha zao.

Amesema Januari 27, 2019 alitoa maagizo kwa Wizara ya Kilimo pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wahakikishe hadi Februari 15 mwaka huu wawe wamekamilisha zoezi la uhakiki na kuwalipa wakulima wote wa zao la korosho.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wadau wa zao la korosho kwenye kikao kilichofanyika mkoani Mtwara, lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupata taarifa juu ya mwenendo mzima wa bidhaa hiyo kwa msimu wa mwaka 2018/2019.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema Serikali haijakiuka sheria kuhusu suala la watumishi kupandishwa mishahara na kwamba ina nia njema ya kuhakikisha wanalipwa mishahara na posho nzuri.

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbozi, Pascal Haonga aliyedai Serikali imekiuka sheria ya utumishi kwa kutopandisha mishahara, ambapo Waziri Mkuu amesema  Serikali haikukiuka sheria, bali iliamua kushughulikia suala hilo kwa kuanza na uhakiki wa watumishi.

Waziri Mkuu amesema baada ya kufanya uhakiki na kubaini uwepo kwa watumishi hewa pamoja na waliokuwa wakitumia vyeti vya kugushi, iliwaondoa na sasa Bodi ya Mishahara na Maslahi ya Watumishi wa Umma inafanya mapitio ya mishahara baada ya kubaini tofauti, hivyo watumishi waendelee kuwa watulivu.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA.
ALHAMISI, FEBRUARI 7, 2019.






Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali kutoka Mbunge wa Mchinga, Hamidu Hassan Bobali ambaye aliuliza swali katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji , Angela Kairuki baada ya kujibu vizuri sana maswali ya papo kwa papo, Bungeni jijini Dodoma, Februari 7, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE 'AIBANA' SERIKALI NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA ,WAZIRI MKUU ATOA MAJIBU

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amelihakikishia Bunge kuwa Serikali inayo nia njema kwa watumishi wote wa umma kwa kuhakikisha wanapata mishahara yao na stahiki zote ambazo wanastahili kulipwa na kwamba mchakato uliopo sasa ni kuangalia kwa kina namna ya kuboresha maslahi yao.

Akijibu swali bungeni leo Februari 7, 2019 , Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imekuwa na mipango mbalimbali na kwamba nia ya Serikali ni njema kwa kuhakikisha watumishi wanalipwa stahiki zao kwa wakati.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya moja ya wabunge kutaka kufahamu ni lini Serikali itaongeza mishahara ya watumishi ambayo ni haki yao kisheria na si takwa la mtu.Hivyo wakati anajibu swali hilo ametumia nafasi hiyo kufafanua dhamira ya Serikali kwa watumishi wa umma ambapo pamoja na mambo mengine ameleeza wazi kila mtumishi lazima apate stahiki yake.

Pia amesema kabla ya kupandishi mishahara kumukuwepo na hatua mbalimbali ambazo zinazchukuliwa na baadhi ya hatua hizo ni kufanya uhakiki wa watumishi baada ya kubainika uwepo wa watumishi hewa ambao walikuwa wanalipwa mishahara na posho.Ameongeza hatua ya pili ikawa ni kuhakiki vyeti na baada mchakato huo Serikali ikawa inalipa na madeni.

"Kuna hatua mbalimbali ambazo Serikali imechukua katika kuhakikisha mishara inakwenda kwa watu wanaostahili.Pia kwa sasa kuna tume ambayo inaendelea kufuatilia mishahara kati ya kada moja na nyingine ambayo hiyo itatoa picha halisi ya viwango vya mishahara kulingana na kazi ambayo inafanywa eneo husika.

"Kumekuwa na toauti kubwa ya mshahara wakati mfanyakazi wa eneo husika amesoma chuo kikuu kimoja na mwingine lakini linapokuja suala la mshahara tofauti inakuwa kubwa.Hivyo yote hayo tume hiyo inaangalia na kisha itakuja na mapandekezo kuhusu viwango vya ishahara.Niwahakikishie wabunge na Watanzania nia ya Serikali ni njema,"amesema Waziri Mkuu.

LEMUTUZ AWAJIA JUU WANAOICHAFUA EQUITY BANK

$
0
0
The Art of FACTS mimi ni mteja wa Equity Bank I was shocked last week kuona habari za kuichafua my Bank ambayo kabla ya kufungua my account tayari nilishafanya utafiti wa kutosha na kuijua vizuri bank hii ambayo wala sio siri kwa maoni yangu ndiyo THE BEST BANK nchini so far ambayo ilianzishwa Mwaka 2012 na kwa sasa ina Branches 15 Tanzania nzima pamoja na Zanzibar na tayari wanazo ATM’s 21 wakiwa na nia ya kubadilisha maisha ya Wananchi wa kawaida kiuchumi kwa kuwapatia huduma bora na fursa. 

 Equity Bank Limited Tanzania ni part of Equity Group Holdings Plc iliyoanzishwa Mwaka 1984 kutokea Kenya na Mkurugenzi wake wa kwanza akiwa Dr. James Mwangi na leo Equity ipo Africa nzima na inaongoza masoko ya nchi za Kenya, Uganda na Rwanda, Congo-DRC, South Sudan. Bank hii ina wateja Millioni 21.8 na mtaji wa jumla ya Dola za Kimarekani USD 5.7 Billioni, kwa ujumla wake ni Bank ambayo inashika nafasi ya 11 Duniani kwa Matokeo na Mali ilizonazo. 

 Mwaka uliopita ilishinda zawadi ya “African Bank of the Year” na Mkurugenzi wake Mkuu Dr. James Mwangi ameshinda pia zawadi ya “African Banker of the Year 2018”. Sasa kwahayo machache naomba kuwakumbusha wale wote wanaohangaika kuichafua Bank hii kwamba mmepotea sana ushindani wa bank ufanyike kwa kazi na sio kuchafuana mitandaoni cause binafsi siwezi kunyamaza kuona Bank yangu inachafuliwa kwa sababu za kiushindani wa kibiashara …

I salute you Equity Bank endeleeni kusaidia Wajasiriamali wanyonge nchini kwa mikopo yenye riba nafuu na pia endeleeni kutusaidia hata sisi wajasiriamali wadogo wadogo kwa mikopo nafuu ..haya makelele ya Social Media niachieni mimi hahahahaha U know …MUNGU AIBARIKI TANZANIA! AMEN! – @ lemutuz_superbrand

SAFARI YA WASANII KUANGALIA UJENZI WA RELI YA KISASA RAHA TUPU...SOMA ALICHOSEMA JB

$
0
0

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SAFARI ya treni ya wasanii mbalimbali imenoga!Hicho ndicho ambacho unaweza kukizungumzia baada ya wasanii hao zaidi ya 300 kupata fursa ya kupanda treni kwa lengo la kuhakikisha wanashuhudia ujenzi wa reli ya kisasa ambayo itatumia umeme (SGR).

Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dk.John Magufuli ambapo reli hiyo pamoja na mambo mengine itasaidia kuinua uchumi wa nchi yetu.

Wasanii hao wameondoka jijini Dar es Salaam leo Februari 7,2019, saa tatu asubuhi kuelekea mkoani Morogoro ambapo wakiwa katika safari hiyo watashuhudia hatua mbalimbali za mbalimbali za ujenzi huo.

Wakizungumzia safari hiyo leo kwa nyakati tofauti wasanii hao kila mmoja ameelezea furaha aliyonayo na hasa kuwa sehemu ya watanzania waliobahatika kushuhudia ujenzi wa reli hiyo ya kisasa.Kiongozi wa msafara huo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Staa wa filamu nchini katika tasnia ya 'Bongo Muvi' Steven Jacob a.k.a Jay B amesema kuwa anajisikia fahari kusafiri na treni ya ndani kwenda kushuhudia ujenzi wa reli ya kisasa. "Leo ni mara yangu ya kwanza kupanda usafiri huu wa treni kwa hapa nyumbani kwetu ila nikiwa China nimewahi kupanda treni inayotumia umeme."

Ameongeza ni matumaini yake kwenye safari hiyo kuna mambo mengi atajifunza na kuwa balozi mzuri wa kuwaambia Watanzania wengine kuhusu ujenzi wa reli hiyo.Wasanii wengine ambao wamezungumzia safari hiyo wamesema wanampongeza Rais Dk.John Magufuli kutokana na jitihada ambazo anafanya katika kuleta maendeleo ya Watanzania.

Kwa upande wake msanii Steven Nyerere wakati anazungumzia safari hiyo ameeleza kuna mambo mengi ambayo yamefanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na hivyo ni vema wasanii wakawa sehemu ya mabalozi kwanza kwa kutembelea miradi hiyo na kisha kuielezea vema.

"Huu ni mwanzo tu, kwani kutokana wingi wa miradi ambayo inafanywa na Serikali chini ya Rais wetu Dk.John Magufuli naamini tutapata fursa ya kushuhudia mradi mmoja baada ya mwingine.Nitumie nafasi hii kutoa pongezi kwa Rais kwa hatua anazochukua katuka kuleta maendeleo nchini kwetu.Wasanii tunaahidi kumuunga mkono kwa kila jambo analofanya kwa maslahi ya Waanzania wote,"amesema Steven Nyerere.

TPSF YAJADILI MAPENDEKEZO SERA YA KODI BAJETI YA 2019/2020

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na Wadau wake kukamilisha zoezi la kukusanya maoni juu ya mapendekezo ya marekebisho ya Kodi kuelekea Bajeti ya 2019/2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye amesema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya msisitizo wa Mhe. Rais kuwa na haja ya kuangalia au kufumua upya mfumo wa Kodi pamoja na Sera yenyewe inayoonekana kuwa mzigo mkubwa kwa Wafanyabiashara.

Simbeye amesema kazi hiyo imeanza tangu Novemba, 2018 , amesema wamekuwa wakikusanya maoni tofauti ili kujadiliana kwa pamoja na kupata maoni hayo yatakayopelekwa Serikalini kwa ajili yakuingia kwenye maboresho ya sera ya Kodi au mfumo wa Kodi nchini.

‘’Sisi kama Sekta Binafsi tunatimiza wajibu wetu kuchangia mawazo namna gani bora ambavyo tunaweza kuweka mfumo wa Kodi ili iwe rahisi kufanya biashara Tanzania nakuweza kukuza Uwekezaji’’, amesema Simbeye.

Kwa upande wake, Mmoja wa Wanachama wa Sekta hiyo, Mwakilishi kutoka Chama cha Waajiri nchini (ATE), Dan Sora Tandasi amesema lengo lakukutana kama Wadau kutilia mkazo kwenye masuala ya Kodi, amesema Wafanyabiashara wanapata fursa kujadili changamoto zao katika Kodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Godfrey Simbeye 
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images