Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Mwacheni Rais afanye kazi/Rais Magufuli anapenda Haki-Mbunge Timotheo Mzava


TAARIFA KWA UMMA- MWONGOZO WA UHAKIKI UONGEZAJI THAMANI MADINI KABLA YA KUSAFIRISHWA NJE YA NCHI

MTAKA AWALIPA WANARIADHA MADENI YAO

$
0
0

WAKATI Tanzania ikielekea kwenye maandalizi ya mbio za dunia za nyika mwaka huu, Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Anthony Mtaka amefanikiwa kutimiza ahadi ya kuwalipa wanariadha wote waliokuwa wana madeni yao kwa shirikisho hilo. 

Wanariadha waliolipwa ni pamoja na wasichana sita waliofanya vizuri kwenye mbio za Dunia za Nyika mwaka 2017 nchini Uganda kiasi cha shilingi milioni 4.8 kwa mgawo wa shilingi laki nane (800,000) kila mmoja fedha zilizokuwa zimetolewa na shirikisho la riadha la dunia (IAAF). 

Wanariadha hao ni pamoja na Failuna Abdi Matanga, Anjelina Daniel Tsere, Magdalena Shauri, Sara Ramadhani, Mayselina Mbua, Siata Kalinga ambao waliibuka washindi wa sita kwa upande wa timu na kuifanya Tanzania kuzawadiwa kiadi cha dola 6000. 

Wengine waliolipwa fedha zao ni wanariadha watatu wa Mbio za dodoma Marathon mwaka 2016, ambao walikuwa wazawadiwe mabati lakini zilipotea chini ya mikono ya uongozi wa RT. 

Wanariadha Gabriel Geay (kwa upande wa wanaume) na Fadhila Salum (Kwa upande wa wanawake) waliokuwa washindi wa pili katika mbio zile alitakiwa kulipwa bati 100 kila mmoja ambapo walifidiwa kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja (1,000,000) huku Catherine Lange aliyeshika namba tatu alikuwa anadai bati 40 alipatiwa kiasi cha shilingi 400,000. 

“Katika kuelekea mashindano mapya ya kimataifa, yaliyoko kwenye kalenda ya Shirikisho tumeona tulipe kwanza madeni yote ya wanariadha waliokuwa wanadai maana naona yanaleta maneno maneno mengi na yanaweza kuwa sio mazuri kwa afya ya mchezo wa riadha,” alisema Mtaka 

Akitoa sababu za wanariadha kucheleweshewa fedha hizo, Mtaka alisema kuwa fedha hizo ziliingizwa na Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) kwenye akaunti isiyo sahihi ya RT, hivyo walilazimika kutoa taarifa wazirudishe kwao na watume tena kwenye akaunti sahihi ya shirikisho hali iliyochukua mda mrefu. 

Akipokea fedha hizo mmoja wanariadha hao Anjelina Tsere alimshukuru Mtaka kwa kutimiza ahadi hiyo ambayo walishaikatia tamaa ya kuipata tena ambapo amesema hali hiyo imerudisha Imani yao kwa shirikisho na kuahidi kufanya vema zaidi mwaka huu. 

“Kwanza nitumie nafasi hii kukushukuru Rais kwa kutimiza ahadi hii maana ilitugharimu sana nguvu zetu hivyo kimya cha mda mrefu cha viongozi wetu ilitufuta kabisa matumaini ya kupata fedha hizi lakini leo tumepata ni jambo jema na imetutia moyo katika mapambano ya kuelekea mashindano ya nyika ya dunia tunaahidi tutafanya vema zaidi” 

Kwa upande wake kocha mwandamizi wa riadha nchini Zacharia Barie alisema kuwa hatua ya shirikisho kulipa madeni hayo yatarahisisha kazi za makocha watakaopata nafasi ya kuwanoa wakiwa kambini na kuwataka wanariadha kulipa fadhila hiyo waliyotendewa huku wakiiamini shirikisho lao.

WAKIMBIZI KUPEWA VITAMBULISHO

$
0
0


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiongozana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillippo Grandi baada ya kumaliza kikao cha ndani ambacho mambo mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillippo Grandi (kushoto) baada ya kumaliza kikao cha ndani ambacho mambo mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Katikati ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Serikali imelitaka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) kusaidia katika utoaji wa vitambulisho kwa wakimbizi wote walioko katika makambi pamoja na kusaidia uanzishwaji wa kanzidata ya wakimbizi nchini itakayomilikiwa na serikali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhnadisi Hamad Masauni wakati akizungumza katika kikao cha ndani na Ujumbe ulioongozwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Fillippo Grandi,ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri Masauni alisema Serikali ya Tanzania imekua na historia ndefu katika jukumu la kuhifadhi wakimbizi wanaokimbia machafuko katika nchi zao lakini wakimbizi hao wanatakiwa kutokua sehemu ya watu wanaovunja sheria pindi wawepo makambini.

“Ni muhimu sasa UNHCR wakasaidiana na serikali katika kuboresha orodha ya wakimbizi walioko nchini sambamba na ugawaji wa vitambulisho kwa wakimbizi watakaothibitika kisheria kuwa ni wakimbizi huku ikisaidia katika kupokea wakimbizi halali na sio wahamiaji haramu” Alisema Masauni

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Fillippo Grandi aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kupokea wakimbizi kwa muda mrefu na akiweka wazi lengo lao la kushirikiana na nchi zinazopokea wakimbizi katika kusimamia zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi wanaotaka kurudi kwao kwa hiyari

“Tutahakikisha tunasimamia wakimbizi kutii sheria za nchi husika ikiwemo uhifadhi wa mazingira katika makambi na kusaidia urejeshwaji wa wakimbizi walio tayari kurejea katika nchi zao baada ya kurejea kwa amani” alisema Filippo

Tanzania inahifadhi zaidi ya wakimbizi Laki Tatu katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli zilizopo mkoani Kigoma.

Wakimbizi kupewa Vitambulisho

$
0
0
Serikali imelitaka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) kusaidia katika utoaji wa vitambulisho kwa  wakimbizi wote walioko katika makambi  pamoja na kusaidia uanzishwaji wa kanzidata ya wakimbizi nchini itakayomilikiwa  na serikali.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhnadisi Hamad Masauni wakati akizungumza katika kikao cha ndani na Ujumbe ulioongozwa na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Fillippo Grandi,ambaye yuko nchini kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri Masauni alisema Serikali ya Tanzania imekua na historia ndefu katika jukumu la kuhifadhi wakimbizi wanaokimbia machafuko katika nchi zao lakini wakimbizi hao wanatakiwa kutokua sehemu ya watu wanaovunja sheria pindi wawepo makambini.

“Ni muhimu sasa UNHCR wakasaidiana na serikali katika kuboresha  orodha ya wakimbizi walioko nchini sambamba na ugawaji wa vitambulisho kwa wakimbizi watakaothibitika kisheria kuwa ni wakimbizi huku ikisaidia katika kupokea wakimbizi halali na sio wahamiaji haramu” Alisema Masauni

Akizungumza katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR) Fillippo Grandi aliishukuru serikali ya Tanzania kwa kupokea wakimbizi kwa muda mrefu na akiweka wazi  lengo lao la kushirikiana  na nchi zinazopokea wakimbizi    katika kusimamia zoezi la urejeshwaji wa wakimbizi wanaotaka kurudi kwao kwa hiyari

“Tutahakikisha tunasimamia wakimbizi kutii sheria za nchi husika  ikiwemo uhifadhi wa mazingira katika makambi na kusaidia urejeshwaji wa wakimbizi walio tayari kurejea katika nchi zao baada ya kurejea kwa amani” alisema Filippo

Tanzania inahifadhi zaidi ya wakimbizi Laki Tatu katika kambi za Nyarugusu, Nduta na Mtendeli zilizopo mkoani Kigoma.  
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akiongozana na   Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillippo Grandi baada ya kumaliza kikao cha ndani ambacho mambo mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Kulia  ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na    Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) Fillippo Grandi (kushoto) baada ya kumaliza kikao cha ndani ambacho mambo mbalimbali kuhusiana na wakimbizi yalijadiliwa. Katikati   ni Katibu wa Naibu Waziri, George Mwansasu.Kikao hicho kimefanyika leo katika Ofisi Ndogo ya wizara jijini Dar es Salaam.

DKT. MABODI ASHIRIKI UJENZI WA TAIFA KUSINI UNGUJA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema viongozi wa CCM nchini wanasherekea miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama hicho kwa kushuka kwa wananchi,huku wakitekeleza kwa vitendo falsafa ya Tanzania Mpya na CCM Mpya.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani na kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa kwa  CCM ambapo ziara hiyo imefanyika katika Mkoa wa Kusini Kichama Unguja.

Amesema CCM ndani miaka 42 imepambana na mawimbi na mikwamo ya kisiasa mbali mbali na ikafanikiwa kushinda bila kuyumba wala kugawanyika hali inayodhihirisha kuwa taasisi hiyo bado ipo imara pia ni chaguo la wananchi.

Ameeleza kuwa kuimarika kwa misingi ya Demokrasiam,haki za binadamu na utawaka bora wa kisheria pamoja na ustawi wa maendeleo katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii havikupatikana kirahisi bali vimetokana na Sera,miongozo na mipango endelevu ya kiutendaji inayosimamiwa na CCM.

Amesema makada,wanachama na viongozi wa CCM wanajivunia kuwa na taasisi inayojali utu na maendeleo ya wananchi wote bila ubaguzi wa kisiasa,kidini na kikabila.

Amesema CCM imepiga hatua kubwa katika usimamizi wa Ilani yake kwa kuimarisha sekta za Elimu,Afya, Kilimo,Miundombuni ya usafiri wa anga na baharini pamoja na amani na utulivu wa nchi.

Ameeleza kwamba pamoja na mafanikio hayo bado wanachama wa CCM wana jukumu la kulinda urithi wa Mapinduzi ya mwaka 1964,Uhuru, Muungano na taasisi ya CCM ili azna hizo zirithiwe zikiwa katika mikono salama kwa viazi vijavyo.

Dk.Mabodi akiwa katika ukarabati wa Tawi la CCM Ng’ambwa amesema Tawi hilo ni la kihistoria kwani harakati za ukombozi zilifanyika katika eneo hilo hivyo wanachama wa chama hicho wanatakiwa kulinda historia ya Tawi hilo.

Akiwa katika Tawi hilo ameagiza fedha za mfuko wa Jimbo la Tunguu  ambazo ni zaidi ya milioni 90  zitumiwe kumaliza changamoto za wananchi na vilelezo vya matumizi ya fedha hizo viwasilishwe kwa wakati katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Amesema fedha za jimbo ni mali ya wananchi na kiongozi yeyote atakayekwamisha matumizi ya fedha hizo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa miongozo mbali mbali ya kanuzi ya CCM.

Akiwa katika ziara yake hiyo amesema CCM imejipanga kuhakikisha inaandika historia mpya ya ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa dola mwaka 2020.

Amesema siasa za kuuza maneno na kutoa ahadi zisizotekelezwa zimepitwa na wakati kwani wananchi wanahitaji kuona maendeleo ambayo ndio msingi wa ustawi wa kijamii.

Ameeleza kwamba kuna baadhi ya Vyama vya siasa nchini havina Sera wala dira ya kisiasa bali kazi zake ni kubeza mambo mema yanayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hali ya kuwa hata baadhi ya viongozi wa vyama hivyo bado wanalipwa mafao na serikali iliyopo madarakani.

Akizungumza katika ziara hiyo Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Ndugu Simai Mohamed Said ameeleza kwamba toka aingie madarakani amekuwa karibu na wananchi kwa kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Amesema amekuwa mstari wa mbele kuimarisha Sekta za elimu, afya miundombinu ya barabara, vikundi vya ushirika na kusaidia mitaji kwa vikundi vya vijana mbali mbali, huku akitafuta ufumbuzi wa kudumu wa kutatua changamoto ya upungufu wa maji safi na salama kwa baadhi ya maeneo.

Naye Mwakilishi wa tiketi ya CCM Jimbo la Paje Unguja, Mhe.Jaku Hashim Ayoub amesema ametekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, na bado anaendelea kutatua changamoto mbali mbali zinazojitokea katika jimbo hilo.

Katika ziara hiyo amefuatana na Kamati za Siasa za CCM Wilaya ya Kusini, CCM Wilaya ya Kati , CCM Mkoa wa Kusini, Viongozi wa Halmashauri za Wilaya ya Kati na Kusini Unguja, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa ndugu Abdallah Haji Haidari pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Zanzibar Othman Ally Maulid.

Ziara hiyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM sambamba na kufanya shughuli za kijamii, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Naibu Katibu Mkuu huyo Dk.Mabodi, ametembelea maeneo mbali mbali yakiwemo kijiji cha Uchukuni katika ujenzi wa skuli ya msingi na maandalizi,Kisiwa cha Uzi kujenga Tawi la CCM Ng’ambwa,kukagua eneo la daraja lililopendekezwa kujengwa na marehemu Mzee Abeid Karume huko Uzi, Tawi la CCM Mungoni pamoja na kuweka jiwe la msingi maskani ya CCM Mawe Mawili huko Mtule Paje.
 NAIBU Kaibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akijenga msingi wa shule ya maandalizi na msingi ya Uchukuni.
 NAIBU Kaibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akishiriki kumwaga zege katika Tawi la CCM Ng’ambwa Mkoa wa Kusini kichama Unguja.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akiweka jiwe la msingi katika maskani ya CCM Mawe Mawili iliyopo kijiji cha Mtule Paje Mkoa wa Kusini Kichama Unguja.

Uturuki kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa watanzania

$
0
0
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener akisoma taarifa ya mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo na kulazwa katika chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazotoa na kuona namna wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja ya kutoa matibabu ya moyo kwa watanzania.
Afisa Muuguzi bingwa kutoa Connecticut Children’s Medical Center nchini Marekani ambaye yupo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kujitolea kuwafundisha wauguzi jinsi ya kuwahudumia wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Mollie Mullaney akiongea jambo na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener. Prof. Ener alitembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa ikiwa ni pamoja na kuangalia miondombinu iliyopo.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener akiangalia jinsi madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanavyofanya upasuaji alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazozifanya na kuona namna wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja ya kutoa matibabu ya moyo kwa watanzania.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener akiangalia jinsi madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wanavyofanya upasuaji alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazozifanya na kuona namna wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja ya kutoa matibabu ya moyo kwa watanzania.
Afisa Muuguzi wa chumba cha upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faustina Mwapinga akimweleza jinsi wanavyoandaa vifaa vya upasuaji Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wnazozitoa ikiwa ni pamoja na kuangalia miondombinu iliyopo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa na kuona namna wanavyoweza kufanya kazi kwa pamoja ya kutoa matibabu ya moyo kwa watanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kutoka Hospitali ya Medicana , Bursa ya nchini Uturuki Prof. Serdar Ener pamoja na wageni wengine kutoka nchini humo mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo wanazozifanya na kuangalia miundombinu iliyopo. Picha na JKCI

Watalaam wa Radiolojia kutoka Marekani wawasili Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila

$
0
0


Wataalam wa Radiolojia wakijengewa uwezo wa namna ya kutoa sampuli kwa kuongozwa na mashine ya Utrasound.
Radiolojia jpeg 03
Waalam wa Radilojia kutoka Marekani pamoja na wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila wakisoma kipimo cha Mamografia ili kubaini uvimbe uliopo kwenye matiti.
Radiolojia jpeg 04
 Dkt. Mwajuma Jumbe akitumia mashine ya Utrasound kupima uvimbe kwenye titi ili kubaini sehemu ambayo uvimbe upo.
Radiolojia 05
Dkt. Tim Rooney (kulia) pamoja na Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila wakitoa sampuli ya uvimbe kwenye titi bila kufanya upasuaji (Core Biopsy) kwa kuongozwa na mashine ya Utrasound leo hospitalini hapo.
Radiolojia jpeg 01
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru akipokea maelezo mara baada ya kuwasili kwa timu ya watalaam wa Radiolojia kutoka nchini Marekani.

                                                        Timu ya watalaam wa Radiolojia kutoka nchini Marekani wamewasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa ajili ya kuwajengea uwezo watalaam wa hospitali hiyo wa kutoa sampuli kwenye vivimbe vya kwenye matiti kupitia njia ya kitaalam (Core Biopsy).

Watalaam hao kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Mloganzila watatoa sampuli kwa watu zaidi ya 50 ambao wana vivimbe kwenye matiti ambapo watashirikiana kutoa huduma hiyo kwa zaidi ya wiki mbili.

Februari 02 hadi Februari 03 mwaka huu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mloganzila kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania-MEWATA- walitoa huduma bure ya uchunguzi awali wa kuangalia uvimbe kwenye matiti.Katika zoezi hilo watu zaidi ya 130 walifanyiwa uchunguzi, kati ya hao 36 wamekutwa na vivimbe.

TWPG WAKUTANA NA WAFADHILI WA MRADI WA LSP II

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake  Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta akizunguma katika kikao cha baadhi ya wajumbe wa umoja huo pamoja na wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Wakurugenzi wa Idara na Vitengo katika Ofisi ya Bunge wakiwa katika Kakao cha pamoja na wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) wakifuatilia jambo Katika kikao cha pamoja  na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo katika Ofisi ya Bunge  kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania  (TWPG), wakiwa katika kakao pamoja na wafadhili wa Mradi wa Kulijengea Bunge Uwezo Awamu ya Pili (LSP II) kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

ZERO 68 KATIKA SHULE YA SEKONDARI HASSANAL DAMJI ZAMCHEFUA RC NDIKILO

$
0
0
 NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 
MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na matokeo ya kidato cha nne shule ya sekondari Hassanal Damji, kata ya Magomeni, Bagamoyo kwa kupata zero wanafunzi 68 na utoro uliokithiri. Kutokana na matokeo hayo ametoa miezi miwili kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, watendaji wa mitaa, kata na vitongoji kufuatilia chanzo kilichosababisha wanafunzi hao kufeli kiasi hicho wakati shule hiyo ina walimu 57 ambao wanatosha.
Akizungumza na viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule hiyo, wakati wa ziara yake mkoani hapo, Ndikilo alisema ameudhika na matokeo hayo hivyo kuna kila sababu ya kuchukua hatua mapema. Aliwaasa wanafunzi hao kuacha pia utoro na kupotelea vichakani muda wa masomo ili kuinua taaluma zao. Ndikilo aliwaambia, waache kuchezea elimu kwani ni msingi na ufunguo wa maisha yao baadae. 

"Mnakunywa uji shuleni, walimu wapo wa kutosha, kwanini wanafunzi wahaudhurii masomo??? "Namba hii sio ya kufurahisha, division one hakuna hata mmoja, division two ni wanafunzi 2,division three ni wanafunzi sita,na Four wapo 72, na zero 68 ufaulu huu lazima tuuchukulie hatua ili wanafunzi waweze kufaulu zaidi "alisisitiza Ndikilo.  Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema utoro shuleni hapo upo kwa asilimia 15 jambo ambalo sio zuri. Alisema amejipanga kuanzisha kampeni ya TOKOMEZA UTORO ili kuondoa changamoto hiyo mashuleni. 

MAFUNZO YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI YA MWAKA 2019/2020 YAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi ya Mwaka 2019/2020 yaliofanyika Chuo cha Karume Mbweni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mayasa Mahfudha Mwinyi akitoa hotuba ya kumkaribisha Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi ya Mwaka 2019/2020 yaliofanyika Chuo cha Karume Mbweni Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Baadhi ya Washiriki (WADADISI)wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi ya Mwaka 2019/2020 wakimsikiliza mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Mafunzo hayo yaliofanyika Chuo cha Karume Mbweni Wilaya ya Magharibi B Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MAHAKAMA MKOANI TABORA YATAKIWA KUANZISHA MAHAKAMA ZINATEMBEA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT
SERIKALI Mkoani Tabora imeiomba Mahakama kuanzisha mahakama inayotembelea katika maeneo ambayo hayana huduma hizo ili kuwasogezea wananchi huduma hizo karibu. Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya Sheria nchini.

 Alisema hatua itasaidia kuharakisha utoaji wa haki kwa wananchi wanaoishi mbali na maeneo yenye Mahakama kama vile wilaya ya Sikonge na Uyui. Mwanri aliongeza kuwa zoezi hilo pia litasaidia kusababisha mrundikano wa ksei katika Mahakama ya Tabora.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wanajamii kuwajibika katika kuhakikisha wanawalea watoto wao katika maadili mema ambayo hayatawasababisha kujikuta wakivunja Sheria za Nchi na kukamatwa na vyombo vya dola. Alisema kabla ya jamii kunyoshea kidole Mahakama ni lazima ihakikishe nayo imesimama katika nafasi yake katika kuzuia ovu.

 Mwanri amewataka watendaji hao watimize majukumu yao huku wakijua kwamba mahakama  ndio kimbilio la wanyonge kupata haki. Mkuu huyo wa mkoa aliitaka Mahakama kuhakikisha  maamuzi wanayotoa yawe sahihi ili yasije yakaleta madhara kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Aliwaonya watendaji wake kutojihusisha na vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo vimekuwa vikilalamikiwa sana na wananchi ambao wamekuwa wakifika katika mahakama kutafuta haki zao.

 Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole alisema  kuwa utoaaji haki kwa wakati ni wajibu wa wadau wote. Aliwataka wadau kushirikiana wote wakiwemo Polisi, Mahakimu , Mawakili, Ofisi ya Mwanasheria, Mashahidi na jamii ili kuhakikisha wananchi wanapata haki mapema bila kuchelewa.

 Jaji huyo alisema ucheweshaji wa kesi unachangia kurudisha nyuma maendeleo ya mtu na wakati mwingine Taifa kwa ujumla. Jaji Bongole alisema wadau wakishirikiana na kufanyakazi katika muda unaotakiwa watasaidia kuhakikisha wananchi wanadai haki hawapotezi muda na mali zake wakati wa kufuatilia haki zake.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Askofu mkuu wa kanisa Katoliki jimbo kuu la Tabora Paul Ruzoka amewaasa Majaji na Mahakimu kutoa haki bila ya kupokea shinikizo wakati wanaposikiliza mashauri yanayofikishwa mbele yao na kuyatolea maamuzi.

Kiongozi huyo wa Kanisa katoliki mkoani Tabora amewaomba Majaji na Mahakimu kutotumia mashinikizo ya washauri wa Mahakama bali  watimize wajibu wao kwa haki ili amani iweze kutawala. Katika hotuba yake iliyosomwa na katibu wake Padre Novatus Safari Askofu Ruzoka amewaasa watumishi hao wa Mahakama kutoa Hukumu kwa haki bila ya upendeleo.
 Brass Band ya Chuo cha Ualimu Tabora ikiongoza maandamano ya kuadhimisha siku ya Sheria Mkoa wa Tabora leo
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye suti nyeusi) na Majaji na Mawakili wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Baadhi ya Mawakili mkoani Tabora wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Jeshi la Polisi kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoani tabora  wakiwa katika gwaride maalumu la kuadhimisha siku ya sheria leo
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) akibadilishana mawazo na jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Julius Malaba(kulia) wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (katikati) akisalimiana na  Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole (kulia)  na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Dkt. John Utumwa (kushoto)  wakati wa  kuadhimisha siku ya sheria leo
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole (kulia) akibadilishana mawazo na Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Dkt. John Utumwa (kushoto)  wakati wa  kuadhimisha siku ya sheria leo
  Baadhi ya wakazi wa Manispaa  ya Tabora wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria leo.
 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Tabora Salvatory Bongole akitoa hotuba wakati wa   kuadhimisha siku ya sheria leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akihutubia wakazi wa Tabora na wanasheria wakati  kuadhimisha siku ya sheria leo

Watuhumiwa 29 wa Mauaji Njombe Wakamatwa

$
0
0
Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Watu 29 wamekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya utekaji na mauaji ya watoto Mkoani Njombe.

Akiwasilisha bungeni leo Jijini Dodoma taarifa ya Serikali kuhusu mauaji hayo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola amesema Serikali imeshachukua hatua mbalimbali katika kutatua na kuzuia matukio hayo sanjari na kutoa maelekezo ya hatua za kupambana na uhalifu huo ikiwemo kuwatia mbaroni watuhumiwa.

"Mpaka sasa hatua zilizochukuliwa na Serikali zimefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 29 kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi na kazi bado inaendelea" ameongeza Waziri Lugola.

Mhe. Lugola amebainisha kuwa,  hivi karibuni kumejitokeza matukio yasiyo  ya kawaida ya utekaji na mauaji ya watoto yaliyokuwa yakihusishwa na imani potofu za kishirikina katika Mkoa wa Njombe.

"Kufuatia matukio hayo hadi sasa watoto saba wa umri chini ha miaka 16 wameripotiwa kuuawa, mmoja kujeruhiwa na wawili kupotea na badae kuonekana, matukio haya yametokea  katika maeneo ya Ikando, Matembwe, Mjimwema, Msitu wa Sekondari ya Njombe, Lukosa, Sido na Mfekere," ameeleza Waziri Lugola.

Akifafanua zaidi, Lugola amesema kuwa, mbali na juhudi za Serikali, Jeshi la Polisi kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe imechukua hatua mbalimbali kuzuia aina hiyo ya uhalifu kwa kutumia timu ya wataalamu wa upelelezi kuvisaidia vyombo vya dola kuchunguza matukio hayo.

Pia kutumia falsafa ya ulinzi shirikishi wa jamii kwa kutoa elimu mashuleni kwa walimu ili kuweza kuwaelimisha wanafunzi kuongeza umakini katika mienendo yao, kutumia vyombo vya habari kutoa elimu kwa wazazi na wananchi kwa ujumla juu ya elimu ya ulinzi na usalama, vikao na waganga wa kienyeji, viongozi wa dini, Wazee wa Mila, Viongozi wa Kata pamoja na kufanga doria na misako kwenye maeneo mbalimbali ya misitu na nyumba za kulala wageni zilizopo pembezoni, ni mbinu zilizotumika kuzuia vitendo hivyo.

Hata hivyo, Mhe. Lugola ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha na matukio hayo na itikadi za kisiasa, imani za kidini au shughuli za kibiashara.
Aidha, amebainisha kuwa Serikali itachukua hatua kwa wale watakaojihusisha na vitendo vya usambazaji wa taarifa za kichochezi mitandaoni hivyo amewaasa Watanzania kuacha kusambaza taarifa za uzushi mitandaoni  kwa nia yoyote ile kwani ni takwa la Sheria ya Mtandao.

Mbali na hayo amesema kuwa, Serikali itahakikisha wote waliohusika na mauaji wanaendelea kusakwa, kuhojiwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria bila kujali nafasi zao katika jamii.

Hivi karibuni yamajitokeza matukio ya utekaji na mauaji ya watoto wadogo Mkoani Njombe, jambo ambalo limezua taharuki mkoani humo na nchini kote kwa ujumla.

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AIPATIA CHANNEL TEN MILIONI 200 KAMA ALIVYOAHIDI JANA

$
0
0
 Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten Bi. Siri Pambe akisoma hundi ya Shilingi Milioni 200 kabla hajaikabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL)  Jaffari Haniu kama ilivyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike
 Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimkabidhi  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL)  Jaffari Haniu hundi ya shilingi Milioni 200 aliyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike
  Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiongea machache baada ya kumkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL)  Jaffari Haniu hundi ya shilingi Milioni 200 aliyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike
 Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Media Group Limited (AMBL)  Jaffari Haniu akitoa shukurani  baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi Milioni 200 aliyoahidiwa jana na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kununua vifaa kuimarisha utendaji wa televisheni hivyo. Akishuhudia kulia ni Katibu wa Mwenyekiti wa CCM Ndg. Ngusa Samike. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI, AZINDUA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua rasmi gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, , Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Sophia Mjema wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea  baada ya kuizindua rasmi akiwa na  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk, Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Bi. Bella Bird, wakati wa   maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019. Anayetoa maelekezo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalege na Kulia kabisa ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania Mhe. Eva Nkya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye gari maalumu litakalotumika kama Mahakama inayotembea baada ya kulizindua rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA wa Mahakama ya Tanzania Bw. Enock Kalegebaada ya kuzindua rasmi Mfumo wa Kielektroniki wa Kuratibu Mashauri (DSDS ll)  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Majaji Wakuu Wastaafu Mhe. Augustino ramadhani na Mhe. Mohamed Chande Othmana kabla ya kupiga nao picha ya kumbukumbu kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Spika Job Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer Fereshi na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Mbarouk Salum Mbarouk  baada ya kuhudhuria   kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.
PICHA NA IKULU

SAFARI ZA NDEGE KWENDA DODOMA KUANZA APRILI MOSI MWAKA HUU- PRECISION AIR

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Shirika la ndege la Precision Air limetangaza  rasmi kuanza kwa safari za ndege  kati ya Dar es Saalaam – Dodoma na Kiilimaanjaaro-Dodoma kuanzia tarehe 1, Aprili 2019.

Meneja Masoko na Mahusiano wa Shirika hilo, Hillary Mremi, amesema kwamba Precision Air itakua ikafanya safari sita kwa wiki kuelekea Dodoma kati ya siku za Jumatatu,Jumanne,Jumatano, Alhamisi,Ijumaa na Jumamosi.

Amesema kuwa, katika siku za Jumatano na Ijumaa safari za Dodoma zitakua zikipitia Kilimanjaro na kwa siku zilizobakia safari ziatakua ni za moja kwa moja.

“Safari zetu hizi mpya zitaiiunganisha Dodoma na mikoa mingine kama Mtwara, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Nairobi kupitia Dar es Salaam na Kilimanjaro. Abiria kutoka maeneo haya wataweza kuunganisha safari zao kuelekea Dodoma kupitia mtandao wetu wa safari, na hivyo kuunganisha jamii jambo ambalo ni moja kati ya malengo yetu makuu.” alisema Mremi.

Mremi ameeleza zaidi kuwa kwa safari za moja kwa moja Ndege itakua ikiondoka Dar es Salaam saa 3:15 Asubuhi na kufika Dodoma saa 4:20 Asubuhi, huku kwa safari za kupitia Kilimanjaro Ndege itakua ikondoka Dar es Salaam saa 8:00 Mchana na kufika Dodoma saa 10:15 Mchana.

Amesema kwa safari za moja kwa moja kutokea Dodoma, Ndege itakua ikiondoka saa 4:45 Asubuhi na kufika Dar es Salaam saa 5:50 Asubuhi, huku kwa safari za kuptia Kilimanjaro Ndege itakua ikiondoka saa 11:15 Jioni na kuwasili Kilimanjaro saa 12:15 Jioni na Dar es Salaam saa 2:05 usiku.

Shirika hilo lilitangaza kuanza kwa safari za ndege kuelekea Jiji la Dodoma ikiwa ni katika kurahisisha usafiri kwa watendaji wa serikali baada ya Makao Makuu ya nchi kuhamia rasmi kwenye Jiji hilo.
Meneja Masoko na Mahusiano wa ShiShirika la ndege la Precision AirHillary Mremi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florens Luoga amesema kuwa  kupeana taarifa za mikopo kunapunguza tofauti ya upatikanaji wa taarifa miongoni mwa wakopeshaji na wakopaji na kupunguza gharama za kutafuta taarifa hizo na hivyo kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa sehemu kubwa ya wananchi.

Prof.Luoga ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kuelimisha umma kuhusu taarifa za mikipo na elimu ya fedha.Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alipaswa kuwa Waziri wa Fedha lakini kutokana na majukumu mengine amewakilishwa na Gavana wa BoT.

Akifafanua zaidi wakati wa uzinduzi huo , Profesa Luoga amefafanua kampeni hiyo ya uhamasishaji na elimu kwa umma kuhusu taarifa za wakopaji ambayo imeandaliwa na BoT kwa kushirikiana na International Finance Corporation, ambalo ni mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia. 

"Elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo mzima wa taarifa za mikopo. Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini. 

"Mpango huu ni sehemu ya mpango mpana zaidi wa kukuza elimu kuhusu masuala ya fedha kwa lengo la kukuza huduma jumuishi za kifedha Tanzania kutoka asilimia 65 mwaka 2018 hadi asilimia 75 ya watu wazima wanaotumia huduma za kifedha ifikapo mwaka 2022,"amesema.

Ameongeza kampeni hiyo inaangalia masuala muhimu kuhusu taarifa za mikopo ambazo ni pamoja na maana ya taarifa ya mikopo, kwa nini taarifa hizo ni muhimu kwa wakopaji na wakopeshaji, namna gani watumiaji wa huduma za fedha wanaweza kupata taarifa za mikopo, umuhimu wa kuwa na historia nzuri ya ukopaji na umuhimu wa kuangalia taarifa zako za mikopo mara kwa mara kutoka taasisi zinazoandaa taarifa hizo ili kuhakikisha taarifa za mikopo zinakuwa nzuri.

Prof. Luoga amesema BoT ilizindua mfumo wa taarifa za mikopo Septemba mwaka 2012 ilipotoa kanuni zilizotokana na Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 

2006, yaani kanuni za Kanzidata ya Taarifa za Mikopo za mwaka, 2012 na Kanuni za Kampuni za Taarifa za Mikopo, 2012. "Hivi sasa kuna taasisi mbili zinazoandaa taarifa za mikopo ambazo zimesajiliwa na zinazofanya kazi hapa Tanzania. Taasisi hizo ni Dun & Bradstreet Credit Bureau 
Tanzania Limited na Creditinfo Tanzania Limited,"amesema.

Amesema taasisi hizo zinapata taarifa zake kutoka Kanzidata ambayo inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania na taarifa (data) nyingine kutoka taasisi zingine zinazotoa huduma mbalimbali, kama kampuni za simu, wakala wa kukusanya madeni, wauzaji wa jumla na reja reja wanaotoa bidhaa na huduma kwa mkopo, taasisi za umma kama vile Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na Masijala za Mahakama. 

Amesema taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo hutayarisha taarifa hizo na kuzitoa kwa wakopeshaji na watumiaji wengine kwa ada fulani wanapozihitaji ili kuweza kujua hali ya kifedha ya watu wanaotaka kupata mikopo kutoka kwao na kwamba taarifa za mikopo ni muhimu pia kwa watumiaji wengine, ikiwemo BoT kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya fedha, wakala za serikali na sekta nyingine katika uchumi kama waajiri, watoa huduma za bima, wauzaji wa jumla na reja reja, kampuni za karadha na mawakala wa mikopo ya nyumba.

"Aidha, kushirikishana taarifa za mikopo kunachangia katika kujenga nidhamu ya ukopaji kwa kuepuka kukopa bila sababu na kuchukua mikopo mikubwa. Kwa wakopeshaji, taarifa za mikopo zinarahisisha kuangalia vihatarishi na kufanya maamuzi bora wakati wa kutoa mikopo kwa taasisi na wajasiriamali wadogo pamoja na kufuatilia wakopaji kwa ufanisi zaidi,"amesema.

Prof.Luoga amesema pia kubadirishana taarifa sahihi kati ya taasisi za fedha na wadau wote ni muhimu katika mchakato wa maamuzi, kupunguza gharama ya mikopo na wakopaji wasiolipa madeni yao. Katika kipindi cha muda mrefu, mfumo huu unatarajiwa kuchangia kupunguza gharama za mikopo, mikopo chechefu na kukuza uthabiti wa sekta ya fedha.

Amefafanua faida za kuwaruhusu wakopaji kupata taarifa zao za mikopo ni kujenga uaminifu, uwazi na usahihi wa taarifa. Ili kuhakikisha kwamba matakwa ya kisheria na usimamizi na kukuza kukubalika kwa mfumo wa taarifa za mikopo, Benki Kuu ya Tanzania inasimamia uendeshaji wa Kanzidata ya Taarifa za Mikopo na Taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo.
Amesea BoT imekuwa ikifanya kazi ya kukuza mfumo wa taarifa za ukopaji ili kuboresha usimamizi wa vihatarishi vya mikopo katika benki na taasisi za fedha na taasisi nyingine zinazotoa mikopo, lengo likiwa ni kuongeza upatikanaji wa mikopo na kukuza huduma jumuishi za kifedha. 

Prof.Luoga amesema katika kufanya hivyo, pamoja na mambo mengine walihitaji kupata msaada wa kitaalamu kutoka Benki ya Dunia kupitia shirika lake tanzu la International Finance Corporation katika maeneo manne ambayo ni kuimarisha uwezo wa Benki Kuu ya Tanzania kudhibiti na kusimamia shughuli za taarifa za mikopo;

Pia kuwezesha kuunganishwa kwa huduma ndogo za fedha na taasisi zingine za mikopo ambazo hazisimamiwi katika mfumo wa taarifa za mikopo, kusaidia uimarishaji wa elimu kwa wadau na uhamasishaji kuhusu taarifa za mikopo na usaidia uanzishaji wa Kikosi Kazi Cha Wadau kushirikiana katika kuboresha na kuendeleza mfumo wa ubadilishanaji taarifa za mikopo.

Hivyo amesema uzinduzi huo unaonesha jitihada za BoT na wadau wengine katika kukuza uelewa kuhusu mfumo wa taarifa za mikopo na elimu ya fedha kama vitu muhimu katika uendeshaji wa soko la mikopo, uthabiti wa sekta ya fedha na maendeleo ya uchumi wa taifa kwa ujumla.

"Inatarajiwa kupitia kampeni hii ya uhamasishaji, wadau mbalimbali watajua faida za kutumia mfumo wa taarifa za mikopo. Ujumbe utaelekezwa kwa wakopeshaji na wakopaji kwa lengo la kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa taarifa za mikopo na faida kwa makundi yote mawili,"amesema.

DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE

$
0
0
*Ataka kila muhimili uachwe ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba 
*Agusia pia uhaba wa Majaji, azindua Mahakama inayotembea 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

RAIS Dk. John Magufuli ameeleza kuwa katika uongozi wake amejitahidi kuhakikisha haingilia muhimili mwingine huku akisisitiza kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya muhimili mmoja na mwingine katika kutekeleza majukumu yao.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali,Bunge na Mahakama kila mmoja kwa nafasi yake umekuwa ukitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kwamba hata akiona baadhi ya watu wanatukana anachokifanya ni kubadilisha chaneli.

Rais amefafanua ni vema watumishi au watendaji wa mihimili hiyo wakahakikisha wanaendeelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya nchi yetu.Rais ambaye mbali ya kutoa maelezo hayo amezindua Mahakama inayotembea.Kuhusu kila muhimili kufanya kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Rais Magufuli amesema hata yeye amekuwa makini kwa kuhakikisha anajitahidi kufanya kazi zake bila kuingilia muhimili mwingine na tangu ashike nafasi hiyo amekuwa makini katika hilo na kwamba amesisitiza kila mmoja wetu kufanya kazi kwa kufuata taratibu na 
sheria.
"Tangu niwe kwenye nafasi hii nimekuwa nikijitahidi kufanya kazi kwa kufuata utaratibu na sheria na ndio maana hajawahi kuingilia muhimili wowote.Leo hii nimefurahi kumuona Spika wa Bunge yupo hapa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo, Waziri Mkuu na viongozi wengine, hii inathibitisha namna ambavyo mihimili yetu ambavyo inafanya kazi kwa ushirikiano,"amesema.

Kuhusu Siku ya Sheria ,Rais Magufuli amesema ametumia nafasi hiyo kumpongeza Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Musa kwa uongozi wake na katika kipindi kifupi cha uwepo wake kwenye eneo la Mahakama kuna mabadiliko makubwa.Pia amesema anatambua changamoto zinazowakabili watumishi wa Mahakama na idara nyingine lakini amewaomba zisiwakatishe tamaa kwani hata zikimalizike zote zitajitokeza zingine tu.

Hivyo amewaomba waendelee kufanya kazo kwa bidii na kwamba atachambua changamoto hizo na zile ambazo zinaweza kutafutiwa ufumbuzi wake haraka atafanya hivyo."Nieleze tu ukweli karibu taasisi zote zinachangamoto ikiwemo ya uhaba wa watumishi na pamoja na Serikali kuajiri watumishi 52,000 ambao wamegawanyika katika sekta mbalimbali lakini bado uhaba upo.Ni vema kila idara ikatumia watu walionao kwa uaminifu mkubwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto zilizopo ambapo kiukweli haziwezi kumalizika kwa wakati mmoja,"amesema.

Akizungumzia baadhi ya maombi ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma ambaye amezungumzia uhaba wa majaji, Rais Magufuli amesema licha ya uteuzi wa majaji ambao ameufanya hivi karibuni bado kuna haja ya kuwatumia Mahakimu ambao wanasifa ujaji ili kukabiliana na msongamano wa kesi."Natambua kwa mujibu wa kifungu... cha Sheria kuna Mahakimu ambao waliteuliwa 
na Waziri husika, nadhani wale wanaweza kufanya kazi za ujaji ,najua wapo kama 
195 hivi watumike ili kukabiliana na uhaba huu," amesisitiza Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Magufuli ameitaka Mahakama kusimamia haki za wamama wajane kwani wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika kupata haki zao hasa katika suala linalohusu mirathi.
"Jaji Mkuu na hapa niseme kama kuna uwezekano wa kupata gari lingine la Mahakama inayotembea basi ni vema ikatembea huko kwa wananchi kwa maana wajane hawa wanapata tani sana.Pia nimuombe Mwakilishi wa Benki ya Dunia kuangalia uwezekano wa kupata gari nyingine hata kama mawili ili kusaidia kundi hilo kubwa la akina mama wajane,"amesema.

Kwa upande wake Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ili Muhimili wa Mahakama uendelee kufanya kazi zake vizuri unahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi huku aliwataka wananchi kusoma Sheria na si lazima hadi wasome shuleni.

"Rais hapa nawaomba pia wananchi wajaribu kusoma Sheria kupitia vitabu mbalimbali ili angalau kupata uelewa wa mambo yanayohusu Sheria na kuepuka kuelekezwa katika kila kifungu cha Sheria na hata Mpiga chapa wa Serikali anatakiwa aweke sheria zote mtandaoni kwa lengo la kumrahisishia mwanachi kusoma Sheria,"amesema Prof.Juma.Amemueleza Rais Magufuli mafanikio mbalimbali na hatua ambazo wamezichukuwa hususani kwa watumishi ambao walipatikana na makosa ya rushwa na hata vyeti isivyokuwa na sifa .

Kuhusu Mahakama ya kutembea Prof.Juma amemueleza Rais Dk.Magufuli kuwa Mahakama hiyo itaaza kutoa huduma katika mikoa miwili, mkoa wa Dar es Salaam katika maeneo ya Bunje B iliyopo wilayani Kinondoni, Buza wilayani Temeke, Chanika wilayani Ilala, na katika mkoa wa Mwanza maeneo ya Busweru,Buhongwa,pamoja na Igoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.

Watuhumiwa wa ujambazi wauawa Jijini Mwanza

$
0
0
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuawa na Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza katika Mtaa wa Nyakabungo, Kata ya Isamilo Jijini Mwanza, usiku wa kuamkia leo Februari 06, 2019.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Advera Bulimba amesema miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure kwa ajili ya utambuzi na kwamba katika tukio hilo, inadhaniwa watuhumiwa wengine watatu walifanikiwa kutoroka.
Na George Binagi, BMG

AGPAHI YAKABIDHI MAGARI KUKABILIANA NA UKIMWI SHINYANGA, RC APONGEZA

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack ameipongeza Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) kwa jitihada inazozifanya katika kuboresha utoaji wa huduma za Virusi Vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI mkoani Shinyanga.

Mhe. Telack ametoa pongezi hizo leo Jumatano Februari 6,2019 wakati akipokea magari mawili aina ya Nissan Patrol yenye thamani ya shilingi milioni 186.5 yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu.

Alisema AGPAHI wamekuwa wadau bora katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwahudumia wananchi.

Alisema kutokana na juhudi zinazofanywa na wadau wakiwemo AGPAHI kwa kushirikiana na serikali takwimu za maambukizi ya UKIMWI mkoani Shinyanga zimepungua kutoka asilimia 7.4 mwaka 2011/2012 hadi kufikia asilimia 5.9 mwaka 2016/2017. “Kazi mnayofanya ni ya kujenga familia za Watanzania,niwashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia,naomba tuendelee kushirikiana”,alisema Mhe. Telack. 

“Leo nimepokea magari haya mawili na sasa idadi ya magari yaliyotolewa na AGPAHI mkoani hapa tangu ilipoanza kazi zake,yanakuwa manne,naomba mtupatie pia magari kwa ajili ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga kwani napo bado wananchi wanahitaji elimu ya VVU na UKIMWI”,aliongeza Mkuu huyo wa mkoa. 

Aidha aliahidi kuwa, magari hayo yatatumika kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwataka Wataalamu wa afya kutumia magari kuwafikia wananchi wengi zaidi yakiwemo maeneo ya wachimbaji madini na kuwaelimisha kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI. 

Akikabidhi magari kwa mkuu wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa alisema magari hayo yatasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza tija katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI. 

“Tunatambua kuwa wilaya ya Kahama ina kiwango kikubwa cha maambukizi ya VVU, ndiyo maana tumeona vyema tutoe magari Kahama Mji na Ushetu kwani uhitaji ni mkubwa ili kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI tukishirikiana na serikali”,alisema Dk. Sekela. 

“Mbali na kutoa magari pia tulishatoa pikipiki na baiskeli. Aidha tumekarabati vituo vya kutolea huduma na tumewezesha ajira na mafunzo mbalimbali ya utoaji huduma za VVU na UKIMWI”,alisema. 

Aidha alieleza kuwa, katika kipindi cha kuanzia Januari 2017 hadi Disemba 2018, AGPAHI imefanikiwa kupima VVU watu 905,724 mkoani Shinyanga ambapo watu 27,724 wanaoishi na VVU walianzishiwa dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) katika vituo 107 vya kutolea huduma. 

“Katika kipindi hicho pia akina mama wajawazito 140,173 walipimwa VVU ambapo 6,555 walionekana kuambukizwa.WAVIU wamama 6,481 (98.9%) walianzishiwa dawa na watoto 4,877 (96%) walizaliwa bila maambukizi”,alifafanua Dk. Sekela. 

Magari hayo yamekabidhiwa na AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya Vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC). 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati Asasi ya AGPAHI ikikabidhi magari mawili yenye thamani ya shilingi milioni 186.5 kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa, kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Muonekano wa magari yaliyo magari mawili yaliyotolewa na AGPAHI kusaidia utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri za wilaya za Kahama Mji na Ushetu. 
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akimweleza jambo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack wakati akimkabidhi funguo za moja ya magari hayo ili akague. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akijiandaa kuingia ndani ya gari wakati Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akikagua gari. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akiwasha gari ikiwa ni sehemu ya ukaguzi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Augustino Matomora (wa kwanza kushoto mwenye suti nyeusi) na Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu, Juma Kimisha (katikati).
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack akimkabidhi ufunguo wa gari Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kahama Mji, Anderson Msumba (kushoto).
Kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Ushetu, Juma Kimisha akipokea kadi ya gari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa wakibadilishana hati za makabidhiano ya magari.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa wakisaini hati za makabidhiano ya magari mawili aina ya Nissan Patrol yenye thamani ya shilingi milioni 186.5.
Mratibu wa Mradi AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Dk. Gastor Njau (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Ushetu, Michael Augustino Matomora nao wakisaini hati za makabidhiano ya magari.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack nakala ya Mpango Mkakati wa AGPAHI 2018-2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa (kulia) akieleza mafanikio ya AGPAHI hadi kufikia Septemba 2018 ambapo alisema watu 395,777 wanapatiwa huduma za VVU na UKIMWI katika vituo vya kutolea huduma katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara. Watu 248,000 wakiwemo watoto 13,600 wanatumia dawa za kupunguza makali ya VVU.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dk. Rashid Mfaume akiishukuru AGPAHI kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutoa huduma za VVU na UKIMWI. 
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa (kushoto) akiagana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack baada ya kukabidhiana magari. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images