Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba kimetimiza miaka 59 tangu kuasisiwa kwake.

$
0
0
Leo (jana) Februari 5/2019 ni siku ambayo Chuo kikuu Cha Urafiki cha Watu wa Urusi(Peoples’ Friendship University of Russia) au maarufu kama Chuo Kikuu Cha Patrice Lumumba kimetimiza miaka 59 tangu kuasisiwa kwake.

Kama Raisi wa Umoja wa vijana wa nchi zote za Afrika chuoni hapo niliwakilisha Waafrika wote katika jopo la Kimataifa katika kusheherekea siku hii kubwa kwa kuongozana na Mkuu wa Chuo hicho Vladimir Philipov na maraisi wa Vijana wa nchi za Kiarabu, nchi za Asia na tulipozuru makao Makuu ya Shirika kubwa la Habari la Urusi la RIA NOVOST na RUSSIA TODAY na kumsikiliza Mkuu wa Chuo akifanya mahojiano na waandishi wa habari na kushiriki mkutano wa Kimataifa. 

Pia nilipata nafasi ya kukutana Naibu Waziri wa Elimu wa Gambia na Balozi wa Gambia kwa Urusi walipohudhuria Mkutano huu.Mkutano huu ulihusu vipi Chuo hiki kuendelea kuanzisha zaidi Uhusiano na vyuo vyengine duniani na kutoa kozi na mafunzo mbalimbali kwa mtandao duniani zaidi ya nchi 70 ikiwepo nchi 20 za Afrika chini ya Programu yake ya GLOBAL CLUSTER PROGRAM. 

Nchi za Afrika zaidi zilizopo kaitka programu hii ni kutokea kusini kama Zambia,Namibia,Zimbabwe, Angola, Msumbiji, Botswana, Afrika ya Kusini. Tanzania imetajwa katika kupata msaada wa mafunzo kwa usafiri wa reli chini ya shirika la TAZARA. 

Hakika tunaendelea kuliwakilisha Taifa Kimataifa zaidi.

Ahsante sana!

Mohamed Mansour.


SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA KUTOKA UTURUKI OFISINI KWAKE JIJINI DODOMA

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Wafanyabishara kutoka Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki walipomtembelea mapema leo Ofisini kwake Jijini Dodoma.
 Rais  wa  Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki Bw. Mehment Nazif Gunal akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai wakati walipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.
  Spika wa Bunge (kulia) katika picha ya pamoja na Rais  wa  Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki Bw. Mehment Nazif Gunal mara baada ya kuzungumza naye Ofisini kwake Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai katika picha ya pamoja na Wafanyabishara kutoka Kampuni ya MNG ya nchini Uturuki mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dodoma.

PICHA NA BUNGE

MAMA ASHA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO JIMBONI

$
0
0
Uongozi wa Jimbo la Mahonda umejikita kuimarisha Sekta ya Michezo katika azma nzima ya kuinua kiwango cha Michezo kitakachowawezesha Vijana ndani ya Jimbo hilo kujiwekea njia ya kupata ajira kupitia fani hiyo muhimu kwa sasa hapa Duniani.

Mke wa Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mama Asha Suleiman Iddi amesema hayo baada ya kushuhudia pambano la kirafiki la Mchezo wa Mpira wa Pete {Netball} uliozikutanisha Timu za Madada wa Fujoni dhidi ya Kitope lililofanyika katika uwanja wa mahonda Kiwandani.

Mama Asha amesema utaratibu wa kuwapatia vifaa katika Michezo tofauti Vijana wa Jimbo hilo utaendelea ili kuwajengea ari ya kupenda Michezo licha ya kuimarisha Afya bora zitakazowaepusha na Maradhi mbali mbali pamoja na kuwa mbali na vikundi vya kihuni.

Amewataka Vijana hao kujikita katika masuala ya Kijamii na kuacha kasumba na mambo yanayoendelea kuenezwa na Watu walioshindwa kutafuta masuala ya msingi yatakayowawezesha Vijana hao kujitegemea zaidi.

Katika pambano hilo mbali ya kutafuta Timu ya Kombaini ya Netball ya Jimbo la Mahonda lakini pia ulikwenda sambamba na shamra shamra za maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 42 ya Chama cha Mapinduzi tokea kilipoasisiwa kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar mnamo Mwaka 1977.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Febuari 05, 2019


 

Mawaziri wa Tanzania, Rwanda na Burundi wakagua kazi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa Rusumo

$
0
0

 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kulia), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza  (wa kwanza kushoto) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (wa Tatu kulia mstari wa pili) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo itakayozalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo lililopo mpakani mwa nchi ya Rwanda na Tanzania.
 Maporomoko ya maji ya Mto Kagera,  yatakayotumika kuzalisha umeme wa megawati 80 kwa ajili ya nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi.
 Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (katikati) akifuatilia kikao cha Mawaziri wa Rwanda, Tanzania na Burundi kilichohusu utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati), Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza  (kushoto kwa Dkt. Kalemani) na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete (kulia kwa Dkt  Kalemani) wakiwa katika kikao chao na wataalam mbalimbali wanaosimamia mradi wa umeme wa Rusumo kilichofanyika Rusumo mkoani Kagera.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa tatu kushoto) pamoja na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Lt. Col. Michael Mntenjele  (wa nne kushoto) wakitoka kukagua eneo kutakapojengwa mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 80 katika eneo la Rusumo mkoani Kagera.
Na Teresia Mhagama,
Mawaziri wanaohusika na utekelezaji wa mradi wa umeme wa maji wa Rusumo (MW 80)  kutoka Tanzania, Rwanda na Burundi wamekagua kazi ya ujenzi wa mradi huo wilayani Ngara mkoa wa Kagera na kutoa maelekezo mbalimbali yatakayowezesha kasi ya utekelezaji wa mradi huo kuongezeka.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani ndiye aliyewaongoza, Waziri wa Nishati na Migodi wa Burundi, Come Manirakiza na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Claver Gatete katika kukagua kazi mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwemo ujenzi wa eneo itakapojengwa mitambo ya kuzalishia umeme na ujenzi nyumba za wafanyakazi.

Baada ya kukagua kazi zinazoendelea kufanyika, Mawaziri hao walifanya kikao chini ya uenyekiti wa Dkt Medard Kalemani na kuiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya mradi huo kusimamia ipasavyo kazi mbalimbali za ujenzi ili mradi huo ukamilike mwaka 2020 kama ilivyo katika makubaliano.

Dkt. Kalemani alisema kuwa, kazi ya ujenzi wa mradi huo ilianza mwezi Februari mwaka 2017 na inapaswa kukamilika ndani ya miezi 36 hivyo Bodi hiyo yenye wajumbe kutoka nchi zote Tatu ihakikishe kuwa mkandarasi anakamilisha kazi kwa wakati.

“ Pia tumeiagiza Bodi na wataalam walioko katika mradi huu, wahakikishe kuwa wanashirikisha Mamlaka na Taasisi mbalimbali zilizopo katika maeneo ya mradi katika nchi zote Tatu hasa katika masuala yanayohusu jamii zinazozunguka mradi na stahili za wafanyakazi ili kutokuwa na vikwazo katika utekelezaji,” alisema Dkt Kalemani.

Kuhusu faida za mradi huo, alisema kuwa, kila nchi itapata megawati 27 na kujenga miundombinu ya usafirishaji umeme wa kV 220 ambapo kwa upande wa Tanzania, itajengwa miundombinu hiyo kutoka Rusumo kwenda Nyakanazi  kwa umbali wa kilometa 98.

Aliongeza kuwa, miundombinu hiyo ya usafirishaji umeme, kwa upande wa Tanzania, itaingiza umeme katika gridi ya Taifa kupitia njia  ya umeme inayotoka Geita na kwamba, vijiji  13 vinavyopitiwa na mradi wa Rusumo vitasambaziwa nishati hiyo.

Kuhusu gharama za mradi, alisema kuwa, kila nchi imegharamia mradi huo kupitia wadau wa maendeleo ambao ni Benki ya Maendeleo Afrika (AfdB) na Benki ya Dunia (WB) ambapo kwa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kila nchi imechangia takribani Dola za Marekani milioni 113.

Kwa upande wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, alisema kuwa kila nchi imechangia kiasi cha  Dola za Marekani milioni 36.7.

Kwa ujumla, alisema kuwa, Mawaziri wa nchi hizo Tatu wameazimia kuwa, mradi huo utekelezwe kwa kasi usiku na mchana bila kuwa na visingizio na kama kuna muda uliopotezwa na mkandarasi wa mradi, ufidiwe kwa njia mbalimbali ikiwemo kuongeza nguvu kazi.

Aidha, ili kuongeza usimamizi katika mradi huo, Mawaziri hao  ambao kwa kawaida hukutana kila baada ya miezi Sita, wameamua kufanya vikao vya dharura kila itakapohitajika ili kuhakikisha kuwa yale wanayoaagiza yanatekelezwa kwa ufanisi.

UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE TANZANIA (TWPG) WAJADILIANA KUHUSU UJENZI WA VITUO KWA AJILI YA WANAWAKE WANAOHASIRIKA KINJISIA

$
0
0
 Mwenyekiti Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta (katikati)akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa umoja huo (hawapo kwenye picha) wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Mhe. Susan Lyimo na Katibu Mhe. Lolensia Bukwimba
Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia, Bajeti kwa Mtazamo wa kijinsia na Haki za Binadamu, Ndg. Gemma Akilimali akizungumza na wajumbe wa Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Muwezeshaji kutoka TGNP, Ndg. Zainab Mmary akizungumza na Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Mjumbe Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Zainab katimba akizungumza na wajumbe wa umoja huo pamoja na wawezeshaji kutoka TGNP wakati wa semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
 Viongozi kutoka Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakiwa katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyekiti Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG), Mhe. Margaret Sitta, wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo, Mhe. Susan Lyimo, Katibu Mhe. Lolensia Bukwimba (kulia) na Mratibu, Ndg. Angelina Sanga.
  Wajumbe Umoja wa Wabunge wanawake Tanzania (TWPG) wakiwa katika semina ya kushauriana na kujadiliana kujenga vituo kwa ajili ya wanawake wanaohasirika kijinsia iliyofanyika leo tarehe 5 februari, 2019 katika ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

WABUNGE WA EALA WATOA ELIMU YA MTANGAMANO WA EAC

$
0
0

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Abdallah Makame na Katibu wake, Mhe. Josephene Sabastian wakiwa katika kikao na Wbunge wenzzao wa Tanzania, maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bunge la EALA na Trade Mark East Africa katika Hoteli ya Serena. Mkutano huo ni maandalizi ya zoezi la siku nne la kutoa elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzaia tarehe 04 hadi 07 Februari 2019 jijini Dar Es Salaam. 
Mhe. Habib Mnyaa, Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Marym Ussi wakishiriki kikoa cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Pamela Maasay (kulia) na Mhe. Happiness Legiko wakifjiandaa kukutana na wadau mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu ya Mtangamano. 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambao Wizara yao ndio mratibu w mauala ya Mtangamano wakiwa katika kikao cha maandalizi cha kutoa elimu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Maafisa kutoka Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika kikao cha maandalizi ya zoezi la kutoa elimu kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Mhe. Dkt. Abdallah Makame akitoa maelekezo kwa Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa dawati la Bunge. 
Kikao kinaendelea 

Mkutano wa Waandishi wa Habari
katkik
Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuwaeleza zoezi walilopanga la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya AAfrika Mashariki.
Waandishi wamefurika kusikiliza Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu zoezi la kuelimisha wadau kuhusu Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 
Waheshimiw wabunge (kushoto) na wandihi w habari wkiendelea na mkutano wao. 

Bandari ya Dar Es Salam 
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar Es Salaam akiwakaribisha Wabunge wa EALA katika Bandari ya Dar Es Salaam. Waheshimiwa Wabunge walienda Bandari ya Dar Es Salaam kuona maboresho yanayofanywa na bandari hiyo pamoja na kusikiliza wadau wanotumia bandari hiyo changamoto wanaokutana nazo. 
Waheshimiwa Wabunge walienda kutembelea gati namba moja ambalo ni moja ya mageti ynayofnyiwa maboresho makubwa. 

Siku ya Kuzaliwa
Mheshimiwa Maryam akisherehekea Siku yake ya kuzaliwa tarehe 04 Februari kwa kuwalisha keki Wabunge wenzake. 
Happy Birthday kwa Mhe. Maryam Ussi kutoka kwa Mhe. Fancy Nkuhi.

Misri yakubaliana na Tanzania kujenga kiwanda kikubwa cha nyama na ngozi

$
0
0
Na. Saja Kigumbe

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema serikali za Tanzania na Misri zimekubaliana kuanzishwa kwa kiwanda kikubwa cha nyama na mazao ya ngozi hapa nchini.

Waziri Mpina amebainisha hayo jana Februari 5,2019 ofisini kwake jijini Dodoma mara baada ya kupata ugeni kutoka nchini Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit.

“Tunaenda kujenga kiwanda kikubwa cha kusindika nyama, cha kusindika ngozi, cha kusindika mazao ya ngozi, kiwanda ambacho hakipo katika nchi hizi zote za Afrika ya Mashariki na Kati.” Alisema Mhe. Mpina

Waziri Mpina amemuhakikishia waziri huyo wa Misri kuwa rasilimali za mifugo na uvuvi zilizopo nchini zipo salama na kwamba wizara imekuwa ikifanya jitahada kuhakikisha samaki hawavuliwi kwa njia haramu na hakuna biashara haramu ili kuhakikisha rasilimali hizo zinanufaisha viwanda vya ndani na wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta hizo.

Aidha Waziri Mpina amemuarifu Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit kuwa hakuna mifugo inayoruhusiwa kuingia nchini kutoka nje ya nchi bila ya kuwa na vibali na kuwa usimamizi wa nchi katika rasilimali za mifugo na uvuvi uko salama.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, makatibu wakuu wa wizara hiyo pamoja na manejimenti ya wizara.
Waziri wa Kilimo wa Misri Prof. Ezzaldin Aboussteit (kulia) akifafanua jambo katika kikao hicho huku akisiskilizwa kwa makini na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallaha Ulega na wajumbe wengine hawapo pichani
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina (wa tatu kushoto) akizungumza ofisini kwake baada ya kutembelewa na ujumbe kutoka Misri ukiongozwa na Waziri wa Kilimo wa nchi hiyo Prof. Ezzaldin Aboussteit

MABADILIKO YA BEI ZA NISHATI YA MAFUTA

$
0
0
Bei za mafuta yanayopitia bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa mwezi wa pili mfululizo na kufikia shilingi 2,120 kwa lita moja ya petroli, 2,080 kwa dizeli na 2,046 kwa mafuta ya taa. 

Kwa kila lita kumekuwa na punguzo la shilingi 175 kwa petroli, shilingi 144 kwa dizeli na shilingi 156 kwa mafuta ya taa, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nistahi na Maji (EWURA) iliyotolewa jana mjini Dodoma. Bei hizo zitaanza kutumika kesho tarehe 6 Februari, 2019. 

Hii ina maana pia kwamba kwa mwezi Januari na Februari 2019, bei za rejareja za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa jumla ya Shilingi 316, Shilingi 356 na Shilingi 323, mtawalia.
Taarifa hiyo imeeleza pia kwamba bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Tanga zitaendelea kuwa zile za mwezi uliopita kwa sababu hakukuwa na shehena mpya. 
Hali kadhalika, bei za mafuta yaliyopitia bandari ya Mtwara zitaendelea kuwa zile zile zilizotangazwa Januari 25 2019, ambapo petroli ilipungua kwa shilingi 271 na dizeli shilingi 221 kwa lita.    

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, 
EWURA.  


DKT. KIJAJI - UTARATIBU UFUATWE ILI KUFUNGUA KITUO CHA FORODHA MANDA

$
0
0
Na Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali imemtaka Mbunge wa Ludewa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Njombe kuandaa andiko la kuwasilisha Serikalini katika hatua ya kufungua Kituo kipya cha forodha katika bandari ya Manda iliyopo katika Ziwa Nyasa.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Ludewa Mhe. Deogratias Ngalawa, aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanzisha Kituo cha Forodha katika bandari ya Manda, ili kurahisisha huduma kwa wananchi wanaokwenda nchi jirani hasa kwa shughuli za biashara.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, utaratibu wa kufungua kituo kipya cha forodha unatakiwa kuzingatia Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Mwaka 2004, ambayo inaitaka nchi mwanachama kuwasilisha kwenye Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki maombi ya idhini ya kuanzisha kituo kipya cha forodha na hatimaye kutangazwa kwenye gazeti la Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kupata nguvu ya kisheria.

“Mchakato wa ndani wa kuwasilisha maombi ya kufungua kituo kipya cha forodha unaanza katika ngazi ya mkoa ambapo mkoa unatakiwa kuwasilisha maombi ya kufungua kituo kipya cha forodha katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa baada ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujiridhisha itamfahamisha Kamishna Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kufanyia kazi maombi husika kwa kuzingatia sheria ya forodha ya afrika ya mashariki na hatimaye kuwasilisha maombi hayo kwenye sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

WATENGENEZA RISITI BANDIA ZA EFDS WADAKWA JIJINI DODOMA

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

$
0
0


Job Announcement at the Commonwealth Secretariat



The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Business Analystavailable at the Commonwealth Secretariat.



In line with the Comonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.


Application details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobs. Closing date for application is Sunday 17th February, 2019.


Issued by;

Government Communication Unit,

Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,

Dodoma.

6th February, 2019.

UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO (SIDO)

UJENZI WA DARAJA LA MBEZI LINALO WAUNGANISHA WAKAZI WA SALA SALA NA KINZUDI KUMALIZIKA HIVI KARIBUNI.

$
0
0


Mafundi wa kampuni ya Kika Constractions co. LTD ya jijini Dar es Salaam, wakiendelea na ujenzi wa daraja la mto Mbezi litakalo waunganisha wakazi wa Salasala Wilaya ya Kinondoni na wakazi wa Kinzudi wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam. Likiwa katika hatua kuelekea kukamilika wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakipata shida ya usafiri wakati wa kipindi cha masika kiasi cha kuwafanya wanafunzi kukosa kwenda shule. (Picha na Albart Jackson)
Ujenzi wa daraja hilo ukiendelea



Kauli ya Serikali kuhusu Mauaji na Utekaji wa Watoto Mkoani Njombe

Mkazi wa Keko na mkewe wavuna milioni 10 za Biko

$
0
0
Na Ripota Wetu, Dar es Salaam.
 
Mkazi wa Keko jijini Dar es Salaam, Yusuph Julla, ameibuka na ushindi wa sh milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya biko, huku akimchagua mke wake Mwanaidi Salumu kuwa mpendanao wake kutokea kwenye vuna fedha za wapendao.

Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam, kwa kuwakabidhi chao wapendanao hao wenye maskani yao Keko wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ili waendelee na harakati zao za kimaisha.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Julla aliishukuru Biko kwa kumpatia fedha zake mapema akisema kuwa fedha hizo zitawanufaisha yeye na mkewe kwenye familia yao hiyo.

Kucheza Biko sasa ni kuanzia sh 500 na sh 1000 na kuendelea, huku ushindi wake ukianzia sh 1000 hadi sh 100000 kwa watakaocheza sh 500 hadi sh 9500 wakati  watakaocheza kwa sh 1000 na kuendelea, mchezaji anaweza kujishindia zawadi ya papo kwa hapo kuanzia sh 5000 hadi sh milioni moja bila kusahau wote kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili.

Bahati nasibu ya Biko inachezwa kwa mitandao ya simu minne ambayo ni Tigo Pesa, M-Pesa, Artel Money na HaloPesa, ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu namba 2456, huku Watanzania wakiweza kujishindia zawadi kubwa katika droo ya Jumatano na Jumapili.
 Mshindi wa sh milioni 10 kutoka Bahati nasibu ya Biko, Yusuph Julla, akiwa na mkewe baada ya kukabidhiwa fedha zake za ushindi kutoka kwenye bahati nasibu hiyo huku Julla akimtaja mkewe Mwanaidi Salimu kuwa mpendanao wake hivyo kugawana fedha hizo kwa pamoja kwa ajili ya kufanyia mambo ya kimaendeleo. Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi huku washindi wa droo kubwa wakipatikana Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo.

 

MKURUGENZI MKUU TBC ASIFU UHUSIANO WAKE NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Utangazaji ( TBC) Dkt. Ayub Rioba akibadilishana mawazo na Mawakili wa Serikali Obadia Kajungu na Anna Mkongwa wakati alipotembelea Banda la Maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Mkurugenzi Mkuu amesifu uhusiano na ushirikiano mzuri wa kikazi kati ya TBC na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.



Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Dr. Ayoub Rioba, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Utangazaji ( TBC), amesifu na kupongeza ushirikiano mzuri anaoupata kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Amesema, uhusiano wa kikazi kati ya Taasisi hizi mbili, umekuwa na tija katika utekelezaji wa majukumu ya Chombo hicho cha Taifa cha Habari na kwamba, ni matumaini yake uhusiano huo utaendelea kwa maslahi na maendeleo ya Taifa. 

Ameyasema hayo siku ya Jumanne, wakati alipotembelea Banda la maonesho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere ‘ Square’, Jijini Dodoma 

“ Hongereni sana kwa maonesho haya. Mimi niwashukuru sana kwa ushirikiano na mahusiano mazuri ambayo tunayo na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Hasa katika eneo la mikataba. Sisi kama Chombo cha Habari cha Serikali tunaitegemea sana Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kwa ushauri wa kisheria na upitiaji wa mikataba yetu ya kibiashara” akasema Mkurugenzi Rioba 

Na kuongeza “ Kwa mazingira ya kazi zetu, na hasa pale tunapohitaji kununua vifaa au mitambo ya radio au televisheni ni lazima tulete mikataba yetu kwenu ili iweze kupatiwa ushauri wa kisheria. Kwa hiyo upitiaji wa mikataba yetu na kutolewa kwa wakati ni jambo lenye tija kwetu na katika utekelezaji wa majukumu yetu kwa maneno mengine sisi ni wadau wenu”. 

Akatoa mfano kwa kusema pala kifaa kinapo haribika labda kwa kupigwa na radi ni wazi kwamba mchakato wa kukinunua ukiwamo mkataba lazima ufanyike na uhusishe Ofisi yenu, na uharaka wa ununuzi wa kifaa hicho na kwa kuwa radio au televisheni haiwezi kutokuwapo hewani kwa muda mrefu ndiyo maana kutoka na unyeti huo hata mchakato wake unabidi uwe wa haraka lakini kwa kuzingatia matakwa ya kisheria. 

Mawakili wa Serikali, Obadia Kajungu na Anna Mkongwa waliokuwa wakitoa huduma za ushauri kwa wageni waliokuwa wakifika katika Banda la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, walimshukuru Mkurugenzi Mkuu wa TBC kwa kufika katika banda hilo. 

“Tunakushukuru kwamba unaridhishwa na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo baina yetu. Ushauri ulioutoa hasa wa upitiaji wa mikataba na kuitoa kwa wakati tutauzingatia na kuufisha ngazi za juu. Tukushukuru pia kwa kututembelea katika banda letu na kujielimisha kuhusu majukumu na utendaji kazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu” akasema Wakili Obadia Kajungu. 

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ikiwa ni Mdau wa Mahakama ilishiriki maonesho hayo yaliyoanza Januari 31 na kukamilika Februari Tano. Huduma zilizotolewa na Mawakili wa Serikali kwa wageni waliofika kwa shinda mbalimba ni pamoja na, kutoa ushauri wa kisheria, kujibu na kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto za kisheria ambazo baadhi ya wageni walikuwa nazo, kuelezea na kufafanua nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ujumla. 

Baadhi ya wageni walielekezwa wapi au Taasisi gani wanapashwa kwenda kupata msaada ziadi wa shida zao. Pia Mawakili wa Serikali hao walitoa huduma ya uelimishaji kwa wanafunzi wa sekondari na Vyuo Vikuu waliofika au kupangiwa katika banda la Mwanasheria Mkuu ikiwa ni sehemu ya mfunzo . 

WAUGUZI WANNE KITUO CHA AFYA MKOANI WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOA LUGHA CHAFU KWA MGONJWA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 


SERIKALI mkoani Pwani pamoja na idara ya afya mkoani humo,imewasimamisha kazi wauguzi wanne katika kituo cha afya kiitwacho Mkoani ,baada ya kudaiwa kutoa lugha chafu kwa mama aliyempeleka mtoto wake aliyekuwa amekwamwa na chaki kooni. 


Aidha mkoa huo imeelekeza fedha kiasi cha sh. milioni 400-500 zinazopelekwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya zitumike vizuri bila ubabaishaji. Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo aliyasema hayo, wakati alipotembelea kituo cha afya cha Matimbwa kata ya Yombo, Bagamoyo kuangalia ujenzi unavyoendelea,na kusema wauguzi hao ni wale waliokuwa zamu siku ya tukio . 

Alisema, wauguzi hao wamewasimamisha wiki iliyopita na tayari wameandika barua za kujieleza ,ambapo vimeundwa vyombo vya uchunguzi kujua chanzo na ukweli wa jambo hilo. Ndikilo alisema, endapo wakibainika kuhusika na kitendo hicho hatua itachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine .

"Baada ya kufikishiwa malalamiko hayo kutoka kwa mama wa mtoto, nilikutana na mganga mkuu wa mkoa, katibu afya, mkurugenzi wa halmashauri na muuguzi mkuu kujadili suala hilo na kuchukua hatua za awali ""Wahusika wameandika barua za kujieleza, na kati ya hao wengine tumegundua mafaili yao yanaonyesha kupewa onyo mara kadhaa kutokana na tabia hiyo hiyo. "alifafanua Ndikilo. 

Mkuu huyo wa mkoa, alieleza serikali inaelekeza nguvu zake kuboresha huduma za afya kwa kutoa mabilioni ya fedha, hivyo vituo vya afya vyote viendane na utoaji wa huduma bora. Nae mganga mkuu wa mkoa wa Pwani, dokta Gunini Kamba alisema inadaiwa mama huyo alipoona karushiwa maneno makali na wauguzi hao aliondoka kwenda hospital nyingine na baadae aliamua kwenda kutoa malalamiko hayo ambayo yameanza kuchukuliwa hatua hizo. 

Alitoa onyo kwa watumishi na wauguzi wa afya ambao wanakiuka taratibu na maadili waliyopatiwa. 
 Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo

Mradi wa umeme wa maji wa Rusumo(MW 80) kukamilika Februari 2020

Waziri Lukuvi Akata Mzizi wa Fitna Suala la Kufuta Mashamba

ZERO 68 KATIKA SHULE YA SEKONDARI HASSANAL DAMJI ZAMCHEFUA RC NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amechukizwa na matokeo ya kidato cha nne shule ya sekondari Hassanal Damji, kata ya Magomeni, Bagamoyo kwa kupata zero wanafunzi 68 na utoro uliokithiri .#

Kutokana na matokeo hayo ametoa miezi miwili kwa mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, watendaji wa mitaa, kata na vitongoji kufuatilia chanzo kilichosababisha wanafunzi hao kufeli kiasi hicho wakati shule hiyo ina walimu 57 ambao wanatosha.

Akizungumza na viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule hiyo, wakati wa ziara yake mkoani hapo, Ndikilo alisema ameudhika na matokeo hayo hivyo kuna kila sababu ya kuchukua hatua mapema. 

Aliwaasa wanafunzi hao kuacha pia utoro na kupotelea vichakani muda wa masomo ili kuinua taaluma zao. Ndikilo aliwaambia, waache kuchezea elimu kwani ni msingi na ufunguo wa maisha yao baadae. 

"Mnakunywa uji shuleni, walimu wapo wa kutosha, kwanini wanafunzi wahaudhurii masomo??? 

"Namba hii sio ya kufurahisha, division one hakuna hata mmoja, division two ni wanafunzi 2,division three ni wanafunzi sita,na Four wapo 72, na zero 68 ufaulu huu lazima tuuchukulie hatua ili wanafunzi waweze kufaulu zaidi "alisisitiza Ndikilo. 

Awali mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa alisema utoro shuleni hapo upo kwa asilimia 15 jambo ambalo sio zuri. Alisema amejipanga kuanzisha kampeni ya TOKOMEZA UTORO ili kuondoa changamoto hiyo mashuleni.
 
MKUU wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo
 mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images