Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 270 | 271 | (Page 272) | 273 | 274 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Viongozi mbali mbali, wakipata maelezo ya ujenzi wa Barabara za Wilaya ya Wete,zikiwemo Kipangani-Kangani,Chwale-Likoni,na nyengine zinazojengwa kwa ufadhili wa Shirika la MCC la Marekani,kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu,Injinia R.D.Sharma,wa kampuni ya Lea Associates south Asia PVT,wakati wa ziara ya Wilaya ya Wete Pemba.

   Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza pamoja na wananchi wa Mzambarau Takao,baada ya kupata taarifa za Ujenzi wa Barabara za Wilaya ya Wete zinazojengwa na mfuko huo jana akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi  wa Mzambarau Takao,alipokuwa katika ziara ya kuzitembelea Barabara zilizojengwa na Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC   katika Wilaya ya Wete , Mkoa wa Kaskazini Pemba jana,(kulia ya Rais ) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ,Haji Omar Kheir.
  Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0


  The Leed Central Seventh-day Adventist church is organising a Special Day of Prayer for the Philippines at 169 Meanwood Road, Leeds LS7 1JW, on the 23rd of November 2013 to remember Philippines and all those who were affected by the Typhoon Haiyan.
  A special collection will be made for ADRA, a charity working in the Philippines at the moment. 
  The service will begin at 11am-1pm, which will be followed by fellowship meal in the church hall.
  We would like to extend this invitation to you and request that if possible, we could have your presence at the occasion. 
  Please pass the message along and if you can't make it, then join us in prayer on the day wherever you are.
  Regards,
  Pastor Ikwisa Mwasumbi  0 0
 • 11/19/13--18:24: Article 12


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jestina Mhagama mara baada ya kuwasili katika eneo la Seminari Kuu wilaya ya Peramiho.
   Wanachama wa shina namba 28 wakishangilia hotuba ya  Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua uhai wa chama katika Mkoa wa Ruvuma.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi na wananchi wa Peramiho wakishiriki kubeba matofali ya ujenzi wa Zahanati ya Kahegwa,Kinana aliahidi kutoa mifuko ya sementi 100 pamoja na bati 100 kukamilisha suala la ujenzi wa zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wananchi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jenista Muhagama ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na wakikata utepe wa kufungua jengo la Zahanati ya   Lusonga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Peramiho ambapo aliwapongeza kwa kuwa wakulima wazuri wenye kujituma kwa juhudi kubwa katika suala zima la kilimo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Peramiho ,wilaya ya Songea Vijijini  mkoani Ruvuma.
   Mbunge wa Jimbo la Peramiho  Ndugu Jestina Muhagama akihtubia wakazi wa Peramiho na kuzungumzia kero sugu zinazowasunbua wananchi wa jimbo lake, hasa ukosekanaji wa Pembejeo na kutolipwa pesa wanayoidai serikali kwa wakati.

   Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tarafa Ndugu Salima Mapunda baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizindua rasmi mradi wa umeme wa Berega.Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amezindua mradi mkubwa wa umeme uliopo katika kata Barega iliyopo katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro. Aidha alitembelea miradi mingine inayotekelezwa na MCC na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wananchi. Pia alitembelea nyumba ambayo amewahi kuishi mwaka 1979 wakati akifanya utafiti wa miamba huko Kibaoni katika wilaya ya Mvomero ikiwa ni pamoja na kuonana na mwenyeji wake ambaye wameishi katika nyumba moja mwaka 1979-
   Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa umeme wa Berega. Mradi huu umefadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
   Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo akisoma  taarifa ya hali ya umeme katika wilaya ya Kilosa kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
   Wakazi wa kata ya Berega iliyopo katika wilaya ya Kilosa wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ( hayupo pichani).

  0 0


  0 0


  0 0
 • 11/19/13--20:00: IN LOVING MEMORY
 • Our dearest father Nehemiah Mushi, It is six years now since you suddenly left us on 20/11/2007. 
  Years have passed but whenever we remember you it feels like yesterday you passed away. 
  No one can fill the gap you left but God who loved you more gives us comfort and consolation when hardship confront us.
  You were a great man, a friend, a teacher and most of all a loving father and husband.The love, vision and values that you instilled in us have been guiding pillars in our lives. 
  You are missed and remembered by your loving wife, your children, your brother, sisters, close relatives, neighbors and friends
  2 Timothy 4:7-8

  0 0


  0 0

  SHIRIKA LA MAJISAFI NA MAJITAKA DAR ES SALAAM (DAWASCO) LINAHIMIZA WATEJA WAKE WOTE KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM, MIJI YA KIBAHA NA BAGAMOYO KULIPA BILI ZAO KWA WAKATI NA KABLA MWEZI HAUJAISHA.

  MTEJA ULIYETUMIA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA, NENDA SASA KALIPIE KABLA HUDUMA HIYO HAIJASITISHWA NA WAKAGUZI WANAOPITA NYUMBA KWA NYUMBA.

  ZOEZI LA USITISHWAJI WA HUDUMA YA MAJI LIMEANZA RASMI NA LITAHUSISHA WAKAZI WOTE WANAOHUDUMIWA NA DAWASCO.

  KUMBUKA PINDI UTAKAPOSITISHIWA HUDUMA HII GHARAMA YA KURUDISHIWA NI TSH 15,000/ = KWA WATUMIAJI WA MAJUMBANI NA TSH 50,000/= KWA TAASISI NA MAKAMPUNI. EPUKA USUMBUFU LIPIA HUDUMA HII SASA.

  MALIPO YAFANYIKE KUPITIA:

  LIPA BILI YA MAJI KUPITIA BENKI ZA CRDB- 01J1021921900, NMB-20103300047, BARCLAYS- 0014003711 NA BOA-02022460009; MPESA, TIGOPESA, AIRTEL MONEY NA EZYPESA; MAXMALIPO NA SELCOM; AKIBA MOBILE, EXIM MOBILE, NMB MOBILE NA TPB POPOTE; ATM ZA UMOJA SWITCH.

  LIPA BILI YAKO YA MAJI UKIWA MAHALI POPOTE NA KWA WAKATI WOWOTE
  DAWASCO IMESOGEZA HUDUMA KARIBU NA MTEJA

  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
  DAWASCO MAKAO MAKUU

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa maji wa Moivaro na Mlangirini wilayani Arumeru akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo Novemba 19, 2013. Kushoto ni mkewe Mama Tunu Pinda.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee kabla ya kuzindua mradi wa maji wa Moivaro na Mlangirini wilaya Arumeru akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo Novemba 19, 2013. . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Na Ally Kondo, Kuwait

  Serikali ya kuwait imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni moja (1) kwa ajili ya kuzipatia nchi za Afrika mikopo ya masharti nafuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Tangazo hilo lililotolewa na Amir wa Kuwait ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Tatu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Ushirikiano baina ya Nchi za Afrika na Kiarabu (Third Afro Arab Summit), Sheikh Sabah Al-Ahnad Al-Sabah wakati alipokuwa anatoa hotuba ya ufunguzi ya mkutano huo nchini Kuwait siku ya Jumanne tarehe 19 Novemba, 2013.

  Sanjari na kiasi hicho cha fedha, Sheikh Al-Sabah alitangaza kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni moja (1) kwa ajili ya kufadhili shughuli mbalimbali za utafiti zenye lengo la kuibua fursa za maendeleo katika nchi za Afrika.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  The Counsel to the Community, Hon Wilbert TK Kaahwa contributes to a motion on the ATNR Report on Investments in Agriculture.
  Hon Emerence Bucumi makes her contribution on the floor of the House.
  Hon Adam Kimbisa speaks addresses the House as other Members pay attention.

  EALA today resumed its Sitting in Nairobi and adopted the Report of the Committee on Agriculture, Tourism and Natural Resources on agricultural investments in the continent.

  In his remarks during the opening of the Session, Speaker of the Kenya National Assembly, Rt. Hon Justin Muturi urged the Partner States to uphold good governance through adherence to the principles of democracy, rule of law, accountability and transparency.

  Rt. Hon Muturi maintained that Kenya National Assembly would remain steadfast in its support for EALA as necessary to actualize the realization of the dream and mandate of bringing East Africans together.

  The Speaker of EALA, Rt. Hon Margaret Nantongo Zziwa hailed the Kenya National Assembly for its contribution to the EAC process.

  Article 49 of the Treaty for the Establishment of the EAC envisages the liaison with the National Assemblies of the Partner States on matters related to the Community.  


  0 0  Mafundi wa kampuni ya SMH/Rail ya nchini Malaysia wakiendelea na kazi ya kuunda upya moja wapo ya vichwa vya treni ambavyo vinaundwa kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro. Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi alitembelea karakana hiyo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Vichwa hivyo ambapo wamemuahidi kichwa cha kwanza kitakabidhiwa kwa Serikali mwanzoni mwa mwezi Disemba 2013.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akiongea na vibarua walioajiriwa na kampuni ya SMH/Rail kutoka nchini Malaysia, asubuhi alipofanya ziara kwenye karakana ya Reli mkoani Morogoro kuangalia maendeleo ya uundwaji upya wa Vichwa vya Treni vya Shirika la Reli Tanzania(TRL). Naibu Waziri huyo ameuagiza uongozi wa kampuni hiyo kuhakikisha kuwa vibarua hao wanapewa mikataba kama watafanya kazi zaidi ya miezi mitatu kama sheria za kazi zinavyowataka.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akioyeshwa mpango kazi wa kampuni ya SMH/Rail na Mhandisi wa Kampuni hiyo, Eng. Mohd Hisham(Kulia kwa Naibu Waziri) ambayo inaunda upya vichwa vya treni katika karakana ya Reli Mkoani Morogoro. Naibu Waziri ametembelea karakana hiyo leo Asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni ambavyo viko kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa kwenye sekta ya Uchukuzi.
  Naibu Waziri wa Uchukuzi akiongea na Naibu Mtendaji Mkuu, Uendeshaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Paschal Mafikiri (wa kwanza kushoto), wakati alipotembelea Karakana ya Reli Mkoani Morogoro, leo asubuhi kuangalia maendeleo ya undwaji upya wa vichwa vya treni. Kichwa cha kwanza kinategemea kukamilika mwanzoni mwa Mwezi wa Disemba 2013.

  0 0

  DSC05297
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (kushoto) akiwasili katika Hoteli ya New Palm Tree iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kufungua mkutano wa nne wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (COMNETA) akiwa ameongozana na wenyeji wake Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin (wa pili kulia), Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii ya Wilayani Karagwe ya FADECO Bw.Joseph Sekiku (wa pili kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa COMNETA ambaye pia ni Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Telecentre Sengerema FM mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye.
  Na.Mwandishi wetu
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni,(UNESCO), limeiomba Serikali kutambua mchango wa redio za jamii katika maendeleo nchini na hivyo kufanya nao kazi kwa karibu.
  Ombi hilo limetolewa jana na Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari na mratibu wa miradi ya UNESCO , Yusuph Al-Amin wakati wa mkutano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii nchini (Community Media Network of Tanzania – COMNETA)unaofanyika mjini Bagamoyo.
  Akizungumza kwenye mkutano huo, Al-Amin aliwapongeza COMNETA kwa kufanikiwa kuanzisha umoja huo ambao awali kulikuwa na vituo viwili tu vilivyokuwa vikitambuliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), huku kwa sasa vikifikia vituo zaidi ya 27, kwa nchi nzima ikiwemo Tanzania Bara na Visiwani.
  DSC05299
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Assah Mwambene akibadilishana mawazo na wenyeji wake kabla ya kufungua mkutano wa nne wa COMNETA unaoendelea Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  Akifafanua zaidi, Al-Amin alisema UNESCO imekuwa ukiisaidia COMNETA kufikia malengo yake kwa kutambua kuwa radio hizo zinafanya kazi katika jamii na zina uwezo mkubwa wa kuifikia jamii inayoizunguka.
  “Zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania wako vijijini na hawa wanafikiwa kwa karibu zaidi na radio jamii, kwa kupata taarifa za kina na za haraka” alisema Al-Amin.
  Alitoa mfano wa Radio ya jamii iliyoko Micheweni, Pemba ambayo uwepo wake umesaidia sana kuleta mabadiliko ya maendeleo wilayani hapo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma ambapo wilaya hiyo likuwa nyuma sana kimaendeleo.
  ‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema, Al-Amin. Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

   

  AllanKingdomTop10.jpg
                                                                    Allan Kingdom

  On a night that was essentially a spirited coming-out party for both GRRRL PRTY and Four Fists, the young MC Allan Kingdom (of Tanzanian origins)  damn near stole the show. Breaking out a slew of tracks from his vibrant recent release Talk to StrangersKingdom and his crew even overcame a laptop crashing in the middle of the performance and delivered a memorable set. Allan's buoyant stage presence and boundless lyrical talents can win over any crowd. His rhymes are imaginative as well as enlightened. The Twin Cities music scene has warmly embraced a series of local hip-hop stars who have gone on to break it big on a national and worldwide stage, and all signs point to Allan Kingdom being the next one.

  0 0


  The project is a comprehensive and informative resource that ranks each university in America by size, degrees offered, tuition costs, admission rates, graduation rates, and retention rates. 
  While entire institutions can earn regional accreditation to ensure that the school as a whole meets educational standards, specific departments and degree programs also pursue specialized educational accreditation for departments or degree programs.

  This type of information is valuable to today's students who are not only dealing with a more competitive higher learning environment but also with the rising costs associated with getting a diploma.  0 0
 • 11/20/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • 0 0


  BENDI za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao kutoka Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha kubwa la Gurumo 53 litakalofanyika mwezi huu.

  Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi Maalim Gurumo (pichani) litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe Jumamosi Desemba  14, 2013.

  Kwa mujibu wa kamati ya watu sita inayoratibu tamasha hilo, Gurumo anaagwa baada ya kutangaza rasmi kuachana na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.

  Mratibu wa kamati hiyo Juma Mbizo amesema kutakuwa pia na wasanii wa bongo fleva, vichekesho na sarakasi.

  Aidha Mbizo amesema tamasha litatanguliwa na bonanza la soka la maveterani.

  Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma ambayo hapo awali ilijulikana kwa majina ya NUTTA, Juwata na OTTU. Gurumo ameitumika Msondo katika majina yote ya nyuma.

  Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali Yahaya na Boniface Kachala, Benno Villa Anton, Tshimanga Kalala Assossa na Ibrahim Mwinchande.

  Baadhi ya wasanii wengine watakaotumbuiza ni Komandoo Hamza Kalala, Kassim Mapili, Hafsa Kazinja na Waziri Ali.


  Kamati ya Gurumo iko chini ya uenyekiti wa Asha Baraka, makamu ni Waziri Ali na katibu ni Said Mdoe huku mratibu akiwa Juma Mbizo, wajumbe ni Said Kibiriti na Richardson Sakala. 


  0 0
 • 11/20/13--19:30: KUMBUKUMBU

 • MARY JOHN MWINGIRA

  5.5.1946-21.11.2010

  Leo ni Miaka 3 tangu ulipotuacha hapa Duniani kwa simanzi kubwa tarehe 21.11.2010. Ni kama juzi kwetu mama, kidonda hakijapona kabisa, uchungu mkubwa ndani ya  nyoyo zetu zimetawala kila saa mama. Ulijua kifo chako na ulikuwa unatuonea huruma sana ukijua tutakavyoumia.
  ”Samahani na poleni wanangu” yalikuwa ndio  maneno yako kila mara na hatukuwa tunaelewa kwa nini ulikuwa unasema vile.
  Ulitufundisha kusali sala nyingi tukiwa wadogo na tunaamini  usemi wa Mapenzi ya Mungu yametimizwa mama.
  Tutaonana siku ya Mwisho Paradiso!!!

   Tunaaminini upo karibu na MUNGU  kama ulivyokuwa hapa duniani .Ujumbe  wako mkuu uliotuachia tunajitahidi kuuteleleza  na kuishi katika  hilo “Upendo usio na masharti kati yetu wanao na wanaotuzunguka”.
  Tunasema asante sana kwa malezi na maelekezo kuhusu maisha ambayo ulikuwa unatupa kila siku ukishirikiana na baba na ndugu na jamaa. Tunashukuru kwa Baraka za  MUNGU na  tunaamini kwa maombezi yako na baba tunamudu Maisha ya kila siku yaliyojaa Baraka tele.

  Sisi wanao, wajukuu,mama yako, wakwe, Wadogo zako, shemeji zako , ndugu na Jamaa wote tuakumbuka na Kuusifu wema wako usio na kipimo. Tunakuadhidi kuundeleza kwa nguvu zetu zote na daima hatutakusahau Mama yetu na Rafiki yetu Mary John Mwingira  Ustarehe kwa Amani mama yetu Mpendwa!

  AMINA

older | 1 | .... | 270 | 271 | (Page 272) | 273 | 274 | .... | 3272 | newer