Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 271 | 272 | (Page 273) | 274 | 275 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  (watatu kushoto) na baadhi ya viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa magugu na visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na vijana wajasiriamali katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,  alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari 500. Mbali na  kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa mchango wa kiasi cha shilingi milioni nne kwa ajili ya mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia).
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo yalitochukuliwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi pikipiki 50 zilizotolewa na mbunge kwenda kwa watendaji wa vijijini.
  Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga mjini, mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi, alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Aman Makolo waliojitokeza nyumbani kwa Balozi Hilda Komba wa shina namba 9 ,Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma.
   Wanachama wapya wa Tawi la Amani Makolo wilayani Mbinga wakila Kiapo cha Uanachama wa CCM mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye leo amefanya ziara katika wilaya ya Mbinga.
   Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma ya Mganda wakati akiwasili kwenye eneo la mkutano wilayani Mbinga.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimueleza Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose uzoefu wake wa kuendesha  pikipiki,kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga  Ndugu Senyi Ngaga.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mbinga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanika kwenye viwanja vya michezo vya Mbinga mjini ambapo aliwaeleza wananchi kuwa chama cha Mapinduzi kitasaidia kutoa ushauri kwa mazao ambayo bei yake inashuka na kupanda.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa Wilaya wa zamani Ndugu Osmund Kapinga.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mzee Osmund Kapinga Mkuu wa Wilaya mstaafu mara baada ya kukamilika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya michezo  vya Mbinga mjini mkoa wa Ruvuma.

  0 0

  DSC_1899
  Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji akibadilishana mawazo na aliyekuwa Rais wa Botswana Mh. Festus Gontebanye Mogae alipomtembelea rafiki yake Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji (katikati) ofisini kwake.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group Mh. Mohammed Dewji siku ya jana alipata nafasi ya kuzungumza na rafiki yake, aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae. 
  Mh. Mogae ambaye pia amewahi kuwa mshindi wa tuzo ya Mafanikio katika Uongozi itolewayo na mfanyabiashara mzawa wa Sudan Bwana Mo Ibrahim mwaka 2008, alikuwa na mazungumzo binafsi na Mohammed Dewji (Mo) alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar-es-salaam.
  Tuzo hiyo ya Mo Ibrahim, humuwezesha mshindi kupata kitita cha dola za Kimarekani millioni 5, na dola za Kimarekani 200,000 kila mwaka kwa maisha yake yote. Hizi ni baadhi ya picha, zilizopigwa na mpiga picha wetu  jana kwenye ofisi za MeTL Dar-es-salaam.
  president (1)
  Mh. Mohammed Dewji katika picha ya pamoja na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.
  DSC_1903
  Mwenyekiti wa MeTL Group Bw. Gulam Dewji kwenye picha ya kumbukumbu na aliyekuwa Rais wa Botswana (1998 hadi 2008) Mh. Festus Gontebanye Mogae.

  0 0

   Ibanda Ruhumbika born to Dr. and Mrs. Gabriel Ruhumbika of Ukerewe, Tanzania, is a world renowned, classically trained Jazz musician. He is a member of the Jonathan Baptiste and Stay Human Band which recently completed its European Tour. The band is set to embark on the second leg of their  US Tour starting this January. For more details on the band and tour schedule, please go to:
   At 22, Ibanda Ruhumbika is quickly becoming one of the most recognized tuba players in the United States. A native of Athens, Georgia, he has won numerous national and international music competitions, in addition to being featured on several nation-wide television and radio broadcasts. Ibanda has been a soloist with members of the New York Philharmonic Brass Section as well as with “The President’s Own” Marine Band. Classically trained, he is well versed in jazz and other styles of music. 
  He is a member of Jonathan Batiste and the Stay Human Band, where he is helping to revolutionize the role of the tuba in the modern-day jazz ensemble.


  0 0

   Mhe Job Ndugai,Naibu Spika akipokelewa kwa ngoma za kihabeshi wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa Bole jijini Addis Ababa,Ethiopia.Mhe Ndugai Yuki nchini Addis Ababa kuhudhuria mkutano wa Mabunge ya nchi za Afrikaans,Caribbean na Pacific ambapo anaongoza ujumbe wa Bunge la Tanzania unaojumuisha Mhe Mussa Zungu,Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje name maafisa wengine.
  Mhe Naibu Spika Ndugai akipewa neno la ukaribisho na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Bw.Ndatta katika uwanja wa ndege wa Bole jijini Addis Ababa. Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.

  0 0
 • 11/20/13--23:30: Article 14
 • In Loving Memory

  Rehema Chiponde Msilu

   22 May 1958 – 22 November 2012
  Our Dearest Mom, 
  God saw you were getting tired
  and a cure was not to be
  so he put His arms around you
  and whispered, "Come to Me".
  With tearful eyes I watched you,
  and saw you pass away.
  Although I loved you dearly....
  I could not make you stay.
  A golden heart stopped beating,
  hard working hands at rest.
  God broke my heart to prove to me
  He only takes the best.
  0 0
 • 11/21/13--01:38: bei ya Madafu leo

 • 0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete is flanked by Ministers of state in the Vice President's office Dr Theresia Huvisa (right) and Zanzibar's Minister of State in the Second Vice Predident 's office Hon Fatma Fereji President Kikwete at. The High Level Mineserial Dialogue on Durban Platform on enhanced Action under the Conference of the Parties.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisitiza jambo kwenye kikao hicho. Katika kikao hicho Balozi Alexandre Leveque ameahidi kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya gesi na mafuta kwa wawekezaji waliopo nje ya nchi.
  Balozi wa Canada Nchini Mhe. Alexandre Leveque (kulia) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo mara walipokutana kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kukuza ushirikiano baina ya Tanzania na Canada kwenye sekta ya gesi na mafuta.

  0 0

  Je umeshawahi kufikiria ni jinsi gani watu wananyohangaika kufika mtaani kwenu kama huo mtaa jina lake halieleweki au kukumbukika kirahisi? Chukulia mtaa wenu unaitwa "Kwa mporomosha matikiti", siyo tu hili jina ni refu, bali linajumuisha maneno ambayo yanachanganya sana "mporomosha" kwani sisi wengine tutaita "mpolomosha".

  Majina ya Website ama kwa kingereza wanaita "Domain Names", kama ilivyo anuani za mitaa au nyumba zina maana kubwa sana kwenye ulimwengu wa Website. Uchaguzi wake ni moja ya vitu muhimu sana katika maisha ya website, jina lisiloeleweka, siyo tu litaweza kumpa faida mpinzani wako, bali kuwachanganya wateja na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wako kwenye mtandao.


  0 0

  Asanteni kwa wote mlioshiriki katika shindano la MPENDEKEZE ASHINDE vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni Tano. 

  Jopo la majaji lilikutana na kuchagua kwa umakini kabisa watano bora. Hatua ya uhakiki imeanza tutawaomba kuwapigia kura hapa hapa mtandaoni watano bora ili kumpata mshindi ambaye atakuwa Mama Shujaa wa Chakula Mtandaoni kwa mwaka 2013. 

  Fahamu zaidi kuhusu Grow kwa kutembelea https://www.facebook.com/GrowTanzania

  Tazama video hii kufahamu sababu za Masoud Kipanya kuiunga mkono kampeni ya chakula ya GROW.

  0 0

   Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kushoto) akipeana mkono na Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Younqing wakati akipokea Msaada wa Pikipiki 20 zilizotolewa kwa Kampuni ya Uchapishaji wa Magazeti ya Serikali (Tanzania Standard Newspapers),wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo nje ya Jengo la Golden Jubilee,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN,Gabriel Nderumaki.

  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (kushoto) na Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Younqing wakiwa wamepanda pikikipi hizo ikiwa ni ishara ya kuzizindua kwa ajili ya Matumizi.Katikati yao ni Mwenyekiti wa Bodi ya TSN,Prof. Moses Warioba.
  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara akipanda kwenye moja ya pikipiki hizo.
  Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Younqing akizunzumza machache wakati wa hafla hiyo.


  0 0
 • 11/21/13--04:19: TAARIFA KUTOKA TFF LEO

 • 0 0

  Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw.. Peter Ngota akizungumza na kamati ya michezo kutoka DIT(hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa michezo sehemu za kazi na faida za michezo kwa afya zetu. Kushoto ni meneja rasililimali watu na mahusiano kazini Bw. Lawrence Thobias kulia meneja biashara Bw. Nicodemus Mngulu.
  Afisa Mkuu wa Mauzo na masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akikabidhi sehemu ya vifaa vya michezo kwa Mwenyekiti wa DIT Sports Club Dr. Simeon Rwandallah.
  Mwenyekiti wa DIT Sports Club Bw. Simeon Rwandallah akitoa neon la shukrani kwa Afisa mkuu wa mauzo na masoko baada ya kukabidhiwa vifaa vya michezo.
  wawakilishi kutoka Taasisi ya teknolojia Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Fidea Chale Mwenyekiti DIT Sports Club, Dr. Godwin Ndeki katibu - DIT sports club, L. Sombi Afisa utawala na rasilimali watu, Dr. Simeon Rwandallah Mwenyekiti wa DIT Sports Club, Zuhura Haruna mhazini Michezo DIT, na James Issack Katibu msaidizi Michezo DIT.

  0 0

  IMG_2247
  United Nations Resident Coordinator in Tanzania, Dr. Alberic Kacou speaks to invited dignitaries during the official launching of the Least Developed Countries Report 2013 today at the ILO conference room in Dar es Salaam.IMG_2252
  Ambassador Maral Namfua addresses the invited dignitaries and reporters during the official launching of the LDCs report 2013 which highlighted the challenges of employment and demographic increases in LDCs countries especially in Africa.IMG_2257
  United Nations Resident Coordinator in Tanzania, Alberic Kacou and Ambassador Maral Namfua and International Labour Organization Deputy Country Director Ms.Hopolang Phororo cuts a ribbon to officiate the LDCs report 2013 in Dar es Salaam at the ILO conference room.


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Ofisi kwake Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Sinikka Antila alipofika kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Tanzania na Finland zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na utawala bora.
  Mhe. Dkt. Maalim akimweleza jambo Mhe. Antila wakati wa mazungumzo yao.
  Mhe. Antila naye akifafanua jambo kwa Mhe. Dkt. Maalim wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bibi Victoria Mwakasege (kulia mwenye nguo ya njano), Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Ulaya na Amerika akifuatiwa na Bi. Upendo Mwasha, Afisa Mambo ya Nje. Kushoto ni Bw.Jussi Nummelin, Afisa katika Ubalozi wa Finland hapa nchini.

  0 0

   Kampeni ya Kili Nani Mtani Jembe itaendelea kuunguruma tena Jumapili wiki hii na kuwapa nafasi mashabiki wa Simba na Yanga walioko Dodoma, Musoma na Singida na kuchuana vikali katika michezo mbalimbali huku wakihakikisha timu zao zinaibuka na kitita cha shilingi milioni mia moja zilizotengwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya Watani wa Jadi kupitia kampeni hiyo.

  Mratibu wa mabonanza hayo, Lawrence Andrew amesema jijini Dar es salaam jana kwamba mashabiki watapata fursa ya kushiriki katika michezo mbalimbali kama vile foosball, kuvutana kamba, soka la wachezaji saba kila upande maarufu kama “Seven aside” na kuongeza kuwa ili kuhakikisha mashabiki hao wanafurahia ipasavyo burudani mbalimbali za muziki zitakuwepo pamoja na Nyama choma.  Andrew alisema kuwa katika mji wa mji wa Dodoma bonanza la Kili Nani Mtani Jembe litafanyika katika uwanja wa shule ya Dodoma Sekondari ambapo bendi maarufu ya The TNC Band itatumbuiza. Na huko Musoma bonanza litafanyika katika uwanja wa Mukonde na kupambwa na bendi ya Musoma Stars huku mkoani Singida likifanyika katika Uwanja wa Namfua na burudani kabambe ikishushwa na Wana Pamba Music Band aka Watoto wa Mujini bendi ambayo imejizolea umaarufu mkubwa sana mkoani humo.

  Andrew pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba mabonanza hayo ambayo yatafanyika katika mikoa hiyo kwa mara ya kwanza kupitia Nani Mtani Jembe. 

  Kampeni hii ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha mapenzi kwa timu zao.


  Mabonanza hayo yanalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo inafanyika nchi nzima ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia kampeni hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo zinashindaniwa na mashabiki wao.


  Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu nyingine.

  Akielezea namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna namba ya kushiriki.

  Alisema baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.

  Alisema baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 10,000 kutoka kwenye fungu la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi 10,000 kutoka kwa Simba.

  Kwa mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo Desemba 14, mwaka huu siku ambayo watani wa jadi Simba na Yanga watacheza mechi ya kuhitimisha kampeni hiyo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. 

  0 0


  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete addresses African Ministerial Conference on the Environment (AMCEN) Ministers and African Group of Negotiatiors (AGN) in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Warsaw National Stadium in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
  President Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with the Commissioner of Agriculture and Rural Economy of the Africa Union in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
  President Jakaya Mrisho Kikwete greets the Secretary General of the World Meteorological Organisation Mr Michael Jarraud as the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi looks on in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in Warsaw, Poland, November 21, 2013.
  President Jakaya Mrisho Kikwete poses with the Secretary General of the World Meteorological Organisation (WMO) Mr Michael Jarraud, Assistant Secretary General pf WMO Ms Elena Manaenkova and the Director General of the Tanzania Meteorological Agency Dr. Agnes Kijazi when they met in the margins of the UN Climate Change Conference (COP19/CMP9) at the Bristol hotel in in Warsaw, Poland, November 21, 2013.


  0 0

  Washiriki wa mbio za mitumbwi zinazodhaminiwa na bia ya Balimi Extra Lager wanawake Ukerewe wakianza rasmi mbio hizo zilizofanyika katika Ufukwe wa Monarch Ukerewe mwishoni mwa wiki.
  Mabingwa wa mbio za mitumbwi zinazodhaminiwa na bia ya Extra Lager,kikundi cha nahodha Mhete Muhoja wakiwasili katika ufukwe wa Monarch wakati wa mbio hizo zilizofanyika mwishoni mwa wiki.

  KIKUNDI cha Nahodha Totoji Mazinge Ngoroma kutoka Wilayani Ukerewe kimetwaa ubingwa wa mashindano ya mbio za Mitumbwi zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini kupitia Bia ya Balimi Extra Lager na hivyo kujitwalia zawadi ya fedha taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe katika mashindano ya Kanda yanayotarajiwa kufanyika jijini Mwanza hivi karibuni.

  Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Toto Sebastiani ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe pia katika fainali za Kanda pale jijini Mwanza ,nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Simon Fundi ambao walizwadiwa fedha taslimu shilingi 500,000

  Upande wa Wanawake kikundi cha nahodha mwanamama Mhete Muhoja nakujitwalia ubingwa na hivyo kuzawadaiwa fedha taslimu Shilingi 700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Kisiwa cha Ukerewe kwenye mashindano ya Kanda pale jijini Mwanza mwezi ujao.

  Nafasi ya pili upande wa wanawake ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Jenifer Elias na ambao walijinyakuliwa zawadi ya fedha taslimu shilingi 600,000/= pamoja na kuwakilisha kisiwa kwenye fainali za Kanda upande wa Wanawake pale jijini Mwanza,nafasil ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha nahodha Edna Chambo ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 400,000.

  Akizungumza na wananchi waliofurika kwa wingi katika ufukwe wa Monarch Galu Beach meneja mauzo wa TBL wilaya ya Ukerewe, Josephat Changwe amesema kuwa licha ya mchezo huo kuwa burudani Kampuni yake imenuia kuyaboresha mashindano hayo ili yapate sura ya kimataifa huku yakibadili maisha ya wananchi kama sehemu ya mitaji.

  Fainali za Kanda za mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Decemba 7,2013, katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo watashindana mabingwa wa Kanda nzima ambao ni kutoka Kigoma, Kagera,Ukerewe,Musoma na wenyeji Mwanza.

older | 1 | .... | 271 | 272 | (Page 273) | 274 | 275 | .... | 3284 | newer