Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 269 | 270 | (Page 271) | 272 | 273 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji.
  Kimbisa akizungumza na wanahabari Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
  wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephrahim Mafuru akitoa neno kwa wageni waalikwa(hawapo pichani)katika usiku wa Wanamasoko uliofanyika mwishoni mwa wiki katika hotel ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wageni waliohudhuria Marketers Night Out
   Wageni waalikwa walipata nafasi kuonja na kufurahia bidhaa za Kampuni ya bia ya Serengeti, mmoja ya wageni akimiminiwa kinywaji cha Johnie Walker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti.
   Msemaji mkuu wa Marketers Night Steve Gannon ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti akitoa somo kwa wanamasoko waliohudhuria katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0
 • 11/18/13--11:35: SHUKURANI
 • MAREHEMU MRS MAUA MPANKULI


  Familia ya marehemu Maua Mpankuli tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Ndugu, Jamaa, Marafiki, Wafanyakazi, Majirani na watu wote kwa ujumla waliojitoa kwa hali na mali katika msiba wa mpendwa wetu aliyeaga dunia tarehe 1 Novemba, 2013 huko Uingereza na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania tarehe 9 Novemba, 2013.


  Tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa wafuatao:

  * Madaktari na wauguzi wote wa hospitali ya St James ya Leeds, Uingereza kwa jitihada zao kubwa za kujaribu kuokoa maisha ya marehemu.


  * Jumuiya ya Watanzania wote walioko Uingereza na sehemu zingine za dunia waliojitolea kwa hali na mali hadi kuweza kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka  Uingereza hadi Tanzania kwa mazishi.

  * Uongozi na waumini wa Kanisa la Christ Temple of Worship Leeds Uingereza kwa maombezi na ushikiano wao.

   * Uongozi na waumini wa Kanisa la RCCG la  Leeds, Uingereza kwa ushirikiano wao.
  * Uongozi na waumini wa Kanisa la Full Gospel Bible Church, Dar es Salaam kwa huduma za kiroho wakati wote wa msiba na katika mazishi ya marehemu.

  * Kampuni ya Hugh Gooding Funeral Services ya Leeds, Uingereza iliyoshughulikia kuusafirisha mwili wa marehemu kutoka Leeds hadi Dar es Salaam kwa mazishi.

  * Wafanyakazi wote waliowahi kufanya kazi na marehemu katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam.

  *Jamii na viongozi wa Issamichuzi blog. Asanteni kwa kuturuhusu Kutumia mtandao wenu.

  Tungependa sana kuwashukuru kila mmoja wenu kwa majina lakini kwa ajili ya wingi wenu tunaomba mpokee shukrani zetu hizi za kipekee kwa ujumla wenu.

  Mwenyezi Mungu awazidishie baraka zake nyingi kwa Huduma zenu mlizotoa. Asanteni sana.

  Waefeso 1: 15 – 16.


  15 Hii ndio sababu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana wetu Yesu, na juu ya upendo mlio nao kwa watu wa Mungu,16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu.


  0 0

  0 0

  Marehemu  John Mwankenja, enzi za uhai wake
  Kushoto Hakimu Mwakalinga ambaye ni mshtakiwa wa kwanza kuhukumiwa kunyongwa
  Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya mahakama wakisubiria matokeo ya hukumu. Picha na Ezekiel Kamanga, Mbeya yetu
  Washtakiwa wawili kati ya wanne  wa kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya.

  Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe chini ya Jaji Samweli Karua, baada ya kuahirishwa kutolewa kwa hukumu hiyo kwa zaidi ya mara tatu na kuzua hali ya sintofahamu kwa ndugu wa washtakiwa na wafuatiliaji wa kesi hiyo.

  Awali kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo Mwendesha mashtaka wa Serikali., Archiles Mulisa, aliwataja watuhumiwa wote wanne kuwa ni Hakimu Mwakalinga, Daudi Mwasipasa, Obote Mwanyingili na Kelvin Myovela wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa maksudi aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe John Mwankenja.

  Alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 131/2012 walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

  Mulisa aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali Lugano Mwakilasa kwa upande wa mashtaka huku  Watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili ambao ni Victor Mkumbe na Simon Mwakolo.

  Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa kesi inayowakabili  watuhumiwa hao walilitenda Mei 19,2011 kwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja kinyume na kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

  Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua ambaye alianza majira ya saa 14:37 mchana na kukamilisha saa 15:37 alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka na utetezi haubishaniwi kuhusu kifo cha marehemu.

  Aliongeza kuwa pande hizo mbili pia hazibishaniwi kuhusu ripoti za kitaalamu na dhamira za mauaji hayo bali kinachobishaniwa ni uhusika wa watuhumiwa hao dhidi ya mauaji hayo.

  Alisema katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulileta mashahidi 11 ambao wote kwa pamoja  wakiongozwa na shahidi namba moja waliwatuhumu washtakiwa kuhusika na tukio hilo.

  Shahidi huyo namba moja Weston Jacob(17) mkazi wa Kiwira Mwanafunzi kidato cha Tatu katika shule ya Sekondari Kipoke ambaye pia ni Mjomba wa marehemu ambaye aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio akiwa nyumbani akijisomea majira ya 2: 30 usiku ambapo marehemu alifika nyumbani na kupiga honi ya gari akitaka afunguliwe mlango.

  Mbali na ushahidi huo Jaji Karua alisema pamoja na ushauri wa wazee wa baraza la mahakama ambao pia wanawatuhumu washtakiwa hao kuhusika na tukio hilo nae anakubaliana nao lakini siyo kwa watuhumiwa wote.

  Kutokana na ushahidi huo alisema Mshtakiwa namba moja na namba mbili ambao ni Hakimu Mwakalinga na Daudi Mwasipasa wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa moja na mauaji kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua maelezo na  vipimo vya vinasaba.

  Alisema Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye anatiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji hivyo yeye hausiki moja kwa moja na kosa hilo.

  Jaji karua alisema kwa upande wa mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela anatiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika nkatika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja.

  Aliongeza kuwa kutokana na kifungu cha sheria cha mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba 300 na 217 washtakiwa namba tatu na namba nne wanatiwa hatiani na mahakama.

  Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa, aliiambia mahakama hiyo kwamba itoe adhabu kali kutokana na kitendo alichofanyiwa marehemu na iwe fundisho kwa watu wengine.

  Kwa upande wa utetezi ambao siku ya hukumu uliwakilishwa na Wakili Merick Luvinga alisema mahakama iwanee huruma washtakiwa kwa kuwa wote umri wao ni mdogo wanaweza kujifunza na kurudi kuungana na jamii pia ni kosa lao la kwanza hivyo wasipewe adhabu kali.

  Kutokana na utetezi huo, Jaji Karua alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika pasipo shaka kwa washtakiwa namba moja na namba mbili hivyo adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa.

  Aliongeza kuwa Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili anayehusika kumhifadhi mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka saba kwa kosa hilo sambamba na mshtakiwa namba nne  Kelvin Myovela aliyehifadhi silaha iliyotumika kwenye mauaji.

  Alisema kutokana kosa hilo mtuhumiwa huyo atatumikia kifungo jela miaka saba ingawa pia tayari alikuwa amehukumiwa kifungo jela cha miaka 20 kwa kosa la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

  Wakati huohuo

  MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 35 mtuhumiwa wa mauaji dhidi ya watoto huku mwingine akiachiwa huru baada ya kukutwa bila hatia.

  Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya Samweli Karua mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa katika vikao vilivyofanyika katika Mahakama ya wilaya ya Rungwe.

  Awali mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakama kuwa washtakiwa Baraka Mwandibwa na Zuberi Lwila walifikishwa mahakamani hapo wa kosa la kumlawiti na kumuua mtoto Esta James(5) Novemba 21, 2010.

  Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 196 (16) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambalo walilifanya katika kijiji cha Bulyaga Wilayani Rungwe baada ya kumteka mtoto huyo.

  Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua alisema Mshtakiwa namba moja anatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambao ulitoka kwa shahidi namba moja ambaye ni mtoto aliyejulikana kwa jina la Marietha.

  Alisema mtoto huyo ambaye alisema siku ya tukio alikuwa akicheza na marehemu ambapo mtuhumiwa alifika na kumpa pipi aina ya Ivory marehemu kisha kuondoka naye ambapo shahidi huyo aliwerza kumtambua mtuhumiwa katika gwaride la utambuzi.

  Mbali na hilo alisema ushahidi mwingine ni ushaidi wa Vinasaba ambao unawahusisha moja kwa moja watuhumiwa wote wawili ikiwa ni pamoja na ushaidi wa kimazingira unaomhusisha mtuhumiwa wa kwanza.

  Alisema kutokana na ushahidi huo Mtuhumiwa wa kwanza anahusika moja kwa moja na mahakama inamtia hatiani ingwa kwa mujibu wa ushahidi hakuua kwa makusudi kutokana na kutokuwa na vifaa vya mauaji kama visu panga na silaha zingine.

  Alisema katika mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa unadamu na mbegu za kiume sehemu zake za siri na hakuwa amejeruhiwa nsehemu yoyote, hivyo mahakama iliona mtuhumiwa hakuua kwa kukusudia bali ilikuwa ni bahati mbaya.

  Hata hivyo upande wa Mshtaka uliomba mahakama itoe adhabu kubwa na kali dhidi ya washtakiwa kutokana na mazingira aliyofanyiwa mtoto huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za kuwalaghai watoto wadogo.

  Akitoa hukumu hiyo Jaji karua alisema anakubaliana na ushauri wa upande wa mashtaka kwamba tukio hilo ni kubwa na mstakiwa wa kwanza Baraka Mwandibwa ataenda jela kwa miaka 35 huku mshtakiwa wa pili Zuberi Lwila akiachiwa huru baada ya kutokuwa na ushahidi wa kuhusika katika tukio hilo.

  0 0  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya SAUT, St.Joseph na Chuo cha Ualimu Matogoro kwenye ukumbi wa Songea Club.
   Wanafunzi wapatao 650 wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa Songea Club.
   Mkuu wa Wilaya ya Songea mjini Ndugu Joseph Joseph Mkirikiti(wa kushoto) akiwa pamoja na wadau wa elimu wa Wilaya ya Songea wakimsikiliza Karibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
   Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo Songea .
   Katibu wa Mkoa wa Vyuo vya Elimu ya Juu Ndugu Christopher Ngubiagai akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu vya mjini Songea wakati wa kikao cha wanafunzi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Klabu ya Songea
  Baadhi ya wanafunzi wakisikiliza kwa makini masuala mbalimbali yaliyokuwa yanajadiliwa kwenye kikao kilichowahisusha wanafunzi wa vyuo vikuu na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye ukumbi wa klabu ya Songea.

  0 0

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Anne  Makindaakihojiwa   na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
  Mkutano wa nane uliwaokutanisha maspika wanawake duniani umemalizika mwishoni mwa juma mjini New York huku mjadala mkubwa ukiwa ni mkakati wa usawa wa kijinsia kuwa sehemu ya malengo endelevu ya milenia baada ya 2015.
  Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Joseph Msami amekutana na kufanya mahojiano na miongoni mwa waliotoa mada katika mkutano huo, spika wa kwanza mwanamke nchini Tanzania Anna Makinda ambaye pamoja na mambo mengine anasema anazungumzia suala la mabadiliko ya sheria ya ndoa nchini humo inayoruhusu msichana mwenye umri wa miaka 18 kuolewa.Spika anasema mlolongo wa mabadiliko ni mrefu kulikoni? Kwanza Makinda anaanza kwa kueleza mjadala mkuu wa mkutano huo. Kusikiliza bonyeza hapa http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2013/11/spika-makinda-asema-mabadiliko-ya-sheria-ya-ndoa-yana-mlolongo-mrefu/

  0 0

  Serikali wilayani Chato imeitaka Halmashauri ya Wilaya ya Chato kuendeleza mafunzo ya Mgambo kwa watumishi vijana ili waweze kujenga uzalendo na kuwa imara mahala pa kazi.

  Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo wakati akifunga mafunzo ya miezi mitatu ya Mgambo yaliyowashirikisha watumishi mbalimbali wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato yaliyofanyika kwenye uwanja wa Sekondari ya Chato.

  Mkuu wa Wilaya amesema watumishi waliohitimu mafunzo ya Mgambo ni mfano mzuri wa kuigwa na watumishi wengine na hivyo kumwomba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Clement Berege kuhakikisha watumishi wote ambao hawakupitia jeshi la kujenga Taifa AU Mgambo kuhakikisha pia wanashiriki katika awamu nyingine ya mafunzo.

  Katika risala yao kwa mgeni rasmi, wahitimu hao wameshukuru kwa kupata mafunzo hayo ambayo yamewajenga na kuwafanya wawe imara hata mahala pa kazi.

  Mafunzo hayo yaliyoanza mwezi Julai 2013 yalifunguliwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Rodrick Mpogolo na ameyafunga leo ambapo jumla ya watumishi 65 wameitimu mafunzo hayo.
  Watumishi Wanamgambo wakipita mbele ya Mgeni Rasmi.
  Kamanda Mkuu wa kikosi cha kwanza Bi. Felicia ambaye ni katibu Muhitasi idara ya Afya akiongoza kikosi kupita mbele ya Mgeni Rasmi.
  Wanamgambo baada ya kula kiapo.
  Wahitimu ya Mafunzo ya Mgambo kwenye picha picha ya pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Chato.

  0 0

  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Hellen Kilawe akionyesha namba ya pikipiki aliyokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu. Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa promosheni hiyo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu(kulia)akimfungia kamba ya kofia ngumu”Helmet”Mshindi wa Promosheni ya “Timka na BodaBoda Bw.Joseph Mambo, Katika Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao.anaeshuhudia kushoto ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Rashid Maggid.Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipanda kwenye pikipiki yake aliyoshinda katika promosheni hiyo huku akisaidiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kulia)wakati wa Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.
  Mshindi wa Pikipiki katika Promosheni ya Timka na BodaBoda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Bi.Aziza Suleiman akipunga mkono wakati akiondoka na pikipiki yake mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina nkurlu(kushoto)wakati wa Hafla ya kukabidhi pikipiki kwa washindi wa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani. Jumla ya pikipiki 25 na fedha taslimu zilikibidhiwa kwa washindi hao. Wanaoshuhudia ni washindi wengine wa pikipiki hizo. Ili kujiunga na Promosheni hiyo tuma neno Promo kwenda 15544.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa,alipowasili Mchangamdogo kukifungua Kituo cha Polisi,akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kama ishara ya Ufunguzi wa kituo cha Polisi Mchangamdogo , akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi na Jeshi Polisi katika Kituo cha Polisi Mchangamdogo Wilaya ya Wete,baada ya kikufungua rasmi akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.
  Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Mchangamdogo Kaskazini pemba wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi hao baada ya kukifungua Kituo cha Polisi katika shehia hiyo leo, akiwa katika ziara Mkoa wa Kaskazini Pemba leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akizungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada la Hanns Seidel Foundation masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na shirika hilo. Wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Dk. Peter Witterauf, anayefuata ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert, na Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo nchini Tanzania, Konrad Teichert. Viongozi wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Misaada la Hanns Seidel Foundation, Dk. Peter Witterauf. Kulia ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert. Viongozi wa Shirika hilo kutoka Makao Makuu, Kanda ya Afrika pamoja na Mwakilishi Mkazi wa shirika hilo nchini walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na shirika hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Misaada la Hanns Seidel Foundation. Katikati ni Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Dk. Peter Witterauf, wa pili kulia ni Mkuu wa shirika hilo, Kanda ya Afrika, Klaus Liepert. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo nchini, Konrad Teichert na kulia ni Naibu Kamishina wa Polisi Makao Makuu, Tathimini na Ufuatiliaji, (DCP) Omar Rashid. Viongozi wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake jijini Munich nchini Ujerumani walimtembelea Waziri Nchimbi ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya wizara yake na Shirika hilo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani.

  0 0

  Mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samata, akimtoka mchezaji wa Zimbabwe, Simba Sithole, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilitoka suluhu.
  Mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbwana Samata, akimtoka mchezaji wa Zimbabwe, Simba Sithole.
  Mshambuliaji wa taifa Stars, Shomari Kapombe akichuana na beki wa Zimbabwe.
   Shomari Kapombe akipiga pira wa kichwa ambao haukuzaa goli baada ya kutoka nje ya lango la Zimbabwe.
   Golikipa wa Zimbabwe akijaribu kuokoa moja ya hatari langoni mwake. (Picha na Francis Dande)


  0 0

  MWIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili Solomon Mukubwa atashiriki Tamasha la Krismasi lililopangwa kufanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa tayari wamemalizana na Mukubwa, ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya.

  “Pia tumemalizana na mwimbaji wa hapa nchini anaitwa John Lissu ambaye ni mmoja kati ya waimbaji mahiri na wenye mashabiki wengi.

  “Dhamira yetu ni kuwa na wasanii wote wanaokubalika na mashabiki,” alisema Msama na kuongeza kuwa Desemba 26 mwaka huu tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.

  Mukubwa ametamba na albamu mbalimbali ikiwemo Usikate Tamaa, ambayo ina nyimbo kama Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri na Usikatae Tamaa. Pia Mukubwa amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

  Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. 

  Wasanii wengine ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo la nyimbo za kusifu na kuabudu ni Watanzania, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo Kilahiro wakati wa nje ni Ephraim Sekeleti wa Zambia.

  0 0

  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake mwishoni mwa wiki.(picha na Denis Mlowe).
  ========  ======  =======
  MBUNGE AVITAKA VYOMBO  VYA DOLA KUTENDA HAKI
  Na Denis Mlowe,Iringa
  MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa (CCM) Lita Kabati amevitaka vyombo vya sheria hususan mahakama na Jeshi la Polisi kutenda haki kwa watuhumiwa wanaofika katika idara hizo wanapopatwa na matatizo na kesi mbalimbali.

  Akizungumza na mwandishi wa habari Ofisini kwake Kabati alisema hayo baada ya kutembelea Idara ya Magereza ya Mkoa wa Iringa na kukutana na wafungwa na mahabusu walimpatia kero zao kwa lengo la kuzifikisha katika mamlaka husika.

  Alisema watuhumiwa wengi wamevitupia lawama vyombo hivyo kwa kuwasingizia kesi mbalimbali hususani jeshi la polisi na kwa upande wa mahakama kutoa vifungo ambavyo wengi wao wamembakiwa na jeshi hilo.

  kabati alisema mahakama na jeshi la polisi vinatakiwa kufanya uchunguzi wa kina katika kubaini makosa ya watuhumiwa na kutenda haki kwa kufata sheria za nchi kuliko ilivyo sasa wengi walioko katika kifungo na mahabusu wanalalamika kutondewa haki na kubambikiwa kesi ambazo haziwahusu.

   "Mahakama ni moja ya vyombo vya vinavyotetea haki ya mtuhumiwa hivyo kama mtu ametenda uhalifu kwa namna yoyote lazima uchunguzi wa kina ufanyike kwa lengo la kutenda haki kwa watuhumiwa, wengi wao wametoa malalamiko kuhusu jeshi la polisi na mahakama kuwa rushwa inatawala katika vifungo vyao na wanaomba msaada wa kusaidiwa kutendewa haki" alisema Kabati

  Alisema viongozi wako kwa ajili ya kutetea haki za msingi za mwananchi na rasilimali zake na kumletea maendeleo hivyo mahakama na jeshi la polisi waepuke kuwabambikia kesi wananchi.Kabati alisema lazima tuwe wakweli  jeshi la polisi limekuwa likielemewa kwa kiwango kikubwa tuhuma za kuwanyanyasa na kuwakandamiza watuhumiwa kutokana  na malalamiko kutoka kwa wafungwa na mahabusu wenyewe kwa hili linatakiwa kubadilika.

  "Imenisikitisha sana kwa kuwa kuna watu wanajifanya Miungu mtu katika hizi Idara za mahakama, na jeshi la polisi kuweza kuwabambikia kesi watu hivyo kusababisha mrundikano mkubwa wa kesi mahakamani na kujaza watu katika magereza zetu, mie naomba kabisa wazifatilie na hili jambo sitalifumbua macho kuanzia sasa na nitalivalia njuga na nitahakikisha kwamba katika ubunge wangu nilionao hizi changamoto zinatatuliwa kwa wakati" alisema Kabati.

  alisema atapigia haki ya wananchi wa Iringa kutoendelea kunyanyasika na vyombo hivi vya dola  kwa kupakaziwa kesi ambazo haziwahusu na kila mwananchi ana haki ya kutendewa yaliyo mazuri kwa kufuata sheria za nchi.

  0 0

  Golikipa wa Mashabiki wa Yanga, Sengerere Yussuf (kushoto), akiluka juu kuokoa mpila ulioelekezwa golini kwake katika Bonanza lililowakutanisha Mashabiki wa Simba na Yanga kupitia Kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kweuwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Morogoro jana.
  Beki wa mashabiki wa Yanga, Mussa Said (kushoto) akipambana na mshambilia wa mashabiki wa Simba wakati wa Bonanza liliwakutanisha Mashabiki wa timu mbili hizo kupitia Kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Morogoro jana.
  Mashabiki wa Simba na Yanga wakipimana ubavu wa juvuta kamba wakati wa Bonanza ililofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Uwanja wa Ndege jana wakati wa kutangaza Kampeni ya Nani Mtani Jembe inayoendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Simba iliwashinda wenza wa yanga.
  Shabiki wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Yassin Mwange (kulia), akipuliza Vuvuzela wakati Tamasha la Bonanza lililoandaliwa na Bia hiyo kwaajili ya Mashabiki wa Simba na Yanga Bonanza hilo lilifanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Mkoa wa Morogoro jana.

  0 0

  Na Hassan Hamad wa OMKR
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amesema nchi za Afrika zinaweza kujifunza usuluhishi wa migogoro kupitia maridhiano yaliyofiwa Zanzibar na kupelekea kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. 
  Amesema Zanzibar ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na migogoro ya kisiasa kwa kipindi kirefu, lakini baada ya viongozi wazalendo kukaa pamoja kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, suluhu ya maridhiano ilipatikana, na kwamba matunda ya umoja huo yanaendelea kuistawisha Zanzibar kijamii na kiuchumi. 
  Akifungua mkutano wa Kimataifa wa wapatanishi wa migogoro kutoka nchi za Afrika unaofanyika hoteli ya MELIA Zanzibar, Maalim Seif amesema migogoro ya Afrika itatatuliwa na Waafrika wenyewe. Amefafanua kuwa hii haina maana ya kuzitenga nchi na Jumuiya za Kimataifa kusaidia kusuluhisha migogoro ya Afrika, lakini msingi mkubwa wa utatuzi wa migogoro hiyo uko kwa nchi husika. 
  Makamu wa Kwanza wa Rais amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili vyanzo vya migogoro inayozikabili nchi za Afrika, ili kuweza kutambua kwa urahisi njia muafaka za kusuluhisha migogoro hiyo. 
  Amewashukuru waandaaji wa mkutano huo kwa kuamua kuufanya tena Zanzibar kwa mara ya nne, hali ambayo inadhihirisha mazingira bora na salama ya kufanyika mikutano ya Kimataifa. Ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za usuluhishi wa migogoro zinazochukuliwa barani Afrika, ili kuliwezesha bara hilo na sehemu nyengine duniani kuwa katika hali ya amani, utulivu na usalama. 
  Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dkt. Salim Ahmed Salim amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imekuja baada ya mgogoro wa muda mrefu, na kwamba ni mafanikio ya kujivunia kwa bara zima la Afrika. 
  Nae Mkurugenzi wa kituo cha misaada ya kibinadamu chenye makao makuu yake Mjini Geneva Dr. David Harland amesema mkutano huo utajadili mambo mbali mbali yakiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya, utawala wa sheria, haki za binadamu, demokrasia na utawala bora. 
  Amesema matatizo mengi ya Afrika yatapatiwa ufumbuzi kutokana na juhudi za Waafrika wenyewe kuweza kusimamia usuluhishi wa matatizo yanayowakabili. 
  Mkutano huo unawashirikisha wapatanishi waandamizi wa migogoro kutoka nchi za Afrika akiwemo Mwenykiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dkt. Salim Ahmed Salim.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim (kushoto), pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wapatanishi wa Afrika huko hoteli ya MELIA Mkoa wa Kaskazini Unguja
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dr. Salim Ahmed Salim, akitoa hotuba ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Maalim Seif kufungua mkutano huo.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wapatanishi wa Afrika huko hoteli ya MELIA Mkoa wa Kaskazini Unguja. 
  Picha na Salmin Said wa OMKR

  0 0

   Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United, raisi mpya wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamal Malinzi
   Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde ambaye alichukua kwa niaba ya wapenzi wa mpira.
  Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham  (wa kwanza kushoto). Kutoka kulia niMkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw.  Leornad Thadeo, Raismpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde muda mfupi baada ya uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. 
  BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 269 | 270 | (Page 271) | 272 | 273 | .... | 3286 | newer