Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

NJOMBE MJI YAIPIGA MSASA SUMBAWANGA

$
0
0
 Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga wakiwa kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe mara baada ya kuwasili kwa lengo la kujifunza maswala ya usafi wa mazingira na ukusanyaji mapato. (Aliyesimama) ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Illuminata Mwenda
 Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Njombe Bi. Dorcas Mkello akiwasilisha mada ya ukusanyaji mapato kwa Wahe. Madiwani na Wataalamu kutoka Manispaa ya Sumbawanga

 Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji Njombe Lawi Bernard, akitoa mpango mkakati wa Halmashauri ya Mji Njombe wa utunzaji na uthibiti wa taka ngumu kwa Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga wakati wa ziara ya mafunzo ya timu hiyo katika Halmashauri ya Mji Njombe. 
 Afisa TEHAMA kutoka Halmashauri ya Mji Njombe Isack Mapunda akitoa ufafanuzi wa matumizi bora ya mashine za ukusanyaji mapato (POS) kwa Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga wakati wa ziara ya mafunzo ya timu hiyo katika Halmashauri ya Mji Njombe.
Mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi unaofadhiliwa na benki ya dunia kupitia mradi wa uboreshaji na uimarishaji Miji (ULGSP) katika Halmashauri ya Mji Njombe  ni miongoni mwa mradi uliotembelewa na  Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka Manispaa ya Sumbawanga.




=========  ============   ================  ============

MARA BAADA YA KUZIBURUZA HALMASHAURI ZA MIJI KWENYE MASHINDANO YA USAFI, HALMASHAURI YA MJI NJOMBE YAIPIGA MSASA MANISPAA YA SUMBAWANGA.

Hyasinta Kissima-Njombe

Halmashauri ya Mji Njombe imepokea ugeni wa Waheshimiwa Madiwani wakiambatana na Wataalamu kutoka katika Manispaa ya Sumbawanga lengo ikiwa ni kujifunza na kuongeza maarifa kuhusiana na maswala ya mapato na usafi wa Mazingira.

Haya yamebainika wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni hao iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe, ambapo ugeni huo ulikiri wazi kuwa wamevutiwa kufika Halmashauri ya Mji Njombe kujifunza kutokana na sifa ambazo Halmashauri imekuwa ikijizolea kila mara katika eneo la usafi wa Mazingira pamoja na ukusanyaji mapato.

“Halmashauri ya Mji Sumbawanga kwa mwaka wa fedha 2017/2018 tulikasimia kukusanya bilioni mbili na milioni mia tano, lakini hatukufanikiwa kukusanya asilimia 80 kwa mujibu wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu tulikusanya asilimia 54 pekee. Kwa upande wa mashindano ya usafi na Mazingira tulishika nafasi ya pili kutoka mwisho kutokana na ukosefu wa vyoo bora na matumizi bora ya vyoo.”Alisema Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Mhe. Justin Emmanuel Malisawa.

Alifafanua kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili ni kwenye utekelezaji wa sheria ndogo ndogo za Halmashauri na changamoto kutoka kwa wanasiasa ambao wamekuwa wakipinga na kutotekeleza ipasavyo baadhi ya maazimio waliyojiwekea kwenye ukusanyaji wa mapato na utunzaji Mazingira na ndio maana waliona umuhimu wa kuja kujifunza kutoka Njombe.

Akielezea mafanikio ya Halmashauri ya Mji Njombe ambayo imefikia kwa upande wa usafi wa Mazingira sambamba na ukusanyaji mapato, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe, Bi Illuminata Mwenda amesema kuwa mafanikio hayo yalitokana na utayari na kujitoa kwa Madiwani bila kujali itikadi za vyama vyao na ushirikiano wa Wataalamu.

“Madiwani ndio wanaotaka Halmashauri yao iweje, hivyo ndivyo ninavyofahamu. Mnaweza mkawa na mipango mizuri lakini Waheshimiwa Madiwani wakisema hapana inakuwa ndivyo. Madiwani wetu agenda zao kuu ni mapato na usafi. Na hata katika vikao vya wataalamu tumekuwa tukijadili na kuboresha mapungufu yanayojitokeza na kuweka mikakati thabiti kwenye ukusanyaji mapato na usafi wa Mazingira na tumekuwa tukifanikiwa kwa kiasi kikubwa.”Alisema Mwenda.

Dorcas Mkello ni Mweka Hazina wa Halmashauri ya Mji Njombe ambaye yeye amesema kuwa miongoni mwa mbinu ambazo wamekuwa wakizitumia kwenye ukusanyaji mapato ni sambamba na utoaji wa motisha ya pikipiki kwa watendaji wanaofanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato na kutoa milioni 5 kwa kila Diwani kwa kila robo ya mwaka fedha ambazo hukabidhiwa kwa diwani wa Kata husika kwa ajili ya kuchochea maendeleo kwenye Kata yake. Hivyo kupitia fedha hizo, kila diwani amekuwa mlinzi kwenye usimamizi wa mapato kwani wasipofanya hivyo wanaelewa fika fedha hizo hazitapatikana bila kukusanywa kwa nguvu kubwa.

Afisa Mazingira Halmashauri ya Mji Njombe Lawi Bernard amesema kuwa licha ya kuwa na mwamko chanya wa wananchi kwenye uchangiaji wa tozo za taka, Halmashauri kupitia mapato ya ndani imekua ikiona umuhimu wa kuiwezesha idara hiyo na ndio maana kwa mwaka wa fedha 2018/2019 walifanikiwa kutenga fedha kupitia mapato ya ndani na kununua tractor kwa ajili ya kubeba taka na hivyo kuzuia mlundikano wa taka katika maeneo ya Mji kutokana na uwepo wa vitendea kazi vya kutosha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Edwin Mwanzinga alisema kuwa, siri ya mafanikio ni umoja baina ya Waheshimiwa Madiwani na wataalamu kwani wamekuwa wakipokea maelekezo ya wataalamu na panapokuwa na mapungufu wamekuwa wakishirikiana kuboresha kwa manufaa ya Halmashauri nzima.

“Wenzangu wa Sumbawanga niwaombe muwe na ushirikiano katika ukusanyaji mapato. Maendeleo ni ya wananchi wote na hayana vyama, naomba pia mfahamu kuwa katika swala la Usafi na Mazingira hamtaweza kufanya vizuri kwa kutegemea Halmashauri itaondoa taka yenyewe, lazima mzalisha taka awe na jukumu la kuondoa taka kwa kuchangia gharama.”Alisema Mwanzinga.

Aidha, Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu kutoka Manispaa ya Sumbawanga wameishukuru Halmashauri ya Mji Njombe kwa elimu waliyoipata na wamepongeza ujenzi wa kiwango cha hali ya juu unaoendelea katika kituo kipya cha Mabasi na wameahidi kutengeneza mtandao wa mawasiliano na Halmashauri ya Mji Njombe ili kuendelea kupata ujuzi na mbinu mpya katika maeneo mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Njombe kwa miaka miwili mfululizo; 2017/2018 na 2018/2019 imepokea wageni kutoka Halmashauri nane za Mikoa ya Songwe, Singida, Shinyanga na Rukwa kwaajili ya kujifunza mbinu na siri ya ushindi inayotumia Halmashauri ya Mji Njombe katika kuimarisha hali ya usafi katika maeneo yake yote.

SHIRIKA LA BIMA ZANZIBAR LADHAMINI MASHINDANO YA RIADHA

$
0
0
Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Shirika la bima Zanzibar limedhamini mashindano ya riadha ya Mererani Tanzanite Half Marathon ambayo yatafanyika mwishoni mwa wiki na kujumuisha idadi kubwa ya wanariadha kutoka mikoa ya Arusha,Manyara na Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa shirika la bima Zanzibar kanda ya Kaskazini Hamis Matumla alisema hayo Jana wakati akikabidhi kiasi cha shillingi milioni mbili ambazo ni udhamini was shirika hilo ikiwa ni njia mojawapo ya kuunga mkono michezo na kuhamasisha umuhimu wa afya kwa wachezaji.
Matumla alisema kuwa kuelekea Mashindano ya Riadha ya Mbio fupi yajulikanayo kama Mererani Tanzanite Half Marathon yatakayofanyika huko Mkoani Manyara ,Wadau wa Michezo wanapaswa kujitokeza kushiriki pamoja na kudhamni Mashindano hayo yenye lengo la kutangaza madini hayo yanayopatikana Tanzania Pekee.

"Jamii inatapaswa kujenga utamaduni wa kupenda kushiriki Michezo kwani michezo ni ajira na michezo ni afya pia" Alisema Matumala

Kwa upande wao waandaaji wa Mashindano hayo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Charles Mnyalu wanasema uandikishaji unaendelea katika Vituo mbalimbali vilivyopo hapa nchini na Washiriki na Washindi watapata Zawadi Mbalimbali.

Alisema Mbio hizo zitakazofanyika mnamo tarehe 27 mwezi huu katika Viunga vya mji wa Mererrani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara zitashirikisha wanariadha wa kilometa tano ambao ni Watoto pamoja na Kilometa ishirini na Moja kwa Watu Wazima huku zaidi wanariadha elfu moja mia tano wakitarajia kushiriki.

Mjumbe Kamati ya Mashindano Alfredo Shahanga aliwataka Wakazi wa manyara ,Arusha na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo.

FIFA YAMFUNGIA MAISHA MICHAEL WAMBURA KUJISHUGHULISHA NA MASUALA YA MPIRA WA MIGUU DUNIANI KOTE.

VIONGOZI WANAOKIUKA KIAPO CHA MAADILI KUCHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU - NAIBU WAZIRI MWANJELWA

$
0
0
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imetakiwa kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wanaokula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu na kutoa Tamko la Rasilimali na Madeni lakini wanashindwa kutekeleza kiapo hicho.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipofanya ziara ya kikazi makao makuu ya ofisi hizo jijini Dodoma yenye lengo la  kuhimiza uwajibikaji, kufahamu kwa kina majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na kujiridhisha namna inavyotekeleza wajibu wake.

Dkt. Mwanjelwa amesema, baadhi ya viongozi wamekuwa wakila Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu na kusoma Tamko la Rasilimali na Madeni lakini maisha na tabia zao ni tofauti kabisa na viapo wanavyoapa, hivyo ameisisitiza Sekretarieti ya Maadili kutumia sheria kuwawajibisha viongozi wa namna hiyo kwani ni mzigo kwa taifa. Dkt. Mwanjelwa amesema viapo na matamko ni lazima viendane na uhalisia, hivyo ameitaka Sekretarieti hiyo kufanya ufuatiliaji na kuchukua hatua bila uwoga wowote kwa kiongozi anayeenda kinyume kwani kiongozi wa namna hiyo anakosa sifa ya kuwa kiongozi bora. 

Dkt. Mwanjelwa amesema ni lazima kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na viongozi ambao hawana maadili mema ili kuleta maendeleo kwa taifa. Aidha, Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Sekretarieti hiyo kuishi na kufanya kazi katika maadili mema ili wawe mfano kwa wanaowasimamia katika suala zima la maadili. “Ni lazima maadili mema yaanzie kwetu sisi ili tunapozungumza na kutoa elimu ya maadili kwa viongozi tuwe kioo kwani huwezi ukazungumzia maadili kwa viongozi kama wewe mwenyewe huna maadili, hivyo ni lazima kuonyesha mfano,”  Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela amesema, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma yeyote kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba masharti ya Sheria ya Maadili ya viongozi wa umma yanazingatiwa ipasavyo. 

Nsekela ameyataja majukumu ya Sekretarieti kuwa ni pamoja na kupokea matamko ya viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni yanayopaswa kutolewa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kuanzisha na kufanya uchunguzi wowote kuhusu ukiukwaji wa maadili yaliyotajwa na Sheria, kupokea na kushughulikia malalamiko na taarifa za ukiukwaji wa maadili kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kutoka kwa wananchi na kufanya uhakiki wa Tamko la Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma wanaotajwa na Sheria.

 Nsekela ameyataja baadhi ya matarajio ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwa ni kujenga na kuimarisha maadili ya kitaifa na kuyafanya yawe sehemu ya jamii ili kuzuia mmomonyoko wa maadili katika nchi kwa kujumuisha somo la maadili katika mitaala kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, kufanya marekebisho ya Sheria zinazohusu ukuzaji wa maadili nchini ikiwemo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma pamoja na kutungwa kwa Sheria ya Kudhibiti Mgongano wa Maslahi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kushoto ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Harold Nsekela.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mst. Harold Nsekela (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuhusu majukumu ya ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, alipoitembelea ofisi hiyo kuhimiza uwajibikaji jijini Dodoma.
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao cha kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika katika ofisi ya Sekretarieti hiyo jijini Dodoma.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma jijini Dodoma kwa ajili ya kuhimiza uwajibikaji.

Sherehe za Maulidi ya Idara ya wanawake wa Masjid Akram Mbezi Beach Dar es Salaam

MAKAMU WA RAIS AFUNGA MKUTANO MKUU WA KISEKTA WA MADINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye ukumbi wa mkutano tayari kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati  hafla ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini ulioandaliwa na Wizara ya Madini ambapo wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini walikutana kwa siku mbili katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimaji Wadogo (FEMATA) Ndugu John Binna (kushoto) akimkabidhi maadhimio ambayo yamejumuisha maoni na mapendekezo ya kuboresha biashara na shughuli za uchimbaji madini kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Mashaka Biteko (katikati), kulia Makamu wa Rais akishuhudia makabidhiano hayo mara baada ya Mkutano Mkuu wa Kisekta ulioandaliwa na Wizara ya Madini kukamilika.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe, Samia Suluhu Hassan akipokea maadhimio ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini  kutoka kwa Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini uliofanyika
kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe, Samia Suluhu Hassan akisoma maadhimio ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na wadau wa madini  mara baada ya kuyapokea wengine pichani Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko (katikati) na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimaji Wadogo (FEMATA) Ndugu John Binna (kushoto) mara baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Kisekta wa Madini uliofanyika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA DINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea wakati alipokutana na viongozi wa dini Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 23, 2019.  PICHA NA IKULU

BREAKING NEWZZZZZ: Mwanamuziki Oliver Mtukudzi afariki dunia

$
0
0
Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia.

Amefariki hii leo katika hospitali ya Avenues mjini Harare.

Mtukudzi amekuwa akiugua kwa muda sasa. 

Alilazimika kukatiza miadi kadhaa katika fani hiyo ya muziki katika mataifa mbali mbali duniani kutokana na kuugua kwake.Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.

Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith. 

Baada ya uhuru wa nchi hiyo, aliitumia sauti yake kuzungumzia masuala ya kisiasa na ya kijamii.Kwa mara nyingi ujumbe ndani ya muziki wake ulikuwa ni wa ndani kukwepa mkono wa serikali iliyokuwa haipendelei kukosolewa.

Mtukudzi amekuwa katika taaluma ya muziki kwa zaidi ya miongo minne, na amefanikiwa kutoa albamu 67.Albamu yake ya mwisho imeangazia hali ya kisiasa hivi sasa Zimbabwe na matatizo ya kijamii. 

Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa anapewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii kama Hugh Masekela, Steve Dyer, Miriam Makeba, Yousssou N dour, Angelique Kidjo, Yvonne Chaka Chaka na Lady Smith Black Mambazo.


TIC YAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KUWAPA KIPAUMBELE WAWEKEZAJI

DC MBONEKO AKABIDHI VITENDEA KAZI VYA MILIONI 19.4 VILIVYOTOLEWA NA RAFIKI SDO KWA WAWEZESHAJI WA VIKUNDI

$
0
0
Shirika la RAFIKI SDO ‘Rafiki Social Development Organization’ limekabidhi vitendea kazi ikiwemo baiskeli 76 na mabegi 76 vyenye thamani ya shilingi milioni 19.4 kwa wasichana na wanawake ‘Wawezeshaji wa vikundi’ kwenye wilaya ya Shinyanga ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vizuri katika mitaa na vijiji wanavyohudumia.
Hafla fupi ya makabidhiano ya vitendea kazi hivyo imefanyika leo Jumatano,Januari 23,2019 katika ofisi ya RAFIKI SDO mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack.
Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a alisema vitendea kazi hivyo vitatumika kwenye kata ambako shirika lao linatekeleza shughuli za miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa baiskeli hizo zinakamilisha idadi ya baiskeli 148 kwani tayair walishatoa zingine 72.
“Wawezeshaji hawa 76 tuliwapa elimu,sasa wanakwenda kuunda vikundi vya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 kwa ajili ya kuwafundisha masuala ya ujasiriamali,malezi,mabadiliko ya tabia na masuala mtambuka,watatumia vitendea kazi hivi kuwafikia wananchi kwenye maeneo yao kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga”,alisema Ng’ong’a.
“Shirika letu limeajiri wawezeshaji wa vikundi 131 kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2019,kati ya 72 ni wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na 59 halmashauri ya Shinyanga,tunawapatia mishahara kila mwezi,wanalipiwa NSSF na wameunganishwa na mfuko wa huduma za afya”,aliongeza Ng’ong’a.

Kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alilipongeza shirika la RAFIKI SDO kwa kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo huku akibainisha kuwa shirika hilo linatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwezesha wananchi kiuchumi.
Mboneko aliwataka Wawezeshaji hao kutumia vyema vitendea kazi walivyopatiwa ,kuomba mikopo kwenye halmashauri na kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa shughuli za maendeleo.
Mkuu huyo wa wilaya alitumia fursa hiyo pia kuwahimiza wanawake kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiwashauri kutumia mikusanyiko ya watu kutangaza na kuuza bidhaa wanazotengeneza.
Aidha aliwaagiza maendeleo ya jamii kutembelea vikundi vilivyoanzishwa na kuvishauri huku akizitaka halmashauri kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyo mstari wa mbele kwenye masuala ya maendeleo.
Nao wawezeshaji hao walilishukuru shirika hilo kuwa karibu nao na kueleza kuwa hivi sasa wameweza kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi lakini pia tabia hatarishi zimepungua na wanaendelea kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akimkabidhi begi na baiskeli Anna Kulwa kutoka kijiji cha Kizungu kata ya Lyamidati halmashauri ya wilaya ya Shinyanga . Wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Deus Mhoja na Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga, Jackson Njau, wa kwanza kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a wakishuhudia zoezi la makabidhiano ya vitendea kazi. 
Anna Kulwa akishikana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikabidhi vitendea kazi kwa  Rahim Ibrahim kutoka kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Baiskeli na mabegi yaliyotolewa na RAFIKI SDO kwa wawezeshaji wa vikundi. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitendea kazi vilivyotolewa na shirika la RAFIKI SDO kwa Wawezeshaji wa vikundi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Charles Maugira.
Mkurugenzi Mtendaji wa RAFIKI SDO, Gelard Ng’ong’a akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitendea kazi kwa wawezeshaji wa vikundi.
Kulia ni Msaidizi wa Meneja shirika la RAFIKI SDO, Neema Lweeka akielezea kuhusu shirika hilo na shughuli za maendeleo wanazotekeleza hususani miradi ya afya,elimu,uwezeshaji kiuchumi,ulinzi wa mtoto,haki na utawala na utoaji elimu ya stadi za maisha.
Wawezeshaji wa vikundi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiagana na wawezeshaji wa vikundi.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MBARAWA AIVUNJA BODI YA MAJI MJI MDOGO KIBAIGWA KWA UTENDAJI MBOVU

$
0
0
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi juu ya mradi wa Tanki la Maji litakalochukua lita milioni tatu na kumaliza tatizo la maji katika baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kongwa.
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza jambo  na Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai wakati waziri  uyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika eneo hilo.
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wakazi wa Mtanana Wilayani Kongwa  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji.
  Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji mji mdogo wa Kibaigwa Mhandisi Bonifas Bihemo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maji katika eneo hilo.Kushoto kwake ni Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa(Kushoto) kukagua miradi ya maji Wilayani Kongwa.Pembeni ya Waziri ni Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
 Mbunge wa Kongwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akizungumza na wananchi wa Kibaigwa (Hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa kukagua miradi ya maji na kutatua changamoto mbalimbali za maji.

 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoa tamko la kuivunja Bodi ya Maji Mji mdogo wa Kibaigwa kutokana na utendaji mbovu na kushindwa kutekeleza  majukumu yake vyema.
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Wilayani Chamwino.Picha na Daudi Manongi,MAELEZO

NAIBU WAZIRI ULEGA AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUFUFUA MIUNDOMBINU YA KUPAKIA NA KUSHUSHA NG'OMBE

$
0
0

Na Amisa Mussa

Naibu Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Adballah Ulega amesema kuna haja ya kufanya mazungumzo ya kina na Wizaraya Ujenzi na Mawasiliano kuhusu Kuishauri Wizara hiyo kuona umuhimu wa kufufua Miundombinu ya kupakia na kushusha Ng'ombe Wanaosafirishwa Kupitia Usafiri Wa Treni Ya Mizigo Hatua Ambayo Itasaidia Kupunguza Adha Kubwa Ya Usafishaji Mifugo Wanayokumbananayo Wafanyabiashara Ya Ng’ombe.

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo wakati alipotembelea kituo  cha usafishaji cha Reli ya Kati Mjini Tabora na Kukagua Miundombinu ya Kupakia Na Kushusha Ng'ombe Wanaosafirishwa Kwa Usafiri Wa Treni.

Aidha Miundombinu Katika Kituo Cha Usafirishaji Cha Reli Ya Kati Mjini Tabora Inaonekana Kusahaulika Ambapo Naibu Waziri Huyo Amesewasihi Wafanyabiashara Ya Ng’ombe Wilayani Humo Kuendelea Kufanya Biashara Katika Mnada Wa Ipuli.

Awali Mkuu Wa Wilaya Ya Tabora Mjini KOMANYA ELIC KITWALA Na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora LEOPAD ULAYA Wamesema Miundombinu Inayotumiwa Na Wafanyabiashara Na Wafugaji Wa Ngombe Ni Finyu Hatua Ambayo Inasababisha Wafanyabiashara Hao Kupata Usumbufu Wawapo Kituoni Hapo

Aidh Naibu Waziri Ulega amewasihi Wafanyabiashara wanaotumia Mnada wa Ipuli Mjini Tabora kufuata  na kuzingatia Sheri, Kanuni na Taratibu ili kuepuka Migongano isiyokua ya lazima.

TTCL CORPORATION YAZINDUWA DUKA JIPYA LA HUDUMA KARIAKOO

$
0
0



Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akishuhudia tukio hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia).
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TTCL wanaotoa huduma ndani ya duka hilo jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililopo Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TTCL, Mhandisi Omary Nundu akimsikiliza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (kulia) akiingia kwenye duka hilo mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba (wa pili kushoto) wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega (kulia) pamoja na Kaimu Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar Es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Kindamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa TTCL, Ndugu Ally Mbega wakionesha baadhi ya bidhaa za TTCL zinazopatikana katika duka jipya la TTCL lililozinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa duka jipya la TTCL lililo zinduliwa leo eneo la Kariakoo Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam.



SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo limezinduwa duka jipya na kituo cha huduma Kariakoo eneo la Mtaa wa Mafia na Msimbazi jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania ( TTCL), Mhandisi Omary Nundu alisema kwa Mwaka 2019, TTCL imejipanga vyema kuhakikisha kuwa Huduma za Shirika hilo zinasambaa zaidi kote nchini huku ikisimamia ubora na unafuu wa gharama ambazo zitakuwa nafuu kwa wananchi.

"...Tunakusudia kuendelea kufanya mageuzi makubwa ndani ya Shirika ili kuliwezesha kushindana kikamilifu katika Soko la Huduma za Mawasiliano Nchini sambamba na kutimiza wajibu wa kimsingi wa kuwa mchangiaji muhimu katika Pato la Taifa," alisema Mhandisi Omary Nundu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Waziri Kindamba awali akizungumza alisema uzinduzi huo wa duka na kituo cha Huduma kwa Wateja ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitatu, 2016-2019 ambao umeweka msisitizo mkubwa katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja.

"Uzinduzi wa leo unaonesha kwa vitendo jinsi gani TTCL mpya ilivyojipanga vyema kuhakikisha huduma zake zinawafikia Wateja katika mazingira mazuri, yanayovutia na kuwakilisha hadhi ya Shirika letu. Kukamilika kwa Duka hili/ Kituo hiki cha Huduma kwa Wateja kuonaongeza idadi ya Maduka mapya ya TTCL kufikia maduka 10 ambayo yamejengwa kwa viwango vya hali ya juu na kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya utoaji bora wa Huduma kwa Wateja,"

Aidha aliongeza kuwa TTCL itaendelea kuboresha Maduka na Vituo vyetu Nchi nzima, sambamba na Ofisi zake za Mikoani na Wilayani ili ziweze kuwa mahali bora kabisa kwa Watumishi wa TTCL wanaotoa huduma na Wateja wote watakaofika kupata huduma za aina mbalimbali.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA MAJAJI NA MAHAKIMU WANAWAKE TANZANIA

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Prof. Ibrahim Juma kabla ya akihutubia hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) Jaji Imani Aboud (kulia) wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa TAWJA uliofanyika kwenye Hotel ya Verde, Mtoni Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAGAZETI YA LEO AL HAMISI JANUARI 24,2019


EAE FOUNDATION INAWAALIKA KATIKA HAFLA YA FUNDRAISING KUKAMILISHA UNUNUZI WA JENGO LA COMMUNITY

WALIOHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA SAME WATAKIWA KUWA MFANO WA KUIGWA KATIKA JAMII

$
0
0
  Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule,  amehimiza matumizi mazuri ya mafunzo ya Jeshi la Akiba kwa wahitimu wa mafunzo hayo kwa kuwataka kuwa mfano wa kuigwa ndani ya jamii.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kufunga mafunzo ya Jeshi la Akiba wilayani Same ambapo pia amewasisitiza waliohitimu mafunzo hayo kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kufanyakazi kwa kujitolea.

Mkuu wa Wilaya huyo amewahakikishia waliohitimu mafunzo hayo kupewa kipaumbele usaili JKT na ajira wakiwa na sifa. 

Pia amewaagiza kukomesha biashara ya mirungi na vibaka Makanya. "Hakikisheni kupitia mafunzo ambayo mmeyapata na kuzuia biashara ya mirungi."

Katika mafunzo hayo jumla ya wahitimu 108 wapata vitambulisho. Wananchi wametumia nafasi hiyo kupongeza utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli kwani Makanya wana mradi wa maji unaendelea, waahidiwa fedha kuanza kidato cha tano. 
 Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wakila kiapo cha utii mbele ya Mkuu wa Wilaya Mh.Rosemary Staki Senyamule (hayupo pichani).
 Picha ya pamoja

 
 Mkuu wa Wilaya Mh.Rosemary Staki Senyamule Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba wakiwa katika picha ya pamoja.

MASHIRIKA YAUNGANA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA MASOKONI MKOANI MBEYA NA SHINYANGA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola wakionesha mkataba wa ushirikiano wa kupinga ukatili wa kijinsia katika masoko ya Mikoa ya Shinyanga na Mbeya baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa Bodi ya EfG, Penina Leveta (kulia), akiwa na viongozi wa mashirika yaliyofanya mkataba wa ushirikiano. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga na Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga. 
Mtathimini Miradi wa EfG, Samora Julius, akitoa mada katika semina ya maofisa wa mashirika hayo iliyofanyika hivi karibuni.
Maofisa wa mashirika hayo wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
Mwezeshaji katika semina hiyo, Pentaleon Shoki akitoa mada.
Usikivu katika semina hiyo.
Mwonekano wa chumba wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika moja ya kumbi zilizopo Baraza ka Maaskofu Kurasini jijini Dar es Salaam. 
Picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa semina hiyo na kusaini mkataba wa ushirikiano.



Na Dotto Mwaibale

MASHIRIKA matatu yasiyo ya kiserikali yametiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuongeza nguvu ya kupinga ukati wa kijinsia kwenye masoko`katika mikoa ya Mbeya na Shinyanga.

Mkataba huo ulihusisha shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, Shirika la Miiko la mkoani Mbeya na Shirika la Equality for Growth (EfG) la jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufunga semina ya siku tatu iliyowashirikisha maofisa kutoka katika mashirika hayo jijini Dar es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita alisema wameona waungane ili kuongeza nguvu ya kampeni ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika masoko ndani ya mikoa hiyo.

"Sisi shirika letu kwa hapa Dar es Salaam tulianza na mradi wa mpe riziki si matusi ambao ulilenga kuwalinda wanawake wafanyabiashara sokoni dhidi ya ukatili. Katika kupunguza ukatili dhidi ya wanawake katika masoko mradi huo umeweza kubadilisha mtazamo na tabia dhidi ya ukatili kwa wamawake, kuwahakikishia waathirika wa ukatili wanapata hakizao" alisema Magigita.

Alisema utafiti uliofanywa na EfG mwaka 2015 katika masoko 6 kuhusu ukatili wa kijinsia na uelewa wa sheria katika Wilaya za Temeke na Ilala jijini Dar es Salaam ulionesha kuwepo na ukatili dhidi ya Wanawake katika masoko ambapo asilimia 95.97 ya waliohojiwa katika masoko yote walisema kulikuwa na ukatili dhidi ya wanawake kwenye masoko yao.

Alisema zaidi ya wafanyabiashara 6500 waliweza kufikiwa na kampeni za kupinga ukatili, kampeni za kuongeza uelewa juu ya ukatili dhidi ya wanawake, sheria na haki za binadamu.Mkurugenzi wa Shirika la Agape Aids Control Program la mkoani Shinyanga, John Myola alisema sasa wanakwenda kufanya kampeni kubwa ya kupinga ukaliti wa kijinsia katika Soko Kuu, Nguzonane, Kambarage, Ngokolo, Ndembezi na Majengo Mapya.

Na Mkurugenzi wa Shirika la Miiko la mkoani Mbeya, Adamu Siwinga alisema kampeni hiyo wataifanya katika masoko yote ya jijini humo.

INTRODUCING: NITADATA by Alicios (Official Video)

GAVANA SHILATU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA ZAHANATI*

$
0
0
*~ Wananchi waanika hali ilivyo*


Na Ripota wetu, Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Zahanati ya Mkoreha iliyopo Kata ya Mkoreha ili kubaini ukweli juu ya huduma zitolewazo.

Gavana Shilatu alitembelea Leo Jumatano Januari 23, 2019 ambapo amebaini uwepo wa huduma nzuri inayoghubikwa na changamoto ya uwingi wa Wagonjwa na kutoa maagizo kwa watoa huduma kuongeza kasi ya utoaji huduma.

*"Wananchi wanakiri huduma ni nzuri, nawapongeza. Japo Kuna changamoto ya uwingi wa Wagonjwa. Nawapa maelekezo Wauguzi jitahidini kuongeza kasi ya Watu kuhudumiwa kwa haraka, muhakikishe mnatoa dawa kwani nimeziona zipo nyingi.",Alisema Gavana Shilatu.

Gavana Shilatu amewasihi Wauguzi kuzingatia maadili, nidhamu, miiko na uwajibikaji zaidi kazini ili kuleta tija zaidi kwani maendeleo ya Watu yanategemea zaidi uwepo wa afya njema.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images