Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

DC JOKATE ALIA NA UKOSEFU WA MAJI KISARAWE

$
0
0

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo amemuomba Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso kuhakikisha Wilaya hiyo inapata Maji yakutosha kutokana nakuwepo changamoto kubwa ya upatikanaji wa Maji hayo.

Akizungumza na Watendaji wa Wilaya hiyo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso - Jokate ameshukuru kuwepo mradi wa Maji unaotoka Ruvu Juu, amesema mradi huo umekaa kimkakati kutokana na Wilaya hiyo kuwa na Viwanda vingi.

Hata hivyo, Jokate amesema maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe yamekwamishwa kwa ukosefu wa Maji Safi na Salama hivyo kuna nia yakuhakikisha Maji hayo yanapatikana. ‘’Haileti maana kama Kisarawe haina Miundombinu yakuwezesha Viwanda mbalimbali kustawi, hata uwepo wa Bandari na Kiwanja cha Ndege’’, amesisitiza Jokate.

‘’Watu wengi wamekuwa na imani Kisarawe kuwa sio eneo la Makazi, wengi wanaishi Gongo la Mboto, Chanika kutokana nakukosekana huduma ya maji’’, ameeleza Jokate.

Jokate ameshukuru kuwepo ziara ya Naibu Waziri wa Maji ambapo amemuomba kuangalia kwa umakini miradi hiyo, Je inatekelezwa ipasavyo?
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso akisisitiza jambo wakati alipowasili katika Ofoisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wilayani humo.Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwangelo akizungumza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso wakati wa ziara yake yakutembelea miradi mbalimbali ya Maji Wirani Kisarawe Mkoa wa Pwani.


ULEGA AAGIZA AFISA MIFUGO MANISPAA YA TABORA AUCHUNGUZWE

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameagiza Afisa Mifugo wa Manispaa ya Tabora Cornelius Masawe achunguzwe na achukuliwe hatua baada ya kutuhimiwa na wafanyabiashara wa mifugo wa Mnada wa Ipuli kuwanyanyasa ikiwemo kuwatoza malipo zaidi bila kuwapa stakabadhi.

Alisema tuhuma hizo ni nzito kwa kuwa zinaweza kusababisha Serikali kukosa mapato yake ikiwa wafanyabaishara hao watakaa kupeleka mifugo mnadani.

Ulega alitoa kauli hiyo leo wakati wa mkutano na wafanyabiashara wa mifugo kuhusu kuondoa mvutano ulikouwa umezuka katika Mnada wa Ipuli uliopo Manispaa ya Tabora kuhusu utaratibu wa usafirishaji ng’ombe kutoka na kuingia.

Alisema kuwa ni vema vyombo vinavyohusika ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na vyombo vingine kuchunguza tuhuma zilizotolewa na wafanyabiashara hao wa mifugo dhidi ya Masawe za kutoza fedha za faini ya mifugo bila ya kukatia stakanadhi au kutoa ambayo halingani na malipo yaliyotolewa.

Kufuatia tuhuma hizo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliagiza Masawe akamatwe na Polisi kwa ajili ya mahojiano na TAKUKURU , kwa kushirikiana na Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kiusalama. Alisema wafugaji kama makundi mengine Mkoani Tabora wana haki sawa na haipaswi kunyanyaswa na ikitokea wamenyanyaswa ni vema wakatoa taarifa mapema ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Mwanri alisema tuhuma zilizotolewa na wafanyabiashara hao ni nzito haiwezekani zikapuuziwa ni vema hatua zikachukuliwa ili kubaini ukweli na ikibidi na hatua za kulifilisha katika maamuzi zifanyike haraka. Baadhi ya wafanyabishara walisema Masawe wakati wa kuendesha operesheni amekuwa akiwakata na kuwapiga watu wanaokutwa na ng’ombe katika maeneo ambayo hayakatazwi kisheria. Walisema ameweka migambo katika kila pande ya kuelekea Mnadani ili kuwavizia na anawakamata anawatoza shilingi 50,000/- kila ng’ombe kwa madai kuwa wanapita njia zisizo rasmi.

Walisema Masawe alishawi kupokea shilingi 900,000/- lakini aliandika stakabadhi ya laki 5 tu. Walisema amekuwa akiendesha zoezi hilo wakati akijua njia za kupitishia mifugo kwenda Mnadani zimevamiwa na watu mbalimbali na kujenga.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo amsema kuwa utaratibu wa nyuma wa kupeleka mifugo katika Mnada wa Ipuli uendelee kutumika wakati suluhusho la kudumu kuhusu kuendelea au kuhamisha likifanyiwa kazi kutokana na eneo hilo kuwa katikati ya mji hivi sasa likitafutwa na pande zote.

Aliwataka wafugaji kuendelea kutii Sheria zilizopo za Manispaa wakati wanaendelea kulitafutia ufumbuzi wa kudumu suala lao la kupitisha ng’ombe kutoka kwao kwenda mnadani.

Ulega alisema tatizo kubwa lilisababisha mvutano huo ni makosa yaliyofanyika nyuma ya kushindwa kulinda njia ya kusafirisha ng’ombe kutoka maeneo mbalimbali na kwenda katika Mnada wa Ipulu na kusababisha watu kujenga.
 Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi jana kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maelezo mafupi jana wakati wa Mkutano wa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega na wafanyabiashara wa ng'ombe.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara wa mifugo katika Mnada wa Ipuli mkoani Tabora jana

BASATA YAWAACHIA HURU WASANII DIAMOND,RAYMOND PAMOJA NA TAMASHA LA WASAFI 2018.

MRADI WA NJIA KUU YA UMEME KUIUNGANISHA TANZANIA NA KENYA WAANZA KUTEKELEZWA

$
0
0
*TANESCO yazungumzia faida zake ikiwamo ya kuiwezesha Tanzania kuuza au kununua umeme kwa nchi nyingine za Afrika
*Wananchi ambao mradi huo unapita washauriwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kazi inakwenda kama ilivyokusudiwa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MRADI mkubwa wa umeme unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) ambao utaiwezesha nchi kununua au kuuza umeme katika nchini za Afrika umeanza kutekelezwa ambapo kwa sasa mradi wa kuunganisha umeme katika nchi za Kenya na Tanzania umeanza.

Mradi huo unafahamika kwa jina la Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP) ambapo kutakuwa na hatua mbalimbali za kuutekeleza mradi huo uliogawanywa katika hatua nne za utekelezaji wake huku TANESCO ikifafanua umuhimu na faida lukuki za mradi utakapokamilika na kwa sasa wakandarasi wapo kazini na kanzi imeanza kufanyika.

Kwa mujibu wa TANESCO awamu ya kwanza itakuwa ni kuzinganisha nchi za zilizopakana na Tanzania kuwa na umeme wa uhakika huku awamu ya pili ya mradi huo ukihusisha nchi za Tanzania na Zambia (ZTK) ambao nao tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara imeanza.Akiuzungumzia mradi huo jana jijini Arusha, Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye, amefafanua mradi huo wanaamini utakamilika kwa wakati kama ambavyo wamekubaliana na wakandarasi ambao tayari kazini na vifaa vyote muhimu vimefika na kazi ya kusimika nguzo imeanza.

Ameongeza kuwa mradi huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa Regional Power Connection ambao lengo lake ni kuunganisha mfumo wa umeme wa Tanzania na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini na baada ya kukamilika utekelezaji wake itakuwa inaunganisha mifumo ya nchi Kusini mwa Afrika, kupitia mradi wa Southern Africa Power Pool (SAPP).

Amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kwai itakuwa na sehemu tatu za mradi huo ambapo ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa wakati sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya ambapo kuna kituo kimoja kinachoitwa Isinya.

"Jumla ya mradi wote una umbali wa kilometa 510 lakini kwa upande wetu Tanzania tunazo kilometa 414 na upande wa Kenya nao wanakilometa 96.Kwa upande wetu tunakwenda vizuri kwani kila kipande cha ujenzi wa mradi kuna mkandarasi wake na kila mmoja yupo hatua mbalimbali za ujenzi.Kupitia watalaam wetu tumekuwa tukifuatilia hatua kwa hatua na wakati huo huo wapo watalaamu wengine ambao nao wanafanya kazi hiyo hiyo kuhakikisha kila kinachofanyika kimezingatia mahitaji na vigezo vya viwango vya ubora,"amesema Mhandisi Kigadye.

Amefafanua pia kutakuwa na sehemu ya tatu ambayo ni Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambako kuna kilomita nyingine 624, hivyo baada ya kukamilika kwa mradi Tanzania itakuwa imekamilisha ule mkongo wa msongo wa Kilovoti 400.Lengo kuu la kuunganisha nchi yetu na ukanda nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia maana yake ni kuifanya Tanzania kuingia kenye mfumo wa umeme ambao utahusisha nchi mbalimbali za Afrika.

"Tunafahamu mradi huu wa njia ya umeme ya Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, unatarajiwa kukamilika Aprili 2020 na ule Zambia Connector utakamilika mwaka 2022.Hivyo maana yake ni kwamba hii itakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu na nchi yetu.Kupitia huu mfumo nchi hizo zitakuwa zimeingia kwenye biashara ya umeme na hakutakuwa na tatizo la umeme tena,"amesisitiza.

Kuhusu mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection kwa maelezo ya Mhandisi Kigadye amesema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.

"Kama ambavyo nimeeleza awali jumla ya kilometa za mradi huo ambapo utapita ni 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilomita kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga-Arusha Kilomita 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilomita 150, na Bababti-Singida kilomita 150.Kiasi cha fedha ambacho kitatumika kwa ajili ya mradi huo ni dola za Marekani milioni 258,"amesema Mhandisi.

Wakati huo huo Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na miradi Mhandisi Emmanuel Manirabona amesema katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati tayari vifaa vyote muhimu tayari vipo maeneo y mradi na wakandarasi wanaendelea na ujenziAmetumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa wananchi ambapo mradi utapita kutoa ushirikiano ili kufanisha mradi na hasa kwa kuzingatia TANESCO imeshalipa fidia kwa watu wote ambao wanastahili na hivyo haitarajii kuona watu wengine wanajitokeza na kukwamisha ujenzi huo kwa kigezo cha kudai fidia.

Mhandisi Manirabona ameelezea matumaini ya TANESCO baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao utatoa fursa ya nchi moja kununua umeme kwa nchi nyingine iwapo itahitajika kufanya hivyo lakini kwa Tanzania mradi huo umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia nchi inatekeleza ujenzi wa viwanda , na hivyo mwito wao ni kuhamasisha watu kuwekeza kwa kujenga viwanda maeneo mbalimbali nchini kwani hakuna tatizo la nishati ya umeme.
Baadhi ya vifaa ambavyo vipo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme unaoendelea mkoani Arusha.

 Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) anayehusika na miradi Mhandisi Emmanuel Manirabona akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa mradi wa kuunganisha umeme unaendelea mkoani Arusha
 Shughuli za ufungaji vifaa ukiendelea 

TAnTrade,NEEC WAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA KUWEZESHA WANANCHI SEKTA ZOTE ZA KIUCHUMI IKIWEMO MASOKO

$
0
0
 Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi (NEEC) jana Januari 22 , 2019 wakubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo ya kuwezesha wananchi wa Watanzania katika sekta zote za kiuchumi na kuwawezesha upatikanaji wa masoko. Kikao kazi cha mkakati kiliongozwa na Bw Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade na Bibi Beng'i Issa Katibu Mtendaji wa NEEC .Picha na TanTrade 

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI APIGA 'STOP' KAMATAKAMATA YA NG'OMBE WANAOZAGAA MTAANI MANISPAA YA TABORA

$
0
0
Na Amisa Mussa

NAIBU Waziri Wa Mifugo Na Uvuvi Abdallah Ulega ameiagiza Serikali ya Mkoa wa Tabora kuitaka Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kusitisha mchakato wa ukamataji wa ng'ombe ambao wanadaiwa kuzagaa mitaani baada ya kuonekana kuna harufu ya rushwa.

Mbali ya rushwa katika kuutekeleza mchakato huo imedaiwa linawaumiza wafugaji na wafanyabiashara ya ng'ombe ambao wanafanyabiashara mnada wa Ipuli wilayani humo.

Kutokana na kuwepo kwa gogoro baina ya wafugaji na Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora Naibu Waziri Ulega mmetembelea mkoani humo ili kujionea hali halisi ambapo baada ya kusikiliza malalamiko kutoka kwa wafugaji ameamua kutoa maagizo ya kukamatwa kwa watendaji wa halmashauri waliohusika kutekeleza mchakato huo kwani kuna harufu ya rushwa.

Pia ameagiza Ofisa Mifugo Msaidizi Cornelius Masawe akamatwe na hivyo alikamatwa huku akimtaka ofisa hiyo kufanyiwa uchunguzi kwani ndio amekuwa akitekeleza agizo hilo la kukamata ng'ombe ndani ya manispaa hiyo.

Baada ya uamuzi huo Naibu Waziri huyo alipata fursa ya kusikiliza malalamiko ya wafugaji na wafanyabiashara ya ng'ombe ambao hawakusita kpaza uauti zao."Kilichofanyika sasa hivi ni kushika mashavu basi, tunamshukuru Mungu kwa sababu mimi nilikuwa na ng’ombe 45 kwa kumatwa na Masawe zimebaki ng’ombe 13 Nyingine zimeshaliwa,”alisema Alon mmoja wa wafugaji

Wafugaji Emmanuel Cosmas na Jani Kasunzu wamemueleza Naibu Waziri kuwa imefika wakati suala la suala la ng’ombe limekuwa ni dili kwa baadhi ya watumishi.Akiwa katika mnada wa Ipuli Manispaa ya Tabora na kusikiliza kilio cha wafugaji hao Naibu Waziri Ulega ameonesha kuguswa na malalamiko hayo ambapo aliamua kutoa msimamo wa Wizara.

“Ni lazima Oparesheni hii isimame ili iratibiwe vyema na hatimaye baadae ndio iendelea lasivyo tutawadhuru watu ambao hawana hatia,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aidha mwishoni mwa Wiki iliyopita wafugaji na wafanyabiashara wa ng’ombe waliingia katika mgogoro na Halmashauri ya Manispaa Ya Tabora hatua ilyosababisha jamii hiyo ya wafugaji kugoma kutumia mnada wa Ipuli kuuza na kununua ngo’mbe wilayani humo kwa kile kinachodaiwa kamatakamata ambayo imekuwa ikifanywa na Manispaa ya Tabora.
 Baadhi ya Mifugo

 Baadhi ya Wafugaji walipokuwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara wa mifugo katika Mnada wa Ipuli mkoani Tabora jana

Naibu Katibu Mkuu UWT Taifa ampongeza Rais Magufuli kwa kutoa fedha ujenzi wa kituo cha afya Pangani

$
0
0

BMG Habari .


Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Bara kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jesca Mbogo ametoa pongezi kwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha za ujenzi wa Kituo cha Afya Mwera kilichopo Wilaya ya Pangani mkoani Tanga.


Mbogo alitoa pongezi hizo jana ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Tanga, yenye lengo la kujionea utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/20 na namna inavyogusa maisha ya akina mama.


"Namshukuru sana Rais Magufuli kwa kuboreshea Kituo hiki kwani akinamama sasa watapata huduma za afya hapa na kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kwa kivuko hadi Pangani kutafuta matibabu". Alisema Mbogo ambaye ameanza ziara yake ya kwanza mkoani Tanga tangu ateuliwe kuwa Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara.


Mbogo pia alipokea shukrani za akina mama wilayani Pangani waliomshukru Rais Magufuli kwa juhudi zake za kuboresha huduma za afya nchini ikiwemo ujenzi wa Kituo cha Afya Mwera kitakachowarahisishia upatikanaji wa huduma za afya.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akisaini kitabu cha wageni.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo.

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akizungumza na akina mama wilayani Pangani (hawako pichani).

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo akizungumza na akina mama wilayani Pangani.

Akina mama wilayani Pangani wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo.

Zawadi

Naibu Katibu Mkuu UWT Tanzania Bara, Jesca Mbogo alipata fursa ya kupata mche maalumu kama ishara ya mwanzo moya wa maboresho ya huduma za afya kwa akina mama.

WAFUGAJI WAMPA ZAWADI YA DUME RAIS DK JOHN MAGUFULI,WAANDAMANA KWA AMANI BABATI

$
0
0
 Wafugaji kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wakiwa kwenye maandamano ya amani mjini Babati mkoa wa Manyara kumuunga mkono Rais John Magufuli kuhusu uamuzi alioutoa hivi karibuni juu haki za wafugaji nchini.
 Wafugaji kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wakiwa kwenye maandamano ya amani mjini Babati mkoa wa Manyara wakiwa na mifugo ambayo ni zawadi  ya Rais John Magufuli kuhusu uamuzi alioutoa hivi karibuni juu haki za wafugaji nchini.
 Wafugaji kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara wakiomba dua kwenye ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara mjini Babati wakiwa na mifugo ambayo ni zawadi  ya Rais John Magufuli kuhusu uamuzi alioutoa hivi karibuni juu haki za wafugaji nchini.
 Mkuu wa wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu akizungumza baada ya kupokea maandamano ya wafugaji kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara.
 Wafugaji wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara wakiwa kwenye maandamano ya amani mjini Babati mkoa wa Manyara wakiwa na mifugo ambayo ni zawadi  ya Rais John Magufuli kuhusu uamuzi alioutoa hivi karibuni juu haki za wafugaji nchini.
Mkuu wa wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu(kushoto) akipokea zawadi za mifugo kutoka kwa wafugaji baada ya kupokea maandamano ya amani ya wafugaji kwaniaba ya Mkuu wa mkoa wa Manyara.

WATENDAJI WATAKIWA KUYAFANYIAKAZI MAAGIZO WANAYOPEWA

$
0
0
Na Sekela Mwasubila, Afisa Habari Kondoa Mji
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa amewataka watendaji wa kata na mitaa kuyafanyia kazi maagizo yanayotolewa kutoka halmashauri kwani wananchi wana imani nao katika kuwaletea maendeleo.

Aliyasema hayo wakati akifungua kikao kazi kati ya watendaji hao na wakuu wa Idara kilichofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Uwekezaji Kondoa Mjini. Alisema kuwa watendaji hao ndio wasimamizi na wakurugenzi katika maeneo yao ya kazi hivyo wanapaswa kuwajibika ili kuhakikisha kata na mitaa yao inakuwa na maendeleo na huduma za msingi zinapatikana.

“Mkifanya vibaya nyie halmashauri yote itaonekana imefanya vibaya sababu tunafanya kazi kama timu ila nasikitika watumishi ngazi ya wilaya wanafanya sana kazi lakini ikifika kwenu hamfanyi kazi na kutimiza majukumu yenu mjitathmini.”Alisema Dakawa

Aidha aliongeza kwa kuwataka kusimamia miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato na kuwachukulia hatua wale wote ambao miradi itatekelezwa chini ya kiwango  na wao kutochukua hatua zozote kwa kisingizio cha kutokushirikishwa kwani miradi yote ipo chini yao.

“Pia kuna watendaji hapa nimepata habari ni wababe kwa wenyeviti wao wa mitaa hadi wanaogopwa hii haipendezi mkafanye kazi kwa kushirikiana lengo liwe moja tu kuwaletea maendeleo wananchi.” Alisisitiza Dakawa

Kwa upande wake Afisa Sheria wa Halmashauri Wakili Edward Mhina aliwataka watendaji kuepuka tabia ya kuingia mikataba na watu mbalimbali bila kushirikisha ofisi ya Mkurugenzi kwani mikataba yote ambayo haijapitiwa na Mwanasheria ni batili.

“Nawakumbusha watendaji ambao walipewa mashine za kukusanyia mapato na hawakupeleka fedha benki kufanya hivyo ndani ya wiki moja hadi jumatano ijayo wote wapeleke fedha benki ambao hawatapeleka tutawafikisha mahakamani.”Alisema Mhina

Akiongea kwa niaba ya watendaji Mtendaji wa Kata ya Kingale Samson Mtui aliushukuru uongozi wa halmashauri kwa kikao kazi hicho kwakuwa kimewakumbusha majukumu yao ambayo mengi walikuwa wakiyafanya kinyume na kuahidi kwenda kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Kikao kazi cha uongozi wa halmashauri na watendaji wa kata na mitaa kimefanyika kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao na kupatiwa mada mbalimbali kutoka idara na vitengo vya sheria, Manunuzi, Fedha,Mipango, Elimu Sekondari na Utumishi.
 Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Msoleni Dakawa akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi cha wakuu wa Idara na Watendaji wa kata na mitaa
  Watendaji wa kata na mitaa wakisikiliza kwa makini mada zilizowasilishwa katika kikao kazi kati yao na wakuu wa Idara.
 Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa Kaunga Amani akiwasilisha mada ya usimamizi wa miradi kwa watendaji wa kata na mitaa

Shule ya kata iliyoachwa kwa miaka 10 kusajiliwa mwaka huu Rukwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi kuhakikisha Shule ya Sekondari ya Ntatepa iliyopo kata ya Myula, Wilayani Nkasi inasajiliwa mwezi wa tatu mwaka 2019 ili kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao watahamishwa kutoka shule za kata za jirani na hatimae kuwapunguzia umbali wa kutembea wanafunzi wanaotoka katika kata hiyo kwenda kata za jirani kusoma. 

Amesema kuwa ili kuhakikisha kasi ya ujenzi wa shule hiyo inaongezeka atachangia bati 100 na kuwataka viongozi wote wa serikali za vijiji vitano vinavyounda kata hiyo vyenye kaya 2547 kuhakikisha kila kaya inachangia shilingi 5000 ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambao ulianza mwaka 2008 na kuwekwa jiwe la msingi mwaka 2013 na aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri.

“Mimi inaniuma sana kuona tangu mwaka 2008 hii shule, haijaanza, haijasajiliwa, lile jengo pale la waalimu nimesoma pale lile jiwe la msingi liliwekwa na Mwanri wakati huo akiwa Naibu Waziri TAMISEMI mwaka 2013 leo hii ni mkuu wa Mkoa wa Tabora, najisikia vibaya, miaka mingi 11 shule haianzi, basi na ianze mwaka huu, nitumie nafasi hii kuwahamasisha wanakata wote wa Myula, tuchangie shule imlizike,” Alisema.

Aliyasema hayo tarehe 11.1.2019, alipotembelea shule hiyo ili kubaini mkwamo uliopelekea shule hiyo kushindwa kusajiliwa na kuweza kusomesha wanafunzi, Aidha Wangabo alirudi tena tarehe 22.1.2019 kufanya harambee ili kupata fedha za kufanya ukarabati wa madarasa manne ya wanafunzi, nyumba ya mwalimu mkuu ambayo ilikuwa tayari pamoja na kumalizia madara mawili na maabara ambayo ilikuwa ndio kikwazo cha kusajiliwa kwa shule hiyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Nkasi Kusini Desderius Mipata alisema kuwa shule ambazo walitakiwa kufungua pamoja na shule hiyo tayari zimeshaanza kutoa wanafunzi wa kidato cha nne na baada ya kuona kuwa mwaka huu ufaulu umeongezeka ndipo alipoushirikisha uongozi wa wilaya ili kuona namna ya kukabiliana na vikwazo vinavyoifanya shule hiyo isisajiliwe ili waweze kuvikamilisha.

“Hatujafanikiwa hapa kwasababu viliongezeka vigezo vya kufanya shule isifunguliwe lakini pia na mkazo wa kusaidia, mwaka huu baada ya kuona ongezeko kubwa sana la ufaulu na upungufu wa madarasa tulikaa na Mkuu wa Wilaya tukatembelea hapa na kuhamasisha vijiji vyote kufanya songambele na kuwezesha kuendeleza miundombinu hii, madarsa mawili na maabara moja ili iwe ni vya kuanzia,” Alisema.  

Wakati akielezea sababu za kushindwa kusajiliwa kwa shule hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Missana Kwangura alisema kuwa uchache wa wanafunzi ulikwamisha kusajiliwa kwa shule hiyo pamoja na kutokuwepo kwa maabara lakini sasa wanafunzi ni wengi mno hivyo ni kuamilisha maabara tu ndio kutapelekea shule hiyo kusajiliwa na kuongeza kuwa shule hiyo inaweza kuanza kama shule shikizi ya shule ya sekondari Kate ambayo ni kata ya jirani wakati taratibu za usajili zikiendelea.

“Mkuu wa Mkoa tutapambana mwaka huu ili walau shule hii iweze kuanza mwaka huu hata kama kuwa shule shikizi ya shule mama ya Sekondari ya Kate, kata hii pia ina vijiji vitano kama ilivyo kata ya Kate, tuombe tu kushirikiana wote na wananchi na ushauri ambao umeutoa walau wa kutumia eneo hili vizuri, tutahakikisha hii shule walau inaweza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza na hata waalimu wachache wa kuanzia,” Alimalizia. 

Katika harambee iliyoendeshwa na Wangabo ii kumalizia shule hiyo zilipatikana shilingi milioni 6.9, mifuko ya saruji 240, mbao za kupaulia 200, maguni ya mahindi 3, gunia 1 la maharage, mbuzi 1, kondoo 1, na kuku pamoja na gunia 2 za mbegu za maharage kwaajili ya kilimo hicho katika eneo la shule lenye ukubwa wa ekari 100. Michango yote ikiwa ni ahadi pamoja na mawasilisho.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akihamasisha uchangiaji wa fedha na vifaa katika kuhakikisha Shule ya Sekondari Ntatepa inakamilika na kusajiliwa mwaka huu 2019.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Myula, Wilayani Nkasi walioshiriki kwenye Harambee ya kuchangia umaliziaji wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Ntatepa.
  Picha ya pamoja kati ya Wananchi wa Kata ya Ntapepa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo mara tu baada ya kufanya harambee ili kuhakikisha shule ya Sekondari Ntapepa, Kata ya Myula, Wilayani Nkasi. 
  Majengo ya madarasa yanayotakiwa kukarabatiwa ili shule ya Sekondari Ntapepa iweze kuanza, madarasa hayo yameanza kujengwa tangu mwaka 2008.
 Nyumba ya Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Ntapepa iliyojengwa na kuwekewa jiwe la Msingi mwaka 2013.
 Majengo ya Maabara na madarasa yanayotakiwa kumaliziwa ili shule ya Sekondari Ntapepa iweze kusajiliwa na wananfunzi waanze kusoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 07 kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbalimbali ikiwemo kuingiza bidhaa bila kulipia ushuru

$
0
0
Kuhusiana na uingizaji bidhaa nchini bila kulipa kodi Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wanne, wakiwemo, Obley Sambakusi (32) raia wa Malawi, Mfanyabiashara na Mkazi wa Lilongwe, Tamandani Kachimela [31] Mkazi wa Lilongwe Malawi, Imtiaz Ahmed (45) dereva na Mkazi wa Kyela, Boaz Salvatory (28) dereva na Mkazi wa Kyela.

Watuhumiwa hao walikamatwa tarehe 21.01.2019 majira ya saa 21:15 usiku katika Roadblock Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoani Mbeya wakiwa na bello hamsini (50) za vyandarua, kila bello moja likiwa na vyandarua 50 ikiwa ni jumla ya vyandarua 2500 wakiviingizwa nchini bila kulipia ushuru wakitumia gari zenye namba za usajili T.471 DDY aina ya Toyota Noah na T.301 CTX aina ya Toyota Noah kutoka nchini Malawi na kuhusiana na shtaka hilo Upelelezi unaendelea.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linalishikilia gari lenye namba za usajili T.867 DHK aina ya Toyota Noah likiwa limebeba mafuta ya kula aina ya MERU GOLD ndoo 45 zenye ujazo wa lita 20 na mafuta aina ya NONA PALM dumu kumi zenye ujazo wa lita 20 toka nchini Malawi. 

Gari hilo likiwa na bidhaa hizo ambazo hazijalipiwa ushuru lilikamatwa tarehe 22.01.2019 saa 06:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya baada ya dereva wake kusimamishwa na askari na kukaidi amri halali na ndipo askari walipotumia mbinu za nyingine na kufanikiwa kukamata gari hilo. Dereva wa gari hilo alikimbia na kutelekeza gari hiyo. Juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia Enele Kakisungu (31) Mkazi wa Kagwina, Grace Evance (36) Mkazi wa Uyole, na Ruth Andrew (35) Mkazi wa Kiwira Road wakiwa na mafuta ya kupikia lita 50 aina ya Kook Well toka nchini Malawi na Juice box 11 za unga aina ya Baks kwa ajili ya kutengenezea juice. Watuhumiwa walikamatwa tarehe 19.01.2019 saa 15:00 alasiri huko katika road block - Kayuki, Kata ya Ilima, Tarafa ya Pakati, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa walikuwa wakiingiza bidhaa hizo nchini bila kulipia ushuru kwa kupitia njia za panya.
 Magari yaliyokamatwa kwenye matukio mawili tofauti yakiwa na bidhaa zilizokwepa ushuru
 Meneja wa Forodha Mikoa ya Mbeya na Songwe Johnmasa Michael akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuhusiana na uingizaji bidhaa nchini bila kulipa kodi 
 Ndoo za mafuta ya kupikia na vyandarua vilivyokamatwa kwa kukwepa kulipia ushuru wa forodha.

FEMINA YAWAKUTANISHA VIJANA KOTE NCHINI KUSHEREKEA MIAKA 20 YA SHIRIKA HILO

$
0
0
* Wanafunzi waiomba serikali kutambua na kuunga mkono jitihada za FEMINA nchini kote.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
SHIRIKA lisilo la kiserikali la FEMINA linaloshughulika na masuala ya vijana hasa kwa kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia pamoja na shughuli ya ujasiriamali limetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake kwa kuwakutanisha vijana kutoka klabu zote nchini na kutoa elimu kuhusiana masuala ya afya na fursa za kiuchumi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Meneja wa idara ya uhamasishaji jamii kutoka FEMINA Nashivai Mollel amesema kuwa licha ya kusherekea miaka 20 ya FEMINA wamewakutanisha vijana hao kwa lengo la kutoa mafunzo kama vile elimu ya afya ya uzazi na fursa za kijasiriamali bila kutegemea kuajiriwa pekee.

Amesema kuwa  malengo ya mkutano huo ni kuleta mabadiliko chanya pamoja na kutatua changamoto hizo kwa vijana kwa kushirikiana na walimu walezi wa klabu hizo.

Pia ameishukuru Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa afya, maendeleo ya jamii, wazee, jinsia na watoto Ummy Mwalimu kwa jitihada wanazoonesha katika kuwasaidia vijana. Na amehaidi kuwa wataendelea kuwasaidia vijana katika nyanja mbalimbali kwa kuwasaidia vijana wengi zaidi.

Kuhusiana na mchango wa klabu za FEMA katika kuchangia ufaulu wa wanafunzi mashuleni, mlezi wa klabu ya Mnyuzi, Charles Mayombo amesema kuwa klabu hizo zimekuwa chachu kubwa kwa wanafunzi katika kufanya vizuri katika masomo yao, hiyo ikiwa ni pamoja na sifa mojawapo ya kuwa mwanaklabu ya FEMA lazima mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yake na hiyo imedhihirika kwa matokeo ya kidato cha pili yaliyotoka hivi karibuni kwa walezi wote wa klabu za FEMA kuleta mrejesho mzuri kuhusiana na matokeo hayo ambapo wanafunzi wengi walionekana kufanya vizuri.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki mkutano huo wameeleza kuwa klabu hizo zinasaidia sana kwa kuwa wanapata elimu ya kujitambua, nidhamu pamoja na kupambana na changamoto wanazopitia katika masuala ya ukuaji na wameiomba Serikali kuzitambua na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na FEMINA.
 Meneja idara ya uhamasishaji jamii Nashivai Mollel akizungumza na wanafunzi kutoka katika Mikoa mbalimbali nchini katika mkutano huo uliowakutanisha katika kusherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, leo jijini Dar es Salaam.
 Walimu walezi wa klabu za FEMA, (Walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa FEMINA mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao kwa kuonesha mchango chanya katika klabu hizo mashuleni.
 Mkurugenzi wa Habari wa FEMINA Amabilis Batamula (katikati) akizungumza katika mkutano huo wa kuadhimisha miaka 20 ya FEMINA uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Meneja idara ya uhamasishaji jamii kutoka FEMINA, Nashivai Mollel.
 Walimu kutoka Mikoa mbalimbali nchini wakiwa na vyeti walivyotunukiwa katika mkutano wa kuadhimisha miaka 20 ya FEMINA uliofanyika leo jijini Dar es Salaam na hiyo ni kutokana  na  kuonesha juhudi za ziada katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia vijana.
Meneja idara ya uhamasishaji Jamii, Nashivai Mollel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.

TANESCO ARUSHA,DC MURRO WADHIBITI VISHOKA ARUMERU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
 
SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) Mkoa wa Arusha limesema kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jery Murro wamefanikiwa kudhibiti vishoka na wahujumu wa miundombinu ya shirika hilo.

Hayo yameelezwa na Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Herini Mhina wakati anazungumzia hatua ambazo zimefanyika katika kukabiliana na vishoka pamoja na wahujumu wa miundombinu.

Kuhusu vishoka amesema TANESCO wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kukabiliana na vishoka na baadhi ya hatua hizo kwa wale ambao wanabainika wanachukuliwa hatua.Pia wamekiwa wakiondoa miundombinu ya umeme ambayo imewekwa na vishoka.

"Maeneo ya USA tuling'oa nguzo ambazo ziliwekwa na vishoka,pia tumekuwa tukiondoa hata LUKU ambazo tunabaini zimewekwa na hao vishoka.Tumechukua mbalimbali ikiwamo ya wanaobainika kuchukuliwa hatua ya kupelekwa Polisi sheria ichukue mkondo wake.Tumefanikiwa sana kuwadhibiti vishoka kwani TANESCO tupo makini .

" Tunashirikiana kwa karibu na Mkuu wa Wilaya Murro,kila tunapomueleza katika hili anatoa ushirikiana na kwenye matukio mengi yanayohusu kukamata vishoka au wanaohujumu miundombinu amekuwa pamoja nasi,"amefafanua Mhandisi Mhina.

Kwanini Murro amekuwa akishiriki kwa karibu kukomesha vishoka,Meneja Mhina amejibu kuwa katika Wilaya ya Arumeru tatizo la vishoka na wanaohujumu moundombinu lilikuwa kubwa na katika kulishughulikia walimpa taarifa Mkuu huyo wa Wilaya na tangu alipofika wanashirikiana sana.

Ameongeza katika hujuma ya miundomboni nayo wamefanikiwa na wanaendelea kufuatilia hatua kwa hatua ili kuwabaini wenye kuiharibu miundomboni."Kuna watu wanaiba waya wa mita 10,sasa hiyo ni hujuma ya miundombinu ya umeme."

Kwa upande wake  Menaja Mwandamizi wa Miradi TANESCO Mhandisi Emmanuel Manirabona amezungumzia mikakati ya shirika hilo la kudhibiti vishoka ambapo amefafanua moja ya mkakati ni kuhakikisha vifaa vyote vya shirika hilo vinabaki kuwa mali ya shirika.

Amesema hivyo hata mfanyakazi au mtumishi yoyote wa TANESCO ataruhusiwa kutumia mali ya shirika hilo akiwa mfanyakazi na baada ya hapo hataruhusiwa.

"Ukifuatilia utaona matangazo pale inapotokea kuna mfanyakazi wetu ameondolewa TANESCO na wakati mwingine tunasema kuwa mtu fulani si mfanyakazi wetu na hatutahusika na chochote ambacho atakifanya,"amesema Mhandisi Manirabona.

Balozi Possi awasilisha Hati za Utambulisho Bulgaria

$
0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anawakilisha pia nchini Bulgaria , Mhe. Dkt. Abdallah Posi akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Bulgaria, Mhe. Rumen Radev. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu ya nchi hiyo hivi karibuni. 
Mhe. Balozi Dkt. Posi akizungumza na Mhe. Rais Radev mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho 
Mhe. Balozi Dkt. Posi akiagana na Mhe. Rais Radev mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho 
Mhe. Balozi Dkt. Posi akiwa mbele ya gwaride la heshima alipowasili Ikulu ya Bulgaria kwa ajili ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa nchi hiyo. 

POLISI KILIMANJARO YANASA DAWA ZA KULEVYA KILO 80.

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga,Moshi.

KIKOSI cha  Pikipiki cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kimefanikiwa kukamata kilogramu 80 za Dawa za Kulevya  aina ya Mirungi iliyokuwa ikisafirishwa kwa kutumia pikipiki kutoka nchi jirani ya Kenya kuelekea mkoa wa Arusha.

Majani hayo ya Miringi yaliyokuwa yamefungwa katika vifurushi vidogo vidogo zaidi ya 50 na kisha kuwekwa kwenye mfuko mmmoja  mkubwa maarufu kama Kiroba yalipatikana baada ya askari Polisi kujaribu kumkimbiza msafirishaji wa Mirungi ambaye alitekeleza pikipiki na mzigo huo.

Kamanda wa Polisi mkao wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa alithibitisha kukamatwa kwa Dawa hizo za kulevya katika eneo la Uchira ambapo msafirishaji huyo alifanikiwa kukimbia na kuiacha pikipiki aliyokuwa akitumia.

“Mkoa wa Kilimanjaro kumekuwa na tatizo kubwa sana, linalohusiana na usafirishaji wa Mirungi  na wasafirishaji  wamekuwa  wakitumia barabara kuu, sasa askari wa pikipiki  ambao wanafanya kazi hii ya kufukuzana na hawa watu wa mirungi wamefanikiwa kukamata kilogramu 80 za Mirungi”alisema Issah.

Alisema kundi la wasafirishaji wa Dawa hizo za kulevya ambao wamekuwa wakisafirisha kutoka nchi ya Kenya kupitia mpaka wa Holili pindi linapoingia barabarani limeonekana kuwa tishio na hatari kwa usalama wa watu wengine barabarani kwa namna wanavyoendesha pikipiki zao.

“Siku ya leo(Jana) imekamatwa pikipiki moja yenye namba MC 168 CAZ ambayo imetoka nchini Kenya lakini  ni ya Tanzania  na ikiwa na gunia moja kubwa lenye uzito wa kilo 80,nah ii inaonyesha ilikuwa bado  hawajagawana kabisa  lakini askari wetu kwa ushujaa wao wamewafukuza hawa watu  na matokeo yake wamekamata”alisema Issah .

Kamanda Issah alisema  baada ya kufungua mfuko huo walibaini uwepo wa vifurushi vingi vikiwa vimefungwa Majani ya Mirungi kwa njia tofauti tofauti huku ikiwa imepewa majina maalumu ya wahusika wa Dawa hizo.
 MIrungi hiyo naona ilivyohifadhiwa na watuhumiwa hao tayari kwa kusafirishwa. 
 Kamanda wa Polisi mkao wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issa akionesha Dawa za kulevya aina ya Mirungi walioikamata eneo la Uchira,ambapo msafirishaji huyo alifanikiwa kukimbia na kuiacha pikipiki aliyokuwa akitumia.
 Mirungi iliyokamatwa ikikusanywa na kuwekwa vizuri


DAWASA YAMTUA NDOO YA MAJI MAMA MARIA NYERERE

$
0
0
Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere (kulia) akiwakaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kulia) pamoja na wageni wengine waliokuwa wameambatana nao kukabidhi mradi wa tenki la maji lililokarabatiwa na DAWASA. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni. Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni. Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja akitoa maelezo machache kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange na wageni waalikwa. Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA Neli Msuya akitoa ufafanuzi wa mradi huo. Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja akitoa maelezo juu ya mradi huo mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (wa pili toka kushoto) na Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere pamoja wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange (Katikati), akizungumza mbele ya wanahabari juu ya mradi wa ukarabati wa tenki la maji alilokabidhiwa Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere (kushoto). Pembeni ni Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja (kwanza kulia). Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere akitoa shukrani zake mbele ya wageni waliohudhuria hafla ya kukabidhi tenki la maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere lililokarabatiwa na DAWASA hivi karibuni. Wafanyakazi wa DAWASA, Wanahabari na wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini. 


Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) mapema leo amekabidhi tenki la maji lenye ujazo wa lita 170,000 kwa mke wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere. Tenki ambalo lilikuwa halitumiki na sasa litatumika na litawawezesha kupata maji nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumaliza kukabidhi tenki hilo Msasani, jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amesema wameamua kukarabati tenki hilo lilokuwa halitumiki kwa muda mrefu kutokana na miundombinu ya tenki kuwa chakavu nakupelekea kuwa na ukosefu wa maji ya kutosha nyumbani kwa Mama Nyerere.

Amesema maji ni kila kitu katika maisha ya binadamu hivyo hatuna budi kuyalinda na kuyatunza ili yaweze kututunza pia. Nae Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Makongoro Nyerere ameishukuru DAWASA kuweza kulikarabati tenki hilo lililokuwa limekufa na halitumiki kwa muda mrefu. 

"Kiukweli sina cha kusema zaidi ya kutoa shukrani zangu za pekee kwenu kwa niaba ya mama yangu, hili tenki lilikuwa halitumiki kwa muda mrefu ila nyie mmelifufua na sasa tunapata maji ya kutosha," amesema Makongoro Nyerere. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema wao walijitoa kukarabati tenki hilo kwa kuondoa laini ndogo ya inchi moja ilikuwa inasababisha kutumia mota kuvuta maji ilikuwezesha kupata maji yakutosha hivyo kupelekea bili ya maji kuwa kubwa pamoja gharama za umeme.

KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII YAPOKEA TAARIFA YA BODI YA MIKOPO

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Ndg. Abdul Razaq Badru  akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu kwa kipindi cha nusu mwaka 2018/2019 mbele ya  Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.
 Mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mheshimiwa Hawa Ghasia akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokuwa ikipokea na kujadili Taarifa ya utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu kwa kipindi cha nusu mwaka 2018/2019 katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Selukamba akifafanua jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokuwa ikipokea na kujadili Taarifa ya utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu kwa kipindi cha nusu mwaka 2018/2019 katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.

TICTS yaweka rekodi mpya, kiwango cha kuhudumia kontena kufikia 592,000 mwaka 2018

$
0
0
*TICTS yatoa shukrani kwa Serikali, TPA, TRA, wateja na hasa kwa wafanyakazi wa TICTS kwa kufanikisha mafanikio haya makubwa.

Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini (TICTS), ikiwa kama kampuni pekee ya huduma kwa kontena inayofanya kazi katika bandari kubwa nchini Tanzania imefikia hatua mpya ya mafanikio na kuweka rekodi mpya ya kuhudumia shehena ya kontena 592,000 katika mwaka 2018. Rekodi ya mwisho iliwekwa na kampuni hiyo mwaka 2017 ambapo ilihudumia kontena 501,690. Katika mwaka wa 2018, TICTS pia iliweka rekodi ya mwezi katika mwezi wa Agosti kwa kuweza kuhudumia kontena 54,447 na rekodi ya kontena 31,239 zilihudumiwa katika mageti katika mwezi Machi 2018.

Ongezeko la shehena ya ndani na kwa ajili ya  nje ya nchi imeongezeka kwa asilimia 18, zaidi ya mwaka 2017. Mizigo ambayo ni kwa  nchi mbalimbali zinazotumia bandari yetu iliongezeka kwa wastani zaidi ya asilimia 38.9 kwa mwaka 2018.Ongezeko la shehena linahitaji ufanisi na uharaka katika utoaji mizigo ili kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini na hivyo kuwezesha TICTS na Bandari kuongeza ufanisi na uwezo wa kuhudumia shehena kubwa zaidi. Kampuni imefanikiwa ukuaji huu licha ya changamoto za mazingira ya kiabiashara kimataifa na katika kanda.

Afisa mkuu Mtendaji, Jared Zerbe alisema, "Msaada na ushirikiano tunaopata kutoka kwa Serikali ya Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA), wafanyakazi wetu, wateja na wadau wanaotumia bandari hii ndio imekuwa chanzo cha ukuaji wa huduma za TICTS katika mwaka 2018. Binafsi, najivunia sana kwa timu yetu nzuri sana ya wafanyakazi wa TICTS ambao wamekuwa wakifanya kazi pamoja vizuri sana wakipambana na changamoto ya kuhudumia ongezeko la shehena."

Kuongeza ufanisi ili kuweza kuhudumia shehena hii inayokua, TICTS itaendelea kufanya kazi na Serikali ya Tanzania, TPA, TRA na wateja na kufanyia kazi changamoto zote zinazoathiri utolewaji haraka wa mizigo katika bandari ya Dar-es-salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Kimataifa ya kuhudumia shehena ya kontena bandarini (TICTS), inayoshughulika na huduma za kontena katika bandari ya Dar es Salaam, Tanzania, Mr Jared Zerbe akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu TICTS kuweka rekodi mpya ya kuhudumia shehena ya kontena 592,000 katika mwaka 2018. Kulia ni Mr Donald Talawa, Mkurugenzi wa shirika na maendeleo (Director of Corporate and Development).

Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kuchapisha Taarifa za uongo dhidi ya Rais Dkt. Magufuli

$
0
0
 Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
MFANYABASHARA, Henry  Munisi (30). Mkazi wa mkoani Mbeya, leo Januari 22, 2019 amepandishwa katika kizimba  cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais Magufuli.

Akisoma hati ya Mashtaka wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Desemba 28, Mwaka Jana huko Jijini Mbeya.
Imedaiwa kuwa,  siku ya tukio mshtakiwa Munisi kupitia ukurasa wake wa Facebook  alichapisha taarifa  za uongo zinazosema "Jinsi Magufuli alivyochota TRIL. 1.5 za ATCL akitumia  ujanja wake wa kuleta ndege ili atuibie" huku akijua taarifa  hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha umma. 

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana a baada ya kufanikiwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini bond ya Sh. Laki tano.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka,  upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 6. 2019.

BENKI YA NMB YASAIDIA ELIMU WILAYA ZA MOMBA NA ILEJE

$
0
0



Wanafunzi wa Shule ya sekondari Ileje wakionyesha furaha yao baada ya kupokea msaada wa viti (stuli) 184 vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 ambavyo ni miongoni kwa msaada uliotolewa na NMB Bank kwaajili ya kuboresha masomo ya sayansi mashuleni wilayani Ileje na Momba za jijini Mbeya. Benki ya NMB juzi ilitoa bati 254 kwa Halmashauri ya Tunduma wilayani Momba, Madawati 50 kwa shule ya msingi Nyerere na Stuli 184 kwa shule za sekondari Ileje na Kafule vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

Wanafunzi wa Shule ya sekondari Ileje wakiwa wamebeba madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwaajili ya shule ya Msingi Nyerere Wilayani Ileje Mkoani Songwe. Benki ya NMB juzi ilitoa bati 254 kwa Halmashauri ya Tunduma wilayani Momba, Madawati 50 kwa shule ya msingi Nyerere na Stuli 184 kwa shule za sekondari Ileje na Kafule vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

Wanafunzi wa Shule ya sekondari Ileje wakiwa wamebeba madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwaajili ya shule ya Msingi Nyerere Wilayani Ileje Mkoani Songwe. Benki ya NMB juzi ilitoa bati 254 kwa Halmashauri ya Tunduma wilayani Momba, Madawati 50 kwa shule ya msingi Nyerere na Stuli 184 kwa shule za sekondari Ileje na Kafule vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 25.

 
WAKUU wa Wilaya za Ileje na Momba Mkoani Songwe wamewapigita magoti taasisi, makampuni na mashirika kujitokeza kusaidia miundombinu ya elimu ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitohaza za Serikali kuwahudumia wananchi.

Wakuu hao ni Jumaa Irando wa Momba na Joseph Mkude wa Ileje walitoa rai hiyo jana kwa nyakati tofauti wakati wakipokea msaada wa vifaa vya shule kutoka Benki ya NMB ambayo ilitoa bati 254 kwa Halmahauri ya Tunduma Wilaya ya Momba na madawati 50 kwa shule za Msingi Nyerere na sturi 184 za maabara shuleni kwa shule za Sekondari za Ileje na Kafule zote za Wilayani Ileje huku vyote vikigharimu Sh25 milioni.

Irando alisema Mji wa Tunduma ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi kutokana na ongezeko kubwa la watu hivyo wamekuwa na changamoto lukuki kwenye suala la miondombinu ya shule kwa Serikali pekee kulitimiza bali kwa kuungwa mkono na wadau mbalimbali kama walivyofanya NMB.“Kwa kweli tunachangamoto kubwa sana hapa Tunduma, kuna ongezeko kubwa la watoto wanaoanza darasa la kwanza kila mwaka tofauti na makisio au matarajio tunayokuwa tumejiwekea.

Jambo hili linafanya kuwa na msongamano mkubwa mashuleni kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati pia, hivyo NMB mmetuangalia kwa jicho la pekee kabisa kuona tunahitaji msaada wenu na wadau wengine waige hili jambo kwa ajili ya kuisadia jamii yetu,”

Alisema mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu yanahitaji kuungwa mkono na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kama inavyofanywa na Benki ya NMB.Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Joseph Mkude alisema imetekeleza wajibu wao na thamani yao kwa Watanzania hususani wananchi wa Ileje ambao kimsingi wapo pembezoni kabisa mwa nchi.

Alisema ‘Nawashukuru sana NMB kutukubalia ombi letu na leo hii kutuletea sturi na madawati kwetu sisi tunauthamini mno mchango wenu na katika hili tunazidi kuwaunga mkono kwa jitihada zenu, na tuwaahidi tutahakikisha vifaa hivi vinatunzwa ili vidumu kwa muda mrefu’.

Awali Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola alisema benki ya NMB inatambua umuhimu wa elimu na afya kwa Watanzania hivyo katika kipindi cha mwaka huu wa 2019, NMB imetenga Sh1 bilioni kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwamo afya, elimu na majanga ya dharula kwa nchi nzima.

Hivyo benki hiyo itaendelea kusaidia katika sekta hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za Serikali za kuwahudumia wananchi wake. Alisema NMB ni wadau muhimu kwa Serikali na Watanzania hivyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa sababu jamii wanayoisaidia ndiyo inayowawezesha kupata faida katika biashara yao.

“Tunambatua changamoto ya elimu na afya, sisi NMB tunazipa kipaumbele sana kwa sababu hizi sekta mbili ni muhimu mno katika ustawi wa jamii yetu,” alisema Chilongola.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images