Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Maalim Seif akutana na Wazanzibar wanaoishi jijini Dar

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wazanzibar wanaoishi Dar es Salaam, wajitokeza kumsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, katika hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwapungia mkono wananchi wakati akitoka katika ukumbi wa hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam, baada ya kuzungumza na Wazanzibari wanaoishi Dar es Salaam. (picha ya Salmin Said, OMKR.

MHE. ASHA ROSE MIGIRO ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA, LONDON

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Dk. Asha-Rose Migiro atembelea Ubalozi wa Tanzania hapa London, kwa lengo la kuwasabahi maafisa wa Ubalozi na kuwapatia taarifa mbalimbali za maendeleo ya ushiirikiano na vyama marafiki na CCM, hususan Chama cha Labour cha Uingereza.

Mhe. Dk. Migiro alipita Ubalozini akitokea mji wa Brighton, Kusini mwa Uingereza alikokuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa wa Chama cha Labour uliofanyika huko kuanzia tarehe 22 hadi 25 Septemba 2013. Katika mazungumzo yake na maafisa hao Dk. Migiro aliwadokeza kuwa akiwa Brighton alifanikiwa kukutana na kuanzisha mawasiliano na maafisa mbalimbali wa Chama cha Labour kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano wa vyama vyao.
Mheshimiwa Dk. Migiro akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Ubalozi. Kutoka kushoto ni Amos Msanjila, Allen Kuzilwa, Rose Henry Kiondo, Wema Kibona, Idris Zahran, Caroline Kitana Chipeta na Yusuf Kashangwa.

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya Kilwa Jazz Band ya 'Napenda nipate lau nafasi' si ya kawaida

MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JUMUIYA YA MADOLAWAFANYIKA MJINI NEW YORK.

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akiwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Kamalesh Sharma  mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola uliofanyika tarehe 26 Septemba, 2013 Mjini New York sambamba na Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ili kujadili masuala muhimu kuhusu jumuiya hiyo.


Mhe. Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Peter Kalaghe wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya hiyo .

Mhe. Membe akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, Mhe. G.L. Peiris kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoandaliwa na nchi hiyo na kufanyika mwezi Novemba, 2013

 Mhe. Peiris akimpatia maelekezo Afisa wake huku Mhe. Membe akisikiliza.




Mhe. Membe akiteta jambo na Balozi Adonia Ayebare ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola

Mhe. Membe akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Mhe. Hannah Tetteh mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola.
 ----------------------------------------
Habari na picha na Rosemary Malale
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Mjini New York sambamba na Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kujadili masuala mbalimbali muhimu kuhusu Jumuiya hiyo.
Wakati wa Mkutano huo, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Kamalesh Sharma alitoa taarifa kwa Mawaziri kuhusu kupitishwa kwa Mpango Mkakati wa miaka minne  kuanzia mwaka 2013/2016 ulioandaliwa na Sekretarieti ya Jumuiya hiyo ili kuiwezesha kukidhi mahitaji ya nchi wananchama. Mpango Mkakati huo umezingatia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha nchi wanachama zinafuata utawala wa sheria, zinaimarisha demokrasia, zinaheshimu haki za binadamu pamoja na kuzingatia usawa wa kijinsia.
Katika maelezo yake, Mhe. Sharma alisema kuwa, Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola inaendeleza jitihada zake kuzisaidia nchi wanachama kuimarisha demokrasia na maendeleo endelevu ambapo pamoja na mambo mengine waangalizi katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika nchi wanachama wamekuwa wakipelekwa ikiwa ni pamoja chaguzi zilizofanyika hivi karibuni katika nchi na Ghana, Maldives na Sri Lanka.
Aidha, Mawaziri hao walipata fursa pia ya kupitia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Jopo la Watu Mashuhuri wa Jumuiya hiyo (EPG) kuhusu mageuzi katika Jumuiya hiyo. Vile vile ilielezwa kuwa, Katika kutekeleza mapendekezo hayo, Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola imeanzisha mipango mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuunda Kikundi cha Wataalam kwa ajili ya kutafuta fedha  ili kuiwezesha Sekretarieti kuzisaidia nchi wanachama zilizoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na zile zinazoendelea.
Katika hatua nyingine, Mawaziri  hao  walipokea  taarifa kuhusu maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali (CHOGM) unaotarajiwa kufanyika mjini Colombo, nchini Sri Lanka mwezi Novemba, 2013.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo wa CHOGM ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sri Lanka, Mhe. G.L. Peiris alisema kuwa, nchi yake imekamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mkutano huo na kuwahakikishia Mawaziri hao kuwa hali nchini kwake ni ya amani na usalama tofauti na taarifa zinazotolewa na baadhi ya nchi kuwa hali si shwari nchini humo.
Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama 54 wa Jumuiya ya Madola ambayo Kiongozi wake Mkuu ni Malkia Elizabeth II wa Uingereza.

Article 14

NMB YADHAMINI WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UWEKEZAJI

$
0
0
 Afisa wa Benki ya NMB Curthbert Zimbwe akiwaelezea Wajasiriamali jinsi ya kupata mikopo midogo midogo kutoka NMB. Wajasiriamali wanaohudhuria mafunzo mbali mbali ya siku tatu Kwenye viwanja vya Mnazi mmoja kutoka kwa wadau tofauti NMB ikiwa miongoni mwa wadau na wafadhili wakubwa wa mafunzo hayo.

Afisa wa Benki ya NMB Abdul Kandoro akiwaonyesha wajasiriamali kadi ya Benki ambayo mteja anaipata papo hapo kwa kufungua akaunti ya Chap Chap. Wajasiriamali wanaohudhuria mafunzo mbali mbali ya siku tatu Kwenye viwanja vya Mnazi mmoja kutoka kwa wadau tofauti NMB ikiwa miongoni mwa wadau na wafadhili wakubwa wa mafunzo hayo.

NATURAL PRODUCTS FOR your skin

$
0
0

Aloe Fleur de Jouvence-Flower of Youth is one of the most effective restorative beauty collections ever assembled. It is a collection of six wonderful components – each designed to fill a special part in a complete regimen of facial skin care.

To create one of the most effective restorative beauty regimes ever assembled, we took pure, stabilized Aloe Vera gel, combined it with nature’s own collagen, and added exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants.

Each product in Aloe Fleur de Jouvence has been developed with great care and attention to the daily needs of your skin. We start with pure, Stabilized Aloe Vera gel, and combine it with nature’s unique cellular substance, Collagen, along with exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants. This creates a unique skin care range that helps counteract the threat of time, weather and environmental elements. The preventive and restorative Aloe Fleur de Jouvence program provides a daily skin care regime to help promote the naturally occurring attributes of youth, vigor, freshness and radiance of the skin.

Aloe Vera has always been great for the skin. Now, pamper yourself even more with Aloe Fleur de Jouvence!

The Aloe Fleur de Jouvence Collection includes:
Aloe Cleanser
Rehydrating Toner
Firming Day Lotion
Recovering Night Creme
Mask Powder
Aloe Activator
Mixing spoon, applicator brush

For more information Call 0718 14 40 39 / 0786 76 60 28

Ufunguzi wa tawi la CCM Ohio Jumamos Columbus, Ohio

$
0
0
Watanzania wenzetu,
 
Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba Jumamosi hii (i.e. September 28th, 2013) kutakuwa na ufunguzi wa tawi la CCM Ohio kuanzia saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni  kwenye ukumbi wa Palace The Square ( 5817 Emporium Square, Columbus Ohio 43229)
 
Mgeni rasmi katika ufunguzi huu atakuwa Mheshimiwa  Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania (pichani).
 
Hii ni nafasi ya sisi wote kama Watanzania, sio lazima uwe mwanachama wa CCM au chama chcochote cha siasa, kupata fursa ya kukutana na watanzania wenzako kutoka miji mbalimbali ya Ohio na Kiongozi/Viongozi wa nchi yetu.
  
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
 
Fredd Mujuni - Mwenyeketi : 216- 225-1585
E. Joe Ngwilizi Muhaya - Katibu Mkuu - 330-361-1933
Kelvin Mkwawa - Katibu mwenezi- 614 -596-3762
Tumaini Mosha - Mjumbe Mkuu - 216- 645-6171
 
 Ahsanteni,
 
Mungu Ibariki Tanzania

Pinda atembelea Maghala ya Kitengo cha Usalama wa Chakula, (NFRA) mjini Arsha

$
0
0

 Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akikagua akiba ya mahihindi wakati  alipotembelea   Maghala ya Kitengo cha  Usalama wa Chakula, (NFRA) mjini Arusha . Kulia  kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo,  chakula   na Ushirika, Mhe Adam Malima.
Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda akikagua akiba ya mahihindi wakati  alipotembelea  Maghala ya Kitengo cha  Usalama wa Chakula, (NFRA) mjini Arusha. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo,  chakula   na Ushirika, Mhe Adam Malima.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

somo la jinsi ya kufunga tai

Mwanamuziki Jhiko Man alonga na Globu ya Jamii

$
0
0
Timu ya Globu ya Jamii imeweza kumtembelea Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kiafrika,Jhiko Man mwenye makazi ya Mjini Bagamoyo mkoani Pwani na kufanya nae mahojiano mafupi juu ya Muziki wa Kitanzania na Kiafrika kiujumla.

mnuso wa chadema uk reading oktoba 5, 2013

$
0
0
CHADEMA UK inawakaribisha waTanzania na wapenzi wote wa CHADEMA kwenye barbeque (End of the Year BBQ) party itakayofanyika Comunity Hall/Back Garden, 44 Watlington street, RG1 4RJ Reading tarehe 05-10-2013. 
Mgeni rasmi atakuwa ni mwanasiasa mwenye kipaji cha pekee na muhimili muhimu wa CHADEMA – katibu wa CHADEMA Arusha na kanda ya kaskazini ndugu Amani Golugwa.
Itakuwa ni siku nzuri kujiburudisha kwa nyama choma, vinywaji na muziki free of charge. Lengo ni kuwakutanisha wapenda maendeleo katika kubadilishana mawazo na kujumuika katika harakati za kimaendeleo kwa taifa.
Hii shughuli si kwa wanaCHADEMA peke yake. Kila mTanzania mpenda maendeleo anakaribishwa kuhudhuria. Ni wakati mzuri kukaa pamoja tukijiburudisha huku tukibadilishana mawazo on party lines kiutu uzima bila malumbano. Wakati ni huu kuonesha utashi na ukomavu wa kisiasa.

Chakula na vinywaji bure!!!


Karibuni wote

MTANZANIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA KAMATI YA WATAALAMU NA MAMENEJA YA AFRICA NA PIA MAKAMU RAIS WA DUNIA

$
0
0
 Ndugu Francis Joseph Assenga ambaye ni mfanyakazi katika Benki Kuu ya Tanzania (katikati) mara baada ya kuchaguliwa kushika nyadhifa za Rais wa UNI Africa Professional & Managers na Vice-President UNI Global Professionals & Managers Committee kwenye Hotel ya Hilton Mjini Nairobi. Kulia kwake ni Rais wa Kamati ya Dunia Bwana Ulf Bengtsson akifuatiwa na Mkurugenzi wa UNI Global Professionals & Managers Bwana Pav Akhtar na Kushoto kwa Bwana Assenga ni Makamu Rais UNI Africa Professional & Managers  Mama Olasanoye Oyinkan kutoka Nigeria, akifuatiwa na Wagombea wengine wa Urais ambao ni Ousmane Diagne kutoka Senegal na Pierre Louis Mouangue kutoka Cameroun. 
Ndugu Francis Josseph Assenga (kushoto) akipongezwa na Mwakilishi wa Rwanda Bwana Alexis  kwenye Mkutano wa Bara la Afrika wa Kamati ya Wataalam na Mameneja na Makamu wake Olasanoye Oyinkan wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa UNI Africa Professional & Managers kwenye Hotel ya Hilton Mjini Nairobi.

VODACOM YAENDELEA KUTOA MAFUNZO MAONESHO YA WIKI ZA HUDUMA YA KIFEDHA YANAYOENDELEA

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu kushoto akifuatilia kwa umakini jinsi Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude, anavyomuelekeza Bw. Mweusi Mohamed Mweusi, namna ya kifaa cha kuchajia simu kwa kutumia umeme wa Jua (Readset Solar Charger)kinavyounganishwa na kuanza kufanya kazi  leo  Katika banda la kampuni ya Vodacom lililoko katika  maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa maofisa wa Vodacom akitoa maelezo kwa baadhi ya wajasiriamali wanaopata mafunzo katika maonesho ya Wiki ya Huduma za kifedha na uwekezaji yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam, Kampuni ya Vodacom imetoa mafunzo kwa wajasiriamali hao ya namna ya kujiunga na kunufaika na fursa ya mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kwa wanawake wajasiriamali  wadogowadogo MWEI.

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI KATIKA KIJIJI CHA GYKRUM,ARUSHA

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya akisoma hotuba fupi mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifungua rasmi jiwe la msingi katika mradi wa maji wa kijiji cha Gykrum, Karatu Mjini, mkoani Arusha.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelekezo kutoka Kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA), Bi. Ruth Koya pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maji, Dk. Binilith Mahenge, katikati ni Mama Tunu Pindi.

MAONYESHO YA UWEKEZAJI KANDA YA KASKAZINI YALIYO DHAMINIWA NA NMB YAFANA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa (kushoto) alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga 26-27/9/2013. Walioambatana naye ni Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji Mhe. Dr. Mary Nagu, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kapteni Mstaafu Mh. Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Mkutano wa Uwekezaji Nd. Salum Shamte pamoja na viongozi na washiriki wengine.

Naibu Waziri TAMISEMI Mh. Aggrey Mwanri akisaini kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho hayo. Kutoka kulia ni Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo, Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa pamoja na wafanyakazi wa NMB Tawi la Madaraka Tanga.

Mkurugenzi Ukaguzi wa ndani wa Makampuni ya Impala Bw. Julius Makara (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja Mahusiano Mwandamizi wa Wateja Wakubwa Bw. Nsolo Mlozi baada ya kutembelea banda la NMB

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mulongo (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Pangani Farms Bw. Charles Makoi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Pride (T) Limited Bw. James Obama (kushoto) akipewa maelezo ya kuhusu Huduma Mbalimbali za Benki ya NMB toka kwa Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo. Pembeni yake ni Meneja wa Tawi la NMB Madaraka Tanga Bw. Juma Mpimbi, Meneja Uwekezaji wa NSSF Bw. Abdallah Mseli na Meneja Mahusiano Wateja Wakubwa Bi. Shilla Senkoro katika maonesho hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mh. Majid Mwanga (kati) akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB Bi. Josephine Kulwa, Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa NMB Bi. Vicky Bishubo baada ya kutembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Jijini Tanga.

Mbunge wa Kilindi Mh. Beatrice Shelukindo akiwa na maofisa wa NMB alipotembelea banda la NMB katika maonesho ya Uwekezaji Kanda ya Kaskazini.

Sekretarieti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola yawasili Seychelles tayari kwa Mkutano wa Maspika wa Jumuiya ya Madola Afrika

$
0
0
 Spika wa Bunge la Seychelles,Mhe Dr.Patrick Herminie (kulia) akiwa na Katibu wa Bunge la nchi hiyo,Bi.Azarel Ernesta wakipata maelezo kuhusu Maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Bara la Afrika.Jumla ya Maspika toka nchi 19 za Afrika watahudhuria mkutano huo.Maafisa wa Sekretarieti watakaohudumia mkutano huo ni Ndugu Demetrius Mgalami,Katibu Msaidizi wa CPA Afrika(wa kwanza kushoto),Ndugu Saidi Yakubu,Mratibu wa Chama hicho bars Afrika(wa pili kushoto) na Ndugu Ephraim Jane toka Bunge la Namibia.Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola kwa Bara la Afrika kinaundwa na nchi 19 ambazo ni Botswana,Cameroon,The Gambia,Ghana,Kenya,Lesotho,Namibia,Nigeria,Malawi,Msumbiji,Mauritius,Rwanda,Seychelles,Afrika Kusini,Swaziland,Sierra Leone,Tanzania,Uganda na Zambia.Makao Makuu ya Chama hicho yapo katika Bunge la Tanzania ingawa pia maafisa wengine huombwa toka Mabunge mengine kulingana na mahitaji
Picha ya pamoja baina ya Spika wa Bunge la Seychelles Mhe.Dr Patrick Herminie na Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha maandalizi.Kikao hicho kilifanyika katika Bunge la Seychelles mjini Mahe. Pichani toka kushoto ni Bi Azarel Ernesta,Katibu wa Bunge la nchi hiyo,Nd.Ephraim Jane,Afisa wa Sekretarieti toka Namibia,Nd.Demetrius Mgalami,Katibu Msaidizi wa CPA barani Afrika, Spika Herminie,Nd.Saidi Yakubu,Mratibu wa CPA Barani Afrika  na Nd.Molathe Moshifane,Afisa wa Sekretarieti toka Afrika Kusini. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

mambo ya gado

IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA 8 TANZANIA

$
0
0
 Kwa mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu mkutano wa nane wa mwaka wa  taasisi hiyo  na kupata nafasi ya kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
 Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecela amesema mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.

 Daktari. Mwelecele Malecela amesema katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari. Hussein Mwinyi.
Makamu huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.
"Mkutano pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia (MDG's).
Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii" 
Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.

SHUKURANI

$
0
0
Familia ya Yagaza tunapenda kutoa shukhrani za dhati kwa ndugu, jamaa,  na marafiki walioweza kushiriki nasi katika hali na mali wakati wa msiba wa mtoto, kaka, baba, na mjomba mpendwa Mwl. Osckar P. Yagaza (pichani). 

Mungu aliye asili ya wema wote azidi 

kuwabariki kila iitwapo leo.

Raha ya milele uumpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani.

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images