Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

CHAP CHAP DECORATE and MUZIKI ACOUSTIC at Nafasi Art Space on saturday

$
0
0
Dear All.
 Join us this Saturday, the 28th of September for CHAP CHAP DECORATE We will decorate five new containers with Graffiti and Paint, Wachata Graffiti and Nafasi artists will support you At 18.30 MUZIKI ACOUSTIC – we gather around the fire place for an open stage and jam session, bring your own instruments and join in, or relax and enjoy the music


Waziri Mkuu Mizengo Pinda awasili Mkoani Tanga tayari kwa ufunguzi wa Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Mizengo Pinda akiwasili katika uwanja wa ndege wa Mkoa wa Tanga kwa ajili ya Kongano la Uwekezaji Kanda ya Kaskazini litakalofanyika Septemba 26-27 mwaka huu. Mara baada ya Mapokezi Mhe. Pinda atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga katika ukumbi wa mikutano wa Tanga Beach resort.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Mizengo akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bw. Benedict Ole Kuyan. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Chiku Gallawa.
Mhe. Pinda akisalimiana na Viongozi wa ngazi za juu katika Mkoa wa Tanga.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Mizengo akifurahia burudani ya vikundi mbalimbali vya ngoma ( havipo pichani) mara tu baada ya kuwasili katika Mkoa wa Tanga. ( wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. Halima Dendego na kulia kwake ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.
Burudani mbalimbali. Picha zote na Monica Laurent, Afisa Habari Mkoa wa Tanga.

KIWANDA CHA PARETO(PCT) WAPATA HASARA BILIONI 1.4

$
0
0

Meneja wa kiwanda cha Pareto Martin Oweka kilichoko Wilayani Mufundi katika mji wa Mafinga.
========  ======  ========
KIWANDA CHA PARETO(PCT) WAPATA HASARA BILIONI 1.4

Na Denis Mlowe,Mufindi

KIWANDA cha Pareto(PCT) cha Wilayani Mufindi, mkoani Iringa kimepata hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 baada ya kushindwa kununua pareto kwa wakulima na kuizalisha kwa kipindi cha miezi miwili. Meneja wa kiwanda Martine Oweka alisema mpaka sasa mitambo ya kuzalishia zao hilo ilisimama kwa muda kutokana na kukosekana kwa malighafi hiyo baada ya kuwepo kwa wanunuzi wengi, ambao wamekuwa wakisafirisha nje ya nchi licha ya kuwepo kiwanda.

Alisema hasara kubwa inatokana na uwekezaji wao katika zao hilo ambapo, kwenye msimu wa kilimo walitumia Sh milioni 500, kuwanunulia wakulima miche ya pareto, elimu juu ya kilimo hicho sambamba na ujenzi wa maeneo ya kukaushia zao hilo, ili kuongeza sumu. " Mwezi Julai ilikuwa tupate tani 100 za pareto kwa wakulima lakini tuliambulia tani 20 wakati mwezi huu wa agosti kati ya tani 200 ambazo ilikuwa tukusanye, tumeambulia tani 30 tu, hii ni hasara kubwa sana kwetu hatukuwa na kibali cha kununua pareto kwa wakulima japo hiki ni kiwanda pekee Tanzania,”alisema Oweka.

Alisema kibali cha kununua zao hilo kwa wakulima ilikuwa wapatiwe mwezi juni mwishoni, lakini badala yake walipewa August 21, mwaka huu kikiwa kimechelewa kwa miezi miwili.Hata hivyo alisema hasara ya Sh Bilioni 1.4 waliyoipata kwa kushindwa kuzalisha zao hilo, inawaghalimu wakulima ambao, wengi wao wamehifadhi pareto ndani kinyume cha taratibu za zao hilo, ambalo ubora wake hutegemea ukali wa sumu.

“Mkulima akivuna Pareto halafu akahifadhi ndani kwenye unyevu kwa muda mrefu inapoteza sumu kiasi ambacho hata sisi wanunuzi inakuwa vigumu kuinunua kwani, ubora wa pareto ni kiwango cha sumu iliyopo,”alisema.Aliongeza kuwa kushindwa kununua pareto hiyo kumeisababishia hasara serikali kwa kuwa imekosa fedha za kigeni ambazo hutokana na mauzo ya nje ya zao hilo mara baada kuzalishwa kiwandani hapo. Aliwataka wakulima kutokata tamaa na badala yake waendelee kuzalisha zao hilo na kuiomba serikali kulinda soko la pareto.

Kwa upande wao wakulima, wameiomba serikali kuhakikisha kuwa zao hilo halifi na kuona namna ya kulinda viwanda vya ndani vyenye uhakika wa soko badala ya kuruhusu soko huria, wakati malighafi hiyo hata ndani ya nchi haitoshelezi mahitaji. Uwezo wa kiwanda cha Pareto cha Mafinga ni kuzalisha tani 6,000 kwa mwaka lakini badala yake, kimekuwa kikiambulia tani 2,5000 pekee.

Timu ya mpira wa pete ya Utumishi yanusa robo fainali katika michezo ya shimiwi dodoma

$
0
0
Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendeleza ubabe katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendela katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma baada ya kuichakaza timu ya Mifugo kwa magoli 28 kwa 15 jana jioni. 
Mchezo huo ulioanza kwa kasi huku kila timu ikimsoma mpinzani wake hata hivyo Mifugo ilipelekwa kasi na Utumishi kwa kukubali magoli 16 kwa 6 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Katika kipindi cha kwanza Mifugo walipoteza pasi 10 kwa kudhibitiwa na Monica Aloyce (GK) na Amina Ahmed (WD) wa Utumishi. Kipindi cha pili kwa kiasi kikubwa kilimilikiwa na Utumishi hali iliyowafanya wachezaji wa Mifugo kucheza ndivyo sivyo. 
Mchezo wa rafu ulisababishwa mechi hiyo kusimamishwa mara kadhaa ambapo Fatma Ahmed (GS) na Secela Shabani (WA) wote wa Utumishi kuumizwa. Katika kipindi hicho Utumishi ilijiongezea magoli 12 na Mifugo kuambulia 9. 
Baada ya mchezo huo Kocha wa timu ya Utumishi Bw. Mathew Kambona alisema mechi ilikua nzuri licha ya wachezaji wake kuumizwa kutokana na mchezo wa rafu.
 “Tunajipanga vizuri ili kuhakikisha wachezaji walioumizwa wanakuwa sawa kwa michezo inayokuja” Kambona alisema. Hata hivyo, kocha wa Mifugo Bi. Nora Nchuwekeleze alisema bado anaamini timu yake ni nzuri. Nchukuwekeleze alisema mchezo ulikuwa mzuri na wenye wenye ushindani. 
Mwanamkasi Abbasi (GK) anayeichezea Mifugo alisema walizidiwa kutokana na wachezaji watatu tegemeo kuwa majeruhi hivyo kuzidiwa mbinu na maarifa na wapinzani wetu. Timu ya Utumishi itaingia katika mzunguko wa pili wa Michezo ya SHIMIWI kwa upande wa mpira wa Pete baada ya kupatikana kwa mshindi katika mchezo kati ya Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Katiba na Sheria mechi itakayochezwa leo jioni.
 Timu ya mpira wa pete ya Utumishi kabla ya kuanza kwa mechi kati yake na Wizara ya Mifugo katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma.
 Timu ya Wizara ya Mifugo kabla ya kuanza mechi kati yake na timu ta Utumishi katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma.
 Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikisalimiana na timu ya Mifugo kabla ya mechi kuanza katika viwanja vya UDOM.
 Timu ya Utumishi ikimenyana na timu ya Mifugo katika viwanja vya UDOM mjini Dodoma 

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, atembelea timu yake dodoma

$
0
0
  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati walipokuwa katika mazoezi yao leo asubuhi kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kwa ajili ya mashindano ya SHIMIWI. Katibu Mkuu alipita kuwajulia hali wachezaji wake na kujua maendeleo ya kambi hiyo. 
 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akizungumza na wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati alipowatembelea kuwajulia hali katika Kambi yao mjini Dodoma leo wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI. 

 Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Saaz Salula, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ofisi yake, wakati alipofika katika Kambi ya timu hiyo kuwajulia hali mjini Dodoma leo asubuhi, wakiwa katika mashindano ya SHIMIWI. Picha na OMR

KARAMA NYILAWILA KUZIPIGA NA SADO PHILEMON OKTOBA 20, 2013

$
0
0

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Karama Nyilawila (pichani) alishawahi kuubeba ubingwa wa dunia wa  WBF –middle weight  kwa kumpiga Kreshnik Qato wa Czech Republic, katika ukumbi wa Sparta arena, Plaque.

Ubingwa  huo ambao una hadhi kama aliokuwa nao Francis Cheka kwa sasa, baadae aliupoteza kwa kutoutetea kutokana na kukosa wadhamini wa kumsaidia kuutetea ubingwa wake huo, na kushawishika kucheza na Francis Cheka  katika pambano alilopoteza na kukaa kimya muda mrefu bila kucheza  pambano la ndani ya nchi.


Karama anategemea kupanda ulingoni  tena tarehe 20 ya mwezi wa kumi katika ukumbi wa ccm mwinjuma.Mwananyamala  kuzipiga na sado philemon katika pambano lililoandaliwa na  Bigright promotion.
Akilizungumzia pambano hilo Ibrahim kamwe anaeleza kuwa maandalizi mpaka sasa yanaenda vizuri pindi yapo katika mazingira magumu kwa wale watakaocheza utangulizi wanajiandaa kiukataukata kwa ajili ya pambano hilo ambalo litakuwa na mapambano mengi ya utangulizi, ukizingatia hatujapata mdhamini wa kudhamini pambano hili ili liwe katika ubora unaotakiwa , lakini tunapambana na tutajitahidi  pambano lifanyike vema tuwatie moyo hawa mabondia wanaochipukia na kuusimamisha vizuri mchezo wetu wa masumbwi.
Karama na mwenzie Philemon wameshasaini makubaliano ya mchezo huo na wapo katika hali nzuri ya kimchezo.

dkt nchimbi alipotembela banda la tanroads katika maonesho ya wiki ya usalama barabarani Mwanza

$
0
0
  Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Mazingira wa TANROADS, Zafarani A Madai akimwonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi,jinsi madereva wanavyopaswa kutumia barabara ili kuepusha ajali kwa kutumia michoro mbalimbali . 

 Mhandisi wa TANROADS Jonas Matete, akiwapa maelekezo ya matumizi ya barabara vijana wawili ambao walitembelea banda la wakala huyo wa barabara ili kufahamu mambo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Usalama Barabarani yanayofanyika jijini Mwanza. Picha na Aisha Malima

kionjo cha JCB ft Professor Jay

$
0
0
Pata kusikiliza kionjo cha JCB ft Professor Jay, wimbo unaitwa "Drive Slow" ikiwa ni kazi toka Mj Records chini ya MarcoChali,  powered by www.vmgafrica.com


VYAMA VYA UPINZANI KATIKA MKUTANO WA KATIBA MPYA ZANZIBAR

$
0
0

Mshikamano: Wenyeviti wa vyamba vya upinzani nchini wakishikana mikono kuonyesha mshikamano kabla ya kuanza mkutano kwenye Uwanja vya Kibandamaiti, Zanzibar leo.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) akiteta jambo la Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Joseph Mbatia wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanji wa katiba mpya.

Umati: Wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kutafuta katiba mpya.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia wananchi wakati wa mkutano wa kuungwa mkono na wananchi katika upatikanaji wa katiba mpya.
Lipumba akisalimiana na Mbowe. Picha kwa hisani ya Global Publishers 

fastjet first international route temporarily postponed

$
0
0
26th September 2013 - fastjet, Africa’s low cost airline, announces that its first international flight between Dar es Salaam and Johannesburg, previously scheduled to take place on Friday 27 September 2013, has been temporarily postponed.
 
This postponement is due to unexpected administrative delays caused by the South African Department of Transport this week making a very late request for additional documentation.
 
Although, fastjet delivered these documents without delay, the South African Department of Transport has said it will take several days to process these documents, thus delaying the start of fastjet flights on this international route. The delayed launch of this route is not expected to have any material effect on the financial performance of fastjet Tanzania.
 
Commenting on the news, fastjet Chief Executive Ed Winter said: “This postponement is very disappointing. Unfortunately however, administrative delays of this nature are not unusual in the markets in which we operate. Having complied with all the requests made of us and secured all the necessary licenses and permits in an extremely diligent and timely fashion, fastjet was led to believe that we were fully on-track to launch this route on the 27th September.”
 
fastjet would like to apologise to its customers for the inconvenience. All passengers affected by this delay will receive a full refund and assistance with re-booking a complimentary seat to fly within the next month.
 
Tanzanian based customers can contact fastjet customer services on +255 685 680 537 and oncustomer.tanzania@fastjet.com for any queries.
 
“Launching flights on this route remains a key priority for fastjet, and we are confident we will be operating on this service by mid-October, starting a new era of choice for passengers who continue to suffer inflated prices on flights between two of Africa’s largest and fastest growing cities” Winter continued.
 
Flights between the two cities will initially be operated by fastjet three times a week on Mondays, Wednesdays and Fridays, increasing in frequency as soon as consumer demand dictates.
 
“fastjet has been on an incredible journey since we started flying domestically in Tanzania with a single A319 plane nearly 12 months ago between Dar es Salaam, Mwanza, and Kilimanjaro,” said Winter.
 
“Our Johannesburg route, where we will compete head-to-head with South African Airways to provide real value for money flights, represents the next step on that journey. Healthy and fair competition is vital in any economy and in any industry. Competition will bring choice and lower fares – a win-win for consumers,” he concludes.

TAARIFA KWA UMMA

Ray C kurejea upya kwenye anga ya muziki wa bongofleva.

$
0
0
 Staa wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Rehema Chalamilla 'Ray C', akiingiza sauti ndani ya Studio za THT, chini ya maprodyuza Emma The Boy na Tudy Thomas,ambao wamepania kumrejesha katika game kwa kishindo msanii huyo, ambaye alipotea kwenye ulimwengu wa Burudani baada ya kutopea katika utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa sasa ameachana nayo na kumrudia mwenyezi Mungu sambamba na kuendelea kutumia dozi ya kuondoa sumu ya madawa hayo.
 Prodyuza  Tudy Thomas (kulia), akijadiliana jambo lililotokana na majadiliano ya kuboresha ngoma mpya ya Ray C, pichani kati ni  Emma The Boy akipiga mzigo tayari kwa kumkamilishia Ray C ngoma yake mpya ambayo anatarajia kuiachia hivi karibuni.
 Ray C, akijaribu kutoa akapela kwa Maprodyuza hao, wakati wakiendelea kuiboresha ngoma yake mpya.

DKT. NJELEKELA AWAAGIZA WAFANYAKAZI MUHIMBILI KUBUNI VYANZO VYA MAPATO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimimbili Dkt. Marina Njelekela amewaagiza wafanyakazi wa Hospitali hiyo kutafuta mbinu mbalimbali za kuongeza mapato, kupunguza matumizi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato. Dkt. Njelekela ametoa agizo hilo leo alipokuwa akifunga Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi hao uliofanyika katika Hoteli ya Landmark iliyoko Jijini Dar Es Salaam.
Description: DSC07539
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela hayupo pichani

“Ninawaagiza Wakurugenzi, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Vitengo, Mameneja wa Majengo mlioko hapa leo kushirikisha wafanyakazi walioko chini yenu ngazi zote ili kuja na mikakati, mbinu za kubuni vyanzo vipya vya mapato katika maeneo yenu ya kazi, kutoa maoni yenu ni wapi mnafikiri kuna matumizi zaidi ili yapunguzwe na pia ni wapi mnaona kuna mianya ya upotevu wa mapato ya Hospitali ili tuweze kushirikiana kuziba mianya hiyo” amesema Dkt. Njelekela.


Amesema kuwa ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kupanga, kutekeleza shughuli mbalimbali za Hospitali ni muhimu kwani unatoa fursa kwa wafanyakazi kujua Hospitali inafanya nini, kwa wakati gani, nani anayepaswa kufanya nini, kwa kutumia mbinu gani na rasilimali gani zipi na kiasi  gani zitahitajika ili kufanya kazi hiyo.

Kwa sasa tunamalizia mpango wetu wa kazi kwa robo ya kwanza ya mwaka kwa misingi hiyo natoa mwezi mmoja wa Oktoba kuhakikisha maagizo niliyotoa yanatekelezwa ili kutoa nafasi ya mapendekezo, mbinu, mikakati yenu kufanyiwa kazi vizuri katika robo ya pili na ya tatu ya mwaka wa fedha 2013/2014, alisisitiza Dkt. Njelekela.
Fuatilia habari zaidi katika picha zifuatazo;
Description: DSC07529
Description: DSC07520
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela hayupo pichani

TUMESHERIA SPORTS WANAUME YAANZA VYEMA MICHUANO YA SHIMIWI KATIKA MCHEZO WA KAMBA KWA KUISHINDA WIZARA YA MAWASILIANO

$
0
0
Kikosi cha Timu ya Kamba Wanaume cha TUMESHERIA SPORTS kikiingia uwanjani kuchuana na Wizara ya Mawasiliano katika michezo ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Dodoma.
Timu ya Kamba wanaume ya Wizara ya Mawasiliano ‘wakiburuzwa’ na TUMESHERIA.
Kikosi cha TUMESHERIA kikiwavuta wenzao wa Wizara ya Mawasiliano.

KAULI YA MHE. SOFIA SIMBA KUHUSU KAULI ZA WANASIASA

$
0
0
KAULI ZA KISIASA
 Hivi karibuni mnamo tarehe 21/09/2013 vyama vya siasa kadhaa vilifanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani, Pamoja na mambo mengine yaliyo zungumzwa, mimi kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nimestushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi. Ambao unaweza kuleta madhara kwa jamii, hususan wanawake, watoto, wazee, walemavu n.k.
                                    
Kwanza, Kauli ya Mhe. Lipumba
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema pale Jangwani, nadhani jamii inahitaji kutafakari na kuhoji; maana ya kauli yake aliposema, “Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika” Tujiulize, Je, ni mazoezi ya aina gani? Yanafanyikia wapi? Yanalenga kufanya nini? Lakini mwisho wa yote ni muhimu Watanzania wakajikumbusha mwenendo wa siku za nyuma za hao wanaoitwa vijana wake!

Wito wangu kwa vijana wasikubali kutumiwa katika mambo yanayo wahatarisha wao na jamii kwa ujumla, kwani hayana tija. Wananchi kumbukeni kuwa yanapotokea matatizo, akina mama ndio walezi wa majeruhi, wagonjwa na pia walezi wa watoto wa walioathirika.

Pili, Kauli ya Mhe. Mbowe
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema, nilipatwa na butwaa kwa kauli yake aliposema:- “Siku ya tarehe 10/10/2013 ni Siku Maalum ya Kitaifa ya “Civil Disobedience”. Hii ni kauli hatari, yenye kuashiria uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mkononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.

Tujiulize “Siku Maalum ya Kitaifa ya Civil Disobedience” maana yake nini? Kwa Kiswahili maana yake ni Siku Maalum yaKitaifa ya Jamii Kutotii, kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Hayo yakitokea itakuwa ni Siku ya Maangamizi. JAMII KUTOTII ni utovu wa Nidhamu, ambao husababisha Uvunjaji wa Sheria na kuhamasisha kujenga Mazingira ya Vurugu.

Kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nasema hii ni hatari. Na athari zake naziona kubwa kwa wanawake, watoto, walemavu na wazee.

Tatu, Kauli ya Mhe. Mbatia
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema, nadhani jamii inahitaji kutafakari na kumpongeza kwa kauli yake aliposema:- Bado anaamini kwamba “Kuna fursa ya kukaa katika round table na kuyazungumza”. Hii kauli ni ya kizalendo na ya kiungwana. Nampongeza sana. Inavyoonekana, Mhe. Mbatia ni mtu mwenye kutambua kwamba ana dhamana ya kuilinda familia yake na jamii ya Watanzania kwa ujumla.

Tahadhari ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii
Mwenendo wa kauli hizi, si mzuri kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu kijamii na kiuchumi. Hii ina maana siku hiyo ya Civil Disobedience, Mama Lishe na Wajasiriamali wengine hawatofanya biashara zao, watoto wetu hawatoenda shule na huduma nyingine za kijamii zitakwama wakati wao wakitekeleza mipango waliyopanga kwa tarehe hiyo.

Amani na usalama ni mtaji wa maendeleo
Kama jamii tunapaswa kutambua kwamba amani na usalama, ndio mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wetu kama jamii ya Watanzania au kama familia au mtu mmoja mmoja unahitaji uwepo wa amani, utulivu na usalama. Kwa sababu kunapotokea vurugu/Civil Disobedience wanaoathirika zaidi ni wanawake, watoto, wazee na walemavu.Leo nimeona niongelee hili ambalo linawagusa wadau wangu moja kwa moja ambao wapo chini ya Wizara yangu.
Asanteni.

MUNDE TAMBWE, MBUNGE WA VITI MAALUMU AWA MGENI RASMI MAHAFARI YA DARASA LA 7 ISIKE S/MSINGI

$
0
0
MH. MUNDE TAMBWE (KATIKATI), MBUNGE WA VITI MAALUMU NA MJUMBE WA NEC, MGENI RASMI MAHAFARI YA DARASA LA SABA KATIKA S/M ISIKE MJINI TABORA LEO
KUSHOTO NI KADUCHA J, ZINDUNA KISAMBA, CHARLES KIDIFU, MUNDE TAMBWE, ALLY KITENGE (M/KITI KAMATI YA SHULE)
MGENI RASMI AKIKABIDHI VYETI KWA WAHITIMU
KATIKA MAJIBU YA RISALA YAKE AMETOA TASILIMU LAKI TATU (300,000/=) KAMA MCHANGO KWA BAADHI YA MAPUNGUFU YALIYOPO SHULENI HAPO.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Airtel yapiga jeki mbio za Rock City Marathon 2013

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari fomu ya usajili ya mbio za Rock City Marathon 2013 iliyodhaminiwa na kampuni yake jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia).
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam jana kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI). Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia). 
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Bw. Jackson Mbando (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam jana kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI). Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bw. Geoffrey Nangai na Meneja Matukio wa CPI, Bw. Mathew Kasonta (kulia) 
Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Mathew Kasonta (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon 2013 jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mbando na Meneja Uhusiano wa CPI Bw. Geoffrey Nangai.

============   =========  ==========
Airtel yapiga jeki mbio za Rock City Marathon 2013

KAMPUNI ya Airtel ya Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money kwa mara ya tano mfululizo imetangaza kudhamini mbio za Rock City Marathon za mwaka huu zilizopangwa kufanyika mkoani Mwanza tarehe 27, Oktoba 2013 ikiwa na lengo la kukuza maendeleo ya mchezo wa riadha nchini.

Airtel imekuwa mdhamini mkuu kwa upande wa mawasiliano katika mbiyo hizo, wakishirikiana na wadhaminiwa wengine kama NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Bank M, PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications pamoja na Umoja Switch, ili kutoa fursa ya kuinua mchezo wa riadha inchini.
Akizungumza wakati wa tukio fupi lililofanyika katika makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Bw. Jackson Mmbando alisema kampuni yake imejidhatiti kusaidia  shughuli mbali mbali za maendeleo ya jamii na mbio za Rock City Marathon pia ni fursa pekee ya kukuza vipaji katika michezo huo kwa ujumla.

“Kampuni ya Airtel Tanzania kwa mwaka wa tano mfululizo, leo hii tunatangaza udhamini wa mbio za Rock City Marathon za mwaka huu ikiwa ni sehemu ya jitihada zetu za kusaidia maendeleo ya michezo nchi nzima. “Tunaamini kuwa mchango wetu utasaidia katika kuvumbua vipaji vipya vitakavyoshiriki si tu kwa mashindano ya kitaifa lakini pia na ya kimataifa,” alisema. 

Mmbando aliongeza kuwa washiriki kwa mwaka huu wataweza kusajili moja kwa moja kupitia huduma ya kampuni yake ya Airtel Money kwa kutuma malipo yao kwa neno MARATHON na kuhifadhi ujumbe kwa ajili ya kuuonyesha wakati wa kuchukua fomu katika vituo mbali mbali.

Kwa upande wake mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta wakati wa tukio alisema kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa kubwa na bora zaidi kwa kuleta pamoja washiriki kutoka ndani ya nje ya nchi.

 “Kwa mwaka huu tumeungana na kampuni ya Airtel lakini kupitia Airtel Money ili kutanua wigo wa ushiriki zaidi. Katika miaka iliyopita, watu wengi wamekuwa wakikosa nafasi ya kushiriki au wakilazimika kusafiri umbali mkubwa kwenda kwenye vituo vichache tulivyoviandaa ili waweze kununua fomu za usajili, kwa kupitia Airtel Money zoezi hili litakuwa limerahisishwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Kasonta.

Kasonta aliongeza, “ukishamaliza zoezi hilo, utapokea ujumbe utakaouonyesha pale utakapokwenda kuchukua fomu za usajili katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mbeya, Arusha na Mwanza.”

Alisema kuwa washiriki wenye vigezo pia wataweza kusajili kwa kupata fomu zipatikanazo katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza, na katika ofisi za kampuni ya Capital Plus International zilizopo ghorofa ya tatu, upande wa kulia katika jengo la ATC, Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.

Kasonta alibainisha kuwa fomu za usajili zitapatikana katika viwango vya bei vifuatavyo; shilingi 5,000 kwa mbio za km 21 (kwa watu wote), shilingi 3,000 kwa mbio za km 5 (mbio kwa makampuni na taasisi). Alisema kuwa fomu kwa mbio za kilometa 3 (kwa wazee kuanzia miaka 55 na watu wenye ulemavu wa ngozi) na mbio za kilometa 2 kwa watoto (wenye umri wa miaka 7 mpaka 10) zitapatikana bure.

nguzo za umeme zilivyonusurika kuteketea kwa moto kwenye msitu wilayani Makete

$
0
0
 Masalia ya msitu uliopo kwenye kijiji cha Luvulunge wilaya ya Makete mkoa wa Njombe mara baada ya moto kuuteketeza msitu huo ambao mbali na kuwa na miti pia nyaya za umeme wa gridi ya taifa unaotoka mkoa jirani wa Mbeya kuja Makete zimepita katika eneo hili lililoungua
 Nguzo za umeme zikiwa zimeponea chupuchupu kuteketezwa na moto huo.
Mojawapo ya nguzo zilizopo kwenye msitu huo kama unavyoziona, na sipati picha kama zingeungua nini kingetokea?(Picha zote na Edwin Moshi, Makete)

Moja ya maonyesho kwenye Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

WAFANYABIASHARA MAKETE WAANDAMANA HADI OFISI ZA CCM

$
0
0
 Mwenyekiti wa soko kuu Makete mjini akizungumza kwenye ofisi za CCM.
 Mfanyabiashara Mia Sanga akizungumza ya moyoni mwake.
 Mfanyabiashara Andrea Sanga akiweka wazi aliyonayo
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula akizungumza na wafanyabiashara hao.
======
Na Edwin Moshi,Globu ya jamii Makete
Wafanyabiashara eneo la sokoni Makete mjini ambao wanatakiwa kubomoa mabanda yao ya biashara kupisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, wamebisha hodi kwenye ofisi za chama cha mapinduzi wilaya hiyo kupeleka malalamiko yao kufuatia kuandikiwa barua na halmashauri ambayo wamedai inawaumiza

Wakiwa katika ofisi hizo, Mwenyekiti wa soko hilo Hosea Mpandila alitoa sababu za wao kuongozana kwa pamoja hadi kwenye ofisi hizo kuwa wanasikitishwa na kitendo cha wao kuzuiwa na halmashauri kuendelea na ujenzi wa vibanda vyao kwenye eneo ambalo walipangiwa awali na halmashauri licha ya baadhi yao kupeleka vifaa vya ujenzi kwenye eneo hilo

Amesema jana waliandikiwa barua na mkurugenzi wa halmashauri ya Makete (mtandao huu unayo barua hiyo) ambayo amedai ina masharti ambayo hawawezi kuyatekeleza kwa kuwa yanawaumiza, ikiwemo la kutakiwa kuomba upya kupatiwa viwanja vya kujenga mabanda, na mabanda wakishayajenga wanatakiwa kuainisha gharama za ujenzi kwa halmashauri ambapo watakuwa wakilipa kiwango nafuu cha ushuru na kiasi kingine cha fedha kinachukuliwa na wafanyabiashara hao na wakisharudisha gharama za ujenzi, vibanda hivyo vitakuwa mali ya halmashauri na watakuwa na mamlaka ya kumpangisha yeyote wanayemuona anafaa

"Kwa kweli inatusikitisha sana, hivi inawezekanaje sisi tujenge vibanda kwa gharama zetu wenyewe halafu tuje kurejeshewa gharama kidogokidogo na zikishakamilika mabanda yawe ya halmashauri, hii ina maana gani? kama ndivyo basi halmashauri ijenge vibanda itupangishe sisi" alisema Andrea Sanga

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mia Sanga amepinga uamuzi wa wao kuomba upya kupewa viwanja hivyo wakati wote walishapimiwa na serikali na kuruhusiwa kuendelea na ujenzi, na kuitaka serikali kuwarejeshea kama walivyowapa awali ili waendelee kujenga kwa kuwa muda waliopewa wa kubomoa mabanda yao kwa hiari unakaribia kuisha
 
Akizungumza na wafanyabiashara hao kwenya ofisi za CCM wilaya hiyo, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula, amewapa pole wafanyabiashara hao na kushangazwa na barua hiyo waliyopewa na kuwataka kuwa na subira kwani wamefikisha malalamiko yao kwenye eneo sahihi na kuahidi kulishughulikia
 
Chaula amesema haimuingii akilini wafanyabiashara hao kusimamishiwa ujenzi na kutakiwa kuomba upya huku akisisitiza wao kama chama watafika kwenye ofisi ya mkurugenzi kupata muafaka wa suala hilo mara moja
 
Mtandao huu ulipofika kwenye ofisi ya mkurugenzi mtendaji kuzungumzia suala hilo, haukumkuta na badala yake mwandishi wetu alijibiwa kuwa mkurugenzi amesafiri kwenda Matamba kwa ajili ya kuangalai maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru 
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images