Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 264 | 265 | (Page 266) | 267 | 268 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Naibu Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Mambo ya Nje na Jumuiya ya madola, mhe. Mark Simmonds walipokutana kwa mazungumzo Mjini New York wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
  Ujumbe ulioambatana na Mhe. Simmonds.
  Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Simmonds kuhusu masuala ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
  Ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Dora Msechu, akifuatiwa na Bi. Tully Mwaipopo, Bw. Grayson Ishengoma na Bw. Togolani Mavura Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Picha na habari na  Rosemary Malale, New York


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) ameishukukuru na kuipongeza Serikali ya Uingereza kwa kuanzisha huduma mpya itakayowawezesha Watanzania kupata viza za kuingia nchini humo kwa haraka.
  Huduma hiyo ambayo ilitangazwa na nchi hiyo hivi karibuni kupitia Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose ni moja ya mipango ya nchi hiyo ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili. Huduma hiyo hukamilika kwa takribani siku tano hadi kupata viza.
  Akizungumza hivi karibuni na Naibu Waziri wa Uingereza anayeshughulikia Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola, Mhe. Mark Simmonds Mjini New York, Marekani wakati wa Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mhe. Membe alisema kuwa anaishukuru nchi hiyo kwa kuichagua Tanzania katika mpango huo ikiwa ni mshirika wake muhimu wa maendeleo na kwa kuzingatia kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa haraka katika siku za hivi karibuni hivyo itarahisisha na kuimarisha biashara baina ya nchi hizi mbili.
  Aidha, Mhe. Membe aliongeza kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakijishighulisha na biashara mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Uingereza hivyo mpango huo wa viza za haraka utawasaidia kuimarisha biashara zao badala ya kukatishwa tamaa na mlolongo mrefu wa kufuatilia viza uliokuwepo hapo awali.
  “Tunaishukuru sana Serikali ya Uingereza kwa kuanzisha huduma hiyo ya utoaji viza za haraka, hata hivyo bado tunaiomba ifikirie tena uwezekano wa kurejesha huduma ya utoaji viza Jijini Dar es Salaam badala ya kufuatilia viza hizo Nairobi nchini Kenya”, alisema Waziri Membe.
  Aidha, aliomba kiwango cha nyongeza kilichowekwa cha shilingi laki mbili na nusu kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa viza hiyo ya haraka kipunguzwe kwani ni kikubwa kwa Watanzania.
  Akizungumza kwa upande wake, Mhe. Simmonds alisema kuwa Uingereza itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.
  Mkutano huo wa Mhe. Waziri Membe na Mhe. Simmonds ulihudhuriwa na Wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu.

  0 0

  Na Dixon Busagaga 
  wa Globu ya Jamii, Moshi. 
   WAHAMIAJI haramu wapatao 18 wote raia wa Ethiopia,wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa njiani kusafrishwa kwenda mikoa ya kusini na baadaye kuvuka mpaka wa Tanzania kwenda Afrika Kusini. 
   Wengi wa wahamiaji hao haramu ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 20 na 27 ambao wlikamatwa majira ya saa 6:30 usiku wa kuamkia leo wakiwa ndani ya gari lenye namba za usajaili T858AHW likiwa na tela lake lenye namba za usajili T419AAE mali ya kampuni ya SUNVIC ya Jijini Arusha. 
   Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule amesema wahamiaji hao haramu walikamatwa katika eneo la Kichwa ng’ombe wilayani Mwanga kwa ushirikiano na maofisa wa uhamiaji na askari wa jeshi la polisi. 
   Alisema baada ya kukamatwa kwa gari hilo dereva alifanikiwa kuchomoa funguo wa gari na kisha kukimbia kusikojulikana na kuamua kilitelekeza gari hilo katika katika eneo la Kifaru na kwamba juhudi za kumtafuta dereva huyo zinaendelea. 
   Msumule alisema kutokana na kitendo hicho cha dereva kukimbia na funguo wa gari hilo,Maofisa wa uhamiaji walilazimika kuwasiliana na wamiliki wa gari ambao ni kampuni ya SUNVIC ndipo walipowapatia funguo nyingine. 
   “Baada ya dereva wa gari kukimbia na funguo tulishindwa kuliondoa katika eneo la tukio ndipo tukawasiliana na kampuni inayomiliki Lori hilo iliyoko jijini Arusha ambao walitupatia ushirikiano mkubwa ,hatimaye mchana walituletea funguzo za gari hilo.”alisema Msumule. 
   Msumule alitoa onyo kwa wahamiaji haramu pamoja na wale wanao wasaidia ikiwa ni pamoja na kuwasafirisha pamoja na kuwahifadhi kuwa idara yake imejipanga vyema kukomesha biashara hiyo. 
   “Kama nilivyozungumza hapo siku za mwanzo,tunataka biashara hii katika mkoa weru wa Kilimanjaro ifutike kabisa,hatuna utani na hatutaki mtu achezee shughuli hii tunayoenda kuifanya “alisema Msumule.
   Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Mwanga wakiwa katika gari lenye tela.baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii

  0 0

  Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga akijaribu kuendesha gari walilopewa na Wizara ya Afya naUstawi wa Jamii  jijini Dares Salaam.

  Waziri  wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya wa pili (kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya watu wakati  hafla fupi ya kukabidhi gari   aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  jijini Dares Salaam 
  Picha zote na Magreth Kinabo –MAELEZO
   Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga(aliyesimama) akiishukuru Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa msaada wa gari hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Crispin Meelana kulia ni Mganga Mkuu wa Wilaya.

  NA   MAGRETH KINABO- MAELEZO
  WAZIRI   wa  nchi  Ofisi ya Rais (Kazi maalumu), Profesa Mark Mwandosya amesema Tanzania itafikia maendeleo ya hali ya juu ifikapo mwaka 2025 hadi mwaka 2030 ikiwa watu watafanyakazi kwa upendo, uzalendo na kujiamini.

  Aidha Profesa Mwandosya amesema kwamba Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake kwa  karibu na wananchi, licha ya kuwepo kwa changamoto za kielimu na miundombinu, lakini mambo mengi yanafanyika,hivyo wenye macho wanaona.

  Kauli hiyo imetolewa na  Profesa Mwandosya wakati hafla fupi ya  kukabidhi gari  aina ya ‘Toyota double Cabin’ kwa ajili  ya huduma ya chanjo kwa Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo lenye thamani ya  Sh. milioni 38  iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya  Afya na Ustawi wa Jamii jijini Dares Salaam.

  “ Mimi nina matumaini makubwa  na nchi yetu ifikapo mwaka 2025 hadi 2030 tutakuwa ni nchi yenye watu wenye kipato cha kati.Pia ifikapo mwaka 2050 nchi yetu itakuwa imeendelea hakutakuwa na mtu mwenye kipato cha kati wala cha chini kama ilivyo nchi ya Singapore,” alisema Profesa Mwandosya.

  Profesa Mwandosya aliongeza kuwa  gari hilo ni moja ya juhudi za Serikali za kuhakikisha kuwa huduma  zake zinaifikia jamii  kila mahali hususan  kwenye maeneo ya vijijini.

  “Serikali inajitahidi kufikisha huduma zake mfano katika sekta ya elimu kuna mambo mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika ikiwemo katika sekta nyingi kama vile kwenye nishati  gesi  tunakwenda vizuri.  Tukisimamia vizuri rasilimali zetu ,basi   hata  huduma tutazifikisha vizuri kwa wananchi,” alisisitiza.

   “ Kila mtu duniani anasema Tanzania inapiga kasi  katika kuwaletea maendeleo  wananchi . Mimi  nadhani hatutarudi nyuma. Wale wanaopiga kelele hautajafanya kitu ,lakini mwenye macho wanaona,” alisisitiza Profesa Mwandosya.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Charles Pallangyo akizungumzia kuhusu gari hilo alisema litasaidia kuhimarisha huduma za chanjo katika halimashauri hiyo na kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito na watotowenye umri wa chini ya miaka mitano ili kutimiza malengo ya millinea ya namba 4na 5 ifikapo mwaka 2015.

   Naye Mganga Mkuu wa Serikali Dk. Donan Mmbando alisema nchi hivi sasa imefikia wastani wa asilimia 92 katika huduma za chanjo kutoka asilimia 90 ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

  Mwenyekiti wa halimashauri hiyo,Meckson Mwakipunga aliishukuru wizara hiyo kwa msaada huo ,ambapo alisema gari hilo litatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuinua kiwango cha huduma hiyo kwenye eneo hilo.

   ya Rungwe Dk. Gilibert Tarimo.
  0 0

  Mkurugenzi wa masoko wa Airtel Levi Nyakundi akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza timu akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt.
  katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt. 
  Kocha wa timu ya wasichana ya Airtel Rising stars Rogatician Kaijage akiongea wakati wa halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Airtel Rising stars mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars nchini Nigeria. halfa hiyo ilifanyika jana katika hoteli ya Hyatt. 
  Wachezaji waliozawadia kwa kungara katika michuano ya Airtel Rising stars pamoja na captain wa timu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Leonard Thadeo (mwisho kushoto) katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Angetile Osiah.


  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Bi. Juliet Kairuki (kushoto) akifafanua jambo wakati wa ziara ya Gavana wa kisiwa cha Anjouan Bw. Anissi Chamsidine katika kituo hicho jana jijini Dar es Salaam. Gavana huyo yuko nchini kwa ziara ya wiki moja. Katikati ni mke wa Gavana huyo, Bi. Laouya Shamsidine.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki (katikati) akimkabidhi zawadi ya picha Gavana wa kisiwa cha Anjouan Bw. Anissi Chamsidine (kulia) ambaye yupo nchini kwa ziara ya wiki moja. Gavana huyo alitembelea kituo hicho jana. Kushoto ni mke wa Gavana, Bi. Laouya Shamsidine.

  Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kisiwa cha Anjouan nchini Comoro ili kukuza na kuendeleza ushirikiano uliopo kwa maslahi ya kijamii na kiuchumi kati ya pande hizo mbili.

  Gavana wa Anjouan, Bw Anissi Chamsidine alieleza hayo alipotembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) jana jijini Dar es Salaam. “Tuna fursa nyingi za uwekezaji katika kisiwa cha Anjouan na tunaamini watanzania wako katika nafasi nzuri ya kuzitumia,” alisema na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni wa damu na wa kihistoria.

  Alisema kuwa kuna unmuhimu wa kuendelea kushirikiana katika eneo la uwekezaji na kutaja maeneo ambayo yanahitaji uwekezaji kuwa ni elimu, utalii, nishati na katika sekta ya afya.

  “Tuna hospitali kubwa zinajengwa lakini tatizo ni kukosekana kwa wataalamu wa afya ikiwemo wauguzi na madaktari hivyo tunaomba watanzania waje kutusaidia katika eneo hilo,” alisema.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Juliet Kairuki amesema kuwa ujio wa Gavana huyo na ujumbe wa wawekezaji utasaidia kufungua fursa za uwekezaji na ushirikiano mzuri kiuchumi kati ya nchi hizo.

  “TIC na serikali inathamini ziara ya Gavana na ujumbe wake, mahusiano yetu ni ya siku nyingi na tungependa kuyaimarisha,” alisema na kuongeza kuwa ziara hiyo itasaidia kuvutia uwekezaji kutoka katika kisiwa hicho.

  Kama moja ya ratiba zake akiwa hapa nchini, Gavana huyo anatarajiwa kushiriki katika kongamano kubwa la uwekezaji kanda ya kaskazini linalotarajiwa kuanza mkoani Tanga asubuhi hii.

  Benki mbalimbali, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Mamlaka ya Uwekezaji Tanzania (EPZA) na Muungano wa wenye viwanda Tanzania (CTI) ni baadhi ya walioalikwa kwenye kongamano hilo.

  Kongamano hilo linatarajia kuvutia washiriki 1,500 toka ndani na nje ya nchi, ikiwemo China.

  Baadhi ya vivutio katika kanda ya kaskazini ni ardhi yenye rutuba kwa kilimo cha mazao ya biashara, mbogamboga na matunda, madini, na utalii.

  Gavana huyo atakutana pia na wakuu wa mikoa inayounda kanda hiyo ya kaskazini, mmoja mmoja wakati wa kongamano hilo. Mratibu wa ziara hiyo kwa upande wa Anjouan, Bw. Allaoui Toihirdine alisema kuwa mahusiano ya Anjouan na Tanzania ni ya kihistoria na kwamba ziara hiyo itaimarisha uhusiano huo.

  Alisema, Anjouan inatambua mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania katika kukikomboa kisiwa hicho mwaka 2009 na kukirudisha katika utawala wa muungano wa visiwa vya Comoro.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za Rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bibi Fatma Mwassa kufuatia kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bibi Anna Magoa kilichotokea tarehe 24 Septemba, 2013 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar-Es-Salaam.

  Katika salamu hizo, Rais amemuelezea Bibi Magoa kuwa alikuwa kada na mchapakazi hodari ambaye ameacha pengo kubwa katika Chama na Serikali.

  “Kwa hakika umepoteza moja ya nguzo zako mkoani Tabora. Bibi Anna amekua kada na mtumishi wa kutumainiwa katika Chama chetu cha Mapinduzi na serikali kwa ujumla. Tumeondokewa na mtu muhimu na mchapa kazi hodari” Rais amesema na kumuomba Bibi Fatma Mwassa kumfikishia salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki zake wote.

  Rais pia amewatumia salamu za pole wafanyakazi na wananchi wa Urambo ambao marehemu amekuwa akifanya nao kazi tangu alipohamia Wilayani humo Mwaka 2010.

  Marehemu ameacha mtoto mmoja wa kike na wajukuu wawili. Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Mkoani Iringa kwa maziko.

  Imetolewa na:

  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
  Ikulu
  Dar-Es-Salaam, Tanzania
  25 Septemba, 2013

  0 0

  MCHUNGAJI Ambilikile Mwaisapila wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonyesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

  Ametoa kauli hiyo jana asubuhi (Jumanne, Septemba 24, 2013) mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.

  Mchungaji Mstaafu Mwaisapila maarufu kama Babu wa Samunge alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa.


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo , Prof. Elisnate Ole Gabriel, (kulia) akiongea na Bondia Mstaafu Rashid Matumla(wenye fulana ya mistari) leo jijini Dar es Salaam, ambapo ametakiwa kurithisha kipaji chake kwa vijana nchini (kushoto) ni Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo Leonard Thadeo.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ,Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akiongea na Bondia Mstaafu ,Rashid Matumla leo jijini Dar es Salaam alipomtembelea,(Pichani mwenye koti jeusi) Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo, Leonard Thadeo,(mwenye fulana ya mistari) ni Bondia Mstaafu Rashid Matumla,.. (kushoto) Afisa Vijana katika wizara hiyo Amina Sanga.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) pamoja na Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari ) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Michezo katika Wizara hiyo Leonard Thadeo(kushoto) wakati akitoa maelezo leo jijini Dar es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye miwani) Mkurugenzi wa Michezo katika wizara hiyo Leonard Thadeo( mwenye koti jeusi kulia), Bondia Mstaafu Rashid Matumla (mwenye fulana ya mistari)), pamoja na Afisa Vijana katika wizara , Amina Sanga(kushoto). Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

  Na Concilia Niyibitanga

  Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemtaka Bw. Rashid Matumla ambaye ni bondia mstaafu katika mchezo wa ngumi za ridhaa kurithisha kipaji chake kwa vijana wengine.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel wakati akiongea na Bw. Matumla alipomtembelea ofisi kwake.

  Prof. Gabriel amemtaka kuanzisha kikundi cha vijana ambacho ataweza kukifundisha mchezo huo ili kipaji chake kisipotee ukizingatia kuwa Tanzania ina wachezaji wachache katika mchezo huo.

  “Ni vema ukarithisha ujuzi wako katika mchezo wa ngumi kwa vijana chipukizi kwa kuwafundisha na kuwashauri katika mchezo huo” Amesema Prof. Gabriel.

  Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wake katika mchezo wa ngumi hapa nchini na hivyo si vema akakaa na ujuzi wake ukizingatia kuwa yeye amestaafu katika mchezo huo.

  Aidha, Prof. Gabriel ameongeza kuwa kwa kufanya hivo Matumla atawasaidia vijana chipukizi kuwa Mabondia wazuri wa baade ikiwa ni pamoja na kujiajiri badala ya kujihusisha na vitendo vibaya kama matumizi ya madawa ya kulevya n.k

  Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leonard Thadeo amesema kuwa kikundi hicho kinaweza pia kikajihusisha na ujasiriamali kwa kuomba mikopo katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuwa wanamichezo pia wanatakiwa kujishughulisha na ujasiriamali ili kujiongezea kipato.

  Kwa upande wake Bw. Matumla amesema kuwa amefurahi na amefarijika sana kuongea na viongozi wa wizara inayosimamia michezo na vijana kwa kuwa wameonesha kutambua mchango alioliletea Taifa hili katika mchezo huo.

  Matumla amesema kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha kuwa anawarithisha mabondia chipukizi na vijana wengine kipaji chake katika mchezo huo ili wawe mabondia bora wa baadaye.

  0 0

  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Simbani, Bw. Ombeni Ally (katikati), akipokea vitabu toka kwa mwakilishi wa shirika la HUC Bw. Ramadhani Kuchimba, Jumatatu Septemba 23, 2013. Kulia ni Afisa Mtendaji wa Simbani, Bw. Kuboja Majogoro.
  Ndivyo wasemavyo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Simbani iliyo mkoa wa Pwani, wakifurahia vitabu vya msaada toka HUC, Jumatatu, Septemba 23, 2013. HUC ni shirika lisilo la kiserikali lenye makao yake Marekani, linalosaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama na vifaa vya elimu kwa maeneo yenye upungufu wa huduma za kijamii.
  Mwakilishi wa Shirika la HUC nchini Tanzania, Bw. Ramadhan Kuchimba (kushoto), akimkabidhi vitabu Meneja wa Kibaha Children’s Village Centre, Bw. Deogratius Mosha, Jumatatu Septemba 23, 2013, Mkoani Pwani.
  Wafanyakazi wa Kibaha Children’s Village Centre wakigawa vitabu vya msaada toka Shirika la HUC. Kushoto ni Mwakilishi wa HUC Tanzania, Bw. Ramadhan Kuchimba.
  Meneja Mtandao usio wa Kijamii wa HUC, Bw. Nathan Mpangala (kushoto) akigawa vitabu kwa watoto wa Kibaha Children’s Village Centre, Jumatatu Septemba 23, 2013. Kituo hiko kiko Kibaha, Pwani.
  Wakati wa kujisomea: Watoto wa Kibaha Children’s Village Centre wakifurahia vitabu vya msaada toka Shirika la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), Jumatatu septemba 23, 2013.
  Muda mfupi baada ya HUC kukabidhi vitabu vya msaada katika kituo cha Kibaha Children’s Village Centre.

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Francis Chaula akimkabidhi Sadock Mahenge  shilingi laki moja.
   Mlemavu Sadock Sanga Mahenge akishukuru kwa kupewa fedha hiyo.
  ======
  Na Edwin Moshi 
  wa Globu ya Jamii, Makete
  Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimetekeleza ahadi yake kiliyoitoa mwezi uliopita kwa mlemavu Sadock Mahenge ya kumpatia shilingi laki moja kwa ajili ya kukarabati baiskeli yake.
  Akimkabidhi fedha hizo taslimu nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Francis Chaula amesema kwa kuwa walimuahidi kumsaidia kurekebisha baiskeli yake na yeye kuaninisha gharama, ndipo wamempatia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya marekebisho hayo ili kumsaidia kutembea.
  "Nakumbuka wakati wa ziara yangu mwezi uliopita nilikuahidi mimi kwa niaba ya chama, hivyo ahadi hiyo tumeitekeleza naomba nikukabidhi fedha hizi shilingi laki moja zilizotolewa na CCM" alisema Chaula
  Kwa upande wake Sadock Sanga Mahenge amekishukuru chama hicho kwa kutekeleza ahadi hiyo, na kuahidi kuzitumia fedha hizo kama zinavyotakiwa kwa kurekebisha baiskeli yake ili imsaidie kuzunguka maeneo mbalimbali kutekeleza wajibu wake  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver Hoxhaj walipokutana Mjini New York kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
  Mhe. Membe akizungumza na Mhe. Hoxhai.
  Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Mhe. Membe wakati wa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo. Kulia ni Grayson Ishengoma, Afisa Mambo ya Nje, Bi. Tully Mwaipopo, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York na Bw. Togolani Mavura, Msaidizi wa Waziri.
  Mhe. Hoxhaj akizungumza na Mhe. mhe. Membe ambapo aliishukuru Tanzania kwa kuitambua nchi yake na kuomba ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili uimarishwe.
  Mazungumzo yakiendelea.
  Picha na Rosemary Malale

  0 0

  NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta ajira vijana pindi watakapokuwa tayari kuienzi kwa vitendo na kuisomea. 
  Mhe Makala alisema hayo mjini Bagamoyo  alipokuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tamasha la 32, la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lenye kauli mbiu ‘Sanaa na Utamaduni katika kukuza utalii’ linaloshirikisha vikundi zaidi ya 70, kutoka ndani na nje ya Tanzania. 
   Akihutubia, umati wa wananchi,wanafunzi wa chuo hicho cha sanaa na vikundi mbalimbali vinavyoshiriki, Waziri Makala alisema akiwa waziri mwenye dhamana atahakikisha utamaduni na sanaa nchini inakua huku ikiwanufaisha watu wote kwa vizazi vya sasa na vya baadae. “Katika kuenzi Sanaa na Utamaduni, Wizara ina mipangilio mingi ikiwemo ya kuhakikisha tunakuza utamaduni wa Taifa letu na hata ajira kwa vijana ambao watajiunga na sanaa hivyo tutaendelea kushirikiana na chuo cha TasuBa na wadau wengine katika kufikia malengo” alisema Makala. 
   Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Michael Kadinde alisema watahakikisha tamasha hilo kongwe nchini wanafikia vikundi na wasanii mbalimbali ilikupata kushiriki na kuonesha kazi zao. 
   “Lengo kufikia wasanii wote na hilo tunafanya kila mwaka na zaidi milango ipo wazi kwa mashirika binafsi ya ndani na nje kuja kuwekeza na kukuza sanaa zetu” alisema Kadinde Na kuongeza kuwa kwa sasa TaSUBa ina enzi na kulithisha sanaa na utamaduni kwa vitendo ikiwemo kutoa mafunzo kwa watoto wadogo na wale wa elimu ya msingi. .. 
  Kwa upande wa Vikundi vinavyoshiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na ; Alisema, vikundi 40 kati ya 60, ni kutoka Tanzania na vingine ni kutoka nje ya nchi vikiwemo vilivyowahi kushiriki tamasha hilo na vipya ambavyo itakuwa ni mara ya kwanza kuja. 
   Alivitaja vikundi vya Tanzania kuwa ni Ngome International Magic Show – JWTZ, Splendid Theatre, Kigamboni Community Centre, Malezi Youth Theatre na Jivunie Tanzania Sanaa. Vingine ni Mapoloni Culture Centre, Albino Revolutionary, Cocodo African Music, Imani Theatre, Safi Theatre, Imara Boma, Bagamoyo House of Talents, Bwagamoyo Africulture, Godykaozya & Tongwa Band na Mtoto Mchoraji. Vimo pia Shada Acrobatics.
  Vingine ni Bagamoyo Players, Bayoice, Jikhoman & Afrika Sana Band, Vitalis Maembe & The Spirit Band na Bagamoyo Dance Company. Aidha, kuna vikundi vya Makini Organization (Arusha), Tumaini Group (Manyara), Kimanzichana Vijana Group (Mkuranga), Utandawazi Theatre Group (Matwi Gha Chalo), kutoka visiwa vya Ukerewe, Hiari ya Moyo (Dodoma), Moshi Police Academy (Moshi), CBM Acrobatic Group, Man Kifimbo Band na Midundo ya Sanaa.
   Pia kuna vikundi kutoka Ethiopia , Kenya , Norway , Uganda , Rwanda na Ujerumani
   “WANACHUO TUNACHEZA HIVI’wanachuo wa chuo cha sanaa bagamoyo wakicheza ngoma kwenye tamasha la sanaa la kimataifa linalofanyika katika viwanja vya chuo cha sanaa bagamoyo wakionyesha umahili wao wa kuisakata ngoma .mbele ya mgeni rasimi jana katika ukumbi wa chuo bagamoyo mkoani pwani.
   Watoto wadogo Gozibet Bwere miaka minne na mwingine  Nyambuli Aginess Muganga wa kikundi cha ngoma cha Utandawazi  Theater Group Matwigachallo, kutoka kijijij cha Nansore Wilaya ya ukerewe mkoa wa mwanza wakiwa wanacheza ngoma jana katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamo kwenye Tamasha  la kimataifa la  32la sanaa na Utamaduni Bagamoyo, kauli mbiu ni sanaa na utamaduni katika kukuza Utalii linalo endelea katika chuo cha sanaa bagamoyo mkoani Pwani
   msanii maarufu hapa nchi wa muziki wa kisasa Misoji  Nkwambi   wa katika  wa kushoto ni mwanachuo  Safina Amani na wakulia ni Clement Chares akicheza ngoma na hivi sasa misoji ni mwanachuo wa chuo cha sanaa bagamoyo
  Wanakikundi wa ngoma ya Utandawazi  Theater Group Matwigachallo, kutoka kijijij cha Nansore Wilaya ya ukerewe mkoa wa mwanza wakifanya vitu vyao.Picha kwa Hisani ya Simon Makala, Mwanamakala.blogspot.com)

  0 0


  Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe Kushoto akizungumza na Waandishi wa Habari wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba na Kulia ni Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR-MAGEUZI James Mbatia muda mfupi baada ya kuwasili zanzibar kwa ajili ya mkutano wawa hadhara wa pamoja kuwashawishi wananchi kuukataa mchakato wa katiba 
   
  Kamanda wa Polisi wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam,  alithibitisha kuwa wamepokea barua ya maombi hayo na tayari wameshawaruhusu, lakini kwa kufuata masharti yakiwamo kutotoa lugha za matusi katika majukwaa na kutoa kauli ambazo hazitahamasisha chuki.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano, Habari na Haki za Binadamu wa CUF, Salum Bimani, alisema tayari maandalizi yameshakamilika na wameshapokea kibali cha kufanya mkutano huo kutoka kwa Jeshi la Polisi ukiwa na lengo la mshikamano wa vyama vya upinzani kuhusu muswaada wa rasimu ya katiba.

  Alisema mkutano huo utahusisha chama cha CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi. Pia mkutano huo utahudhuriwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano Zanzibar, Mzee  Hassan Nassor Moyo.

  Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi na Bimani, mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Kibanda Maiti.

  0 0


   Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akizindua Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli  jijini Dar es Salaam.
   Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki akionesha kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” alichokizindua leo makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
   Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu) akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam. (Katikati) ni Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki, Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyeki wa THBUB Mahfoudha Alley Hamid.
   Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Mary Massay akiwasisitiza washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika katika ofisi za THBUB zilizopo mtaa wa Luthuli leo jijini Dar es Salaam. Wakwanza ni ni Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki (katikati) ni Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu).
   Naibu Waziri Wizara ya  Katiba na Sheria Mhe. Angellah Kairuki  akiongea na washiriki waliohudhuria uzinduzi wa kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” leo katika ofisi za  Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) zilizopo mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyeki wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Amiri Manento (Jaji Kiongozi Msaafu).
  Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Angellah Kairuki baada ya kuzindua Kijitabu cha “Mwongozo wa Utawala Bora” uliofanyika makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) mtaa wa Luthuli  jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO

  0 0

  The Tanzania Tourist Board (TTB) in collaboration with the Tourism Confederation of Tanzania (TCT) presented the International Marketing Strategy to Ambassadors whose countries are among the major tourist source markets for Tanzania. 
  The event, held at the Serena hotel in Dar es salaam last night, was  aimed at introducing the strategy to the diplomatic corps and seeks their cooperation in the implementation of the strategy in their respective countries. Among the countries which are targeted in the International Marketing strategy include the United Kingdom, United States of America, Germany, Italy, France, Netherlands, Canada, Australia, and Spain. 
  South Africa,India, China, Russia, Turkey, Brazil and the Gulf countries will also be monitored closely. 
   The Executive Secretary of the Tourism Confederation of Tanzania (TCT) MrRichard Rugimbana, makes his presentation
   The Managing Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki presents the International Marketing Strategy to the Ambassadors.
  A section of members of the diplomatic corps  listening to the presentations.


  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mkutano wa 'celebrating humanitarian champions and partnerships in Africa' ulioshirikisha viongozi wa juu wa bara hilo. Mkutano huo ulifanyika huko New York nchini Marekani tarehe 25.9.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Bwana Bekele Geleta, Katibu Mkuu wa International Federation of the Red Cross na kushoto kwake ni Mheshimiwa Aisha Abdullahi, Kamishna wa Masuala ya Siasa wa Kamisheni ua Afrika akifuatiwa na Mheshimiwa Valerie Amos, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya huduma za kibinadamu na dharura-Humanitarian Affairs and Emergency Relief. 
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa viongozi wa juu wa Afrika ulioratibiwa na Umoja wa Mataifa na kufanyika New York tarehe 25.9.2013.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia katika mkutano huo
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa 'celebrating humanitarian champions and partnerships in Africa' 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na washiriki mbalimbali waliohudhuria mkutano wa kusherehekea humanitarian partnership in Africa tarehe 25.9.2013. Picha na John Lukuwi  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets the CEO of the Millenium Challenge Corporation (MCC) Mr.Daniel Yohannes in New York
    Zanzibar's Minister for Labour, Economic Empowerment and Cooperation Mr.Haroun Ali Suleiman meets MCC CEO Mr.Daniel Yohannes in New York
   President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete meets and hold talks with the Foreign Minister of the Sultanate of Oman Mr.Yousef Bin Alawi Bin Abdullah in New York

  Rais Kikwete: Tunaifanyia mageuzi makubwa TANESCO


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake inalifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa nia ya kuharakisha jitihada za Serikali kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi.


  Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali imechukua hatua nyingi na kali za kupambana na rushwa kwa nia ya kukomesha vitendo hivyo katika Tanzania na kuinua kiwango cha utawala bora.


  Rais Kikwete ameyasema hayo Jumatano, Septemba 25, 2013 wakati alipokutana na kuzungumza na ujumbe wa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani la Millennium Challenge Corporation (MCC)ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wake, Bwana Daniel W Yohannes.


  Ujumbe huo umekutana na Rais Kikwete katika Hoteli ya JW Marriott mjini New York ambako Rais Kikwete amefikia kwa ziara yake ya kikazi katika Marekani ambako miongoni mwa mambo mengine atahutubia Mkutano wa 68 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) ulioanza jana, Jumanne, Septemba 24, 2013.


  Katika mazungumzo hayo, Bwana Yohannes amemwelezea Rais Kikwete kuhusu maendeleo ya ombi la Tanzania kuingizwa katika awamu ya pili ya misaada ya Serikali ya Marekani kupitia MCC chini ya Akaunti ya Milenia Tanzania (MCA(T)). Nchi nyingine za Afrika ambazo maombi yao yanafikiriwa katika awamu hiyo ya pili ni Morocco, Mozambique na Lesotho.

             

  Tanzania ndiyo nchi iliyopokea sehemu kubwa zaidi ya msaada wa MCC duniani katika awamu ya kwanza ambako ilipewa kiasi cha dola za Marekani milioni 698 ambazo zimeingizwa katika miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, usambazaji wa umeme vijijini, miradi ya maji na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia.


  Serikali ya Tanzania imeamua kuwa fedha za awamu ya pili ya MCC zitaingizwa kupanua zaidi huduma za umeme na ujenzi wa barabara za vijiji kwa nia ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaopata huduma za umeme na kwa nia ya kuboresha barabara za vijijini katika maeneo yanayozalisha mazao kwa wingi zaidi.


  Serikali ya Rais Kikwete imeliweka suala la usambazaji umeme kwa Watanzania mijini na vijijini miongoni mwa maeneo yake ya kipaumbele. Wakati anaingia madarakani mwaka 2005, ni asilimia 10 tu ya Watanzania waliokuwa wanapata umeme. Katika miaka saba iliyopita, asilimia hiyo imepata hadi kufikia 21 ikiwa ni asilimia 11 zaidi kuliko katika miaka yote 50 ya Uhuru. Lengo la sasa ni kuifikisha asilimia 30 ama zaidi mwaka 2015.


  Katika mazungumzo hayo na Rais Kikwete, Bwana Yohannes ametaka kujua ni hatua zipi Serikali inazichukua kurekebisha changamoto zinazoikabili TANESCO na hatua gazi zinachukuliwa kuzidi kukabiliana na matatizo ya rushwa.


  Rais Kikwete amemweleza Bwana Yohannes: “Kama unavyojua, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepitia safari ngumu na kukabiliwa na changamoto nyingi lakini sasa tumeamua katika Serikali kulifanyia mageuzi muhimu na marekebisho makubwa kwa maana ya muundo wake na pia kuangalia viwango vya malipo ambayo Shirika hilo linawatoza wateja wake. Mageuzi haya katika TANESCO ni muhimu sana na yameanza kufanyika na kwa hakika Serikali imedhamiria kukayamilisha mageuzi hayo katika muda mfupi iwezekanavyo.”


  Kuhusu rushwa, Rais Kikwete amemwambia Bwana Yohannes, “Jitihada zetu katika kupambana na rushwa zinaendelea. Tumeimarisha taasisi inayohusika na kuzuia na kupambana na rushwa.Tumeimarisha mtandao wa kukabiliana na balaa hili na Serikali yangu imewafikisha mahakamani waliopata kuwa viongozi na maofisa waandimizi wa umma katika Serikali kujibu mashitaka ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.”

  Imetolewa na:

                                                     Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,


  DAR ES SALAAM.


  0 0

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa vya michezo muda mfupi kabla ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa. Vifaa hivyo vitatumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom ilikabidhi jezi za soka seti 12, mipira 40 na kombe kubwa la Mshindi

   Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea kombe kubwa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa mashindano maalum kwa shule za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa na Wizara.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi pia jezi za soka seti 12 na mipira.
  ---------------------------

  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala leo amepokea vifaa vya michezo kutoka Vodacom kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano maalum ya sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es salaam.

  Akipokea vifaa hivyo ambavyo ni jezi seti 12 na mipira 40 pamoja na kombe kwa ajili ya bingwa wa michuano hiyo Waziri Dk Mukangala ameelezea kufurahishwa kwake jinsi ambavyo Vodacom walivyopokea ombi la Wizara la kusaidia mashindano hayo.

  Amesema lengo la mashindano hayo ni kuendeleza azima ya serikali ya kutengeneza fursa ya ukuzaji na uendelezaji michezo kwa ngazi za chini kupitia falsafa ya michezo jamii.

  “Michezo ni gharama inahitaji fedha nyingi kugharamia vifaa, mafunzo kwa walimu, viwanja na gharama nyengine za uendeshaji ndio maana naipongeza sana Vodacom kwa kukubali ombi letu la kusaidia mashindano haya maalum yatakoyoshirikisha shule 12 za sekondari za Mkoa wa Dar es salaam.”Alisema

  “Mashindano haya ni ya majaribio tukiangalia namna ambavyo tunaweza kuwekeza vya kutosha kwenye michezo ngazi ya mashuleni kwa nchi nzima, tutaanza na mchezo wa soka ila mipango ni kupanua wigo kwa kuongeza mpira wa pete na riadha kwa hapo mwakani ikihusiha mikoa mingi zaidi.”Alisema Dk. Mukangala

  Waziri Dk. Mukangala amesema Wizara yake inaimani kubwa juu ya mpango huo huku akizitaka jamii kuyapokea na kuyaona kuwa ni sehemu yao ili pamoja na kuyapapa mafanikio bali pia kuwatia moyo watoto wakati wote watakapokuwa waskishiriki.

  Amesema kuwa anatambua kuwa mahitaji ni makubwa na kwamba kila shule hapa nchini ingependa kushiriki lakini kwa kuanzia watachagua shule 12 za sekondari kama majaribio huku mipango ikiendelea kuwekwa sawa ili mashindano hayo yawe mapana zaidi kwa hapo mwakani.

  “Tuna shule nyingi hapa tu Dar es salaam tumepata wakati mgumu sana kuchagua wawakilishi wa kila Wilaya lakini kwa sasa tunaanza na hizo chache tukiwa na Vodacom na baada ya kumalizika tutafanya tathmini kuona namna ya kuyaongezea wigo wa ushiriki na wa kijiografia.”Alisema Dk. Mukangala

  Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa amesema Vodacom inatambua umuhimu wa kuwaandaa wachezaji katika ngazi za chini ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya michezo nchini.

  “Kukubali kwetu kuwa wadhamini kumesukumwa na imani yetu juu ya maendeleo ya michezo nchini tukiamini katika kuwekeza kwa wanafunzi mashuleni, leo tunafuraha kuwa sehemu ya miapngo ya serikali kukamilisha kile ambacho kila mtu anapenda kukiona kikifanyika katika michezo.”Alisema Twissa

  “Tumekuwa wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa kimaendeleo hasa kwenye eneo la ushindani hivyo ili mafanikio hayo yawe endelevu ni lazima tuwe na misngi mzuri wa kuzalisha wachezaji wenye ubora na viwango na kwamba njia moja ya msingi ni kuwa na mashindano ya ngazi za chini hasa mashuleni”Alisema Twissa

  Amesema vifaa walivyovitoa ni sehemu ya Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali za kutekeleza mikakati ya uzalishaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na kwamba Vodacom inafurahia mpango huo.


  Mashindno hayo maalum yataratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa – BMT na kwamba utaratibu umewekwa wa kuapat sekondari 12 kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es salaam ambapo kila Wilaya itatoa sekondari  4.

   


  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  akitia saini kitabu cha maombolezi katika ubalozi wa Kenya nchini Tanzania kufuatia mashambulizi ya Kigaidi nchini Kenya yaliyotokea hivi karibuni.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania George Awenour baada ya kutia saini kitabu cha maombolezi.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akiangalia bidhaa mbali mbali katika maonyesho ya India yaliyofanyika viwanja vya sabasaba Dar es Salaam.
   Waziri wa Nchi, Biashara na Viwanda wa India Dr. D. Purandeswari, akitoa maelezo kuhusiana na maonyesho ya biashara ya India yanayofanyika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
   Kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara wa India Sanjay Kirloskar, akimkabidhi zawadi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar  Maalim Seif Sharif Hamad katika maonyesho ya biashara ya India yanayofanyika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akihututubia katika ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya India katika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi mbali mbali wakiingia katika ukumbi wa mikutano katika viwanja vya saba saba Dar es Salaam. Picha na Hassan Kombo

  0 0
 • 09/26/13--00:18: Vacancies

 • 1. CLAIM OFFICER - One position

  2. PRINCIPAL OFFICER - One position
  3. BUSINESS DEVELOPMENT MANAGER - One Position  Experience preferably 3 Years, Send your CV without forgetting your phone


older | 1 | .... | 264 | 265 | (Page 266) | 267 | 268 | .... | 3270 | newer