Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 267 | 268 | (Page 269) | 270 | 271 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0
 • 11/16/13--03:06: Tuzo kwa AZAKI bora 2013.
 • Tamasha la 11 la AZAKI limemalizika rasmi usiku wa kuamkia leo kwa dhifa ya utoaji tuzo kwa AZAKI Bora, iliyofanyika katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Plaza, jiji Dar es Salaa ambapo mgeni rasmi ni Naibu Waziri, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu.
  Kushoto ni Mh. Ummy Mwalimu( Naibu Waziri, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ) Akikabidhi Tuzo kwa Mwakilishi wa Jumuiya ya kuelimisha Athari za Madawa ya Kulevya UKIMWI na Mimba Katika Umri Mdogo  Ya Pemba- Mshindi, Asasi Bora 2013
  Mh. Ummy Mwalimu( Naibu Waziri, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Dk. Stigmata Tenga- Rais wa FCS, katika picha ya pamoja na ashindi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  TUMEPUNGUZA BEI ZA KUSHIP MAGARI KWENDA DAR/MOMBASA
  4 X 4 CARS TO DAR/MOMBASA NOW FROM  £800
  SALOON CARS NOW FROM £700
  TUNATOA  25 DAYS FREE STORAGE IN MOMBASA
  TELEX RELEASE KWA MOMBASA NI FREE

  20' CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,350
  OUR AGENT IN DAR; TORNADO TEL; +255 713607116

  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477


  0 0

   Council  Members Casting their votes
  Ambassador Macharia Kamau, Permanent Representative of the  republic of Kenya to the UN addressing the Council
  Amb. Takeda Alam ( Center) Permanent Representative of Ethiopia to the UN and head of the African  Union group fromed to address the question of ICC trials speakes to the press following the vote. With him are Amb. Nelosn Messone  of Gabon to the UN and Kenya's  Amb. Macharia Kamau.
  For full story CLICK HERE

  0 0

  Dk Kamala akiangalia malighafi itakanayo na maua ya pareto alipozuru kiwanda cha Pareto Mafinga.

  Martin Oweka Meneja wa PCT akimuonesha Dk Kamala shehena ya maua ya pareto ikiendelea kupimwa  
  Akielezwa jinsi ubora wa pareto unavyochunguzwa katika maabara ya kiwanda
  Akielezwa mitambo ya kiwanda inavyofanya kazi

  .................

  BALOZI wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dk Diodorus Kamala amekitafutia soko la malighafi inayozalishwa kutokana na maua ya pareto, Kiwanda cha Pareto Tanzania (PCT).

  Hatua hiyo ni utekelezaji wa diplomasia ya uchumi inayomtaka kila balozi kutafuta masoko ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
  Katika ziara yake aliyofanya  katika kiwanda hicho juzi, Balozi huyo alisema “ nilikuja nchini na wafanyabishara na wawekezaji 65, wametembelea sehemu mbalimbali za uwekezaji bara na visiwani.”
  Alisema katika utendaji wake kazi za kibalozi nchini Ubelgiji alikutana na kapumi ya Nilo Vital France/Belgium iliyoonesha nia ya kuendeleza sekta ya kilimo cha pareto nchini.
  “Kampuni hiyo inataka kufanya biashara na PCT na kwa kuanzia imeahidi kununua tani 40 za malighafi itokanayo na maua ya pareto kila mwaka,” alisema.
  Mbali na kununua malighafi hiyo, Dk Kamala alisema kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na kiwanda hicho kuboresha miundombinu ya kiwanda na kutoa misaada ya kitaalamu na kifedha kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji.
  “Hii ni kampuni kubwa yenye leseni ya kufanya biashara hiyo katika nchi zote za Ulaya; mkiingia nayo mkataba mtaongeza namba ya masoko, ushindani na hatimaye faida zaidi,” alisema.
  Akimshukuru balozi huyo kwa kujali maenddeleo ya sekta ya kilimo hicho, Meneja wa PCT, Martin Oweka alisema aliishauri serikali kurekebisha utaratibu wa utoaji leseni ya ununuzi wa zao hilo kutoka kila baada ya mwaka mmoja na kuwa kila baada ya miaka mitano.
  Pamoja na kurekebisha utaratibu huo alisema PCT inapendekeza kampuni zote zenye leseni ya biashara ya pareto ziwe na utaratibu wa kuingia mikataba ya biashara na wakulima ili kuwapa uhakika wa soko.
  Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Martin Oweka, Bodi ya Pareto Tanzania ndiyo yenye jukumu kwa niaba ya serikali ya kutoa leseni hizo.
  Akizungumzia uzalishaji, alisema umeongezeka kutoka tani 50 mwaka 2007 hadi tani 3,000 mwaka huu.
  Alisema kiasi kilichonunuliwa hakikidhi mahitaji ya kiwanda chao kilichopo mjini Mafinga chenye uwezo wa kusaga hadi kufikia malighafi dondoo tani 5,000 za maua ya pareto kwa mwaka.

  0 0

  MALINZI KUFUNGUA MICHUANO YA UHAI 2013

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi  (pichani) atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.

  Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika kesho (Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.

  Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa Karume).

  Kundi C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, na kwenye uwanja huo huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania Prisons.
  RAMBIRAMBI MSIBA WA NYOTA COPA COCA-COLA
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Sayari, Fatuma Bahau ‘Crouch’ kilichotokea jana (Novemba 15 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.

  Msiba huo ni mkubwa katika mpira wa miguu kwani Fatuma ndiyo kwanza alikuwa anachipukia katika mpira wa miguu wa wanawake ambapo alikuwa mfungaji bora wa michuano ya U15 Copa Coca-Cola ya mwaka huu akichezea timu ya Ilala, hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima.

  Kwa mujibu wa mlezi wa mchezaji huyo, Stephania Kabumba, marehemu anasafirishwa kesho kwenda kwao Mwanza kwa ajili ya maziko ambapo kifo chake kimesababishwa na ugonjwa wa malaria.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bahau, klabu ya Sayari, Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  Mungu aiweke roho ya marehemu Fatuma mahali pema peponi. Amina

   Boniface Wambura Mgoyo
  Kaimu Katibu Mkuu
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0


  0 0

  Photo0001
  KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA LIMITED (MeTL) Makao Makuu inatangaza kwa umma wa watanzania kwamba Meneja wa MeTL tawi la Iringa Mr Aamir Iqbal anatafutwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi wa mamilioni.
  Mr Iqbal (pichani juu) aliyekuwa Meneja wa tawi la MeTL Iringa anatuhumiwa kwa kosa la kumwibia mwajiri wake mamilioni ya pesa na yeyote atakayewezesha kukamatwa au kutoa taarifa zake katika kituo chochote cha Polisi zawadi nono itatolewa.
  Tukio hilo lililotokea jana mchana Iringa na limeripotiwa Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na RB ya Polisi ni ref no. IR/RB/7229/2013.
  Kampuni ya MeTL Group itatoa zawadi nono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwake.
  Au piga simu namba: 0755 030 014 , 2118930/1, 0713 324 332, 0715 030 024
  PASSPORT AAMIR IQBAL 
  Hati ya kusafiria ya Aamir Iqbal.
  RPB AAMIR IQBAL 
  Kibali cha kazi cha Meneja huyo.

  0 0

  Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha nchini Sri lanka leo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Kiongozi wa Gangaramaya Temple Van Kirinda Assage.
    Mama Salma Kikwete akifuatana na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola wanaohudhuria mkutano wa Madola mjini Colombo nchini Sri lanka wakipokewa na mwenyeji wao Mama Shiranthi  Rajapakse wakati walipotembelea maonesho ya kazi za mikono  yaliyoko eneo la Janakala Kendraya katika vitongoji vya mji wa Colombo.   0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akisikiliza taarifa ya utekezaji wa kazi za Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, iliyosomwa na Waziri Said Ali Mbarouk,(kushoto)  katika mpangilio wake wa kuzungumza na kila Wizara katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,(katikati) Katibu Mkuu Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee

  Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa  Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,wakiwa,katika mkutano wa
  utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, katika utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo,katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar
   Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa  Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,wakiwa,katika mkutano wa
  utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika  Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar

  Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa  Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,wakiwa,katika mkutano wa
  utekelezaji wa Mpango wa kazi za Wizara hiyo. Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu, Zanzibar

  0 0

  Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akimkabidhi Sister Scholastica Mwembezi wa Masista Maria Mtakatifu Malkia wa Afika ambao ni wamiliki wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala Mkoani Rukwa viatu pea sitini zilizotolewa na Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Tunu Pinda ikiwa ni ahadi aliyoitoa alipotembelea kituo hicho mapema mwaka huu. Aidha Sister Mwembezi amemuomba Katibu Kanyanda kumfikishia salamu za shukrani Mama Pinda ikiwa ni pamoja kumkumbusha ahadi ya gari aliyoitoa kwa kituo hicho.  
   Ndugu Charles Kanyanda akimvisha viatu mmoja ya watoto yatima katika kituo hicho baada ya kukabidhi zawadi hizo kutoka kwa Mama Tunu Pinda. Mzee Kanyanda amewataka wadau mbalimbali kuonyesha moyo wa upendo katika kusaidia mahitaji mbalimbali kwa watoto na kituo hicho.
  Katibu wa Waziri Mkuu Jimbo Ndugu Charles Kanyanda akiimba moja ya wimbo na watoto wa kituo cha kulea mayatima cha Katandala.
  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0
 • 11/16/13--09:39: TOYOTA PASSO FOR SALE
 •  MAKER: TOYOTA
  MODEL: PASSO
  YoM: 2004
  ODO: 56247
  COLOR: MAROON
  HAIJATUMIKA BONGO.......
  PRICE: MIL 8 NEGOTIABLE
  MAWASILIANO 0713 344 399

  0 0

   Mke wa  Makamu wa Raisi Mama Aisha Bilali akiongea katika  kongamano la wanawake wajasiliamali namna ya kuwainua wanawake wa Tanzania kiuchumi lililofanyika leo katika ukumbi wa Mayfair Hotel , jijini Dar-es-salaam. 

   Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Women Footprints Initiative (WOFI) Vida Nasari Mndolwa  akiongea katika  kongamano la wanawake wajasiliamali namna ya kuwainua mwanamke wa Tanzania kiuchumi lililofanyika leo katika ukumbi wa Mayfair Hotel , jijini Dar-es-salaam. 

   Kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu  Mama Tunu Pinda  katikati ni Mke wa  Makamu wa Raisi Mama Aisha Bilali na Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Women Footprints Initiative (WOFI)  Vida Nasari Mndolwa katika  kongamano la wanawake wajasiliamali namna ya kuwainua wanawake wa Tanzania kiuchumi lililofanyika leo katika ukumbi wa Mayfair Hotel , jijini Dar-es-salaam
   
  Mke wa  Makamu wa Raisi Mama Aisha Bilali akiangalia bidhaa za waajasiliamali katika  kongamano la wanawake wajasiliamali namna ya kuwainua wanawake wa Tanzania kiuchumi lililofanyika leo katika ukumbi wa Mayfair hotel , jijini Dar-es-salaam.  Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda  katikati ni  Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Women Footprints Initiative (WOFI)  Vida Nasari Mndolwa. 


  0 0

  IMG_4606
  Mwana Fa mara tu alipowasili ofisi za VOA Washington Dc na kupokelewa na mkuu wa idhaa hiyo Dkt. Mwamoyo Hamza siku ya Ijumaa na kati kati ni Bibie Khadija Riyami na watangazaji wa idhaa (hawapo pichani ) kabla ya kuingia kwenye kipindi cha Live Talk kinachorushwa kila Ijumaa na VOA.  IMG_4630
  Mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya VOA Dkt. Mwamoyo Hamza (kushoto) na Mwana Fa na mwenyeji wake Dj.Rich Mwandemane
  . IMG_4626
  Bibie Khadija Riyami kushoto akiwa na Mwana Fa na Dj Rich wakiwa na prodyuza wa idhaa ya Kiswahili Duane Collins.
  Kwa picha zaidi ungana na sundayshomari.com. 
  Pia msikilize Mwana FA akiwa na AY na J. Martins hapo chini na ngoma yao inayotesa sasa ya 'Bila kukunja goti

  0 0

  Kijana mwenye umri wa miaka 18 Ibanda Ruhumbika (kati) mwanamuziki wa KiTanzania anayekuja juu katika ulimwengu wa Jazz. Hivi karibuni  alitumbuiza wapenzi wa Jazz (akiwa na Jon Batiste) kwenye Club maarufu ya Ronnie Scotts jijini London. 

  0 0


  0 0

  Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana  akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya Wananchi na chama kwa ujumla.
  Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini  wakishangilia  jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
  Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
  Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.
  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
  Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA NA HAPA

  0 0
  0 0

  Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt.Sengondo Mvungi, likiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo kwa ajili ya kuagwa
   Jeneza likipelekwa sehemu iliyoandaliwa
   Mashada ya maua na picha ya marehemu
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kutoka salamu za rambi rambi za serikali wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Sinde Warionba akiongea machache wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
   Makamu wa Rais Dkt Gahlib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Katiba Jaji Joseph Warioba, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angela Kairuki na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia wakiwa katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi,kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 
  Misa wakati wa shughuli hiyo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo.
  Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Dkt.Sengondo Mvungi, wakati wa shughuli ya kuagwa mwili huo iliyofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,leo. 

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0
 • 11/16/13--19:00: ngoma azipendazo ankal

 • Mzee mzima Luciano Pavarotti alipopanda jukwaani na  Tracy Chapman kuimba 'Baby Can I Hold You tonight' ilikuwa balaa

older | 1 | .... | 267 | 268 | (Page 269) | 270 | 271 | .... | 3284 | newer