Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

LUGOLA AWATAKA NIDA WAPITIE UPYA USAJILI, UTOAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA MIKOA YA KAGERA NA KIGOMA KWA LENGO LA KUWABAINI NA KUWAONDOA RAIA WA NCHI JIRANI

$
0
0

Na Felix Mwagara, MOHA-Kyerwa.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Kyerwa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa sokoni mjini humo, leo, Lugola alisema baadhi ya raia wa nchi jirani wamejipenyeza na kujipatia vitambulisho vya taifa ama kwa kuwatumkia wenyeji ama nguvu ya fedha.

“Hii haikubaliki na lazima tuwe makini katika hilo, nimepata taarifa kuhusu watu waliojipatia vitambulisho hivyo ambao hawastahili, kutokana na hilo natoa agizo kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA ahakikishe anapitia upya zoezi la kusajili ili aweze kuwabaini ambao walijipatia kwa njia ambazo sio halali,” alisema Lugola.Lugola alisema kuwa, utoaji wa vitambulisho hivyo katika mikoa hiyo unasuasua kwasababu ya umakini unaofanyika katika kusajili waombaji wa vitambulisho.

“Hakuna Mtanzania atakayekosa vitambyulisho vya taifa, kilka mtu anatapa ili mradi tu awe na sifa, na pia mpaka upate lazima upitie mchujo maalumu ili tuhakikishe wewe tunakupa kitambulisho ni Mtanzania halisi au sio.” Alisema Lugola.Aidha, Lugola pia juzi alimuagiza alimpa wiki mbili Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt Anna Makakara, awe amefika katika mikoa hiyo kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kufanya operesheni kubwa ya kuwaondoa Wahamiaji haramu katika Mikoa hiyo kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa mjini Kyerwa Mkoani Kagera, katika Mkutano uliofanyika katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo. Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiwasalimia viongozi wa Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera, wakati alipokuwa anawasili katika uwanja wa sokoni mjini humo, leo, kwa ajili ya kuzungumza na wananchi. Katika hotuba yake, Lugola amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa apitie upya usajili na utoaji wa vitambulisho vya taifa katika mikoa ya Kagera na Kigoma ili aweze kuwabaini na kuwaondoa raia wa nchi jirani zinazoizunguka mikoa hiyo.


DKT BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

$
0
0


Na Stella Kalinga, Simiyu

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.

Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.

Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna wanavyosimamia shughuli za maendeleo.

“Niwapongeze kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema

Aidha, amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa. 
Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wakifurahia jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa. 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi mara baada ya kuwasili wilayani humo kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya CCM ya Wilaya, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019 . 
Baadhi ya viongozi wa CCM wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05 na Januari 06 , 2019. 

MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO

$
0
0


NA ALFRED MGWENO TEMESA

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya ziara katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wafanyakazi wa Wakala huo katika mikoa hiyo kuongeza juhudi katika kazi ili kuhakikisha wanazalisha kipato cha kutosha kuweza kufikia malengo au hata kuzidi mapato waliyojiwekea kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.

Akizungumza na wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti, Mhandisi Maselle alisema anatambua kwamba TEMESA inakumbwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi hasa vya karakana pamoja na upungufu wa wafanyakazi lakini aliwataka mameneja wa mikoa hiyo pamoja na watumishi wake kujitahidi kufanya kazi zao kwa ufansi na kwa ushirikiano huku akiangalia namna ya kuwaongezea vitendea kazi na kujaza nafasi za watumishi zilizoachwa wazi baada ya kustaafu.


Katika mazungumzo yake Mhandisi Maselle alisisitiza kwamba, Kiongozi mzuri ni yule ambaye anafanya kazi bega kwa bega na wafanyakazi wenzake pale anapoona mapungufu na kuwatia moyo hivyo meneja ajitahidi kuwa karibu na watumishi wake.

Awali, Meneja wa TEMESA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo, alimpitisha Mtendaji Mkuu katika karakana ya mkoa ambapo alipata nafasi ya kukagua mashine na mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana hiyo na baadae alimkaribisha katika kikao na watumishi na kumkumbushia kuhusu changamoto zinazoukumba wakala kubwa likiwa ni upungufu wa wafanyakazi ambapo karibu kila kitengo kina mtumishi mmoja mmoja ikiwemo kitengo cha uhasibu na kitengo cha manunuzi na kumuomba kuzifanyia kazi kwa wakati ili kuhakikisha watendaji wa mkoa huo wanapata wasaidizi ili waweze kutenda kazi zao kwa ufanisi.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya kuchongea vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akielezea jinsi mashine ya kubadilishia tairi za magari inavyofanya kazi wakati akikagua mashine mbalimbali zilizopo katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro. Kushoto ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akitoa maelekezo kwa mafundi na wafanyakazi wa karakana ya mkoa wa Arusha mara baada ya kukagua mtambo wa kuchenjua na kuchakata kokoto (Crusher) unaoonekana pichani.
????????????????????????????????????
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati (aliyevaa koti) akikagua mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana ya wakala huo mkoani Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

VIONGOZI NA WANANCHI WILAYANI NEWALA WAJUMUIKA NA WAZIRI MKUCHIKA KUOMBOLEZA KIFO CHA MAMA TECLA MKUCHIKA

$
0
0
Viongozi mbalimbali wa serikali, dini, vyama vya siasa, watumishi wa umma na wananchi wilayani Newala wamejitokeza kwa wingi kuungana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt. (Mst) George Mkuchika (Mb) kuomboleza kifo cha mama yake mzazi, Bibi Tecla Bernadetha Mkuchika aliyefariki tarehe 2, 2019 akiwa na umri wa miaka 93 na kuenzi mchango alioutoa katika taifa enzi za uhai wake akiwa mtumishi wa umma na mtumishi katika hospitali zinazoendeshwa na taasisi za kidini. 

Akisoma wasifu wa marehemu wakati wa ibada takatifu ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana la Msalaba Mtakatifu lililopo kijiji cha Nambunga wilayani Newala, Msemaji wa familia Bw. Noel Boma alisema marehemu alijiunga na Mafunzo ya Ukunga katika Chuo cha kanisa Anglikana (UMCA) mwaka 1943 na mara baada ya kuhitimu alianza kazi St. Mary’s Hospital Newala.

Bw. Boma aliongeza kuwa, marehemu Bibi Mkuchika alihamishiwa Serikalini kutokana na uchapakazi wake, weledi na uadilifu aliokuwa nao wakati akifanya kazi kwenye zahanati ya kanisa la Nambunga na Mnyambe.
Bw. Boma aliainisha kuwa, marehemu akiwa serikalini alifanya kazi katika zahanati za Mihambwe, Mchichira, kitangari, Kilidu na Nambunga mpaka anastaafu.

Aidha, Bw. Boma alisisitiza kuwa, marehemu Bibi. Mkuchika ataendelea kukumbukwa na jamii kwa mchango wake mkubwa alioutoa wakati akihudumu Zahanati ya Kilidu ambayo hivi sasa inatambulika kama Samora kwa kitendo cha kushiriki kikamilifu kutoa huduma usiku na mchana kwa majeruhi wa vita vya ukombozi wa Msumbiji ambavyo vilipamba moto wakati huo. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwaongoza wanafamilia kuwasha mishumaa juu ya kaburi la Bibi Tecla B. Mkuchika, aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu.  
Askofu wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, Dkt. James Almasi Askofu Mstaafu Dkt. Mwachiko Boma, Askofu Oscar Mnung’a wa Dayosisi ya Newala na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika ibada ya mazishi ya mama mzazi wa Mhe. Mkuchika kabla ya kumpumzisha mama Tecla B. Mkuchika katika nyumba yake ya milele kijiji cha Nambunga Wilayani Newala. 
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kushiriki ibada ya mazishi ya Bibi Tecla B. Mkuchika ambaye ni mama mzazi wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb), aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya  Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu. 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika (Mb) akiwa na ndugu zake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao mpendwa, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu. 
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiweka shada la maua kwenye kaburi la mama mzazi wa Mhe. Mkuchika, Bibi Tecla B. Mkuchika aliyefariki tarehe 2 Januari, 2019 katika Hospitali ya Misheni Ndanda alikopelekwa kupatiwa matibabu. 



MICHUZI TV: POLE POLE ALIVYOMSHUKIA MAALIM SEIF KAMPENI ZA UDIWANI MAGAMENI

ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WIILAYA MBALIMBALI AFARIKI DUNIA

$
0
0
ALIYEWAHI kuwa mkuu wa wilaya tofauti hapa nchini wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na baadaye kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ,Waziri Juma Waziri amefariki dunia akitibiwa hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es salaam Juzi na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwao Sungwi baada ya swala adhuhuri.

Kwa mujibu wa watu wa karibu na mzee Waziri, msiba upo nyumbani kwake Tandika Berege Nyumba namba tatu.Mzee Waziri ambaye mwaka huu anatimiza miaka 89 alikufa siku chache tu baada ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa.Akiwa amehudumu katika wilaya mbalimbali zikiwamo Ngara, Pangani , Morogoro, Dodoma, Singida ni mmoja wa watumishi wa serikali waliofanyakazi kubwa ya kupambana na Nyarubanja, mfumo wa umiliki uliokuwa ukiendeshwa Mkoa wa Ziwa Magharibi.

Akiwa amesoma shule ya Msingi Pugu na kisha kusoma sekondari ya Minaki ni mmoja wa watanzania wa mwanzo waliokuwa na kazi kubwa ya kuonesha njia katika siasa za ujamaa na kujitegemea wakifuata maelekezo ya mwalimu.Katika mahojiano yake ya Mwisho na wandishi wa habari waliokuwa wanatengeneza dokumentari, alisema kwamba wakati wa utawala wa mwalimu Nyerere, rushwa na matumizi amabaya ya ofisi yalikuwa ni mambo yasiyovumilika.

Aidha alisema kwamba viongozi walikuwa na kazi kubwa ya kuelimisha watu kuelewa utawala maana yake nini na kushiriki katika kazi za kujenga taifa kwa uhuru na kujituma zaidi.Mzee Waziri ameacha watoto kadhaa, wajukuu na vitukuu.Miongoni mwa watoto wake ni Maida Waziri ambaye ni mjasiriamali na mhamasishaji maarufu wa ujasiriamali nchini na barani Afrika.

Aidha Maida Waziri ni mmoja wa wanawake wanaojulikana sana katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania akimiliki kampuni ya ujenzi ya Ibra Contractors.

WAZIRI UMMY ASHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIRARE JIJINI TANGA.

$
0
0

MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameshiriki ujenzi wa bweni la Wasichana kwenye shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga ambalo litakapokamilika litawasaidia kuwaepusha na vishawishi wanavyoweza kukutana nazo wanapokwenda shuleni na kukwamisha ndoto zao.

Ummy ambaye alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Tanga akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Thobias Mwilapwa ambapo alikwenda Kata ya Kirare kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya bweni hilo na zahanati ya mapojoni alipofika kwenye eneo hilo la ujenzi huo alichanganya mchanga na sarauji na baadae kuchapia ukutani.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali wa kilomita kumi na tano kufuata huduma ya elimu jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ujenzi huo Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga alisema atashirikiana na wananchi kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili zinapatia ufumbuzi. Alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi haraka na kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga jana mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata ya Kirare (CCM) Mwagilo 
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katika akishiriki ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo anayefurahia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.

Introducing "Hali Yangu" Official Audio by Lameck Ditto


MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 7,2019

SERIKALI KUTUMIA SH.TRILIONI 1.3 KWA AJILI YA MIRADI YA MAJI MIJI 28 NCHI NZIMA-PROF. MKUMBO

$
0
0
SERIKALI inatarajia kutumia Shilingi Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28 nchi nzima ili kukabiliana na tatizo la maji. 

Hayo yamebaimnishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo alipofanya ziara katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo.

Profesa Mkumbo alifanya ziara katika mamlaka hiyo kwa ajili ya kujionea utendaji wa kazi zao na zaidi kuona changamoto zinazowakabili watumishi hao na mamlaka husika na namna ya kuzitafutia ufumbuzi. Profesa Mkumbo alisema katika fedha hizo zaidi ya Shilingi Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.

Alisema katika Miji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Shilingi Bilioni 22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na Handeni BILIONI 112.5(HTM). “Matarajio ya Serikali ni kuhakikisha inapunguza kwa kiasi kikubwa kero ya maji vijijini na mijini na kufikia malengo yaliyojiwekea hadi kufikia mwaka huo wa 2025”Alisema Profesa Mkumbo.

Aidha lisema mchakato wa miradi hiyo mikakati umekwisha anza kwa hatua za awali ya usanifu na kupata Mtaalamu mshauri kwa ajili ya miradi hiyo katika Miji ambayo imebainishwa kunufaika na fedha hizo kwa nchi nzima. Alisema hadi kufikia juni mwaka huu miradi hiyo itakuwa imekwisha dizainiwa na mwezi Sept wakandarasi watatkiwa kuwa katika maeneo ya kazi katika miji hiyo 28 kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwataka makandarasi kuhakikisha wanafanyakazi kwa uwadilifu na watambue Serikali haitomzulumu mkandarasi yoyote na fedha zao zitalipwa bila ya mashaka yoyote. “Tunajua madai ya makandarasi wengi nchi nzima lakini tutawalipa waondoe shaka koila mwezi tulipa shilingi Bilioni 8-12 hivyo tutwalipa tu”Alisema.

Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema changamoto kubwa kwa sasa mkoani hapa ni namna ya kuongeza huduma ya taka ndani ya Jiji.“Mbali na fedha zilizoainishwa na Katibu Mkuu lakini tunatarajia kupokea zaidi ya shilingi bilioni 400 kwa ajili ya miradi ya maji taka,kubadilisha miundombinu ya mabomba,ujenzi wa matank”Alisema Mhandisi Hilly. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo kulia akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA RAIS DK.MAGUFULI

$
0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii(SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam.

Taarifa ya NSSF kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Januari 6,2019 imesema Mfuko unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.

Imesema madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. Meneja Kiongozi wa Matekelezo (Chief Manager Compliance and Data Management ) Cosmas Sasi amesema NSSF inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati. Kwa upande wa mafao ya uzeeni takribani Sh. bilioni 5 zimekuwa zinalipwa kila mwezi kwa wastaafu wetu kuanzia julai 2018.Wakati kwa pensheni ya Desemba,2018 Sh. Bilioni 4.83 kimeshalipwa kwa wastaafu 18,631 walikuwepo kwenye daftari la wastaafu.

Kwa upande wa malimbikizo ya mafao hadi kufikia julai 2018 jumla ya Sh. bilioni 108 zilikuwa zinadaiwa kwenye Shirika, ambapo kiasi cha Sh. bilioni 85 kimelipwa kwa wanachama waliokuwa na madai mbali mbali baada ya uhakiki kukamilika, kiasi kilichobaki cha sh. bilioni 23 kitalipwa baada ya uhakiki unaondelea kukamilika.

Wakati huo huo Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa UmaLulu Mengele amesema Mfuko ulianza mchakato wa kuhakiki wastaafu wake kuanzia Desemba 1, 2018 na bado unaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara ."Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF.
Meneja Kiongozi wa Matekelezo ,Cosmas Sasi Kutoka Shirika NSSF,akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar kuhusu namna ambavyo NSSF imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli aliyoyatoa katika mkutano kati ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA), watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Chama cha waajiri uliofanyika Desemba 28, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam.


Sasi alisema kuwa NSSF ilianza mchakato wa kuhakiki wastaafu wake kuanzia Desemba 1, 2018 na bado unaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara ."Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF",alisema.Pichani kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma,Lulu Mengele
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma,Lulu Mengele akizunguma na Waandishi wa habari (hawapo pichani) jana jijini Dar akifafanua kuhusu uhakiki wa Wananchama wao,Lulu alisema kuwa Mfuko wa NSSF unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.

"Madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake. kwa hiyo NSSF kwa sasa inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati,",alisema Lulu.Pichani kushoto ni 
Meneja Kiongozi wa Matekelezo ,Cosmas Sasi Kutoka Shirika NSSF.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MICHUZI TV: TAASISI YA IMETOSHA YAJITOLEA KUSOMESHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)

DKT. NDUGULILE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WAKANDARASI UTEKELEZAJI MIRAD

Mkazi wa Zanzibar aondoka na 15m/ -za Tigo Jigiftishe

$
0
0
Mkazi wa Unguja kisiwani Zanzibar Abdulrazak Abdallah, ameibuka mshindi wa zawadi ya shilingi 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe.

Abdulrazak ni mmoja kati ya washindi wakubwa watatu wa promosheni ya Tigo Jigiftishe. Wengine ni Emma Kauka mkazi wa Dar es Salaam aliyejishindia shilingi milioni 25 na Sadiki Kilipamwambu mkazi wa Songea alijishindia shilingili milioni 50.

Akipokea zawadi yake kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratius David, mshindi huyo alisema zawadi hiyo ya fedha imekuja wakati muafaka kutokana na kuwa anakabiliwa na shida ambazo zinahitaji fedha ili kuweza kuzitatua.“Hii kwangu ni zawadi ya kipekee ambayo Mungu amenipatia kupitia Tigo. Nitatumia sehemu ya fedha kukarabati nyumba ninayoishi ambayo ni kama gofu ili iweze kuwa nyumba kama zilivyo nyumba nyingine. Namshukuru Mungu na Tigo kwa zawadi hii,” alisema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kwa kanda ya Pwani Deogratias David alisema ni jambo la furaha kuona Promosheni ya Tigo Jigiftishe imekwisha huku ikiwa imeboresha na kubadilisha maisha ya wateja wake.

“Promosheni ya Tigo Jigiftishe imetoa jumla ya shilingi milioni 600 kwa wateja wake. Tunayo furaha kuonna kuwa fedsha hizi zimeweza kuboresha maisha ya wateja wetu,” alisema.Promosheni ya Tigo Jigiftishe ililenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu na mwaka mpya.

Kupitia promosheni hiyo, wateja kumi wa Tigo waliweza kujishindia shilingi milioni moja kila siku, huku mshindi mmoja wa wiki akijishindia shilingi milioni 10 huku washindi wakubwa wakijishindia shilingi milioni 15, milioni 25 na milioni 50.
Mshindi wa Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah  (wa tatu kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Sh 15m/- kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Deogratias David (wa pili kulia) huku akishangiliwa na baadhi ya wafanyakazi wa Tigo na mtangazaji wa Clouds FM Meena Ally (kushoto) katika hafla iliyofanyika katika viwanja vya Jang’ombe kisiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki.
Mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni iliyomalizika ya Tigo Jigiftishe kutoka Zanzibar Abdulrazak Abdallah, akimuonyesha mtangazaji wa Radio Clouds FM Meena Ally hali ya nyumba anayoishi. Mshindi huyo alisema atatumia sehemu ya fedha alizoshinda kukarabati nyumba hiyo.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar waliofika katika viwanja vya Jang’ombe kushuhudia mshindi wa zawadi ya Sh 15m/- katika Promosheni ya Tigo Jigiftishe Abdulrazak Abdallah kutoka visiwani humo akikabidhiwa zawadi yake katika hafla iliyofanyikaa mwishoni mwa wiki.

NAIBU WAZIRI,KANYASU ATEMBELEA IHUMWA MJI WA SERIKALI KUKAGUA UJENZI JENGO LA MALIASILI NA UTALII

$
0
0

NA.LUSUNGU HELELA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.

Ameyabainisha hayo wakati alipotembelea eneo hilo kwa ajili ya kukagua maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi wa jengo hilo. “Kazi hii inafanywa kwa uhodari mkubwa, nawapongeza kwa maendeleo yaliyofikiwa na ninaamini kwamba Jengo hili litakamilika ndani ya muda uliopangwa’’

Aidha, Mhe. Kanyasu wakati alipotembelea eneo hilo ameweza kukutana na timu ya Wakadiliaji Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao kwa pamoja na Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo.

Kwa upande wake, Mkandarasi wa SUMA JKT, Luteni Mturi amemueleza Naibu waziri huyo kuwa wanatarajia kumaliza ndani ya muda uliopangwa kwa vile kwa sasa kuna upatikanaji wa uhakika wa vifaa vya ujenzi ikiwematofali ya kutosha na yenye ubora wa hali ya juu pamoja na wafanyakazi wa kutosha

‘’Kesho tunategemea kuanza kumwaga zege katika kipande cha kwanza ambapo hadi kesho kutwa tutamalizia kipande cha pili’ ameeleza Mturi. Hata hivyo, Mkandarasi huyo ameeleza changamoto ya utayari wa wafanyakazi kufanya kazi usiku kuwa wengi wao wamekuwa hawapo tayari kufanya kazi muda huo licha ya kuwa awali SUMA JKT ilipanga kujenga jengo hilo mchana na usiku.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akiangalia hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojengwa ndani ya mji wa Serikali wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo hilo katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkandarasi wa Suma JKT, Luteni Mturi wakati alipotembelea kwa ajili ya kukagua maendeleo ya jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma., kushoto ni Fundi Sanifu Ujenzi, Agastoni Kayugwa ambaye ni Muwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa pamoja wameeleza kuwa wanaridhishwa na spidi inayoendelea katika ujenzi wa jengo hilo. 
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya jengo jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii linalojenga katika mji wa serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.


SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA BILIONI 2.9 KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

$
0
0
Na Nyamagory Omary wa PMO
Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House). 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo  Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro. 
Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Agriculture  Group Ltd, na SUGECO. 
Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni  kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo  kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (greenhouse). 
“Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”alisisitiza Mavunde. 
Aidha, Amewataka vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua na changamoto za ajira na kuelezea umuhimu wa kilimo katika kuongeza pato la Taifa na kuchangia katika uchumi wa viwanda nchini.

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na mtaalamu wa masuala ya kilimo cha kisasa kwa  kutumia mabwawa ya samaki (Acquculte) alipotembelea kukagua mradi huo, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Ofisi hiyo Mhe Stella Ikupa
 Manaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia kiazilishe katika moja ya banda la maonesho la vijana walioshiriki mafunzo ya Kilimo cha kisasa cha kitalu nyumba. Katikati ni Mhe.Stella Ikupa anayeshughulikia Wenye Ulemavu na Kushoto ni Mhe.Anthony Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira).

 Baadhi ya viongoizi wakishuhudia Naibu Waziri Ofisi ya Waziri (Wenye Ulemavu) Mhe.Stella Ikupa akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Muongozo wa masuala ya kilimo cha Kitalu Nyumba wakati wa warsha hiyo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akikagua biskuti zilizotengenezwa kwa kutumia nanasi ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotengenezwa na vijana waliopewa mafunzo na SUGECO wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario .
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akiangalia mapapai yaliyolimwa kwa njia ya kisasa katika mashamba ya SUGECO katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro.

ALEX KAJUMULO'S 2019 PLANS and VISION

$
0
0
By Alex Kajumulo

I just finished a meeting with the owner of African Lions FCwho plays in the Tanzania Premier League, Mr  Rahim Kangezi

(pictured left) I will be working with him to develop youth soccer players in Tanzania who want to go professional and want to play outside of Tanzania. This month I will be traveling to Tanzania to finalize the deal between Pass Academy and African Lions and the Tanzania Police FC


When I’m in Tanzania I will go to Zanzibar to finalize the contract with Jangombe FC and have a discussion with Zanzibar Football Federation, plus I will come back to Dar Es Salaam to have a meeting with the Young Africans and Tanzania Football Federation (TFF)

I will conduct two coaching sessions for the coaches who want to pursue their career in youth academy development for boys and girls and they will be able to watch the way I conduct my sessions with the African Lions
I will visit and conduct one of the coaching classes in Bukoba the region where I’m from and another session in Muleba the town where I was born. When I’m in my hometown I will visit two elementary schools that I went to when I was a little kid. This year I decided to go again to Tanzania to develop the sport because the current President of Tanzania made that happen for me. Every club in Tanzania is welcome to join.

I will have a discussion about high school and professional coaches and about team/club owners. We will discuss soccer development plus the business behind soccer and how to develop the players to get into US colleges and how to get them into US Major League Soccer. There’s been A LOT OF RUMORS in Tanzania, people are struggling to know which team I support between the Young Africans and Simba. In reality I support the sport, I love the game but if I had to pick a team I would pick the Young Africans. 
The reason that I pick Young Africans is this, Simba used to be Sunderland and Sunderland was ran by a British colony when Tanzania was colonized. The Tanzanians struggled very hard to put together a team to compete against the Sunderlands. They started the team from scratch, and if you remember I helped the Young Africans before, I paid the money for the team to go to the Eastern Central Championships in Uganda when the Young Africans became the Champion and it didn’t stop me from supporting another club in the country. My job is to try to keep that vision going.  
Every Tanzanian knows I love my country and Young Africans represents the struggle for Tanzania. There’s nothing wrong with either team and I have nothing against either one of them. I love the sport, it doesn’t matter if it’s Sunderland or Simbas. Soccer is a sport for the people, the club is for the people. 
This time I want to push the Young Africans to help them to become one of the best clubs in Africa. All Africans know I have done this before with Accra Hearts of Oaks SC, we won all of the Major African Cups and the team was placed number 8 in the world. This time I want to see one of the teams from my country go to the top. Stay tuned for my schedule, it will be out soon. 
I CAN’T FORGET TO MENTION THAT WHEN I’M IN DAR ES SALAAM I WILL BE MEETING WITH SONGBIRD SAIDA KAROLI ABOUT HER TRAVELING TO WASHINGTON STATE FOR THE COFFEE FARMERS MUSICAL FESTIVAL. The date to be announced soon!!

MICHUZI TV: WASTARA afichua siri nzito, kutapeliwa mamilioni ya pesa...

MICHUZI TV: TAASISI YA IMETOSHA YAJITOLEA KUSOMESHA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO)

"MUSWADA WA SHERIA WA VYAMA VYA SIASA UTASAIDIA KUONDOA UKILITIMBA NA UMUNGU MTU KATIKA VYAMA VYA SIASA"

Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images