Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live

INTRODUCING "HUSTLER" BY HAROON MANYA FT ABBAS PIRA


MICHUZI TV: MABONDIA WOTE WAKUBWA TANZANIA NIMEWAPIGA,CHEKA ALIZIMA PALE ULINGONI - DULLA MBABE

Vodacom waendelea kugawa Tuzo Points

$
0
0
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania wakiwazawadia wateja wa mtandao huo Tuzo Points pamoja na zawadi nyingine katika kampeni ya 'Baki Mule Mule Utuzwe na Tuzo Points' iliyofanyika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza. 
Wateja wa Vodacom wanaweza kupata Tuzo Points pale wanaponunua salio au kufanya miamala kupitia M-Pesa . Pointi hizo zinaweza kubadilishwa kuwa fedha, salio au bando. Katika msimu huu wa sikukuu, Vodacom Tanzania inawazawadia wateja wao pointi za Tuzo zenye thamani ya shilling Bilioni moja.

MAPINDUZI YA KIJESHI YAHOFIWA KUTEKELEZWA NCHINI GABON

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii

JESHI la wananchi nchini Gabon limeshikilia kituo cha redio cha taifa nchini humo na kutangaza kutoridhishwa na hali ya kiafya na Rais wa nchi hiyo Ali Bongo Ondimba anayetibiwa nchini Morocco akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi huku amri ya kutotoka nje ikitolewa. Luteni kanali Ondo Obiang kiongozi wa kundi la harakati za ulinzi na usalama wa vikosi vya Gabon amesema kuwa ujumbe wa mwaka mpya uliotolewa na Rais Bongo umezidi kuwapa nguvu ya kutoamini uwezo wake katika kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake ya kiuongozi.

Katika hotuba yake ya kutoa salamu za mwaka mpya Rais Bongo alisema kuwa hali yake si ya kuridhisha ila anaendelea kupata matibabu na kupata afueni. Shirika la AFP limesema kuwa milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa nchi hiyo Libreville na karibu na kituo hicho cha redio ya taifa tangu majira ya saa 10 alfajiri  huku ikisemekana mapinduzi hayo yanatekelezwa na kikundi kidogo cha askari.

Bongo (59) alilazwa nchini Saud Arabia Oktoba 28 mwaka jana akipatiwa matibabu mara baada ya kupata kiharusi na baadaye Novemba  kwenda nchini Moroco ambako bado anaendelea na matibabu zaidi. Ali Bongo Ondimba alizaliwa Februari 9, 1959 ambapo alimrithi baba yake Omar Bongo aliyetawala tangu mwaka 1967 hadi kifo chake mwaka 2009 na katika utawala wa baba yake Ali Bongo aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Waziri wa mambo ya nje kwa miaka kadhaa.

Inasemekana kuwa utawala wa muda mrefu wa familia hiyo ndio unapelekea mapinduzi haya na taarifa kuhusiana na hali hiyo itatolewa na msemaji wa Rais muda mfupi ujao.

MICHUZI TV: WASTARA afichua siri nzito,kutapeliwa mamilioni ya pesa.

SIMANJIRO WAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amezindua utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwataka wafanyabiashara wakubwa na wakati kutojihusisha na zoezi hilo.  Magessa aliyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, wakati wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.

Magessa alisema wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye mfumo wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) hawapaswi kupatiwa vitambulisho hivyo. "Serikali ipo pamoja nanyi wafanyabiashara wadogo, ndiyo sababu Rais John Magufuli akawatambua na kuagiza vitambulisho vyenu vitengenezwe," alisema Magessa. 

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi alisema wafanyabiashara wanapaswa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ili kufanikisha maendeleo. "Kupitia kodi ndiyo serikali inafanikisha maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga vyumba vya madarasa yahoo shule za sekondari na msingi ambavyo watoto wetu watasoma," alisema  Myenzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred Myenzi akizungumzia umuhimu wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Zuwena Omary akielezea namna ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Tumaini Magessa akielezea sifa za wafanyabiashara wadogo wanaopaswa kupata vitambulisho hivyo vilivyotolewa na Rais John Magufuli. 
Wafanyabiashara wadogo wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wakifuatilia kikao cha Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Tumaini Magessa wakati wa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo wilayani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. NDUGULILE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA WAKANDARASI UTEKELEZAJI MIRADI WIZARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kutekeleza  miradi inayohusu Wizara  bali kutumia mtindo wa 'Force Account' yani mafundi wa kawaida katika kutekeleza miradi hiyo.

Ametoa agizo hilo mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na  kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale katika ziara yake ya kikazi mkoani humo. Naibu Waziri huyo amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya madarasa na ukuta wa Chuo cha Waganga mkoani humo ambao ungegharimu zaidi ya Shillingi 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Force Account' zingejenga zaidi madarasa hayo na ukuta.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi za Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na yeye kama Naibu Waziri ataisimamia kwa karibu Miradi hiyo. Amesisitiza kuwa ujenzi wote wa miradi utakaohusu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii utazingatia utaratibu wa 'Force Account' na kibali cha wakandarasi kitatolewa na Mawaziri pekee na sio vinginevyo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na baadhi ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa  Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa  ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.
 Baadhi ya ya wakufunzi, wafanyakazi na wananfunzi wa wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (hayupo pichani) wakati wa  ziara ya Naibu waziri huyo chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali.

 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akikagua mradi wa ujenzi wa chumba cha pampu ya maji katika Chuo cha maendeleo ya Jamii Mlale unaogharinu Shillingi Millioni 3 unaosimamiwa na Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi katika ziara yake mkoani Ruvuma kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale mkoani Ruvuma wakati wa  ziara yake chuoni hapo kujionea Ujenzi na Ukaratabi wa miundombinu mbalimbali  kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema na Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Luciana Mvula.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Amb. Nassor Present Letters of Credence to the President of Palestine

$
0
0
The Ambassador of Tanzania to Egypt, H.E Issa Suleiman Nassor (R) who is also accredited to the State of Palestine  presents his letters of credence to the President of Palestine, H.E Mahmoud Abbas in Cairo Yesterday. H.E  Nassor presented the letters of Credence when President Abbas was in a working visit in Egypt.


MICHUZI TV: WASTARA ALIA NA WANAOMUITA TAPELI,AKANA KUFANYA UKAHABA

MICHUZI TV:SAID FELLA AWAJENGEA KITUO CHA POLISI KILUNGULE, APEWA MILIONI 324 ZA MAENDELEO NA RAIS MAGUFULI ALIMPA MIL 300/-

CCM IRINGA WAPATA MWENYEKITI MPYA

$
0
0
NA DENIS MLOWE, IRINGA

CHAMA cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, kimemchagua mwadhili wa chuo kikuu cha Ruaha mkoani hapa, Dk. Abel Nyamahanga kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho kuchukua nafasi ya mwenyekiti aliyejiuzulu ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila.

Wajumbe 597 kati ya 631 waliohudhuria wa Mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa wametumia haki yao ya kidemokrasia kwa kufanya uchaguzi wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho chini ya msimamizi wa uchaguzi aliyekuwa waziri mkuu awamu ya nne, Mizengo Pinda.

Mkutano huo maalum uliohudhuriwa na wadau mbalimbali mkoani hapa ulikuwa wa upinzani mkali ambapo kutokana na wajumbe waliozidi akidi ya matakwa ya mkutano wa CCM mkoa kwa mujibu wa maelekezo ya kanuni za uchaguzi wa CCM wajumbe wote ni 631.

Wajumbe hao walitakiwa kuwapigia kura wanachama watatu ambao ni Vitusi Mushi, Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga ambao majina yao yalirudishwa kutoka kamati kuu ya CCM taifa kwa lengo la kupigiwa kura. Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kichangani, wajumbe walilazimika kurudia uchaguzi kwa awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza mshindi kutovuka nusu ya kura zilizopigwa kutokana na upinzani mkali.

Baada ya matokeo kutoka ndipo wa majina mawili ya Amani Mwamwindi na Dk. Abel Nyamahanga yalipigiwa kura kutokana na wajumbe 548 waliobaki baada yaw engine kutoka ukumbini na kuweza kupata mwenyekiti mpya baada ya Vitus Mushi kupata kura chache zaidi ambazo hazikukidhi kanuni za uchaguzi wa CCM. 
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa Dk Abel Nyamahanga akiwa na wagombea wa nafasi hiyo. kushoto kwake ni Aman Mwamwindi na kulia kwake ni Vitus Mushi.

 Baadhi ya wajumbe wa mkutano maalum wa uchaguzi wa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa wakiwa ukumbini kabla ya zoezi la kupiga kura
 Msimamizi wa uchaguzi wa mwenyekit wa ccm mkoa wa Iringa Mizengo Pinda akizungumza kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza katika uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Iringa uliofanyika katika ukumbi wa Kichangani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

BENKI YA NMB YATUNUKIWA TUZO YA KUWA MSHIRIKA BORA KATIKA MASUALA YA KIFEDHA AFRIKA KWA MWAKA 2018

$
0
0
NMB Bank PLC imeshinda tuzo na kutajwa kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha Afrika kwa benki zinazofanya kazi na Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC) la Benki ya Dunia. Hafla ya kukabidhiwa Tuzo hiyo ilifanyika Jijini Dar es Salaam. 

Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa IFC Afrika Mashariki (IFC Resident for East Africa) Bw. Dan Kasirye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna alisema "Tumefurahishwa kwa namna ya pekee kupokea tuzo hii ya Kimataifa kutokana na mafanikio yetu; ni ushuhuda wa uwekezaji wetu katika teknolojia huku tukipanua mtandao wa matawi yetu na kuimarisha uwezo wetu wa kutoa huduma nzuri na za kisasa kwa wateja wetu." 

Aidha, Bi. Zaipuna aliongeza kuwa “katika miaka minne iliyopita, tumetoa huduma na bidhaa za kisasa na kuendelea kukidhi mahitaji ya wateja wetu nchini kote na kuziba pengo lililoachwa na benki nyingine katika soko. Kwa sasa tuna mtandao mpana zaidi nchini wenye matawi 228, ATM zaidi ya 800 na NMB Wakala zaidi ya 6,000 na hivyo kufanya upatikanaji wa huduma zetu nchini kuwa kwa asilimia 100%”. 

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa IFC kwa Afrika Mashariki Bw. Dan Kasirye alisema “NMB Bank imeshinda tuzo hii kutokana na uwezo wake wa kutoa huduma mseto za kifedha zinazomfikia mtumiaji wa chini kabisa. NMB Bank ni mshindi wa ushirikishwaji wa kifedha barani Afrika iking’ara zaidi kuliko benki nyingine zote ambazo zimeshafanya kazi na IFC. NMB imeonyesha uwezo wake katika kuwashirikisha wanawake, biashara ndogo, kubwa na za kati, pamoja na biashara ya kilimo Tanzania.” 

TUZO NYINGINE AMBAZO BENKI YA NMB IMESHINDA 
Katika kipindi cha miezi 12, Benki ya NMB imeshinda tuzo nyingine mbili za kimataifa ambazo ni; Benki Bora Tanzania kutoka Euromoney Awards for Excellence; Benki Bora ya Wateja Wadogo na Benki Bora ya Biashara Tanzania kutoka Banker East Africa Magazine. Pia benki ya NMB imeshinda tuzo mbalimbali za ndani kama vile; tuzo ya Afya na Usalama Kazini (OSHA) 2018 na tuzo ya utoaji wa taarifa bora za kifedha 2018 kutoka Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu (NBAA). 

Kaimu Mkurugenzi wa NMB Bank – Ruth Zaipuna akiwa na tuzo kutoka Shirika la Kimataifa la Fedha ambalo ni tawi la Benki ya Dunia ((IFC) iliyoitaja benki hiyo kuwa Mshirika Bora katika Masuala ya Kifedha kwa nchi za Afrika miongoni mwa benki zinazofanya kazi na shirika hilo.

TUCTA YAWATAKA WANASIASA KUTOWATUMIA KUJIPATIA UMAARUFU

$
0
0
*Waziri Mkuu apokea maandamano ya wafanyakazi wakimpongeza Rais 
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeyataka makundi ya wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa kuzungumzia masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu wanajitosheleza.

 Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano pamoja na rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya ajira zao.

Hayo yamesemwa leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.

Watumishi wa taasisi mbalimbali leo wameandamana jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Squarekwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kufuta kikotoo kipya cha mafao ya wafanyakazi kilichopendekezwa katika kanuni za sheria ya Mifuko ya jamii.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia watumishi katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza kwenye maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.
 Makamu wa Rais TUCTA Qambos Sule, akizungumza mbele ya watumishi katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwapungia watumishi katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019.
 Makatibu Wakuu wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati akizungumza na watumishi katika maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi, yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma, Januari 7, 2019. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


IGP Simon Sirro akutana na kufanya mazungumzo na Brigedia Jenerali, Itai Veruv wa Israel

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipokea zawadi kutoka kwa Brigedia Jenerali Itai Veruv wa Israel baada ya kukutana na kufanya mazungumzo, Makao makuu ya Jeshi la Polisi ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika masuala ya usalama. picha na jeshi la polisi.
Brigedia Jenerali Itai Veruv (katikati) akizungumza na Balozi wa Israel nchini Noah Gal Gendler kutoka kushoto Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, Walipofika makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mazungumzo. picha na jeshi la polisi

LUGOLA: SERIKALI ITAWASHUGHULIKIA VIONGOZI WA DINI WALIOJIPENYEZA KUANZISHA MAKANISA NA MISIKITI KWA LENGO LA KUFANYA UCHOCHEZI, KUVURUGA AMANI NCHINI

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Ngara.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema baadhi ya viongozi wa dini nchini wamejipenyeza na kuanzisha makanisa na misikiti kwa lengo la kuanzisha vichaka vya kujificha ili tujue ni watu wa Mungu kumbe wanataka kufanya uchochezi na kuvuruga amani nchini. 
Lugola amesema Serikali ya Rais Dkt. John Magufuli haitawavumilia wale wote walioanzisha taasisi hizo kwa lengo lao binafsi na itahakikisha inawashughulikia ipasavyo bila kuwaonea huruma.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara, leo, Lugola amesema makanisa na misikiti ambayo imesajiliwa na Wizara yake hatakubali kuona viongozi hao ambao wanajifanya kuwa na watu wa Mungu kumbe wanamalengo hayo binafsi.
“Makanisa na miskiti itakayobainika ina malengo hayo, sitaona haya kuifutia usajili, na pia nawataka viongozi wa dini endapo migogoro inaibuka hakikisheni  mnaitatua wenyewe kwa amani,” alisema Lugola.
Lugola ameongeza kuwa, Serikali inaheshimu imani ya dini na pia viongozi wao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya nchi kutokakana na maombi pamoja na kuwaongoza waumini wao vizuri, lakini pia wapo baadhi ya viongozi hao wa dini, wanaingiza masuala ya siasa makanisani na misikitini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Mji wa Ngara, Mkoani Kagera (hawapo pichani), katika Mkutano wa hadhara uliofanyika mjini humo, leo. Katika mkutano huo, Lugola amesema baadhi ya viongozi wa dini nchini wamejipenyeza na kuanzisha makanisa na misikiti kwa lengo la kuanzisha vichaka vya kujificha ili tujue ni watu wa Mungu kumbe wanataka kufanya uchochezi na kuvuruga amani nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Askari na Watumishi wa Wizara yake wa Wilaya ya Ngara, Mkoani Kagera (hawapo pichani), katika kikao hicho, Lugola aliwataka watumishi hao wafanye kazi kwa kujituma bila kuchukua rushwa. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Luten Kanali Michael Mtenjele. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi.
Baadhi ya Askari na Watumishi wa Mjini Ngara, Mkoani Kagera wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (hayupo pichani) wakati alipokua anajibu maswali ya watumishi hao kuhusu masuala mbalimbali ya Wizara yake, katika kikao kilichofanyika mjini humo, leo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


ZOEZI LA UGAWAJI WA VITAMBULISHO KWA WAJASIRIAMALI LAMALIZIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MKOA wa Dar es Salaam umemaliza zoezi la utoaji wa vitambulisho kwa wajasriamali na kuwa kinara kwa kutimiza agizo la Rais  Mh Dkt. John  Magufuli la kutoa vitambulisho hivyo bure kwa wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kwa nia ya kurasimisha sekta hiyo Muhimu katika ujenzi wa Taifa.

Zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho 25,000 kwa awamu ya kwanza limekamilika  tarehe Januari 3 mwaka huu na kuufanya Mkoa huu kuwa Mkoa wa kwanza kitaifa katika kukamilisha zoezi la ugawaji wa vitambulisho hivyo. Baada ya kukamilisha zoezi hilo kwa haraka jijini Dar es Salaam tayari wamepokea  vitambulisho vingine 25,000 kwa ajili ya kuendelea kwa ugawaji wa vitambulisho hivyo kwa awamu ya pili.

Akizungumza katika makabidhiano ya vitambulisho hivyo kwa wakuu wa wilaya wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemshukuru Rais Magufuli  kwa kukubali ombi la nyongeza ya vitambulisho vingine 25,000 kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salam na kueleza kuwa ugawaji wa vitambulisho hivyo utaanza ambavyo vitaanza kugaiwa katika wilaya zote kuanzi kesho.

 Makonda amesisitiza ufuatajwi wa sheria na kanuni katika ugawaji wa vitambulisho hivyo na kusisitiza kuwa vitambulisho hivyo haviuzwi bali kiasi cha shilingi  20,000 inayotolewa na wafanyabiashara wadogo ni mchango wa gharama za utengenezwaji  na si vinginevyo, na amekemea vikali ulanguzi wowote ambao unaweza kutokea katika zoezi hili la ugawaji.

Vitambulisho hivyo vimekabidhiwa kwa wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam na kupokelewa Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kwa niaba yao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (kushoto) akimkabidhi kasha la vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo Mkuu wa Wilaya wa Temeke Felix Lyaniva (kushoto) katikati ni katibu tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abukar Kunenge.

MICHUZI TV: AGIZO LA RAIS MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA NA NSSF

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO GHOROFA MBILI LA KITUO CHA MAMA NA MTOTO KMKM KIBWENI ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanaotoa huduma katika sekta ya afya kutoa Huduma bora.Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo cha Mama na Mtoto katika hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya maadhimisho ya shamrashamra za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais ametoa rai kwa Wataalamu wa Afya nchini kutambua kuwa wanatakiwa kutumia utaalamu wao katika kuokoa maisha ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi kwa ajili ya kujenga Taifa lenye kizazi imara. “Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika sekta ya afya nchini” alisema Makamu wa Rais.

Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto ni la ghorofa mbili na limegharimu jumla ya shilingi 3, 648,400,000/- na kuzingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Huduma zitakazopatikana kwenye jengo hilo la ghorofa mbili ni Huduma ya Mama na Mtoto, Wodi ya Wazazi na Watoto,Huduma ya Upasuaji kwa Mama Wajawazito, Huduma ya Vipimo X Ray, Utra Sound na Maabara, Ofisi za huduma za madaktari, wauguzi na wahudumu wengineo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akipiga makofi ya pongezi mara baada ya kukata utepe kuashiri uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar wengine pichani ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Haji Omar Kheir (kulia) na kushoto ni Mkuu wa KMKM Komodoo Hassan Mussa Mzee
:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Sehemu ya waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alikuwa mgeni rasmi.
 Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni, wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini Magharibi, Unguja ambalo limefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikiwa sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAAGIZO YA SPIKA WA BUNGE KWA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

$
0
0
*Amtaka kumthibitishia maneno yake kuwa Bunge nichombo dhaifu
*Amtaka ajitafakari ...asema kauli zake nje ya nchi zimemsikitisha 

Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

HATIMAYE Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa maagizo ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad kufika katika Kamati ya Maadili ya Bunge ifikapo Januari 21 mwaka huu na iwapo atashindwa kufika atapelekwa akiwa kwenye pingu.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Mjini Dodoma wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini alipokuwa akielezea namna ambavyo Prof.Assad ametoa kauli ambayo haikustahili kuitoa kwa Bunge.

Siku za karibuni Prof.Assad wakati anahojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ambapo aliulizwa kuhusu jitihada ambazo ofisi ya CAG inafanya kila mwaka kwa kukagua na kutoa ripoti ambazo zinaoonesha kuna ubadhirifu wa fedha ambapo alijibu kazi yake ni kufanya ukaguzi na kukabidhi ripoti kwa Bunge, hivyo Bunge ndilo dhaifu kwa kushindwa kufanyia kazi ripoti hizo.

Hivyo kauli hiyo ya Profesa Assad kudai Bunge ni dhaifu ndiyo iliyosababisha Spika wa Bunge leo kutangaza kumuita Kamati ya Maadili ili akahojiwe na kamati hiyo na iwapo atakaidi atapelekwa kwa pingu na hiyo itatosha kuthibitisha Bunge si dhaifu.

"Bunge tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli ya Profesa Assad.Anataka kuonesha kuwa ripoti ambazo anazitoa kwa Bunge hazifanyiwi kazi au zikifika Bungeni basi hakuna kinachoendelea kwa kuwekwa pembeni bila kufanyiwa kazi.Hii si kweli kabisa,"amesema Spika Ndugai na kuongeza "CAG na maofisa wake wamekuwa wakiingia kwenye Kamati ya Kudumu ua Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma.

"Ripoti za CAG zikifika kwenye kamati hizo ambazo kimsingi zinaongozwa na upinzani , maofisa wa ofisi ya CAG wanakuwepo kueleza mapungufu waliyobaini wakati wa ukaguzi na hatua ambazo zinastahili kuchukuliwa.Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani kuna jitihada kubwa zimefanyika na zinaendelea kufanyika katika kudhibiti matumizi ya fedha za umma, kuna mabadiliko makubwa yamefanyika kwa ushauri wa CAG,"amesema.

Pamoja na hayo Spika Bunge amehoji ni hatua gani ambazo Profesa Assad anataka zichukuliwe huku akitumia nafasi hiyo kuwataka maofisa wa Serikali kuacha kutoa kauli za kulidhalilisha na kwamba Bunge linaweza kukosolewa lakini si kwa kauli za dharau.Pia amesema si uungwana kuisema nchi yako vibaya ukiwa nje ya nchi huku akitumia nafasi hiyo kumtaka Profesa Assad kujitathimini kwani Bunge haliko tayari kufanya kazi na mtu ambaye anaona chombo hicho ni dhaifu.

"Kwa mujibu wa kifungu cha 4, kifungu kidogo cha kwanza A, cha nyongeza ya nane ya kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016 suala hili nalipeleka katika kamati ya haki , maadili na madaraka ya Bunge ili walifanyie kazi na kunishauri na kwa maana hiyo kulishauri Bunge.

"Hivyo Profesa Assad anatakiwa kujitokeza Januari 21,2018 aende kujieleza kwenye kamati hiyo ili akathibitishe maelezo yake ambayo ameyatoa mahakamani.Na mnafahamu pamoja hatuna polisi, hatuna nini ila tunaweza kumleta mtu kwa pingu kwani tunataka kumthibitishia sisi sio dhaifu,"amesema Spika Ndugai.
 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb), aalipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma   leo kuhusu kauli za kudhalilisha Bunge zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),  Profesa Mussa Assad na Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee. 
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Mb), akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu kauli za kudhalilisha Bunge zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),  Profesa Mussa Assad na Mbunge wa Kawe, Mhe. Halima Mdee.

TAASISI YA FLAVIANA MATATA YAMWAGA VIFAA VYA KUJIFUNZIA SHULE YA MSINGI MSINUNE

$
0
0
Leo  muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019 umeanza. Taasisi ya Flaviana Matata ambayo ni walezi wa Shule ya Msingi Msinune imeendelea na utaratibu wake wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima. 
Kwa mwaka 2019, watoto 284 wa Shule ya Msingi Msinune kila mmoja kapata begi la shule, kalamu za wino 50 , kalamu za risasi 50 na vifutio ambavyo vitakidhi mahitaji yao kielimu kwa mwaka huku wazazi wakitimiza mahitaji mengine yaliyobaki. Upande wa walimu taasisi imetoa kalamu, chaki, rejista za masomo na karatasi (reams) kwa ajili ya kudurufu (copy) mitihani na kazi za masomo.
 mpaka mwaka jana Taasisi ya Flaviana Matata imefanikiwa kukamilisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, ofisi za walimu, vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi na mradi wa maji safi katika shule hiyo ya Msingi Msinune.
Kwa mwaka 2019-21 Taasisi hiyo itajikita zaidi kwenye ujenzi wa nyumba za walimu shuleni kutatua changamoto ya makazi ya walimu shuleni hapo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali .  
Mafanikio ya hili yatajenga mazingira rafiki zaidi kwa walimu kufanya kazi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.  Bado tunazidi kuwaasa Watanzania kuendelea kujitolea kwa namna moja au nyingine katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini.
Viewing all 110109 articles
Browse latest View live




Latest Images