Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

DKT.NDUGULILE ATEMBELEA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA,AKAGUA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA BORA KWA WANANCHI

$
0
0

NaWAMJW - SONGEA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya bora kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vifaa vyote vilivyoharibika vinatengenezwa na kuanza kufanya kazi mara moja.Kwa upande mwingine ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanatumia Fedha vizuri katika kufanya maboresho ya majengo ya Hospitali hiyo, ikiwemo kutumia Forced account katika ujenzi huo.

Pia, Dkt. Ndugulile ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha kila mtoa huduma za Afya anaandika muda kwa usahihi aliomuhudumia mgonjwa kuanzia anapopokelewa, anapofanyiwa matibabu mpaka anapoandikiwa dawa jambo litalorahisisha kubaini mtenda kosa endapo mgonjwa atapata tatizo.

Aidha, Serikali imeahidi kuwapa gari la kubebea wagonjwa katika Hospitali hiyo ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika endapo gari hilo litakuwepo ikiwemo vifo vya mama na mtoto.

Mbali Na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza Watoa Huduma za Afya katika Hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiwatia moyo kuwa Serikali inafahamu mchango wao na itaendelea kuboresha mahitaji yao.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua karatasi ya idadi ya wagonjwa waliofika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine akikagua hali ya upatikanaji wa Dawa kwenye chumba cha kuhifadhia Dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine akimjulia hali mtoto aliyepelekwa kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. faustine Ndugulile akikagua miguu bandia katika chumba cha kuhifadhia vifaa mbali mbali vya Hospitali, ikiwa ni ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.


WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI UKARABATI WA JENGO SONGEA

$
0
0
*Ni la wajawazito wanaosubiri kujifungua, limegharimu sh. milioni 129 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.

Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.

Waziri Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019) wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni 129.

“Sijaridhishwa na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara, jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”

Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi inalingana na thamani ya fedha.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati wanatakiwa watibiwe bure.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.

WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA TAARIFA YA KUZUIWA KWA NGUZO ZA UMEME

$
0
0
*Aitisha kikao na viongozi wa maeneo hayo pamoja na Mawaziri husika

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote zinazozalisha nguzo za umeme katika mkoa huo kufika ofisini kwake ili waeleze sababu za kuzuia nguzo hizo zisitoke. 

“Wanieleze kwa nini wanazuia nguzo,Wakati wananchi wanasubiri kuunganishiwa huduma ya nishati ya umeme wao wanazuia nguzo wanasubiri posho, Wanaidai Serikali wakati ni wao ni sehemu ya Serikali Tutakutana ofisini kwangu Januari 7, saa tano kamili asubuhi.”

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni, wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alisema jambo hilo linakwamisha zoezi la usambazaji umeme.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walilalamikia kitendo cha kutofikishiwa huduma ya umeme katika maeneo yao kutokana na kukosekana kwa nguzo ambazo zimezuiwa kwa sababu ya wahusika wanaidai Serikali posho.

Waziri Mkuu alisema viongozi wengine watakaokuwepo kwenye kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, Wenyeviti wa halmashauri hizo zilizozuia nguzo ili wamueleze sababu za kuzuia nguzo hizo.

POLEPOLE ACHARUKA UZINDUZI WA KAMPENI KATA YA MAGOMENI ASEMA WAPINZANI WANABWABWAJA TU

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Humphrey Polepole amefungua Kampeni na kumnadi mgombea Udiwani wa kata ya Magomeni, Shaweji Mkubura, katika Viwanja vya Magomeni Makuti.

Akifungua Kampeni hizo Polepole amewaambia wakazi wa magomeni kuchagua mgombea kutoka CCM kwani Wapinzani wameishiwa sera wanabwabwaja tu mitandaoni na kuisema vibaya Tanzania kwa mataifa Rafiki.

“siku zote Mnyororo huwa unafanana sasa ni aibu kama mtachagua wapinzani ambao wao kazi yao kubwabwaja kila kukicha kuanzia mitandaoni kazi kuisema vibaya serikali yetu aitoshi wamesafiri kwenda nje kutusema vibaya kana kwamba awaoni Maendeleo yanayoletwa na Mwenyekiti wa chama chetu”alisema Polepole

“Mzee mwenye Madevu ametembea nchi za ulaya wa marafiki zetu kuwasihii wasitusadie baada ya ziara hiyo tukasikia nchi kadhaa zinatuchimba mkwara kwa mambo yanayotuhusu wenyewe matokeo yake wakatuambia kama unataka msaada lazima tufuate sera za ushoga jambo ambalo serikali ya CCM Imegomea”.

Alisema Sasa chama cha uliberali ambacho hakieleweki kina Makatibu wawili,Wenyeviti wawili na mlengo wao kila kitu hewala, hivyo wao suala la vijana wa kiume kuvaa madela kwao ni sawa tu hivyo sio watu wakuwachagua.

Polepole alisema kuwa CCM inayoongozwa na Rais Magufuli inamleta kwenu Shaweji kwa wakazi wa kata ya Magomeni waweze kumchagua ifikapo January 19 aweze kuwaongoza wakazi wa magomeni.Alimaliza kwa kusema kuwa Magomeni ndipo waktoka watoto wa Mjini hivyo wakazi wa magonei awatakiwi kukosea kwa kupiga kura kwa wapinzani bali wanatakiwa kupeleka kura zote kwa shaweji.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole, akimnadi Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Magomeni Ndugu Shaweji Mkumbura wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Jijini Dar es Salaam leo.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Magomeni kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Ndugu Shaweji Mkumbura akiwa amepiga magoti kuomba kura kwa wakazi wa Magomei waliofika katika uzinduzi wa kampeni zake zilizofanyika katika Viwanja vya Magomeni Makuti Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole, akihutubia wakazi wa Kata ya Magomeni eneo la Magomeni Makuti wakati akimuombea kura Mgombea wa CCM aweze kuchaguliwa kuwa Diwani katika wa kata hiyo.
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba akizungumza na wakazi wa kata ya Magomeni eneo la Makuti B kumnadi Mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia CCM
MNEC wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam , Yusuph Nassoro akihutubia wakazi wa Magomeni wakati wa uzinduzi wa Kampeni za udiwani wa kata hiyo
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa wa Dar es SalaaSimon Mwakifamba akipokea kadi na kumkaribisha Mwanachama Mapya wa CCM kutoka Chadema
Baadhi ya Wanachama waliofika katika Mkutano huio wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa udiwani kata ya Magomeni

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 6,2019

MAJALIWA AZINDUA X- RAY YA KIDIGITALI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua  X-Ray ya kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt, Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5739
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5787
PMO_5803
Wananchi wa Songea wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Mashine ya  X-Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO_5605
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu kuhusu ukarabati wa Jengo la Wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,  wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

WAZIRI UMMY ASHIRIKI UJENZI WA BWENI LA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI KIRARE JIJINI TANGA

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameshiriki ujenzi wa bweni la Wasichana kwenye shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga ambalo litakapokamilika litawasaidia kuwaepusha na vishawishi wanavyoweza kukutana nazo wanapokwenda shuleni na kukwamisha ndoto zao.

Ummy ambaye alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Tanga akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Thobias Mwilapwa ambapo alikwenda Kata ya Kirare kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya bweni hilo na zahanati ya mapojoni alipofika kwenye eneo hilo la ujenzi huo alichanganya mchanga na sarauji na baadae kuchapia ukutani.

Ujenzi huo wa Bweni la Wasichana kwenye shule hiyo litasaidia kuondosha changamoto ya watoto kutembea umbali wa kilomita kumi na tano kufuata huduma ya elimu jambo ambalo linaweza kupelekea kukumbana na vishawishi ambavyo vinaweza kukwamisha ndoto zao.

Akizungumza mara baada ya kushiriki ujenzi huo Waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) mkoa wa Tanga alisema atashirikiana na wananchi kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazowakabili zinapatia ufumbuzi.

Alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuchapa kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kutatua changamoto wa wananchi ili ziweze kupata ufumbuzi haraka na kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao na jamii zinazowazunguka.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akishiriki katika ujenzi wa vyumba vya bweni la Wasichana shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga jana mara baada ya kuwakabidhi mabati 100 kwa ajili ya zahanati ya Mapojoni na bweni hilo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za wananchi kushoto ni Diwani wa Kata hiyo (CCM) Mwagilo
MBUNGE wa Viti Maalumu mkoani Tanga (CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameshiriki ujenzi wa bweni la Wasichana kwenye shule ya Sekondari Kirare Jijini Tanga ambalo litakapokamilika litawasaidia kuwaepusha na vishawishi wanavyoweza kukutana nazo wanapokwenda shuleni na kukwamisha ndoto zao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ASASI ya Uzalendo nchini (AWAMATA) imemtunuku cheti cha uzalendo Rais Dkt. John Magufuli kwa  kufanya vizuri katika kipengele cha uzalendo kwa mwaka 2018.

 Akizungumza katika  mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa City Garden jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Asasi hiyo Chief Daudi   Mrindoko ameeleza kuwa Rais Magufuli amejitoa katika kupambana na rushwa pamoja na kuanzisha miradi mikubwa yenye lengo la kuboresha uchumi na hali ya wananchi wa kawaida, hivyo mchango wake unapaswa kutambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa. 

 Mrindoko amesema  kuwa mipango ya Asasi hiyo ipo  katika kueneza elimu ya uzalendo kwa kuanzisha chuo cha Uzalendo kitakachotoa Elimu ya Uzalendo, Ujasiriamali na kuwajengea vijana uwezo   wa kujitegemea na kuwa zao bora kwa taifa.

Pia Asasi hiyo imetoa picha maalumu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha mwaka 2018 na kuelezwa kuwa kuwa kasi anayoenda na Mh. Rais ni kuleta neema kwa wananchi wengi.
 Mwenyekiti wa AWAMATA Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeshika picha) na katibu wa taasisi hiyo Pilly Kimario(aliyeshika cheti kushoto) wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wadau na washiriki wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa AMATA  Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeketi kushoto) na katibu wa Asasi hiyo  Pilly Kimario(aliyeketi kulia)wakiwa Pamoja na wakurugenzi wapya wa Asasi waliotangazwa katika mkutano mkuu wa mwaka, jijini Dar es Salaam.
 Cheti cha pongezi na kutambua mchango kupitia kipengele  cha uzalendo kwa mwaka 2018 kilichotolewa na taasisi ya uzalendo nchini kwa Rais Dkt.John Magufuli, jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Waziri Mbarawa akagua uwekaji wa mifumo ya Maji na Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara Ihumwa Jijini Dodoma

$
0
0
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akikagua miundombimu ya maji katika tanki  ambalo litasambaza  maji katika mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa leo Jijini Dodoma.Tanki hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua lita milioni moja. 
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa  akishiriki  ujenzi wa jengo la Wizara yake unaoendelea katika Mji wa Serikali Ihumwa,Jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo  Bw.Barnabas Ndunguru juu ya ujenzi wa kisima cha maji  kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Wizara hiyo katika eneo la Mji wa Serikali.
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiangalia ramani ya uwekaji  wa mifumo ya Maji  katika chanzo ambapo Serikali inachukua maji  na kupeleka katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dodoma(DUWASA) Mhandisi David Palangyo.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.06.01.2019

BALOZI SEIF ALI IDI AFUNGUA SKULI YA SEKONDARY YA GHOROFA TATU MTONI ZANZIBAR

$
0
0

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akikunjuwa kitambaa kuashiria ufunguzi wa  Skuli ya  Sekondary ya Ghorofa  Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.

  Katibu mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Radhia Rashid Haroub akitoa taarifa ya ujenzi wa Skuli ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU baada ya kufunguliwa na makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji daraja la Pili na Mkuu wa Elimu ya Kompyuta Yussuf Khatib Mirahi mara baada ya kuingia katika chumba cha Kompyuta ilikuona Vifaa hivyo katika Ufunguzi wa  Skuli ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiiwasha moja kati ya Kompyuta zilizowekwa kwa ajili ya mafunzo baada ya kuingia katika chumba cha Kompyuta katika Ufunguzi wa  Skuli ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja.
 Baadhi ya Wanafunzi wanaosoma katika Skuli ya Sekondary ya JKU  waliohudhuria katika Ufunguzi wa Skuli yao mpya ya Sekondary ya Ghorofa Tatu ya JKU Mtoni Wilaya ya Magharibi A Unguja. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UVCCM YASEMA WANASIASA UCHWARA HAWAJIAMINI

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) umesema ukuaji wa Demokrasia umetoa fursa pana kwa kila mwananchi kufanya mambo yake kwa uhuru bila usumbufu wa aina yoyote katika jamii. 

Umebainisha kuwa wapo baadhi ya wanasiasa uchwara wanaokesha wakiwaaminisha na kuwapotosha Wafuasi wao kuwa Demokrasia imebinywa jambo ambalo sio la kweli kwani Demokrasia isingekuwepo hata hizo Kauli wanazotoa zisingeweza kusikika nchini. Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar  Mussa Haji Mussa katika hafla ya uzinduzi wa Matembezi ya kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964,ambapo hafla hiyo imefanyika katika Kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani Pemba. 

Alisema wanasiasa wanaoilalamikia serikali kuwa imebana Demokrasia ni wale waliozoea siasa za vurugu, vitisho na migogoro ya kisiasa hivyo kwa sasa wanaona hawana tena nafasi ya kufanya matukio ya aina hiyo ndio maana wanalalamika na kueleza bila aibu kuwa Tanzania na Zanzibar kwa ujumla hakuna demokrasia na uhuru wa kutoa na kupkea habari. 

Naibu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM Mussa alisema Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 umeenda sambamba na matakwa ya ASP katika upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi nchini.  Amesema mbali na kuimarika kwa huduma za kijamii na kiuchumi kwa asilimia 100 pia CCM na Jumuiya zake wameendelea kuwa vinara wa Demokrasia na Utawala bora hali inayotoa fursa pana kwa wananchi wa Zanzibar kushiriki kwa uhuru katika shughuli za kimaendeleo.
 NAIBU Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Mussa Haji Mussa akisoma taarifa ya Matembezi ya kuenzi miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Pemba.
BAADHI ya Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Zanzibar wakisikiliza nasaha mbalimbali zinazotolewa na viongozi katika hafla ya Matembezi hayo.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MTENDAJI MKUU TEMESA AFANYA ZIARA MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO

$
0
0
NA ALFRED MGWENO TEMESA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya ziara katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na kuwataka wafanyakazi wa Wakala huo katika mikoa hiyo kuongeza juhudi katika kazi ili kuhakikisha wanazalisha kipato cha kutosha kuweza kufikia malengo au hata kuzidi  mapato waliyojiwekea kwa mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.
Akizungumza na wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti, Mhandisi Maselle alisema anatambua kwamba TEMESA inakumbwa na changamoto nyingi za kiutendaji ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi hasa vya karakana pamoja na upungufu wa wafanyakazi lakini aliwataka mameneja wa mikoa hiyo pamoja na watumishi wake kujitahidi kufanya kazi zao kwa ufansi na kwa ushirikiano huku akiangalia namna ya kuwaongezea vitendea kazi na kujaza nafasi za watumishi zilizoachwa wazi baada ya kustaafu.
Katika mazungumzo yake Mhandisi Maselle alisisitiza kwamba, Kiongozi mzuri ni yule ambaye anafanya kazi bega kwa bega na wafanyakazi wenzake pale anapoona mapungufu na kuwatia moyo hivyo meneja ajitahidi kuwa karibu na watumishi wake.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (kulia) akikagua mashine ya kuchongea vipuri vya injini za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake mkoani humo kukagua utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (kulia) akitoa maelekezo wakati akikagua mashine ya kubadilishia tairi za magari katika karakana ya TEMESA mkoa wa Kilimanjaro alipotembelea kujionea utendaji kazi na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi wa wakala huo. Kushoto ni Meneja wa TEMESA mkoani humo Mhandisi Ferdinand Mishamo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (kushoto) akitoa maelekezo kwa mafundi na wafanyakazi wa karakana ya mkoa wa Arusha mara baada ya kukagua mtambo wa kuchenjua na kuchakata kokoto (Crusher) unaoonekana pichani.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati (aliyevaa koti) akikagua mitambo mbalimbali iliyopo katika karakana ya wakala huo mkoani Arusha.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI HASUNGA AZITAKA NFRA NA BODI YA NAFAKA NA MAZAO MCHANGANYIKO KUWA NA MKAKATI WA KUNUNUA NAFAKA ZA WAKULIMA NCHINI

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo nunua mazao ya wakulima nchini.


Wakati NFRA imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje ya nchi.


Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa.

Alisema kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli haitalifumbia macho kamwe.

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa  Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa  Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga (Mb), akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, tarehe 5 Januari 2019.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Idadi ya abiria bado kubwa Ubungo.

$
0
0
*Wengi ni wanafuzi katika mikoa ya Tanga,Morogoro na Dodoma

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii

Idadi ya abiria katika kituo cha mabasi Ubungo imeendelea kuongezeka kwa kwa sehemu kubwa wakiwa wanafunzi.

Akizungumza na Michuzi Blog Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria Hassan Mchanjama amesema kuwa abiria katika kituo cha Ubungo ni kubwa lakini wanasafiri kutoka na baadhi daladala kupata vibali.

Amesema abiria wengi ni mikoa ya Tanga, Dodoma pamoja na Morogoro ikiwa sehemu kubwa abiria hao ni wanafunzi.

Mchanjama amesema abiria wanavyofika katika kituo cha mabasi Ubungo wakate tiketi ndani ya Kutuo.Mmoja wa abiria Hamis Seif amesema kuwa kuna changamoto ya Usafiri katika msimu wa siku kuu na kuomba yaongezwe mabasi hata daladala katika mikoa ya jirani na Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa suala la ukaguzi katika kituo cha mabasi Ubungo ni mzuri na kutaka na mikoa mingine wafanye hivyo kwa ajili ya usalama wa abiria.
 Askari wa usalama barabarani Grant Pawa akiandika makosa ya basi wakati wa ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Moja ya tiketi aliyekatiwa msafiri ambaye kampuni ya basi hilo halipo katika kituo cha Ubungo abiria anadai kuwa aliyemkatia na kutia saini ni Rama Tall.
 Abiria wakiwa wamefurika katika katika Kituo cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani katika kituo cha mabasi Ubungo wakiwa na fundi wakufanya ukaguzi wa basi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nuru Hussein akifanya Ukaguzi katika basi kuangalia uimara wa Gurudumu pamoja na Brenk katika kituo mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUENDESHA OPARESHENI KUBWA KUWAONDOA WAVAMIZI WA HIFADHI YA MISITU NA MAPORI YA AKIBA

$
0
0
Serikali kuendesha operesheni kubwa kuwaondoa wavamizi wanaofanya shughuli za kilimo na ufugaji pamoja na watu wengine wanaofanya shughuli zisizo halali katika misitu na mapori yaliyohifadhiwa kisheria zikiwemo hifadhi za misitu ya serikali Kuu na halmashauri za vijiji.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo wakati akisoma  maazimio ya kikao cha mawaziri watano kilichofanyika mkoani Kigoma leo kutafuta utatuzi wa mgogoro wa matumizi ya ardhi katika hifadhi na Mapori ya Akiba ya Moyowosi.

Jafo alisema, wale wote  waliovamia hifadhi wanatakiwa kuondoka kwa hiari kabla ya zoezi la kuwaondoa kwa lazima, operesheni hiyo itafanyika wakati wowote ndani ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 2019.

Na kusisitiza kuwa wale wenye mazao katika hifadhi na mapori ya akiba wanaweza kuomba idhini ya kuvuna mazao yao.Jafo alisema Serikali imetenga jjmla ya hekta 10,012.61 kutoka kwenye hifadhi ya msitu wa Makere kusini kwa ajili ya kilimo na mipango ya halmashauri ya wilaya ya Kasulu ambapo Hekta 2,174 kwa ajili ya kijiji cha Mvinza, hekta 2,496 kwa kijiji cha Kagerankanda na halmashauri ya wilaya ya Kasulu Jumla ya hekta 5,342.61.

Kwa mujibu wa Jafo uamuzi huo unafuatia kuwepo kwa changamoto katika maeneo ya hifadhi za misitu na mapori ya Akiba ambapo maeneo mengi yamevamiwa kwa shughuli za kilimo na ufugaji  na hivyo kupoteza uoto wa asili katika hifadhi na mapori ya Akiba.
 Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakiwasikiliza Mawaziri walipofanya ziara katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere lililopo Kasulu Kigoma.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili kilichopo Kasulu Kigoma wakati wa ziara ya Mawaziri watano kukagua eneo la hifadhi la Msitu wa Makere.
 Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akikatiza katika moja ya vichaka vilivyopo kwenye hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma wakazi wa ziara ya Mawaziri watano kukagua msitu.
 Mawaziri Dk Hamis Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii, Suleiman Jafo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwasikiliza wananchi wa kijiji cha Kabulanzwili alipofanya ziara  katika eneo la hifadhi la Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Suleiman Jafo akiwaongoza Mawaziri wenzake kukagua maeneo mbalimbali katika hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.
 Moja ya eneo ndani ya hifadhi ya Msitu wa Makere uliopo Kasulu Kigoma ambapo Mawaziri watano walibaini uendeshaji shughuli za kilimo ukifanyika ndani ya hifadhi.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Musa Sima (kushoto), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina na Dk Angeline Mabula Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiwa katika gari wakati wa kukagua hifadhi ya Msitu wa Makere Kasulu Kigoma.


MCHANGE AWAVAA WAPINZANI WANAOPOTOSHA MSWAADA WA VYAMA VYA SIASA

$
0
0
Humphrey Shao, Globu ya Jamii

ASASI ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) imesema kuwa muswada mpya wa sheria wa vyama vya siasa uliyotolewa hivi karibuni una lengo la kudhibiti kikamilifu fedha za ruzuku za vyama vya siasa.

Asasi hiyo pia imesema muswada huo kama utapitishwa na kuwa sheria rasmi, utadhibiti ukomo wa uongozi wa juu katika vyama vya siasa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Habibu Mchange alisema kwa sasa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikilaumiwa juu ya matumizi mabaya ya fedha hivyo anaamini uwepo wa muswada huo ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria itadhibiti jambo hilo.Alisema licha ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuulalamikia muswada huo, yeye kama mwanademokrasia nchini anaamini kuwa sheria hiyo itasaidia kukuza na kuvijenga vyama vya siasa.

“Mimi na asasi yangu pamoja na vijana wenzangu tunamshukuru aliyependekeza muswada huu, kwani huko nyuma niliwahi kukandamizwa nikiwa katika vyama kutokana na kutokuwepo kwa sheria hii.“Kupitia muswada huu ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria utakwenda kusimamia vema ruzuku za kila chama cha siasa, kwani Sheria inaeleza kuwa Msajili wa vyama vya siasa atatoa ruzuku kwa vyama na kuelekeza namna ya kuzisimamia , nashangaa kwanini baadhi ya vyama vya upinzania vinapinga jambo hili,” alisema.

Alisema demokrasia ni kugombea nafasi na si watu kushikiria madaraka muda mrefu kwa kuwakandamiza wanasiasa waliopo hivyo kwa kupitia sheria hiyo itawafanya wanasiasa wote kuwa sawa.“Kutugwa kwa muswada huu kutawasaidia wanasiasa wanaoumia ndani ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kuondoa ukilitimba na Umungu watu,” alisema na kuongeza kuwa

“Viongozi wa chama wengi wamekuwa wakijimikisha vyama kwa kudai wanamichango mikubwa ndani ya vyama, sheria hii itaondoa migogoro na kuwa sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi,” alisema.Aidha alisema Muswada huo utampa nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi za wananchi ipasavyo pasipo kuingiliwa na chama chochote cha siasa.

“Ndani ya vyama vya siasa kuna watu ambao awandi vyeo kila siku wana cheo kilekile, hii yote ni kutokana na uwepo wa mfumo usiokuwa bora wa chaguzi ndani ya chama,” alisema.Hata hivyo, Mchange amewataka watanzania kutambua kuwa mabadiriko ya Katiba ni pamoja na mabadiriko ya sheria ndogo ndogo ikiwemo ya vyama vya siasa.“Sheria itakayotungwa itawapa wanasiasa sehemu moja ya kulalamika na kuwaweka kati wanasiasa wote kwa kuongea lugha mojab,”alisema .Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu muswaada huu unafaida kubwa kwa nchi kwani itasaidia kudhibiti fedha za ruzuku na kukuza vipawa kwa wanachama
.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange akizungumza na Waandishi wa habari juu ya upotoshwaji unaofanywa na vyama vya upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 
  Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi  ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJULIA HALI DKT SALIM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisindikizwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakati  alipomjulia hali  Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam, Januari 6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PMO 6198  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   wakisindikizwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati alipomjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam Januari 6, 2018. Watatu kushoto ni Mama Amen Salim. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO JIPYA OFISI YA ZURA ZANZIBAR

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akikunjuwa Kitambaa kuashiria Uwekaji wa Jiwe la msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein akiwa na Viongozi mbalimbali wakilitembelea Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)baada ya kuliwekea jiwe la Msingi Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
-Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba Maji na Nishati Ali Khalil Mirza akisoma risala katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Salama Aboud Talib akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jengo jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)lililowekwa jiwe la msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohamed Shein Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar(ZURA)waliohudhuria katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi Jengo Jipya litakalokuwa na Ghorofa Saba la mamlaka hio Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.Ikiwa ni Shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Mbunge Nyamagana akagua miradi mbalimbali ya maendeleo 'vyoo vinatisha'.

$
0
0
Mbunge Jimbo la Nyamaganamkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ameendelea na ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika Jimbo hilo ikiwemo elimu, afya, maji na barabara kusaidia ukamilishaji wa miradi hiyo kupitia fedha za mfuko wa jimbo.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ziara ya mbunge Stanslaus Mabula pia ilifika katika Shule ya Msingi Amani Kata ya Butimba na kujionea hali tete ya vyoo na kuchangia ukarabati wake.
Mbunge Stanslaus Mabula alifika katika Shule ya Msingi Amani iliyopo Kata ya Butimba na kutoa fedha kwa ajili ya kukamilisha jengo hili kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa.
Mbunge Stanslaus Mabula pia aliwasili katika Shule ya Msingi Igoma C na kusaidia ukarabati wa shule hiyo.
Ukarabati ukiendelea katika Shule ya Msingi Igoma C Jijini Mwanza.

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Green Agriculture Group Ltd, na SUGECO.

Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (Green House).

“Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”Alisisitiza Mavunde.

Mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu Mh Ikupa Stella Alex wakiangalia moja ya bidhaa wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House). 
mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) akitembelea moja ya shamba darasa.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana **Mhe.Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).
Moja ya Green House
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images