Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

WAZIRI HASUNGA ATEMBELEA STUDIO ZA KIDIGITALI ZA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE NA UKOMBOZI WA AFRIKA

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) Leo tarehe 21 Disemba 2018 ametembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika iliyozinduliwa miezi mitano iliyopita na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam.


Mhe Hasunga ametembelea Studio hiyo yenye kuhifadhi historia ya kumbukumbu ya ukombozi barani Afrika zilizopo katika kanda za sauti na video ikiwa imetengenezwa kwa ushirikiano kati ya TBC na Umoja wa Ulaya (EU), Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na wadau wengine wa maendeleo.


Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi, amemueleza Waziri wa kilimo kuwa Kuwapo kwa studio hiyo kumelenga kuongeza uwajibikaji, uwezo wa kupata taarifa za zamani na kuongeza uratibu wa menejimenti ya hifadhi ya mambo muhimu ambayo ni ya urithi wa Tanzania.

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akitazama ubadilishaji wa hotuba za Mwalimu Nyerere kutoka kwenye Analogi kwenda Digitali wakati alipotembelea studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) mitambo ya makumbusho iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.
Mkurugenzi wa huduma za Redio-TBC Bi Aisha Dachi akimuonyesha Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) meza iliyotumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius  Kambarage Nyerere kwa ajili ya mahojiano iliyopo kwenye studio za Kidigitali za Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Ukombozi wa Afrika zilizopo katika ofisi za Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) katika majengo yake yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, Tarehe 21 Disemba 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NAIBU KATIBU MKUU MSTAAFU WA WAZAZI AKABIDHI MIKOBA KWA NAIBU KATIBU MKUU MPYA

$
0
0
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya ya Wazazi Zanzibar,Najma Murtaza Giga, amemtaka Naibu Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo, Othman Ally, kuendeleza mabadiliko yaliofanyika ndani ya jumuiya ikiwemo kutunza na kuthibiti mali za jumuiya hiyo. Giga alisema jumuiya hiyo kwa sasa inaendana na mabadiliko hayo ambayo jumuiya imeshirikiana na chama katika kuzitunza mali hizo.

Alisema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi(CCM),kimefanikiwa kuwabaini na kuwatia nguvuni waliohusika na upotevu wa mali za jumuiya hiyo hivyo ni vyema kwendana na mabadiliko hayo. Mbali na hilo, Giga alisema jumuiya hiyo iko salama na kwamba hakuna tuhuma zozote zilizoikumba wanachama wa jumuiya katika suala la usaliti na mambo mengine.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akimkabidhi ofisi mjini Unguja ambapo alisema anamkabidhi jumuiya hiyo ikiwa katika hali ya usalama ikiwemo kutokuwepo kwa majungu na makundi. "Hali hii inatokana na kuwepo kwa upendo baina ya viongozi wa jumuiya hiyo ikumbukwe katika jumuiya hii hakuna viongozi waliopatikana na suala la usaliti wa tuhuma zozote zile," alisema.
NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid akifafanua namna atakavyoongoza Jumuiya hiyo kwa kufuata Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2017.
 NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Wazazi Ndugu Najma Giga akizungumza katika hafla ya mapokezi Naibu Katibu Mkuu mpya ndgugu Othman Ally Maulid katika Kikao cha kujitambulisha kwa viongozi na Watendaji wa ngazi mbali mbali za Jumuiya hiyo hapo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
 VIONGOZI mbalimbali wa Jumuiya ya Wazazi wakisikiliza kwa makini nasaha mbali mbali zinazotolewa na Naibu Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Ndugu Othman Ally Maulid.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DKT. ABBASI: SERIKALI ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI HAKI ZA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0


Na Mwandishi Wetu,MAELEZO,DAR ES SALAAM.

SERIKALI imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi  na kuimarisha misingi ya haki na wajibu ya waandishi wa vyombo vya habari nchini ili kuwawezesha kutekeleza vyema majukumu yao yaliyoanishwa katika Mikataba na Sheria mbalimbali za kitaifa na Kimataifa.

Hayo yamesema leo Jumamosi (Desemba 22, 2018) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi na wahariri wa vyombo vya habari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu ya Shia Ithsheriya.

Dkt. Abbasi alisema kwa kuzingatia Mikataba na Sheria mbalimbali za Kimataifa ikiwemo Kifungu cha 19 cha Mkataba wa Kimataifa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kiutendaji ili kuhakikisha maboresho na tasnia ya habari na utangazaji inapiga kubwa za maendeleo.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema moja ya mafanikio ya Serikali ni pamoja na kutungwa kwa Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari na Sheria Haki ya Kupata Taarifa ambazo kwa kiasi zimeweka mazingira wezeshi ikiwemo kuwepo kwa vipengele vya kisheria zinazopaswa kutekelezwa na Taasisi za umma na Binafsi katika utoaji na upatikanaji wa taarifa kwa umma.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi mara baada ya kuwasili katika semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambako Dkt. Abbasi alikuwa Mgeni Rasmi.
3
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala( wa tatu kulia)  akitoa moja ya maada zilizokuwa zikijadiliwa kwenye Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam,  kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya Shekhe Mkuu wa Tanzania, Haris Othmani na Kushoto ni `Mkurugenzi Mkuu TAMWA Eda Sanga, Mwanyekiti wa Blogu (Bloggers ) Joachim Mushi, Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
4
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina ya Jukumu la Mwanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam
5
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akisisitiza jambo kwa washiriki wa semina Jukumu la wanahabari wakati wa utoaji maada katika semina hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi wakifuatilia semina hiyo.
6
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akitoa hotuba fupi kuhusu maada ya  uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo.
9
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akisisitiza jambo  kuhusu maada ya uhuru wa habari kwa mwandishi katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) Shekhe Hemmed Jalala akifuatilia hotuba hiyo na kushoto ni Mwenyekiti Msaidizi T.I.C Ramadhani Mlekwa wakifuatilia maada hiyo.
10
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari –MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa dini pamoja na watoa maada katika Semina ya Jukumu la Mwanahabari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

Yapi Merkezi yafanya usafi Ufukwe wa Coco

$
0
0
Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii .

Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga Reli ya Kisasa imefanya usafi katika ufukwe wa Coco, ikiwa ni utunzaji wa Mazingira katika jamii inayowazunguka katika mradi wa Reli hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jioni ya leo, Mratibu wa Mazingira wa Kampuni hiyo Evodiaglory Mrengo amesema kuwa katika Ujenzi wa Reli wanatambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira katika kujenga afya salama kwa jamii wanayoizunguka katika miradi.

Amesema kuwa kufanya usafi  Ufukwe wa Coco ni mojawapo ya kazi za kijamii na Mazingira,na kwama kila Kampuni ikipata muda wa kufanya kazi ya kijamii ni vyema ikafavya hivyo.Mrengo amesema kuwa kufanya usafi ni kuhamasisha Wafanyakazi na jamii ya Mkoa wa Dar es Salaam kuwa mstari wa mbele katika utunzaji na uhifadhi wa fukwe za bahari ikiwa ni sehemu muhimu za mapumuziko.

Mjumbe wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Oysterbay Peter Mushi amesema wanatambua mchango wa Kampuni ya Yapi Merkezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco.
 Wafanyakazi wa Yapi Markezi wakiweka Takataka katika mifuko walivyofanya usafi katika ufukwe wa Coco, leo jijini Dar es Salaam.
 Kiongozi Mkuu wa Afya na Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Erdem Yuksel akizungumza  kuhusiana na Kampuni hiyo kutoa mchango katika maeneo mbalimbali ikiwemo kufanya usafi katika ufukwe wa Coco leo  jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira wa Mtaa huo Peter Mushi akizungumza kuhusiana na Ujio wa Kampuni ya Yapi Markezi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco,jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Mazingira wa Kampuni ya Yapi Markezi Evodiaglory Mrengo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na usafi wa Kampuni hiyo waliofanya katika Ufukwe wa Coco ,jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa Yapi Markezi wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco ikiwa ni kutoa msaada kwa jamii

AIRBUS YATUA GHANA, KUTUA DAR KESHO SAA NANE UNUSU MCHANA

$
0
0
Accra, Ghana.
Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania imewasili Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini.

Ndege hiyo itawasili kesho majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo imetua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege.

Balozi Mboweto wafanyakazi na baadhi ya abiria waliokuwapo katika uwanja huo wameonesha shauku kubwa ya kutaka kuiona ndege hiyo ambayo ni ya kwanza kutua Barani Afrika tangu kampuni ya Air-Bus ianze kutengeneza ndege za kizazi cha A220. “Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona Twiga na jina la nchi yetu Tanzania ambalo lina sifa kubwa duniani” amesema Balozi Mboweto.

Balozi amesema Watanzania waishio Nigeria na Ghana wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano na Mhe. Rais Magufuli kwa mafanikio haya makubwa ambayo yatasaidia kukuza uchumi kupitia usafiri wa anga, utalii na uwekezaji.Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada jana saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko.

Hii leo imetua Accra Ghana majira ya saa 4:00 kwa saa za Ghana na kupokelewa na Balozi Muhidin Mboweto wa Nigeria anayehudumia na Ghana. Pamoja na marubani wa kampuni ya Air-Bus na Marubani wa Tanzania walioongoza katika safari ya ndege hiyo kuja nchini Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ndiye anaongoza safari ya ndege hiyo kutoka Canada hadi itakapowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kesho Itatua  saa 8:30 mchana.

Mbunge Zungu azinduwa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga, Ilala

$
0
0
MBUNGE wa Ilala, Mussa Azzan Zungu amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.

Mbunge Zungu aliwataka wananchi wa Ilala kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana kutumika kuleta maendeleo kwa jamii.

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala (kulia).

Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala kuhamashisha matumizi ya huduma na bidhaa za Shirika la TTCL.

Baadhi ya wacheza shoo wakiwaburudisha wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo.

Shishi Baby aka Shilole akikimbiza katika kampeni hizo zilizofanyika uwanja wa Karume.


Msanii nguli Dully Skykes akiwapagawisha mashabiki wake katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga, Wilaya ya Ilala.
 
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya ya Ilala, Uwanja wa Karume wakifuatilia burudani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UJENZI

$
0
0


Karibu Tuelimishane Mambo Muhimu Kadhaa Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Ujenzi

Unaweza Ku-Share Na Watu Zaidi Ujumbe Huu, Unaweza Ukawasaidia Sasa Au Hata Wakati Mwingine Kwa Namna Moja Au Nyingine


NOTE: Kufuata taratibu za kitaalamu katika UJENZI kunaweza kukusaidia kupunguza gharama za ujenzi mpaka 15% pamoja na kukuepushia hasara inayoweza kutokea mbeleni, sambamba na kukupatia kitu bora, kizuri na chenye thamani

1. Baada Ya Kuwa Umetayarisha Kiwanja Chako Kizuri Katika Eneo Ulilochagua, Anza Kujiridhisha Na Unachotaka Kujenga, kwa mfano

(i) Matumizi, jengo lako ni kwa ajili ya matumizi gani, makazi, biashara, ofisi, taasisi, starehe, godown/kiwanda n.k.

(ii) Jengo la aina gani, ghorofa au nyumba ya chini ya kawaida?

(iii) Unahitaji kuwe na vyumba vya matumizi gani(functional requirements) kama vile vyumba vingapi vya kulala pamoja na nini cha ziada kama vile movie theatre, maktaba n.k, kwa jengo la nyumba ya kuishi, au kama ni matumizi mengine ujue mahitaji yake

2. Tafuta mtaalamu wa majengo, msanifu au mbunifu majengo(architect), huyu ana utaalamu juu ya jengo, kazi zake na mipangilio yake yote ya kitaalamu. Atakushauri na kukuongezea uelewa wa sayansi ya majengo kwa ujumla

-Baada ya kumpeleka kuona eneo lako(site visit) mkajadiliana mkaelewana mwambie akafanye michoro ya mwanzo arudi mjadiliane na kujiridhisha kama kilichofanyika kimeendana na mahitaji yako, kisha mkishapitisha akafanye michoro ya 3D's(picha) za muonekano wa jengo husika uzione na ujiridhishe kama umeridhika na muonekano huo kisha ndio umruhusu amalizie michoro ya mwisho kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri husika
 
NB; Ni muhimu sana kujiridhisha na jengo lako usije kujuta baadaye au kujikuta unabomoa na kubadilisha baada ya kuona makosa, kwa sababu unakwenda kuweka pesa zako nyingi sana usije ukaingia gharama zaidi baadaye ambazo ungeweza kuziepuka mapema kwa kujiridhisha wakati wa michoro
Likifanyika vile unavyotaka utalifurahia na hutaona umepoteza

3. Kama jengo lako ni la ghorofa hutaishia hapo, unalazimika kumtafuta mtaalamu mwingine wa kutengeneza muundo wa mihimili ya jengo(structural engineer au mhandisi mihimili). Huyu hataongeza au kupunguza chochote ila atatumia michoro iliyofanywa na architect kutengeneza michoro ya muundo wa mihimili inayoshikilia jengo, kisha atakukabidhi michoro hiyo iliyopigwa mhuri kabisa kwa ajili ya kufuatilia kibali cha ujenzi halmashauri

4. Umeshakabidhiwa michoro yote ya msanifu/mbunifu majengo(architect) ambayo ni (architectural drawings) na ya mhandisi mihimili(structural engineer) ambayo ni (structural engineering drawings) yote ikiwa imepigwa mhuri utaenda nayo katika halmashauri yako kuomba kibali cha ujenzi ukiwa pamoja na hati yako ya kiwanja

5. Baada ya kupata kibali cha ujenzi halmashauri unaweza kuanza ujenzi lakini kama jengo lako ni la ghorofa utatakiwa kufuatilia vibali vingine kutoka kwenye bodi mbalimbali za ujenzi kutegemeana na ukubwa na matumizi ya jengo lako.

Manispaa ya Ilemela yajipanga kutekeleza vyema ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, John Wanga akizungumza kwenye kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo, hii leo Disemba 22, 2018.
Mhadhiri kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Nasibu Mramba akiwasilisha mada kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.
Mhadhiri kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dkt. Nasibu Mramba akiwasilisha mada kwenye kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.
Mratibu wa Sekta isiyo rasmi Manispaa ya Ilemela, Raphael Mphuru (kulia), akiwasilisha mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shiriki la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, Yassin Ally.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (katikati), Kaimu Naibu Meya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Alfred Wambura (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando (kulia), wakifuatilia mada wakati wa kikao maalum/ cha dharura cha Baraza la Madiwani kilicholenga kujadili mapendekezo ya utekelezaji wa zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI kwa kushirikiana na taasisi ya I4ID limewasilisha mapendekezo ya zoezi la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Mapendekezo hayo yamewasilishwa leo Disemba 22,2018 kwenye kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Ilemela, kabla ya zoezi hilo la ugawaji vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo kuzinduliwa rasmi Alhamisi Disemba 27,2018.

Hatua hiyo imejiri baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuzishirikisha taasisi hizo kama mdau wa maendeleo katika Halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha zoezi hilo linakuwa na mafanikio makubwa hususani vitambulisho hivyo kuwafikia walengwa.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyowasilishwa ni pamoja na uundaji wa Kamati Maalum ya kusimamia zoezi la ugawaji vitambulisho hivyo ambayo inajumuisha Watendaji wa Kata, Watendaji wa Mtaa, Polisi Kata, Maafisa Maendeleo, Maafisa Biashara, Viongozi wa Wajasiriamali wadogo (Mwenyekiti na Katibu), Mwakilishi wa Wajasiriamali Wanawake pamoja na Mwakilishi wa Wajasiriamali Vijana.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, John Wanga pamoja na Mkurugenzi wa KIVULINI, Yassin Ally kwa pamoja wamesema lengo ni kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na mafanikio makubwa na Halmashauri hiyo inakuwa ya mfano nchini kwa kutekeleza vyema zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali wadogo.

HASUNGA ASIMIKWA KUWA CHIFU NZUNDA, ASEMA HAKUNA MBADALA WA CCM

$
0
0
Na Mathias Canal, Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) amesimikwa kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa.

Mhe Hasunga amesimikwa kuwa Chief na Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.

Sambamba na kusimikwa kuwa Chief Nzunda vilevile amekabidhiwa silaha za jadi ikiwemo mkuki wa kujilinda na maadui kutoka kwa Chifu huyo wa Mbozi.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Mhe Hasunga amewashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa mbunge wa Jimbo hilo katika uchaguzi wa Octoba 25, 2015 jambo lililompelekea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kumteua kuhudumu katika Wizara muhimu nchini ya Kilimo.

Alisema ushindi wake katika kiti cha ubunge ulisababishwa na imani kubwa ya wananchi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwani pamoja na changamoto mbalimbali ambazo zinaendelea kupatiwa ufumbuzi na serikali ya Awamu ya tano lakini CCM Pekee ndicho kitakachowaletea maendeleo ya Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa hivyo wananchi wanapaswa kuendelea Kukiunga mkono.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Katikati) amesimikwa Kiongozi wa Machief katika Wilaya ya Mbozi Chief Muleshwelwa Nzunda kuwa Chief Nzunda kutokana na majukumu makubwa anayoyafanya katika wizara yake sambamba na uwajibikaji uliotukuka katika Jimbo la Vwawa, Tarehe 22 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018. 
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) akicheza ngoma ya jadi, mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ajili ya ziara ya kijimbo, Tarehe 22 Disemba 2018. 
Baadhi ya Machief Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 katika viwanja vya Stendi ya Maroli akiwa katika ziara ya siku tano ya kijimbo.
Baadhi ya wananchi Wilayani Mbozi wakifatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Ngailonga Hasunga wakati akihutubia kwenye mkutano uliofanyika leo tarehe 22 Disemba 2018 wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe.


HII NDIYO MISINGI YA HAKI KWA WAANDISHI WA HABARI DUNIANI KOTE

WAFANYAKAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU WASHEREHEKEA SIKU YA FAMILIA KUAGA MWAKA 2018

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Acacia kupitia migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao wamesherehekea siku ya Familia ‘Buzwagi &Bulyanhulu Family Day 2018’ kuaga mwaka 2018 na kukaribisha mwaka 2019.

Sherehe hiyo iliyofanyika Jumamosi Disemba 22,2018 katika Viwanja vya Mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama,pia imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambapo mgeni rasmi alikuwa Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta.

Akifungua sherehe hizo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Bi. Janeth Reuben aliwashukuru wafanyakazi wote wa migodi hiyo kwa juhudi walizofanya katika mwaka 2018 kuhakikisha kampuni ya Acacia inaendesha biashara kwa ufanisi.

“Sote tunatambua jinsi Acacia tulivyopitia katika mazingira magumu sana mwaka huu na uliopita,lakini tumepata faraja kubwa sana kutoka kwenu kwa sababu mmeweza kufikia na kuvuka malengo tuliyojiwekea ikiwemo malengo ya uzalishaji na ya kiusalama,naomba tuendelee na kasi hiyo hiyo mwaka 2019”,alieleza.

“Nawashukuru sana pia wanafamilia waliofika hapa na wale ambao hawakuweza kufika,sisi wafanyakazi hasa wa migodi tunahitaji na tunapata ushirikiano na upendo mkubwa sana kutoka kwa wenzi wetu na watoto kwa sababu mazingira ya kazi yanatulazimu wengi wetu kuwa mbali na familia”,aliongeza Bi. Reuben.
Meneja Mkuu anayehusika na Ufanisi wa Kampuni ya Acacia, Bi. Janeth Reuben akifungua sherehe za Siku ya Familia ya Buzwagi na Bulyanhulu niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Peter Geleta Disemba 22,2018 katika viwanja vya Mgodi wa Buzwagi uliopo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu , Bw. Benedict Busunzu akielezea kuhusu Siku ya Familia ya Acacia mwaka 2018. Alisema kwa mara ya kwanza wameamua kuadhimisha siku ya Familia kwa kuwaleta pamoja wafanyakazi wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na familia zao ili kuimarisha ushirikiano zaidi.
Wanafamilia wakipata huduma ya chakula.
Meneja wa NHIF mkoa wa Shinyanga Imani Emmanuel akitoa maelezo kuhusu bima za afya.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia Janeth Reuben akiangalia mafuta ya kupaka yaliyotengenezwa kwa asali na kikundi cha wajasiriamali wa Mwendakulima waliowezeshwa na Acacia.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog .



DKT BASHIRU ASIMIKWA UCHIFU KWAO, ASEMA VIONGOZI WA CCM WENYE UCHU WA MADARAKA HAWATAVUMILIWA

$
0
0
Na Abdullatif  Yunus wa Globu ya Jamii, Kagera
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt Bashiru Ally Kakurwa amewasisitiza wale wote wanaohitaji Uongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, Kujipanga kwa Sifa, Sera nzuri zitakazowauza na si kwa kurubuni, wala kuhonga Wananchi.
DKT. Bashiru amesema hayo Desemba 22, 2018 Baada ya kuwasili Nyumbani kwao Kanazi Mkoani Kagera wakati akizungumza na Viongozi wa Chama na Serikali pamoja na Wananchi Waliojitokeza Kumpokea na Waliomsindikiza hadi Nyumbani kwake Nje kidogo ya Mji wa Bukoba.
Dkt. Bashiru amesisitiza juu ya Wagombea kufanya Siasa za Maendeleo, na sio Siasa chafu za Kugawa watu, kujikomba, kurubuni wala kutoa hongo huku akiwataka Wanachama Kuanza kubaini Wanachama wenye sifa, wenye Uchu na Maendeleo  na wasioweka weka mbele masilahi yao Binafsi, ili Uchaguzi ujao uwe wa Mfano, kama Chaguzi Zilizofanyika enzi za TANU.
Sambamba na hilo Dkt. Bashiru amenukuliwa akisema kuwa Kiongozi atakaechaguliwa kwa kutumia Njia za Ulaghai hata kama atakuwa amepitishwa, akibainika ataenguliwa mara moja.
Katika hatua nyingine Dkt. Bashiru amewataka Viongozi waliopo Madarakani waachwe wafanye Kazi, Kwani Muda wa Kuanza kunadi Sera bado, hivyo kwa wale ambao wameaanza kupita pita kwa Wanachama waache Mara moja kwani tayari Orodha yao tayari anayo kwa Nchi nzima. 
 Kuhusu wawekezaji, Dkt. Bashiru amesema Nchi ya Tanzania Bado ni maskini na Nyenzo pekee ya kujikwamua kutoka katika Umasikini huo ni kupitia Sekta ya Kilimo, hivyo hapendezwi na hali iliyopo kwa sasa ya kuwaruhusu wawekezaji kutoka Nje ya Nchi kufanya shughuli za Kilimo, Ufugaji Na Uvuvi hapa Nchini. Hivyo amemuagiza Naibu Waziri wa Kilimo Ndg. Innocenti Bashungwa kuwa kwa wale ambao wameshapewa nafasi ya Kufanya shughuli hizo wawe wa mwisho,  na kwamba Ardhi ya Tanzania ilimwe na Watanzania wenyewe, na kuanzia sasa Wizara haitatakiwa kutoa Vibali kwa wawekezaji katika Sekta ya Kilimo kufanya Kilimo ndani ya Nchi yetu.
Dkt. Bashiru yupo Mkoani Kagera kwa Mapumziko mafupi pamoja na Ziara ya Kikazi Ambapo Kuanzia Desemba 26, Mwaka huu ataanza Ziara hiyo kwa kukutana na Viongozi wa Chama Kutoka Missenyi, Bukoba na Bukoba Mjini.
Mzee Masabala Akiongoza tukio la Kumsimika Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Kuwa Chifu mara baada ya Kuwasili Kijijini Kwao Kanazi - Bukoba.


 Dkt. Bashiru Anaonekana ameshikilia  Mkuki na Mundu Mara Baada ya kusimikwa na Wazee wa Kimila.
Dkt. Bashiru Ally Katibu Mkuu CCM - Taifa Akizungumza na Wananchi pamoja na Viongozi wa Serilkali na Chama, Nyumbani Kwao Kanazi, Kemondo mara Baada ya ulakiwa na Kusimikwa na Wazee.

INTRODUCING "NICHEMSHIE" OFFICIAL VIDEO BY JAY DABA FT TABUYA

HII NDIYO MISINGI YA HAKI KWA WAANDISHI WA HABARI DUNIANI KOTE - DKT ABBASI

AHSANTENI WATANZANIA KWA KUTUMIA USAFIRI WETU WA RELI - MKURUGENZI MKUU TRC ATOA SALAMU ZA MWAKA 2019


Mkazi wa Kivule Dar aondoka na 10m/-za Jigiftishe

$
0
0
Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam Bi Jane Jisandu, ameibuka mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo.

Jane anakuwa mshindi wa tano wa zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaam, Mbwana Mbela mkazi wa wMpwapwa mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam, Jane alisema zawadi hiyo ni muujiza na kuongeza kuwa itasaidia kuokoa maisha ya mwanaye ambaye anatakiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu.“Kwangu huu ni muujiza mkubwa sana. Nina mtoto mgonjwa na ambaye nimeambiwa anaweza kutibiwa lakini mpaka nchini India. Gharama za matibabu yake ni kubwa, nilikuwa nikiwaza wapi ningepata fedha za matibabu lakini Mungu amenitendea muujiza kupitia Tigo, naishukuru Tigo kwa kuokoa maisha ya mwanangu,” alisema

Jane alisema amefanikiwa kushinda zawadi hiyo baada ya kuwa antumia huduma za Tigo kama kuweka kuma wa maongezi, kununua vifurushi mbali mbali pamoja na kutuma pesa kwa njia ya Tigo Pesa huku akiwataka watu kutumia huduma za Tigo ili kujishidia zawadi za fedha taslimu.
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa pili kushoto) akifurahia mfano wa hundi  kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa (wa pili kulia). Wanaoshguhudia wa kwanza kushoto ni mtangazaji wa radio clouds FM Mina Ally na wa kwanza kulia ni Deogratius  David kutoka Tigo.

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni kumi katika Promosheni ya Tigo igiftishe Jane Jisandu (wa tatu  kushoto) akiwa kaika picha ya pamoja na washindi wa shilingi milioni moja moja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

TAZAMA LIVE LIVE RAIS DKT MAGUFULI AKIPOKEA NDEGE MPYA YA AIRBUS A220-300

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220 - 300 (DODOMA) ILIYONUNULIWA NA SERIKALI YA TANZANIA

$
0
0
  Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
  Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Rubani mstaafu Kapteni Mapunda kutokana na uzalendo wake kwa Taifa kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na  Rubani mstaafu Kapteni Mapunda na mkewe kutokana na uzalendo wake kwa Taifa  na kumpa zawadia ya kiasi cha Tsh Milioni kumi kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 - 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya ndege na Mkewe Janeth Magufuli ,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na simu alipokuwa anakagua ndege mpya ya Airbus 220-300 ndani ya ndege hiyo na mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege mpya aina ya Airbus 220-300 na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge Job Ndugai,Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli ,Balozi wa Canada Pamela O’donnel ,Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na viongozi na Wafanyakazi wa Shirika La ndege la Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23, 2018. PICHA NA IKULU

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

HDIF YAWANOA INSPIRE JUU YA 7 PRINCIPAL OF DIGITAL

$
0
0
--
Mtaalamu kutoka HDIF, Simon Mtabazi akizungumza na Vijana wa Inspire Project kuhusu umuhimu wa 7 Digital Principal kwa ajili ya ugunduzi wa mambo mbalimbali ya ubunifu kwa jamii ya sasa
Meneja mradi wa Inspire , Agnes Mwangongoka akizungumza na Wataalamu ambao watashiriki katika Boot Camp ya Wanafunzi wa Sekondari itakayofanyika kwa siku nne jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wanafunzi wa masuala ya Sayansi.
Mmoja wa Wataalamu wa watakaotoa Mafunzo katika Bootcamp, Dr .Michael Magoti akieleza namna watakavyoweza kuwasaidia Wanafunzi kuelewa kuhusu Masuala mbalimbali ya kisayansi katika Kilimo.
Mtaalamu wa Masuala ya Uhandisi wa Maji akieleza namna atakavyotumia uzoefu wake kuwafundisha Wanafunzi watakao shiriki BootCamp ya Inspire
Jopo la Wataalmu kutoka sehemu Mbalimbali watakaoshiriki BootCamp kwa ajili ya kuwanoa wanafunzi  masuala ya kisayansi Jijini Dar es Salaam(Picha na Humphrey Shao wa MMG)

Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza awekwa wakfu

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Mwanza, Askofu Philipo Magwano (pichani) hii leo Disemba 23, 2018 amewekwa wakfu na kusimikwa kazini katika ibada maalum iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini, Askofu Mussa Magwesela katika kanisa la AICT Makongoro Jijini Mwanza.
Jopo la Maaskofu wa Kanisa la AICT wakimweka wakfu na kumsimika kazini Askofu Mkuu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Mwanza, Askofu Philipo Magwano.
Mgeni rasmi kwenye ibada hii maalum ya kumweka wakfu na kumsimika kazini Askofu Mkuu Kanisa la AICT Dayosisi ya Mwanza alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto).Tazama BMG Online TV hapa chini.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images