Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO

$
0
0
Na. Vero Ignatus, Arusha 

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Musilimu amewaomba abiria kulisadia jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona dereva amekaidi sheria ya usalama barabarani, wasisubirie hadi ajali itokee ndipo waanze kutoa malalamiko

Hayo ameyasema leo Jijini alipokuwa akifanya ukaguzi wa magari pamoja na askari wa usalama barabarani na wadau wengine wa usalama katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ambapo aliwataka abiria kutokufumbia macho uzembe wowote atakaoufanya dereva wa kuhatarisha maisha ya abiria awapo safarini.

Aidha ameeaagiza abiria hao punde wanapomuona dereva anaotaka kulipita gari lingine kimakosa, mwendo kasi, lugha chafu kwa abiria, kuongea na simu sambamba na viashiria vyote vinavyoweza kupelekea kutokea ajali watoe taarifa kwa namba 0656111444

'' Piga simu muda wowote tunapambana sisi tunapambana na madereva wazembe hadi kuhakikisha tunakuwa salama barabarani "'' Tunapozungumzia maisha ya watu hatuna mchezo wacheni uzembe na mambo ya kitotokitoto muwapo barabarani dereva unakimbia kwenda wapi gari limejaa udereva ni taaluma, zingatia sheria uwapo barabarani"alisema Muslimu

Muslim ametahadharisha madereva ambao hawatazingatia na kutii sheria za usalama barabarani kuwa jeshi la polisi halitawafumbia macho sheria itafuata mkondo wake. Pia amesisitiza kuwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani lipo tayari kwaajili ya waananchi na kuhakikisha usalama wa maisha yao wawapo safarini. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Baraka Msangi amesema zoezi la Abiria paza sauti sambamba na ile ya Nyakua ya jeshi la polisi imesababisha ajali zimepungua katika Jiji la Arusha
Amewataka Madereva kuendelea kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwasababu abiria wanawategemea wao wawapo safarini 
Wa Pili kutoka kulia ni Kamanda wa kikosi cha uslama. Barabarani SACP Fortunatus Musilim, akifuatiwa na Mrakibu msaidizi Joseph Bukombe mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha, Mjumbe wa Baraza la usalama barabarani Taifa Hamza Kasongo na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bakari Msangi wakiwa stendi kuu leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchi SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na abiria leo asubuhi katika stendi ya mabasi Jijini Arusha kabla hawajaanza safari. Picha na Vero Ignatus
Magari yakiwa yanatoka stendi kuu ya mabasi Arusha. Picha na Vero Ignatus 
Baadhi ya mabalozi wa usalama barabarani wakiwa tayari kwa kupaza sauti stendi kuu ya mabasi jijini Arusha. 
Kutoka kulia ni Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani SACP Fortunatus Musilim ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Arusha Joseph Bukombe, Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi. Picha na Vero Ignatus.


INTRODUCING:MBOSSO - TAMU (OFFICIAL AUDIO)

MICHUZI TV: SHANGWE LA HAJI MANARA, MASHABIKI BAADA YA SIMBA SC KUFUZU MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MICHUZI TV: RAIS DKT MAGUFULI AMPA MILIONI KUMI RUBANI ALIYEITOROSHA NDEGE NCHINI KENYA

MICHUZI TV:SIMBA SC YAFUZU HATUA YA MAKUNDI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, TAZAMA MABAO YOTE 3-1 DHIDI YA NKANA

MICHUZI TV: FURAHA YA RAIS DKT MAGUFULI WAKATI WA KUIPOKEA NDEGE MPYA AINA YA AIRBUS A220-300

MGALU ACHANGIA MIFUKO YA SARUJI UJENZI WA OFISI MBILI ZA CCM KIBAHA VIJIJINI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA VIJIJINI 

MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu ameunga mkono jitihada za ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi kata ya Mtongani na Mlandizi kwa kutoa mifuko ya saruji 40 yenye thamani ya zaidi ya laki sita.

Kati ya mifuko hiyo amechangia mifuko ya saruji 20 kwa kata ya Mtongani na mingine 20 kwenye kata ya Mlandizi . Subira alitoa mifuko hiyo ya saruji wakati alipokutana na baadhi ya viongozi wa chama ikiwa ni moja ya kazi za kichama. Alieleza hatochoka kushiriki kusaidiana kutatua changamoto zilizopo kichama na serikali. 

“Ni wakati wa chama kukiimarisha kwa kujenga na kukarabati ofisi zetu, kuongeza vitendea kazi kwakuwa CCM mpya inajengwa lazima kwenda na wakati “alieleza Subira. Hata hivyo Subira aliwataka ,wanawake wasikate tamaa wathubutu kujitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali. 

“Tukaemkao wa kula sasa, tunaelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, tusiogope, wanawake tujiamini “alifafanua Subira. Nae diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala, alisema Hili ulilolitenda leo ni kubwa kwa wanaCCM na wananchi kijumla, hivyo aliwaomba wadau wengine kujitolea kushirikiana ili kumaliza kama sio kuzitatua kero za zinazowakabili kichama”

Katibu wa Jumuiya ya wanawake (UWT) Kibaha Vijijni Janeth Mnyaga alimshukuru mbunge huyo kuwa bega kwa bega kushiriki nao kwenye shughuli za jumuiya na chama. Wakati huo huo Subira alitembelea kituo cha afya Mlandizi kujionea hali ya upanuzi wa majengo kwa gharama ya sh. Milioni 400 ambazo zimetolewa na serikali.
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) wakati alipokwenda kutembelea kituo cha afya Mlandizi kujionea hali ya ujenzi wa upanuzi wa kituo hicho ukiendelea, wa kwanza kulia mwenye kofia ni mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
MBUNGE wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu (wa kwanza kushoto) akipewa mkono wa pongezi na mmoja wa viongozi wa CCM kata ya Mtongani. (Picha na Mwamvua Mwinyi) 

WAZIRI JAFO AKABIDHI KOMPYUTA 25 KWA SHULE ZA SEKONDARI 14 KATIKA WILAYA YA KISARAWE

$
0
0

VICTOR MASANGU, KISARAWE

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amewaagiza wakurugenzi wote wa halmashauri nchini pamoja na maafisa elimu kuachana kabisa na vitendo vya kuwanyima fursa walimu ambao wanahitaji kujifunza somo la tehema na badala yake wahakikishe wanatoa vibali bila ya kuwa na ukilitimba wowote kwa lengo la kukuza teknolojia na mawasiliano.

Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi kompyuta 25 ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasilino kwa wote ambapo zitazinufaisha shule za sekondari 14 zilizopo katika halmashauri ya Kisarawe.

Jafo alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawajengea uwezo walimu ambapo hadi sasa tayari walimu wapatao 570 wameshapatiwa mafunzo maalumu kwa ajili ya somo la tehema ili kuendana na kasi na mabadiliko ya kiteknolojia.

“Kitu kikubwa sisi kama serikali kwa sasa tumejipanga kuhakikisha kwamba somo hili la Tehama kwa walimu linapewa kipaumbele zaidi, lakini sipendi kuona walimu wananyimwa vibali kwa ajili ya kwenda kuongeza ujuzi katika somo hilo hivyo kuanzia sasa ofisi yangu italisimamia hili na kwamba wakurugenzi wote na maafisa elimu msiwanyime vibali kabisa wapeni acheni roho mbaya,”alisema Jafo.



Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) kati kati akimkabidhi kompyuta mmoja wa walimu wa shule za sekondari,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo katika halfa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo kati kati akiwa ameshika moja ya kompyuta ambazo zmezitoa kwa niaba ya serikali, kushoto kwake ni Naibu waziri wa uchukuzi na Mawasialiano Injinia Atashasta Nditiye, na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kisarawe Mussa Gama wa kwanza kulia akishuhudia ugawaji wa kompyuta hizo ambazo zimetolewa na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote ambapo shule 14 za sekondari zimeweza kunufaika na msaada huo.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 24,2018.

WADAU WA ELIMU WACHANGIA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 250 UJENZI WA MADARASA BUSEGA SIMIYU

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu 

Wadau mbalimbali wa elimu wamechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu katika Harambee iliyofanyika Mjini Nyashimo, ambapo zimepatikana jumla ya shilingi 254, 969,000/= fedha taslimu zikiwa ni shilingi 15,360,000/= ahadi shilingi 241,809,000/= na mifuko ya saruji 127.

Akiongea na wadau hao Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma amesema upo umuhimu wa kuhakikisha watoto wanapata elimu kwa kuwa elimu ni urithi hivyo kila mmoja awe na uchungu wa kuona watoto wanasoma. 


“Hakuna urithi tunaoweza kuwapa watoto wetu zaidi ya elimu tusipowapa elimu rasilimali zote ambazo tunazipigania leo hii, tunavyopambana kulikomboa Taifa letu kiuchumi itakuwa kazi bure kwa sababu tutabaki na Taifa la watu ambao ni watumwa wa watu wenye elimu” alisema Mshashi

Awali akitoa taarifa ya hali ya vyumba vya madarasa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Bw. Anderson Njinginya amesema halmashauri hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa 107.

Mmoja wa Wadau wa elimu katika Wilaya ya Busega, Bw. Deo Kumalija ambaye alichangia katika harambee hiyo ametoa wito wadau wa maendeleo na wananchi kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo waliyopo, ikiwemo ujenzi wa shule kwa kuwa maendeleo yao yataletwa na wao wenyewe.
Wadau wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 

Wadau wa elimu na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Simiyu wakichangia katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 
Mkuu wa Wilayaya Busega Mhe. Tano Mwera (kushoto) na Mbunge wa Busega,Mhe. Dkt. Raphael Chegeni wakiteta jambo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo. 
Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ambaye alialikwa  kama Mgeni rasmi wa Harambee hiyo, Luteni Kanali Josephat Mshashi, Mkuu wa Kikosi cha 27 Makoko Musoma akizungumza na wadau wa elimu, katika harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wilayani Busega, iliyofanyika Mjini Nyashimo lengo likiwa ni kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa wilayani humo.  

KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI

$
0
0

Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mjini Unguja na kumweleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahakikisha miradi inayohusu wavuvi inawanufaisha moja kwa moja.

Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Makame Ali Ussi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw. Islam Seif Salum pamoja na watendaji wengine wizara, Mhe. Ulega amesema lengo kuu la ziara yake ya siku moja kisiwani Zanzibar ni kutazama shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu Zanzibar kupitia mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH).

“Tunahitaji tuone rasilimali za bahari zinatunufaisha, mchango wake bado ni mdogo sana mradi wa SWIOFISH una pesa nyingi lakini bado hatujaona mafanikio ya moja kwa moja kuwasaidia wananchi tulikubaliana kuna mambo ya kurekebisha.” Alisema Mhe. Ulega

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema uchafuzi wa bahari, uwepo wa maharamia na uvuvi haramu ni mambo ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kukabiliana nayo ili kuhifadhi bahari na kufanya sekta ya uvuvi kuwa yenye tija kwa wananchi.

Mhe. Juma pia amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala yanayohusu uvuvi ili kubadilishana uzoefu hasa baada ya hivi karibuni kuhudhuria mkutano wa “Blue Economy” nchini Kenya ambapo nchi washiriki wa mkutano huo walikubaliana kusimamia mambo mbalimbali ili kulinda rasilimali za Bahari ya Hindi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma.



WAKULIMA TUMIENI MBOLEA YA SAMADI KUONGEZA UZALISHAJI WA MAZAO MBALIMBALI-RC TABORA

$
0
0
NA TIGANYA VINCENT

WAKULIMA wilayani Nzega wametakiwa kutumia mbolea aina ya samadi ya ng’ombe wakati wa upandaji wa mazao kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ikiwemo pamba ili kuwa na malighafi za wingi za viwanda.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa elimu ya kuzingatia Sheria na Kununi 10 za kilimo cha pamba wilayani Nzega.

Alisema kilimo kinachoendelea wilayani humo kwa wakulima wengi kulima bila kutumia mbolea wala samadi hakitawasaidia wakulima wa Wilaya ya Nzega kuwa na ziada ya kuwasaidia kusonga mbele. Mkuu huyo wa Mkoa alisema samadi itasaidia kurudisha uhai wa ardhi yao ambayo imeanza kuchoka na pia itasaidia kutunza unyenyevu wakati wa ukame na hivyo kumwezesha mkulima kuwa na uhakika wa mavuno mazuri.

Mwanri alisema wawezekaji wanahitaji kuweka mitaji yao sehemu ambayo wanakuwa na uhakika wa malighafi za kutosha kuendesha viwanda vyao wakati wote na sio kwa kipindi kifupi.Aliongeza kuwa ziada ndio itawasaidia kupata ziada ya kuwauzia wawekezaji na hivyo kuwa fedha kwa ajili ya kuboresha maisha yao ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa, kula vizuri, kupata matibabu mazuri na kusomesha watoto wao.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa alisema Ofisi yake kwa kushirikiana na Chama Kikuu cha Ushirika wa Wakulima wa Pamba Mkoani Tabora Ingembensabo wanaendelea na mpango wa kutafuta Matreka kwa ajili ya kuvikopesha Vyama vya Ushirika Vya Msingi ili kuongeza ukubwa wa eneo la ulimaji wa zao la pamba na mazao mengine.

Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa kilimo Mkoani Tabora cha pamba na mazao mengine kinakuwa cha kisasa na chenye kuzalisha mazao mengi ambayo yanatoa ziada.Kwa upande wake Ofisa Kilimo Mkoa wa Tabora Modest Kaijage aliwataka wakulima Mkoani humo kuzingatia kanuni za kilimo bora ikiwemo kupanda kwa kutumia mbolea, upandaji mazao kuzingatia vipimo vya zao husika na kufuata mistari.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuwa na idadi ya miche (crop population) inayotakiwa kitaalamu katika shamba na hivyo kuwa na uzalishaji wenye tija unaolingana na ukubwa wa eneo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akitoa elimu ya Sheria ya Pamba na kununi 10 za zao pamba na unyunyuziaji dawa za kuua wadudu  kwenye eneo la Nzega Ndogo jana.

MKUU WA MKOA WA MTWARA ASIFU JUMUIYA YA WAISLAMU AHMADIYYA

$
0
0

Kupitia mkutano wa Amani ambao umeandaliwa  na waislamu na jumuiya ya waislam Ahmadiyya mkutano ambao uliwakutanisha viongozi wa asasi sizizo za kiserikali,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa serikal mkutano ambao ulifanyika siku ya ijumaa tarehe 21/12/2018. Mgeni maalumu alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa ameipongeza Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya kwa kufanya mkutano wa amani ikiwa ishara tosha kabisa kuelezea islamu na amani amendelea kuwasisitiza viongoz wa dini kuwakumbusha waumini swala la amani.

Pia katika mkutano huo mkuu wa mkoa alifungua rasmi kituo cha kurushia matangazo cha radio ahmadiyya 99.3 mHz ambacho kwa sasa kinasikika ndani ya manispaa ya mtwara mikindani na kuwataka wanahabari kufanya kazi kwa weledi na uadilifu na kushirikiana na serikali ufahasa kupitia redio huku akiendelea kusisitiza watu kuienzi amani.

Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa Ahmadiyya  kwa kuenzi amani na kuiga kutoka kwao kwa kufanya mikutano kama hii mara kwa mara na kutoa pongezi kwa jumuiya kwa kutoa mafundisho ya utii wa serikali pia ametahadharisha wote ambao watakaovunja amani kwa kisingizio cha dini watashughulikiwa kama wahalifu.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akimkabidhi zawadi ya vitabu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mtwara Titus Mdoe
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akimkabidhi zawadi ya vitabu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akitoa hotuba siku ya mkutano wa amani ulifanyika katika viwanja wa MAsjid Batul Karim Mkoani Mtwara.
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu Ahmadiyya Sheikh Tahir Mahmood akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasuis G. Byakanwa na baadhi ya waumini wa dini hiyo katika uzinduzi wa radio ahmadiyya .mh mkuu wa mkoa alikuwa mtu wa kwqanza kusaini kitabu cha wageni .

Vyumba vya madarasa 99 vyawazuia Wakurugenzi kula Christmas

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakurugenzi kutosheherekea sikukuu ya Christmas mpaka watakapopata ufumbuzi wa ujenzi wa madarasa 99 yanayohitajika kwaajili ya kutumiwa na wanafunzi 4930 waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2019.

Amesema kuwa ufaulu mwaka huu 2018 umekuwa kwa asilimia 73 ukilinganisha na mwaka 2016 ambapo ulikuwa ni wa asilimia 68 na hivyo wanafunzi 4930 kukosa kuingia madarasani kutokana na changamoto ya upungufu wa madarasa.

Ameongeza kuwa serikali ya Mkoa imejipanga vilivyo kuhakikisha hakuna hata mwanafunzi mmoja anakosa nafasi ya kusoma hali ambayo itawafanya wanafunzi wote waliokosa nafasi kupatiwa fursa ya kuendelea na masomo yao kwa mwaka 2019 na kuwaomba wanachi kwa kushirikiana na halmashauri kuhakikisha vyumba hivyo vinapatikana hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa pili.

 “Hawa wanafunzi tusiwakatishe tamaa ya kukosa nafasi ya kwenda kidato cha kwanza, hakuna mwanafunzi hata mmoja ataacha kwenda kidato cha kwanza, wakuu wa wilaya wote wasimamie zoezi hili na hakuna likizo na wale wakurugenzi wote hakuna kwenda likizo mpaka vyumba vya madarasa vyote view vimekamilika,” Alisema.

Ametoa maagizo hayo wakati akitoa salamu zake za Christmas kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa na kuwatakia wananchi wote kusherehekea sikukuu hiyo pamoja na kuukaribisha mwaka mpya kwa amani na utulivu kwani walianza vizuri na wamalize vizuri na kuwaomba kuendeleza mshikamano na ushirikiano kwa miaka inayofuata.

Kati ya hayo madara 99, halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga inatakiwa kujenga madarasa 41 yatakayotumiwa na wanafunzi 2,042, huku Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikihitaji madara 27 ili kutumiwa na wanafunzi 1,365 na halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ikihitajika kujenga madarasa 19 kwaajili ya wanafunzi 925 na halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ikitakiwa kujenga madarasa 12 kwaajili ya wananfunzi 598.

PILIKAPILI ZA WAKAZI WA GOBA JIJI LA DAR ES SALAAM KUELEKEA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA

$
0
0

 Wakazi  wa mkoa  Dar es Salaam na  baadhi  wageni  mbalimbali  kutoka mikoani kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya wakiwa kwenye pilipilika za kununua mahitaji mbalimbali kwenye soko la Goba  leo.(Picha na Emmanuel Massaka, MMG)
Baadhi ya Wakazi wa Dar es Salaam wakichagua mahitaji mbalimbali  katika soko la Goba.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AREJEA DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto) wakiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge wakati walipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Dodoma wakirejea kutoka Dar es salam, Desemba 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga

$
0
0
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,Harrison Mwakyembe amekubali mwaliko wa kutembelea kijiji cha wasanii Mwanzega kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za wasanii.

Katibu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela akizungumza jana wakati wa hafla ya  kukabidhi nyumba 15 kwa wasanii na wanamichezo alisema katika mazungumzo ya SHIWATA na Waziri Mwakyembe kuomba kijiji chao chenye nyumba za makazi kutambuliwa wizarani yamefanikiwa.

"Nawataarifuni kuwa SHIWATA inafanya kazi zake kwa uwazi na kufuata taratibu za kiserikali, tumemuomba Waziri Mwakyembe atutembelee na yeye amekubali kuja hapa kijijini kwetu huo ni ugeni uliopo mbele yetu "alisema Kagondela. Mmoja kati ya waliokabidhiwa nyumba hizo Mwanabaraka Mchinga alishukuru kukabidhiwa nyumba yenye thamani ya sh. Mil. 4.3 alizochangia kidogo kidogo mpaka kukamilisha kiasi hicho na kukabidhiwa nyumba yake.

Mwanachama mwingine anayeishi kijijini hapo Monica Humba alisema ameona mafanikio makubwa kutoka ahamie kijiji cha wasanii kwa sababu anaishi maisha ya gharama ya chini kwa sababu kila kitu analima na kufuga mwenyewe. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanzega, Kitongoji cha Gomapembe Seif Katundu aliwashauri wasanii kuwekeza kijijini kwa kumalizia ujenzi wa nyumba kwa vile Serikali ya awamu  ya tano ni sikivu itatekeleza kero zote za wananchi wake za maji,barabara na zahanati.

SHIWATA ambayo mbali ya kuendesha matamasha ya wasanii wa fani mbalimbali pia inajenga nyumba kwa wanachama wake na kumiliki shamba la ekari 220 katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga. Wakati huo huo uchaguzi wa viongozi wa SHIWATA utafanyika Januari 19,2019 kama ulivyopangwa awali na fomu zitaendelea kutolewa na kurudishwa mpaka Januari 4, mwakani ni mwisho.

Zimamoto watoa Elimu ya Uokozi kwa Abiria Stendi ya Ubungo

$
0
0
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini limeanza kutoa elimu ya Uokozi kwa abiria wanaosafiri kwenda mikoa mbalimbali nchini ikiwa ni mkakati wa kupunguza majanga pindi inapotokea dharura pale vyombo vya usafiri vinapopata matatizo njiani.

Akitoa elimu hiyo katika mabasi mbalimbali Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Temeke, Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, alisema jeshi limejipanga kutoa elimu katika stendi za mikoa mbalimbali nchini hasa baada ya abiria wengi kutoelewa elimu ya uokoaji pindi yanapotokea majanga njiani.

“Tunahudumia Watanzania na tunapenda kuona wananchi wanaenda kushuerehekea Sikukuu za mwisho wa mwaka  na wanarejea katika maeneo yao salama,na sisi kama jeshi tutahakikisha askari wetu wanakuwepo kazini masaa ishirini na nne ili watoe msaada pale utakapohitajika” alisema Kamanda Puyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti abiria wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali nchini wamesema wanashukuru kuona jeshi la zimamoto limejiongeza na hii  ndio inavyotakiwa kwani kumekua na majanga mengi njiani yanayosababisha watu kupoteza maisha.

“Hatukua na elimu ya kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, tunarishukuru jeshi kwa kutoa elimu hiyo na tunaomba waendelee na utaratibu huo sio katika kipindi hiki cha sikukuu tu bali iwe programu endelevu” alisema Ayoub Mtekela.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Temeke, Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi, akitoa Elimu ya Uokozi kwa abiria katika Stendi ya Ubungo wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali nchini katika kipindi hiki cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.Jeshi hilo linatoa elimu hiyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza safarini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

DStv wagawa zawadi za Kapu la sikukuu

$
0
0
Katika kusherekea msimu huu wa sikukuu kampuni ya MultiChoice Tanzania kupitia kisimbusi chake maarufu cha DStv  imemwaga zawadi za makapu ya sikukuu kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani yaliyosheheni vyakula mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, sukari, na viungo mbalimbali muhimu kwa ajili ya sikukuu bila kusahahau mbuzi mzima kwa kila mshindi na zaidi   visimbusi vya kisasa vya DStv vilivyounganishwa na vifurushi vya mwezi mzima wa Bomba kwa washindi wote wa shindano la ‘Kapu la Sikukuu’ lilioendeshwa mapema mwezi huu kwa kushirikiano na kituo bora cha redio cha E Fm  .

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Afisa Masoko kutoka MultiChoice Tanzania Esther Mtei  amesema kuwa, “Msimu huu wa sikukuu ni muda mzuri na sahihi wa kukaa nyumbani na familia na hii ndiyo sababu DStv leo tumewazawadia washindi hawa jumla ya makapu 30 ya vyakula yaliyosheheni mahitaji yote ya muhimu kwa ajili ya jikoni, mbuzi mzima kwa kila mshindi  sambamba na  visimbusi  vya DStv kwa kila mmoja pamoja na kufungiwa bure ili kuwawezesha kusherekea sikukuu wakiwa majumbani mwao huku wakipata burudani  ya kipekee kupitia vipindi bora vinavopatikana ndani ya king’amuzi cha DStv ikiwemo ligi kuu ya Uingereza (EPL) , vipindi maalum vya watoto pamoja na sinema kadha wa kadha maalum kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu” alisema Esther.

Naye meneja mkuu wa E Fm Radio na Tv E Mohamed  Lukwili alieleza kuwa,” Shindano hili liliwataka wasikilizaji wa E Fm radio kusikiliza na kufatilia vipindi tofauti kwa kipindi cha mwezi mmoja kisha kujibu maswali yaliyoulizwa ili kuweza kujishindia zawadi hii nono ya kapu la sikukuu kutoka kwa DStv”, alisema Lukwili.

Kwa upande wake bi. Mariam Mkwanje mmoja kati ya washindi wa shindano  la kapu la sikukuu alisema, “Kwa niaba ya washindi wenzangu  tuliofika mahali hapa asubuhi ya leo, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya MultiChoice Tanzania pamoja na E FM radio kwa kuweza kutukumbuka katika kipindi hiki cha sikukuu, tumefurahi sana na hakika tunaahidi kuendelea kuangalia DStv pamoja na kuwa wasikilizaji wazuri wa E Fm radio.
Washindi wa Kapu la sikukuu katika picha ya pamoja na maafisa wa MultiChoice Tanzania mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Afisa masoko MultiChoice Tanzania Esther Mtei (kushoto) akikabidhi zawadi kwa moja kati ya washindi wa Kapu la sikukuu Bw Mohamed kutoka Mbezi.

Baadhi ya washindi wa Kapu la sikukuu kutoka DStv wakipokea zawadi zao kutoka kwa Grace Mgaya Afisa Uhusiano MultiChoice Tanzania na Meneja Mkuu wa E Fm Radio na Tv E Mohamed Lukwili.

MAAMUZI YA NEC KUHUSU RUFAA MOJA YA UCHAGUZI MDOGO WA TAREHE 19 JANUARI, 2019 KWA KATA YA MAGOMENI JIMBO LA KINONDONI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea Rufaa moja (1) kutoka kwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Magomeni katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Tume imepokea rufaa hiyo kwa kuzingatia kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na kanuni ya 28(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015,

Rufaa hiyo iliwasilishwa na mgombea Udiwani wa Chama cha Wananchi (CUF) Ndg. Ngude Athumani Yusuph akitaka arejeshwe kuwa mgombea udiwani katika Kata ya Magomeni kupitia chama hicho.

Kuenguliwa kwake kulitokana na pingamizi lililowekwa na mgombea mwenzake kwa madai kuwa Sio Raia wa Tanzania, hakudhaminiwa na chama chake cha siasa kugombea udiwani na fomu yake ya uteuzi haikujazwa kikamilifu. Msimamizi wa Uchaguzi alikubaliana na pingamizi hilo, hivyo kumuengua mgombea.

Tume katika kikao chake cha tarehe 24 Disemba 2018, ilipitia vielelezo vilivyowasilishwa na kujiridhisha kuwa mrufani ni Raia wa Tanzania na kwamba alidhaminiwa na chama chake cha siasa na kwamba fomu yake ya uteuzi ilijazwa kwa ukamilifu na hivyo, kuelekeza arejeshwe kuendelea kuwa mgombea udiwani katika Kata ya Magomeni, Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni

Aidha, Tume ilipokea malalamiko kutoka kwa Ndg. Ngulangwa Eng Mohamed Mshamu wa Chama cha Wananchi (CUF) akipinga  uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Temeke kumuondoa kwenye orodha ya wagombea Ubunge na kumtangaza Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Abdallah Ally Mtolea  kuwa amepita bila kupingwa.

Kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mgombea akitangazwa kuwa amepita bila kupigwa Tume haina mamlaka juu ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi. Hivyo, malalamiko hayo yaliyowasilishwa na Ndg. Ngulangwa Eng. Mohamed Mshamu na pia hayana sifa ya kuwa rufaa.

Taarifa za maamuzi ya rufaa na malalamiko, zimetumwa kwa wahusika kupitia kwa Wasimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri husika.

Imetolewa leo  Tarehe  24 Disemba, 2018 na: 
Giveness Aswile
 MKURUGENZI WA HABARI NA ELIMU YA MPIGA KURA
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images