TWANGA PEPETA NDANI YA VILLA PARK JIJINI MWANZA DESEMBA 28, 2018
↧
↧
DC Chongolo azinduwa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo amezinduwa rasmi kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga inayoendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation ikiwa ni kuhamasisha uzalendo kumuunga mkono Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kauli ya Juni 21, 2018 alipokuwa akipokea gawio la Tsh Bilioni moja na nusu kutoka TTCL Corporation.
Akizungumza DC Chongolo katika uzinduzi huo ulioenda sambamba na burudani toka kwa wasanii mbalimbali, aliwataka wana-Kinondoni kuwa wazalendo kwa kutumia huduma za TTCL ili kukuza uchumi wa Tanzania moja kwa moja kutokana na faida zinazopatikana. Alisema TTCL ni Shirika la umma na linapofanya vizuri kifaida Watanzania wenyewe ndio ufaidika tofauti na makampuni mengine yanayomilikiwa na watu wa nje ya nchi.
"...Mmesikia hivi karibuni Shirika hili lilitoa fedha shilingi bilioni moja na nusu na kuipa Serikali kama gawio, fedha hizi za Serikali hutumika kujenga miundombinu na shughuli zingine za maendeleo kwa Watanzania," alisema DC Chongolo.
Alisema kadri kampuni hii inavyofanya vizuri kifaida na jamii inanufaika hivyo kuwaomba wananchi kutumia bidhaa na huduma za TTCL Corporation ili isonge mbele zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo (katikati) akionesha bango kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, Bw. Ally Mbega wakishiriki. Kampeni hiyo naendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga katika wilaya hiyo usiku huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba akizungumza katika kampeni hizo zilizofanyika katika Uwanja wa CCM Mwinjuma.
Msanii Shilole akiwapagawisha washiriki katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Wasanii Shilole na Man Fongo (kulia) wakiwapagawisha washiriki katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation.
Meza kuu katika kampeni ya Mkoa kwa Mkoa, Rudi Nyumbani Kumenoga ya Shirika la Mawasiliano Tanzania-TTCL Corporation, katika Uwanja wa CCM Mwinjuma, wakishuhudia burudani za wasanii anuai.
↧
WIZARA YA ELIMU YAPIGA MAARUFUKU KUSAMBAZA NYARAKA ZA SERIKALI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema ni kosa kusambaza nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini ya Mamlaka husika, hivyo ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu na za kisheria kwa watumishi watakaobainika kusambaza nyaraka hizo.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifunga semina ya mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu kwa baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo na kusisitiza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa serikali asiyefahamu kuwa kutoa nyaraka za serikali bila idhini ni kosa la jinai.
“Kumekuwa na usambazaji wa nyaraka za serikali katika mitandao ya kijamii bila idhini na kwa bahati mbaya wakati mwingine unakuta nyaraka imewekwa mhuri wa siri lakini bado unaikuta huko, watumishi wa serikali lazima watambue kuwa kuna utaratibu wa kutoa nyaraka za serikali na kuna sheria ambazo zinawabana wale wote wanaotoa taarifa hizo bila kuidhinishwa”alisisitiza Naibu Waziri Ole Nasha.

Mhe. Ole Nasha amewataka watumishi hao kutambua kuwa hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya kazi bila kuwa na kumbukumbu au nyaraka hivyo amewataka kuhakiksha utunzaji mzuri na salama wa nyaraka hizo kwani ni nguzo muhimu katika kufanikisha utendaji wa majukumu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu, Moshi Kabengwe amesema mafunzo hayo yametolewa ili kusaidia watumishi kufanya kazi ambazo zitaleta tija kwa jamii inayohudumiwa na kuondoa changamoto ambazo zimebainika katika utoaji wa huduma.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku tano na yameshirikisha watumishi zaidi ya 50 kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Makao Makuu, Vyuo vya Ualimu vilivyopo Morogoro na baadhi ya watumishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA).
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akizungumza na washiriki wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) waliohudhuria mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamekamilika leo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya siku tano ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu ambayo yamefungwa leo mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya Huduma kwa Mteja na Utunzaji wa Kumbukumbu.
↧
KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA
↧
HAFLA YA UFUNGAJI MAFUNZO (Passing Out) YA KOZI YA MAAFISA NA WAKAGUZI WA POLISI.
↧
↧
MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI APITA BILA KUPINGWA
MGOMBEA Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Utiri wilaya ya Mbinga Aidan Nombo, amepita bila kupingwa kufuatia wagombea wa vyama vingine kushindwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho.
Nombo ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya Chadema kuanzia mwaka 2015 hadi Oktoba 2018 alipojivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM alikuwa mgombee pekee ambaye alijitokeza kuomba kugombea nafasi hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbinga mjini ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Grace Quintine alisema, kwa mamlaka aliyonayo kama msimamizi wa uchaguzi amemteua mgombea wa CCM kuwa diwani wa kata ya Utiri.
Alisema, kwa mujibu wa kifungu cha 45(2) cha sheria za uchaguzi za serikali za mitaa cha mwaka 1979 sura ya 292 amelazimika kumteua Aidan Nombo wa CCM kuwa diwani baada ya kupita bila kupingwa wakati taratibu za kumtangaza rasmi zikisubiriwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwa upande wake Nombo alisema, ushindi huo alioupata bila kupingwa ni ishara tosha kuwa Chama cha Mapinduzi kimekubali sana kwa watanzania na ndiyo sababu inayopelekea hata wagombea wake wa nafasi mbalimbali kushinda kwa kura nyingi na wengine kupuita bila kupingwa.
Alisema, mara atakapoanza majukumu yake,kipaumbele cha kwanza ni kukamilisha miradi ya maendeleo ili iweze kuwasaidia wananchi wa kata ya Utiri kupata muda mwingi wa kushiriki katika kazi za kiuchumi.
Aidha, amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumpa ushirikiano na kuhaidi kuwa ataendelea kuwa mtiifu na mwaminifu kwa chama chake na viongozi ili kwa pamoja waweze kutekeleza Ilani ya Chama ambayo imedhamiria kuondoa kero na changamoto kwa Watanzania.
Alisema, awali alilazimika kujivua uanachama wa Chadema na na hivyo kupoteza nafasi ya udiwani kupitia chama hicho kujiunga na ccm baada ya kuona viongozi wa Chadema wanakifanya Chama kama mali yao binafsi na kuwataka wanachama wengine kutopoteza muda wao ndani ya Chama.
Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Mbinga mjini ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Grace Quintine kushoto akikabidhi cheti cha ushindi kwa diwani wa kata ya Utiri kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Aidan Nombo ambaye alipita bila kupingwa.
↧
BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO
*Ni baada ya kusambaza taarifa ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii kutoka kundi la WCB Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz 'na Msanii mwenzake Raymond Mwakyusa 'Rayvan' kuacha kusambaza taarifa za uongo.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Onesmo Kayanda baada ya wasanii hao kutoa kauli jana ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi baada ya kuwaandikia barua baraza na kuwaomba na wakawaruhusu.
Baraza limekanusha habari zinazosambaa kwenye vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii kuwa limewaruhusu Diamond na Rayvan.
Mnamo Desemba 18 2018, Baraza liliwafungia wasanii hao kutokujiahughulisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kutokana na kutumia kwa makusudi wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa kwa sababu za kimaadili.
Baraza limeendelea kusisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao Diamond na Rayvan kufanya onesho lolote la sanaa ndani na nje ya nchi.
Aidha, baraza kwa mara nyingine linawataka wasaii hao kutii maagizo waliyopewa na kuacha mara moja kupotosha umma kwa kusambaza taarifa za uongo kabla ya hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi yao.
↧
WAZIRI WA UCHUKUZI AENDA KIMYA KIMYA KITUO CHA MABASI UBUNGO,ABAINI UPANDISHWAJI NAULI KIHOLELA
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
HALI ya usafiri katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo jijini Dar es Salaam hasa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka inaonekana kubadilika kutokana na nauli kupandishwa kiholela bila kufuata utaratibu was Serikali.
Uwepo wa madalali katika kituo hicho nao umeelezwa unachangia kuongezeka kwa adha ya usafiri na hivyo abiria kutoa ombi kwa Serikali kuhakikisha kituoni hapo taratibu zinafuatwa.
Hayo yamebainika baada ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe kufaya ziara kituoni hapo kuona hali ya usafiri akiwa kama abiria ambapo hata yeye alipewa nauli mpya ambayo haiko katika bei elekezi.
"Nimefika kitoni hapo saa 11:15 alfajiri nakuzunguka kwenye baadhi ya mabasi na kubaini baadhi ya abiria kulipishwa nauli tofauti na bei elekezi ya Serikali,"amesema Mhandisi Kamwelwe.Amesema baada ya ukaguzi amebaini abiria kulipa nauli tofautitofauti inatokana na kuwepo kwa madalali nje ya kituo.
Hivyo amesema kuna haja yakupekeka mapendekezo bungeni ili kuwepo kwa tiketi za mfumo wa kieletroniki zitakazosaidia kuondokana na ulanguzi unaoumiza abiria.Baadhi ya abiria wamesema kinachosababisha nauli ipande ni madalali wanaokatisha tiketi nje ya kituo.
Mmoja wa abiria Joseph Malisa amesema unapoenda kwenye ofisi au gari husika unaambiwa gari limejaa lakini nje ya kituo unakuta madalali wanauza tiketi za basi hiyo waliodai kuwa imejaa."Unapofika kwenye gari au ofisi zao unaambiwa nafasi zimejaa lakini nje ya kituo madalali wanauza tiketi kwa bei ya juu na mimi nataka kusafiri inanililazimu kukata bei ya juu" amesema Malisa.
Abiria nwingine Emili Msuya amesema kupanda kwa nauli kiholela kumechangiwa na watu wasio rasmi ikiwemo wapiga debe wanaolundikana ndani ya kituo, hivyo Serikali iangalie utaratibu wa kuwaondoa.Meneja wa Kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam Imani Kasagala amesema mabasi yote yanapaswa kuingia ndani ya kituo cha mabasi Ubungo badala ya wamiliki kupaki nje na kutafuta madalali ambao ndio chanzo cha kwa nauli hizo kupanda.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima amesema kuwa abiria wakiona kuna kupandishiwa nauli wanatakiwa kutoa taarifa.Amesema mabasi yote yanakaguliwa na kupongeza Ukaguzi unaofanywa katika kituo hicho.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akiwa katika basi mara alipofanya ziara katika kituo Kikuu cha Mabasi ikiwa ni kuangalia hali ya usafiri kuelekea siku za mwisho wa mwaka,jijini Dar es Salaam.
Askari wa Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akifanya ukaguzi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ramadhan Kailima akipewa maelekezo na Askari wakati alipofanya ziara kuangalia Usalama wa abiria katika mabasi wanayosafiri nayo leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Madereva Wafanyakazi (TADWU) Shaban Mdemu akizungumza na waandishi habari wakati ukaguzi wa mabasi ya mikoani kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Ramadhan Kailima Kailima akizungumza na waandishi wa habari wakati alipofanya ziara katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Akabidhi Vyeti kwa Wahitimu 345 wa Fani ya Uandishi wa Habari Chuo cha Uandishi wa habari DJS
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akikabidhi cheti kwa wahitimu waliofanya vizuri katika vitengo mbalimbali kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism) ,DSJ katika mahafli ya 23 ya chuo hicho iliyofanyika leo 20 Desemba, 2018 katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi( watatu kushoto aliyeshika maiki) akiwatunuku vyeti vya kumaliza Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari wanafunzi kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism) DSJ, mahafali ilifanyika leo chuoni hapo
Wahitimu wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo cha Uandishi DSJ wakivaa Kofia zao mara baada ya kutunukiwa vyeti vyao katika mahafali iliyofanyika leo chuoni hapo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari- MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wanafunzi wahitimu wa stashahada na Astashahada katika fani ya Uadishi wa Habari( hawapo pichani) katika mahafari ya 23 ya Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism ) DSJ iliyofanyika leo katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo na kushoto ni Rais wa Serikali ya wanafunzi katika chuo hicho Ester Zalamula na Mwalimu kutoka chuo hicho.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wanafunzi na wazazi katika mahafali ya 23 ya kutunuku stashahada na Asatashaha katika fani ya Uadishi wa Habari DSJ iliyofanyika leo katika ukumbi wa chuo hicho kilichopo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (Dar es Salaam School of Journalism) DSJ pamoja na Walimu wa chuo hicho mara baada ya kwatunuku vyeti wahitimu 345 wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari katika mahafali iliyofanyika leo chuoni hapo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwaaga wahitimu na Wazazi mara baada ya kutunuku veyti kwa 345 wa Stashahada na Astashahada ya Uandishi wa Habari katika mahafali iliyofanyika leo Desemba 20, 2018, chuoni hapo wapili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo.Picha na Idara ya Habari-MAELEZO
↧
↧
MWENYEKITI WA UVCCM SONGWE AKUTANA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI WILAYA YA ILEJE,ACHANGI LAKI TANO
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, mapema leo amekutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mbali na maagizo na maelekezo mbalimbali aliyowapa, lakini pia aliwachangia fedha taslim shilingi Laki Tano ( 500,000/-) ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM ambapo inahitajika milion 2 kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.
Ndg Kadege amesisitiza hadi januari mwishoni lazima tuwe tumemalizana na jambo la fidia kisha tuanze mchakato mapema wa kupata hati na kuanza kutekeleza mipango yetu ya kuhakikisha UVCCM tunakuwa na miradi mbalimbali na kukuza uchumi na kujitegemea ili kuepukana na hii omba omba toka kwa wadau ambao mara zote wamekuwa na masharti ya kiuchaguzi.
Pia kamati ya Utekelezaji UVCCM wilaya ya Ileje ilimpatia zawadi ya kuku kwa ajili ya Christmass.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege, akikabidhi kiasi cha shilingi laki tano kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje ili kulipia fidia ya eneo la zaidi ya ekari 20 la UVCCM, ambapo inahitajika milion mbili kulipia fidia na baadae taratibu za kupata hati miliki zitafuata.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akipokea Zawadi ya Jogoo wa sikukuu kutoka kwa kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje mara baada ya kukutana nao mapema leo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Songwe ndg Andrew Kadege akisaini kitabu cha wageni mapema leo baada ya kukutana na kamati ya Utekelezaji ya wilaya ya Ileje
↧
WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji wa Mkoa wa Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujenga mazingira rafiki na kuboresha mazingira ya biashara.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha Baraza La Biashara Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo Desemba 21, 2018 katika Chuo cha Mipango.Dkt.Mahenge aliwataka watendaji kuzingatia utendaji wenye weledi, tija na unaovutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo kwa kuzingatia kuwa ndiyo Makao Makuu ya Nchi.“lazima utendaji wetu uwe wa namna bora na upekee katika kuweza kuvutia wawekezaji kwa kuwa na miundombinu rafiki ya biashara na kutatua changamoto zozote zinazoweza kuwakwamisha wawekezaji”.Alieleza Dkt.Mahenge.
Aliongeza kuwa, Halmashauri zote zione umuhimu wa kuboresho mazingira ya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo katika kufikia malengo ya kujenga uchumi endelevu.“Nivyema sasa kila Halmashauri ikaona fursa na kuzitumia ikiwemo zile za kifedha na kuhusisha taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki ili kuona kila lengo linafikiwa na kuwa na uwekezaji wenye tija nchini”.alisisitiza Dkt.Mahenge
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi alieleza umuhimu wa kuzitumia fursa zilizopo Dodoma na kuwa na uwekezaji wenye tija kwa kila eneo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.
“Lazima fursa zilizopo Dodoma zitumike kwa malengo yenye tija kwa kuhakikisha mkoa unabaki kuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ,”Alieleza Kunambi.Aliongeza kuwa Jiji hilo limetenga maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuyapima kulingana na mahitaji ya uwekezaji ikiwemo ya viwanda, Biashara na makazi.Kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kimefayika ili kupitia muongozo wa uwekezaji katika mkoa wa huo hali itakayochochea uwekezaji na kukuza uchumi na kuchochea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Muwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Bw. Patrick Mavika akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Wajumbe wa Baraza la Biashara la mkoa wa Dodoma wakifuatilia kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akizungumzia fursa zilizopo katika Jiji Dodoma wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Bw. Mussa Martine akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
↧
WAGONJWA WA SARATANI WAONGEZEKA KUTOKA 2500 HADI 6500.
Na.WAMJW-LINDI
SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kutoka kipindi cha mwaka 2002 mpaka hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la Wagonjwa wa Saratani kutoka wagonjwa 2500 hadi wagonjwa 6500, kutokana na mitindo tofauti ya maisha na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiwa katika ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya na uhamasishaji kwa wakulima kujiunga na mfuko wa Bima ya afya (#UshirikaAfya) katika Mkoa wa Lindi.
"Kama Serikali, Tumeshtushwa na ongezeko la Wagonjwa wa Saratani na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza, mwaka 2002 wagonjwa wa Saratani nchini walikuwa kati 1500 mpaka 2000, lakini kwa takwimu za mwaka Jana, wagonjwa wa Saratani wameongezeka kutoka 2500 hadi 6500" alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa Serikali imeona upo ulazima wa kuchukua hatua za makusudi katika kupambana na Saratani ya Mlango wa kizazi na magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza yakiwemo shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na ugonjwa wa Kisukari.
Pia, Waziri Ummy alisema kuwa katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa 34 ni wa Saratani ya mlango wa Kizazi, Wagonjwa 12 ni wa Saratani ya Matiti, kibaya zaidi katika kila Wagonjwa 100 wa Saratani, Wagonjwa 80 wanafika wakiwa wamechelewa na wengine ugonjwa ukiwa katika hatua ya tatu au ya nne, hivyo kupona kwao kunakuwa ni kugumu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa maelekezo ndani ya chumba cha kuhifadhi Dawa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi mkoani Lindi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akimjulia hali mtoto aliyefika kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi.
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akikagua miundombinu katika chumba cha X- ray wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati akiongea na wananchi (Hawapo kwenye picha) waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya kwa wananchi.
↧
KUMBUKUMBU
“Hata ingawa ninatembea katika bonde lenye kivuli kizito, Siogopi chochote kibaya,Kwa maana wewe uko pamoja nami; Fimbo yako na gongo lako ndivyo vitu vinavyonifariji.” (Zaburi 23:4)
LUTENI KANALI (MSTAAFU) WILLY JOHN MASOI
Miaka 4 imetimia leo tangu Mwenyezi Mungu alipokuita kwake. Hata hivyo kutokana na upendo wako kwetu tunaamini Baba yetu kipenzi unaendelea kutulinda, kutusimamia na kutuongoza katika kila tufanyalo. Baba, endelea kuimba na Malaika.
Unakumbukwa na mke wako kipenzi Mary-Salome, watoto, wakwe, wajukuu, shemeji, ndugu, jamaa, marafiki na majirani zako.
Raha ya Milele umpe, ee Bwana, na Mwanga wa Milele Uingazie Roho ya Marehemu Luteni Kanali (Mstaafu) Willy John Masoi. Apumzike kwa Amani, Amina. Zab: 23:4
↧
↧
INTRODUCING: JAY DABA FT TABUYA _ NICHEMSHIE OFFICIAL VIDEO
↧
UJUMBE MAALUM KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)
↧
Real Madrid kubeba Klabu bingwa ya Dunia bila Ronaldo
Kwa msimu wa tatu mfululizo klabu ya Real Madrid inafika fainali ya Klabu bingwa ya dunia, lakini safari hii wanaingia uwanjani bila Cristiano Ronaldo ambaye mwanzoni mwa msimu alijiunga na Klabu ya Juventus. Real Madrid wamefika fainali baada ya kuwafunga Kashima Antlers 3-1 siku ya Jumatano.
Katika mchezo wa fainali Real Madrid watacheza dhidi ya Al Ain FC kutoka Falme za Kiarabu. Fainali za Klabu bingwa ya Dunia mwaka huu zinachezwa katika jiji la Al Ain, Abu Dhabi ambapo ndio nyumbani kwa klabu ya Al Ain FC. Al Ain FC wao wamefika fainali baada ya kuwafunga River Plate kwa mikwaju ya penati siku ya jumanne.
Mchezo wa fainali utapigwa leo jumamosi majira ya saa 1:30 Usiku saa za Afrika Mashariki na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football kwenye king’amuzi cha StarTimes pekee.
Pia kutakuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu ambao utapigwa mapema saa 10:30 jioni na kuwakutanisha Kashima Antlers dhidi ya River Plate. Mchezo huo pia utaonyeshwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee.
Wateja wa StarTimes wataweza kuona mechi zote hizi pamoja na Bundesliga kwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 tu kwa watumiaji wa Antenna na kifurushi cha SMART Tsh 21,000 tu kwa watumiaji wa dikoda za Dish. StarTimes pekee ndio wenye kibali cha kuonyesha michuano hii nchini Tanzania.
↧
WAZIRI MKUU AKUTANA NA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU NA WATENDAJI WA WIZARA TATU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Kikao cha Kazi alichokiitisha Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam, Desemba 22, 2018. Kikao hicho kiliwahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu na Watendaji kutoka Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na baadhi ya Taasisi zilizo chini ya Wizara hizo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
↧
↧
DKT. MWANJELWA AELEKEZA KUSIMAMISHA MISHAHARA YA WAAJIRI NA MAAFISA UTUMISHI WATAKAOWASILISHA TAARIFA ZISIZO SAHIHI KWENYE MFUMO WA MALIPO YA MISHAHARA (HCMIS)
Mishahara ya Waajiri na Maafisa Utumishi watakaobainika kuwasilisha taarifa za kiutumishi zisizo sahihi kupitia Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini (HCMIS) itasimamishwa mara moja na Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuwakumbusha waajiri na maafisa hao kuhakikisha wanawasilisha taarifa sahihi na kwa wakati.
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji na kufahamu vema majukumu ya idara hiyo.
Ili kuimarisha nidhamu ya utendaji kazi, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu Serikalini kutosita hata mara moja kusimamisha mshahara wa mwajiri au afisa utumishi yeyote atakaebainika kuwasilisha taarifa zenye udanganyifu na kuwataka kutozifanyia kazi na kuzirejesha mara moja kwa waajiri na maafisa hao.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameainisha kuwa, lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa Ofisi ya Rais-Utumishi hata kosa linapokuwa kwa waajiri, hivyo amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanatenda haki kwa kuwasilisha taarifa sahihi na kwa wakati ili ziweze kufanyiwa kazi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimali Watu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Ibrahim Mahumi (kushoto) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Baadhi ya watumishi wa Idara ya Usimamizi wa Rasimaliwatu katika Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipoitembelea idara hiyo jijini Dodoma kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji

WAZIRI KALEMANI AIBUA SHANGWE IPARAMASA
Na Veronica Simba – Chato
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewasha umeme katika Kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita, tukio lililoibua shangwe na nderemo kwa wananchi wa eneo hilo. Tukio hilo lilifanyika jana, Desemba 21, 2018 kijijini hapo, wakati Waziri akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na kuzungumza na wananchi.
Akizungumza na wananchi, Waziri Kalemani aliwataka wautumie umeme huo katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuendeshea viwanda vidogovidogo vya kusaga na kukoboa nafaka, kuchomelea vyuma na vingine vya aina hiyo. “Umeme huu siyo kwa ajili ya kuwasha taa tu. Ni umeme unaotosha kwa matumizi ya viwanda, hivyo basi utumieni ipasavyo ili kuboresha maisha yenu,” alisisitiza Waziri.
Aidha, aliwahamasisha wananchi ambao hawajalipia, waendelee kulipia ili waunganishiwe huduma hiyo muhimu. Halikadhalika, aliwashauri wananchi wenye matumizi madogo ya umeme, kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ili kuondokana na gharama za kufunga nyaya katika nyumba zao.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita, akiwa katika ziara ya kazi Desemba 21, mwaka huu ambapo pia aliwasha rasmi umeme kijijini hapo.
Wananchi wa kijiji cha Iparamasa wilayani Chato, wakiwa wamejipanga kumpokea na kumsalimia Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), alipowasili kuzungumza nao na kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, akiwa katika ziara ya kazi, Desemba 21 mwaka huu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (mwenye shati la bluu), akijumuika kucheza na wananchi wa kijiji cha Iparamasa wilayani Chato, wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 21, mwaka huu.
Mzee Yohana Masanyiwa akisoma risala kwa niaba ya wazee wa kijiji cha Iparamasa, Wilaya ya Chato; kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa hafla ya kuwasha rasmi umeme kijijini hapo, Desemba 21, mwaka huu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
↧
MGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI APITA BILA KUPINGWA
MGOMBEA Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika kata ya Utiri wilaya ya Mbinga Aidan Nombo, amepita bila kupingwa kufuatia wagombea wa vyama vingine kushindwa kushiriki katika kinyang’anyiro hicho. Nombo ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kwa tiketi ya Chadema kuanzia mwaka 2015 hadi Oktoba 2018 alipojivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM alikuwa mgombee pekee ambaye alijitokeza kuomba kugombea nafasi hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbinga mjini ambaye pia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Grace Quintine alisema, kwa mamlaka aliyonayo kama msimamizi wa uchaguzi amemteua mgombea wa CCM kuwa diwani wa kata ya Utiri. Alisema, kwa mujibu wa kifungu cha 45(2) cha sheria za uchaguzi za serikali za mitaa cha mwaka 1979 sura ya 292 amelazimika kumteua Aidan Nombo wa CCM kuwa diwani baada ya kupita bila kupingwa wakati taratibu za kumtangaza rasmi zikisubiriwa kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kufanya hivyo.
Kwa upande wake Nombo alisema, ushindi huo alioupata bila kupingwa ni ishara tosha kuwa Chama cha Mapinduzi kimekubali sana kwa watanzania na ndiyo sababu inayopelekea hata wagombea wake wa nafasi mbalimbali kushinda kwa kura nyingi na wengine kupuita bila kupingwa. Alisema, mara atakapoanza majukumu yake,kipaumbele cha kwanza ni kukamilisha miradi ya maendeleo ili iweze kuwasaidia wananchi wa kata ya Utiri kupata muda mwingi wa kushiriki katika kazi za kiuchumi.
Aidha, amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kumpa ushirikiano na kuhaidi kuwa ataendelea kuwa mtiifu na mwaminifu kwa chama chake na viongozi ili kwa pamoja waweze kutekeleza Ilani ya Chama ambayo imedhamiria kuondoa kero na changamoto kwa Watanzania.
Alisema, awali alilazimika kujivua uanachama wa Chadema na na hivyo kupoteza nafasi ya udiwani kupitia chama hicho kujiunga na ccm baada ya kuona viongozi wa Chadema wanakifanya Chama kama mali yao binafsi na kuwataka wanachama wengine kutopoteza muda wao ndani ya Chama.
Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Mbinga mjini ambaye pia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Grace Quintine kushoto akikabidhi cheti cha ushindi kwa diwani wa kata ya Utiri kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Aidan Nombo ambaye alipita bila kupingwa.
↧
More Pages to Explore .....