Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Idara ya Uhamiaji Tanzania inaadhimisha Siku ya Wahamaji Kimataifa.

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Siku hii ya Kimataifa ya Wahamaji huadhimishwa Duniani kote tarehe 18/12 kila mwaka ikiwa ni kutambua mchango wa Wahamaji katika kukuza uchumi wa nchi za ugeni (horst country) na wanakotoka (origin) kadhalikaa kuheshimu uhuru na haki zao za kibinadamu.

Katika maadhimisho ya Mwaka huu yanapambwa na kauli mbiu isemayo Uhamaji unaozingatia Utu.

Akizungumza na Michuzi Blog Msemaji wa Idara hiyo Ally Mtanda amesema kuwa katika kuadhimisha siku hii, Idara ya Uhamiaji inafanya Maonesho maalum katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa kutoa pasipoti za kielektroniki kwa Watanzania.

Aidha, elimu kwa Umma kuhusu Uraia, Viza na Vibali vya Ukaaazi itatolewa. Pia Wananchi watapata fursa ya kujua mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda Moshi (Tanzania Regional Immigration Training Academy-TRITA)

"Ninawasihi Watanzania, Taasisi, Makampuni na Mashirika mbalimbali kutumia fursa ya maonesho haya kupata huduma zetu kwa kufika wenyewe na kuepeukana na vishoka" Aliongeza Mtanda.

Maadhimisho hayo huanza Desemba 16 na kufikia kilele chake Desemba 17.
 Picha ya pamoja wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji Duniani yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Grace Rutachokozibwa akitoa huduma katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wahamaji Duniani yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Shule za Jumuia ya Wazazi (CCM) kufundisha ufugaji nyuki

$
0
0
Na Joseph Zablon

Jumuia ya Wazazi (CCM), imeanza kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya ufugaji nyuki kibiashara kwa wanafunzi wa shule zote zinazomilikiwa na jumuia hiyo na kwa wananchi wa wilaya zote nchini kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na pia kutoa ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari

Akizungumza na waandishi wa habari kufuatia ziara ya hivi karibuni ya kukagua utekelezaji wa mpango huo, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dk Edmund Mndolwa alisema ufugaji nyuki licha ya kuwezesha upatikanaji wa asali lakini pia kuna mazao mengi yanayotokana na wadudu hao.

“Tutalenga kwanza kwenye asali ingawa kuna mazao mengi na yenye thamani kubwa kuliko asali” alisema na kuongeza kuwa ameziagiza shule zote 55 za sekondari za wazazi nchi nzima kuhakikisha hadi Aprili 2019 mazao ya kwanza au kabla ya hapo” alisema mwenyekiti huyo.

Alisema anawapongeza viongozi na watendaji wa shule hizo kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwani utakuwa na mchango mkubwa katika kuitoa ajira kla vijana,jamii, pato la ndani la Taifa, upatikanaji wa fedha za kigeni, huanzishwaji wa viwanda vidogo na kupunguza umaskini kwa jamii.

Alisema mpango huo ambao ulibuniwa na yeye mwenyewe, ukakubaliwa na kamati ndogo ya baraza, kisha ukapitishwa na Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Taifa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kuziendesha shule hizo na kuziimarisha kiuchumi tofauti na ilivyokuwa awali.
Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (CCM) Taifa, Dk Edmund Mndolwa (kulia), akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo jijini Dar es Salaam, kuhusiana na kuanza kutekeleza kwa mradi wa mafunzo ya ufugaji nyuki mashuleni kwa shule zinazomilikiwa na jumuia hiyo. Picha na Joseph Zablon.

https://michuzi-matukio.blogspot.com/2018/12/shule-za-jumuia-ya-wazazi-ccm.html

Jumia yazindua Ripoti ya Utalii Afrika 2018/2019

$
0
0
Toleo hili la pili la Ripoti ya Utalii Afrika kutoka Jumia inaangazia masuala mbalimbali yaliyotokea barani kwa mwaka 2017/2018 katika sekta za huduma za utalii, usafiri, ukarimu na anga. 
 
Inatoa mwanga wa kutosha kwenye ukuaji wa kuridhisha wa sekta za utalii na usafiri Afrika iliyoonyesha kwa miaka ya 2017 na 2018 ambapo imeonyesha kuongezeka kwa wageni kutoka mataifa ya nje. Ripoti hii kutoka Jumia inaenda mbele zaidi kwa kuainisha mchango wa sekta hizi kwenye uchumi, changamoto zilizopo na mustakabali wake kwa siku zijazo, ukizingatia sekta ya utalii Afrika inazidi kukua.

“Soko la usafiri kwa njia ya mtandaoni barani Afrika bado linakua na bila shaka linaonyesha matarajio makubwa. Tunayo furaha kubwa kwa mara nyingine tena kuwaletea ripoti hii iliyosheheni masuala tofauti kwenye sekta za ukarimu na anga Afrika. Na hili limefanikiwa kwa ushirikiano wa karibu na washirika wetu wa karibu,” amesema Bw. Joe Falter, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Travel na Food.

Kusoma ripoti kamili bonyeza hapa

Kubadilika kwa hali ya Usafiri wa Ndani

Ingawa bara hupokea 5% ya wasafiri wote wa nje, sekta ya usafiri na utalii Afrika inazidi kuendelea kuonyesha ukuaji mwaka hadi mwaka. Mwaka 2017, bara lilipokea idadi ya juu ya watalii milioni 63 kutoka mataifa ya nje ukilinganisha na watalii milioni 58 mwaka 2016 (9% zaidi ukilinganisha na 2016). Kutokana na unafuu na urahisi wa kusafiri, utalii wa ndani unakua Afrika, takwimu zinaonyesha 60% walisafiri ndani ya mipaka yao ukilinganisha na 40% kwenda nje.

WAZIRI MPINA ATANGAZA NEEMA KWA WAFUGAJI KWA KUGAWA EKARI 972,500 ZA ARDHI

$
0
0

NA JOHN MAPEPELE, RUKWA .

Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina ametangaza neema kwa wafugaji kwa kugawa ekari 972, 500 za ardhi ajili ya wafugaji wanaotangatanga kutafuta malisho ya mifugo yao ili kupata ufumbuzi wa kudumu ambao utamaliza kabisa migogoro baina ya wafugaji na wakulima iliyodumu kwa miaka mingi na kusababisha uvunjifu wa amani.

Akizindua zoezi la ugawaji wa ardhi hizo kwa wafugaji nchini katika Ranchi ya Kalambo wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Waziri Mpina amesema uamuzi huo wa Serikali umekuja kufuata wafugaji wengi nchini kuhangaika kila mahali kutafuta malisho na kusababisha migogoro mingi baina ya wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa ardhi.

“Pia wafugaji wengi walipata harasa kubwa kwa mifugo yao kutaifishwa kutozwa faini kubwa na hata mingine mingi kufa kutokana na kukamatwa kisha kushikiliwa kwa muda mrefu bila huduma muhimu ikiwemo maji, malisho na matibabu kwenye hifadhi mbalimbali za taifa nchini.” Alisisitiza Mpina

Alisema hadi sasa ekari 25,000 zenye uwezo wa kuhifadhi mifugo 6,000 katika Ranchi ya Kalambo mkoani Rukwa wafugaji zimemegawiwa ambapo na jumla ya ng’ombe 3,000 wameshaingia kwenye ranchi hiyo wakati Serikali na wafugaji wenyewe wakiendelea kutafuta suluhisho la kudumu la kupata malisho.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akimwangalia farasi anayetumika kwenye doria katika ranchi ya Kalambo Mkoani Rukwa
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh Luhaga Joelson Mpina akiangalia nyama inayochakatwa katika kiwanda cha SAAFI mkoani Rukwa kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda hichi Dkt Chrisant Mzindakaya .
Kundi la Ng'ombe bora katika ranchi ya Kalambo mkoani Rukwa .

TAMASHA LA MAPINDUZI FESTIVAL LAZINDULIWA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MABINGWA wa burudani ya muziki wa kizazi kipya visiwani Zanzibar jana wameonyesha uwezo wao katika kuiwakilisha vyema sanaa ya muziki nchini. Wasanii hao wamezitumia vyema sauti, kumiliki jukwaa pamoja na kucheza na hisia kali za mashabiki waliobobea katika uwanja wa burudani ambapo yote hayo yalionekana kwa kila msanii aliyepanda kuimba katika Tamasha hilo la 'Safari ya muziki miaka 55 Mapinduzi' .

Akizindua Tamasha hilo Naibu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar  Bimkubwa Sukwa katika Uwanja wa Mpendae Shule ya Sekondari  Wilaya ya Mjini , aliitaka jamii kuunga mkono juhudi za wasanii wa kizazi kipya waliojitolea kwenda kwa wananchi kujitangaza na kuonyesha vipaji vyao.

Alisema umefika muda mwafaka wa Serikali na wadau mbali mbali wa maendeleo ndani na nje ya Zanzibar  kuwa mstari wa mbele kusaidia juhudi za wasanii kwani sanaa ya muziki ni sehemu pana ya vijana wengi kujiajiri wenyewe. Katika maelezo yake Naibu Mstahiki Meya, alieleza kuwa tamasha limebeba tunu ya nchi ambayo ni Mapinduzi ya miaka 55 jambo ambalo wasanii hao wameonyesha uzalendo wa kweli wa kuenzi falsafa ya Mapinduzi.


 Wasanii mbali mbali wa muziki wa kizazi kipya wakionyesha uwezo wao wa kuteka jukwaa huko katika Tamasha la Safari ya Muziki Mapinduzi Festival lililozinduliwa jana katika Jimbo la Mpendae Wilaya ya Mjini Zanzibar.

 NAIBU Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mjini Bimkubwa Sukwa akikagua Timu ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya waliocheza na Timu ya Mpendae ikiwa ni sehemu ya wasanii kuwa karibu na jamii.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Musoma
WAKAZI wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.

Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao

"Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma" alisema Bi. Happy Mjito
 Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzo wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
 Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Maafisa wa Mahakama Kuu-Musoma na Wakandarasi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, wakinyanyua kofia za usalama baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa  Mahakama hiyo uliofikia asilimia 80 na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.2

 Mwonekano wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma ambalo ujenzi wake unaendelea na umefikia asilimia 80 na unatarajia kukamilika ifikapo mwezi April, 2019, kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 6.2.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAFANYA MKUTANO WAO MKOANI MBEYA

$
0
0
ZAIDI ya wakulima 1,032 wameanza kutumia Teknolojia ya Kilimo Hifadhi inayomuwezesha mkulima kukabilaina na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kupata mavuno mengi zaidi tofauti na Kilimo cha mazoea cha kutegemea Mvua Pekee.Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ubia wa kilimo Tanzania mwaka 2018 ulio chini ya baraza la kilimo Tanzania imesema wakulima hao ni kutoka Wilaya za Same, Moshi Vijini, Babati, Monduli na Kiteto ambapo wakulima zaidi ya 2500 walipata mafunzo kuhusu kilimo hifadhi.

Hayo yalielezwa na Mratibu Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe waliohudhulia Warsha ya wadau TAP II iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya ambapo aliwaeleza kuwa teknlojia hiyo inamsaidia mkulima kupata mavuno mengi huku akitumia sehemu ndogo ya ardhi. 

“Mpaka sasa TAP II tumekwisha fanikiwa kutoa mafunzo ya stadi za kilimo biashara kwa wakulima 700 kutoka kwa wilaya 7 za Meru, Kiteto, Babati, Kilombero, Morogoro Vijijini, Namtumbo na Songea Vijijini lengo ikiwa ni kuendelea kuwajengea uwezo wakulima nchini, “Lakini pia AMCO 20  zilijengewa uwezo juu ya masuala ya mikopo na kuwaunganisha na watoa huduma za kifedha kwenye wilaya 10 ambazo ni Sumbawanga, Mpanda, Kyela, Mvomero, Morogoro Vijijini,Kilombero, Ulanga, Mufindi, Iringa na Mbeya” ilisema taarifa hiyo iliyosomwa na Mark Magila mratibu wa taifa wa TAP II.
 Mratibu wa Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TAP II kwa Mwaka 2018 kwa wajumbe waliohudhulia  warsha  ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
 Afisa Masoko wa Ubia wa KIlimo Tanzania Alinanuswe Ambalile aakiwasilisha mada kwa wajumbe waliohudhulia warsha ya wadau wa TAP kuhusu mnyororo wa thamani kwenye mazao.
 Mwakilishi wa Ubia wa kilimo Tanzania kwa  ZONE 1 yenye mikoa ya katavi, songwe na rukwa, Wilson Ernest Loth (wa pili kulia) akiwa na wadau wengine wa TAP wakifuatilia warsha ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja ya wadau wa TAP iliyifanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RC Wangabo atoa tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kwa waathirika wa mvua kali Rukwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amezitahadharisha kaya ambazo bado hazijaweza kurudi katika makazi yao kutokana na nyumba zao kuezuliwa na upepo na mvua kali na kuwafanya kuishi kwa mikusanyiko katika majengo ya serikali juu ya usafi wa mazingira ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko kutokana na uchache wa vyoo katika maeneo hayo.

Amesema kuwa ili kuhakikisha mlipuko huo hautokei ni vyema waathirika hao wakajibana kwa ndugu ambao nyumba zao hazikuathirka na kusisitiza kuwa kujisitiri katika majengo ya serikali ni kwa dharura tu huku wakiendelea kutafuta ufumbuzi wa misaada kwa wadau mbalimbali wa ndani nan je ya mkoa ili kuweza kuzisaidia familia hizo kurudi kwenye makazi yao ya kudumu.

“Tusingependa wandelee kukaa pale, kuna atahari nyingine ya magonjwa ya mlipuko kuwaweka watu zaidi ya 200 sehemu kama ile, miundombinu ya vyoo haitoshi, kwahiyo pale ni pa muda mfupi, jamani wale watu si wana ndugu? Hatuwezi kubanana banana huko, naiachia Halmashauri ndio maana nikasema Mkurugenzi ashuke huku ayaangalie yote haya,” Alisisitiza.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (Kushoto) na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kipeta Galus Gauwo (Kulia) wakitembelea moja ya mabweni ya Wasichana ya Sekondari ya kipeta yaliyoathiriwa na Mvua na Upepo mkali uliotokea usiku wa tarehe 8.12.2018. 
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alipotembelea eneo la maafa yaliyosababisha kuharibiwa kwa nyumba 336 katika vijiji vya kilyamatundu na kipeta.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo alipotembelea eneo la maafa yaliyosababisha kuharibiwa kwa nyumba 336 katika vijiji vya kilyamatundu na kipeta.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akikabidhi misaada kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kipeta Leonard Ndenje wakati alipokwenda kutoa pole kwa waathirika hao hivi karibuni. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

$
0
0
Zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi inayotolewa katika kampeni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, ilikabidhiwa mwishoni mwa wiki kwa Flora Somba ambaye ni mkazi mjini Morogoro . 

Flora anakuwa ni mshindi wa nne kupata zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaama pamoja na Mbwana Mbela mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Akiongea huku akibubujikwa na machozi wakati akikabidhiwa zawadi yake, Flora ambaye anafanya kazi za vibarua kwenye ujenzi kama kubeba zege, alisema Mungu amemtendea miujiza kupitia Tigo Jigiftishe. 

“Nalea watoto wawili peke yangu, mimi ndiyo baba na mimi ndiyo mama. Binti yangu Irene alilazimika kuacha shule kwa sababu sikiuweza kumlipia ada, nashukuru Mungu sasa ataweza kurudi shuleni,asante Tigo kwa kubadilisha naisha yangu” alisema .Flora alisema fedha atakazopata pamoja na kusaidia ada za watoto, atajitahidi kujenga nyumba walau ya vyumba viwili ili kuachana na nyumba za kupanga na kuongeza kuwa fedha itakayobaki atafungua biashara itakayomsaidia kuhudumia familia yake. 

Hafla ya kukabidhi mshindi wa milioni 10 zawadi yake, ilienda sambamba na kuwakabidhi washindi wengine saba wa shilling milioni moja moja kutoka mkoa wa Morogoro zawadi zao .Akiongea wakaati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Tigo kwa Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema promosheni ya Jigiftishe inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu. 
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa kwanza kushoto) akiwa na uso wa furaha na binti yake Irene Hatibu (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake.  Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa. Wengine ni Viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro akijifuta machozi  ya furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo kanda ya Pwani.

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa tatu kulia), akiwa na washindi wa shilingi milioni moja moja kutoka mkoani Morogoro muda mfupi baada ya wote kukabidhiwa zawadi zao. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.

LIVE : MAADHIMISHO YA KILELE CHA MIAKA HAMSINI YA BAKWATA

TCAA YASITISHA SAFARI ZA NDEGE ZA FASTJET, YATOA NOTISI SIKU 28 KUJIPANGA UPYA

$
0
0
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema kuwa kwa sasa wameamua kuwapa notisi ya siku 28 ili waweze kujipanga upya kama wanaweza kuendelea na biashara au imeshawashinda kutokana na mwenendo mzima wa biashara wanavyoiendesha. 

Amesema kuwa Fastjet limepoteza sifa ya kufanya biashara nchini, na wameizuia ndege moja waliyonayo kuruka kutokana na matatizo ya mara kwa mara na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika.

"Tumekuwa tukiwaandikia barua ya kuwataka watueleze kuhusu mwenendo wao wa biashara tangu Fastjet Plc wajiondoe lakini pia shirika limekuwa na madeni mbalimbali ambayo hayajalipwa. Tukiomba watupe mpango wao wa fedha na biashara kwa mujibu wa sheria hawafanyi hivyo," amesema Johari. 
Amesema shirika hilo linadaiwa na watoa huduma wake wengi ikiwemo TCAA inayolidai Sh1.4 bilioni lakini pia halina meneja mwajibikaji ambaye ni mtaalamu wa masuala ya ndege anayepaswa kutoa majibu ya hali ya ndege. 

"Kwa sasa fastjet hawana ndege. Ndege yao tangu jana tumeizuia kuruka kwa kuwa imekuwa ikipata hitilafu mara kwa mara na hawana mtu ambaye anaweza kutoa taarifa kuhusu mwenendo wake jambo ambalo linahatarisha usalama endapo itaruka," amesema Johari.

 Amewaomba wananchi kuepuka kutapeliwa na wale watoa huduma watakaowakatia tiketi za Fastjet wakati hazifanyikazi kwa sasa, hawana ndege wameyumba. Mapema leo FastJet imesimamisha safari zake zote na tayari imetangaza kuanzia Desema 20, kuwarudishia nauli kwa abiria waliokuwa wasafiri Disemba na Januari mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA) , Hamza Johari akitangaza notisi ya siku 28 ya kusudio la kusitisha leseni ya kampuni ya FastJet kutoa huduma za usafiri wa anga Tanzania. 
Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA) , Hamza Johari wakati akitoa ufafanuzi juu ya notisi ya siku 28,
Wanahabari wakiuliza maswali. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mamlaka ya safari za anga Tanzania (TCAA), imetangaza kuwa kampuni ya ndege ya Fastjet imepoteza sifa za kufanya biashara nchini. TCAA imetoa notisi ya siku 28 ya kusudio la kusitisha leseni ya kampuni ya kutoa huduma za usafiri wa anga Tanzania. 

MICHUZI TV: DIAMOND ALICHELEWA NDEGE, TIKETI YAKE IMEANDIKWA ISACK NASIB-ATCL

WAZIRI LUKUVI ALINIKABA NA KUNIPORA MKOBA WANGU ULIOKUWA NA FEDHA-KILUWA.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MSHITAKIWA Mohamed Kiluwa (50) anayekabiliwa na shtaka la kutoa rushwa ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameieleza mahakama ya Wilaya ya Ilala kuwa Waziri Lukuvi alimkaba na kumpora mkoba uliokuwa na fedha zake. 

Kiluwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone amedai hayo leo Desemba 17.2018 wakati akitoa utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas.

Akiongozwa na Wakili wake Imani Madega kutoa utetezi wake, Kiluwa amedai Julai 14 mwaka huu  alipata taarifa kutoka kwa  Shabani Selemani aliyemtaarifu kuwa anatakiwa kupeleka hati zake za viwanja ofisini kwa Waziri Lukuvi, ndipo Julai 16, 2018 alifanikiwa kufika ofisini hapo kwa Waziri na kumkuta akiwa peke yake.

Amedai baada ya kumuelekeza Mahali pa kukaa alimuuliza hati zake ziko wapi na yeye akamjibu kuwa anazo mbia mwenzake ambaye kwa wakati ule alikuwa amesafiri. Aliendelea kudai kuwa, Waziri Lukuvi  alimuuliza tena kuwa hati ziko wapi na kumjibu kuwa mwenzake akirudi ataziwasilisha kwake baada ya majibu hayo Waziri Lukuvi alikaa kimya kama dakika tatu kisha akanyanyuka na kumuuliza kwenye mkoba wake amebeba nini.

Nilimwambia kuna fedha za shoping za ofisini kwangu, baada ya jibu hilo Waziri aliinuka na kuniambia nimpatie mkoba huo, mimi nikawa namwangalia, ikafika wakati alinishika, akaniinua na kuninyanganya begi kisha akalifungua  akatoa fedha na kuziweka juu ya meza."Baada ya kitendo kile cha kuninyanganya begi nikawa napiga kelele nikisema nisaidieni.... Muda mfupi kidogo mlango ulifunguliwa na akaingia mtu mmoja na kuniambia nipo chini ya ulinzi lakini Kabla hajamaliza akaingia mwingine naye akasema nipo chini ya ulizi nirudi nyuma hatua mbili, "alidai Kiluwa.

Baada ya watu hao kuingia Waziri Lukuvi alitoka nje ya ofisi na kumuacha yeye pamoja na watu hao wawili waliongia na kumuweka chini ya ulinzi,  ambapo walianza kujiuliza maswali juu ya nani wamfanye shahidi katika tukio hilo. "Tumfanye nani shahidi,  waliulizana mmoja akajibu muulize mheshimiwa ndipo akatoka nje,  aliporudi akasema Waziri amesema wamwite Sekretari wake ili awe shahidi, Sekretari alikuja na wakamwambia kuwa asome namba za kila fedha iliyopo mezani na ndivyo alivyofanya, "alidai Kiluwa.

Akizidi kujitetea,  Kiluwa ameiomba mahakama imuachie huru kwa kuwa si Waziri Lukuvi wala mashahidi wa upande wa mashitaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi waliothibitisha kuwa alitoa rushwa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

DKT MWAKYEMBE-HATUMTAMBUI MANJI KUWA NI MWENYEKITI WA YANGA

$
0
0
Na Agness Francis blogu ya Jamii. 

SERIKALI imesisitiza mustakabali wa tarehe ya uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kufanyika Januari 13 mwakani kama ilivyopangwa hapo awali. 

Amesema hayo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo katika ukumbi wa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kukubaliana kwa pande zote, shirikisho la Mpira wa miguuTanzania (TFF), Baraza la michezo Tanzania BMT pamoja na uongozi wa Klabu ya Yanga. 

Waziri Mwakyembe amesema kuwa wamehimiza kamati ya uchanguzi ya Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF ishiriki kwa karibu sana na kamati ya uchanguzi ya Klabu ya Yanga waliochaguliwa kusimamia uchaguzi huo ili kuokoa soka la Tanzania kusonga mbele. 

Aidha Dkt Mwakyembe amesema kamaa wizara hawaitambui hoja ya wanachama wa Yanga suala la kuwa aliekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kuwa bado anakaimu nafasi hiyo Klabuni hapo. 

Waziri Mwakyembe amesema kuwa kama alikuwa anajua yeye bado ni Mwenyekiti wa Yanga angepaswa kuhudhuria vikao, lakini takribani kama vikao 10 vya wajumbe hakuhudhuria ambapo pia hajafanya kazi katika Klabu hiyo ndani ya mwaka. 

"Na sisi tumesema Kama wanachama wana mtaka aendele kuwa kiongozi wa Klabu ya Yanga wamchukuliwe fomu ya uchaguzi lakini cha kushangaza mpaka sasa hajachukuliwa, kurudi kwake Manji ni lazima achukue fomu"amesema waziri Mwakyembe. Dkt Mwakyembe amesisizia kuwa wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili kuifanya timu yao kuwa imara na kuepukana na migogoro ya kila siku isiyoleta faida kwao. 

"Yanga ni Klabu kubwa hapa nchini ikiteseka soka la Tanzania litateseka kwa ujumla, wanachama wajitokeze kupiga kura kuchagua kiongozi atakayekuwa ana maslahi na manufaa kwa timu yao"Amesema Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es Salaam, akifafanua mustakabali  kuhusu uchaguzi mkuu wa Yanga, ambapo Serikali iliingilia kati suala hilo kwa kushirikiana na Shirikisho  la mpira  wa Miguu Tanzania  TFF, Baraza la michezo Tanzania BMT pamoja na uongozi wa Klabu ya Yanga, na kuamua ufanyike tarehe hiyo hiyo ilivyopangwa hapo awali, Januari 13 mwakani.

SERIKALI YAONYA WADANGANYIFU KWENYE BIMA ZA AFYA

$
0
0
Serikali imewaonya watu wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu kwenye sekta ya Bima ya Afya nchini ikieleza kuwa mkono wa sheria hautawaacha salama.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, katika mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Makampuni ya Bima ya Afya Tanzania (ATI), Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile alisema kuwa Serikali inatambua kuwa udanganyifu huo hufanywa na baadhi ya watoa huduma za afya na watu wanaotibiwa kwa mfumo huo. Aliongeza kuwa wakati mwingine vitendo hivyo hufanywa kwa ushirikiano kati ya wafanyakazi wasio waaminifu pamoja na wateja.

Dkt. Ndugulile ametoa onyo kwa wanaojihusisha na udanganyifu kwa lengo la kuhujumu huduma za Bima ya Afya, kuwa kitendo hicho ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo jela pamoja na faini

“Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi wa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapinga kwa vitendo rushwa na udanganyifu; na yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo huchukuliwa hatua kali za kisheria. Serikali hii imeelekeza nguvu zake katika kujenga mfumo na taifa lenye uadilifu,” alisema.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile katika picha ya pamoja na wakuu wa taasisi binafsi za bima ya afya, kwenye mkutano wa wadau wa Bima ya Afya nchini uliofanyika Jumatatu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Mwenyekiti wa Kamati ya Makampuni Binafsi ya Bima ya Afya, Bi. Violet Mordichai katika Mkutano wa wadau wa Bima ya Afya nchini, uliofanyika Jumatatu katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Picha  ya pamoja

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA WA DAWA KUTOKA CHINA WENYE THAMANI ZAIDI YA SHILING BILIONI MOJA

$
0
0
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar                  
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed amewataka wafanyakazi wa Bohari Kuu kutumia mifumo ya kisasa ya kuagiza dawa kujuwa takwimu sahihi ya dawa zilizopo kuepuka kununa dawa ambazo zipo kwa wingi katika Bohari na hazitumiki kwa wingi ili kuzinusuru kuharibika .

Waziri Hamad ameeleza hayo Bohari Kuu ya Dawa Maruhubi alipokuwa akipokea msaada wa dawa tafauti na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kutoka kundi la Madaktari wa China wanaofanyakazi Hospitali ya Mnazimmoja na Abdalla Mzee Mkoani.

Alisema kuwa na takwimu sahihi ya dawa, matumizi ya kila siku na sehemu ambazo aina ya maradhi yanawasumbua zaidi wananchi ni hatua muhimu ya kufanikisha kutoa huduma bora ya matibabu kwa wananchi.

Waziri wa Afya aliishukuru Serikali ya Watu wa China kwa misaada mikubwa wanayotowa katika kusaidia sekta ya Afya ikiwemo dawa na vifaa tiba na kufanya tafiti za magonjwa mbali mbali yanayosumbua Zanzibar na hatimae kuyatafutia suluhisho bila ya kuweka masharti.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar  Xie Xiaowu wakisaini hati ya makabidhiano ya dawa zilizotolewa na Serikali ya watu wa China.
 Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu akimkabidhi Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed msaada wa dawa uliotolewa na Serikali ya China, makabidhiano haya yamefanyika Bohari Kuu ya dawa Maruhubi Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed akizungumza na wafanyakazi wa bohari kuu ya dawa mara baada ya makabidhiano ya dawa yaliyofanyika katika Ofisi hiyo Maruhubi Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Muhamed katikati na Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu katika picha ya pamoja na timu ya madaktari wa china wanaofanyakazi Hospitali kuu ya Mnazimmoja. Picha na Makame Mshenga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amezindua Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali.

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa,  jukumu la Baraza la Famasi ni kuleta msukumo wa utoaji huduma bora ya afya kwa mtanzania.  Hili linawezekana kwa kuhakikisha kuwa wanataaluma wanazingatia maadili na nidhamu ya taaluma katika ununuaji, utunzaji na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba vilivyo salama na ubora wa hali ya juu. 

Amesema, anapenda nisisitize kuwa Baraza lione umuhimu wa kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili  tuwe na wanataaluma  wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu katika maeneo yote ikiwamo uzalishaji wa dawa Viwandani ili kwenda sambamba na adhima ya Serikali kuelekea uchumi wa Viwanda.

Ummy anesema anapenda kuwahakikishia kuwa, jamii ya watanzania wanahitaji huduma hii, hali inaonesha kuwa, kupitia takwimu mbalimbali zaidi ya 40% ya wananchi wanapopata tatizo la afya huanza kwenda kupata huduma ya awali kwenye maduka ya dawa (famasi na maduka ya dawa muhimu), hivyo basi kushindwa kuwa na huduma bora katika maeneo hayo  na inahatarisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi. 

"Wataalam wa fani ya famasia ndio wahusika wakuu katika masuala yote yanayohusu dawa katika kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini. Serikali kwa upande wake imeongeza bajeti ya Dawa kutoka Shilingi bilioni 30 mwaka 2015/2016 hadi Tsh 270 Bilioni mwaka 2018/2019, hivyo ni Wataalamu hawa wa Famasi wanaotakiwa kuhakikisha kuwa ongezeko la bajeti linaenda sambamba na upatikanaji wa dawa na matumizi sahihi kwa kuzingatia miongozo ya tiba," Ummy
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali leo Jijini Dar es Salaam.
  Msajili wa Famasi Elizabeth Shekalaghe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi leo Jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa tuzo kwa kwa wajumbe wa baraza la famasi lililomaliza mda wake, Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi.

TANESCO YAANZA OPERESHENI YA KUWANASA "WACHEPUSHA" UMEME, WATU KADHAA "WADAKWA"

$
0
0

NA K-VIS BLOG
SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limeanza operesheni ya na kuwanasa wachepusha umemeteja kadhaa eneo la Kinondoni Kaskazini.

Operesheni hiyo imeanza leo Desemba 17, 2018 ambapo wateja kadhaa wamebainika kufanya vitendo hivyo vya kuchepusha umeme ili usipite kwenye mita kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa matumizi yake na hivyo kuliibia Shirika.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia wateja wakubwa, Mhandisi Frederick Njavike, alisema sio tu wateja binafsi wanaofanya hujuma hizo, lakiini pia taasisi za umma likiwemo shirika moja la umma (jina linahifadhiwa).

Mhandisi Njavike alisema kwa kawaida kila mwisho wa mwaka Shirika hupanga siku za kufanya ukaguzi wa kushtukiza ili kuangalkia sehemu gani TANESCO inapoteza mapato “Tumekuta kuna miundombinu ya TANESCO imechezewa na mbaya zaidi ni kwamba hata taasisi za umma zinashiriki vitendo hivyo, wito wetu tunaomba taasisi zote za serikali kujaribu kupitia miundombinu yote ya umeme na vile vile kuangalia watu waliowapangisha kwenye vitegauchumi vyao.” Alisema. Alisema TANESCO ni shirika la umma hivyo amewaomba wateja na wasio wateja kutoa taarifa kwa wale wote wanaochezea miundombinu kwani watakuwa wamesaidia shirika lao kuokoa fedha kutokana na wizi huo.

Wataalamu wa TANESCO wakichunguza moja ya vifaa vilivyohujumiwa ili kufanya wizi wa umeme huko Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa TANESCO anayeshughulikia wateja wakubwa, Mhandisi Frederick Njavike (kulia), akizunhumza jambo na Afisa Uhusiano wa TANESCO, Bi. Samia Chande, wakati wa operesheni hiyo.

 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BARABARA YA MORO- DOM KUFANYIWA USANIFU ILI KUJENGWA UPYA

$
0
0
Na John Nditi, Morogoro
NAIBU Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa amesema , Serikali inatarajia kufanya usanifu wa  barabara ya Morogoro- Dodoma yenye urefu wa kilometa zipatazo 259 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa ajili ya kupata michoro na gharama halisi ili kujengwa  upya kwa   viwango  cha ubora   na mahitaji ya sasa .

Naibu Waziri alisema hayo  mjini Morogoro  alipofanya ziara ya ukaguzi wa matengenezo ya barabara  katika maeneo mbalimbali kutoka Dodoma hadi Moropgoro  yakiwemo ya Kibaigwa , Gairo  na kuangalia shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa Magereza  barabara ya Morogoro- Dodoma .

Alisema , licha ya kuendelea kuihudumia   barabara kuu hiyo ,  kwa sasa Serikali imekuja na mpango mwingine wa kufanya usanifu kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019 ili kupata michoro ambayo itaelezea  gharama halisi ya kujenga barabara mpya katika  kiwango cha ubora na mahitaji ya sasa.

Naibu Waziri alisema,  Serikali inatenga  fedha nyingi kila mwaka fedha kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu ikiwemo ya Morogoro- Dodoma  ili ziweze  kutoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo ambapo kwa baabara hiyo iliyojengwa miaka zaidi ya 30 iliyopita kwa hali yake ya  sasa imechakaa  na kuzeeka.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akipata maelezo  ya   Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya  Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia) alipokagua  shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara  kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni na (  anayemfuatia Naibu Waziri ) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti)  akisisitiza  jambo wakati akikagua shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara  kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni na ( wapili kushoto) ni Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga.
 Naibu  Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa ( kaunda suti) akikagua  shughuli za  ujenzi wa mizani mpya ya  kisasa  eneo la  Dakawa  Magereza  barabara kuu ya Morogoro- Dodoma  hivi karibuni akiongozwa na  Mhandisi mkazi wa Kampuni ya uhandisi ya  Ambicon , Mustafa Kasmir ( kulia)  akiambatana na  Meneja wa Wakala wa Barabara ( TANROADS )  mkoa wa Morogoro,   Mhandisi Doroth  Mtenga ( wapili kushoto)  pamoja na Wakala wa Mradi kutoka Kampuni ya Group  Six International Ltd , Mhandisi Abdallah Rashid.( Picha na John Nditi).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

UJERUMANI YATOA MSAADA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KIBINADAMU ZA WFP KWA WAKIMBIZI NCHINI TANZANIA

$
0
0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limepokea mchango wa Euro milioni 3.25 kutoka Jamhuri ya Kifederali ya Ujerumani ili kusaidia kazi yake ya kuhudumia wakimbizi na watafutao hifadhi nchini Tanzania kwa mwaka 2018-2019.
“WFP inatoa shukrani za dhati kwa mchango huu mkubwa kutoka kwa Serikali na watu wa Ujerumani,” alisema Michael Dunford, Mwakilishi wa WFP nchini. “Ujerumani ni mshirika muhimu wa programu za WFP ambazo hutoa msaada wa chakula ulio muhimu sana kwa wakimbizi waishio nchini Tanzania.”

WFP hutoa mgao wa chakula cha kila mwezi unaojumuisha nafaka, kunde, mafuta ya mimea na chumvi na vilevile vyakula vya nyongeza vilivyoongezewa virutubisho kwa ajili ya akina mama wajawazito walio hatarini na akina mama wanaonyonyesha, watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, watu wenye utapiamlo wanaoishi na VVU/UKIMWI na wagonjwa waliolazwa hospitali. Licha ya hayo, biskuti zenye kutoa wanga wa kiwango cha juu pia hugawiwa kwa wakimbizi walio katika vituo vya muda.

Tanzania inawahifadhi takribani wakimbizi 290,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, hasa katika kambi za wakimbizi za Nduta, Nyarugusu na Mtendeli katika Mkoa wa Kigoma, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Zaidi ya asilimia 70 ya wakimbizi hawa wanatoka Burundi, na waliobaki wanatoka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

“Nchi yangu inajivunia kuiwezesha WFP kuwahudumia wale walio katika uhitaji ambao wamepata hifadhi nchini Tanzania,” alisema Dkt. Detlef Waechter, Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania. “Ni muhimu sana kuweka sawa hali ya kisiasa nchini kwao kabla wakimbizi hawa hawajarudi nyumbani kwao kwa hiyari na usalama.”

Upungufu wa fedha ulilazimisha kupunguzwa kwa mgao wa chakula kati ya Februari, 2017 na Oktoba, mwaka huu, kwa hiyo, kuongezeka huku kwa misaada kutoka kwa wahisani, ikiwemo nchi ya Ujerumani, kumewezesha mgao huo kuanza kutolewa tena katika ukamilifu wake. WFP inaendelea kukusanya fedha ili mgao wa chakula usipunguzwe katika miezi ijayo. 

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images