Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

Wajasiriamali 777 Wajengewa Uwezo na MKURABITA Singida

$
0
0
Wajasiriamali 777 wa mjini Singida wamenufaika na mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge (MKURABITA) ili kuwajengea uwezo wa kurasimisha biashara  zao na kutoa mchango stahiki katika ujenzi wa uchumi.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wajsiriamali hao mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuwawezesha wajasiriamali kufanya biashara kwa tija na kuchochea maendeleo.

"Mafunzo haya yametolewa kwa namna itakayowawezesha wajasiriamali wetu hapa Singida kuwa na mfumo bora wa kufanya biashara  na kuleta mabadiliko makubwa kwa wajasiriamali" Akifafanua amesema kuwakila majasiriamali anapaswa kuwa mwadilifu, mzalendo  na mwenye mpangilio mzuri wa namna yakuendesha biashara yake, anayethemini muda, anayetii sheria na kujali wateja anaowahudumia ili kuchochea ukuaji wa Biashara husika.

Aliongeza kuwa wananchi mkoani humo wana imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa inajali ustawi wa wanyonge ndio maana imeweka mkazo katika kuwawezesha kupitia mipango na pragramu mbalimbali zinazotekelezwa ikiwemo uwezeshaji kupitia MKURABITA unaolenga kuwapa ujuzi wa namna bora ya kufanya biashara.
Aidha aliwaasa wajasiriamali hao kuhakiksiha kuwa wanatumia vizuri mikopo watakayopata kutoka katika taasisi za fedha ili iweze kuwasaidia kukuza biashara zao na kufikia malengo kusudiwa ya kuanzisha biashara husika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) Bw. Japhet Werema akizungumzia faida za mafunzo kwa wajasiriamali hao zaidi ya 777 waliopatiwa mafunzo ili waweze kurasimisha biashara zao.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Bi. Severina Kilala akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 Mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtunuku cheti Bw.Haji Ramadhani ambaye ni mjasiriamali wa mjini Singida wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini humo baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa mafunzo mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 777 mjini Singida baada ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge ( MKURABITA) kuwajengea uwezo ili waweze kurasimisha biashara zao na hivyo kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wa Taifa.


Puma Energy yaendelea kung’ara tuzo za Mwajiri Bora

$
0
0
Kampuni ya Mafuta ya Puma Energy Tanzania imeendelea kung’aa kwenye Tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 baada ya kuibuka mshindi wa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (the Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018.

Pamoja na tuzo hiyo kampuni hiyo ambayo imekuwa miongoni mwa wadhamini wakubwa na tuzo hizo, pia ilifanikiwa kutwaa tuzo nyingine ya mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations). Kila mwaka Chama cha Waajili Tanzania (ATE) kimekuwa kikiandaa tuzo maalum kutambua wanachama wake wake ambao wanafanya vizuri katika masuala mazima ya rasilimali watu ikiwemo kuwa sera nzuri katika nyanja hiyo.

"Mafanikio ya Puma katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu kwa kiasi kikubwa yanachangiwa na jitihada madhubuti zinazofanywa na wafanyakazi wetu ikiwemo kujitoa kwa dhati katika kutimiza majukumu yao," alisema Dominic Dhanah, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. 

Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah akitoa neno la shukrani wakati wa Tuzo za Mwajiri Bora (EYA) za mwaka 2018 zilizoandaliwa na Chama cha Waajili Tanzania (ATE) na kufanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Puma Energy ilifanukiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations).
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah (kulia) pamoja na Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Loveness Hoyange wakionyesha tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations) mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo kwa niaba ya kampuni hiyo.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah (wa tatu kulia waliokaa), Meneja Rasilimali Watu Kampuni ya Puma Energy Loveness Hoyange (kulia kwake) wakifurahia pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya ushirikishaji mzuri wa wafanyakazi (Employee Engagement Company of the Year 2018) kwa mwaka 2018 pamoja na Tuzo ya Mahusiano mazuri ya kikazi (Industrial relations) kwenye wa hafla hiyo.

NAIBU WAZIRI MHANDISI HAMAD MASAUNI AFANYA ZIARA WILAYANI MKALAMA MKOANI SINGIDA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na watumishi wa Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida leo   baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mbunge  wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula, akiwa ndani ya gari la polisi  muda mfupi  baada  ya  kukabidhiwa na  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani  ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), alipokuwa ziara katika Wilaya hiyo, lengo ikiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara za wizara, mkoani Singida. 
 Mbunge  wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula(kushoto), akimshukuru Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya  Nchi, Mhandisi  Hamad Masauni baada ya kushuhudia gari la polisi (pichani), lililoletwa  kwa  ajili  ya  shughuli  za kudhibiti uhalifu, Naibu  Waziri yupo mkoani Singida  lengo ikiwa ni kukagua  shughuli  mbalimbali  zinazofanywa  na  Idara  za wizara.
 Naibu Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza   na Askari Polisi wa Kituo cha Nduguti kilichopo  Wilayani ya Mkalama, mkoani Singida leo   baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi  ya  kukagua shughuli zinazofanywa na Idara  zilizopo  chini  ya  wizara. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Polisi wilayani Mkalama, John Ntalima, mkoani Singida Leo, ikiwa  ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MAGEREZA YAZINDUA MAKAKATI WA KUMALIZA UHABA WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI HILO, DODOMA LEO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akikata utepe kuashiria  uzinduzi wa miradi ya ufyatuaji matofali za kuchoma na hydrofom kitaifa kutegemeana na hali ya udongo katika kituo husika. Zoezi la uzinduzi kitaifa limefanyika leo Desemba 6, 2018 katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga, Dodoma. Kulia ni Kamishna wa Fedha na Mipango,Gedeon Nkana, Kamishna wa Miundombinu ya Magerezana Uzalishaji, Tusekile Mwaisabila na Mkuu wa Gereza Isanga ACP Keneth Mwambije. Kushoto ni Kamishna wa Huduma za Urekiebishaji Augostine Mboje na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum.
Mtaalam na msimamizi wa mradi wa ufyatuaji tofali katika Gereza Kuu Isanga Dodoma Sajin Modern Mwakialinga wa Gereza Isanga akitoa maelezo kwa viongozi mbalimbali wa Jeshi la Magereza  juu ya namna mradi huo unavyotekelezwa.
Baadhi ya wafungwa waliopo katika programu za urekebishaji ambao wanafundishwa kufyatua, kuchoma tofali na wengine kujenga nyumba wanaotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba za kujitolea katika Gereza Kuu Isanga mkoani Dodoma wakionesha umahiri wao wa kufyatua tofali  leo Desemba 17, 2018.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi la magereza nchini.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akiangalia ubora wa tofali  za kuchoma alipofanya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za maafisa na askari wa Jeshi hilo ili kukabiliana na tatizo la makazi kwa watumishi.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Makamishna, Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Mikoa ya kiutawala ya Magereza waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa programu ya ufyatuaji tofali kitaifa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kujitolea za maafisa na askari wa Jeshi hilo. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Gereza Kuu Isanga Dodoma leo Desemba 17, 2018.Katika hafla hiyo Kamishna Kasike amewataka Wakuu wa Magereza wa Mikoa yote nchini kwa wale ambao hawajaanza utekelezaji wa agizo la ufyatuaji tofali kuanza mara moja kwa kuzingatia hali ya udongo katika maeneo yao. Jeshi la Magereza linaupungufu wa nyumba za watumishi zaidi ya 9000 kote nchini.
Muonekano wa sehemu ya tofali 100,000 moja zilizofyatuliwa na kuchomwa tayari kwa ujenzi wa nyumba 30 za maafisa na askari wa Gereza Kuu Isanga na Ofisi ya Mkuu wa Magereza wa Mkoa wa Dodoma.Nyumba hizo zitakuwa na vyumba vitatu kila moja na mambo mengine muhimu kama sebule, choo, bafu, jiko na store na zinatarajiwa kukamilika kwa mwaka 2019. 
Picha zote na Jeshi la Magereza)

MAAFISA UGANI WANOLEWA KUFUFUA KAHAWA KILIMANJARO

$
0
0

Na Vero Ignatus,Kilimanjaro.

Mafunzo yametolewa kwa Maafisa Ugani 30 kutoka katika kata mbali mbali za wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kujua kanuni bora za kilimo cha kahawa yatakayosaidia kufufua zao hilo na kuhamasisha kilimo cha zao hilo ili kukuza pato la mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Dafrosa Sanga ni Meneja Uendeshaji wa Shirika la Cafe Africa lililoendesha Mafunzo hayo amesema kuwa wameamua kujikita katika zao la kahawa kwani ni moja kati ya mazao yaliyopewa kipaumbele na serikali ikiwemo Korosho,pamba na chai.Dafrosa amesema kuwa mafunzo hayo huendeshwa kwa vitendo kuanzia kwenye kutesha miche,kuvuna na mnyororo wa thamani ili Maafisa Ugani hao waweze kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha kahawa.

Kipi Warioba ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi amewataka Maafisa Ugani hao wasikae Maofisini bali waende kupeleka ujuzi na marifa waliyoyapata kwa wakulima ili kuongeza uzalishaji wa kahawa kwani uchumi wa mkoa huo umekua ukitegemea zao hilo kwa miaka mingi.Warioba alisema kuwa soko la kahawa la dunia bado linafanya vizuri hususan kwa kahawa bora imekua ikipata bei nzuri ukilinganisha na kahawa isiyokua na ubora imekua ikipata bei ya chini.

Mwakilishi wa Mafisa Ugani hao Magnus Mwang`ata alisema kuwa wanatarajia kuandaa mpango kazi pamoja na kuwa na mashamba darasa kila kata ili kuweza kuwaelimisha wakulima juu ya kilimo bora cha kahawa kitakachowasaidia kuinua pato la mkulima.

Magnus alisema kuwa Mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza mbinu mpya za kilimo cha kahawa kwani teknolojia hubadlika kadiri miaka inavyokwenda hivyo ushirikiano wa Cafe Africa na Jukwaa la Wadau wa Kahawa (ANSAF) utawajengea uwezo Maafisa hao kukuza zao la kahawa.

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kipi Warioba akiotesha Kahawa katika shamba darasa katika kijiji cha Mwasi Kusini

TaSUBa, Jhikoman wazindua albam ya Safari ya gitaa baridi

$
0
0
Na Andrew Chale, BAGAMOYO
MWANAMUZIKI nguli wa miondoko ya Afro reggae, Jhikolabwino Manyika maarufu Jhikoman kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Ijumaa ya 14 Desemba, 2018, amezindua rasmi albam yenye nyimbo sita tukio lililofanyika mjini Bagamoyo,Mkoani Pwani.

Jhikoman  ambaye anatoka kwenye lebo ya AfriKabisa ameweza kuonesha ukongwe  katika muziki huo kwa kufanya kazi pamoja na vijana wadogo ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Sanaa TaSUBa  na kukonga nyoyo mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo.

Albam hiyo ina beba nyimbo kama: Mara ya kwanza, Ndotoni, Safari, Bad mind,Time to love na Kuagana zilizo kwenye mtindo wa regge.

Katika uzinduzi huo, Msanii Vitalisi Maembe na wengine wakiwemo Sinaubi Zawose, Voice of Revolution, K’Gwana Shija pamoja na Bocka T waliwez kupamba jukwaa katika kusindikiza uzinduzi huo kwa kuimba nyimbo zao mbalimbali.

Jhikoman ameshukuru uongozi wa TaSUBa kwa ushirikiano  wa kutayarisha albam na kuirekodi kupitia studio ya chuo hicho.

“Wasanii waliopiga vyombo na kuimba na mimi hapa jukwaani  ndio nilioshirikiana nao katika albam hii ni wa TaSUBa. Nashukuru kwa Uongozi kuwapa fursa ya kufanya kazi hii. Lakini pia nawashukuru Watanzania kuendelea kutuunga mkoni katika kazi zetu na kwa sasa albam itakuwa inapatikana pale Afrikakabisa hapa Bagamoyo na maeneo mengine tutaendelea kuwatangazia” alieleza Jhikoman.

Na kuongeza albam hiyo imebeba ujumbe mbalimbali  hivyo itakuwa inaburudisha na pia kufundisha Jamii.

Msanii Jhikoman wa Afrikabisa akishirikiana na Wanafunzi wa TaSUBa wakiimba baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albam ndogo ya Safari ya Gitaa Baridi iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa TaSUBa na Afrikabisa wakati wa uzinduzi huo Usiku wa Ijumaa ya 14 Desemba 2018. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU JIJINI DAR ES SALAA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu (CC) ya CCM kilichokutana jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.PICHA NA IKULU

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ZANAKI WATEMBELEA HIFADHI ASILI YA MAGAMBA LUSHOTO, TANGA

$
0
0
 Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga ni moja ya vivutio vya hifadhi 12 za mazingira asilia vinavyosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Watu wengi wamekuwa wakisahau kuwa utalii wa ikolojia nao unafaida kwa jamii yetu ili iweze kujifunza mambo mbali mbali kuhusu misitu na viumbe hai. 

Wakizungumza kwa wakati tofauti mara baada ya kutembelea hifadhi ya mazingira ya Magamba, Mfaume Salehe Msasa amesema “Kuwa Coordinator wa ni bahati kwangu na furaha pia kwa kuwa nimejifunza vitu vingi sana tangia nimeaza kuvolunteer @greathopetz pia naendelea kujifunza kwamaana kuwa kujifunza hakunaga mwisho," Kwa kwaida kila mwaka @greathopetz hua tunatoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi pamoja na shule zinazofanya miradi bora zaidi. Mwaka huu tulikua na shule 100 ambazo zimefanya mradi na shule ambayo imefanya mradi bora zaidi nakuweza kuwa mshindi wa kwanza ni Shule ya Sekondari Zanaki.

 “Miradi ya mwaka huu imekua ni ya tofauti kubwa kwa mshindi wa mradi wa Uwezo Award kupata zawadi nyingi na wamepewa safari ya kitalii ya kwenda msitu wa Magamba kwa kudhaminiwa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). 

 Nae Meneja wa Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) ameshukuru jinsi wanafunzi walikuwa na moyo wa kujifunza kuhusu mazingira na kuomba shule pamoja na wazazi waweze kujitokeza kuwapeleka watoto wao katika vivutio mbali mbali vya utalii wa ikolojia ambao watu wengi wamekuwa wakiusahau.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba (katikati) akitoa maelezo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Zanaki jijini Dar es Salaam waliopata ufadhili wa kutembelea hifadhi hiyo waliopewa na Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kupitia mradi wa Uwezo Award uliendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la Great Hope Foundation. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG - Lushoto.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akiwa ameongozana na kuwapa maelezo wanafunzi na  wanahabari waliokuwa katika ziara hiyo.
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Mazingira Asili ya Magamba iliyopo Lushoto, Tanga Samiji Mlemba akitoa maelezo machache wakati wanafunzi hao walipofika kituo cha Mshai wakielekea katika kilele cha mlima Kigulu Hakwewa.
Wanafunzi wakifurahia katika mlango wa pango la Wajerumani walilolitumia katika vita vya kwanza vya dunia vilivyotokea mwaka 1914 - 1918.


RAIS DKT MAGUFULI AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA BAKWATA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry shilingi milioni 30 taslimu wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Hati ya Heshima Mzee Mohamed Songambele, mmoja wa wazee mashuhuri wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. Wengine katika meza kuu ni pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na waumini wa Kiisalamu kinamama akishiriki katika dua wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018. Kulia kwake ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa na Jajji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary bin Zubeiry na viongozi mbalimbali wakishiriki katika dua wakati wa maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam leo Desemba 17, 2018.

BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 17/12/2018

VOA SWAHILI: Fastjet yasimamisha safari za ndege Tanzania

NEWS ALERT: NDEGE MPYA AIRBUS A220-300 IKIWA TAYARI KULETWA TANZANIA KUTOKA CANADA

$
0
0
 Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi ikiwa imebatizwa jina la Ngorongoro
 Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Mmoja wa wajumbe wa Tanzania kwenye akipata maelezo ya Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
 Ujumbe wa Tanzania ukiwa na Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi
Ndege mpya aina ya Airbus A220-300 ikiwa kwenye matayarisho ya mwisho mwisho kabla ya kuanza safari kutoka Montreal, Canada, kuja Tanzania tayari kuanza  kazi

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 18,2018

WAZIRI MBARAWA AKAGUA MRADI WA MAJI KIMARA BONYOKWA,ATOA NENO KWA DAWASA

$
0
0
Na Stahmil Mohamed

Dawasa wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kufanikisha malengo ya miradi kama ilivyopangwa na serikali ili kufanikisha malengo iliyojipangia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Proffesa Makame Mbarawa alipokuwa katika ziara yake ya kukagua maeneo mbalimbali yanayojengwa miradi ya maji iliyoanzishwa ikiwemo Kimara Bonyokwa,Kinzudi ,Salasala na Saranga ambako amebaini chamgamoto mbalimbali zinazosababishwa na wafanyakazi wenyewe wa Dawasa ikiwemo kuchelewesha kufungia wateja mabomba,kuandikisha wateja hewa pamoja na,kuwalipisha gharama zisizostahili

Hata hivyo Prof Mbarawa amemtaka Meneja mradi Mhandisi Ramadhani Mtindasi kushughulikia dosari zilizojitokeza kwa muda wa siku tatu na ikiwa hajatekeleza maagizo yake atawasimamisha kazi kutokana na uzembe wa kuwacheleweshea wananchi huduma.

Pia Professa Mbarawa amewataka wananchi kutoa taarifa mara moja iwapo watatakiwa kulipa gharama kwani huduma ya ufungaji mabomba ni bure .Professa Mbarawa ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa wahandisi katika maeneo yote yanayochimbwa mitaro kwa ajiri ya kupitisha mabomba kutowawekea vikwazo ili mradi ukamilike kwa wakati.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha mabomba wakati alipokagua maeneo ya mradi wa maji Kimara Bonyokwa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya mabomba yanayotumika katika mradi huo.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akikagua maeneo mbalimbali katika mradi wa maji unaoendelea Kimara Bonyokwa.
Waziri wa Maji Mh. Profesa makame Mbarawa akiangalia mabomba hayo.
Moja ya matenki ya kuhifadhia maji yaliyojengwa katika mradi huo.


MICHUZI TV: SERIKALI YAJA NA MIKAKATI MITATU KUBORESHA BIMA YA AFYA


MICHUZI TV: CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE CHAKUTANA NA WADAU WA ARDHI, PROF. KIRONDE ATOA NENO...

MASHEIKH WA BAKWATA MIKOA YOTE NCHINI WAMPONGEZA MUFTI KWA KUWAUNGANISHA

$
0
0
*Ni kupitia kauli mbiu yake ya Jitambue,mabadilika,acha mazoea...Makonda atoa neno


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MASHEIKH wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania( BAKWATA) katika mikoa yote ya Tanzania wamempongeza Sheikh Mkuu Aboubakary Zubeiry kutokanana namna ambavyo amejenga umoja na mshikamano ndani ya baraza hilo.

Wametoa kauli hiyo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kutimiza miaka 50 ya BAKWATA tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968.Akizungumza kwa niaba ya masheikh wa mikoa, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema wanampongeza wanampongeza Muft Zubeiry kwa namna ambavyo amefanya mabadiliko makubwa ya kuwaunganisha Waislamu nchini.

"Wakati leo tunasheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa BAKWATA ,salamu za kipekee tunazipeleka kwa Mufti wa Tanzania kwani maadhimisho hayo yanamkuta yakiwa mikononi mwake."Chini ya Mufti wetu Sheikh Zubeiry BAKWATA imekuwa mpya,na walio chini yake tunapendana,tunaheshimiana na tunajitambua .Kupitia kauli mbiu yake ya Jitambue, Mabadilaka,Acha mazoea hakika imetusaidia kutubadilisha na kila mmoja wetu anajua majukumu yake," amesema Sheikh Alhad.

Amesisitiza kupitia Mufti wa Tanzania BAKWATA imeunganishwa na walio chini yake wamekuwa waaminifu na walio tayari kuhakikisha baraza hilo linasonga mbele kimaendeleo.Pia amesema kuwa BAKWATA kwa sasa wamekuwa na uhusiano mzuri na taasisi nyingine na chini ya Mufti Zubeiry kuna maendeleo makubwa yanaendelea kufanyika ukiwamo wa ujenzi wa msikiti mkubwa ambao unajengwa katika makao makuu ya baraza hilo jijini Dar es Salaam.

TAEC YAFUNGA VITUO 69 VYA AFYA TANZANIA BARA

$
0
0
Na Vero Ignatus, Arusha 


Tume ya nguvu za Atomic Tanzania (TAEC) imefungia vituo 69 vya afya Tanzania bara kwa kutotimiza vigezo vya kuendesha vituo hivyo

Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa tume ya nguvu za atomic Tanzania Dkt. Wilbard Muhogorawakati akifungua mafunzo hayo ya kitaifa ya kinga ya mionzi kwenye uchunguzi wa magojwa kwa madaktari kutoka Tanzania bara ambayo yamefanyika jijini Arusha 

Amesema sheria ya nguvu za atomic inatoa vipengele ambavyo vinataka mafunzo kwa wafanyakazi wote waliopo kwenye sehemu ya mionzi yaweze kufanyika kwa kuwa kinga ya mionzi itatolewa kwa watu wrote."Mpaka sasa tumefungia vituo 69 kwa kutokuwa na leseni na mafunzo kwa wafanyakazi wanaotumia vipimo vya diology, na kutokuwa na ubora wa maamshine na majengo hiyo ndo sababu iliyofanya tukafungia vituo hivyo" alisema Dkt. Wilbard

Amewataka waajiri kuwapeleka wafanyakazi wao kwenye mafunzo ya kinga ya mionzi ili kuweza kupata elimu na hiyo imewekwa kila baada ya miezi mitatu kwa kila mkoa.Kwa upande wake Bakari Msongamwanja kutoka taasisi ya mifipa na mishipa ya fahamu Moi amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatawasaidia kujua umuhimu wa kumlinda mgonjwa na waliowazunguka na kupitia elimu hiyo watawalinda wagonjwa

Aidha amesema kupitia mafunzo hayo ataenda kuisaidia jamii hasa katika kutoa elimu kwa jamii na kupunguza changamoto zinazotokana na madhara ya mionzi.Kelvini James ni mmoja wa mshiriki ambaye ametokea hospital ya Ikonda amesema umuhimu wa mafunzo hayo yatasaidia kuwalinda wao kujikinga na madhara ya mionzi ambapo changamoto ambayo imekuwepo ni wagonjwa wanaokwenda hospitali kutokujua namna ya kujikinga na mionzi

Hata hivyo amewataka waajiri kutimiza wajibu hasa kwa wafanyakazi kuwa na elimu ya kinga ya mionzi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya vituo vya afya hapa nchini.Hata hivyo mafunzo hayo ni kwa ajili ya vituo vya afya na yataendelea kufanyia na watu wa migodini na viwandani pamoja na kufanya ukaguzi maeneo mbalimali hapa nchini.

WAZIRI MKUU AZUNGUMZIA UONGOZI WA SHEIKH MKUU ALIVYOZIMA MIGOGORO KATIKA MISIKITI, AGUSIA MCHANGO WAO

$
0
0
Na Said Mwishehe ,Globu ya jamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amempongeza Mufti wa Tanzania kwa namna ambavyo uongozi wake umemaliza migogoro ambayo ilikuwa inaibuka kwenye misikiti mbalimbali nchini na kwamba kwa sasa Waislamu ni wamoja.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kuzungumzia hali ya amani nchini ambayo msingi wake unatokana na viongozi wa dini zote ambao wamekuwa wakihimiza umoja na mshikamano.

Majaliwa amesema hayo jana mbele ya Rais Dk.John Magufuli aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za BAKWATA kufikisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake Desemba 17 mwaka 1968 ambapo amesema dini zote zimekuwa mstari wa mbele katika kushiriki katika maendeleo nchini.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Mufti wa Tanzania ambavyo chini ya uongozi wake ambavyo amesaidia kuwafanya Waislamu nchini kuwa wamoja na kushiriki kwenye maendeleo ya nchi yao.

"Leo hii tunashudia chini ya Mufti wa Tanzania,hatusikii migogoro ambayo tulikuwa tunaisikia siku za nyuma.Kumetulia na mambo yanakwenda vizuri.Hongera Mufti Sheikh Aboubakary Zubeiry kwa uongozi wako mahiri.Tangu uwe kwenye nafasi hiyo sasa ni mwaka wa tatu,umetuunganisha ," amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Wakati huo huo amezungumzi mchango wa viongozi wa dini zote pamoja na waumini wa dini hizo kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao na kuunga mkono juhudi za Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo.

TAA Kutekeleza Mradi wa Bil. 55 Mkoani Mtwara

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege inatekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege Mtwara utakaogharimu Shilingi Bilioni 55.

Akizungumza moja kwa moja baada ya kuunganishwa mbashara redioni na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela aliwahakikishia wananchi wa Mtwara kuwa kazi ya upanuzi mkubwa wa uwanja huo itaanza.

“Kuna mradi wa takribani shilingi Bilioni 55 kupanua Uwanja wa Ndege wa Mtwara na kazi inakwenda kuanza.Pia kuna kazi za ukarabati Uwanja wa Songea na Nachingwea yote ni katika kulifungua eneo la Kusini," alisema. Aidha, Mayongela Alisema kuwa mradi huo una lengo la kuimarisha kuimarisha usafiri wa anga katika maeneo ya kusini mwa Tanzania ili kuiunganisha na mikoa mingine.

Mayongela aliongeza kuwa Mradi huo utatekelezwa na mkandarasi kutoka China na tayari yupo katika eneo la mradi Kwa upande wake Dkt. Abbasi amesema kuwa  Serikali itaendelea kuhakikisha inazijenga na kuziboresha barabara za vijijini kupitia Taasisi ya TARURA iliyopewa jukumu la kusimamia eneo hilo.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano Maalum na Radio Safari Fm ya mkoani Mtwara kuhusu miaka mitatu ya utekelezaji katika Serikali ya Awamu ya Tano
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live




Latest Images