Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

VODACOM TANZANIA WASHEREHEKEA KUUAGA MWAKA 2018

0
0

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Tanzania PLC, wakisakata muziki wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano, Rosalynn Mworia, (Kushoto) akimsikiliza Goodluck Mushi, wakati akishukuru kwa kutunukiwa tuzo ya mfanyakazi bora wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City Jijijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi (kushoto) akimpongeza Christina Murimi, mara baada ya kukabidhiwa TUZO ya mfanyakazi bora, wakati wa sherehe ya kuuaga mwaka 2018 iliyofanyika Mlimani City Jijijini Dar es Salaam.

MICHUZI TV: ASHA BARAKA:MZIKI WA DANSI KUNUNULIWA KWA BIA!

CHAMA CHA WAAJIRI TANZANIA (ATE) YAANDAA TUZO ZA MWAJIRI BORA WA MWAKA 2018

0
0



Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Disemba 14 2018 kimeandaa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, tuzo hizo zimejikita katika kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa guvu kazi na rasilimali watu kwa lengo la kuwawezesha kutimiza wajibu wao kikamilifu na kupelekea kukuza uzalishaji wa kibiashara.

Tuzo hizo zilihudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Jenista Mhagama, Mh. Anthony Mavunde, Mhe. Stella Ikupa, Mkuu wa Mkoa DSM, Mhe. Paul Makonda, Balozi wa Norway nchini, Bi. Elisabeth Jacobsen, Balozi wa Denmark nchini, Bw. Einer H. Jensen na Balozi wa China nchini Nd. Wang Fe, pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA na ILO.

Tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka zimasaidia kuhamasisha wanachama kuchukulia masuala ya ajira na usimamizi wa rasilimali watu kama misingi muhimu katika kumwezesha mwajiri kuwana wafanyakazi wenye uwezo na ueledi ili kukidhi mahitaji ya ushindani katika biashara.

Sherehe ya utoaji tuzo iliyohudhuriwa na Mhe. Jenista Mhagama (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu akiwa Mgeni Rasmi, zimekuwa maarufu hapa nchini katika muktadha wa biashara hasa kwa kuhamamasisha makampuni makubwa na madogo na ya ukubwa wa kati kuhusu umuhimu wa kuzingatia misingi bora ya kufanya biashara nchini.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bi. Jayne Nyimbo-Taylor akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya kutoa Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na chama hicho katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akiwa mgeni rasmi ilitoa tuzo kwa kutambua vipengele 17 kutambua waajiri wenye misingi bora ya usimamizi wa nguvu kazi na rasilimali watu.
Image002
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) akihutubia wageni waalikwa katika hafla ya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City. tarehe 14 Disemba. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo Mh. Anthony Mavunde (MB), Mhe. Stella Ikupa (MP), wawakilishi wa balozi za Norway, Denmark, China  pamoja na taasisi mbali mbali ikiwemo TUKTA na ILO na waajiri mbali mbali nchini.
Image003
Mwakilishi wa Tanzania Cigarette Company (TCC), akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi afasi ya tatu katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
Image004
Mwakilishi wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Bi. Lilian Makau akipokea Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 baada ya Kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya pili katika hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba mgeni rasmi akiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB).
Image005
Wafanyakazi wa Geita Gold Mine (GGM) wakifurahiya Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2018 pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (MB) baada ya kampuni hiyo kuibuka washindi nafasi ya kwanza kwenye hafla iliyoandaliwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) katika ukumbi wa Mlimani City, tarehe 14 Disemba 2018.


WAJUMBE BARAZA LA WATOTO TAIFA WACHAGUA VIONGOZI WAKUU WA BARAZA LAO

0
0


Baraza la watoto la Taifa leo limepata uongozi mpya baada kukamilisha uchaguzi wa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Baraza hilo na pia uchaguzi wa Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti, Katibu na Mweka hazina wa Baraza hilo uchaguzi uliofanyika jana katika Manispaa ya Singida.

Akiongea mara baada ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi huo Mwenyeliti wa Uchaguzi wa Baraza hilo Bi. Joyce Mugambi amewataka viongozi wa Baraza hilo kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwa kushirikiana na viongozi wa Wizara Mama ili kuleta ufanisi kiutendaji.

Uchaguzi wa Viongozi wa Baraza hilo ufanyika kila baada ya kipindi cha miaka miwili kwa kuwa na Wajumbe kutoka Tanzania Zanzibar ambao kwa pamoja wanaunda wajumbe wa Baraza Kuu la Baraza hilo ambapo Mwenyekiti na Makamu wake wanaweza kutoka upande wowote wa Muungano, ikitokea mwenyekiti katokea  Zanzibar inabidi Makamu wake pia atokee huko ili Katibu atoke Tanzania Bara.

Viongozi walioshinda kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Johel Festo kutoka Mkoa wa  Mwanza, Makamu Mwenyekiti ni Aidath Ismail pia kutoka Mkoa wa Mwanza, Katibu ni Thuwaiba Abdallah anayetokea  Unguja Magharibi na viongozi hao utadumu kwa kipindi cha miaka miwili.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian Kitiku amemtaka Mwenyekiti mpya wa Baraza la Watoto Taifa kuhakisha anaongeza  idadi ya mabaraza katika ngazi ya Mkoa na Wilaya na kumtaka kufanya hivyo kwa kushirikiana na Wizara ili kila mkoa upate uwakilishi wake.
 Wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii muda mchache kabla ya kuanza uchaguzi wa viongozi wa Baraza hilo Kitaifa.
2
Mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto akikusanya kura kutoka kwa wajumbe wa Baraza wakati wa zoezi la kuwapigia kura wagombea wa uongozi wa Baraza la Taifa la Watoto.
3
Baadhi ya Wagombea wa uongozi katika Baraza la Watoto Taifa wakisubiri matokeo kujua kama bahati iko upande wao wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Taifa la Watoto jana katika Manispaa ya Singida.
4
Viongozi wa nafasai nne za juu za Baraza la Taifa la Watoto wakiwa tayari kwa majukumu mapya wakawanza kushoto ni mweka hazina mpya wa Baraza hilo Ince Frank kutoka mkoa wa Mbeya, wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Aidathi Ismail kutoka Mkoa wa Mwanza na katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joel Festo kutoka Mkoa wa Mwanza na kulia kwake ni Katibu wa Baraza Thuwaiba Abdallah kutoka Unguja Magharibi.

Nyongo Aitaka Tume ya Madini kuchunguza Chanzo cha Mgogoro wa Wachimbaji Madini, Kilwa

0
0

Na Greyson Mwase, Kilwa.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameitaka Tume ya Madini kufanya uchunguzi kuhusu mgogoro kati ya kampuni inayojihusisha na uchimbaji wa madini ya jasi ya Kizimbani inayomilikiwa na Seleman Mohamed na wananchi wa kijiji cha Hotel Tatu kilichopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi.

Naibu Waziri Nyongo ametoa agizo hilo leo tarehe 15 Desemba, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho wakati wa utatuzi wa mgogoro huo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku mbili katika mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua shughuli za madini, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wa madini.

Alisema kuwa, baada ya kusikiliza pande zote mbili imeonekana kuna haja ya  Tume ya Madini kufanya uchunguzi ili kubaini namna utoaji wa leseni ya uchimbaji wa madini ya jasi kwa kampuni ya Kizimbani ulivyofanyika kabla ya kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na kanuni za madini.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Nyongo alisisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini haitasita kuwaondoa maafisa madini wakazi wa mikoa watakaobainika kuwa ndio chanzo cha migogoro kwenye maeneo ya uchimbaji wa madini.

“ Kama Serikali tunataka kuhakikisha leseni za utafiti na uchimbaji wa madini zinatolewa kwa kufuata sheria na kanuni za madini bila kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote, aidha hatutasita kumwondoa afisa madini mkazi yeyote atakayebainika kuwa chanzo cha migogoro kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini,” alisema Naibu Waziri Nyongo huku akishangiliwa na wananchi. 

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akielekeza jambo kwenye sehemu ya kukusanya madini ya jasi iliyopo katika eneo la Hoteli Tatu Wilayani Kilwa mkoani Lindi. Kushoto mbele ni Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Sophia Omari.
PICHA NA 5
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) akiangalia madini ya chumvi katika eneo la Jangwani kwa Chinja lililopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi.
PICHA NA 6
Sehemu ya wazalishaji wa madini ya chumvi katika eneo la Kilwa Masoko lililopo Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika katika eneo hilo wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero zao.

MASAUNI: TUTADHIBITI UHALIFU MAENEO INAKOPITA MIRADI YA SERIKALI

0
0

Serikali iko katika mpango wa kujenga Kituo cha Polisi katika Halmashauri ya Itigi ikiwa ni juhudi za kulinda hujuma na uhalifu katika Ujenzi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge) na Mradi wa Umeme katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) baada ya wavamizi kuingia eneo la hifadhi ya Rungwa ambayo kuna mito 18 ambayo ni chanzo cha Mto Rufiji ambako mradi wa umeme unajengwa. 

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea na kukagua Mradi wa Kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Manyoni na kukagua eneo linarotarajiwa kujengwa Kituo cha Polisi Itigi lengo ikiwa kudhibiti matukio ya uhalifu. 

Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni, Naibu Waziri Masauni amesema Serikali iko tayari kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha miradi mikubwa ambayo Serikali ya Awamu ya Tano imeianza inakamilika bila kufanyiwa hujuma zozote na wahalifu. 

“Miradi mikubwa ambayo Rais wetu Dkt. John Magufuli na serikali anayoiongoza ameianzisha ni muhimu ikalindwa ili ilete manufaa kwa nchi pindi itakapokamilika na sisi kama wizara tutahakikisha tunasogeza huduma za Ulinzi na Usalama katika maeneo yote ambayo miradi hiyo inapitia, ndio maana leo nimetembelea ujenzi wa Kituo cha Polisi Manyoni ambacho kiko mbioni kukamilika lengo ikiwa ni kulinda miradi hiyo mikubwa,” alisema Masauni 

Akizungumza katika ziara hiyo, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Daniel Mtuka amekiri kuwepo na haja ya kituo katika Wilaya za Manyoni na Itigi ili kuweza kuboresha usalama katika maeneo hayo ambayo yanapitiwa na miradi hiyo mikubwa miwili huku akiiomba wizara kuleta askari katika vituo hivy pindi ujenzi utakapokamilika. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni wakati wa ziara ya kikazi, lengo ikiwa ni kuweka mikakati ya kudhibiti hujuma na uhalifu katika maeneo inapopita miradi mbalimbali ya serikali. Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto), akiangalia ramani ya eneo linarotarajiwa kuejngwa kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Manyoni Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati mstari wa mbele), akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Manyoni kuingia katika Kituo cha Polisi cha Manyoni kinachojengwa baada ya kituo cha awali kupitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa . Naibu Waziri yuko mkoani Singida kwa ziara ya kikazi. 
Muonekano wa nje Kituo Kipya cha Polisi Wilaya ya Manyoni ambacho kipo mbioni kukamilika ambacho kinategemewa kudhibiti hujuma na uhalifu katika maeneo mbalimbali inakopita miradi mikubwa ya serikali .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 

WATOTO 10 WAANZA KUSIKIA KWA MARA YA KWANZA

0
0



kumi ambao wamewekewa vifaa maalum vya kusaidia kusikia (Cochlear Implant) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo wameanza kusikia kwa mara ya kwanza baada ya kuwashiwa vifaa hivyo (switch on).

Watoto hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Dar es Salaam, Kilimanjaro, Tanga, Pwani na Ruvuma walifanyiwa upasuaji Novemba 12 hadi Disemba 16 mwaka huu ambapo zaidi ya asilimia 90 ya upasuaji huo ulifanywa na watalaam wa Muhimbili.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa magonjwa ya Pua, Koo na Masikio, Dkt. Edwin Liyombo amesema mbali na zoezi hilo la kuwawashia vifaa vya kusaidia kusikia, lakini pia watoto wengine ambao waliwekewa vifaa hivyo nao wamekuja kwa ajili kuangaliwa maendeleo yao na kupatiwa elimu ya kutunza mashine hizo.

Kwa mujibu wa Dkt. Liyombo, tangu kuanza kwa huduma hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Juni 2017 mpaka Disemba 2018, watoto 21 tayari wamewekewa vifaa hivyo ambapo jumla ya shilingi milioni 777 zimetumika kwa ajili ya upasuaji huo na endapo wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi Serikali ingetumia shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kufanikisha matibabu hayo.Hivyo kutokana na upasuaji huo wa ubingwa wa juu kufanyika hapa nchini Serikali imeokoa shilingi Bilioni 1.3.

“Lengo la hospitali ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, kwani matibabu haya yanagharama kubwa kwani kupeleka mtoto mmoja nje ya nchi kwa ajili ya kupandikizwa kifaa cha usikivu ni shilingi milioni 100 wakati akipatiwa matibabu hayo Muhimbili hugharimu shilingi milioni 37 kwa mtoto mmoja,” amesema Dkt. Liyombo.
 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwawashia vifaa vya kusaidia kusikia kwa watoto 10 waliopandikizwa vifaa hivyo Novemba 12 hadi 16, 2018. Kutoka kushoto ni mtaalam wa usikivu, Fayaz Jaffer na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Masikio, Pua na Koo wa Muhimbili, Dkt. Aveline Aloyce .
????????????????????????????????????
Wazazi wa watoto wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Dkt. Liyombo kabla ya vifaa hivyo kuwashwa  tangu walipopandikizwa Novemba 12 hadi 16, 2018.
003
Mtoto Rehoboth Kivuyo akisikia kwa mara ya kwanza tangu wazazi wake walipobaini kwamba ana tatizo la kusikia.

SHEHIYA 388 KUEKWA ALAMA MPYA ZA MIPAKA ZANZIBAR

0
0
Khadija Khamis –Maelezo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheir ametangaza uwekaji wa alama za mipaka ya shehia zote za Unguja na Pemba. Akitoa taarifa ya uwekaji wa Mipaka mbele ya Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani, Waziri Haji Omar Kheir alisema zoezi hilo litaanza rasmi Disemba 18, 2018 katika Wilaya ya Mjini na baadae kuendelea katika Wilaya nyegine.

Alisema usimamizi wa kazi hiyo inafanywa kwa mashirikiano makubwa na Taasisi muhimu za Serikali zikiwemo Kamisheni ya Ardhi na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali. Alisema kukamilika kwa kazi hiyo haitanufaisha Wizara hiyo peke yake bali   itawasaidai wahusika wengine kufanyakazi zao zikiwemo za utafiti, mipango miji na vijiji, utafutaji wa rasilimali, sense, uandikishaji wa raia, ulinzi na usalama, mipango ya kijamii na kiuchumi pamoja na ukusanyaji wa takwimu

Waziri Haji Omar Kheir aliweka wazi kuwa lengo la uwekaji wa mipaka hiyo ni kurahisisha shughuli za kiutawala na utowaji bora wa huduma kwa wananchi na halihusiani na masuala mengine yoyote na hakuna haja ya kuanzisha ajenda itakayoleta mifarakano ndani ya shehia. Aliwataka viongozi wa shehia na wananchi kwa jumla kutowa ushirikiano kwa maafisa watakaoendesha zoezi hilo na kufuata maelekezo watakayopewa ili liweze kufanikiwa kama lilivyokusudiwa.

Waziri Haji Omar Kheir alisema Zaidi ya shiling milioni 37 zimetumika kwa kutengeneza alama (Bicon) ambazo zitawekwa katika shehia zote 388 Unguja na Pemba. Katika mwezi wa Mei, 2015 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alifanya maamuzi ya kuigawa Zanzibar katika maeneo ya  Shehia Wilaya na Mikoa na maeneo mengine ya kiutawala  kwa mujibu wa uwezo aliopewa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Sheria ya Tawala za Mikoa ya Mwaka 2014.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheir akiwa na uongozi mzima wa Wizara yake akitoa tamko la uwekaji wa alama za mipaka ya shehia zote za Unguja na Pemba kwa wandishi wa habari huko katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Mjini Unguja.
Baadhi ya viongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo (hayupo pichani) alipokuwa akitoa tamko la uwekaji wa alama za mipaka ya shehia katika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Mjini Ununga.

Picha na Makame Mshenga.

Benki ya FINCA Microfinance yatoa zaidi ya milioni 10 kwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo kupitia shindano la ‘Kuza Ofisi na FINCA’

0
0
Shindano hilo lililodumu kwa kipindi cha miezi mitatu lilikuwa na lengo la kutoa elimu ya stadi za biashara na fedha kwa wafanyabiashara wadogo. 

Benki ya FINCA Microfinance imeendelea kuwa benki ambayo inaunga mkono ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi cha uwepo wake nchini Tanzania. Bugingo Emmanuel ameibuka mshindi wa shindano la biashara la Kuza Ofisi na FINCA na kuondoka na kiasi cha TZS milioni 10 baada ya shindano la muda wa miezi mitatu na lililokuwa na zaidi ya washiriki elfu moja walioshiriki, ni washriki wanne ndio waliowasilisha mipango yao ya biashara kwa jopo la majaji na kupigiwa kura na watazamaji. 

Akiongea katika onyesho la mwisho la shindano la Kuza Ofisi na FINCA jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde aliipongeza FINCA kwa kutekeleza jitihada za kibunifu kwa ajili ya kusaidia kukuza wajasiriamali wadogo kwa wakati. Alisema kwamba serikali inaendelea kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya maendeleo ya biashara nchini.

“Ninatoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na mifuko ya uwezeshaji ya serikali ambayo imetengwa kwaajili ya maendeleo ya biashara. Vile vile aliipongeza benki ya FINCA Microfinance kwa jitihada zake zenye lengo la kusaidia kukuza wafanyabiashara wadogo SMEs nchini ‘Ninaipongeza FINCA kwa kubuni mipango hii ya kibunifu ambayo sio tu kwamba inasaidia kukuza biashara ndogo ndogo lakini pia inawapatia vijana ujuzi na stadi za biashara alisema Mavunde. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 jana kwa mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Emmanuel Bugingo mkazi wa Mbagala Kuu. Shindano hilo lililoandaliwa na Benki ya Finca Microfinance linashindaniwa kwa washiriki kubuni mradi wenye kuweza kumletea kipato kwa kupitiwa na majaji waliompata mshindi. Pichani Kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Walemevu, Mhe. Anthony Mavunde akitangaza mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA lililofikia kilele jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Shindano lililoendeshwa kwa miezi mitatu kwa washiriki kubuni mradi chanya wenye kumuwezesha kupata kipato. Wengine pichani kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin na washiriki walioingia nne bora. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 5 jana kwa mshindi wa pili wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Sadiki Hassani mkazi wa Manzese, Kushoto ni Alfred Vanderlin, Afisa Mkuu Uendesheji wa Finca. 

NHIF YAWAFIKIA WAKULIMA WA KAHAWA MKOA WA ARUSHA

0
0
Na mwadishi wetu,Arusha .

Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)umewataka wanachama wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Mazao kujiunga na Bima ya Afya kwaajili ya kupata matibabu bora ambao ni mpango wa serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 idadi kubwa iwe imejiunga na mfuko huo.

Meneja wa NHIF mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu amesema Ushirika Afya ni mpango mahususi ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika vya msingi kwa kuanzia na mazao matano. Ameyataja mazao hayo matano ya kimkakati kuwa ni Korosho,Pamba,chai,Kahawa na Tumbaku ambayo baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa mwaka huu mfuko ulianza kutoa huduma za matibabu kwa wakulima.

Shekifu amesema mkulima anatakiwa kulipa kiasi cha Sh 76,800 ukiwa ni mchango wake kwaajili ya kupata Ushirika Afya na itamwezesha kupata huduma ya matibabu kwa mwaka mzima pia ataruhusiwa kuwakatia bima hiyo kwa mwenza,mzazi,mkwe na watoto. Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka amesema mpango huo utasaidia wanachama wake kunufaika na matibabu yanayotolewa na mfuko huo hatua itakayoongeza tija katika shughuli zao za kilimo cha Kahawa.

Amesema gharama za matibabu bila kutumia bima ya afya zipo juu na kuwataka viongozi hao wa ushirika kuwahamasisha wanachama wao kujiunga kwa wingi ili kuanza kunufaika na mpango wa serikali wa mazao matano ya kimkakati unaleta matokeo yaliyokusudiwa.

Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazaoa na mfuko huo,kushoto ni Afisa Matekelezo wa NHIF,Miraji Kisile na Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazao mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwaajili ya kuwapa uelewa wa namna ya kujiunga jana,Emmanuel Sanka.Picha na Filbert Rweyemamu 

UJENZI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MUSOMA WAENDELEA KWA KASI

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Musoma 

WAKAZI wa mkoa wa Mara wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za Mahakama Kuu mkoani Mwanza, umbali wa zaidi ya kilometa 200 kutoka mjini Musoma, baada ya ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma kukaribia kukamilika mapema mwakani.

Wakizungumza na timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, baadhi ya wakazi wa mji wa Musoma Mary Mohamed na Happy Mjito, wamesema kuwa hivi sasa wanatumia fedha nyingi kufuatilia haki zao Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hali inayowafanya wengi wao kukata tamaa kufuatilia kesi zao hivyo kupoteze haki zao

“Ukikata rufaa ya kesi unaambiwa uende Mwanza wakati hata Mahakama Kuu yenyewe ya Kanda ya Mwanza hatuijui mahali ilipo, sasa tunafurahi kwamba tutakuwa tumiendesha kesi zetu hapa hapa Musoma” alisema Bi. Happy Mjito

Akielezea hatua ya ujenzi wa Mahakama hiyo Kuu Kanda ya Musoma ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6 nukta 2, Wakala wa Mkandarasi anaye jenga Mahakama hiyo, Kampuni ya DF Mistry, Mhandisi Uday Dadrawalla, ameiambia timu hiyo ya Wizara ya Fedha na Mipango inayofuatilia utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani Mara kwamba ujenzi huo umefikia asilimia 80.

“Mkataba wetu unaonesha kuwa tunatakiwa kukabidhi jengo ifikapo tarehe 21 mwezi Mei, 2019 lakini kwa kasi tunayokwenda nayo tutakabidhi jengo hili mapema zaidi Mwezi April, 2019” alisema Mhandisi Dadrawalla.

Mradi huu unaotekelezwa na Mahakama Kuu Nchini ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele iliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/18 hivyo utekelezaji wake ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2021, hususani katika eneo la Utawala Bora.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzo wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania.
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, wakipata maelezo na ufafanuzi mbalimbali kutoka msimamizi wa Ujenzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, Mhandisi Uday Dadrawalla (kulia) walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miundombinu ya Mahakama hiyo unaosimamiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania kwa gharama ya shilingi bilioni 6.2. 
Timu ya Maafisa kutoka Wizara ya Maji, Wizara ya Ujenzi, Miundombinu na Mawasiliano wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Maafisa wa Mahakama Kuu-Musoma na Wakandarasi wa Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, wakinyanyua kofia za usalama baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa Mahakama hiyo uliofikia asilimia 80 na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 6.2 .(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango- 

MICHUZI TV: MNGEREZA ATOA KAULI KUHUSU OMBI LA WASANII KUONGEZEWA MUDA WA KUFANYA KAZI

MICHUZI TV: IGP SIRRO ALIVYOWAPANDISHA VYEO ASKARI WA JESHI LA POLISI

MICHUZI TV: Mchambuzi wa Soka Abbas Pira asema Boban ni Usajili Mzuri kwa Yanga

Michuzi TV: Mchambuzi Mkubwa wa Soka Tanzania Abbas Pira asema pamoja na kufungwa Simba bado Watafuzu.


MICHUZI TV: DKT MWAKYEMBE AVAMIA USIKU WA TWANGA PEPETA, AONGELEA MUDA WA MAONESHO

MICHUZI TV: Ufafanuzi namna ya utaratibu mpya wa ukokotoaji wa mafao ya wastaafu

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 17,2018

NAIBU WAZIRI KUFUATILIA TATIZO LA UCHELEWESHAJI WA MIRADI ILIYO CHINI YA TBA

0
0
RS TABORA

MKANDARASI wa Ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Mji Nzega wenye thamani ya bilioni 4.8 ametakiwa kuhakikisha mradi huo unakamilika katika kipindi ambacho kimekubalika katika mkataba.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali (OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa ziara yake wilayani Nzega.

Alisema Wakandarasi wanaopatiwa fursa ya kujenga miradi ya Serikali ikiwemo ile ya Halmashauri ni vema wakajitahidi kuhakikisha wanaitekeleza kwa kiwango cha hali ya juu ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Akijibu hoja za Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) kuchelewesha miradi mingi mkoani Tabora ikiwemo ukarabati wa Shule Kongwe ya Milambo na huo wa ujenzi wa Ofisi hizo alisema atajitahidi kulifikisha katika Wizara inayoisimamia Wakala hiyo ili watekeleze miradi yao kwa wakati.

Alisema TBA kama sehemu ya Serikali ni lazima wabadilike na kuharakisha utekelezaji wa miradi wanayopewa kusimamia ili kutosababishia kuongezeka kwa gharama kutokana na mradi kuchelewa kuanza. Awali Mahandisi wa Halmashauri ya Mji Nzega Mwita Said alisema ujenzi wa Ofisi hizo ulioanza Mei mwaka huu unatarajia kukamilika Novemba mwakani .

Alisema hadi hivi wameshapokea bilioni 2 na wamemlipa Mkandarasi ambaye ni Mzinga Holding milioni 700 na Msimamizi ambaye ni TBA milioni 200. Said alisema mradi huo uko katika hatua ya Msingi ambao umekumbana na matatizo ya kuwepo kwa mvua, ardhi kuwa na mwamba na upungufu wa vibarua unasababisha kazi kwenda polepole.

WAZIRI WA NISHATI AAGIZA BODI TANESCO ICHUKUE HATUA SUALA LA KUKATIKA UMEME

0
0

Na Veronica Simba - Dodoma

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuchukua hatua za makusudi ikiwemo kuwavua nyadhifa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji, Mhandisi Abdallah Ikwasa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Usambazaji, Mhandisi Kahitwa Bashaija; kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa sasa.

Alitoa maagizo hayo Jumamosi Desemba 15, mwaka huu alipokutana kwa dharura na wajumbe wa Bodi hiyo Makao Makuu ya Wizara jijiji Dodoma.

Akizungumzia sababu za kutaka wakurugenzi hao wawajibishwe, Waziri Kalemani alisema ni kutokana na tatizo la kukosekana kwa umeme sehemu kubwa ya nchi mara nne na kwa kipindi cha muda mrefu unaofikia nusu saa, kwa sababu ambazo zimekuwa zikielezwa kuwa ni kutoka kwa Gridi ya Taifa, wakati nchi ina ziada ya umeme inayofikia wastani wa megawati 250.

Akifafanua zaidi, alisema kutokea kwa tatizo hilo kunamaanisha kuna uzembe katika usimamizi au kutokufuatilia maelekezo ya Serikali, au kunaweza kuwepo na hujuma kwa baadhi ya watumishi wasiokuwa wazalendo. “Nchi inapokuwa gizani hata kwa sekunde moja, maana yake hakuna usalama. Aidha, hakuna sababu ya wananchi kukosa umeme katika mazingira ambapo kuna umeme wa ziada.”

Katika maagizo yake kwa Bodi, mbali na kutaka Wakurugenzi husika wawajibishwe, aliagiza pia wachunguzwe ikiwa ni pamoja na waliohusika kwa namna moja ama nyingine. Aidha, aliitaka Bodi kuunda Timu mahsusi kuanzia siku hiyo (Desemba 15), ili ichunguze na kufuatilia suala hilo, ikihusisha tasnia na taasisi mbalimbali, zaidi ya TANESCO.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) (hawapo pichani) kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) alipokutana nao na kuwapa maagizo kuhusu hatua za kuchukua kutokana na suala la kukatika umeme sehemu kubwa ya nchi mara kadhaa. Waziri alikutana na Bodi hiyo Desemba 15, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.

 
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images