Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Timesofmoney yadhamiria Kuingia katika Soko la Tanzania

$
0
0
KAMPUNI kubwa duniani yenye utaalamu wa kuwezesha uhamisho wa fedha kwa njia ya mtandao (online) ya Timesof Money, imedhamiria kuingia katika soko la Tanzania, kama sehemu ya mpango wake wa upanuzi barani Afrika.

Katika mpango wake huo, kampuni hii yenye makao yake makuu jijini Mumbai nchini India, inatajaria kuzindua mpango/mfumo wa kutuma fedha nchini toka kwa Watanzania walioko nje ya nchi (remittance) kwa njia ya mtandao (Online).  Mfumo huo ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa nchini, utawawezesha Watanzania kupata/kutuma fedha kutoka mahali popote duniani moja kwa moja katika akaunti zao za benki, kadi za malipo ya kabla (pre-paid cards) pamoja na simu zao za mkononi.

“Katika mkakati huo huo wa kujitanua barani Africa, hivi karibuni tumeingia mkataba na Benki ya Diamond Trust nchini Kenya kutoa huduma kwa wateja wake wa mfumo wa ‘NationHela’,” alisema Afisa Mtendaji mkuu wa TimesofMoney, Avijit Nanda.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, idadi ya Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchi mbalimbali duniani/ughaibuni (diaspora) inakadiriwa kuwa zaidi ya million mbili. Na kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia, inakadiriwa kuwa Watanzania hao waliingiza nchini kiasi cha shillingi billion 120 (US$ 75million)mwaka jana. Kwa kutumia huduma hii, Watanzania wanaoishi nje ya nchi wataweza kutuma pesa kwa jamaa na marafiki zao nyumbani, hivyo kuondoa usumbufu wa kusimama katika foleni kwa mawakala wa kuhamisha fedha.

"Idadi ya raia wa nchi za Afrika Mashariki na hasa Tanzania wanaoishi nje ya nchi zao inaendelea kuongezeka na hii ina maanisha uhitaji wa kutuma fedha nyumbani (remittance) pia unaongezeka. Ni kwa sababu hii tumeona kuna umuhumi wa kuingia katika soko hili. Tukiwa na teknolojia ya kisasa, tunatoa ahadi ya huduma bora kwa kutumia wataalamu wenye uzoefu mkubwa katika nyanja hii,” alisema Bw Nanda.

Bara la Afrika linakadiriwa kuwa na idadi ya watu zaidi ya million 30 wanaoishi nje ya nchi zao za asili. Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo-- International Fund for Agricultural Development (IFAD), unakadiria kwamba mwaka jana (2012) wahamiaji hao kwa pamoja wamechangia/ wametuma kiasi cha dola za marekani millioni 38.6 katika fedha kutoka nje, kwa familia na jamii zao nyumbani.

Hata hivyo, moja ya kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa mtiririko kutuma fedha nyumbani (remittance) katika nchi za Afrika hasa zile zilizopo Kusini mwa jangwa la Sahara, ni gharama kubwa ya kutuma fedha. Wastani wa gharama ya kutuma fedha kwa Afrika ni karibu 12 % ya juu kuliko wastani wa kimataifa wa 8.96 % na karibu mara mbili ya gharama ya kutuma fedha kwa Asia ya Kusini.

"Gharama kubwa za ada zinazotozwa na makampuni na mawakala wa kuhamisha fedha barani Africa, imekuwa ni kikwazo na imeathiri mtiririko wa kuingiza fedha toka nje ya nchi. Mtumiaji wa mwisho ndiye anayeathirika na kubeba mzigo wa gharama/ada kwa kiasi kikubwa. Kwa kupitai mfumo wa mtandao (online-transactions) tunatarajia  inaweza kusaidia kupunguza gharama hizi kwa kiasi kikubwa, jambo ambalo litatao ahueni kubwa kwa mtumiaji wa mwisho,” bosi huyo wa TimesofMoney alisema.

Maelezo zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya kampuni www.timesofmoney.com .


UTAMBULISHO WA TANZANITE FOUNDER FOUNDATION (TAFFO) KATIKA SIKU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 46 YA UVUMBUZI WA MADINI YA ZOISITE INAYOJULIKANA LEO HII KAMA TANZANITE.

$
0
0
 Mwenyekiti wa TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, Bi. Asha Ngoma akionyesha cheti cha Uvumbuzi kilichotolewa na serikali mwaka 1984, mbele ya waandishi wa habari, katikati ni Mzee Jumanne Mhero Ngoma, Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Kulia ni Bw. Baraka Msuya, Mjumbe wa taasisi. Bi. Ngoma amesema  azma ya taasisi hiyo ni kuwawezesha vijana kupata utaalam (elimu), Kuwawezesha kupata nyenzo za uchimbaji madini NA Kuenzi na Kuhifadhi historia ya uvumbuzi wa madini ya TANZANITE kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. 

Mwenyekiti wa TANZANITE FOUNDER FOUNDATION, Bi. Asha Ngoma akikifanunua jambo kuhusu shughuli za taasisi akiwa pamoja Mzee Jumanne Mhero Ngoma, Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite na Bw. Baraka Msuya, Mjumbe wa taasisi.

child-go-free offer from skylink

$
0
0
Since the festive season is approaching, Skylink would like to offer you a child-go-free offer in Hong Kong, end of season Europe offer and various combinations for Malaysia and Singapore. Below find an array of options for you to choose from.

Timu ya Netiboli ya Utumishi yaicharaza Ujenzi mabao 48-5

$
0
0
Mchezaji wa Timu ya Netiboli ya Utumishi Fatma Ahmed (GS) akidaka mpira hewani wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Utumishi Anna Msulwa (GA)(kulia) akifunga bao wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.
Mchezaji wa timu ya Netiboli ya Wizara ya Ujenzi Anjela Mvungi (GK) akidaka mpira wakati wa mechi kati ya Utumishi na Wizara ya Ujenzi mjini Dodoma.

MAONESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAINGIA SIKU YA PILI JIJINI MWANZA LEO.

$
0
0
 Polisi wa Kitego cha Elimu, Trafiki Mkoa wa Mwanza, Francis Muganyizi akitoa elimu kwa wananchi jinsi madereva wanatakiwa wawe waangalifu kwa kujua alama za barabarani wakati wanapokuwa wanaendesha gari barabarani. Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa jana kitaifa Mkoani humo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi yameingia siku ya pili leo ambapo wananchi mbalimbali jijini humo wanaingia kwenye mabanda mbalimbali katika Uwanja wa CCM Kirumba jiji humo kujifunza masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kauli mbinu ya maadhimisho ya mwaka huu ni USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE
 Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, SGT Pili Kaku akisikiliza kwa makini maswali mbalimbali ya mwananchi wa jijini Mwanza (kushoto) aliyetaka kujua jinsi jeshi hilo linavyofanya kazi ya uzimaji moto pamoja na uokoaji. Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yalifunguliwa jana kitaifa Mkoani Mwanza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi yameingia siku ya pili leo ambapo wananchi jijini humo wanaingia kwenye mabanda mbalimbali katika Uwanja wa CCM Kirumba kujifunza masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kauli mbinu ya maadhimisho ya mwaka huu ni USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE.
 
 Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CPL Ibrahim Luena akitoa elimu kwa wanachi juu ya buti za usalama wakati wa kuzima moto. Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yalifunguliwa jana kitaifa Mkoani Mwanza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi yameingia siku ya pili leo ambapo wananchi jijini humo wanaingia kwenye mabanda mbalimbali katika Uwanja wa CCM Kirumba kujifunza masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kauli mbinu ya maadhimisho ya mwaka huu ni USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE
  1. Wananchi wakiwa ndani ya Banda la Wizara ya Ujenzi wakiuliza maswali mbalimbali jinsi wizara hiyo inavyosimamia ujenzi wa barabara nchini. Maonesho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo yalifunguliwa jana kitaifa Mkoani Mwanza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi yameingia siku ya pili leo ambapo wananchi jijini humo wanaingia kwenye mabanda mbalimbali katika Uwanja wa CCM Kirumba kujifunza masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kauli mbinu ya maadhimisho ya mwaka huu ni USALAMA BARABARANI UNAANZA NA MIMI, WEWE NA SISI SOTE. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Gentriez Belle 9 & Yung D after Vocal Session @ Noizmekah Studios

AAR YATOA HUDUMA YA AFYA KWA WASHIRIKI WA BSS 2013

$
0
0
AAR Healthcare imefanya vipimo vya afya kwa washiriki wa Bongo Star Search mwaka 2013, vipimo hivyo vikiwamo BMI, BP pamoja na kipimo cha kisukari Washiriki hao ambao kwa sasa wamebaki 15 ,walipewa pia mafunzo ya kiafya kutoka kwa Madactari wa AAR ya jinsi ya kuishi maisha yao kwa afya njema. 
 “Dhumuni la kuwafanyia washiriki vipimo vya afya, ni wao wenyewe kuweza kutambua afya zao kabla ya kuanza kupanda jukwaani, kupata ushauri wa jinsi ya kutunza afya zao kwa kipindi chote cha mashindano na hata baada ya mashindano” . Alisema Afisa Mahusiano wa AAR Amisa Juma. Bi. Juma alimalizia kwa kusema “ Sisi kama wadau wakubwa katika afya nchini, tumegundua vijana ndo waathirika wakubwa wa afya, kwa hiyo tumeamua kutumia jukwaa hili la BSS kuweza kusaidia na kutoa mchango mkubwa kwa washiriki na jamii kwa ujumla” . 
 Hii ni mara ya pili kwa AAR kudhamini mashindano haya ya BSS, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2011.
 AAR Healthcare wakiwa na washiriki wa BSS 2013
 Afisa Mahusiano wa AAR HealthCare Amisa Juma akiwapa mafunzo washiriki wa BSS 2013 kuhusu afya zao ,kuchoto ni Bi, Fatma Omary, Maina Thadei na Amina Chibaba
 Dr. Bamuhimbisa Richard kutoka AAR Healthcare akitoa mafunzo kwa washiriki wa BSS 2013 ya jinsi ya kuishi maisha bora kwa kuwa waangalifu na afya zao,walipokua kwenye kambi yao Mbezi Beach
 Muuguzi Salome Mkilima kutoka AAR akimpima BP mshiriki wa BSS 2013 kambini Mbezi Beach Dar-es-salaam
Washiriki wa Bongo Star Search wakipata vipimo vya BMI na BP kabla ya kupanda jukwaani

MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA KHADIJA MWANAMBOKA AZINDUA PROJECT YA VVK-GROW CAMPAIGN

$
0
0
MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA,KHADIJA MWANAMBOKA LEO AMEZINDUA PROJECT YA VVK-GROW CAMPAIGN.

PROJECT HII NI KAMPENI ILIYOBUNIWA NA KUENDESHWA NA BALOZI WA OXFAM,KHADIJA MWANAMBOKA IKIWA NA LENGO LA KUAINISHA CHANGAMOTO ZA SOKO KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE,KUANIKA DHULUMA WANAYOFANYIWA WAKULIMA WA CHAKULA WANAWAKE NA KUHAMASISHA WATUMIAJI WA BIDHAA ZA CHAKULA MIJINI,KUTAMBUA THAMANI YA CHAKULA NA KUWA SOKO LENYE TIJA KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE.

KAMPENI HII INAHUSISHA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO -MODELS WATAKAOKUWA WANAPITA KWENYE MIKUSANYIKO MBALI MBALI, MAOFISINI NA KWENYE TAASISI MBALI MBALI KUHAMASISHA NA KUUZA BIDHAA ZA WAKULIMA WADOGO WANAWAKE.
MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA,KHADIJA MWANAMBOKA AKIONYESHA BANGO LENYE UJUMBE.
SEHEMU YA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA.

Waziri Nchimbi akutana na wanahabari leo kutoa taarifa ya Maendeleo ya Operesheni Kimbunga

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi aliyeketi katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya Maendeleo ya Operesheni Kimbunga ili kuwabaini wahamiaji haramu inayoendelea hapa nchini, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mbarak Abdulwakil na wa kwanza kutoka kulia ni Kaimu Kamishna wa Uraia na Passpoti Victoria Lembeli.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alihutubia Taifa leo

$
0
0
The four-day-long siege of an upscale mall in Nairobi by Islamist militants has ended with the deaths of five militants and 11 in custody, Kenyan President Uhuru Kenyatta declared Tuesday night. 
 He announced three days of mourning for the more than 60 people killed in the attack, a death toll that is expected to rise with the recovery of more bodies from the mall, Kenyatta said. "As a nation, our head is bloodied but unbowed," he said in a televised address. "We have ashamed and defeated our attackers."

MSAADA TUTANI:NATAFUTA KADI ZA SIMU KUPIGA TANZANIA KUTOKEA MAREKANI

$
0
0
                                                   
 Ningependa kuwauliza wale watanzania walio Marekani kama tunaweza ku-share ni kadi gani za simu zenye dakika nyingi kupiga Bongo cell phones.   Wengi wetu kupiga simu nyumbani ni muhimu, sio kila siku ila mara kwa mara. Na gharama za kadi kiasi fulani ni kubwa, mimi kadi ambazo natumia online nyingi ni 17c per minute (.17/min).. which means unapata karibia dakika 58 kwa $10.. Naelewa kuna apps kama viber ambazo zinasaidia kiasi fulani, ila ni vigumu kumwambia bibi akiwa Masasi kwamba weka viber kwenye simu. 
Kwa hiyo kama mtu anajua website gani wana kadi zenye deal zenye rates nzuri kupiga Tanzania please naomba tuambizane. Kama itakuwa ya mtanzania itakuwa bora zaidi, kuinuana muhimu. Au kama kuna means za kupiga simu besides kadi mtu unajua please let us share.

MOTO WATEKETEZA MISITU MAKETE

$
0
0




Taswira za jinsi  moto ulivyoacha madhara makubwa kwa wenye misitu hii wilayani Makete baada ya kuteketeza miti na mimea mingine iliyokuwa katika eneo hilo. Haijafahamika mara moja nini chanzo cha moto huo. PICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI, WA GLOBU YA JAMII

JK na mama salma wakutana na Michelle na Barack Obama na melinda gates

$
0
0
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa na mwenyeji wao Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya viongozi wanaohudhuria Mkutano Mkuu wa 68 wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Picha kwa Hisani ya Rae Lynn Wargo wa  Umoja wa Mataifa.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama Melinda Gates wa Bill and Melinda Gates Foundation walipokutana katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini New York leo. Picha na Freddy Maro

President Kikwete addresses Roll Back Malaria meeting in New York

$
0
0
 President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete Speaks during a special meeting to launch a framework Road map on a Multi-sectoral Approach to combat Malaria held at UN Secretariat Building in New York this morning.

 A Roll Back Malaria Partnership Representative Mr.Herve Verhoosel hands over a mosquito repellent to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in recognition for his efforts in combating malaria in Tanzania during a meeting on Multi-Sectoral approach to combat Malaria held in New York.Photos by Freddy Maro

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA CHUO KIKUU CHA MONMOUTH, NEW JERSEY, MAREKANI

$
0
0
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
 .  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea katika kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu  4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin. Picha na John Lukuwi

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Ngoma ya 'Kalubandika' ya Maquis haichuji. Sikia mpini huo wa Vumbi Dekula

mpiganaji athumani hamisi atangazwa kuwa balozi wa baraza la taifa la usalama barabarani

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisalimiana na Mhariri wa Picha wa zamani wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi na kumtangaza kuwa Balozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani wakati wa ufunguzi wa wiki ya Usalama Barabarani jijini Mwanza.
Mpiganaji Athumani Hamisi akiwa na waratibu wa shughuli zake
za ubalozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.
-------------------------------------

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, amemtangaza Mhariri wa Picha wa zamani wa magazeti ya Daily News na Habari Leo, Athumani Hamisi , kuwa Balozi wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani.

Hamisi, ambaye aliwahi pia kuwa mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited kama Mpigapicha, alipata ajali mbaya mwaka 2008 na kupooza sehemuya mwili.
Katika uteuzi huo uliotangazwa na Waziri Nchimbi jana, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani litamtumia Hamisi kutoa elimu na hamasa kwa Watanzania kuepuka ajali kwa kuwa zina madhara makubwa kwa maisha ya binadamu.

Aidha, Waziri Nchimbi alisema ajali za barabarani zimeendelea kuwa janga linalogharimu maisha ya watu wengi, hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuzidhibiti.
Alisema hayo jijini jana alipokuwa akizindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kwa mujibu wa Waziri Nchimbi, hali hiyo inatokana na ukweli kwamba, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2,012, jumla ya watu 17,820 wamekufa katika ajali za barabarani.

Miongoni mwao ni abiria 5,237, watembea kwa miguu 5,771 na madereva 1,292. Vifo vilivyotokana na ajali 98,693 za barabarani, kuna waendesha pikipiki 2,887, waendesha baiskeli 2,385 na wasukuma mikokoteni 245.

Katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti, mwaka huu, ajali 15,682 zimetokea na kusababisha vifo 2,541 na majeruhi 13,752. Kati ya ajali hizo, pikipiki ni 5,433, ambazo zilisababisha vifo 704 na majeruhi 4,312.

“Hali hii ya matukio ya ajali za barabarani inatisha. Lazima tuchukue hatua madhubuti kukabiliana nazo kwani zinapoteza maisha ya watu wengi na kusababisha ulemavu wa kudumu na hivyo kupunguza nguvu kazi ya taifa,” alisema Waziri Nchimbi.
Chanzo: NIPASHE
Kupata mkasa mzima wa yaliyomsibu 
mpiganaji Athumani Hamisi

CCM YAFANYA MKUTANO MKUBWA SHIRATU

$
0
0
  • KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE
  • MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
  • VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
  • WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO

 Mbunge wa Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na mshikamano walio nao.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote za kisheria.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
 Sehemu ya Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba 2013.


ogopa matapeli mtandaoni: ukikutana na kanyaboya kama hii piga chini haraka!

$
0
0

Diplomat Arrived and misplaced your address

Beneficiary,
We wish to inform you that our diplomat agent conveying the
consignment box valued the sum of $1,000,000 United States Dollars and
inside the consignment box, there is an ATM CARD valued the sum of
$200,000 USD again.
He arrived Yesterday around 8:45 PM, to your Country and misplaced
your address and he is currently stranded at airport in your country
now.
We required you to re-confirm the following information's bellow so
that he can deliver your consignment box to you as soon as possible.
YOUR FULL NAME==========
YOUR ADDRESS:===========
MOBILE PHONE NO:==========
NAME OF YOUR NEAREST AIRPORT:=========
A COPY OF YOUR IDENTIFICATION : ========
Please do contact him with this email Address bellow with the
information's required because he is in your Airport now.
Contact Diplomat Name : Augustine Jim.
We are waiting to hear from you today with the informations:
NOTE That The Diplomat agent did not know the content of the
consignment box and on no circumstances should you let him know the
content,The consignments was moved from here as a family treasures, so
never you allow him to open the box,valued of the Consignment box is
$1,000,000 USD Together with ATM CARD valued $200,000 USD.Kindly
contact him and also,get back to us Immediately you finish reading
this mail so that he can Proceed on the Delivery.
Regards
Chucks Malick

MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFUNGULIWA, TTB YAPONGEZWA KWA KUFUNGUA OFISI MWANZA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kufungua ofisi jijini Mwanza kwa kuwa hatua hiyo itaharakisha maendeleo ya sekta ya utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa.
Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka wananchi wa Mwanza kukuza utalii wa ndani kwa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Mwanza, Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla na kuondokana na dhana kuwa utalii ni kwa ajili ya wazungu tu. 
Eng. Evarist Ndikilo amayasema hayo wakati akizindua maadhimi misho ya siku ya Utalii duniani ambayo kitaifa mwaka huu yanafanyika mkoani Mwanza katika uwanja wa Nyamaga. 
Amesema mkoa wa Mwanza una vivutio vingi sana vya utalii ingawa bado havijatangazwa kikamilifu lakini kufunguliwa kwa ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania, kupata fursa ya kuandaa maadhimisho ya siku ya Utalii duniani kwa mara ya pili mfululizo pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa Kimataifa wa ndege wa Mwanza ni masuala ambayo yatachagiza maendeleo ya sekta ya Utalii mkoani Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla. 
Pamoja na hayo mkuu huyo wa mkoa ameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana kwa karibu sana na Chama cha Utalii Mkoani Mwanza (MTA) na akasisitiza umuhimu wa kuwashirikisha waandishi wa habari wa mkoani Mwanza katika kusaidia kutangaza vivutio vya mkoa huu na kanda nzima ya Mwanza 
“ Niiombe Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana kwa karibu na MTA na wadau mbali mbali wa sekta ya utalii mkoani Mwanza bila kusahau kuwashirikisha wandishi wa habari kwani kalamu zao zitatusaidia sana katika kutangaza vivutio vyetu vya Mwanza na kanda ya ziwa” alisema Eng. Ndikilo Akizungumzia kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo “Utalii na Maji kulinda hatma yetu” Mkuu huyo mkoa amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda vyazo vya maji na kuhakikisha kuna kuwa na matumizi sahihi na endelevu ya maji kwani maji ni muhimu sana kwa maendeleo ya sekta ya utalii. 
Amedokeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la Utalii duniani UNWTO matumizi ya maji duniani yanatarajiwa kuongezeka maradufu kutokana na kuendelea kuongeza kwa watalii duniani na miundo mbinu mbalimbali ya sekta ya utalii duniani. Mapema mkuu huyo wa mkoa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi aitembelea mabanda ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Maji, taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na binafsi na wadau wa sekta ya utalii wanaoshiriki maonesho hayo kutoka Dar es salaam, Mwanza, Kagera, na nchi jirani ya Uganda. 
 Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake Septemba 27, 2013 ambayo ndiyo siku ya Utalii duniani, lakini yatahitimishwa tarehe Sptemba 29, 2013.
 Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania –TTB Bw. Geofrey Tengeneza akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo namna Bodi hiyo ya Utalii inavyotekeleza majukumu yake.  

 Eng. Evarist Ndikilo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza akitia saini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Maliasili na utalii wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza muda mfupi baada ya kufungua maadhimisho ya siku ya utalii duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza. Kulia kabisa ni Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya Utalii Bibi Uzeeli Kiange.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (Mwenye suti nyeusi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya Utalii duniani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza.

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images