Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 262 | 263 | (Page 264) | 265 | 266 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Ambassador Mbelwa Kairuki, Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation welcomes H.E. Lu Youqing, Ph.D., Ambassador of the People's Republic of China to the United Republic of Tanzania prior to their meeting earlier today in the Ministry. 

  Ambassador Kairuki assured H.E. Ambassador Lu of the Government's readiness to continue its strong bilateral ties with the Government of the People's Republic of China.
  The meeting continues between Ambassador Kairuki and H.E. Ambassador Lu Youqing, Ph.D.
  H.E. Ambassador Lu Youqing (left), Ambassador Kairuki (2nd left), listening to Mr. Lin Zhiyong, Chief Representative (Economic and Commercial) for the Embassy of the People's Republic of China in the United Republic of Tanzania.  Also in the photo is Ms. Wang Fang (right), Third Secretary and Representative of Economic and Commercial in the Chinese Embassy. 
  A group photo. 

  By TAGIE DAISY MWAKAWAGO


  The Ambassador of the People's Republic of China says his Government is ever-ready to continue development projects geared for Tanzania, in efforts to alleviate poverty in the long run.

  Speaking during his courtesy visit to the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation earlier today, Ambassador Lu Youqing said there are currently various projects in place that include the gas pipeline project, the Mchuchuma-Liganga twin project that have coal and iron ore deposits that can be mined for over 100 years to come, and the Bagamoyo port, including other infrastructure projects.

  Scheduled for completion by 2017, the port at Bagamoyo is geared to handle 4 million containers. The port also will be joined by a new 34-kilometres road from Bagamoyo to Mlandizi and a 65 kilometres of railway connecting Bagamoyo to the Tanzania-Zambia Railway (TAZARA) and Central Railway.

  For his part, Ambassador Kairuki thanked Ambassador Lu Youqing for his country's continued support.  He highlighted that China has been a strong partner in development of the country in various projects that have direct impact to the people.

  Ambassador Kairuki further assured of the Tanzania Government's cooperation in all projects, which some are expected to be ready during the upcoming 50 years celebration of the friendship, economic and trade cooperation between Tanzania and the People's Republic of China.

  Ambassador Lu Youqing met with Ambassador Mbelwa Kairuki, Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs as further efforts to continue cooperation between the two countries.

  The two countries have had strong bilateral ties dated back to the 1960s, during the time of the founding fathers of these two great nations, that is Mao Zedong and Julius Kambarage Nyerere.

  The 50 years celebration is scheduled to be held next year in China. 

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.

  Ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013..
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara .
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.
   Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.
  Sehemu ya wakazi wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya kuyatatua.
  ==== ======  =====
  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,leo amefanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara .
   Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.

  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.

  Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.
  • Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo
  • Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.
  • Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi.

  0 0


  0 0

  Hello! I know you've been wondering what I have been up to lately since my last release Mapenzi Sumu. Well, I've been preparing something new for You my esteemed supporters... traveling has been also part of the process and during one of my recent trips to Tanzania I hooked up with the young and talented Mr T Touchez of Seductive Records and this Zouk piece "Wasiwasi" is what we came up with. Please find attached a quality mp3 file of "Wasiwasi" single, Wav file available on request! Produced by Mr T Touchez & Mad Ice Recorded at Seductive Records & Epic Studios - Dar es salaam, Tanzania. ©Recordhouse Music
   LISTEN ON SOUNDCLOUD https://soundcloud.com/madiceofficial/wasiwasi
   P.S. Your Feedback, Reviews, Comments and Ratings are more than welcome!
   WASISI VIDEO COMING SOON!! TO BE FILMED & DIRECTED BY SOLOMON LAMBA OF EMPTYSOULZ PRODUCTIONS

  0 0

  OMMY DIMPOZ akifanya vitu vyake
       Poz kwa Poz akifanya vitu vyake
  Maana ya TUPOGO = TUPO NA TUNA GO maisha yanakwenda mbele
  Mwanamuziki Mtanzania aishiye Marekani AJ Ubao Katika Picha na Dimpoz
  Super Promoter DMK Akipata Interview ya Swahili TV na Ommy Dimpoz back stage kabla ya kupanda jukwaani.Mbali na Kuwa Mkurugenzi wa DMK Global Promotions huyu Ndugu pia ni Mkurugenzi wa MMK Media Group,Kampuni ambayo inamiliki Swahili Radio Online,Swahili TV online,na Blog hii ya Swahilitv Blog.
  MR "DMK"  akipata Ukodaki na Warembo ..
  Pia DMK alisherekea Bday Yake siku hiyo hiyo
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA SWAHILITV.BLOGSPOT.COM  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimsikiliza  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Kamalesh Sharma walipokutana mjini New York kwa mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Jumuiya hiyo, ikiwemo maandalizi ya Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali (CHOGM)  unaotarajiwa kufanyika nchini Sri Lanka mwezi Novemba, 2013. Mhe. Membe yupo mjini New York kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68  cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
  Picha na Rosemary Malale

  0 0

  DSC_1114
  Elizabeth Mwase Programu Manager wa Mtandao wa Watoto na Vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) akimpokea Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu wa awamu ya pili ambaye alikuwa mgeni rasmi ya Siku ya Kimataifa ya Amani iliyoadhimishwa mwishoni mwa Juma jijini Dar es Salaam ukumbi wa Don Bosco.
  DSC_1121
  Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akisalimiana na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa jumuiya za maendeleo za nchi wa hisani wakati wa maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
  DSC_1120
  Mgeni Rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akipokea mfano wa ndege wa Amani kutoka kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani duniani jijini Dar.
  DSC_1196
  Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akihutubia wageni waalikwa (Hawapo pichani) wakati wa sherehe za Siku ya Kimataifa ya Amani leo asubuhi jijini Dar. Kulia ni balozi wa Rwanda nchini Ben Rugangazi na kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) Jama Gulaid.
  DSC_1126
  Meza kuu.
  DSC_1130
  Baadhi ya wanafunzi wa sekondari mbalimbali za jijini wakitumbuiza kwa nyimbo mbalimbali zenye ujumbe wa kudumisha Amani na upendo duniani.
  DSC_1216
  Mgeni Rasmi Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mabalozi na wawakilishi wa ofisi za mabalozi waliohudhuria sherehe hizo kwenye ukumbi wa Don Bosco.
  DSC_1143
  Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hizo.
  .awaasa vijana kutotumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao
  .ashangaa wajuzi walivyompachika jina la Ruksa enzi za miaka 1990s
  Na.Mo Blog Team
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema kuna baadhi ya watu katika jamii hutumia elimu, ujuzi na maarifa yao kuangamiza, kubomoa na kudumaza Ustawi wa Jamii kwa maslahi binafsi na si ya Umma. Mo blog inaripoti.
  Mzee mwinyi amesema hayo wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Amani Duniani inayoadhimishwa 21th Septemba kila mwaka ambayo imefanyika katika ukumbi wa Don Bosco jijini Dar es Salaam, amesema kuna baadhi ya watu wanatumia elimu yao vibaya kwa kupanga kuua watu wengine kwa maslahi yao aidha ya kisiasa au ya kiuchumi.
  “Elimu kwa kawaida kuleta matokeo mazuri kwa jamii husika endapo itatumika sawia kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa maendeleo endelevu ya taifa kwa ujumla, ila kuna baadhi ya wanajamii kutumia ujuzi huu vibaya na kuangamiza ustawi wa jamii husika,” amesema.
  Mzee Mwinyi aliendelea kusema kwamba katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya amani duniani yenye kauli mbiu “Education for Peace” ni lazima elimu kwa ajili ya amani iwe endelevu hapa duniani ili iweze kuleta suluhu na utengamano katika jamii na mataifa yote duniani.
  Amesema kwamba vijana nchini lazima waepuke kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao ya kisiasa na wajifunze kutatua matatizo yao kwa njia ya amani bila ya kuwa na mihemko, jazba, misongo na hasira ili kuendelea kudumisha amani na upendo katika nchi yetu ambayo ni kisiwa cha amani.
  “nawaasa vijana wakitanzania wa leo hata kama mmenyimwa haki zenu ni bora kutumia njia ya kistaarabu na kutumia elimu mnayopata mashuleni bila kusahau macho, masikio na vipawa vyenu mlivyopewa na mwenyezi mungu katika kutafuta haki yenu kwa njia ya amani bila misukosuko,” aliongeza.
  Mzee Mwinyi alitumia nafasi hiyo kuwashangaa baadhi ya watu kwa kutumia ujuzi na elimu yao kwa kumpachika jina la Ruksa bila yeye kujua wametumia muktha gani kumpa jina hilo, lakini Mzee Mwinyi alitumia jukwaa hilo pia kuwapa ruksa vijana kutumia elimu yao kuleta hali ya amani na utulivu ndani ya nchi.
  Kwa upande wake, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) Jama Gulaid amesema kwamba Umoja wa Mataifa uliweka maazimio siku ya kimataifa ya amani duniani ili watu wanaogombana na kupigana kwa shida mbalimbali kupata nafasi ya kuweka silaha zao chini katika siku hii adhimu.
  Amesema kupitia azimio hilo ambalo lilizinduliwa mwaka 1982 kwa mara kwanza linatambua uwepo wa watu wanaoathirika na vita katika sehemu mbalimbali duniani na waliokwishapoteza maisha kutokana na matatizo vita vya wenyewe kwa wenyewe.
  Naye Mratibu na Mtathimini wa Mtandao wa watoto na vijana kutoka Imani Mbalimbali (GNRC) Bi, Joyce Mdachi amesema swala la amani na utulivu linaanzia kwenye kaya hadi ngazi ya taifa kwahiyo ni muhimu kwa jamii na vijana kuelewa amani inaanzia nyumbani.
  “jamii iliyolelewa katika mazingira mazuri ina nafasi kubwa ya kuleta matokeo chanya kwenye mustakabali wa taifa kwa ujumla lakini jamii iliyolelewa vibaya haiwezi kubadilisha taifa kwa sababu ni zao la tunda baya,” alisema.
  Mdachi alisisitiza kwamba kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii ya leo swala hilo pia lilianzia kwenye kaya ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa ambapo leo hii taifa linashuhudia mambo ya kifisadi, rushwa na ubadhilifu wa mali za umma kunakofanywa na viongozi waandamizi.

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania
   Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars wakishangilia ushindi
   

   Mwakilishi wa Airtel Tanzania bi Lilian Kibiriti akifurahia ushindi na Wachezaji wa timu ya wasichana ya Tanzania ya Airtel Rising stars mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika
  Kikosi cha timu mabigwa ya Airtel Rising stars Afrika cha wasichana cha Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja pichani waliosimama  (wa mwisho kushoto) ni kocha wa timu ya wavulana Abel Mtweve na wa mwisho kulia ni kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage


   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Nigeria Segun Ognsanya Katikati akiwakabithi captain wa timu ya wasichana Tanzania na kocha wa timu ya wasichana Rogacian Kaijage zawadi za ushindi mara baada ya kuibuka mabigwa wa michuano ya Airtel Rising stars ya Afrika.
  ----------------------------------------
  Timu ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu  nchi Nigeria
  Tanzania ilipata ubigwa huo baada ya kuchuana vikali na timu ya Kenya katika mechi ya Fainali  na kuifunga Kenya goli moja bila na kuibuka mabingwa . Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania.
  Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone , Malawi , na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1 , wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1
  Wakashinda 4-2 katika mikwaju ya penati dhidi ya DRC katika robo fainali mechi zilizopigwa katika uwanja wa NIS Sports. Na wakawatoa Uganda kwa mvua ya magoli 8-1
  Mbali na ushindi huo wa wasichana watanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface
  Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.
  Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita . Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda
  Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo

  Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na  Main bowl .
  Kulianza na “ gala night” jumapili usiku ikafatia  sherehe za ufunguzi , na mechi za ufunguzi za makudi katika uwanja wa AgegeTownship .
  Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili , mashindano haya yamekua bora kwa vijana wadogo na kwakuzingatia jinsia.  0 0


  0 0

  Naibu Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos Makala(wa tatu kulia) akimkabidhi kikombe nahodha wa klabu ya Topland ya mkoa wa kimichezo wa Kinondoni,Omari Akida mara baada ya kuibuka mabi ngwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari National Pool yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Mweka hazina wa chama cha Pool Taifa(TAPA), Zaholo Ligalu.

  KLABU ya Top Land kutoka mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika fainali za kitaifa za mashindano ya Safari Pool 2013, yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Morogoro.

  Top land walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga klabu ya Mpo Afrika ya Temeke 13-10 na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 5,000,000/=, Kikombe na medali za Dhahabu kwa kila mchezaji.

  Mshindi wa pili katika fainali hizo ni klabu ya Mpo Afrika ambayo ilizawadiwa fedha taslimu shilingi 2,500,,00/= na Medali za Fedha kwa kila mchezaji.

  Mshindi wa tatu ni klabu ya Supersport kutoka mkoa wa Manyala ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,250,000/= na medali za shaba na mshindi wan ne ni klabu ya Mashujaa kutoka mkoa wa kimichezo wa Ilala ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi 1,000,000/=

  Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume(singles), mchezaji Festo Yohana kutoka klabu ya Mashujaa ya mkoa wa kimichezo wa Ilala alitwaa ubingwa wa Taifa kwa kumfunga Mussa Mkwega kutoka Morogoro 5-1 na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 700,000/=,Kikombe na medali ya dhahabu ambapo mshindi wa pili ulichukuliwa na Mussa Mkwega ambaye alijinyakulia fedha taslimu shilingi 350,000/= na medali ya Fedha.

  Mshindi wa tatu ni Mohamed Idd kutoka klabu ya Atlantic ya mkoani Dodoma ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/= na medali ya shaba ambapo mshindi wa nne ni Ernest John kutoka Tabora ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/=.

  Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanawake(Singles), mchezaji Rose Deus kutoka mkoa wa Morogoro alitwaa ubingwa wa kitaifa kwa kumfunga Cecilia Kileo kutoka Ilala 5-4 na hivyo Rose kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 350,000/= Kikombe na medali ya Dhahabu ambapo Cecilia alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa fedha taslimu shilingi 200,000/=na medali ya Fedha.

  Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mchezaji Merry Gumbu kutoka Arusha ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 150,000/= na medali ya shaba na nafasi ya nne ilichukuliwa na Judith Machafuko kutoka mkoa wa Kinondoni ambaye alizawadiwa fedha taslimu shilingi 100,000/=.

  Fainali hizo za kitaifa zilihudhuliwa na Naibu Waziri wa Utamaduni,Vijana na Michezo, Amos Makala ambaye alikipongeza chama cha Pool Taifa(TAPA) kwa kuufikisha mchezo hapo ulipo ambapo mpaka sasa umesambaa katika mikoa 17 ambayo ilishiriki mashindano hayo na kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kama serikali kwa kuutambua na kutoa mchaada watakapohitaji.

  Makala pia aliipongeza TBL kupitia Bia ya Safari Lager kwa kuendelea kudhamini mchezo wa Pool kwa mwaka wa sita sasa na kuwaomba waendelee kudhamini kwa miaka ijayo.Lakini pia alimpongeza Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo kwa Brand yake ya Safari kuwa bia namba moja Afrika na kumuomba aendelee kudhamini Pool ikamate namba moja katika mashindano ya Pool ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Malawi hivi karibuni.

  Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo alikipongeza chama cha Pool kwa kumaliza fainali salama na kuahidi kuendelea kudhamini mashindano hayo, lakini pia aliwapongeza Mkoa wa Pwani ambao mwaka huu ni mra yao ya kwanza kushiriki fainali hizo.

  0 0
 • 09/23/13--22:17: ngoma azipendazo ankal

 • Jide haachi kutushangaza. Hebu sikiliza ngoma yake hii mpya 'Yahaya'

  0 0

  Watanzania wenzetu,
   
  Tunapenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba Jumamosi inayokuja (i.e. September 28th, 2013) kutakuwa na ufunguzi wa tawi la CCM Ohio kuanzia saa kumi kamili jioni.
   
  Mgeni rasmi katika ufunguzi huu atakuwa Mheshimiwa  Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania.
   
  Hii ni nafasi ya sisi wote kama Watanzania, sio lazima uwe mwanachama wa CCM au chama chcochote cha siasa ,kupata fursa ya kukutana na watanzania wenzako kutoka miji mbalimbali ya Ohio na Kiongozi/Viongozi wa nchi yetu.
    
  Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
   
  Fredd Mujuni - Mwenyeketi : 216- 225-1585
  Joe Ngwilizi Muhaya - Katibu Mkuu - 330-685-8625
   
  NB: Maelezo ya jina na anwani ya ukumbi yatafata siku chache zinazokuja
   Ahsanteni,
   Mungu Ibariki Tanzania

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere wa CHADEMA, katika hutoba yake fupi, aliwambia   wana DMV kuhusu swala la mchakato wa katiba pamoja na uraia wa nchi mbili na haki ya kupiga kura, aliwataka wana Diaspora wa DMV wambane Rais wa Jumuiya ya Tanzania DMV Bwna Iddy Sandaly.
  Pia mchumba wa Dr Slaa Mama Josephine Mushumbuzi alitoa hotuba fupi katika Mkutano wa CHADEMA DMV Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani.
  Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA, Mke wa Dr Slaa Mama Josephine Mushumbuzi,  katika mkutano wa Tawi la Chadema DMV
  Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA alipokua akitoa hotuba fupi katika Mkutano wa CHADEMA DMV katika ukumbi wa  Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland  Nchini Marekani.
  Hii ni Hotuba fupi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA alipoongelea mchakato wa Katiba mpya na Uraia wa Nchi mbili, katika Mkutano wa CHADEMA DMV Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani.  0 0

  Mhe. Harrison Mwakyembe alipotembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Tanzania House, Washington DC. Katikati ni Mhe. Waziri Harrison Mwakyembe akiwa na ujumbe wake akiwa na baadhi ya maofisa wa Ubalozi huo Bw. Paul Mwafongo (wa tatu Kushoto) na Bw.Suleiman Saleh (wa tatu kulia).
  Mhe. Harrison Mwakyembe(Mb.)Waziri wa Uchukuzi akipokewa na mwenyeji wake Bw.Robert Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Michigan mara baada ya kuwasili hotelini alikofikia.
  Mhe.Waziri Mwakyembe katika picha ya pamoja na Bw. Shumake na Bw. Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC.
  Juu na chini ni Mhe. Mwakyembe katika taswira mbali mbali na Bw. Joelson, Mmiliki wa kituo cha kufundisha Urubani cha DCT katika ziara yake kituoni hapo ambapo alionyeshwa ndege za aina mbali mbali pamoja na kupata historia ya kituo hicho.
  Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati) na Ujumbe wake Bw. Peter Lupatu , Mkurugenzi wa Huduma za Usafiri,Wizara ya Uchukuzi, Bw.Suleiman Saleh Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Eng.K . Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga, Mkurugenzi wa Mradi (Terminal 3 Building), na Bw. Andrew Magombana katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya General Electric ya Erie, Pennsylvania.

  Na Mwandishi wetu, Washington, DC
  Mheshimiwa Dk.Harrison Mwakyembe(Mb.),Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya kikazi nchini Marekani katika miji ya Washington DC, Erie, Pennsylvania na Detroit, Michigan, kuanzia tarehe 18 -22 Septemba, 2013, kwa mwaliko wa Bw. Robert Shumake, Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jimbo la Michigan. 
  Wakati wa ziara hiyo, Mhe.Mwakyembe ambaye alifuatana na Bw. Lupatu, Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji katika Wizara ya Uchukuzi, Eng. K. Kisamfu, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli la Tanzania, Bw. Mohamed Millanga,Mkurugenzi wa Mradi, Terminal Building 3, na Bw. Andrew Magombana, Msaidizi wa Waziri . Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Washington DC na kisha kusafiri hadi Erie,Pennsylvania, kufanya mazungumzo na uongozi wa Juu wa kampuni ya General Electric inayotengeneza injini za treni. 
  Katika mkutano wake huo Mhe.Mwakyembe na ujumbe wake ulipata fursa ya kuelezwa shughuli mbali mbali za kampuni hiyo pamoja na kutembelea karakana kuu ya kampuni hiyo yenye watumishi zaidi ya laki tatu. Akiwa mjini Erie, Mhe.Mwakyembe alipata fursa ya kueleza mikakati iliyopo ya kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania pamoja na kujenga mashirikiano zaidi baina ya kampuni na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha azma hiyo. 
  Baadae Mhe. Mwakyembe na ujumbe wake ulisafiri hadi katika mji wa Detroit,Michigan, ambapo alipokelewa na alifanya mazungumzo na Bw.Shumake,Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye makazi yake katika mji wa Detroit. 
  Akiwa mjini humo Mhe. Mwakyembe alitembelea kituo cha mafunzo ya Urubani ambapo alielezwa historia ya kituo hicho pamoja namna ambayo kituo hicho kitasadia katika kuanzisha kituo cha Mafunzo ya Urubani nchini Tanzania. 
  Aidha Mhe.Mwakyembe alipata wasaa wa kuonyeshwa aina ya ndege mbali zinazotumika katika mafunzo hayo. Kituo hicho kimetoa mafunzo mafunzo kwa marubani 3500 tangu kianzishwe miaka kumi na nane iliyopita.

  0 0

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a High-level meeting on Scaling up Nutrition  in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member

  Each year since 2010 there has been a High-Level Meeting and a series of other gatherings held in New York during the United Nations General Assembly, to increase political attention to the issue of nutrition and encourage greater support for the efforts of SUN countries and the Movement.
  As a result of the dramatic increase in political attention to nutrition throughout 2013, SUN countries and stakeholder groups have sought to create space for more in-depth, structured interaction. The SUN Movement Global Gathering offers an opportunity for this form of interaction. Representatives from SUN countries and across the Movement will participate in the workshop-style event to solve practical bottlenecks and achieve concrete results.
  The purpose of the 2013 SUN Movement Global Gathering is to enhance the Movement’s impact through:
  1. *Demonstrating results in SUN countries – contributing to the learning agenda by focusing on how results can best be achieved;
  2. *Enabling countries to seek solutions to help them scale up nutrition from other countries and networks;
  3. *Bolstering mutual accountability within the Movement – with all constituents – countries, networks, Secretariat and members of the Lead Group giving accounts of their contributions; and
  4. *Envisioning the Movement beyond 2015.
  5. For more CLICK HERE
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks during a meeting on Scaling up Nutrition held in New york this morning. To his left is Dr. Ngozi Okonjo-Iweala, Nigeria's Minister of Finance, and SUN Lead Group Member, behing hi with red tie is Tanzania's Minister for Health Dr Hussein Mwinyi, left is personal assistant to the President on Nutrition  Dr Wilbrad Lorri

  0 0


  MABINGWA ARS KUPONGEZWA DAR
  Timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Airtel Raising Stars (pichani) ya Tanzania imeandaliwa hafla ya kuipongeza kwa kunyakua ubingwa katika mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Nigeria.

  Hafla hiyo ya kuipongeza pamoja na kupata chakula cha mchana itafanyika leo (Septemba 24 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski na kuongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.

  Timu hiyo iliyorejea nchini jana (Septemba 23 mwaka huu) usiku katika mchezo wa fainali ya mashindano hayo iliifunga Kenya. Kwa upande wa wavulana, timu hiyo ilitolewa na Zambia katika hatua ya nusu fainali.

  Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka nchi za Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, Gabon, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Kenya, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia.

  Kombaini ya timu hizo zilizokuwa chini ya makocha Rogasian Kaijage na Abel Mtweve iliundwa baada ya mashindano ya Airtel Raising Stars yaliyohusisha wasichana na wavulana wenye umri wa chini ya miaka 17 na kufanyika jijini Dar es Salaam wiki ya kwanza ya Septemba mwaka huu.

  TWIGA STARS YAPANGIWA ZAMBIA AWC
  Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) imepangiwa kucheza na Zambia katika mechi za kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika mwakani nchini Namibia.

  Twiga Stars itaanzia ugenini jijini Lusaka ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Februari 13 na 15 mwakani wakati ile ya marudiano itafanyika kati ya Februari 28 na Machi 2 mwakani jijini Dar es Salaam.

  Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia, raundi ya pili ambayo ndiyo ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe. Mechi ya kwanza itakuwa Dar es Salaam kati ya Mei 23 na 25 mwakani wakati ile ya marudiano itakuwa kati ya Juni 6 na 8 mwakani.

  Nchi 25 zimeingia katika mashindano huku mabingwa watetezi Equatorial Guinea, makamu bingwa Afrika Kusini na Cameroon iliyoshika nafasi ya tatu katika fainali zilizopita zikiingia moja kwa moja katika raundi ya pili.

  RHINO KUIKARIBISHA ASHANTI ALI HASSAN MWINYI
  Rhino Rangers na Ashanti United zinapambana katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) itakayochezwa kesho (Septemba 25 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

  Wakati Rhino Rangers ilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi yake iliyopita jijini Tanga dhidi ya Mgambo Shooting Stars, Ashanti United inashuka uwanjani huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kutandikwa mabao 3-0 na Kagera Sugar katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Ofisa Habari
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

  0 0

  Mnara wa CN (The CN Tower) uliopo katikati ya jiji la Toronto, Canada, una urefu wa mita 553.33 ama futi 1,815.4, ambao hutumika kama mnara wa mawasiliano na pia kituo cha kuangalia mandhari, ulikamilika kujengwa mwaka 1976 na kuwa jengo refu linalosimama pekee kuliko yote duniani wakati huo.

  Mnara huu ulishikilia rekodi hiyo ya dunia kwa miaka 34 mfululizo kabla ya kukamilika kwa ujenzi wa jengo la Burj Khalifa (urefu mita 829.8 ama futi 2,722) huko Dubai ambao ndio mnara mrefu kuliko yote duniani kwa sasa na Mnara wa Canton huko Guanzhou, China (urefu mita 600 ama futi 2000) ambao ni wa pili kwa urefu,  mwaka 2010. Ila hadi leo mnara huu unabakia kuwa ndio mrefu kuliko yote katika ukanda wa Magharibi, ukiwa alama kuu ya Toronto na nembo ya nchi ya Canada, ukivutia watalii takriban milioni mbili kwa mwaka.

  Jina lake la CN linatokana na lile la Canadia National, ambalo ni shirika la reli la Canada lililoujenga. Kufuatia uamuzi wa kubinafsisha mali za shirika hilo mwaka 1995, umiliki wake ukahamishiwa kampuni ya ardhi (Canada Lands Company.

  Mwaka 1995 mnara wa CN ukatangazwa kuwa moja ya maajabu saba ya dunia na jumuiya ya wahandisi wa majengo ya Marekani, na pia ni mojawapo ya majengo yaliyo chini ya Shirikisho la Minara Mikubwa duniani, mnara wa CN ukishika nafasi ya pili.

  0 0


  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) na Rais wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China Tanzania (CBCT), Bw. Zuang Zaisheng wakitiliana saini mkataba wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu).  Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginald Mengi (waliosimama kushoto) na Balozi wa China Tanzania, Balozi Lu Youqing.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) akibadilishana nyaraka ya makubaliano ya mkataba wa ushirikiano na Rais wa Umoja wa Wafanyabiashara wa China Tanzania (CBCT), Bw. Zuang Zaisheng baada ya kutiliana saini katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu).  Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginald Mengi (wa pili kushoto) na Balozi wa China Tanzania, Balozi Lu Youqing (wa pili kulia).

  -----------------------
  Taasisi ya sekta Binafsi nchini (TPSF) imewashauri wafanyabiashara wa China kuingia ubia na watanzania kwa faida ya nchi zote mbili.
  Mwenyekiti wa TPSF, Dkt. Reginald Mengi ametoa rai hiyo katika hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya kushirikiana kati ya TPSF na umoja wa Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania (CBCT).
  “Tunapenda kuona wakishirikiana na wafanyabiashara wa Tanzania hasa katika uwekezaji wa viwanda kwa lengo la kusaidia maendeleo ya nchi hii,” alisema Dkt. Mengi mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu).
  Alisema kama wawekezaji wa China watakuja na kuwekeza bila kuwashirikisha watanzania, uwekezaji huo utakuwa wa upande mmoja na watanzania wataendelea kuwa masikini.
  Alitoa changamoto kwa wawekezaji wa China kuwekeza kwenye viwanda vya kuyaongezea thamani mazao ya Tanzania ili bidhaa zake zipelekwe kwenye masoko ya China na nchi mbalimbali na kuuzwa kwa bei nzuri.
  “Pia wafanyabiashara wa China wafuate sheria za nchi wanapoingiza bidhaa zao na kuzingatia ubora,” alisema.
  Alisema makubaliano yaliyofikiwa kati ya CBCT na TPSF yatazidi kuchochea mahusiano mema ya kijami, kisiasa na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
  Naye Balozi wa China nchini, Bw.Lu Youqing alisema China na Tanzania zina historia ndefu za urafiki.
  “Tuna ushirikiano mkubwa na sasa mahusiano ya kibiashara yamekuwa makubwa sana,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa kuna wafanyabiashara zaidi ya 500 wa Kichina hapa Tanzania.
  Aliongeza kusema kuwa wameingiza utalaamu na teknolojia katika uzalishaji katika kuelekea kwenye mapinduzi ya viwanda.
  Alisema mahusiano ya kibiashara kati ya TPSF na CBCT ni chachu na ni moja ya hatua katika kukuza uchumi wa Tanzania.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Bw.Godfrey Simbeye alisema wafanyabiashara wa China kupitia CBCT wamesaini makubaliano hayo katika jitihada za kuimarisha ushirikiano na biashara hapa nchini.
  “TPSF ni chombo cha juu cha sekta binafsi, wakiwemo wafanyabiashara wa ndani na wageni na ndicho kinacho wasemea wote serikalini,” alisema.
  Alisema makubaliano hayo yatawawezesha wafanyabiashara hao kuweza kutoa maoni yao juu ya maswala mbalimbali yanayowahusu kibiashara hapa nchini kupitia TPSF.
  Aliongeza kusema taasisi yao inaendelea kuzungumza nao ili CBCT iweze kuwa mwanachama kamili wa TPSF.
  Rais wa CBCT, Bw. Zuang Zaisheng alisema mahusiano hayo ya kibiashara yanalenga wafanyabiashara wa china na Tanzania kuwa kitu kimoja kibiashara.
  “CBCT itaendelea kuwaeleza wafanyabiashara wake waje kufanya  biashara Tanzania na kuwekeza zaidi huku wakiheshimu utamaduni na sheria zilizopo,”alisema.


  0 0
 • 09/24/13--00:49: KIJIWE CHA UGHAIBUNI

older | 1 | .... | 262 | 263 | (Page 264) | 265 | 266 | .... | 3285 | newer