Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MICHUZI TV: HARMONIZE AWASHA MITAMBO ZANZIBAR WASAFI FESTIVAL 2018


BENKI YA NMB KUWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 100 WATEJA WAKE!

$
0
0



Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa (katikati) akizungumza na wanahabari Dar es Salaam leo (hawapo pichani) kuhusiana na kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki na Mauzo wa NMB, Omari Mtiga (kushoto) akifafanua jambo kwa wanahabari katika mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa akifuatilia.
Mkutano na wanahabari ukiendelea Ofisi Kuu za Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam leo.



BENKI ya NMB imezinduwa kampeni ya matumizi ya 'NMB Mastercard' au 'NMB Masterpass' inayojulikana kama 'MastaBata', ambapo wateja wanaofanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo huo watajishindia fedha taslimu, simu janja pamoja na safari ya kwenda mapumzikoni Dubai.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Kadi wa Benki ya NMB, Bw. Boma Raballa alisema katika kampeni hiyo zaidi ya shilingi milioni 100 zitashindaniwa.Alisema takribani wateja 200 wa NMB ambao watafanya malipo kwa mfumo wa 'NMB Mastercard au 'NMB Masterpass' watakuwa kwenye uwezekano wa kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ile kubwa ya kujishindia safari ya mapumziko iliyolipiwa kila kitu kwenda Dubai ukiwa na mwenza wako kwa siku nne.

Aliongeza kuwa shindano hilo litaendeshwa kwa miezi miwili kuanzia leo , huku likiwa na lengo la kuwahamasisha wateja wetu kutumia 'NMB MasterCard' kulipia huduma na bidhaa kwenye vituo vya malipo hayo (POS) au malipo kutumia mtandao (E-commerce). Aidha wateja wa NMB wanaofanya malipo pia kwa kutumia 'NMB MasterPass QR pia wanaingia katika kampeni hiyo.

"Kampeni hii licha ya kuhamasisha matumizi ya malipo kwa kutumia kadi pia imelenga kuwazawadia wateja wetu ambao wanaenda sambamba na safari ya mabadiliko kuingia mfumo wa huduma za kidijitali za kibenki," alisema Raballa.Akifafanua zaidi alisema kutakuwa na washindi 20 kwa kila wiki ambao watajishindia shilingi 100,000 ndani ya kipindi hicho cha miezi miwili, huku washindi wengine 6 wa mwezi kuibuka na simu janja za kisasa 'Samsung S9+' na mwisho washindi wengine 3 kati yao wawili kujishindia safari ya mapumziko kwenda Dubai iliyolipiwa kila kitu.

Aidha alibainisha kuwa, washindi wa Safari hiyo ya mapumziko wataruhusiwa kwenda pamoja na rafiki mmoja chaguo la mshindi na kulala katika hoteli ya hadhi ya nyota tano Dubai kwa siku 3.

Wataalam Muhimbili Wapigwa Msasa Kuhusu Sheria ya Manunuzi

$
0
0




Mtoa mada kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Mary Swai akitoa mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 kwa wataalam wa manunuzi, fedha, wakaguzi wa ndani pamoja na wataalam wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mafunzo hayo ya siku nne yamebeba mada mbalimbali kuhusu sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.
????????????????????????????????????
Washiriki mbalimbali wakimsikiliza mtoa mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011 kwenye ukumbi wa NPC I katika hospitali hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa hospitali hiyo, Gerald Jeremiah akifuatilia mada na aliyesimama ni mtoa mada wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Castor Komba akiwa pamoja na washiriki.
????????????????????????????????????
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo leo yanayohusu sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.
????????????????????????????????????
Mtoa mada kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Mhandisi Mary Swai akisisitiza jambo katika mafunzo hayo leo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada kuhusu sheria ya manunuzi ya mwaka 2011

Article 8

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 12,2018

JAFO AWATAKA WAKANDARASI KUONGEZA KASI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amewataka wakandarasi wanaojenga barabara ya lami ya Kisarawe – Maneromango kwa kipande kinacho endelea cha wastani wa Kilometa sita kuongeza kasi ya ujenzi. 

Waziri Jafo amewataka wakandarasi hao wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayojengwa wilayani Kisarawe. Barbara hiyo yenye urefu wa kilometa 54.8 inayojengwa kwa awamu mbalimbali itawasaidia sana wananchi wa wilaya ya Kisarawe na watalii mbalimbali wanaokwenda kutembelea mbuga ya selous kupitia Kisarawe .


Waziri Jafo ambaye ni Mbunge wa Kisarawe akiongea na moja ya mkandarasi anayejenga barabara ya Kisarawe – Maneromango kwa kipande cha Kazimzumbwi 

 Waziri Jafo akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Kisarawe katika ukaguzi wa barabara ya Kisarewe – Maneromango 

 Wakandarasi wakina katika harakati za ujenzi eneo la Kazimzumbwi .

MAHAKAMA YAAMURU MADINI YA THAMANI YA 2.5/- YATAIFISHWE KUWA MALI YA SERIKALI

$
0
0
Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru madini yenye thamani ya Sh. bilioni 2.5 yataifishwe na kuwa mali ya serikali kwasababu ukwepaji wa kodi ya mrabaha unasababisha Taifa likose mapato.

Pia Mahakama imeamuru wafanyabiashara watatu wa madini wakiwemo raia wawili wa China na mmoja wa India kulipa faini ya Sh.milioni moja kila mmoja au kutumikia kifungo cha miezi miwili kila mmoja.

Wafanyabiashara hao ni Chang Xu, Kai Jiang, Ashok Lavingia na Kampuni ya Sino Africa Collection Ltd waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kuwasilisha taarifa za uongo kwa Kamishna wa Madini kwa lengo la kukwepa malipo sahihi ya mirahaba.

Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema washitakiwa wanatiwa hatiani kwa kukiri kosa na katika kila kosa kila mshitakiwa atatakiwa kulipa Sh. 200,000 na kifungo cha miezi miwili ambapo jumla ni Sh.milioni nne na kifungo cha miezi miwili.Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori aliiomba Mahakama kutaifisha madini hayo chini ya Sheria ya Madini inayosomwa sambamba na sheria ya Uwazi na Uwajibikaji ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, alidai washitakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na makosa yao yanagusa masuala ya rasilimali za nchi.Alidai kesi hiyo inalenga ukwepaji kodi ambayo ndio uchumi wa nchi na unategemewa katika vitu vyote vinavyofanyika kwa wananchi wa Tanzania, hivyo wanaomba adhabu kali itolewe kwa washitakiwa kulingana na sheria zilizopo kwa lengo la kutunza rasilimali za madini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

NAIBU WAZIRI OLE NASHA ASHIRIKI ‘MSARAGAMBO’ WILAYANI SAME

$
0
0

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameshiriki ‘msaragamo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro.

Mheshimiwa Ole Nasha ameshiriki ujenzi huo na Wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani wakati wa ziara ya kukagua miradi ya Elimu katika Wilaya ya Same ambapo amewataka wananchi kuendeleza jitihada hizo ili kuweza kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusoma.

Kufuatia jitihada hizo za Wananchi Naibu Waziri Ole Nasha kupitia Wizara yake ameahidi kujenga vyumba viwili vya madarasa, mabweni mawili na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Ruvu ikiwa ni kuunga mkono juhudi ambazo wananchi wa kijiji cha Ruvu Darajani wameonesha lakini pia kuwezesha wanafunzi kutulia shuleni na kusoma.

“Serikali ikiona eneo ambalo wananchi wameanza na wana hamasa kubwa ya kujiletea maendeleo haiwezi kusita kuja kusaidia, Wilaya ya Same mmeonesha mfano kupitia utaratibu wenu wa msaragambo tunaunga mkono jitihada hizo kwa kuwajengea vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo,” aliongeza Naibu Waziri Ole Nasha.

Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani ambao wanajihusisha na shughuli za ufugaji kutotumia watoto kuchunga mifugo badala yake kuhakikisha wanatumia fursa ya Elimu bure kuwaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki alimweleza Naibu Waziri wa Elimu kuwa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Ruvu imetokana na ongezeko la Wanafunzi waliohamishiwa shule hiyo kutokana na shule walizokuwa wakisoma miundombinu yake kuathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua za masika zilizonyesha mwaka huu.

Katika ziara hiyo Naibu Waizri Ole Nasha pia alitembelea shule ya Sekondari Makanya, Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Same na Shule ya Sekondari Same ambapo ameridhishwa na namna ukarabati ulivyofanyika katika shule hiyo kongwe.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akishiriki ‘Msaragambo’ wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Ruvu iliyoko Kata ya Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara kukagua miradi ya Elimu inayotekelezwa katika Wilaya hiyo. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akikagua ukarabati wa miundombinu uliofanyika katika Shule ya Sekondari Same iliyoko Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Ameridhishwa na namna ukarabati huo ulivyofanyika na kuwataka kutunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ruvu Darajani Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Amewataka kutumia fursa ya Elimu bure kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule. 

BENKI YA TPB YAANDAA MKUTANO WA BENKI ZA AKIBA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0


FUATILIA
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kwa makini mkutano wa mabenki ya akiba Afrika Mashariki. Mkutano huo uliofanyika Zanzibar ulijumuisha wajumbe kutoka benki ya akiba Uganda na Kenya. Dhumuni la mkutano huo ni kujadili changamoto pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia benki za akiba nchini humo.
pamoja
Uongozi wa Benki ya TPB wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wa mabenki ya akiba Afrika Mashariki. Mkutano huo uliofanyika Zanzibar ulijumuisha wajumbe kutoka benki ya akiba Uganda na Kenya. Dhumuni la mkutano huo ni kujadili changamoto pamoja na fursa mbalimbali zilizopo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia benki za akiba nchini humo.

RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO

$
0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu

Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara wa Halmashauri mkoani hapa jumla ya vitambulisho 25,000, vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.

Akikabidhi vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia wajasiriamali wadogo kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu na kuwafanya kunufaika na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa vitachangia pia kuwaibua wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais, huku akiwaonya na kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa njia ya udanganyifu.

“Niwatahadharishe wafanyabiashara wasije wakatumia nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali wadogo, kufanya udanganyifu wowote wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo; huu udanganyifu hatutaupa nafasi na sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha kila mtu anachofanya, mahali anapokaa, historia yake ya biashara”

“Ofisi za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha maafisa Biashara kwenda vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini walengwa wa vitambulisho hivi ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho hicho,kwa hiyo kuna kadi zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali walipo walengwa” alifafanua Mtaka.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka, ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.

WAZIRI MHAGAMA AITAKA MENEJIMENTI YA OFISI YA WAZIRI MKUU KUZINGATIA HAKI NA USAWA KUTATUA KERO ZA WATUMISHI

$
0
0



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ameitaka Menejimenti ya Ofisi yake kushughulikia kero za watumishi kwa haki na usawa ili kumaliza kero zilizopo.

Ameyasema hayo wakati wa Mkutano na Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu walipokutana kujadili masula yanayowakabili wawapo kazini uliofanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi wa LAPF Dodoma.

Waziri aliwataka Watendaji wa ofisi yake kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watumishi kuhusu madai mbalimbali ikiwemo; kupanda madaraja, uhamisho, usalama mahali pa kazi na masuala ya kuzingatia afya wawapo kazini ili kuhakikisha wanatekeeleza majukumu yao katika mazingira rafiki.

“Kama kuna motisha kubwa kwa mtumishi ni kumsaidia kutatua kero yake inayohusiana na utumishi wake kwa uzito unaolingana na tatizo au uhitaji wake ili kusaidia kuongeza morali yake katika kufanya kazi.”Alisema Mhagama.Sambamba na hilo waziri aliwaasa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia mabaraza ya Wafanyakazi katika kujadili na kutatua kero wanazokabiliana nazo wawapo kazini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akiongoza kikao cha pamoja na Watumishi wa Ofisi hiyo walipokutana akujadili masuala yao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kuendelea kufanya kazi kwa umoja, mkutano huo ulifanyika Desemba 10, 2018 katika Ukumbi Mikutano wa LAPF Dodoma.
P2-min
Katibu Mkuu Ofisi yaWaziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
P6-min
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mkutano huo.
P3-min  
Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama  (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

NAIBU WAZIRI AWESO ATOA MAAGIZO KWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI PROFFESA MKUMBO

$
0
0

NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Kitila Mkumbo kumtafutia kazi nyingine Mhandisi wa maji Wilaya ya Pangani Novath Wilson kutokana na kushindwa kusimamia ipasavyo miradi ya maji wilayani humo na kupelekea wananchi kushindwa kupata huduma hiyo muhimu kwa wakati.

Ametoa agizo hilo wakati akiwa wilayani Pangani ikiwa ni ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga alipotembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa wilayani humo na kutokuridhishwa nayo kutokana na utekelezaji wake kuwa chini ya kiwango hatua iliyomlazimu kuzivunja baadhi ya kamati za usimamizi wa maji ambapo ziara hiyo alianzia wilayani Muheza

Licha ya mhandisi huyo kutoa sababu mbalimbali ya baadhi ya miradi kukwama kutoa maji lakini Naibu Waziri huyo alionyeshwa kutokuridhishwa na majibu hayo kutokana na baadhi ya maelekezo aliyokuwa akimpa ili kuweza kukabiliana na changamoto juu ya miradi hiyo.

“Nimekuita marangapi Wizarani tena nikakukutanisha na viongozi wengi labda watakusaidia na kila mara nakupigia simu lakini bado unaonekana si mtendaji wa kazi sasa nitamwambia Katibu Mkuu wetu akutafutie kazi sehemu nyingine lakini sio hapa Pangani”Alisema Aweso.

NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso wa kwanza kulia akikagua mabomba yatakayotoa maji eneo la Kilapula ambayo yatapeleka maji wilayani Muheza  kutoka Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Tanga kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maji kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Tanga Uwasa Mhandisi Jofrey Gerald
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia wakati wa ziara yake
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua moja ya miundombinu ya maji wilayani Pangani
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akipanda juu kuangalia tanki ya kuhifadhiwa maji eneo la Ngomeni wilayani Muheza ambapo mradi huo unatoa maji katika eneo la Pongwe Jijini Tanga na kuyapeleka wilayani humo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.


TAZAMA LIVE RAIS DKT.MAGUFULI NA WAZIRI MKUU WA MISRI WAKISHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI MRADI WA UMEME RUFIJI

MTALAAM BoT AFAFANUA UKUAJI WA UCHUMI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

UKUAJI wa uchumi wa Taifa kutojionesha katika  kuongezeka kwa kipato cha kila mwananchi ni jambo la kawaida ambalo halimaanishi kuwa takwimu za ukuaji huo wa uchumi ni za kupikwa.

Hayo yameelezwa kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Suleiman Missango alipokuwa akitoa mada katika semina kwa waandishi wa habari za uchumi na biashara
inayoendelea jijini Dodoma.

Akifafanua Dk Missango alisema kuwa takwimu za ukuaji wa uchumi zinatokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa jumla katika taifa ambapo mapato yake yanatofautiana katika kumwendea kila mmoja kutegemeana na shughuli za uzalishaji.

Akitoa mfano kuhusiana na suala hilo, alisema kuwa shughuli za uzalishaji za jamii moja zinaweza kuwa zimeongezeka kwa kuhesabu wastani wa ongezeko la uzalishaji, lakini haina maana kuwa kila mwanajamii atakuwa ameona ongezeko katika kipato chake, kutokana
na shughuli za kiuchumi alizonazo.

Katika siku za karibuni kumekuwa na malalamiko miongoni mwa wananchi wakihoji takwimu za ukuaji wa uchumi zinazoonekana kuimarika ilhali wananchi wengi wamekuwa hawana pesa. Uchumi wa Tanzania unakaridiwa kukua kwa kasi ya asilimia 7 kwa mwaka.Dk Missango alisema kuwa hali ya baadhi ya wananchi kupungukiwa fedha mifukoni inatokana na kupunguza matumizi yao ya kawaida na kuyaelekezwa katika matumizi ya maendeleo, ambapo athari za kushuka chini (trickledown effect) hupungua.
 Mkurugenzi wa Sera za Uchumi na Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Suleiman Misango akifafanua kuhusu hali ya uchumi kwenye mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na biashara mjini Dodoma
Meneja wa Idara ya Itifaki na Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zaria Mbeo (kushoto), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Idara ya uchumi wa BoT, Tawi la Dodoma
 Mwenyekiti wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na fedha, Nurdin Selemani kutoka Azam Media, akijadiliana jambo na mtunza muda wa mafunzo hayo, Bakari Kimwanga kutoka Gazeti la Mtanzania Bakari Kimwanga (aliyekaa)
 Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) wakifuatilia mjadala wakati wa semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha inayoendelea mjini Dodoma.


BREAKING NEWZZZZ:MAHAKAMA KUU KITENGO CHA UHUJUMU UCHUMI YAMHUKUMU RAIA WA MSUMBIJI KIFUNGO CHA MAISHA

$
0
0
Ni baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 3.03

 Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar  es Salaam, imemuhukumu Mwanamke mmoja  wa Msumbiji Ana Moisie Chissano kifungo cha maisha  baada ya kupatikana na hatia  katika  shtaka  la kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.

Mshtakiwa  amefungwa chini  ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria Kuzuia na kusababisha na kupambana na dawa za kulevya.

Hukumu  hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Jaji Lilian  Mashaka baada upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka hayo pasipo Kuacha shaka baada ya kuridhika na ushahidi  wa mashahidi sita wa  upande wa mashtaka waliofika mahakamani  hapo kutoa ushahidi wao.

Aidha Mahakama  imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.
 Mshtakiwa Ana Moisie Chissano raia wa Msumbiji  aliyehukumiwa kifungo cha maisha  baada ya kupatikana na hatia  katika  shtaka  la kukutwa na Kg 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
Pichani kati ni Mshtakiwa  akiwa  katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi akisubiri kusomewa hukumu yake


MAJALIWA AMPOKEA WAZIRI MKUU WA MISRI, DKT. MOSTAFA MADBOULY

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkaribisha Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly ambaye aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Desemba 11, 2018 kwa ziara ya siku mbili nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na  Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly ambaye aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Desemba 11, 2018 kwa ziara ya siku mbili nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa  Madbouly kwenye hoteli ya Hyyat Regency  jijini Dar es salaam, Desemba 12, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  

Serikali yaipongeza Xprize Foundation kwa kuonesha njia ya kusaidia watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu

$
0
0
SERIKALI imepongeza mradi wa XPRIZE kwa kuonesha njia nyingine ya kuwapatia elimu ya kusoma, kuandika na kuhesabu watoto wengi walio nje ya mfumo rasmi wa elimu. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wakati alipotembelea wilaya ya Mkinga, ikiwa ni mojawapo ya wilaya sita (6) za Mkoa wa Tanga, zinazonufaika na mradi huo. 
Akizungumza katika mahojiano, Katibu Mkuu huyo alisema kwamba kinachowaondoa watoto wengi katika masomo si lazima iwe mimba kwani wapo watoto wengi hasa wakiume ambao wanakimbia majumbani na kukosa haki yao ya msingi ya elimu. “Huu mradi umetuonesha njia nyingine kabisa ya kukabiliana na tatizo hili. “ anasema Dk Akwilapo ambaye amesema ni sera ya serikali ya kuhakikisha kwamba watoto wote hata wale ambao hawakuingia katika mfumo rasmi wanaingiza katika mfumo wa elimu kwa kupitia taratibu mbalimbali. Miongoni mwa taratibu hizo ni utaratibu wa MEMKWA kwa elimu ya msingi na MESPA kwa sekondari. Alisema mradi huo wa MEMKWA umeonesha matokeo mazuri kwa sasa kwani tayari watoto 800 wamefikishwa katika shule wakafanyiwa mitihani na kuingizwa kuendelea na madarasa ya pili.
Mradi wa XPRIZE ambao utamalizika mwaka kesho ukitumia vishkwambi katika mafunzo kwa watoto waliokosa elimu ya msingi kufikia miaka 9, ni mradi wa dunia ambapo teknolojia inajaribiwa kusaidia wale waliokosa nafasi ya kuingia shule. Akizungumzia hatima ya mradi huo, Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  alisema kwamba mafanikio yake yatawezeshwa kutengenezwa kwa moduli za kufundishia watoto walio nje ya mfumo rasmi wanaotumia lugha ya Kiswahili.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akibadilishana mawazo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham mara baada ya kuwasili katika ofisi za mkoa wa Tanga mwishoni mwa juma wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham pamoja na Mwakilishi wa Global Learning Xprize, Elianne Philibert  wakipokea taarifa fupi kwenye ofisi za Kaimu Katibu Tawala wa  mkoa wa Tanga Bi Monica Kinanan kabla ya kuelekea kukagua mradi wa XPRIZE uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo (kulia), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos(kushoto) wakipata maelezo ya kifaa maalum kinachotumia umeme wa jua kuchajia Vishkwambia kutoka kwa Mtaalamu wa Tehama wa mradi wa XPRIZE Tanga, Bw. Xavery Njovu wakati wa ziara ya kukagua mradi huo uliopo katika kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo akiangalia jinsi mmoja wa watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu anavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE.
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (WFP), Wendy Bigham wakitazama jinsi watoto wa kijiji cha Mwanyumba, kitongoji cha Majengo, Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga walio nje ya mfumo rasmi wa elimu wanavyojifunza kusoma, kuandika na kuhesabu kupitia Vishkwambi hiyvo wakati wa ziara ya kukagua mradi wa XPRIZE mkoani humo mwishoni mwa juma.oa wa Tanga.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAHAFALI YA MRADI WA MALEZI NA MAKUZI KWA WATOTO (PLAY LAB) YAFANA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


MRADI wa malezi na makuzi kwa watoto (Play lab Program) wamefanya maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.

Mradi huo wa malezi na makuzi kwa watoto hujifunza kupitia elimu ya malezi kwa wazazi, ulinzi na usalama kwa watoto.

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana amesema elimu waliyoipata watoto hawa ni msingi mkubwa katika kuwaandaa na elimu ya awali na wenine shule ya Msingi ambapo imetia chachu katika kuwaimarisha watoto katika maendeleo ya kiakili , kimwili, kihisia na lugha.

John amesema, kupitia mradi huu wazazi wa watoto wamepewa mafunzo ya malezi kwa watoto wao kwani ni muhimu sana kwa sababu msingi wa ukuaji wa motto huanzishwa na mzazi mwenyewe.

Pia. Amesema wazazi wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki kazi mbalimbali za mradi kama utenenezaji wa vifaa vya asili kwa ajili ya watoto kutumia katika mafunzo yao na hii imesaidia katika kuwajenga watoto wetu kuwa na ujasiri , ukakamavu, kujiamini, kuchangamana na watoto wengine , kuwa na nidhamu bora na hata kuwa na msaada kwa wazazi wake.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke John Bwana akitoa vyeti kwa watoto waliohitimu mafunzo ya malezi na makuzi (play lab) unaoratibiwa na Shirika la Brac Nchini wakati wa mahafali ya pili yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mtathmini wa mradi wa malezi na makuzi (play lab) Lilian Josephat akitoa risali wakati wa maadhimisho ya mahafali ya pili ya watoto kwa mwaka 2018 uliotekelezwa na Shirika la Brac Tanzania na jumla ya watoto 1200 wamefanikiwa kumaliza mafunzo hayo.Watoto wakiwa katika matukio tofauti.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUDAIWA KUTOA RUSHWA KUPATA AJIRA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, MKURANGA 

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa ,Mkoa wa Pwani imemfikisha mahakamani Naziru Mwakangali aliyekuwa anafanya kazi kama kibarua katika mamlaka ya bandari Dar es salaam kwa makosa ya kuahidi kutoa rushwa ya sh.laki nne na kutoa rushwa ya kiasi cha shilingi 390,000,kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa na. 11 ya nwaka 2007. 

Mwakangali alifunguliwa kesi ya jinai namba. 4 ya mwaka 2018 katika nahakama ya wilaya ya Mkuranga, Mkoani hapo.

Akisoma mashtaka mbele ya hakimu wa wilaya ya Mkuranga Tumsifu Barnabas, mwendesha mashtaka wa TAKUKURU, Euphrazia Kakiko ,aliieleza mahakama kwamba mshitakiwa alitenda kosa la kuahidi kutoa rushwa laki nne kwa mtoa taarifa ili ampatie ajira katika kiwanda cha Knauf Gypsum Tanzania Limited wilayani Mkuranga.

Aidha aliieleza ,mahakama kwamba nshitakiwa alitoa rushwa sh. 390,000 kwa mtoa taarifa, jambo ambalo pia ni kosa kisheria .Mshitakiwa alikiri kutenda makosa yote mawili, ambapo alitiwa hatiani na hivyo kupewa adhabu ya kutumikia kifungo jela kwa muda wa miaka mitatu kwa kila kosa ambapo mahakama iliamuru vifungo vyote viende pamoja ama kulipa faini ya sh. 500,000 kwa kila kosa kwa mujibu wa sheria ya kanuni za adhabu, sura ya 16 ya sheria za Tanzania.

Vilevile, mahakama iliamuru fedha zilizokamatwa kwa lengo la kutolewa na mshitakiwa kama rushwa zitaifishwe kuwa mali ya umma kwa mujibu wa sheria.Hata hivyo ,mshitakiwa alilipa faini kama Mahakama ilivyoelekeza.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani, Suzan Raymond anatoa wito kwa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa na badala yake wafuate taratibu zinazotakiwa katika suala zima la utafutaji wa ajira . 

MSANII WA KIZAZI KIPYA DIAMOND PLATNUMZ ATEMBELEA KITUO CHA AFYA CHA CHUMBUNI ZANZIBAR

$
0
0
 Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Nasibu Abdull ( Diamond Platnumz) akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili na Ujumbe wake katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
 Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Nasibu Abdull ( Diamond Platnumz) akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Juma (Pondeza)wapili kushoto na Wasanii wengine mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kituo cha Afya Cha Chumbuni Dkt Mohamed Muslim Mohamed alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
 Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Juma (Pondeza)akitoa hotuba ya makaribisho kwa Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Nasibu Abdull (Diamond Platnumz)kuzungumza na Vijana na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
Msanii wa kizazi kipya ambae ni mkuu wa Wasafi Group Nasibu Abdull ( Diamond Platnumz) akizungumza na Vijana na Wananchi mbalimbali waliohudhuria katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar alipokwenda kutoa msaada kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
 Baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika katika kituo cha Afya cha Chumbuni Zanzibar ili kumuona Nasibu Abdull (Diamond Platnumz) wakati alipofika kituoni hapo na ujumbe wake kwa ajili ya kutoa msaada wa Vitu mbalimbali kwa ajili ya Kinamama wanaokwenda kujifungua kituoni hapo.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>