Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Jumia yazindua BOOM BAMIZA, yakabidhi pikipiki na luninga kwa wateja

$
0
0
Jumia imewakabidhi wakazi wa jijini Dar es Salaam, Bw. Johnson Kiama na Dismas Kamalamo zawadi za pikipiki na luninga mpya ya kisasa walizojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’

Shindano hilo lilikuwa likifanyika kila siku ya Ijumaa kupitia kampeni kubwa ya mauzo ya mwaka ya Jumia inayokwenda kwa Black Friday. Kampeni hiyo ambayo ilianza Novemba 16 na kufikia ukomo Ijumaa iliyopita ya Desemba 7, imewawezesha wateja kufanya manunuzi yao ya msimu huu wa sikukuu kwa ofa na punguzo kubwa la bei mpaka 70%!

Zawadi zote mbili za pikipiki na luninga zilifichwa kwenye mtandao wa Jumia ambapo wateja walitakiwa kuzisaka na kukabidhiwa kwa punguzo la asilimia 99 mara baada ya kuzipata. Zoezi hilo lilifanyika kupitia njia ya App ya Jumia inayopatikana kwenye simu zote za iPhone (Apple Store) na Android (Google Play Store). Dhumuni lilikuwa ni kuwawezesha wateja wengi zaidi, ambao wanamiliki simu za kisasa za mkononi, kushiriki mahali popote na muda wowote walipo.

Pikipiki hiyo aliyokabidhiwa mshindi, aina ya Skymark, inauzwa kwa shilingi 1,850,000 katika mtandao wa Jumia. Lakini mshindi amekabidhiwa kwa kulipia shilingi 18,500 tu ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 99!Huku naye mshindi wa luninga mpya na ya kisasa aina ya Bruhm yenye ukubwa wa inchi 32 yenyewe inauzwa kwa shilingi 570,000 kwenye mtandao wa Jumia. Lakini mshindi amekabidhiwa kwa kulipia shilingi 5,700 tu ambayo ni sawa na punguzo la asilimia 99!

Akielezea namna atakavyoitumia zawadi yake ya pikipiki mara baada ya kukabidhiwa, Bw. Johnson Kiama, amesema kuwa, “siamini kama leo hii nimekabidhiwa hii pikipiki maana ilinichukua muda mrefu kuipata. 
 Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar leo wakati wakikabidhi  wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam, Bw. Johnson Kiama na Dismas Kamalamo zawadi za pikipiki na luninga mpya ya kisasa walizojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’
 Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi  mbele ya Waandishi wa habari,Bw. Johnson Kiama luninga mpya ya kisasa aliyojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’
Meneja Mahusiano ya Umma wa Jumia Tanzania, Kijanga Geofrey akimkabidhi  ufunguo wa piki piki Dismas Kamalamo mbele ya Waandishi wa habari, aliyojishindia kupitia shindano la ‘Treasure Hunt.’


PLATNAM YAISAIDIA VIFAA VYA MICHEZO JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Na Moses Sebastian

Taasisi ya kifedha ya Platnam Limited inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa watumishi wa Umma na binafsi imegawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa Jeshi la Magereza ili viwasaidie katika michezo ya Majeshi inayotarajia kuanza mwezi Februari 2019.Akimkabidhi vifaa hivyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Musa Kaswaka,Meneja uendeshaji wa biashara Julius Mawinda alisema kuwa vifaa alivyoleta leo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto za upungufu wa vifaa kwa Jeshi la Magereza kwenye mashindano hayo.

“Tutaongeza vifaa vingine baada ya wiki kadhaa ili timu iweze kutokana kabisa na changamoto ya vifaa vya michezo katika michezo hiyo” Alisisitiza Meneja Julius. Akiongea kwa niaba ya Kamishna Jenerali,Kamishna Msaidizi Mwandamizi Musa Kaswaka alimshukuru Meneja uendeshaji wa biashara Julius kwa kuendelea kulijali Jeshi kwa kulipatia vifaa hivyo ambavyo vitaisaidia timu kwenye michezo hiyo.

“Tunashukuru sana kwa kutupatia vifaa hivi na tunaomba msikwamie hapo kwani Jeshi linashiriki katika michezo mingi na linahitaji ‘sapoti’ kutoka kwenye taasisi kama yenu” Aliongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Kaswaka. Vifaa vilivyopokelewa ni pamoja na seti mbili za jezi ya kijani na nyeupe ambazo zitatumika kwenye michezo ya mpira wa wavu(volley ball) na mpira wa mikono(hand ball).  Baadhi ya vifaa vilivyoahidiwa kuletwa hapo baade ni pamoja na shinigads( vikinga ugoko),soksi na mipira. Taassi ya Platnam imekuwa mdau wa siku nyingi na muhimu katika kusaidia shughuli mbalimbali za Magereza na hasa zile zinazohusu michezo.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Musa Kaswaka (kulia) akiwa na Meneja Uendeshaji wa Biashara wa Platnam Julius Mawinda(wa pili kulia) pamoja na maofisa michezo wa Jeshi,wakionesha baadhi ya jezi zilizokabidhiwa leo tarehe 11 Disemba 2018 na Taasisi ya Platnam Makao Makuu ya Jeshi la Magereza. Wa pili toka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Makusanyo wa Platnam Matana Maduhu.

RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. Kikao hicho cha Siku Moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Kupitia Kikao hicho  Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, aliwapongeza Wanachama, Watendaji na Viongozi wote wa CCM kwa kufanikisha Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe ambapo aliyekuwa Mgombea wa CCM Mhe.Ramadhan Hamza Chande alishinda kwa  kura 7,274 sawa na asilimia 90.5.

Dk.Shein alieleza kuwa ushindi huo haukuwa wa bahati mbaya bali ulitokana na ridhaa ya Wananchi wa Jimbo hilo kwa kuridhishwa na kasi ya Utekelezaji kwa vitendo Sera na mipango endelevu ya maendeleo inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Katika maelezo yake Dk.Shein aliwasisitiza Wajumbe wa Kikao hicho na Wana CCM kwa ujumla kuwa Ushindi wa CCM Jang’ombe ni sehemu ya maandalizi ya Ushindi wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa ambao pia ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saada Mabodi(wa kwanza kulia) , Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (wa kwanza kushoto), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto), wakiimba mara baada ya kuingia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Kisiwandui Zanzibar.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kulia) mara baada ya kuwasili Kisiwandui kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum.(Picha na Hussein Khamis na Thani Mosi).

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



NEC YAWATAKA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUZINGATIA SHERIA, TARATIBU ZA UCHAGUZI

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia kanuni,sheria  na miongozo ya Uchaguzi wanaposimamia na kutekeleza majukumu ya uchaguzi. Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaafu Mery Longway katika ufunguzi wa mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Dodoma leo.

Ameeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye jukumu la kusimamia , kuendesha na kuratibu Uchaguzi , lakini wanaosimamia jukumu hilo kwa ukaribu zaidi ni wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo , Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata pamoja na Watendaji wa vituo  vya kupigia Kura.

“Nawakumbusha kuzingatia kanuni, Sheria na Miongozo yote iliyotolewa na itakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kusimamia jukumu hili kwa ufanisi na mafanikio makubwa”. Amesema Mh. Longway.

Aidha amewakumbusha wasimamizi hazo wa Uchaguzi kuwa Uchaguzi ni Mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa ndio msingi wa Uchaguzi kuwa huru wa haki na kupunguza kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa Uchaguzi na hivyo kupunguza kesi mahakamani baada ya Uchaguzi.

Amesema kuwa pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo kuwa wazoefu katika kuendesha Uchaguzi washiriki hao wametakiwa kuhakikisha wanazingatia maelekezo watakayopewa na wakufunzi wa Tume, haitokuwa vyema kutekeleza majukumu hayo kwa mazoea bali wanatakiwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia zoezi la Uchaguzi

Washiriki wa Mafunzo hayo ni Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo , Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata ambao watasimamia Uchaguzi Mdogo wa Umbunge Jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46  utafanyika Januari 19 mwaka 2019.
 Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Mstaafu), Mary Longway akifungua mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo  wa Ubunge utakaodanyika katika jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46 za Tanzania Bara jijini Dodoma.
 Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kutoka katika maeneo mbalimbali wakila kiapo cha kutekeleza majukumu ya usimamizi wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Katika jimbo la Temeke na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara jijini Dodoma.

LUGOLA ATANGAZA KUFUNGUA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO JIMBONI KWAKE MWIBARA, MARA

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola ametangaza kufungua miradi mikubwa mitano ya maendeleo jimboni kwake, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa katika mikutano yake kwa wananchi wa jimbo hilo siku za nyuma. Lugola amesema tayari mipango imepangwa katika kufanikiwa miradi hiyo inafunguliwa jimboni humo ikiwa ni hatua ya kuondoa umaskini kwa wananchi na kuliletea mafanikio makubwa jimbo hilo na Wilaya ya Bunda kwa ujumla, 

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Namhula, Wilayani humo, leo, Lugola alisema mradi mkubwa wa Maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya kumwagilia mazao mbalimbali ikiwemo zao la mpunga katika Bonde la Namhula tayari wataalamu wamefika kulipima bonde hilo pamoja na kuanza mchakati wa mradi huo, pia uwepo wa maji hayo yatasaidia kumwagilia mazao mengine ya nafaka jimboni humo. 

“Mradi mwingine ni wa ufugaji wa kuku wa kienyeji na tuna mashine kubwa za kuangulia vifaranga, maandalizi yapo tayari na eneo la ufugaji huo utakua shule ya Msingi Magunga Kata ya Neluma, pia mradi wa ufugaji wa ng’ombe nyati na ufugaji huo pia utafanyika Sekondari ya Neluma katika Kata hiyo hiyo, na pia tutakuwa na ufugaji wa samaki katika mabonde,” alisema Lugola.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Wananchi wa Kata ya Namhula, Jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola alitangaza kufungua miradi mikubwa ya maendeleo jimboni humo hivi karibuni. Kulia ni Mfanyabiashara wa Chakula cha Samaki cha Aluzola, Saimon Katolilo, ambaye aliitwa na Mbunge huyo kutoa elimu kuhusu bidhaa hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akizungumza na viongozi wa Kata ya Muranda, Jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola alitangaza kufungua miradi mikubwa ya maendeleo jimboni humo hivi karibuni. Kulia ni Diwani wa Kata hiyo, Jogolo Biswalo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Muranda, Juma Mapole. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KAMISHNA WA UTAWALA NA FEDHA WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AAPISHWA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kushoto) akimvua cheo cha zamani na kumvisha cheo kipya cha Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Mbaraka Semwanza katika ukumbi wa mikutano Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi Dar es salaam mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
Kamishna (CF) Mbaraka Semwanza akiapa baada ya kuvishwa cheo kipya cha Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.
Kamishna wa Utawala na Fedha (CF) Mbaraka Semwanza (kushoto) akipokea nyaraka mbalimbali za ofisi ya Utawala na Fedha kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias Andengenye (kulia), baada ya kuapishwa katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.
Makamishna, Wakuu wa Vitengo, Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakishuhudia kuapishwa kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, katika ukumbi wa mikutano Makao Makuu ya Jeshi hilo mapema leo asubuhi tarehe 11/12/2018.

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA JAJI MKUU WILAYANI KONGWA

$
0
0
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa akizungumza jambo katika Kikao kilichoendeshwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa Watendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji mbalimbali wa Wilaya ya Kongwa.
pika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kongwa akizungumza jambo katika Kikao kilichoendeshwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa Watendaji wa Mahakama ya Wilaya ya Kongwa.

President Uhuru's speech as he launches the new currency


BENKI KUU YATAJA FAIDA YA DHAMANA ZA SERIKALI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU

$
0
0

Na Said Mwishehe Globu ya Jamii Dodoma

WATANZANIA wameshauriwa kushiriki kikamilifu katika minada ya dhamana za Serikali kwani faida zake ni kubwa kwa Taifa ikiwamo kufanya shughuli za maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Masoko na Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Alexander Ng'winamila wakati akiwasilisha mada katika mafunzo kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha yalioandaliwa na BoT kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za fedha na uchumi.

Akizungumza wakati akitoa mada inayohusu uwekezaji katika dhamana za Serikali; faida zake kwa Taifa na wawekezaji ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye midana ya dhamana za Serikali.

Amesema ametoa ombi kuendelea kuhamasisha kutolewa kwa elimu kwa umma ili waweze kushiriki kikamilifu na hatimaye kuifanya serikali iweze kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa fedha za ndani."Ombi letu kwa vyombo vya habari tunaomba muendelee kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye dhamana za Serikali.

Kuna faida nyingi na mojawapo ushiriki wao utawezesha Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za ndani badala ya kwenda kukopa nje ya nchi,"amesema.

Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tazania Bw. Alexander Nw'winamila akitoa mada ya uuzaji wa Hati Funagani na Amana za Serikali katika semina ya waandishi wa habari za Fedha na Uchumi inayofanyika jijini Dodoma katika tawi la Benki Kuu ya Tanzania BoT Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo hayo.

Bi. Zalia Mbeo Meneja Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki (BoT) akitoa mchango wake katika semina hiyo kuhusu mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
Mshauri wa Benki Kuu ya Tanzania BoT tawi la Dodoma akifafanua jambo katika semina hiyo inayoendelea jijini Dodoma.

Ukaguzi wa mabasi ni endelevu

$
0
0
Mkurugenzi wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Johansen Kahatano amesema kuwa basi likiwa bovu halina na nafasi ya Kusafirisha abiria kwenda mikoani. Kahatano ameyasema hayo wakati alipokuwa katika ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mabasi yote yaliyokuwa na kasoro askari wameyakagua na hawajaweza kufanya safari mpaka watakapotengeneza.

Amesema kuwa baadhi ya basi walipandisha nauli wameweza kuwabaini na wamewapiga faini ya shilingi 250,000. Kahatano amesema kuwa wamejipanga sawa katika kufanya  ukaguzi  katika cha mabasi Ubungo. Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kutetea Abiria (Chakua) Hassan Mchachama amesema kuwa kazi ya Chakua ni  kutetea abiria kwa mjibu wa sheria. Amesema kuwa abiria akicheleweshwa ndani ya masaa mawili ya asubuhi kampuni husika inalazimika kuwanunua kifungua kinywa kwa abiria wote pamoja na kutafuta mbadala wa basi. Amesema Chakua ndio kimbilio la abiria katika kutafuta haki ya safari.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akifanya kukaguzi katika basi katika kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askari wa Kikosi cha  Usalama wa Barabarani waking'oa namba ya usajili katika basi baada ya kuwa na makosa mengi katika kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Abiria wakiwa wameshuka katika basi walilokuwa wanasafiri na kupatiwa basi mbadala  na kampuni hiyo ni mara baada ya kuibanika na hitilafu nyingi katika ukuaguzi wa mabasi katika kituo mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

WATUMISHI WA UMMA MSIJIINGIZE KWENYE UTUMWA WA MIKOPO YA TAASISI ZISIZO HALALI-WATARA

$
0
0
WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuacha kujiingiza katika mikopo inayowasababisha kuuza uhuru wao na kuwa watumwa kwa wakopeshaji wasio halali na ambao hawajasaliwa na Serikali. Kauli hiyo imetolewa wilayani Nzega na Igunga na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa vikao vya majumuisho na Watumishi wa Wilaya hizo.

Alisema baadhi ya wanawakopesha hawakusajiliwa na hawalipi kodi za Serikali na hivyo kuendesha biashara hiyo kinyume cha Sheria na taratibu za nchi. Waitara alisema wakopeshaji hao wamekuwa wakikopesha kwa riba kubwa ambazo zimewafanya baadhi ya watumishi kuishi maisha magumu yaliyojaa utumwa ndani yake.

Alisema baadhi ya watumishi ambao ukopa wamekuwa wakikabidhi hata Kadi za kuchukua Fedha (ATM) kwa wakopeshaji na inapofika mwisho mwa Mwezi ndio upiga simu kwake ili waende kwenye ATM achukue fedha kwa ajili ya kulipa deni na kidogo za matumizi na baada ya hapo anarudisha kadi mdai wake.

Waitara alisema kitendo kinafanya taarifa za mshahara wa mtumishi kutokuwa siri kwake bali kuwa wazi hata kwa mkopeshaji jambo ambalo ni kuuza uhuru wake. Aliwataka Watumishi wa umma kuishi kulinga na mishahara wanayolipwa na kujiepusha na tamaa ambazo zinaweza kuwasababisha kujiingiza katika matatizo.
 Diwani wa Kata ya Mwanzoli wilayni Nzega Mathias Nyelo (mwenye Kaunda Suti nyeusi) akimwonyesha jana ,Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mwita Waitara( mwenye suti ya kijivu) eneo la Shule ya Sekondari ya Mwanzoli linapoishi wakati kiongozi huyo alipotembelea Wilaya hiyo kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akitoa maelekezo jana kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Nzega Mji inayojengwa eneo la Kitangili mjini Nzega wakati akipokwenda kukagua mradi huo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara(aliye mbele)  akikagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za  Halmashauri ya Nzega Mji inayojengwa eneo la Kitangili mjini Nzega wakati akipokwenda kukagua mradi huo jana.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara(aliye suti kijivu)  akikagua jana maendeleo ya ujenzi wa madarasa katika Shule shikizi ya Izimbili wilayani Igunga.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara akifundisha Hesabu wanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Ziba mada baada ya kumaliza kukagua mradi wa ujenzi wa Hosteli shule hapo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KUHUSU MLIMA WA VOLKANO WA OLDONYO LENGAI

$
0
0
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini Tanzania (GST) inapenda kuufahamisha umma kuhusiana na taarifa ambazo zimesambaa kupitia baadhi ya vyombo vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii juu ya uwezekano wa kulipuka kwa Mlima wa Oldoinyo Lengai ulioko Mkoani Arusha. Mnamo tarehe 9/12/2018 vyombo vya habari vya Aljazeera na CGTN vilitangaza taarifa iliyoelezea kuwepo kwa uwezekano wa kulipuka kwa Mlima Oldoinyo Lengai. Taarifa hizo ambazo zilitolewa kwa lugha ya kiingereza na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zilidai kwamba Mlima Oldoinyo Lengai ungeweza kulipuka muda wowote.

Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na watafiti wa masuala ya jiosayansi ambao wamekuwa wakifanya tafiti za jiosayansi katika eneo la mlima Oldoinyo Lengai hususan kuratibu uwezekano wa kulipuka. Kwa bahati mbaya taarifa zinazopatikana au kutolewa na wataalamu hao huwa sio rasmi kulingana na hatua ya utafiti ambayo inakuwa imefikiwa kwa wakati huo. Taarifa hizo husambaa na kutolewa katika tafsiri nyingi zinazotofautiana na hatimaye kusababisha taharuki na sintofahamu miongoni mwa jamii.

Mlipuko wa volcano ni matokeo ya fukuto la joto kali katika matabaka ya miamba kwenye kina kirefu sana cha ardhi. Fukuto hilo la joto husababisha matabaka ya miamba kuyeyuka na kuwa katika hali ya uji-uji. Kutokana na nguvu za mgandamizo zinazosababishwa na kina cha miamba tabaka hilo la uji-uji (magma) husukumwa na kuelekea juu ambapo hurushwa juu ya uso wa ardhi na hiyo ndiyo volkano. Tabaka hilo la uji-uji huwa lina mchanganyiko wa vitu vingi kutegemeana na kiasili cha miamba iliyohusika katika kuzalisha tabaka hilo. 

Hali kadhalika, linaweza likasababisha kutiririka kwa lava, au kurushwa hewani kwa majivu ya miamba iliyoungua, na vipande vya miamba ambapo huambatana na gesi zenye sumu au kutokea vyote kwa pamoja. Mlima Oldoinyo Lengai ni mlima wenye Volkano ambayo ni ya kipekee duniani kote, ambayo hurusha majivu na lava ya Natrocarbonatite, ambapo majivu huambatana na gesi ya
  
kabon dayoksaidi ambayo husababisha kuwasha au hata kubabuka ngozi na inaweza kusabababisha kushindwa kupumua na hatimaye kupoteza Maisha. Madhara haya ni kwa viumbe wote hai wakiwemo binadamu,wanyama, ndege na wadudu. Lakini pia majivu na lava ya volcano husababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji, kuchafua anga, kufukiwa kwa nyumba na mashamba na maeneo ya malisho ya mifugo. 

Mlima wa Oldonyo Lengai ni miongoni mwa volcano hai duniani. Kumbukumbu zinaonesha kwamba Oldonyo Lengai uliwahi kulipuka mwaka 1883, 1904, 1910, 1913, 1915, 1917, 1926. 1940, 1954, 1955, 1958, 1966, 2007, 2008, 2010 na 2013. Kutokana na historia na ukweli kwamba Oldonyo Lengai ni volcano hai, timu za wataalamu kutoka nchi mbalimbali hususan Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya wamekuwa wakifika kwa lengo la kufanya utafiti ambao hadi hivi sasa haujaweza kutoa taarifa ya kina ya kitaalamu kuhusiana na kutokea kwa volcano hiyo.

Ikumbukwe kwamba kutokea kwa mlipuko wa volkano kunategemea mabadiliko ya miamba hususan kiwango cha joto na nguvu ya msukumo na mgandamizo katika kina kirefu cha ardhi hali ambayo hutokana na nguvu za asili. Kutokana na hali hiyo inakuwa ni vigumu kuweza kutabiri muda, (saa na siku) utakaohitajika kwa eneo husika kufikia kiwango cha msukumo kuweza kusababisha kutokea kwa volcano. Aidha volcano inapofukuta kulipuka husababisha matetemeko ya ardhi pamoja na maporomoko ya udongo katika eneo husika. 

Hii hutokana na kupanda kwa uji wa volcano ambao huiunguza miamba katika njia yake na kusababisha miamba hiyo kukatika na hivyo ardhi kutikisika. Kutokana na maelezo hayo, GST inapenda kutoa tahadhari kwa umma pindi wanapoona dalili za kulipuka kwa volcano wachukue tahadhari, ikiwa ni pamoja na kuondoka katika eneo la kuzunguka mlima umbali wa kilomita 50 ili kuepuka madhara ya majivu, gesi na vipande vya miamba vinavyorushwa kutoka kwenye volcano. 

Hata hivyo GST inashauri kwamba eneo la mlima Oldonyo Lengai siyo eneo salama kwa Maisha ya binadamu na mifugo kwavile hewa inayotokana na volcano ya Oldoinyo Lengai ni hewa ya sumu ambayo haiwezi kuonekana kwa macho kwavile haina rangi. Tunapenda kutoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua stahiki ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa kuhakikisha kwamba watu hawaweki makazi ya kudumu kwenye eneo la mlima Oldonyo Lengai.

IMETOLEWA NA TAASISI YA JIOLOJIA NA UTAFITI WA MADINI TANZANIA
11/12/2018

Tigo Wazindua Malipo ya kielekroniki Serikalini Arusha

$
0
0
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (Auwasa) wamezindua mfumo mpya wa malipo ya kielekroniki serikalini (GePG) katika mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara.

Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa Ankara mbalimbali pamoja na kufanya malipo kutokana na huduma wanazopata kutoka taasisi za serikali zaidi ya 300 lengo ikiwa ni kurahisisha watumiaji wa huduma kutokaa katika misururu. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua mfumo huo , Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Nancy Bagaka alisema kuwa mfumo huo utapunguza kwa kiwango kikubwa ubadhirifu jambo ambalo litaongeza mapato ya serikali.

“Kutokana na mfumo huu faida nyingi zitapatikana ikiwemo kuongeza mapato ya serikali kupitia taasisi na mashirika , kuboresha uwekaji na utunzaji wa kumbukumbu , utoaji taarifa za mara kwa mara pamoja na kuondoa ubadhirifu na wizi” alisema Bagaka. Aidha alisema ili kuweza kulipia Ankara mteja wa Tigo atatakiwa kupiga *150* 01# kisha atachagua kulipia ankra ambapo eneo la malipo ya serikali itajitokeza na kuingiza tarakimu 12 kwa taasisi anayotaka ipokee malipo .

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Auwasa Edes Mushi alisema kutokana na mfumo huo mpya sasa wateja wa Mamlaka hiyo hawatolazimika kukaa katika misururu mirefu wakisubiri kulipia Ankara za maji. “Auwasa kwa kushirikiana na Tigo tunaendelea kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kutumia mfumo huu wa GePG ambao tayari taasisi na mashirika mengi yanautumia” “Mbali na Auwasa, tayari Wizara ya Ardhi na Maenedeleo ya Makazi wanatumia, Shirika na Ndege ATCL , Bodi ya Utalii , Hospitali zote za umma , Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) Wizara ya Mifugo nk .”

“Matumizi ya mfumo huu wa kielektroniki umerahisha utoaji huduma kwa wananchi na umeleta tija kubwa na kuongeza mapato hivyo tunasisitiza wateja wa Tigo wautumie ikiwa ni pamoja na kuulizia ankara zao za malipo ya maji” alisisitiza Mushi. Mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watumiaji milioni 7 wa huduma ya Tigo pesa wanafanya malipo kwa haraka bila usumbufu kwenda kwa wakala ,idara na taasisi kadha wa kadhaa za Serikali.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi akizungumza na wanahabari mjini Arusha jana kuhusu matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG) utakaokuwa ukifanywa kwa kutumia Kampuni ya Tigo kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka. 


Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha jana kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi. 


Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka (kushoto)akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi muda mfupi kabla ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa Kieletroniki wa malipo ya Serikali (GePG), mjini Arusha leo wazungumzaji wakiwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi Arusha (AUWASA), Edes Mushi Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo, Nancy Bagaka 

Jaji Mkuu wa Tanzania akagua shughuli za Mahakama Wilayani Chamwino na Kongwa

WAZIRI WA KILIMO AITAKA TFC KUSHIRIKIANA NA NJORECU KUHARAKISHA UJENZI WA KIWANDA CHA MBOLEA

$
0
0
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza Shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania (TFC) kushirikiana vyema na Chama Kikuu cha Ushirika Njombe (NJORECU) kuhakikisha kuwa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea unaanza mapema kabla ya mwezi June mwaka 2019.

Alisema kuwa ujenzi wa kiwanda cha Mbolea utakapokamilika utawanufaisha wanaushirika wa chama hicho cha NJORECU sambamba na wakulima wote nchini kwani kitaongeza urahisi wa upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu kwa kuzalishwa hapa nchni.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 11 Disemba 2018 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China.

Mhe Hasunga aliwashauri kuandaa andiko la mradi huo litakaloeleza aina ya mbolea itakayozalishwa na taarifa zote zinazohitajika katika kufanikisha mradi huo kuanza.Wawekezaji hao kutoka nchini China kwa kushirikiana na chama kikuu cha Ushirika Njombe (NJORECU) wanataka kuwekeza katika ujenzi wa Kiwanda cha mbolea na kiwanda cha kufungasha Viuatilifu vinavyotumika katika mazao ya Kilimo.

Katika kikao hicho walieleza kuwa wawekezaji hao wapo tayari kuchangia asilimia 40% na NJORECU (kwa maana ya Tanzania) asilimia 60% katika ukamilifu wa ujenzi wa kiwanda hicho.Kutokana na umuhimu na uhitaji wa Mbolea nchini mjumbe wa bodi ya NJORECU alimweleza Mhe Waziri wa Kilimo kuwa wamekwishapeleka maombi ya kuomba kushirikiana na NSSF katika uwekezaji huo na wanasubiri majibu. 

Wakati huo hu, Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI).

engo la mkutano huo ilikuwa ni watendaji wakuu hao kujitambulisha na kumueleza Waziri wa kilimo shughuli wanazozifanya ili kuongeza ufanisi katika ushirikiano na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.BNI ni muungano wa makampuni 8 yanayowahusisha wafanyabiashara kati ya 30 Duniani.
Waziri wa Kilimo Mhe Hasunga (Mb) Mwenye Tai, akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni mbalimbali zinazojihusisha na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi-Business Network International (BNI) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na watendaji hao Jijini Dar es salaam, leo tarehe 11 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Njombe, Mjumbe kutoka Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) pamoja na muungano wa makampuni ya uwekezaji kutoka China, leo tarehe 11 Disemba 2018 Jijini Dar es salaam.


WATEJA 434 WAREJESHEWA HUDUMA YA MAJI KUPITIA KAMPENI YA #DAWASATUNAWAHITAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamefanikiwa kurejesha wateja 434 waliokuwa na madeni baada ya kuanzisha kampeni ya Dawasa Tunawahitaji.

Wateja hao waliokuwa wamekatiwa huduma ya maji na DAWASA wamekubali kulipa madeni yao yenye jumla ya thamani ya Milioni 204.3 kutoka maeneo mbalimbali. 

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa idara ya huduma kwa wateja, Ritamary Lwabulinda amesema mpaka sasa mikoa yote 10 ya DAWASA inaendelwa na kampeni hiyo inayolenga kuwavutia wateja waliokuwa wamekatiwa huduma kutokana na madeni sugu. Amesema, hadi sasa Mkoa wa Magomeni ndio unaongoza kwa kurejeaha huduma ya maji kwa wateja 81 wenye kudaiwa jumla ya Miliioni 39.44 ikifuatiwa na Mkoa wa Temeke uliofanikwa kurejesha wateja 60 waliokuwa wanadaiwa Milioni 23.01. 

Ritamary amesema mikoa mingine na kiasi cha fedha kinachodaiwa katika mabano ni Bagamoyo wateja 59 (mil 22.9), Tegeta wateja 59 (mil 27.21), Tabata wateja 49 (mil 27.52) na Kinondoni wateja 28 (mil 13.24). Sehemu zingine ni Ubungo wateja 27 (mil 17.23), Kibaha wateja 25 (mil 8.77), Ilala wateja 24 ( Mil 12.36) na Kawe wateja 22 (mil 12.58). 

Kufuatia mpango huo wa #Dawasa Tunawahitaji kwa sasa Mamlaka hukusanya kiasi cha Shilng Milion 36.41 kila mwezi baada ya wateja hao kuingia mkataba wa kulipa kidogo kidogo kila mwezi na katika kipindi kifupi cha utekelezaji wa kampeni hiyo jumla ya Milion 59.39 zimekusanywa kutoka katika vituo mbalimbali. 

Kampeni hiyo ilizinduliwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kampeni ya ' Dawasa Tunawahitaji' lengo kuu ni kuona wateja wote takribani 10000 waliokatiwa maji wanaanza kupata tena huduma hiyo. 

Kampeni hiyo itawahusisha wateja wote waliokatiwa huduma ya maji na kupitia kwa mameneja wa mikoa yote ya DAWASA kwa pamoja wakubaliane watalipa kwa miezi mingapi madeni ambayo wanadaiwa.
Mafundi wakiwa wanasoma mita ya maji ya mteja.

TAA YAENDELEA KUTOA KWA JAMII

$
0
0

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli mbali mbali za jamii, kwa kutoa misaada yenye tija.

Hilo limekuwa bayana leo tarehe 12 Disemba, 2018 kwenye Kijiji cha Makumbosho Jijini Dar es Salaam, ambapo TAA imetoa msaada wa fulana 100 kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajiwa kufanyika tarehe 22 Disemba, 2018 katika Uwanja wa Mazaina Chato.

Akizungumza katika Mkutano wa waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Bw. Abdi Mkwizu amesema Mamlaka ina wajibu mkubwa wa kuunga mkono shughuli za kijamii, kwa kutoa misaada ya mbalimbali.

“Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania ina wajibu wa Kusimamia, kuendesha, kuboresha na kuendeleza Viwanja vya Ndege Tanzania lakini pia mbali na kutoa huduma hizo tuna wajibu wa kushiriki katika shughuli za kijamii, kwa wadau ambao wanatufanya sisi tuwepo,” amesema Bw. Mkwizu.

Pia Bw. Mkwizu amebainisha kwamba TAA inahudumia Viwanja 58 vilivyopo Tanzania Bara chini ya serikali, hivyo ni wajibu wao kushiriki katika shughuli za kusaidia jamii sehemu yeyote ile kulingana na uhitaji na bajeti iliyopo.
Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga akizungumza mbele ya waandishi wa habari kuhusu Tamasha la Utamaduni la Chato linalotarajia kufanyika Disemba 22, 2018. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Abdi Mkwizu (kulia) na Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi G;unze (kushoto). Mkutano huo wa waandishi wa habari umefanyika leo katika Kijiji cha Makumbusho. 
Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze (kushoto), Mkurugenzi wa Chief Promotions Bw. Amoni Mkoga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia) kwa pamoja wakionesha tangazo la tamasha la Utamaduni la Chato lenye kauli mbiu ya “Maendeleo ya Viwanda yasiache Utamaduni nyuma”. Tukio hilo limefanyika leo kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari katika Kijiji cha Makumbusho. 
Kaimu Mkurugenzi Rasilimali Watu na Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Abdi Mkwizu (kulia), akikabidhi moja ya fulana 100 zilizotolewa na TAA kwa muandaaji wa Tamasha la Utamaduni la Chato, Bw. Amon Mkoga (kushoto), Katikati anayeshughudia ni Mwenyekiti Bodi ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Bw. Habbi Gunze. Tamasha hilo litafanyika Disemba 22, 2018. 

WAKAZI WA ITILIMA MKOANI SIMIYU WAFURAHIA KUKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI

$
0
0


Na Benny Mwaipaja,WFM, Simiyu

ZAIDI ya Wakazi elfu 2 wa Mji wa Lagangabilili, Tarafa ya Kanadi, Wilayani Itilima, mkoani Simiyu, wameondokana na adha ya kukosa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mradi wa maji ya bomba wa Lagangabilili uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 900.

Wakizunguza mbele ya timu maalumu ya wataalam wanaofuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka baadhi ya Wizara wakiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Baadhi ya wakazi wa Mji huo wa Lagangabilili wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mradi huo wa maji.

“Tunaishukuru sana Serikali kwa kutuletea maji tunayapata kwa urahisi, zamani tulikuwa tukihangaika sana akina mama walikuwa wakiyafuata mto Simiyu, mbali sana, walikuwa wakitoka saa kumi usiku na kurudi saa tatu asubuhi” alisema Bw. Chonza Maduhu, mkazi wa Lagangabilili, Simiyu
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Itilima, Bw. Goodluck Masige, amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumefanya kiwango cha upatikanaji maji safi na salama kwenye mji huo ambao ndio makao makuu ya wilaya ya Itilima, kupanda kutoka asilimia 20 za awali hadi kufikia asilimia 100.

“Tumejenga tenki lenye ujazo wa lita 225,000, vituo 21 vya kuchotea maji, tumejenga mtandao wa bomba za kusambaza maji nyenye urefu wa mita 29,000 na kufunga pampu 1 ya kusukuma maji” aliongea Mhandisi Masige
  

Mhandisi Christer Mchomba (mwenye kofia), kutoka Wizara ya Maji, akiandika maelezo ya Mhasibu wa Kamati ya Maji ya Mji wa Lagangabilili, Bi. Kundi Paulo, wakati Timu Maalum ya Serikali ikiongozwa na Wizara ya Fedha na Mipango, ilipokuwa katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 
3-min
Mkazi wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Bi. Pendo Tindigwe, akiwa amebeba ndoo yake yenye maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji Lagangabilili uliojengwa na Serikali kwa gharama ya Sh. 907m.
4-min
Tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mji wa Lagangabilili, Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, lenye uwezo wa kubeba lita 225,000 za maji kwa wakati mmoja kwa ajili ya kuwahudumia wakazi 2,212 wa Mji huo wa Lagangabilili.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

WATUMISHI WA UMMA MSIJIINGIZE KWENYE UTUMWA WA MIKOPO YA TAASISI ZISIZO HALALI-WATARA

$
0
0


NA TIGANYA VINCENT ,RS TABORA 

WATUMISHI wa Umma wametakiwa kuacha kujiingiza katika mikopo inayowasababisha kuuza uhuru wao na kuwa watumwa kwa wakopeshaji wasio halali na ambao hawajasaliwa na Serikali. 

Kauli hiyo imetolewa wilayani Nzega na Igunga na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara wakati wa vikao vya majumuisho na Watumishi wa Wilaya hizo. 

Alisema baadhi ya wanawakopesha hawakusajiliwa na hawalipi kodi za Serikali na hivyo kuendesha biashara hiyo kinyume cha Sheria na taratibu za nchi. Waitara alisema wakopeshaji hao wamekuwa wakikopesha kwa riba kubwa ambazo zimewafanya baadhi ya watumishi kuishi maisha magumu yaliyojaa utumwa ndani yake. 

Alisema baadhi ya watumishi ambao ukopa wamekuwa wakikabidhi hata Kadi za kuchukua Fedha (ATM) kwa wakopeshaji na inapofika mwisho mwa Mwezi ndio upiga simu kwake ili waende kwenye ATM achukue fedha kwa ajili ya kulipa deni na kidogo za matumizi na baada ya hapo anarudisha kadi mdai wake. 

Waitara alisema kitendo kinafanya taarifa za mshahara wa mtumishi kutokuwa siri kwake bali kuwa wazi hata kwa mkopeshaji jambo ambalo ni kuuza uhuru wake. Aliwataka Watumishi wa umma kuishi kulinga na mishahara wanayolipwa na kujiepusha na tamaa ambazo zinaweza kuwasababisha kujiingiza katika matatizo.
 Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(OR TAMISEMI) Mwita Waitara 
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images