Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Viwanda Atembelea Eneo Litakalotumiwa Kubangua Korosho ya Serikali

$
0
0


Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akiwaonyesha mtambo maalum wa kuchemsha korosho wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele. Wataalam hao wametembelea eneo la SIDO kujiridhisha kama linafaa kwa ajili ya kuanza kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali.
Kaimu Meneja wa SIDO mkoa wa Mtwara, Zamla Dongwala, akimuonyesha mashine ya kukausha korosho Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji (hayupo pichani) wakati alipotembelea eneo la SIDO, mkoani Mtwara leo. Eneo hilo ni moja ya maeneo yaliyochaguliwa kuanza kutumiwa wa wabanguaji wa korosho wadogo kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali.
Fundi umeme akiwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha matengenezo ya mashine ya kuchambua korosho kama alivyokutwa na mpiga picha wetu eneo la SIDO mjini Mtwara leo. (Picha na Idara ya Habari-MAELEZO

Washiriki Miss Journalism World Watua Kwa Tambo

$
0
0


YAMETIMIA! Hatimaye warembo kutoka nchi kadhaa wanaowania taji la Miss Journalism World 2018, ambalo litafanyika hapa nchini Ijumaa ya Desemba 14, mwaka huu wamewasili.

Warembo hao waliwasili nchini jana kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), huku wachache waliobaki wakitarajiwa kuwasili leo. Wengi wa warembo hao walitamba kufanya kweli katika shindano hilo, huku waandaaji wakisema kila kitu kmekamilika. Shindano hilo linatarajiwa kufanyika jijini Arusha, katika ukumbi wa Kimataifa wa Aim Mall, huku waandaaji wakisema yatakuwa ya aina yake.

Akizungumza na waandishji wa habari jana, mratibu wa shindano hilo, Samwel Chazi, alisema warembo 16 wanatarajia kuwasili kesho mchana wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya mpambano huo unaosubiriwa kwa hamu. Mmoja wa warembo hao kutoka China, Chen Sitong, alisema ana uhakika mkubwa wa kushinda, kwani amejiandaa. Mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi, aliwataja warembo hao na nchi wanazotoka zikiwa kwenye mabano kuwa ni Pauline Murati (Ufaransa), Nina Yetvushenko (Ukraine), Linda Plaude (Latvia), Fatima Kahametova (Urusi) na Zainab Mkuwu (Malawi).

Wengine ni Wioletta Tupko (Poland) na Noelia Ovejo (Hispania), Juliana Nare (Zimbabwe), Arlette Akimana (Burundi) na Chen Sitong (China). Wapo Roseline Ogunyale (Nigeria), Gisele Umwiza (Rwanda), Cassandre Joseph (Haiti), Wendy Omanga (Kenya) na mwenyeji wao Witness Kavumo (Tanzania). “Kila kitu kimekamilika, hili ni shindano la kimataifa nab ado nafasi za kudhamini zipo, hii pia ni fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania katika sekta ya utalii,” alisema Chazi. Alitaja viingilio katika shindano hilo ni Sh 100,000 kwa viti vya hadhi ya juu (VVIP), Sh 50,000 kwa viti maalumu (VIP) na viti vya kawaida Sh 30,000

“Tumeshusha viingilio ili kuwapa fursa Watanzania wapate kushuhudia warembo hawa wa dunia pale Aim Mall kwa mara ya kwanza,” alisema Chazi.

Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Journalism World wakiwa na mwenyeji wao ambaye ni mratibu wa shindano hilo, Sam Chazi (mwenye fulana) nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), walipowasili nchini jana. .

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA MASUALA YA KIMATAIFA WA CANADA

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea na kuzungumza nae Ikulu Jijini Dar es salaam,Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga .Desemba 10,2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga alihudhuria mazungumzo hayo.Desemba 10,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Bw. Marc-Andre Fredette Mkurugenzi Mkuu Masuala ya Kimataifa wa Canada alipotembelea na kuzungumza nae Ikulu Jijini Dar es salaam.Mazungumzo ambayo pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Agustine Mahiga alihudhuria.Desemba 10,2018. . PICHA NA IKULU

TANZIA.

SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameitaka Serikali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo cha VETA Simanjiro ili miundombinu ya chuo hicho iweze kujengwa kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Hiari ECLAT.

Alisema ni vizuri Mamlaka husika zikahusishwa katika ujenzi wa Chuo hicho tangu hatua za awali na kumtaka Mkurugenzi wa VETA kanda na yule wa Mkoa kufika katika eneo la Emboreet ambako mradi utajengwa kwa lengo la kuongea na wananchi pamoja na wafadhili wa mradi huo ili wazo ambalo limeanza liweze kutekelezwa kwa utaratibu unaostahili.

“Ninyi Halmashauri mnataka kujenga chuo cha Ufundi ni wazo zuri lakini ni lazima kijengwe kwa utaratibu sio kiholela kwa sababu vilianza kuibuka vyuo ambavyo mtu anakuwa na jengo moja anasajili kinaitwa chuo, kuna viwango na masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla chuo kuruhusiwa kufanya kazi, fuateni taratibu hizo ili muweze kuanzisha chuo cha Ufundi,” aliongeza Naibu Wazizri Ole Nasha.







Naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi kuhusu namna walivyojipanga kujenga Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya katika eneo la Mradi la Emboreet lililoko katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kitwai A aliyefanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2018. Shule ya Msingi Kitwai A imefaulisha wanafunzi 25 kati ya 28 waliofanya mtihani mwaka huu. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wakazi wa Kata ya Kitwai A iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amewataka kuhakikisha wanaandikisha shule wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule bila kuwaacha nyumbani na kuwapangia majukumu mengine. 

MAONYESHO YA CHAKULA, KAHAWA NA CHOCOLATE YAFANYIKA SAUDI ARABIA

$
0
0
Maonyesho ya chakula, kahawa na chocolate yamefanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia. Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ulishiriki kwa kuwaalika baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na wafanyabiashara raia wa Tanzania wanaoishi Saudi Arabia.

Katika maonyesho hayo bidhaa za kahawa ya kijani (green beans) zilionyeshwa na kuvutia wanunuzi wengi wa Saudi Arabia ambao waliweka miadi ‘order’ za kuagiza. Bidhaa zingine zilizowekewa miadi ya kuagizwa ni pamoja na korosho, chai, karafuu, hiliki na viungo. Pia watu walitembelea banda la Tanzania walipata fursa ya kuuliza maswali na kupokea taarifa kuhusu uagizaji wa bidhaa na mazao ya kilimo kutoka Tanzania. 

Kampuni mbili za Saudi Arabia ambazo zilipata taarifa za kahawa kutoka Tanzania katika maonyesho yaliyotangulia ya mwaka 2016 na 2017 zilishiriki na kuuza kahawa iliyokaangwa (roasted) kutoka Tanzania kwa wingi. Kampuni hizo ni Roasting House ambayo kahawa yao huipata kutoka Ruvuma, kampuni nyingine ya pili ni Filter Coffee Roasters ambayo kahawa yao huipata kutoka Songwe. Watu wengi walifurika katika mabanda ya makampuni hayo mawili ya Saudi Arabia kununua kahawa ya kutoka Tanzania kwa kuwa ina ubora wa hali ya juu ukilinganisha na kahawa za kutoka maeneo mengine ambayo zilikuwa ikiuzwa. 
 Watu mbalimbali wakipata maelezo ya bidhaa za Tanzania katika banda la Tanzania katika maonyesho ya chakula, kahawa, chai na chocolate mjini Riyadh, Saudi Arabia.
 Wateja wakiwa wamefurika katika banda la kampuni ya Saudi Arabia iitwayo Roasting House ambayo inauza kahawa iliyoakaangwa kutoka mkoa wa Ruvuma nchini Tanzania.

 Watu waliotembelea banda la Tanzania mjini Riyadh wakionja chai na kahawa ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kupata vipeperushi vinavyolelezea kuhusu mazao ya Tanzania.

Mmoja ya wafanyabiashara mwanamama kutoka Tanzania akipanga bidhaa zake za asali kahawa na chai katika banda la Tanzania mjini Riyadh, Saudi Arabia.

JAJI MKUU ATOA WITO KWA VIONGOZI KUELIMISHA WANANCHI TARATIBU ZA UPATIKANAJI WA HAKI

$
0
0
Na Lydia Churi- Mahakama Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa wito kwa viongozi wa Mahakama, Serikali pamoja na Dini kuwaelimisha wananchi taratibu mbalimbali za upatikanaji wa haki. 
Akizungumza na wakuu wa wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma leo, Jaji Mkuu amesema wananchi wengi hawafahamu taratibu za upatikanaji wa haki hivyo viongozi hao wanao wajibu wa kuwaelimisha kwa lugha ya upole wanapofika kwenye maeneo yao ya kazi.
Alisema kutokana na kutokufahamu taratibu za upatikanaji wa haki, wananchi wengine wamejikuta wakipoteza haki zao na wengine kutumia muda mwingi kushughulika na kesi ambazo thamani yake hailingani na muda na mali iliyotumika. 
“Wengine hudhani kupata haki ni kushinda kesi hawajui kwenye kesi kuna kushinda na kushindwa, dhana hii ndiyo inayoibua migogoro hivyo wananchi hawana budi kuelimishwa kuwa haki kwa aliyeshindwa ni kukata rufaa”, alisema Jaji Mkuu. Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania imejiwekea vigezo ili kuhakikisha inaboresha huduma zake na wananchi wanapata haki kwa wakati. Vigezo hivyo ni pa moja na kuhakikisha kesi inamalizika ndani ya miaka miwili kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 kwenye Mahakama za Hakimu Mkazi pamoja na Mahakama za Wilaya  na miezi sita kwenye Mahakama za Mwanzo.
Kigezo kingine ni mapambano dhidi ya rushwa ambapo alisema Mahakama imesambaza nchi nzima mabango yenye ujumbe wa mapambano dhidi ya rushwa, simu za mikononi na pia imewapatia watumishi wake wote vitambulisho. Alisema Mahakama inaimarisha vitengo vya usuluhishi kikiwemo kitengo cha usuluhishi na mabaraza ya kata hasa kwenye maeneo  yasiyokuwa na Mahakama za Mwanzo.  Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama pia hutoa nakala za hukumu bure na kuhakikisha nakala hizo zinatoka ndani ya siku 21, kupatikana kwa mienedo ya kesi ndani ya siku 30 ili kuwafikia wananchi na kutoa haki kwa wakati. 
Akizungumzia ushirikiano na mihimili mingine, Jaji Mkuu alisema mihimili yote ya dola inategemeana hivyo Mahakama haina budi kushirikiana ili wananchi wapate haki kwa wakati. Naye Mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga akimkaribisha Jaji Mkuu wilayani kwake alisema wilaya yake itaendeleza ushirikiano kati yake na Mahakama ya Tanzania.Jaji Mk u wa Tanzania ameanza ziara ya siku mbili katika mkoa wa Dodoma ambapo leo ametembelea wilaya ya Chemba pamoja na Mahakama ya wilaya ya Kondoa na kukagua shughuli za Mahakama.

MKURABITA Yawajengea Uwezo Wajasiriamali 1000 Singida ili Waweze Kurasimisha Biashara Zao

$
0
0
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) unaendesha mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali 1000 wa Mkoani Singida ikiwa ni hatua mojawapo yakuwawezesha kushiriki katika ujenzi wa uchumi kwa kufanya biashara katika mfumo rasmi.
Akizungumza mjini Singida wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo  leo mjini humo, Mkuu wa Wilaya hiyo Bw.Pascas Muragiri amesema kuwa  mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka ambapo Serikali inasisitiza wajasiriamali kufanya biashara katika mfumo rasmi ili waweze kukuza biashara zao na kuongeza tija.
“Mafunzo haya ni nyenzo muhimu kwa wajasiriamali wetu hapa Singida kwani yatawawezesha kuwa na uwezo wa kutambua na kuzingatia taratibu zote zinazosimamia biashara hali inayotoa fursa kwao kurasimisha biashara zao.” Alisisitiza Muragiri. Akifafanua amesema kuwa katika mafunzo hayo wajasiriamali hao watajifunza namna ya kutunza hesabu, Urasimishaji, taratibu za kupata leseni za biashara,umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara na umuhimu wa bima ya afya.
Aliongeza kuwa wajasiriamali hao wanajukumu la kuzingatia yale watakayojifunza wakati wa mafunzo hayo na hivyo kuendana na dhamira ya Serikali kuwawezesha kukuza uwezo wa kufanya biashara baada ya kurasimisha biashara zao hali itakayowawezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha ili kukuza mitaji yao na pia kuwezesha kukua kwa biashara katika mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri akizungumzia faida za kurasimisha Biashara kwa wajasiriamali wa mjini Singida wakati akifungua mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini humo (hawapo pichani) yaliyolenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao, Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikina na Halmashauri ya Manispaa ya Singida.
 Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida Alhaji Gwae Mbua akisisitiza jambo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini Singida (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufungua mafunzo kwa wajasiriamali hao mjini humo mapema Novemba 10, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Urasimishaji kutoka MKURABITA Bw. Japhet Werema.
 Sehemu ya Washiriki wa Mafunzo yakuwajengea uwezo wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini Singida wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri wakati wa hafla yakufungua mafunzo hayo mjini humo Novemba 10, 2018.
 Mkuu wa Wilaya ya Singida Bw. Pascas Muragiri (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya washiriki na watoa mada wa mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 1000 wa mjini humo yaliyolenga kuwajengea uwezo ili warasimishe Biashara zao, Mafunzo hayo yanaendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikina na Halmashauri ya Manispaa ya Singida.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


SERIKALI YAAGIZA VIONGOZI WA WILAYA YA KILOSA KUHAKIKISHA WANAWAONDOA WAVAMIZI WALIOVAMIA RANCHI YA NARCO MKATA

$
0
0
Serikali imewaagiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kata ya Parakuyo kuhakikisha wanawaondoa wavamizi waliovamia Ranchi ya Narco Mkata. Agizo ilo limetolewa na Naibu waziri wa mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati alipokuwa anafanya ziara wilaya Kilosa kwa lengo la kusikiliza kero za wafugaji. "Msimuonee mtu ambae analima nje Ranchi NARCO na hakikisheni mnawapokonya vitalu waliopewa wakashindwa kuviendeleza ili wapewe wafungaji wengine alisema Ulega"

Mhe Ulega aliwaeleza wafugaji maagizo yake kwa viongozi wa wilaya juu ya kuwaondoa wavamizi katika Ranchi ya NARCO Mkata na wote wanaolima katika maeneo hayo na wakodishiwe wafugaji kwa ajili ya kunenepesha Mifugo yao katika vitalu vitakavyokuwa vimeandaliwa. Alisema Wilaya inakuja na majina ya wafugaji na idadi ya mifugo yao wanaohitaji vitalu hivyo. 

"Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na Rais wetu anawapenda sana wafugaji na watu wote anatupenda na alishatupa maagizo kama wizara kuwaondoa watu waliohodhi maeneo ya Ranchi na kuwapa wafugaji wetu"
Wakati Mhe. Ulega akijibu hoja ya wafugaji kukosa elimu ya ufugaji wa kisasa wenye tija ikiambatana na elimu ya uzalishaji wa malisho aliwaagiza wataalam wa mifugo kutoka Wakala wa Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Mifugo (LITA) alioongozana nao katika ziara hiyo kupeleka wanafunzi kujifunza kwa vitendo katika kata ya Parakuyo na maeneo mengine ya wafugaji ili waweze kusambaza elimu hizo kwa wafugaji kuliko wanafunzi hao kufanya  mafunzo hayo maeneo ya mijini.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafungaji  katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Parakuyo wilaya Kolosa mkoa wa Morogoro ambapo amewahakikishi kuwa Serikali  itaendelea kuboresha miundombinu,majosho mabirika ya maji.

Baadhi ya wafungaji wa wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro  wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega.
 Meneja wa Rachi ya Mkata wilaya ya Kilosa, Sadalah Athuman(kulia) akitoa taarifa  fupi ya mikakati waliyoiweka kuwasaidia wafungaji wa  wilaya hiyo kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mikataba ya wakandarasi wa umeme vijijini kupitiwa na wanasheria wa Serikali

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameeleza kuwa, Wanasheria wa Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wataanza kupitia mikataba ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini ili kuchukua hatua za kuwawajibisha wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kwa kusuasua.

Aliyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao chake na Mameneja wa TANESCO wa Kanda, Mikoa, Wilaya na wasimamizi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kutoka Wizara ya Nishati, REA na TANESCO.

“ Yako baadhi ya maeneo ambayo Wakandarasi hawafanyi vizuri kama vile Mtwara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Shinyanga, Singida, Tabora (Kaliua, Uyui, Urambo), Dodoma na Tanga (Wilaya ya Korogwe, Mkinga na Pangani), ambao utekelezaji wao katika mradi wa usambazaji umeme wa Awamu ya Tatu, mzunguko wa kwanza, wako chini ya asilimia 20,” alisema Mgalu.

Naibu Waziri alitoa agizo kuwa, wakandarasi katika maeneo hayo wahakikishe kuwa, wanafanya kazi kwa kasi na ufanisi ikiwemo kuweka magenge mengi ya kazi, uwepo vifaa na wasimamizi wa miradi wa kutosha ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria na Serikali na pia kutorudisha nyuma juhudi za Serikali za kusambaza umeme vijijini.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati), akimsikiliza Mwakilishi wa Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Haji Janabi wakati wa kikao kazi na watendaji wa REA na TANESCO na wasimamizi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kutoka REA, TANESCO na Wizara ya Nishati. Wengine katika picha ni Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka (wa pili kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga  (wa kwanza kulia).
 
Baadhi ya watendaji wa REA na TANESCO na wasimamizi wa miradi ya usambazaji umeme vijijini kutoka REA, TANESCO na Wizara ya Nishati wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (hayupo pichani)  wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

PROFESA KABUDI ATEMBELEA IHUMWA KUKAGUA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi (mwenye shati jeupe) akiangalia moja ya mipaka katika kiwanja cha kujenga jengo la Wizara hiyo eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. sifuni Mchome na aliyepo  katikati ni fundi ujenzi.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akiangalia ramani ya ujenzi wa Jengo la Wizara katiika eneo la Ihumwa Mkoani Dodoma.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wakati alipotembelea eneo la kiwanja cha Wizara Ihumwa.
 Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akipanda excavator ili kuishuhudia namna linavyofanya kazi wakati akikagua eneo la kiwanja linapojengwa jengo la Wizara ya Katiba na Sheria Mkoani Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palmagamba Kabudi akijadiliana jambo na Mkandarasi na viongozi wa Wizara wakati akikagua eneo la ujenzi wa jengo la Wizara hiyo.

SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA WAGENI KUTOKA NCHINI NAMIBIA

$
0
0
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na mgeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.mgeni huyo alieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokea zawadi kutoka kwa mgeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.mgeni huyo alieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akionyeshwa mchoro wa Kituo cha Kimataifa kitakachojengwa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika kutoka kwa Ndugu Desmond Amunyela aliyemtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma aliyembatana na Ndugu Iyaloo ya Nangolo wote wakitokea Nchini Namibia.
 Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwaonyesha Ukumbi wa Bunge la Tanzania waeni wake kutoka Nchini Namibia Ndugu Desmond Amunyela na Ndugu  Iyaloo ya Nangolo  mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake Jijini Dodoma.wageni hao walieleza kusudio la Namibia la kujenga Kituo cha Kimataifa Wilayani Kongwa  cha Kumbukumbu ya Kupigania uhuru wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU ZOEZI LA UHAKIKI WA WANACHAMA WASTAAFU WA NHIF

WWF WAANDESHA MAFUNZO YA MAWASILIANO

$
0
0
Na Yeremias Ngerangera…Bagamoyo.
Mfuko  wa hifadhi ya mazingira wa dunia (WWF-World  Wide  Fund for Nature)  unaendesha mafunzo  kwa viongozi wa jumuiya  za uhifadhi  kuwajengea uwezo wa  kuimarisha mawasiliano kati ya wanajumuiya na nje ya Jumuiya. Mafunzo hayo yanafanyika katika Hoteli ya Millenium sea breeze mjini Bagamoyo ambapo washiriki zaidi ya 48 kutoka mikoa ya lindi ,Mtwara, Pwani  na Ruvuma wanashiriki mafunzo hayo ya mawasiliano thabiti   kwa lengo la kujengewa uwezo wa kufanya mawasiliano na wananchi kwenye maeneo yao ya uhifadhi .

Akifungua mafunzo  hayo Drt  Severin Kalonga aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kujifunza mbinu, njia na namna ya kufanya mawasiliano na jamii zilizopo katika mazingira yao ili waweze kutoa ujumbe kwa jamii ukiwa sahihi kwa watu sahihi na kwa wakati sahihi na mwishowe kupatikana kwa matokeo chanya kwa wakati. Awali Drt Kalonga aliwaeleza washiriki wa mafunzo hayo namna WWF inavyofanya kazi katika kuhakikisha hifadhi zilizopo zinaendelea kutunzwa na kubaini njia pekee ya kuendelea kutunza hifadhi hizo ni kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa wananchi kwa kuwa na mawasiliano  yaliyorafiki na viongozi wao wa jumuiya.

Aidha  Kalonga aliwaambia washiriki hao kuwa upangaji wa matumizi bora ya ardhi yanaumuhimu mkubwa  katika jamii lakini akabainisha kuwa mbinu ,njia na namna ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa viongozi wa jumuiya akazitiia mashaka.  Profesa Noah Sitati naye alisema katika uhifadhi wanakumbana na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na shughuli za kibinadamu kama kilimo na ufugaji kufanyika ndani ya hifadhi hivyo kuathiri wanyamapori na ukataji hovyo wa misitu.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

TAKUKURU YAELEZA ILIVYOKUTA BAHASHA YA KAKI MEZANI KWA WAZIRI LUKUVI

$
0
0
Na Karama  Kenyunko, Blogu ya Jamii

KAIMU Kamishna Msaidizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maendeleo  ya Makazi Wilson Luge (39) ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kuwa fedha alizoenda kuhakiki katika ofisi  ya Waziri  wa  Ardhi   zinazodaiwa  kutolewa kama rushwa kwa Waziri William Lukuvi zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko wa kaki.

Luge ameyasema hayo leo  Desemba  11, 2018  wakati anajibu swali la  Wakili  wa utetezi Imani Madega dhidi ya kesi ya tuhuma za rushwa  ya Sh. Milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone,Mohamed Kiluwa alipokuwa akitoa ushahidi  wake mbele ya Hakimu Mkazi Samwel Obasi.

Amedai mahakamani hapo kuwa Julia  16 mwaka huu akiwa kazini kati ya saa saba mchana hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri, Esquires na Kamishna Mkuu wa Ardhi Mary Makondo na kuwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

Pia amedai walipoingia walikuta watu mbalimbali huku mezani kukiwa na mfuko wa kaki uliokuwa umefungwa ambao hakujua ndani  yake kulikuwa na nini na kwamba mfuko huo ulifunguliwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru na kutoa fedha ambazo ni mabunda manne ya Dola za Marekani 40,000 ambapo waliwataka  yeye na Hellen Philipo walihakiki fedha hizo.

Mapema akiongozwa kutoa ushahidi na Wakili wa Takukuru Maghela Ndimbo, shahidi huyo wa sita amedai Julai 16, mwaka huu alikuwa ofisini kwake Kanda ya Dar es Salaam ambayo zamani ilikuwa Makao Makuu ya Wizara hiyo.Alidai kati ya saa saba hadi saa 10 jioni, walikuwa wanaangalia mfumo wa kielekroniki wanaoutumia kama unafanya kazi vizuri ambapo Kamishna Mkuu wa Ardhi, Mary Makondo aliwaita akiwaelekeza waende ofisi ya Waziri Lukuvi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

MICHUZI TV:DIAMOND PLATNUMZ APAGAWA NA GIGY MONEY(PRE PART WASAFI FESTIVAL) ZANZIBAR

TNGP YAZIDI KUENDELEZA MIKAKATI KUPUNGUZA UKATILI YA KIJINSIA KWA ASILIMIA 50 IFIKAPO 2030

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MTANDAO wa ujinsia nchini (TNGP) umefanya mkutano na mjadala kuhusiana na haki ya afya ya uzazi uliowakutanisha wadau mbalimbali wanaofanya kazi katika sekta ya afya ikiwa ni katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Akizungumza katika mkutano huo Afisa programu wa wanaharakati na ujenzi wa pamoja (TNGP) Anna Sangai amesema kuwa lengo la kufanya mkutano huo ni kufanya tathimini ya wapi walipo na wanapoenda kuhusiana na hali ya jinsia nchini.

Akieleza tathimini ya nchi Sangai amesema kuwa Tanzania inafanya vizuri kiutekelezaji katika kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto. Pia ameeleza kuwa changamoto zinazozikabili mapambano hayo ni pamoja na kutofika kwa  elimu ya afya ya uzazi katika maeneo mbalimbali, utekelezaji wa sheria na mipango dhidi wanaovunja sheria na kufanya vitendo vya ukatili pamoja na mazingira magumu ya upatikanaji wa haki kwa kuwa kesi huchukua muda mrefu huku waathirika wakisumbuka kutafuta haki zao.

Sangai amesema kuwa mjadala huo utaweka mazingira wezeshi na kutoka na kampeni mbalimbali zitakazohusisha wadau  kutoka sekta ya afya nchini kote na hiyo itasaidia kufikia malengo  ya kupunguza asilimia 50 ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ifikapo 2030. Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, Sophia Komba amesema kuwa katika mkutano huo watazungumzia haki ya afya ya uzazi ambayo imekumbwa na na matukio ya unyanyasaji hasa kwa vijana na wanawake.
Afisa programu wa wanaharakati na ujenzi wa pamoja kutoka mtandao wa ujinsia nchini (TNGP) Anna Sangai akizungumza wakati wa mkutano huo uliolenga kujadili haki ya afya ya uzazi uliofanyika leo jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa wanaendelea na mikakati ya kufikia malengo ya kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia ifikapo 2030.
Mshauri wa masuala ya kijinsia kutoka Afrika kusini Kubi Rama akifafanua jambo katika mkutano uliolenga hasa kujadili haki ya afya ya uzazi  ulioandaliwa na mtandao wa ujinsia nchini (TNGP) na kueleza kuwa usawa lazima uwepo na kuzingatia kwa kuwa matukio mengi ya unyanyasaji hutokea pale ambapo mtu hukosa chanzo chochote cha kupata kipato hasa kwa wanawake.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kuzuia unyanyasaji wa kijinsia Sophia Komba akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam na kueleza matatizo ya ubakaji na kulawitiwa lazima yazungumzwe ili yaweze kukoma.
Mkutano ukiendelea

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: MWANAMKE ALIYETHUBUTU HUYU HAPA/UROJO WA ZANZIBAR NI BALAA

MICHUZI TV: IJUE ZANZIBAR (FORODHANI) KIVUTIO KWA WATU WENGI...

Vodacom Tanzania yawatunukia watumiaji wa mtandao wake bomba kwa Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1

$
0
0
Vodacom, kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao

Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.

“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huu umechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetu Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,” alisema Hisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. 
“Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatia pointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham. 

Wateja hao wanatunukia Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi za Tuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).

“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu – Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham. 

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (katikati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu na mwaka mpya yenye kaulimbiu 'Nabaki mulemule na Vodacom'. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo Rossalyn Mworia na Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Linda Riwa .

Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC Rossalyn Mworia, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, juu ya kuwatunuku watumiaji wa mtandao wa Vodacom, points za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1 katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu yenye kauli mbiu “Nabaki mulemule na Vodacom.” Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Kaimu Mkurugenzi wa biashara, Linda Riwa .
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>