Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA UWT UKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Thuwaiba Editon Kisasa, kulia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi na kushoto Mwenyekiti wa UWT Gaudensia  Kabaka, walipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mwenyekiti wa UWT Taifa  Kabaka.10-12-2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania,(UWT) Gaudensia Kabaka,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake wa Viongozi wa UWT.kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT  Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT. Queen Mlozi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka,Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT.B. Queen Mlozi, wakiwa katika ukumbi wa mkutona Ikulu leo wakati wa mazungumzo yao walipofika kujitambulisha.kwa Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WAZIRI MKUU AHUTUBIA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU KITAIFA JIJINI DODOMA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa  kwenye Kiwanja cha Nyerere Squre jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
 Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika  Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi (katikati ) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni  (mstaafu), George Mkuchika baada ya kuhutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi  baada ya kuhutubia katika Kilele cha Maadhimisho ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa kwenye Kiwanja cha Nyerere Square jijini Dodoma, Desemba 10, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAHAKAMA YAELEZWA MKURUGENZI KAMPUNI YA KILUWA STEAL GROUP CO.LTD ALIVYOPATA HATI ZA VIWANJA 70 KIHALALI

0
0
*Shahidi asema Kiluwa alipata viwanja hivyo kwa utaratibu wa kawaida
*Akana kuomba wala kupokea rushwa...aeleza namna hati zilivyomfikia

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imeelezwa kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone, Mohamed Kiluwa (50)  alipata hati za viwanja 70 
kihalali kwa kufuata taratibu zote za ardhi.

 Kamishna Msaidizi wa Ardhi, Mathew Nhonge ambaye ni shahidi wanne wa upande wa mashtaka, ameyasema hayo leo  mbele ya Hakimu Mkazi Samweli Obas, alipokuwa akitoa ushahidi dhidi ya kesi ya kutoa rushwa Sh.milioni 90 kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi

Akijibu maswali ya Wakili wa utetezi Imani Madega, shahidi huyo amedai Kilua alipata viwanja hivyo kutoka Halmashauri kwa utaratibu wa kawaida na viwanja hivyo vyote vilipimwa na ardhi.

Anadai hati zote zilizosainiwa kila kitu katika hati hizo kilikuwa sawa sawa na aliridhika nazo ndio sababu alisaini. Alipohojiwa kama katika mchakato wote huo walimuomba fedha mshtakiwa au alipewa fedha yoyote, shahidi alikana kuwa hajapewa fedha wala kuomba hela kwa Kilua. Pia amedai hakuona wakati rushwa hiyo ikitolewa, hati za mshtakiwa alizipata kihalali na endapo Mahakama itaamua vinginevyo Wizara haitabisha .

Wakati akitoa ushahidi wake, shahidi huyo akiongozwa  na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Maghela Ndimbo, shahidi Mathew amedai Kampuni ya Kilua iliomba kumiliki ardhi maeneo ya Kikongo wilayani Kibaha, hati za kumiliki 
viwanja 73 zilimfikia kwa ajili ya kuzisaini. 

Amedai katika hati hizo, hati 70  zilisainiwa kisha kupelekwa kwa Msajili wa hati na hati tatu hazikusainiwa kwa sababu zilikuwa na mapungufu.Shahidi huyo amedai, baada ya kusainiwa kwa hati hizo, Julai 13 mwaka huu alipigiwa simu na Waziri Lukuvi akimuelekeza amfahamishe Kilua aende ofisini kwake akiwa na hati zake. 

JAJI MKUU AKITAKA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO (IJA) KUFANYA TAFITI

0
0
Jaji mkuu wa Tanzania Mh. Ibraham H. Juma, amekitaka Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kufanya tafiti na kutoa ushauri wa namna ya kuondoa migongano ya kisheria wakati Mahakama ikiendelea kuangalia namna bora ya kusimamia sheria ili kupunguza au kuondoa kabisa migongano hiyo.

Mh. Jaji Mkuu ametoa agizo hilo leo wakati akizindua baraza la tatu la wafanyakazi la Chuo Cha (IJA), katika hafla ya uzinduzi wa balaza hilo, iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Kumbukumbu Tuli cha Taifa jijini Dododma.

Kupitia hotuba yake Mh. Jaji Mkuu, mbali na kuzitambua changamoto zinazokikabili Chuo hicho, ikiwemo upungufu wa vitendea kazi na watumishi kwa kada ya utawala, aliwakumbusha watumishi wa Chuo hicho kuzingatia uadilifu katika kutekeleza shughuli zao za kila siku.

“Tunawajibika kufanya kazi kwa weledi, uthubutu na uadilifu wa hali ya juu, ili tuwawakilishe vyema wale waliotuamini sambamba na kuiwezesha serikali kufikia malengo yake ya kukuza uchumi wa viwanda na kuondoa umasikini” alisistiza Mh. Jaji Mkuu.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis akizungumza wakati wa akizindua Baraza la tatu la  wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa  Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma Mhe.Ignas Kitusi na Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo na Mwenyekiti wa  Baraza hilo Jaji  Dkt Paul Kihwelo.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto wakifuatilia hotuba ya  Jaji Mkuu wa Tanzania Prof.Ibrahim Hamis(hayupo pichani) wakati akizindua Baraza la tatu la  wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Leo Jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis  akiwa kwenye picha ya pamoja 

SERIKALI HAITOMVUMILIA KIONGOZI ATAKAYEKIUKA MAADILI-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuenzi misingi ya utawala bora haitamvumilia kiongozi yeyote wa umma atakayekiuka misingi hiyo na kutanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma katika utendaji wake.

Amesema mgongano wa maslahi umechangia rasilimali za nchi kunufaisha watu wachache huku wananchi wengi kuendelea kuwa fukara, wakati wachache wakijitajirisha isivyo halali, hivyo Serikali itaendelea kuziba mianya, kwani ikiachiwa iendelee, itarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufikia Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema mmomonyoko wa maadili umechangia sana kutozingatiwa kwa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali katika utumishi wa umma, tatizo ambalo limesababisha mgongano wa maslahi.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 10) kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu yaliyofanyika Kitaifa jijini Dodoma, ambapo ametumia Napenda fursa hiyo kuwaasa viongozi wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao kwani hiyo ndio njia pekee itakayoepusha mgongano wa maslahi.

Waziri Mkuu amesema mgongano wa maslahi ni miongoni mwa mambo yaliyochangia kuisababishia hasara Serikali kwa muda mrefu, tatizo ambalo lazima lidhibitiwe kwani mara kadhaa baadhi ya viongozi au watumishi wa umma wamekuwa wakifanya maamuzi kwa mambo wanayojua wazi kuwa wana maslahi binafsi nayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma kuzungumza na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Desemba 10, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchil Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavinde na kulia ni  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu, Profesa, Faustine  Kamuzora. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

KIKAO CHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI NA MAWAZIRI,WAKUU WA MIKOA NA UONGOZI WA TRA NCHINI

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA UAE NCHINI TANZANIA LEO IKULU

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi Mpya wa UAE Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzooqi, alipofiki Ikulu Zanzibar leo 10-12-2018, kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar na kufanya mazungumzo Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi Mpya wa UAE Nchini Tanzania Mhe, Khalifa Abdulrahman Al Marzooqi, alipofika Ikulu Zanzibar leo, kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar na kujitambulisha.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Ali Mohamed Shein, akizungumza na mgeni wake Balozi Mpya wa UAE Nchini Tanzania alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Ikulu leo.10-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mgeni wake Balozo wa UAE Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzooqi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar, alipofika kujitambulisha leo,10-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi Mpya ya UAE Nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Al Marzooqi, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo.10-12-2018.(Picha na Ikulu)

RAIS DKT. MAGUFULI AGAWA VITAMBULISHO 670,000 KWA WAKUU WA MIKOA KWA AJILI YA MATUMIZI YA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO (MACHINGA) KATIKA MIKOA YOTE YA TANZANIA BARA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizingumza na Wakuu wa Mikoa, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa baadhi ya Wizara, Mameneja wa Mikoa wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA, Waakilishi wa Machinga kabla ya kutoa Vitambulisho kwa ajili ya Wafanyabiashara wadogo wadogo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Vitambulisho hivyo vitagharimu kiasi cha Shilingi 20,000/ kwa kila kimoja.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyokuwa akiitoa katika ukumbi wa katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa wa Mbeya.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga kwa ajili ya mkoa huo wa Kiliamnjaro.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia wakati mkuu wa mkoa wa Njombe Cristopher Ole Sendeka alipokuwa akisaini hati ya makabidhiano ya vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wadogo machinga.
  PICHA NA IKULU


BADILISHA SIMU YAKO NA CAMON 11 MPYA

0
0
TECNO, miongoni mwa kampuni bora za simu ulimwenguni imezindua rasmi TECNO camon 11 ikiwa ni mwendelezo wa toleo la simu za TECNO camon. Simu za TECNO camon zimekuwa zenye ushawishi mkubwa sana kutokana na uwezo wa kamera na muonekano wake kwa ujumla, na katika uzinduzi huo TECNO ilitoa tamko rasmi kuhusiana na zoezi la ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 mpya ikiwa imeambatana na ofa ya GB 15 kwa miezi mitatu bure kutoka Vodacom Plc.
Na kama haukua unafahamu TECNO camon 11 ni simu ya kwanza ya TECNO kuwa na teknolojia ya AI kwenye kamera za pande zote mbili zenye kubeba pixel 16 mbele na 13+2 nyuma, na kioo chenye notch. 
Muonekano wa nje wa TECNO camon 11 unaofahamika kama ‘diamond fire design’ unaifanya camon 11 kuwa simu yenye kuvutia zaidi kati ya zote. Na japokuwa ni simu ya kwanza kuzalishwa na kampuni ya TECNO yenye teknolojia mpya katika kioo inayofahamika kama ‘notch’ lakini bado TECNO imehakikisha inaongeza mvuto katika simu hiyo kwa umbo jembamba lenye upana wa nchi 6.2HD+ na uwiano wa 19:9.
Mteja akibadilisha simu ya camon x kwa camon 11 katika duka la TECNO Smart Hub Kariakoo.
Zoezi zima la ubadilishaji wa simu za TECNO camon (camon cx, camon cx air, camon cm, camon x na x pro) linafanyika katika mikoa sita katika maduka ya TECNO yenye promosheni ambayo ni TECNO exclusive Bus Terminal, TECNO Triple B, TECNO Exclusive CCM Babadi Arusha shop, TECNO Exclusive China Plaza Smart Hub, TECNO Exclusive Mlimani City Smart Hub, TECNO Exclusive Samora Smart Hub, TECNO Exclusive Pablo Dodoma, TECNO Exclusive Mbeya Muna Shop, TECNO Exclusive Jambo Mwanza Shop na TECNO Exclusive Tabora Shop.
Ofa hii ya ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 litakuhitaji kufika kati ya maduka hapo juu ukiwa na simu ya TECNO camon na mshiko kidogo ili uweze kupatiwa camon 11 mpya na ofa ya GB 15 kuanzia sasa hadi tarehe 30 ya mwezi huu wa sikukuu za Christmas.

Idris Sultan avunja rekodi nyingine tena

0
0
Mchekeshaji Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la Komedi litakalofanyika mwezi huu nchini Afrika kusini lililoandaliwa na Comedy Central , moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji.

Mualiko wa Idris unakuja baada ya msanii huyo wa tasnia ya uchekeshaji kufanya Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu ya wapenzi wa comedy hapa nchini .Kwa mujibu wake mualiko wa huo ni sifa kubwa kwa Taifa, baada ya bongo flava kutoboa kimataifa, sasa ni zamu ya tasnia ya uchekeshaji wa Tanzania.

Akizungumzia kuhusu tamasha la Sex Tour Idris alisema lilikuwa na lengo kuu ya kuburudisha na kuelimisha watu katika ma swala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.“Tarehe 1 December Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena. Watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket.

SexTour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa ya muziki” anasema.Likibeba ujumbe "Kutokupima hakubadili matokeo"tamasha hilo lilihudhuriwa na wachekeshaji mbali mbali akiwemo Jaymondy, Mkaliwenu, Dogo pepe, Coy Mzungu, Blackpass,kitenge,Nalimi ,Optalema Deo, Max, Young Unstopable ,D comic na wengine wengi huku upande ma muziki wa kizazi kipya ukiwalishwa vyema naa Whozu na Billnass


Idris sultan akiendelea kuvunja mbavu za maelfu za wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika jukwaa la Club next door Arena katika Tamasha la komedi maarufu kama Sex Tour liliofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Maelfu ya wakazi wa jiji wakifurahia burudani za wachekeshaji mbali waliotumbuiza katika onesho la Sex Tour lilofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
Idris akiwa anapima afya yake katika madhimisho ya siku ya ukimwi duniani huku akiongozana na wachekeshaji wenzake kuhamasisha vijana kutokuwa na woga wa kupima na kujua hali zao.

TIMU YA MICHEZO YA BUNGE MSHINDI WA JUMLA WA MEDALI KATIKA MICHEZO YA MABUNGE YA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akimpongeza Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma akitokea Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Naibu Spika aliongoza msafara wa timu ya michezo ya Bunge. Kushoto ni katibu wa Bunge, Mhe. Stephen kagaigai
Wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge wakipokelewa na uongozi wa Bunge, watumishi wa Bunge wakiongozwa na Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai walipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma wakitokea katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akipokea cheti cha ushiriki wa michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ambae ni kiongozi wa msafara wa wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Bujumbura, Burundi katika tukio lililofanyika leo tarehe 10 Desemba, 2018 katika uwanja wa ndege Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye koti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge walioongozwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (mwenye tisheti nyeusi) baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mjini Dodoma wakitokea Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wanamichezo wa timu ya michezo ya Bunge na watumishi wa Ofisi ya Bunge leo tarehe 10 Desemba, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma, wakati timu hiyo ilipowasili kutoka Bujumbura, Burundi katika michezo ya Mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ikiwa ni kuwaeleza kwa ufupi mafanikio waliyoyapata katika mashindano hayo na ushirikiano ulioonyeshwa na watumishi wa ofisi ya Bunge kabla na baada ya mashindano

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

MITANDAO YA KIJAMII YAELEZA INAVYOIONA BENKI KUU YA TANZANIA, YATOA USHAURI

0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WAANDISHI wa habari kutoka mitandao ya kijamii nchini hasa wanaondika habari za uchumi na fedha nchini wametoa mtazamo wao kuhusu namna ambavyo wanaitazama Benki Kuu ya Tanzania(BoT).

Mtazamo huo umetolewa leo Mjini Dodoma kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.

Akitoa mada kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi leo Mjini Dodoma ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT),Mmiliki wa Blog ya K-VIS Blog Khalfan Said amesema mtandao wa kijamii ni aina ya tovuti au Application inayowaruhusu watumiaji kuwasiliana kwa kuchapisha jumbe kwa njia ya maandishi, picha au video kwa kutumia computer au Smart phones.

Amesema unapozungumzia mitandao ya kijamii inayofahamika sana na jamii yetu ni pamoja na Blogs, Youtube, Facebook, Instagram, Flicker, Tweeter, Whatsaap na LinkedIn na kwamba faida ya mitandao ya
kijamii inasaidia kutengeneza mahusiano mapya kati ya mtu na mtu, mtu na taasisi au taasisi na taasisi.


Mmiliki wa Blog ya K-VIS Blog Khalfan Said akitoa ufafanuzi kuhusu namna mitandao ya kijamii inavyofanya kazi,wakati wa emina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.



Mwakilishi wa Michuzi Blog Said Mwinshehe akiwa kama sehemu ya washiriki kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi ambayo imeandaliwa na Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa ajili ya kuwajengea uwezo waandishi wa vyombo vya habari nchini ambapo kabla ya kutolewa kwa mtazamo huo imefafanuliwa kwa kina nini maana ya mitandao ya kijamii na nguvu yake katika kuhabarisha umma.


Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Richard Wambali( wa nne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wengine wa Benki Ku wakiwa pamoja na waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya waandishi wa habari za uchumi na fedha leo jijini Dodoma.

Wateja wa Tigo kuvinjari na Chopper

0
0



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (wanne kulia) na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tigo na Uber muda mfupi baada ya kuzindua promosheni itayowawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari (kushoto) , akipeana mkono wa pongezi na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo, muda mfupi baada ya kuzindua promosheni ambayo itawawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tigo Simon Karikari ( kulia) akibadilishana mawazo na Meneja wa Uber Tanzania Alfred Msemo (wa pili kulia) na Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Hussein Sayed muda mfupi kabla ya uzinduzi wa promosheni ambayo itawawezesha wateja wa Tigo wanaotumia Uber pamoja nabaadhi ya washindi wa promosheni ya Jigiftishe kupanda helkopta siku ya Ijumaa na kufurahia mandhari ya Dar es Salaam wakiwa angani

Taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko ya Wajumbe wa bodi TAWA

Serikali Yaanza Rasmi Kubangua Korosho


KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

UONGOZI WA PRECISION AIR WAOMBA RADHI ABIRIA NDEGE ATR 72 KUPATA HITILAFU

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

SHIRIKA la Ndege la Precision Air wameomba radhi abiria wao baada ya ndege yao ATR 72 kupata hitilafu ya kushambuliwa na ndege wakubwa na kushindwa kuendelea na safari. 

Uongozi wa Precision Air umethibitisha kuwa ndege yao PW 722 itokayo Nairobi kupitia Kilimanjaro hadi Mwanza ilipa hitilafu na kushindwa kuendelea na safari.

Wakitoa taarifa hiyo uongozi wa Precision Air amesema kuwa ndege hiyo PW 722 ilipata hitilafu ila ilifanikiwa kutua katika Uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza. Wamesema kutokana na uwezo na ujuzi walionao marubani pamoja na wahandisi waliweza kufanikisha kutua salama. 

Ndege hiyo ilitua salama kabisa na kuhusu timu ya wahandisi wameendelea na kurekebisha thanzo cha tatizo na wameahidi abiria wote watafika sehemu wanazoenda salama. Aidha, abiria wote waliothirika wameshauriwa kubadilisha ndehe na wameombwa radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na timu yao inaendelea kulifanyia kazi hilo ili kuweka ratiba sawa. Shirika la ndege la Precision Air daima litaendelea kuhakikisha usalama wa abiria na mamlaka husika itahakikisha kuwa matukio kama hayo hayajitokezi tena. 

Ndege ilipata hitilafu hiyo baada ya kuvamiwa na kundi la ndege wakubwa, ndege hiyo aina ya PW 722 ilibeba abiria 68 na wahudumu wanne.
Ndege aina ya ART 72 ilipotua salama kwenye Uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kushambuliwa na ndege wakubwa.

HOSPITALI YA MNAZIMMOJA YAFANYA UCHUNGUZI WA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

0
0
Na Ali Issa Maelezo Zanzibar

Jumla ya kinamama 1,339 wamejitokeza katika uchunguzi pamoja na kufanyiwa vipimo vya maradhi ya kensa ya shingo ya kizazi katika hospitali kuu ya mmanazi mmoja mjini Unguja.

Mratibu wa mradi wa uchunguzi wa kensa ya shingo ya kizazi,Dk. Omar Mwalimu Omar alitoa kakwim hiyo huko hospitali ya mnazi mmoja wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara maalum ya kutembelea eneo linalo endeshwa zoezi hilo. Amesema katika zoezi hilo lililoanza Jumatatu iliopita hadi leo (Jumatatu) watu 36 kati hao wametiliwa mashaka na kufikia maamuzi ya kuchukuliwa vinyama ili kuchunguzwa kwa hatua nyengine na baadaye yatatoka majibu rasm ya afya zao.

“Mara baada ya kuwafanyia uchunguzi mwengine na pindi tukibaini kuna mwenye maradhi hayo , tutaanza naye kwa kumpata tiba kwa kutumia dawa kwa mujibu wa taratibu za kitaalam”alisema Dk Omar. Naye mtaalamu wa magonjwa ya saratani katika hospitali ya mnazi maoja, Dk Abdalla Yussuf Mohamed alisema katika zoezi hilo wanachunguza vinasaba vyote vya akinamama hao ambavyo ni muhimu katika uchunguzi huo.

Mapema Naibu Spika Mgeni Hassan Juma alisema ni vyema wakaongezwa wataalamu wazalendo katika kupata kujifunza kutoka kwa watalamu wakichina waliopo. Aidha aliwapongeza akinamama hao waliojitokeza katika zoezi hilo na kuwataka waendelee kuwahamasisha wenzao ili zoezi hilo lifanikiwe kama lilivyokusudiwa.
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi Zanzibar Dkt. Omar Mwalim Omar akimkaribisha Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma katika Tiba ya Uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi inayofanyika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar. 
Mratibu wa Mradi wa Uchukuzi wa Saratani ya Singo ya Kizazi Zanzibar Omar Mwalim Omar akimuonyesha jambo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipowatembelea Madaktari wanaoendelea kutoa matibabu Hospitalini hapo. 
Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Maabara Kibwana Omar Kibwana wakati alipotembelea Chumba hicho cha Maabara Hospitalini hapo (kulia) Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman. 
Mtaalamu wa Magonjwa ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt. Abdalla Yusssuf Mohamed akimpatia maelezo Naibu Spika Mhe. Mgeni Hassan Juma wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi mmoja Mjini Zanzibar. 

MIL. 800 ZATAKIWA KUKAMILISHA MAKAZI MRADI WA STIGLERS GORGE

0
0
NA MWAMVUA MWINYI, RUFIJI .

NAIBU Waziri wa Ujenzi ,Elias Kuandikwa amemuagiza mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) awasiliane na wizara ya nishati ,kuharakisha upatikanaji wa sh.milioni 800 ili kumalizia ukarabati wa nyumba za makazi 34 zinazojengwa katika ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme wa stiglers gorge Rufiji mkoani Pwani. 

Aidha amemtaka msimamizi wa ujenzi wa nyumba hizo kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo wiki nne zijazo. Kuandikwa alielekeza hayo, wakati alipotembelea ujenzi wa barabara kutoka Kibiti -Mkongo na upande wa Mkoa wa Morogoro kupitia Ngerengere hadi Ubena-zote kuelekea kwenye mradi wa stiglers gorge. 

Alisema,wizara kupitia TBA ilikuwa na jukumu la kukarabati maeneo ya makazi na kutakiwa kumaliza mwezi Novemba mwaka huu lakini kutokana na changamoto ya kifedha ujenzi upo hatua ya umaliziaji. ” Nyumba hizi ni muhimu na kuna haja ya kuzikamilisha mapema ili mkandarasi akifika kuanza kazi akute mazingira ya makazi yako vizuri.” 

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UJUMBE WA UWT UKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAKE

0
0


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania.(UWT) Thuwaiba Editon Kisasa, kulia Katibu Mkuu wa UWT, Queen Mlozi na kushoto Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka, walipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mwenyekiti wa UWT Taifa Kabaka.10-12-2018.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania,(UWT) Gaudensia Kabaka,alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar,akiwa na Ujumbe wake wa Viongozi wa UWT.kulia Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT. Queen Mlozi.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Gaudensia Kabaka,Makamu Mwenyekiti wa UWT Thuwaiba Editon Kisasa na Katibu Mkuu wa UWT.B. Queen Mlozi, wakiwa katika ukumbi wa mkutona Ikulu leo wakati wa mazungumzo yao walipofika kujitambulisha.kwa Rais wa Zanzibar.(Picha na Ikulu)
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images