Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

BANDARI TANGA KUHUDUMIA SHEHENA YA NCHI SABA KWA KUTUMIA MPAKA MMOJA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Bandari ya Tanga inaelezwa kuwa bandari ya kipekee na ya aina yake barani Afrika inayoweza kuhudumia nchi saba kwa kutumia mpaka mmoja.

Hayo yameelezwa na Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama, ofisini kwake jijini Tanga wakati akizungunza na waandishi wa habari kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika kuhakikisha wanaongeza ufanisi wa bandari hiyo.

Amesema mbali na kuwa na uwezo wa kuhudumia nchi saba bandari ya Tanga kijografia ina sifa ya kuwa bandari pekee ya asili kutokana na kuwa na kina cha maji cha asili cha kuanzia mita tano hadi 30 huku ikizungukwa na visiwa vya asili ambavyo husaidia kupunguza nguvu ya mawimbi.

"Serikali ya awamu ya tano kwa kuona upekee wa bandari ya Tanga iliamua kutoa fedha za kuwekeza katika miradi ya uboreshaji ili kuongeza ufanisi," amesema.

Salama alifafanua kuwa maboresho makubwa ya bandari hiyo ambayo kwa sasa inaongoza kuwa bandari inayohudumia mizigo kwa kasi Afrika Mashariki, yamefanyika katika nyanja ya ukatabati na ununuzi wa mitambo mipya, ujenzi wa miundombinu ya kuhifadhia mizigo, na uboreshaji wa mifumo ya teknolojka ya habari na mawasiliano.
Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama,akizungumza na Waandishi wa habari juu ya mipango ya kuboresha bandari ya Tanga na mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitatu ya Rais Magufuli.
Meneja wa bandari hiyo, Percival Salama, akiwaonyesha waandishi wa Habri baadhi ya mashine mpya za kupakulia mzigo zilizoletwa katika Bandari ya Tanga
Bandari ya Tanga ikonekana kwa juu kama ilivyopigwa na Mpiga picha wetu alipotemblea Bandari hiyo .
Mdaki mpya wa kukagua mizigo uliopo katika Bnadari ya Tanga.


BITEKO AICHARUKIA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI KIJIJI CHA MANGAE , WILAYANI MVOMERO

$
0
0
Na Mwadishi wetu, Morogoro
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko ameiagiza Menajimenti ya Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji ch  Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro kusimamisha uchimbaji  hadi itakapokamilisha taratibu za kisheria za Serikali  zinazosimamia madini  pamoja na kuwalipa fidia wananchi waliohamishwa meneo yao  waliokuwa wakiishi.

Biteko alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo kwenye  eneo la mgodi huo uliopo katika vijiji vya Mtupule na Mangae  na  kubaini imekuwa ikeindelea kuchimba madini  ya dhahabu kinyume na sheria  licha ya kutakiwa kukamilisha kwanza  utaratibu waliopewa wa kisheria .

Mbali na hilo , Naibu Waziri alionya na kutoa wito  kwa Watanzania wote wanapoamua kuingia mikataba na mikataba ya  wachimbaji wadogo ni lazima itambuliwe na serikali kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji  sekta ya madini na si vinginevyo.

Naibu Waziri alisema , kufuatwa kwa sheria na  utaratibu wa mikataba na wawekezaji wa n je inalenga kuwalinda   uwekezaji wao  ili  baadaye wasione wananyanyaswa pale  mikataba walioingia na watu wasio waaminifu inakinzana na sheria mpya  ya  madini

Hata hivyo alisema ,  manufaa ya madini kwa wananchi wa eneo hilo hayawezi kupatikana  endapo mahusiano kati ya mgodi na wananchi hayatakuwa mazuri na kwamba  rasilimali za nchi lazima ziwanufaishe Watanzania  wote yakiwemo Madini.
 Mkazi wa kijiji cha Mangae , kata ya Mangae, wilayani Mvomero mkoani Morogoro, Anita John  akitoa malalamiko yake  kwa Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko ( hayupo pichani )  kuhusu  Kampuni ya MMC ya uchimbaji wa  dhahabu  katika eneo la kijiji hicho kuendesha shughili zao pasipo kuwafidia  makazi yao  waliyokuwa wakiishi kupisha uchimbaji wake.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  akisoma  baadhi ya nyaraka za  Kampuni ya MMC  ya  uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara ya  kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo na ( wapili kulia) ni Mkuu wa wilaya hiyo, Mohamed Utaly.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akipewa maelezo na kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  wakati wa  ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.
 Naibu  Waziri wa Madini, Doto Biteko  ( aliyeweka mikono mfukoni) akiteremka chini kutoka kuangalia mashine  za  Kampuni ya MMC zilizofungwa kwenye mgodi wa uchimbaji wa  dhahabu katika kijiji cha Mangae  wilayani Mvomero, mkoani Morogoro   wakati wa ziara  ya kukagua  shughuli zinazofanywa  na Kampuni hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Taasisi za Umma Zashauriwa Kuwa na Akaunti za Makusanyo Kwenye Benki Zaidi ya Mojaoja

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO

Taasisi za Umma zimeshauriwa kuwa na akaunti za makusanyo kwenye benki zaidi ya moja kati ya benki zilizoungwa na Mfumo wa Serikali wa Ulipaji wa Kielektroniki (GePG) ili kuwarahisishia walipaji wa huduma za serikali.

Ushauri huo umetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu wakati akifungua mkutano wa mwaka wa watumiaji wa mfumo wa GePG katika ukusanyaji wa fedha za umma uliozishirikisha taasisi za Umma zinazotumia Mfumo huo pamoja na timu ya GePG kwa ajili ya kujengeana uwezo wa namna bora ya kutumia mfumo huo.

Dkt. Kazungu amesema kuwa utaratibu wa malipo kupitia GePG unatoa fursa ya kuwa na njia nyingi za kulipia fedha za umma pamoja na kuwapa walipaji wa huduma za serikali utaratibu rafiki na machaguo mengi ya kufanya malipo.

"Kwa kuwa malipo yote yanayopitia GePG hayatozwi ada za miamala na benki hizo hivyo kuongeza akaunti za makusanyo katika benki hakutoongeza gharama za miamala kwa taasisi za umma bali kufanya hivyo kutaondoa hatari ya Ofisi husika kukosa huduma ya malipo endapo benki inayotumika itashindwa kutoa huduma kwa sababu mbalimbali", alisema Dkt. Kazungu.

Dkt. Kazungu ameongeza kuwa utaratibu huo wa makusanyo kupitia GePG unaenda sambamba na utekelezaji wa maelekezo mengine ya Serikali yanayohusu makusanyo ikiwemo yale yanayotaka akaunti kuu za makusanyo za taasisi za umma kuwepo benki kuu ya Tanzania (BoT).

KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KAMATI Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar imekutana chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, imeunga mkono juhudi za Serikali kusaini Makubaliano ya Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) na Kampuni ya RAKGAS ya Ras al Khaimah ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Akitoa ufafanuzi jana Disemba 11, mwaka 2018 juu ya masuala mbali mbali yaliyoazimiwa kupitia Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, ameeleza kwamba Kikao hicho kimeipongeza Serikali kwa kusaini mkataba huo na kueleza kuwa ulifuata taratibu zote za kisheria.

Dk. Mabodi aliongeza kwamba maamuzi ya kusaini mkataba huo yametokana na kukamilika kwa taratibu mbali mbali za kisheria kwa pande zote za Muungano ambapo kupitia maamuzi ya kisheria Zanzibar imepewa mamlaka ya kuchimba na kusimamia yenyewe masuala ya Mafuta na Gesi.

Alisema kuwa kufanikiwa kwa mchakato huo wa kusainiwa mkataba huo ni hatua kubwa ya maendeleo iliyofanywa na Dk.Ali Mohamed Shein, kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jonh Pombe Magufuli.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIA WA MSUMBIJI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kitengo cha makosa ya rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imemuhukumu Mwanamke mmoja Ana Moisie Chissano (36)raia wa Msumbiji kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kukutwa na Kg 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.

Mshtakiwa aliyekuwa amefunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi namba 6/2016 amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria Kuzuia na kusababisha na kupambana na dawa za kulevya. 

Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba 12.2018 na Jaji Lilian Mashaka baada upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka hayo pasipo Kuacha shaka baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.

Aidha Mahakama Imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Lilian Mashaka amesema ametoa adhabu hiyo kulingana na kifungu cha sheria namba 15 (1) (b) cha Sheria namba 5 ya 2015 ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

Jaji Mashaka amesema sheria hiyo inaelekeza mtu yoyote anayejihusisha na dawa za kulevya anapopatikana na hatia anapaswa kutumikia kifungo cha maisha jela."Nimezingatia sababu zilizotolewa na mshitakiwa, lakini mahakama pia imezingatia sheria ambayo imeweka adhabu kwa mtu kupitia kifungu hicho inayosema mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa makosa ya dawa za kulevya basi adhabu yake ni jela maisha.

RAIS DKT.SHEIN AFUNGUA KONGAMANO LA PILI LA KISWAHILI LA KIMATAIFA ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akinesha Kitabu cha Mtunzi Shafi Adam Shafi cha Mtoto wa Mama, baada ya kukizinduwa leo wakati wa hafla ya Kongamalo la Pili la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil ,kulia Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, Katibu Mtendaji wa BAKIZA Bi. Mwanahija Juma na kushoto Mtunzi wa Kitabu hicho cha Mtoto wa Mama Mzee Shafi Adam Shafi akipiga makofi baada ya uzinduzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Vitabu mbalimbali vya Kiu na Nyota ya Rehema na mtunzi wa Vitabu hivyo Ndg. Mohammed Suleiman, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idirissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi Cheti Mtunzi wa Vitabu vya Kuli, Vuta N’kuvute, Haini, Mbali na Nyumbani , Kasiri ya Mwinyi Fuad na Mtoto wa Mama kilichozinduliwa leo.Ndg. Shafi Adam Shafi na kulia Waziri wa Vijana Utamaduni,Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozui Ali Karume, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Mohammed Seif Khatib, (katikati) wakati akitembelea maonesho ya Vitambu mbalimbali katika viwanja vya Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil , akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakiangalia vitabu hivyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Alim Mohamed Shein, akiangalia Vitambu mbalimbali vya Wachapishaji wa Vitabu kutoka Tanzani na Kenya wakati wa maonesho hayo yaliokwenda sambamba na Ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili LILILOFANYIKA Zanzibar katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

MHANDISI MANYANYA ATEMBELEA MAONESHO YA TATU YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA

$
0
0
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiMhandisi Stella Manyanya (Mb)  akisikiliza wafanyakazi wa TanTrade namna huduma ya Kliniki ya Biashara inavyofanya kazi ya kutatua changamoto za wafanyabiashara kwenye Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yalifanyika tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2018 katika uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere Dar es Salaam 
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiMhandisi Stella Manyanya (Mb) akisikiliza wafanyakazi wa TanTrade namna huduma ya Kliniki ya Biashara inavyofanya kazi ya kutatua changamoto za wafanyabiashara kwenye Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yalifanyika tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2018 katika uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere Dar es Salaam. Katikakati ni Mhe Constantine Kanyasu (Mb) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na kushoto ni Bw. Edwin Rutageruka Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade   
 Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na UwekezajiMhandisi Stella Manyanya (Mb)  akitoa maelekezo kwa Bw Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade na wafanyakazi wa TanTrade ya namna ya kuwafikia wananchi ili kupata huduma ya Kliniki ya Biashara inayotolewa bure na TanTrade kwenye Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yalifanyika tarehe 5 hadi 9 Desemba, 2018 katika uwanja wa Maonesho wa Mwl J.K.Nyerere Dar es Salaam. Katikakati ni Mhe Constantine Kanyasu (Mb) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

KAMPUNI YA SETEWICO LIMITED DODOMA YAIOMBA SERIKALI KUANGALIA NAMNA YA KUPUNGUZA UTITIRI WA KODI ZILIZOPO

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

UTITIRI wa kodi ambazo zinalipwa na wawekezaji nchini bado umeonekana kuwa changamoto kubwa kwao na hivyo kutoa ombi kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli kuangalia namna ya kupunguza utitiri huo wa kodi ambao umekuwa mzigo kwao pamoja na wananchi kwa ujumla.

Ombi hilo limetolewa Mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl baada ya baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) pamoja na waandishi wa habari wa habari za fedha na uchumi kufanya ziara ya kutembelea kampuni hiyo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.Waandishi hao wapo kwenye mafunzo ya kuandika habari za fedha na uchumi yaliyoandaliwa na BoT ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari nchini.

"Kwa upande wangu lazima niseme nimeona ushirikiano wa hali ya juu katika Serikali yangu Dodoma kwani nikiwa na tatizo lolote ninakwenda katika ofisi za Serikali yangu ya Dodoma, hivyo imeonesha uthamini wa kiwango kikubwa wa kazi tunazofanya" ameongeza Katrin.

Amesema kampuni yao inapongeza juhudi za Serikali katika ujenzi wa Tanzania ya viwanda nchini ili kufikia uchumi wa kati na wamedhamiria kuunga mkono kwa vitendo kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu lakini changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo ni uwepo wa kodi nyingi ambazo zinawafanya wanakuwa katika wakati mgumu kutekeleza majukumu yao ya uzalishaji kwai gharama ni kubwa.

Waandishi wa habari wakiwa pamoja na maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl wakati anafafanua namna kampuni yao inavyotengeneza mvinyo unaotokana na zabibu ya Dodoma.Waandishi na maofisa hao wametembelea kampuni hiyo kama sehemu ya mafunzo kwa vitendo.
:Mwenyekiti wa mafunzo ya waandishi wa habari za uchumi na fedha Nurdin Selemen (kulia) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl wakati wa waandishi wa vyombo mbalimbali walipotembelea kwenye kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za fedha na uchumi na maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) baada ya kutembelea kampuni yake kuangalia shughuli za uzalishaji.
Meneja Msaidizi Uchumi na Takwimu wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Kanda ya Kati, Dk. Zegezege Mpemba akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Ushirikiano na Uhusiano wa Jamii wa Kampuni ya Cetewico Limited Katrin Boehl() baada ya waandishi wa habari walioko kwenye mafunzo ya habari za fedha na uchumi kutembelea kampuni hiyo.



MMILIKI MABASI YA PRINCES MURO ALIPA FAINI YA MILIONI 115/-AKWEPA KWENDA JELA MIAKA NANE

$
0
0
*Ni baada ya kukiri makosa ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la kuiba mafuta bomba la bandari

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro Majid Kimaro kulipa faini ya Sh. milioni 115 au atatumimia kifungo cha miaka nane jela baada ya kukiri mashtaka yanayomkabili ya kutakatisha fedha na kuongoza genge la uhalifu ili kuiba mafuta katika bomba linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Pia Mahakama imeamuru gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 856 ADH ambalo lilitumika kuiba mafuta hayo ambayo ni zaidi ya lita 26,875.25 ya dizeli na petroli litaifishwe na kuwa mali ya Serikali.

Hukuumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kuhukumiwa na jopo la mawakili likiongozwa na Wakili wa Serikali Wankyo Simon akisaidiana na Jackline Nyantori, Patrick Mwita

Alitoa Hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema, Mahakama imemtia hatiani mshitakiwa kwa makosa mawili baada ya kukiri kutenda makosa hayo mwenyewe.

Akisoma adhabu, amesema, katika shitaka la kuongoza genge la uhalifu, Muro anahukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano na iwapo akishindwa atatumimia kifungo cha miaka mitatu gerezani. Wakati katika shtaka la utakatishaji fedha, mshtakiwa ameamriwa kulipa faini ya Sh.milioni 110 au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.

Pichani mshtakiwa Majid Kimaro ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya mabasi ya Princes Muro akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kufanikiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 115 na kukwepa kutumikia kifungo cha miaka nane gerezani.

Real Madrid kutafuta hat-trick ya Klabu Bingwa ya Dunia

$
0
0
Kama Real Madrid walihitaji kujua ni nani wa kumuhofia kwenye fainali za mwaka huu za Klabu bingwa ya Dunia, basi majibu yalipatikana Jumapili iliyopita ambapo miamba kutoka Amerika ya Kusini, River Plate na Boca Juniors waliumana katika dimba la Santiago Bernabeu na Rive Plate kuibuka vinara. Bingwa wa Ulaya na wa Amerika ya Kusini huingia katika hatua ya nusu fainali na mara nyingi (mara 10 kati ya fainali 13 zilizopita) hukutana fainali.

Real Madrid wameshinda fainali mbili zilizopita za Klabu Bingwa ya Dunia na baada ya kumjua mpinzani wao kutoka Amerika ya Kusini wikendi iliyopita watakuwa wanajipanga kushinda kwa mara ya tatu mfululizo kama walivyofanya kwenye Kombe la Klabu bingwa Ulaya. River Plate walishinda mchezo wa pili wa fainali ya CONMEBOL ambao ulichezwa jijini Madrid katika uwanja wa nyumbani wa klabu ya Real Madrid, Santiago Bernabeu baada ya mechi hiyo kuahirishwa mara mbili jijini Buenos Aires, mara ya kwanza kufuatia mvua kubwa na mara ya pili basi la Boca Juniors kushambuliwa na mashabiki wa River Plate.

Wapenzi wa soka barani Africa wataweza kutazama michuano hii kupitia chaneli za michezo za StarTimes ambao ndio warushaji rasmi wa michuano hii kwa ukanda wa Africa. Beki wa kati wa Klabu ya Real Madrid Raphael Varane ambaye mwaka huu alishinda Kombe la Dunia na timu ya taifa ya Ufaransa tayari ameshacheza fainali 3 za Klabu bingwa ya Dunia na kushinda zote, aliiambia tovuti ya timu hiyo kwamba wanakwenda Abu Dhabi kushinda tena.

“Tunapenda kuendelea kuweka historia, tuna shauku kubwa kwa sababu sio rahisi kufika hatua hii, unahitaji kushinda ligi ya mabingwa “Hakuna timu ambayo imewahi kushinda mara tatu Kombe hili na sisi tunataka kuweka historia mpya. Tunafahamu ni ngumu lakini lakini tunayo njaa na ari ya kushinda” alisema Varane. Kwa mwaka huu Klabu bingwa ya dunia itachezwa katika Falme za Kiarabu kuanzia tar 12 hadi 22 Disemba. Mchezo wa kwanza unawakutanisha Al Anin ya nchini humo na Team Wellington ya New Zealand saa 12:30 jioni na utarushwa moja kwa moja kupitia ST World Football.

VIONGOZI KUTOKA CUBA NA UMOJA WA MATAIFA WAFANYA ZIARA ZA KIKAZI NCHINI

$
0
0

Viongozi kutoka nchini Cuba na Umoja wa Mataifa wanafanya ziara za kikazi nchini Tanzania zenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na mamlaka hizo.

Naibu Waziri wa Kilimo wa Cuba, Mhe. Jose Miguel Rodriguez de Armas na ujumbe wake waliwasili nchini tarehe 12 Desemba 2018 na watakuwepo hadi tarehe 19 Desemba 2018.


Ziara ya Mhe. Naibu Waziri wa Cuba na ujumbe wake hailengi tu kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kihistoria kati ya Cuba na Tanzania, bali  inalenga pia kufanya majadiliano na wadau husika, ya namna ya kuondoa changamoto zinazokikabili kiwanda cha Labiofam ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.  


Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Naibu Waziri anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Kilimo na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).


Kiwanda cha Labiofam kimejengwa Kibaha mkoani Pwani kwa msaada wa Serikali ya Cuba kwa ajili ya kutengeneza viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaosababisha ugonjwa wa malaria.


  Kwa upande wa Umoja wa Mataifa, ujumbe wa Umoja huo ukiongozwa na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Misheni za Ulinzi na Amani, Bw. Jean- Pierre Lacroix na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO utafanya ziara nchini tarehe 13 na 14 Desemba 2018.


Ziara hiyo ni sehemu ya kuadhimisha mwaka mmoja tokea shambulizi lililofanywa na waasi wa Allied Democratic Forces dhidi ya kombania ya Tanzania katika maeneo ya Simulike, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Askari 14 wa Tanzania walipoteza maisha katika shambulizi hilo.


Ujumbe huo unatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kuhusu kuboresha ushiriki wa Tanzania katika vikosi vya kulinda amani.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma

 12 Desemba 2018


Arsenal na Chelsea kutua dimbani kesho UEFA Europa League

$
0
0
Kocha Maurizio Sarri na Unai Emery wako katika nafasi nzuri kwenye makundi yao na wala hawana presha ya matokeo kuelekea mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi hivyo tutarajie upangaji wao wa vikosi kuwapumzisha wachezaji nyota. Kikosi cha Sarri (Chelsea) licha ya kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City wikendi iliyopita tayari wameshajihakikishia kumaliza wakiwa vinara wa kundi L katika ligi ya Europa.

Kocha huyo muitalia anatarajia kuwapatia nafasi wachezaji ambao huwa hawapati namba kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Na mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Eden Hazard amesema wanahitaji kuachana na ushindi wa lioupata dhidi ya Manchester City na kuangalia mechi zijazo. “Unahitaji kuangalia zaidi kile unachotakiwa kufanya. Sisi tunataka kushinda, tunafurahi tumeshinda mchezo uliopita na tunajiandaa na mchezo wa Alhamisi (dhidi ya MOL Vidi)

Kwa upande wa kocha wa Arsenal, Unai Emery yeye ana Vijana zaidi ya 10 walio chini ya umri wa miaka 20 na huenda akawatumia hao katika mchezo wao dhidi ya Qarabag huko nchini Azerbaijan.
Kutoka Bundesliga klabu ya RB Leipzig ambayo msimu uliopita ilicheza kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, safari wanahitaji kushinda mchezo wao dhidi ya Rosenborg huku wakitegemea ndugu zao Red Bull Salzburg washinde jijini Glasgow dhidi ya Celtic.

Balaa lingine ni kwa klabu ya AC Milan ambao wanafunga safari hadi Ugiriki kuumana na Olympiacos, wakiruhusu kufungwa magoli 2 watakuwa mameaga mashindano. Michezo yote hii itaonyeshwa moja kwa moja kupitia StarTimes. MOL Vidi vs Chelsea saa 1:55 Usiku kupitia ST World Football, Arsenal vs Qarabag saa 5:00 Usiku kupitia World Football na Olympiacos vs AC Milan saa 5:00 Usiku kupitia ST Sports Premium. Chaneli zote hizo zinapatikana katika kifurushi cha MAMBO (Antenna) kwa Tsh 14,000 tu kwa mwezi na SMART (Dish) kwa TSh 21,000 kwa mwezi, ambapo katika msimu huu wa Siku kuu kila mteja atapata kifurushi cha juu zaidi kila anapolipia kifurushi chake kwa mwezi.

VIGOGO 18 TRL KORTINI ,WASOMEWA MASHITAKA 15 YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

VIGOGO 18 wa Kampuni ya Reli Tanzania(TRC) wamefikishwa katika  Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 15 ya matumizi mabaya ya madaraka  yakiwemo ya 
Kuidhinisha michoro 274 ya mabehewa ya mizigo kwa Kampuni ya Hindusthan kinyume na mkataba wa zabuni. 

Washtakiwa hao wamesomewa  mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Maghela Ndimbo.

Washtakiwa katika kesi  hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Kipallo Kisamfu, Gilbert Minja, Pascal Mafikiri, Mathias Massage,  Anthony Munishi, Charles Ndenge, Ferdinand Soka,  Muungano Kaukunda,  Joseph Mlinda, Kedmond Mapunda, Lowland Simtengu, Ngoso Mwakilembe, Yonah Shida, Malumbo Malumbo, Stephen Kavombwe, Donatus Bandebe, John Charles na Ally Mwangila.

Katika shtaka la kwanza dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TRL,  Kipallo Kisamfu inadaiwa Machi 21 mwaka 2013 huko katika makao makuu ya kampuni hiyo, alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa zabuni kwa Kampuni ya Hindusthan Engeering and Industries Limited bila kuhakiki  mkataba huo utatekelezeka kwa kuzingatia masharti ya mkataba. 

Aidha imedaiwa, Kaimu Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Paschal Mafikiri, anadaiwa kati ya Februari 21 na Agosti 15 mwaka 2013  alishindwa kutoa taarifa ya mkataba wa zabuni wa kampuni hiyo na kusababisha Kampuni hiyo ijipatie manufaa. 

Pia inadaiwa, Mafikiri aliidhinisha michoro 274 ya mabehewa ya mizigo kwa Kampuni ya Hindusthan kinyume na mkataba wa zabuni. 

Mshtakiwa huyo pia anadaiwa kwamba kinyume na mkataba aliidhinisha michoro ya mabehewa iliyoandaliwa na Kampuni ya Hindusthan. 

Aidha mshtakiwa Kaupunda, kiwa Kaimu Mhandisi wa Ufundi na Mkuu wa Idara anadaiwa  Kuidhinisha a mchoro wa mabehewa na mafuta iliyoandaliwa na kampuni hiyo. 

Pia,  washtakiwa, Kaupunda, Syaizyagi, Mapunda na Simtengu  wanadaiwa kati ya Januari 10 na Februari 20 wakiwa waajiriwa wa TRL kwa nafasi zao za Mhandisi Mkuu wa Ufundi, Mchoraji Mkuu na Msaidizi Mkuu wa Meneja wa Usafirishaji wa Reli na wote wajumbe Kamati ya uthamini walitumia madaraka vibaya kwa kushindwa kufanya uchambuzi za zabuni. 

Shtaka la saba kwa mshtakiwa Munishi , Meneja Mkuu wa Usambazaji, anadaiwa kuidhinisha usambazaji wa mabehewa 274 Febriaro11,2013 bila kuwasilisha ripoti hiyo kwenye bodi ya zabuni .

Washtakiwa Minja, Mafikiri, Massae,  Munishi na Ndenge, wanadaiwa Februari 20,2013 kwa kutumia madaraka yao vibaya waliidhinisha mapendekezo ya kamati ya uthamini katika mkataba wa Kampuni ya Hindusthan kusambaza mabehewa 274 .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Bonde ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wananchi wafuate sheria

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu imesema kuwa haiwezi kuwavumilia wananchi wanaharibu vyanzo vya maji.  Hayo ameyasema Afisa   wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana na wananchi kufanya shughuli mbalimbali ndani ya mita 60 katika vya vyanzo vya maji ambapo wameweza kukata mazao mbalimbali katika eneo la Ruvu.

Amesema Bonde la Wami/Ruvu  ilishatoa elimu kwa wananchi kuacha kufanya shughuli za kilimo ndani ya mita 60 lakini utekelezaji wake umekuwa wa ukisuasua na kulazimika kuvyeka mazao  yaliyokuwa yanalimwa na wananchi hao.

Simon amesema kuwa vyanzo vya maji lazima vilindwe kwani wananchi wakikosa huduma za maji watawalalamikia  serikali hasa wale watu waliopewa dhamana ya kusimamia.  Aidha amesema wananchi wa Ruvu kila walipokutana walikuwa wanasema wakishavuna wanaacha kilimo hicho katika Kingo mto Ruvu matokeo yake walikuwa wakivuna na kupanda tena na kuomba tena ambapo ukawa ndio mchezo wao.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi waliopo katika Bwawa la Mindu Morogoro walishalipwa tangu mwaka 1970 matokeo yake watu wanauziana maeneo hayo wakitaka kuwaondoa wanadai fidia wakati watu walishalipwa. Amesema hatabaki  mtu salama kwa kutokana na vitu vyote viko kisheria katika kulinda vyanzo vya maji na wasimamizi wako.
Ngonyani amesema kuwa watu wafuate sheria kwani wakiwa kinyume na sheria watakuwa wanalalamika tu huku wakijua walikuwa wamevunja sheria. "Mimi nitaendelea kusimamia sheria na ndio kazi yangu ili kuhakikisha vyanzo vya maji vinatumiwa kwa uangalifu"amesema Ngonyani.
Afisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na hatua wanazozichukua katika utunzaji wa vyanzo vya maji katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.

RAIS DKT. MAGUFULI PAMOJA NA WAZIRI MKUU WA MISRI DKT. MOSTAFA MADBOULY WASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA UJENZI WA MRADI WA KUZALISHA UMEME MEGAWATI 2100 KATIKA MTO RUFIJI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco Dkt. Tito Mwinuka wapili kutoka kulia akifatiwa na Mwanasheria wa Shirika hilo Isdori Nkindi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji kati ya Waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly, Waziri wa Nishati Medard Kalemani wakipiga makofi wakati waakilishi wa Kampuni ya J.V Arab Contractors/El Sewedy Electric kushoto pamoja na Waakilishi wa Shirika la Umeme nchini Tanesco wakionesha vitabu vya mikataba hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly akizungumza na wageni mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kushuhudia utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi mara baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly kabla ya tukio la la kihistoria la utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme megawati 2100 katika mto Rufiji ambao utagharimu zaidi ya kiasi cha Shilingi za kitanzania Trilioni 6.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

SIMIYU KUANDAA MWONGOZO WA UWEKEZAJI KWA KILA KIJIJI

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkoa wa Simiyu umejipanga kuandaa mwongozo wa uwekezaji  kwa kila Kijiji na Mtaa utakaobainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika kijiji na mtaa husika katika vijiji vyote 471 na Mitaa 92 ya wilaya zote tano za Mkoa huu, ikiwa ni maandalizi ya utekelezaji wa Falsafa ya Bidhaa Moja Kijiji Kimoja(OVOP) mwaka 2019/2020.

 Hayo yamebainishwa  Desemba 11, 2018 Mjini Bariadi katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Mitaa 92, Watendaji wa Kata 130 na Maafisa tarafa 16 juu ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ESRF), ambalo pia limewahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.

Awali akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huu unatekeleza Falsafa ya Bidhaa Moja Wilaya ambayo ilianza baada ya ESRF kufanya utafiti na kuibua fursa 26 ndani ya mkoa na sasa inajipanga kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na kuanza utekelezaji wa Bidhaa Moja Kijiji Kimoja.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 katika kongamano lililolenga kuwajengea uwezo wa namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, kwa kushirikiana na Wataalam kutoka ESRF, ambalo pia liliwahusisha viongozi na watendaji wa Chama na Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa.
  Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Prof. Samwel Wangwe akiwasilisha mada kwa Watendaji wa Vijiji 471, Watendaji wa Kata 130, Maafisa Tarafa 16 juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa mkoani Simiyu, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
Baadhi ya Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani)  katika kongamano la kuwajengea uwezo Watendaji hao juu ya  namna ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11,2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wataalam kutoka ESRF, Viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiwemo Watendaji wa Vijiji, mitaa na kata (wenye fulana za rangi ya yachungwa na nyeupe) , baada ya kongamano la kuwajengea uwezo viongozi hao juu ya namna ya kuibua fursa za uwekezaji, kwa ajili ya kuandaa mwongozo wa uwekezaji kwa kila kijiji na mtaa, lililofanyika Mjini Bariadi Desemba 11, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Mahiga: Tuadhimishe Uhuru kwa kuwakumbuka waliopigania Uhuru huo

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine Mahiga amesema kuwa wakati wa kuadhimisha Uhuru ni lazima kuwakumbuka viongozi waliopigania Uhuru huo. Mahiga aliyasema hayo wakati sherehe za Uhuru wa Nchi ya Kenya kwa Wakenya waishio Tanzania iliyofanyika katika ukumbi Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Kenya inaadhimisha miaka 55 ni kutokana na Baba wa Taifa wa nchi hiyo Jomo Kenyatta kupigana mpaka kupatikana kwa Uhuru ambao wa Kenya wanaendelea kuwa wamoja. Mahiga amesema Tanzania na Kenya zina uhusiano ambao ulitokana na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Kenya Hayati Jomo Kenyatta na aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambapo mafanikio hayo ndio nchi mbili zinaendelea kufaidi. Aidha amesema miaka 55 ni mingi kwa Kenya kuendelea kulinda misingi iliyoachwa na viongozi waliopigania Uhuru.

Nae Balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kazungu amesema kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa na historia na kufanya wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uchumi unaotegemeana katika biashara pamoja na Uwekezaji. Amesema kuwa Tanzania zimefungua Milango ya biashara kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya kuwa na nia njema kurahisha biashara pamoja na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema Kenya zimefungua milango kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya Uwekezaji pamoja na biashara bila vikwazo vyovyote. Katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Kenya viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine Mahiga akizungumza kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu akizungumza na wageni waalikwa kutoka Balozi mbalimbali pamoja na viongozi wa serikali ya Tanzania wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa KTN, Mark Masai akitoa historia jinsi nchi ya Kenya ilivyopata uhuru wakati wa hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine(wa kwanza kulia) pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakikta keki kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa , Balozi Augostine pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla fupi ya kusherekea miaka 55 ya Uhuru wa Nchi ya Kenya iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

BASHUNGWA AKUTANA NA TBL KUJADILI NAMNA YA KUFUNGAMANISHA KILIMO NA VIWANDA

$
0
0


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda.

Amesema kuwa kampuni hiyo inazalisha bia kwa wingi nchini Tanzania hivyo mazungumzo hayo yataongeza chachu na tija katika kuongeza masoko ya wakulima nchini.

Mhe Bashunwa ameyasema hayo leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam na kuhudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi wa sera na Mipango, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya usalama wa chakula, Kaimu Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya mazao.

Wengine ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti Tanzania (TARI), Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo (TADB) na Benki ya Uwekezaji (TIB), Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko, na Muwakilishi wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi  kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee. 
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akiongoza kikao kazi  kilichofanyika katika ofisi za wizara ya Kilimo maarufu Kilimo 1 Jijini Dar es salam leo tarehe 12 Disemba 2018 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee. 
Kikao kikiendelea 
Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Afrika Mashariki wa kampuni (TBL) Ndg Gareth Da Gee akifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) kujadili namna ya kufungamanisha Kilimo na Viwanda nchini.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 13,2018

Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images