Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

DKT. MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO WA KUIGWA KIUTENDAJI NA TAASISI NYINGINE ZA UMMA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine kiutendaji kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na weledi ili kujenga misingi bora ya utumishi wa umma nchini.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na menejimenti ya ofisi yake, lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wamepewa dhamana ya kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa na tija na maslahi kwa maendeleo ya taifa hivyo hawana budi kutekeleza wajibu wao kikamilifu.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, watumishi wakifanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma iliyopo, malalamiko yasiyo ya lazima kwenye eneo la utumishi na utawala bora yatapungua kwa kiwango kikubwa.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, mtumishi wa umma anatakiwa kupimwa kwa utendaji kazi wake kwa matokea chanya ili atakapopanda daraja ajivunie utendaji kazi wake na kuongeza kuwa, upimaji huo utapunguza malalamiko ya kutopandishwa madaraja kwa watumishi ambao hawawajibiki ipasavyo.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amekutana na menejimenti ya ofisi yake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuripoti na kuanza kazi rasmi tarehe 14 Novemba, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018 na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kikao cha menejimenti ya ofisi yake (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.


MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA OFISI YAKE KUWA MFANO WA KUIGWA KIUTENDAJI NA TAASISI NYINGINE ZA UMMA

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine kiutendaji kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na weledi ili kujenga misingi bora ya utumishi wa umma nchini. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na menejimenti ya ofisi yake, lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wamepewa dhamana ya kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa na tija na maslahi kwa maendeleo ya taifa hivyo hawana budi kutekeleza wajibu wao kikamilifu. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, watumishi wakifanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma iliyopo, malalamiko yasiyo ya lazima kwenye eneo la utumishi na utawala bora yatapungua kwa kiwango kikubwa. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, mtumishi wa umma anatakiwa kupimwa kwa utendaji kazi wake kwa matokea chanya ili atakapopanda daraja ajivunie utendaji kazi wake na kuongeza kuwa, upimaji huo utapunguza malalamiko ya kutopandishwa madaraja kwa watumishi ambao hawawajibiki ipasavyo. 
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kikao cha menejimenti ya ofisi yake (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.


SERIKALI YATOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI SIMU ZA MKONONI NCHINI

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi ametoa vyeti vya mafunzo ya muda mfupi kwa mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe
“Nawapongeza mafundi simu wa kike watatu kwa kuwa suala la ufundi linachukuliwa kuwa ni la wanaume, naamini ninyi watatu mtakuwa chachu kwa wanawake wengine kujiunga na mafunzo haya,” amesema Dkt. Yonazi wakati akitoa vyeti kwa mafundi simu za mkononi 68 waliohitimu mafunzo hayo ambapo kati yao watatu ni wanawake waliohudhuria mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai mwaka huu. Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa mafundi simu za mkononi kwa kuwa yatawawezesha kulinda usalama wa taarifa, yataleta tija na kuweza kuingiza fedha za kigeni kupitia Sekta ya Mawasiliano. 
Amefafanua kuwa mafunzo hayo yako sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo Serikali imejipanga kutekeleza Ilani hiyo kupitia kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa viwanda ambapo tayari Kampuni ya IPP Touchmate Tanzania Ltd itajenga kiwanda cha simu za mkononi nchini na wako tayari kuwapa ajira wahitimu hao kwa kuwa ni mafundi simu wa kwanza nchini kupata mafunzo hayo rasmi
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kulia) akikabidhi cheti kwa Mwanahamis Abdul Salim aliyehitimu mafunzo ya kutengeneza simu za mkononi kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT). Anayeshuhudia wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi simu za mkononi wa kike watatu (waliosimama) kati ya 68 waliohitimu mafunzo DIT, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara hiyo Mulembwa Munaku na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Patrick Nsimama 
Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na meza kuu na wadau waliohudhuria hafla ya utoaji vyeti na leseni kwa mafundi simu za mkononi wa kwanza waliohitimu mafunzo yao, Taasisi ya DIT, Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo Mulembwa Munaku na wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Taasisi ya DIT, Prof. Patrick Nsimama
Naibu Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mafundi simu za mkononi waliohitimu mafunzo hayo kwenye Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam na baadhi ya wadau wa Sekta hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MAFUNZO YA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI ZA JINSIA DODOMA Inbox

KAMPUNI YA GOOD JOB ENTERTAINMENTS YANDAA SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TARANGIRE

$
0
0
Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

KAMPUNI ya Good Job Entertainments imesema imeona umuhimu wa kutoa fursa kwa Watanzania kuwa na mazoea ya kutembelea utalii wa ndani zikiwamo mbuga za wanyama.

Hivyo kampuni hiyo imeamua kuandaa safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire mkoani Manyara katika msimu huu Sikukuu ya Krismass ambapo Mratibu wa Safari ya keenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Juma Mtetwa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa safari hiyo itaanza Desemba 24 na kurudi Desemba 26 mwaka huu.

Amefafanua lengo la kuandaa safari hiyo ni kuhamasisha na kuuza elimu ya maisha ya wanyamapori na kupata muda wa kumpumzika katika msimu huu wa Sikukuu ya X-Mas huku akisisitiza uamuzi huo pia unalenga kuunga mkono kauli mbili ya kuhamasisha utalii wa ndani vitendo.

"Washiriki wa safari hiyo wanatakiwa kufanya maombi ya ununuzi wa tiketi mapema Good job Entertainment ambapo Bibi na Bwana itakuwa Sh.350,000 na kwa mtu mmoja ni Sh.200,000,"amesema.Kwa upande wake Ofisa Masoko wa Tarangire National Park Gedfrey Mbona amesema kuwa 

Watanzania watumie fursa ya kuhamasika kutembelea utalii wa ndani ambao baada ya hapo watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea utalii wetu kwa wageni wanaotoka nchi mbalimbali kuja nchini."Tarangire ni nyumbani kwa tembo kwani kuna idadi kubwa ya wanyama hao kuliko mbuga zote hapa nchini.Pia kwenye hifadhi zetu tunao Simba, Duma, Chui, Twiga na wengine wanyama wengine wengi.Tumeajindaa vizuri kuwapokea watalii wetu na tunaimani mtakaporudi majumbani mtakuwa wajumbe wazuri kwa wengine,"amesema.

WAZIRI WA KILIMO ASISITIZA MAWAZIRI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUONGEZA MSHIKAMANO SEKTA YA KILIMO

$
0
0

Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo-Arusha

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe Japhet Hasunga amewataka mawaziri wenzake wa sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya katika Uzalishaji wa bidhaa bora za Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo Leo tarehe 7 Disemba 2018 wakati akizungumza mara baada ya kumalizika mkutano wa 12 wa Baraza la kisekta la mawaziri wa Kilimo na usalama wa chakula wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini.

Mhe Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la bidhaa katika jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla.Aidha, amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani kwa kiasi kikubwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mipango hiyo.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati), Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina (Kushoto) na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe Christophe Bazivamo, Waziri anayeshughulikia EAC nchini Burundi Mhe Isabelle Ndahayo, Waziri wa Kilimo nchini Kenya Mhe Mwangi Kiunjuri, Katibu Mkuu wa Kilimo nchini Rwanda Ndg Musabyimana Jean Claude, Waziri wa Kilimo Sudani Kusini Mhe Onyoti Adigo Nyikwec, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Tanzania Mhe Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Kilimo Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb), na Waziri wa Kilimo, Mifugo, Maliasili na Utalii-Zanzibar Mhe Rashid Ally Juma wakiwa katika picha ya pamoja katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha, Leo tarehe 7 Disemba 2018.


MANAIBU MEYA WAWILI KUPEANA ZAMU YA KUONGOZA JIJI LA DAR

$
0
0
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

HATIMAYE Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limeamua kutumia busara kwa kufanya maridhiano ya kupata manaibu meya wawili kwa ajili ya kuongoza Jiji hilo ambapo wamekubaliana kila Naibu Meya ataongoza kwa miezi mitatu.

Hatua hiyo imefikiwa leo na Baraza hilo ambalo lilikutana kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa Naibu Meya lakini yaliibuka malumbano makali kati ya wajumbe wa baraza hilo upande wapinzani dhidi ya CCM.Pia malumbano kati ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salam Spora Liana na upinzani.

Wakati wa malumbano hayo ikafikia hatua baadhi ya wajumbe wakaamua kuweka wazi hawapo tayari kuendelea kulumbana wao kwa wao na kusababisha vinyongo katika kupata Naibu Meya kwani malumbano yanakwamisha maendeleo ya Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakiwamo wabunge na madiwani waliweka wazi idadi ya wapiga kura kwa CCM ni 12 na upinzani ni 12, hivyo watavutana bila sababu ya msingi na kila wanapokutana fedha za umma zinatumika na hakuna muafaka.Hivyo walimua leo iwe iwavyo ni lazima wafanye uchaguzi na Naibu Meya apatikane.

Kutokana na maridhiano hayo wagombea Mariam Rulida ambaye ni Diwani wa Kata ya Mchafukoga kupitia CCM na Alli Mohammed ambaye ni Diwani wa Kata ya Makumbusho kupitia CUF ndio wamepitishwa na baraza hilo kushika nafasi hiyo ya Naibu Meya.Akitangaza uamuzi huo Meya wa Jiji la Dar es Salaam Issaya Mwita amesema wajumbe wa baraza hilo ambalo ndio wapiga kura wamekubaliana Naibu Meya aMariam Rulida aanze kushika nafasi na kwamba ataanza kuitumia kuanzia Desemba 30, 2018 hadi Machi 30 mwaka 2019 na baada ya hapo Naibu Meya mwingine Alli Mohammed atashika nafasi hiyo kuanzia Machi 30 hadi Juni 30 mwaka 2019.

"Tumekubaliana na kuridhia wote kwa pamoja tuwe na manaibu meya wawili na wataongoza kwa zamu nafasi hiyo.Tuanza na Naibu Meya wa CCM na kisha atafuata Naibu Meya kutoka CUF.Tumefanya hivi kwa nia njema na yenye maslahi mapana kwa Jiji la Dar es Salaam.Hatutaki kuendelea kulumbana kila linapofika suala la kuchagua Naibu Meya,"amesema Meya Mwita.
Wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha kujadili uchaguzi wa kumpata Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam. Baraza hilo limekutana leo jijini.

NJOO TUSHEREHEKEE PAMOJA DESEMBA 25 XMAS DAY

$
0
0
Stokhom Sweden karibuni kweny get together party December 25 Xmas day tusherehekee pamoja na familia zetu kwa kiingio cha kr 200 kwa wakubwa, watt weny miaka 13-18 ni 100kr na miaka 6-12 ni kr 50 na chini ya miaka 5 free

Hii itaambana ta na kinywaji kimoja bure na misosi ya kitanzania tutakuwa na buffé ya vyakula vya kitanzania!! Lipia sasa kuweka booking yako na familia tusherekee pamoja!!

@mamambila_openkitchen_sweden👩‍🍳🇸🇪 akishirikiana na Active Chef issa 

Mtawa awataka wauguzi nchini kuzingatia miongozo ya kazi

$
0
0
Wauguzi nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi kwa kufuata miongozo iliyopo ikiwamo taratibu, kanuni na sheria.

Hayo yamesemwa na Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa katika mkutano wa kikao kazi uliowashirikisha wauguzi wakuu wa mikoa ya Tanzania, wauguzi wakuu wa hospitali za rufaa za kitaifa na hospitali maalum, baadhi ya wakuu wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya uuguzi na ukunga pamoja na baadhi ya wauguzi wakuu wa wilaya nchini.

Bi. Mtawa amesema kwamba taaluma ya uuguzi inaongozwa na sheria na kanuni ambazo zimeainisha miongozo jinsi ya kumuwajibisha muuguzi anayekwenda kinyume na taratibu na maadili.“Kutokana na muongozo huu, viongozi wa baraza ngazi ya mikoa, wilaya na vyuo wanapaswa kutimiza wajibu wao katika kusimamia miongozo,” amesisitiza Bi. Mtawa.

Mkurugenzi huyo amewataka wauguzi kuzingatia pia matumizi ya miongozo mipya kama muongozo wa kusimamia utoaji wa huduma ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) uliyoboreshwa yaani NIMART, muongozo wa mafunzo ya kujiendeleza yaani CPD, muongozo wa ufuatiliaji wa huduma za uuguzi na ukunga pamoja na mfumo mpya wa TEHAMA ambao utasaidia kuweka kumbukumbu za huduma zinazotolewa na wauguzi na wakunga kwa kielectroniki.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwaonyesha washiriki sheria na kanuni inayosimamia taaluma ya uuguzi na ukunga nchini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kikao hicho ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa ofisi za baraza hilo, Wilaya ya Kibaha, mkoani Pwani.
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi. Agnes Mtawa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa baraza hilo.

DIAMOND ATUA KIBABE SUMBAWANGA... SHANGWE LA MASHABIKI KAMA LOTEEE

$
0
0
Na Baba Faisal 

SHANGWE za kibabe zimetawala leo katika Mji wa Smbawanga mkoani Rukwa baada ya msanii mwenye nyota yake ya kupendwa na anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa sasa Naseeb Abdull a.k.a Diamond kutua katika mji huo.

Diamond akiwa ameambatana na wasanii wengine kutoka lebo ya WCB wakiwa pamoja na wasanii wengine nchini wametua kwenye mji huo wa Sumbawanga kwa ajili ya kufanya tamasha la Wasafi Festival.Wakati msanii huyo anawasili mashabiki wa muziki wa kizazi kipya waliamua kujitokeza kwa wingi kumpokea.

Hivyo muda wote mashabiki walikuwa wakipaza sauti zao zilizoambatana na shangwe la aina yake wakiimba "Simbaa...Simba...Simba ...Simba..."wakiwa na maana ya kumuita  Diamond ambaye huwa anapenda kujiita Simba.Diamond ameenda Sumbawanga kwa akiwa na ndege ndogo ya kukodi ambapo kabla ya kushuka mshabiki wa burudani waliamua kuizunguka ndege hiyo na kisha wakishangilia kwa sauti ya juu. 

Hata hivyo Diamond alikuwa wa mwisho kushuka ndani ya ndege hiyo ambapo mbali ya shangwe kutawala wapo mashabiki walioona isiwe tabu bwana, hivyo walichukua simu zao na kisha kuanza kupiga selfie.Baada ya kutua kwenye mji huo kikubwa ambacho mashabiki wa burudani wanakisubiri ni kumuona Diamond akiwa jukwaani akiwapagawisha kwa nyimbo zake mbalimbali.

Michuzi TV: Taasisi ya PLPDF yaadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani...

MICHUZI TV: DUDU BAYA AZUNGUMZIA WASAFI FESTIVAL

MICHUZI TV: LAVALAVA afunguka rasmi kuacha mziki kulizwa kisa mapenzi,amehamia kwenye mziki wa burudani.

MICHUZI TV: Mpenzi wa MONI CENTROZONE, NAI afunguka haya usiku wa WOLPER

MICHUZI TV: SHILOLE afunguka mazito ya CHID BENZ kudhalilishwa hadharani


MICHUZI TV: ALICHOZUNGUMZA RAIS MAGUFULI NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, APSON MWANG'ONDA

Harusi Ya Mwandishi wa Shirika la Reli Ben Mwanantala alivyoungwa Mkono na Wafanyakazi wenzake..

ITV: TAARIFA YA HABARI SAA MBILI KAMILI USIKU DESEMBA 7, 2018

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha

$
0
0

NA WAMJW, DAR ES SALAAM

WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao Milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza Kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha (Ngirimaji) pamoja na minyoo ya tumbo, kuanzia Disemba 15 hadi 20, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD), Dkt. Upendo Mwingira wakati wa Warsha ya Wanahabari kuhusu magonjwa hayo hapa nchini.

Dkt. Upendo Mwingira amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwani kingatiba hiyo itatolewa bila malipo katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam.“Hii sio chanjo. Ni kijngatiba na zoezi hili linaenda kumkinga mtu dhidi ya magonjwa ya mabusha na matende pamoja na minyoo na itatolewa kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea” Amasema Dkt.Upendo Mwingira.

Ameongeza kuwa, “Wananchi watakaojitokeza watamezeshwa kingatiba hizo papohapo na zoezi hili utolewa kila mwaka mara moja” amebainisha.
Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni pamoja na Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha (Ngirimaji), na Minyoo ya tumbo.

Zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali, maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.
Mratibu wa Haifa wa Mpan go wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Dkt.Upendo Mwingira akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi la umezeshaji wa Kinga Tiba za matende na mabusha(ngirimaji ) kwenye warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika ofisi ndogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Afisa Mpango Oscar Kaitaba akiwaonesha Kinga tiba hizo waandishi wa habari(hawapo pichani).Zoezi la umezeshaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam linalotarajiwa kuanza disemba 15 hadi 20 mwaka huu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali ,Wziara ya Afya Catherine Sungura akiongea na waandishi wa Habari wakati ya warsha hiyo kulia ni afisa Mawasiliano kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Said Makora Waandishi wa Habari walioshiri warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wandishi wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Waandiahinwa Habari walioshiri warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images