Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live

MNZAVA: WAKULIMA,WAFUGAJI ONDOENI UBINAFSI

$
0
0


MBUNGE wa korogwe vijijini Mh Timotheo Mnzava amewataka wananchi jamii ya wafugaji na wakulima waishio katika kata ya Mkalamo na Magamba Kwalukonge kumaliza tofauti zao na kuachana na ugomvi baina yao na malumbano yasio na tija ili kuleta maendeleo ya kata zao na Korogwe na taifa kwa ujumla. 

Ameyazungumza hayo leo katika mikutano yake na wananchi hao alipotembelea katika kata hizo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukutana na wananchi ambapo lengo kuu ni kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo. 

Mnzava amezitaka jamii zote mbili za wafugaji na wakulima kuondoa ubinafsi katika mioyo yao na kwa pamoja wawe na upendo baina yao na kuishi kindugu ili kulinda amani ambayo ni tunu kwa taifa la Tanzania. 

“Natambua changamoto yetu ya Ardhi, na naamini hata siku moja hatuwezi kufuta mashamba yote, kwasababu uwekezaji pia tunauhitaji lakini uwekezaji wenye tija, lakini hata ikitokea siku moja mashamba yote tukapewa kama hatuna matumizi bora ya ardhi, kama hatutaacha ubinafsi na kuchukiana, mgogoro wa wakulima na wafugaji hauwezi kwisha. Tupendane, tuishi kama ndugu na kuheshimu shughuli za wenzetu”. Alisema Mnzava 

Mnzava amewaahidi wananchi hao kuendelea kuwasemea juu ya tatizo la uhaba wa Ardhi na amewaomba wavute subira kwani serikali ya Rais Magufuli inalifahamu tatizo hilo na kwakuwa Rais anawajali watu wake litapata suluhisho.

KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

$
0
0
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametaka kero ya maji kwa wakazi wa Mtoni itatuliwe haraka iwezekanavyo mara baada kujionea hali huduma ya maji kwa wananchi. 

Amezungumza hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kusiskiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam, na kuitaka DAWASA itafute suluhisho la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ukizingatia uwepo wa chanzo cha maji na mtambo wa kusafishia maji katika eneo la Mtoni.

Profesa Mbarawa amesema haoni sababu ya wananchi hao kukosa maji kwa kuwa kuna chanzo cha maji cha uhakika, kinachohitajika ni kuweka mkakati mzuri wa ujenzi wa miundombinu itakayofikisha maji kwa wananchi kwa kuwa chanzo kipo. Akiwa kwenye Mtaa wa Mashine ya Maji, Profesa Mbarawa amekutana na kero ya maji kutoka kwa wananchi ambao wamesema maji wanayotumia yanayotoka kwenye kisima usalama wake ni mdogo, kumuomba Waziri wa Maji awatatulie changamoto hiyo.

Aidha, wamemuomba Waziri wa Maji aipatie ufumbuzi changamoto ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Temeke kilichokuwa kikitumika awali kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi kuhodhiwa na mtu binafsi wakati wao wakiwa na uhitaji mkubwa wa maji. Akijibu hoja za wananchi hao Profesa Mbarawa amesema atatuma timu ya wataalamu wa DAWASA ifike eneo hilo Jumatatu ijayo, ili waweze kufuatilia jambo hilo kabla ya kuchukua hatua zinazostahili. Pia, waangalie namna jinsi watakavyoweza kufanikisha zoezi la kufikisha huduma ya maji kwa wakazi hao.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku tano katika Jiji la Dar es Salaam; ambapo ametembelea maeneo yenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ya Kimara, Bonyokwa, Salasala na Mtoni kusikiliza kero za wananchi ambazo amekuwa akizisikia kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi. Pamoja na Kiwalani ambapo alikwenda kupata mrejesho kutoka wa wananchi kuhusu maendeleo ya Mradi wa Maji Kiwalani uliozinduliwa hivi karibuni.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akijibu hoja za wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao eneo la Mtoni, katika Wilaya ya Temeke. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Mtoni, Wilaya ya Temeke wakati akielezea kero yake kuhusu maji. 


Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Mtambo wa Maji Mtoni, Mhandisi Deusdedit Rwegasila alipokuwa ziarani katika eneo la Mtoni, wilayani Temeke. 
Fundi Sanifu Mwandamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Robert Chenge akitoa maelezo kuhusu hali ya huduma ya maji kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa eneo la Mtoni.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo yaanza maandalizi ya ujenzi wa ofisi Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

$
0
0

PIX 1
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarish ambaye ndio mratibu wa ujenzi wa Mji wa Serikali akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo leo Jijini Dodoma mara baada kukagua eneo la Wizara hiyo ambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara hiyo Bw.Nicholaus William.
PIX 2
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mhandisi Hagai Mziray kutoka Kampuni ya Mzinga Cooperation ya mkoani Morogoro anayejenga Ofisi za Wizara hiyo wakati alipokagua eneo hilo ambalo limefanyiwa usafi tayari kwa  kuanza ujenzi wa ofisi leo Jijini Dodoma.Weingine ni baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo.
PIX 6
Eneo linapojegwa ofisi za Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo katika mji wa Serikali Jijini Dodoma linavyoonekana baada ya kufanyiwa  usafi.(Picha na Shamimu Nyaki –WHUSM)

MICHUZI TV: SHUHUDIA TUKIO LA MTOTO ALIYEVUNJIKA UTI WA MGONGO JIJINI MBEYA

MWANAMKE APAMBANA NA JAMBAZI MWENYE SILAHA AKIMUOKOA MUMEWE,

$
0
0
Na Felix Mwagara, (MOHA) MARA. 

Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Kata ya Nyamihyolo, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Busimba Malegesi amemuokoa mumewe asiuawe na jambazi mwenye silaha ambaye alivamia katika nyumba yao na kuanza kumshambulia mwanaume huyo kwa kumkatakata mapanga mwili mzima.

Busimba alimrukia jambazi huyo kiunoni na kumuangusha chini na kufanikiwa kumnyang’anya panga pamoja na tochi ambazo alikua nayo wakati anamshambulia mumewe aitwaye Samson Malegesi (62).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 7:30 usiku wa kuamkia Ijumaa wakati familia hiyo ikiwa imelala ndipo jambazi huyo alivunja mlango na kuingia moja kwa moja chumbani kwa wanandoa hao na kuwasha tochi kumsaka Malegesi na baada ya kufanikiwa kumuona alianza kumshambulia kwa kumpiga mapanga kichwani, mikononi, kwenye mbavu na kusababisha damu nyingi kumwagika.

Wakati jambazi hilo akiendelea kumshambulia Malegesi, mkewe alikua naye anapambana kwa kumzuia asimshambulie mumewe, lakini jambazi hilo lilizidiwa baada ya mwanamke huyo kupata nguvu zaidi na kufanikiwa kumuangusha chini na kuhakikisha silaha aliyoishika mkononi akinyang’anywa kwa urahisi kutokana na kubanwa kwa juu na mwanamke huyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo, Busimba Malegesi (katikati), alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Mgonjwa huyo amelazwa katika Hospitali ya Kibara, Wilayani humo akiendelea kupewa matibabu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimwangalia mgonjwa ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mahyolo, Wilayani Bunda, Samson Malegesi aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Muuguzi wa hospitali ya Kibara, Godliver Josephat, ambapo mhonjwa huyo amelazwa akipatiwa matibabu. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akiingia Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiondoka Hospitali ya Kibara Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, mara baada ya kumwangalia mgonjwa aliyevamiwa na jambazi na kukatwakatwa mapanga mwili nzima, jana. Hata hivyo, Mke wa mgonjwa huyo alifanikiwa kumuokoa mumewe kwa kumnyang’anya silaha jambazi hilo. Kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibara, Wilayani humo, Mkaguzi Boniface Mwalupale.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

TUMEANZISHA BENKI YA KILIMO ILI KUTOA MITAJI KWA WAKULIMA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania kwa lengo la kuwasaidia wakulima wapate mitaji ili waongeze tija.

Pia amewataka wakuu wa wilaya za Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro wahahakikishe wanawahamasisha wananchi katika maeneo yao kuchangamkia fursa ya kilimo cha miwa.Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipotembelea shama la miwa Mkulazi na MbIgiri mkoani Morogoro alipokuwa njiani kwenda jijini Dodoma.

Alisema lengo la kuanzishwa shamba la mwa la Mkulazi ni katika jitihada za Serikali za kuhakikisha mahitaji ya sukari nchini yanafikikia katika kiwango kinachohitajika.Waziri Mkuu alisema Serikali imepanga kuzalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na njia pekee ni kuboresha kilimo cha miwa, kujenga viwanda vitakavyozalisha sukari ya kutosha.

Alisema shamba hilo linaendeshwa kwa ubia kati ya NSSF na Jeshi la Magereza, hivyo, aliiagiza Menejimenti mpya ya Mkulazi kuhakikisha shamba hilo linasimamiwa kikamilifu.Waziri Mkuu pia, alimuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike apeleke wataalamu wengi wa kilimo katika shamba hilo ili wasaidie kusimamia kitaalamu.

“Nataka shamba hili lisimamiwe kitaalamu, uzalishaji uwe wa kitaalamu na liwe mfano na mashamba mengine, tusishindwe na watu binafsi,” alisema.Kuhusu suala la maji hususan kipindi cha mvua ambayo huaribu shamba, Waziri Mkuu aliwataka watafute namna nzuri ya kuyahifadhi ili wayatumie kipindi cha kiangazi.


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama (kulia)  wakati alipowasili kwenye shamba la miwa la Mkulazi na Mbigiri mkoani Morogoro,
PMO_1450
          Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembalea shamba la miwa la Mkulazi na Mbigiri mkoani Morogoro, Desemba 7, 2018. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stevene Kebwe.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


TAZAMA LIVE MISS WORLD 2018 KUTOKA SANYA, NCHINI CHINA

URASIMISHAJI BANDARI BUBU KUINGOZEA TPA MAPATO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, amesema mpango wa kufufua bandari bubu ambazo zipo zaidi ya 250 nchi nzima utaongeza mapato ya mamlaka kwa kiasi kikubwa sambamba na kudhibiti bidhaa za magendo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam Kakoko alisema jumla ya mapato ya bandari hizo yanakadiriwa kuweza kufikia theluthi moja au nusu ya mapato ya Bandari ya Dar es Salaam.

Bandari ya Dar es Salaam ambayo imefikia kuhudumia shehena za tani milioni 16.2 kwa mwaka inaingiza Sh bilioni 70 kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za TPA za mwaka 2017.

Kakoko alisema zipo hatua kadhaa zinazochukuliwa katika mpango wa kufufua bandari bubu ikiwemo kuzianisha, kuwashirikisha wadau, kuzifanyia tathmini, kuandika ripoti ya kuanisha bandari zenye sifa za kuweza kufufuliwa na kisha kuipeleka kwa wizara husika kwaajili ya mapitio na kupitishwa.Alisema kwa sasa zoezi la kuzitambua na kuzianisha zinaendelea na kwamba zoezi hilo linatarajia kukamika mwezi huu, "tunatarajia zoezi likikamilika tunaweza kupata bandari bubu zaidi ya 300."

"Tayari tumeshafanya vikao na wakuu wote wa mikoa na wilaya ambazo zina bandari bubu na nusu ya viongozi wote wa vijiji na kata katika maeneo hayo tayari tumeshazungumza nao na zoezi hilo linaendelea," alisema Kakoko.

Alisema ushirikishwaji huo wa wadau umefanyika ili kupata ushirikiano katika utekelezaji wa usimamizi wa bandari hizo pindi zitakaporasimishwa na kutopata mapingamizi.Kuhusu gharama za kuendesha bandari hizo pindi zitakaporasimishwa alisema kwa kiasi kikubwa hazihitaji gharama kubwa kwani zitakodishwa kwa halmashauri, vijiji au watu binafsi ili kuziendesha na kukusanya mapato kwa niaba ya TPA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya urasimishaji wa bandari Bubu na Umuhimu wake katika kukuza pato la Taifa.
Waandishi wa Habari kutoka Vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Deusdedith Kakoko .



WAJUMBE ALAT SHINYANGA WATEMBELEA ILEMELA,SENGEREMA KUPIGWA MSASA

$
0
0

Na Robert Hokororo

Wajumbe wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Shinyanga wamefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Wilaya ya Sengerema jijini Mwanza kujifunza namna ilivyofanikiwa katika miradi ya maendeleo.

Miradi iliyotembelewa na wajumbe hao ni pamoja na urasimishaji na upimaji wa ardhi manispaa ya Ilemela pamoja na mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema. Ziara hiyo ilihusisha wajumbe wa ALAT kutoka Halmashauri za Wilaya za Kishapu, Ushetu Msalala, Shinyanga, Mji wa Kahama na Manispaa ya Shinyanga pamoja na baadhi ya wataalamu wake.

Katika kikao kilichowakutanisha wataalamu wa Ardhi na ujumbe huo kutoka mkoani Shinyanga walipata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara hiyo ambazo zimesaidia kutatua migogoro ya ardhi. Akielezea kuhusu miradi hiyo, Afisa Mipango Miji Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisema katika mwaka uliopita walipanga kupima viwanja 16,000 na hadi sasa wamepima 33,200 huku matarajio ni kufikia 52,000.

Wajumbe wa ALAT wakipata ufahamu wa namna maji ya Ziwa Victoria yanavyovutwa na kusafishwa kasha kusambazwa kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema. 
Wajumbe wa ALAT wakiwa katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema. 
Wajumbe wa ALAT waendelea kupata elimu katika mtambo wa kusafisha maji kabla ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema. 
Wajumbe wa ALAT wakipanda tangi la kuhifadhi na kusambaza maji ya Ziwa Victoria walipotela ya kusambaza kwa wananchi walipfanya zaiara wilayani Sengerema. 


TAARIFA KUTOKA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ)

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa kesho tarehe 09 Desemba, 2018litaadhimisha Sikukuu ya miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya shughuli mbalimbali na kutoa huduma za Kijamii kwa Wananchi.

JWTZ litatoa huduma za tiba kwa kuwapima Wananchi magonjwa mbalimbali bila malipo.  Zoezi hilo la tiba litafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kesho Jumapili tarehe 09 Desemba 2018 kuanzia saa mbili (2.00) Asubuhi hadi saa nane (8.00) Mchana.

Wananchi wanataarifiwa kujitokeza ili kupima afya zao. Huduma za tiba zitakazotolewa ni pamoja na Ushauri Nasaha na Upimaji wa Virusi vya Ukimwi, Huduma za Mama na Mtoto, Upimaji wa Uzito, Shinikizo la Damu na Kisukari, Afya ya Kinywa na Meno pamoja na Uchangiaji wa Damu Salama.
 Aidha, kutakuwepo na “Press Conference” na Waandishi wa Habari katika viwanja hivyo kesho saa 4:00 Asubuhi.JWTZ linakialika chombo chako cha habari wakati wa “Press Conference” hiyo.

WANANCHI WA KIJIJI CHA NDUNYUNGU WILAYANI LIWALE WASIMAMISHA MSAFARA WA AWESO; WATAKA MRADI UKAMILIKE HARAKA

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha Ndunyungu kilichopo Wilayani Liwale Mkoani Lindi wamelazimika kusimamisha msafara wa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokuwa njiani kwenda kukagua mradi wa maji wa Barikiwa Wilayani humo. 

Wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wa kumtaka Nambu Waziri awasaidie kupata maji, pia walieleza adha inayowakumba ya kusubiria maji kwa muda mrefu katika eneo wanalochetea maji jambo ambalo linawasababishia kuchelewa kufanya shughuli za kimaendeleo. 

Baada ya kuwasikiliza kero zao Mheshimiwa Aweso alilazimika kwenda kuona chanzo pekee ambacho wananchi hao wanapata huduma ya maji, ambapo alijionea kisima kinachotumia pampu ya kusukuma kwa mkono na kuongea na wananchi walijitokeza kwa wingi. 

Naibu Waziri Aweso alisema kuwa tayari mkandari anayejenga mradi kwa ajili ya kijiji hicho ameshalipwa pesa kiasi cha shilingi milioni mia moja na moja, hivyo hana sababu za kutokukamilisha mradi na kutokulipa vibarua waliochimba mitaro ya kufukia mabomba ya maji. 

Aidha, akiwa katika kijiji cha Barikiwa swala la kutokulipwa kwa vibarua waliojenga mradi pia liliibuka jambo ambalo lilimlazimu Naibu Waziri kumsimamisha Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Liwale kujibu hoja za wananchi. 

Mheshimiwa Aweso alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Liwale awasimamie wananchi hao walipwe kabla ya mwisho wa wiki ijayo. Naibu Waziri bado yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi kwa kukagua miradi ya maji.
Naibu Waziri wa maji Juma Aweso akipampua maji katika kijiji cha Ndunyungu Liwale 
Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso akiwahutubia wananchi wa Barikiwa wilayani Liwale 

KOROSHO ZOTE ZITABANGULIWA NCHINI – WAZIRI WA KILIMO

$
0
0

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo- Mtwara

Serikali imeagiza korosho zote inazonunua kwa wakulima kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko kuanza kubanguliwa nchini.

Agizo hilo la serikali limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 8 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho kwenye ukumbi wa mikutano kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Hasunga alisema kuwa Mkakati wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli ni kuwanufaisha wakulima nchini hivyo maamuzi ya kununua korosho ni sehemu ya maamuzi mema kwa manufaa ya wakulima wote.

Alisema wakati serikali inaendelea kukamilisha uhakiki wa wakulima wa korosho pamoja na kuendelea na malipo ya wakulima mpaka hivi sasa tayari wakulima 77,380 wamekwishalipwa hivyo hakuna korosho itakayoruhusiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi bila utaratibu maalumu badala yake korosho zote zitabanguliwa nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Kushoto ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akijadili jambo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) wakati wa Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Joseph Kakunda (Mb) akizungumza kwenye Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018. 
Kushoto ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof Joseph Buchweshaija na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakifatilia Mkutano wa wamiliki wa viwanda vya kubangua korosho katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara leo tarehe 8 Disemba 2018

Uhamiaji wameaza kutoa viza na vibali vya Kielektroniki

$
0
0

Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Idara ya uhamiaji imeanza kutoa visa na vibali vya ukazi vya kiletroniki ili kurahisha upatikanaji wa viza kwa watalipa na vibali ya ukazi kwa wageni wanaokuja Tanzania kwa madhumuni mbalimbali.
Hayo ameyasema Mtendaji wa Idara ya Uhamiaji Mrakibu wa Uhamiaji Ally Mtanda  katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwandani yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Amesema  kuwa utoaji wa viza na vibali vya ukazi kutarahisha uingiaji kwa wageni na watalii kwani wageni watakapofika kituo cha kuingia na kutoka nchini wataonyesha taarifa ya viza walizopewa kupitia barua Pepe zao kwa uhakiki na kisha kuruhusiwa kuingia nchini hii ni tofauti ya mfumo wa sasa kwa mteja kukaa foleni kwa ajili ya kulipia viza kupitia benki na foleni nyingine kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuingia nchini.Mtanda amesema mfumo huo ni pamoja na kuimarisha usalama kwa unatunza kumbukumbu kwa wageni na matukio mbalimbali.

Aidha katika utaratibu huo itaondoa usumbufu wageni katika vituo vya kuingia nchini na kuikoa gharama zisizo za ulazima kwani kwa kuwa idara itakuwa na taarifa sahihi za wageni kabla hawajawasili nchini.Mfumo utarahisisha ukusanyaji wa maduhuli ya serikali. Tangu kuzinduliwa kwa mfumo wa viza tayari maombi ya waliopewa viza wageni 140 ambapo Tanzania Bara 89 Zanzibar 40.

41 wamewasilisha maombi hayo katika ofisi mbalimbali za uhamiaji ambapo vibali hivyo vinafanyiwa kazi.Waliomba vibali katika za Uhamiaji Makao Mkuu 32,  Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC) Watano, pamoja na EPZA watano. Tangu  kuanzishwa kwa mfumo wa hati ya Kusafiria Kieletroniki jumla ya passport 55078 zimetolewa hadi kufikia Novemba.

Afisa wa Passport Vedasto Rweikiza akimuhudumia mwananchi katika maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Maafisa wa Idara wakitoa huduma katika Maonesho ya Tatu ya Bidhaa za Viwanda Tanzania yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AKAGUA MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD KARIAKOO

$
0
0
Na Veronica Kazimoto

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, amefanya ziara ya kushtukiza katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara hiyo katika maduka mbalimbali, Naibu Waziri huyo amesema kuwa, bado kuna wafanyabiashara ambao hawatoi risiti za EFD na wengine hawatumii kabisa mashine hizo.

“Nimekuwa nikifanya uchunguzi wangu binafsi na wa kiofisi kujiridhisha kama wafanyabiashara wanatoa risiti za kieletroniki na nilichobaini ni kwamba bado kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao hawatoi risiti na wananchi wengi hawaombi risiti za EFD,” alisema Dk. Ashatu.

Dk. Ashatu amebainisha kuwa, alifanya uchunguzi binafsi ambapo alikwenda kama mnunuzi na alipoomba risiti za EFD aliambiwa mashine za kutolea risiti hizo ni mbovu na kupewa risiti za kawaida.Miongoni mwa wafanyabiashara waliotembelewa na Naibu Waziri huyo ni Faridi Mohamed ambaye ni muuzaji wa Vifaa vya Michezo katika Mtaa wa Lindi eneo la Kariakoo aliyemuuzia Dk. Ashatu bidhaa mbalimbali na kumpatia risiti isiyo ya kielektroni na alipoulizwa alidai kuwa mashine ni mbovu.

Dk. Ashatu hakuridhishwa na majibu hayo na kuamua kufanya ziara kukagua maduka yaliyopo katika maeneo hayo ambapo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutoa risiti kila wanapouza bidhaa na huduma mbalimbali na wananchi kudai risiti kila wanapofanya manunuzi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kulia) akizungumza na wauzaji wa Duka la Vifaa vya Michezo lililopo Mtaa wa lindi – Kariakoo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kulia) akikagua Kitabu cha Risiti za Kawaida katika moja ya Maduka ya Vifaa vya Michezo lililopo Mtaa wa lindi – Kariakoo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua matumizi ya Mashine za Kielektroniki za EFD. 
Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Abdul Mapembe (wa kwanza kulia) akiwasiliana na Kampuni ya Paragon ambayo ni moja ya mawakala wa Mashine za EFD. 

MICHUZI TV: TANZANIA YAPONGEZWA KWA UKUAJI UCHUMI WA KASI AFRIKA


WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MRADI WA VIOSKI TEMBEZI JIJINI DODOMA

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amezindua mradi wa vioski tembezi wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC).

Akizungumza leo Disemba 8, 2018 Waziri Mhagama amesema kuwa mradi huo utasaidia wajasiriamali wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kuweza kujiajiri na kupata kipato kitakacho wanufaisha kiuchumi.“Hii ni faraja kubwa kwetu kama Serikali kuona mnaunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za ajira nchini kwa kuwawezesha wajasiriamali kuchangamkia fursa za kujiendeleza kibiashara”, alisema Mhagama.

Aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau na kuwataka wawekezaji wengine waweze kubuni miradi kama hiyo yenye manufaa kwa wananchi.Aidha, Mhe. Mhagama aliipongeza kampuni ya Sigara Tanzania kwa ubunifu na kuwasihi waendelee kufanya vizuri katika nyanja nyingine kwa manufaa ya watanzania kwa ujumla.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa ni jambo la faraja mradi huo umezinduliwa Jijini Dodoma ikiwa ni fursa kubwa kwa wajasiriamali kuweza kunufaika kiuchumi.

Naye, Mkurugenzi wa Masoko, Bi. Awaichi Mawalla amesema kuwa Vioski 400 vitagawiwa nchi nzima kwa wajasiriamali wadogo ambao wamekuwa wakifanya kazi na kampuni ya TCC na wataweza kuuza bidhaa mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo wa vioski wa kampuni ya Sigara Tanzania (TCC). (Kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na Naibu Waziri Mhe. Anthony Mavunde (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi (kushoto) wakimsikiliza Fundi Mkuu wa Vifaa Saidizi kwa Watu wenye Ulemavu Bw. Mwita Marwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughilikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Viungo Dodoma, Bw. Hassan Hussein.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali walioweza kunufaika na mradi huo, mara baada ya uzinduzi wa hafla hiyo iliyofanyika Jijini Dodoma, Disemba 8, 2018.





UJENZI WA GATI NYAMISATI WAANZA, SHEHENA YA VIFAA YAANZA KUWASILI -KUANDIKWA

$
0
0













NA MWAMVUA MWINYI, KIBITI 

NAIBU waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa amesema ujenzi wa gati, uliokuwa ukisubiriwa kwa kipindi kirefu na wakazi wa Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani umeanza ambapo shehena ya vifaa vya ujenzi vimeanza kuwasili tayari kwa ajili ya kazi. 

Aidha amewatoa wasiwasi wakazi wa Mafia kuhusu gati la Kilindoni ,kwamba linatarajiwa kuboreshwa kwa kuondoa dosari ndogondogo zilizopo ili liwe la kisasa. 

Akizungumza na wananchi wakati alipotembelea eneo litakapojengwa gati hilo, katika muendelezo wa ziara yake mkoani hapo, Kuandikwa alisema ujenzi utakuwa wa miaka miwili kwa gharama ya sh. bilioni 14 .

Alimtaka , mkandarasi wa gati hilo kufanya kazi inayotakiwa kwa kuhakikisha, ujenzi unakamilika kwa wakati ikiwezekana kuukamilisha kabla ya miezi 24.
Kuandikwa alisema, ujenzi umeshaanza na mkataba ulisainiwa tarehe 24,octoba mwaka huu, ombi lake ni kuona mkandarasi anamaliza kazi haraka.
“Fedha zipo hatutaki kuona mkandarasi anasuasua, gati litasaidia kurahisisha usafiri kwani ndio kiu ya wakazi wa Nyamisati na Mafia”
“Itakuwa gati la kisasa na sasa tunakwenda kufanya maboresho katika gati la Kilindoni wilayani Mafia ili kuwa na gati la uhakika ,kwa kuwa itazingatia ubora, teknolojia mpya kwa lengo la magati haya yaweze kudumu kwa miaka mingi “alisisitiza Kuandikwa. 

Pamoja na hayo, alielezea ujenzi huo utakwenda pamoja na maboresho ya barabara ya Bungu -Nyamisati itakayosaidia kurahisisha usafiri .
Akiwa barabara ya barabara ya Mkuranga -Kisiju kiwango cha lami, yenye urefu wa 1.8km alimpongeza meneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Pwani, Yudas Msangi kwa kubana matumizi kwenye miradi na kuweza kutumia katika miradi mingine. 


Msangi alisema kwasasa wanaendelea na kazi za kufungua na kuboresha baadhi ya barabara muhimu kuelekea katika miradi mikubwa mbalimbali.

MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZA NA NDUGU BASHIRU ,AMTAKA ASONGE MBELE KUREJESHA CHAMA KWENYE MISINGI

$
0
0
Mjane wa Mwalimu Nyerere Mwenyekiti wa Kwanza wa CCM na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mama Maria Nyerere amekutana na kuwa na mazungumzo na Ndugu Bashiru Ally Kakurwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mama Maria ametumia mkutano huu kumpongeza Ndugu Katibu Mkuu kwa juhudi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya za kumsaidia Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukirejesha Chama na Serikali kwenye misingi ambayo baba wa Taifa aliisimamia.

Mama Maria kwa umahususi na kwa kupitia kwa Ndugu Bashiru amempongeza Ndugu Magufuli kwa kazi nzuri ya ujenzi wa vituo vya afya zaidi ya 200 kote nchini Tanzania ndani ya kipindi kifupi cha miaka miwili, vituo ambayo vina huduma ya afya timilifu (comprehensive health care). Mama Maria ameeleza vituo hivi vitakuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma za afya hasa kwa mama, watoto na wazee. Katika Mkutano huo Mama Maria ametoa wito kwa CCM kuendelea kuisimamia Serikali na kuimarisha lishe bora kwa watoto, watu wazima na umma ili kujenga Taifa imara na la watu wenye nguvu ya kuendelea kuchapa kazi sambamba na kauli mbiu ya Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu!
Akipokea pongezi hizo Ndugu Bashiru Ally, amemshukuru Mama Maria kwa kuendelea kutujali, kutukumbusha, kutushauri na kutuombea kila anapopata nafasi. Ndugu Bashiru amemjulisha Mama Maria kwamba tarehe 17 na 18 Desemba kutafanyika vikao vya Uongozi vya Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Halmashauri Kuu ya Taifa ambapo serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zitatoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa Mwaka 2015 – 2020.

Huu ni muendelezo wa ziara na mazungumzo ya Ndugu Bashiru Ally na viongozi, makada na wanachama wa CCM ili kupokea ushauri, kubadilishana nao uelewa, mipango, mikakati na taarifa za ujenzi wa Chama.

NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

$
0
0

LUSUNGU HELELA-GEITA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesali katika Kanisa la Wasabato la Geita Kati mkoani Geita ambako ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.

Lengo la kuendesha harambee hiyo ni kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazotumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kanisa la Wasabato kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo kitakachosaidia kuihudumia jamii.

Katika harambee hiyo Naibu Waziri Mhe. Kanyasu aliambatana na wadau wake ambapo kwa pamoja waliweza kukabidhi Sh15 milioni zikiwa ni fedha taslimu kama mchango wao.Katika harambee hiyo, ahadi mbali mbali zimeweza kutolewa ikiwemo matofali, saruji pamoja na malori ya mchanga na mawe.

Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuwa na mpango huo wa kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa jamii ambayo kimsingi ni kazi ya Serikali,”Suala la kujenga vituo vya afya ni jukumu la serikali lakini ninyi mmeamua kuisaidia serikali nawapongezeni sana na msisite kunishirikisha kwa lolote.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita

Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa  kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa waumini waliojumuika katika ibada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita. 


MBUNGE MAVUNDE AZINDUA TAASISI YA WASANII DODOMA,AKABIDHI OFISI NA STUDIO

$
0
0
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde jana amezindua rasmi Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma.

Uzinduzi huo umefanyika jana katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road,Dodoma kwa kujumuisha wasanii wa ndani na nje ya Dodoma.Ofisi hizo na studio.Zitatumiwa na Wasanii wote kupitia umoja wa na Vilabu vya wasanii.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge Mavunde amewataka wasanii wa Dodoma kuwa na UPENDO,MSHIKAMANO na UMOJA ili kufikia mafanikio na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanafika mafanikio ya juu katika sanaa.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Patrobas Katambi amempongeza Mbunge Mavunde kwa namna anavyowatumikia wana DODOMA na kuahidi kushirikiana nae kuwasaidia Vijana wakiwemo wasanii ili wapige hatua zaidi katika mafanikio ya kwenye sanaa.
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road.
Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini,Mh Anthony Mavunde pamoja na MKuuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi wakiwa samamba na baadhi ya wasanii waliokuwa wakitumbuiza jukwaani wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kupiga ngoma kwenye moja ya kikundi cha ngoma za asili kwenye hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
Mbunge Wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde akishiriki kucheza muziki jukwaani sambamba na baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya katika hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Wasanii Dodoma na kukabidhi ofisi na studio kwa wasanii wa Dodoma,hafla hiyo ilifanyika katika katika eneo la Mapinduzi Club-Bahi Road
Viewing all 110002 articles
Browse latest View live




Latest Images