Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

Vifo vya akina Mama na Watoto bado changamoto

$
0
0
Takwimu zinaonyesha vifo vya kina mama na watoto  bado ni Changamoto hapa nchini ambapo   kina mama 556 kati ya laki moja hufariki Dunia wakati wa kujifungua. Akizungumza Jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya afya unahusu Afya ya Mama na mtoto  Mkuu wa Chuo Cha Udaktari bingwa Cha Aga Khan Prof. Hussein Kidanto amese kuwa tatizo lipo Duniani kote ambapo zaidi ya kina mama 303 kati ya laki moja wanaozaa watoto hai hufariki Dunia.

Aidha ameongeza kuwa mimba za utotoni zimeonekana kuwa Sababu kubwa ya vifo hivyo ambapo asilimia 27 ya watoto wa kike wenye umri miaka 14_16 hupata mimba za utotoni na wengine tayari wanawatoto. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ahmed Makuwani amesekuwa Serikali imefanikiwa kufanya ukarabati wa vituo vya Afya hapa nchini ili kuboresha huduma ya Afya ya mama na Mtoto.

Dkt. Makuwani ameongeza kuwa vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 54 katika vizazi hai elfu moja huku kwa zaidi ya miaka 10 vifo vya kina mama vikibaki kuwa palepale ambapo ni kati ya kina mama 400 hadi 600 hupoteza maisha. Naye Mkurugenzi wa wauguzi toka Hospitali ya Aga Khan Lucy Hwai amewataka madaktari na wauguzi kwenda vijijini kukidhi mahitaji ya afya kwa akina mama na watoto ambao wanachangamoto ya upatikanaji wa huduma za kiafya.
 Wadau wa Afya ya uzazi wakiwa katika mkutano wa siku mbili ilioandaliwa na na Chuo cha Udaktari Bingwa cha Aga Khan Uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Ahmad Makuwani akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Serikali ilivyochukua hatua katika utoaji wa huduma za Afya kwa Mama na Mtoto
 Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali Lucy Kwai akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Afya ya Uzazi kwa wanawake wa Tanzania katika mkutano unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Udaktari Bingwa Aga Khan Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Chuo hicho kuandaa mkutano katika kukabiliana na changamoto ya Afya Uzazi ya Mama na Mtoto Uliofanyika jijini Dar es Salaam

Dkt. Ulisubisya azindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa huduma za afya nchini

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akiongea na wanahabari baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akikagua mabanda ya washirika akiongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed  baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akikagua mabanda ya washirika akiongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed  baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akikagua mabanda ya washirika akiongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed  baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akikagua mabanda ya washirika akiongozana na Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed  baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018
Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed  pamoja na washirika baada ya kuzindua Mkutano wa Kutoa matokeo ya mpango mkakati wa uboreshaji wa  huduma bora za afya nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Desemba 7, 2018. Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa. Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma. Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.

Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika. Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaresti Ndikilo akizungumza  kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  ili azungumze  wakati Waziri Mkuu alipotembelea kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018.
Wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra Cashew cha Kibaha kwa Mathias wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Meneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Korosho cha Terra Cashew, Leonardo Denti  (wapili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Kibaha kwa Mathias, Desemba 7, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO APOKEA MSAADA WA MBOLEA TOKA GSM TANZANIA

$
0
0
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Onesmo Buswelu(kushoto)ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha,akipokea msaada wa mifuko 70 ya Mbolea aina ya Urea kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo,Msaada huo umetolewa na GSM Tanzania na kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Group,Matina Nkurlu(kulia)anaeshuhudia katikati ni Afisa mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kaskazini Nurdin Mangenya 
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Onesmo Buswelu(kulia)ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha,akihesabu mifuko ya 70 ya Mbolea aina ya Urea mara baada ya kukabidhiwa kama msaada  kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo,Msaada huo umetolewa na GSM Tanzania na kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Group,Matina Nkurlu(kushoto)
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Onesmo Buswelu(kulia)ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha,akihesabu mifuko ya 70 ya Mbolea aina ya Urea mara baada ya kukabidhiwa kama msaada  kwa ajili ya vikundi vya kina mama wanaojishughulisha na kilimo mkoani humo,Msaada huo umetolewa na GSM Tanzania na kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa GSM Group,Matina Nkurlu(katikati)anaeshuhudia kushoto ni Afisa mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kaskazini,Nurdin Mangenya 

Mwenyekiti Tume ya Madini, atatua mgogoro sugu wa madini, Nzega

$
0
0
Na Greyson Mwase, Nzega
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula leo tarehe 06 Desemba 2018 ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya vikundi viwili vilivyokuwa vinajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika eneo la Mwamikola lililopo Wilayani Nzega mkoani Tabora.

Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha Mwaguguli Mining Society na kikundi cha Mwamikola Gold Mining Society ambapo mgogoro wao ulitokana na mwingiliano wa maombi ya leseni za uchimbaji mdogo wa madini.

Profesa Kikula aliyekuwa Wilayani Nzega kwa ajili ya kutatua mgogoro huo aliambatana na watendaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki, Meneja wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Mhandisi Zephania Maduhu na Mwanasheria kutoka Tume ya Madini, Hadija Ramadhani.

Wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni pamoja na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Mayigi Makolobela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Onesmo Kisoka, Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Wilaya pamoja na waandishi wa habari.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (katikati kushoto) na Kamishna kutoka Tume ya Madini, Dk. Athanas Macheyeki wakikagua moja ya mashimo ya kuchimba dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Mwamikola katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora tarehe 06 Desemba, 2018
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kushoto) akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu  katika kijiji cha Mwamikola  kilichopo katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora
Mmiliki wa eneo lililopo katika kijiji cha Mwamikola kilichopo katika Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Rashid Kavula ( kushoto) pamoja na Katibu wa Kikundi cha wachimbaji wa madini ya dhahabu kilichokuwa kinaendesha shughuli zake za madini katika eneo hilo cha Mwaguguli Mining Society, Nyansaho Sumar (kulia) wakishikana mikono kama ishara ya kumaliza mgogoro baina yao kwenye mkutano wa wachimbaji wadogo wa madini uliofanyika katika kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula ( wa nne kutoka kulia mbele), Kamishna kutoka Tume ya Madini Dk. Athanas Macheyeki ( wa tatu kutoka kulia mbele) na Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Onesmo Kisoka ( wa tano kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya watendaji kutoka Tume ya Madini na wachimbaji wa madini katika eneo la Mwamikola lililopo Wilayani Nzega mkoani Tabora mara baada ya kutatua mgogoro huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

NHIF KUFANYA ZOEZI LA UHAKIKI WA WANACHAMA WASTAAFU

WALIOPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA AJILI YA KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU WAENDELEA NA SAFARI

$
0
0
Anaandika Dixon Busagaga kutoka Mlima Kilimanjaro.

Siku ya kwanza ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 57 ya Uhuru ilivyo anza na kumalizikia kituo cha kwanza cha Mandara.

Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali ,George Waitara ndiye anaongoza wa kundi la watu 52 kupanda mlima Kilimanjaro wakiwemo Maafisa wa jeshi la Wananchi wakiongozwa na Mnadhimu wa jeshi Mstaafu.Luteni Jenerali ,James Mwakibolwa.

Wengine wanaopanda ni kundi la waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari,Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taiga (TANAPA) ,Maofisa kutoka urafiki kati ya Tanzania na China,Waadhiri kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Maofisa kutoka taasisi ya Mkapa.

Safari kwa wapandaji hao inaendelea ambapo watapunzika kituo cha Horombo kabla ya kuelekea kituo cha Kibo tayari kuelekea kilele cha Uhuru.


MFANYABIASHARA DAR AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUKWEPA KODI, KUJIPATIA BILIONI 188.9/-

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

MFANYABIASHARA Mustapha Kambangwa (34) ambaye ni Mkazi wa Kongowe Mbagala, jijini Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka manne likiwemo la kukwepa kodi na kujipatia Sh.bilioni 188.9 kupitia mashine ya kieletroniki (EFD).

Mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtenga imedaiwa na Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Christopher Msigwa kuwa katika siku tofauti kati ya Juni Mosi ,2016 na Novemba 2, 2018 mshitaka Kambangwa alijifanya kama mtu aliyesajiliwa kuwa mlipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kukusanya kodi ya VAT  Sh.188,928,752,166 kwa kujifanya anakusanya fedha hizo kwa niaba ya TRA.

Katika shtaka la pili, Msigwa amedai kati ya Juni Mosi, 2016 na Novemba 2, mwaka huu, mshtakiwa kwa udanganyifu alitumia mashine ya kieletroniki (EFD) yenye namba 03TZ842011315 iliyosajiliwa kwa jina la Kampuni ya Abraham's Group LTD kukwepa kodi ya VAT yenye thamani kiasi hicho cha fedha.

Aidha mshtakiwa amedaiwa kuwa katika tarehe na kipindi hicho alijipatia au kujimilikisha fedha hizo alizozipata kutokana na makato ya kodi ya VAT ambazo zilipaswa kutolewa kwa Kamishna wa TRA, ikadaiwa mshitakiwa alitenda kosa hilo huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la ukwepaji kodi.


Pia imedaiwa kuwa mshtakiwa kwa vitendo vya makusudi vya kukwepa kodi alitumia mashine ya EFD na huku akijua kwamba hajasajiliwa kama mlipakodi ya VAT na aliisababishia TRA hasara ya 188,928,752,166.


Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote Mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Hata hivyo, Wakili wa Utetezi, Shamo Shadrack aliomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili kupinga  mashitaka hayo dhidi ya mshitakiwa  Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 17.2018 kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi w shauri hilo bado haujakamilika.

WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WAPIGWA MSASA JUU YA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Profesa. Faustin Kamuzora akifafanua umuhimu wa kuizingatia sheria ya usimamizi wa maafa ya mwaka 2015 wakati wa kutoa elimu juu ya usimamizi wa maafa nchini kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendelea mjini Dodoma.

Timu ya wataalamu wa Ofisi ya waziri Mkuu wanaohusika na shughuli za kuratibu usimamizi wa maafa nchini, pamoja na timu ya wataalamu wa uokoaji ya Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa. Faustin Kamuzora wametoa elimu kwa wakuu wa mikoa na makatibu Tawala, juu ya menejimenti ya maafa nchini.

Akiongea wakati wa uwasilishaji mada za usimamizi wa maafa nchini kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao yanayoendelea mjini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora amewashauri viongozi hao kuizingatia sheria ya usimamizi wa maafa nchini ya mwaka 2015 inayozitaka kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kutafuta rasilimali za usimamizi wa maafa katika ngazi husika.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifafanua juu ya masuala ya menejimenti ya maafa wakati wa majadiliano ya mada ya Usimamizi wa maafa nchini kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendelea mjini Dodoma.

“Ningependa niwashauri tumieni kamati zenu katika mkoa na wilaya ambazo zitawasaidiia kujua rasilimali mlizo nazo na kujua utaalamu wa kutumia, hivyo mtaweza kujenga uwezo mkubwa wa kukabili maafa yanayowapata na hayatahitaji kufika ngazi ya kitaifa na kwa kuzingatia ngazi ya kitaifa tunategemea mfuko wa maafa ambao bajeti ni finyu hivyo jitahidini kutumia rasilimali zenu katika kujiandaa zaidi kuliko kusubiri kutumia rasilimali nyingi wakati wa kukabili“ Amesisitiza,  Kamuzora.

Awali akiongea katika Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Timu ya Wataalamu wa uokoaji ya Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava, alifafanua kuwa timu hiyo imeundwa mahususi na mkoa huo ili kuwezesha kamati ya maafa ya mkoa huo kufanya shughuli za usimamizi wa maafa  kwa weledi, tayari imefanikiwa kuzijumuisha asasi na taasisi zote za Serikali, zisizo za Kiserikali na za watu Binafsi zinazoshughulika na maafa katika Mkoa huo na kutengeneza Mpango mkakati wa kukabili maafa mkaoni humo.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akifuatilia majadiliano wakati wa majadiliano ya mada ya Usimamizi wa maafa nchini kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendelea mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha  majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na  Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.

WANAHABARI WAFUNDWA KUHUSU KINGATIBA YA MAGONJWA YASIYOPEWA KIUPAUMBELE

$
0
0
 Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kiupaumbele, Dkt. Upendo Mwingira akitoa mada kwa waandishi wa habari kuhusu kampeini kutoa kingatiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kiupaumbele ambayo ni Matende na Mabusha(Ngirimaji), Usubi, Kichocho, Minyoo nk. iliyofanyika katika ofisi ya Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
 Afisa Mipango- Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa hayapewi Kiupaumbele,  Osca Kaitaba  akitoa mada kwa waandishi wa habari kuhusu kampeini kutoa kingatiba kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kiupaumbele ambayo ni Matende na Mabusha(Ngirimaji), Usubi, Kichocho, Minyoo nk. iliyofanyika katika ofisi ya Wizara ya Afya jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuhusu kutoa kingatiba ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kiupaumbele iliyofanyika leo katika ukumbi wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.

NEC YATANGAZA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA TEMEKE NA KATA 46 ZA TANZANIA BARA.

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara.

Akitangaza kufanyika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba 2018.

"Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 21 Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe 19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.Jaji Kaijage amebainisha kuwa Tume imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika jimbo hilo.

Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam kufuatia Kujiuzulu uanachama wa Chama Wananchi CUF kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Maulid Said Abdllha Mtolea.

WAZEE WAMPA USHAURI MZITO SHEIKH WA MKOA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WAZEE wa dini ya Kiislamu jijini Mwanza wameushauri uongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kumtanguliza Mungu, ukubali kukosolewa na kuacha kuwapokea mafisadi baada ya kupenyezewa bahasha.

Walitoa rai hiyo ilitolewa jana walipokutana na kuzungumza na Kaimu Sheikh wa Mkoa, Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke ili  kutoa ushauri wao kwa viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza.
Wazee hao walisema ili uongozi wa baraza hilo uende vizuri ukubali kukosolewa na zaidi wamtangulize Mwenyezi Mungu katika kutenda na kuwatumikia waislamu na kuwa wakweli.

“ Aliyewazidi  wenzake ni mcha Mungu na hivyo timu hii izidishe ucha Mungu.Msiwapokee mafisadi kwa kupenyezewa bahasha baada ya kuwa wamefanya ufisadi misikitini.Bahasha hizo zinaidhoofisha BAKWATA na kuonekana ni jalala,” alisema Sheikh Rajab Charahani.

Alisema yapo malalamiko katika misikiti mingi yakiwatuhumuwa viongozi wa wilaya kupokea bahasha ili kufumbia macho mambo ya ovyo na kuutaka uongozi wa BAKWATA Mkoa ujiepushe na bahasha hizo na wakubali kukoselewa ikizingatiwa kila binadamu anakosea na hata yeye (Charahani) alikosea, wakifanya hivyo wazee watawapa ushauri.
Sheikh Rajab Charahani mmoja wa wazee maarufu wa Dini ya Kiislamu jijini Mwanza akitoa nasaha kwa uongozi wa BAKWATA mkoani humu (hawapo pichani) baada ya kukutana kwenye kikao cha ushauri kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Salum Ferej wilayani Nyamagana. Picha na Baltazar Mashaka
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hassan Musa Kabeke akizungumza na wazee maarufu wa dini ya Kiislamu jijini Mwanza (hawapo pichani) jana. Picha na Baltazar Mashaka 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU AMUAGIZA SIMBAKALIA AFUATILIE KIBALI WIZARA YA ARDHI

$
0
0
*Ni cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi Chalinze
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, George Simbakalia afuatilie Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu kibali cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi kinachotakiwa kujengwa Chalinze. Ametoa agizo baada ya Mkuu wa mkoa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo kumuleza kuwa kuna muwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha H and J cha Chalinze ambacho ujenzi wake umekwama kutokana na mwekezaji kutopewa kibali cha ardhi.

Waziri Mkuu ametoa agzo hilo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaunga mkono wawekezaji na kuwafanya wawekeze bila ya urasimu, hivyo amemuagiza kiongozi huyo wa EPZA kuhakikisha kibali kinapatikana.

“Nakuagiza Mkurugenzi ufuatilie kibali hicho na nikifika Dodoma nipate majibu. Hatuwezi kuchelewesha uwekezaji nchini kwa ajili ya urasimu, kila mtendaji ahakikishe anatekeleza majukumu yake ipasavyo.”

Akizungumzia kuhusu uwekezaji katika sekta ya viwanda kikiwemo na kiwanda cha Twyford, Waziri Mkuu amesema uwekezaji huo unafaida kubwa kwani licha ya mapato ya Taifa kuongezeka kupitia kodi pia wananchi wananufaika kwa kupata ajira

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda cha  Sayona kilichopo eneo la Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018.    Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha Sayona kilichopo eneo la Chalinmze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018. Wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel na Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda  cha Sayona kilichopo Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018,  Wapili kushoto ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Motisun, Subash Patel  na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAZIRI LUGOLA AMBANA AFISA ELIMU KWA KUKATAA KUANDIKISHA WANAFUNZI DARASA LA KWANZA

$
0
0
 Mwandishi Wetu, MARA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni kwake Mwibara, Wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.  Lugola ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, amemtaka Afisa Elimu wa Kata ya Chitengule, Jimboni humo, Thadeo Lukinisha kuruhusu shule za msingi zilizopo katika Kata yake kuandikisha wanafunzi hao bila kikwazo chochote kwakuwa elimu ya shule ya msingi ni bure nchi nzima.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Nakatuba katika Kata hiyo, Lugola alipiga marufuku utaratibu huo ambao amesema hauna msingi wowote kwasababu unawaonea watoto ambao hawana kosa lolote hata kama kuna madeni ambayo wazazi wa wanafunzi hao wanadaiwa kutokana na watoto wao wanaoendelea na masomo katika shule zilizopo jimboni humo. 

 “Huu utaratibu sio sawa, haukubaliki, kipindi hiki wanafunzi wanaandikishwa kuanza darasa la kwanza waandikishwe bila kikwazo chochote ili waweze kupata elimu yao kama inavyostahili, michango yenu haihusiani na wanafunzi kuanza shule,” alisema Lugola. 

Hata hivyo, Afisa Elimu huyo tukio hilo lipo lakini walifanya hivyo kutokana na baadhi ya wazazi kutolipa kiasi cha shilingi mia nne ambayo inachangwa kwa ajili ya kila mwanafunzi anachangia kwa ajili ya kumlipa mpishi pamoja na mafuta ambayo fedha hiyo inalipwa kwa mwaka. Lugola alipata taarifa hiyo ya wazazi kukataliwa kuandikishwa watoto wao kuanza darasa la kwanza, baada ya mzazi mmoja kuulalamikia utaratibu huo na kuwafanya wazazi kutokuanidisha watoto hao kutokana na kudaiwa michango hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namalebe, Kata ya Chitengule, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Kaswanila Molore kabla ya kuanza mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kijiji hicho. Akizingumza na wananchi wa Kata hiyo, Lugola amepiga marufuku wanafunzi wanaoanza darasa la kwanza kutokuandikishwa mpaka wazazi wao walipe michango wanaodaiwa katika shule mbalimbali jimboni humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WENYE VIWANDA YA SHARJAH IKULU LEO

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara   Wenye Viwanda ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi ya Sharja Bw.Abdallah Sultan Owais, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar Ikulu leo,akiwa na Ujumbe wake kulia Sheikh.Majid Faisal Khalid Al.Qasemi Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.(Picha na Ikulu)
 //RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza mgeni wake Mwenyekiti w a Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda ya Sharjah,ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi, Bw.Abdallah Sultan Owais, wakiwa nje ya ukumbi baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika leo Ikulu Zanzibar,7-12-2018.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanja Sharjah  ambae pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Al Rawabi Bw.Abdallah Sultan Owais, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar, leo 7-12-2018.(Picha na Ikulu)

SALAMU ZA RAIS MAGUFULI KUELEKEA SHEREHE ZA UHURU DESEMBA 9, 2018

$
0
0
*Atoa msamaha kwa wafungwa 4400, awapongeza awamu zote 
zilizopita
*Asisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kujenga uchumi wa nchi 
yetu

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli amewatakia Watanzania wote nchini kutafakari tulikotoka, tulipo na tunakokwenda huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kufanya kazi ili kujenga uchumi imara hasa kwa kuzingatia kwa sasa tupo kwenye vita ya kiuchumi ambayo lazima wote tushirikiane kuishinda.

Ametoa kauli hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati anatoa salamu za kuwatakia kila laheri Watanzania katika kuelekea kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9, 2018 ambapo itakuwa Jumapili ya wiki hii na kufafanua siku hiyo itakuwa ni ya mapumziko, ambayo itumike kutafakari tulikotoka na tunakokwenda.

"Kila laheri Watanzania katika kusherehekea miaka 57 ya Uhuru wa Tanganyika.Kama ambavyo mnafahamu tayari fedha Sh.bilioni moja 
zilitengwa kwa ajili ya kufanikisha sherehe hizo lakini nimeshatoa maelekezo fedha hizo zitumike kujenga Hospitali Dodoma ambayo itaitwa Hospitali ya Uhuru,"amesema Rais Dk.Magufuli na kufafanua kwa kuwa Serikali inahamia Dodoma kuna umuhimu wa kujengwa kwa hospitali nyingine ili ziwepo mbili,"amesema.

Amesema kuwa tayari sehemu ya watumishi wa Serikali wapo Dodoma na amebaki yeye tu ambaye naye anajiandaa kuondoka siku za hivi karibuni na hivyo ndio maana ni muhimu kujengwa kwa hospitali ya pili ili isaidiane na Hospitali ya Mkapa.

Serikali yahimiza Usawa wa Jinsia

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.

Hayo yamesemwa na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua   Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo  jijini Dar es Salaam .

Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala  za Serikali, Mamlaka  za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili  kushoto), na Viongozi  Waandamizi  wa  Jeshi  la Magereza  wakikata utepe  kuashiria  Uzinduzi  wa  Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati) akimkabidhi tuzo Mwakilishi wa Benki ya NMB,ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo ya kifedha  katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(katikati), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Wanawake(TAWLA), ikiwa  ni ishara ya kutambua mchango wa taasisi hiyo katika uanzishwaji wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa inayotengenezwa na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzinduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa  na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee,leo jijini Dar es Salaam..Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUZI TV: SHILOLE kingereza kitamtoa roho,ashangaza usiku wa WOLPER

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA HALMASHAURI KUSHIRIKISHA WATU WENYE ULEMAVU PROGRAMU YA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zitakazojengwa vitalu nyumba kushirikisha vijana wenye ulemavu. Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma na Iringa kukagua maeneo yatayojengwa na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo alisema kuwa katika halmashari zote 83 ambapo teknolojia ya kilimo cha kitalu nyumba itaanzishwa, idadi ya vijana 100 watakaopata mafunzo hayo ijumuishe na wenye ulemavu.

“Halmashauri zitengeneze mfumo madhubuti wa kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika mradi huu, kwani wanaouwezo wa kufanya kazi kama ilivyo vijana wengine na wakiwezeshwa wanaweza”, alisema Mhagama.

Pamoja na hayo, Mhagama amehimiza halmashauri hizo zisimamie vyema mradi huo kwa kuufanya unakuwa endelevu na kuwaunganisha vijana kwenye vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia programu hiyo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa vijana na wakazi wa Mkoga alipofanya ziara ya kikazi Mkoa wa Ruvuma na Iringa kwa lengo la kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya Kilimo cha kitalu nyumba.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bw. Ahmed Njovu akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoani humo.
 Afisa Maendeleo ya Vijana Bw. Atilio Mgamwa akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa programu ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.
 Mratibu wa Mradi wa Kitalu Nyumba Bi. Elizabeth Kalilowele akielezea utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba ulipofikia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS DKT.MAGUFULI ATOA SALAMU ZA KUMBUKUMBU MIAKA 57 YA UHURU WA TANZANIA BARA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa Salamu za miaka 57 ya Uhuru wa Tanzania Bara Ikulu jijini Dar es Salaa. PICHA NA IKULU

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images