Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

Experts meet in Dar to discus food safety concerns in Africa

$
0
0
By Correspondent

African food experts, researchers and stakeholders will meet in Dar es Salaam today to discuss challenges and concerns related to food safety, food borne diseases and chart out strategies on the best ways to improve food safety, nutrition and security for millions of Africans.

The international meeting is part of the commemoration of the Africa Day for Food and Nutrition Security 2018, is organized under the main theme “Sustained Food Safety Action for Improved Nutrition and Health of Africans,” bringing together participants from various African countries and key international and national agencies, World Food Programme, UNICEF, World Health Organization, Food and Agriculture Organization of the United Nations, African Union Commission, NEPAD and Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA).

The main agenda of the meeting, expected to be graced officially by the Permanent Secretary in the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Women, is food safety concerns and their associated main outcome, food-borne diseases, according to an official statement issued by the organizing agency, TFDA.

“Food-borne disease imposes large direct and economic burdens worldwide…Africans are not exception to this…” noted TFDA statement.


Dr. Kandida Shirima, Director of Food Safety at TFDA, presenting a paper on food safety status in Africa at the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference being held in Dar es Salaam which discusses food safety concerns in Africa.
Participants to the Africa Day for Food and Nutrition Security—2018 conference following proceedings of the meeting being held in Dar es Salaam which will discuss food safety concerns in Africa.



MBWATE WACHOSHWA NA KERO YA UKOSEFU WA MAJI NA UMEME

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha 
WAKAZI wa mtaa wa Mbwate,kata ya Mkuza Kibaha Mjini mkoani Pwani, wanatatizo kubwa la ukosefu wa maji safi na salama ,hali inayosababisha kutumia maji ya kisima licha ya kuishi mjini. Aidha wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa nishati ya umeme ambapo tangu wawekewe nguzo ni takriban miezi nane bila muendelezo wowote.

Wakielezea kero zinazowakera ,akiwemo Kambangwa Kilema na Editha wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ,kata ya Mkuza, walisema inashangaza kutumia maji yasiyo salama kwa kushirikiana na ngedere. Alisema ,wanataabika na hali hiyo licha ya serikali kuahidi kumtua ndoo mama kichwani. 

"Sijui tuko mjini ya wapi, hatupishani na wanaoishi kijijini, hatuna maji salama, hatuna umeme, tunaiomba serikali ituangalie kwa jicho la tatu ili nasi tufaidike na huduma hizi muhimu "alifafanua Kilema. Hata hivyo, Kilema aliweka bayana juu ya changamoto ya ukosefu wa umeme, na kudai wamekuwa wakienda shirika la umeme Tanesco kuomba wasaidiwe lakini hakuna msaada wanaoupata. 
 Kufuatia changamoto hizo, Koka aliunda kamati iyohusisha na wananchi kwenda kufuatilia hatua zinazochukuliwa na DAWASA kuanza kusambaza maji pamoja na Tanesco kuhusu umeme ili kuondokana na shida hizo. Pamoja na hayo, Koka alisema ameshatoa kiasi cha sh. milioni tano kwa ajili ya kujenga madaraja madogo mawili katika miundombinu ya barabara mtaa wa Mbwate .
 Nae ofisa uhusiano na huduma kwa wateja Tanesco mkoani Pwani, Adrian Severin ,alisema mradi wa umeme unaopita Mbwate unahitaji nguzo zaidi ya 300. Alisema tatizo lilipo sasa ni upungufu wa upatikanaji wa vifaa ikiwa ni pamoja na nguzo. 

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti na Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma

MICHUZI TV: Harmonize agombanisha mashabiki jukwaani kisa hiki hapa

Wekezeni kwenye afya kwa kujiunga na NHIF- Waziri Ummy

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Bernard Konga katika mkutano wa hadhara Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba Mkoani Mtwara wakati wa uhamasishaji wa wananchi kujiunga na NHIF, kupitia Mpango wa Ushirika Afya.

Na Grace Michael

Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kufanya uwekezaji kwenye afya zao kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote. Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wananchi katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba mkoani Mtwara.

Amesema kuwa ili kila mwananchi aweze kuwa na uhakika wa kufanya shughuli zingine za maendeleo na uwekezaji mwingine lazima awe na uhakika na afya yake kwa kuwa na uhakika wa kupata matibabu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akikagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara. 

“Nawaomba sana wananchi wa Mtwara wekezeni kwenye eneo la afya zenu na uwekezaji mzuri ni kuwa na Bima ya Afya kupitia NHIF ili iwawezeshe kupata huduma zote za matibabu kwa ngazi mbalimbali za vituo vya kutolea huduma kuanzia ngazi ya Zahanati hadi Hospitali ya Taifa,” alisema Mhe. Ummy.

Alisema kuwa Serikali imeweka utaratibu mzuri wenye gharama nafuu wa kupata huduma za matibabu kupitia NHIF, utaratibu ambao unamtaka mwananchi kujiunga kabla ya kuugua ili aweze kunufaika na huduma za matibabu wakati wowote anapopatwa na maradhi.

“Wengi wetu hapa mmeuza mazao yenu na mnalipwa fedha nyingi, kati ya fedha mnazopata hakikisheni mnatenga shilingi 76,800 tu kwa ajili ya kukata kadi ya bima ya afya ambayo itakusaidia kupata huduma mahali popote ndani ya nchi kwenye zaidi ya vituo 7000 vilivyosajiliwa na NHIF,” alisema Mhe. Ummy wakati akizungumza na wananchi wa Nanyamba Mkoani Mtwara.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimhamasisha mmoja wa akina mama kumwandikisha mtoto wake na mpango wa Toto Afya Kadi ili awe na uhakika wa kupata matibabu. 

Aliwahakikishia wananchi upatikanaji wa huduma za matibabu katika hospitali zote nchini kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imeongeza kwa kiasi kikubwa bajeti ya afya hususan bajeti ya dawa.

KAMATI YA UONGOZI WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA YAKUTANA

$
0
0
Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

Akizungumzia agenda za kikao, Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda amesema kuwa kikao hicho kitakuwa na ajenda ya kujadili muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 2018 na uchaguzi wa Viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa.

Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa inaundwa na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Wenyeviti na Makamu wenyeviti wa kamati nne za Baraza la Vyama vya Siasa.Naibu Msajili wa vyama vya Siasa (kushoto ) akipokea Nakala ya Maelezo ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa yenye ushauri wa jinsi ya kuunda siasa adilifu na bora za kujenga ustawi na maendeleo ya jamii, uchumi na Taifa iliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu , Mhe. Kassim Majaliwa mapema mwaka huu kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Bw. Abdalah Juma Saadalla .
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Bw.John Magale Shibuda afafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa kimefanyika leo Disemba 4, 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu. Kulia kwake ni Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Ohammed Ali Ahmed na kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Bw. Abdalah Juma Saadalla 
Kikao kikiendelea.

CEO DAWASA AHIDI KUPELEKA HUDUMA YA MAJI BONYOKWA

$
0
0
Afisa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa ahadi ya kupeleka maji Bonyokwa wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa.

Prof Mbarawa amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na huduma ya Maji katika eneo hilo. 

Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa eneo hilo limekosa huduma ya Maji kwa muda mrefu kutokana na kukosa chanzo cha Maji cha Karibu na hivyo DAWASA imeamua kulaza bomba kubwa litakalo chukua Maji kutoka mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu ili kuhudumia wakazi wa eneo hilo.

“Sisi DAWASA tutaleta huduma ya Maji hapa Bonyokwa kwa kuwa ni muda mrefu mmeteseka na tatizo kubwa la eneo hili ni kukosa chanzo cha Maji cha kuhudumia hapa kutokana na jiografia yake ila sasa tumeamua kutoa Maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na kuyaleta hapa, tayari pia baadhi ya vifaa vimefika hapa na kuanzia Siku ya Jumatatu tutaanza kazi rasmi ya kulaza mabomba hivyo wananchi mjitokeze kwa ajira uchimbaji mitaro” alisema mhandisi Luhemeja.

Aidha Prof. Makame Mbarawa katika mkutano huo amewatoa wasiwasi wakazi wa eneo hilo kwa kuwaeleza kuwa atahakikisha DAWASA inafikisha huduma ya Maji kwa wakati na kumuagiza meneja wa DAWASA Mkoa wa Tabata kusimamia hilo. Pia amebainisha kuwa lengo la serikali ni kufikisha huduma ya Maji safi kwa asilimia tisini na tano kwa maeneo yaliyopo mijini kufika 2020.

Kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo Meya wa Ilala na Diwani wa eneo hilo Charles Kwiyeko ameshukuru jitihada za serikali pamoja na DAWASA zakutaka kufikisha huduma ya Maji kwa kuwa ni kero kubwa na ya muda mrefu kwa wananchi wake.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Bonyokwa na kuwaondoa hofu na kuwahakikishia watapata maji kwenye maeneo yote yaliyokuwa hayana maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa anatembelea maeneo ya Bonyokwa akiwa ameambatana na Meneja wa DAWASA Tabata na Diwani wa kata hiyo.
Wananchi mbalimbali waliofika katika mkutano huo.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA TIC AITAKA IMALIZE URASIMU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake. Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam. “Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.” 

Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa. Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.

“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.” Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali. 

Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji. Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwenye viwanja vya Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Afisa wa NEMC katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Linda Mutafungwa wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (wapili kulia) na Helen Haule (kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda (kulia) na Helen Haule ( wapili kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati alipotembelea Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu 



CEO WA DAWASA AHAIDI KUPELEKA HUDUMA YA MAJI BONYOKWA

$
0
0
OFISA mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka  Dar es Salaam  (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametoa ahadi ya kupeleka maji Bonyokwa  wakati wa ziara ya Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa.

Prof. Mbarawa amefanya  ziara ya kusikiliza kero za wananchi kuhusiana na huduma ya Maji katika eneo hilo. 

Mhandisi Luhemeja ameeleza kuwa eneo hilo limekosa huduma ya Maji kwa muda mrefu kutokana na kukosa chanzo cha Maji cha Karibu na hivyo DAWASA imeamua kulaza bomba kubwa litakalo chukua Maji kutoka mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu juu ili kuhudumia wakazi wa eneo hilo.

“Sisi DAWASA tutaleta huduma ya Maji hapa Bonyokwa kwa kuwa ni muda mrefu mmeteseka na tatizo kubwa la eneo hili ni kukosa chanzo cha Maji cha kuhudumia hapa kutokana na jiografia yake ila sasa tumeamua kutoa Maji kutoka mtambo wa Ruvu juu na kuyaleta hapa, tayari pia baadhi ya vifaa vimefika hapa na kuanzia Siku ya Jumatatu tutaanza kazi rasmi ya kulaza mabomba hivyo wananchi mjitokeze kwa ajira uchimbaji mitaro” alisema mhandisi Luhemeja.

Aidha Prof. Makame Mbarawa katika mkutano huo amewatoa wasiwasi wakazi wa eneo hilo kwa kuwaeleza kuwa atahakikisha DAWASA inafikisha huduma ya Maji kwa wakati na kumuagiza meneja wa DAWASA Mkoa wa Tabata kusimamia hilo. 

Pia amebainisha kuwa lengo la serikali ni kufikisha huduma ya Maji safi kwa asilimia tisini na tano kwa maeneo yaliyopo mijini kufika 2020.

Kwa niaba ya wakazi wa eneo hilo Meya wa Ilala na Diwani wa eneo hilo  Charles Kwiyeko ameshukuru jitihada za serikali pamoja na DAWASA zakutaka kufikisha huduma ya Maji kwa kuwa ni kero kubwa na ya muda mrefu kwa wananchi wake.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi wa Bonyokwa na kuwaondoa hofu na kuwahakikishia watapata maji kwenye maeneo yote yaliyokuwa hayana maji.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akiwa anatembelea maeneo ya Bonyokwa akiwa ameambatana na Meneja wa DAWASA Tabata na Diwani wa kata hiyo. 
Wananchi mbalimbali waliofika katika mkutano huo.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 5, 3018

TAEC YAWAKUTANISHA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUTATUA CHANGAMOTO MADHARA YA MIONZI

$
0
0
Na Vero Ignatus,Arusha
Tume ya nguvu za ATOMIC Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya ya umoja wa Ulaya EU imeandaa warsha ya siku 3 kwa ajili ya utowaji wa leseni ya madini yatoayo mionzi ya kujikinga na madhara yake nchini Tanzania

Warsha hiyo iliyofanyika jijini Arusha katika Ofisi za Atomic zilizopo Njiro ambapo lengo ni kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta mbalimbali ili kuweza kutatua changamoto zinazotokana na madhara ya mionzi

Mkurugenzi wa tume ya nguvu za Atomic Tanzania Prf. Lazaro Lusagara amesema kuwa wameendelea na warsha hiyo ili kuweza kuhakikisha wanaziba mianya ambayo imekuwa wazi na kuweza kuwafikia watanzania wote kwa wakati ili kuweza kuwapa elimu ya kutosha

Mkurugenzi wa lessen za madini pamoja na mifumo ya TEHAMA nchini Tanzania Bw. Thomas Ngole Pamoja Khadija ramadhani kutoka tume ya madini Tanzania wamesema semna hiyo itasaidia kuongeza nguvu katika utendaji kazi na kusaidia Radio active Material kuwaweka watu salama

Kwa upande wake Afisa mazingira kutoka baraza la taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira Bw. Abel Nestori Sembeka amesema kuwa semina hiyo itasaidia kuboresha namna ya utendaji kazi ili kuweza kujua shughuli za kusimamia madini ya URANIUM na utendaji wa kazi mzuri na kufanya kazi kwa ushirikiano

Hata hivyo wadau mbalimbali walioshiriki ni pamoja na, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, wizara ya maliasili na utalii, baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC, tume ya madini, tume ya nguvu za Atomic Tanzania, na wizara ya elimu sayansi na Technologia.

NAIBU WAZIRI TAMISEMI AFUNGUA KONGAMANO LA 10 LA WADAU WA ELIMU

$
0
0
NAIBU wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege leo amefungua kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi kwa wanafunzi ili uwasaidie kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa sasa.

Kongamano hilo lililoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) limefunguliwa leo Jijini Dodoma na Mh. Kandege kwa niaba ya waziri wake huku akiwapongeza wadau hao kwa juhudi za kuendelea kuiboresha elimu, hivyo kuwahakikishia Serikali inasubiri kwa hamu mapendekezo ya kongamano ili iyafanyie kazi.

Alisema hapo nyuma ilifika kipindi vijana walikuwa wakifundishwa namna ya kujibu mitihani jambo ambalo limekuwa changamoto kijana huyo anapoingia mtaani na kukuta mambo tofauti. "Tunasema tunataka kufanya mapinduzi lazima hivyo lazima twende pamoja kama hivi na kuibuka na majibu," alisema.

"...Haya ambayo mnaenda kuyafanya kwa siku mbili hizi mnazokutana tunaamini kazi nzuri ambayo unaenda kuifanya inakwenda kuliokoa taifa la Tanzania kutoka katika hali ambayo watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka juu ya elimu yetu...na sasa tunakwenda kuwa taifa litakalopigiwa mfano kwa ubora wa elimu."
Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege ambaye pia ni mgeni rasmi akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kongamano hilo. 
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (wa pili kulia) akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kongamano hilo na Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege, pamoja na Mkurugenzi wa Right To Play Tanzania, Josephine Mukakausa. 
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale (katikati) akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mwl. Augusta Lupokela na kulia ni mgeni rasmi. 
Mkurugenzi wa Right To Play Tanzania, Josephine Mukakausa (kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege, na Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

BENKI YA NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA MIKOCHENI SEKONDARI DAR

$
0
0

BENKI ya NMB imetoa msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta hizo, Dar es Salaam leo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alisema kompyuta hizo zitachangia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji hasa kipindi hiki ambacho dunia inaongea zaidi juu ya sayansi na teknolojia.

"Kompyuta tunazozitoa leo hii ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii tunaimani zitaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi hususani kwenye masomo ya Tehama" alisema Idd.Aliongeza kuwa kompyuta hizo tano zitasaidia kuimarisha mafunzo ya Tehama shuleni hapo na kuongeza uelewa mzuri wa masomo ya Tehama kwa wanafunzi wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza masomo yao.

Idd alisema kuwa kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta 150 zinazopelekwa mashuleni kwa mwaka huu ambapo pia katika Wilaya ya Same wamebahatika kupata mgao wa kompyuta tano.

Akizungumzia kuhusu benki hiyo alisema ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi 228, ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB wakala zaidi ya 6000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 3 idadi ambayo ni hazina kuwa ukilinganisha na benki zingine na kuwa imezifikia wilaya zote kwa asimilimia 100 pamoja na kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimkabidhi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, moja kati ya kompyuta tano zilizotolewa na benki hiyo leo hii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo. Wa pili  kutoka kushoto ni Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo. Wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.
 Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akizunguza wakati akipokea msaada huo.
 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Dk Mengi afungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa Kichina

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amewaalika wafanyabiashara kutoka China washirikiane naye kuwekeza nchini kwa ubia katika miradi mbalimbali, wakati huu  ambapo Tanzania inapojizatiti kuwa ya viwanda.
Dr Mengi ametoa rai hiyo jijini Dar es salaam wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia  wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji, walioambatana kwenye hafla hiyo na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke.
Amesema Tanzania ni nchi iliyojaaliwa fursa nyingi za uwekezaji kutokana na utajiri wake wa  raslimali na kusisitiza kuwa waliotayari kushirikiana naye katika miradi mbalimbali kama ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Uganda wajitokeze.
Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa China nchini  Mhe. Wang Ke amesema ofisi yake itakuwa kiunganishi  baina ya Wafanyabiashara wa China na Dr Mengi katika kufanikisha pendekezo la kuanzisha kwa ubia hapa nchini viwanda mbalimbali.
Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara hao Bw. Lyu Xinhua amesema amekuja na ujumbe kutoka makampuni 17 ya China yanahusika na shughuli mbalimbali kuanzia ujenzi wa miundombinu, uhandisi, teknolojia ya mawasiliano nk, na kuahidi kuwasilisha mapendekezo yaliyotolewa kwa makampuni husika kwa ajili ya hatua zaidi za utekelezaji.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi akizungumza wakati wa chakula cha mchana alichowaandalia wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Bw. Louis Accaro, Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua, Balozi wa China nchini  Mhe. Wang Ke, Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe.
 Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua kutoa salamu wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni  Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa  IPP Touchmate, Bw. Victor Tesha (wa pili kulia) pamoja Msaidizi wa Dk. Mengi, Bw. Godfrey Bitesigirwe (kulia).
 Kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China, Bw. Lyu Xinhua akitoa salamu kwa niaba ya ujumbe huo wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi kwa wawakilishi wa makampuni   17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji katika hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi


Sehemu ya wafanyabiashara wawakilishi wa makampuni  17 kutoka China waliopo nchini kutafuta fursa za uwekezaji waliposhiriki hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa Dr. Mengi iliyofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC NAMTUMBO AIAGIZA TAKUKURU KUICHUNGUZA HALMASHAURI .

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Mfaume Kizigo ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wilayani Namtumbo kuchunguza shilingi milioni 950 zilizobadilishiwa matumizi na Halmashuri ya Namtumbo.

Kizigo aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano wa baraza la madiwani wilayani humo baada ya kubaini baraza la madiwani kutoridhika na taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashauri hiyo juu ya kubadilisha matumizi ya fedha shilingi milioni 950.

Taarifa ya mkaguzi wa ndani wa Halmashuri hiyo bwana John Mwingira ilidai Halmashuri hiyo imebadilisha matumizi ya fedha kiasi cha shilingi milioni 950 na kutumika kwa matumizi mengineyo tofauti na ilivyokusudiwa .

Aidha bwana Mwingira katika taarifa yake hiyo alidai kuwa fedha hiyo imetumika kwa nia njema lakini zinatakiwa kurudishwa katika shughuli iliyokusudiwa na serikali kwa kutumia mapato ya ndani ambayo kwa sasa yanasuasua.

Taarifa hiyo ilisema katika shilingi milioni 950 milioni 500 zilikuwa Ruzuku ya serikali zikiwa na lengo la kujenga Hospitali ya wilaya ambapo katika fedha hiyo milioni 200 zilibadilishwa matumizi na kumalizia zahanati saba viporo vya Halmashuri hiyo na kuanza kutumika na milioni 20 nazo zilibaki kujenga jengo moja katika Hospitali ya wilaya na milioni 156 zilipelekwa kukamilisha chumba cha upasuaji katika kituo cha afya lusewa katika mamlaka ya mji mdogo wa Lusewa.

Milioni 450 kati ya hizo milioni 950 zilipokelewa na Halmashuri hiyo kutoka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa LGLB ambazo nazo zililenga kujenga soko zilibadilishwa matumizi na kulipia deni la vifaa vya viwandani milioni 214 zilizokopa Halmashuri hiyo na milioni 26 zilitumika kununulia mashine ya kukusanyia ushuru (POS)ishirini.


Tony Elumelu kufungua dirisha Programu ya Wajasiriamali Afrika, Januari 1, 2019

$
0
0
Na Bakari Kimwanga -DAR ES SALAAM 

TAASISI ya Tony Elumelu (TEF), imetangaza kufungua mzunguko wa tano wa programu ya Wajasiriamali Afrika kuanzia Januari 1, 2019 

Maombi hayo yatatumwa na kushughulikiwa kwenye kwenye jukwaa kubwa la mitandao kwa wajasiriamali wa Afrika, TEFConnect - www.tefconnect.com

Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Tony Elumelu yenye makao makuu yake Lagos, nchini Nigeria ilieleza kwamba kuanzia Januari 1, 2019, saa 12 asubuhi, Tony Elumelu itaanza kupokea maombi ya mzunguko wa tano wa Programu ya Wajasiriamali. Ambapo waombaji 1,000 waliochaguliwa wataunganishwa msimamizi wa sasa wapatao 4,470 katika program hiyo. 

Tangu mwaka 2015, Mpango wa Biashara wa TEF – imekuwa ni kichocheo kiliasisiwa kwa misingi ya Afrika ambapo aina hiyo, imewawezesha wajasiriamali 4,470 wa Afrika, ambao kila mmoja amenufaika kwa kupatiwa Dola 5,000 kila mmoja. Hatua hiyo huenda sambamba na mjasiriamali kuhudhuria mafunzo ya biashara yanayoendeshwa kwa wiki 12, ambao hupata ushauri na uzoefu na kujifunza zaidi mazingira ta Biashara ya Afrika. 

Wanufaika wa Programu wamefanikiwa kuhojiwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Forbes (Afrika) 30 chini ya orodha 30. Ambapo wamevutia wawekezaji, na pia wamepewa tuzo za Impact Google na Tuzo ya "Venture" kwa wajasiriamali. 
Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo. Mkutano huo ulifanyika Lagos, Nigeria Oktoba mwaka huu.
Sehemu ya vijana walioshiriki jukwaa kubwa la wajasiriamali Afrika, lilofanyika Oktoba mwaka huu, Lagos, Nigeria.

BENKI YA EXIM YATOA MILIONI 10/- KUSAIDIA KAMBI MAALUM YA TAFITI ZA MAGONJWA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Exim Bank Ndugu Stanley Kafu  (wan ne kulia) akikabidhi Mfano wa Hundi ya Shilingi Millioni 10 kwa kamati tendaji ya “Rotary Oyster Bay Corporate Cricket Gala 2018” ikiwa ni sehemu ya kuchangia kambi maalumu ya tafiti za magonjwa mikoani inayoendeshwa na taasisi hiyo ya Rotary.

BORA TUKAWIE LAKINI TUJIRIDHISHE NA MIKATABA – WAZIRI KALEMANI

$
0
0
Na Veronica Simba – Mtwara
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amesema Serikali itatumia muda mwingi kadri itakavyoona inafaa ili kujiridhisha na manufaa ambayo Taifa litapata kabla ya kusaini mikataba mbalimbali ya sekta ya nishati, hususan ya mafuta na gesi. Aliyasema hayo Mtwara jana, Desemba 4 wakati akizungumza na uongozi wa Kampuni ya kigeni ya mwekezaji Maurel & Prom kutoka Ufaransa, wanaotafiti na kuchimba gesi eneo la Mnazi Bay.

Waziri Kalemani alitoa msimamo huo wa Serikali baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi wa kampuni hiyo iliyowasilishwa na Makamu Mkurugenzi Mkuu, Elias Kilembe, ambayo pamoja na mambo mengine, waliomba Serikali iharakishe mchakato wa utiaji saini mikataba ya uwekezaji zaidi katika sekta husika, ambayo walikwisha kuwasilisha. Akifafanua, Waziri Kalemani alisema, Serikali haikusudii kumchelewesha mwekezaji bali kinachofanyika ni kujiridhisha hatua kwa hatua, namna Taifa litakavyonufaika.

“Tutatumia muda wa kutosha kujiridhisha, hata kama ni miaka 40, lakini lazima mikataba iwe na manufaa. Huo ndiyo msimamo wa Serikali.” “Sisi tunapenda wawekezaji, tunataka waendelee kuwekeza ili tupate manufaa ya gesi na mafuta, lakini tusiibiwe,” alisisitiza.
 Wananchi wa Mtaa wa Ufukoni, Manispaa ya Mtwara wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (kulia) kuwasha umeme katika nyumba ya mmoja wa wananchi wa eneo hilo pamoja na kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kazi Desemba 4, 2018.
 Taswira ya sehemu ya mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba kama ilivyonaswa wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani Desemba 4, 2018.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati-mbele) na Ujumbe wake, akikagua Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba mkoani Mtwara, akiwa katika ziara ya kazi Desemba 4, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (mwenye shati ya bluu-katikati) na Ujumbe wake, wakikagua sehemu ya mitambo ya kuchakata gesi Mnazi Bay, Mtwara alipokuwa katika ziara ya kazi, Desemba 4, 2018.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Sheria Mpya ya Zana za Kilimo kuchochea Mapinduzi ya Viwanda – Mhandisi Mtigumwe

$
0
0
Sheria Mpya ya Zana za Kilimo kuchochea Mapinduzi ya Viwanda – Mhandisi Mtigumwe Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikati akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chisawilo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo sambamba na Wadau wa Zana za Kilimo mara baada ya kuufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Zana za Kilimo Wizara ya Kilimo, Mhandisi Joseph Lubilo akitoa maelezo ya utangulizi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikaki akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chiswalo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam .

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Zana za Kilimo wenye lengo la kupitia rasimu ya maboresho ya Sheria ya Zana za Kilimo nchini na kusisitiza kuwa Sheria mpya itatosaidia kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo ndiyo malighafi za viwanda vingi nchini. 

Akifungua mkutano huo, Mhandisi Mtigumwe amesema kilimo cha Tanzania kimepitia mageuzi mengi ya kisera na kimkakati na kwamba maboresho ya sheria ambayo Wadau wamekutana ili kuiboresha Sekta ya Zana za Kilimo, yana nafasi kubwa ya kuongeza tija na uzalishaji mkubwa katika kilimo na kuongeza kuwa ni vyema Wataalam wakijikita katika kutoa maoni na michango mizuri itakayochangia katika kuboresha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikati akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chisawilo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo sambamba na Wadau wa Zana za Kilimo mara baada ya kuufungua mkutano huo jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Zana za Kilimo Wizara ya Kilimo, Mhandisi Joseph Lubilo akitoa maelezo ya utangulizi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe aliyevaa koti la kahawia katikaki akiwa pamoja na Mhandisi Peter Chiswalo kulia kwake ambaye alikuwa Mwenyekiti wa mkutano huo, jana katika ukumbi wa Mvuvi House, Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA WOTE KUSHIRIKI KATIKA KUIMARISHA UTAWALA BORA ILI KUTOA MCHANGO KATIKA MAENDELEO YA TAIFA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika kuzungumza na wadau wa maadili na haki za binadamu, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika, akizungumza na wadau wa maadili na haki za binadamu wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa, jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa wakimkabidhi zawadi  Mlezi wa Klabu ya Maadili wa shule ya Sekondari Dodoma, Mwalimu Marco Benedict Magwa,  mara baada ya kuzindua maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa,  jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kapt (Mst) George Mkuchika akisoma Kauli Mbiu ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu Kitaifa mara baada ya kuzindua rasmi siku hiyo jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa.
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images