Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MKUU WA WILAYA TARIME AANZISHA MICHEZO ILI KUTETEA UHURU WA MTOTO WA KIKE

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiongea na wachezaji jana timu ya Veterans Tarime pamoja na timu ya Halmshauri ya mji wa Tarime katika uzinduzi rasmi wa bonanza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga akiwa na wadau wa michezo wakitazama mpira katika viwanja vya chuo cha ualimu TTC Mjini Tarime Mkoani Mara jana.

Na Frankius Cleophace Tarime

Mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga ameanzisha bonanza la Michezo mbalimbali huku kauli mbiu ikiwa ni kutetea na kulinda haki za  mtoto wa kike  ambapo timu 12 za mpira wa miguu kwa wanaume zinashiriki pia na timu Nne za Wanawake zinashiriki mpira wa miguu  katika viwanja vya Chuo cha Ualimu TTC Mjini Tarime.

Luoga amesema kuwa katika wilaya ya Tarime mwanamke amekuwa hakinyimwa uhuru pamoja na mtoto wa kike hivyo kupitia michezo hiyo mashirika na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia watatumia michezo hiyo ili kutaoa elimu juu ya madhara ya ukatili ili kulinda na kutetea mtoto wa kike wilayani Tarime Mkoani Mara.

“Michezo hii kilele chake ni tarehe tisa Desemba mwaka huu siku ya Uhuru hivyo nimetumia siku hiyo ya uhuru ili kulinda na kutetea uhuru wa mtoto wa kike hapa Tarime bado mtoto wa kike  hajapata uhuru  pia michezo yote itakuwepo kama vile kukimbia, kilometa ndefu na fupi, Mpira wa pete, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku katika viwanja vya chuo cha ualimu alisema Luoga”.

Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameongeza kuwa Michezo hiyo itaboresha mahusiano baina ya Jamii na watumishi wa serikali katika wilaya ya Tarime kwani nao wanashiriki Michezo hiyo.

Jovitus Alphonce ni afisa miradi kutoka shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto CDF Tarime  amesema kuwa wao kama shirika wanaendelea kushirikiana na serikali kulinda na kutetea haki za mtoto wa kike hivyo kupitia Tamasha hilo la michezo wao kama wadau wataendelea kupinga ukatili.

Alphonce ameongeza kuwa wanatumia siku 16 za kupinga ukatili kutoa elimu pia kupitia michezo hiyo kwa kuwa pia mwaka huu ni wa ukeketaji hivyo lazima watumie mbinu zote ili kuokoa mtoto wa kike.

 Kwa upande wake  Shaban Shaban kutoka Shirika la Plan Intertaniona akieleza jinsi amabvyo wanatumia michezo kufikisha ujumbe amedai kuwa michezo imekuwa ikikusanya watu wengi hivyo kupitia mikusanyiko hiyo wanatoa elimu ya kupinga ukatili wa aina zote ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike na kuhakikisha wanamlinda mtoto huyo  ili aweze kupelekwa shule ili kutimiza ndoto zake za kimasomo.

Katika uzinduzi wa Mashindano hayo Tarime Veteran imeminyana vikali na Timu ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ambapo Timu ya Halamshauri ya Mji wa Tarime imeibuka kidedea kwa kuilaza timu ya veterans kichapo cha bao 4-2.

SERIKALI YAOMBWA KUWEKA JICHO LA PEKEE KUNUSURU ZAO LA NGOZI

$
0
0
Umoja wa Wataalam Wasaidizi Tanzania (TAVEPA), umeiomba Serikali kuweka mkakati wa makusudi wa kunusuru zao la ngozi kwa kuwa sasa hivi hakuna soko la uhakika la zao hilo.
Mwenyekiti wa (TAVEPA) Bw. Salim Msellem, alisema hayo leo (03.12.2018) Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa wataalam wasaidizi wa afya ya mifugo nchini.

“Ngozi nyingi hutupwa, kitu ambacho kinaletea hasara taifa kwa kukosa fedha za kigeni, pia kudhoofisha uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja wa ngozi hapa nchini,” alisema Bw. Msellem. Alisema pia lazima kuwe na mkakati wa dhati wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kuchakata ngozi utasaidia kunusuru zao la ngozi.

Akizungumzia uwezo mdogo wa wahitimu wa stashahada ya afya na uzalishaji mifugo (DAHP), alisema, TAVEPA imepata malalamiko toka maeneo mbalimbali ya nchi kuhusu suala hilo. “Wahitimu wa DAHP imebainika muda wa mwaka mmoja wa masomo ya stashahada ya afya ya Mifugo (DAHP) hautoshi, ombi letu tunaomba stashahada iwe kama awali, ya miaka miwili au miaka mitatu na msisitizo uwe mafunzo kwa vitendo ili kumuandaa mhitimu kufanya kazi kwa ufanisi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Kwa sasa inaonekana wanasoma kwa ajili ya kwenda vyuo vikuu na siyo kwenda kuwasaidia wafugaji kule vijijini, hakika uwezo wao kwa vitendo ni mdogo sana,” alisema Bw. Msellem. Aidha umoja huo umeiomba serikali kuandaa mkakati wa dhati wa kusimamia mafunzo rejea kwenye tiba, matumizi sahihi ya dawa, ukaguzi wa vyama, ubora wa ngozi na ubora wa wanyama wanaotaka kuchinjwa kwa watumishi wa umma na sekta binafsi mara kwa mara ili kuwajengea uwezo.

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Mifugo (TVA), Prof. Dominic Kambarage, alisema Tanzania ina ng'ombe wengi na inauza ng'ombe hizo nchi mbalimbali za Afrika Mashariki hivyo ni vyema wafugaji wakachangamkia Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Prof. Kambarage alisema ni vyema sasa wafugaji wakapewa elimu ya kutosha pamoja na upatikanaji wa chanjo za mifugo ili kudhibiti magonjwa pamoja na kupata masoko ya uhakika ili kila mtu anufaike na rasilimali hiyo.  "Sekta ya mifugo ni sekta muhimu katika ukuaji wa uchumi na Tanzania ni ya pili Barani Afrika kwa kuwa na mifugo mingi, hivyo mifugo hiyo ikitumika vyema itasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuongeza kipato, " alisema.

Naye Msajili wa Baraza la  Veterinari (VCT) nchini, Dkt. Bedan Masuruli, alisema ni vyema kudhibiti magonjwa yatokanayo na mifugo kwani asilimia 70 ya magonjwa ya kupe yanaua mifugo hivyo ni vyema wafugaji wakaogesha mara kwa mara mifugo yao ili kudhibiti ugonjwa wa kupe.
 Prof. Dominic Kambarage akitoa maelezo juu ya umuhimu wa sekta ya mifugo nchini kwa wanachama wa Umoja wa Wataalam Wasaidizi Tanzania (TAVEPA) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa wataalam wasaidizi wa afya ya mifugo nchini uliofanyika Jijini Arusha.
Wanachama wa TAVEPA wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi   (Hayuko pichani).

MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NCHI YA FALME ZA KIARABU NCHINI

$
0
0
Balozi  wa  Nchi  ya  Falme  za  Kiarabu  hapa  nchini, Khalifa  Abdulrahman Mohamed  Al- Marzooqi (kushoto),  akizungumza  na  Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya  Nchi ,Mhandisi  Hamad  Masauni  kuhusu ushirikiano wa nchi  hizo  mbili katika  masuala ya Ulinzi na Usalama, baada  ya  kumtembelea  katika  Ofisi Ndogo  za  wizara  hiyo, jijini  Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Ubalozi huo, Saddam Ahmed Ally.
Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi   Hamad Masauni (kulia),  akizungumza  na  Balozi  wa  Nchi  ya  Falme  za  Kiarabu  hapa  nchini, Khalifa  Abdulrahman  Mohamed  Al- Marzooqi (kushoto)   kuhusu ushirikiano wa nchi  hizo  mbili katika  masuala  ya  Ulinzi  na  Usalama, baada  ya  kumtembelea  katika  Ofisi  Ndogo  za  wizara  hiyo,  jijini  Dar es Salaam. Katikati   ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Ubalozi huo, Saddam Ahmed Ally.
Balozi  wa  Nchi  ya  Falme  za  Kiarabu  hapa  nchini, Khalifa  Abdulrahman Mohamed  Al- Marzooqi  akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Ofisi  Ndogo  za  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya  Ndani  ya  Nchi, Mhandisi Hamad  Masauni (kushoto), jijini  Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.SHEIN AZUNGUMZA NA MWAKILISHI MKAAZI WA (WHO) NCHINI TANZANIA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Dkt. Tigest Ketsela Mengestu, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo 4/12/2018, kushoto kwa Rais, Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed, anayefuata  Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania, Dkt. Tigest Ketsela Mengestu, alipofika Ikulu Zanzibar leo, 4/12/2018 kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiongozana na mgeni wake Mwakilishi wa Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Nchini Tanzania Dkt. Tigest Ketsela Mengestu, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo, 4/12/2018.

Ofisi ya Makamu wa Rais Kuwa Mfano Utunzaji Mazingira Mji wa Serikali

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba akisalimiana na Mkurugenzi wa Mazingira toka Ofisi hiyo, Profesa. William Mwegoha alipotembelea eneo zinapojengwa Ofisi za Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma leo tarehe 4, Desemba, 2018. Katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (katikati) akiteta jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Sima (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph Malongo wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya hatua za awali za ujenzi wa Ofisi za Makamu wa Rais zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma leo tarehe 4, Desemba, 2018. 
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akimuonyesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (mwenyeshati ya njano) eneo lenye ukubwa wa ekari 8 katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma zinapojengwa Ofisi za Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira leo. Wapili kutoka kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Sima.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba akielezea jambo alipokuwa akitazama mandhari ya eneo linalojengwa Ofisi za Makamu wa Rais alipofanya ziara katika eneo hilo lililopo Ihumwa jijini Dodoma leo.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira wakimskiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya hatua za awali za ujenzi wa Ofisi za Makamu wa Rais zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa jijini Dodoma leo tarehe 4, Desemba, 2018. 
Pichani kiwanja cha ukubwa wa ekari 8 ambacho panajengwa Ofisi za Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kikiwa kimefanyiwa usafi tayari kwa kuanza ujenzi wa ofisi hizo. (Picha na: Frank Shija - MAELEZO, Dodoma)

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAWATAKA WAAJIRI NCHINI KUWAPATIA HUDUMA STAHIKI WATUMISHI WA UMMA WENYE ULEMAVU

$
0
0
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imetoa wito kwa waajiri nchini, kuwapatia huduma stahiki watumishi wa umma wenye ulemavu kwa mujibu wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008 kwa lengo la kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma. Bi. Mwaluko amesema, walemavu kama walivyo binadamu wengine, wana wajibu wa kutoa mchango katika maendeleo ya taifa, hivyo ni wajibu wa waajiri wote nchini kuwapatia huduma zinazostahili ili waweze kutimiza wajibu wao.
Bi. Mwaluko amefafanua kuwa, watumishi wa umma wenye ulemavu hawana tofauti na watumishi wengine isipokuwa wana mahitaji yao ya msingi ambayo usipowapatia yanakwamisha utendaji kazi wao, hivyo waajiri hawana budi kuzingatia mahitaji ya kundi hilo ambalo baadhi ya waajiri hulisahau. Kwa upande wake, Mratibu wa Dawati la Watumishi wenye Ulemavu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Elibariki Funga Kahungya amesema, Ofisi kama msimamizi wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008, inawawezesha watumishi sita waliopo wenye ulemavu kupata huduma muhimu kama mwongozo unavyoelekeza ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akifungua kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi Mkurugenzi wa Sera, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bi Agnes Meena, Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa mwaka 2008  ili aweze kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa mwongozo huo katika taasisi za umma nchini.
Afisa Tawala Mkuu, Ofisi ya Rais, Utumishi,  Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika utumishi wa umma wakati wa kikao kazi  cha Watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi baada ya kufunga kikao kazi cha kuadhimisha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi hiyo jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

JICHO LA MICHUZI BLOG MTAANI LEO

$
0
0
Bodaboda na waenda kwa miguu wakiwa wamesongamana katika barabara ya mabasi ya mwendo kasi,eneo la Kariakoo jirani na makutano ya barabara ya Msimbazi na Uhuru, jijini Dar es Salaam leo. Hali imekuwa ikileta usumbufu kwa madereva wa mabasi hayo na pia kuchangia ajali za barabarani, zinazotokea mara kwa mara katika eneo hilo. Picha na Joseph Zablon.

WAZIRI MKUU MSTAAFU DKT SALIM ATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA MSIBA WA RAIS WA ZAMANI WA MAREKANI

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) Dr Salim Ahmed Salim leo asubuhi ametembelea ubalozi wa taifa la Marekani kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Marekani kutokana na msiba wa Rais wa 41 wa taifa hilo Bwana George W. H Bush. 
 

Mheshimiwa Salim ni mmoja wa watanzania wachache waliopata nafasi ya kufanya kazi na kumjua Marehemu Bush Snr wakati Mheshimiwa Salim alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Rais Bush Snr akiwa Mwakilishi wa Kudumu wa Taifa la Marekani .

Moja ya mambo yaliyowakutanisha ni pamoja na harakati na hatimaye tukio la Taifa la China kurejeshewa haki na hadhi yake ya Uanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1971.

Pichani Mheshimiwa Salim akipokewa na Kaimu Balozi wa Marekani Bwana Andy Karas na Naibu Kaimu Balozi Bwana Brian Rettmann.

CGP KASIKE AFUNGUA MKUTANO WA WANGANGA WAKUU WA VITUO VYA AFYA VYA MAGEREZA NCHINI LEO DESEMBA 4, 2018

$
0
0
Na ASP Deodatus Kazinja, Dodoma.
Wataalam wa  afya wa vituo vya magereza nchini wameaswa kufanya kazi kwa weledi na juhudi kubwa ili kutimiza malengo yanayotarajiwa na jeshi la magereza na taifa kwa ujumla. Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Phaustine Kasike wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku moja wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya Jeshi la Magereza uliofanyika katika Ukumbi wa Morena Hoteli leo jijini Dodoma.
Aidha, CGP Kasike amemuagiza Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza kufuatilia kwa ukaribu utendaji wa kituo kimoja kimoja na kuhakikisha wataalam waliopo jeshini wanafanya kazi zao kwa uweledi ikiwa ndiyo matarajio ya jeshi. Wakati huo huo CGP amewatolea wito wataalam hao wa afya magerezani kuhakikisha wanatekeleza muongozo wa serikali unaoagiza kuwaanzishia dawa watu wote wanaogundulika kuwa na maambukizi ya VVU na kuhakikisha wanakuwa na ufuasi mzuri wa dawa.
Waganga wakuu wa vituo vya afya katika Jeshi la magereza wapo katika mkutano huo  unaofadhiliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  ukiwa na lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18. Asasi ya JSI AIDS Free chini ya serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Wziara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa miaka minne sasa imekuwa ikishirikia na Jeshi la Magereza katika kuboresha Huduma za Afya hasa mapambano ya Ukimwi.
Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akisalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa Asasi ya kiraia ya JSI AIDS Free mara alipowasili leo Desemba 4, 2018  katika viwanja vya Morena Hotel jijini Dodoma kwa ajili ya ufunguzi wa kikao cha siku moja cha kutathmini ya mwenendo  wa  Mradi wa Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18.
 Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike akitoa hotuba katika mkutano wa waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza yote nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya kutathmini ya mwenendo wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 leo Desemba 4, 2018 Morena Hoteli jijini Dodoma.  Kushoto ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Omary Salum, Mtendaji Mkuu wa AIDS Free Tanzania Dkt. Deogratias Kakiziba. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Jeshi la Magereza INSP Adili Kachima na wapili kulia  ni SSP Dkt. Richard Mwakina kutoka kituo cha afya chama magereza Ukonga, Dar es salaam.
Washiriki wa kikao wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) katika kikao cha waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza nchini kilichoandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free  kwa ajili ya ufuatiliaji wa mwenendo  wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya polisi na magereza kwa mwaka 2017/18 kilichofanyika leo tarehe 04 Desemba, 2018 jijini Dodoma.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Gereza Kuu Butimba Mwanza ASP. Dkt.  Alex Lukuba akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi (CGP Kasike) ikiwa ni utambuzi wa kufanya vizuri kwa kituo anachokisimamia katika kusimamia masuala yahusuyo Ukimwi katika kituo chake. 
Kamishna Jenerali wa Magereza  (CGP) Phaustine Kasike (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waganga wakuu wa vituo vya afya vya magereza kote nchini na watendaji wakuu wa Asasi ya isiyo ya kiserikali ya JSI AIDS Free ambayo ndiyo wafadhili wa Mradi Uimarishaji wa Huduma za Ukimwi katika vituo vya afya vya Magereza na polisi nchini. (Picha zote na Jeshi la Magereza)

Halotel, Biko kunogesha michezo msimu wa sikukuu.

$
0
0

      Na.Khadija seif,globu ya jamii

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel nchini  imeingia katika makubaliano rasmi na kampuni ya michezo ya kubahatisha na kubashiri ya Biko ili kuongeza msisimko na ushiriki kwa wadau wa michezo hiyo nchini katika msimu wa huu sikukuu.

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Ofisi za Halotel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda amesema ushirikiano huu baina ya Kampuni ya Halotel na Biko utawezesha wateja wetu kuweza kushiriki na kupata fursa ya kujishindia fedha zitazowawezesha kujiongezea kipato na hivyo kuboresha maisha yao.

Pia ameeleza kuwa hii ni fursa kwa wateja  wote wa Halotel mijini na vijiini kuweza kushiriki katika michezo ya kubahatisha na kubashiri kama vile mpira wa miguu , mpira wa kikao,rugby,cricket,Tennis na mingineyo ambapo hapo kabla hawakuweza kupata fursa kushiriki katika michezo hiyo.

Kwa upande wake Meneja Masoko Biko Goodhope Heaven  amefafanua kuwa Biko ni kampuni kubwa na madhubuti inayojihusisha na michezo ya kubahatisha kwa kufanya miamala Kwenye simu za Mkononi.

Aidha heaven ameeleza ushirikiano huo utawezesha wateja wanaotumia mtandao wa Halotel kupitia huduma ya kifedha ya Halopesa kupata fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko kwa kubahatisha na pia kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali na Bikosports.

Biko inaendelea kusisitiza wabashiri kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea na mpaka sasa watu waliobashiri na kubahatika kushinda wameneemeka kwa kutokana na kushinda zawadi za fedha,pikipiki na nyuma aliongezea  heaven.
 Mkuu wa mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda  akizungumza na waandishi wa Habari jinsi mteja wa Halopesa anavyoweza kujiunga na kushiriki katika michezo ya kubashiri inayoendeshwa na kampuni ya Biko. Pamoja nae kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven (kulia) na Mkuu wa Biashara wa Halopesa Magesa Wandwi.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven, akizunguzumza na  waandishi wa Habari  jinsi mteja wa Halotel  anavyoweza kushiriki mchezo wa bahati nasibu ya biko na kupata nafasi ya kushinda Nyumba na Mamilioni ya Biko katika msimu huu wa sikukuu (kulia) ni Mkuu wa mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda (kushoto).

ITC YA OBREY CHIRWA YATUA, TAYARI KUITUMIA AZAM FC

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa Klabu ya Azam umeweka wazi kuwa usajili wa mshambuliaji mpya Obrey Chirwa umekamilika  kwa asilimia 100 baada ya Chama cha Soka nchini Misri (EFA) kuiachia Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa kuituma kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Nurdin Amin ‘Popat’, amesema kuwa tayari kibali hicho kimeshatumwa TFF na sasa wanachosubiri ni kukamilika kwa vibali vyake vya kufanya kazi nchini pamoja na leseni itakayomwezesha kucheza soka nchini.


EFA imeachia ITC yake baada ya Nogoom FC kuithibitishia kuwa wameachana na mchezaji huyo na yupo huru kujiunga na timu yoyote, ambapo wiki chache zilizopita Azam FC ilimaliza taratibu za kumuhamisha kwa kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja.


“Tunamshukuru Mungu jana jioni TFF imetupa taarifa ya kupokea ITC ya Chirwa kutoka Misri alipokuwa akicheza awali, hataweza kuiwahi mechi ya leo kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza ligi na kibali chake cha kufanya kazi kutokamilika, tunatarajia atacheza mechi ijayo ya Ijumaa dhidi ya Mbao,” alisema.

WAKILI MWAE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 5 AU KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 200

$
0
0

NaVero Ignatus ,Arusha

Hukumu ya kesi ya utakatishaji fedha haramu iliyokuwa inamkabili wakili maafuru Jijini Arusha Mediam Mwale imetolewa desema 3 na Jaji Isa Maige wa Mahakama kuu kanda ya Arusha ambapo amemuhukumu kwenda jela miaka mitano au kulipa faini ya shilingi milioni 200

Mshtakiwa analazimika kulipa faini na kama akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitano na kwa kipindi ambapo atakuwa hajakidhi matakwa ya adhabu hiyo atabaki kizuizini

Jaji Isa ameiambia mahakama kuwa mshitakiwa Mediam Mwale amekiri makosa kwa hiari yake mwenyewe na kwamba hiyo ni dalili tosha ya kuwa ameungama na anajutia makosa na kukiri kwake kuna faida mbili katika mfumo mzima wa haki jinai mshtakiwa ameokoa muda na rasilimali za mahakama

Ameiambia mahakama kuwa kukiri kwa mshtakiwa wakwanza kumeondoa uwezekano kukwepa kwa njia za kiufundi hayo ameyazingatia kwani mshtakiwa ni kosa lake la kwanza siyo mkosaji sugu asiyeweza kurekebishika, kuungama kwake kunaonyesha kuwa yupo tayari kujirekebisha

''kwa minajili hiyo muelekeo wa wa kujirekebisha ni hatua stahiki katika kutoa adhabu hiyo''''Mshtakiwa amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miaka saba tangia alipokamatwa kama mambo yote yangeenda katika hali ya kawaida si ajabu kwamba mshtakiwa wa kwanza angelikuwa ameshahukumiwa na kutuikia kifungo cha zaidi ya miaka saba'' alisema Jaji Maiga

Akisoma hukumu hiyo Jaji Issa Maige Mahakama kuu kanda ya Arusha adhabu makosa 30 yanaomkabili mshatakiwa wa kwanza ambayo ni makosa ya kughushi kinyume na kifungu namba 337 kwa ambapo adhabu yake kifungo cha miaka 5 kwa kila kosa ,kughushi kinyume na kifungu namba 338 adhabu yake miaka 7

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MICHAEL WAMBURA ARIPOTI TFF NA BARUA YA MAHAKAMA

$
0
0
Baada ya Mahakama Kuu kumrejesha kwenye nafasi yake ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Michael Wambura Novemba 30, leo amewasili ofisini hapo kuripoti kwa mujibu wa Mahakama Kuu.

Wambura amesema kuwa majukumu yake aliyopewa na Mahakama Kuu ameyatekeleza hivyo kwa sasa yeye ni Makamu wa Rais wa TFF kwa kuwa hakufutwa cheo chake bali alifungiwa kutojihusisha na masuala ya soka. 

"Ofisini wengi nimekuta hawapo zaidi ya mkurugeni wa fedha, na wahudumu wengine wa chini, ila kikubwa nimeweza kutimiza masharti ya Mahakama ambayo kwanza ni kuripoti ofisini, pili naleta taarifa ya mahakama ambayo imepokelewa na nimeweza kufika, kama utekelezaji hautafanyika basi nitarejea mahakamani. 

"30 Novemba nilianza kazi baada ya mahakama kuu ilipotoa maagizo, cha msingi ni kwamba nilikuja kutoa taarifa kwamba mimi nipo, walinisimamisha kujihusisha na soka ila hawakufuta cheo changu cha umakamu wa rais," alisema. 

Machi mwaka huu Kamati ya Maadili ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni ilimfungia maisha Wambura kutojihusisha na masuala ya soka kwa kumtuhumu kwa makosa matatu. Katika taarifa yake, TFF ilisema kwamba ilichukuwa hatua hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. 

WAZIRI HASUNGA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO KUMSIMAMISHA KAZI MTUMISHI MMOJA KWENYE TIMU YA OPARESHINI KOROSHO

$
0
0

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe kumsimamisha kazi mtumishi George Mboje na kumuondoa kwenye timu ya Operesheni Korosho.

Pamoja na kumundoa kwenye timu hiyo pia Katibu Mkuu ametakiwa kumuondoa kwenye Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko."Katibu Mkuu, nataka umuondoe huyu George kwenye hii timu na pia sitaki kumuona kwenye Bodi na Taasisi yoyote katika Wizara ya Kilimo" Alisisitiza Mhe Hasunga .

Mhe Hasunga ametoa agizo hilo leo tarehe 4 Disemba 2018 wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Watendaji wa timu ya Oparesheni korosho kilichofanyika katika ukumbi wa CBT Mkoani Lindi na wakati wa kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018.

George Mboja ambaye yupo kwenye timu ya Oparesheni Korosho akiwakilisha Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko anatuhumiwa kwa Utovu wa nidhamu sambamba na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo wakati wa Oparesheni Korosho inayoendelea nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo. (Picha Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Sarah Chiwamba, Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe Christopher Ngubiagai wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akizungumza kwenye kikao kazi na watendaji wa serikali sambamba na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Lindi katika ziara yake ya kikazi aliyoianza leo tarehe 4 Disemba 2018 mkoani humo.

RAIS DKT.SHEIN AZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA UNICEF NCHINI TANZANIA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Bi. Maha Damaj, Mkuu wa Shirika la Mfuko wa Umoja wa Mataifa Unaoshughulikia Maendeleo ya Watoto (UNICEF) Ofisi ya Zanzibar, alipofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha kwa Rais wa Zanzibar leo ,4/12/2018.(Picha na Ikulu )
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania,Bi.Maniza Zaman,(katikati) alipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mkuu wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar Bi. Maha Damaj,kwa Rais wa Zanzibar, leo Ikulu 4/12/2018 na kufanya mazungumzo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na wageni wake kutoka Shirika la la Mfuko wa Umoja wa Mataifa Unaoshughulikia Maendeleo ya Watoto (UNICEF) katikati Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Bi. Maniza Zaman na Mkuu Mpya wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar Bi. Maha Damaj, alipofika Ikulu Zanzibar kutambulishwa kwa Rais wa Zanzibar leo 4/12/2018.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mwakilishi wa UNICEF Nchini Tanzania Bi. Maniza Zaman, alipofika Ikulu Zanzibar kumtambulisha Mkuu wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar, Bi.Maha Damaj, kwa Rais wa Zanzibar. (Picha na Ikulu)

DKT. MABODI AWATAKA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA KUWA KARIBU NA WANANCHI

$
0
0
Na Is-Haka Omar, Zanzibar
WATENDAJI wa Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kufanya ziara za kiutendaji kwa wananchi wa ngazi zote ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zinazowakabili wananchi. Rai hiyo ameitoa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi katika mwendelezo wa ziara zake za kukagua utekelezaji wa Ilani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja.

Amesema lazima watendaji na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia mfumo wa ugatuzi washuke kwa wananchi kwa lengo la kufuatilia masuala mbali mbali yatakayosaidia kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi katika ngazi za serikali za mitaa. "Lengo la Serikali Kuu kushusha madaraka katika Serikali za Mitaa kupitia dhana ya ugatuzi ni kuongeza ufasini wa uimarishaji wa huduma za kijamii kwa wananchi, hivyo watendaji nyote mlioaminiwa na kupewa dhamana ya kuwahudumia wananchi lazima muwe katibu na jamii", amesisitiza Dk.Mabodi.

Katika maelezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo, amewataka wamewasihi watendaji hao kuwa wabunifu katika kuibua miradi mbali mbali ya kijamii inayoweza kuongeza ufanisi wa kutoa huduma bora kwa wananchi. Pia Dk. Mabodi kupitia ziara yake hiyo ameelezea kuridhishwa kwake na utendaji mzuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini 'A' katika kutekeleza vizuri miradi inayotekelezwa kupitia ugatuzi.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kaskazini 'A' katika mwendelezo wa ziara yake katika Mabaraza ya Manispaa na Halmashauri za Wilaya Unguja.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akionyesha moja ya ripoti za ukaguzi wa miradi ya mfuko wa maendeleo wa majimbo huku akisisitiza uwajibikaji na uwazi juu ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Wabunge na Wawakilishi Zanzibar.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akiwa na wananchi wa shehia ya Mbuyu Tende wakielekea kukagua mradi wa umeme na maji katika kijiji cha Zingani.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla Mabodi akigagua mashine ya kukoboa mpunga aina ya G-20 inayomilikiwa na kikundi cha ushirika wa 'Nguvu kazi tusizembee' huko Shehia ya Kisongoni Wadi ya Kinyasini Unguja.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

LSF yazindua kampeni ya upatikanaji wa huduma ya bure za msaada wa kisheria

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk amesema wananchi wengi wanashindwa kupata huduma za msaada kisheria kutokana na kukosa uelewa wa kupata watoa huduma za msaada wa Kisheria. Groenendijk ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la "Siyo Tatizo" inayolenga  kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusiana uwepo wa upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa Kisheria , amesema jamii imezungukwa na matatizo yanayotokana na kukosa msaada wa kisheria na kufanya kukosa haki zao.

Groenendijk amesema Kampeni hiyo ni kuongeza ngumu  ya uelewa kwa jamii juu ya upatikanaji wa huduma ya bure za msaada wa kisheria zitolewazo na wasaidizi wa kisheria. "LSF Tanzania kwa dhati inalenga kuleta unafuu  zaidi  hasa kwa wanawake wenye hali ngumu  ambao haki zao za msingi zimepewa zikifinywa au kukosekana kutokana na sababu mbalimbali hali hiyo imechangiwa zaidi na ukosefu wa usaidizi wa kisheria" amesema Groenendijk. Amesema kuwa kampeni hiyo watawafikia wananchi wote katika kampeni hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk akizungumza na waandishi habari wakati wa uzinduzi wa Kampuni  ya Siyo Tatizo Tena ya upatikanaji wa huduma za bure za  msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Miradi wa LSF Scholastica Tully akizungumza kuhusiana kampeni ya kutoa huduma kuhusiana na upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo  iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas akizungumza kuhusiana na kutoa elimu ya upatikanaji wa huduma za bure za msaada wa kisheria katika uzinduzi wa LSF iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Lameck Ditto 'Dogo Ditto' akizungumza jinsi atavyohamasisha kuhusiana na kampeni ya kutoa huduma za bure za msaada wa kisheria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Kees Groenendijk(wa kwanza kulia) akipeana mkono na Balozi wa Kampeni ya Huduma za bure za msaada wa kisheria Mwasiti Almas wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya inayojulikana  kwa jina la Siyo  inayohusuUpatikanaji wa Huduma za bure za msaada wa kisheria iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam

Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, imesaini mkataba wa Bilioni 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo litakalojengwa na wakala wa Majengo Nchini (TBA). Akizungumza wakati wa utiaji saini ujenzi wa jengo hilo la Utawala leo jijini Dar es Salaam, Meya Jacob amesema ni matarajio yake ujenzi huo utakamilika kwa wakati kama walivyopanga katika kuondokana na ofisi za kupanga

Amesema Serikali Kuu ilitoa mwongozo wa kuhakikisha wanawatumia TBA katika mradi huo lakini angekuwa yeye binafsi angependekeza kushindanisha wakandarasi kadhaa wakiwamo Suma JKT ili kupata mkandarasi mwingine. "Naomba nitoe tahadhali kwa TBA mkajipime kabl hamjaanza ujenzi huu kwani mkionyesha kusuasua mimi ndio ntakuwa wa kwanza kulalama kwa vile wadau wetu wa pili wa mradi huu ambao ni Serikali wamewateua nyie mjitahidi msiwaangishe ili kuendelea kuwa na imani na nyie" amesema Jacob.

Aliweka  angalizo hilo kwa sababu ya historia fupi ya TBA kwenye baadhi ya mikoa ambapo wameshindwa kutekeleza mikataba na kusababisha mingine kunyang'anywa. "Tumeskia huko mikoani baadhi ya miradi mliporwa kwa sababu ya uzembe wa watendaji wenu wa huko lakini kwa hapa Dar ea Salaam hamjapata kashfa hiyo hivyo naomba mjipange vyema katika mradi huu kwa kufanya kuwa na jengo,"alisema Jacob.
 Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai(kulia) na  Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey(kushoto) wakibadilishana hati za  makubaliano ya ujenzi  ofisi ya manispaa hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)
Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza na waandishi habari mara baada kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA)  Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey.
TBA na Manispaa ya Ubungo wakisaini Mkataba ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai akizungumza na waandishi habari namna waliyojiwekea mazingira ya ujenzi wa Manispaa hiyo wakati wa kuliliana saini na TBA.
Picha ya pamoja ya watendaji na Manispaa ya Ubungo na TBA na baadhi ya Madiwani

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa kufanya malipo kwa kutumia Mfumo wa Kielekroniki wa Malipo Serikalini (GePG)

$
0
0
Wateja wa Kampuni ya Tigo wa mikoa ya Kanda Ziwa sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa. 

Akiongea katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Mecky Manyama alisema mfumo wa GePG umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi na kuongeza kuwa umeleta faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza ubadhirifu na kuongeza mapato kwa idara mbali mbali na taasisi za Serikali 

“Mfumo wa GePG, pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali ikiwa ni pamoja na za kutoka MWAUWASA. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufurahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao.,” alisema Manyama 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo mkakati yetu,” alisema Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthuman Madatti 
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akionyesha namna ya kutumia simu ya kiganjani kufanya malipo, wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti.

 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG)uliofanyika jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Meck Manyama (kulia), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) , wakati wa uzinduzi wa  Mfumo wa Kielektronic wa malipo ya serikali (GePG), ambao utatumika kufanya malipo kwa taasisi zaidi ya 300 za Serikali kwa kutumia mtandao wa Tigo.Anayefuatia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Uthumaan Madatti na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo Ally Maswanya.



WANANCHI WA LINDI, PWANI KUPATA MAWASILIANO YA UHAKIKA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amewahakikishia wananchi wa baadhi ya vijiji ambavyo havina mawasiliano mkoani Lindi na Pwani kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inahakikisha kuwa wananchi waishio kwenye vijiji hivyo wanapata huduma za mawasiliano ya uhakika

Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kukagua changamoto za hali ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya Liwale, Lindi Vijijini, Mtama, Kibiti na Rufiji kwenye mkoa wa Lindi na Pwani baada ya kupata kilio kutoka kwa wabunge wanaowakilisha wanananchi wa maeneo hayo wakati wa kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania cha mwezi Novemba mwaka huu

Amesema kuwa Sekta ya Mawasiliano ni sekta inayoshika nafasi ya pili kwa kuchangia pato la taifa katika kipindi cha mwaka 2016/2107 kwa kiwango cha asilimia 13.1 ambapo mawasiliano yana changui kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu na mawasiliano ndiyo kila kitu. “Wananchi mkiwasiliana kwa kununua vocha, kupiga simu na kutumia intaneti, Serikali inatoza kodi kidogo, ambayo wala haiumizi na wala mwananchi hausikii, lakini Serikali inapata mapato yake,” amesema Nditiye.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye akifafanua jambo kwa wananchi wa kijiji cha Chihuta, Mtama mkoani Lindi kuhusu upatikanaji wa huduma za mawasiliano wakati wa ziara yake mkoani humo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (alyeinua mikono) akijadiliana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sara Chiwamba kuhusu upatikanaji wa mawasiliano kwenye kata ya Marui wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua ukosefu wa mawasiliano. Wa kwanza kulia mwenye kofia nyeupe ni Mbunge wa jimbo hilo Zuberi Kuchauka.
 Wananchi wa kijiji cha Chihuta, Mtama mkoani Lindi wakimuonesha Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Nditiye (hayupo pichani) namna wanavyotega mawasiliano kwenye simu zao wakati wa ziara yake ya kukagua changamoto za mawasiliano mkoani humo.
Wananchi wa kijiji cha Marui, Wilaya ya Liwale mkoani Lindi wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua changamoto za upatikanaji wa huduma za mawasiliano mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>