Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

MAHAFALI YA 12 YA CHUO KIKUU ARDHI (ARU) YAFANA

$
0
0
 

Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Ardhi, Profesa Evaristo Liwa akimkaribisha Mkuu wa Chuo, Mhe Cleopa David Msuya kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyfanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Cho, Balozi Costa Kahalu na viongozi waandamizi wa ARU. (Imeandaliwa na Robert Okanda) .
Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo, Balozi Costa Mahalu akitoa hotuba yake wakati wa kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Jumla ya wahitimu 974 wa shahada mbalimbali walitunukiwa stahili zao.

Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi, Mhe. Cleopa David Msuya akimtunuku Samweli Sanga Digrii ya uzamivu (Doctor of Philosophy) ya ARU wakati wa kuhudhurisha mahafali ya 12 ya chuo Kikuu Ardhi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 1. 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la Chuo, Balozi Costa Kahalu na Makamu Mkuu wa ARU, Profesa Evaristo Liwa. Jumla ya wahitimu 974 wa shahada mbalimbali walitunukiwa stahili zao.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

MAHAFALI CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI MUHIMBILI (MUHAS) YAFANA JIJINI DAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu MUHAS, Profesa Andrea Pembe. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Andrea Pembe akisoma hotuba yake wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Bi. Mariam Mwaffisi.
Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wahitimu waliotunukiwa astashahada, stashahada, shahada za awali na shahada za uzamili wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) jijini Dar es salaam.

WANANCHI WAASWA KUITUMIA OFISI YA URATIBU WA SHUGHULI ZA SMZ

$
0
0
Wakati umefika kwa Watanzania wote kuitumia Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam ili kupata maelekezo na Ushauri utakaowawezesha kupata huduma mbali mbali zinazotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ngazi na Sekta zote.

Uamuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa kuanzisha Ofisi hiyo muhimu Mwaka 2013 kuratibu wa Shughuli za Serikali umelenga kuwaondoshea usumbufu Wananchi wanaoishi upande wa Tanzania Bara pamoja na Taasisi za Kimataifa zinazohitaji huduma za Serikali.

Mratibu Mkuu wa Ofisi ya Uratibu wa shughuli za SMZ Dar es salaam Ndugu Issa Mlingoti Ali alitoa kauli hiyo katika Kipindi Maalum cha matayarisho ya maandalizi ya sherehe za kutimia Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 hapo Ofisini kwake Mjini Dar es salaam.

Ndugu Mlingoti alisema huduma za Ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa hivi sasa zinatumiwa zaidi na Viongozi Wakuu na wale Waandamizi jambo ambalo bado halijakidhi azma ya kuanzishwa kwake licha ya kwamba yapo mambo mengi na ya msingi yanayoweza kuratibiwa ambayo yanamuhusu pia Mwananchi wa kawaida.

Alisema Ofisi hiyo kupitia Maafisa wake wa Sekta Tofauti ina mamlaka ya kusikiliza na kuyachukulia hatua matatizo yanayowakumba Wananchi sambamba na kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya ushirikiano baina ya Taasisi za SMS na zile za Tanzania Bara pamoja na za Kimataifa katika Sekta tofauti.
Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali Kushoto akisalimiana na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa huku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifurahia wakati walipofika Nyumbani kwake Dar es salaam kutambulishwa Rasmi baada ya kuteuliwa kuwa Mratibu Mkuu.
Mratibu Mkuu wa Uratibu wa Shughuli za SMZ Dar es salaam Nd. Issa Mlingoti Ali akisalimiana na baadhi ya Mabalozi wa Nchi za Nje waliopo Tanzania wakati akiwa katika ziara za kuimarisha ushirikiano kati ya Ofisi hizo za Kidiplomasia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

RAIS DKT MAGUFULI ASALIMIA WANANCHI WA MIANZINI WILAYA YA ARUSHA

POLISI YAONYA WIZI MAFUTA UJENZI RELI YA KISASA

$
0
0



Na Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanza kwa Operesheni kali ya kuwabaini na kuwasaka watu wote wanaojihusisha na wizi wa mafuta katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi wa reli hiyo katika kambi ya ujenzi ya Soga mkoani Pwani na Ngerengere wakati wa ziara yake katika mradi huo kufuatia kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mafuta.

Sabas amesema Operesheni hiyo haitamwacha salama yeyote atakayekutwa akishiriki na kufanikisha vitendo vya wizi katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao kuwa wa kwanza kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya wizi katika maeneo yao ili mradi huo uwe salama.

“Polisi tutatumia kila aina ya nguvu zetu kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa salama na tukikamata mwizi wa mafuta katika mradi huu hatasahau maisha yake yote kwa kuwa kuhujumu mradi huu muhimu kwa taifa ni kosa kubwa hasa ukizingatia gharama kubwa ambazo Serikali inatua kufanikisha jambo hili” Alisema Sabas.
Katika hatua nyingine DCP Sabas amewaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Pwani na Morogoro kuweka mikakati kabambe kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Reli ili kufanya doria za mara kwa mara katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kwa kuwa ndipo kulikobainika kuuzwa mafuta ya wizi wa mradi huo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Reli amesema wamekuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara na wadereva wa mitambo na magari katika mradi huo kwa lengo la kuwataka kushiriki katika kutoa taarifa za wizi na kuacha kujihusisha na vitendo hivyo ambapo waliokamatwa tayari wamefikishwa Mahakamani.

Homera aongoza maadhimisho ya siku ya UKIMWI kimkoa wilayani Tunduru

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera (Julia) akipokea taarifa ya mkoa kuhusu hali ya maambukizi ya UKIMWI toka kwa Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Magdalena Zenda (kushoto).Tukio hili limefanyika Leo mjini Tunduru wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI kimkoa 

 Sehemu ya wananchi wa Tunduru waliojitokeza kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI kimkoa wakiwa na mabango yenye ujumbe maalum.
Vikundi vya burudani vilivyotumbuiza kilele cha siku ya UKIMWI mkoa wa Ruvuma iliyofanyika wilaya ya Tunduru leo

DKT ABBASI AWAUNGANISHA 'LIVE' MAAFISA HABARI WA TAASISI ZA UMMA KUFAFANUA KERO ZA WANANCHI*

$
0
0
SERIKALI ya Awamu ya Tano imeendelea kutumia ubunifu katika kuwahudumia wananchi ikiwemo kujibu na kufafanua kero zao papo kwa papo.

Katika hatua isiyokuwa ya kawaida, Msemaji Mkuu wa Serikali leo akiwa ziarani mkoani Morogoro alilazimika kuwapigia simu baadhi ya watendaji wa Serikali akiwa moja kwa moja studio za Redio Abood FM na ATV ili wajibu kero za sekta zao.

Afisa wa kwanza kukumbana na "kibano" hicho alikuwa Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bw. Paschal Shelutete ambaye alipigiwa kwa mstukizo na kuunganishwa moja kwa moja studio ili ajibu swali la mwananchi aliyelalamikia tembo kutoka hifadhi mbalimbali kuvamia mashamba ya wananchi na kuharibu mazao.

Bw. Shelutete akionekana kulijua vyema eneo lake alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo Tanapa na Mamlaka nyingine za Serikali kama Idara ya Wanyamapori zimekuwa na programu za kuwaelimisha wananchi wanaokaa karibu na hifadhi na mapori ya akiba.

"Tunaendelea kuwaelimisha wananchi wahakikishe wanatoa taarifa hizi kila wanapowaona wanyama wa porini wanarandaranda katika maeneo yao ili mamlaka zichukue hatua stahiki," alifafanua akitoa maelekezo ya hatua za kufuatwa.

PROFESA JAY AZUNGUMZIA MRADI WA SGR


RELI TV: TAZAMA MUONEKANO WA STESHENI ZA TRENI YA MWENDO KASI ZITAKAVYO KUWA NI MFANO WA KUIGWA AFRIKA

Wasafi Festival 2018 ndani ya uwanja wa Samora mjini Iringa

MICHUZI TV: Utalii mnono unapatikana ndani ya Mkoa wa Morogoro, unakaribishwa kujionea

MICHUZI TV: Ukimwi wazidi kuwa tishio mkoani Morogoro (Siku ya ukimwi Duniani)

MICHUZI TV: MBUNGE WA KASULU VIJIJINI AONGELEA MRADI WA RELI YA MWENDOKASI

BMG ONLINE TV: Raia wa kigeni wakamatwa mgodini, wengine walikuwa wamefichwa chooni

ALICHOKISEMA RAIS UHURU KENYATTA MBELE YA MAGUFULI BODA YA NAMANGA


MSD YATAKIWA KUKAMILISHA VIFAA VYOTE VINAVYOHITAJIKA KATIKA VITUO VYA AFYA VILIYOBORESHWA

$
0
0

Na WAMJW – MISUNGWI, MWANZA

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Bohari Kuu ya Dawa nchini (MSD) kuhakikisha wanakamilisha kuleta vifaa vyote vinavyohitajika katika vituo vya Afya vinavyoboreshwa nchini kabla ya Januari 15, 2019 ili wananchi waweze kupata huduma.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy wakati akiweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije na kukagua hali ya utoaji Huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

“Haina maana ya kuwa na majengo makubwa na mazuri ya Vituo vya Afya kama hakuna vifaa vinavyohitajika, huku Wananchi wanaendelea kupata tabu”, alisema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewahasa Wazazi na Wananchi wote kwa ujumla kutodharau huduma za Chanjo, hivyo kuwahimiza Wananchi wote kuwapeleka katika vituo vyakutolea chanjo watoto waliofika umri wa kupata chanjo

“Kifafa, Kifaduro,Donda koo, Surua, hayapo siku hizi kwasababu ya Chanjo, kwahiyo tusije tukadharau chanjo, tuhakikishe kila mtoto mwenye umri wakupata chanjo , akapate chanjo” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifunua kitambaa, ishara ya kuweka jiwe la msingi la ukarabati wa kituo cha Afya Koromije, ikiwa in sehemu ya majukumu katika ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiendelea na ukaguzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Koromije, ikiwa in mwendelezo wa ziara yake ya kukagua hali ya ubora wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. 
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe.Charles Kitwanga akisema jambo mbele ya wapiga kura wake (hawapo kwenye picha) katika kijiji cha Koromije Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Waziri wa Afya ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya kijijini hapo. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akihutubia wanakijiji wa Koromije (hawapo kwenye picha) pindi alipofanya ziara yake ya kukagua hali ya utoaji wa huduma za Afya Mkoani Mwanza. . 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiangalia gharama za matibabu kwenye mbao ya matangazo katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi. 


RAIS DKT MAGUFULI KUZINDUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI MKUBWA WA MAJI JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
Na. VERO IGNATUS, ARUMERU

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe John pombe magufuli anatazamia kuweka jiwe la msingi katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru

Mradi huo uliotiliwa saini hivi karibuni utazinduliwa katika kijiji cha kimyaki majira ya saa nne asubuhi na baadae kuzungumza na wananchi katika kijiji cha mringarimga

Wakizungumzia hali ya maji mkazi wa eneo mringaringa Josephat Joshua amesema wakinamama wanalazimika kwenda kutafuatamaji ya kunywa kutoka mringaringa kilometa mbili katika sehemu inayoitwa njoro au kwa wavii.Wakati mwingine sisi wakina baba tunabakia na watoto nyumbani.

'' Wakinamama wanafuata maji, hadi arudi nyumbani anakuwa tayari amechoka sana kutokana na kufuta maji umbali wote huo bado majukumu mengine yanamsubiria"alisema Joshua.Kwa akizungumza kwa bi Miriam Zakayo amesema inawalazimu kutembea umbali mrefu na kushindwa kutimiza majukumu yao kwa wakati 

'' Maji tunayoayatumia ni ya mto nayo yanachukua muda mrefu hadi kufunguliwa kwa sababu wengine tunayatumia katika mifugo, mashamba, hivyo tukitaka maji ya kunywa tunayafuata mbali"alisema Miriam.Mkazi mwingine wa kijiji hicho Saning'o Lebang'ute Laizer amesema kwa ujio wa Rais Magufuli kwao ni neema kwani itawatatulia tatizo hilo sugu la maji safi, barabara na umeme

''Tunashukuru sana kwa kuja kutufikia kwetu ni neema, barabara, hii inawahudumia watu wa kimmyaki, Ilikiding' a na Sambasha, mradi wa umeme, ni fursa kwetu pia"alisema Laizer.
 Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo akienda kufuata maji safi umbali wa km mbili kutoka kijiji cha Kimnyaki.Aidha katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji  Maji safi na salama wilayani Arumeru linapungua ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli leo anatarajia kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi Mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
Mkazi wa kijiji cha mringarimga Miriam Zakayo na wananchi wengine wakienda kufuata maji safi umbali wa km mbili kutoka kijiji cha Kimnyaki,katika kuhakikisha tatizo la upatikanaji wa Maji safi na salama wilayani Arumeru,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dkt John pombe magufuli anatarajia kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Arusha na baadhi ya maneo ya wilaya ya Arumeru.
Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo na Wananchi wa Arumeru akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro kwa pamoja wakimkaribisa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara rasmi ya kikazi katika wilaya ya Arumeru leo Jumapili katika kata ya Kimnyak na kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa visima vikubwa vya maji zaidi ya 20 ambavyo ni Sehemu ya Mradi mkubwa wa Maji Kwa Jiji la Arusha ambao utasaidia pia kutoa huduma ya Maji katika kata Saba za Wilaya ya Arumeru , Mradi utakuwa na thamani ya zaidi ya Bilioni 500.

HAFLA YA UWEKAJI JIWE LA MSINGI MRADI WA UBORESHAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI ARUMERU - JIJINI ARUSHA

TAARIFA YA TANGAZO LA KUHAIRISHWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA

TAARIFA YA KUAHIRISHWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>